Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 848 | 849 | (Page 850) | 851 | 852 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Jamii nchini imeaswa kuendelea kujenga familia imara kwa kuwa ndicho kitovu cha mabadiliko katika jamii na maendeleo ya kiuchumi.

   Aidha, imekumbushwa kuwa masuala mbalimbali  hujadiliwa, kupangwa na kutekelezwa kuanzia ngazi ya familia kwa ajili ya kuimarisha ushiriki thabiti wa jamii katika maendeleo ya taifa.

  Hayo yamo katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa maadhimisho  ya Siku ya familia iliyofanyika Mei, 15, 2016.

  Taarifa hiyo imeeleza kuwa Tanzania iliadhimisha siku hiyo chini ya kauli mbiu ya isemayo “Familia Yenye Afya Bora ni Mwanga wa Maendeleo”

  Taarifa hiyo imebainisha kuwa familia ni kitovu cha Maendeleo katika jamii hivyo haina budi kutambua kuwa uzingatiaji wa masuala ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupaswa kujadiliwa, kupangwa na kutekelezwa kuanzia ngazi ya familia kwa ajili ya kuimarisha ushiriki thabiti wa jamii katika maendeleo ya taifa.

  Imebainisha kuwa  maendeleo ya nchi hayawezi kufikiwa kama familia hazitakuwa na afya bora hivyo kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kuchochea mafanikio ya malengo ya Maendeleo Endelevu yatakayozingatia uboreshaji wa huduma ya afya bora ya familia, malezi bora ya watoto na utunzaji wa afya ya watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu.

  “ Kila mwanafamilia anahitajika kushiriki  katika maadhimisho ya siku hii muhimu kwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo, ikiwemo  vyombo vya habari kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa maadhimisho haya ili kuharakisha uboreshaji wa afya za wanafamilia wote katika nchi yetu” imeeleza sehemu taarifa hiyo. 

  Katika  hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) Bi. Lilian Liundi akiizungumzia siku hiyo katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW) ameeleza kuwa hali ya familia katika maeneo mbalimbali haiko salama kutokana na changamoto za kiuchumi.

  Ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto ya tatizo la mimba za utotoni kwa watoto wa kike na wanawake kuachiwa familia hivyo misingi ya familia inakuwa siyo bora kutokana na kuwepo kwa malezi ya upande mmoja.

  Naye mchambuzi wa Masuala ya Siasa kutoka nchini Kenya Bw. Bobby Mkangi  ameeleza kuwa kufuatia hali ngumu ya uchumi misingi ya familia imevurugika na hivyo kupelekea kuwepo na ajira za watoto ambao badala ya kuwa shule wanafanya kazi ndogondogo kusaidia kipato cha familia.


  Siku ya Familia Duniani  huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu  wa Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa namba 47/257 la Septemba 20, 1993.

  0 0


  Anitha Jonas - MAELEZO

  TANGU enzi za Azimio la Arusha, suala la maadili limekuwa likisisitizwa kama nguzo muhimu katika utoaji wa huduma kwa umma. Lengo lilikuwa ni kuhakakisha kwamba kila mtumishi wa Umma anatekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa.

  Kutofanikiwa kwa Azimio la Arusha kulitokana na baadhi ya Viongozi kujua kwamba utekelezaji wa malengo ya azimio hilo ungekwamisha nia ovu waliyokuwanayo kama Watumishi wa Umma katika kuwahudumia Wananchi. Ndio maana juhudi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere za kutaka azimio hilo liungwe mkono hazikuzaa matunda.

  Pamoja na kuwepo sheria, kanuni, miongozo na mikakati ya kukuza maadili kwa watumishi wa Sekta ya Umma na watu binafsi, wananchi bado wamekuwa wakilalamika kuwepo urasimu usio wa lazima wenye lengo la kutengeneza mazingira ya rushwa na huduma zisizoridhisha. Aidha, wapo baadhi ya wafanyabishara binafsi wasiozingatia maadili na hata kufikia hatua ya kuchochea utoaji wa rushwa au kuzalisha bidhaa zisizo na viwango.

  Katika jitihada za kuhakikisha kwamba watumishi wa Umma wanakuwa waadilifu na wanafuata maadili mema, Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ilibuni mikakati ya kuwa na utaratibu mpya kwa viongozi na watumishi wa Sekta za Umma na Binafsi kusaini Ahadi ya Uadilifu (integrity pledge).

  Ahadi ya Uadilifu ni tamko rasmi na bayana la dhamira ya kuwa na mwenendo wa kimaadili na kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya maadili na mapambano dhidi ya rushwa. Kwa kusaini tamko hilo, mhusika au taasisi inakuwa imejipambanua kwa Umma kuwa haitajiingiza katika masuala yasiyo ya kimaadili katika utoaji huduma na uendeshaji wa biashara.

  Kwa mujibu wa Kamishina wa Maadili Jaji Salome Kaganda, kuna aina tatu za hati za Ahadi ya Uadilifu yaani; Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi ili kila kundi liwajibike kwa namna yake.

  Akizindua Hati za Uadilifu mwezi agosti 2015, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema, kuwepo kwa Hati hizo ni hatua kubwa muhimu na ya kihistoria katika safari ya kuboresha na kuhuisha mifumo ya uadilifu iliyopo ili iweze kwenda sambamba na mazingira na nyakati zilizopo.

  Dkt. Kikwete hakusita kuelezea chimbuko la Hati ya Madili kwa kusema, “Kwa muda mrefu kumekuwepo na changamoto kubwa katika kupambana na rushwa kama moja ya tatizo kubwa la utovu wa uadilifu nchini.

  Tumechukua hatua kadhaa ikiwemo kutengeneza Mkakati wa Mapambano Dhidi ya Rushwa na mabadiliko katika Sheria ambayo ilisaidia kuanzishwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Tumepata mafanikio makubwa na ya kutia moyo ingawa bado zipo changamoto na manung’uniko ambayo hatuwezi kuyapuuza.”

  Dkt. Kikwete alifafanua kuwa, kwa madhumuni ya kuyaongezea mapambano haya nguvu na kasi, Serikali iliamua Mpango wa Mapambano dhidi ya Rushwa uingizwe katika Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ili kutoa msukumo wa pekee katika utekelezaji wake.

  Akielezea juu ya Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Mkurugenzi Mtendaji wa BRN Bw. Omar Issa alisema kuwa Ahadi ya Uadilifu ni moja ya maeneo 12 yaliyo katika Mpango wa Mapambano dhidi ya Rushwa chini ya Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa (BRN).

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, matokeo ya utafiti uliofanywa katika kutekeleza mpango huo imeonekana kwamba moja ya changamoto iliyoonekana katika eneo la utoaji huduma na uendeshaji biashara nchini ni tatizo la rushwa na utovu wa maadili katika taasisi za umma na binafsi. Hivyo kulikuwa na haja ya kuweka mikakati ya uwajibikali na kufuata maadili katika utumishi wa Umma na Sekta binafsi.

  Katika kuweka msisistizo wa suala la maadili na uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma, Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa watumishi wote wa umma kujaza Hati ya Ahadi ya Uadilifu (integrity pledge) ambayo imeeleza wazi masharti ya namna mtumishi wa Umma anavyopaswa kufanya kazi.

  Lengo ni kusaidia kukuza maadili na mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa katika Sekta ya Umma na binafsi kwa kuwa ahadi au tamko hilo linashawishi viongozi, watumishi wa Umma na Makampuni binafsi kuwa tayari kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadili na kupambana na rushwa kwa hiari yao wenyewe.

