Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 868 | 869 | (Page 870) | 871 | 872 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotpka kila wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.

  Habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa "Government by gesture, A President who looks good but governs impulsively"

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi wa habari hiyo Kaimu  Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa."Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma" alisema Zamarad.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na imelenga kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli aingie madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya watanzania na wageni.

  Biganda alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa imesajiliwa na TIC.
   Kaimu  Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mchana huu wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mwandishi wa " The Ecomist" Gazeti la Kiingereza linatoka kwa wiki dhidi ya Serikali ya Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda. 
   Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda (kulia), akitoa ufafanuzi wa Uchumi tangu Rais Dk. John Magufuli aingie madaraka na miradi iliyosajiliwa na kituo hicho.
   Mkutano na wanahabari ukiendelea.
   Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  Taarifa akichukuliwa na wanahabari.


  0 0

  MJUMBE mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Ali Mzee (katikati), akipanda mti katika zoezi la upandaji miti lililofanyika uwanja wa michezo Malindi mjini Zanzibar jana, kwa lengo la kuhuisha mandhari ya eneo hilo ambalo limeanza kuathiriwa na athari za kimazingira. Kushoto ni Mwenyekiti wa jumuiya ya Green World Family Foundation iliyodhamini zoezi hilo Nazir Ahmad Bachoo iliyodhamini shughuli hiyo. (Picha na Haroub Hussein).

  Na Salum Vuai, MAELEZO

  JAMII nchini imehimizwa kujenga utamaduni wa kupanda miti ili kuirejeshea Zanzibar uoto wa asili na kuiepusha na janga la kimazingira.Akizindua zoezi la upandaji miti lililofanyika pembezoni mwa uwanja wa soka wa klabu ya Malindi mjini Zanzibar, mjumbe mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Ali Mzee, amesema miti ni uhai kwa kila binadamu.

  Mzee alisema ni jambo la kusikitisha kwamba mazingira ya Zanzibar yamegeuka kutoka rangi ya kijani iliyokuwepo zamani na kuwa yabisi, hali inayosababisha kuongezeka kwa joto.“Bila miti, viumbe hutaabika na nchi inakuwa kavu na maradhi hasa presha huongezeka kila uchao. Lazima tuzinduke kwani tusipopanda miti, tunakaribisha janga kwa taifa,” alisema Mzee. 

  Aidha alivitaka vyombo vya habari kuandaa vipindi na makala mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupanda miti.
  Mapema, Mwenyekiti wa jumuiya ya Green World Family Foundation iliyodhamini zoezi hilo Nazir Ahmad Bachoo, alisema jumuiya yake inathamini mazingira na imeamua kulifanya zoezi la upandaji miti kuwa endelevu.

  Alisema ni jambo lililo wazi kwamba dunia nzima sasa inalia na hali ya joto litokanalo na ongezeko la hewa ukaa (carbon dioxide), inayosababishwa na upungufu wa miti na kuongezeka kwa vyombo vya usafiri barabarani vinavyozalisha moshi kwa wingi.“Umefika wakati sasa kila mmoja ahamasike kupanda na kuitunza miti katika eneo analoishi na yale yanayomzunguka, ili ilete manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho,” alisisitiza.

  Kwa upande wake, mratibu wa zoezi hilo na mwanaharakati wa mazingira Mohammed Abdulrahman Bajbeir, alisema Zanzibar imejaaliwa kuwa na wataalamu wengi wa masuala ya mazingira, lakini bado hawajatumika kikamilifu kuisaidia nchi.

  Kwa hivyo amezishauri mamlaka za juu kutanabahi na janga la kimazingira linaloinyemelea Zanzibar kutokana na utashi wa binadamu ambao wamekuwa wakikata miti ovyo bila kupanda mingine.
  “Zanzibar ya sasa sio kama ile ya zamani ambayo ilijaa kila aina ya miti pembezoni mwa barabara na mitaani. Tunafyeka miti kujenga nyumba za makaazi na maduka tukisahau kwamba miti ni muhimu kwa uhai wetu. Tubadilike,” alieleza Bajbeir.

  Wananchi mbalimbali wa mitaa ya Malindi, Mchangani na Mbuyuni wakiwemo wanasoka wa zamani wa klabu ya Malindi SC walioshiriki zoezi hilo, walieleza umuhimu wa kuilinda miti hiyo ili kuunusuru uwanja wa michezo, kwani umekuwa ukiharibiwa sana na watu wanaoweka magari pamoja na mifugo.

  Jumla ya miti 41 ya aina mbalimbali ilipandwa kuzunguka uwanja huo, na itakuwa ikilindwa na wananchi kwa kushirikiana na vijana wa ulinzi shirikishi na polisi jamii wa shehia ya Malindi.

  0 0

  Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es salaam siku ya Jumatatu, Juni 6, mwaka huu.
  Uzinduzi wa jukwaa hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa Akaunti ya Malaika kwa ajili ya kuwafungulia akaunti wanawake wajasiriamali wadogo wa hapa nchini.  
  Hafla hiyo inategemewa kuhudhuriwa na watu wapatao 1,000 kutoka makundi ya wadau mbalimbali wakiwemo wanawake wajasiriamali wa Tanzania Bara na Visiwani.
  Jukwaa hilo litatoa uelewa kwa washiriki hususan kuhusu fursa zilizopo na mikakati ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali katika  harakati za kuinua wanawake kiuchumi.
   
