Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

SIKU YA VIPIMO DUNIANI: VIJANA WA KITANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MAFUNZO KATIKA FANI YA VIPIMO ILI KUKIDHI MAHITAJI YA AJIRA KWENYE VIWANDA, GESI NA MAFUTA

$
0
0
 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (kulia) akiangalia moja ya mashine ya kisasa inayotumika kufundishia wanafunzi wa Fani ya Mizani na Vipimo ndani ya karakana ya chuo hicho leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyoongozwa na kauli mbiu isemayo Vipimo katika dunia inayobadilika.
Mkufunzi wa Mizani na Vipimo wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi Dar es salaam Ishigita Shunashu akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaosomea fani hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vipimo duniani.

 Baadhi ya wanafunzi wa kike wa mwaka wa kwanza katika Fani ya Mizani na Vipimo katika Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE). wakiangalia moja mashine ya kujifunzia masomo hayo iliyofungwa ndani ya Karakana ya Idara ya Vipimo na Mizani.
Mkufunzi katika Idara ya Mizani na Vipimo ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Bi. Rabia Katula akitoa ufafanuzi kuhusu namna wanavyowajengea wanafunzi wa kuhakiki ubora wa mizani  na kushughulikia matatizo mbalimbali ya mizani.

 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakufunzi wa chuo hicho, Idara ya Vipimo na Mizani.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaosomea shahada ya mizani na Vipimo.




Na. Aron Msigwa –  Dar es salaam.

Vijana wa kitanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za mafunzo katika fani ya vipimo na uendeshaji wa mitambo mbalimbali ili Tanzania mpya ya viwanda iweze kujengwa na wataalam wazawa kutoka ndani ya nchi.


Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanuel Mjema mara baada ya kutembelea maonesho ya mizani na vipimo kwa vitendo vitendo yaliyoandaliwa na walimu na wanafunzi wa chuo hicho yakihusisha matumizi ya vifaa na teknolojia ya kisasa  ya Mizani na Vipimo.


Amesema Tanzania inahitaji wataalamu wengi wa vipimo kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa katika sekta ya Mafuta kwenye makampuni yanayouza mafuta, mafundi wa pampu za mafuta pia kwenye mitambo ya Gesi na kuongeza kuwa mahitaji wa wataalam hao kwa sasa ni makubwa kuliko idadi ya wataalam wanaozalishwa kwa mwaka.


Ameeleza kuwa sekta ya vipimo duniani kote ni sekta mtambuka kwa kuwa inagusa maeneo mbalimbali ya maisha ya mwanadamu na huchangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa maendeleo katika maeneo mbalimbali ikiwemo mazingira,teknoloji, Gesi, ubunifu ambayo yote yana vipimo vyake.


Amesema kuwa CBE kama chuo kinachofundisha fani ya Mizani na Vipimo nchini kimeungana na taasisi nyingine za elimu duniani kuadhimisha Siku ya Vipimo duniani ambayo mwaka huu inaongozwa na kauli mbiu isemayo Vipimo katika ulimwengu unaobadilika kuweka msisitizo katika ufundishaji unaokwenda sambamba na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayotokea duniani  ili kukidhi mahitaji ya soko.


Amesema Siku hiyo iliasisiwa mwaka 1870 kwa lengo la kuweka viwango kwenye upimaji wa kutumia Mita na kuongeza kuwa kuanzia wakati huo siku hiyo imekuwa ikiadhimishwa duniani kote.


Amefafanua kuwa chuo cha CBE kimedhimisha siku hiyo kwa kuwa ni chuo pekee kinachotoa taaluma ya elimu na watalaam wa Vipimo Afrika Mashariki, Kati na Kusini na kubainisha kuwa nchini Tanzania taasisi za Serikali ikiwemo Wakala ya Vipimo ambayo watalaam wake wengi wamefunzwa katika chuo hicho.


Prof. Mjema amesisitiza kuwa suala la vipimo linagusa maisha ya kila siku ya wananchi kutokana na umuhimu na kuzitaja sekta kama vile viwanda, madini na uchimbaji wa Mafuta na Gesi haziwezi kufanikiwa bila kuwa na watalaam vipimo.


Ili kuhakikisha sekta ya vipimo na Mizani katika chuo hicho inakwenda  na mabadiliko yanayotokea duniani chuo hicho kimekuwa kikibadilisha mbinu za kufundishia wanafunzi na kuandaa mitaala mipya ili kukidhi mabadiliko hayo.


Aidha, amesema wao kama watalaam wa vipimo wanasimamia na kutoa ushauri kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kupiga vita ufungashaji wa mazao kwa kutumia vifungashio vilivyozidi maarufu kama Lumbesa ambayo vinamnyonya mkulima na kusababisha apate kiwango kisichoendana fedha na wingi wa mazao yake.


Amefafanua kuwa katika kukabiliana na changamoto  ya mabadiliko inayotokana na uvumbuzi wa Gesi na Mafuta nchini Tanzania  CBE ilianzisha mitaala ya ufundishaji wa nishati hizo kuwajengea uwezo wanafunzi wanaodahiliwa ili waweze kumiliki uchumi na kusimamia rasilimali za taifa kwa manufaa ya watanzania.


Prof. Mjema ameeleza kuwa licha ya vifaa vya kisasa vya kufundishia kupatikana gharama kubwa,chuo hicho imeendelea kufanya maboresho ya ndani kununua teknolojia mpya za kisasa zinazotumia mfumo wa digitali ili kuwawezesha wanafunzi kutumia mitambo mipya.


