Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE AZINDUA KITUO CHA TAASISI YA KIMATAIFA YA KILIMO CHA KITROPIKI (IITA) DAR ES SALAAM

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakifungua kituo hicho

Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo pamoja na Rais Mstaafu,Mh. Benjamin Mkapa wakizindua rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Picha ya pamoja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo baada ya uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chifu Olesegun Obasanjo akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakionja mikate iliyotengenezwa kwa unga wa muhogo wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mazungumzo na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo baada ya uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakisikiliza maelezo ya kitaalamu juu ya utafiti wa maradhi ya migomba toka kwa Profesa Rony Swennen wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakiangalia mashine ya kuvunia mihogo
Wadau wakionja vyakula mbalimbali vinavyotengenezwa kwa unga wa muhogo
Wadau wakiwa katika sherehe hizo
Mmoja wa watafiti akielezea kazi yake kituoni hapo
Watafiti wakielezea kazi zao
Wadau wa ITTA ambao ni wapenzi wa Globu ya Jamii
Wadau shereheni
Wageni waalikwa


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakifungua kituo hicho
Rais Dkt. Jakaya Kikwete achunguza kitu kwa kutumia kifaa cha kisayansi katika taasisi hiyo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Benjamin Mkapa pamona na Balozi wa Marekani nchini Tanzania wakiagalia sehemu ya vifaa vya kisayansi katika taasisi hiyo.

Mstahiki Meya Jerry Silaa afungua tawi jipya la Ofisi DStv Tanzania barabara ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar

$
0
0

Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la Ofisi za DStv Tanzania zilizopo barabara ya Msimbazi Kariakoo karibu na Diamond Trust Bank. Kulia ni Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kufungua rasmi tawi jipya la Ofisi za DStv Tanzania liliopo barabara ya Msimbazi Kariakoo karibu kabisa na Diamond Trust Bank. Anayeshuhudia tukio hilo ni Branch Coordinator Prosper Sangawe.
Mgeni rasmi stahiki Meya Jerry Silaa akifanya malipo ya akaunti yake ya King'amuzi cha DStv kwa Ezekiel Mwasuluko wa kitengo cha Huduma kwa wateja katika tawi hilo jipya kuashiria ufunguzi rasmi na utoaji huduma umeanza kazi.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha ankara yake ya malipo kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani).
Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakipiga makofi baada ya tukio hilo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mutlichoice Tanzania baada ya kuzindua rasmi tawi jipya la kutoa huduma kwa wateja wa DStv lililopo barabara ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar.





Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Furaha Samalu katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi.

Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akisalimiana na Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa mara baada ya kuwasili kuzindua tawi jipya la ofisi za DStv Tanzania lilolopo Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank jijini Dar. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi mara baada ya kuwasili. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi akiwakaribisha wageni waalikwa na wakazi wa jijini Dar kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa tawi jipya la Ofisi za DStv zilizopo Karikakoo barabara ya Msimbazi karibu kabisa na Diamond Trust Bank ambapo amesema Mutlichoice Tanzania inawajali wateja wake ndio maana imeamua kusogeza huduma hizo karibu na wateja wake na kuwataka Watanzania kujipatia king'amuzi cha DStv pamoja na huduma ya ufungaji kwa bei poa ya Tshs 149,000 tu ofa hii ni kwa kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 13th May mpaka 18th May, 2013.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Multichoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua tawi hilo katika sherehe zilizofanyika jana jijini Dar.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Ofisi za DStv zilizopo Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank jijini Dar.
Mstahiki Meya Jerry Silaa amewapongeza Multichoice Tanzania kwa kuwa wakongwe wa Digitali Tanzania na kuwataka kuendelea kutoa huduma bora zenye viwango ili kuendelea kuwa vinara wa kutoa huduma ya Digitali Tanzania na pamoja na hayo amefurahishwa kusogezwa karibu kwa huduma DStv katikati kabisa ya jiji zitakazowasaidia wakazi Manispaa ya Ilala.
Picha juu na chini Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wakimsikiliza mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Kijana mtanashati Ezekiel Mwasuluko Multichoice Tanzanua wa kitengo cha huduma kwa wateja akiwa tayari kukuhudumia wewe Mtanzania katika tawi lao jipya la Ofisi za DStv barabara Msimbazi Kariakoo jijini Dar.
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo (mwenye miwani nyeusi) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake nje ya Ofisi mpya za DStv zilizopo maeneo ya Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank.
Meneja Masoko ya Multichoice Tanzania Furaha Samalu na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi na Revina Bandihai katika pozi matata kuonyesha furaha ya ufunguzi wa Tawi lao jipya lililopo Kariakoo barabara ya Msimbazi karibu na Diamond Trust Bank.
Muonekano wa nje wa Ofisi za DStv Tanzania zilizopo barabara ya Msimbazi - Kariakoo karibu kabisa na Diamond Trust Bank jijini Dar es Salaam.
Vibajaji vya DStv vikiwa tayari kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji kutoa huduma kwa wateja wao.

DIAMOND MUSICA WALIPAMBA SHINDANO LA THE MIC KING

$
0
0
Washiriki wote tisa wakiwapungia mikono mashabiki wao.
Majaji wakitoa ushauri kwa washiriki.
Kiongozi wa Bendi ya Diamond Musica, Liva Hassan 'Sultan' (kushoto), akiimba sambamba na waimbaji wake....Akizikonga nyoyo za mashabiki wa Dar Live.Wacheza shoo wakionyesha machejo yao.Mpiga drums akionyesha ufundi wake.
SHINDANO la The Mic King jana liliendelea kushika kasi katika ukumbi wa kisasa wa Dar Live ambapo bendi ya Diamond Musica ilitoa burudani kulipamba shindano hilo. Wakali wa Mic walichana mistari mbalimbali wakielekea mwishoni mwa mchuano huo utakaomalizika Mei 25, mwaka huu katika ukumbi huo.
(PICHA NA ISSA MNALLY / GPL)

JAPHET KASEBA KUZICHAPA NA MMALAWI JUNE 8 DDC KONDOA

TIMU YA MWISHO KUTOKA AFRIKA MASHARIKI YASAKA NAFASI YA KUFUZU KUINGIA NUSU FAINALI YA GFC

$
0
0
  Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha tisa(robo fainali ya 4) cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kutoka kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), bluu na kijani ni timu kutoka Cameroon na nyeusi ni yimu kutoka Ghana. 



TIMU YA MWISHO KUTOKA AFRIKA MASHARIKI YASAKA NAFASI YA KUFUZU KUINGIA NUSU FAINALI GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.


