Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 846 | 847 | (Page 848) | 849 | 850 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0


  Jana May 13,2016 Tanzania imeungana na Mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha "SIKU YA WAUGUZI DUNIANI" ambapo Kitaifa Maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Geita.

  Imeandaliwa na BMG

  Jijini Mwanza, Maadhimisho hayo yalifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambapo huduma yaliambatana na huduma mbalimbali ikiwemo wananchi kuchagia damu.

  Katika Maadhimisho hayo, Wauguzi katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza, walihimiza zaidi kuondolewa kwa matabaka yaliyopo baina yao na Watendaji wengine wa afya wakiwemo Madaktari kwa kupewa thamani sawa hususani kuboreshewa maslahi yao ikizingatiwa kwamba hakuna huduma bora ikiwa Wauguzi pamoja na Madaktari watafanya kazi bila ushirikiano.

  Uongozi wa Hospitali hiyo ulikiri kwamba Wauguzi ni watu muhimu katika sekta ya afya na kwamba mahitaji yao yataendelea kuboreshwa zaidi ili kuendana na umuhimu wao.
  Kauli Mbiu; Maslahi Bora kwa Wauguzi, Vifaa Tiba vya Kutosha, Chachu ya Kutoa Huduma Bora kwa Wagonjwa/Wateja.
  Baadhi wa Wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Manesi Duniani, ambapo waliiomba Hospitali hiyo kuondoa matabaka miongoni mwao na madaktari hususani kuboreshewa maslahi yao ikiwemo malipo ya muda wa ziada kazini kama ilivyo kwa Madaktari.
  Baadhi wa Wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Manesi Duniani, ambapo waliiomba Hospitali hiyo kuondoa matabaka miongoni mwao na madaktari hususani kuboreshewa maslahi yao ikiwemo malipo ya muda wa ziada kazini kama ilivyo kwa Madaktari.

  0 0

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akihitimisha majumuisho ya makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma usiku huu.
   Waziri Ummy Mwalim akipanga vizuri nyaraka tayari kuhitimisha majadiliano ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Viongozi wa wizara hiyo wakifuatilia majadiliano ya wabunge kuhusu bajeti hiyo.
   Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hamis Kigwangallah akijibu moja ya hoja za wabunge.

   Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo akichangia wakati wa majadiliano ya Bajeti ya wizara hiyo
   Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda (Chadema), Mkoa wa Mbeya, akichangia hoja wakati wa makadilio ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa iliyopitishwa bungeni Dodoma
   Naibu Waziri wa Afya, Hamisi Kigwangala akisalimiana na wanafunzi wanaosomea utabibu katika Chuo Kikuu cha Dodoma waliozuru bunge mjini Dodoma

   Mbunge akiingia bungeni Dodoma leo
   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), kushoto, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Anthony Komu (Chadema), walipokuwa wakiingia bungeni Dodoma
   Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga akitaniana na wanahabari (hawapo pichani) alipokuwa akiingia bungeni Dodoma. Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Ali Mwinyi.
   Wabunge wakiingia bungeni Dodoma

   Mbunge wa Segerea, akiichangia hoja wakati wa wizara ya Afya. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum,  Bupe Mwakang'ata.
   Mbunge wa Donge, Sadifa (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju (kulia). Kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Bunge wa Serikali, Jenista Mhagama.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina (wa pili kulia) akizungumza na wawakilishi wa wafugaji wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi waliofika bungeni Dodoma, kukutana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba kujadiliana jinsi ya kutatua tatizo la malisho.


  0 0

  Jumba la kifahari la mapumziko la Shirika la Ndege la Etihad Airways katika uwanja wa ndege wa Melbourne, Australia.

  Shirika la ndege la Etihad leo limefungua rasmi jumba jipya la kifahari kwa ajili ya kupumzikia abiria wake katika uwanja wa ndege wa Melbourne, Australia. Jumba hilo ni mahususi kwa kuwapatia abiria mazingira tulivu ambayo wanaweza kupumzika, kuongeza nguvu, kula, kufanya kazi au kuburudishwa kabla ya safari.

  Ni eneo ambalo limejawa na nuru ya asili yenye vioo tokea sakafuni hadi katika dari, inatoa mtazamo mpana wa eneo la kurukia ndege. Lina zaidi ya mita za mraba 800 yenye viti vya kukaa hadi kufikia wageni 133, ni nyumba ya kupumzika ya shirika la ndege la Etihad ambayo ni kubwa zaidi iliyoko nje ya Abu Dhabi.


  Sehemu ya katikati ya nyumba hii ya kupumzika ni eneo la kulia chakula lenye viti 26 vya ukaribu. Sehemu hii wageni watafurahia alama ya ukarimu ya shirika hili kwa kula katika Mgahawa unaotoa huduma ya chakula cha pekee na buffet la kimataifa.

