Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

TFF yatakiwa kusimamia ligi kwa ustadi-Meya wa Jiji la Dar

$
0
0
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Issaya Mwita ameiomba shirikisho la Michezo wa mpira wa miguu nchini (TFF) kuendelea kusimamia ligi kwa ustadi kulingana na ratibu na taratibu za mpira wa miguu kama zililivyoanishwa na Shirikisho la Soka Duniani( FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF).

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa Mstahiki Meya huyo inasema kuwa TFF inatakiwa kusimamia ligi hiyo ili kuainisha, kubainisha, kutajirisha na hatimae kutatua changamoto husika na kuwa na kiwango stahiki katika msimu unaofuata ukilinganisha na changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita.

Aidha, ameipongeza klabu ya Yanga Africans Football Club kwa kunyakua ubingwa wa Tanzania bara kwa mara ya ishirini na sita(26) tangu kuanzisha kwa mashindano ya ligi kuu Tanzania yajulikanayo kama Vodacom Premier League.

Alifafanua kuwa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam inaiomba klabu hiyo kuthamini ubingwa wao kwa kuonyesha viwango vya kimataifa ili kufanya jiji kuwa chuo cha mafunzo ya michezo wa mpira miguu, bila kuridhika na kiwango walichonacho.

Mbali na hayo alitoa wito kwa wadau wa mchezo wa  mpira wa miguu kushirikiana ipasavyo ili kufanya ligi ya Tanzania iwe miongoni mwa ligi bora Barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Serikali za Vijiji zakumbushwa kusimamia Sheria ya Ardhi.

$
0
0

Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

SERIKALI za Vijiji nchini zimekumbushwa kusimamia vizuri Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999 ambayo imeweka utaratibu wa kufuata kwa mtu anayehitaji kupata ardhi kwa matumizi mbalimbali.

Agizo hilo limetolewa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Chemba, Mhe. Juma Nkamia ambaye alitaka kujua utayari wa Serikali wa kufuta uamuzi uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara wa kuwazuia wakulima ili kuondoa mgogoro wa muda mrefu.

Mhe. Jafo ameeleza kuwa, tamko lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara liliwahusu wakulima waliokuwa wavamizi katika eneo la hifadhi ya Wanyamapori ya Makame kutoka katika Wilaya za Kiteto, Babati, Chemba, Kondoa na Mkoa wa Iringa waliokuwa wanaendesha shughuli za kilimoi katioka hifadhi hiyo kinyume cha Sheria.

Amefafanua kuwa, uamuzi huo ulitolewa kufuatia azimio la kikao cha pamoja cha Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya za Kiteto cha Chemba kilichokaa tarehe 12 Novemba, 2015.

“Kikao hicho kilishirikisha viongozi wa Vijiji vitano vinavyounda Mamlaka ya Hifadhi (WMA) ambavyo ni Ngobolo, Katikati, Ndedo, Irkiushbor na Makame pamoja na wawakilishi wa wakulima 10 kutoka kila Wilaya”, alisema Mhe. Jafo.

Aidha, kwa mujibu wa Sheria, hairuhusu shughuli yoyote ya kibinadamu ikiwemo kilimo, ufugaji au makazi kuendeshwa katika hifadhi.

“Naomba kutoa wito kwa wananchi kuzingatia Sheria za nchi ili kuepuka migogoro katika jamii, Serikali za vijiji zinakumbushwa kusimamia vizuri Sheria ya Ardhi Na. 5 ya mwaka 1999 ambayo imeweka utaratibu wa kufuata kwa mtu anayehitaji kupata ardhi kwa matumizi mbalimbali, lengo ni kuzuia migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima ambayo kwa sehemu kubwa inatokana na kutozingatiwa kwa Sheria za ardhi”, alisema Mhe. Jafo. 

WAFANYABIASHARA WA MADINI WALALAMIKIA KUZALILISHWA

$
0
0
 

Na Woinde Shizza ,Arusha 

Chama cha  wanunuzi na wauzaji wa Madini Tanzania TAMIDA kimetoa tamko la kulaani  kitendo cha uongozi wa  Haliamshauri ya Simanjiro  kuwavamia wafanyabiashara wa madini  wa jijini Arusha maofisini wakiwa wameambatana na Askari wenye silaha za moto na pingu  kuwalazimisha kulipa  kodi ya tozo ya huduma ya Madini.

Akitoa tamko hilo katika mkutano wa wafanya biashara wa Madini uliofanyika katika Ofisi za wizara ya madini Kanda ya Kaskazini jijini hapa  Makamu  mwenyekiti wa TAMIDA Thomas Munis alisema kitendo hicho hakikubaliki na kimelenga kuwadhalisha wafanyabiashara hao pamoja na wateja wao.

Thomas aliutaka uongozi wa Wilaya ya Simanjiro kukaa chini na kukubaliana  namna ya ulipaji wa tozo hiyo inayofikia kiasi cha shilingi Milioni 20 hadi 60 kwa mwaka, jambo ambalo alisema hawawezi kulipa mara mbili kwa halimashauri ya Arusha pamoja na Halimashauri ya Simanjioro.

"Sisi kama wafanyabiashara hatupingi kulipa kodi yoyote ya madini ili tunacho sikitishwa nacho ni hatua ya uongozi wa Simanjiro kutufuata maofisini wakiwa na silaha za moto na pingu, kutaka tulipe kodi Huduma ambayo kimsingi tumekuwa tukilipa kila mwaka katika halimashauri ya Arusha", Alisema Thomas.

Aidha aliongozea kusema kuwa wao kama wafanyabiashara wa madini hawapingi kulipa kodi yoyote inayotozwa kutokana na biashara ya madini ila wanachopinga kodi hiyo kutozwa mara mbili kwa mwaka katika halimashauri zote swala ambalo wameliomba serekli kupitia wizara ya madini kuingilia kati swala hilo na kutatua mkanganyiko huo.