  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Dar es salaam

  03/06/2016

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO


  Shirikisho la Muziki Tanzania limewataka wananchi kuwapuuza wanamuziki wasio na maadili ili kuondokana na mmomonyoko wa maadili unaosababishwa na shughuli zao za kimuziki.

  Tamko hilo limetolewa leo Jijini Dar es Saalam na Rais wa Shirikisho hilo, Addo November alipokua akimtambulisha Katibu Mkuu wa Shirikisho la muziki ambaye ni John Kitime.“Mchakato wa kumtafuta Katibu Mkuu tumeufanya bila kukurupuka, nimefarijika sana kwa kukubali kwake ili kuhakikisha tunawakwamua wanamuziki kwasababu changamoto za muziki tulizokuwa nazo ni nyingi ikiwemo ya wanamuziki wasio na maadili”, alisema November.

  November aliongeza kuwa changamoto kubwa ni Sheria mbovu ya Haki Miliki ambayo mchakato wa kuirekebisha sheria hiyo pamoja na marekebisho ya sera ya utamaduni upo katika hatua za mwisho pia shirikisho limefanya jitihada za kuweka kipengele kinachozungumzia masuala ya sanaa kama haki ya msingi katika mchakato wa katiba mpya.

  Aidha, alisisitiza kuwa shirikisho hilo halipo kwa kumsaidia mwanamuziki mmoja mmoja bali ni kuhakikisha mfumo mzima wa muziki nchini unaweza kuwanasua wanamuziki wote na tasnia kiujumla ili muziki uwe na heshima.Naye, Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo, John Kitime amesema kuwa anategemea kutoa elimu kwa wanamuziki kuhusu kazi zao kupitia semina mbalimbali pamoja na kuimarisha shirikisho hilo ili vikundi vya wanamuziki viweze kusimama na kukuza muziki ili iwanufaishe wanamuziki wenyewe.

  “Sheria ya Haki za Binadamu namba 245 iko wazi kuwa kila mtu anastahili kupata mafao yake yanayotokana na ubunifu wake kwahiyo kutowalipa ni kuvunja haki hiyo ya binadamu, kazi kubwa tuliyonayo ni kuwaelimisha wanamuziki kufahamu haki zao”, alisema Kitime. 

  Shirikisho la Muziki Tanzania linajumuisha mwanamuziki mmoja mmoja pamoja na vikundi ambalo limeundwa na vyama 7 ambavyo vimesajiliwa na Baraza la Sanaa Tanzania vifuatavyo; Chama cha Muziki wa Taarabu, Chama cha Muziki wa Rhumba, Chama cha Muziki wa Dansi, Chama cha Muziki wa Asili, Chama cha Muziki cha Wapiga Muziki wa Diski, Chama cha Muziki wa Kizazi kipya pamoja Chama cha Muziki wa Injili.

  0 0

  Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Klabu ya Yanga, Salvatory Edward (kushoto) akisaidia kupima eneo atakalokabidhiwa mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga.Kulia ni Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib.

  SHEREHE za kukabidhi kiwanja cha ekari tano kwa mchezaji bora barani Afrika, Mbwana Ali Samatta unafanyika Jumapili 5,2016 kwenye kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga.

  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib alisema jana jijini Dar es SAlaam kuwa maandalizi yamekamilika na Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya TAifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi.

  Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha ya wanachama 180 waliokwisha kabidhiwa nyumba zao.

  Alisema SHIWATA imemzawadia Mbwana ekari tano ili ajenge kituo cha michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania watakaolitangaza taifa hili kwenye medani ya michezo kimataifa.

  Taalib alisema mtandao huo unaomiliki eneo la ekari 300 za kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji.

  Alisema sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185 wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana.

  Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa HAbari, Utamaduni na Sanaa, NApe Mnauye ambaye atakuwa waziri wa pili kutembelea kijiji hicho baada ya NAibu WAziri wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka huu.

  Viongozi wengine waliowahi kutembelea kijiji hicho ni kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2014, Wakuu wa wilaya ya Mkuranga wastaafu, Mercy Silla, Clemency na Mkuu wa wilaya hiyo wa sasa, Abdallah Kihato.

  Wageni wengine walioalikwa kwenye sherehe hizo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ITFF), Jamal Malinzi viongozi wa Serikali wa Wilaya ya Mkuranga na wasanii maarufu nchini.

  0 0


  Katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili

  Na EXAUD MTEI 

  Story ambayo bado ipo maskioni mwa watanzania walio wengi ni mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na mizengwe yake ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama vya upinzani kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti tofauti akiwemo mbunge kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO ZUBERI KABWE na wabunge wa vyama vya UKAWA.

