More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 1721 to 1740 of 37937)
- 05/19/13--21:04: _Montage yaikabidhi ...
- 05/20/13--01:30: _gazeti la dira liko...
- 05/20/13--02:21: _PICHA ZA WAREMBO WA...
- 05/20/13--02:26: _Viongozi wa Man U k...
- 05/20/13--03:24: _HIVI PUNDE KUTOKA B...
- 05/20/13--04:04: _Flaviana Matata kus...
- 05/20/13--05:25: _REDD’S MISS KURASIN...
- 05/20/13--05:28: _RAIS JAKAYA KIKWETE...
- 05/20/13--05:34: _MAKAMU WA RAIS DKT....
- 05/21/13--05:21: _UTAMBULISHO WA USIK...
- 05/21/13--05:44: _PROF JAY KAJIUNGA N...
- 05/21/13--06:21: _Wasanii Dina Mapund...
- 05/21/13--06:27: _Neno La Leo: Tukich...
- 05/21/13--06:30: _HAPPY BIRTHDAY MR G...
- 05/21/13--06:55: _WATANZANIA NUSU FAI...
- 05/21/13--12:05: _Mwana FA awataka wa...
- 05/21/13--12:08: _RAIS KIKWETE AONGO...
- 05/21/13--12:22: _Mkurugenzi Mkuu wa ...
- 05/21/13--12:27: _MAKAMU WA RAIS DKT....
- 05/21/13--12:31: _Mwanamke kushughuli...
(showing articles 1721 to 1740 of 37937)
Channel Description:
Karibuni Jamvini Wanajamii
Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Kigamboni wakiwa kwenye mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika Ijumaa Juni 7 mwaka huu kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko Kigamboni.
0 |
|
0 |
|
Viongozi wawili kutoka Manchester United -- Anthony Benerjee,
Mkurugenzi wa Uhusiano na Michael Higham, Meneja Uhusiano -- wanatua
jijini Dar es Salaam Jumatano hii kufanya mazungumzo na viongozi wa
Airtel Tanzania namna bora ya kuendesha michuano ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando amesema mkutano huo
utakaojumuisha wadau mbalimbali utafanyika makao makuu ya Airtel
Tanzania jijini Dar es Salaam na kutathimini ARS ya miaka miwili
iliyopita ili kuona namna nzuri ya kuendesha michuano siku za usoni
kuanzia mwaka huu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni moja ya wadau
wataoshiriki mkutano huo ili kutoa mchango wao hasa katika masuala ya
kifundi kama vile upangaji wa ratiba ya mashindano. Ratiba ya kuanza
kwa ARS 2013 inatarajiwa kutangazwa mwezi huu.
Michuano ya soka Airtel Rising Stars ilizinduliwa hapa nchini Tanzania
na sehemu nyingine barani Afrika mwaka 2011 ikiwa na lengo mahsusi la
kusaidia kuvumbua vipaji vya wanasoka chipukizi na kuwafanya waonekane
kwa makocha na mawakala wa kusaka vipaji vya wachezaji nyota.
Mashaindano haya huanzia ngazi ya chini ambapo timu za sekondari ngazi
ya mkoa huchuana ili kupata wachezaji nyota wa kuunda kombaini
inayowakilisha mkoa husika kwenye mashindano ya Taifa ambayo hufanyika
jijini Dar es Salaam. Jumla ya timu 48 zimepata fursa ya kushirikia
ARS katika miaka miwili iliyopita.
Katika mwaka wa uzinduzi 2011 mashindano ya ARS ngazi ya Taifa
yalifuatiwa na kliniki ya kimataifa chini ya usimamizi wa makocha
kutoka Manchester United iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam na kushirikisha wavulana na wasichana kutoka nchi za
Kenya, Malawi, Sierra Leone na mwenyeji Tanzania..
Mwaka jana fainali za taifa za ARS zilifuatiwa na michuano ya
kimataifa ya ARS zilizofanyika jijini Nairobi zikishirikisha nchi
ambazo kampuni ya Airtel hufanya biashara. Vile vile kliniki ya mwaka
jana ilifanyika Nairobi chini ya usimamizi ya makocha wazoefu kutoka
shule za mafunzo ya soka ya vijana za Manchester United ambapo vijana
walipata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za soka.