Wakati huo afisa madini kutoka ofisi hiyo ya kanda Bwana Erick Mpesa amesema kuwa wao kama  kama wasimamizi wa madini katika kanda hii wana ngoja mafikiano ya pande zote mbili ikiwemo halimashauri ya Simanjiro pamoja na jiji la Arusha juu ya Tozo hiyo ya huduma ya Madini.

Kwa upande  mwanasheria Jiji la Arusha  Bahati chojo amesema kuwa sheria inaelekeza wazi kuwa  kampuni yoyote inayofanya bishara ya madini inapaswa kulipa tozo ya huduma kule ilipo ikiwemo kulipa kule ilipo ofisi pamoja na maeneo ya matawi ya ofisi hizo.

MKUTANO WA WAMILIKI WA MAGAZETI NA MSAJILI WA MAGAZETI.

ZAIDI YA TANI 70 ZA SUKARI ZILIZOSALIMISHWA NA WAFANYABISHARA WAKUBWA ARUSHA ZAGAWIWA KWA WANANCHI KWA BEI NAFUU

$
0
0


Na Woinde Shizza,Arusha 

Jumla ya tani 78 za sukari ambazo zilisalimishwa na baadhi ya wafanya biashara wa kubwa wa sukari katika jiji la Arusha zimegaiwa kwa wananchi wa wilaya ya Arusha mjini ambao walikuwa wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa sukari .

Sukari hiyo ambayo ilisalimishwa na wafanyabiashara wakubwa ambao ni Neema Investment imegaiwa katika jumla ya kata 25 zilizopo katika wilaya ya Arusha mjini huku kila kata ikiwa inapatiwa mifuko 1000 kwa ajili ya wananchi wake .

Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arusha ,Afisa tarafa wa kata ya Suye Felician Mtahengerwa alisema kuwa sukari sukari hiyo inayogaiwa kwa wananchi ni ile ambayo iliingizwa hapa mkoani na baadhi ya wafanya biashara wakubwa na kuisalimisha katika ofisi ya mkuuwa mkoa kama agizo lilivyotolewa .

Alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha alisema kuwa mfanya biashara yeyote wa sukari ambaye anaingiza sukari mkoani hapa anapaswa kutoa taarifa katika ofisi yake kabla ya kufanya kitu chochote ikiwemo kabla ya kuuza sukari hiyo ivyo wafanyabishara hawa waliisalimisha sukari hiyo na ndio ambayo inagaiwa kwa kufuata utaratibu.

Alisema awali walishagawa sukari tani 45 na sasa ivi wanagawa tani zingine 33 ambazo zimetoka kwa mfanyabishara Neema intaprasesi ambayo yeye aliingiza sukari hii mara baada ya serekali kutoa agizo hivyo aliamua kuisalimisha kwa kutoa taarifa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na sasa ivi ndio wameigawa .

“kunautaratibu wa wafanyabishara wakubwa wanapoingiza sukar I tu hapa mkoani kutoa taarifa sehemu husika ili sukari ile iweze kugaiwa kwa kufuata utaratibu hivyo huyu alitoa taarifa na ndio maana tumekuja hapa kuungana nae kuakikisha kila kata inapata sukari mifuko 1000 ambayo itauzwa kwa bei halili ya serekali ambayo imeelekezwa”alisema Mtahengerwa.

Alisema kuwa utaratibu huu unaotumika wa kugawa sukari utaendelea hivi hivi na hata sukari ambayo imeagizwa na waziri mkuu iwapo itafika utaratibu huu huu ndio utatumika adi pale tatizo la sukari litakapo malizika kabisa

Alitoa wito kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wanaingiza sukari kutoa taarifa katika ofisi husika kwani wakiingiza bila kutoa taarifa iwapo wakibainika watachukuliwa hatua ya kisheria ikiwa ni pamoja na kutaifishiwa sukari yote.

Aidha pia aliwataka wafanya bishara wadogo wadogo ambao wamepata sukari hiyo kuuza kwakufuata bei elekezi kwani wanapokiuka agizo hilo iwapo watabainika wameuza kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi sheria kali watachukuliwa ikiwemo ya kuwapeleka mahakamani.

Kwa upande wake mfanyabishara mkuu ambaye alijitambulisha kwa jina la Romanusi Mwacha alisema kuwa yeye kama mfanyabishara mkubwa ameamua kumuunga Rais Magufuli mkono kwa kuanza kuuza sukari kwa bei elekezi japo kuwa amepata hasara kubwa.

Alisema kuwa kama yeye amenunua sukari shilingi 1900 kilo na bado ajaweka bei ya usafiri kutoka aliponunua dar adi hapa lakini kutokana na agizo la serekali ameamua kulifuata na kumuunga magufuli mkono na ndio maana pamoja yakuwa amenunua bei gali lakini anauza bei raisi kwa kilo shilingi 1700 ili mfanyabiashara mdogo anaenunua aweze kwenda kumuuzia mlaji bei ya shilingi 1800 kama serekali ilivyoelekeza.

Aliwasihi wafanyabishara wengine ambao wameficha sukari wazitoe na wale ambao wanauza katika maduka ya reja reja wauze bei elikezi ili kutoweza kumuumiza mlaji ambaye ni mwananchi .

UTATA KABURI LA SHEIKH SHAABAN ROBERT KUSHUGHULIKIWA HARAKA

$
0
0
Shaka akiwa na ujumbe wake waliozuru katika kaburi la mwandishi gwiji wa vitabu vya fasihi andishi na simulizi hayati Sheikh Shaaban Robert huku mjinimwema mkoani Tanga 


Na Woinde Shizza,Tanga.

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM) umesema utaieleza serikali mkoani Tanga kuondosha utata na mivutano iliopo katika kijiji cha mji mwema kati ya familia mbili husika mahali ambako amezikwa mwandishi bingwa wa vitabu vya fasihi simulizi na andishi Marehemu Sheikh Shaaban Robert. 

Tamko hilo limetamkwa na Kaimu katibu Mkuu wa Uvccm Shaka Hamdu Shaka aliyefika katika kaburi la Mwandishi huyo galacha Afrika mashariki aliyezaliwa mwaka na kufariki mwaka 1962 .