   Wapishi wenye ujuzi wa hali ya juu huwepo pale muda wote wakipika kila chakula kwa kutumia bidhaa za msimu zilizokusanywa kwa njia ya kawaida. Hii inajumuisha mikate freshi ambayo inaokwa kila siku mara mbili, Grissini bradstick; ya kuchovya kama vile humus, Baba ghanoush na muhammara; piko; labneh; biskuti; na hata ice cream, Jibini, matunda na mboga za majani zinachukuliwa kutoka Victoria suppliers na kahawa inatoka kwa wakaangaji wa kahawa wa Melbourne.

  Sifa nyingine ya kipekee ni bar yenye picha za vinyago, iliyojaa mvinyo kutoka kwa watengenezaji wa Victoria na zaidi ya aina 70 ya vinywaji bora vikali, shamapeni na viamsha hamu. Muongozo wa kuagiza Cocktail pia unapatikana. Uchaguzi wa kibunifu, umetengenezwa kwa ushirikiano na washauri wa mambo ya vinywaji wanaoongoza kutoka London Fluid Movement, inajumuisha aina ya kipekee ya Cocktail yenye majina ya vituo mbalimbali kama Melbourne, Sydney, Paris na New York na Mock tail inayoitwa Abu Dhabi, Controlled Airspace na Winglet. Cocktail na Mock tails ya Controlled Airspace na Winglet. Kama ilivyo kwa vyakula vilivyoko katika orodha ya mwongozo iliyoko katika sehemu ya chakula, zote zimetengenezwa kwa mkono kwa kutumia wachanganyaji waliopitia mafunzo, wakitumia syrup na garnishes kama vile Candy floss na rhubarb zilizokaushwa ambazo zimetengenezwa ndani ya jumba hili na wataalamu wa jadi, bar inatoa uchaguzi wa kisasa, kama vile Mach 10 Majito, ambayo imegunduliwa na kutengenezwa na Fluid Movement. Wapenzi wa Negroni watafurahia kufahamu kuwa kiamsha hamu kimechanganywa, kikavundikwa na kuhifadhiwa nyuma ya bar.

  Ubunifu wa ndani, kanuni ya mtindo, nafasi na utulivu vimekamilishwa na shirika la ndege la Etihad kutoka kwenye bidhaa zake za kipekee za ‘Facets of Abu Dhabi’ ikiwa na mtindo wake wa kijiometri na rangi ambayo inapewa motisha na mandhari ya UAE, ni mwonekano wa kipekee wa karne ya 21 ya ubunifu wa Abu Dhabi.

  Fanicha za kitamaduni – zilizoandaliwa na Boss – zinawapatia wageni wa nyumba hii ya kupumzika uchaguzi wa mtindo wa kukaa, kila mmoja imebuniwa kwaajili ya kuongeza kiwango cha starehe na utulivu wakati wa kula, kufanya kazi na kupumzika.

  Pamoja na kuanza kwa huduma za A380 tokea tarehe 01 Juni, wageni katika daraja la makazi watafurahia upekee wa nyumba ya kupumzikia ya binafsi – ambayo imejengwa kwa makini kabisa kando ya lango kuu la kuingilia katika jumba la mapumziko. Ikiwa na viti vyenye mikono iliyofunikwa kwa ngozi ya Kiitalia ya Poltrona Frau, vilivyokamilishwa kwa vitambaa safi laini vya mahameli, chumba cha peke yake cha kupumzika na mlango wa kujitegemea, Nyumba ya kupumzika ya Daraja la Makazi ina huduma za kuagiza za kitajiri na huduma binafsi ambazo zinalingana na ukarimu wa kiwango cha juu wa shirika hili la ndege.

  Huduma nyingine katika Nyumba kuu ya kupumzikia inajumuisha vyumba tofauti vya kupumzika kwa ajili ya wanawake na wanaume vyenye mabafu pamoja na bidhaa za Scaramouche + Fandago, vyumba maalumu vilivyotengwa kwaajili ya wanawake na wanaume kuchukulia udhu na vyumba tofauti vya kuswalia na chumba cha watoto kucheza na chumba cha mizigo.

  Huduma ya Wi-Fi yenye kasi inakamilishwa na soketi za umeme ambazo zimewekwa kila mahali katika Nyumba ya kupumzikia.
  Makamu wa Rais katika Idara ya Masoko wa Shirika la ndege la Etihad bwana Shane O’Hare, aliyekata utepe wa sherehe akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Melbourne bwana Lyell Strambi katika ufunguzi rasmi leo alisema:

  “Nyumba mpya ya kupumzika ya kifahari iliyoko Uwanja wa ndege wa Melbourne ni daraja la peke yake – ni nyumba ya kupumzikia ya uwanja wa ndege kama ambavyo inajulikana, ambayo imeboreshwa kabisa.

  “Ikiunganisha Mgahawa bora wa chakula na Bar ya Cocktail, Nyumba hii ni maonesho ya ubunifu wa kiwango cha juu na umakini ambao wageni watafurahia kiwango cha juu cha utulivu na starehe, inayokamilishwa na ukarimu wetu wa kiwango cha kimataifa, ubunifu katika mapishi na teknolojia ya kiwango cha juu ya vinywaji.

  “Wakati huo huo, inakuletea hisia kali ya kitamaduni kwa jibini freshi na mvinyo – unaochukuliwa kutoka kwa wakulima, watengenezaji na wasambazaji katika jimbo lote la Victoria – ambayo inawapatia wageni wetu ladha ya kusisimua ya utamaduni na umaarufu wa upishi.