0 |
|
0 |
|
Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata leo atashiriki katika misa maalum ya kuwakumbuka watanzania waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba mwaka 1996.
Misa hiyo itafanyika kwenye eneo la makabuli ya kumbukumbu ya MV Bukoba ambapo Flaviana alipoteza mama yake mzazi na kaka yake katika ajali hiyo.
Mwaka jana, mwanamitindo huyu kupitia shirika lake la Flaviana Matata Foundation alitoa msaada wa maboya yaani vyombo vya kuokoa maisha majini (life vests) 500 kwa mawakala wa meli ya serikali yaani Marine Services Ltd ikiwa ni nja moja ya kujaribu kusaidia usalama majini.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi alisema kuwa mbali ya kushiriki katika misa hiyo, pia mwana mitindo huyo atafanya mazungumzo na wadau mbali mbali jinsi ya kuendeleza juhudi za kuimarisha usalama majini.
Flaviana alisema kuwa juhudi zake kubwa kwa hivi sasa ni kuhakikisha kuwa ajali za vyombo vya kwenye maji zinaepukika na ndiyo maana anapigana huku na kule katika sakata hilo.
Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kuona vyombo vya kuokolea katika kila meli vinapatikana na hasa kwa kutafuta misaada kwa wadau mbali mbali.
“Suala la usalama majini bado haujatiliwa mkazo vya kutosha na jamii pamoja na serikali” alieleza mwanamitindo huyu. “Muda umefika kwa wahusika wote kushirikiana kwa pamoja kuzungumzia na kukabiliana na changamoto hii” alisema Matata.
Mashindano ya Urembo ya Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka 2013 yanazidi kushika kasi, baada ya vituo kadhaa kumaliza mashindano yao sasa ni zamu ya kituo cha KURASINI (REDD’S MISS KURASINI 2013) ambacho kinategemea kuafanya shindano lake siku ya IJUMAA hii ya mei 24 katika ukumbi wa EQUETOR GRILL uliopo Mtoni kwa Azizi Ally,.
Jumla ya washiriki kumi na mbili wamejitokeza na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi huo chini ya mwalimu wao LUPATU ambaye alishiriki mashindano ya Redd’s Miss Tanzania 2012 akitokea Kanda ya Kinondoni.
Yafuatayo ni majina na umri wa warembo hao katika mabano.
1. STELLA MUGANYIZI (19) 7. BANDIO BYELA(20)
2. VIOLET MUSH (20) 8. SVETLANA NYAMEYO (20)
3. JACQUELINE NGOMA (19) 9. CATHERINE MANYAMA(21)
4. DARLINE MMARY (20) 10. MAINDA ABDI (21)
5. MARYCLARA JOHN (19) 11. ELIZA JOHN (19)
6. SHUMESA A (20) 12.LATIFA SULEMAN (20)
Taji la Redd’s Miss Kurasini linashikiliwa na FLAVIANA MAEDA ambaye alibahatika kushiriki katika fainal za Miss Tanzania 2012.
Shindano hili limedhaminiwa na REDD’S PREMIUM COLD, PJ AMUSEMENT, GAZETI LA JAMBO LEO, DODOMA WINE, , NAEEM CLASSIC WERE, KITWE GENERAL SUPPLIES,FATHER KIDEVU BLOG, HOUSE OF NAILS AND EYEBROWES NA CLOUDS FM.
ZUWENA MUSTAFA
MKURUGENZI
0 |
|
0 |
|
Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kukabidhiwa tuzo Mfuko wa GEPF ulipata tuzo kwa kuwa Mfuko unaoongoza katika kutoa huduma katika sekta isiyo rasmi kupitia mpango wake wa VSRS.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi Irene Isaka akiangalia taarifa za michango yake katika mpango wa hiari wa VSRS.
