Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 837 | 838 | (Page 839) | 840 | 841 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Joseph Nyamhanga amewataka watumiaji wa Daraja la Nyerere (Kigamboni) kuzingatia matumizi bora na sahihi ya daraja hilo ikiwemo usafi ili kuliwezesha kukidhi matarajio ya serikali na kudumu kwa muda mrefu.

  Akizungumza katika kikao maalum cha wadau kutathimini viwango vya tozo vitakavyotumiwa katika daraja hilo Eng. Nyamhanga amewataka waendeshaji wa daraja hilo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuimarisha huduma ya ulinzi na usalama na kuwataka watumiaji wa daraja hilo kutumia fursa za uwepo wake kiuchumi na kijamii.

  “Hakikisheni tozo zitakazowekwa ziwiane na hali ya maisha ya wananchi ili kuwavutia wengi kupita katika daraja hili na kupunguza msongamano katika vivuko”, amesema Eng. Nyamhanga.Tozo hizo ambazo zitaanza kutozwa kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere hivi karibuni zinalenga kuwezesha NSSF kurudisha gharama za uwekezaji katika daraja hilo.

  Aidha, Katibu Mkuu huyo amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhujumu miundombinu na kukemea vitendo vya watu kufanya biashara katika daraja hilo.Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara amesema tozo kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere itaanza hivi karibuni baada ya kupitishwa na Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, hivyo amewataka watumiaji wa daraja hilo kutoa ushirikiano kwa watendaji ili kuwezesha huduma kufanyika kama ilivyokusudiwa.

  “Tumejipanga Vizuri na tutaanza kutoza watumiaji wa Daraja la Nyerere muda mfupi kuanzia sasa.” amesema Prof. Kahyarara.Zaidi ya shilingi Bilioni 214 zimetumika katika ujenzi wa Daraja la Nyerere ambapo asilimia 60 zimegharamiwa na NSSF na asilimia 40 zimegharamiwa na Serikali Kuu.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (katikati) akitoa ufafanuzi kwa wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji katika kikao cha kujadili viwango vya tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof Godius Kahyarara na kushoto ni Mkurugenzi wa barabara (Ujenzi) Eng. Ven Ndyamukama.

  Mkurugenzi wa Barabara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Ven Ndyamukama (Kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha wadau kujadili tozo za matumizi ya Daraja la Nyerere (Kigamboni). Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawsiliano Eng, Joseph Nyamhanga
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara (kulia) akitoa taarifa ya namna tozo zitakavyokusanywa kwa wadau mbalimbali wanaotumia Daraja la Nyerere zoezi litakaloanza hivi karibuni.

  Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Baiskeli akitoa maoni ya namna ya kuwahudumia waendesha baiskeli katika kikao cha kujadili tozo zitakazotumika kataka Daraja la Nyerere.
  Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kujadili tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere, Tozo hizo zitatangazwa hivi karibuni.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network'– TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza. 

  Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo leo baada ya kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii (bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.

  TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa aina yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers. 

  Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na kumshangaa mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono agizo hili, na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’ kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine yoyote.

  Imetolewa na;-
  Mwenyekiti wa Muda wa TBN
  Joachim E. Mushi
  03/05/2016

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. James Mlowe amekabidhi Jumla ya madawati 124 kwa ajili ya shule za Manispaa ya Kinondoni, msaada huo umetolewa na taasisi hiyo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 10,000,000/= yamekabidhiwa kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ali Hapi.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Salum Ally Hapi (wa pili kushoto) akimshukuru Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 124 kwa ajili ya Shule ya Msingi Nakasangwe iliyopo Kata ya Wazo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Salum Ally Hapi (kulia) akipokea msaada wa madawati 124 kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa mfuko wa pensheni wa LAPF, James Mlowe kwa ajili ya shule za Serikali Manispaa ya Kinondoni. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Kinondoni, Kiduma Mageni. 
  Mkuu wa Wilayaya Kinondoni, Salum Ally Hapi akizungumza katika hafla ya kupokea madawati 124 yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF jijini Dar es Salaam jana.
  Kaimu Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza katika hafla hiyo.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Bw. James Mlowe akizungumza katika hafla hiyo.

  0 0


  Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Victor Kimaro (wa kwanza kushoto) akizugumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) juu ya uwezo wao wa kumudu ukusanyaji wa kodi vizuri ili waweze kufanikisha vizuri malengo waliyo jiwekea mwaka huu. Pia aliwashukuru (ITA) kwa kujitolea kutoa elimu kwa wawekezaji wote wanaofika hapa nchini iliwaweze kulipa kodi wanapo wekekeza hapa nchini. alizungumza hayo Siku ya maadhimisho ya sherehe ya siku ya kodi zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano (TRA) Mwenge jijini Dar es Salaam 2016 Mdau akifafanua jambo kwenye sherehe ya siku ya kodi zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano (TRA) Mwenge jijini Dar es Salaam 201.
  Sehemu ya wadau mbalimbali waliohudhuria hizo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Victor Kimaro kwenye sherehe ya siku ya kodi zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano (TRA) Mwenge jijini Dar es Salaam 2016

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha walimu CWT Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Hamza Marwile akizungumza na walimu pamoja na viongozi wa halmashauri ya Rufiji katika kikao cha dhararu kilichofanyika nje ya ukumbi wa mikutano kwa lengo la kudai malimbikizo ya madai yao mbali mbali.
  Baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Rufiji wakiwa nje ya ukumbi wa mikutano wakimsubiria mkurugenzi kwa ajili ya kutoa malalamiko ya malimbikizo ya madai yao ya muda mrefu.
   