  Akiunga mkono juhudi za Dkt. Magufuli katika kusimamia nidhamu kwa Watumishi wa Umma, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kwamba Hati ya Uadilifu (integrity pledge) itakuwa chachu ya harakati za kukuza uadilifu na mapambano dhidi ya rushwa nchini. “Ahadi ya uadilifu itaweka kauli thabiti ya kimaadili ambayo itaonyesha nia ya kutekeleza majukumu ya viongozi na watumishi wa umma,” alisisitiza Balozi Sefue.

  Alifafanua kuwa, ujazaji wa Hati hiyo hiyo utakuza utamaduni wa viongozi, watumishi wa Umma na Sekta binafsi kwa ujumla kuwa tayari kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadili na kupambana na rushwa kwa hiari yao. Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Bi. Angela Kairuki amesema kwamba mtumishi wa umma anatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na uadilifu bila kutoka nje ya mstari.

  Mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw Agrey Mwanri amesema atasimamia ipasavyo maadili ya utumishi wa Umma hususan katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika mkoa wake huku akiahidi kuwawajibisha watumishi watakaokiuka maadili ya utumishi wa umma.

  Tangu achaguliwe kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli amewachukulia hatua baadhi ya viongozi wa Umma kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa majukumu waliyopewa. Viongozi hao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato, Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Dkt.

  0 0


  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akizungumza watu wenye ulemavu na wadau wa maendeleo nchini mara baada ya uzinduzi wa kanzidata kwa ajili ya watu wenye ulemavu nchini.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akifatilia uwasilishwaji wa kanzidata ya watu wenyes ulemavu nchini iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO. 

  Na Raymond Mushumbusi - MAELEZO

  Bwana Joachim Marege ni mtu mwenye ulemavu asiyeweza kutembea. Baba huyu anakofanyia kazi inabidi apande lifti hadi ghorofa ya kumi. Siku moja nikiwa nimeongozana naye kwenye lifti mara ghafla umeme ukakatika. Baada ya lift kufunguliwa nikamsaidia kutoka kwenye lift na kuendelea na safari yangu  lakini kwa ndugu huyu haikuwezekana kuendelea na safari yake kwa kupanda ngazi ilibidi asubiri kwa muda  hadi umeme utakaporudi ndo akapanda lift na kwenda ofisini kwake. Hii ni changamoto sana kwa watu wenye ulemavu katika kupata miundombinu rafiki ya kuwawezesha katika shughuli zao za kila siku na ambao idadi yao inaongezeka kila kukicha.

  Mnamo Aprili 11 2016 Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu walizindua kanzi data maalum kwa ajili ya kupata takwimu za watu wenye ulemavu nchini.Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani, zaidi ya watu bilioni moja dunia sawa na asilimia 15 ya watu wote duniani wanakadiriwa kuwa na aina fulani ya ulemavu. Idadi ya watu wenye ulemavu inaongezeka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ajali, majanga ya asili na ya kusababishwa na binadamu, ongezeko la watu hasa wenye umri mkubwa, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa ya akili na matatizo sugu ya kiafya.
   
  Kuongezeka huku kwa idadi ya watu wenye ulemavu, kunasababisha mahitaji makubwa ya huduma muhimu za kijamii. Aidha, maisha ya watu wenye ulemavu yanakuwa magumu zaidi kutokana na unanyanyapaa kutoka kwa jamii kwa ujumla, hali ambayo inahitaji mabadiliko ya kimtazamo. Ni ukweli ulio wazi kwamba watu wenye ulemavu hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania wana matatizo ya upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile elimu na afya ikilinganishwa na watu ambao hawana ulemavu.
   
  Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), karibu asilimia 80 ya watu wenye ulemavu wanaishi katika nchi zinazoendelea. Umaskini hupunguza uwezekano wa watu wenye ulemavu kupata huduma za kijamii na haki nyingine za kimsingi. Kwa bahati mbaya programu nyingi za maendeleo zimeshindwa kuzingatia mahitaji maalum ya watu wenye ulemavu kinyume na makubaliano ya kimataifa yanayosisitiza uzingatiaji huo kwa ajili ya maendeleo endelevu.
   
  Tumeshuhudia majengo yaliyojengwa muda mrefu hata yanayojengwa sasa mengi hayazingatii mahitaji maalum kwa watu wenye ulemavu. Inabidi katika ujenzi miundombinu rafiki kwa wenye ulemevu iwekwe ili kuwapunguzia adha katika maisha watu wenye ulemavu.
   
  Pamoja na umuhimu na uelewa uliopo bado upatikanaji wa takwimu sahihi ni tatizo hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Kwenye ngazi ya kimataifa, bado kuna tofauti kuhusu nini hasa maana ya ulemavu, suala ambalo husababisha ulinganifu wa takwimu kuwa mgumu. Katika ngazi ya kitaifa, taarifa za watu wenye ulemavu hazitoshelezi mahitaji ya kuweka misingi madhubuti ya kupanga na kutekeleza programu za maendeleo zinazolenga kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu.
   
   
  Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita Serikali ya Tanzania kwa kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu, imefanya juhudi kubwa za kukusanya na kuchambua takwimu za watu wenye ulemavu kupitia tafiti mbalimbali na Sensa za Watu na Makazi za miaka ya 2002 na 2012. Pamoja na juhudi hizi bado ukusanyaji wa takwimu hizi mara zote hukabiliwa na changamoto kadhaa. Changamoto kubwa ni ile inayohusiana na mtazamo wa jamii kuhusu ulemavu na watu wenye ulemavu kwa ujumla. Tabia ya kuwaficha watu wenye ulemavu kwa visingizio mbalimbali hukwamisha upatikanaji sahihi wa idadi au taarifa ambazo zinahusiana na watu wenye ulemavu.
   
  Changamoto nyingine ni watu kutojua maana halisi ya ulemavu. Watu wengi huchukulia ulemavu kuwa ni hali ya mtu kutoweza kabisa kufanya jambo fulani. Mfano kutosikia au kuona kabisa na kadhalika. Tafsiri ya ulemavu sio sahihi na huwaacha watu wengi wenye ulemavu katika tafiti na sensa zetu. Maana halisi ya ulemavu ni ile ambayo ilitolewa kwenye Tamko namba 61/106 la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wenye Ulemavu. Kulingana na Tamko hili, watu wenye ulemavu "ni watu wote wale ambao wana matatizo ya muda mrefu ya viungo , akili , uelewa , au hisia ambavyo kwa pamoja na vikwazo vingine vinaweza kusababisha ushiriki wa mtu kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za kijamii kama watu wengine”.
   
  Utafiti kuhusu watu wenye Ulemavu nchini uliofanyika Mwaka 2008, ulionyesha kuwa asilimia 8 ya watu wote nchini wenye umri wa miaka 7 na kuendela walikuwa na ulemavu wa aina moja au nyingine. Taarifa za watu wenye ulemavu pia zilikusanywa kwenye Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 na kuonyesha kuwa asilimia 9 ya watu wote nchini walikuwa na ulemavu. Matokeo ya tafiti hizo na Sensa yanadhihirisha kwamba kiwango cha ulemavu ni kikubwa katika maeneo ya vijijiji kuliko mijini. Kulingana na matokeo ya Sensa ya Mwaka 2012, kiwango cha ulemavu vijijini kilikuwa ni asilimia 9.4 sawa na watu milioni 2.9 ikilinganisha na asilimia 7.3 sawa na watu 560,000 kwa maeneo ya mijini huku kiwango cha ulemavu ni kikubwa kwa Tanzania bara kwa asilimia 9 sawa na watu milioni 4.4 kuliko Tanzania Zanzibar asilimia 7 sawa na watu 55,355.17.  Pamoja na juhudi hizo Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekuwa ikikusanya pia taarifa za watu wenye ulemavu katika tafiti nyingine. Tafiti hizo ni pamoja Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi na Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi.
   