Shaka mara baada ya kusafisha kaburi la marehemu na kuomba duwa akiwa na ujumbe wake alielezea na mjukuu wa marehemu Khatib Mwinjovu kwanba mahali hapo qlipozikwa sheikh Robert pamekuwa na mivutano isio na ulazima toka upande wa familia ya mke wa marehemu Robert.Alisema kaburi hilo ni alama kuu katika Taifa letu hivyo halipaswi kuandamwa kwa mivutano au misuguano isio na sababu na kuahidi kwamba seeikali itatumia uwezo wake kuleta mapatano haraka. 

"Nitaongea haraka na mkuu wa mkoa wa Tanga kuhusu utata huu, uvccm ingependa kuona kaburi la mwandishi huyo bingwa anayetajika duniani linatunzwa kwa heshima zote , ametumia maisha yake yote kuandika ili kuvielimisha vizazi na vizazi hadi sasa.Aidha shaka aliitaka jamii kutambua na kuhshimu nguvu alizozitumia marehemu sahaaban katika uhai wake ambazo sasa alisema zinafaa katkka kizazi hadi kingine wakati yeye akiwa hana tija wala faida.

Kwa upande wake katibu wa ccm mkoa wa Tanga Shija Othman Shija alisema uamuzi wa UVVCM kuja kulizuru kaburi hilo ni tendo la kiungwana hivyo akatoa wito kwa jumuiya nyingine nazo kuiga mfano huo. Shija alisema ni jambo lisilowezekana kuzungumzia nchi yetu kabla na hata baada ya uhuru bila kulitaja jina la marehemu Shaaban Robert kutokana na mchango wake mkubwa hasa katika mitaala ya elimu na ukuzaji lugha ya kiswahili. 

"Robert amekuwa nguzo na kioo ambacho hakutavunjika wala kuingia nyufa wakati wote, maandiko yake yatabaki katika kurasa muhimu toka kizazi kimoja hadi kingine "alisems katibu huyo wa ccm mkoa.

TIKETI ZA TRENI KUNUNULIWA KWA NJIA YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

$
0
0
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inatarajia kuanza kutoa huduma ya uuzaji wa tiketi kwa abiria wanaotumia usafiri wa treni kwa mfumo wa kielektroniki lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kuweza kurahisha ununuaji wa tiketi hizo na kupunguza usumbufu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la nyongeza lililoihusu Wizara yake ambapo ametaja maeneo ambayo mfumo huo utaanza kufanya kazi ni pamoja na Mpanda mpaka Tabora, Kigoma mpaka Tabora.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Sabreen Hamza lililotaka kujua kwanini TRL isianzishe mfumo wa uwakala wa tiketi ili kupunguza adha wanayoipata wakazi alisema kuwa kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri wa treni katika Mikoa ya Kigoma, uuzaji wa tiketi katika Stesheni ya Reli Kigoma umekuwa na changamoto kubwa kutokana na ulanguzi wa tiketi.

Amefafanua kuwa, ili kudhibiti ulanguzi huo, Kampuni ya Reli Tanzania iliamua kubadilisha utaratibu kwa kuuza tiketi siku za safari na kwa kutumia vitambulisho jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ulanguzi wa tiketi hizo.

Ameongeza kuwa, utaratibu huo umekuwa na changamoto zake kwa kusababisha wasafiri kulala stesheni au kuwalazimu kuamka alfajiri ili kuwahi tiketi hizo.

"Ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili si kuanzisha mfumo wa uwakala ambao utaiongezea TRL gharama za uendeshaji, tatizo kubwa lililopo ni idadi ndogo ya safari za .treni ambapo huduma inayotolewa hivi sasa haikidhi mahitaji halisi ya wananchi na hivyo kuwa na uhaba wa tiketi kwa abiria", alisema Mhe. Ngonyani.
Aliongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inatarajia kuongeza idadi ya treni za abiria kwa njia ya Kigoma ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa Mkoa huo

DKT. MENGI ATOA DARASA KWA WASHIRIKI WA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA

$
0
0
Mwenyekiti Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani) katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016.
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama chuoni hapo.
 
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
.(Picha zote na Modewjiblog). 
 

IMELEZWA jukumu la ulinzi na usalama kwa dunia ya sasa halimo kwenye mikono ya polisi na wanajeshi pekee bali ni la kila mtu katika nafasi aliyopo kama amani na demokrasia inatakiwa kuendelea kuwapo.Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed wakati akizungumza na Modewjiblog ofisini kwake baada ya mhadhahara ulioshirikisha wataalamu wa masuala ya habari kutoka sekta binafsi na umma ambao wanachukua kozi ya mbinu za usalama chuoni hapo.

“Zamani mambo ya usalama yalikuwa ya wanajeshi na Polisi lakini kwasasa mambo ni tofauti, kila mmoja anatakiwa kuhakikisha anakuwa mlinzi ili uwepo usalama wa kutosha kwahiyo tunaamini washiriki wakirudi vituoni kwao watazingatia usalama.

“Wote wanaokuja hapa wanakuwa ni viongozi au viongozi watarajiwa na kama sasa tuna wanafunzi 38, 12 sio Watanzania ni kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Nigeria na China,” aliongeza Meja Jenerali Mohamed.

Wataalamu walioendesha mihadhara hiyo ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi ambaye amepata nafasi ya kutoa elimu kuhusu habari kwa sekta binafsi na Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) na mwanazuoni Dk. Ayoub Rioba ambaye aliwasilisha sekta ya umma.

Akielezea ujio wa Dk. Mengi chuoni hapo, alisema wamekuwa na taratibu wa kukaribisha watu mbalimbali ambao wanawaona wana uwezo wa kuelezea uzoefu wao katika mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na faida kwa washirika.Alisema chuo chao kimekuwa hakina walimu wa kudumu hivyo pamoja na kutumia watu mbalimbali kama walivyofanya kwa Dk. Mengi pia wamekuwa wakiwatumia walimu wa vyuo vikuu ili kutoa elimu ambayo itawasaidia washiriki katika masomo yao ambayo wanayapata chuoni hapo.

