Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 836 | 837 | (Page 838) | 839 | 840 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe wakitoka kukagua nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.

   : Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.

  Moja ya nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani. Kaimu Mkurugenzi Mkuu /Mkurugenzi rasilimali Watu na Uendeshaji wa TBC Bi.Joycelin Lugora akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Mkurugenzi wa wilaya ya Kisarawe (DED) Kisarawe Bi. Mwanamvua Mlindoko na kushoto ni
  Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura.
  Baadhi ya wafanyakazi wa TBC na Wanahabari wakitoka kujionea hali halisi wakati Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe alipokwenda kukagua nyumba za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.PICHA NA ANNA NKINDA.


   

  Wambura-Sitakubali Rasilimali za Taifa hili  zichezewe.
  Na.Daudi Manongi-WHUSM

  Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.

  Mhe.Wambura alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011 mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.

  “Taratibu za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema Mhe Wambura.

  Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi  kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa  na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja. 

  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma..

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara baada ya tukio la uapisho.  PICHA NA IKULU.


  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma..

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara baada ya tukio la uapisho.  PICHA NA IKULU.
  0 0

  Kikosi kazi cha watanzania wanaoishi Falme za UINGEREZA na EIRE YA KASKAZINI (TZUK Diaspora Taskforce, kwa kifupi, TZUK-DTF) kiliasisiwa na Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe mwaka 2014, kutokana na kutokuwepo na chombo/Jumuiya madhubuti ya kuwaunganisha Watanzania waishio hapa Uingereza

  TZUK-DTF ilianza na wajumbe 11 wakiwemo maofisa wa ubalozi 2 kikiwa na majukumu makubwa ya kuwa kiunganishi kati ya watanzania na ubalozi wao hapa Uingereza pamoja na kupanga na kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya watanzania ambayo itakuwa shirikishi zaidi na endelevu. Mnamo mwishoni mwa mwaka 2015, chini ya Naibu Balozi, Mheshimiwa Msafiri Marwa, ilikubaliwa kwamba ili kutimiza malengo yake kwa ufanisi zaidi yaliyohusisha kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya watanzania Uingereza na kuhakikisha kwamba Jumuiya hiyo inakuwa na Katiba iliyo bora zaidi, ilionekana ni vyema TZUK-DTF ikawa na wajumbe zaidi watakaojumuisha watanzania wa kada mbalimbali walioko Uingereza wakiwemo waliokuwa viongozi wa mikoa wa Jumuiya na baadhi ya wale walioshiriki katika michakato ya uasisi wa katiba na uundwaji wa Jumuiya ya watanzania Uingereza.

  Kikosi Kazi hiki kipya kilikutana rasmi tarehe 05 Mwezi wa Kumi na Mbili, 2015, chini ya uongozi na ulezi wa Mheshimiwa Naibu Balozi, Msafiri Marwa, ambapo kiliainishiwa majukumu yake kama ifuatavyo:
  1. Kujadili na kuziwekea mikakati ya ufumbuzi changamoto mbalimbali zilizokabiliwa na TZUK-DTF katika kutimiza majukumu yake ikiwemo na zile ambazo ziliikabili Jumuiya ya watanzania iliyokuwepo.
  2. Kupitia maoni ya watanzania yaliyokuwa yamekusanywa tayari, ikiwemo na katiba za Jumuiya ili Jumuiya iwe na katiba bora zaidi itakayoongeza ufanisi katika shughuli zaJumuiya.
  3. Kuhakiki na kuboresha muundo wa Jumuiya utakaokidhi mahitaji ya sasa ya watanzania waishio Uingereza.
  4. Kuzikusanya na kuzipitia taarifa zote zitakazopatikana za fedha za Jumuiya enzi za uhai wake na kuzijumuisha kwenye Jumuiya mpya itakayoundwa
  5. Kutengeneza na kuratibu njia bora zamawasiliano miongoni mwa wanajumuiya.
  6. Kusimamia kipindi cha mpito kitakachopelekea kuundwa kwa Jumuiya ya watanzania Uingereza ikiwemo kuratibu uanzishaji/uimarishaji wa Jumuiya za watanzania za mikoani kwa mujibu wa katiba mpya, na 
  7. Kuandaa na kusimamia mkutano mkuu wa watanzania wote wa Uingereza wenye madhumuni ya kutoa ripoti nzima ya TZUK-DTF, kupitisha katiba mpya, kutambulisha Kamati Kuu na uongozi mpya wa Jumuiya, kujadili na kuhakiki mipango na mikakati ya shughuli mbalimbali za Jumuiya kwa mwaka ujao, na Kikosi Kazi kuvunjwa rasmi na kukabidhi madaraka ya  usimamiaji na uendeshaji wa Jumuiya ya watanzania kwa uongozi mpya wa Jumuiya.

