Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

KATIBU WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA JIMBO LA JIANGSU AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI YA KIKAZI ZANZIBAR

$
0
0
KATIBU wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Jimbo la Jiangsu Luo Zhijun, akivishwa shada la mauwa mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu, akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Jimbo la Jiangsu Luo Zhijun wakati mgeni huyo alipowasili katika uwanja wa ndege mjini Zanzibar.
Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (aliyevaa shati jeupe) Luo Zhijun, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu (wa kwanza kushoto).
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu, akizungumza na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China Jiangsu Luo Zhijun katika ukumbi wa watu mashuhuri (VIP) uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Abeid Karume Zanzibar. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.

MAKAMU WA RAIS AHIMIZA VIONGOZI WA NCHI ZA ACP KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

$
0
0

Na Mwandishi Maalum
Port Moresby - Papua New Guinea
2 June 2016,
 
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameanzisha majadiliano kuhusu umuhimu wa kumwezesha mwanamke kiuchumi kwa viongozi wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP) wakati wa Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi hizo uliofanyika Port Moresby, nchini Papua New Guinea.
 
Katika mkutano huo wa siku mbili uliomalizika jana nchini humo, Makamu wa Rais alikuwa mtoa mada mkuu katika majadiliano ya kumwezesha mwanamke kiuchumi  ambayo yalifanyika sambamba na Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali.
 
Makamu wa Rais ni miongoni mwa wajumbe wa Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ambalo liliundwa kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia Ajenda ya mwaka 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Jopo hilo linakusanya maoni, uzoefu na miongozo kutoka kwa wadau duniani kote kupitia majadiliano.
Mheshimiwa Samia aliuambia mkutano huo kuwa  uwezo mkubwa walionao wanawake kama wazalishaji wakuu bado haujatumika kikamilifu kwa miongo yote katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi katika nchi zao licha ya kwamba wao ni takribani nusu ya nguvu kazi ya dunia na kama wakiwezeshwa mchango wao unaweza kufikia zaidi ya trilion 20 ya pato la dunia.
 
Alisema kuna umuhimu wa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha kuwa wanawekeza katika kuwezesha wanawake kiuchumi ili kufanikisha Ajenda 2030 jambo ambalo litapelekea kupatikana kwa usawa wa kijinsia, kuondokana na umaskini na hatimaye uchumi kukua.
 
"Pamoja na maendeleo yaliyofikiwa, bado uwiano wa kijinsia umebaki kuwa mkubwa kwa wanawake katika sehemu zote za fursa za kiuchumi na matokeo, katika nchi zote wanachama," alisema Mheshimiwa Samia.
 
Makamu wa Rais alielezea matumaini yake kwamba uchumi imara ambao unaonekana katika nchi za ACP katika miaka ya hivi karibuni utaendelea kukua na kusisitiza umuhimu wa kuondoa tofauti za kiuchumi baina ya wanawake na wanaume ili kujenga uchumi ulio imara.
 
“Mara nyingi juhudi zimefanyika za kuleta usawa wa wanawake, kwa mwanamke mmoja mmoja,  katika familia, na kama mwananchi, dunia yetu imeendelea, na wote tumepata ustawi," alisema na kuongeza
 
"Kwa hiyo, tuwe na uhakika wa elimu bora, ajira za uhakika, upatikanaji wa huduma bora za afya na maisha huru bila ukatili na ubaguzi viwe vinawafikia kwa urahisi wanawake na wasichana ili kuleta usawa miongoni mwa jamii. Hivi vigezo vina muunganiko wa moja kwa moja na fursa za kiuchumi, uwezo wa mlaji wa kufanya manunuzi na hatimaye kukua kwa uchumi."  
 

Matokeo ya majadiliano ya katika mkutano huo yatasaidia kushawishi kazi ya Jopo hilo na kuhakikisha mtazamo wa kikanda unaingizwa katika ripoti ya kwanza itakayowasilishwa na jopo hilo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba 2016.

Wadau wa watakiwa kutoa mchango wa kuboresha kanuni za upatikanaji wa mbolea nchini.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

Wadau wa mbolea wameaswa kuangalia namna ya kuboresha sheria na kanuni za kusimamia sekta ya mbolea kwa manufaa ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo ili kiwe na tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea uliofanyika leo jiji Dar es Slaam.

Dkt. Turuka amesema kuwa maeneo ya kuzingatiwa katika warsha hiyo ni pamoja na kuboresha sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya mbolea ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika kuinua kilimo kwa manufaa ya Watanzania.

Gharama hizo zinahusisha kufanyiwa majaribio mbolea zinazotoka nje ya nchi kabla ya kuanza kutumiwa na wakulima ambapo majaribio hayo yanafanyika kwa misimu mitatu ya kilimo.Maeneo mengine ya kurekebisha ni pamoja na mlolongo wa tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kwenye mbolea inayoingizwa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo wajumbe katika warsha hiyo ni kuhakikisha sheria na kanuni wanazozifanyia kazi zitasaidia kuboresha upatikanaji wa mbolea zenye ubora unaotakiwa kulingana na mahitaji ya wakulima na waipate kwa wakati.

“Wakulima hapa nchini wananufaika na huduma zetu ambazo tunatoa ikiwemo kuwaunganisha na mawakala wakubwa wa pembejeo na makampuni yanayozalisha au kuingiza mbolea nchini” alisema Dkt. Msolla.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, Dkt. Msolla amesema kuwa shirika hilo linatoa huduma katika mikoa 12 nchini ambapo wapo mawakala 30 wanahudumia mawakala wadogo 500.

Mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.Mawakala hao msimu wa mwaka 2014/2015 wamefanikiwa kuuza kwa wakulima mbolea tani 60,000 na mbegu tani 3000 ambazo zimekuwa na manufaa katika kuhakikisha upatikanaji wa mazao ya chakula na biashara nchini.

Aidha, shirika hilo limefanikiwa kuwaunganisha wakulima na makampuni ya mbolea sita ikiwemo YARA, Extra Trading, Premium Agrochemical pamoja na Minjingu.Vile vile, Dkt. Msolla amesema kuwa wakulima wamenufaika na kujengewa maghala 14 hadi sasa yameanza kutumika ambayo yanauwezo wa kuhifadhi tani 50,000 kwa wakati moja hatua ambayo inasaidia kusogeza huduma karibu na wakulima wanapozihitaji.

Dkt. Msolla amesema kuwa Shirika hilo lenye makao yake makuu Afrika Kusini linatoa huduma kwa sekta ya mbolea katika nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo nchi tatu za kipaumbele ambazo ni Tanzania, Msumbiji na Ghana, nchi nyingine ambazo shirika hilo linafanya kazi ni Ethiopia, Senegal, Ivory Coast na Nigeria.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA MAKTABA MPYA YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, maafisa wa kampuni ya Kutoka China ya Jiangsu Jiangdu wakiweka mchanga kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Maktaba hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na makamu wa Rais katika serikali ya awamu ya nne Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Spika Mstaafu Pius Msekwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini katika Kitabu maalum cha Kampuni ya Jiangsu Jiangdu construction group inayojenga Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi wa China hapa nchini lu youQing kabla ya kwenda kuzungumza na jamii ya  wanachuo kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akitoa maelezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   kuhusu ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa itakayochukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Wziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipita kwenye mabango ya picha za mfano wa majengo ya Maktaba mpya itakayojengwa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya jamii ya  wanachuo na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba mpya itakayochukua zaidi ya wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli machapisho ya tafiti mbalimbali za madini na mambo mbalimbali ya kimaendeleo zilizofanywa na wahadhiri wa chuo hicho mara baada ya kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha machapisho hayo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kumaliza mkutano huo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU



MAMA MAGUFULI AMSHUKURU MTUMISHI WA MUNGU TB JOSHUA KWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZAKE ZA KUSAIDIA WAZEE

$
0
0
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Chama na Wazee wakati akiwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi pamoja na Vifaa vya Malazi.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula, Mavazi, Madawa pamoja na Vifaa vya Malazi.
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara
Baadhi ya Wazee walimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw. Rashidi Kambona akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika kituo cha Nkaseka Mkoani Mtwara na kumshukuru Mtumishi wa Mungu TB Joshua kuunga mkono juhudi zake za kuwasaidia wazee na watu wasiojiweza kwa kuchangia baadhi ya vitu vilivyotolewa kama msaada kwenye kituo hicho.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE NA MBOBEZI WA PICHA BW. ROBERT ROSS

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous na Mtaalamu wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu , Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip way. Kitabu hicho kinatarajiwa kutumika kama nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiangalia baadhi ya picha katika kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous na mara baada ya kukabidhiwa kitabu hicho na Mtaalamu Kimataifa, Bw. Robert Ross (kushoto) wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa kuzinduliwa leo jioni katika Hoteli ambapo Kitabu hicho kitakuwa ni nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.
Huu ni mwonekano wa nje wa kitabu cha Picha zilizochukuliwa katika Pori la Akiba Selous na Mtaalamu wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert Ross, Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri, Prof. Maghembe ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Injinia Angelina Madete katika hoteli ya Slipway.

UJUMBE WA JIANGSU CHINA WAKUTANA NA DKT SHEIN LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(kushoto) mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(wa tatu kulia) mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bw.Luo Zhijon,(kulia) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bw.Luo Zhijon,(kulia) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.

AFRIKA YATAKIWA KUIMARISHA UTAWALA WA SHERIA: BALOZI MAHIGA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Augustine Maiga akitoa maelezo kwa wadau waliohudhuria mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora (hawapo pichani) uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Maiga akiongea jambo na Balozi wa Italia Nchini Mhe. Luigi Scotto baada ya kumaliza mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa Mkutano wa Utawala wa Sheria kutoka nchi mbalimbali duniani wakifatilia kwa makini mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora ili kufikia agenda ya mwaka 2030 na 2063 ya malengo ya millennia uliofanyika leo jijini Dar es salaam.Picha na Ally Daud- Maelezo

Na: Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe


Dar es Salaam

BARA la Afrika limetakiwa kuimarisha Utawala wa Sheria kupitia vyombo vya dola ikiwemo mahakama na polisi ili kuisaidia mfumo huo kutetea maslahi ya wanyonge.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga wakati alipokuwa akifunga Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na Utawala bora.

“Lazima Afrika iimarishe vyombo vyake vinavyosimamia Utawala wa sheria na Utawala bora kama Polisi na Mahakama pamoja na kuwa na msimamo wa Bara katika kuzungumzia masuala mbalimbali” alisema Balozi Mahiga Balozi Maiga alisisitiza kuwa rushwa imekua adui mkubwa katika Utawala wa Sheria, hivyo ni lazima suala hilo lipatiwe ufumbuzi ili haki iweze kutendeka kwa watu wote.

