Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 845 | 846 | (Page 847) | 848 | 849 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Afisa Sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Hemed Lusungu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maboresho ya sheria mbalimbali yanayofanywa na tume hiyo. Kushoto ni Afisa Sheria wa Tume hiyo Bw. Fredy Kandonga.
  Afisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Fredy Kandonga akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tafiti za kisheria zinazotarajiwa kufanyiwa kazi kwa kipindi cha Mwaka 2016/2017 ikiwemo Mapitio ya Sheria za Uwekezaji. katikati ni Afisa Sheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Bw. Hemed Lusungu na kulia ni Afisa Habari wa Tume hiyo Bw. Munir Shemweta.PICHA NA FATMA SALUM- MAELEZO

  0 0

  1
  Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi akitoa elimu ya mpango mpya na wa gharama nafuu utakaomuwezesha mzazi kumlipia bima ya Afya mtoto chini ya miaka 18 unaojulikana TOTO AFYA KADI,kwenye kliniki ya mama na mtoto (RCH) Hospitali ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
  2
  Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale akitoa rai kwa akina mama walioudhuria kliniki kwa kuchangamkia fursa kwani ni mpango wenye manufaa zaidi na una uwigo wa mafao kwa 50,400 tu.
  3
  Akina mama wakifuatilia elimu ya kitita cha mafao yanayotolewa kwenye mpango wa Toto afya kadi kutoka kwa meneja wa NHIF Lindi hayupo pichani.

  0 0


  Frank Mvungi-Maelezo.


  Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 inatarajia kufanya mapitio katika sheria mbalimbali ili kutoa mapendekezo yatakayowezesha kufanyika kwa marekebisho  au kutungwa kwa sheria mpya kulingana na mahitaji ya sasa.


  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na afisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria  Tanzania Bw. Hemed Lusungu wakati wa Mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kutoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo.Akifafanua  Lusungu amesema kuwa Sheria zitakazofanyiwa utafiti ili ziboreshwe na kuendana na Kasi ya Serikali ya awamu ya Tano ni sheria za uwekezaji (Review  of the legal frame work Governing Investiment for viable economic growth).

  “Tunataka sheria katika eneo la Uwekezaji ziendane na dhana ya mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli inayolenga kukuza viwanda vya ndani hivyo ni lazima tutazame eneo hili ili kuwa na sheria zitakayowezesha suala hili” alisisitiza Lusungu.Akizungumzia mapitio katika sheria za Usafirishaji Lusungu amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na sheria zinazokidhi mahitaji ya sasa hivyo utafiti wao utatoa mapendekezo ili kulinda haki za wasafiri na wasafirishaji.

  Alisema faida za Tafiti zinazofanywa na Tume hiyo ni kusaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea marekebisho ya sheria mbalimbali na pia kusaidia kutungwa kwa sheria mpya kulingana na mahitaji ya wakati akitolea mafano sheria ya Ununuzi wa Umma sura ya 410 .


  Aliongeza kuwa sheria hiyo imekuwa ikilalamikiwa kurefusha mchakato wa manunuzi na kufanya bei ya bidhaa au huduma kuwa kubwa.Kwa kuzingatia umuhimu wa Sheria hiyo Tume imeshafanya mapitio katika maeneo husika na kutoa mapendeklezo ambayo yataondoa kasoro zilizokuwepo awali.

  Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria na ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Sura ya 171.  Majukumu ya tume kama yalivyoainishwa katika kifungu cha 4 (1),(2) na (4) Cha sheria ya Tume ni kufanya mapitio, utafiti na kutathmini maeneo au mfumo wa sheria husika na kutoa mapendekezo kwa Lengo la kuiboresha.


  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  DAR ES SALAAM.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa wakadiriaji majenzi Afrika unaotarajiwa kufanyika tarehe 18-19 Agosti, 2016 jijini Dar es salaam.

  Hayo yamesemwa leo na Rais wa chama cha wakadiriaji majenzi Tanzania (TIQS) Samuel Marwa kuwa Tanzania kwa mara ya kwanza imekuwa mwenyeji katika mkutano huo ukiwa na lengo la kukuza fani ya ukadiriaji majenzi ili mchango wake katika jamii uweze kutambulika.

  Amesema mada kuu ya mkutano huo ni kufikia malengo ya maendeleo endelevu na mchango wa huduma za ukadiriaji majenzi hivyo sekta ya ujenzi na hasa miundombinu ni moja ya vipaumbele vilivyoainishwa kama kichocheo cha kuwezesha kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kukuza uchumi wa nchi.

  “Malengo ya Maendeleo Endelevu yanakusudia kuondoa umaskini na kupambana na udhalimu na kuleta usawa pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kufikia mwaka 2030, hivyo mada hii inaendana na na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo yenye usawa, mafanikio na ustawi wa kila mwananchi”alifafanua Rais huyo.

  Aidha, amesema kuwa  huduma hizo, zikitumika kwa ukamilifu zitasaidia kupambana na rushwa na uwajibikaji dhaifu kwani huduma hiyo ni nguzo muhimu katika kuchangia ufanisi na udhibiti wa gharama za ujenzi  na ukamilishaji kwa muda wa  miradi na kupata dhamani ya fedha.

  Mbali na hayo Rais huyo ameuomba uongozi wa vyuo tofauti nchini kuanzisha na kuzidi kudahili wanafunzi katika taaluma ya ukadiriaji majenzi ili kutatua changamoto zilizopo.

  Nchi zaidi ya 16 za Afrika zilizoko Jumuiya ya Madola pamoja na Angola na Msumbiji  zinatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.