Amesisitiza kuwa CBE imeendelea na program mbalimbali za kuwajengea uwezo wakufunzi wake kwa kuwasomesha ndani na nje ya nchi ili waweze kutoa elimu yenye ubora na viwango vinavyokubalika.


“Ni kweli dunia imebadilika na teknolojia imebadilika sana tofauti na miaka ya nyuma, ili kuendana na mabadiliko haya tumebaresha mbinu zetu za ufundishaji ili wahitimu wetu waweze kumudu mahitaji ya soko kwa kukidhi viwango vya ndani na nje ya nchi kwa kuwa suala la vipimo halina mipaka” Amesisitiza Prof. Mjema.


Kwa upande wake Mkufunzi wa Chuo hicho Bw. Boniface Nyamweru amesema kuwa mafunzo anayoyatoa kwa wanafunzi wake yanalenga kuwajengea ujuzi na uwezo wa kubuni na kuanzisha vifaa vyao wenyewe vinavyoweza kutumika kwenye masuala ya Mizani na Vipimo.


Amesema kuwa yeye kama mtalaam wa masuala ya Mizani na Vipimo anawafundisha wanafunzi wake namna ya kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusiana na ufundi kwenye  Mizani, kufanya ukaguzi wa Mizani na Mita za kupimia vimiminika mbalimbali kama mafuta ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Mizani na vipimo nchini inapata wataalam wa kutosha wenye ujuzi.


“Mpaka sasa tunao wataalam wa ndani wazawa ambao tumewajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi , wengi wao tumewafundisha sisi hapa chuoni na wana uwezo wa kufanya ukaguzi na uhakiki wa Mizani na vifaa mbalimbali vya Vipimo katika viwango na ubora unaotakiwa” Amesisitiza.


Kuhusu matumizi ya huduma ya Mizani na vipimo nchini yanaendeshwa kwa mujibu wa sheria huku akifafanua kuwa vipimo vinavyofanyika nchini ikiwemo matumizi ya mita ya kupimia mafuta (Flow Meter) eneo la bandari ya Dar es salaam vimeruhusiwa kisheria.


Faudhia Nchila mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaosomea fani ya Mizani na Vipimo katika chuo hicho amesema kuwa sekta ya Vipimo na Mizani ina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kwa kuwa inagusa shughuli za kila siku za maisha ya wananchi.


Amesema vipimo vinagusa sekta ya ujenzi, maji, vifaa, teknolojia na shughuli mbalimbali za ufundi katika maeneo mbalimbali nchini huku akisisitiza kuwa mahitaji ya wataalam wa vipimo nchini kwa sasa ni makubwa kutokana na mchango wake katika maendeleo ya nchi na kutoa wito kwa vijana wengi zaidi kujiunga na masomo hayo.


Naye Dunstan Binamu mwanafunzi wa mwaka wa kwanza anayesomea masuala ya sheria katika fani ya Mizani na Vipimo akieleza mchango wa fani anayoisomea katika maendelea ya nchi amesema kuwa inalenga kulinda Haki ya mlaji katika kwa kuhakikisha masuala vipimo na mizani  yanafanyika katika viwango vilivyowekwa.

SIKU YA WAUGUZI, MUHIMBILI WAADHIMISHA SIKU YAO LEO.

$
0
0

Baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo wakifuatilia risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sabastian Luziga. 
PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
  Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akisoma kiapo kwa wauguzi katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika hospitali hiyo. 
 Wauguzi wa hospitali hiyo wakila kiapo katika maazimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Laurence Museru akifuatilia maazimisho ya Siku ya Waaguzi Duniani yaliofanyika leo ukumbi wa CPL kwenye hospitali hiyo.

 Mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Sabastian Luziga akisoma risala ya wauguzi mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Profesa Laurence Museru.
 Wauguzi, Cleopatra Mtei (kushoto) na Nasra Said (kulia) wa hospitali hiyo wakifuatilia risala iliyosomwa leo na mwenyekiti huyo.

KAIMU  Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amewakumbusha wauguzi kufanya kazi kwa kufuata maadili na misingi ya taaluma yao na kuwafichua wachache ambao wanaenda kinyume na maadili kazi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Profesa Museru ametoa wito huo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duaniani , ambapo wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo wameadhimisha siku hiyo.

Katika maadhimisho hayo Profesa Museru amewasisitiza wauguzi hao kutambua kwamba muuguzi ni mtu muhimu katika kutoa huduma, hivyo hawana budi kuwahudumia wagonjwa kwa moyo ili kuondoa malalamiko.

“ Nawaomba muwafichue wale wachache ambao wanatoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa kwani mkifanya hivyo mtatusaidia sana kuondoa kero na malalamiko yanayotolewa dhidi yenu,” amesema Profesa Museru.

Mipango ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akielezea mipango ya MNH Profesa Museru amesema Hospitali hiyo ina mpango wa kuwaendeleza kitaaluma watumishi wake wakiwemo wauguzi ili watoe huduma yenye kiwango cha juu zaidi.
Mpango mwingine ni kuboresha sehemu za kufanyia kazi, kununua vifaa tiba kadiri fedha zinavyopatikana pamoja na kutafuta kibali kwa lengo la kuajiri wauguzi wengine ili wasaidie kutoa huduma kwani wauguzi waliopo sasa hawatoshelezi mahitaji.

Kutekeleza agizo la Rais
Kwa mujibu wa Profesa Museru Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya mabadiliko makubwa katika kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli na kuhakikisha kwamba wagonjwa wanaokuja kutibiwa MNH wanapata dawa na kupata vipimo kwa wakati. 

Hivyo ametoa wito kwa wauguzi kushiriki katika jitihada zote zinazofanywa na Hospitali katika kuongeza mapato ya hospitali hiyo.