Aidha, Balozi Maiga amemshukuru Balozi wa Italia nchini Mhe. Luigi Scott kwa kufanikisha mkutano huo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Sheria (IDLO) Bibi. Irene Khani kwa uamuzi wa wake wa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

“Mkutano huu ni wa kihistoria utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi ama Vyombo vinavyosimamia masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea maendeleo mazuri katika nchi za Afrika” alisema Balozi Mahiga.

Mkutano huo unaomalizika leo ulikua na kauli mbiu isemayo “Kufikia agenda ya 2030 na agenda ya 2063: Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”, umehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Mabalozi kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu ulimwenguni.

WAZIRI WA MALIASILI PROF. JUMANNE MAGHEMBE AIOMBA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KWA VITENDO KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI

$
0
0
Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kulia) akipokea ndege maalum aina ya drones kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (wa tatu kushoto) kwa ajili ya kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wengine katika picha ni kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa WWF - Tanzania, Amani Ngusaru, Meneja wa Pori hilo la Akiba  Selous,  Mabula Misungwi, Mwenyekiti wa bodi ya WWF - Ujerumani, Dkt. Valentin Von Moscow, Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani, Ebenhard Brandes na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuwia Ujangili, Faustine Ilobi Masalu. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Viongozi wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) na Viongozi wengine wa Wizara wakipokea maelekezo kutoka kwa Mtaalam wa uendeshaji wa ndege maalum aina ya drones na jinsi zinavyofanya kazi, Parmena Elisa, ndege hizo zilitolewa na Mfuko wa WWF kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous jana tarehe 1 Julai, 2016 Matambwe Selous.
Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ndege maalum aina ya drones zilizotolewa na Mfuko wa WWF kusaidia doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani, Ebenhard Brandes (kushoto). 
Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini (wa pili kushoto) akimkabidhi, Namsifu Johannes Marwa (Mhifadhi Wanyamapori), Tuzo ya WWF ya Mhifadhi Bora kwa mchango wake alioutoa katika kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani, Ebenhard Brandes na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuwia Ujangili Wizara ya Maliasili, Faustine Ilobi Masalu (wa nne kushoto), tuzo hiyo ilitolewa Matambwe Selous tarehe 1 Julai, 2016. 
Picha ya pamoja.



WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ameiomba Jumuiya  ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita ujangili kwa vitendo katika kuimarisha uhifadhi nchini.



Prof. Maghembe alisema hayo jana, Matambwe Selous, katika hafla fupi ya makabidhiano ya ndege maalum 8 zilizotolewa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.



Ndege hizo ndogo aina ya drones ambazo hazitumii rubani na huongozwa na mitambo maalum zitatumika katika pori la akiba la Selous kwa ajili ya kuimarisha ulinzi wa Wanyamapori kwa kukusanya taarifa za kiitelijensia zitakazosaidia kukamatwa majangili. Ndege hizo zina thamani ya dola za kimarekani 80,000 sawa na zaidi ya Tsh  milioni  172.


"Msaada huu umekuja wakati muafaka ambapo Pori la Akiba la Selous linahitaji teknolojia za kisasa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ujangili ndani na kuzunguka hifadhi hii" alisema Prof. Maghembe.

Alieleza kuwa changamoto kubwa inayoikabidili hifadhi ya Selous ni ujangili ambao kwa kiasi kikubwa umesababisha idadi ya Wanyamapori hususani tembo kupungua kwa kasi kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa mwaka 1986 idadi ya tembo katika pori hilo ilikuwa  50,000, idadi ambayo iliongezeka mwaka 2003 na kufikia 70,000 baada ya Serikali ya Ujerumani kusaidia kuanzishwa kwa Mpango wa Kuendeleza Selous (Selous Conservation Program) na Serikali ya Tanzania kukubali aslimia 50 ya makusanyo yanayotokana na utalii yabaki kuendeleza uhifadhi katika pori hilo.

Alisema kuwa baada ya mradi huo kuisha na mfumo wa “retention” kuondolewa na Serikali hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi ambapo kati ya mwaka 2008 na 2011 vitendo vya ujangili viliongezeka maradufu, sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya tembo hao kupungua hadi kufikia 13,000.

Prof. Maghembe aliongeza kuwa pamoja na hayo Serikali imejipanga kuhakikisha Wanyamapori wanalindwa usiku na mchana na kwamba wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ujangili watakamatwa na kufikishwa mahamani ili sheria ichukue mkondo wake.



"Hatutawavumilia hawa watu wamalize wanyamapori wetu wote tulionao, tunawafuatilia usiku na mchana na lazima tutawakamata" alisisitiza Prof. Maghembe.



Aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na washirika wa uhifadhi imechukua hatua za makusudi za kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuanzishwa kwa mpango wa Kitaifa wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori, mpango ambao umekuwa na matokeo mazuri baada ya kuungwa mkono na washirika hao kwa kusaidia fedha, vifaa na misaada mbalimbali ya kiufundi.


Aliongeza kuwa sehemu ya mpango wa Serikali wa kukabiliana tatizo hilo ni kuanzishwa kwa Jeshi Usu (Paramilitary) ambapo maeneo yote ya hifadhi nchini yatalindwa kijeshi. 

Prof. Maghembe ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine ili kukomesha ujangili ni lazima mataifa yaliyoendelea ambayo ndiko yaliko masoko makubwa ya meno ya tembo na bidhaa zake kusitisha kabisa uingizwaji wa meno hayo katika nchi zao ili kukomesha biashara hii haramu.

“Kuna nchi ambazo tayari zimechukua hatua ya kukataza kabisa uingizwaji wa meno ya tembo nchini mwao, mfano Marekani, tunaiomba sana jumuiya ya kimataifa wakiwemo marafiki zetu China na nchi nyingine wakatae kabisa uingizwaji wa meno haya nchini mwao, hii itasaidia sana kukomesha biashara hii haramu” Alisema.

