Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 847 | 848 | (Page 849) | 850 | 851 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Matairi ya Magari aina ya BF Goodrich KO2 yanayosambazwa na kampuni ya Superdoll baada kuwasili katika kituo cha kisasa cha huduma za magari na Matairi cha Superdoll mjini Arusha kwa ajili ya kuzindua rasmi kituo hicho. Kusshoto Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza kitufe na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif alipokua akizindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif baada ya kuzindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Makamanda wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Vikundi vya Ngoma za aina mbalimbali alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita.
  (Picha na OMR)

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa sana na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo. (It’s a serious graft that needs concerted efforts).

  Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Bibi Justine Greening walipokutana kwenye mkutano huo uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

  Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, alimweleza Bibi Greening kwamba viongozi wa Serikali wa awamu ya tano wameamua kwa dhati kupambana na kila ovu linalotokana na janga la rushwa na pia wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

  “Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi kwelikweli na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga vita rushwa ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongozi mwa watu wetu,” alisema.

  Alipoulizwa ni kitu kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hii, Waziri Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe ama kupokelewa (prevention), kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.

  “Serikali inachukua hatua za kiutawala na kisheria kama vile kuanzisha mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi mwezi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.

  Kwa upande wake, Bibi Greening alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalum wa kushiriki mkutano huo kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na Serikali.

  Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa nia ambayo Serikali ya awamu ya tano imeionyesha katika kuwa na mpango wa kuendeleza viwanda.

  Pia alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania kwenye mpango wake ilionao wa kupeleka umeme vijijini (Rural Electrification Programe). “Tuko tayari kuwasiidia kutekeleza mpango huu kupitia taasisi ya Energy Africa Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID),” alisema.

  Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya kimataifa, Bibi Sarah Sewall ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa na kusisitiza kwamba makampuni mengi ya Marekani yana nia ya kuja kuwekeza Tanzania.

  “Ninaamini uwekezahji huu utasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu wetu. Tunampongeza Rais Dk. Magufuli kwa juhudi anazofanya na nipende kusisitiza kwamba ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani utaendelezwa katika maeneo yetu ya siku zote,” alisema.

  Waziri Mkuu alimshukuru Bibi Sewall na kumsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali zikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini na kuhakiksha kuwa Watanzania wanajifunza teknolojia mpya na za kisasa.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAMOSI, MEI 14, 2016.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje akiwahutubia Wauguzi wa Hospitali Teule ya Mvumi, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma 14 Mei, 2016 wakati wa wakiadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani.Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Farida Mgomi (mwenye hijabu) akiwahutubia Wauguzi wa Hospitali Teule ya Mvumi, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma 14 Mei, 2016 wakati wa wakiadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani.

  ………………………………………………………………………………..

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

  Wauguzi Wilayani Chamwino pamoja na wengineo nchini wamepewa pongezi kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa wa kutoa huduma ya afya kwa jamii ikiwemo kuendeleza huduma hiyo nchini.

  Pongezi hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje katika Hospitali Teule ya Mvumi iliyopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati alipomwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.

  Mhe. Lubeleje amesema kuwa bila kuwepo kwa wauguzi huduma ya afya ingeyumba kutokana na ukweli kwamba Wauguzi hao ni zaidi ya asilimia 60 ya Watumishi wote wa sekta ya afya ambapo wanatekeleza asilimia 80 ya shughuli zote za afya.

  Amefafanua kuwa, Wauguzi ndiyo wenye kuandaa mazingira mazuri kwa daktari kutekeleza majukumu yake kwani baada ya daktari kumaliza kumuona mgonjwa na kutoa maelekezo yake, muuguzi husimamia utekelezaji wa maelekezo hayo pamoja na tiba na huduma kwa mgonjwa husika.

  Ameongeza kuwa, mara nyingi muuguzi ndiye anayefanya kazi ya kuuguza mgonjwa kwani wagonjwa wengi hutumia muda mwingi wakiwa mikononi mwa wauguzi kuliko wanaoutumia mikononi mwa wahudumua wengine wa sekta ya afya.

  Aidha, Mhe. Lubeleji amewapongeza wauguzi hao kutokana na kaulimbiu yao katika Maadhimisho ya Wauguzi Duniani isemayo “Wauguzi; Nguvu ya Mabadiliko: Uboreshaji wa uthabiti wa mifiumo ya afya”ambapo amesema kwamba ni kaulimbiu katika wakati muafaka kwakuwa wauguzi wana nafasi maalum katika maendeleo ya huduma ya afya na sekta yenyewe kwa ujumla.