  Kulingana na Utafiti wa Watu Wenye Uwezo Kufanya Kazi wa Mwaka 2014, mikoa yenye watu wengi wenye ulemavu ni Tanga (asilimia 7.2), Mara (asilimia 6.3) na Dar es Salaam (asilimia 5.8).Pia inaonyesha mikoa yenye watu wengi wenye ulemavu wanaojua kusoma na kuandika ni Dar es Salaam (asilimia 89.5), Kilimanjaro (asilimia 84.7) na Mjini Magharibi (asilimia 83.7).Hali ya ajira kwa watu wenye ulemavu inaonyesha kuwa wengi wameajiriwa kwenye sekta ya kilimo. Hali ya kipato kwa watu wenye ulemavu walioajiriwa kwa mwezi ni kati ya Tshs. 65,000 na Tshs. 500,000, na kwa wale ambao wamejiajiri kipato chao ni kati ya Tshs. 65,000 na Tshs.300,000.
   
  Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 yanaonesha kuwa kiwango cha kujua kusoma na kuandika ni asilimia 70.1 ya watu wote wenye ulemavu wanaojua kusoma na kuandika ikilinganishwa na asilimia 78.9 ya watu ambao hawana ulemavu. Vile vile matokeo hayo yanaonesha kuwa kiwango cha kuandikishwa shuleni kwa watoto wenye ulemavu ni kidogo pia ukilinganisha na watoto ambao hawana ulemavu kwani kulingana na matokeo hayo ni asilimia 75 ya watoto wenye ulemavu wenye umri wa miaka 7 - 13 waliokuwa wameandikishwa shule ukilinganisha na asilimia 77 ya watoto ambao hawana ulemavu.
   
  Tofauti zote hizi ni matokeo ya mtazamo walio nao baadhi ya watu hapa nchini kwamba hakuna sababu ya kumpeleka mtoto mwenye ulemavu shule. Lakini, hata pale ambapo mzazi anakuwa tayari kumpeleka mtoto mwenye ulemavu shuleni miuondombinu isiyozingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu inaweza kumzuia asifanye hivyo. Umbali wa kwenda shule ni chanzo cha watoto wa aina hii kutopelekwa shule.
   
  Pamoja na kuwepo kwa taarifa hizi zinazotokana na Sensa na tafiti, lakini vile vile kuna takwimu ambazo hukusanywa na taasisi mbalimbali wakati wa utekelezaji wa shughuli zao za kikazi. Hata hivyo, takwimu hizi hazijawekwa pamoja na katika hali rafiki ili kumsaidia mtu au taasisi inayozihitaji. Aidha, inawezekana pia kuwa ukusanyaji wa takwimu hauzingatii vigezo vinavyokubalika na Serikali na taasisi za watu wenye ulemavu. 

  kwa kutambua hali hiyo na Wizara inayoshughulikia watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Vyama vya Watu wenye ulemavu iliandaa kanzidata (database) ambayo ina takwimu muhimu kuhusu taarifa za watu wenye ulemavu nchini. Kwa kuanzia, kanzidata hii ina takwimu zinazotokana na Sensa na baadhi ya taifiti ambazo zimefanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
   
  Kanzidata hii itakuwa ikiboreshwa mara kwa mara kwa kuingiza vyanzo vipya vya takwimu hasa vile vitokanavyo na taarifa za kiutawala kila zinapopatikana na inategemea kuwa msaada kwa watu wenye ulemavu kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kichumi kwa sababu takwimu sasa zitakuwepo ambazo zitasaidia Serikali pamoja na asasi mbalimbali kuwawezesha watu wenye ulemavu nchini kujikwamua kiuchumi kwa kuwawezesha mikopo ya kufanya shughuliza za ujasiriamali, kuwawezesha kupata elimu na huduma bora za afya na huduma nyingine za kijamii.
   
  Kanzidata hii itasaidia mambo kadhaa muhimu. Lakini kubwa zaidi ni upatikanaji wa taarifa hizi katika mfumo rafiki utakaosaidia watumiaji kufanya uchambuzi wa kina zaidi kulingana na mahitaji yao. Aidha, kanzidata hii itasaidia uelewa wa watu kuhusu ulemavu kwa ujumla na umuhimu wa kuhusisha mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa ajili ya maendeleo endelevu.
   
  Mwaka huu wa 2016 dunia kwa ujumla itaanza kutekeleza Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals).Utekelezaji huu ni wa miaka 15 ijayo baada ya kukamilika Malengo ya Millenia ya Mwaka 2015. Moja ya mapungufu yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa Malengo ya Milenia ni ukosefu wa takwimu za kutosha kwa ajili ya kufuatilia na kutathmini utekelezaji na kuachwa kwa baadhi ya sehemu ya jamii. Ndio maana, kauli mbiu kuu ya Malengo Endelevu ya Maendeleo ni "Hakuna atakayeachwa Nyuma" (Leaving no One Behind) na hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa kuna taarifa za kutosha kwa ajili ya kufuatilia na kutathmini Malengo mara utekelezaji utakapoanza baadaye mwaka huu.
   
  Suala la watu wenye ulemavu ni mtambuka na hivyo linajitokeza katika Malengo yote yanayozungumzia maendeleo endelevu ya binadamu. Lengo Namba 1, kwa mfano, linazungumzia kumaliza umaskini wa aina zote kwa watu wote. Lengo Namba 4, linazungumzia kumaliza tofauti za aina yoyote kwenye suala elimu n.k. Kwa kutambua ukweli huo, Wizara husika kwa kushirikiana na wadau wengine inaandaa Andiko la Mradi ili kuweza kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi za watu wenye ulemavuni wakati muafaka kwa  wadau wote wa ndani na nje kuwa tayari kuunga mkono juhudi hizi za Serikali mtakapoombwa kufanya hivyo. Juhudi hizi ni pamoja na kujenga mfumo ambao utaiwezesha Serikali kupata takwimu za watu wenye ulemavu kwa haraka na usahihi zaidi.
   
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye Ulemavu Dkt Abdallah Possi ametoa wito kwa Wananchi na wadau wa maendeleo hasa asasi za kiraia kusoma taarifa hizi na kuzitumia vizuri taarifa zilizopo kwenye kanzadata hii kwa kuwa zimezingatia vigezo vyote vya takwimu bora na zimetolewa na taasisi zenye mamlaka ya Kisheria kufanya hivyo. 

  Zitumieni kwa lengo moja kuu ambalo ni kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu nchini kwa kuondoa unyanyapaa katika jamii yetu na kushinikiza mabadiliko katika sera na programu za maendeleo. Wananchi mnaombwa kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wa tafiti zinazolenga kupata taarifa za watu wenye ulemavu. Toeni taarifa zao kamili ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi na hivyo kurekebisha sera na programu zake za maendeleo.