  “Ufunguzi wa huduma hii ya kustaajabisha na uzinduzi wa huduma yetu kuu ya A380 hapo tarehe 1 Juni, unawapa wageni wetu katika ruti ya Melbourne na Abu Dhabi uzoefu wa ushawishi wa huduma ya hali ya juu kuliko zote.”

  Wageni katika Makazi, Apartments za kwanza na Business Studios watakaribishwa kutembelea Nyumba ya kupumzikia kabla ya kusafiri. Wanachama wa Platinum, Dhahabu na Fedha  wa wageni wa Etihad na wanachama wenye sifa wa mashirika ya ndege washirika wa shirika la ndege la Etihad na mpango wa Uaminifu (loyalty) wa mashirika ya ndege washirika wataweza kutumia nyumba hii ya kupumzika wanapokuwa wanasafiri katika Daraja la Economy. Wageni lazima wawe ameorodheshwa katika ndege ya shirika la ndege la Etihad inayofanya kazi siku hiyo.

  Iko katika kituo cha 2 karibu na lango la 10, nyumba ya mapumziko itakuwa wazi takribani masaa matatu kabla ya kuondoka kwa ndege za Etihad mara mbili kila siku katika ruti ya Melbourne kwenda Abu Dhabi.

  Jumba hili linaongeza orodha inayokuwa ya nyumba za kiwango cha juu za kupumzikia zilizoko Sydney, Abu Dhabi, Dublin, Frankfurt, London Heathrow, Manchester, Paris, Washington DC na New York. Njumba ya kupumzikia ya daraja la kwanza iliyoko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi na Jumba jipya la kupumzikia la daraja la Kwanza na business huko Los Angeles yatafuata miezi ijayo.

  Shirika la ndege la Etihad lilianza safari za ndege za kila siku kwenda Melbourne mwezi Machi mwaka 2009. Leo, inafanya safari zake mara mbili kila siku, safari zisizo na ukomo kwenda Abu Dhabi na nje ya GCC, Afrika na Ulaya. Ni shirika pekee la ndege linalotoa safari zisizo na ukomo za kila siku kutoka Melbourne kwenda katika Umoja wa mataifa ya Kiarabu. Wabebaji wa bendera ya UAE watatambulisha ndege yao kuu ya A380 hapa Melbourne kuanzia tarehe 1 June 2016, jambo ambalo litaleta daraja la Makazi katika ruti hii, vyumba vitatu vya peke yake katika ndege ya kibiashara duniani.

  Zaidi ya kufanya safari zake mara mbili kila siku kwenda Melbourne, Shirika la ndege la Etihad inafanya safari zake za kila siku kwenda Brisbane na kwenda Perth na huduma 11 kwa wiki kwenda Sydney. Mashirika ya ndege washirika ya usawa, Virgin Australia, inafanya safari zake tatu nyingeza za kila wiki kati ya Sydney na Abu Dhabi.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na baadhi ya  viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Viongozi wakuu wanchi mbalimbali siku walipowasili Kampala nchini Uganda.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kikundi cha ngoma za asili cha Entebe nchini Uganda wakati akiondoka kurejea nchini.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga katika uwanja wa ndege wa Entebe wakati akiondoka kurejea nyumbani Tanzania.  Waandishi mbalimbali wa Habari kutoa nchi tofauti wakiwa na shauku ya kupata picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni zilizofanyika kwenyeuwanja wa Uhuru wa  Kololo, Kampala nchini Uganda. Katika Picha hiyo Rais Dkt. Magufuli alikuwa akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Picha na IKULU.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (aliyevaa tai) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Blogs (Bloggers) aliowaalika wakati wa kuwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, bungeni Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Annastazia Wambura. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Baadhi ya Bloggers wakiwa bungeni wakati wa Bajeti ya wizara hiyo
  Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ akisoma taarifa ya maoni ya upinzani kuhusu wizara hiyo.
  Baadhi ya Bloggers wakisikiliza mwenendo wa bunge. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Wamiliki wa Bloggers Tanzania (TBN).
  Nape akiwa na Bloggers pamoja na wasanii bungeni Dodoma
  Nape akiwa na Bloggers
  Nape akisalimiana na Blogger Salum Mwinyimkuu
  Mmiliki wa Blog ya Fullshangwe, John Bukuku (kushoto) na Mmiliki wa Matukio360 Blog Salum Mwinyimkuu wakiwa na mwandishi wa habari wa Raia Tanzania, Sharifa Malira

  0 0


  *Waziri Mkuu kukutana na Watanzania kesho, atoa ufafanuzi kuhusu Diaspora

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchini na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.

  Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Mei 13, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.Waziri Mkuu alisema katika kikao cha kwanza kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne.

  Waziri Mkuu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.