  Kama watanzania wa  Uingereza mlivyoshiriki  katika upendekezaji wa katiba mpya na kutoa maoni juu ya Jumuiya yenu, tunaendelea kuwatia moyo kushiriki kwa moyo mmoja na wa kizalendo pindi tutakapoitisha mikutano ya watanzania kwenye mikoa mliyoko mwezekuhakikisha safari hii ya kuwa na Jumuiya iliyo/zilizo imara inafikia mwisho ulio mwema.

  Ahsanteni

  0 0

  Kamati Maalum iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015 imekamilisha rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.

  Akizungumza Katika kikao cha Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mheshimiwa Jaji Mstaafu kwa niaba ya Wajumbe wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume kwa sasa.

  Mheshimiwa Jaji Mstaafu Lubuva amesema Tume yake imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ya Kwanza ikiwa ni pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo na kuongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa Taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais mapema mwezi Julai mwaka huu.

  Aidha pongezi kama hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Ramadhan Kailima wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Tume akieleza kufurahishwa kwake na namna ambavyo dhana ya ushirikishwaji imetumika katika kuandaa Rasimu hiyo.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliratibu na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kuanzia Otoba 25 mwaka jana na kuhitimisha rasmi zoezi hilo Machi 20 mwaka huu kwa Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele mkoa wa Kaskazini Unguja.

  0 0
 • 05/03/16--01:37: Article 1
 • Watch the Media day event live as it happens, celebrated nationally in Mwanza, through barmedas.tv HD on http://www.ustream.tv/channel/barmedasonline-tv


  0 0   RATIBA YA KUWASILI NA MAZISHI YA MPENDWA WETU
  ANDREW NICKY SANGA
  Ndugu zetu pamoja na Marafiki; Kwa niaba ya Familia ya Bwana Nicky Amon Sanga, Kamati ya Maandalizi inapenda kuwajulisha Ratiba ya Safari ya Mpendwa wetu ANDREW NICKY SANGA hapa Tanzania kuanzia kuwasili kwa mwili wa Marehemu hadi tutakapomweka kwenye nyumba yake ya Milele.  Muda
  Tukio
  Mahali
  Wahusika
  DAR ES SALAAM
  Jumanne 3 Mei 2016
  3:55 Usiku
  Mwili kuwasili
  Uwanja wa Ndege: Julius Nyerere
  Familia, Ndugu, Marafiki na Jamaa Wote
  4:30-5:30 Usiku
  Kuelekea Kuhifadhi Mwili
  Hospitali ya Taifa Muhimbili
  Familia, Ndugu na Marafiki na Jamaa Wote
  Jumatano 4 Mei 2016
  4:00-6:00 Asubuhi
  Ibada ya Kuaga
  Kanisa la Kilutheri Ubungo (Nyuma ya Ubungo Plaza)
  Familia, Ndugu, Marafiki na Jamaa Wote.
  6:30 Mchana
  Safari ya Kuelekea Dodoma
  Kanisa la Kilutheri Ubungo
  Wote Waliojiandaa.
  DODOMA
  5:00:-6:00 Asubuhi
  Chakula
  Nyumbani- Kizota
  Waombolezaji Wote
  6:00
  Kuelekea Uwanja wa Mashujaa

  Waombolezaji Wote
  6:30-7:20 Mchana
  IBADA
  Uwanja wa Mashujaa
  Waombolezaji Wote
  7:30-8:45 Mchana
  Heshima za Mwisho
  Uwanja wa Mashujaa
  Waombolezaji Wote
  8:46 Mchana
  Kuelekea Makaburini

  Waombolezaji Wote
  9:20 Mchana
  Mazishi
  Makaburi ya Hijra Chinangali
  Waombolezaji Wote

  Familia inazidi kutoa shukrani za dhati kwenu wote kwa jinsi mlivyokuwa pamoja nasi tangu mwanzo wa tukio hili hadi sasa. Mungu wa Mbinguni Awabariki Sana.


