Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 830 | 831 | (Page 832) | 833 | 834 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na ujumbe kutoka Mtandao Kijinsia Tanzania (TGNP) walipofika ofsini hapo kwa ajili ya kutoa shukrani zao.
  Mwanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP), Bi Gema Akilimali akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada zilizofanyika katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.

  WANAHARAKATI WA Mtandao wa kijinsia “TGNP” wamepongeza juhudi zinazofanywa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), kutokana na Mabadiliko na jitihada zinazofanywa na Dawasco za kuboresha huduma ya Maji pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii inayoizunguka. 

  Akizungumza katika kikao cha pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni ya Maji ya “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha Samwel. Ameitaka Dawasco kuhakikisha inapeleka huduma ya Majisafi na salama katika sehemu zote muhimu ikiwamo mashuleni na hospitalini ili kumpunguzia mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu pamoja na kumuondolea mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa kutokana na kuhangaika kutafuta Maji. 

  “Tunataka kutoa salamu za pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko na jitihada tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya kusaidia jamii, tumefurahishwa na jitihada zenu, tutafanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta Maji kwani kampeni yenu ya “MAMA TUA NDOO YA MAJI KICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi. Martha. 

  Aidha, Mwanaharakati wa mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali, amefurahishwa ya kampeni ya Mama tua ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke kwa kiasi kikubwa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji, pia anaamini utaongeza ufaulu mashuleni kwani badala ya watoto wa kike kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa wataweza kuokoa muda na kuwa kushiriki masomo ipasavyo. 

  “Wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta Maji, hivi ni saa ngapi ataleta maendeleo ya nchi? Lazima tumkwamue mama katika janga hili ili na yeye aweze kujenga nchi yake” alisema Bi. Akilimali. Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amehaidi hadi kufikia Disemba 31 watahakikisha kampeni ya mama tua ndoo ya Maji kichwani itawafikia wakazi wengi wa Dar hususani wale walio katika tabaka la chini. 

  Aidha amehaidi kutoa huduma ya Majisafi na salama bure kwa wazee, walemavu na yatima wote ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kuunganisha huduma ya Maji, pamoja na kujenga pointi za ya kunywea Maji katika sehemu mbalimbali za Jiji ikiwa ni pamoja na maeneo ya stendi ya Mabasi ya Ubungo, Buguruni chama, Magomeni Mapipa na Kisutu stendi ya zamani. 

  “Mimi pamoja na menejimenti yangu tunaenda kumtua mama ndoo ya Maji kichwani mpaka kufikia mwishoni wa mwaka huu, kwani Maji yatakuwa mengi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam pamoja na Pwani” alimalizia Mhandisi Luhemeja

  0 0

  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso akizungumza na wadau wa filamu katika kikao cha usuluhishi wa madai ya kupewa nakala halisi ya filamu kati ya mtengenezaji filamu nchini Bw. Carlos Johns Johns kutoka Happy Time Production na mtunzi wa filamu ya Nyota ya Jaha Bw. Emmanuel Mayunga.
  Mtunzi wa filamu ya Nyota ya Jaha Bw. Emmanuel Mayunga (wa pili kulia) akizungumza katika kikao cha usuluhishi wa madai ya kupewa nakala halisi ya filamu kati yake na mtengenezaji filamu nchini Bw. Carlos Johns kutoka Happy Time Production kilichofanyika chini ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso.
  Mtengenezaji filamu kutoka Happy Time Production Bw. Carlos Johns Johns akizungumza katika kikao cha usuluhishi wa madai ya kupewa nakala halisi ya filamu kati yake na mtunzi wa filamu ya Nyota ya Jaha Bw. Emmanuel Mayunga kilichofanyika chini ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso, kulia ni Afisa Utamaduni Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Simon Peter.
  Maafisa Utamaduni Bodi ya Filamu Tanzania pamoja na wadau wa filamu wakimsikiliza mtunzi wa filamu ya Nyota ya Jaha Bw. Emmanuel Mayunga akijieleza wakati wa kikao cha usuluhishi wa madai ya kupewa nakala halisi ya filamu kati yake na mtengenezaji filamu Bw. Carlos Johns kutoka Happy Time Production kilichofanyika chini ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso.

  0 0

  Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na mali zilizopo jiji la Dar es Salaam kuwa zipo chini ya jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita. 
  Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea akionyesha baadhi ya nyaraka za siri za jiji la Dar es Salaam ambazo wameanza kuzichambua kwaajili za kutambua mali zilizo chini ya jiji la Dar es Salaam. katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Afisa habari wa Ukawa, Gasto Makwembe.
   Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuanza kuchunguza mali za jiji la Dar es Salaam, (Katikati) Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Halima Mdee na Kulia ni Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea wakiwa katika mkutano wa Meya wa jiji la Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  BARAZA la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam limeunda kamati ya kuchunguza mali za jiji hilo kutokana na mali hizo  kugubikwa na mbinu chafu na jiji kushindwa kunufaika mali hizo.