  0 0


  Hussein Makame-MAELEZO.


  UIMARISHWAJI wa miundombinu na uboreshaji wa sekta ya usafiri ni baadhi ya  mihimili inayopewa umuhimu nchini katika kuleta maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla hasa pale usafirishaji unapowezesha abiria na mizigo kufika sehemu kwa wakati na kwa gharama nafuu.


  Juhudi za Serikali ikiwemo Serikali kuu, Serikali za mitaa, taasisi za ndani na nje ya nchi, mjenzi, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa pamoja zimekuwa zikishirikiana kuimarisha mtandao wa barabara ya kutosha kwa nia ya kuwafikia wananchi wote na katika viwango bora.


  Wachumi, wanaeleza kuwa ili taifa lolote liweze kujikwamua kiuchumi ni lazima pamoja na mambo mengine liboreshe sekta ya usafiri kuanzia ndani na nje ya miji ili kurahisisha usafirishaji na kuchangia maendeleo.


  Tanzania inatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa msongamano mkubwa wa magari katika nchi za Jangwa la Sahara huku jiji la Dar es Salaam likiongoza kwa msongamano mkubwa kutokana na kasi ya kuongezeka kwa wahamiaji mijini huku miundombinu yake ya barabara ikibakia ile ile.


  Hali hiyo imekuwa ikiathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla mbali na athari za kiafya na kijamii zinazochangiwa na moshi wa magari na kukaa sana kwenye gari wakati wa asubuhi na jioni, hasa kwa wale wanaokaa mbali na sehemu zao za kazi.Kukamilika kwa barabara katika mfumo wa kisasa wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika jiji la Dar es Salaam kumewezesha kupatikana kwa kilomita 20.9 za barabara.
  Kilomita hizo ni za barabara kutoka Kimara hadi Kivukoni Ferry, Morocco hadi Magomeni na Fire hadi Kariakoo na miundombinu yake ikiwemo karakana na vituo vikuu vya mabasi hayo.Ujenzi huu wa barabara ni kielelezo chanya kuelekea mafanikio ya kuleta mabadiliko ya miundombinu ya usafiri jijini Dar es salaam katika muda mfupi ujao.

  BRT ni mfumo unaoinukia kwa kasi duniani kwa kusafirisha haraka abiria wengi mijini kwa gharama ndogo kwa kulinganisha na ule wa garimosho za mjini.Utafiti uliofanywa na Wakala wa Mradi wa Usafiri wa Haraka (DART) hivi karibuni unaonesha kuwa foleni za magari barabarani hupoteza Shilingi Bilioni 655 kwa mwaka nchini na kusababisha changamoto nyingi.

  Changamoto hizo ni kupata magonjwa ya akili na maradhi ya mfumo wa hewa inayochangiwa na kukaa sana kwenye magari na kuvuta moshi wa magari kwa muda mrefu njiani kutokana na foleni.Tafiti mbalimbali zilizofanywa kuhusu usafiri wa jiji hilo zimebainisha maeneo 56 yanayokabiliwa na changamoto za usafiri ikiwemo kuwepo kwa mfumo wa barabara ambao haukidhi mahitaji na hivyo kukosa uwezo wa kuhimili usafiri wa umma.

  Mbali na msongamano wa magari, pia inaelezwa kuwa jiji hilo linakabiliwa na kuwepo kwa vyombo vya usafiri vibovu, visivyokidhi mahitaji ya jamii ya wakazi, na upande mwingine taa za kuongozea magari ambazo mara kwa mara zinakuwa mbovu na zilizopitwa na wakati.


  Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Mradi wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ya mwaka 2003, msongamano wa magari husababishwa na wingi wa daladala, ongezeko kubwa la magari ya watu binafsi, uendeshaji usiozingatia kanuni na utendaji mbovu kwa baadhi ya askari waongoza magari.


  Ripoti hiyo pia inaonesha kuwa jiji la Dar es Salaam lilikuwa na kilomita 450 tu za lami ambazo ni asilimia 39.5 ya kilomita 1,140 za barabara, wakati kilomita 265 tu ndizo zilizokuwa zinatumika katika usafiri wa mabasi jijini humo.


  Kwa upande wa vyombo vya usafiri wa umma, ripoti hiyo inaonesha kuwa asilimia 90 ya magari hayo yana umri unaozidi miaka 10 na mengi ni chakavu na hutumia muda mwingi barabarani na kwenye karakana kwa ajili ya matengenezo.Ripoti hiyo inabainisha changamoto nyingine kuwa,ni ongezeko la kasi la magari, zikiwemo daladala kwa zaidi ya miaka 16 iliyopita huku kukiwa na usimamizi duni wa magari usiokuwa na mabadiliko wala mkakati mpya mbali na kuwepo na mabadiliko hayo katika jiji.


  Baada ya kubaini changamoto hizo, wataalamu wa kizalendo wa jiji la Dar es Salaam walianza kuweka mikakati ya kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo na hivyo kuiunda DART chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI wakati huo.Lengo la kuanzishwa kwa wakala hiyo lilikuwa ni kutaka kutoa huduma bora ya usafiri kwa gharama nafuu katika jiji la Dar es salaam, ambalo ni ni kitovu kikuu cha biashara nchini.

  Katika kutekeleza azma hiyo DART ilipanga mkakati wa kuwa na miundombinu bora, inayokubalika kimataifa, yenye manejimenti ya oporesheni ya usafirishaji.