  MKURUGENZI wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Rashid Salum pamona na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Hatibu Chaulembo wamelazimika kutoka nje ya kikao cha baraza la madiwani baada ya uongozi wa chama cha walimu (CWT) wilayani humo kuvamia katika kikao hicho kwa lengo la kwenda kulalamikia madai yao ikiwemo malimbikizo ya mishahara yao.

  Walimu hao wa shule za msingi na sekondari wakiongozwa na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Rufiji walifunga safari ya kwenda katika ofisi ya Mkurugenzi huyo lakini waliambiwa yupo kikaoni ndipo walipoamua kuandamana mpaka kwenye ukumbi huo wa mikutano na ndipo walipomwandikia ujumbe wa kutaka kuonana nae ili watoe kilio chao.

  Wakizungumza kwa uchungu mara baada ya Mkurugenzi na Mwenyekiti kuamua kukubali na kuamua kuacha kuendesha kikao na kutoka nje ya ukumbi huo wa mikutano, Mwenyekiti wa CWT Hamza Marwile pamona na Katibu wake Antony Mangwary ndipo walipoamua kutoa malalamiko yao ya malimbikizo ya madai yao mbele ya viongozi hao wa halmashauri katika kikao cha dharura kilichofanyika chini ya mti huku mvua ikiendelea kunyesha.

  Mwenyekiti wa CWT Hamza Marwile alisema kwamba wameamua kufunga safari zaidi ya kilimota 75 kwa ajili ya kwenda katika ofisi za mkurugenzi kwa ajili ya kutoa kilio chao kwa muda mrefu kutokana na walimu walimu wa Wilaya hiyo kunyanyasika kutokana na kutopata haki zao za msingi.

  Marwile alisema katika siku za nyuma walikuwa wanapeleka malalamiko ya madai yao kwa mwajiri wao ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji lakini cha kushangaza madai hayo bado yalionekana kutofanyiwa utekelezaji wa haraka ndio maanda wakaamua kufunga safari ya kwenda kuonana na wahusika.

  Kwa upande wao baadhi ya walimu hao waliofunga safari kwenda kutetea haki zao za msingi akiwemo Yasinta Karo pamoja na Abdalahamani Mtupa walikuwa na haya ya kusema kuhusina na changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao .

  Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Hatibu Chaulembo amewataka walimu hao kuvuta subira na kuwa watulivu katika kipindi hiki cha madai yao kwani suala lao litashughulikiwa haraka iwezekanavyo ili kila mmoja aweze kupata haki yake ya msingi.

  Chaulembo alisema kwamba malalamiko hayo ya walimu yanatakiwa yaangaliwe kwa jicho la tatu kwani walimu katika Taifa hili ni watu wa muhimu sana hivyo kunahitajika kufanyike juhudi za makusudi katika kulivalia njuga suala hilo la kuwalipa madai yao mbali mbali.

  “Jamani pamoja na yote mimi kiukweli hii hali imenisikitisha sana maana leo tupo kwenye kikao chetu cha baraza la madiwani wa Wilaya ya Rufiji, lakini hatua ambayo mmeichukua walimu jamani sio jambo jema maana kikao kinaendelea sisi tupo nje haya mambo ya muhimu ilitakiwa tuyajadili kwa kina tukiwa tumekaa ofisini maana nyinyi walimu ni watu wa muhimu sana,”alisema Chaulembo.

  Akijibu malalamiko hayo kwa walimu katika kikao cha dharura kilichofanyika chini ya mti uku mvua ikinyesha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Rashid Salumu amekiri kuwepo kwa madai hayo ya walimu na kwamba na kuahidi kuyashughulikia.“Ni kweli kuna baadhi ya walimu hawa wanamadai yao mbali mbali lakini kitu kikubwa cha msingi napenda kusema tutashirikiana bega kwa baga na viongozi wao ili tuweze kuona ni namna gani tunaweza kulitafutia ufumbuzi suala hili kwa haraka ili walimu waweze kupata haki yao ya msingi,”alisema Mkurugenzi huyo.

  Aidha Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba kwa sasa changamoto zote zinazowakabili walimu wa wilaya ya Rufiji atayatafutia ufumbuzi wa kudumu kwa kushirikiana na idara mbali mbali na wizara zinazohusika lengo ikiwa ni kuhakikisha madai ya walimu wanafanyiwa utakelezaji na wanalipwa bila uonevu wowote.