  “Ni chachu muhimu ya mabadiliko katika sekta ya afya, na ndiyo rasilimali ya kuwawezesha uboreshaji wa uthabiti wa mifumo ya afya”, alisema Mhe. Lubeleje.

  Akifafanua baadhi ya changamoto zinazoikabili Hospitali Teule ya Mvumi wilayani hapo, alisema kuwa Serikali inaelewa kuhusu mchango wa wauguzi na inauthamini kwa kiasi kikubwa, vile vile amewahakikishia wauguzi hao kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma wakiwemo wa afya, hususani katika masuala ya mishahara na posho mbalimbali.

  “Maombi yenu nimeyapokea na ninaahidi nitayawasilisha kwenye Mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji, yale yanayotuhusu, kama Bunge tutayachukua pia na kuisimamia Serikali ili iyatekeleze na hatimaye tuimarishe huduma za uuguzi na afya kwa ujumla”, alisema Mhe. Lubeleje.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Farida Mgomi amewasisitiza Wauguzi wilayani hapo kujituma kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma ya afya kwa jamii kwani Serikali ya Awamu ya Tano inahitaji mabadiliko yanayoendana na kasi ya “Hapa Kazi tu” kwa kuwahudumia wananchi nchini.

  Aidha, amewapongeza kwa juhudi zao na maarifa katika kazi yao na kuwahakikishia kuwa Serikali itazidi kushirikiana nao katika kuleta maendeleo katika sekta hiyo na kusimamia vema katika masuala yao mbalimbali.

  Sikua ya Wauguzi Duniani huadhimishwa tarehe 12 Mei kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwanzilishi wa Uuguzi Bi. Florence Nightngale aliyezaliwa tarehe 12 Mei, 1820 na kufariki mwaka 1910.

  0 0

  Mwili wa marehemu ukiingizwa katika msikiti wa Al Maamur Upanga jijini Dar es salaam leo tayari kwa kuswaliwa kabla ya mazishi.
  Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimfariji  baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi. 
  Mama wa marehemu (aliyevaa nguo nyeupe) akiwa na ndugu wa karibu wakiomboleza. 
  Baba wa marehemu akiwa na viongozi wa dini wakiombea mwili wa marehemu dua.
  Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na ndugu wa marehemu. 
  Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akipata chakula.
  Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwasili msibani Wazo hill akiwa  na baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
  Baba wa marehemu akiwa na Balozi Cisco Mtiro na baadhi ya waombolezaji.
  Baba wa marehemu (mwenye kofia), Ankal Issa Michuzi akipewa pole na baadhi ya waombolezaji mara baada ya maziko ya mtoto wake Maggid Muhidin Michuzi (18)yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpa pole Issa Michuzi.
  Rais Mstaa mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akimfariji Ankal Issa Michuzi.
  Issa Michuzi (mwenye kofia) akifuatiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe Ombeni Sefue. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi  John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo wakati maziko.
  Waumini wakiomba dua.
  Baba wa marehemu Issa Michuzi (katikati) akiwa na huzuni akiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde 
  Baba mkubwa wa marehemu, Ismail Issa Michuzi akitoa shukrani kwa walioshiriki mazishi ya mtoto wao.
  Mroki Mroki ambaye aliyekuwa MC akitoa muongozo wakati wa mazishi.
  Waombolezaji wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka udongo.
  Waziri Mkuu mstaafu Jaji  Joseph Sinde Warioba akiweka udongo kaburini.
  Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
  Baba wa marehemu Ankal  Issa Michuzi akiweka udongo kaburini.
  Mwili wa marehemu ukiwekwa kaburini.
  Mwili ukiwasili makaburini.

  Rais mstaafu Jakaya Kikwete akimpa pole baba wa marehemu, Ankal  Issa Michuzi. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi  John Kijazi. Picha zote na Francis Dande

  0 0


  Msimamizi wa mradi wa “Tourism Destination Portal” Bw. Rossan Mduma akitoa maelezo kuhusu mradi huo.


  Mmiliki wa Udzungwa Falls Lodge, Bw. Patric (katikati) akitoa neno la shukrani kwa washiriki wa semina hiyo na (kulia) Bi. Mackey Mbotto, Marketing and Sales Executive.