  Suala la miundombinu ya barabara ilikabidhiwa TANROADS na kuanzisha kitengo cha BRT ili kujenga mfumo huo unaoelezwa kuwa bora kiufanisi zaidi duniani ulioanzia katika miji ya Curitiba (Brazili), Quito (Equador) na Bogota (Colombia), na baadaye kuingia nchi za ulaya kama Ufaransa.


  KWA NINI USAFIRI WA MABASI YA HARAKA (BRT)

  “BRT ni aina ya usafiri wa mijini ambao ni nafuu na endelevu kuliko aina nyingine yoyote ya usafiri katika ulimwengu wa leo”

  Haya ni maneno ya utangulizi kwenye kitabu cha Ripoti hiyo ya mwaka 2003 yaliyoandikwa na aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi.


  Mbali na kuwa nafuu na endelevu, BRT inaelezwa kwamba ni mfumo wa usafiri unaohudumia watu wengi kwa haraka na hutumianjia maalum na mabasi makubwa yenye uwezo wa kusafirisha abiria wengi hadi 48,000 kwa saa kwa mwendo wa zaidi ya kilomita 22 kwa saa.


  Mfumo wa BRT unazingatia mahitaji ya watumiaji wengine wa barabara waenda kwa baiskeli, watembea kwa miguu na huduma maalum kwa walemavu na miundombinu yake hutumika kupunguza muda wa safari.

  Moja ya malengo makuu ya mradi huo ni kubadilisha sura ya jiji kwa kuboresha matumizi ya maeneo ya kandokando ya njia kuu ya mradi na kurahisisha maendeleo ya kiuchumi kwa jiji zima.


  Kuanzishwa kwa mradi wa BRT kumetokana na kukosekana kwa mradi wa mabasi madhubuti unaokidhi mahitaji yote ya usafiri.


  HALI YA USAFIRI WA JIJI LA DAR ES SALAAM

  Ongezeko la watu katika jiji la Dar es Salaam linachangia changamoto za sekta ya usafiri na takwimu zinaonesha kwa miaka 20 ijayo, jiji hilo linatazamiwa kuwa na watu 7,614, 459 watakaohitaji huduma ya usafiri.

  Inaelezwa pia wakazi wengi wa jiji hilo hupendelea kutumia usafiri wa umma kutokana na sababu za kiuchumi.Hivyo kuanzishwa kwa BRT kutasaidia wananchi wengi wenye kipato duni.


  Pia imebainika kwamba abiria wengi na magari mengi yanatumia barabara kuu huku msongamano mkubwa ukiwa katika barabara ya Morogoro ikifuatiwa na Barabara ya Kawawa na Uhuru.Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Barabara ya Uhuru miaka 10 iliyopita ilikuwa na abiria wengi kwa kuwa na abiria 15,000 na magari 770 kwa saa, ikifuatiwa na barabara ya Morogoro yenye abiria 9,000 na magari 715.
  Barabara ya Kilwa ilikuwa na 6,200 kwa 549, Kawawa 10,000 kwa 383 kwa saa, Barabara ya Nyerere 8,600 na magari 399 kwa saa na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi abiria5100 na maagari 281 kwa saa.


  Inaonesha pia abiria wengi wanaoelekea katikati ya jiji asilimia 43 hutumia usafiri wa umma, na asilimia 6 hutumia magari binafsi.Daladala hubeba takrbani abiria mil 1.4 kwa siku huku abiria wengi wakielekea Kariakoo, katikati ya mji (Posta) na hospitali ya Muhimbili na mengine ni Ubungo, Mwenge na Kimara.

  UTEKELEZAJI WA MAMBO YA MRADI WA BRT

  Utekelezaji wa mradi wa BRT utafanywa kwa awamu sita ambapo awamu ya kwanza imeshakamilika na huduma imeanza kutolewa baada ya kufikia makubaliano juu ya maslahi ya wananchi na Umma kwa ujumla.

  Awamu hii ya kwanza inaanzia na Barabara ya Morogoro na Kawawa, ikifuatiwa na Barabara ya Uhuru na Nyerere, na Kilwa na ifikapo mwaka 2035 inategemewa asilimia 91 ya wakazi wa jiji wataweza kupata huduma ya mradi huo.


  Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Mradi wa BRT, awamu ya kwanza inahusisha njia kuu na lishi zenye mtandao wa barabara wa kilomita 20.85, vituo vya kawaida 29,vituo vikuu 5 na karakana 2 za Ubungo na Jangwani.

  Mpango wa muda mrefu wa BRT ni kuwa na kilomita 137 za njia maalum ya mabasi na vituo 18 na vituo vya kawaida 228.


  Tayari vituo vikuu viwili vimejengwa vya Kivukoni karibu na kituo cha Kivuko cha Kigamboni na Soko la Samaki na cha Ubungo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani (UBT).


  Vituo vingine vilivyokwishajengwa ni Ubungo, Kimara (Kimara mwisho), Kariakoo (mtaa wa Msimbazi na njia ya Reli) na Morocco ambapo kila kituo kitahudumia mabasi 65 kwa saa kwa kila mwelekeo.Mabasi ya njia kuu yatakuwa aina ya kumbakumba yenye uwezo wa kubabe abiria 140 na kila basi litakuwa na safari ya kilomita 14 kila siku.