  WALIMU hao wa shule za msingi na sekondari katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanadai kisi cha zaidi ya milino 500 kutoka na madai mbali mbai ikiwemo, kupandishwa madaraja,vitambulisho vya kazi,malimbikizo ya mishahara, fedha za likizo,uhamisho, pamoja na matibabu.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (aliyesimama) akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (aliyesimama) akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kushoto Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal. 
  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Kulia) akiwasilisha Mada ya Utambulisho wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuhusu Huduma zitolewazo na Benki, Mpango shirikishi wa Kumsaidia Mkulima Mdogo kupata mkopo na utalaam wa kilimo cha kisasa kwa kuwashirikisha wadau wakuu wa Kilimo katika kumkwamua mkulima mdogo wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (Wapili kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Wapili kulia) wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakulima wadogo waliohudhuria warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.


  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yatoa mkopo wa 890 Milioni kwa wakulima wa zao la mpunga wanaojishughulisha kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Mkula wilayani Kilombero ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga.

  Hayo yaliwekwa bayana na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal wakati wa warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

  Bw. Paschal alisema lengo la mkopo huo unaowanufaisha zaidi ya wakulima 350 ni kuongeza tija na uzalishaji wa mpunga ili Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

  “Mkopo huu na mengine tunayotoa imelenga kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini,” alisema Bw. Paschal.

  Kwa mujibu wa Bw. Paschal mkopo huo utasaidia shughuli mbalimbali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mpunga pamoja na kuwezesha upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na madawa.

  Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Benki imetoa mkopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mpunga ili kuongeza thamani wa zao hilo.

  “Tunaamini mkopo huu utachagiza kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula na Pato la Taifa kutokana kuongezeka kwa tija na uzalishaji hivyo kuwa chachu ya ongezeko la thamani, ukuaji wa viwanda vya mazao ya kilimo hivyo kuchangia kuongezeka kwa ajira nchini,” aliongeza. 

  Akizungumzia mikakati ya TADB kwa sasa, Bw. Paschal alisema Benki imejipanga kutoa mikopo ya Muda Mfupi, Mikopo ya Muda wa Kati na Mikopo ya Muda Mrefu kwa kutumia njia mbalimbali. Mbinu hizo zinajumuisha pamoja na mambo mengine; mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo; kutoa mikopo kwa njia ya marejesho taasisi zinazokopesha; utoaji wa mikopo kwa pamoja na kushirikiana na taasisi/benki zingine; pamoja na mikopo ya miundombinu inayolenga kupunguza mapengo ya upatikanaji wa fedha katika minyororo ya ongezeko la thamani ya kipaumbele.

  “Kwa kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo nane (8) ya minyororo ya uongezaji wa thamani ambayo ni: nafaka, kilimo cha mboga mboga, kilimo cha bidhaa za viwanda, mbegu za mafuta, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji kuku, ufugaji wa samaki na bidhaa za misitu. Benki pia inajitahidi kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambazo zimeelekzwa kwenye kuendeleza kilimo,” alisema.

  Warsha hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe ambaye alitoa rai kwa Wakulima wote waliopata fursa ya kuhudhuria warsha hiyo kujipanga katika kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na TADB. Mhe. Gembe zingatia mada zilizowasilishwa ili waweze kunufaika na Benki hii na shughuli zinazotolewa na Taasisi zingine za serikali

  “Nawasihi mrudishe mikopo mtakayopewa kwa wakati ili wakulima wengine waweze kunufaika zaidi na Benki hii na vile vile kuwezesha Benki kutoa huduma kwenye maeneo mengine ya Tanzania,” alisema.

  0 0

  Picha ya Pamoja Meza kuu na washiriki wa semina hiyo.
  Meneja wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Hiraly Maskini akifungua Mkutano wa wadau wa soko la Bima kutoka Mikoani ya Nyanda za Juu Kusini (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya Mei 3 -2016 mkutano ambao unalengo la kujadili na kutambua changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wadau hao katika kutekeleza majukumu yao.(Picha Emanuel Madafa,Jamiimojablogu-Mbeya) 
  Wadau wa soko la Bima Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juuu Kusini,Mbeya,Iringa,Njombe ,Rukwa ,Songwe na Katavi wakiwa katika umakini kufuatilia agenda mbalimbali katika mkutano huo ulioandaliwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bima Nchini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (TIRA).
  Kaimu Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Mbeya Ndugu Victory Mleleu akichangia moja ya maada katika mkutano huo ulihusisha wadau wa soko la Bima Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) semina ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Mei 3 mwaka huu.
  Mhasibu wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Kurenje Mbura akiwasilisha moja ya maada katika mkutano wa wadau wa Soko la Bima ulioitishwa na Mamlaka hiyo ya (TIRA ) Mei 3 Mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya. 

  Mmoja wa wadau wa soko la Bima Mkoani Mbeya Ndugu Masterdy Luvanda akichangia maada katika mkutano wa wadau wa Soko la Bima ulioitishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) katika Ukumbi wa Mkapa jinini Mbeya Mei 3 mwaka huu, ukiwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali wanazo kutanana nazo wadau hao sanjali na kupeana uzoefu katika sekta hiyo.

  0 0

  a32603a8-b5b0-41d7-8533-7baf03333277

  Mwanzilishi wa Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha moja na Getrude Clement ambaye atalipiwa ada ya kidato cha tano na cha sita.

  Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha miaka ijayo, Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla iliyoanzishwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla imejitolea kumlipia ada Getrude Clement kwa masomo yake ya kidato cha tano na sita.

  Uamuzi huo wa kumsomesha Getrude umekuja baada ya leo kukaribishwa kuongea kwenye kikao cha wabunge watetezi wwa haki za watoto ambapo Getrude alipata nafasi ya kutoa historia yakee ambayo iliwatoa baadhi ya wabunge machozi.

  Getrude aliwaeleza wabunge historia yake na hali yake ya kimaisha na kusema kuwa baba yake ni kinyozi na mama yake anafanya biashara ndogo ndogo za nyanya na vitunguu lakini bado amekuwa akijtuma katika masomo yake ambapo kwa sasa yupo kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Mnarani, Mwanza.

  Baada ya kusema hivyo ndipo Dkt. Kigwangalla aliamua kujitoa kumsaidia mtoto huyo ili aweze kujiendeleza zaidi kielimu na kufikia malengo yake na zaidi akiahidi kumsomesha katika shule za kisasa ili apate elimu bora zaidi.
  ce18d8f2-cd50-4b46-8193-3351745537ac
  “Kwa kuthamini kipaji chake na mchango wake na kutambua nafasi yangu kama Naibu Waziri kwenye Wizara inayosimamia mambo ya Watoto na kama mbunge na mzazi wa mabinti, lakini zaidi kama mtu kutoka kwenye background ya maisha ya chini na ninayethamini mchango wa elimu kwenye maisha yangu, nimeamua kujitolea kumsomesha kidato cha tano na cha sita kwenye shule za kisasa,“Taasisi yangu ya misaada ya kijamii ya Hamisi Kigwangalla Development Foundation itamlipia ada za masomo yake ya high school,” alisema Dkt. Kigwangalla.

  Getrude Clement ambaye ana miaka 16 amepata nafasi hiyo ya kipekee baada ya kupata nafasi ya kutoa hotuba kwa niaba ya watoto na vijana wengine duniani katika mkutano wa Umoja wa Mataifa ambapo alikaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na kusifiwa na watu mbalimbali duniani kutokana na hotuba yake nzuri.
   

  0 0

  Ofisa kilimo wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Claudy Losiock (kulia) akizungumza juzi na baadhi ya madiwani na mkuu wa wilaya hiyo Mahmoud Kambona (kushoto) kwenye shamba lake ambalo ni darasa kwani amelima na kupanda kitaalamu.Madiwani hao walionekana kuvutiwa mno na elimu hiyo ya shamba darasa la Mahindi.(picha na woinde shizza, Simanjiro).

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Mafinga mkoani Iringa Bw Cosato Chumi (kulia) akimpongeza wakili wake Asheri Utamwa baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kutoa hukumu iliyompa ushindi mbunge Chumi kufuatia kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Chadema Bw Willy Mungai. 
  Mbunge wa jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi akiweka sawa bendera ya ubunge leo kabla ya kuondoka viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa baada ya kushinda kesi ya uchaguzi ,kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Bw Jimson Mhagama katibu mtoto nchini Tanzania 
  wakili maarufu wa Chumi Bw Asheri Utamwa (kushoto ) akizungumza na wanahabari baada ya mteja wake Chumi kulia kushinda kesi ya uchaguzi leo .

  Na Fredy Mgunda,Iringa

  CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimempongeza mbunge wa jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi baada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Bw Willy Mungai .

  Akizungumza na wanahabari leo nje ya viwanja wa mahakama kuu kanda ya Iringa baada ya mahakama kutoa huhukumu iliyompa ushindi Bw Chumi ,katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Bw Jimson Mhagama alisema kuwa baada ya hukumu hiyo ya mahakma kumpa haki mbunge huyo wa CCM kazi kubwa iliyobaki kwa sasa ni kuona utekelezaji wa ilani ya CCM unafanywa kwa nguvu zote.

  “Hapa kwa hukumu hii haki imeweza kutendeka kwani kabla ya kutoa hukumu jaji alisoma na kutolea ufafanuzi wa vipengele vyote ambavyo mlalamikaji alikuwa anavilalamikia na baada ya hapo ndipo alipoweza kutoa hukumu ya kesi hiyo “

  Hata hivyo alisema pamoja na hukumu hiyo kutolewa bado wanachama wa Chadema na wale wa CCM katika jimbo la Mafinga hawana budi kuendelea kuwa wamoja ili kushikamana na mbunge wao kuleta maendeleo jimboni .

  Kwani alisema suala hilo la kesi mahakamani mbali ya kuchelewesha majukumu ya mbunge kwa wananchi wake bungeni bado lilikuwa likimfanya mbunge muda wote kuwa ni mtu wa kuwaza kesi badala ya kuwaza namna gani ya kuwatumikia wananchi wake.