  Mafaniko ya uazishwaji na utekelezaji wa matumizi ya kanzi data hii imetokana na  washirika wetu wa maendeleo ambao wamesaidia juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu na Watanzania kwa ujumla. Taarifa nyingi ambazo zipo kwenye kanzidata hii zimepatikana kwa ushirikiano na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.

  0 0

  Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh. Ramo Makani, Amesema serilikali ya awamu ya tano itahakikisha jamii zinazo ishi karibu na shamba la taifa la sao hill, lenye tarafa maalum (4) za Mgololo, Ihalimba, Ihefu na Irundi zinakuwa za kwanza kunufaika na mgao wa vibali vya uvunaji wa misitu ili zishiriki kikamilifu katika kulinda, kuhifadhi na kuiboresha misitu hiyo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

  Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imebainisha kuwa naibu waziri Makani ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi katika shamba la miti la Taifa la sao hill wilayani Mufindi Mkoani Iringa.

  Amesema, ili wananchi waone kuwa msitu huo ni mali yao kama Watanzania, ni lazima wawe wa kwanza kufikiriwa wakati wa ngao wa vibali vya uvunaji kupitia jumuia watakazo ziunda katika maeneo yao.

  Akizungumzia suala la utoaji wa vibali vya uvunaji wa misitu amesema, msitu waSao Hill na mingine nchini ni mali ya Taifa, hivyo, ni haki kwa Mtanzania yeyote popote nchini kupata kibali na akasisitiza kuwa kwa mwaka huu huwenda vibali vikachelewa kutoka kwa kuwa wizara yake iyapiti maombi kwa umakini ili kupunguza malalamiko ya upendeleo katika utoaji vibali.

  shamba la Miti la Sao hill lililopo Wilayani Mufindi ni la kwanza kwa ukubwa nchini kati ya mashamba 18 ya Taifa, ilikiwa na hekita zaidi ya laki moja na 35 elfu na lilianzishwa rasmi mwaka 1960.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani (wa pili kulia) akizindua Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016 leo mjini Dodoma. Wengine ni Mwakilishi wa Balozi wa Finland nchini Oscar Kassy(kulia) , Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aliyeshughulikia mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora( wa pili kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge(kushoto). 
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani akiwahutubia wadau wa TEHAMA wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016 leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016 leo mjini Dodoma.

  Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dodoma.

  Serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya Nchi wameifanyia maboresho Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2003 na kuja ya sera mpya ya mwaka 2016 ili kuunganisha sekta muhimu za uzalishaji na viwanda katika miundombinu ya TEHAMA.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Sera ya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016.

  Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuiwezesha Tanzania kutumia fursa zinatokana na uwepo wa miundombinu ya TEHAMA kuingia katika uchumi wa kati ifakapo 2025 kwa kuimarisha matumizi ya TEHAMa katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini.

  Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa Sera hiyo ni muhimu katika kujenga jamii habari itakayowezesha nchi kufikia maarifa yatakayosaidia kwenda sanajari na mpango wa Taifa kujenga uchumi wa viwanda.

  Alisema kuwa Sera hiyo imejikita katika kukuza matumzi TEHAMA katika uzalishaji ili kuongeza tija , kukuza utafiti na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika TEHAMA kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
  Awali akiongea kabla ya uzinduzi wa Sera hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Mawasiliano) Profesa Faustin Kamuzora alisema kuwa Sera hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa kazi wa kila siku katika sekta mbalimbali nchini.

  Alisema kuwa sera hii itasiaidia kwenda sanajari ya ukuaji wa kasi wa matumzi ya mawasiliano hapa nchini.

  0 0

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezitahadharisha serikali za nchi za Kiafrika kuanza kujiandaa kutumia raslimali zao katika mpango wa kusaidia kaya maskini kwani wahisani hufikia ukomo.
  Mheshimiwa Samia ameyasema hayo leo kwenye ufunguzi wa mkutano wa kubadilishana mawazo kuhusu mpango wa uhaulishaji fedha kwa jamii maskini Afrika unaofanyika katika hoteli ya Ngurdoto mkoani Arusha.
  Mkutano huo wa siku tano ambao unahudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Latin America, Asia na Ulaya umeandaliwa na Benki ya Dunia (WB) na Unicef na kuratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao umeonesha mafanikio makubwa katika mpango wa kunusuru kaya maskini nchini.
  Makamu wa Rais alisema hatua hiyo ya kutumia raslimali za nchi husika itasaidia kuufanya mpango wa kusaidia kaya maskini kuwa endelevu.
  Alibainisha kuwa pamoja na matokeo mazuri yaliyopatikana katika utekelezaji wa mpango wa uhaulishaji fedha kwa kaya masikini, serikali za nchi za Afrika zinapaswa kutambua kuwa miradi ya kutegemea wahisani ina mwisho wake.
  "Serikali zetu zinatakiwa kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya maendeleo endelevu ya wananchi wetu," alidokeza Mheshimiwa Samia.
  Akizungumzia kwa upande wa Tanzania Mheshimiwa Samia alisema Mpaka sasa kaya maskini milioni 1.1 zimefaidika na mpango huo wa uhaulishaji fedha ambapo wanalipwa kila baada ya miezi miwili.
  "Siri ya mafanikio ni kujitoa kwa Watanzania na kuupokea mradi kama wao. Tumeangalia zaidi hali ya maskini kule chini na umepokelewa mradi kama mkombozi," alisema na kuongeza
  "Kuna kaya kama tatu kule mkoani Pwani baada ya kufanya tathmini wamesema hawahitaji tena, sasa hivi wanakula milo mitatu, watoto wao wanaenda shule, wako vizuri."    
  Aliwaeleza wajumbe hao kuwa mkutano huo unafanyika wakati muafaka ambapo dunia inahangaika kujadili namna ya kuondokana na umaskini kupitia Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu Ajenda 2030
  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Arusha
  16/5/2016

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizungumza na watendaji wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi leo.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Mohamed akifungua kikao kabla ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi kuzungumza na watendaji wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro leo
  Mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mafunzo ya Itikadi kutoka Idara ya Itikadi na uenezi Makao Makuu ya CCM, Frank Uhahula akijitambulisha na kutambulisha ugeni uliofuatana na naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajabu Luhwavi kwenye kikao hicho.
   
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizungumza na watendaji wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi leo.
   

  0 0

  Baadhi ya watu wanaotaka kusafiri na mabasi ya yaendayo haraka wakiwa katika kituo cha Posta ya Zamani (Baharini) wakipewa maelekezo kuwa katika kituo hicho mashine za kutolea tiketi zimeleta hitilafu kwa leo.
   Basi la mwendo wa haraka likitoka katika kituo cha Posta ya zamani bila kupakia abiria kutokana na kutokuwepo kwa tiketi kwa sababu ya mashine za kituo hicho kuleta hitirafu ya mtandao wa kutolea tiketi.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.
  NAULI za usafiri wa Mabasi yaendayo haraka zimeanza kutozwa leo katika jiji la Dar es Salaam huku kukiwa na changamoto nyingi katika vituo vya mabasi hayo.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Afisa Uhusiano wa UDART, Deus Bugaywa amesema kuwa changamoto waliokutana nayo ni baadhi ya vituo kukosa mashine za kukatishia tiketi, mafuriko ya watu katika vituo pamoja na chenji kwa wasafiri wanaotumia huduma hiyo.

  Amesema mfumo wa kadi ukianza utaondoa changamoto hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam na mfumo wa tiketi utatumika kwa wale ambao wanaingia katika jiji na kuondoka.