: Jumatano iliyopita kupitia stesheni za ITV na Clouds TV, Waghana Jonathan Naab na Desmond Odaano walifanikiwa kufuzu nusu fainali ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE. Inaweza kusemekana kuwa timu hii ilichagua njia rahisi kwa ajili ya kupata ushindi hadi kufikia hatua ya vikwazo ambapo walikutana uso kwa uso na waghana wenzao.Jonathan na Desmond walifanikiwa kushinda katika vikwazo vyote na kufikia hatua ya ukutawa pesa wa Guinness ambapo walipata  dola za kimarekani 3,000 kuongezea kwenye dola 5,500 walizokuwanazo awali.


Wakiwa na jumla ya dola 8,500 mkononi, Jonathan na Desmond wanajiandaa kutafuta dola 250,000 na ushindi wa Pan-African katika nusu fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.


Watachezea nchi yao pamoja na Emphatus Nyambura na Samuel Papa kutoka Kenya ambao walikuwa washindi wa pili katika robo fainali hyo wiki iliyopita. Katika robo fainali ya mwisho wiki ijayo timu nyingine nne zitaingia uwanjani  kati ya hizo ni timu kutoka Kenya  Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ambao watapeperusha bendera ya Afrika Mashariki ili kupata timu mbili za mwisho.


 “Tumebakiwa na robo fainali moja tu ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE-Je, kuna moja kati ya timu zilizobaki inayoweza kujishindia dau kubwa zaidi ya timu ya Jonathan na Desmond? Washiriki wote wameonesha kuwa wana ujasiri tutaona jinsi timu hizi nne zitakavyocheza wiki ijayo. Ni nani atakayeshinda katika robo fainali ijayo? Tunazitakia timu zote kila la heri katika robo fainali mwisho” alisema Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi.



Timu zitakazoonesha ujuzi wao katika robo fainali ya mwisho:

·         Timu kutoka Kenya Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi katika jezi nyekundu wanaotarajia kushinda baada ya kujitahidi na kupata  dola za kimarekani 1,500 hapo awali. Kenneth atakuwa kichwa cha timu wakati Cris ambaye ni mchezaji wa Springland FC atakuwa akichezea mpira.


·         Maarufu nchini Cameroon kwa kufuata nyayo za shujaa wa kifaransa mwenye majina kama yao Thiery Henry, wachezaji Thiery Teke, kichwa cha timu na Henri Eboule, ambaye ataonesha uwezo wa kucheza soka,  wanatarajia kuongeza fedha kwenye zaidi ya dola 5,500 walizokuanazo awali.


·         Timu ya pili kutoka Cameroon watakaovaa jezi za kijani ni Botafogo Paul Mbuh na mwanafunzi Remy Isong.Timu hii haikufanya vizuri katika sehemu za awali ambapo walijishindia dola 500 tu lakini sasa ina nafasi ya kufanya vizuri zaidi.


·         Katika jezi nyeusi  watakuwa Emanuel Kofi Okarku(27) na Isaac Aryee(25) kutoka Ghana. Emanuel na Isaac ni maarufu kwa kushabikia timu mbili adui lakini wanacheza kwa umoja katika timu baada ya kushinda  dola 3,000 katika mashindano ya kitaifa. Emanuel ni kichwa cha timu na Isaac atakuwa akionesha utaalamu wa kusakata kabumbu.


Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge barani Afrika wanaweza kupima maarifa yao katika kabumbu kupitia GUINNESS® VIP™.  Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.  


Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.

-www.facebook.com/guinnesstanzania


Robo fainali ya mwisho ya Pan-African itarushwa katika televisheni za ITV na Clouds TV usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.


GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.


Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 


Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.

TFDA YAZINDUA RIPOTI YA UFUATILIAJI WA KARIBU WA DAWA YA MALARIA AINA YA ALu KATIKA KUFUATILIA MADHARA YA DAWA

$
0
0
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi akionesha ripoti na machapicho aliyozindua, wengine wanaoshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando
 Waziri wa Afya Dkt. Hussein Mwinyi akihutubia wakati wa uzinduzi huo
  Mkurugenzi Mkuu TFDA, Hiiti Sillo, akiwasilisha maelezo ya utangulizi katika uzinduzi wa taarifa ya ufuatiliaji wa dawa za ALu na machapisho mbalimbali

Mwakilishi wa WHO, Dkt. Rufaro Chatora akiwasilisha salamu za WHO katika uzinduzi huo

=========  ========= ==========

TFDA YAZINDUA RIPOTI YA UFUATILIAJI WA KARIBU WA DAWA YA MALARIA AINA YA ALu KATIKA KUFUATILIA MADHARA YA DAWA
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Hussein A. Mwinyi  amezindua ripoti ya ufuatiliaji wa usalama wa dawa  mseto ya Malaria aina ya Artemether + Lumefantrine (ALu)  na  kusema kwamba imethibitika kisayansi ni salama na haina madhara makubwa  (adverse reactions) na badala yake ina madhara madogo yanayovumilika (side effects).  Ripoti hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa  (TFDA) kupitia mpango wa Ufuatiliaji wa karibu wa madhara ya dawa ya ALu, imezinduliwa mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Hussein Mwinyi amewataka wananchi waliokuwa na wasiwasi juu ya dawa hii  kuendelea kuitumia dawa mseto ya Malaria aina ya ALu kwa kuwa ni salama.
Sambamba na uzinduzi huo, Waziri pia amezindua machapisho yanayotumika katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wagonjwa kwa lengo la kufuatilia usalama wa dawa nchini. Machapisho hayo ni vitendea kazi katika mfumo wa ufuatiliaji wa karibu wa madhara ya dawa ambao unawezesha kukusanya taarifa nyingi zaidi na kuweza kufanya tathmini ya kisayansi ya uhusiano wa dawa na madhara yake.
Kufuatia uzinduzi huo, Waziri amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutumia machapisho husika kama ilivyokusudiwa kwa lengo la ufuatiliaji wa madhara ya dawa kwa kuhakikisha fomu husika zinajazwa na kuwasilishwa TFDA kwa wakati.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Rufaro Chatora, ameahidi kuendelea kuisaidia TFDA katika kuhakikisha kuwa usalama wa dawa unaendelea kudumishwa nchini.
Wakati huohuo, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, amesema kuwa TFDA ipo katika hatua ya kukamilisha maandalizi ya ufuatiliaji wa karibu wa usalama wa dawa za kupunguza makali ya Ugonjwa wa UKIMWI (ARVs) katika mwaka wa fedha 2013/2014.
Mfumo wa ufuatiliaji wa madhara ya dawa ya Malaria unaojulikana kitaalamu kama Cohort Event Monitoring (CEM) ulianza kutekelezwa nchini mwaka 2009 kufuatia mafunzo yaliyotolewa na WHO nchini Ghana ambapo TFDA ilishiriki.