Afisa masoko wa GEPF Mkoa wa Dodoma Bw Josephat Mshana akimkabidhi taarifa (Statemet) ya michango Bi Irene Isaka Mkurugenzi Mkuu wa SSRA.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya kazi za msingi za Mfuko wa GEPF na faida wazipatazo wanachama wa mpango wa hiari kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw Daud Msangi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijaza fomu ya uanachama na kujiunga rasmi katika mpango wa hiari wa kujiwekea akiba katika mfuko wa GEPF akishuhudiwa na Meneja wa Masoko wa GEPF Bw Aloyce Ntukamazina.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Ally Sykes, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiaga na baadhi ya wazee waliohudhuria shughuli za msiba, wakati alipokuwa akiondoka baada ya kuhani msiba wa mwasisi wa TANU, Ally Sykes, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa kuzikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Dar Live Co. Ltd leo umetambulisha tamasha kubwa la kila mwaka la Usiku wa Hip Hop na fainali za kumtafuta Mkali wa Mic zijulikano kama 'The Vodacom Mic King' kwa wanahabari. Tamasha hili litafanyika Jumamosi hii, Mei 25, 2013 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.
Jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. Mbali na zawadi ya gari, mshindi wa kwanza, pili na watatu, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya Prodyuza mahiri nchini, Tudd Thomas, aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi. Majaji katika shindano hili ni mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho, DJ John Dilinga (JD) na Prodyuza Ally Baucha.
Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa wakali wa Hip Hop nchini ambao ni Fid Q, Joh Makini, Stamina, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego pamoja na shoo kali kutoka kundi la Wakali Dancers. Katika usiku huo, zitatolewa tuzo kwa wasanii wa Hip Hop na kwa wimbo bora wa Hip Hop uliofanya vizuri mwaka 2012/13. Kutakuwa na Tuzo kwa Msanii Mkongwe Bora wa Hip Hop na Msanii Chipukizi Bora wa Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop.
(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)
Pichani ni Prof Jay akionesha kadi yake baada ya kukabidhiwa kadi hiyo ya CHADEMA akiwa sambamba na Mh.Joseph Mbilinyi. Professa Jay ametangaza rasmi kuwa mwanachana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria bunge la bajeti mapema jana akiwa sambamba na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Mwanadada Lady Jay Dee. Kwa mujibu wa picha ambazo amekuwa akizisambaza kwenye mitandao ya kijamii msanii huyo alionekana akiwa na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi huku akiwa amekamatia kadi ya chama hicho kama aonekavyo pichani.
Pichani kati ni Msanii maarufu na mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Haule almaarufu kwa jina la kisanii kama Pro.Jay akiwa kwenye mchakato wa kujiunga na chama cha CHADEMA,mjini Dodoma,kwa taarifa zinaeleza kuwa Prof Jay amekwishajiunga na chama hicho akiwa tayari ni mwanachama halali,kulia ni Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA),Mh.John Mnyika na kushoto ni Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini (CHADEMA),Mh.Joseph Mbilinyi.Aidha inaelezwa kuwa Professa Jay amekabidhiwa kadi hiyo na Mbunge wa Mbeya mjini 'Joseph Mbilinyi' a.k.a Sugu.kujiunga kwa msanii huyo katika chama hicho kuna uwezekano akagombea ubunge 2015.!!!!!
Tunapoizungumzia Tanzania na utajiri wake wa wasanii na wanamichezo wenye vipaji,kwa hakika kabisa majina ya wasanii wachanga ndio chachu zinazo umua
burudani moto moto katika jamii...ya watanzania.
Majina ya wasanii wachanga yapo mengi,wasanii ambao kwa namna moja au
nyingine wanahitaji kupigwa jeki na sisi watanzania,ili waweze kufikia kilele cha mafanikio katika sanaa,ambazo pia ndio ajira yao.
Juzi kati katika kupekua pekua majina ya wasanii Mon G na mwanadada Dina Mapunda a.k.a Dina Brown ni wapya na ni moto mkali...tena moto wa kuotea mbali,
Dina Brown na Mon G wanasikika at
0 |
|
0 |
|
Ndugu zangu,
Naiona hatari kubwa nyingine inakuja mbele yetu. Ni haya makundi mawili; MaBodaboda na MaMachinga. Hofu yangu kuna wanasiasa wachache wanaowaona vijana hawa, katika matatizo yao ya kiuchumi, kuwa ni mtaji wa kisiasa. Na kimsingi wanawageuza kuwa ' Shuka za Kisiasa'. Na hapa ni wanasiasa wa vyama vyote.