“Chuo chetu hakina walimu wa moja kwa moja kwahiyo huwa tunatumia walimu kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini lakini pia huwa tunakaribisha watu maarufu wanakuja ku’share’ uwezo wao kwa washiriki ambao wanakuwa wapo masomoni.“Dk. Mengi ameshafika hapa chuoni mara tatu na sio mtu wa kwanza kuja alishakuja Pius Msekwa, Mawaziri, Katibu Mkuu kiongozi na hata jana tulikuwa na (Dkt. Ayoub) Rioba,” alisema Meja Jenerali Mohamed.

TANZANIA OFFICIAL MAP

RUSHWA YA NGONO HUCHANGIA KURUDISHA NYUMA KASI YA MAENDELEO

$
0
0
Mratibu wa Asasi ya kuinua maendeleo ya Jamii na Kuhifadhi Mazingira (Ececo)Ndosho Hamisi akisisitiza jambo wakati akitoa mada juu ya madhara ya rushwa ya ngono iliyofanyika kijiji cha Duga wilayani Mkinga iliyokuwa na lengo la kuwapa uelewa jamii ya wasichana wa wafuigaji wa kimasaia iliyofanyika.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Duga Maforoni wakifuatilia mada mbalimbalio zilizokuwa zikiwasilishwa.

Katibu wa Asasi ya Kuinua Jamii na Kuhifadhi Mazingira (ECECO TANZANIA),Said Kamba akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina hiyo .

Diwani wa Kata ya Duga Maforoni Ally Ally akizungumza katika semina hiyo

IMEELEZWA kuwa rushwa ya ngono imekuwa ni tishio hapa nchini hali inayochangia kurudisha nyuma kasi ya maendeleo kwani imekuwa ikipunguza demokrasia na utawala bora kwa watanzania jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa vitendo.

Hayo yalisemwa juzi na Mratibu wa Asasi ya Kuinua Maendeleo ya Jamii na Kuhifadhi Mazingira (Ececo), Ndosho Hamisi wakati wa semina ya rushwa ya ngono iliyofanyika Kijiji cha Maforoni Kata ya Duga wilayani hapa na kufadhiliwa na Women Fund Tanzania (WTF)iliyokuwa na lengo la kuwapa uelewa juu mambo hayo kwa wasichana na wanawake hasa wa jamii ya wafugaji wa kimasai.

Alisema kuwa tatizo hilo limekuwa likichukua kasi kwenye sekta nyingi na kusababisha kukandamiza haki za wanaostahili kuweza kupata fursa za kuweza kupata nafasi za kukuza uchumi wao na hivyo wengi wao kuishia katika hali duni.

“Ukiangalia leo hii unaweza kutaka kitu Fulani mahali lakini kwa sababu hauna sifa ambazo zinapaswa kukipata basi yanaweza kutumika mazingira ambayo sio sahihi ili uweze kukipata kutokana na kumtimizia mahitaji yake mlengwa na hili limekuwa tatizo kubwa “Alisema.

“Ni kosa kisheria mtu mwenye mamlaka kumpandisha cheo mfanyakazi wake kutokana na kuwepo kwa mazingira ya rushwa ya ngono kwa sababu inasababisha kupunguza ufanisi kazini na hivyo kushindwa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo “Alisema.

Alisema jambo hilo limekuwa na madhara mengi kwa jamii ikiwemo kupata magonjwa makubwa ikiwemo ukimwi lakini pia uzalilishaji kitendo ambacho kinapelekea kushusha utendaji na kuchangia kurudisha nyuma maendeleo.

Awali akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Diwani wa Kata ya Duga, Ally Mohamed aliipongeza asasi hiyo kwa kuona umuhimu kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataweza kuwapa uelewa juu ya madhara ya rushwa ya ngono na kubadilika 

“Unaweza kukuta wakati mwengine watoto wadogo wanazalilika kutokana na kutokujua madhara ya rushwa ya ngono hivyo semina hii itawafungua macho kuona namna ya kuweza kupiga vita vitendo hivyo “Alisema.
 

KITUO CHA KISASA CHA TIBA ASILI, MIZANI HERBAL CHAZINDULIWA SINZA PALESTINA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji na Tabibu mkuu wa Mizani Herbal and Natural Therapies, Bw. Abalhassan Jumar(kulia), akiwa na wasaidizi wake kwenye kliniki hiyo mpya ya tiba asili iliyoko Sinza-Palestina jijini Dar es Salaam.
 NA K-VIS MEDIA
KITUO kipya na cha kisasa cha tiba asili, MIZANI herbal and Natural Therapies kimefunguliwa Sinza Palestina jijini Dar es Salaam.Akizungumza na K-VIS MEDIA jijini Dar es Salaam, Mei 10, 2016, Mkurugenzi  Mtendaji wa kituo hicho Bw. Abalhassan Jumar, amesema kuwa, kliniki yake  inaendesha tiba  asili kwa kutumia sawa zitokanazo na mimea na matunda na kwamba wanatoa matibabu ya aina mbalimbali.

Alitaja baadhi ya magonjwa yanayotibiwa kwenye kituo hicho  ni pamoja na maumivu ya tumbo, kichwa, ganzi katika mwili, kuwashwa mwili, michirizi ya mishipa ya damu katika mwili hususan akina mama, upungufu wa nguvu za mwili na kuongeza hisia mbalimbali katika mwili, tiba  bora ya matatizo ya uzazi kwa mlengwa.
"Pamoja na kutoa tiba kwa kutumia dawa zitokanazo na mimea na matunda lakini pia tunatoa ushauri kwa wale wenye matatizo mbalimbali mwilini." Alisema Bw.Abalhasan.Katika kuhakikisha wagonjwa wanaofika kwenye kituo hicho wanapata huduma katika mazingira bora na ya kisasa, kituo kina ukumbi wa kupumzika watu wanaofika kupata huduma ambapo ofisi  zina viyoyozi na huduma nyingine. Alisema Abalhassan ambaye pia ndiye tabibu mkuu.
Akifafanua zaidi mkurugenzi huyo wa Mizani Herbal and Natural Therapies Ltd alisema, katika kuonyesha mgonjwa anasikilizwa zaidi maelezo yake, ubora na uimarikàji wa afya ya muhusika yatazingatiwa kwanza  kabla mtaalamu wa Mizani  hajaanza kutoa maelezo  yake. Alifafanua Mkurugenzi  huyo.
 Dawa zitokanazo na mines zikiwa kwenye vifungashio

 Tabibu mkuu, Abalhassan akiwa ofisini kwake.