Vodacom yazidi kuimarisha huduma zake vijijini

$
0
0



Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Elius Nyakia akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara mpya wa Vodacom katika kijiji cha Lukanga Wilaya ya Misungwi. Anaemsaidia kukata utepe huo ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Herieth Koka. Wanaoshuhudia uzinduzi huo kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim, Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga Bw Enos Malale na Meneja wa Vodacom Foundation Mwamvua Mlangwa. Kabla ya Vodacom kujenga mnara huo, kijiji hicho hakijawahi kuwa na huduma za uhakika za simu za mkononi.  

=====  =====  ======

Vodacom yazidi kuimarisha huduma zake vijijini.


Wakazi wa kijiji cha Lukanga wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza pamoja na wa maeneo mbali mbali nchini wameendelea kunufaika na teknolojia ya simu za mikononi ikiwemo kupunguza gharama za maisha baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kuendelea kuyafungua na kuyaimarisha kimawasiliano maeneo yao.


Mwishoni mwa wiki iliyopita, Vodacom ilizindua rasmi huduma zake katika kijiji hicho kufuatia kujengwa kwa mnara mpya ambapo kabla ya hapo wakazi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani ikiwemo kijiji cha Ishokera maarufu kwa shughuli za uchimbaji madini hawakuwa na huduma za uhakika za mawasiliano ya simu za mkononi na hivyo kuwalazimu wananchi kusafiri au kulazimika kuvizia mawimbi ya mawasiliano kwa baadhi ya nyakati.


“Tunafuraha kubwa sana leo hapa kijijini, sio ya kuwa na wageni bali kuona nasisi wana Lukanga tukiingia kwenye historia ya kuwa na mnara wa simu unaotupa huduma za uhakika za simu za mkononi,.”Alisema Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga Bw. Enos Malale wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mnara huo.


“Hatuna tena sababu ya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za simu z amkononi au kupanda juu ya vichuguu na milima kupata huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi kwani Vodacom sasa imetuleletea mawasiliano sebuleni na vyumbani kwetu.” Aliongeza.



Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ilikuwa ndoto kwao kuweza kuunganishwa kimawasiliano na sehemu nyingine kwa muda mrefu. “hivyo basi kwa niaba ya wanakijiji wa Lukanga na wa vijiji vya jirani tunawashukuru sana Vodacom kwa hatua hii nasi leo tunaunganishwa na ulimwengu, tutawakumbuka wakati wote”Alisema Mwenyekiti huyo huku akiungwa mkono na mayowe ya wananchi walioonekana kuwa na furaha wakati wote wa hafla hiyo.


Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Misungwi Bw. Elius Nyakia aliipongeza Vodacom kwa kuendelea kuwekeza nchini hususan vijijini na hivyo kuwawezesha watanzania kuishi katika zama za sayansi na teknolojia.


“Hakuna ambae hafahamu kwamba katika karne ya 21 teknolojia ya habari na mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika maisha yetu. Vodacom inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wateja lakini bado wameendelea kuwekeza ili kila mmoja anufaike na huduma za simu za mkononi na kurahisisha maisha.”Alisema Bw. Nyakia.


Aidha Bw Nyakia aliwataka wananchi kutambua fursa zinazopatikana kwa kuwa na huduma za mawasiliano ya simu za mtandao wa Vodacom kubwa ikiwa ni kuitumia kwa ukamilifu huduma ya M-pesa ili kuepukana na vishaiwishi vya wizi, ujambazi au hata kupoteza fedha kwa kukaa nazo majumbani ama kusafiri nazo umbali mrefu.


“Nawaomba sana wakazi wa kijijiji hiki kutumia teknolojia kurahisisha maisha yenu na hasa hii huduma ya M-pesa wote ni mashahidi jinsi inavyotusaidia, hivyo itumieni na muachane na utamaduni wa kuhifadhi fedha majumbani au kwa wale wafanyabishara kusafiri nazo. Kupitia M-pesa mnaweza kutuma au kutoa fedha benki au kufanya malipo ya huduma mbalimbali.”Alisema Nyakia huku akiutaka uongozi wa kijiji kuhakikisha mnara huo na miundombinu yake unalindwa ili kutorudisha nyuma maendeleo.


Awali akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Herieth Koka alisema katika kipindi cha mwaka 2012/2013 kampuni ya Vodacom imefanya kazi kubwa ya kuboresha na kusogeza huduma zake katika maeneo yote ya kanda ya ziwa kazi  ambayo bado inaendelea.


“Mnara tunaouzindua leo ni mwanzo tu, tuna minara mingi mipya tuliyoijenga pamoja na kuiongezea nguvu iliyopo ili kuhakikisha wakazi wa kanda ya ziwa wanaendelea kunufaika na huduma mbalimbali ambazo kutoka Vodacom Pekee unaweza zipata kwa urahisi na wepesi. Lengo letu likiwa ni kuwawezesha wananchi kubadili maisha kupitia teknolojia na huduma ya simu za mkononi”Alisema Herieth  


Amesema Vodacom itaendelea kuwa karibu na wakazi wa mikoa ya kanda ya Ziwa kama inavyofanya maeneo mengine nchini ikitambua umuhimu wa watu katika ustawi wa biashara wa kampuni sanjari na inavyoungwa mkono na watanzania na hivyo kuiwezesha kuwa kampuni inayoungoza nchini.


“Lengo letu sio kuongoza tu bali kuendelea kuwa kampuni iliyo karibu na watu na inayowafikia watanzania kila mahali na kuleta tofauti katika maisha yao. Tumekuwa tukifanya hivyo na ahadi yetu ya kuwaunganisha watanzania kimawasiliano na hatimae kubadili maisha yao bado ipo imara”. Aliongeza Herieth.

Kutoka Vodacom pekee utapata huduma ya M-Pesa ambayo unaweza kulipia huduma mbali mbali zaidi ya mia mbili, kuweka na kutoa pesa kwa kasi na usalama.

   

Wilaya ya Rombo Kutumia Nyuki Kupambana na Tembo Wavamizi

$
0
0
 Baadhi ya mashamba ya wananchi eneo la Rongai, wilayani Rombo ambayo mara kadhaa huvamiwa na tembo waharibifu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya akizungumza na mtandao wa www.thehabari.com hivi karibuni wilayani Rombo.
 Pichani ni baadhi ya majengo ya Shule ya Msingi Rongai, wilayani Rombo. Shule hii ni miongoni mwa maeneo yanayoathiriwa na uvamizi wa tembo waharibifu ambao huathiri taaluma shuleni hapo.