  Sakata hilo limeendelea kuchukua Headline katika maeneo mbalimbali ambapo asubuhi hii chama cha ACT wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO SHAIBU wamejitokeza mbele ya wanahabari kueleza msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.


  Akizungumza na wanahabari leo Katibu huyo wa itikadi mawasiliano na uenezi wa ACT ADO SHAIBU ameeleza kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na adhabu hiyo mapokezi ambayo yanataraji kufanyika Jijini Dar es salaam na baadae kufwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao umepangwa kufanyika katika viwanja vya ZAKIEM mbagala lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge hao kueleza ukweli wa yale yanayoendelea bungeni Dodoma.

  Pamoja na mandalizi hayo chama hicho kimewaandikia barua makatibu wa vyama vya upinzani ambao nao wanapinga adhabu hiyo kutoka CHADEMA,CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba kuungana nao katika mapokezi hayo ambayo yamepewa jina la OPERATION LINDA DEMOCRASIA na bado hawajapata majibu yao lakini wanaamini wataungana nao katika Operation iyo ambayo itafwatiwa na mikoa mingine takribani minne.

  Habari24 tv imekuwekea video ya mkutano huyo wa wanahabari leo asubuhi


  0 0

  Diwani wa Mwanga Kusini mkoani Kigoma, Mussa Maulid akichimba mtaro ili kuzuia maji yaliyokuwa yakijaa madarasani kipindi cha mvua za Masika katika shule ya msingi Muungano Manispaa ya Kigoma Ujiji, shule ambayo alisoma diwani huyo. 
  Diwani wa Kaa ya Mwanga Kusini mkoani Kigoma, Mussa Maulid akikagua mradi wa barabara inayotengenezwa katika mtaa wa Kilimahewa, akimuelekeza Mwenyekiti wa mtaa huo Uhai Ahmed.

  0 0

  Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi, George Mkanza akifafanua jambo kwa madiwani wa halmshauri ya mji wa Kahama wakati ziara ya kutembelea Mgodi huo. 

  Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija(mwenye skafu) pamoja na waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mgodi huo. 
  Afisa mazingira wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Lusajo Njobelo akifafanua jambo kwa waheshimiwa madiwani na mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba wakati wa ziara hiyo. 
  Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Marco Peter katika eneo la uchimbaji. 
  Shimo ambalo shughuli za uchimbaji hufanyika kama linavyoonekana.
  Eneo maalumu la kusagia mawe kabla ya kupelekwa kiwandani kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu.   Madiwani pamoja na wataalamu kutoka halmashauri ya mji wa Kahama wakipiga picha mbele ya moja ya mitambo inayotumika kusomba mawe mgodini hapo.  Meneja Uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi Rodney Burgess (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama. 


  Wataalamu wa halmashauri ya mji wa Kahama wakiwa katika kituo cha kupozea umeme, kituo ambacho kinaelezwa kuwa kitatumika pia kufunga kifaa maalumu kilichonunuliwa na Mgodi wa Buzwagi ambacho kitawawezesha wananchi wa Kahama na viunga vyake kuweza kupata umeme wa uhakika. 

  Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Magesa Magesa akiteta jambo na Katibu wa Mbunge wa Kahama mjini, Abdul Mpei wakati wa ziara ya madiwani ambayo pia ilihusisha wataalamu kutoka halmashauri. 

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Kahama wakati wa kuhitimisha ziara yao walipotembelea Mgodi huo. 

  Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba (Kulia) akiwa na mwenyekiti wa ya wilaya ya Kahama, Abeli Shija wakimsikiliza Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakati alipokuwa anazungumza na madiwani baada ya ziara yao. 

  Picha ya pamoja baina ya madiwani wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wataalamu wa halmashauri hiyo pamoja na maofisa wa Mgodi wa Buzwagi.
  Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.
  Madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama wameupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa namna ambavyo umekuwa ukishiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Kahama na hususuani vijiji vinavyozunguka Mgodi huo.


  Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba ya madiwani hao na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija wakati wa ziara ya siku moja iliyokuwa imelenga kujionea namna Mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchimbaji.

  “Kwa niaba ya halmashauri ya mji tunawapongezeni sana kwa namna ambavyo mmekuwa chachu ya mendeleo kwa wilaya yetu na tunafarijika kwa sababu leo mji wetu uko na barabara nzuri lakini pia wakazi wa Mwendakulima na maeneo ya jirani wanao uhakika wa kupata huduma nzuri za afya katika kituo cha afya ambacho mmeshiriki kukijenga, watoto wetu pia wanaouhakika wa kusoma vizuri kutoka na miundo mbinu mlioiweka katika baadhi ya shule na hasa ujenzi wa maabara za kisasa ” alisema Shija.


  Mwenyekiti huyo pia aliuomba uongozi wa Mgodi kuwezesha upatikanaji wa kifaa kitakachosaidia mji wa Kahama kupata umeme wa uhakika ambao utaendana na Mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwa mji wa Kahama kutokana na line iliyopo sasa kushindwa kukizi Mahitaji ya wakazi wa mji wa huo.