  NJIA KUU ZA MRADI WA MABASI AWAMU YA KWANZA

  Lengo la BRT ni kusafirisha abiria wengi kwa muda mfupi, kufupisha muda wa kusimama vituoni kwa kuimarisha usafiri wakati wa asubuhi na jioni ambapo maahitaji ya awali yalionesha huduma ya mabasi 40 kwa saa na katika vipindi vya kawaida mabasi 10 kwa saa (kila baada ya dakika 5)

  Ilielezwa kuwa usafiri wa BRT utakuwa na safari 7 kupitia njia saba katika barabara kuu, safari za haraka 2 na safari 5 za kawaida na muda wa kazi ni kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 5 usiku kila siku.Hata hivyo huwenda muda huo ukafanyiwa mabadiliko kulingana na mahitaji.

  Kwa mujibu wa DART kila njia kuu itakuwa na vituo vya kusimama kwenye vituo maalum kama inavyoonesha hapo chini.

  DR001-UBUKOO, ni njia inayohusu mabasi yanayotoa huduma kati ya Kituo Kikuu cha Ubungo na Kituo Kikuu cha Kariakoo na yatasimama katika vituo vyote 15 na kuhudumia abiria 3,329 asubuhi na jioni 1,880 kwa mzunguko wa dakika 47.

  DR002-KIMKOO, inahusu mabasi yanayotoa huduma kati ya Kituo Kikuu cha Kimara na Kituo Kikuu cha Kariakoo na yatasimama katika vituo vyote 14 vya Kimara terminal, Resort, Thomas, Baruti, Corner, Kibo, Ubungo, Tanesco, Kituo Kikuu cha Ubungo, Bakhressa, Baptist Church, Fire, Uhuru Street na Kituo kikuu cha Kariakoo).

  Abiria wa asubuhi wanakadiriwa kufikia 6,801 na jioni abiria 3,505 na mabasi hayo yatatumika kwa mzunguko wa dakika 67 na itatoa huduma ya haraka yaani service index katika kiwango cha asilimia 43

  Njia ya DR003-KIMKIV, ni ya mabasi yanayotoa huduma kati ya Kituo Kikuu cha Kimara na Kituo Kikuu cha Kivukoni na yatasimama katika vituo vyote 26 ikiwemo vya Kimara terminal, Korogwe, Bucha, Resort, Thomas, Baruti, Corner, Kibo, Ubungo Tanesco, Kituo Kikuu cha Ubungo, Shekilango, Urafiki, Manzese Tipo Top, Bakhressa, Manzese Agentina, Kagera, Mwembechai, Usalama, Baptist Church, Jngawani, Fire, DIT, Kisutu, Nyerere Square, Posta ya Zamani, Kivukoni na Magogono Ferry.

  Abiria wanaotegemewa kusafiri ni 7,215 wakati wa asubuhi na jioni ni abiria 3,048 na watatumia dakika 82 kwa mzunguko.


  DR004-MORKOO, ni njia inahusisha mabasi yanayotoa huduma kati ya Kituo Kikuu cha Morocco na Kituo Kikuu cha Kariakoo na yatasimama katika vituo vyote 12 (Morocco, Kinondoni B, Mwanamboka, Mkwajuni, Kanisani, Magomeni Hospitali, Baptist Church, Jangwani, Fire, Uhuru Street na Kituo kikuu cha Kariakoo) na mzunguko wa safari ni dakika 38.

  DR005-MORUBU, ni njia ya abiria wanaosafiri kati ya Kituo Kikuu cha Morocco na Kituo Kikuu cha Ubungo ambapo mabasi yatasimama katika vituo vyote 16.Asubuhi inategemea kusafirisha abiria 6,189, jioni abiria 3,419 na itatumia mzunguko wa dakika 24.

  DR006-MORKIV, inahusisha mabasi yanayotoa huduma kati ya Kituo Kikuu cha Morocco na Kituo Kikuu cha Kivukoni na yatasimama katika vituo vyote 25.Asubuhi inategemea kusafirisha niabiria 2,935 na jioni abiria 1,928.Njia hii itakuwa na mzunguko wa dakika 46.

  DR007-, UBUKIV.Hii ni njia ya mwisho itakayosarisha abiria kati ya Kituo Kikuu cha Ubungo na Kituo Kikuu cha Kivukoni na yatasimama katika vituo vyote 12 vya Ubungo terminal, Shekilango,Urafiki, Mahakama, Bakhressa, Magomeni Kagera, Fire, Bibititi, Libya, City Council, Posta ya Zamani, na Kivukoni terminal).

  Inategemea kuwa na abiria 2,726 asubuhi na jioni abiria 1,766. Nji hii itachukua mzunguko wa safari wa dakika 25 na inategemewa kutoa kiwango cha huduma ya haraka kwa asilimia 38.

  Vituo hivi saba vitatoa huduma ya urefu wa kilomita 145.8.Hata hivyo ili kuendana na viwango vinavyohitajika na huduma kuwa endelevu, basi moja linatakiwa kusafirisha abiria 2,000 kwa siku.

  Safari zote zitachukua jumla ya mabasi makubwa 116 ikiwemo mabasi 6 ya akiba na mabasi lishi 237 na inakadiriwa kuwa abiria 350,000 watasafirishwa kila siku.

  Kuhusu nauli, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UDA Rapid Transit (UDART), David Mgwasa  anasema nauli za mabasi zitakuwa shilingi 200 kwa mwanafunzi, shilingi 650 kwa njia maalum na kwa njia lishi nauli ni shilingi 400 na wanaounganisha njia zote za lishi na maalum watalipa shilingi 800.

   Abiria watanunua tiketi zao kwa keshia nayepatikana kwenye kila kituo cha mabasi hayo au watanunua kadi ambayo ataipangusa (tap) kwenye mashine iliyopo kituoni na kupewa tiketi.