======  =====  ======  ========
Na Thehabari.com, Rombo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Rombo imeanza mipango ya kutumia ufugaji wa nyuki kukabiliana na tembo waharibifu ambao mara kadhaa huvamia baadhi ya makazi ya wananchi maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kufanya uharibifu wa mazao pamoja na kuua au kujeruhi wakazi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Judethadeus Mboya alisema tayari halmashauri hiyo imetengeneza mizinga ya nyuki ambayo imesambazwa maeneo kadhaa ili kukabiliana na tembo waharibifu eneo hilo.

"Unajua nimetembea mbuga mbili za Kenya ikiwemo Tsavo ambazo tumepakana nazo eneo hili sehemu ambayo tembo hutokea huko na kuvamia maeneo yetu, sehemu hizi wao wamedhibiti uvamizi wa tembo...wamefuga nyuki wengi sana na maeneo mengine wametumia hadi teknolojia kuwazuia tembo kuvamia makazi ya raia hivyo hawapati madhara kama yetu," alisema Mboya akifanya mazungumzo na gazeti hili ofisini.

Alisema kwa sasa tayari wametengeneza mizinga 50 ya nyuki na kuifunga ukanda wa chini wa vijiji kama Chala, Ibukoni, Ngoyoni na maeneo mengine ambayo tembo huyatumia kama njia kipindi cha uvamizi na kwa sasa mizinga mingine 100 ya nyuki inaandaliwa kuenezwa maeneo mengine kukabiliana na tembo hao hatari.

Alisema viongozi wa halmashauri hiyo pia wametoa elimu kwa wanakijiji maeneo husika ya kuhamasisha uvugaji nyuki katika vikundi ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tembo hao waharibifu ambao idadi kubwa hutokea nchi jirani ya Kenya na kufanya uharibifu pamoja na kutishia maisha ya wanavijiji upande wa Tanzania.

Aidha kiongozi huyo alisema tembo hao mbali na kufanya uhalibifu mkubwa wa mazao ya wanavijijini kipindi cha uvamizi wakati mwingine wamekuwa wakiuwa raia jambo ambalo ni hatari zaidi kiusalama.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini uvamizi wa wanyama hao umekuwa kero kwa maeneo mbalimbali ya vijiji vya wilaya hiyo, kiasi ambacho unatishia shughuli za maendeleo ya wananchi kama kilimo pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla.

Akizungumzia hali ya uvamizi wa tembo na athari za elimu, Mwalimu wa Taaluma Shule ya Sekondari Tanya, Shuma Himidiel alisema miezi ambayo tembo huanza kufanya uvamizi huingilia ratiba za masomo na mara kadhaa kusimama kutokana na hofu ya wanafunzi na usalama wao hasa wanapotoka na kuja shuleni.

"Kimsingi wanyama hawa wanapoanza usumbufu kijiji kizima huwa na heka heka na wakati mwingine hata wanafunzi wanashindwa kuja shule kuhofia maisha yao...hata wazazi huwazuia watoto wao kutoka hadi hali ya hatari inaporejea kuwa ya kawaida.

Akifafanua zaidi mwalimu Himidiel alisema mara ya mwisho tembo kufanya uvamizi katika Kijiji cha Tanya waliua mtu mmoja walipokuwa wakidhibitiwa na askari wa wanyamapori eneo hilo. 

Bonus Balaa ya Zantel yapongezwa na wateja wake

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Zantel, Bi Awaichi Mawalla, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa ya Bonus Balaa, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Zantel, Zanzibar-Mohamed Mussa.
======  =======  =====

Bonus Balaa ya Zantel yapongezwa na wateja wake


Ofa mpya inayotolewa kwa wateja wa Zantel, ya Bonus Balaa, ambayo inawawezesha kupata muda wa maongezi mara mbili ya salio waliloweka kwenye simu zao, imepongezwa na wateja wao kwa kuwasaidia kupunguza gharama za mawasiliano.


Wateja wengi wameonyesha kufurahia huduma hiyo, ambayo, kiupekee kabisa pia inawawezesha wateja wa Zantel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa salio hilo la ziada. ‘Gharama za maisha zimekuwa juu sana, lakini bado mahitaji ya mawasiliano, iwe kikazi au kifamilia yamezidi kuongezeka, hivyo tunashukuru kampuni ya Zantel kwa ofa hii ya kipekee’ anasema Aman Mgaya, mmoja wa wateja wa Zantel, Zanzibar.

Muda huo wa maongezi, ambao ni sawa sawa na ongezeko la aslimia mia moja, ambalo wateja wa Zantel watapata baada ya kuongeza muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi, utatumika ndani ya siku thelathini.  ‘Tumeweka siku thelathini ili mteja wetu atumie pesa yake pale tu atakapojisikia kufanya hivyo na sio kumlazimisha atumie ndani ya siku moja kama ofa nyingine’ alisitiza Afsa Biashara Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Sajid Khan.

Wakati huo huo, wateja wa mtandao wa Zantel Zanzibar wameanza kujishindia zawadi katika promosheni kubwa ya ‘Kwangua na Ushinde’ inayoendelea kisiwani humo. Katika promosheni hiyo ambayo mshindi wake atajinyakulia gari, huku wateja wengine wakijishindia zawadi za kila siku kama muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni  moja, pikipiki aina ya Vespa, komputa ndogo (Huawei Media pads) pamoja na modemu za 3G.

Ili kushiriki katika promosheni hiyo, wateja wapya na wale wa zamani wa Zantel wanapaswa kuweka muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi ili kuingia kwenye droo hiyo.  

Coca-Cola handover balls, bibs for Copa Coca-Cola

$
0
0
 Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka (R) hands over sports kits to TFF football development officer Salum Madadi for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.
 Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka addresses the media at a ceremony where Coca-Cola Tanzania handed over balls and bibs for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.
TFF football development officer Salum Madadi speaks to the media at a ceremony where Coca-Cola Tanzania handed over balls and bibs for the U-15 Copa Coca-Cola tournament at district level. The presentation ceremony was held in Dar es Salaam over the weekend.

======  ====== =======
Coca-Cola handover balls, bibs for Copa Coca-Cola


Coca-Cola has handed over balls and bibs to the Tanzania Football Federation (TFF) for youth teams taking part in this year’s Copa Coca-Cola football tournament which has now moved from U-17 to U-15 in order harness and expose talent from a younger age giving players a better chance of being picked up by local football academies and clubs.