Katika hatua nyingine Prof. Maghembe aliwataka wafugaji walioingiza mifugo katika maeneo yote ya hifadhi nchini waondoe mifugo yao kwa hiari kabla ya kushinikizwa kufanya hivyo na Serikali kwa mujibu wa sheria.

Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 Ibara ya 18 (2) inasema “Si ruhusa mtu yeyote kuingia na kulisha mifugo ndani ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Ardhioevu”

Prof. Maghembe alisema kuwa “mtandao wa ujangili unaanzia na watu wanaoingiza mifugo ndani ya hifadhi, hivyo ni lazima sheria zifuatwe  na waondoke mara moja, watakaokaidi sheria itafuata mkondo wake na mifugo itakayokamatwa itataifishwa na Serikali kwa mujibu wa sheria za nchi, sheria hizi hazina tofauti na sheria zinazokataza watu wasijenge mabondeni au kwenye hifadhi za barabara”  

Awali akitoa taarifa, Meneja wa Pori hilo la Akiba la Selous  Mabula Misungwi alieleza baadhi ya changamoto kuu zinazoikabili hifadhi hiyo kuwa ni pamoja na ujangili, miundombinu mibovu ya barabara kwa ajili ya doria na vifaa ikiwemo magari ya doria na nyumba za watumishi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF) Dkt. Marco Lambertini alisema kuwa ili kuimarisha Uhifadhi nchini ni lazima wananchi waishi karibu na maeneo hayo na pia washirikishwe juu ya umuhimu wake ili wasaidie kuyalinda kwa faida yao na taifa kwa ujumla.
(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii # www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

UZINDUZI WA MWANAMKE SIMAMA IMARA WAFANA JIJINI MBEYA.

$
0
0
Muandaaji wa kongamano la "Mwanamke Simama Imara" Miss Mbeya 2013 Jacklin Luvanda akizungumza jambo kwa Wageni waalikwa hawapo Pichani.
Mshindi wa Shindano la Miss Mbeya kwa Mwaka huu wa 2016 Eunice Robert akiwa ndani ya Vazi lake la Umisi katika Hafra hiyo ya Kongamano la "Mwanamke Simama Imala" lililo fanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa G.R City hotel Soweto Jijini Mbeya.
Baadhi ya Wanawake wa Jiji la Mbeya wakifurahi kwa pamoja huku wakicheza Muziki na Kupigana Picha katika Hafra fupi ya Mwanamke Simama Imara iliyofanyika hivi karibuni. Hafra iliyoandaliwa na Miss Mbeya Mwaka 2013 Jacklin Luvanda na kusapotiwa na Ally Rich Sanaa (Arts) Limited Ann's Statinary na Michuzi Blog kwa lengo la kuwakutanisha Wanawake wa Jiji la Mbeya, kuwa karibu katika harakati za kutafuta Maendeleo, Kupeana Mafunzo ya Ujasilia Mali na kubadilishana Mawazo Mbalimbali.
Mwalimu wa Somo la "Mwanamke Simama Imala" ambae pia ni Muigizaji katika Tasnia ya Filamu Nchini Maarufu kwa Jina la Kemmy akitoa Somo kwa Wanawake wa Jiji la Mbeya hawapo Pichani...
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AKAGUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI, NA KITUO CHA POLISI KUNDUCHI, OYSTERBAY POLISI NA MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tatu kutoka kushoto) akielekea kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za polisi zilizopo katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam jana, wanne kutoka kushoto ni Bw. Bernard Chagula ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Mradi huo anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kutoka kulia) akionyeshwa mchoro wa ramani ya jengo mojawapo linaloendelea kujengwa huko Kunduchi jiji Dar es salaam kwa ajili ya nyumba za kuishi askari wa jeshi la polisi,(wa pili kutoka kulia) ni Bw. Bernard Chagula ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Mradi huo anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Projest Rwegasira aliyenyosha mkono akitoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi juu ya miradi hiyo inayoendelea kujengwa, wanaomsikiliza ni baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Bw. Bernard Chagula (wa nne kutoka kushoto) ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Miradi ya ujenzi wa nyumba za polisi anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi, akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Projest Rwegasira(wa pili kutoka kulia) baadhi ya majengo(hayapo pichani) yanayoendelea kujengwa katika eneo la Polisi Oysterbay jiji Dar es salaam ambapo Katibu Mkuu huyo alifanya ukaguzi kujionea maendeleo yaliyofikiwa tangu kuanza kwa mradi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Projest Rwegasira (watatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, nyuma yao ni baadhi ya majengo yaliyokwisha kujengwa.

NCHEMBA ATAKA RAIS DKT. MAGUFULI AOMBEWE.