  “Ziko sheria ambazo zinafanyiwa kazi hivi sasa ambazo ni lazima zipitishwe na Baraza la Mawaziri kabla mahakama hii haijaanzishwa, zikishapitishwa na Baraza ndipo zitaanza kutumika,” alisema.Akifafanua kuhusu mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya maendeleo, Waziri Mkuu alisema kwamba katika bajeti ya mwaka huu, Serikali imeweza kuongeza kiasi cha fedha zilizotengwa kwa shughuli za maendeleo kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 40.

  “Kuongezeka kwa kiwango hiki ni ishara tosha kuwa tumelenga kutoa huduma kwa Watanzania na muhimu katika rushwa ni udhibiti wa fedha hizo na kuhakikisha zinakwenda kwenye miradi; matuizi mazuri ya fedha za Serikali, matumizi mazuri ya fedha zinazochangiwa na wahisani ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa,” alisema.

  “Tumekubaliana na uwepo wa uwazi na kushirikishana taarifa hasa katika kupeana taarifa za makampuni yanayoanzishwa na kusajiliwa katika nchi zinazoendelea kama njia ya kudhibiti tabia ya nchi ndogo kama Ireland na Panama kupokea na kuficha fedha zinazotoka kwenye nchi zinazoendelea” alisema.Alisema kila nchi imesisitizwa kutumia raia na kuwalinda watoa siri, kutumia mifumo ya kiintelijensia, kutumia wanasheria na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya watu wanaokamatwa kwa masuala ya rushwa.

  Waziri Mkuu alisema alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. David Cameron ambaye mbali na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka huu.

  “Anataka Tanzania iende kwenye mkutano huo ili ikaelezee mafanikio iliyoyapata katika kukabili suala hili, ili pia nchi nyingine ziweze kuiga utaratibu ambao Serikali imeutumia hadi tukafanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ofisi yake haijahusika na kuandaa mkutano wa wanadiaspora waishio Uingereza kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watu maalum wamechaguliwa kushiriki mkutano huo.

  Amesema mkutano huo umepangwa kufanyika kesho (Jumamosi, Mei 14, 2016) na uko wazi kwa Watanzania wote kushiriki ili waje kusikiliza nchi yao imefanya nini na kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi, watapatiwa fursa hiyo.“Kulikuwa na hofu ya watu wanaotoka mbali kutoweza kushiriki sababu ya gharama, lakini nasema yeyote mwenye uwezo wa kuja aje ndiyo maana tumeuweka muda wa asubuhi ili watu waweze kushiriki na kuwahi kurudi makwao,” alisema.

  IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU


  IJUMAA, MEI 13, 2016.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg (kulia) katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Wanne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara.
  ………………………………………………………
  WAZIRI MKUU wa Norway, Bibi Erna Solberg amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahakikishe Tanzania inatuma wawakilishi wa Serikali kwenye mkutano wa uwekezaji unaopanga kujadili fursa za uwekezaji barani Afrika utakaofanyika jijini Oslo, Norway, Oktoba mwaka huu.

  Bibi Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

  Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Waziri Mkuu wa Norway alisema mkutano huo umeandaliwa na taasisi binafsi ya Norway Africa Business Association (NABA) na kwamba anazo taarifa kuwa utalenga kujadili fursa za uwekezaji barani lakini focus ikiwa ni Tanzania.

  “Ni vema Tanzania ikatuma wawakilishi kwenye mkutano ili waje kuelezea fursa zilizoko nyumbani. Serikali ilete watu wa kuja kuelezea hali halisi ikoje nchini Tanzania,” alisema.Alisema ili fursa za uwekeaji ziweze kutumika ipasavyo, ni vema Tanzania ikawa na mfumo wa kimahakama unatoa haki bila upendeleo (a fair judicial system) kwani utasaidia kujenga hali ya kujiamini kwa wafanyabiasha wanaokuja kuwekeza Tanzania.

  “Mfumo huu utaleta hamasa kwa wawekezaji, kwani watajua kwamba mitaji yao iko salama na inalindwa kisheria, hivyo hawatakuwa na hofu,” alisema.“Hata hivyo, napenda kusisitiza kuwa makampuni yanayotoka nje na kuja kuwekeza Tanzania hayana budi kuheshimu sheria za nchi yenu pamoja na za huku wanakotoka,” alisisitiza.

  Akijibu hoja hiyo, Waziri Mkuu alisema usawa wa kisheria upo nchini kwa sababu Tanzania imesaini mikataba ya kimataifa ya MIGA na ICSID (International Centre for Settlement of Investment Disputes) ambayo inahusika na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa alimweleza Bibi Solberg kuwa Tanzania inahitaji kujifunza kutoka Norway katika suala la uanzishwaji wa mfuko wa ili mapato yatokanayo na rasilmali za nchi yatunzwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.

  Naye akaipongeza Serikali ya awamu kwa kuanzisha wazo la kutaka kuanzisha mfuko huo hata kabla ya kuanza kuuza rasilmali hizo. Pia alimtihibitishia Waziri Mkuu kuwa wao wako tayari kubadilishana uzoefu na Tanzania katika suala hilo.

  IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU

  IJUMAA, MEI 13, 2016.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May 12, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  …………………………

  WAZIRI MKUU wa Norway, Bibi Erna Solberg amesema nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania katika suala la kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike.