The first batch of the sports kits which caters for the district level phase of the tournament was received on behalf of TFF by football development officer Mr. Salum Madadi who called on all regional football association to observe rules and regulations governing the tournament. The presentation ceremony was held at Coca-Cola Tanzania offices over the weekend.


He said that some of the districts had already started matches and urged the rest to begin the tournament as soon as possible now that the balls and bibs are available.



Earlier in his remarks, Coca-Cola Tanzania Brand Manager Tanzania Maurice Njowoka underscored Coca-Cola’s commitment and obligation to continue supporting the championships which has played a significant role in identification of football talents in the country.


“Our move from U-17 to U-15 gives COPA players the opportunity to develop their football skills and gain experience early, thus putting them at an advantage over their peers,” said Njowoka.


In Africa, the Coca-Cola COPA tournament is run in over 20 countries giving more than 50,000 young players the opportunity to display their talent. Over the years, bona fide professional stars have emerged from the tournament including Zambian national team goalkeeper Kennedy Mweene and his teammates Nathan Sinkala and Stophila Sunzu; Ugandan international defender Timothy Batabaire; Nigeria FC Porto midfielder Mikel Agu; Kenyan midfielder McDonald Mariga; Tanzanian striker Thomas Ulimwengu; and South African duo Mandla Masango and Happy Jele among others.


“We have many heroes born from the COPA Coca-Cola tournament each year,” said Njowoka. “The professional players who have made it big and inspire us all are heroes. Our players who work hard and support one another are heroes. The parents who offer support and guidance to our players are heroes. The coaches who pour their hearts and souls into their teams are heroes. Even the fans who come out to cheer their teams are heroes and every day, we see new heroes emerge. This formed the thinking behind our new slogan ‘Where Heroes Are Born’ which you will see on all marketing materials going forward,” he added.


This year’s tournament follows a successful campaign last season where the tournament was activated in over 20 markets across Africa with 134 players from Sub-Sahara Africa selected for a two-week international boot camp in Pretoria, South Africa.



MAOFISA WA JESHI KUTOKA CHUO CHA KIJESHI GHANA WATEMBELEA TBL DAR

$
0
0


Maofisa wa Jeshi kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Ghana, wakitembelea Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam, kwa lengo la kujenga ushirikiano katika nyanja za Sayansi, Teknolojia, Kiuchumi na Kijamii.Maofisa wanaosoma katika chuo hicho wanatoka Afrika Kusini, Nigeria, Ivory Coast, Togo, Rwanda na Ghana. (PICHA NA AMANDA WA MATUKIO BLOG).
 Meneja Uhusiano wa TBL, Doris Malulu (kulia) akitoa maelezo kwa maofisa hao kuhusu shughuli mbalimbali za kampuni hiyo.
Maofisa wa Jeshi wakitembelea kiwanda hicho
 Maofisa wa Jeshi wakipata maelezo jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia kompyuta
Maofisa wakiwa na baadhi ya watalaamu wa maabara ya TBL
 Mpishi wa Bia wa TBL, Kelvin Nkya akiwaeleza maofisa hao jinsi bia inavyochachuliwa


 Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam, Calvin Martine (kushoto) akimkabidhi zawadi
Maofisa wa Jeshi wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa TBL baada ya kumaliza ziara.

Rais Kikwete AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO

$
0
0
 
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) leo katika ukumbi wa White House mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na wengine kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu imemteua mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chambani, Pemba Mattr Said .(Picha na Bashir Nkoromo

MDAU NA BLOGGER AMANI MASUE ALA NONDOZZZZZ YAKE YA SHAHADA YA PILI YA ( MASTERS OF FINANCIAL MANAGEMENT) UNIVERSITY OF MYSORE INDIA.

$
0
0
Amani masue akipokea cheti cha kuhitimu shahada yake ya pili ya (Masters of financial management)
Picha ya pamoja wa wahitimu kutoka nchi mbali mbali zipatao 50 wakiwemo watanzania zaidi ya 40 waliohitimu katika shahada mbali mbali.

Picha ya pamoja ya baadhi ya watanzania waliohitimu

pamoja na marafiki





BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI ADMISSION OPEN FOR ACADEMIC  2013/14 UNIVERSITY OF MYSORE INDIA.



WIKI YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII KATIKA PICHA

$
0
0
WajumbewaBodiya SSRA wakiwa katika viwanja vya monyesho vya Nyerere Square mjini Dodoma kutoka kushoto ni Juma Muhimbi, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Jayne Nyimbo na Kabeho Solo.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji cha SSRA, Sara Kibonde akifurahia jambo na Wakuu wa Mifuko ya GEPF, Daud Msangi na mfuko wa LAPF, Eliud Sanga.
 Meneja wa Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele akimkaribisha mjumbe wa bodi ya SSRA, Kabeho Solo katika banda la PPF.
   Meneja Masoko wa GEP, Aloyce Ntukamazi akitoa maelezo ya shughuli na faida wazipatazo wanachama wa GEPF kwa wajumbe wa bodi ya SSRA

 Ofisa wa Uwekezaji wa PSPF, Hamidu Ngororo akiwaeleza wajumbe wa SSRA mradi wa nyumba za bei nafuu za wanachama zilizopo Dar es salaam, Mtwara, Tanga, Shinyanga na Morogoro.

MKUTANO WA KAMATI YA UCHUNGUZI WA MAHESABU YA SERIKALI PAC NA WADAU WAKE

$
0
0

  Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza hesabu za Serekali (P.A.C) Omar Ali Shehe akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wandishi wa habari kwa lengo la kupata mashirikino na ufanisi katika utendaji wa kazi zao. Kikao hicho kilifanyika Baraza la Wawakilishi Mbweni.
 Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahim akichangia katika kikao cha Wadau mbalimbali wakiwemo wandishi wa habari wa vyombo tofauti kwa lengo la kupata mashirikino na ufanisi katika utendaji wa kazi zao, (kulia) Mhasibu Mkuu wa Serekali Omar Hassan, huko Baraza la Wawakilishi Mbweni. 
 Mwandishi Salum Vuai, akitoa mchango wake kuhusu majukumu ya kamati ya kuchunguza hesabu za Serekali. Kikao hicho kilifanyika Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.


=====  ========  ===== =====
Ramadhani Ali-Maelezo Zanzibar                      

Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee  Ibrahim amesema Serikali inawajibu wa kuyafanyia uchunguzi wa kina mapendekezo ya Kamati  za Baraza la Wawakilishi na haipaswi kuwachukulia hatua moja kwa moja watu waliotajwa ndani ya taarifa kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma.