  Akijibu ombi hilo Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema mpaka sasa kifaa hicho kimeisha fika na kinachosubiliwa ni wataalamu waliotengeneza kifaa hicho kutoka ujerumani kuja na kukifunga.

  “Kifaa kimeisha fika na tunachosubiri kwa sasa ni wataalamu tu kuja na kukifunga, matumaini yetu ni kuwa kazi hiyo itakapokamilika wananchi wa Kahama wataondokana na tatizo la umeme usiokuwa wa uhakika.” Alisema Mwaipopo.

  Ziara hiyo ambayo ilihusisha madiwani wa mji wa Kahama, Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba na wataalamu wa halmashauri hiyo, walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya Mgodi huo na kuelezewa namna suala la usalama wa mazingira linavyozingatiwa, ambapo madiwani hao walishangazwa na namna Mgodi huo ulivyozingatia sheria mbalimbali za mazingira na uchimbaji na kulifanya eneo hilo kuwa salama zaidi.


  Madiwani hao waliomba mgodi huo kuongeza ufahamu kwa Jamii kwa kuongeza ziara nyingi zitakazo husisha wananchi wa kawaida kwa lengo la kuwafahamisha shughuli zinazofanywa na Mgodi hali ambayo wamesema itasaidia kupunguza taarifa za uongo ambazo zimekuwa zikisambaa mitaani kutokana na Jamii kutokujua ukweli.


  Mwisho.


  0 0

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiendesha kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
  Wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St. Anne Marie ya Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma leo.
  Baadhi ya Mawaziri Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia jambo kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma leo.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwini Ngonyani akijibu maswali ya wabunge kuhusu uboreshaji wa Mawasiliano ya simu vijijini Bungeni mjini Dodoma.

  Wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

  Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (katikati) akiwa miongoni wa wageni waliolitembelea Bunge kujionea shughuli za kikao cha 36 cha Bunge mjini Dodoma leo.

  Mbunge wa jimbo la Mwibala (CCM) Mhe. Kangi Lugola akiomba mwongozo wa Spika wakati wa kikao cha 36 cha Bunge mjini Dodoma leo.

  Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge (Kulia) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi nje ya ukumbi wa Bunge.

  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa wameambatana na mwanafunzi mwenzao Eva Tolage (16) wa pili kutoka kushoto aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 kati ya 40,000 ambao barua zao zilisomwa waliomtumia barua Rais huyo duniani kote kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi zao kuhusu upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na EVA.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akimsalimia Mwanafunzi Eva Tolage (16) kutoka Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 ambao barua zao zilisomwa kati ya 40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi zao kuhusu upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na EVA.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa akimsalimia Mwanafunzi Eliudi Sanyi wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini akimsalimia wa Tanzania nje ya ukumbi wa Bunge, Dodoma.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini ambao wako kwenye kampeni ya Simama na Eva, Mwanafunzi wa Shule hiyo (katikati) aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani kati ya 40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi kuhusu upatikanaji wa Maji.

  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee nje ya Ukumbi wa Bunge leo. Katikati ni Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akizungumza jambo na Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.Picha/Aron Msigwa –DODOMA.

  0 0

  (Video na Benedict Liwenga, Muswada na Hussein Makame)

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Ofisini kwake,  Balozi wa zamani wa Marekani hapa nchini Tanzania, Balozi Charles Stith, alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dar es Salaam, leo Juni 3, 2016.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na mgeni wake Ofisini kwake,  Balozi wa zamani wa Marekani hapa nchini Tanzania, Balozi Charles Stith, alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dar es Salaam, leo Juni 3, 2016. 

  0 0

  Kampuni ya Safari Indoor Digital pamoja na kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express leo hii wamezindua rasmi huduma ya kisasa ya kutoa elimu mbalimbali kwa abiria kupitia TV (Screen) za kwenye mabasi.

  Hayo yamesemwa na Meneja operesheni wa kampuni ya Safari Indoor Digital Bi.Doreen Minja alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam.

  Bi Doreen amesema kuwa katika programu hiyo kampuni yao ya safari indoor digital watatumia screen za ndani ya mabasi ya kampuni ya Kilimanjaro express na jitihada mbalimbali zinafanyika ili huduma hii kufika katika mabasi yote.

  Aidha huduma hiyo itasaidia kumpatia abiria habari mbalimbali anapokuwa safarini kama haki yake ya msingi katika Nyanja za kijamii,kiuchumi na elimu na hasa elimu ya afya,sheria na biashara uku ikimwezesha abiria kutambua mambo mbalimbali ndani ya nchi na nje.

  Hata hivyo kampuni ya Safari Indoor Digital watakuwa na kipengele cha matangazo kwa kanda ambacho kitasaidia abiria kuweza kutambua fursa mbalimbali za mkoa uendao na hata kujua viongozi wa mkoa husika na watashirikiana na jeshi la POLISI na SUMATRA na chama cha kutetea abiria Tanzania (CHAKUA) kwa ujumla kutoa elimu katika screen hizo kuhusu haki mbalimbali za abiria,sheria za usalama barabarani kwa kutengeneza kipindi maalum kitakachoelimisha jamii kuhusu suala hilo.