  Ndau wa Utalii, Bw. Joel Samuel akifunga semna.


  Washiriki wa Semina wakifuatilia maelezo yalikuwa yanatolea na Bw. Rossan Mduma

  Washiriki wa Semina wakifuatilia maelezo yalikuwa yanatolea na Bw. Rossan Mduma .

  Baadhi ya Wadau wa utalii wanaojihusisha na kutoa huduma mbalimbali za malazi na usafiri kwenye maeneo ya vivutio vilivyopo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania, wamehudhuria semina kuhusu namna watakavyoweza kushirikiana kuvitangaza vivutio hivyo.
  Washiriki wa semina hii iliyoandaliwa na Udzungwa Falls Lodge, waliipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kuweza kuanzisha tovuti “Tourism Destination Portal” inayotoa fursa kwa mtalii kuweza kupata taarifa za utalii wa Tanzania, kufanya malipo ya malazi kupitia mfumo uliyounganishwa kwenye tovuti hiyo.
  Akitoa ufafanuzi wakati wa semina iliyofanyika leo tarehe 14/5//2016.katika Ukumbi wa Mikutano wa Makumbusho ya Taifa, Msimamizi wa Mradi wa Tourism Destination Portal, Bw. Rossan Mduma aliwasisitizia wadau kushirikiana na Bodi katika kutangaza Utalii kwa njia ya TEHAMA pamoja na kuweka matangazo yao kwwenye tovuti hiyo.
  wanaojihusisha na kutoa huduma mbalimbali za malazi na usafiri kwenye maeneo ya vivutio vilivyopo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania, leo hii tarehe wameshiriki semina ya siku moja iliyokusudia kujadili namna ya watakavyoweza kushirikiana katika kuutangaza utalii wa kanda ya kusini.

  0 0


  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV Magogoni umeanza rasmi mara baada ya kusitisha huduma zake hivi karibuni.

  Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la bandari kujionea kazi ya ukarabati kwa kivuko hicho, Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole-kujan amesema kazi ya ukarabati wa kivuko hicho umeanza kwa hatua za awali za kukifanyia usafi ili kuona maeneo yaliyoharibika na kuyafanyia ukarabati.

  “ Muda wake wa matengenezo umefika na ni wakati muafaka kwa kivuko kufanyiwa matengenezo ni muda mrefu kimehudumia wananchi wa Jiji la Dar es Salaam lakini mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kitarudi kutoa huduma kama kawaida” Alisema Mhandisi Manase.

  Mhandisi Manase ameongeza kuwa ukarabati huo utazingatia viwango vya kimataifa ili kukiwezesha kivuko hicho kudumu kwa muda mrefu bila ya kupatwa na hitilafu yoyote ya kiufundi na kuwaasa wahandisi husika kufanya ukarabati huo na kukamilika kwa muda uliopangwa.

  Aidha Mhandisi Mkuu Kutoka kampuni ya Songoro Marine Boat yard LTD Major Songoro amesema kwa kushirikiana na waandisi kutoka TEMESA watahakikisha wanamaliza kazi ya ukarabati kwa wakati na kwa ufanisi wa hali juu ili kurejesha huduma ya Kivuko hicho.

  Kivuko cha MV Magogoni kinachotoa huduma eneo la Magogoni na Kigamboni Jijini Dar es Salaam kimesitisha kutoa huduma kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo makubwa na kwa sasa kivuko cha MV Kigamboni kinashirikiana na MV. Lami kutoa huduma kwa wananchi.

  0 0

  Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi  inapenda kutoa  shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita  na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.

  Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.

  Pamoja  na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na  familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi  Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue  pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa  kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...


  Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi  wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...


  Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote.  ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...


  Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani  za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
  Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba  mfiwa Ankal ni mwanachama. 

  Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, Ruby 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na  Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani pamoja na Ras Makunja Na Ngoma Afrika Band wa Ujerumani na Jeff Msangi wa Canada. 

  TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA  KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
  Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.


  HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...


  Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

  AMIN!