Dkt. Kigwangalla awataka wanafunzi kupenda kusoma masomo ya Sayansi nchini.

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana Mku wa shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Sister Evetha Kilamba wakati wa kuwasili katika eneo la Mahafali ya 19 ya kidato cha Sita ya shule ya St. Mary's Mazinde Juu, Lushoto Tanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea hutuba ya wanafunzi hao wa kidato cha sita.
 (Picha zote na Andrew Chale.Lushoto Tanga).
Baadhi ya wanafunzi wa waliohitimu kidato cha Sita katika Mahafali ya 19 ya Shule ya Wasichana ya St. Marys Mazinde Juu wakiwa katika mahafrali hayo.

Wanafunzi Nchini hususani wale wa wa kike wameshahuriwa kujikita zaidia katika kupenda masomo ya Sayansi kwa bidii zote ili kuifanya Tanzania kufikia kwa haraka malengo yake ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Hii ni pamoja na Ukuaji wa viwanda vya ndani ambavyo vingi vitategemea ujuzi wa Sayansi na teknolojia.


Rai hiyo ametolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa mgeni rasmi wa Mahafali ya 19 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekodari ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Shule hiyo ambayo ni ya Wasichana watupu, jumla ya wanafunzi 136 wanaomaliza kidato cha sita walitunukiwa vyeti vyao vya kumaliza shule.




SERIKALI KUWAWEZESHA WANANCHI KUPATA TAARIFA NA HUDUMA MBALIMBALI KUPITIA SIMU ZAO.

$
0
0
 Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
17/5/2016.

SERIKALI kupitia wakala ya Serikali mtandao imesema kuwa inaendelea kulifanyia kazi suala la uanzishaji wa mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wananchi kupata huduma na taarifa mbalimbali za Serikali kupitia simu zao mkononi mahali popote walipo kwa njia ya mtandao.

Utaratibu huo pia utawawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali vya elimu nchini Tanzania kupata taarifa za ajira za Serikali na kuwawezesha kuomba nafasi hizo, kufuatilia majibu ya usaili walioufanya na kupata taarifa za kuitwa kazini kupitia namba za utambulisho watakazopewa kupitia ujumbe mfupi (sms).

Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari amesema kuwa   mfumo huo utamuwezesha mwananchi kupata huduma za Serikali mahali popote alipo kufuatia mifumo ya TEHAMA kuwasiliana na kubadilishana taarifa.

Amesema kuwa dhana ya Serikali Mtandao  ni kuwa na matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli zote za Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji kwenye huduma za Afya, Utalii, Malipo ya tozo za huduma,vibali, leseni ,elimu na huduma mbalimbali za Serikali.

Dkt. Jabiri amesema  moja ya vitu vinavyosababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na kukosekana kwa Serikali mtandao ni pale wanapohitaji kupata huduma za Serikali ikiwemo Hati ya kusafiria ambapo hulazimika kwenda Idara ya Uhamiaji kujaza fomu maalum na kisha kusubiri kwa muda wa zaidi ya wiki moja ili taarifa zao ziweze kuhakikiwa na taasisi nyingine za Serikali wakati suala hilo lingeweza kuchukua siku moja.

“Matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli za Serikali hurahisiaha sana upatikanaji wa taarifa  kwa kuwa mifumo inawasiliana na kubadilishana taarifa haimlazimu mwananchi kwenda kwenye taasisi zaidi ya tano kupata huduma yake” Amesisitiza Dkt. Jabiri.

Amesema taasisi za Serikali kama Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, RITA na taasisi nyingine ambazo majukumu yao hutegemeana kupitia serikali mtandaomifumo ya taasisi hizo huunganishwa ili ifanye kazi pamoja kwa lengo la kuruhusu mifumo kuzungumza  kumuhudumia mwanachi bila yeye kulazimia kuzifuata taasisi hizo.

Amesema kuwa pamoja na maboresho mbalimbali yanayoendelea ndani ya Serikali ya  kujenga Serikali mtandao imara mfumo uliopo sasa kwenye baadhi ya taasisi humfanya mwananchi achukue muda mrefu kupata huduma.

Ameeleza kuwa taasisi za Serikali zinazofanya kazi katika mazingira yanayofanana zinaposhirikiana katika kutoa huduma Kupitia Serikali mtandao mwananchi wa kawaida hatajua nini kinaendelea, atakachokipata mwisho ni majibu ya huduma aliyoiomba kama ni  Bandarini atachukua mzigo bila usumbufu wowote kwa kuwa suala la kodi, upakuaji na upakiaji wa mizigo na ukaguzi halitamgusa mwananchi.

Ameongeza kuwa ili Serikali mtandao iweze kufanya kazi yake ipasavyo nchini lazima kuwe na miundombinu ndani ya taasisi au nje pia uwepo wa mifumo Tumizi ( Application Systems) inayoshughulikia masuala mbalimbali, wafanyakazi pamoja na Sera, miongozo na taratibu za kusimamia TEHAMA  kuwezesha huduma mtandao ( e - Servieces).



Dkt. Jabiri amesisitiza Tanzania iko kwenye hatua ya kwanza na ya pili, kwa maana ya taasisi nyingi za Serikali zina tovuti zenye taarifa za awali za kumsaidia mtu kujua nini kinapatikana au kutolewa na taasisi za serikali ili aweze kuchukua hatua ya kupata huduma.

Amesema Wakala ya Serikali mtandao imefanikiwa kuweka mifumo kwa maana ya Tovuti kuu ya Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe ya Serikali (GMS) ambayo sasa inatumiwa na jumla ya taasisi 117 za Serikali na Balozi mbalimbali kwa lengo kuepuka matumizi ya barua pepe za muda.