Mkurugenzi huyo ameeleza hayo leo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa pamoja kati ya Kamati ya Uchunguzi wa Mahesabu ya Serikali na Mashirika  (PAC) na wadau wa Kamati hiyo kwenye Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani.  Amesema katika kuyapitia na kuyafanyia uchunguzi mapendekezo ya kamati, wahusika wanaotajwa hupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuyatolea uamuzi na kazi hiyo  huchukua muda kukamilika.

“Serikali haiwezi kuyachukulia hatua mapendekezo yote yanayotolewa na Kamati  ya Baraza bila ya kuwapa nafasi ya kujitetea  watuhumiwa  na kubaini wanaostahiki ili kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wengine kupelekwa mahakamani  kwa mujibu wa sheria za Utumishi wa Umma”, alieleza Ibrahim Mzee.  Ameitaka Kamati ya PAC kuelewa kwamba kuna mchakato mkubwa unaotekelezwa na Serikali  kabla ya kuchukua hatua zinazostahiki kwa wahusika na haipaswi kupewa shinikizo na chombo chochote.

Amesema kazi ya Kamati ya PAC ni kuchunguza na kuishauri Serikali bila ya kutumia vitisho wala kutoa hukumu na kuipa muda Serikali kufanya wajibu unaostahiki ikiwa ni pamoja na kuwachukuliwa hatua waliobanika na makosa. Mkurugenzi wa Mashtka alieleza kwamba kumekuwa na muingiliano wa kazi kati ya kamati moja ya Baraza la Wawakilishi na Kamati nyengine na hivyo kupelekea kamati mbili kuhoji jambo moja.

“Kamati mbili ama zaidi kuhoji kitu kimoja ni kasoro kubwa hivyo inafaa mujipange vizuri  ili kila kamati ijuwe wajibu wake”, alisisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka. Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Khamis Mussa Omar ameitaka kamati ya PAC wanapowasilisha  taarifa katika Baraza  kupunguza hamasa kwani mara nyingi hujenga picha kwa jamii kuwa  wahusika ni wizi na mafisadi.

Akiwashukuru wadau wa PAC Mwenyekiti wa Kamati hiyo Omar Ali Shehe ameomba kujenga mashirikiano ya karibu kati yao na wadau wengine ili kufanikisha majukumu yao yao ya kazi. Amewahakikisha wadau hao kwamba  Kamati ya PAC haina nia ya kumuonea Mtendaji yeyote wa Serikali lakini kubwa wanalofanya ni kuhakikisha rasilimali chache zilizopo Nchini zinawanufaisha Wananchi wote kwa mujibu wa nafasi zao.

Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa mahesabu ya Serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Muhasibu Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka na Vyombo vya Habari.


Barua kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dkt. Abdallah Kigoda : Pendezo kuhusu kuzuia Unyonyaji Dhidi ya Wasanii wa Tanzania katika Biashara ya Miito(Ring back tones)

$
0
0

PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)
 Kwenda kwa:          DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara
 Kuhusu:                    BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)

Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania.  Suala la USIRI lipo Wizara  ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.  Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.
 
USIRI
Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT)  hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao  nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators).

Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo “Network providers” na “Content Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii.  Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content’ nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii.  Wachuuzi (Content Providers) nao  hawatoi taarifa za  mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa  wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya.  Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake.  Hivi sasa biashara hii inathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.

Suluhisho:
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules).  Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)
UNYONYAJI
Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii  wamekuwa wakinyonywa kimapato.  Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake (wimbo) katika mwezi (downloads).
 Lakini mapato yatokanayo na “subscriptions” ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati chochote.  Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za ‘downloads’ na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.

Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public Performances)  na hivyo “copyright Association”  ya Marekani imeweka kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa. Marekani msanii hulipwa asilimia 10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.
SULUHISHO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance’ na kwamba Kampuni za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya  mapato ghafi, ambapo asimilia 10% itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi  na Ulinzi wa kazi za Wasanii.
HITIMISHO
Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones’ na mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni (Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013
 Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma Kaskazini
Dodoma, 13 Mei 2013.

UNESCO yaendesha warsha ya siku moja kujadili Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini.

$
0
0

Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho (katikati) akizungumza wakati kufungua warsha siku moja ya mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchiniambapo warsha hiyo imeshirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo AMREF, UNICEF, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, TGNP, Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na nyinginezo. Kushoto ni Abdoul Coulibaly wa UNESCO na kulia ni Mwezeshaji wa Warsha hiyo kutoka Chuo kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo.
Mwezeshaji wa Warsha hiyo kutoka Chuo kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo akitoa mwongozo kwa washiriki wa warsha hiyo ambapo katika majumuisho yalioamuliwa kwenye warsha iliyofanyika leo ya kujadili Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchiniyatawasilishwa katika mkutano wa Mawaziri utakaohusisha nchi 21 za Afrika Mashariki na Kusini.
Picha juu na chini ni National Program Officer – HIV & Sexuality Education Mathias Herman kutoka UNESCO akichambua mpango wa majukumu ya nchi za Afrika Mashariki na Kusini na kutoa ufafanuzi wa matokeo ya utafiti wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini ambapo ameongeza kuwa nchi inatakiwa kujipanga kwa kusaidiwa na UNESCO pamoja na washirika kuongoza jitihada za kitaifa ambazo zitawawezesha washirika wakubwa ambao ni vijana kushiriki katika mikakati ya kitaifa itakayowasidia vijana nchini kujua mtazamo wao.
Pichani ni Washirki wakifuatilia uchambuzi wa Ripoti uliokuwa ukiwasilishwa na Mathais Herman kutoka UNESCO.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Ufundi stadi Bw. Raymond Benedict (kushoto) akikata kujua kuhusu mapitio ya Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini, huduma zinazotolewa na serikali na nini hatma na vijana wameelewa kwa kiwango gani.
Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO nchini wakichangia maoni yao.Pichani juu Katikati ni Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Lwidiko Edward akiwakilisha vijana na kulia ni Abdoul Coulibaly wa UNESCO
Picha juu na chini ni Washirki wakiendelea kufuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye warsha ya siku moja ya ya mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho.