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimuaga Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela kabla ya kuondoka Tanga, kwenda mkoani Kilimanjaroleo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akikabirishwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martin Shigella, baada ya kuwasili kwenye Ofisi wa mkuu wa mkoa huyo, kuwasilisha kero za Wananchi, baada ya kuzungumza na wanachama wa CCM shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama wilaya ya Tanga mjini leo.
  Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella akimpeleka Ofisini kwake, Luhwavi. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiwasili ndani ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi akisaini kitabu cha Wagemi katika Ofsi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga baada ya kuwasili na ujumbe wake katika ofisi hiyo leo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela
  Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela akifurahi baada ya kukabidhiwa risara yeneye kero za wananchi na wanachamawa CCM Shina namba kumi, tawi la CCM Usagara Mashariki, na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi
  LUhwavi akiwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela kabla ya kuondoka.
  Luhwavi akiagana na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela kabla ya kuondoka
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela kabla ya kuondoka Tanga, kwenda mkoani Kilimanjaroleo

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje akiwahutubia Wauguzi wa Hospitali Teule ya Mvumi, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma 14 Mei, 2016 wakati wa wakiadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani.

  Na Benedict Liwenga, Dodoma.

  Wauguzi Wilayani Chamwino pamoja na wengineo nchini wamepewa pongezi kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa wa kutoa huduma ya afya kwa jamii ikiwemo kuendeleza huduma hiyo nchini.

  Pongezi hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje katika Hospitali Teule ya Mvumi iliyopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakati alipomwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.

  Mhe. Lubeleje amesema kuwa bila kuwepo kwa wauguzi huduma ya afya ingeyumba kutokana na ukweli kwamba Wauguzi hao ni zaidi ya asilimia 60 ya Watumishi wote wa sekta ya afya ambapo wanatekeleza asilimia 80 ya shughuli zote za afya.

  Amefafanua kuwa, Wauguzi ndiyo wenye kuandaa mazingira mazuri kwa daktari kutekeleza majukumu yake kwani baada ya daktari kumaliza kumuona mgonjwa na kutoa maelekezo yake, muuguzi husimamia utekelezaji wa maelekezo hayo pamoja na tiba na huduma kwa mgonjwa husika.

  Ameongeza kuwa, mara nyingi muuguzi ndiye anayefanya kazi ya kuuguza mgonjwa kwani wagonjwa wengi hutumia muda mwingi wakiwa mikononi mwa wauguzi kuliko wanaoutumia mikononi mwa wahudumua wengine wa sekta ya afya.

  Aidha, Mhe. Lubeleji amewapongeza wauguzi hao kutokana na kaulimbiu yao katika Maadhimisho ya Wauguzi Duniani isemayo “Wauguzi; Nguvu ya Mabadiliko: Uboreshaji wa uthabiti wa mifiumo ya afya” ambapo amesema kwamba ni kaulimbiu katika wakati muafaka kwakuwa wauguzi wana nafasi maalum katika maendeleo ya huduma ya afya na sekta yenyewe kwa ujumla.

  “Ni chachu muhimu ya mabadiliko katika sekta ya afya, na ndiyo rasilimali ya kuwawezesha uboreshaji wa uthabiti wa mifumo ya afya”, alisema Mhe. Lubeleje.Akifafanua baadhi ya changamoto zinazoikabili Hospitali Teule ya Mvumi wilayani hapo, alisema kuwa Serikali inaelewa kuhusu mchango wa wauguzi na inauthamini kwa kiasi kikubwa, vile vile amewahakikishia wauguzi hao kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma wakiwemo wa afya, hususani katika masuala ya mishahara na posho mbalimbali.

  “Maombi yenu nimeyapokea na ninaahidi nitayawasilisha kwenye Mamlaka husika kwa ajili ya utekelezaji, yale yanayotuhusu, kama Bunge tutayachukua pia na kuisimamia Serikali ili iyatekeleze na hatimaye tuimarishe huduma za uuguzi na afya kwa ujumla”, alisema Mhe. Lubeleje.Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Farida Mgomi amewasisitiza Wauguzi wilayani hapo kujituma kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma ya afya kwa jamii kwani Serikali ya Awamu ya Tano inahitaji mabadiliko yanayoendana na kasi ya “Hapa Kazi tu” kwa kuwahudumia wananchi nchini.

  Aidha, amewapongeza kwa juhudi zao na maarifa katika kazi yao na kuwahakikishia kuwa Serikali itazidi kushirikiana nao katika kuleta maendeleo katika sekta hiyo na kusimamia vema katika masuala yao mbalimbali.Sikua ya Wauguzi Duniani huadhimishwa tarehe 12 Mei kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwanzilishi wa Uuguzi Bi. Florence Nightngale aliyezaliwa tarehe 12 Mei, 1820 na kufariki mwaka 1910.