  Akizungumza leo na waandishi habari  jijini Dar es Salaam, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa kamati hiyo lazima ichambue mali hizo na kama ziko kwenye mikataba nazo ziangaliwe jinsi walivyoingia.

  Amesema kuwa katika mali hizo ni pamoja na vibanda 130 vilivyo katika Benjamin Mkapa Kariakoo waliopanga vibanda hivyo wanalipa sh.30,000 ambapo kwa kiwango hicho ni kidogo sana kutokana eneo vilipo.

  Mwita amesema kuwa mali za jiji zimekuwa hazinufaishi na kufanya mapato  kukusanywa  sh.bilioni 11.7  hivyo  mali zote zikichambuliwa jiji linaweza kukusanya zaidi ya sh.bilioni 20.

   Aidha amesema kuwa UDA ni mali ya jiji kutokana na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa  Hesabu za Serikali (CAG) kuzungumza kuwa shirika la Uda ni mali ya jiji.

  Mwita amesema vyanzo vingine ambavyo jiji haipati fedha ni Soko la Kariakoo, DDC  hivyo vikiamgaliwa na kamati iliyoundwa itaonyesha hali  halisi na jinsi jiji watavyonufaika.

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
   Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akizungumza wakati wa Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
   Abdul Kitula ambaye ni mtaalam wa fedha wa mradi wa PS3 akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mradi huo wakati wa uzinduzi hii leo mjini Mtwara.
  Mwakilishi wa USAID, Laura Kikuli alikuwepo na kutoa salamu zake katika uzinduzi huo a,mbao ulishirikisha watendaji wa Halamashauri zote za Mkoa wa Mtwara.
   Baadhi ya viongozi wa meza kuu wakifuatilia hotuba za ufunguzi
   Washiriki mbalimbali ambao ni watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
   Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akisema neno.
  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu pamoja na wakuu wa Wilaya za Mkoa huo wakifuatilia mawasilisho kutoka kwa maafisa Mradi wa PS3.
   Afisa Rasilimali watu wa  mradi wa PS3, Godfrey Nyombi akitoa mada.
  **************
  Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Mtwara  siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016.

  Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara. 


  PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.  Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na  Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.

  Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, na uzinduzi ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma ambaye amehamishiwa mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Watu takribani 180 walihudhuria.  Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe  wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. 

  Mkoa wa Dodoma una Halmashauri  nane, ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, na Halmashauri ya Mji wa Kondoa.

  PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.  Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni:  Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. 

  Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

  PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.  Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:

  ·   Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.

  ·   Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi.  Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.

  ·   Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi  katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.

  ·   Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.


  Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa.  Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.        
   Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
   Washiriki wakifuatilia kwa makini.
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisisitiza jambo
  Wakuu wa Wilaya wakifuatilia mada
   
   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimpa mkono wa shukrani Afisa wa Mradi wa PS3, Abdul Kitula baada ya uzinduzi. Kushoto ni Mwakilishi wa USAID, Laura Kikuli.
   
   Wakuu wa Wilaya wakijadiliana jambo

  Picha mbalimbali za makundi tofauti zilipigwa baada ya uzinduzi huo.

  0 0

  Injini ya gesi ya GE aina ya Jenbacher ambayo itauzwa kwa kampuni ya Said Salim Bhakhresa ili kupunguza gharama za uendeshaji.

  KAMPUNI ya GE ambayo imejikita kwenye biashara ya uvumbuzi na usambazaji wa nishati (NYSE: GE) leo imetangaza kuipa mamlaka Kampuni ya Clarke Energy inayojishughulisha na masuala ya Nishati. Kampuni hiyo ambayo huuza injini hizo kwa niaba ya GE itasambaza injini ya gesi aina ya Jenbacher na itaiuza injini hiyo moja yenye ufanisi wa hali ya juu kwa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (Bakhresa) ili kukamilisha kituo cha kufua Nishati ya joto. Kituo hicho kitasambaza umeme huo kwenye Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha Azam kilichopo Dar es Salaam, Tanzania na hivyo kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji za kampuni hiyo kwa mwaka.
  "Sisi tuliwachagua GE pamoja na Kampuni ya Clarke Energy hapa Dar es Salaam kutokana na utendaji wao wenye ufanisi mkubwa katika maeneo mengine nchini Tanzania pamoja na urahisi na upatikanaji wa huduma zao kwa wateja hapa nchini" alisema Rajesh Nair, Meneja Ufundi, Said Salim Bakhresa & Co Ltd.

  Tanzania ina akiba kubwa ya gesi ndani ya mwambao wa Pwani na kusini, kumekuwa na mabomba mawili ya gesi ambayo yamejengwa nchini ili kusafirisha gesi kutoka kitovu cha uzalishaji kuelekea kwenye maeneo ya matumizi. Bomba la kwanza lilikamilika miaka michache iliyopita na idadi ndogo ya viwanda na wauzaji wa matumizi binafsi waliunganishwa katika bomba hilo. Bomba la pili la gesi ndiyo limemalizika hivi karibuni na kufungulia fursa ya ununuzi wa gesi kwa viwanda vingi zaidi.