  Aidha amesema mfumo huo unatakiwa fedha itakayotolewa lazima usome benki kuu kwa kuonyesha kodi katika tiketi, suala la chenji ni chagamoto kutokana na fedha ya chenji waliokuwa nayo ni milioni sita za sarafu lakini zimeweza kuisha.

  Baadhi ya wananchi wanaotumia usafiri wamesema kuwa kuanza kwa usafiri huo umekuwa ni mapema kwa kushindwa kuona changamoto hizo.

  Mmoja wa wananchi, Juma Said amesema kuwa wamekwenda kukata tiketi katika kituo na kuambiwa waende kituo kinachofuata hali hiyo ameona kuwa ni usumbufu.
  Hata hivyo amesema kuwa mtu mmoja anapata tiketi ndani ya dakika 10 ambapo  ni vigumu kwenda na idadi ya watu kuweza kwenda kwa wakati.

  0 0

                         
  Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapa siku 15 Wakuu wa mikoa na wilaya wawe wameondoa mifugo iliyoko katika maeneo ya Hifadhi ya Taifa na mifugo iliyoingizwa nchini kupitia mikoa ya Arusha, Kagera na Geita iwe imerudishwa katika nchi ilikotoka la sivyo watatumbuliwa.
  Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Ngurdoto mkoani Arusha Mheshimiwa Samia alisema Wakuu wa Mikoa na wilaya wanapaswa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kuweka mifugo ambayo itatolewa kwenye Hifadhi hizo hiyo na kwamba zoezi hilo linatakiwa liwe limekamilika tarehe 30/6/2016.
  Alisema Serikali ilikwishatoa tamko hilo kupitia kwa Waziri wa Maliasili ya kuwataka wananchi wote waliovamia maeneo ya Hifadhi kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo kufuga, kulima na makazi kuondoka kwa hiari yao ifikapo tarehe 15/6/2016. na kwamba baada ya tarehe hiyo serikali itawaondoa kwa nguvu.
  "Mimi naongeza muda mpaka tarehe 30/6/2016 mifugo yote iwe imeondolewa kutoka kwenye Hifadhi. Na mifugo iliyoingizwa nchini kwenye mikoa ya Arusha, Kagera na Geita nayo naomba irudishwe katika nchi ilikotoka," alisema na kuongeza
  "Kama hilo halijafanyika baada ya tarehe hiyo Mkuu wa mkoa ataondoka, ng'ombe ataondoka na Mkuu wa wilaya kwenye eneo husika ataondoka," alisema Makamu wa Rais.
  Akizungumzia taarifa iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku kwamba Makamu wa Rais apinga utumbuaji majipu alisema kauli aliyoitoa kwenye siku ya wakunga duniani kwamba viongozi wa kisisa na wa kiserikali wafuate taratibu wanapowawajibisha wauguzi ama wafanyakazi wa maeneo mengine haikuwa na lengo hilo.
  Alisema serikali inaajiri, inateua na kuondoa kwa mujibu wa mamlaka ya Rais, hivyo Rais ana uwezo wa kutumbua majipu wakati wo wote kwa kuwa ana uwezo wa kuteua na kuondoa lakini kwa wale walio katika ajira ya kudumu wanatawaliwa na sheria zao   
  "Haiwezekani Mkuu wa mkoa au Mkuu wa wilaya aende amwajibishe mfanyakazi lazima afuate ngazi za utumishi wa umma," alieleza.Gazeti la Tanzania Daima la tarehe 13/5/2016 Toleo NA. 4179 liliandika habari hizo yenye kichwa cha habari Makamu wa Rais apinga utumbuaji wa majipu.
  Akiwa mkoani Arusha Makamu wa Rais alikabidhi hundi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni mchango wa madawati kwa mikoa 19 inayopakana na hifadhi za Taifa ambayo imetolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika shule za msingi.
  Fedha hizo zitatengeneza madawati 16,500 kwa wilaya 55 nchini sawa na madawati 300 kwa kila wilaya. Madwati hayo yatawezesha wanafunzi 49,500 kuondokana na tatizo la madawati shuleni.
  Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii Professor Jumanne Maghembe alimweleza Makamu wa Rais kuwa hiyo ni hatua ya kwanza na kwamba hatua inayofuata ni kutoa madawati kwa wilaya zote nchini.   
   
  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Arusha

  16/5/2016

  0 0


  Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto, Arusha, Tanzania.
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angella Kairuki akitoa hotuba ya kumkaribisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (Tanzania, Kenya Uganda na Burundi) Ms Bella Bird akitoa hotuba katika Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Mwenyekiti wa kamati ya uongozi taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Dr. Florens Turuka akitoa maelezo ya kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha katika Hotel ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akitoa neno la shukrani baada ya Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan kufungua Mkutano wa Nchi za Afrika Zinazotekeleza Mipango ya Uhawilishaji Fedha .
   
  Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefungua Mkutano wa nchi za Afrika zinazotekeleza Mpango wa Uhawilishaji Fedha kwa kusisitiza kuwa serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa kushirikisha wadau katika mapambano dhidi ya umaskini barani Afrika.

  Mheshimiwa Samia amesema licha ya juhudi kubwa kufanywa na mataifa mbalimbali barani Afrika dhidi ya umaskini, tatizo hilo limeendelea kuwakabili wananchi hivyo kuweko kila sababu ya kubuni mbinu thabiti za kutokomeza adui huyo wa ustawi wa wananchi.Amesema kuanzishwa kwa mipango ya uhawilishaji fedha ambayo imeanza kutekelezwa na nchi mbalimbali barani Afrika katika miaka ya karibuni kutasaidia kwa kiwango kikubwa jitihada za kutokomeza umaskini.

  Ameto mfano wa Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF - ambao umepata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu kuanza utekelezaji wa Mpango wa Uhawilishaji fedha ambapo hadi sasa zaidi ya kaya maskini Milioni Moja na Laki Moja zimeandikishwa na kuanza kupata ruzuku ya fedha kwa ajili ya kuboresha maisha na mkazo ukiwekwa katika sekta ya elimu, afya na lishe huku kaya husika zikijengewa uwezo wa kukuza shughuli za kiuchumi ili hatimaye ziweze kujitegemea.

  Mapema waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mheshimiwa Angellah Kairuki amesema mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika utambuzi, uandikishaji na utoaji wa Ruzuku kwa wakati kwa kaya za walengwa nchini kote, na kuwa changamoto chache zilizojitokeza zinafanyiwa kazi ili kuboresha zaidi Mpango huo.

  Mkutano huo unaoshirikisha nchi 17 na mashirika mbalimbali ya kimataifa umeitishwa nchini Tanzania kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini -PSSN- ambapo pia washiriki hao watapata fursa ya kutembelea kaya za walengwa ili kuona namna wanavyonufaika na huduma za mpango huo.


  0 0


  MILIONI MIA MOJA (100M) KUSHINDANIWA KUPITIA BIA YA TUSKER LAGER

  Dar es Salaam 16 May, 2016; Kwa kutambua thamani ya wateja wake Kampuni ya Bia ya Serengeti imezindua promosheni maalum ya kutoa shukrani kwa wateja wake ambao ni watumiaji wa bia ya Tusker Lager, ambapo watajishindia pesa taslimu Milioni 1 kwa washindi kumi (10) kila wiki kwa muda wa wiki kumi na kufanya jumla ya Milioni mia kushindaniwa na Zawadi za bia kibao. 