  Bibi Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

  Akizungumza na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Lancaster House, jijini London, Uingereza, Bibi Solberg alisema: “Malengo yetu kwa Tanzania ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike,” na kuongeza kuwa mbali ya kuwa ni mdau wa maendeleo kwa miaka mingi, asilimia kubwa ya fedha za bajeti zinazotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya misaada ya maendeleo zinaelekezwa Tanzania.

  “Sasa hivi kuna Serikali mpya iliyoingia madarakani. Tengenezeni ajenda zenu na mzilete ili tuone ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia,” alisema.

  Akizungumzia kuhusu mkutano wa kupambana na rushwa, Bibi Solberg alisema ameufurahia mkutano huo sababu umetoa fursa kwa watu kulizungumzia kwa uwazi tatizo la rushwa. “Watu waliouwa hawalizungumzii suala hilo, hivi sasa wameanza kulijadili na kupanga mbinu ya kukabiliana na janga hilo kubwa,” alisema.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru Serikali ya Norway kwa misaada ambayo imekuwa ikiipatia Tanzania kwa kipindi kirefu.Waziri Mkuu Majaliwa alimhakikishia Waziri Mkuu wa Norway kwamba fedha zote za misaada zinazotolewa kwa Serikali ya Tanzania ziko salama na zitatumika kwa uwazi na kwa malengo yaliyopangwa.

  “Malengo ya Serikali ya sasa ni kuleta maendeleo ya kiuchumi lakini pia nchini mwetu kuna amani na usalama kwa sababu kama hakuna amani ina maana hakuna usalama,” alisema Waziri Mkuu.Alimhakikishia Bibi Solberg kuwa Tanzania ni salama na wala hawana haja ya kutilia shaka juu ya uwepo wa amani. Pia alimtaka awahimize wawekezaji kutoka kwao waje kuwekeza kwenye uchakataji wa gesi ya kimiminika (LNG) kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

  Katika mkutano huu, Waziri Mkuu amefuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU

  IJUMAA, MEI 13, 2016.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


  SERIKALI YATOA BILIONI 2.3 KUWALIPA WAFANYAKAZI WA NIDA

  SERIKALI imeipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shilingi Billioni 2.3 (Bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa waliokuwa watumishi wa muda wa mamlaka hiyo, wapatao 597, waliosimamishwa kazi hivi karibuni.

  Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.Kabla ya NIDA kuwalipa watumishi hao fedha hizo, Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.

  Uhakiki huo ulihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba zao za akaunti za benki zilizokuwa zikitumika kulipa mishahara.

  Katika uhakiki huo imebainika kuwa kulikuwa na kasoro ama changamoto kadhaa zikiwemo za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.Wakati wa zoezi hilo, jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa lakini majina ya watumishi yaliyowasilishwa kuhakikiwa ana kwa ana kutoka NIDA, Tanzania bara yalikuwa 565.Hata hivyo, watumishi 516 pekee ndio waliojitokeza katika zoezi hilo na wengine 49 hawakujitokeza.

  Watumishi wa muda 32 kutoka NIDA Tanzania Zanzibar, wanaofanya jumla ya watumishi wa Mamlaka hiyo waliosimamishwa kazi kufikia 597, walihakikiwa kwa kupitia majalada yao yaliyoko ofisi za NIDA Makao Makuu, na kubaini mikataba yao haikuwa na kasoro.

  Kwa mantiki hiyo watumishi 427 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi.Aidha, watumishi wengine 121, walibainika kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya kufanya malipo hayo.

  Baadhi ya kasoro zilizobainika katika uhakiki huo ni pamoja na kukosekana kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba (kutofautiana tarehe na sahihi za wahusika), kufanana kwa namba za majarada, na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.

  Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya uhakiki na kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa menejimenti ya NIDA.

  Imetolewa na:

  Benny Mwaipaja
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
  13 Mei, 2016

  0 0

  MWENYEKITI wa Jumuia ya Alyamin Dkt. Omar Swaleh akimkabidhi Waziri  wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Msaada wa Maji na vidonge vya kutibu maji ya kunywa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu, (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili. 
  MWAKILISHI wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Andemichael Ghirmay, akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipofika ofisini kwake kukabidhi Vifaa vya kuchunguzia Maji.
  MWAKISHI wa WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo moja ya Vifaa vya kuchunguzia Maji katika hafla ilioyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
  MTAALAMU wa Maji wa WHO Michael Habtu, akikifanyia majaribio kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia kwa furaha.
  MTAALAMU wa Maji kutoka WHO Michael Habtu, akiwaonesha matokeo ya Maji alioyapima kwa kifaa cha kuchunguzia maji huku Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiangalia, wakwanza (kulia ) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Juma Malik Akili na Mwakilishi wa WHO Dkt. Andemichael Ghirmay
  SHEHENA ya Msaada wa Maji ya kunywa uliotolewa na Jumuia ya Alyamin kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu Zanzibar.

  PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


  Mtaalam wa TEHAMA katika moja ya Ofisi za Serikali akiwa kazini.