Hatari yake?
Viongozi wasipokuwa makini, wakaacha kutanguliza busara na hekima kwenye kauli zao, basi, hofu ya kauli kupelekea machafuko na kuvunjika kwa amani itabaki kuwepo.
Maana, hawa MaBodadoba na MaMachinga, pamoja na kuwa wengi wao ni vijana wema kabisa, na ambao, kwenye mahangaiko yao, kama wagonjwa, wanamsikiliza kila anayekuja na kauli za kuwapa matumaini, hata kama ni ya muda mfupi, na hata kama ni kwa kuvunja sheria.
Na kwa vile Elimu ya Uraia iko chini sana katika jamii yetu, hata kwa miongoni mwa viongozi wetu, basi, ndio maana naiona hatari hii kubwa inayokuja mbele yetu. Kwamba MaBodaboda na MaMachinga wakiendelea kutumiwa kama ' Shuka za Wanasiasa', basi, yumkini, huko tuendako Watanzania tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi. Maana, siku zote, maovu huzaa maovu.
MBodaboda au Mmachinga mmoja akiuawa, kuna mia watakaokuja kutaka kulipiza kisasi. Na Polisi mmoja akiuawa, kuna operesheni ya kipolisi itakayofuata. Na polisi wetu hawa ni vijana hawa hawa ambao wengine wameponea chupuchupu kuwamo kwenye makundi haya ya MaBodaboda na MaMachinga, lakini sasa, tumewapa pia silaha za moto wabebe.
Naam, tukichoka kuhubiri Amani, Upendo Na Mshikamano, basi, tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi.
Maggid
Iringa,
0754 678 252
Mtoto aliyezaliwa jana Mr George Kivaria Mkuu wa Idara ya Njia Mbadala aka Alternative Channel ya NMB akikata keki tayari kwa kuwalisha wafanyakazi wa idara yake.
Kata Keki tule.........ndio muda huo uliwadia.
Mtoto aliyezaliwa jana George Kivaria Akiwa amepigwa na butwaa baada ya kupewa suprisezzzzz na baadhi ya wafanyakazi wa idara yake wakati alipokumbushwa siku yake ya kuzaliwa hapo jana
Mh George Kivaria akiwa na furaha wakati wafanyakazi wa idara yake walipomuandalia zawadi ndogo ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake hapo jana japokuwa alikataa kututajia umri wake.
Suprizeeeeeeee Mtoto aliyezaliwa jana Mh George Kivaria (Wa kwanza Kushoto) akipiga picha keki aliyoletewa na wafanyakazi wa idara yake hapo jana
Baadhi ya wafanyakazi wa idara ya Njia Mbadala aka Alternative Channel ya NMB Bank wakiwa makini kusubiria keki ikatwe tayari kwa kuliwa hapo jana katika ofisi ya idara hiyo
Hapa Sasa nyimbo zetu zile "Kata Keki tule ndio ilikua ikisika"
Keki ilipoanza kuliwa.
Uzaliwe tena ndio maneno yaliyosikika hapo.....
Keki tamu hadi inataka kudondoka
Happy Birthday Mr George baada ya Kulishjwa Keki
Operation meneja wa Njia Mbadala Mr Kilongo naye akipatiwa kipande Cha Keki
Hapa Sasa mtoto aliyezaliwa jana akilishwa keki yeye
Da Keki tamu ndio maneno yaliyotamba hapo jana
Cheerzzzzzzzzz...ndio ilifuata baada ya kumaliza kwa zoezi la kula keki.
Happy Birthday Mr George Kivaria Mungu Akuzidishie Nguvu, Upendo na Heri ya Miaka Mingi hapa Dunia.
--
0 |
|
0 |
|
Timu pekee kutoka Tanzania iliyobaki katika mashindano ya Guinness Football Challenge, Mwalimu Akida(kulia) na Daniel Msekwa(kushoto) tayari kwa nusu fainali ya kesho.