  Uzinduzi huo uliofanyika kwa aina yake katika mikoa miwili tofauti kwa wakati mmoja, mikoa hiyo ni Dar es Salaam na Kilimanjaro hii ni tofauti na ilivyozoeleka kwani uzinduzi hufanyika Katika sehemu moja tu. Promosheni hii imeanza rasmi leo na itaendeshwa kwa muda wa wiki kumi. Uzinduzi ulipambwa na maonyesho ya barabarani, msafara ulianzia kiwandani Chang’ombe na kuishia Fyatanga Bar Tegeta huku ukipokelewa na shamrashamra za aina mbalimbali.

  Hii si mara ya kwanza kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti kuendesha promosheni kama hii kwani ni wengi wameshanufaika kupitia promosheni mbalimbali za mfumo huu na hata kubadili maisha ya watumiaji wa bidhaa zake kwa kiasi kikubwa. Kupitia bia ya Tusker Lager Kampuni hiyo inaendeleza kile kilichokuwepo cha kurudisha fadhila na kutoa shukrani kwa watumiaji wa bia ya Tusker Lager. 

  Wateja wanaweza kujaribu mara nyingi kadiri wawezavyo. Ili kuwa mshindi wa Tusker milionea, washiriki wataweza kujishindia pesa taslimu kupitia droo zitakazochezeshwa kila wiki. Unapofungua bia ya Tusker Lager (500ml) chini ya kizibo ukapata kizibo cha Tusker Milionea hii inakuingiza Katika droo ya kupata Milioni moja, au unaweza kupata Bia ya Zawadi – hii inampa mteja wa Tusker bia ya bure papo hapo alipohudumiwa na ikiwa utapata jaribu tena utaendelea kuburudika kistaarabu ili kuongeza nafasi yako yako kuibuka mshindi. Promosheni hii itasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini ili kuleta ufanisi zaidi.

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti alisema promosheni hii si kwa ajili ya kuongeza mauzo tu bali ni kutoa shukrani kwa wateja wao kwa kuwaunga mkono na kusapoti bidhaa zao.

  “Kupitia Bia ya Tusker Lager wateja wetu wanaweza kujishindia shilingi Milioni Moja kwa washindi kumi kila wiki kwa muda wa wiki kumi ambao tutawapata kutoka Katika droo za kila wiki nchi nzima. Lengo kubwa ni kumwezesha mnywaji na mdau wa bia ya Tusker kufanya kweli kupitia bia yetu ya Tusker Lager”aliongeza Bi. Cesear Mloka.

  Kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro uzinduzi ulifanyika katika manispaa ya Moshi huku ukihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wasambazaji na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti na wana habari. Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Mauzo bwana Alain Tsageutayo ambae alisema “Wakati wa kuchagua zawadi za kushindaniwa pesa taslimu ilichukua nafasi ya juu – na kiwango cha Milioni moja kinaweza kusaidia kujikwamua kwa namna moja au nyingine. Wateja wetu ndio wametufikisha hapa tulipo basi nasi hatuna budi kurudisha shukrani kwako mtumiaji wa bia yetu ya Tusker Lager na ndio maana tunatoa kwa washindi 100, milioni 1 kila mmoja katika kipindi cha promosheni.”

  Milioni 100 na Tusker Lager - Fanya kweli na Uwini itadumu kwa muda wa wiki kumi nchi nzima. Kwa washiriki wa Tusker milionea wataweza kushuhudia droo zitakazofanyika kila ijumaa na kuonyeshwa kwenye runinga. Washindi watakaopatikana watakabidhiwa pesa zao kila ijumaa inayofuatia kwenye sherehe maalum ya promosheni. 
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti katika picha ya pamoja wakishangilia uzinduzi wa kampeni ya Tusker Fanya Kweli Uwini kiwandani hapo na baadae kufuatiwa na maonesho ya barabarani jijini Dar es Salaam.
  Vijana wa amsha amsha wakiburudisha barabarani katika jiji la Dar es Salaam.
  Msafara maalum ukielekea katika Bar ya Fyatanga tayari kwa uzinduzi rasmi kwa wateja wa bia ya Tusker
  Mkurugenzi wa Masoko Cesear Mloka (katikati) pamoja na wafanyakazi wengine wa SBL wakishangilia uzinduzi rasmi wa Tusker Fanya Kweli Uwini kwa wateja uliofanyika katika Bar ya Fyatanga nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Kanda ya Kaskazini Amoni Kabagi(kushoto) akieleza jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa 'Tusker Fanya Kweli Uwini' mjini Moshi, pamoja nae ni Meneja wa Mauzo wa Kilimanjaro, Godwin Seleli.
  Burudani ikiendelea katika uzinduzi jijini Dar tusker UTC Launch dance - Burudani ikiendelea katika bar ya Oriento Mjengo, Mjini Moshi

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma ya kifedha kwa njia ya mtandao wa simu wa Airtel huduma ya MR. MONEY.
   Meneja wa Airtel Money, Asupya Nalingigwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa huduma ya MR. MONEY  ambayo itaendeleza kurahisisha matumizi ya huduma ya kifedha kupitia simu za mkononi kwa uhakika katika kufanya miamala mbalimbali kwa gharama nafuu na kuhakikisha muamala wako unakamilika kwa usalama kabisa.
  amesema kuwa huduma ya Airtel Money Tap Tap ni huduma nyingine inayowasaidia wateja wakeinayotoa nafasi kwa wateja kufanya malipo kupitia kadi maalumu bila kuwa na haja ya kuwa na simu ya Mkononi.
  Mkuu wa Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa udiznduzi wa huduma ya MR.MONEY jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa huduma ya MR. MONEY inawezesha wateja wake kupata mkopo ya Timiza isiyo na harama kwa wateja na mawakala wa Airtel Money. 
  Amesema kuwa wateja wa Airtel wanaweza kununua Luku na kupewa muda  unit nyingine za ziada endapo mteja akitumia airtel Mone kununua Umeme. usikose kupata nafuu ya fedha zako unapomtumia pesa wapendwa wako kwa kutumia Artel  Money bila gharama yoyote.
   Kwa kutumia huduma mbalimbali za MR. MONEY piga *150*60# kufurahia huduma.

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Kwa miaka mingi hapa nchini Tanzania, Kilimo kimetajwa kuwa uti wa mgongo wa Taifa. Ikumbukwe kuwa miaka ya Sabini za mwanzoni kuliwahi kuwepo kauli kuhusu kilimo iliyosema “Kilimo cha Kufa na Kupona”. Kauli hii ililenga kuondoa njaa iliyokuwa inalikabili Taifa. Kwa miaka  ya hivi karibuni, serikali ikaja na Kauli Mbiu ya “Kilimo Kwanza”. Hizi zote ni jitihada za kuinua kilimo ambacho kinategemewa na walio wengi hapa kwetu.

  Kilimo ni eneo la kipaumbele katika uchumi wa Tanzania licha ya kuwa  kilimo nchini bado kinategemea kwa kiasi kikubwa mvua na hali ya hewa kwa ujumla .
   
  Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa iliyotolewa na  Mkurugenzi Mkuu Dkt. Agnes Kijazi zinasema mvua za masika zimeshaanza katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Hata hivyo maeneo machache yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.
   