Akisoma risala ya wauguzi, Mwenyekeiti wa chama cha wauguzi Tawi la MNH, Sebastian Luziga amesema changamoto inayowakabili ni kuwapo kwa idadi ndogo ya wauguzi hali inayoathiri utendaji kazi.


“Idadi ya wauguzi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wagonjwa kwani kwa siku muuguzi anahudumia wagonjwa kati ya 20 hadi 30 tofauti na uwiano ambao muuguzi mmoja anatakiwa kuhudumia wagonjwa 6 hadi 8 kwa siku.” Amesema Sebastian.

Kauli mbiu ya siku ya wauguzi Duniani mwaka huu ni “Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko, Uboreshaji wa uthabiti wa mifumo ya afya”

Mei 12 wauguzi wote Duniani wanamkumbuka muasisi wa uuguzi mama Florence Ningtngale.

PIGA *113# AU TUMA SMS KWENDA 113 KUPAMBANA NA RUSHWA IFIKAPO MEI 24,2016.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA.

UZINDUZI WA KAMPENI YA KUELIMISHA UMMA YA
 ‘LONGA NASI’ MEI 24, 2016.
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), katika kutekeleza jukumu la ‘kushirikisha umma katika mapambano dhidi ya rushwa’, imeandaa kampeni ya kuelimisha umma iliyopewa jina la LONGA NASI. 

Kampeni hii itatumika pia kuitangaza huduma mpya ya kutoa taarifa za rushwa kwa kupiga *113# au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kwenda namba 113 kutoa maoni, taarifa au kuuliza maswali kupitia mitandao ya AIRTEL, HALOTEL, TIGO, VODACOM na ZANTEL. Huduma hii ya bure kwa wananchi itazinduliwa rasmi wakati wa uzinduzi wa kampeni tajwa.

Uzinduzi huu unatarajiwa kufanyika Jumanne - Mei 24, 2016 katika uwanja wa Mwembeyanga, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya kuzinduliwa, kampeni hii itafanyika nchi nzima na kushirikisha makundi yote ya jamii.

WANANCHI WOTE WANAKARIBISHWA KUHUDHURIA KATIKA KAMPENI HII.
Imetolewa na Ofisi ya Afisa Uhusiano, TAKUKURU Makao Makuu, Mei 20, 2016.

WATUMISHI SABA WASIMAMISHWA KAZI HALMASHAURI YA KARATU ,KUPISHA UCHUNGUZI

$
0
0

Mbunge wa Karatu Wile Qambalo.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Omary Kaang.


Na Woinde Shizza,Karatu

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Karatu limewasimamisha kazi baadhi ya watumishi kutokana na ubadhilifu wa fedha za Umma.

Mwenyekiti wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye amewataja waiosimamishwa ni Dr.Thobias Nkina ambaye alikuwa mganga mkuu,Judas Mahuma -Afisa Ardhi, George Ndimbo aliyekuwa Mhasibu,Jonathan Rukuntuka-Mtunza fedha,Sigfred Njanga-Mtunza fedha,Rajabu Lingoni alikuwa Muweka Hazina na Gurisha Kavuga -Mtunza stoo, wote hawa wamesimamishwa kwaajili ya uchunguzi.

Amesema kuwa kutokana na tume ya uchunguzi iliyoundwa mwezi mmoja uliopita na kamati ya fedha ya Halmashauri ,ikitaka kufahamu mapato na matumizi ya Kilimo na Afya ,ilibaini mambo kadhaa ambayo iliwasilisha kwenye kikao kwa ajili ya maamuzi,ndipo kamati ya madiwani ilipoamua kuchukua hatua ya kuwasimamisha .

Sambamba na hayo wapo watumishi ambao wamepewa onyo ambao ni Afisa Elimu Bernad Mnyenyelwa, Dr.Kyabaroti Kyabaroti pamoja na Omari Shemdiru,ambapo wapo watumishi wengine 8 ambao wanapaswa kurudisha fedha walizozichukua shilingi milioni 81 kama masurugu ya kufanyia shughuli mbalimbali za idara zao ndani ya siku 14.

Kwa maelezo ya baraza la madiwani limeomba wizara inayohusika kwa mkutugenzi huyo imuwajibishwe kwa kuisababishia Halmashauri hasara ya milioni 800 na kushindwa kuwasimamia watumishi wake na huku miradi ya kilimo na Afya ikiathirika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Moses Mabula amesema kuwa alipohamia katika.Halmashauri ya Karatu mwaka 2013 alikuta zimetumi zaidi ya milioni 200 pia ameongeza kuwa Halmashauri iliazima fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya dharura,kati ya miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa stendi kuu ya Karatu,Zahanati ya Ayalabe iliyoungua moto,Ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya msingi Ayalabe ili kupisha chuo ,ukamilishaji wa mitaro katika jengo la halmashauri,ujenzi wa maabara Endara na Mang'ola,Ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Manusway,Ukamilishaji wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Kansay .

Hata hivyo Moses Mabula amesema kuwa fedha zote ziliripotiwa katika baraza lililopita la madiwani 2015,pia amesema ameyapokea malalamiko yote na atawajibu baraza namna fedha zilivyotumika.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA UJUMBE WA CHUO KIKUU CHA AGHA KHAN

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako (wapili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Agha Khan baada yamazungumzo yao ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Mei 19, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Al - Karim Haji , Firoz Rasul, Amin Kurjina Joel Lugallo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Chuo Kikuu cha Agha Khan, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Mai 19, 2016. Kutoka kushoto ni Al - Karim Haji, Firoz Rasul, Joel Lugallo na Amin Kurji.