  BWANA Ametoa, BWANA Ametwaa, Jina la BWANA Lihimidiwe.


  Imetolewa na Dr. George LongopaKNY Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam

  Simu 0754 870969  0 0

   Washindi wa shindano la bahati Nasibu la Fiesta condoms Bw & Bi. Justin Tinieshimo wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma. Washindi hao waliweza kufurahia siku saba za mapumziko mjini Dubai katika safari iliyodhaminiwa na Shirika la DKT Tanzania katika kutekeleza ahadi ya ushindi wao wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa Chapa mpya ya “Fiesta condoms” miezi miwili iliyopita Ledger Plaza hotel jijini Dar es salaam.
  Mwakilishi wa shirika la DKT Tanzania Bi. Hellen Kimati akitoa zawadi ya shada la maua kwa washindi wa shindano la bahati nasibu la Fiesta condoms Bw & Bi. Justin Tinieshimo mara baada ya wageni hao kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma.
   Mshindi wa shindano la bahati nasibu Bi. Gloria Tinieshimo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili akitokea mapumzikoni Dubai mwishoni mwa juma. (Kulia) ni mume wake Bw. Justin Tinieshimo ambaye aliongozana naye katika safari hiyo ya wiki nzima iliyodhaminiwa na shirika la DKT Tanzania mara baada ya wawili hao kuibuka washindi wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa chapa ya Fiesta condoms miezi miwili iliyopita Ledger Plaza hotel jijini Dar es salaam.

  KATIKA jitihada za kutangaza matumizi ya njia za uzazi wa mpango na kuzuia mimba zisizotarajiwa na magonjwa yanayo ambukizwa kwa kujamiiana (STDs) nchini, miezi miwili iliyopita katika siku ya wapendanao (valentine day), DKT International Tanzania shirika lisilo la kiserikali ambalo ni moja kati ya watoaji wakubwa wa bidhaa za uzazi wa mpango na afya ya uzazi nchini ilifanya uzinduzi wa aina mbalimbali za kondom zenye ubora zilizopewa jina la “Fiesta kondom” huko Bahari Beach Ledger Plaza hotel, Dar es salaam.

  Wakati wa uzinduzi, shindano la bahati nasibu lilifanyika ambapo wanandoa watatu walishinda safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda na kurudi Zanzibar, Afrika ya kusini na Dubai.


  Wakielezea msisimko wao wakati wa kurudi kutoka katika safari yao mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), washindi wa safari ya kwenda Dubai ambao walitembelea Dubai kwa mara ya kwanza walifurahia wiki nzima ya kukaa na kutalii Dubai na Abu dhabi, waliishukuru DKT International Tanzania kwa kutimiza ahadi yao na kwa kuifanya safari yao kuwa ya kukumbukwa.
  Katika mahojiano wakiwa uwanja wa ndege, washindi walisema kuwa safari imewapa fursa ya kutembelea sehemu za kusisimua huko Dubai kama Burj Khalifa, ambalo ni jengo refu kuliko yote Dubai, maduka makubwa ya kufanyia manunuzi pamoja na mashindano ya mbio za magari ya Formula one huko Dubai.