  0 0

  WADAU wa ardhi, mazingira na mambo ya misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba Group wameweka adhma ya kupanda miti milioni 50,000,000 ifikapo mwaka 2020, ikiwa ni mipango yao ya kutunza mazingira na kujikwamua kiuchumi kwa kupitia sekta ya misitu nchini.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, akizungumza jambo katika mkutano wa wanachama wa Maisha Shamba Group wanaojihusisha na mambo ya misitu na mazingira mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa na kiongozi mkuu wa group hilo, Asifiwe Malila, alipokuwa akizungumza na wanachama wake katika mkutano wao wa mwaka, huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, mwishoni mwa wiki, katika Ukumbi wa Shule ya Sheria Tanzania, jijini Dar es Salaam.
  Mdau wa mambo ya ardhi na misitu, Ally Abdallah, akisikiliza kwa makini hutuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, hayupo pichani katika mkutano wa wadau wa misitu wanaojulikana kama Maisha Shamba Group.

  Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, aliwapongeza wadau hao wa mambo ya misitu, akiwataka waendelee kubuni mambo yanayoweza kuwakwamua na kuisaidia nchi katika kutunza mazingira kwa kupitia sekta ya misitu.
  Mheshimiwa January Makamba wakati anaingia eneo la Mkutano huo. Kulia kwake ni mdau wa ardhi na misitu, Ally Abdallah.

  Akizungumzia adhma hiyo, Malila alisema lengo lao linatokana na kujidhatiti kujikwamua kiuchumi kwa kupitia misitu pamoja na utunzani wa mazingira, huku wanachama wote wa group hilo wakimiliki miti 14,000,000, katika wilaya mbalimbali nchini Tanzania.
  Wadau hao wa misitu wakifuatilia mkutano huo kwa umakini.

  “Kwa pamoja tuna mipango kabambe ya kuhakikisha kwamba tunajikita zaidi katika kilimo cha miti, mifugo kama njia ya kukuza uchumi wetu, ndio maana tumeamua kuungana kwa pamoja kushirikiana kwa hali na mali katika sekta hii muhimu,” alisema Malila, katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kujadili muungano wao huo sanjari na kupitisha rasmi rasimu ya Katiba kama njia ya kusajili jumuiya kwa ajili ya kujiwekea malengo ya juu kisheria.
  Mheshimiwa January Makamba akizungumza na wadau hao wa misitu, ardhi na mazingira.

  Makamba alisema serikali itashirikiana na wadau hao wa misitukwa nguvu zote, huku akiwataka washirikiane na viongozi wao, wakiwamo wabunge, ikiwa ni hatua nzuri ya wizara yake kujiandaa kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya mazingira, kuuboresha mfuko wa Taifa wa Mazingira, sanjari na kuuwekea ubora wa utendaji kazi wake, tangu ulipoanzishwa rasmi nchini Tanzania mwaka 2004.

  “Mwaka huu zimetengwa Sh Bilioni 2 kwa ajili ya Mfuko wetu wa Taifa wa Mazingira uweze kufanya kazi, ingawa mahitaji ni zaidi ya sh Bilioni 100, ambapo tunajaribu kutafuta mbinu za kuweza kuzipata fedha hizo kwa sababu mazingira ni jambo nyeti duniani kote, hivyo naamini serikali yetu itashirikiana na wadau wote ili nchi yetu ipige hatua.

  “Endapo tutakuwa na sera mpya, mabadiliko ya sheria pamoja na fedha, hakika yote tunayokusudia tutayafanya kwa wakati muafaka, sanjari na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira ili sekta hiyo iweze kunufaisha nchi pamoja na wananchi wake, wakiwamo wadau wanaojihusisha na mambo ya mazingira kwa namna moja ama nyingine,” alisema Makamba.

  Aidha wanachama hao wa Maisha Shamba Group walitumia muda huo kumuomba Makamba na wizara yake kuweka utaratibu mzuri na rahisi kwa ajili ya wanachama hao wapewe mapori ya serikali ili wayaendeleze, mafanikio yao yarekodiwe, mashamba yao yapimwe na wataalamu wanaopatikana katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, ili iwe njia ya kufanikisha adhma yao ya kuhakikisha kwamba sekta hiyo inapiga hatua nchini.