Amebainisha kuwa Wakala ya Serikali Mtandao kwa sasa eGA katika awamu ya kwanza imeziuganisha taasisi 75 za serikali na Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa, pia Wakala imeziunganisha Taasisi 72 zilizounganishwa kwa simu zinazotumia itifaki ya Intaneti kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.

Akijibu Suala la baadhi ya Taasisi za serikali kukawia kuunganishwa kwenye mtandao amesema kuwa awali hakukuwa na mfumo huo kutokana na baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia utendaji wa shughuli za kila siku serikali lakini sasa kuna mwongozo wa taasisi kuzingatia ili kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali inawasiliana ili kufanya kazi pamoja kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.

Aidha, mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda mfupi.

 Kwa upande wake Meneja Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto amesema kuwa suala la matumizi ya mitandao mbalimbali isiyo rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza kwamba utaratibu unaandali wa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30.

Kwa sasa ni taasisi 72 tu za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na taasisi zimeunganishw, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo wa taifa na kazi ya kuzifikia taasisi zote 500 inaendelea ili kuwezesha zoezi la kufunga huduma za mawasiliano za serikali nje ya mkongo wa taifa.

Takribani taasisi 200 za umma zina tovuti ili kurahisisha upatikanaji wataarifa na huduma kwa wananchi. Changamoto iliyopo ni Tovuti nyingi kukosa taarifa zilizohuishwa pia kuunganisha maeneo ambayo bado hayajafikiwa hasa Halmashsuri na vijiji ili kuwezesha taarifa mbalimbali kupatikana kwa wakati.
  
Wakala imepata mafanikio katika utekelezaji wa jitihada za Serikali mtandao hasa katika uwekaji wa mifumo ya Serikali kwa maana ya Tovuti kuu ya Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe za Serikali ambayo sasa ina taasisi 117 na Balozi mbalimbali zinatumia GMS ili kuepuka matumizi ya barua pepe za muda.

Wakala ya Serikali Mtandao katika awamu ya kwanza imeunganisha taasisi 72 za serikali na Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa pia imeziunganisha taasisi hizo na simu zinazotumia itifaki ya intaneti kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.

Akifafanua kuhusu hatua ya mifumo ya serikali kuchelewa kufanya kazi pamoja amesema hapo awali hakukuwa na mfumo uliowezesha jambo hilo kufanyika kutokana na  baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia masuala ya TEHAMA nchini lakini sasa kuna mwongozo uliotolewa kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali inawasiliana  na kufanya kazi pamoja ili  kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.

Aidha, mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda mfupi.

Meneja Habari, Mawasiliano Suzan Mshekangoto amesema suala la matumizi ya mitandao mbalimbali isiyo rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza kwamba utaratibu unaandaliwa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30 alasiri.

Amefafanua kuwa taasisi 72 za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na Mahakama zimeunganishwa, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo wa taifa na kazi ya kuzifikia zilizobaki inaendelea ili kuwezesha mawasiliano ya serikali kupita kwenye mkongo wa taifa.

Bi. Suzan amesema mpaka sasa takribani taasisi 200 za umma zina tovuti zenye taarifa za huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali huku  Changamoto iliyopo ni baadhi ya Tovuti hizo kukosa taarifa zilizohuishwa. 

SERIKALI YASHIRIKISHA VIJANA KUJADILI AFYA YA UZAZI NA VVU/UKIMWI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya vijana na wadau wa vijana akifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi akizungumza na vijana na wadau wa vijana (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
Vijana wanaoishi kwa matumaini wakitoa nasaha kwa vijana wengine jinsi ya kujitunza na kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Kilimanjaro marathoni changia dola elfu tano kuondoa unyanyapaa, maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na vifo vitokanavyo na ukimwi Bw. Mrisho Mpoto akiteta jambo na vijana jinsi ya kupambana na VVU leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi na vijana walioshiriki katika mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana kujadili masuala mbalimbali ya vijana leo jijini Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo.

Na: Genofeva Matemu – Maelezo

Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa vijana wote nchini wanashirikishwa kikamilifu na kupatiwa huduma zinazotakiwa ili kumaliza uwepo wa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi, kupunguza ubaguzi na unyanyapaa unaotokana na ukimwi pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na ukimwi kwa vijana.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dkt. Abdallah Possi alipokua akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana leo Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Possi amesema kuwa asilimia 2 ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yapo miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo ushamiri kwa vijana wa kike uko juu zaidi ya ule wa vijana wa kiume hasa katika umri wa miaka 23 hadi 24.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji Tume ya kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho amesema kuwa Tume inaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanapata kinga na huduma stahiki kupunguza utegemezi hivyo kuwafanya vijana kujiamini na kujitokeza kupambana na VVU/UKIMWI

“Vijana ni nguvu kazi ya taifa la leo, wakipatiwa nafasi ya kujitambua na kuwasilisha hisia zao utegemezi ndani yao utapungua, ni vyema vijana wakaandaliwa mazingira ambayo watakua huru kushiriki katika masuala ya VVU na UKIMWI” Alisema Bibi. Mrisho.

Aidha Bibi. Mshiro amemtaka kila kijana aliyeshiriki mkutano huo kubeba mambo muhimu manne na kuwafikishia vijana wengine kumi waliopo vijiweni, maofisini ama sehemu nyingine yeyote ile ili kuweza kusambaza elimu waliyoipata kwa kila kijana nchi nzima na kuokoa afya za vijana wenzao.

Kwa upande wake kijana anayeishi kwa matumaini Bi. Wittiness Nakanje ameiomba serikali kuanzisha kliniki maalumu za vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI ili kuwaweka vijana kuwa huru kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya VVU na UKIMWI.

Kulingana na utafiti wa viashiria vya UKIMWI kwa mwaka 2011/2012 tanzania inajumla ya vijana milioni 12 wa umri wa 10 hadi 19 ikiwa ni asilimia 24 na milioni 16 wa umri wa miaka 19 hadi 24 ikiwa ni asilimia 24 ya Watanzania wapatao milioni 44, idadi hiyo ya vijana inajumuisha wasichana wapatao 7,430,840 na wavulana 6,924,612.