  “Nimefurahia sana kupata safari hii ya kusisimua kwenda Dubai na mke wangu. Tuliweza kujionea wenyewe na kushuhudua mengi yanayoongelewa kuhusu jiji la maajabu. Ninapenda kuishukuru DKT International Tanzania kwa fursa hii nzuri na tunaahidi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Fiesta kondom kila wakati ambapo tutahitajika kufanya hivyo. Alihitimisha bwana Justin Tinieshimo.
  Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Fiesta Kondom bwana Davis Kambi amesema “Tunafuraha kuhitimisha safari ya washindi wetu wa safari ya Dubai na wanashukuru kuwa na fursa hiyo ya kukumbukwa wakiwa Dubai.” Nyakati kama hizo ndizo ambazo zinahusu bidhaa ya Fiesta Kondom, kuleta wanandoa karibu katika nyakati za upendo; DKT International Tanzania imejidhatiti kulete wanandoa pamoja chini ya kampeni za Intimacy by Fiesta ambazo zitahakikisha wanandoa wengine wanapata safari ya kwenda katika sehemu za mbalimbali mwaka huu.
  Bwana Kambi alitumia fursa hiyo kuhakikisha kuwa washindi wa zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar tayari walisha kwenda na walisha rejea.
  Aliwashukuru wote walioshiriki katika kuhakikisha kuwa shindano la bahati nasibu la uzinduzi wa Fiesta Kondom Valentine limefanikiwa. Fiesta Kondom itafanya tena tamasha la kukutana la wanandoa mwaka ujao ambapo wanandoa wataweza kushinda zawadi nzuri.
  Bidhaa ya Fiesta Kondom ya DKT International Tanzania ilizinduliwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na inapatikana katika nchi zaidi ya 40 duniani kote na sasa katika mikoa yote mikubwa ya Tanzania. Fiesta ina zaidi ya ladha 55 tofauti za kondom na zaidi ya aina 60 tofauti. Lakini kwa kuanzia DKT International Tanzania imetambulisha aina 5 tofauti; Fiesta Heat, Fiesta Ultra-thin, Fiesta Strawberry, Fiesta Max dotted and Fiesta Neon! DKT International Tanzania inapanga kuzindua aina zingine 3 za kondom zinazokamilishwa kwa utofauti wa aina mbalimbali kabla ya mwisho wa mwaka 2016.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Bw. John Mponda (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
  Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Fransis Songoro (aliyesimama) akiwasilisha mchango ulitolewa katika kamati ndogo ndogo zilizoundwa wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
  Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Hajjat Shani Kitogo (aliyesimama) akiongoza majadiliano jana Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe ya 21 Mei.
  Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Sefania Motela (aliyesimama) akichangia wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.
  Baadhi ya Maafisa Utamaduni na Wadau wa Utamaduni wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea wakati wa kikao cha kamati ya maandalizi ya siku ya Utamaduni Duniani inayotarajiwa kuadhimisha tarehe 21 Mei mwaka huu.Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

  0 0

  Kaimu Muuguzi Mkuu wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Flora Kasembe, (wapili kulia), akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wagonjwa waliolazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi cha JKCI, wakati Naibu Balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (wapili kushoto), alipotembelea kambi ya upasuaji wa moyo iliyoendeshwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya hiari ya Uinegereza ya Muntada Aid, Mei 3, 2016. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Mohammed Y.Janabi, Meneja Mradi wa Muntada Aid, Kabir Miah, Mkuu wa Upasuaji wa JKCI, Dkt.Peter Kisenge, na Daktari Bingwa wa Moyo wa JKCI, Dkt.Tulizo Shem 
  Profesa Janabi (kushoto) na Balozi Sutherland baada ya kutembelea chumba cha Coronary care unit

  NA K-VIE MEDIA/Khalfan Said

  NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, (pichani wapili kushoto), ameisifu taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa.

  Pongezi hizo amezitoa leo May 3, 2016, baada ya kutembelea kambi hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo, na kujionea madaktari wakiendelea na kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini.

  “Nimefurahishwa sana na uamuzi wa JKCI wa kuratibu zoezi hili kwa ushirikiano na wataalamu wa magonjwa ya moyo kutoka nje ya nchi, najua taasisi ya hiari kutoka Uingereza imekusanya fedha na kwa kushirikiana na madaktari wengine, wamewezesha zoezi hili kufanyika kwa mafanikio.” Alisema Balozi Sutherland.

  Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na vifaa, na hatimaye kwa kushirikiana na madaktari na wataalamu wengine kutoka JKCI wameweza kufanya upasuaji wa watoto 20 hadi sasa.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Janabi alisema, chini ya uratibu wa taasisi yake, wataalamu kutoka Australia kupitia Open Heart International, wakishirikiana na wataalamu kutoka JKCI waliendesha kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto 15 kuanzia Aprili 25 hadi Aprili 30.

  “Kambi hii ya sasa, inaundwa na wataalamu kutoka Saudi Arabia chini ya uratibu wa taasisi ya hiari ya Muntada Aid, yenye makazi yake nchini Uingereza, na hadi leo hii Mei 3, 2016, tayari watoto 20 wameshafanyiwa upasuaji na hivyo kufanya jumla ya watoto 40 wamefanyiwa upasuaji tangu kambi hizi mbili zianze.” Alifafanua Profesa Janabi kwenye mkutano na waandishi wa habari.