  "Bakhresa ni moja ya kampuni inayoongoza katika sekta ya viwanda Tanzania na ufungaji wa mtambo huu wa kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia, utasaidia kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa,” alisema Hugh Richmond, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Clarke Energy. "Huu ukiwa kama mradi wa kwanza wa kampuni yetu nchini Tanzania, utasaidia kupunguza gharama ya kiwanda kujiendesha huku ukifua umeme wa kuaminika utakaotosheleza mahitaji," alisema Richmond.

  Ufungaji wa mtambo huu utaiwezesha Kampuni ya Bakhresa kutumia gesi hii mpya kupata nishati za umeme na joto kwa ufanisi na uhakika. Kampuni ya Clarke Energy huuza kwa niaba ya GE aina ya injini ya gesi Jenbacher J612 yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.82 (MW) za nishati ya umeme. 

  Mtambo huu utazalisha pia nishati ya joto ambayo itaingizwa kwenye jiko la mvuke lenye uwezo wa kuzalisha kilowati 1,040. Clarke Energy itakua mvumbuzi kwa kuzalisha nishati ya umeme na joto ambapo hili litafanikiwa kwa kufunga mitambo ya umeme kwenye gridi ya taifa ili kuweza kubeba mzigo wa kilovolti 33”.

  "Injini za mtambo wa gesi aina ya Jenbacher J612 huzalisha hewa chafu kidogo, ila huzalisha umeme kwa ufanisi wa hali ya juu,” alisema Oluwatoyin Abegunde, Mkuu wa Biashara GE Distributed Power kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa nishati katika Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika. Alisema," Kwa kuchanganya teknolojia yetu ya uhakika na utaalamu wa Kampuni ya Clarke Energy, kwa pamoja tutazalisha umeme wa uhakika pamoja na suluhisho la kupunguza gharama kwa Kampuni ya Bakhresa na hivyo kuwasaidia kuwa mbele ya viwanda vingine nchini Tanzania.”

  Kampuni ya Bakhresa, ni moja ya viwanda vinayoongoza nchini Tanzania na Afrika Mashariki ambayo ilizinduliwa mwaka 1970. Leo hii familia ya viwanda vya Bahkresa imezidi kujizolea umaarufu kibiashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki zikiwamo nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi. Pia nchi za Malawi, Msumbiji na Afrika Kusini. Tayari kuna makampuni kadhaa chini ya mwamvuli wake na imewekeza hasa kwenye sekta ya vinywaji, ufungaji vifaa, huduma za baharini, mafuta ya petroli na burudani.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na watumishi,wakuu wa idara za Halmashauri na Wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika wilaya ya Hai wakati wa kikao cha utamburisho kilichoafnyika katika ukumbi wa KKKT Bomang'ombe.
  Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali katika wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
  Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho.
  Baadhi ya watumishi na viongozi mbalimbali wa Dini wakiwa katika kikao hicho.
  Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Hai,Said Mderu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho.
  Baadhi ya Wenyeviti wa vitobgoji na vijiji,


  Baadhi ya Wenyeviti wa vitongoji na vijiji wakiuliza maswali wakati wa kikao hicho.  Viongozi wa dini pia waliwasilisha hoja zao kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

  0 0

  Bw. James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza na waandhishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Benjamin Mkapa wakati akielezea kuhusu waajiri wanaodaiwa madeni sugu ya michango ya wafanyakazi wao na kutamka kwamba wasipolipa michango hiyo mpaka ifikapo Juni 30 mwaka huu shirika hilo linawapeleka mahakamani, kulia ni mmoja wa maofisa waandamizi wa shirika hilo Bw. Salim Khalifan pamoja na maofisa wengine wa shirika hilo waliohudhuria katika mkutano huo.
  Baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwa katika mkutano huo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo wakati Bw James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza nao katika mkutano huo.

  .......................................................................................................................................

  Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla ya tarehe 30.06.2016.

  Waajiri ni moja kati ya wadau wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12 (1) cha sheria ya NSSF, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili. 
  Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa. 
  Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika. 

  Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya NSSF no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.

  Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

  Kitendo cha kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya NSSF na ambayo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.

  Kutowasilisha michango kwa wakati husababisha usumbufu mkubwa kwa wanachama pale wanapostaafu kazi na kutakiwa kulipwa mafao yao ya uzeeni, hali hii husababisha wanachama kucheleweshewa malipo yao kwa makosa ambayo si ya kwao. Na wakati mwingine shirika hulazimika kuwalipa wanachama hawa kwa hasara kwa sababu waajiri wameshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi husika.

  Ili kuendana na kasi ya Mh. Rais John Pombe Magufuli na “motto” wake wa “Hapa kazi tu” shirika limeandaa mpango mkakati wa kuwapitia / kuwatembelea waajiri wote katika jiji la dsm na mikoa yote tanzania bara ambao wanadaiwa michango ya wafanyakazi wao ili kuweza kukusanya michango hiyo . Mpango huu wa kuwatembelea waajiri hawa itaanza rasmi tarehe 2/5/2016. Maafisa wa shirika watawapitia waajiri hawa mmoja baada ya mwingine na hakuna hata mmoja atakayeachwa bila kutembelewa alimradi anadaiwa michango ya wafanayakazi.