  Nao chama cha kutetea abiria Tanzania (CHAKUA) kimewaasa abiria wote nchini kuitumia fursa hii vizuri kwani itawasogezea huduma za muhimu karibu kwani hata namba za simu za Polisi,Sumatra na Chakua zitapatikana katika screen hizo pindi linapotokea tatizo safarini.

  0 0

  Dotto Mwaibale

  NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mbio za Watoto za Azania Kids Run 2016, zitakazofanyika Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016, zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi katika kinyang'anyiro hicho kitakachokuwa na mbio za kategori tano.

  Gidabuday amebainisha kuwa, maandailizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.

  "Mbio hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, zikihusisha watoto chini ya miaka 16, ambako Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi," alisema Gidabuday.

  Amewasisitiza wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

  Gidabuday ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa kukimbia.

  "Barabara zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa watakaohitaji kupatiwa huduma hizo," amesema Gidabuday katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam.

  Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la kihistoria.

  "Mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh. 150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000," amesema.

  Katika mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000 na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.

  Aidha, amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh. 75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh. 40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama kilivyotajwa hapo juu.

  Pia kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini ya miaka mitatu, ambako washindi washindi wote watafunguliwa akaunti katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.
  Waratibu wa mbio hizo wakionesha fulana zitakazotumiwa na watoto watakao kimbia mbio hizo. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Peter Mwita, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.
  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akimkaribisha Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu mbio hizo zitakazofanyika kesho kutwa. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday.
  Mwanafunzi Rachel Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Mwenzake Ali Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wa mbio hizo.
  Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), akizungumzia kuhusu mbio hizo.
  Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday (kulia), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo.
  Wanahabbari wakichukua taarifa hiyo.


  0 0

  The world most famous and travelled beer Heineken, hosted the biggest football viewing party to herald the final of the UEFA Champions League matches between Real Madrid and Atletico in Milano and Dar es Salaam.
  Hundreds of football fans and consumers arrived in plenty at various premium outlets already to partake in once in a lifetime experience.
  Heineken also hosted ‘the Heineken Ibiza Final’ which is held on the weekend of the UEFA Champions League Final and the beginning of the party season in Ibiza – the world’s ultimate Party Island.
  Selected consumers who partake in various promotions were selected to be a part of the event which was also localised for the Tanzanian audience. The lucky fans from around the world had the opportunity of attending the screening party of the Champions League Finals and thereafter party with football stars, celebrities and renowned DJs.
  While the party is going on in Ibiza & Milano, football fans across Tanzania were not left out as Heineken TZ also hosted a special Champions League parties for consumers at George n Dragon, Samaki Samaki outlets and Club 777 to #ChampionTheMatch. Fans were treated to a VIP experience and the premium ambience of various outlets.
  The UEFA Champions League is the most prestigious club league; the premier sporting event has become a global phenomenon that fits perfectly with the Heineken brand, which is enjoyed in almost every country in the world. The Dutch brewer is a keen sponsor of global sports tournaments and unlike other industry players steers clear from sponsoring specific teams.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mfenesini Kichama, Mkoa wa Magharibi wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere Bububu,[Picha na Ikulu.] 03/06/2016
  Baadhiya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika mkutano wa kuwapongeza na kuwashukuru Wananchi na Viongozi wa Chama Wilaya ya Mfenesini Kichama wakiwemo Mabalozi,Wenyeviti wa matawi,Maskani na Makatibu katika ukumbi wa tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere leo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi wa CCM wakiwemo Mabalozi,Makatibu wa Matawi,Maskani na Wenyeviti katika Wilaya ya Mfenesini katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere,Bububu Mkoa wa Magaharibi Unguja leo
  Mwanachama wa Umoja wa Vijana UVCCM Rashid Mohamed Othman alipokuwa akitoa mchango wake uliogusia zaidi uendelezaji wa Matawi ya Chama yaendane na hadhi mchango huo aliutoa leo katika ukumbi wa Chuo cha Tawi la Mwalimi Nyerere Bububu Mkoa wa Magharibi Unguja wakati wa Mkutano wa Kuwashukuru Viongozi wa Mashina,wenyeviyi wa Matawi na Maskani uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein
  Balozi kutoka Koani Mwanahamis Iddi Mwanachama cha Mapinduzi wa Jimbo la Mfenesini Wilaya ya Mfenesini alipokuwa akichangia kuhusu wanachama wanaokiuwa Chama wachukuliwe hatua wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,alipofanya mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama Viongozi wa Wilaya ya Mfenesini kwa ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Tawi la Chuo cha Mwalimu Nyerere,Bububu Mkoa wa Magharibi,
  Mwanachama cha Mapinduzi wa Jimbo la Mfenesini Wilaya ya Mfenesini Mkoa wa Magharibi Mashaka Petro alipokuwa akichangia kukushu matengenezo ya Barabara ya Mwachealale wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,alipokua akizungumza na wanachama hao alipowashukuru na kuwapongeza kwa ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mfenesini Bw. Mjumbe Msuri wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa taCCM Mkoa Amani,.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki (katikati) akiwa na mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (Kulia) na Kamishna wa Tume Bw. Albert Msangi wakishiriki zoezi la Usafi katika eneo la Feri.Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Kyuki akiwa na Kamishna wa Tume Bw. Albert Msangi wakizoa taka katika eneo la FerWatumishi wa Tume wakiwa wamebeba taka wakati wa zoezi la kufanya usafi eneo la Feri.Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Isaya Mngurumi (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi anayemfuatia wakishiriki kufanya usafi.Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki (kushoto ) akiwa pamoja na Mkuu wa Wialaya ya Ilala pamoja na Makamishana wa Tume wakishiriki kufanya usafi.Kamishana wa Tume Profesa Sufian Bukurura (kulia) akiwa na mtumishi wa Tume Bw. Ally Msengi wakishiriki kufanya usafi.Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki akihojiwa na chombo cha habari wakati wa zoezi la kufanya usafi.Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la kufanya usafi katika eneo la Feri.