  Profesa Janabi alisema, malengo yao ni kuwafanyia upasuaji watoto 70 Ifikapo Mei 7. “Tunawashukuru wenzetu hawa kwa kuja kutshirikiana nasi kwani upasuaji unaofanyika ni huu wa kisasa, ambapo hakuna kumpasua kifua mgonjwa bali tunafanya upasuaji kwa kutumia matundu na hili ni jambo muhimu kwa wataalamu wetu ambao wamepata fursa ya kujifunza kutoka kwao.” Alisema.
  Profesa Janabi (wapili kulia), wengine kutoka kulia, ni Balozi Sutherland, Dkt. Shem, na Dkt.Delila Kimambo
  Wataalamu wa JKCI wakiwa kazini kwenye mojaya vyumba vya upasuaji
  Balozi Sutherland, katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka JKCI na wale wa Muntada Aid
  Profesa Janabi, akimsikiliza mgeni wake, Balozi Sutherland
  Dkt.StellaMongella. (kushoto, akimpatia maelezo Balozi Sutherland, alipotembelea wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji (Post Operative Recovery Word), Kulia ni Profesa Janabi.
  Balozi Sutherland, akiwapongeza wataalamu wa moyo kutoka Muntada Aid, wanaoshuhudia ni Profesa Janabi (kulia na Dkt. Tulizo Shem kutoka JKCI.
  Baadhi ya Watanzania wakisubiri huduma ya matibabu ya moyo.
  Kiongozi wa timu ya madaktari kutoka Muntada Aid, (katikati)
  Dkt. Tulizo Shem akiongea
  Balozi Sutherland akipokewa kwenye taasisi alipowasili

  0 0


  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Temesa Mhandisi Manase Ole-Kujan akitoa taarifa juu ya kusimamia kwa huduma za Mv Magogoni inayofanyiwa Matengenzo makubwa.
  Wananchi wakipita katika daraja la Nyerere lilopo Kigamboani Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli hivi karibuni.
  Kivuko cha Mv Magogoni kikiwa katika shughuli zake za kila siku za kutoa huduma kwa wananchi. (Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Kivuko cha Mv Magogoni kinachotoa huduma kwa wananchi kutoka upande wa bahari eneo la Magogoni kuelekea Kigamboni Jiji la Dar es Salaam kimesitisha kutoa huduma kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo makubwa.

  Katika taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase Ole Kujan kwa niaba ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa kuanzia Mei 5 2016 kivuko hicho kitakuwa katika matengenezo makubwa ambayo yatafanya kusitisha huduma zake kwa muda.

  Taarifa hiyo imesema kuwa huduma za kivuko zitaendelea kama kawaida kwani wananchi watatumia huduma ya kivuko cha Mv Kigamboni pamoja na kivuko kilichokodishwa na Serikali kutoka kampuni ya Azam Marine vitavyokuwa vinasaidia kutoa huduma kwa wananchi kwa muda wote ambao Mv Magogoni itakuwa katika matengenezo.

  “ Muda wake wa matengenezo umefika na ni wakati muafaka kwa kivuko kwenda kwenye matengenezo ni muda mrefu kimetumika na kusimama kwa kivuko hiki hakutaleta madhara makubwa kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa daraja la Nyerere hivi karibuni tuna imani wananchi watatumia daraja hili ili kendelea na shughuli zao za kila siku” imesema taarifa hiyo.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo wananchi wenye magari wanaotumia vivuko hivyo wameshauriwa kutumia daraja jipya la Nyerere ili kuepukana na usumbufu wa kusubiri kivuko pekee cha Mv Kigamboni chenye uwezo wa kubeba magari na kufafanua kuwa kivuko kutoka Azam Marine kina uwezo wa kubeba watu peke yake.

  Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa matengenezo ya kivuko cha Mv Magogoni yatafanyika Jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Temesa katika matengenezo ya mitambo na ukarabati na ujenzi utafanywa na kampuni ya kizawa ya na Songoro Marine Transport Yard yenye makao makuu yake Jijini Mwanza.

  Aidha kivuko cha Mv Magogoni kitakabidhiwa kesho kwa kampuni ya Songoro Marine Transport Yard kwa ajili ya matengenzo hayo na mara baada ya mkandarasi kuangalia hali ya kivuko atatoa muda kamili wa kumalizika kwa matengenezo ya kivuko hicho.