WATUMISHI SABA WACHUNGUZWA HALMASHAURI YA KARATU.

$
0
0
.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
Mbunge wa Karatu Wile Qambalo.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye.

Na Woinde Shizza,Karatu.
BARAZA la Madiwani katika Halmashauri ya Karatu limewasimamisha kazi baadhi ya watumishi kutokana na ubadhilifu wa fedha za Umma.

Mwenyekiti wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye amewataja waiosimamishwa ni Dr.Thobias Nkina ambaye alikuwa mganga mkuu,Judas Mahuma -Afisa Ardhi, George Ndimbo aliyekuwa Mhasibu,Jonathan Rukuntuka-Mtunza fedha,Sigfred Njanga-Mtunza fedha,Rajabu Lingoni alikuwa Muweka Hazina na Gurisha Kavuga -Mtunza stoo, wote hawa wamesimamishwa kwaajili ya uchunguzi.

Amesema kuwa kutokana na tume ya uchunguzi iliyoundwa mwezi mmoja uliopita na kamati ya fedha ya Halmashauri ,ikitaka kufahamu mapato na matumizi ya Kilimo na Afya ,ilibaini mambo kadhaa ambayo iliwasilisha kwenye.kikao kwaajili ya maamuzi,ndipo kamati ya madiwani ilipoamua kuchukua hatua ya kuwasimamisha .


Sambamba na hayo wapo watumishi ambao wamepewa onyo ambao ni Afisa Elimu Bernad Mnyenyelwa, Dr.Kyabaroti Kyabaroti pamoja na Omari Shemdiru,ambapo wapo watumishi wengine 8 ambao wanapaswa kurudisha fedha walizozichukua shilingi milioni 81 kama masurugu ya kufanyia shughuli mbalimbali za idara zao ndani ya siku 14

Kwa maelezo ya baraza la madiwani limeomba wizara inayohusika kwa mkutugenzi huyo imuwajibishwe kwa kuisababishia Halmashauri hasara ya milioni 800 na kushindwa kuwasimamia watumishi wake na huku miradi ya kilimo na Afya ikiathirika.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Moses Mabula amesema kuwa alipohamia katika, Halmashauri ya Karatu mwaka 2013 alikuta zimetumi zaidi ya milioni 200 pia ameongeza kuwa Halmashauri iliazima fedha kwaajili yakutekeleza miradi ya dharura,kati ya miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa stendi kuu ya Karatu,Zahanati ya Ayalabe iliyoungua moto,Ujenzi wa.madarasa 4 katika.shule ya msingi Ayalabe ili kupisha chuo ,ukamilishaji wa mitaro katika jengo la.halmashauri,ujenzi wa mahabara Endara na Mang'ola,Ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Manusway,Ukamilishaji wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Kansay .

Hata hivyo Moses Mabula amesema kuwa fedha zote ziliripotiwa katika baraza lililopita la madiwani 2015,pia amesema.ameyapokea.malalamiko yote na atawajibu baraza namna fedha zilivyotumika.

NEYO ALIVYOPPKELEWA JIJINI DAR NA MWANZA,KUTUMBUIZA LEO CCM KIRUMBA

$
0
0
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo amewasili jijini Mwanza jioni hii akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.
Neyo check out from the hotel Hyatt Regency
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akiondoka katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kiliamanjaro kueelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa safari ya jiji Mwanza kutumbuiza kwenye Jembeka Festival 2016 .
IMG_5465
Attu Mynah and Neyo
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group, Attu Mynah ambao wamedhamini usafiri uliotumika kumwendesha msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo gari aina Mercedes Benz GLE 350 D ya mwaka 2016 katika picha ya kumbukumbu na Msanii huyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Neyo ta Hyatt Regency-The Kilimanjaro
Msanii wa kimataifa Neyo aki-show love na walinzi maalum kabla ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya Mwanza.
Neyo official car Mercedes Benz GLE 350 D of 2016
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo akielekea kwenye gari maalum aina ya Mercedes Benz GLE 350 D ya 2016 lilitolewa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Neyo Sorrounded by Tanzanian Bodyguard
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere akiwa amezungukwa na walinzi maalum alipokuwa akielekea jijini Mwanza.
Neyo at Julius Nyerere International Airport
Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na mlinzi wake wakielekea jijini Mwanza leo jioni.
Neyo on Maasai Shuka
Balozi wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza leo jioni.
Getrude Clement na Neyo
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo aki-'show love' na Balozi wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Umoja wa Mataifa, Getrude Clement aliyefika uwanjani hapo kumlaki na kumvisha shuka la Kimasai. 