  Kumbukumbu tulizonazo, kwa mfano katika jiji la Dar es salaam pekee mpaka mwezi machi, 2016 waajiri wapato 3,234 wanadaiwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao wenye jumla ya shs milioni 21,497.35 hali hii haiweze kuvumilika hata kidogo na ni kinyume kabisa na mwenendo kasi wa mh. Rais magufuli katika kukwaletea watanzania maendeleo endelevu na motto wake wa hapa kazi tu.

  Shirika linatoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wanalipa michango ya NSSF ya wafanyakazi wao kwa wakati na linawataka waajiri wanaodaiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo yote ifikapo tarehe 30.06.2016 pia tunawaomba waajiri wote wanaodaiwa watoe ushirikiano kwa maafisa wetu pale watakapowatembelea katika maeneo yao ya kazi ili kufikia muafaka wa pamoja wa jinsi ya kulipa madeni haya ndani ya muda uliowekwa yaani tarehe 30.06.2016.

  Itakapofika mwezi julai, 2016 shirika halitakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuwapeleka mahakamani waajiri wote wanaodaiwa michango ya wafanyakazim, tungependa kila mwajiri atomize wajibu wake ili kuepuka usumbufu wa muda na mambo mengine lengo la nssf siku zote ni kuwa na mahusiano mazuri na waajiri na hatua za kisheria dhidi ya waajiri zinachukuliwa kama hatua za mwisho (Last resort) za kumfanya mwajiri atomize wajibu wake pale ambapo njia zingine zote zimeshindikana (zimegonga mwamba), lakini katika mazingira ya kawaida shirika halitarajii kwamba waajiri watashidnwa kutimiza wajibu wao mpaka wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha kwa upande mwingine, serikali pamoja na vyombo vya sheria, mahakama na ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP) wameahidi kutoa ushirikiano kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii – NSSF katika kutekeleza majukumu yake.

  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla ya tarehe 30.06.2016.

  Waajiri ni moja kati ya wadau wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12 (1) cha sheria ya nssf, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili. 
  Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa. 
  Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika. 

  Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya nssf no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.

  Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

  Kitendo cha kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya nssf na ambayo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.

  Kutowasilisha michango kwa wakati husababisha usumbufu mkubwa kwa wanachama pale wanapostaafu kazi na kutakiwa kulipwa mafao yao ya uzeeni, hali hii husababisha wanachama kucheleweshewa malipo yao kwa makosa ambayo si ya kwao. Na wakati mwingine shirika hulazimika kuwalipa wanachama hawa kwa hasara kwa sababu waajiri wameshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi husika.

  Ili kuendana na kasi ya mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli na “Motto” wake wa “hapa kazi tu” shirika limeandaa mpango mkakati wa kuwapitia / kuwatembelea waajiri wote katika jiji la dsm na mikoa yote tanzania bara ambao wanadaiwa michango ya wafanyakazi wao ili kuweza kukusanya michango hiyo . Mpango huu wa kuwatembelea waajiri hawa itaanza rasmi tarehe 2/5/2016. Maafisa wa shirika watawapitia waajiri hawa mmoja baada ya mwingine na hakuna hata mmoja atakayeachwa bila kutembelewa alimradi anadaiwa michango ya wafanayakazi.

  Kumbukumbu tulizonazo, kwa mfano katika jiji la Dar es salaam pekee mpaka mwezi machi, 2016 waajiri wapato 3,234 wanadaiwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao wenye jumla ya shs. milioni 21,497.35 hali hii haiweze kuvumilika hata kidogo na ni kinyume kabisa na mwenendo kasi wa mh. Rais magufuli katika kukwaletea watanzania maendeleo endelevu na motto wake wa hapa kazi tu.

  Shirika linatoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wanalipa michango ya NSSF ya wafanyakazi wao kwa wakati na linawataka waajiri wanaodaiwa kuhakikisha wanalipa malimbikizo yote ifikapo tarehe 30.06.2016 pia tunawaomba waajiri wote wanaodaiwa watoe ushirikiano kwa maafisa wetu pale watakapowatembelea katika maeneo yao ya kazi ili kufikia muafaka wa pamoja wa jinsi ya kulipa madeni haya ndani ya muda uliowekwa yaani tarehe 30.06.2016.

  Itakapofika mwezi julai, 2016 shirika halitakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuwapeleka mahakamani waajiri wote wanaodaiwa michango ya wafanyakazim, tungependa kila mwajiri atomize wajibu wake ili kuepuka usumbufu wa muda na mambo mengine lengo la NSSF siku zote ni kuwa na mahusiano mazuri na waajiri na hatua za kisheria dhidi ya waajiri zinachukuliwa kama hatua za mwisho (Last resort) za kumfanya mwajiri atomize wajibu wake pale ambapo njia zingine zote zimeshindikana (zimegonga mwamba), lakini katika mazingira ya kawaida shirika halitarajii kwamba waajiri watashidnwa kutimiza wajibu wao mpaka wachukuliwe hatua za kisheria. Aidha kwa upande mwingine, serikali pamoja na vyombo vya sheria, mahakama na ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu wa serikali (DPP) wameahidi kutoa ushirikiano kwa hsirika la taifa la hifadhi ya jamii – NSSF katika kutekeleza majukumu yake.