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 vijana wa umri wa miaka 19 hadi 24 wako 3, 954,039 ambapo wasichana idadi yao ni 2,160,986 sawa na asilimia 55 na wavulana 1,793,053 sawa na asilimia 45.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, DKT. ASHA- ROSE MIGIRO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha – Rose Migiro kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwake jijini Dar es salaam Mei 17, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha – Rose Migiro ofisini kwake jijini Dar es salaam Mei 17, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HUAWEI IMEKUFUNGULIA DUKA JIPYA NDANI YA CITY MALL JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang, akitoa hotuba kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala akitoa hotuba kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala(kushoto) aliyekuwa mgeni rasimi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam akikata utepe wa duka hilo katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang.
Bw. Sylvester Manyara, Mkurugenzi mkuu wa mauzo na usambazaji wa Huawei Devices Tanzania (kushoto) akimuonyesha baadhi ya simu mpya za Huawei Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala aliyekuwa mgeni rasimi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang, na wa pili kulia ni Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania.
Uongozi wa kampuni ya Huawei Devices Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Bw. Sylvester Manyara, Mkurugenzi mkuu wa mauzo na usambazaji wa Huawei Devices Tanzania (kushoto) akimuonyesha baadhi ya simu mpya za Huawei Mh. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala(Kulia) aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa duka la Huawei lililopo City Mall, jijini Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Tahfif Yajizatiti kuinua Elimu

$
0
0
 Mteja akipata huduma katika duka la Tahfif lililopo katika mtaa wa Mansfield  jijini Dar es Salaam. 
 Mteja akipata huduma katika duka la Tahfif.
 Wafanyakazi wa duka la vifaa vya elimu la Tahfif wakiwa kazini.
 Baadhi ya vifaa vya elimu.
 Wafanyakazi wa duka la Tahfif wakiwa katika picha ya pamoja.


Na Maria Inviolata

“Lengo la kuuza vifaa vya shule kwa bei rahisi ni kutoa mchango wetu katika elimu kwa kuwauzia wateja wetu vifaa hivyo kwa bei nafuu ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi nchini” ni kauli ya Mkurugenzi wa duka  la vifaa vya shule na ofisini la Tahfif, Mohamed Merali.

Kwa kuthibitisha kauli yake Merali anafafanua kwa lugha ya Kiarabu neno Tahfif maana yake ni “Rahisi”. Duka hilo linajihusisha zaidi na kuuza vifaa vya shule, ofisini, vifaa vya kompyuta na vifaa vya watu wenye ulemavu wa macho.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mkurugenzi huyo anasema kuwa Tahfif ilianzishwa  kwenye miaka ya 1972 na baba yao na kukabidhi duka hilo mikononi mwa wanafamilia ili kuundeleza adhma yake ya kusaidia elimu nchini, wakisimamiwa na hayati Jargis Merali, ambaye alibuni mpango mwingine wa kudhamini burudani na michezo.

Awali duka hilo lilikuwa maeneo ya Kariakoo tu, kwa juhudi za wanafamilia hao kuenzi kauli ya baba yao ya kuchangia elimu wakafungua duka lingine katikati ya jiji maeneneo ya Posta.

Mwandishi wa makala hii alipotaka kujua siri ya kuuza vifaa vya elimu kwa bei rahisi kama haiathiri biashara hiyo au labda kuna njia nyingine  mbadala inayofidia gharama hizo, Mohamed anasema kuwa siri yao kuu ni kuuza kwa urahisi vitu vingi kwa muda mfupi na kuagiza vingine, kwani ukiuza kwa bei kubwa itakugharimu muda mrefu kumalizia bidhaa zako zilizo sokoni!  

Mkurugenzi huyo anasema kuwa ukiwa makini na faida ambayo kwa macho ya wengi inaoneka ni kidogo, lakini kwa wao ni faida inayojitosheleza kabisa.

Mwandishi alipouliza inakuwaje  baadhi ya wateja wa Tahfif wa bidhaa za jumla wanauza ghali bidhaa hizo kwenye maduka yao, Mkurugenzi huyo anatoa wito kwa wateja hao kutoongeza sana bei, kwani jambo hilo linawaumiza wazazi walio wengi kwa kushindwa kununua mahitaji ya vifaa vya shule, ingawa kibiashara faida inatakiwa ili kulipa gharama na lengo la kibiashara, lakini kwa mfanya biashara makini haitaji kuweka bei ya juu katika biashara zake, jambo hilo linawaathiri wateja wake kwa njia nyingi.

Mkurugenzi huyo anatoa wito kwa wateja wake wenye maduka ya vifaa vya shule na ofisini, kuuza vifaa hivyo kwa bei ambayo haiwaumizi wateja, lengo  kuu liwe ni pamoja na kusaidia wanafunzi ili wapate vifaa shule kwa urahisi, kwani jambo hilo litasaidia kuinua elimu nchini.

Mteja wa duka hilo wa muda mrefu ambaye hakutaka jina lake litajwe, anasema kuwa alianza kununua vifaa vya shule tangu mwanae akiwa darasa la Kwanza hadi sasa ambapo mtoto huyo yupo Kidato cha Tatu, mteja huyo anatoa shukrani kwa duka hilo kwa kuuza vifaa hivyo kwa bei nafuu  na jirani yake aliyemuelekeza ilipo Tahfif, naye mteja mwingine Joseph Mwalugenge anasema kuwa  yeye ananunua vifaa hivyo dukani hapo kwa sababu mahitaji yake yote yanapatikana hapo. 

Mteja mwingine wa muda mrefu dukani hapo, anasema inambidi kutoka Kigamboni ili kukidhi mahitaji yake ya kupata vifaa hivyo.

Hivi sasa Tahfif inatoa huduma ya kuuza vifaa vya watu wenye ulemavu wa macho, kama vile Kompyuta maalum na vifaa vyote vya kisasa vinavyohitajika watu hao.