  Hali ya unyevunyevu wa udongo inatarajiwa kuwa ya kutosheleza shughuli za kilimo katika maeneo mengi.Hata hivyo, mvua za juu ya wastani zinazoendelea kunyesha zinaweza kusababisha hali ya unyevunyevu wa udongo kupita kiasi hivyo kuathiri mazao na hata kusababisha mafuriko na kuharibu mazao.
   
  Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, msimu wa mvua za Masika katika kipindi cha miezi ya Machi hadi Mei, 2016 ni mahususi katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), Pwani ya Kaskazini, (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-Kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani kwa maeneo mengi ya ukanda huo isipokuwa maeneo ya Kusini mwa ukanda huo yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani.
   
  Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha tahadhari imetolewa kwa wakulima wote kuwa makini na mvua hizi za masika zinazoendelea kwani zinatarajiwa kunyesha kwa wingi katika baadhi ya maeneo kulingana na uelekeo wa upepo katika maeneo mengi ambayo yanayopata mvua za msimu wa masika.
   
  Mwelekeo wa mvua uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa hivi karibuni umezingatia zaidi kipindi cha msimu(miezi mitatu) na hali ya mvua katika maeneo makubwa. Hivyo, viashiria vinavyochangia mwenendo wa mifumo ya mvua na mabadiliko ya muda mfupi katika maeneo madogo utazingatiwa katika uchambuzi wa utabiri wa muda wa kati na mfupi.
   
  Wakulima wanashauriwa kuendelea na shughuli za kawaida za kilimo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu za kuongeza uzalishaji, kupanda mazao na miti kuzuia mmomonyoko wa udongo pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalam wa kilimo katika matumizi sahihi ya ardhi na mbegu. Hata hivyo, katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za  chini ya wastani,upungufu wa unyevunyevu wa udongo unaweza kujitokea hususan katika vipindi vya kukosekana kwa mvua. Wakulima waendelee kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa maafisa ugani katika kutekeleza shughuli zao.
   
  Aidha wataalamu wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) katika tafiti zao wametoa ushauri kuhusu namna bora ya kilimo cha baadhi ya mazao kwa kuzingatia taratibu sahihi za kilimo za mazao hayo wakati huu wa mvua za masika.
   
   
  Ushauri kuhusu mtama
   
  Mtama unatarajiwa kukua vizuri wakati wa masika. Wakati wa kupanda mtama, wakulima wanashauriwa kuanza utayarishaji wa mashamba kabla ya mvua. Upandaji kavu (yaani upandaji kabla ya mvua) unapendekezwa sana kwa mtama na ni bora wakulima wapande katika wiki za tatu na nne za Machi. Wakulima wanaweza kuanza kupanda mtama katika mwezi wa pili (Februari) kabla ya kupanda mimea mingine. Katika upandaji kavu, kina cha udongo (yaani urefu wa shimo kwenda chini) kinahitajika kuwa sentimeta tano ikilinganishwa na upandaji unyevu (yaani upandaji wakati udongo una maji) ambapo kina kinahitajika kuwa kama sentimita mbili nukta tano (2.5) hadi sentimita nne.
   
  Wakulima wanashauriwa kuweka mbolea vizuri kwa kuchanganya na udongo.Wakulima wanashauriwa pia kupalilia angalau mara mbili wakati wa kukua kwa mimea.
   
  Ushauri kuhusu Maharagwe
   
  Ili kupata  mazao bora ya maharage, umwagiliaji wa maji ni muhimu. Kwa ajili ya mvua ya kawaida au nyingi inayotarajiwa, uhifadhi wa maji ya mvua unahitajika ili maji haya yatumike wakati wa mvua chache. Wakulima wanashauriwa kutumia mbinu za umwagiliaji wa mifereji ya juu au chini wakati wa ukavu kwa milimita 50 kwa wiki hadi mwisho wa msimu. Kwa kawaida, joto huwa haina athari mbaya kwa maharage, kama kiwango kizuri cha maji kimo mchangani.
   
  Ushauri kuhusu Mahindi
   
  Wakulima wanashauriwa waanze kupanda mahindi kabla ya mwanzo wa mvua katika wiki ya tatu au nne ya Machi. Mahindi yanafaa kupandwa punde tu hali ya udongo na joto lake linapofaa kwani kuchelewesha upandaji kunaweza kusababisha upungufu wa mavuno,kwa sababu mahindi yanahitaji unyevu bora zaidi wa udongo wakati wa upandaji, wakulima wanashauriwa kutumia hatua zinazofaa za kuhifadhi udongo.
   
  Kutumia mbinu za ukulima bora ni pamoja na upandaji miti na ukulima wa mseto ambao unaweza kupunguza mmomonyoko wa udongo na kuongeza ubora wa maji na udongo. Wakulima wanahimizwa wawe na mbinu ya kuondoa maji katika maeneo yanayopata mvua nyingi ili kuzuia uharibifu wa mimea. Uchimbaji wa mitaro ya kuondoa maji haya unaweza kuzuia mafuriko na pia mmomonyoko unaopoteza udongo wa juu wenye rutuba. Kuchanganya mchanga na mbolea ya shamba kunaweza kutayarisha udongo kwa unyonyaji wa maji.
   
  Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa wito kwa wakulima wote nchini kuzingatia ushauri kutoka kwa wataalamu wa kilimo ili kuondokana na usumbufu utakajitokeza katika msimu huu wa masika unaoendela nchini.
   
  Mamlaka ya hali ya hewa imewaomba watanzania kufuatilia utabiri wa saa 24, siku 10 pamoja na mwezi kama unavyotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania ili kujua hali inayotarajiwa kuwepo kwa kipindi chote hiki cha msimu wa mvua za masika.

  0 0  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akichokoza mada wakati wa kongamano la Elimu juu ya maafa katika jimbo hilo baada ya kukumbwa na mafuriko ,Kongamano lililofanyika katika shule maalum ya Viziwi na kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa,Vijiji na Vitongoji,Maofisa watendaji,Madiwani,wakuu wa idara mbalimbali katika jimbo hilo.
  Baaadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
  Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akichangia mada katika kongamano hilo ambalo alikuwa mgeni rasmi pia,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia na kulia Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.


  Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akichangia mada katika kongamano hilo lililotumika pia kuondoa itikadi za kisiasa huku akitoa wito kwa viongozi wote katika jimbo hilo kufanya kazi za maenedeleo bila ya kujali itikadi za kisiasa.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akichangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akielea namna ambavyo Wilaya hiyo ilivyopata athari kutokana na mvua zilizonyesha Aprily 24 na 25 mwaka huu.
  Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himbo ,Hussein Jamal akichangia mada katika kongamano hilo.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga,(kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji (katikati) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila wakiteta jambo wakati kongamano hilo.

  0 0

  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benno Sanga akifafanua kuhusu matumizi ya sheria ya manunuzi ya umma na umuhimu wake leo Jijini Dodoma.
  Baadhi ya Mawakili wa Serikali waliohudhuria semina hiyo wakisikiliza kwa makini mafunzo hayo yaliyofanyika leo Mjini Dodoma.

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  Serikali imezitaka taasisi zake zote kufuata sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na taratibu zake kwa manunuzi mbalimbali ya vifaa vya ofisi ili kuhakikisha fedha iliyotumiwa inalingana na huduma iliyopatikana.

  Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benno Sanga kwenye Mafunzo ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 kwa Mawakili wote nchini iliyofanyika mjini Dodoma.Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yamelenga kuwapa mawakili ujuzi katika utoaji mzuri wa ushauri wa kisheria kwa Taasisi za Serikali.