  0 0

  akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama waChama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa lengo la kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya Chama hicho.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Wawakilishi na Wanachama wa Chama cha SKAUT Nchini wakati ujumbe wa wawakilishi hao ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa ajili ya kumuelezea Makamu wa Rais shuhuli zao za kiutendaji hasa katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa Mtoto wa kike.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiungumza na Katibu Mkuu Kiongozi Baolozi Peter Kijazi Baada ya kuapishwa kwa Makatibu wa Mikoa leo April 27,2016 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR)

  0 0

  Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu akizungumza katika moja ya mikutano yake na wanahabari.
  Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO-Dar es salaam

  Jumla ya wagonjwa 267 wa mkoani Njombe wamenufaika na huduma za matibabu za madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali za hapa nchini.

  Takwimu hizo zimetolewa leo mkoani Njombe na Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu wakati akitoa taarifa za maendeleo ya zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa wananchi chini ya ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

  Amesema kuwa kati ya wagonjwa hao, 13 wamepatiwa huduma ya upasuaji kutoka kwa madaktari bingwa pia huduma hizo zinaendelea kutolewa katika Hospitali ya Kibena mkoani humo.

  “Tunawashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuitikia wito wetu, leo ni siku ya tatu lakini tumeshawapatia matibabu jumla ya wananchi 267 kati ya hao wagonjwa 13 wamepatiwa huduma ya upasuaji, tunawasihi waendelee kuja kwakua bado tuna siku mbili za kuendelea kuwapatia huduma za afya”alisema Singu.

  Amefafanua kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa waliopatiwa matibabu mkoani hapo ni wanawake ambao wengi wao wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo pamoja na mfumo wa mkojo.

  Lengo wa mpango huu wa kutumia madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Rufaa za Kanda ni kuhakikisha kuwa huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa zinawafikia wanachama wa Mfuko huo na Watanzania kwa ujumla popote walipo.

  Mpaka sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umepeleka huduma ya madaktari bingwa katika Mikoa 14 ikiwa na lengo la kuhakikisha huduma bora za matibabu zinatolewa kwa usawa.

  Singu ametoa wito kwa wananchi wa mkoani Njombe kuendelea kujitokeza kwa wingi kujipatia matibabu kwa kuwa huduma hizo zinatolewa kwa gharama nafuu.

  0 0

  Wanamuziki wa dansi, taarab, bongo fleva na wadau wa muziki waishio Dar es Salaam, Alhamisi hii watakutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ili kubadilisha mawazo juu mwenendo wa kazi zao.

  Wasanii na wadau hao watakutana na Makonda ndani ya ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni kuanzia saa 5asubuhikatika mkutano utakaohudhuriwa pia na wamiliki wa kumbi za starehe wa mkoa wa Dar es Salaam.

  Mkutano huo umeandaliwa na kamati ya ushirikiano ya wanamuziki wa dansi, taarab na wamiliki wa kumbi za starehe iliyoundwa hivi karibuni ili kujadili kwa undani changamoto za sheria ya biashara ya vileo na burudani ambazo ziko tangu mwaka 1968 na 1972.

  Mmoja wa wasemaji wa umoja huo wa wanamuziki wa dansi, taarab na wamiliki wa kumbi za starehe, Juma Mbizo, ameuambia mtandao huu kuwa maombi yao ya kumwalika Mkuu wa Mkoa katika mkutano huo, yameshawasilishwa kwa Mkuu huyo wa Mkoa.

  Jumba Mbizo amewataka wanamuziki, wadau wa muziki na wamiliki wa kumbi za starehe watakaopata taarifa za mkutano huo kwa njia yoyote ile, wafike kwa wingi Vijana Social.

  Mbizo amesema mkutano huohauhusiani na chama chochote cha muziki, bali umeandaliwa na waathirika wakuu sheria hizo za burudani na vileo ambao ni wanamuziki na wamiliki wa kumbi za starehe.