  “ Ninawaomba wenzetu Chadema wasifikilie kukata rufaa kuendelea na kesi hiyo kwani katika hoja zao zilizopelekea kwenda mahakamani ufafanuzi umetolewa vizuri na jaji hivyo kuendelea kukata rufaa ni kuendelea kuwacheleweshea wananchi wa jimbo la Mafinga kupata maendeleo “

  Pia alimtaka mbunge huyo Bw Chumi kufidia muda ambao ameupoteza kwa kushinda mahakama kusaka haki kwa kwenda kuwatumikia wananchi wake kwa kasi ya hapa kazi tu ili jimbo hilo lizidi kusonga mbele kwa maendeleo.

  Kwa upande wake Mbunge Chumi alisema anapenda kuwashukuru wananchi wake wa jimbo la Mafinga ambao walitoa ushirikiano kwa kufika mahakamani kutoa ushahidi muda wote na kuwa zaidi anamshukuru mwenyezi Mungu kwa kusimamia haki katika kesi hiyo . 

  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.

  Serikali itaendelea kusimamia haki ya mtoto wa kike ya kupata elimu na kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwapeleka mahakamani wale wote wanaowapata ujauzito wanafunzi na kuwakosesha kupata elimu ambayo ni haki yao ya msingi.

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seriklali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Janeth Mbene wa Ileje baada ya kujibu swali la msingi lililohoji kuhusu kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.

  “Serikali haitamvumilia mwanaume yeyote atakayempa ujauzito mwananfunzi na kukwamisha kupata elimu kwa wakati na kumharibia malengo ya maisha yake” alisema Naibu Waziri Jafo.Hatua hiyo ya Serikali itawahakikishia na kuwawezesha watoto wa kike nchini kusoma na kumaliza masomo yao hatua ambayo itakuwa msaada kwa watoto hao wa kike, familia zao na taifa kwa ujumla. 

  Akisistiza msimamo wa Serikali kuhusu wanaume wanaowapa ujauzito wanafunzi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa Serikali haipo tayari kuwavumilia wanaume wenye tabia ya kuwakwamisha watoto wa kike kupata elimu kwa kuwapa ujauzito na itahakikisha sheria inachukua mkondo wake ili kukomesha tabia hiyo.

  Akizungumzia tatizo hilo la wanafunzi kupata ujauzito wakiwa shuleni, Mbunge wa Jimbo la Igunga Seif Khamis Gulamali alisema kuwa tatizo hilo lipo sehemu mbalimbali nchini ambapo watoto hubebeshwa mimba wakiwa katika umri mdogo wa kuwa shuleni na tatizo hilo linaendelea kuleta hasara kubwa kwa wanafunzi wenyewe, familia zao na taifa kwa ujumla.

  Gulamali alisema kuwa hali hiyo inatokana na hulka ya makabila mengi nchini hasa ya wafugaji hali inayosababishwa na tabia ya kuhama hama kutafuta malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao.“Wapo wazazi wanaowapa maelekezo watoto wao wasifaulu mitihani yao ili waweze kuolewa na wamegeuzwa kuwa sehemu ya kipato cha familia zao kwa kupata mahari” alisema Gulamali.

  Ili kukomesha tabia hiyo ya kuwapa ujauzito watoto wenye umri mdogo hasa kwa wafugaji, Gulamali alisema kuwa ipo haja ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuweka mazingira mazuri ambayo yatawapa wananchi wengi fursa ya  kuwekeza kwenye sekta ya kilimo na mifugo kwa kuwahakikishia upatikanaji wa maji kwa wingi ili wananchi wazalishe na kuondokana na tabia ya kuhama hama kwa wazazi wao ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa watoto kupata elimu. 

  Kuhusu shilingi milioni 50 zilizoahidiwa na Serikali kwa kila kijiji hapa nchini, Gulamali alisema kuwa ni vema ufikiriwe mfumo wa kupeleka hizo fedha ambao utakuwa wa tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla utakaohkikisha fedha hizo zitakuwa endelevu na kuwarahisishia wananchi kazi na kuongeza uzalishaji wa mazao yatakayowaongezea kipato.

  Hatua hiyo itasaidia taifa kuwa na matumizi bora ya rasilimali fedha zinazotolewa na Serikali kwa kuwekeza kwenye sekta za viwanda, mifugo, uvuvi na kilimo ambapo Tanzania kuna mvua ya kutosha, mabonde yenye rutuba, mito, maziwa, bahari pamoja na watu ambao ndio msingi wa maendeleo kwa taifa kwa kuongozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa ifikapo 2025 Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.

  0 0

  Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa ikiwemo kutumbuiza.Pia imeufungia wimbo na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini.

  Taarifa hiyo imetolewa mapema leo na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp.

  Ameeleza kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.


  0 0

  Mkurugenzi wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege akimuelezea jambo Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

  TIB Corporate Bank imefadhili mkutano mkuu wa bodi ya usajili wa wakandarasi nchini unaotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya Malaika kuanzia tarehe 5 hadi 6 mwezi huu wa tano ikifuatiwa na mkutano mwingine utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond Jubilee kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano. 

  Mkutano huo, ambao mwaka huu una kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu: Changamoto na Mipango ya baadae?, unalenga kuwakutanisha wadau na wakandarasi kujadili mchango wa wakandarasi na ushiriki wao katika kukuza uchumi wa nchi.