  Serikali katika katika jitihada za kupunguza msongamano katika vivuko hivyo imeamua kwenda kukifanyia ukarabati mkubwa ili kukiongezea uwezo na ufanisi wa kuhudumia wananchi kwa kusaidiana na daraja jipya la Nyerere lililozinduliwa na Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt john Pombe Magufuli hivi karibuni ili kuondoka na tatizo la msongamono kwenye vivuko vya Kigamboni.

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU. 

  0 0

   Afisa Habari toka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bwana Saidi Makola akichangia mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.
   Dkt. Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye alimwakilisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina kwa Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi akisoma taarifa ya Mkurugenzi toka Wizarani leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
  Afisa Habari toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Catherine Sungura akichangia mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam.
   
   Msimamizi wa Mradi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Geofrey Mchau akitoa mada mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko ya tabianchi nchini wakati wa Semina Maalum kwa Waandishi hao leo 3 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam. 


  Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

  Wanahabari nchini wametakiwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na afya.

  Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Bi. Neema Rusibamayila wa Wizara hiyo, Dkt. Azma Simba wa Kitengo cha Epidemolojia amesema kuwa suala la kuielimisha jamii lina umuhimu ndo maana kuna haja ya Wizara kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza suala hilo.

  Ameeleza kuwa Shughuli za kibinadamu zinachangia kwa kiasi cha asilimia 95 katika kuzalisha na kuongeza kiasi cha gesi joto katika kwenye anga hewa ambapo amezitaja baadhi ya shughuli hizo zikiwemo za uzalishaji viwandani, uzalishaji nishati, kilimo,ufugaji, ukataji miti, uchomaji misitu, usafirishaji, pamoja taka. 

  Akitaja athari za mabadiliko ya tabianchi, Dkt. Azma ameeleza kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa joto juu ya wastani, ukame, mafuriko, vimbunga, kubadilika kwa mgawanyo na muda mvua kunyesha pamoja na kuongezeka kwa kina cha bahari.

  ‘’Sisi sote ni mashahidi wa mabadiliko ya hali hewa yalivyokuwa tishio katika afya ya binadamu. Mabadiliko hayo yameendelea kuleta athari mbalimbali kwa jamii, mazingira na afya ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, hewa safi, uhakika wa upatikanaji wa chakula na makazi salama’’, alisema Dkt. Azma.

  Ameongeza kuwa athari hizo zimepeleke uwepo wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambikiza ikiwemo malaria, kuhara, kipindupindu, homa ya bonde la Ufa, denge, utapiamlo, magonjwa ya mfumo wa upumaji na magonjwa ya mfumo wa fahamu.

  ‘’Jamii ina fursa ya kuboresha afya yake na vizazi vijavyo endapo itaamua kubadilisha mfumo wa maisha unaochangia uzalishaji na ongezeko wa jotogesi unaoharibu (ozone) yaani tabaka hewa’’, aliongeza Dkt. Azma.

  Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa Global Framework For Climate Services toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Geofrey Mchau amesema kuwa halli ya hewa na tabianchi vinaweza kubadilika kiuhalisia (Naturally) au binadamu wenyewe ambapo amefafanua kuwa lengo la semina hiyo ni kuoingeza wigo wa matumizi wa taarifa ya hali ya hewa katika sekta mbalimbali ikiwemo afya pamoja kuwajengea uwezo Wataalam katika ngazi ya Wizara kimkoa pamoja na Wilaya.

  ‘’Tupatapo taarifa zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa toka Mamlaka ya Hali ya Hewa tunazitafsiri na tunazitumia kwa manufaa ya jamii’’, alisema Dkt. Mchau.

  Naye Afisa Habari toka Hospitali ya Taifa Muhimbili Bwana Saidi Makola ameeleza kuwa tafiti zinazoendelea zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la magonjwa yatonayo na mfumo wa hewa na hayo yanatokana na mabailiko ya tabianchi, hivyo uwepo wa semina hiyo kwa Wanahabari utasaadia kutambua masuala mbalimbali na kuwajengea uwezo katika kuelimisha jamii.

  Aidha, Afisa Habari toka Wizarani hapo, Bi. Catherine Sungura amewaasa Wanahabari kuzingatia katika kutafuta taarifa mbalimbali ili kuweza kuelimisha jamii kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu afya.

  Semina hiyo imehusisha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).