  Anasema UDART kwa sasa iko kwenye mchakato wa kuhakikisha abiria anaweza kulipia nauli kwa kutumia simu ya mkononi au kupitia benki.


  Mwisho
  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi akivishwa Skafu na Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Omari Salum, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, Wilayani Kibaha mkoani humo leo. Katikati ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga na kulia ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Kibaha, David Malecela.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajab Luhwaavi, akiongozana na Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga, kwenda Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, wilayani Kibaha leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwai akisalimia baada ya viongoi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kuzungmza na wafanyakazi wa CCM mkoa wa Pwani wilayani Kibaha leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwai akisalimia baada ya viongoi baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, kuzungmza na wafanyakazi wa CCM mkoa wa Pwani wilayani Kibaha leo 
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi akisaibi kitabu cha wagei katika Ofisi ya CCM mkoa wa Pwani, wilayani Kibaha leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Joyce Masunga.
  Watumishi wa CCM wakimkaribisha ukumbini Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajab Luhwavi akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa CCM wilaya za mkoa wa Pwani katika kikao alichofanya na wafanyakazi hao katika Ofisi ya CCM ya mkoa iliyopo wilayani Kibaha.
  Naibu Katibu Mkuu Luhwai baada ya kuwasili ukumbini
  Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akisoma taarifa 
  Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akisoma taarifa
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi akizungumza na wafanyakazi wa CCM kutoka wilaya zote za mkoa wa Pwani, katika kikao chake na wafanyakazi hao kilichofanyika wilayani Kibaha mkoa wa Pwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa kuingia kwenye ukumbi wa Lancaster House, London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, May 12, 2016. Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki katika Mazungumzo Rasmi ya Wakuu wa Nchi katika Mkutano kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwenye ukumbi Lancster House, London, nchini Uingereza May 12, 2016. Majaliwa alimwkilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mkufunzi na Mwalimu wa Sauti Tony Joett akitoa mafunzo ya sauti kwa washiriki waliochaguliwa kuingia tano bora katika fainali za  shindano la Airtel Trace Music Stars zilizopangwa kufanyika tarehe 20 mei 2016 hapa jijini Dar es Saalam. . Mshindi ataondoka na zawadi ya shilingi milioni 50 na kupata nafasi ya kuiwakisha Tanzania katika mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Nigeria
   Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (wa pili kulia) wakijipongeza kwa pamoja na washiriki waliochaguliwa kuingia tano bora katika  shindano la Airtel Trace Music Stars ambapo fainali zake zitakafanyika tarehe 20 mei 2016 hapa jijini Dar es Saalam. Mshindi ataondoka na zawadi ya shilingi milioni 50 na kupata nafasi ya kuiwakisha Tanzania katika mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Nigeria
  Washiriki waliochaguliwa kuingia tano bora katika  shindano la Airtel Trace Music Stars wakifurahia ushindi huo uliowapa tiketi ya kuingia katika fainali zitakafanyika tarehe 20 mei 2016 hapa jijini Dar es Saalam. Mshindi ataondoka na zawadi ya shilingi milioni 50 na kupata nafasi ya kuiwakisha Tanzania katika mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Nigeria.  Kutoka kushoto ni Benny Sule, Nicole Grey, Salim Mlindila,  Nandi Charles na Melisa Elina John

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza washiriki waliongia kwenye tano bora katika shindano kubwa Afrika la kusaka vipaji vya muziki lijulikanalo kama Airtel Trace Music Stars.

  Ikiwa ni miezi mitatu tangu kuanza kwa msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars na kushirikisha  maelfu ya vijana wa kitanzania, Airtel imetangaza majina ya washiriki wa tano bora walioingia kwenye fainali za kitaifa ambao ni pamoja na Benny Sule, Nicole Grey, Nandi Charles, Melisa Elina John na Salim Mlindila.

  Washiriki hawa walichaguliwa na jopo la majaji  mahiri akiwemo mtangazaji wa TV mahiri, Mwanamuzi, Mwigizaji na msanii aliyejikita katika maeneo mengi, Jokate Urban Mwegelo,  mtunzi wa nyimbo na mwalimu wa sauti Tony Joett pamoja na mtengenezaji wa Muziki na mfanyabiashara Luciano Gadie Tsere.

  Akitangaza walioingia tano bora, Afisa Uhusiano wa Airtel , Jane Matinde  aliwapongeza washiriki hao kwa kufika katika hatua ya fainali na kusema “ msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Music Stars umekuwa ni wa mafanikio makubwa na leo tunayo furaha kutangaza majina ya washiriki waliofanya vizuri zaidi na kuwa kwenye nafasi ya kushinda na  kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars ya Afrika”.

  “Tunaamini Airtel Trace Music Stars ni  Fursa muhimu ya kuwainua wanamuziki chipikizi kuweza kuonyesha vipaji vyao na hatimae kuzifikia ndoto zao. Airtel itaendelea kuwawezesha vijana wa kitanzania kutambua uwezo wao na kuishi ndoto zao na shindano hili la Airtel Trace Music Stars ni kielelezo tosha cha dhamira hii”. Aliongeza Matinde

  Kwa upande wake mmoja ya washiriki waliotinga tano bora , Benny Sule alionyesha furaha yake ya kufika katika finali na kusema “ mashindano haya yamenipa Fursa kubwa kiasi ambacho nashindwa kuelezea. Nimejipanga vyema kushiriki katika fainali zinazofanyika wiki ijayo na natumaini kushinda na kuiwakilisha vyema nchi yangu

  Aliongeza kwa kusema “Huu ni mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mwanamuziki nyota ndani na nje ya nchi. Nawashukuru sana Airtel kwa mpango huu ambao umewawezesha vijana wengi barani Afrika  kuonyesha vipaji vyao na kuzifikia ndoto zao.”