  0 0
 • 06/04/16--02:50: MUHAMMAD ALI AFARIKI DUNIA
 • Bingwa wa zamani wa mchezo wa Masumbwi Dunia kwa uzito wa juu (World Heavyweight Champion) aliyeaminika kuwa mmoja kati ya Mabondia bora zaidi kuwahi kutokea, Muhammad Ali maarufu kama "The Greatest" amefariki Dunia leo katika hospitali ya Phoenix-area iliyopo Phoenix, Arizona alipokuwa amelazwa kwa matibabu. 
  Ali ambaye alikuwa ni Bingwa mara tatu wa  ngumi za Uzani wa Juu Duniani, amefariki akiwa na umri wa Miaka 74.

  Muhammad Ali aliyestaafu ndondi za kulipwa mwaka 1981 aligundulika kuwa na ugojwa wa Parkinson (Parkinsons Disease) Mwaka 1984 na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo hadi alipopatwa na mauti.

   Mbali na ugonjwa huo pia Ali alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi pamoja na maambukizi katika njia ya mkojo.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. Amina

  **********  *********
  HISTORIA FUPI YA MUHAMMAD ALI.

  Muhammad Ali alikuwa bondia kwa sababu kuna mtu aliyemuibia baskeli yake. Alikuwa na umri wa miaka 12 wakati ule na alikuwa akiishi Louisville katika jimbo la Kentucky akijuilikana kwa jina la Cassius Mercellus Clay Jr.

  Joe Martin, aliyekuja kuwa kocha wake baadaye, anaelezea jinsi kijana huyo alivyokuwa akilia huku akiahidi kumtandika magumi aliyemuibia baskeli yake pindi akimpata. Kocha huyo wa ubondia alimchukua Clay, kijana mweusi anayetokea katika familia ya watu maskini, na kumjumuisha na watoto wengine aliokuwa akiwafundisha.

  “Alikuwa na bidii zaidi kuliko waatoto wote wengine niliokuwa nikiwasimamia,” anasema Joe Martin.
  Ingawa Clay wakati ule hakuwa na nguvu ya kuvurumisha masumbwi, alikuwa mwepesi wa kuranda randa kupita kiasi. Mnamo mwaka 1960, akiwa na umri wa miaka 18, alishinda katika pambano la ndondi la michezo ya Olympiki mjini Rome, Italia. Medali yake ya dhahabu inasemekana aliitupa ndani ya Mto Ohio kwa sababu alikasirishwa na jinsi watu weusi wanavyobaguliwa nchini mwake.

  Cassius Clay alikamilisha michuano ya wasiolipwa baada ya kuibuka na ushindi mara 100 katika jumla ya mapambano 108 aliyopigana. Wafanyabiashara 11 wa Kizungu kutoka Louisville walishirikiana ili kumfungulia njia Cassius Clay ya kuingia katika ulingo ya mabondia wa kulipwa.

  Bondia huyo mwenye kipaji alikuwa akitajikana pia kuwa ni mtu aliyekuwa na majivuno na mdomo mpana. Kabla ya mapambano yake, Cassius Clay daima alikuwa akijinata kuwa yeye “ndie mbabe wa wababe na mzuri kuliko mabondia wote na kuwakejeli wapinzani wake.

  Katika pambano lake la kwanza la kuwania ubingwa wa dunia Februari 1964 dhidi ya mtetezi wa taji hilo, Sonny Liston, Clay hakuwa akijulikana ni nani na watu waliamini angeshindwa tu. Lakini baada ya raundi ya sita, Liston aliungama. “Mie ndie mbabe,” alinguruma Cassius Clay kupitia kikuza sauti.

  *Mwaka huo huo, alisilimu na kujiunga na kundi la Nation of Islam lililokuwa likiongozwa wakati huo mwanaharakati wa haki wa Wamarekani Weusi, Malcolm X. Akabadilisha jina la Cassius Clay na kujiita wakati huo huo Muhammad Ali*

  Muhammad Ali hakuwa bondia tu, alikuwa mwanaharakati pia. Alipinga vita vya Marekani nchini Vietnam na alikataa kutekeleza sheria ya kutumikia jeshi. Mnamo mwaka 1967, akapokonywa sio tu leseni yake ya ubondia, bali pia alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, ingawa baadaye bondia huyo wa aina pekee aliachiwa kwa dhamana.