  ………………………
  Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

  Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) imezitaka taasisi zote zilizounganishwa kwenye mfumo wa simu zenye itifaki ya intaneti (Internet Protocol (IP) ambazo zinatumia intaneti kuzitumia simu hizo katika mawasiliano yao kila siku ili kuboresha utendaji kazi na kupunguza gharama za mawasiliano Serikalini.

  Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto amesema kuwa Serikali imeamua kusisitiza matumizi ya simu hizo ili kuziwezesha taasisi za Serikali kuwa na mawasiliano yaliyo bora, salama na kupunguza gharama za mawasiliano.

  Amesema kuwa Serikali kupitia Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) imeunganisha taasisi za Serikali 72 ambazo zinajumuisha Wizara, Idara zina zojitegemeana na Wakala za Serikali na kuongeza kuwa taasisi hizo zimeunganishwa na Mtandao wa Mawasiliano wa Serikali yaani ‘Government Communication Network (Govnet)’ unaowezesha mfumo wasimu hizo kufanya kazi kwa ufanisi.

  “ Kupitia mfumo wa simu hizi zenye itifaki ya intaneti mtumishi wa taasisi iliyounganishwa anaweza kupiga simu kwenda taasisi nyingine ya nje ikawa kama amepiga simu ya ‘extension’ ndani ya ofisi moja” Amesema Bi. Suzan.

  Aidha, amesema Taasisi za umma zitanufaika moja kwa moja na simu hizo kwa kuwa, taasisi hizo zitaweza kubadilisha na taarifa kupitia mtandao mmoja tuwa Mawasiliano wa Serikali kwa usalama na uhakika. Pia simu hizo zitawawezesha watumishi wa taasisi mbalimbali kufanya mkutano kwa njia ya simu wakiwa kwenye ofisi zao na hivyo kuokoa muda na gharama za usafiri.

  Hata hivyo amesema taasisi za umma zilizopo katika mtandao wamawasiliano wa Seikali zitaendelea kuwasilia na na taasisi zilizo nje ya mtandao huo kwa kupitia mtoa huduma wa simu za mezani (PSTN Provider) kama vile TTCL.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi
  Anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza (Minister of
  State for International Development) , Justine Greening katika
  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye
  ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. Wapili
  kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje , Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,
  Kikanda naKimataifa, Augustine Mahiga na watatu kushoto ni Jaji Mkuu,
  Mohamed Othman.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
  Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia)
  wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg katika Mkutano
  kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May12, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Norway,
  Erna Solberg katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa
  uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12,
  2016. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya
  Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
  Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili
  kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Norway, Erna Solberg (kulia)
  katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika
  kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. anne 
  kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman na watatu kushoto ni
  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika `Wizara ya Mambo ya Nje,
  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph
  Sokoine
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland katika Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Kaimu Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ally Samaje akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu Tathmini ya maonesho ya tano ya kimataifa ya madini ya vito yaliyofanyika Jijini Arusha mwezi April mwaka huu yaliyohudhuriwa na washiriki 813 kutoka nchi 26 duniani. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bi. Asteria Muhozya.
  Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huoPICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
  ………………………………………………………
  Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa madini Tanzania (TAMIDA) iliendesha Maonesho ya tano ya Kimataifa ya Madini ya Vito yaliyofanyika Jijini Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. Maonesho haya hufanyika kila mwaka Jijini Arusha na hukutanisha washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wachimbaji, Wafanyabiashara wa madini ya vito wa ndani na nje, wanunuzi wa madini wa ndani na nje, na wataalam mbalimbali wenye uzoefu wa shughuli za madini ya vito. 

  Maonesho hayo yalihudhuriwa na washiriki 813 kutoka katika nchi 26 duniani ambazo ni Tanzania Marekani, Sri Lanka, India, Kenya, China, Ujerumani, Namibia, Australia, Austria, Israel, Italia, Uingereza, Hong Kong, Switzerland, Zambia, Madagascar, Afrika Kusini, Msumbiji, Urusi, Cameruni, Canada, Malawi, Sudani, Malta, na Thailand). Aidha, wanunuzi (buyers) wa madini walikuwa 353, Walioshiriki kuonesha madini kwenye mabanda (Exhibitors) 300, na wageni mbalimbali 160.

  Lengo kubwa la Maonesho haya ni kama ifuatavyo: kufanya Arusha kuwa kitovu cha madini ya vito katika Afrika ili hatimaye iwe ni kitovu cha biashara ya madini hayo; fursa ya masoko kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa mdini ya vito nchini; na kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito hapa nchini.

  Katika maonesho hayo, madini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 4.5, sawa na Shilingi Bilioni 9.9 yaliuzwa.

  Serikali ilipata jumla ya Shilingi bilioni 1.71, ambapo Shilingi bilioni 1.3 zilitokana na mnada wa madini yaliyokamatwa na kutaifishwa na Serikali, Shilingi milioni 388 zilitokana na mrabaha uliolipwa kutokana na madini yaliyonunuliwa, na Shilingi milioni 26 zilitokana na vibali vya kusafirisha madini nje ya nchi.