  Washiriki waliongia tano bora wanategemea kushindana katika kinyanganyiro cha mshindi wa Airtel Trace Music Stars wa Tanzania katika finali zitakazofanyika tarehe 20 Mei 2016.  Mshindi ataondoka na zawadi ya shilingi milioni 50 na kupata nafasi ya kuiwakisha Tanzania katika mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini Nigeria ambapo atapata nafasi ya kushinda na kusaini mkataba wa  mafunzo.

  Tunatoa wito kwa watanzania kuwapiigia kura washiriki ili kupata mshindi atakayetuwakalisha vyema  katika mashindano ya Afrika, ili kupiga kura weka jina la fumbo (nickname) ya mshiriki kisha tuma kwenda namba 15594 .  zifuatazo ni jina la fumbo (nickname ) za washiriki  Beny  Sulle “Ben”, Nicole Grey “Nic, Nandi Charles”Nan”,Melissa John “Mel”na Salim Mlindila “Sal”.

  0 0

   Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo aliemuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar akisoma hotuba katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahale Mjini Zanzibar.
   Brasbendi ya Chipkizi ikiongoza matembezi ya wauguzi yakipita katika maeneo ya Kisonge kuelekea Studio za Rahaleo ambapo sherehe hizo ziliadhimishwa rasmi.
   Waandamanaji wakiingia kwa furaha eneo la Studio za Rahaleo ambapo sherehe za sikuya Waguzi Duniani ziliadhimishwa.
   Mrajis Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Vuai Kombo Haji akiongoza kiapo cha wauguzi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaeo.  
   Mkurugenzi Tiba Katika Wizara ya Afya Dkt. Salhia Ali Muhsin akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliemwakilishi Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika maadhimisho hayo. 
   Baadhi ya wauguzi walioshiriki maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo, Mjini Zanzibar.  
  Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa wauguzi na Mgeni rasmi, Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.


  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Chama cha Ushirika (NANYUM) wilayani Lindi kitatakiwa kulipa deni la sh. milioni 433 kwa wakulima wa korosho wilayani humo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio la wizi wa fedha hizo lililodaiwa kufanyika Januari, mwaka huu.

  Katika taarifa iliyotolewa leo (Mei 12,2016) na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi inasema kutokana na tukio lililotokea mnamo Januari 7, mwaka huu majira ya saa 12:30 za jioni huko kijiji cha Nambahu majambazi wapatao watatu wakiwa na bunduki huku wakitumia usafiri wa pikipiki walivamia Ofisi ya NANYUM na kupora pesa taslimu sh. milioni 433.

  Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa siku ya tukio hilo, kiasi cha fedha hizo zilichukuliwa kutoka Benki ya  NMB ya Lindi Mjini zikisindikizwa na polisi hadi kijijini Nambahu wakiwa na viongozi wa chama hicho Bw. Mohamedi Chilumba na Bw.Hassani Mundedu na fedha hizo zilikabidhiwa na kupokelewa na chama kupitia vitabu vya mahesabu.

  “Baada ya kupata taarifa ya tukio kutoka kituo cha polisi Tandahimba, polisi walikwenda kijiji hapo majira ya saa 4:30 usiku na kuchukua maelezo ya viongozi tisa wa NANYUM juu ya tukio hilo ambapo walitaka kupewa taarifa kama  kulisalia kiasi chochote cha fedha baada ya tukio.Lakini viongozi hao wote walikana kwamba hakuna hata kiasi kilichobakia” ilieleza taarifa hiyo.

  Aidha taarifa hiyo ilifafanua kwamba katika uchunguzi wa polisi ulibaini kati ya sh. milioni 443 zilizokabidhiwa kwenye chama hicho kutoka benki ya NMB tawi la Lindi hazikuibiwa zote. Hivyo baada ya wajumbe wa bodi hiyo kuhojiwa na polisi jumla ya sh. milioni 32 zilipatikana.Hadi sasa baadhi ya wajumbe hao wanashikiliwa na polisi ili kubaini upotevu wa fedha hizo.

  Taarifa hiyo ilieleza kwamba kama itathibitika kisheria kwamba viongozi wa chama hicho wamehusika katika tukio hilo na kupatikana na hatia ya wizi watalazimika kulipa fedha hizo na Serikali itaendelea kufuatilia matukio kama hayo na kuhakikisha kwamba wakulima wanapata haki zao.

  0 0

   Pichani pili kulia ni Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela na Katibu wa CCM Ndugu Mtaturu (kulia),wakiwa kwenye kivuko akitokea Mkoani Mwanza kuelekea Mkoani Geita kwenye ziara ya kikazi leo hii.
   Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene wakijadiliana jambo .

  0 0

  Assalaam aleikum,

  Mazishi ya mtoto wetu Maggid Michuzi aliefariki majuzi huko Afrika ya Kusini alikokuwa masomoni yamepangwa kufanyika Jumamosi saa 10 makaburi ya Kisutu jijini Dar. 

  Mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili kesho Ijumaa na Emirates kutokea Dubai ambako unapitia na kulala leo. Usafiri wa moja kwa moja wa Durban-Dar umeshindikana na ndio sababu ya kuchelewa kuwasili.

  Ratiba itaanza saa nne asubuhi Jumanosi kota za Wazo Hill cement, kisha msafara wa kuelekea makaburini kupitia Msikiti wa Maamur Upanga utaanza.