Bujora Cultural Troup Mwanza entertain Neyo
Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora Cultural Troupe cha jijini Mwanza akimshikisha nyoka aina chatu msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Neyo playing with a snake in Mwanza
Jembe FM Journalist Interviewing Neyo
Waandishi wa habari wa jijini Mwanza wakiwemo wa JEMBE FM wakifanya mahojiano na msanii Neyo alipowasili jijini Mwanza.
IMG_5666
Wakazi wa jijini Mwanza wakisalimana na msanii Neyo kwa shangwe na furaha waliofika kumlaki katika uwanja wandege wa jijini Mwanza.
IMG_5667
IMG_5662
IMG_5305
Msafara wa msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo ukielekea hotelini baada ya kuwasili jijini Mwanza.
Neyo at Malaika Resort
Msanii Neyo alipowasili kwenye hoteli ya Malaika Resorts ya jijini Mwanza akiwapungia wafanyakazi pamoja na wateja katika hoteli hiyo.
Justine Ndege and Neyo
Mwanasheria wa Jembe Media Group, Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.
Sebastian Ndege na Neyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo anayetarajiwa kutumbuiza kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Costantine Magavilla and Neyo
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (t-shirt ya blue) na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakijianda kupanda ndege ya Shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea jijini Mwanza. Shirika la Ndege la Fastjet ni miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo.
Neyo Crew to Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akiwa na 'crew' iliyoambatana na msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakipanda ndani ya ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza.
Jembeka Festival 2016 boarding Fastjest Airline
Neyo arrived in Mwanza
Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya Shirika la Fastjet ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Jembeka Festival 2016 mara baada ya kutua jijini Mwanza. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
IMG_5597
Baadhi ya wapiga vyombo waliombatana na msanii wa Marekani, Neyo wakishuka kwenye ndege ya shirika la Fastjet katika uwanja wa ndege wa jijini Mwanza jioni. Kampuni ya simu mkononi Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Costantine Magavilla
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla (wa pili kushoto) na Mwanakamati ya Jembeka Festival 2016, Sharon wakiwasili na katika uwanja wa ndege wa Mwanza jioni hii.
Sebastian Ndege
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla, Afisa Habari wa Jembe Media Group, Gsengo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege katika picha ya pamoja.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndio wadhamini wakuu wa Jembeka Festival 2016 kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Fastjet, SYSCORP Cooperation, CF Hospitals, KK Security, Samsung, EF Outdoor, Lacairo Hotel, Ndege Insurance, Jembe Media Group pamoja na Coca Cola.
Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo kwa kupiga 'Live Music' katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo msanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.

RC PAUL MAKONDA AFUNGUA MACHINJIO YA VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakati alipowasili kuzungumza na wafanyabiashara wa nyama katika Machinjio ya Vingunguti kabla ya kuifungua rasmi jana. Katikati ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto (wa pili kulia), akielekeza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Isaya Mngurumi.



 RC Makonda akiongoza ukaguzi huo.
 Taswira ya choo cha kisasa kilichojengwa kwenye machinjio hiyo.
 Wafanyabiashara katika machinjio hiyo wakimsikiliza Makonda (hayupo pichani)
 Mwonekano wa machinjio hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati.
 Wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo wa ufunguzi wa machinji hiyo.
 Makonda akisalimiana na wafanyabiashara baada ya kufungua machinjio hiyo.
Wafanyabiashara wakimkabidhi zawadi ya mbuzi RC Makonda, DC Raymond Mushi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi katika hafla hiyo ya ufunguzi wa machinjio hiyo.

SUKARI "YAKAUKA" MANISPAA YA KIGOMA-UJIJI, HATA ILE YA KILO SH. ELFU 5,000 HAKUNA

$
0
0
Mzunguko (Roundabout) na Stesheni kuu ya reli Kigoma. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

NA K-VIS MEDIA
MKOA wa Kigoma umekaukiwa na sukari kuanzania Ijumaa Mei 20, 2016 na taarifa ya Ofisi ya Biashara ya Mkoa, imesema, Wakazi wa Manispaa ya Kigoma –Ujiji wavumilie hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, kabla ya siku ya Ijumaa, sukari iliuzwa kwa bei ya shilingi elfu 5,000 kwa kilo, kwenye eneo la Manispaa ya Kigoma-Ujiji, lakini Ijumaa maeneo yote ya manispaa hiyo hayakuwa na sukari hata hiyo ya shilingi elfu 5.
Akizungumzia uhaba huo mkubwa wa sukari mkoani humo, Afisa biashara wa mkoa wa Kigoma Deogratius Sanga, amekiri kuwepo kwa uhaba huo na kuwataka wananchi wa Manispaa hiyo kwua wavumilivu wakati serikali ya mkoa inatafutia ufumbuzi tatizo hilo. “Taarifa toka bodi ya sukari ni kwamba ile sukari iliyoahidiwa na waziri mkuu itafika mwisho wa mwezi huu, na tunategemea kuanzia mwezi ujao tatizo hili litakwisha”.alisema Sanga



 Bandari ya Kigoma

 Mwalo wa Kibirizi
 Manispaa ya Kigoma- Ujiji
Uwanja wa Lake Tanganyika

SERIKALI YAOMBWA KUPITISHA FEDHA ZA MAENDELEO YA KILIMO KATIKA BENKI YA TADB.

$
0
0
Na Tiganya Vincent, Dodoma.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeiomba Serikali kupitishia fedha zote za maendeleo katika sekta ya kilimo katika Benki hiyo ili ziweze kuwafikia walengwa kwa urahisi zaidi.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB Thomas Samkyi wakati akitoa taarifa yake ya utangulizi kwenye semina ya wabunge wa Bunge la Jamhuri Muungano wa Tanzania kuhusu kuanzishwa kwa TADB na majukumu yake.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia Benki hiyo kuwa imara ili iweze kutoa huduma zinazotarajiwa kwa wakulima ambao wengi wako vijijin .Samkyi aliongeza kuwa kuimarika kwa Benki hiyo kutaiwezesha kutoa mikopo kwa wakulima wengi hasa wa vijijini ambao hawawezi kupata mikopo au mitaji katika Benki za biashara wala kuhimili gharama zake.

Alisema kuwa mtaji uliopo ni kidogo ambao benki hiyo haiwezi kukopesha miradi mikubwa wala mikoa mingi kwa muda mrefu kwani itakosa ukwasi katika kipindi kifupi.Aida ,Mkurugenzi huyo alisema kuwa pamoja na uhaba wa mtaji TADB imeweza kutoa elimu kwa wakulima 45,987 ili waweze kupatiwa mikopo.