Tahfif inaagiza bidhaa zake kutoka katika nchi za China, Dubai na India, licha ya kuuza vifaa vya elimu kwa bei rahisi, Tahfif hutoa misaada mbalimbali kwa watoto na watu wenye uhitaji kama vile kwenye vituo vya kulelea watoto yatima nakadhalika.

Lengo kuu la maduka ya Tahfif ni kuendelea kutoa huduma ya kuuza vifaa vya kisasa zaidi vya Shule na  Ofisini ili kukidhi mahitaji ya Wanafunzi kwa kuinua elimu nchini, pia kutoa udhamini wa michezo na burudani kwa lengo la kuzalisha wanamichezo bora, anasema Mohamed Merali.

Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris zasaidia madawati 60 shule ya msingi Loiborsiret Wilayani Simanjiro

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, Harpreet Brar, wakiwa na moja kati ya madawati 60 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwenye shule ya msingi Loiborsiret.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, Harpreet Brar, wakifurahia jambo baada ya kampuni hiyo kugawa madawati 60 kwenye shule ya msingi Loiborsiret
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona (kushoto) akimpa mkono wa pongezi Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Lucas Mweri, baada ya kumkabidhi madawati 60 ya shule ya msingi Loiborsiret yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, Harpreet Brar.
 

Wanafunzi wa shule ya msingi Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameondokana na adha ya ukosefu wa madawati baada ya kukabidhiwa madawati 60 na kampuni za Tanzania Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris.

Hivi karibuni, wanafunzi wa shule hiyo, pia walikabidhiwa madawati 100 na  diwani wa kata hiyo ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga (Maridadi) ambaye alidhibitisha kwa vitendo adhma yake ya kuona tatizo la madawati linamalizika.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mahmoud Kambona, akizungumza jana wakati akipokea madawati hayo 60 kwa mkurugenzi wa kampuni ya Bundu Safaris na Rungwa Game Safaris, alisema huu ni wakati wa jamii ya wafugaji kupata elimu.

Kambona aliwataka wazazi wa jamii ya wafugaji wa eneo hilo kutumia fursa ya kuwepo kwa madawati hayo kwa kuwahimiza wanafunzi wasome kwa bidii ili wapate elimu bora itakayowasaidia kwa siku za usoni kwani elimu ndiyo hazina.

“Nimetembelea shule nyingi za msingi kwenye hii wilaya yangu lakini sijaona shule yenye maktaba kama yenu hivyo hongereni, ila wazazi mjitahidi kuwapa chakula wanafunzi wanaotoka mbali ili wasome vizuri,” alisema Kambona.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa kampuni hizo, Harpreet Brar alisema hiyo siyo mara ya kwanza kusaidia jamii inayozunguka eneo hilo kwani alishachangia sh10 milioni za ujenzi wa maabara na kusomesha wanafunzi wawili kila mwaka.

Brar alisema pia katika kuhakikisha anaendelea kusaidia jamii ya eneo hilo alishatoa sh500,000 za ujenzi wa choo, alitoa madawati 75 na chakula kwenye shule ya Namelock na ataendelea kushirikiana kwenye suala maendeleo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson Sipitieck alitoa wiki mbili kwa uongozi wa kata ya Loiborsiret, kuhakikisha wanajenga nyufa zilizojitokeza kwenye baadhi ya madarasa ya shule hiyo.

“Sisi jamii ya wafugaji ni matajiri mno kwani tuna mifugo mingi sasa itakuwa jambo la kushangaza kusikia eti darasa limeanguka na kusababisha matatizo kwa watoto wetu, hivyo mkarabati haya madarasa,” alisema Sipitieck.

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI AONGOZA MKUTANO WA 23 WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Jijini Dar es Salaam. 

Katika salamu zake amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao katika kutekeleza lengo kuu la Wizara ambalo ni kuendeleza uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kukuza Utalii nchini. 

Amewataka watumishi wote wa Wizara kuwa waadilifu, wabunifu, kufanya kazi kwa ushirikiano, kuepuka vitendo vya rushwa na makundi yasiyokuwa na tija kwa Wizara na Serikali kwa ujumla. 

Alionya kuwa, Mtumishi yeyote atakeenda kinyume cha sheria na taratibu hatosita kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya "HAPA KAZI TU"

Maj. Gen. Milanzi alimuwakilisha Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ambaye yupo Mkoani Dodoma kwa ajili ya majukumu mengine ya Kiserikali (Bunge la bajeti).
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii wakiimba wimbo wa kuashiria umoja wa wafanyakazi (Solidarity Forever). 
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati),  Naibu Katibu Mkuu Angelina Madete (kulia) na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii Wilfred Msemo (kushoto) wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana tarehe 17 Mei, 2016 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, tawi la Bustani, Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakiimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi "Solidarity Forever"(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA WANAHISA MEI 21

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei leo tarehe 18/05/2016 amezungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kuzungumzia kuhusu mkutano mkuu wa wanahisa wa Benki ya CRDB unaotarajia kufanyika jijini Arusha tarehe 21/05/2016 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC. 

Mkutano huo wa wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa wa Benki hiyo itakayofanyika tarehe 20/05/2016 katika ukumbi huo huo ambapo pamoja na mambo mengine wanahisa wa Benki ya CRDB watapata kufahamu juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa sehemu ya wanahisa wa Benki hiyo. 

Dk. Kimei amechukua fursa hiyo kuwakaribisha wanahisa wote wa Benki ya CRDB kuweza kushiriki katika semina na mkutano mkuu na kusisitiza kuwa mkutano wa mwaka huu utakua ni wa kipekee ikizingatiwa kuwa Benki ya CRDB ipo katika maadhimisho ya miaka 20 tangu ilipoanza rasmi mnamo mwaka 1996 baada ya utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akionyesha kitabu cha taarifa ya Mwaka ya benki hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma Shirikishi, Esther Kitoka na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay. Benki hiyo inatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanahisa Mei 21.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, TullyEsther Mwambapa, Mameneja wa Idara hiyo Ena Mwangama na Godwin Semunyu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images