  0 0

  Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akiwajazia fomu baadhi ya wanachama wapya katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 walijiunga na NSSF.
  Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni kwa katika banda la NSSF kwa ajili ya kujiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. (Picha na John Dande).
  Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amani Marcel (kushoto) akiwakabidhi fulana wanachama wapya, Emmanuel Joseph na Prisca Mwamsojo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama 214 waliandikishwa. 
  Ofisa Msajili wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Grace Mutegeki (kushoto) akiwaelekeza jambo baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na mfuko huo katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilayaya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango akimjazia fomu ya kujiunga na NSSF mchuuzi wa mayai wakati wa kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Jumla ya wanachama wapya 214 walijiunga na NSSF. 
  Baadhi ya wananchi wakisoma fomu kabla ya kujiunga na NSSF katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachama wa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam.
  Watu mbalimbali wakisubiri kujiandikisha.
  Afisa Uandikishaji wa NSSF, Amina Kisawaga, kushoto akiwaelekeza jambo baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika kampeni maalumu ya kuelimisha na kuandikisha wanachamawa Hiari kampeni zilizoanzia Wilaya ya Temeke kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam juzi. Zaidi ya wanachama 20 walijiandikisha.

  0 0

  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila akiongea na Viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na SUMA – JKT kwenye Ofisi za Bunge, Jijini Dar es Salaam kuhusiana na namna walivyojipanga katika kutekeleza jukumu la utengenezaji wa Madawati ya shule hapa nchini. 
  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila akiongoza mazungumzo na Viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na SUMA – JKT(hawapo pichani).
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo wakifuatilia kwa makini mazungumzo na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Thomas Kashilila(hayupo pichani).
  Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri akifuatilia mazungumzo hayo na Maofisa Watendaji wa Shirika hilo la SUMA – JKT.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja akiteta jambo na Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C. Yateri walipokutana leo Mei 3, 2016 katika Ofisi za Bunge, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri tarehe 03 Mei, 2016 katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma.PICHA NA IKULU

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika.
  Spika wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Seneta la Lesotho Mhe Seeiso Berenge Seeiso na kushoto ni senate kutoka Bunge la Afrika Mhe. Bennette hayatoe
  Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Tanzania wakila kiapa cha uaminifu. Kutoka kushoto ni Mhe. Asha Abdalah Juma, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. David Silinde na Mhe. Mboni Mhita.

  Na Owen Mwandumbya, Midrand Afrika Kusini.

  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika liweze kuwa Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina budi kujikita katika umoja na mshikamono.

  Mhe. Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.

  Akizungumzia changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi alisema nchi nyingi barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana ambayo ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo ambayo yanahitaji suluhisho la Pamoja kuyakabili..

  “ katika duniani ya sasa ni vyema tukakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa pamoja. Matajiri hawawezi kuepuka athari za umasikini na ukosefu wa amani. Kinachotokea eneo moja kinaathiri maeneno mengi mathalani vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi katika maeneo mengi duniani” alisema Ndugai

  Akizungumzia nafasi ya wabunge katika kupiga vita changamoto zinazolikabili bara la Afrika, Mhe. Ndugai amesema wabunge wa Bunge la Afrika kama wawakilishi wa Manbunge ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanawajibu wa kutetea maslahi ya Bara la Afrika bila kujali itikadi za kisiasa, maeneo wanayotoka na mambo mengine yanayoweza kuligawa bara la Afrika.

  “ Mkiwa Wabunge mnaowakilisha nchi zenu katika Bunge hili, nilazima mhakikishe Umoja wa Afrika unasimamia ipasavyo masalahi ya bara la Afrika ili kutimiza ndoto waliokuwa nayo waasisi wa umoja huu wa Afrika. Kwa mfano baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere alisema lazima tukimbie wakati wengine wakitembea” aliongeza Ndugai

  Mapema akitoa salamu za Bunge la Lesotho, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Mhe. Nthloi Motsamai alisifu juhudi za Mwalimu Julius Nyerere pamoja na waasisi wengine wa bara hili katika kuimarisha umoja wa Afrika na kuwataka wabunge wa Bunge la afrika kuhakikisha mawazo ya viongozi hawa ya kulifanya bara la afrika kuwa moja yanatimia.