Mkurugenzi wa ILO Tanzania atembelea vikundi vya jamii vinavyonufaika na mradi wa ILO wa UKIMWI

$
0
0

Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo akikagua kinywaji aina ya ‘paw paw wine’ na mkononi akiwa ameshika matunda aina ya ‘rozela’ yanayotumika kwa kutengenezea ‘juice’ wakati alilipotembelea kikundi cha Chimbuko kinachoundwa na watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Mjini Kyela mnamo tarehe 2, Aprili 2013 ili kujua maendeleo yao. Kikundi cha Chimbuko ni moja kati ya vikundi vya kijamii vinanvyonufaika na mradi wa UKIMWI kwa njia ya uwezeshaji Kiuchumi unaoratibiwa na ILO katika maeneo ipitayo njia kuu ya Tanzania – Zambia. (yaani Chalinze, Ilula, Mafinga, Makambako, Kyela na Tunduma).
Mwenyekiti wa kikundi Cha Chimbuko Bi Sara Mwakinyuke akimwelezea Ndugu Alexio Musindo, Mkurugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania kuhusu matumizi ya bidhaa aina Rozela. Alifafanua pia miongoni mwa bidhaa wanazotengeneza ni pamoja na mmea wa asili aina ya mlonge ambapo alisema mlonge hutumika kama dawa inayotibu malaria. Kushoto kwake ni Afisa Mratibu Mkuu wa ILO nchini Tanzania Ndugu Anthony Rutabanzibwa aliyeongozana na Mukurugenzi wa ILO katika ziara hiyo.
Miongoni mwa vitu vilivyowashangaza maafisa wa ILO walipotembelea kikundi cha Chimbuko ni mmea wa Rozela na matunda yake kwani miongoni mwao hawajawahi kuona mmea huo bali matunda yake yakiwa tayari yameshahifadhiwa katika vifungashio. Sambamba nalo ni kitafunwa aina ya keki ya muhogo ambayo Mkurugenzi wa ILO kanda ya Afrika Mashariki alishangazwa baada ya kula keki hiyo namna ambavyo hata unga wa muhogo pia unaweza kutengenezwa keki na ikawa tamu kwelikweli!
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani Kanda ya Afrika ya Mashariki nchini Tanzania Ndugu Alexio Musindo akiangalia bidhaa aina ya unga uitwao ‘SHIBE’ wenye mchanganyiko wa ulezi, soya lishe, mchele, karanga na mahindi unaosindikwa na kikundi cha chimbuko kama lishe bora inayoweza kutumiwa na watu wa rika zote wakiwemo wanaoishi na VVU na UKIMWI, wazee na watoto
Mwenyekiti wa vikundi cha Chimbuko Bi. Sara Mwakinyuke akimwelezea Ndugu Alexio Musindo, Mkururugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania juu ya changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kujipatia kipato kupitia bidhaa wanazozalisha ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifungashio kwa ajili ya bidhaa wanazozalisha, kutoshiriki katika maonyesho ya Kitaifa ya biashara na ujasiriamali na kukosa elimu ya kutosha kuhusu uzalishaji wa bidhaa zao. Ndugu Alexio Musindo aliwaahidi kuwawezesha kupata vifungashio na Uongozi wa Halmashauri ya Kyela kupitia idara ya UKIMWI kuwaahidi kuwawezesha ili washiriki katika maonyesho ya saba saba mwaka 2013 yatakayofanyika mjini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Faith kilichopo Mjini mbeya Bi Helene Sanga akifafanua jambo baada ya kutembelewa na Ndugu Alexio Musindo, Mkururugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania mnamo tahere 2 Aprili 2013 kuhusu bidhaa wanazotengeneza aina ya BATIKI na changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ufinyu wa mtaji wa kikundi ili kuweza kuzalisha aina mbalimbali za BATIKI na kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya kibiashara. Kikundi cha Faith ni moja kati ya vikundi vya Kijamii na Vyama vya Ushirika mjini Kyela vinavyonufaika na mradi wa UKIMWI na uwezeshaji wa Kiuchumi unaoratibiwa na ILO.
Katibu wa Kikundi cha Mshikamano wajasiriamali mjini Kyela mkoani Mbeya Bw. Nazar Mwaipasi akifafanua kuhusu maendeleo ya kikundi ikiwa ni pamoja na kuanzisha SACCOS punde baada ya kutembelewa na Ndugu Alexio Musindo, Mkururugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania mnamo tahere 2 Aprili 2013.Bw. Nazar aliongeza kuwa kikundi cha Mshikamano kinachoundwa na wanawake na vijana wa kike na kiume wanaojihusisha na biashara binafsi na usindikaji wa vyakula kama mafuta ya mawese, samaki, mapishi na biashara ya mchele, kiliundwa baada ya mafunzo ya ujasiriamali na UKIMWI yaliyotolewa kwa wanawake na vijana kupitia mradi wa UKIMWI na uwezeshaji wa Kiuchumi wa ILO.
Moja kati ya maeneo ya uzalishaji wa kinywaji kiitwacho ‘wine’ katika kikundi cha Chimbuko alipotembelea Ndugu Alexio Musindo, Mkururugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania mnamo tahere 2 Aprili 2013. Ndugu Musindo aliwaeleza wanawake wa Kikundi cha Chimbuko kuwa malengo ya shirika la kazi Duniani katika kuwasaidia wanawake wajasiriamali yatawezekana tu pale ambapo Serikali itakuwa na Sera thabiti za kuwasaidia kuwalinda na kuwawezesha kiuchumi ndipo tutakapopata uzalishaji utakaowawezesha kimapato na kuwekwa sheria zitakazowalinda kijamii.
Mkururugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania Ndugu Alexio Musindo (wa pili kushoto)akinunua baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wanaoishi na VVU Chimbuko mjini Kyela baada ya kutembelea katika jengo wanalouzia bidhaa zao mapema tarehe 2 Aprili 2013 ili kujua maendeleo ya mradi wa UKIMWI unaoratibiwa na ILO katika wilaya ya Kyela. Kutoka kulia ni Afisa Maendeleo Mkuu wa Wilaya ya Kyela ndugu Omari Mungi, Afisa Mratibu Mkuu wa ILO nchini Tanzania ndugu Anthony Rutabanzibwa, na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa UKIMWI ILO nchini Bi. Getrude Sima (kushoto).