  Wasanii na wasomi mfano wa Richard Burton na Henry Fonda au mwandishi vitabu Truman Capote wakampigania mpaka Muhammad Ali akaruhusiwa tena kurejea ulingoni baada ya kulazimika kukaa nje kwa miaka mitatu.

  Machi 8, 1971 Muhammad Ali aliteremka ulingoni Madison Square Garden mjini New York kwa kile kilichotaajwa “kuwa pambano la ndondi la karne” dhidi ya bingwa wa wakati ule, Joe Frazier. Lilikuwa pambano kati ya mafahali wawili, kati ya mpinzani na yule aliyekuwa akiangaliwa kama mwakilishi wa mtindo wa maisha wa Kimarekani. Katika pambano hilo la kusisimua la zaidi ya raundi 15, Frazier akashinda kwa pointi. Ali akalazimika kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ubondia kunusa jamvi.

  Yakafuata mapambano mengine ya kusisimua mfano wa lile la mjini Kinshasa dhidi ya George Foreman mnamo mwaka 1974, ambapo Muhammad Ali anasema “aliranda mfano wa kipepeo na kuuma kama nyuki”

  Muhammad Ali alilipiza kisasi dhidi ya Joe Frazier mwaka 1975 na kumlazimisha kusalimu amri mnamo rauni ya 14. Mohammed Ali alistaafu mwishoni mwa mwaka 1981 baada ya kuranda kwa karibu miaka 40.

  Wakati huo tayari alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Parkinson. Licha ya maradhi hayo, Muhammad Ali ndiye aliyewasha mwenge wa Olimpiki huko Atlanta mnamo mwaka 1996 na kuusisimua ulimwengu mzima. Mwaka 1999 aliteuliwa na kamati kuu ya michezo ya Olimpiki kuwa “mwanaspoti bora wa karne.”

  Mpinzani wake wa zamani George Foreman amegeuka hivi sasa kuwa rafiki yake mkubwa na kuungama “Muhammad Ali ndie bingwa wa mabingwa.”


  Mpaka leo june 4 2016. Muhhamad Ali anapoteza maisha ndie mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. aliepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu.

  0 0

  Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya siku tano kwa njia ya mtandao akipokea cheti chake toka kwaMkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Senkondo (katikati) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoaratibiwa na Ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Wadau kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video (Tele Conference) wakati wa Mafunzo ya Siku Tano yaliyolengwa kwa ajili ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhusiana na masuala mbalimbali yanayaohusu majengo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
  Wadau kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video (Tele Conference) wakati wa Mafunzo ya Siku Tano yaliyolengwa kwa ajili ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhusiana na masuala mbalimbali yanayaohusu majengo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mafunzo toka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Dickson Mwanyika akiwashukuru wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakati wa ufungaji jan 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Mdau kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma akichangia mada kuhusiana na mafunzo ya siku tano waliyopatiwa na Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga akitoa neno la sukurani kwa mtoa mada (hayupo pichani) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano yaliyoaratibiwa na Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondoakiwashukuru wateja wake mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tano yaliyoaratibiwa na Ofisi yake 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya siku tano kwa njia ya mtandao akipokea cheti chake toka kwaMkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Senkondo (katikati) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoaratibiwa na Ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) 3 Juni, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Bw. Charles Senkondo (katikati) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA), Bw. Elius Mwakalinga (kulia) wakikata keki.

  0 0

  Katika kutambua mchango wa Tanzania katika uendelezaji wa makazi ya watu na kuweka mbele utu wa binadamu wa mahitaji ya msingi ikiwemo nyumba, wajumbe kutoka nchi 44 za kiafrika waliohudhuria Mkutano wa 35 wa Shirika la Makazi la Afrika Jijini Abuja Nigeria, kwa pamoja wameiteua na kuiidhinisha Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Shirika hilo utakaofanyika mwaka 2018.

  Katika Mkutano Mkuu wa Abuja changamoto iliyojitokeza ni uwezo wa nchi za kiafrika wa kuwapatia wananchi wake nyumba za gharama nafuu, huku wajumbe wakitoa rai kwa serikali zao kuainisha vigezo vya kutambua nyumba ya gharama nafuu. Aidha, wajumbe wa Mkutano huo wanaona changamoto kubwa ya wananchi wengi wa Afrika kuweza kumiliki nyumba ya gharama nafuu ni uwezo mdogo unaotokana na vipato vidogo, kutokuwepo sera ya kuwezesha raia kumiliki nyumba za gharama nafuu, kukosekana kwa miundombinu katika makazi ya gharama nafuu, riba kubwa za mikopo ya ujenzi wa nyumba nafuu na ukosefu wa ardhi ya kujenga nyumba hizo.

  Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi hizo ni kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. Hivyo, Mkutano Mkuu huu umeazimia nchi wanachama kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya nyumba kwa kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na maisha bora ya watu.(Habari za mkutano huo katika picha na Muungano Saguya, Abuja, Nigeria).