  Wakili Mwandamizi Sanga alisema kuwa msingi mkubwa wa sheria hiyo ni ushindanishwaji wa wazabuni unaoweza kuiletea Serikali thamani ya fedha.“Kila taasisi ya serikali lazima ifuate sheria ya manunuzi kwa manunuzi mbalimbali ya vifaa vya ofisi,sheria hii imeweka utaratibu wa kuhakikisha fedha iliyotumiwa inalingana na huduma inayopatikana”,alisema Sanga

  Akitoa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mikataba (Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) Bi.Monica Otaru alisema mafunzo hayo yatawasaidia mawakili kufanya upekuzi wa mikataba kwa makini na uhakika zaidi.“Pamoja na kuwa kazi ya kupekua mikataba ni sehemu ndogo ya kazi zetu lakini inachukua muda mwingi, hivyo mafunzo haya yatawaandaa Mawakili wa Serikali walioko katika Ofisi za Kanda kuweza kufanya upekuzi wa mikataba kwa umakini na uhakika zaidi”,alisema Bi. Otaru.

  Aidha, Bi. Otaru amezitaja baadhi ya changamoto zinazosababisha kazi ya uhakiki wa mikataba kutofanyika kwa usahihi zikiwemo za mikataba kukosa maelezo na maoni kamili ya taasisi husika.Alitaja changamoto nyingine kuwa ni gharama za kusafirisha mikataba kutoka taasisi husika,ugumu wa njia za mawasiliano pamoja na kutoshirikishwa kwa taasisi husika katika mchakato wa manunuzi na uandaaji wa mikataba.

  Naye Wakili wa Serikali Mwandamizi Divisheni ya Mikataba, Said Kalunde ameelezea juu ya mambo muhimu ya kuzingatia katika kufanya upekuzi wa mikataba ya ununuzi ikiwemo ujazaji wa fomu mbalimbali zinazotumika katika uhakiki wa mikataba kwa mujibu wa Sheria hiyo ya manunuzi.

  “Ni muhimu sana kwa wakili kujiridhisha kama taratibu za ujazaji wa fomu zimefuatwa na fomu zimejazwa kwa usahihi,endapo wakili hatojiridhisha kwa kuhakiki fomu hizo huenda akapatwa na matatizo makubwa ya kiutendaji”,alisema Kalunde.Mafunzo hayo yametolewa kwa mawakili wa serikali divisheni ya mikataba ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza jukumu la kuhakiki mikataba inayotokana na wazabuni.

  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeundwa chini ya kifungu cha 59 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mshauri wa masuala ya kisheria kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya kifungu cha 59(3) cha Katiba ya mwaka 1977.

  0 0
 • 05/17/16--01:10: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

 • 0 0

  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London
  Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kikiongozwa na Mubelwa Bandio toka Beltsville Maryland, USA, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.

  Ni Tanzania kutoka jicho la DIASPORA
  Na katika kipindi cha juma hili, tulizungumza na Chris Lukosi, ambaye alitupa muhtasari wa ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa huko nchini Uingereza.
  Muhtasari huo ulizua na mjadala mkali juu ya ahadi za serikali kuhusu vibali maalum kwa waTanzania waishio nje ya nchi.
  Karibu

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya Novatus Makunga na Kamanda wa Polisi ,Wilbroad Mutafungwa wakati wakimngojea mmiliki wa ghala hilo.
  Mmiliki wa ghala la kuihifadhia bidhaa za kampuni ya Marenga Investment,Joseph Kimosso (katikati) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa Saidi Mecky Sadicky mara baada ya kuwasili katika ghala hilo.
  Sehemu ya Mchele ukiwa katika gunia .
  Mmiliki wa Ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali za kampuni ya Marenga Investment,Joseph Kimosso akiumuongoza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky kutembelea maeneo zilipohifadhiwa bidhaa mbalimbali.

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akitembelea kukagua ghala la kampuni ya Marenga.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akikagua moja ya bidhaa ili kujua endapo muda wake wa matumizi umemalizika ama la.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akikagua sukari ilifungwa katika mfuko maalum ya uzito wa Kg 2 alipotembelea Super Market ya Marenga iliyopo Kiboriloni mjini Moshi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akizungumza na wateja waliofika katika duka la Marenga kwa ajili ya kununua Sukari.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akitoka katika Duka la Marenga Investment.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiagana na mmiliki wa kampuni ya Marenga Investment ,Joseph Kimosso baada ya kutembelea Maduka ya kampuni hiyo pamoja na kufanya ukaguzi katika maghara ya kampuni hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwasili katika ghala la kuhifadhia bidhaa la Kampuni ya Marenga Investment alipofanya ziara ya ghafla kwa lengo la kujionea hali ya upungufu wa sukari pamoja na kufanya ukaguzi mwingine.aliiongozana nao ni kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwa katika ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali la kampuni ya Marenga Investment.kulia ni kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa.
  Mifuko ya Sukari iliyopo katika ghala hilo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwana Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa wakimngojea mmiliki wa Ghala hilo .
  Sehemu ya Sukari inayozalishwa na kampuni ya sukari ya TPC ikiwa katika mifuko ya kilogramu 2.
  Sehemu ya bidhaa ya unga ikiwa katika Ghala hilo.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Halmashauri ya Kahama kufanya kazi saa 24.

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

  SERIKALI imekanusha madai kuhusu mashine za kukoboa mpunga na mahindi katika Halmashauri ya Mji wa Kahama kufanya kazi wakati wa usiku au saa 24.

  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salome Makamba ambaye alitaka kujua utayari wa Serikali kuviruhusu Viwanda Wilayani Kahama kufanya kazi masaa 24 ili kufidia uzalishaji uliokuwa haufanyiki kipindi umeme unapokatika wakati wa mchana.

  Akijibu swali Mhe. Jafo amesema kuwa, Serikali haijatoa zuio lolote kwa Halmashauri hiyo kwa mashine za kukoboa nafaka kufanya kazi nyakati za usiku ambapo amefafanua kuwa changamoto iliyopo ni kwamba viwanda hivyo vinatumia umeme wa jenereta ambao umekuwa hautoshelezi kuendesha mashine wakati wote hali iliyopelekea kuwepo kwa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.

  “Halamshauri imewasiliana na Meneja wa Shirika la Ugavi Umeme Tanzania (TANESCO) Kahama na yatari tatizo hilo limeanza kushughulikiwa ili kupata umeme wa uhakika kutoka Gridi ya Taifa ambapo tayari kituo cha usamabazaji kimeanza kujengwa Kahama”, alisema Mhe. Jafo.

  Ameongeza kuwa, Halmashauri wilayani hapo inahamasisha Wawekezaji wa viwanda vidogo vikiwemo vya kukoboa mpunga, mahindi pamoja na mazao mengine ili kupanua wigo wa mapato kupitia ushuru wa huduma (Service Levy) na ajira kwa vijana.

  “Hakuna sababu yoyote kwa Serikali kuzuia wawekezaji katika viwanda vidogo na vikubwa, azma ya serikali ni kupanua uwekezaji wa viwanda kadri iwezekanavyo kwa kuzingatia fursa zilizopo, tunachofanya ni kuboresha mazingira yatakayosaidia uwekezaji huo kufanyika kwa faida ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba umeme wa uhakika unakuwepo.

older | 1 | .... | 848 | 849 | (Page 850) | 851 | 852 | .... | 1898 | newer