  Katika hatua nyingine, wabunge wa Tanzania wanaowakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika walikula kiapo cha uaminifu kuwa wabunge wa Bunge hilo baada ya Bunge la Tanzania kuwachagua mapema mwezi Januari.

  Wabunge hao ni pamoja na Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. Mboni Mhita, Mhe. David Silinde na Mhe. Asha Abdalah Juma. Mhe. Ndugai anatarajia kurejea nchini kesho jumatano ambapo Bunge la Afrika linaendelea na Vikao vyake hadi tarehe 13 Mei, 2016.

  0 0

  Mwenyekiti wa taasisi ya Muzdalifa Shekh Abdalla Hadhar Abdalla akimkabidhi Mchele Afisa msaidizi wa kambi ya wahanga wa mafuriko Makame Khatibu Makame iliopo Skuli ya Mwanakwerekwe C Mjini Zanzibar.
  Afisa msaidizi wa Kambi ya Mafuriko iliyopo Skuli ya Mwanakwerekwe C Makame Khatib Makame, akitoa shukrani kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Muzidalifa Shekh Abdalla Hadhar Abdalla kwa msaada waliowatia.
  Baadhi ya Misaada mbalimbali iliyotolewa na Taasisi ya Muzdalifa.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Muzdalifa Shekh Abdalla Hadhar Abdalla akimkabidhi Box la dawa Daktari dhamana kanda ya Unguja Fadhili Moh’d, katika Kambi ya kipindupindu iliopo Mtaa wa Chumbuni Zanzibar.
  Daktari dhamana kanda ya Unguja Fadhil Moh’d, akitoa shukurani kwa msaada waliopatiwa na Taasisi ya Muzdalifa
  Baadhi ya Madawa mbalimbali iliyotolewa.Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.

  0 0


  Meneja Rasilimali watu wa Airtel, Bi, Gabriella Kaisi (kulia) akiwapongeza James Kwayu (katikati) na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na aiira katika kampuni ya Airtel kupitia ushirikiano kati ya Airtel na chama cha wanafunzi vyuoni Tanzania AIESEC wenye lengo la kuwawezesha vijana walioko vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
  Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Bi, Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi Abubakar Nassor baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka. 
  Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi akimkabithi cheti cha pongezi James Kwayu baada ya kufaulu mitihani na kuajiriwa na Airtel katika kitengo cha huduma kwa wateja kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika katika makampuni mbalimbali kila mwaka
  Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na James Kwayu na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na ajira kupitia ushirikiano kati ya Airtel na AIESEC Tanzania (chama cha wanafunzi vyuoni) wenye lengo la kuwawezesha vijana waliokoa vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.

  ·        Airtel yatoa ajira kwa wanafunzi wenye vipaji katika vyuo vikuu

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini kongamano la ajira  kwa vijana wa chuo kikuu linaloandaliwa na AIESEC Tanzania  lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri (makapuni) na waajiriwa watarajiwa (wanafunzi)  kwa lengo la kuwapatia Fursa zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli za kiuchumi.

  Kila Mwaka AIESEC huandaa kongamano la ajira kwa vijana linaloshirikisha wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Kuanzia mwaka jana Airtel  imejikita na kushiriki  katika kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.

  Akiongea kuhusu mpango huo, Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Tunaamini kila kijana ana nafasi ya kufikia ndoto zake  na ndio mana tunatoa fursa  kwa vijana kufanya kazi pamoja nasi. 

  Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu kutoka vyuo vikuu vya IFM pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam kupata ajira katika ofisi zetu za Airtel. Vijana hao ni pamoja na Abubakar Nassor ambaye anafanya kazi katika kitengo cha masoko James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.

  Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika makao makuu ya Airtel  nchini Kenya na India  kwa muda wa mienzi miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangia kufanya katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi aliongeza Kaisi

  Akiongea kuhusu program hiyo, moja kati ya waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema” najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi 2 nitakayokuwa  nchini India na Nairobi,   nahaidi kuitumia fursa hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu

  Mwaka huu Airtel imejipanga kuendelea kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kutoa ajira kwa vijana wengine watano ambao watafanya vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali inayoendelea kwa sasa.  Airtel itatangaza majina ya wanafunzi wengine watakaofudhu na kuchaguliwa kwa mwaka huu mara baada ya hatua za uajiri zitakapokamilika


older | 1 | .... | 836 | 837 | (Page 838) | 839 | 840 | .... | 1898 | newer