  0 0


  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
  Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akimvisha cheo cha RSM mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili.
  Baadhi ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza kama wanavyoonekana katika picha.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
  Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni kama wanavyoonekana katika picha.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano na baadhi ya Wawakilishi wa Vyombo vya Habari, Mkoani Morogoro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza waliosimama mstari wa nyuma.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo( wa pili kulia), Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(wa pili kushoto) na Maneja wa ampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo kwa pamoja wakionesha kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampunia uchimbaji wa Dhahabu ZEM Tanzania Limited,uchimbaji wa madini hayo utafanyika katika kijiji cha Nyasirori Wilayani Butiama Mkoani Mara kuanzia mwezi Desemba mwaka 2016.
  Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(kushoto) akiweka saini kitabu cha wageni ofisi kwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo(kulia) mara baada ya kumaliza kutano wao.
  Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kulia), Wakibadilishana mawazo na Kansela wa ubalozi wa China, Gou Haodong(wa pili kushoto) katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini baada ya kumaliza kusaini kibali cha kuhamisha leseni chimbaji wa madini katika kijiji cha Nyasirori wilayani Butiama utakaoanza mwezi Desemba mwaka huo, Maneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo(kulia).
  Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo,(katikati) akiwa na ujumbe utoka ubalozi wa china ukuongozwa na kansela Gou Haodong (kulia kwa Waziri) pamoja na watendaji wa Wizara wakiwa katika kikao cha pamoja kabla ya kusainiwa kwa kibali cha uhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo-ngeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu EM Tanzania Limited.
  Waziri wa Nishati Profesa Sospeter Muhongo akisaini kibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo- Engeneering ( Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu ZEM Tanzania Limited, tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini .

  0 0

  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Muh’d Dahoma akifungua mafunzo ya siku moja kwa wandishi wa Habari kuhusu maradhi ya kipindupindu katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Zanzibar Nd. Kheri Makame Kheri akitoa ufafanuzi kuhusiana na maradhi hayo na kuwataka waandishi kujikita zaidi kuelimsha jamii.
  Mwandishi wa habari kutoka Zenj F M Radio Mustafa akichangia mada zilizowasilishwa katika mafunzo ya siku moaja ya waandishi wa habari iliyofanyika Wizara ya Afya Zanzibar Mnazimmoja.
  Mtaalamu wa mabadiliko ya tabia katika afya na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Salum Aboubakar akitoa tathmini ya maradhi ya kipindupindu tokea yalipoanza mwezi Septemba mwaka jana mpaka hivi sasa.
  Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya siku moja juu ya maradhi ya kipindupindu wakifuatilia mafunzo hayo katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  Na Ramadhani Ali/MAELEZO ZANZIBAR 

  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Muh’d Dahoma amesema ili ugonjwa wa Kipindupindu umalizike inategemea zaidi maamuzi ya familia na jamii kwa jumla kukubali kubadilika.

  Amesema desturi potofu na tabia za wananchi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa maambukizi ya kipindupindu nchini.Akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa wa kipindupindu yaliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Dkt. Dahoma amewataka waandishi wa habari kutoa elimu zaidi kwa jamii ili wajue sababu zinazopelekea kuongezeka ugonjwa huo na njia za kujikinga.

  Amesema bado wananchi wanakuwa wagumu kubadili mfumo wao wa maisha licha ya juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya za kimataifa, taasisi za Serikali na binafsi pamoja na vyombo vya habari.‘’Bado watu wanaishi katika mazingira machafu, wengine hawana vyoo na wapo hawataki kuyatibu maji ya kunywa, mambo yanayochangia mambukizi ya kipindupindu,’’ alisisitiza Dkt. Dahoma.

  Ameishauri jamii kuwa tayari kubadilika baada ya kupata elimu ya maradhi ya kipindupindu ili kupunguza vifo vinavyotokana na maradhi hayo.Akitoa takwimu ya maradhi ya kipindupindu tokea yalipoanza mwezi Septemba mwaka jana, amesema wananchi 3,700 wameugua maradhi hayo na 46 kati yao wamefariki na Wilya ya Magharibi inaongoza kwa kutoa wagonjwa wengi zaidi.

  Mtaalamu wa mabadiliko ya tabia katika afya na mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Nd. Salum Aboubakar amewashauri wahariri wa habari kuvipa kipaumbele vipindi na habari zinazohusu Kipindupindu katika vyombo vyao ili wananchi waweze kuzinduka.Nae Ofisa Afya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Ofisi ya Dar es salaam Dkt. Neema Kileo ameshauri vipindi vinavyozungumzia kipindupindu vipangwe katika muda ambao wananchi wengi wanaweza kuvisikiliza.

  Washiriki wa mafunzo hayo wamekubali kutoa muda zaidi katika vyombo vyao vya habari kwa maafisa wa Kinga na Elimu ya Afya ili kutoa elimu zaidi katika kukabiliana na maradhi hayo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia ) na ujumbe wake kabla ya mazungumzo yao , Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dk. Koh Poh Koon, amesema wamepanga kutumia bandari ya Dar es Salaam kuwa kiunganishi cha biashara kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

  Dk. Koon ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 27, 2016), wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma, na kwamba Singapore ipo tayari kutoa fursa kwa wataalam wa Tanzania kwenda kufanya kazi katika Bandari ya Singapore ili kupata uzoefu utakaosaidia uendeshaji wa bandari za Tanzania.

  Dk. Koon ambaye ameambatana na wafanyabiashara wakubwa wapatao 40, amemweleza Waziri Mkuu kwamba kampuni ya Hyflux ya Singapore imeanza kuwekeza nchini kwa kujenga eneo maalum la uchumi (Special Economic Zone) mkoani Morogoro ambapo ndani ya kipindi cha miaka mitano wanatarajia kujenga miundombinu wezeshi ya kuweka viwanda vya kati (light industries), maeneo ya biashara na nyumba za makazi zipatazo 37,000.