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa na viongozi wa Taifa la Nigeria na Shirika la Makazi la Afrika Jijini Abuja wakati ukipigwa wimbo wa Taifa la Nigeria katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula (wan ne kulia) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique). Wengine ni Waziri wa Nishati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde Fashiola (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shelter Afrique Bw. James Mugerwa (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shelter Afrique Bw. Jean-Paul Missi (wa kwanza kulia). Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje (wa pili kushoto) akiwa miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique uliofanyika Jijini Abuja wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.

  Mchoro huu juu na chini unaonyesha taswira ya mji wa kisasa unaotabiriwa kuwa Dubai ya Nigeria unaojengwa nje kidogo ya Jiji la Abuja ujulikanao kama Centenary City Abuja ambao wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika waliweza kuutembelea na kujionea ndoto ambayo wanigeria wameamua kuitekeleza.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa meza kuu baada ya Tanzania kuteuliwa na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique Jijini Abuja kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 utakaofanyika nchini Tanzania mwaka 2018.Kulia kwa Naibu Waziri ni Waziri wa NIshati, Ujenzi na Nyumba wa Nigeria Mh. Babatunde Raji Fashola ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.Wajumbe kutoka nchi 44 za Afrika na wageni waalikwa kutoka nchi na mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakiendelea na Mkutano wa 35 wa Shirika la Makazi la Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton Jijini Abuja, Nigeria. Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula.


  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usanifu wa Miji na Uendelezaji Upya Maeneo, kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Immaculata Senje.

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula akiwa katika kilima cha Katampe Jijini Abuja, ambacho ni katikati ya nchi ya Nigeria alipotembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika (Shelter Afrique). Kutokana na hali ya amani katika nchi hiyo, Naibu Waziri alipata ulinzi wa kutosha kama inavyoonekana alipopiga picha ya pamoja na walinzi walioandamana na wageni kutoka nchi mbalimbali katika ziara hiyo. Tudumishe amani yetu Tanzania.
  Wajumbe wa Mkutano wa 35 wa Shelter Afrique wakiwa katika eneo la centenary city unaotarajiwa kuwa mji wa kibiashara Jijini Abuja mji ambao unajengwa na serikali ya Nigeria kwa kushirikiana na sekta binafsi.

  0 0

  Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Iringa. Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi na Kushoto Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza.
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuanza ziara ya siku nne mkoani Iringa.

  Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa Eng. Daniel Kindole wakati wa ukaguzi wa barabara ya Dodoma –Iringa KM 260 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami.
  Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza akitoa taarifa ya hali ya Miundombinu kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara ya waziri huyo katika mkoani Iringa.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wakazi wa mikoa ya Dodoma na Iringa kutumia fursa ya kukamilika kwa kiwango cha lami barabara ya Dodoma Iringa kufanya shughuli za uzalishaji ili kujiletea maendeleo.

  Akizungumza wakati akikagua barabara ya Dodoma Iringa KM 260 Profesa Mbarawa amesema Barabara hiyo imelenga kufufua uchumi wa mikoa ya Iringa na Dodoma hususani hifadhi ya Ruaha na Vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa.

  “Barabara hii tuIiigawa katika sehemu tatu Iringa-Migori KM 95.2, Migori- Fufu KM 93.8 na Fufu –Dodoma Km 70,9 ili ikamilike kwa haraka na hivyo kuharakisha maendeleo ya watu wa Dodoma na Iringa “. Amesema Profesa Mbarawa.

  Profesa Mbarawa amesema kiasi cha sh. bil 4.6 itatolewa na Serikali ili kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa barabara ya Iringa mchepuo KM 7.3 itakayoanzia Kihesa –Kilolo kupitia Chuo Kikuu cha Iringa hadi Igumbilo ili kuondoa msongamano wa magari katikati ya Mji wa Iringa.

  Waziri Mbarawa amesisitiza nia ya Serikali ya kuukarabati uwanja wa Ndege wa Nduli mkoani Iringa ili kuwawezesha watalii wanaokwenda katika hifadhi ya Ruaha na Vivutio vingine vya Utalii Mkoani Iringa kutumia uwanja huo ili kuhamasisha uchumi wa mkoa wa Iringa.

  Naye Mbunge wa Isimani Mhe. Wiliam Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Iringa amemshukuru Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa kwa kukubali kujenga barabara ya Mchepuo ya Iringa na kumuomba aangalie uwezekano wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Iringa-Kalenga hadi katika hifadhi ya Taifa Ruaha yenye urefu wa KM 104.

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupanua barabara ya TANZAM eneo la Mlima kitonga na kumalizia ujenzi wa barabara ya Tosamaganga –Ugwachanya kwa kiwango cha lami na Ujenzi wa daraja la Tosamaganga ili kupunguza changamoto za usafiri kwa wakazi wa Iringa.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano yupo katika Ziara ya siku nne mkoani Iringa kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu mkoani humo.

older | 1 | .... | 868 | 869 | (Page 870) | 871 | 872 | .... | 1898 | newer