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe kulia akiwa na waziri Nchemba.
Waziri wa kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akizindua tamasha la urafiki katika viwanja vya Ndege mjini Morogoro jana Juni 2 ,tamasha lililoandaliwa na ushirikiano wa makanisa katika mkoa wa Morogoro na kuongozwa na mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe kulia na waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi wakiwapungia wananchi wa Morogoro mikono wakati wakiwasili katika viwanja vya Ndege kwa ajili ya uzinduzi wa tamasha la Urafiki lililoanza jana Juni 2 hadi Jumapili Juni 5.
Waziri wa kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae ni mbunge wa jimbo la Iramba akiwapungia mikono wananchi wa Morogoro wakati akiwasili katika viwanja vya Ndege kuzindua tamasha la Urafiki.
Mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren ambae anaongoza tamasha la Urafiki mjini Morogoro akimpongeza waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba baada ya kuwasili mkoani Morogoro kuzindua tamasha hilo.
Waziri Nchemba akimsikiliza mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren.
Mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren akiwa katika picha ya pamoja na waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba.
Waziri Nchemba akipokelewa na RC Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe .
Waziri Nchemba akiwasili uwanja wa mkutano.
Mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren wa pili kushoto akiwa na waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba pamoja na viongozi waandaaji wa tamasha la Urafiki Morogoro kushoto wa kwanza ni Askofu wa kanisa la Philndelphia Dr Yohana Masingu
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kabwe Steven Kabwe kulia akimwongoza waziri Nchemba.
Mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren akiteta jambo na waziri Nchemba 


Mapokezi ya waziri Nchemba Morogoro.








Kwaya ikitumbuiza katika uwanja huo.



Waziri Nchembe akizindua tamasha hilo.

Mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren akiendelea kuhubiri 
Wananchi wakiwa katika viwanja hivyo.





Mtoto ambae alikuwa hasikii toka azaliwe akijaribiwa baada ya kuombewa na kupona.
Mwanamke aliyekuwa kapooza akitembea baada ya maombi.
Mmoja kati ya watu walioanguka kwa mapepo uwanjani wakati wa maombi.
Mkazi wa Morogoro aliyekuwa anatembea kwa shida baada ya kuotwa na uvimbe mkubwa eneo la siri akiruka ruka kwa furaha baada ya kuombewa na kupona na mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren.
Mwanamke ambae alikuwa na matatizo ya kusikia kwa miaka zaidi ya 15 akitoa ushuhuda baada ya kuombewa na mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren kushoto .
Mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren akihubiri katika tamasha la Urafiki mjini Morogoro .
Na MatukiodaimaBlog, Morogoro.
WAZIRI wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba amelaani mauwaji ya kinyama kikatili yanayoendelea kuibuka nchini kuwa yasipewe nafasi na kutaka kila mtanzania kwa imani yake kuliombea Taifa kuondokana na mauwaji hayo pia wakati wote kutoacha kumwombea Rais Dr John Magufuli kwani kazi anayoifanya ni ngumu zaidi.

Huku akichangia Tsh milioni 2 ili kuchangia huduma za tamasha la Urafiki la kuliombea Taifa mkoani Morogoro kuendelea mjini Morogoro kwa madai kuwa huduma hiyo ni tiba ya maovu yanayoendelea kujitokeza hapa nchini kwa watu kuchinjwa kikatili kila kona ya nchini.

Waziri Nchemba alisema kuwa tukio la mashekhe na waumini wao kuchinjwa msikitini si jambo ambalo watanzania tumezoea kuliona ama kusikia pia mauwaji ya Mwanamke Aneth Msuya wa Dar es Salaam na watu nane kuchinjwa Tanga na lile la Mwanza si matukio ambayo yamezoeleka Tanzania , hivyo kutaka suala hili lisiachwe kuendelea na badala yake kuzidi kuliombea Taifa . 

“ Tunapokusanyika na tunapokuwa faragha katika ibada zetu tuliombee taifa letu ……jambo la pili kwa uzito huo huo tumwombee Rais wetu mpendwa Dr John Magufuli kazi anayoifanya ni ngumu … kazi anayoifanya ni kwa niaba ya watanzania wote na utashi ule anaoendanao ninyi wenyewe mliomba sana kabla ya kumpigia kura ….uzoefu unaonyesha mabadiliko huwa hayaji rahisi rahisi adui huwa hakubali kushindwa kirahisi kwa hiyo kila tunapoongea na Mungu wetu tukumbuke kumwombea Rais wetu ili kila mema anayoliwazia Taifa yaweze kutimia” alisema waziri Nchemba 

Kuwa kwa upande wake kila anapoona watumishi wa Mungu wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya huduma huwa haachi kuwasogelea japo kushikana nao mikono kama sehemu ya kupokea baraka kutoka kwao kwani wapakwa mafuta wakisema tu ubarikiwe Mungu juu mbinguni huweka tiki ya baraka. 

“Na hivyo ndivyo nilivyopata hata ubunge nilikuwa sina gari wala baiskeli na wazazi wangu walikuwa wanaishi katika nyumba ya tembe wakiwa na maisha magumu nikaenda kanisani kulikuwa na Harambee japo sikuwa na pesa nyingi niliamua kuchangia kidogo tu …..watumishi wale wakasema Ee Mungu mjalie haja ya moyo wake huyu kijana na mimi nilikuwa nikiwaza ubunge kweli ubunge ukatiki …..na hivi leo amekuja mhubiri wa kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren akasema kwa lugha ya kiingereza kuwa Ee Mungu timiza ndoto ya kijana huyo na mimi ndogo hiyo inaendelea kuota hivyo hivyo kwa hiyo najua na ninyi mtanikumbuka katika majukumu ambayo nimepewa na Rais ……leo baada ya saa 4 asubuhi hatukuwa na ratiba ya vikao vya bunge nimelazimika kuja Morogoro kuifanya kazi hii na leo hii nitageuza bungeni “ 

Kwani alisema majukumu ambayo anayatumikia pia yana harufu ile ile ya ambayo amewaomba kuzidisha maombi kuliombea Taifa kwani yana harufu ya umwagaji wa damu . 
Alisema waziri Nchemba kuwa alipoteuliwa na Rais Dr Magufuli kabla hata ya kuapishwa alipata taarifa ya mifugo kuuwawa na watu kuchinjana kwa kukatana mapanga mkoani Morogoro ambayo yalimkumbusha mapigano ya chuki na wivu kwa Abeli na Kaini mmoja akiwa mkulima na mwingine mfugaji.