  “Jiwe la msingi la mradi huo litawekwa tarehe 29 Aprili 2016 na Waziri wa Biashara,Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage,” alisema.

  Mbali na ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji, Dk Koon amweleza Waziri Mkuu kwamba nchi yake itaisaidia Tanzania kujenga uwezo wa kiufundi katika maeneo mbalimbali ya menejimenti na uendeshaji wa bandari na ufundi katika sekta ya gesi na mafuta.

  “Hadi sasa makampuni ya Singapore yaliyowekeza nchini ni pamoja na Pavillion Energy ambayo imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 1.2 katika sekta ya gesi na inatarajia kuwekeza zaidi dola za kimarekani bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa kinu cha kuchakata gesi (LNG plant) kitakachojengwa mikoa ya Kusini kwa ubia na makampuni ya gesi kutoka Ulaya na Marekani”.

  Amesema kampuni ya PIL ya Singapore inatarajia kuwekeza Dola za Kimarekani milioni 400 kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kutoa huduma kwa makampuni ya gesi.

  Amesema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa hayo pamoja na kuweka mikakati ya kuinua uchumi na kupanua wigo wa biashara. 
  Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa ameishukuru Serikali ya Singapore kwa uwekezaji unaofanywa na makampuni yake nchini na kwa misaada ya kiufundi ambayo wameitoa kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali.

  Ili kusaidia juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kukuza uchumi, Waziri Mkuu ameyakaribisha makampuni mengine ya Singapore kuja nchini kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda, mahoteli, kilimo na nishati.

  Amemuahidi Dk. Koon kwamba Tanzania ipo tayari kukamilisha mazungumzo ya kusaini Mkataba wa Kuvutia na kulinda uwekezaji baina ya nchi mbili (Bilateral Investment Protection and Promotion Agreement) na Mkataba wa Kuepuka kutoza ushuru mara mbili (Double Taxation Avoidance Agreement) ili kuvutia uwekezaji zaidi kutoka Singapore. 

  Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka Watanzania kutumia fursa ya ushirikiano kati ya Singapore na Tanzania kuanzisha biashara mpya zitakazowanufaisha wote.
  Waziri Mkuu amesema Singapore ina uwezo mkubwa kibiashara pamoja na uzoefu wa siku nyingi kwenye uendeshaji wa bandari hivyo Tanzania itapata nafasi ya kujifunza namna ya uendeshaji katika sekta hizo.

  Amesema Tanzania imefungua milango ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wa Singapore kuja kuwekeza katika sekta za viwanda, usafiri wa anga na kwenye Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZ).

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihitimisha hoja ya makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akijibu baadhi ya hoja za kuhitimisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge ,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akijibu baadhi ya hoja za kuhitimisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na wabungeu)baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na wabungeu)baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akipongezwa na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Angella mabula (kulia) na Mbunge wa Buchosa, Dkt. Charles Tizeba baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Makatibu Wakuu wa Ofisi yake baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Kutoka kushoto ni Erick Shitindi, Dkt. Hamis Mwinyimvua na Uledi Mussa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Wengine pichani ni Makatibu Wakuu wa ofisi ya Waziri Mkuu, Erick Shitinidi ( kushoto) na Dkt. Hamis Mwinyimvua (watatu kushoto)) na Dkt 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. Wengine ni Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto) na na wapili kushoto ni Uledi Mussa.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyakazi na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Watendaji wakuu wa mifuko ya Jamii baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Watendaji wakuu wa mifuko ya Jamii baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Wafanyakazi na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. 
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watndaji wa Ofisi na Taasisi zilizochini ya Wizara yake baada ya bunge kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma Aprili 27,2016. 

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya dola viimarishe ulinzi kwenye mipaka ya nchi na hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi.

  Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Aprili 27, 2016) wakati akijibu hoja za wabunge na kuhitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

  “Napenda kuviagiza vyombo vya dola viendelee kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi. Endapo patatokea upungufu wa mchele nchini, Serikali itaangalia uwezekano wa kuruhusu kuagiza mchele kutoka nje,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha miaka sita iliyopita, kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 katika uzalishaji wa mpunga hapa nchini na hivyo kufanya kiwango cha uzalishaji kiwe ni kikubwa kuliko mahitaji.

  “Takwimu za uzalishaji mpunga zinaonesha kuwepo ongezeko katika kipindi cha miaka sita iliyopita ambacho kiliongezeka kutoka tani 1,699,825 mwaka 2009/2010 hadi kufikia tani 1,936,909 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 14. Katika kipindi chote hicho, kiwango cha uzalishaji wa mpunga kimekuwa kikubwa kuliko mahitaji,” amesema.

  “Kutokana na mwenendo huo mzuri wa uzalishaji wa mpunga hapa nchini, Serikali ilisitisha kutoa vibali vya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi tangu Machi, 2013. Hatua hii itasaidia wakulima wetu kupata soko la uhakika na bei nzuri, jambo ambalo linawaongezea kipato na pia kuwahamasisha kuongeza uzalishaji zaidi,” amesema.