  Akizungumzia udhamini wa katika mkutano huo, Mkurugenzi wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege alisema benki yake inazifahamu changamoto zinazowakabili wakandarasi wengi nchini ikiwemo ukosefu wa fedha ambao unazuia kupanua na kuendeleza uwezo wao wa kushindana katika sekta ya ujenzi hasa katika kupata zabuni na utekelezaji wa mikataba.

  TIB Corporate Bank imeweka misingi ya kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake na ndio maana tumeweza kuja na suhulisho kwa ajili ya kuwasaidia wakandarasi kuweza kuendesha shughuli zao kwenye mazingira yao ya kazi’ alisema Bw.Nyabundege.

  Bwana Nyabundege pia alisema udhamini wa mkutano wa wakandarasi unalenga kujenga na kuimarisha uwezo wa wakandarasi kupata fursa ya kuendeleza sekta ya ujenzi nchini.TIB Corporate Bank ilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za nyongeza za kibenki kama mtaji wa kufanyia kazi, mikopo pamoja na uwezeshaji wa kibiashara kwa ajili ya wateja mbalimbali kupitia ubunifu wa teknolojia, kukuza thamani kwa wadau na pia kuchangia katika ujenzi wa taifa kwa kutoa huduma mtambuka za kifedha na kuchangia ukuaji wa uchumi shindani sambamba na Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025.

  TIB imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo cha huduma zote za kifedha kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa ndani wote kwa lengo la kusukuma maendeleo ya uchumi wa taifa.

  0 0


  Sehemu ya wadau mbalimbali waliohudhuria hizo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Victor Kimaro kwenye sherehe ya siku ya kodi zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano (TRA) Mwenge jijini Dar es Salaam 2016. Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Victor Kimaro (wa kwanza kushoto) akizugumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) juu ya uwezo wao wa kumudu ukusanyaji wa kodi vizuri ili waweze kufanikisha vizuri malengo waliyo jiwekea mwaka huu. Pia aliwashukuru (ITA) kwa kujitolea kutoa elimu kwa wawekezaji wote wanaofika hapa nchini iliwaweze kulipa kodi wanapo wekekeza hapa nchini. alizungumza hayo Siku ya maadhimisho ya sherehe ya siku ya kodi zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano (TRA) Mwenge jijini Dar es Salaam 2016.
  Mdau akifafanua jambo kwenye sherehe ya siku ya kodi zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano (TRA) Mwenge jijini Dar es Salaam 2016.

  0 0

  Teresia Mhagama na Mohamed Saif

  BENKI ya Dunia (WB) imeahidi kutoa Dola za Marekani milioni 4 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 8, kwa ajili ya Ruzuku  katika shughuli za uchimbaji mdogo wa madini nchini.


  Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumaliza kikao na watendaji Wakuu wa Benki ya Dunia wanaosimamia Miradi ya Sekta ya Madini.


  Profesa Muhongo alisema kuwa sehemu ya fedha hizo za Ruzuku ambayo ni ya Awamu ya Tatu zitatolewa mwezi Septemba, 2016.

  Aliongeza kuwa fedha hizo zitatumika kufadhili uendelezaji wa vituo Saba vya mfano vya utafutaji na uchimbaji mdogo wa madini ambavyo vitachaguliwa na Wizara baada ya kufanya tathmini ya maeneo yanayoweza kuwekwa vituo hivyo.


  “Sio hivyo tu, Fedha hizi za Benki ya Dunia zinalenga kuwafadhili wanawake kwenye shughuli za uchimbaji mdogo wa madini, ukataji na uchongaji wa madini ya vito ili idadi ya wanawake wanaojishughulisha na Sekta ya Madini iongezeke,” alisema Profesa Muhongo.


  Aidha, Profesa Muhongo alitoa wito kwa wataalam wote wanaosimamia miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia katika Sekta ya Madini kuhakikisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo uende kwa kasi ili kuleta matokeoyaliyotarajiwa.                                                                                                                                                                                                                                                           
  Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeendelea kutoa Ruzuku katika Uchimbaji madini mdogo ambapo katika mwaka wa Fedha 2015/16 zilitengwa takribani Shilingi bilioni 7.2 ambazo zilitolewa kwa vikundi 111 vya wachimbaji wadogo na watoa huduma mbalimbali katika sekta ya uchimbaji madini mdogo.


  Vilevile, katika mwaka wa Fedha 2013/2014, Fedha za Ruzuku zilizotolewa kwa Wachimbaji Wadogo zilikuwa ni Dola za Marekani 500,000 sawa na takribani Shilingi Bilioni 1 zilizotolewa kwa waombaji 11. Fedha hizi ziliwalenga wachimbaji madini wadogo pekee tofauti na awamu zilizofuata.


  Utoaji huo wa Ruzuku unaenda sambamba na utoaji wa elimu na mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini waliopata ruzuku husika ili kuhakikisha kuwa shughuli zilizopata ufadhili zinaleta tija.