  Ankal na familia yake wanatoa shukrani sana kwa upendo na faraja mnaoendelea kuwapatia wakati huu mgumu.

  NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
  Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement Wazo, mbele mkono wako wa kulia utaona Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona uzio wenye rangi ya njano umeandikwa Twiga Cement, unakatisha hapo upande huo huo wa kulia. ukikatisha tu utaona kuna mtaa mwingine unaingia upande wa kulia, uache na usogee mbele, utaona mtaa mwingine unaingia kulia, ingia nao huo na utakuwa umefika msibani.

  Innalillah wa inna ilayhi raajiun
  -AMIN.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
   Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya tukio la uapisho. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Mwinyi alihudhuria pia sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Kikwete pia alihudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini wa Taifa la Uganda katika viwanja vya Kololo jijini Kampala. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Picha na IKULU

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa wa Sudani Kusini Salva Kir mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Picha na IKULU
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Picha na IKULU
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Picha na IKULU


  0 0

  Mhe. Makamu wa Rais leo ametembelea Wilaya ya Sengerema kata ya Sima ambapo usiku wa kuamkia jana kulifanyika mauwaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.Mhe. Makamu wa Rais Mama Suluhu Hassan ametoa masaa 24 kwa uongozi wa mkoa wa Mwanza pamoja na jeshi la polisi na vyombo vingine kuwatia nguvuni wale watu wote waliohusika na mauaji hayo.
  Pichani ni makaburi yakiandaliwa kwaajili ya kuzikwa kwa miili saba ya familia moja mapema leo Wilayani Sengerema .
  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akisalimiana na kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki kufuatia mauaji hayo ya watu wilayani Sengerema
  Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi Zainab Telack pamoja na Mkuu wa mkoa wa jiji la Mwanza Mh.John Mongella wakiwa na Mgeni wao Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu alipokewenda kutoa pole kwenye tukio la mauwaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ndani ya wilaya hiyo katika kijiji cha Sima mkoani Mwanza .
  Makamu wa Rais Mh Samia Sulluh akizungumza kwenye tukioa la mauwaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Mh.Samia ametoa sa a 24 kukamatwa kwa wale wote waliohusika na tukio hilo la Kinyama.

  0 0

  NAIBU Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameliambia Bunge Mjini Dodoma, leo tarehe 12 Mei, 2016, kwamba serikali inaandaa sera ya Taifa ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2016, itakayosimamia na kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo

  Alisema kuwa sera hiyo itawasilishwa mbele ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni kabla ya kupelekwa bungeni hatimaye itapatikana sheria ya kusimamia taasisi ndogo za fedha-microfinance Act, 2016.“Serikali inatambua changamoto ya taasisi binafsi za fedha zinazosumbua wananchi, hivyo sheria hiyo ikitungwa itasaidia kuondoa matatizo hayo” alisisitiza Dkt. Kijaji

  Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Rahisa Abdalah Musa (Viti maalumu), aliyetaka kujua serikali ilikuwa na mpango gani wa kudhibiti utitiri wa taasisi za fedha pamoja na mabenki ili yalete tija kwa Taifa kwa kuwakopesha wananchi

  Akijibu swali la msingi na maswali ya nyongeza yaliyoulizwa na Mhe. Faida Mohamed Bakar (Viti maalumu) aliyetaka kujua mikakati ya serikali ya kuanzisha benki ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili kuwawezesha kupata huduma bora, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa serikali haina mpango wowote wa kufanya hivyo.

  Alisema kuwa badala yake serikali inafanya jitihada za kuimarisha benki zake zilizopo ikiwemo Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya Rasilimali (TIB) ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara wa kada mbalimbali.

  “Serikali imeiboresha kimuundo, Benki ya Rasilimali (TIB) kwa kuunda kampuni tatu zinazofanyakazi kwa kujitegemea lakini kwa ushirikiano wa karibu” alisisitiza Dkt. Kijaji

  Alizitaja kampuni hizo kuwa ni TIB Benki ya Maendeleo itakayotoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa wafanyabiashara wakubwa na wa kati, TIB Benki ya Biashara itakayowahudumia wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na TIB Rasilimali itakayohusika na masuala ya ushauri kwenye Soko la Hisa na Mitaji la Dar es salaam

  “Pamoja na mambo mengine, kampuni hii inawajibika kuwashauri wafanyabiashara, hususan wa sekta ndogo ya fedha kupata mitaji kupitia Soko la Hisa la Dar es salaam” aliongeza Dkt. Kijaji

  Dkt. Kijaji alisema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kuboresha benki hizo, ikiwemo Benki ya Posta, Serikali kupitia Benki Kuu (BOT) inaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kutunga sheria, kanuni na taratibu za kusaidia nguvu za wananchi na sekta binafsi kuanzisha benki au taasisi za fedha katika maeneo yao

  “Ni matarajio yetu kuwa wananchi wanatumia fursa ya mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo nchini kuwekeza wao wenyewe au kuzishawishi benki za biashara kuanzisha huduma za kibenki katika maeneo yao” alisema Dkt. Kijaji

  Kuhusu ombi la mbunge huyo kuitaka serikali iingilie kati masuara ya riba zinazotozwa na taasisi za fedha na kuwaumiza wananchi, Dkt. Kijaji alisema kuwa serikali haiwezi kudhibiti wala kuingilia jambo hilo.

  Alisema kuwa Serikali ilijitoa katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za kifedha tangu mwaka 1991 ili kuruhusu ushindani huru na kuboresha huduma katika sekta ya fedha hivyo viwango vya riba na mikopo vinavyotozwa na benki hizo na taasisi nyingine za fedha zinapangwa kutokana na nguvu ya soko.