Naye Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera wa TADB Francis Assenga Benki hiyo imeiomba Wizara ya Fedha na Mipango kuweka angalau tengo la shilingi bilioni 200 katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha wakati taratibu za hati fungamani zikikamilishwa.Aliongeza kuwa Benki hiyo iliweza kuwekeza sehemu ya mtaji uliopatikana kwenye masoko ya fedha na kupata faida kidogo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB Robert Pascal alitaja maeneo 14 ya kipaumbele ya bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kupatiwa mikopo kuwa ni kilimo cha nafaka, kilimo cha mazao ya viwanda(miwa na korosho) na ufugaji wa ng’ombe.Maeneo mengine ni kilimo cha mbogamboga(matunda,mboga mboga na viungo) na kilimo cha mbegu za mafuta ,kilimo cha mazao ya misitu(ufugaji wa nyuki) , ufugaji wa kuku wa kienyeji na kuku wa kisasa na ufugaji wa samaki.

RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Kitwanga, Waziri Mkuu atoa ufafanuzi wa hatua hiyo

$
0
0
 Mh. Charles Kitwanga aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini. 

“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.                                                   
Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli. 

“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu. 

Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, MEI 20, 2016.

WATUMISHI WA UMMA 210 WAIDHINISHIWA MIKOPO YA NYUMBA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.3

$
0
0
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma

Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema jumla ya Watumishi wa Serikali 210 wameidhinishiwa mikopo nyumba yenye thamani shilingi bilioni 2.3 baada ya kukidhi vigezo vya Bodi ya Mfuko wa Mikopo ya Nyumba za Watumishi wa Serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuwi wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.

Alisema kuwa Serikli imekamilisha uhakiki wa maombi mapya 191 ya watumishi wa umma waliomba mkopo wa nyumba katika maeneo mbali.Mhe. Lukuwi aliongeza kuwa kati ya maombi hayo watumishi 181 yamekidhi vigezo vya mfuko huo na yanatarajiwa kuidhimishwa mwishoni mwa mwezi huu.

Aidha , alisema kuwa Serikali kupitia Watumishi Housing Company (WHC) imeanza kujenga nyumba za kuuza kwa watumishi wa umma katika mikoa ya Morogoro, Dar es salaam, Pwani, Tanga na Mwanza

Mhe. Lukuwi alisema kuwa watumishi wa umma wanaotaka kununua nyumba hizo wanawaweza kupata mikopo yenye mashrti nafuu kupitia Benki za Azania , CRDB, NMB, BoA na Exim zilizoingia makubaliano na Watumishi Housing Company wanaojenga nyumba kwa ajili ya kuwauzia watumishi wa umma katika maeneo mbalimbali nchini.

MASHINDANO YA KOMBE LA MKUU WA MAJESHI KUFUNGULIWA MEI 24 MWAKA HUU

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa ya ufunguzi wa mashindano ya kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF CUP) ambayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 24 Mei 2016 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe: Nape Nnauye.

Mashindano haya yalianzishwa mwaka 2014, awali JWTZ lilikuwa likiteua wanamichezo wa kushiriki michezo ya kimataifa kupitia timu teule za Jeshi hali iliyopelekea kutovumbuliwa kwa vipaji vipya katika michezo, ikaonekana upo umuhimu wa kubadili mfumo wa uteuzi. Hivyo kuanzisha mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP) ambayo huanzia ngazi za vikosi hadi kufikia ngazi za brigedi.

lengo la mashindano haya ni kudumisha mshikamano, kuvumbua na kukuza vipaji, pia mashindano hayo yatatumika katika kuteua kombaini ya timu ya JWTZ itakayoliwakilisha Jeshi na Taifa kwa ujumla katika mashindano ya michezo ya majeshi na utamaduni kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika nchini Rwanda mwezi wa nane mwaka huu.

Kauli Mbiu ya mashindano haya ni “Michezo ni Ulinzi na Umoja Daima”

Timu zinazoshiriki mashindano haya ni Ngome (Makao Makuu JWTZ), Kamandi ya Jeshi la nchi kavu ikiwakilishwa na timu za Tembo, Faru, Nyuki, Mbuni na Chui, Kamandi ya Jeshi la Anga, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT).

Mashindano haya yatahusisha michezo ifuatayo, Mpira wa miguu kwa wanaume, Mpira wa kikapu kwa wanaume, Mpira wa mikono kwa wanaume, Mpira wa pete kwa wanawake na Mbio za nyika kwa wanaume na wanawake.Michezo hii itafanyika katika viwanja vya Twalipo vilivyopo Mgulani pamoja na uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Mashindano haya yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 06 Juni 2016. Mgeni rasmi katika ufungwaji wa mashindano haya anatarajiwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange.

Wananchi wote wanakaribishwa hakuna kiingilio.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.

TIKETI ZA BAHATI NASIBU YA TAIFA ZAANZA KUUZWA

$
0
0

Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandziwa Profesa Bongani Aug Khumalo,akitoa maelekezo ya mchezo huo kwa waandfishi wa habari na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kuuza tiketi, (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba na katikati ni Meneja mradi wa Kampuni hiyo,Brett Smith.Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Michezo ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba akijaribu mashine za michezo zinavyofanya kazi
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Gidani wakisikiza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Michezo ya kubahatisha,Abbas Tarimba (hayuko pichani) muda mfupi baada ya hafla ya uzinduzi wa kuuza tiketi.