  0 0

   Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania Mariam Mwapinga akisisitiza jambo mbele ya waandishi (hawapo pichani)  kuhusu kampeni maalumu kuhamasisha matumizi ya kituo  cha  huduma  kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu cha benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.. Wengine ni pamoja na Mkuu wa kitengo cha hazina wa benki hiyo , Bw. George Shumbusho (katikati) na Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja  wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro (kushoto).
  Mkuu wa kitengo cha hazina benki ya Exim Tanzania , Bw. George Shumbusho (kulia), akikata utepe kuzindua kampeni maalumu kuhamasisha matumizi ya kituo cha  huduma  kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu cha benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni pamoja Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja  wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro (kushoto).

  BENKI ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalumu kuhamasisha matumizi ya kituo chake cha  huduma  kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuhakikisha inawarahisishia wateja wake upatikanaji wa huduma  zake kupitia  teknolojia ya mawasiliano.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa hafla fupi ya kuzindua kituo hicho,  Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja  wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro alisema matumizi ya kituo hicho  yatawawezesha wateja wa benki hiyo kupata taarifa za kina kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
  “Ni matarajio yetu kwamba wateja wetu watafurahia zaidi huduma bora kutoka kwa wahudumu wenye vigezo na uelewa wa kutosha kuhusiana na masuala ya kibenki kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni na siku za Jumamosi kuanzia saa 3 kamili asubuhi hadi saa 7:00 mchana kupitia namba yetu ya 0784 107 600,’’ alisema.
  Kwa mujibu wa Bw Matoro kituo hicho tayari kimekwisha anza kutoa huduma huku akibainisha kuwa malengo ya kampeni hiyo ni kuhakikisha wateja wa benki hiyo wanatambua uwepo wa kituo hicho na kutumia ipasavyo huduma zitolewazo na kituo hicho.
  “Katika kuhakikisha kwamba kampeni hii inaleta mafanikio, itaambatana na  droo ndogo ndogo zitakazowezesha utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wateja  zikiwemo fulana zenye nembo ya benki, muda wa maongezi pamoja na simu mpya aina ya iPhone 5s,’’ alitaja.
  Aliongeza kuwa huduma zinazotolewa na kituo hicho zinatolewa kupitia mazungumzo kwa njia simu, mitandao ya kijamii ikiwemo ukurasa wa Facebook na njia nyingine za kimtandao kama vile website na barua pepe.
  Bw. George Shumbusho, mkuu wa kitengo cha hazina aliongeza kwamba: “Pia tunatarajia kwamba mafanikio ya huduma hii yatatuongezea ukubwa wa soko kwa kuwa itapanua wigo wa kuwafikia wateja, kujiongezea ukuaji wa fursa  sambamba na kutoa fursa kwa wateja wetu waweze kutupa mrejesho wa huduma mbalimbali tunazowapatia,’’

  0 0

  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akitoa hoja kwa Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma huku akishudiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo (hayupo pichani) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wake Maria Mnkumbo (katikati) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma. Kushoto ni mke wa Waziri Mwigulu Neema.
  Mwalimu msataafu Maria Mnkumbo aliyemfundisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma.

  0 0

  Mhusika Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda) akimbembeleza muigizaji na mtayarishaji wa filamu hiyo Bi Sarah Nyika (Asha Mauno) mara baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kusitizaji usambazaji wa filamu hiyo.( Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO).
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso akizungumza na waigizaji wa filamu ya “Imebuma” (Hawapo Pichani) wakati wa ukaguzi wa filamu hiyo kabla ya kupelekwa sokoni kulia ni 2 Afisa Utamaduni Bw. Julius Tairo.
  Afisa Utamaduni Bw. Julius Tairo (wa Pili Kushoto) akitoa maelekezo kwa waigizaji wa filamu ya “Imebuma” (Hawapo Pichani) wakati wa ukaguzi wa filamu hiyo kabla ya kupelekwa sokoni kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso.
  Mhusika Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda) akitoa maelezo kuhusu filamu hiyo wakati wa ukaguzi wa filamu ya “Imebuma” kabla ya kupelekwa sokoni kulia ni waigizaji wa filamu hiyo.( Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM)

  Na Shamimu Nyaki WHUSM

  Bodi ya Filamu Tanzania imesitisha usambazaji wa filamu ya “Imebuma” mpaka pale maudhui yake yatakapofanyiwa marekebisho.

  Akisitisha usambazaji wa filamu hiyo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso amesema mtengenezaji wa filamu hiyo hana kibali cha kutengenza filamu kutoka Bodi ya Filamu na hajazingatia Sheria na kanuni za utengenezaji wa filamu.

  Bi Joyce Fisso amesema filamu hiyo imesitishwa kwenda sokoni kutokana na kukiuka vifungu vya kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 2011 ambayo inakataza kuonesha namna yoyote ya udhalilishaji wa kibinadamu katika filamu na maigizo.

  “Baada ya kuangalia kwa makini filamu hii na kuona mapungufu ambayo yanakinzana na Kanuni za Sheria ya filamu na Michezo ya kuigiza nimeamua kuisitisha usambazaji wake mpaka pale wahusika watakaporekebisha maudhi yake” Alisema Bi Joyce.

  Bi Joyce amefafanua kuwa filamu hiyo imeonesha baadhi ya matukio ya udhalilishaji wa kibinadamu, ushawishi wa matendo ya ngono na ushoga ambayo ni kinyume na madili ya mtanzania.