  0 0

   Mafundi wa Kampuni ya Songoro Marine Boat yard Ltd wakiendelea na kazi ya ukarabati  wa kivuko cha Mv Magogoni kilichosimamisha huduma zake kwa ajili ya ukarabati mkubwa.(Picha na Theresia Mwami – TEMESA)


  0 0

  Na Mwandishi Maalum  – Dodoma.


  16/5/2016 Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wameiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

  Ombi hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kamati hiyo Hashim Lundenga wakati akiongea na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokutana nao mjini Dodoma.

  Lundenga alisema changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa ni kupata ufadhili wa mashindano hayo ambayo yanafaida kwa mabinti wanaoshiriki hii ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa kuwa viongozi wazuri wa baadaye.

  “Mwezi wa tisa warembo wanatarajiwa kuingia kambini watakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja ambako watapewa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja kufundishwa jinsi ya  kujitambua na kujiendeleza kielimu”, alisema Lundenga.

  Kwa upande wake Mhe. Wambura aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kuandaa mashindano hayo na kuwaahidi kushirikiana nao ili  kuhakikisha mashindano yanafanyika kama ilivyotarajiwa.

  Mhe. Wambura alisema, “Nawapongeza washiriki wa mashindano haya walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia kwani wameweza kushika nafasi nzuri katika mashindano ya makundi mbalimbali pia hawajawaangusha waandaaji wa mashindano kwa kuwa wanaendelea kuisaidia jamii inayowazunguka.

  Naye Miss Tanzania,  Lilian Kamazima  alimshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kukubali kukutana nao na kusema kuwa mashindano hayo yanaumuhimu mkubwa lisha ya washiriki kupewa zawadi mbalimbali  lakini pia   wakiwa katika maandalizi ya mashindano  wanafundishwa jinsi ya kuwa wanawake wa kuigwa katika jamii, kuishi na kuisaidia jamii inayowazunguka.


  Mashindano ya Miss Tanzania Taifa yanatarajiwa kufanyika mwezi wa kumi, hivi sasa mashindano ya vitongoji (Vituo) yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini baada ya hapo yatafuatiwa na mashindano ya Kanda.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA.
   JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
  WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUFANYIKA MSAKO ENDELEVU WA KUSAKA NA KUKAMATA WAHALIFU JIJINI MWANZA.

  MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AMEFARIKI DUNIA NA MWINGINE KUJERUHIWA VIBAYA BAADA YA PIKIPIKI ZAO KUGONGANA.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA.
  KATIKA MISAKO INAYOENDELEA YA KUSAKA NA KUKAMATA WAHALIFU JIJINI MWANZA JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATU WAWILI AMBAO NI CHACHA MWITA MIAKA 34 NA RASHIDI MOHAMED MIAKA 33 WOTE WAKAZI WA KITANGIRI WAKIWA NA BHANGI MISOKOTO SITA (6) KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI ZINAVYOELEKEZA. MSAKO HUO UMEFANYIKA MNAMO TAREHE 14.05.2016 MAJIRA YA SAA 14.05HRS KATIKA KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA.

  ASKARI POLISI WAKIWA KWENYE DORIA WALIWEZA KUFANIKIWA KUPATA TAARIFA ZA WATU HAO, AMBAO WALIKAMATWA NA SASA WAPO KITUO CHA POLISI KWA MAHOJIANO KWA AJILI YA KUWEZA KUPATA TAARIFA ZA WATU WENGINE ZAIDI WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HIYO HARAMU. PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI AMESEMA  “KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA UHALIFU WA AINA HIYO HAPA MKOANI MWANZA JESHI LA POLISI LINAFANYA MISAKO ENDELEVU YA KUSAKA NA KUKAMATA WAHALIFU KATIKA SEHEMU ZOTE”, HIVYO TUNAOMBA USHIRIKIANO NA WANANCHI WENYE TAARIFA ZA WATU WANAO JIHUSISHA NA BIASHARA HIYO ILI TUWEZE KUWAKAMATA. 

  KATIKA TUKIO LA PILI
  MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI AMEFARIKI DUNIA NA MWENGINE KUJERUHIWA VIBAYA ALIJULIKANA  KWA JINA LA STANLEY MAIMU MIAKA 24 MKAZI WA MABATINI  BAADA YA  PIKIPIKI ZAO KUGONGANA.

  AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.05.2016 MAJIRA YA SAA 15:30HRS KATIKA BARABARA YA NYERERE ENEO LA MABATINI SINAI WILAYA YA NYAMAGANA MKOA WA MWANZA AMBAPO PIKIPIKI NAMBA T.451 BBR AINA YA SANYA IKIENDESHWA NA STANLEY MAIMU ILIGONGANA NA PIKIPIKI NAMBA T.580 CBY AINA YA SANLG AMBAPO MTU ALIYEKUWA AKIIENDESHA PIKIPIKI HIYO ALIFARIKI PAPO HAPO NA KUPELEKEA KUSHINDWA KUFAHAMIKA JINA LAKE PAMOJA NA MAKAZI.

  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI KWA WAENDESHA PIKIPIKI WOTE WAWILI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUAGANDO NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA MATIBABU LAKINI HALI YAKE BADO SIO NZURI.
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI AMETOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO HASWA WAENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALA BARABARANI ILIKUWEZA KUZUI AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
  IMESAINIWA NA:
  SACP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

  0 0

  --

  0 0
 • 05/16/16--04:25: MATUKIO BUNGENI LEO.
 •  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) pamoja na Mbunge wa Viti Maalul CCM, Mhe. Halima Bulembo wakielekea Bungeni kwa jili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba, Mhe. Najma Giga wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini Dodoma.
   Baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya bunge hususan kusikiliza Bajeti ya Wizara ya Mambo y Ndani ya Nchi 16 Mei, 2016 mjini Dodoma.
   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kulia) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini Dodoma
  PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.

  0 0

  Meneja wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Devotha Rubama (katikati) akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kuisaidia taasisi Tushikamane Pamoja jijini Dar es Salaam jana (kulia) ni Meneja Mahusiano na Mauzo wa Toyota Tanzania, Kadiva William. Taasisi ya Karimjee Jivanjee ilichangia shilingi milioni 10.

   Meneja wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Devotha Rubama (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi Mwenyekiti wa Taasisi ya Tushikamane Pamoja inayoshughulika na kutoa huduma kwa wazee, Rose Mwapachu wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kuisaidia taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana (katikati) ni Meneja Mahusiano na Mauzo wa Toyota Tanzania, Kadiva William.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya Masikini kwa Nchi Jumuiya za Afrika uliofunguliwa leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.
   Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.    
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki kabla ya kufungua Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.                                                 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anaeshughulikia Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bibi. Bella Bird walipokutana katika ukumbi wa Mikutano wa Ngurudoto Mjini Arusha leo Mei 16, 2016, ambapo Makamu wa Rais alifungua mkutano wa kwanza wa TASAF kuhusu Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela  kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mikoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha. Katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe (Picha na OMR)     
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya  Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili yakukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mikoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha.katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe.

  0 0

  Naibu waziri wa maliasili na utalii Mh. Ramo Makani, Amesema serilikali ya awamu ya tano itahakikisha jamii zinazo ishi karibu na shamba la taifa la sao hill, lenye tarafa maalum (4) za Mgololo, Ihalimba, Ihefu na Irundi zinakuwa za kwanza kunufaika na mgao wa vibali vya uvunaji wa misitu ili zishiriki kikamilifu katika kulinda, kuhifadhi na kuiboresha misitu hiyo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

  Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imebainisha kuwa naibu waziri Makani ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi katika shamba la miti la Taifa la sao hill wilayani Mufindi Mkoani Iringa.

  Amesema, ili wananchi waone kuwa msitu huo ni mali yao kama Watanzania, ni lazima wawe wa kwanza kufikiriwa wakati wa ngao wa vibali vya uvunaji kupitia jumuia watakazo ziunda katika maeneo yao.

  Akizungumzia suala la  utoaji wa vibali vya uvunaji wa misitu amesema, msitu waSao Hill na mingine nchini ni mali ya Taifa, hivyo, ni haki kwa Mtanzania yeyote popote nchini kupata kibali na akasisitiza kuwa kwa mwaka huu huwenda vibali vikachelewa kutoka kwa kuwa wizara yake iyapiti maombi kwa umakini ili kupunguza malalamiko ya upendeleo katika utoaji vibali.

  shamba la Miti la Sao hill lililopo Wilayani Mufindi ni la kwanza kwa ukubwa nchini kati ya mashamba 18 ya Taifa, ilikiwa na hekita zaidi ya laki moja na 35 elfu na lilianzishwa rasmi mwaka 1960.