  Dkt Kijaji alieleza kuwa katika upangaji wa viwango vya tozo na riba mbalimbali benki na taasisi za fedha huzingatia gharanma za upatikanaji wa fedha, halikadhalika gharama za uendeshaji na sifa alizonazo mkopaji”Alisisitiza Dkt Kijaji

  Imetolewa na:

  Benny Mwaipaja
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango

  DODOMA
  12/5/2016

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe ( wa nne kutoka kulia) akisoma hotuba ya ufungaji wa mkutano wa siku tatu uliokutanisha wataalam wa masuala ya jotoardhi kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Marekani, New Zealand na Djibouti kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro nchini Uganda.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifunga mkutano huo. Kulia ni Mjiolojia Mkuu kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Jacob Mayalla.
  Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe (hayupo pichani)

  0 0

  Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha Dkt. Mohammed Alawi akiongea na baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani, ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Lyndsey Wajert akiwa tayari kufanyiwa vipimo vya malaria na Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha wakati wa ziara ya waandishi wa Habari hao ambao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mtaalamu wa Maabara Apolinary Mushi anayefanya kazi katika zahanati ya Ithna-Asheri iliyopo jijini Arusha akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Katy Migiro wa Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara mkoani Arusha kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari uwanja wa ndege wa Arusha kwa safari ya kuelekea mkoani Tanga.
  Eneo la ukingo wa Bahari ya Hindi mkoani Tanga ambapo karibu na eneo walipofikia waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakati wa ziara yao mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Tanga)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni jijini Kampala mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais Museveni.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni jijini Kampala mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nchini Uganda. PICHA NA IKULU.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Mei, 2016 amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo iliyofanyika katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.


  Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amempongeza Rais Museveni kwa kuapishwa kuwa Rais wa Uganda kwa kipindi kingine cha miaka 5 na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi Uhusiano, ushirikiano na udugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo.


  Viongozi hao pia wamezungumzia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima (Ziwa Albert) nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo pamoja na kuishukuru Uganda kwa uamuzi wake wa kuamua bomba hilo lipitie Tanzania, Rais Magufuli amemshauri Rais Museveni kufupisha muda wa ujenzi wa mradi huo, kwa kutumia mbinu inayojumuisha usanifu na ujenzi (Design and Construct method) na kutumia wakandarasi wengi watakaogawanywa katika vipande tofauti badala ya kutumia mkandalasi mmoja.


  "Nashauri tutumie mbinu ya usanifu na ujenzi pamoja, hii ni njia ya haraka zaidi, na pia tugawe vipande vya ujenzi kwa njia yote ya bomba la mafuta yenye urefu wa kilometa 1,410 tunaweza kuwa na Wakandarasi watano mpaka sita ambao watatumia njia hiyo mpya ya usanifu na ujenzi.


  "Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza muda utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, inaweza hata kuchukua mwaka mmoja tu" Amesema Rais Magufuli.


  Rais Magufuli amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo faida za mradi huo wa mafuta zitaanza kupatikana mapema badala ya kusubiri miaka miwili au mitatu ijayo, na kwamba hiyo itakuwa inaendana na kauli mbiu yake ya "Hapa Kazi Tu"Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kuipa Tanzania umiliki wa asilimia 8 katika mradi huo wa bomba la mafuta.

  Kwa upande wake Rais Museveni amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake kubwa ambazo amezifanya katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania.


  "Napenda kasi yako ya uongozi, napenda jinsi unavyopambana na rushwa, kwa sababu rushwa ilikuwa inazaa matatizo mengine kama vile ucheleweshaji wa mizigo bandarini na vikwazo vya mpakani, hivyo nakupongeza sana kwa hilo" Amesema Rais Museveni.


  Katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais Museveni iliyofanyika kabla ya mazungumzo hayo, pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine kutoka Tanzania waliohudhuria ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU

  Kampala

  12 Mei, 2016

  0 0

  Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva akiongea na mwandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Luis Velarde wakati wa ziara ya waandishi hao katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Mtaalamu wa maabara katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga akiendelea na kazi ya kufanya vipimo vya malaria kwa kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) ambayo majibu yake hutolewa baada ya dakika 15.Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa tayari wamewasili Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe.
  Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakimsikiliza Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja (hayupo pichani) walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
  Familia ya Salumu Rashidi wa kijiji cha Masatu kilichopo wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakiwa na mtoto wao Mohammedi Salimu ambaye ni miongoni mwa watoto waliopo kwenye mradi wa kudhibiti malaria wilayani huo. Kushoto ni mama yake Mohammedi Monica Mugunda.
  Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) wakitumbuiza wakati wa zaira ya waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani walipotembelea zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Tanga)

  0 0

  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akizungumza na wadau wa Habari kutoka Jukwaa la Wahariri, TMF, Sikika, Baraza la Habari Tanzania, Jukwaa la Katiba na TAMWA.
  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akimsikiliza Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw Deus Kibamba wakati alipokutana na wadau wa Habari Ofisini kwake.
  Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw Nevelle Meena akizungumza wakati wa Mkutano kati ya Katibu wa Bunge na wadau wa Habari.
  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw Theophil Makunga wakati wa Kikao kati ya Katibu wa Bunge na wadau wa Habari. Picha na Ofisi ya Bunge

older | 1 | .... | 845 | 846 | (Page 847) | 848 | 849 | .... | 1898 | newer