  Aidha kwa upande wake Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Julius Tairo amewataka waandaaji na waigizaji wa filamu nchini kufanya utafiti wa kutosha kuhusu maudhui ya filamu kabla ya kutengeneza ili kuondokana na utengenezaji wa filamu zisizofata Sheria na kanuni za utengenezaji wa filamu Tanzania.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Zawadi Msalla (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapopichani) wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu kusitishwa kwa wimbo wa Msanii Snura Mushi ujulikanao kwa jina la Chura kwa kukiuka maadili kushoto ni Mwanasheria wa wizara hiyo Bw. Patrick Kipangula na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi. Lily Beleko.
  Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Patrick Kipangula akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapopichani) wakati wizara hiyo ikitoa tamko la kusitishwa kwa wimbo ujulikanao kwa jina la Chura ulioimbwa na msanii Snura Mushi kwa kukiuka maadili, kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi. Zawadi Msalla.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa naMichezo Bi. Zawadi Msalla (hayupopichani) wakatia kitoa tamko la Serikali kuhusu kusitishwa kwa wimbo wa Msanii Snura Mushi ujulikanao kwa jina la Chura kwa kukiuka maadili.


  Serikali imesitisha wimbo na Video ya Muziki wa Chura wa Msanii Snura Mushi kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuanzia leo mpaka pale msanii huyo atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo.

  Usitishwaji huo umetokana na maudhui ya utengenezwaji wa Video hiyo ambayo haiendani na maadili ya Mtanzania.

  Pia Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya mwanamziki huyo mpaka pale atakapo kamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

  Serikali inawataka wasanii kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za Sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao watazipokeaje? Wavae nafasi ya wale wanaowadhalilisha, Waelewe kwamba Sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu hata kidogo..

  Aidha Serikali imechukizwa na kazi hiyo ambayo si tu inadhalilisha tasnia ya Muziki bali inadhalilisha utu wa mwanamke na inaifanya jamii kuanza kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya Sanaa kwa ujumla.

  Serikali inawakumbusha wananchi wote kutokujiingiza katika makosa ya sheria ya mtandao kwa kusambaza wimbo huu kwa njia yoyote ile ya kimtandao

  Pia inavitaka Vyombo vya habari viwe vya kwanza kuchuja maudhui ya kazi yoyote ya Sanaa kabla ya kuwa mawakala wa uharibifu wa jamii kupitia kucheza kazi chafu za Sanaa.

  Serikali inatoa wito kwa wasanii wote kuzingatia maadili ya Kitanzania kabla ya kutoa kazi zao kwani haitawavumilia ‘wasanii’ wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya Sanaa kuwa sehemu ya uvunjifu wa maadili.

  Imetolewa na Zawadi Msalla

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

  0 0

  Katibu Mkuu wa National Reconstruction Alliance (NRA) Hassan Kisabya Almas amewataka Watanzania wanaoomba Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonyeshwa  kupitia matangazo ya moja kwa moja (Live) kuomba  kwa utaratibu bila kuharibu amani ya Tanzania.

  Aidha Katibu Mkuu wa Chama hicho, amesema  kwamba   amani iliyoko ni hazina kubwa ambayo nchi nyingine inatamani kuwa nayo. 

  Almas aliyasema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO). 

  “Leo hii tupo tunaopigania kutaka kuona Bunge Live, lakini yote haya ni kwa kuwa Tanzania amani tunayo, sidhani kama nchi kama Afghastan siku watakayoamua kuonyesha Bunge Live kwa mwaka mzima, kwa saa 24 kama wataweza kukaa kuangalia Bunge hilo, hivyo basi wale wanaotaka hayo, kwanza tudumishe amani  yetu,” alisema Almas.

  Almas alieleza kuwa, amani ya Tanzania ni zaidi ya dhahabu ambayo Tanzania inajivunia hivyo ni lazima Watanzania kuitunza na kuithamini amani ambayo ipo kwa sasa na kuacha kuchochea mambo ambayo yanaweza kuleta machafuko katika nchi na amani ambayo leo haithaminiwi ikaja kukumbukwa siku moja.

  Pia, alisema yeye ni mmojawapo wa watu wanaopenda kuona Bunge Live lakini jambo hilo halishadadii kama inavyofanywa na watu wengine kwani anajua kwa kufanya hivyo anaweza kuhatarisha Amani ya Tanzania na hata hilo Bunge halitaweza kuliona tena kutokana na kutokuwa na Amani ndani ya nchi.

  Vilevile, amewataka waandishi wa habari kuandika yale yaliyo mazuri ya nchi kuliko mabaya machache ili kuzidi kuitangaza Tanzania vyema kimataifa, kwani sio uzalendo kuona mambo yote mabaya yanakuwa ukurasa wa kwanza, bali kwanza yarekebishwe kwakuwa ni makosa yanayoweza kurekebishwa. Kalamu za waandishi wa habari ni chachu ya amani na maendeleo ya Taifa la Tanzania.

older | 1 | .... | 837 | 838 | (Page 839) | 840 | 841 | .... | 1898 | newer