  Manufaa mengine yaliyopatikana wakati wa maonesho ni pamoja na wageni kuingiza fedha za kigeni hapa nchini ambazo hutumika kwa ajili ya malazi, usafiri, chakula na kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii hapa nchini.

  Ili kuweka utaratibu utakaodhibiti shughuli za madini ya vito hususani tanzanite, Serikali inakusudia kuanzisha minada ya ndani mbali na mnada unaofanyika wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Vito Jijini Arusha. Minada hiyo itatoa fursa kwa wafanyabishara wa ndani kununua madini kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani madini hayo na kutengeneza vidani mbalimbali. 

  Ili kuimarisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito nchini, Serikali inakusudia kuimarisha Kituo cha Jimolojia kilichoko Arusha (Tanzania Gemmological Centre -TGC) ili kufundisha na kuzalisha vijana wa Kitanzania wa kutosha wenye ujuzi wa kusanifu na kung’arisha madini ya vito. Tayari vijana 29 wameshapata mafunzo ya miezi 6 ya ukataji wa madini ya vito kutoka kwenye kituo hicho tangu 2014. Wanafunzi wengine 18 wanaendelea na mafunzo ya miezi 6 yaliyoanza mwezi Machi, 2016.

  Aidha, upo mpango wa kuanzisha EPZ eneo la Merelani ambapo ni karibu na machimbo ya tanzanite kwa lengo la kupata eneo maalum ambapo shughuli za biashara ya madini na uongezaji thamani madini ya tanzanite zitafanyika kwa uhuru na wazi. Pamoja na juhudi zote hizo, Serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa madini mbalimbali nje ya nchi ikiwemo Tanzanite kwenye viwanja vya ndege na kwenye migodi ambapo madini yanazalishwa. 

  Wito wa Serikali ni kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuzingatia sheria zilizopo wakati wa kufanya shughuli zao.

  Imetolewa na;

  KAIMU KAMISHNA WA MADINI

  MHANDISI ALLY SAMAJ

  0 0

  Assalaam Aleikhum,

  Updates za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18),  aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini:

  Mwili wa Marehemu umeshawsili  nchini jana Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa tisa  mchana kwa  ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa  ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban). Mwili wa kijana wetu umepokelewa na ndugu, jamaa, majirani na marafiki katika   uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.

  Mazishi yamepangwa  kufanyika leo  Jumamosi saa 10  alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu  za kuandaa mazishi zitaanza  saa 4 asubuhi leo  Jumamosi, nyumbani  kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.
   Jeneza lenye mwili wa marehemu Maggid baada ya kuwasili Dar es salaam jana Ijumaa
  Ankal akiwa na ndugu, jamaa na  marafiki mara baada ya kuwasili na mwili wa marehemu katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam, ambako unahifadhiwa hadi baadae leo kabla ya kupelekwa Wazo Hill saa nne kwa dua na baadaye kurudi hapo msikitini kuswaliwa na hatimaye kupelekwa makaburi ya Kisutu kwa mazishi saa 10 Alasiri.
  Ankal akiwa na ndugu, jamaa na  marafiki mara baada ya kuwasili katika msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es salaam

  Ankal akiwa msibani Wazo Hill na wanahabari wenzie usiku huu. Kutoka kushoto ni Faraja Mugwabati, Maggid Mjengwa na Sufiani Mafoto.

  NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
  Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa "Twiga Cement",  hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.
  Innalillah wa inna ilayhi raajiun
  -AMIN.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika sehemu ya kuwasili abiria ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, upande wa uwanja wa zamani (Terminal One) wakati wa ziara yake ya ghafla aliyoifanya Ijumaa tarehe 13 Mei, 2016. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na kushoto ni Kaimu Meneja uendeshaji Lilian Minja.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuuliza maswali Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha, kuhusu dosari zilizopo katika mashine za kukagulia mizigo ya wageni wanaowasili kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, upande wa uwanja wa zamani (Terminal One)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwabana maswali maafisa wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuhusu dosari ya kutofanya kazi kwa mashine za ukaguzi katika sehemu ya kuwasili abiria ya uwanja wa zamani (Terminal One)
  .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal One) Jijini Dar es salaam.


  Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.


  Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.


  "Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili. Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege.


  "Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege ndogondogo napita tu" Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. 


  Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam

  13 Mei, 2016  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisalimiana na Kada wa CCM, Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman
  Vijana wa Umoja wa CCM mkoa wa Tanga, wakimfanyia mapokezi maalum, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
  Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Tanga, akila kiapo cha utiifu wakati walipomfanyia mapokezi rasmi Katibu Mkuu wa CCM- Bara, Rajabu Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. 
  Kijana wa wa UVCCM, Mwanakombo Mwakulo akimvisha Skafu Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara, Rajab Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. Kulia ni kada wa CCM Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella.
  Kijana wa UVCCM akimpigia saluti Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajabu Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisindikizwa na Katibu wa CCM mkoa wa alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. 
  Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman akimwelkeza jambo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akisalimiana na vijana waliompokea, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimsalimiana kwa furaha na Katibu wa CCM wilaya ya Muheza, Nassoro Moyo, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. Wapili kulia ni Katibu wa CCM mkoa huo, Shija Othman.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiingia katika ukumbi wa ofisi ya CCM mkoa wa Tanga, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
  Baadhi ya watumishi wa CCM kutoka wilaya za mkoa wa Tanga, wakiwa wamesimama kumlaki Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Tanga kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akiwa tayari ukumbini, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Tanga kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi akiwa tayari ukumbini, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Tanga kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa huo leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman na kulia ni Kada wa CCM Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella.
  Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga, Mathew Mganga akizungumza kumkaribisha ukumbini Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi alipowasili katika ukumbi wa Ofisi ya CCM mkoa huo kuzungumza na watumishi wa CCM kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga leo
  Wasanii wakichangamsha ukumbi kabla ya Luhwavi kuzungumza na watumushi wa CCM katika wilaya zote za mkoa wa Tanga
  Wasanii wakichangamsha ukumbi kabla ya Luhwavi kuzungumza na watumushi wa CCM katika wilaya zote za mkoa wa Tanga
  Msanii, Hassani akionyesha umahiri wake wa kuimba huku akiwa amevalia kisanii mavazi ya kike, kuchangamsha ukumbi kabla ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi kuzungumza na watumishi wa Chama kutoka wilaya zote za mkoa wa Tanga leo.. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO

  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeazimia kupima jumla ya viwanja 2180 katika Kijiji cha Chasimba,wilayani Kinondoni baada ya kuisha kwa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na Kiwanda cha Saruji (Twiga Cement).

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Usanifu wa Miji wa Wizara hiyo, Bi.Immaculata Senje alipokuwa akifafanua juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu kukosa huduma za umeme na maji katika eneo hilo.“Baada ya kupatikana kwa suluhisho la mgogoro huu, zoezi la upimaji viwanja linaendelea ambapo hadi sasa tumeshapima jumla ya viwanja 370 kati ya viwanja 2180 vinavyotarajiwa kupimwa kwenye Kijiji hicho,”alisema Bi Senje.

  Bi Senje aliongeza kuwa kazi ya kupima viwanja hivyo ilianza mwezi Agosti mwaka jana baada ya Wizara kuunda timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili waweze kutambua mipaka ya eneo kwa ajili ya kuweka miundombinu.

  Aidha, Bi. Senje amesisitiza kuwa wananchi wawe wavumilivu kwani huduma za miundombinu kama vile maji, umeme na barabara zitawekwa baada ya upimaji wa viwanja hivyo kukamilika.Mgogoro huo ulimalizika mnamo Juni 13 mwaka jana baada ya uongozi wa Wizara kuweka kikao na uongozi wa Kiwanda cha Saruji pamoja na wananchi wa Chasimba ambapo uongozi wa Kiwanda ulikubali kuachia sehemu ya ardhi ambayo ilishaendelezwa na wakazi wa eneo hilo kwa makubaliano ya kupewa fidia na Wizara.

  0 0  KOMBE LATUA JANGWANI: Chereko na nderemo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Kilimo Mwigulu Nchemba akiikabidhi Yanga Kombe la Ligi Kuu. Huu ni ubingwa wa 26.Yanga walikabidhiwa kombe hilo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh Mwigulu Nchemba, ambae ndie alikuwa mgeni rasmi.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Jumuiya ya Madola inaweza kuiga mbinu ambazo Tanzania imetumia katika kupambana na rushwa zikiwemo za kujumuisha wadau tofauti kwenye vita hiyo.

  Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Bibi Patricia Scotland walipokutana kwenye mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

  “Tanzania iko tayari kushirikiana na ninyi katika kujenga timu hii na ili uweze kupata picha halisi, nakukaribisha Tanzania uje ujionee hatua ambazo tumechukua hadi kufikia hapa tulipo kwenye vita hii dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.

  Alimweleza Katibu Mkuu huyo kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kupambana na rushwa kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa wananchi. “Wananchi wanafurahia juhudi za Serikali, vyama vya kiraia pia vinaunga mkono jitihada zetu na vyombo vya habari vinashirikiana nasi katika vita hii,” alisema.

  Waziri Mkuu alitoa wito huo baada ya kuelezwa na Bibi Scotland kwamba anataka kuanzisha idara malum kwenye Jumuiya hiyo ambayo itasimamia mapambano dhidi ya rushwa na makosa ya jinai.

  “Nataka tuwe na idara yenye watu mahiri wa idara za uhasibu, mahakama yenyewe ikiwemo waendesha mashtaka na wanasheria kutoka kwenye nchi kadhaa ili washirikishane uzoefu kutoka kwenye nchi zao. Ninaamini katika nchi 53 ambazo ni wanachama wetu, sitakosa watu wa aina hii,” alisema.

  Alisema ameamua kufanya hivyo ili aweze kuendanana na malengo makuu matatu ya jumuiya hiyo ambayo ni kupiga vita rushwa, kuhimiza utawala bora na usimamizi wa demokrasia.

  IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU

  JUMAMOSI, MEI 14, 2016.

older | 1 | .... | 846 | 847 | (Page 848) | 849 | 850 | .... | 1897 | newer