  Akizungumzia kuhusu deni la sh. bilioni 134 ambalo Serikali inadaiwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD), Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kulishughulikia deni hilo kwa kumwelekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ahakiki deni hilo. “Mpaka sasa CAG amehakiki madai ya jumla ya shilingi bilioni 67 na kazi ya uhakiki inaendelea.”

  Akifafanua kuhusu vigezo vilivyutumika kugawanya majimbo mapya ya uchaguzi, Waziri Mkuu alisema mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea maombi 77 ya kuanzishwa majimbo mapya, ambapo Halmashauri 37 ziliwasilisha maombi ya kugawa majimbo ya uchaguzi na maombi 40 yalitoka katika majimbo yaliyokuwepo yakiomba kugawanywa. Kati ya maombi yaliyowasilishwa, maombi 35 tu ndiyo yalikidhi vigezo na yalistahili kugawanywa.

  “Kutokana na ongezeko la Halmashauri mpya ambazo kisheria ni majimbo ya uchaguzi, ongezeko la idadi ya wabunge wanawake wa viti maalum na uwezo wa ukumbi wa Bunge; Tume iliamua kutumia vigezo vitatu tu ili kupata idadi ya majimbo yanayoweza kugawanywa. Vigezo hivyo ni: Wastani wa idadi ya watu (Population Quota), mipaka ya kiutawala na uwezo wa ukumbi wa Bunge,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema chini ya mchakato huo, Tume ilianzisha majimbo mapya 25 ambapo majimbo 19 yalitokana na ongezeko la Halmashauri mpya; na majimbo sita yalitokana na kigezo cha wastani wa idadi ya watu.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu alibainisha kwamba kwa sasa Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo mapya ya utawala zikiwemo wilaya na mikoa mipya kwa sababu bado inaendelea kujengea uwezo wa rasilmali watu na vitendea kazi katika maeneo mapya ya utawala yaliyopo hivi sasa.Bunge limepitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017.

  0 0

  Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam. Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa..
  Mama Maria Nyerere na Mwanae, Mh. Makongoro Nyerere wakimbelea eneo la Daraja hilo.
  Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

  Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongolo Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.

  Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.

  "Mimi ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni nani?" Amesisitiza Mama Maria Nyerere.

  Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 3.2, njia sita za magari na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  27 Aprili, 2016

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO-Dar es salaam

  Jumla ya wagonjwa 267 wa mkoani Njombe wamenufaika na huduma za matibabu za madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali za hapa nchini.

  Takwimu hizo zimetolewa leo mkoani Njombe na Afisa Mawasiliano Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu wakati akitoa taarifa za maendeleo ya zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa wananchi chini ya ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

  Amesema kuwa kati ya wagonjwa hao, 13 wamepatiwa huduma ya upasuaji kutoka kwa madaktari bingwa pia huduma hizo zinaendelea kutolewa katika Hospitali ya Kibena mkoani humo.

  "Tunawashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuitikia wito wetu, leo ni siku ya tatu lakini tumeshawapatia matibabu jumla ya wananchi 267 kati ya hao wagonjwa 13 wamepatiwa huduma ya upasuaji, tunawasihi waendelee kuja kwakua bado tuna siku mbili za kuendelea kuwapatia huduma za afya"alisema Singu.

  Amefafanua kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa waliopatiwa matibabu mkoani hapo ni wanawake ambao wengi wao wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo pamoja na mfumo wa mkojo.

  Lengo wa mpango huu wa kutumia madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Rufaa za Kanda ni kuhakikisha kuwa huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa zinawafikia wanachama wa Mfuko huo na Watanzania kwa ujumla popote walipo.

  Mpaka sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umepeleka huduma ya madaktari bingwa katika Mikoa 14 ikiwa na lengo la kuhakikisha huduma bora za matibabu zinatolewa kwa usawa.Singu ametoa wito kwa wananchi wa mkoani Njombe kuendelea kujitokeza kwa wingi kujipatia matibabu kwa kuwa huduma hizo zinatolewa kwa gharama nafuu.

  0 0

  Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai Mmoja wa wafanyakazi wa UN nchini Tanzania (kulia), akitoa somo kwa Wanafunzi wa 'International School of Tanganyika-IST' waliotembelea ofisi hiyo nchini Tanzania kujifunza shughuli mbalimbali za msingi zinazofanywa na UN. Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakijibu maswali mara baada ya kuelezwa namna ofisi ya Umoja wa Mataifa, UN zinavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto. Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakifuatilia maelezo toka UN ya namna ofisi hizo za Umoja wa Mataifa zinavyofanya kazi hasa kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto. Nyuma ni baadhi ya walimu wa IST walioambatana na wanafunzi hao. Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama mbele), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai. Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama kulia), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao mara baada ya ziara yao ya mafunzo kutembelea Ofisi za UN Tanzania.

  0 0
 • 04/27/16--23:12: DONDOO ZA MAGAZETI

older | 1 | .... | 830 | 831 | (Page 832) | 833 | 834 | .... | 1897 | newer