“ Tuliombee Taifa letu kila mmoja afanye kazi inayomlete kipato pasipo kuwa na wivu na bila kuwa na dharau kwa kazi ya mwenzake ….kila nikipita huwa nawaeleza watumishi wangu kuwa hakuna mali ,mifugo,shamba ama kitu chochote chenye dhamani kubwa kuliko uhai wa mwa wanadamu” 

Kuwa serikali itatengeneza mazingira bora ya wakulima ama wafugaji kufanya kazi zao kwa uhuru na amani japo kila mmoja anapaswa kutambua kuwa uhai ni zaidi ya yote. 


Kwa upande wake mhubiri wa huyo kimataifa toka nchini Canada Dr Peter Youngren limpongeza waziri Nchemba kwa kujiweka mbele katika huduma&nbs ...

WADAU WATAKIWA KUTOA MCHANGO WA KUBORESHA KANUNI ZA UPATIKANAJI WA MBOLEA NCHINI.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka akifungua warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Lazaro Kitandu akibainisha baadhi ya changamoto zinzoikabili sekta ya mbolea nchini ikiwemo bei ya mbolea kulingana na uwezo wa wakulima wengi na muda mrefu wa majaribio kwa mbolea inaingia nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa mbolea kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla. Wa kwanza kushoto Mgeni rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka.
Mtaalamu wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Dkt. Consolatha Mhaiki akichangia mada juu ya matumizi ya mbolea ni yanavyopaswa kuendana na aina ya udogo kwa uzalishaji bora wa mazao wakati wa warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada wakati wa warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka (katikati aliyekaa )akiwa picha ya pamoja na wadau wa mbolea mara baada ya kufungua warsha ya wadau ha oleo jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi MAELEZO)


Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Wadau wa mbolea wameaswa kuangalia namna ya kuboresha sheria na kanuni za kusimamia sekta ya mbolea kwa manufaa ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo ili kiwe na tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea uliofanyika leo jiji Dar es Slaam.Dkt. Turuka amesema kuwa maeneo ya kuzingatiwa katika warsha hiyo ni pamoja na kuboresha sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya mbolea ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika kuinua kilimo kwa manufaa ya Watanzania.

Gharama hizo zinahusisha kufanyiwa majaribio mbolea zinazotoka nje ya nchi kabla ya kuanza kutumiwa na wakulima ambapo majaribio hayo yanafanyika kwa misimu mitatu ya kilimo.Maeneo mengine ya kurekebisha ni pamoja na mlolongo wa tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kwenye mbolea inayoingizwa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo wajumbe katika warsha hiyo ni kuhakikisha sheria na kanuni wanazozifanyia kazi zitasaidia kuboresha upatikanaji wa mbolea zenye ubora unaotakiwa kulingana na mahitaji ya wakulima na waipate kwa wakati.

“Wakulima hapa nchini wananufaika na huduma zetu ambazo tunatoa ikiwemo kuwaunganisha na mawakala wakubwa wa pembejeo na makampuni yanayozalisha au kuingiza mbolea nchini” alisema Dkt. Msolla.Kuhusu hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, Dkt. Msolla amesema kuwa shirika hilo linatoa huduma katika mikoa 12 nchini ambapo wapo mawakala 30 wanahudumia mawakala wadogo 500.

Mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.Mawakala hao msimu wa mwaka 2014/2015 wamefanikiwa kuuza kwa wakulima mbolea tani 60,000 na mbegu tani 3000 ambazo zimekuwa na manufaa katika kuhakikisha upatikanaji wa mazao ya chakula na biashara nchini.

Aidha, shirika hilo limefanikiwa kuwaunganisha wakulima na makampuni ya mbolea sita ikiwemo YARA, Extra Trading, Premium Agrochemical pamoja na Minjingu.Vile vile, Dkt. Msolla amesema kuwa wakulima wamenufaika na kujengewa maghala 14 hadi sasa yameanza kutumika ambayo yanauwezo wa kuhifadhi tani 50,000 kwa wakati moja hatua ambayo inasaidia kusogeza huduma karibu na wakulima wanapozihitaji.

Dkt. Msolla amesema kuwa Shirika hilo lenye makao yake makuu Afrika Kusini linatoa huduma kwa sekta ya mbolea katika nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo nchi tatu za kipaumbele ambazo ni Tanzania, Msumbiji na Ghana, nchi nyingine ambazo shirika hilo linafanya kazi ni Ethiopia, Senegal, Ivory Coast na Nigeria.

AMERICAN REGULATORS WIELD A BIG STICK, BUT NOT ALWAYS FAIRLY

$
0
0

LIKE politicians, financial regulators know that late on a Friday is a good time to slip out bad news. The Financial Crimes Enforcement Network (FinCEN), part of America’s Treasury, chose February 19th to announce it had rescinded a devastating finding against a European bank suspected of facilitating money-laundering. The withdrawal, less than a year after the designation, looks like a climbdown.

In March 2015 FinCEN branded Banca Privada d’Andorra (BPA) as a “primary money-laundering concern”, saying its top managers had moved cash for criminal groups. This so-called “311” measure (after the relevant section of the Patriot Act of 2001) is usually crippling for the bank concerned, because in effect it cuts it off from the American financial system and any banks that participate in it. 