  0 0

  MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanza kutua mafunzo kwa madaktari nchi nzima kuhusu namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yanatosababishwa na kazi. Jumla ya madaktari 380 wa hospitali za rufaa mikoani na wilayani watafaidika na mafunzo hayo.

  Mafunzo yatatolewa kwa siku tano katika vituo vikubwa vinne ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. Wataalamu kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dr. Jacques Pelletier na Dr. Sylvie Thibaudeau ndio watakaoendesha mafunzo hayo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba amesema kwamba mafunzo haya ni hatua muhimu sana kwa Mfuko kwani Mfuko unaanza rasmi ulipaji wa mafao tarehe 01 Julai 2016 kwa Wafanyakazi wote watakaopata ajali au magonjwa kutokana na kazi. Miongoni mwa mafao yataayotolewa ni Huduma ya matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, Fidia kwa ulemavu wa kudumu, Ukarabati na ushauri nasaha, Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, gharama za mazishi endapo mfanyakazi atafariki na fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi pia atafariki.

  Bw. Masha Mshomba akifafanua dhumuni kubwa la kufanya haya mafunzo alisema, “Kazi kubwa ya madaktari hawa itakuwa ni kufanya tathimini ya magonjwa yanayotoka na kazi na kutupa ushauri wa kuendelea na malipo kama wahusika watakuwa wamepata ajali au kuugua na wakapata ulemavu”.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba akielezea malengo ya Mfuko na kazi zake, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kwenye jengo la LAPF jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016. Mafunzo hayo yanalenga kuwaelimjsha madaktari namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, SSRA., Bi. Irene Isaka, akitoa hotuba ya ufunguzi.

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  Baadhi ya washiriki wa mafnzo wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu.
   

  0 0


   Uelewa mdogo kuhusiana na sumu aina ya aflatoxin hapa Tanzania umesababisha vita dhidi yake kuwa na changamoto.

  Aflatoxins ni kemikali yenye sumu inayoweza kusababisha saratani; huzalishwa na aina ya fangasi wanaoishi katika udongo au mimea na nafaka zinazooza.Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka amesema hali hiyo inasababisha usalama mdogo wa chakula na kuhatarisha afya za walaji.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, hali hiyo sio tu inahatarisha afya za walaji, bali pia kuharibu biashara ya bidhaa za mazao hasa nafaka.Alikuwa akiongea wakati wa mkutano uliozungumzia mapambano dhidi ya sumu hiyo hapa nchini. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  Pamoja na mambo mengine, wajumbe wa mkutano huo walijadili namna bora ya kuhusisha mapambano ya sumu hiyo kwenye miradi, programu na mipango mbalimbali.Kwa sababu hiyo, Dkt. Turuka alisema, serikali itatoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha kuwa juhudi zote za mapambano dhidi ya aflatoxin zinafanikiwa.“Serikali itafanyia kazi mapendekezo ya mkutano huu ili kupata mafanikio,” alisema.

  Kwa mujibu wa kiongozi huyo, aflatoxin ni tatizo kubwa kwenye mfumo wa chakula hapa nchini hasa mahindi, karanga na maziwa.Vyakula hivi ni kati ya vinavyoliwa kwa wingi hapa nchini.Dkt. Turuka alisema bado juhudi kubwa zinatakiwa kufanywa ili kuondokana na tatizo hilo ambalo huweza kusababisha saratani ya ini.

  Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa maeneo ya ukanda wa Mashariki na Magharibi hapa nchini ndio yaliyoathirika zaidi na sumu hiyo katika mfumo wa vyakula.Aliishukuru Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa juhudi zake za kudhibiti aflatoxin na timu nzima ya Partnership for Aflatoxin Control in Africa (PACA) kwa kuratibu mkutano huo.

  Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wajumbe kutoka nchi za Gambia, Malawi, Senegal na Uganda.PACA inafanya kazi na serikali za Afrika katika kupambana na kudhibiti changamoto ya aflatoxin.

older | 1 | .... | 847 | 848 | (Page 849) | 850 | 851 | .... | 1897 | newer