========= ====== = =====
* WATANZANIA NUSU FAINALI WIKI HII TAYARI KUWANIA UBIGWA WA PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE *
Mei 15, 2013 Dar es Salaam, Jumatano iliyopita kupitia televisheni za ITV na Clouds TV timu ya Ghana iliyoshinda katika kipindi cha Tisa cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE walifurahia kupata nafasi katika nusu fainali kwa kucheza azonto ambayo iliwafanya watangazaji Larry na Mimi kujiunga nao. Kofi Okarku na Isaac Aryee ingawa hawakufanya vizuri katika hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness walifanikiwa kupata dola za kimarekani 1,500 na waliufanya uwanja wote kunyanyuka na kucheza.
Timu iliyoshinda ilifanya vizuri katika hatua za mwanzo na kujipatia alama 16 pamoja na kuonesha uwezo mzuri ufahamu wa soka. Waliwashinda Wakenya katika hatua ya penati, hata hivyo timu ya Kenya imefuzu nusu fainali kama washindi wa pili.
Emanuel, Kenneth, Chris na Isaac wataendelea kuziwakilisha nchi zao katika hatua ya nusu fainali, wakiwa na ndoto za kufanya vizuri na kuwa washindi wa Pan-African Guinness Football Challenge.
Meneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi alisema, “Nusu fainali ya kwanza inatarajia kufanyika wiki ijayo tukisubiri kuona ni nani atakayefanikiwa kutinga fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE. Timu kutoka Dar-es-Salaam,Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad watapeperusha bendera ya taifa letu na kuwakilisha Afrika mashariki hivyo tunawatakia kila la heri. Tunazisifu timu zote na sasa timu bora zitakutana kuwania kufuzu kuingia fainali”
Timu zitakazoendelea na michuano ni pamoja na;
KWA WATANZANIA
· NDANI YA JEZI ZA KIJANI-Kutoka Dar-es-Salaam, Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao awali walijishindia dola za kimarekani 5,500 katika mashindano ya kitaifa na waliishia katika hatua ya penati kwenye robo fainali wataweza kufikia hatua ya pesa ukutani katika nusu fainali?
KWA WAKENYA
· NYEUSI-Kenneth Kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi.Ken ni kocha na Wills ni dereva.Timu hii ilijishinda katika robo fainali ya pili na kuongeza dola 1,500 kwenye dola 3,000 walizokuwa nazo awali.
· JEZI NYEKUNDU-ni timu ya pili kutoka Kenya,Francis Ngigi kutoka Nairobi na Kepha Kimani kutoka Thika.Timu hii ilipata dola 3,000 katika hatua za kitaifa na walifika hatua ya penati katika robo fainali.
KWA WAGHANA
· JEZI ZA BLU- Timu ya Ghana iliyopata fedha nyingi zaidi katika hatua ya kitaifa, Jonathan Naab kutoka Tindogo na Desmond Odaano kutoka Larteh wamefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kupata jumla ya dola 8,500. Je, watafanikiwa kuingia fainali?
Nusu fainali ya kwanzaitarushwa na televisheni za ITV na Clouds TV usikose kuangalia mchezo huu na kushangilia timu yetu.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge nchini wanaweza kupima maarifa yao katika soka kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.
Usikose kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.
Msanii mahiri wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA (pichani) ambae ni Balozi wa Chapa Vodacom amesema hadhi na heshima ya mwanaume katika jamii itakuwa na uzito mbele ya uso wa jamii kwa wao kuwa tayari kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabili jamii na wala si vinginevyo.
Mwana FA ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati wa kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu fistula iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square kuelekea siku ya fistula dunaini Mei 23. Kampeni hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Vodacom na Vodafone ya Uingereza ikiihusisha mikoa mbalimbali.
Balozi huyo amesema ni wazi kwamba wanaume wamekuwa wamiliki wa maamuzi katika jamii huku wakitajwa kuwa nguzo ya familia lakini sifa hizo na mamlaka hayo yatakuwa na dosari kubwa iwapo hawatokuwa pia mstari wa mbele katika kuhakikisha jamii inapata suluhisho la matatizo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe, wakati wa Kikao Cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, kilichofanyika leo May 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kufungua kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, leo Mei 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakiwa mkutano wa Kamati hiyo, leo Mei 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.Picha na Bashir Nkoromo.