Hili ni jengo linalomilikiwa na Kikundi cha Chimbuko katika Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya na ndilo eneo wanalouzia bidhaa zao mahali ambapo mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini ndugu Musindo alipata fursa ya kutembelea mnamo tarehe April 2, 2013. Wito wa Chimbuko kuomba wahisani ikiwemo serikali kuwaboreshea mazingira yao ya kazi ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokidhi mahitaji na kupata ushindani mzuri katika soko kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuongeza kipato, ajira na kuondokana na umasikini.
Mkururugenzi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki nchini, Ndugu Alexio Musindo akipeana mkono na Meneja wa Kimbalu SACCOS ndugu Aggrey Mwambije alipotembelea ofisini hapo mnamo tarehe 2 Aprili 2013 kujua maendeleo ya wanaonufaika na mradi wa UKIMWI na uwezeshaji Kiuchumi unaoratibiwa na ILO. Kimbalu SACCOS ipo mpakani mwa Tanzania na Malawi (Kasumulu)katika wilaya ya Kyela na wanachama wake wananufaika na mradi huo.
Wakionekana wenye nyuso za furaha ni wanachama wa Kimbalu SACCOS katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania ndugu Alexio Musindo punde baada ya kupata taarifa ya mafanikio ya mradi mnamo tarehe 2 Aprili 2013. Kimbalu SACCOS in waelimisha rika mahiri 21 waliopata elimu ya UKIMWI kupitia mradi wa ILO wa UKIMWI.
Mkurugenzi wa ILO nchini Tanzania akinong’ona jambo na Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji Mdogo Tunduma Bi. Deonisia Kafuka wakielekea katika ziara ya kutembelea vikundi vya kijamii vinanvyonufaika na mradi wa ILO wa UKIMWI na uwezeshaji wa Kiuchumi mnamo tarehe 2 Aprili 2013. Katika ziara hii Ndugu Musindo pia alipata fursa ya kufanya kikao na viongozi wa serikali wa Halmashauri ambapo alipata kuelezwa kuwa Tunduma ni mji unaokuwa kwa kasi kibiashara na pia tatizo la utumikishwaji wa watoto ni kubwa hivyo kutoa wito kwa ILO na UNICEF waangalie jinsi gani wanaweza kusaidia kutatua tatizo hili.
Wanawake wa Kikundi cha Amani ‘A’ kinachojishughulisha na shughuli za usindikaji wa vyakula, ufumaji wa mashuka na mikeka na kilimo pia waliweza kutembelewa na Mkurugenzi wa ILO nchini Tanzania. Wakinamama hawa walipata wasaaa wa kumwelezea Mkurugenzi wa ILO nchini kuhusu maendeleo wanayopata kupitia shughuli zao sambamba na kupata mafunzo ya ujasiriamali kutoka ILO kupitia waelimishaji wake. Pia waliweza kubainisha changamaoto zinazowakabili kama upungufu wa vifaa vya uzalishaji zikiwemo cherehani na mitaji midogo. Mkurugenzi wa ILO nchini aliwaahidi kuwa ILO itazidi kuwasaidia ili waweze kuondokana na hali ya umasikini na athari zitokanazo na UKIMWI.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini ndugu Alexio Musindo akiwa katika moja ya kiwanda cha ufumaji cha wana kikundi wa Amani ‘A’ mjini Tunduma baada ya kuwatembelea mnamo tarehe 2 Aprili 2013. Kikundi hiki ni moja ya vikundi vilivyopokea elimu ya ujasiriamali na UKIMWI inayotoelewa na ILO chini ya Mradi wa UKIMWI.
Hizi ni baadhi ya mashine mbili za ushonaji (vyerehani) zinazomilikiwa na kikundi cha Amani ‘A’ mjini Tunduma.
Mkurugenzi wa ILO pia alipata nafasi ya kuonana na viongozi na baadhi ya wanachama wa SACCOS ya Lulu Tunduma ambayo pia inanufaika na elimu ya mradi wa ILO wa UKIMWI. Tunduma Lulu SACCOS ina jumla ya waelimisha rika mahiri 9 waliopata mafunzo kupitia mradi huu ambao huendeleza mafunzo kwa wanachama wao.

Mradi wa kupunguza uwezekano wa kuambukizwa virusi vya Ukimwi and kuwezeshwa kiuchumi ni mpango wa kikanda unaofadhiliwa na Sida wenye lengo la kusaidia pale ambapo panagundulika kuna shida.

Kwa hapa nchini Tanzania mpango huu unawalenga wafanyakazi wanaohama katika maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Zambia. Mpango umewatambua watu ambao wako hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa urahisi na lengo ni kupunguza uwezekano wa kuenea kwa maambukizi hayo kupitia kuwawezesha watu kiuchumi kupitia Mashirika ya Kiuchumi ya Jamii (SEOs).

Mashirika hayo ya hiari yameundwa na makundi ya watu ambao wanatjadili mambo ambayo yanawagusa. Mpango huu unalenga kuwawezesha wanawake na vijana wa kiume ambao wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa urahisi zaidi. Kupitia mpango wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa Anzisha na Boresha Biashara Yako, mradi unasaidia SEOs kufikisha huduma kwa wanachama wao wa kiume na kike.

PPF YAENDELEA KUANDIKISHA WANACHAMA WAPYA KATIKA WIKI YA HIFADHI YA JAMII

$
0
0
Mbungewa Jimbo la Tabora Mjini Mh. Aden Rage akikabidhi mchango wake wa kwanza kwa Mhasibu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Grace Fihavango mara baada ya kujiunga na Mfuko huo. Mheshimiwa Rage alijiunga na PPF chini ya mfumo wa hiari alipotembelea banda la PPF kwenye wiki ya Hifadhi ya Jamii inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. William Erio.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. William Erio (kushoto) akimkabidhi kitambulisho cha uanachama wa PPF Mbunge waTabora Mjini Mh. Aden Rage (katikati) mara baada ya kujiunga na Mfuko huo. Mheshimiwa Rage alijiunga na PPF chini ya mfumo wa hiari alipotembelea banda la PPF kwenye wiki ya Hifadhi ya Jamii inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Eliudi Sanga.

 MbungewaJimbo la TemekeMh. Abbas  Mtemvu akipata maelezo ya fomu ya kujiandikishana Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Afisa Michango wa PPF Bi. Herieth Magala. Mhe.Mtemvu aliamua kujiunga na PPF alipotembelea kwenye banda hilo, katika wiki ya Hifadhi ya Jamii inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.

Mbungewa Jimbo la TemekeMh. Abbas Mtemvu akikabidhi mchango wake wa kwanza kwa Mhasibu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Grace Fihavangomara baada ya kujiunga naMfuko huo. Mheshimiwa Mtemvu alijiunga na PPF chini ya mfumo wa hiari alipotembelea banda la PPF kwenye wiki ya Hifadhi yaJamii ya inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.  Katikati ni Afisa Michango wa Mfuko huo Bi. Herieth Magala akishuhudia tukio hilo. 

GOETHE INSTITUT-TANZANIA INVITE YOU TO AN OPEN STAGE NIGHT

$
0
0

On our OPEN STAGE NIGHT we invite you to perform. Whatever your talents might be, everyone is welcome to show them on stage. Please register now by sending us an e-mail or call us.E-mail: intern@daressalaam.goethe.org, Tel.:  075 375 152 and Tell us what you are planning to perform and the required technical equipment. 

Musicians can also bring their own instruments. entrance is fees.

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images