-Mshindi wa kitita cha milioni 100 kujulikana Jumamosi

Kampuni ya Murhandziwa Limited ya Afrika ya Kusini ambayo imepewa leseni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa leo imeanza kuuza tiketi nchini kote na droo ya kwanza ya mchezo huo itafanyika jumamosi ya wiki ijayo ambayo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 100.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kuuza tiketi jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania,Abbas Tarimba amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kushiriki bahati nasibu inayoendeshwa kitaalamu na inayowezesha washindi kujishindia donge nono na kubadilisha maisha yao.

“Zawadi ya milioni 100 sio ndogo itasaidia kubadilisha maisha ya mshindi pia zitatolewa zawadi mbalimbali na serikali inategemea kupata mapato kwa njia ya kodi Zaidi ya dola milioni 40 kwa mwaka kutokana na uwekezaji huu katika sekta hii na aliwataka watanzania wachangamkie kununua tiketi na kushiriki katika mchezo huu.

Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandizwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo alisema kuwa watanzania wategemee kuona michezo ya kubahatisha ikiendeshwa kitaalamu na kubadilisha maisha ya washindi kutokana na zawadi nono watakazopata washindi.

“Tiketi za Bahati nasibu hii zitauzwa kwa shilingi 500 na zitapatikana kwa mawakala waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washitiki wa mchezo huu wa Bahati Nasibu ya Taifa wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea,vilevile droo nyingine za mchezo zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Jumamosi na kuwezesha wananchi wengi kushinda”Alisema.

Alisema mbali na mchezo huu kuwanufaisha washindi binafsi utawawezesha watanzania wengi kupata ajira Zaidi ya 1,000 za moja kwa moja na zisijo za moja kwa moja ambapomkwa sasa imeajiri watanzania 40 na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu inatarajia kuwa imeajiri wafanyakazi Zaidi ya 1,000.

MATUKIO YA PICHA BUNGENI DODOMA, JUMAMOSI 21 MEI, 2016

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Vangimembe Lukuvi akisoma Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 leo Bungeni mjini Dodoma 21 Mei, 2016.
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Mhe. Edwin Amandus Ngonyani (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Alphonce Kolimba Bungeni Mjini Dodoma 21 Mei, 2016.
Naibu Waziri, Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Eng. Ramo Matala Makani (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Selemani Saidi Jafo Bungeni mjini Dodoma 21 Mei, 2016.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Mhe. Jenista Joackim Mhagama (kushoto), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles John Mwijage (katikati) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Alphonce Kolimba wakiteta jambo leo Bungeni Mjini Dodoma 21 Mei, 2016.
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Mhe. Edwin Amandus Ngonyani (kulia) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhe. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe wakijadiliana jambo leo Bungeni Mjini Dodoma 21 Mei, 2016.
Mbunge wa CHADEMA, Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara (kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge mwenzie kuelekea ndani ya Bunge mjini Dodoma leo 21 Mei, 2016 kwa ajili ya vikao vya asubuhi siku ya Jumamosi bungeni hapo.

NAPE ATOA WITO WA WA ELIMU YA UOKOAJI IFUNDISHWE MASHULENI

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto), Flaviana Matata na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakiweka shada la maua kwenye kaburi la pamoja ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoaja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakijiandaa kuwasha mishumaa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto) akiweka mshumaa kwenye kaburi pamoja na Flaviana Matata kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa MV. Bukoba ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia) akimsikiliza Flaviana Matata muda mfupi kabla ya kupiga picha ya pamoja za kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Picha ya Pamoja.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa kuangalia mazoezi ya uokoaji majini yaliyofanywa na vijana 50 waliohitimu mafunzo ya uokoaji yaliyodhaminiwa na Flaviana Matata Foundation pamoja na UTT wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba yaliyofanyika mjini Mwanza ambapo mamia ya watu walifariki akiwemo mama mzazi na binamu wa Flaviana Matata.
Sehemu ya waliofuzu mafunzo ya uokoaji wakionyesha namna ya kuokoa watu majini wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, Mhe. January Makamba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula na Flaviana Matata
Sehemu ya makaburi ya pamoja ya waliofariki kwenye ajali ya MV. Bukoba mwaka 1996 ambapo leo imetimia miaka 20 tangia ajali hiyo imetokea.
Viongozi wa Dini walioshiriki kwenye kutoa ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kutokea kwa ajali ya MV. Bukoba.
Sheikh Hassan Kabeke akiongoza dua wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 ya ajali ya MV. Bukoba ambapo mamia ya watanzania walifariki dunia.
Flaviana Matata (kushoto) akiwa amejiinamia kwa huzuni wa kumbukumbu ya ajali ya MV.Bukoba ambapo alipoteza Mama Mzazi pamoja na Binamu, katikati ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Kepteni Winton Mwasa na kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
Mchungaji Obadi Ruralila wa KKT akiongoza ibada ya kuwaombea marehemu kwenye kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba ambapo mamia ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiongozwa na Flaviana Matata walijitokeza kwenye makaburi ya pamoja ya Igoma mjini Mwanza.
Shemasi John Kasembo wa Parokia ya Ilemelea akitoa neno la mungu wakati wa kilele cha kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba. 
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Kepteni Winton Mwasa akizungumza machache juu ya uboreshaji wa elimu ya uokoaji waliyoitoa kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation pamoja na UTT ambapo watu 50 walihitimu mafunzo ya kuokoa majini.