Mkurugenzi Mkuu wa Helvetic Solar
Contractors Eng. Patrick Ngowi akiwa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alipofika katika ofisi hizo mapema leo kwa ajili ya mazungumzo na kuhojiwa katika kipindi cha Business Edition, kitakachorushwa Ijumaa hii saa 2 na dakika 15 usiku, Capital TV.
Dar es Salaam. 21 Mei, 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa Helvetic Solar Contractors Eng. Patrick Ngowi ameendelea kutoa rai kwa vijana nchini Tanzania kuwa na moyo na bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao za maendeleo na kujikwamua kiuchumi.
Eng. Ngowi ambaye pia ni mshindi wa ‘Forbes 2013: 30 under 30: Africa’s Best Young Entrepreneurs’ alisema maneno hayo mapema leo katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alipofika kufanya ziara na mahojiano maalum katika kituo hicho.
“Vijana wa kitanzania wanafursa nyingi sana katika nchi yetu, imefika wakati sasa vijana wajitambue kwamba wanaweza kutimiza ndoto zao kadiri bidii zao zitakavyowatuma. Kwa mfano, mi nilianza na mtaji wa shilingi milioni mbili, lakini hivi sasa nilipofikia biashara yangu imekua na nimeweza kufanya maajabu makubwa katika soko ukizungumzia
swala ya nishati ya jua,” alisema Eng. Ngowi.
Aliongeza, “Kinachotakiwa ni kuwa mbunifu katika biashara unayofanya, kuwa na ujasiri pamoja na umakini wa kile unachokipenda na pale unapotaka kufika. Yote yanawezekana na kijana yeyote
anaweza fanikiwa.”
Pamoja na hayo Eng. Ngowi aliwapongeza sana IPP media kwa mafanikio yao waliyopata katika kipindi chote tangu kianzishwe, ikiwemo tuzo ya ‘Number 1 Super Brand’ katika Afrika Mashariki hivi karibuni.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa ITV na Radio One Bi. Joyce Mhavile alimpongeza kwa mafanikio yake na kumshukuru sana Eng. Ngowi kwa ugeni wake.
Kampuni ya Helvetic Solar Contractors ambayo Eng. Ngowi ni muasisi wake, mwaka jana iliweza kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya ‘100 Top Mid-Sized Company in Tanzania.’ Mwezi Machi mwaka huu Eng. Ngowi aliweza kuorodheshwa katika kundi la wajasiriamali bora 30 vijana barani Afrika wenye umri chini ya miaka 30 ijulikanayo kama
‘Forbes 30 under 30:
Africa’s Best Young Entrepreneurs’
.
Picha
na habari na Amani Nkurlu.
0 |
|
0 |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya washiriki wa mkutano huo, baada ya ufunguzi. Picha na OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Mkoma, wakati akiondoka kwenye chumba cha mkutano baada ya kufungu rasmi mkutano huo wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Mimi ni mmama wa kawaida elimu yangu ni ya kaiwada ila ni mama
mjasiliamali napenda kujishughulisha na vitu mbali mbali hasa kilimo,
ufugaji na mambo mengine mengi ya kuinua kipato.
sasa Dina natafuta
wamama au wadada ambao wako serious na kujituma na kazi tuungane
tuanzishe kitu ambacho tukifanya waseme kuna wanawake Tanzania
wanaweza. Nahitaji wa mama wa kaiwaida ambao tukipanga kitu
tunafanya kwa moyo mmoja na nia moja na wawe ni wakujituma wasiopenda
kulalamika, wenye kuona mbele. mfano.Tukisema tunashughulika na kilimo
ni kilimo hasa sio mchezo tukisema tunafuga tunafuga kweli.
Nimejifunza ili uheshimike mwanamke unapaswa kujishulisha pasipo
kuangalia aliyeko mbele yako, nyuma yako, kulia kwako au kushoto
kwako. Ningependelea wenye elimu ya kawaida nina maana yangu. mama au
dada wa hali ya kawaida tumekuwa tukilalamika kwamba hatukwenda shule
ndo maana tunamaisha ya kawaida sasa nataka tuungane tufanye kitu.
nahitaji wa mama 6 tu
atakayekuwa tayari awasiliane na mimi kwenye mail: devota_michael@yahoo.com
Devotha