BPA was no exception: the government of Andorra, a mountainous financial haven nestled between France and Spain, ended up taking over the bank despite objections from its majority shareholders, the Cierco family; its Madrid-based wealth-management arm was liquidated. The Ciercos, insisting there was no legal basis for FinCEN’s move, sued in the American courts.

FinCEN’s explanation for its reversal was that Andorra had taken steps to protect BPA from money-laundering risks, and the bank therefore no longer poses a threat. The Ciercos are having none of this. They argue that it was instead a “blatant effort to avoid judicial scrutiny” of the 311 measure. They point to the timing: the court was to hear a motion to dismiss the case next month. That would have required much more detailed evidence to be aired in support of the 311 action.

The Americans wanted to avoid this because their case was flimsy, critics say. The Ciercos have argued from the start that it was based on cases of suspected money-laundering which the bank itself had reported to Andorran regulators and had brought in KPMG, an accounting firm, to investigate.

If BPA was already cleaning up its act, why go after it at all? Some suspect the bank was a pawn in a tussle between governments: miffed that Andorra was slow to adopt American-style anti-money-laundering rules, including limits on cash transactions, America decided to show who was boss by selecting a bank to pick on. There is some evidence to support this sacrificial-lamb theory. In unscripted comments last year, for instance, an American diplomat suggested that America chose to “use the hammer” on BPA as a way of resolving wider concerns about Andorra. (FinCEN referred questions from The Economistto the Department of Justice, which declined to comment on the ground that lawsuits are under way.)

The Treasury has been challenged in another 311-designation case. FBME Bank of Tanzania sued it after being accused of servicing all manner of bad guys. Last autumn an American court issued an injunction blocking the government’s action until the bank received more information about why it was deemed a threat to the financial system. The case continues. Meanwhile, FBME’s operations have been severely disrupted: it has sought an injunction to stop the authorities closing an important subsidiary in Cyprus.

These cases highlight two problems with FinCEN’s money-laundering cudgel. The first is double-standards. It tends to go after only small banks in strategically unimportant countries; its use of 311 has been likened to using a sledgehammer to crack nuts. The second is its lack of openness. It faces no requirement to make detailed evidence public, or even available to a court, at the time of action. By the time any challenge is heard, it may be too late for the bank in question.

BPA is not dead, but it is seriously wounded. Much of the value may have already vanished from a bank that was worth €600m ($680m) before the debacle—though there are substantial assets left thanks to a freezing order. The Ciercos want the Andorran authorities to halt the disposal of its assets and enter into “remedial negotiations”. They have hailed FinCEN’s about-face as a “momentous victory”. But will it be a hollow one?Source: The Economist.

TANGAZO LA WASTAAFU WOTE KUTOKA LAPF

$
0
0
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WAANDAA ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA PENSHENI NA MFUKO HUO

 

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOLIPWA PENSHENI NA LAPF KUWA KUTAKUWA NA ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU NCHI NZIMA KUANZIA TAREHE 13.06.2016 HADI TAREHE 24.06.2016 KUANZIA SAA MBILI KAMILI ASUBUHI. TAREHE KAMILI KWA KILA WILAYA INAPATIKANA KWENYA MAGAZETI YA MWANANCHI YA TAREHE 06.06.2016, 08.06.2016 NA 10.06.2016, DAILY NEWS LA TAREHE 07.06.2016 NA 09.06.2016 NA TOVUTI YA MFUKO www.lapf.or.tz KILA MSTAAFU ANATAKIWA KUFIKA NA PICHA MOJA NDOGO (PASSPORT SIZE) NA KITAMBULISHO CHOCHOTE.

KILA MSTAAFU ANAYELIPWA PENSHENI NA LAPF UNAOMBWA UJITOKEZE KWENYE OFISI ZA HALMASHAURI ZILIZO KARIBU NAWE.

KWA MAELEZO ZAIDI PIGA 0767-600043 AU 0753-999991.

“STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF”

MASHAUZI, SNURA, ROMA MKATOLIKI NA WAZEE WA SINGELI KUISHIKA DAR LIVE JUMAMOSI HII

$
0
0
Jumamosi hii ya Juni 4 mbona ‘kitanuka’ Dar Live! Ni usiku wa nani mkali kutoka kwa mastaa wa taarab, bongo fleva na singeli.

Ni onyesho kubwa la na mwisho kabla kuelekea mapumziko ya mwezi mtufu wa Ramadhan ambapo Isha Mashauzi akiwa na kundi zima la Mashauzi Classic ataumana jukwaa na Snura, Roma Mkatoliki, Sholo Mwamba na Man Fongo.

Msemaji wa ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo amesema onyesho hilo la kipekee limezingatia muziki wa kila njanja ili kuleta ladha isiyochuja mwanzo hadi mwisho wa show.

Mbizo amesema kupitia onyesho hilo mashabiki watajionea wenyewe ni mzuiki upi wenye nguvu zaidi kati ya taarab, bongo fleva, singeli na hata rumba kutokana na ukweli kuwa Isha Mashauzi mbali na taarab lakini pia ana ngoma zake kali za muziki wa rumba.

Naye Isha Mashauzi amesema atalitendea haki onyesho hilo hasa kutokana na ukweli kuwa hajapanda jukwaa la Dar Live kwa takriban miaka miwili na hivyo hiyo ni nafasi pekee ya kutaka kiu ya mashabiki wake watakaofika kwenye ukumbi huo mkubwa zaidi wa burudani ulioko maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam. 