Flaviana Matata akizungumza wakati wa kumbukumbu ya miaka 20 ya ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Bukoba ambapo alipoteza Mama Mzazi pamoja na Binamu yake.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya jali ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauyeakizungimza wakati wa maadhimisho yamiaka 20 ya kumbukumbu ya ajali ya MV. Bukoba ambapo alisema imefika wakati elimu uokoaji itolewe kwa vijana wadogo ili wawe na uelewa mkubwa wa kukabiliana na matatizo yanapotokea.
Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza ambao walipoteza ndugu , jamaa na marafiki 




MWANACHUO BENADETHA MSIGWA ANAOMBA MSAADA ILI AKATIBIWE MACHO

$
0
0
Jaman wapendwa kuna mwanafunzi mwenzetu amepata upofu akiwa chuo na sisi kama wanafunzi tumeamua kumchangia pesa kama inawezekana akatibiwe ila inahitaji kama milion 30 kwa hiyo kwa yeyote atakaeguswa anaweza tuma chochote kupitia namba hizo hapo kwenye hicho kipeperushi.

MANDHARI ZA KUVUTIA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

$
0
0
Miti ya Mibuyu iliyochimbwa na Tembo ni moja vivutio katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Uoto wa asili katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ni kivuto kingine.
Mkundi ya Tembo ni sehemu pia ya vivutio vinavyo ibeba Hifadhi ya Taifa ya Tarangire,
Ndege wa aina mbalimbali pia wanaweka mvuto katika Hifadhi hiyo
Mnyama Ngiri ni miongoni mwa wanayama wanaoonekana kwa urahisi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Muonekano wa Mibuyu iliyochimbwa na Tembo.
Tumbili pia wamo.
Sehemu ya Chanzo cha Mto Tarangire.
Mnyama Kuro pia ni kivutio kimoja wapo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Kundi la Tembo likivuka mmoja wa mito iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Maandhari ya uoto wa asili unavyoonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WACHAGA WAKUMBUSHWA KUISAPOTI TIMU YAO YA KILIMANJARO INAYOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akizungumza wakati wa kuwaaga mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro, timu ya Kitayosce wanaojiandaa kuelekea mkoani Singida kushiriki ligi ya Mabingwa wa mikoa katika kituo hicho.
Baadhi ya wachezaji timu ya Kitayosce wakiwa katika uwanja wa Meimoria ambako waliagwa na uongozi wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)
Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Mohamed Musa akizungumza wakati wa kuiga timu ya Kitaysce.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kitayosce.
Mjumbe wa kamati ya kuisadia timu ya Kitayosce,Dalabu Maulid Dalabu akizungumza katika hafla hiyo fupi.

Mwenyekiti wa Chama cha soka Manispaa ya Moshi (MMFA) Japhet Mpande akitoa nasaha zake kwa wacheaji wa timu ya Kitayosce wakati wa kuiaga timu hiyo.
Kocha wa timu ya Kitayosce,Hamad Haule akielezea matarajio yao katika ligi ya mabingwa ambapo timu yake imepangwa kituo cha Singida.
Nahodha wa timu ya soka ya Kitaysce ,Chimko Vidic akieleza namna walivyojiandaa na ligi hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Godluck Mosha akimkabidhi Mweka hazina wa timu ya Kitaysce ,Festus nauli kwa ajili ya safari ya kuelekea Singida ,KRFA imetoa nauli ya kwenda Sindida na kurudi.
Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akikabidhi mpira kwa ajili ya timu ya Kitayosce.
Mwenyekiti Mosha akikabidhi kiasi cha Sh Laki moja kwa nahodha wa timu ya Kitayosce kwa ajili ya kunua viatu kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.
Wachezaji wa Kitayosce wakiagana na Viongozi wa KRFA katika uwanja wa Meimoria. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro,Timu ya Kitayosce inataraji kuondoka jumapili hii kuelekea Singida huku ikikabiliwa na ukata .

Kamati ya kuisadia timu hiyo imeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali wa soka hasa wale ambao ni wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kuisadia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuuwakilisha vyema mkoa wa Kilimanjaro.

Hata hivyo kamati inatoa pongezi kwa Kampuni inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA(KADCO) kwa msaada wa awali iliyotoa huku ikiwakumbusha wadau wengine waliofikishiwa barua za ombi la msaada kwa timu hiyo kuzifanyia kazi.

Kwa sasa kamati ya kuisadia timu hiyo inakusanya michango kupitia namba za simu 0715331274 na 0746331274.

MUFTI WA TANZANIA ALAANI KITENDO CHA MAUAJI YALIYOTOKEA MKOANI MWANZA.

$
0
0
 Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir (Mwenye kofia Nyeupe katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

SHEKHE Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir pamoja amelaani vikali tukio la kinyama lililotokea Mei 17 mwaka huu katika Msikiti wa Ibanda Mkolani, Masjid Rahmaan mkoani Mwanza. 

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa  kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na hakivumiliki.

Tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu na kusababisha mauaji ya waumini watatu wa Msikiti wa Ibanda Mkolani waliokuwa katika Ibada  miongoni mwao akiwa ni Imam wa Msikiti huo ikiwa na wengine kujeruhiwa.

"Kwaniaba ya Baraza kuu la Waislam wa Tanzania(Bakwata) tunalaani vikali tukio hili pamoja na kuwataka Waislam wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu" Amesema Shekhe Zuberi.

Amewaomba Waislam na wananchi kwa ujumla kuvipa ushirikiano wa hali na mali vyombo vya usalam ili hatimae kuwapata waharifu hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria.



Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, na kulaani kitendo cha mauaji ya watu wasio na hatia katika Msikiti huko Mkoani Mwanza. Kulia ni Msaidizi katika ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe, Ally Khamisi Ngeruko. na Kushoto ni Shekhe, Abuubakari Kharid.
Baadhi ya waamini wa dini ya Kiislamu pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images