Banc ABC yaanzisha huduma ya kukuza biashara Afrika

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John Kazimoto, Jones Mwalemba, naJohn Du Toit.
 Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akibadikishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo, John Du Toit katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni  BancABC Tanzania, Khalifa Zidadu (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa Superdoll, Sateesh Babu Desu na Prasanthar Govinder pia wa Superdoll.

 Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk. Mabouba Diagne (wa pili kulia), akifafanua jambo mbele ya baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani), katika hafla waliyowaandalia  wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Bank ABC imeanzisha huduma mpya kwa wafanyabishara wakubwa kuhamisha and kuingiza mitaji yao ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya elektroniki.Akizungumza katika hafla iliyofanyika Jumatano hii, Mkuu wa kundi la Benki hiyo katika ukanda wa Afrika, Dk. Mabouba Diagne alisema wametenga Dola za Kimarekani milioni 20 (zaidi ya Sh billion 40) kwa ajili ya mpango huo unaolenga kuimarisha biashara miungoni mwa nchi za Afrika.

“Tumeanzisha huduma hii mpya kwa ajili ya kurahisisha na kukuza biashara miungoni mwa wafanyabishara wakubwa barani Afrika. Tunataka wafanyabiashara waweze kufungua milango yenye fursa nyingi za kibishara barani Afrika,” Dk. Diagne alisema.Alisema Banc ABC imezimia kuwawezesha Watanzania kutumia teknolojia mpya ya kuhamisha mitaji na fedha nyingi si ndani ya nchi tu bali nje ambako kuna fursa nyingi za biashara zisizotumika.

“Mara nyingi wafanyabishara wengi wa hapa nchini wanaofanyabishara nan chi jirani wamekuwa wakilalamika kukosekana kwa huduma bora za kuhamisha fedha kwa wingi. Sasa jawabu limepatikana kwa Banc ABC kuanzisha huduma za kisasa za kuhamisha mitaji,” alisema.

Alisema watu wanaweza kuhamisha mitaji hata fedha nyingi nchi za nje kwa kutumia simu za mkononi bila kuathiri biashara.“Tumeanzisha huduma hii kwa sababu biashara baina ya nchi za Afrika ni jambo muhimu la kuwezesha nchi na wafanyabishara waweze kutumia fursa nyingi zilizomo barani Afrika kutokana na bara hili kuwa na rasilimali nyingi asilia,” alisema kiongozi huyo msomi mwenye shahada ya juu ya uzamili ya hisabati.

Alisema suala la kubadilishana na kuhamisha mitaji ni biashara kubwa duniani kwa sababu mitaji ni bidhaa muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu.Mapema mkurugenzi wa Banc ABC Tanzania, Bw Dana Botha alisema tayari benki hiyo imeanzisha mtandao wa matawi 100 hapa nchini na kuwa miungoni mwa benki imara.Naye Mtendaji Mkuu wa kundi la benki hiyo Dk. Blessings Mudavanhu alisema kuwa benki hiyo ambayo imesajiliwa katika soko la fedha la London, ilizindua aina ya bidhaa yake mpya na kujitanua kimataifa baada ya kuungana na Atlas Mara.

“Tutatumia jamvia la teknolojia ya habari na mawasiliano. Tunataka watu waanchane na kuandika cheki nyingi na kutumia gharama kubwa za miamala ya katatazi badala yake watumie simu za mkononi,” alisema Dk Madavanhu.Alisema benki hiyo ambayo inaendesha biashara katika nchi za Tanzania, Nigeria, Afrika kusini, Botswana Zimbabwe, Rwanda, Burundi na Zambia imedhamiria kuwa benk kubwa inayokuza biashara miungoni mwa nchi za Afrika.

Katika hafla hiyo kampuni kadhaa kubwa zilishiriki na kuvutiwa na huduma hiyo mpya itakayotolewa na benki hiyo ya kimataifa. Kampuni hizo ni; Statoil, Mount Meru (T) Ltd, Lake Oil. Superdoll na Puma Energy.

KATIBU MKUU CHAMA CHA KIKOMINISTI BW. LIU ZHIJUN AKAMILISHA ZIARA YAKE ZANZIBAR NA KUELEKEA DAR-ES SAALAM

$
0
0
VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi CCM wakimsindikiza mgeni wao Katibu Mkuu Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun wakati alipofika Bandarini Mjini Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Baraza La Mapinduzi Issa Haji Gavu akizungumza na Mgeni wake Katibu Mkuu Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun baada ya kukamilisha ziara yake Nchini Zanzibar.
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mjini Borafya Silima Juma akiagana na Katibu Mkuu Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun alipokuwa akiondoka Bandarini na kuelekea Dar es Saalamu.
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohammed akiagana na Katibu Mkuu Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun alipokuwa akiondoka Bandarini na kuelekea Dar es Saalamu.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Baraza La Mapinduzi Issa Haji Gavu akiagana na Katibu Mkuu Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun alipokuwa akiondoka Bandarini na kuelekea Dar es Saalamu.KATIBU Mkuu Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun aliyevaa nguo nyeusi akiingia katika Boti ya AV KILIMANJARO alikielekea Dar es Saalamu baada yakumaliza ziyaza yake Zanzibar.PICHA NA MIZA OTHMAN – HABARI MELEZO ZANZIBAR.

JK AOMBELEZA MSIBA WA RAIS WA SAHARA MAGAHARIBI

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mama Salma Kikwete.
Mke wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikete.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa nchi ya Sahara Magharibi Brahim Salem Buseif mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI PAPOA NEW GUINEA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea Baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Picha yenye Nembo inayotumika Nchini Papua New Guinea kutoka kwa Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana. (Picha na OMR).
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images