Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 823 | 824 | (Page 825) | 826 | 827 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mtoto Anisha Juma (2) mkazi wa Morogoro mjini aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa matibabu leo April 17.2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuangalia utendaji kazi na utoaji huduma kwa Jamii.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Bibi Fausta Andreas na Mtoto wake Vayalet Michael (2) aliyelazwa katika Hospitali ya rufaa Mkoa Morogoro kwa matibabu wakati alipotembelea Hospitali hiyo leo April 17.2016 kwa ajili ya kuangalia utendaji na utoaji huduma kwa Jamii. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro leo April 17,2016, wakati alipowasili Hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolea kwa Jamii katika Hospitali hiyo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. kulia Daktari Mfawizi wa Hospitali hiyp Dr. Rita Lyamuya.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mafundi Seremala cha (Kimasemo) kiliopo Sabasaba Mkoani Morogoro, wakati alipotembelea Kiwanda hicho leo April 17.2016 kwa ajili ya kukagua kazi zinazofanywa na kikundi hicho ambapo ameahidi kuchangia jumla ya Tshs 10 milioni kwa ajili ya kuendeleza utendaji wa kiwanda hicho. Makamu wa Rais yupo Mkoani Korogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na watoto baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea kiwanda cha Mafundi Seremala cha (Kimasemo) kiliopo Sabasaba Mkoani Morogoro leo April 17.2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Korogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu(Picha na OMR)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na watoto baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea kiwanda cha Mafundi Seremala cha (Kimasemo) kiliopo Sabasaba Mkoani Morogoro leo April 17.2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Korogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu(Picha na OMR)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi hundi ya Tshs 10 Milioni kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha vijana cha Mafundi Seremala (Kimasemo) Habibu Said zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Azizi Aboud kwa ajili ya kuendeleza utendaji wa kiwanda hicho. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

  0 0

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  TAARIFA KWA UMMA
  Gazeti la Raia Tanzania Toleo Na.0615 la Tarehe 15 Aprili, 2016 liliandika taarifa  yenye kichwa cha habari “Mbunge apewa mgodi hifadhini” huku likieleza kuwa Mbunge wa Meatu, Salum Khamis Salum (CCM), ametumia ushawishi alionao kisiasa kufanikisha upatikanaji wa leseni ya kuchimba shaba katika eneo la Gururum lililomo ndani ya Hifadhi ya Mwiba, Meatu mkoani Simiyu.


  Gazeti hilo lilieleza kuwa leseni hiyo ilitolewa na Ofisa Madini Kanda ya Ziwa, Mhandisi Juma Sementa, yenye uhai wa miaka Saba na kwamba upatikanaji wa leseni hiyo haujawaridhisha wadau kadhaa wa ardhi na mazingira kwani mbali na sheria ya kuzuia uchimbaji madini ndani ya maeneo ya hifadhi nchini, wadau wengine hawakuhusishwa katika upatikanaji wake.


  Wizara inapenda kutoa taarifa kuwa, wilayani Meatu kuna hifadhi ya Maswa (Maswa Game Reserve) na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika eneo la Makao (JUHIWAPOMA) ambapo Jumuiya hiyo ilipitisha Mpango wa Kanda za Matumizi ya Rasilimali kwa mwaka 2015-2017 na kutenga eneo la Gururum lenye ukubwa wa kilomita 16.5 sawa na asilimia 2 ya eneo lote, kama kanda ya uchimbaji madini baada ya madini ya shaba kugundulika katika eneo hilo.


  Katika eneo hilo la Gururum mpaka sasa jumla ya viwanja 82 vya uchimbaji mdogo wa madini (PML) vimetolewa ambapo kwa sasa hakuna shughuli zozote za uchimbaji zinazoendelea hadi tathmini ya uharibifu wa mazingira (EIA) itakapokamilika ambayo ipo katika hatua ya uwasilishwaji.

  \
  Hivyo tunautaarifu Umma kuwa mpaka sasa hakuna mgodi katika hifadhi ya Mwiba na kwamba leseni za uchimbaji mdogo wa madini zimetolewa katika eneo lililorusiwa tu kwa ridhaa ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika eneo la Makao (JUHIWAPOMA).


  Tunawaasa waandishi wa habari kuhakiki taarifa wanazotoa katika vyombo vya habari kwa kuwasiliana na wahusika wanaotajwa katika habari husika ili kuepuka kutoa taarifa potofu kwa Umma.


  IMETOLEWA NA WIZARA YA NISHATI NA MADINI


  18 APRILI, 2016


  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile ambaye pia ni meneja wa bondia Francis Cheka akimwaga sera baada ya kupitishwa kuwania nafasi ya Ukatibu Mkuu kwa Chama Cha Soka cha Manispaa ya Kinondoni (KifA)
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile (wa kwanza kushoto) akiwa na bondia wake Francis Cheka wakati wa kukabidhi mkanda wa ubingwa Super Middle kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (wa kwanza kulia).

  Meneja wa bondia Francis Cheka, Juma “Chief” Ndambile amesema kuwa ameamua kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Cha Kinondoni (KIFA) kwa lengo la kuendeleza mchezo huu katika manispaa hiyo.Uchaguzi Mkuu wa Kifa umepangwa kufanyika Mei Mosi na utawashirikisha jumla ya wagombea 33 waliopitishwa na kamati ya Uchaguzi ya chama hicho.

  Ndambile ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni maarufu ya ulinzi yaAdvanced Security Co. Limited alisema kuwa kabla ya kuamua kuwania nafasi hiyo, alifanya uchunguzi wa kina na kugundua kuwa pamoja na Kinondoni kuwa na wachezaji wengi wenye vipaji, tatizo kubwa ni uongozi.

  Ndambile alisema kuwa Kinondoni ina wadau wengi wa mpira wa miguu, lakini cha kushangaza mpaka sasa hakuna timu inayoshiriki LigiKuu ya Tanzania Bara na kubaki na timu za daraja la kwanza, pili na madaraja mengine ya chini.

  Alisema kuwa Kinondoni ina timu nyingi sana za mpira wa miguu ambazo zinaibua vipaji kutoka chini na wengine kuwa wachezaji wa kutegemewa wa timu za Ligi Kuu na timu ya Taifa, lakini kutokana na mfumo wa uongozi kuwa si mzuri, wachezaji hawa wanahamia timu nyingine na kuzipandisha daraja kucheza ligi kuu na Kinondoni kubakia nyuma.

  “Kungekuwa na uongozi bora ambao ungekuwa unafuatilia kikamilifu wachezaji na klabu, leo tusungekuwa na timu mbili tu daraja la kwanza, Friends Rangers na KMC zingekuwa ligi kuu na nyingi zingekuwa daraja la kwanza, sisi tumekuwa mishumaa wa kutoa mwanga huku tukiteketea,”

  “Siri kubwa ya kuondokana na hili ni kutafuta wadhamini kwa timu zetu na kuboresha hali ya wachezaji, Kinondoni ni Manispaa tajiri Tanzania kwa kutumia wadhamini, waachezaji wangepata vipato vizuri na kupunguza kazi kwa viongozi kuhangaika huku na kule kusaka fedha za uendeshaji wa timu,” alisema Ndambile.

  Alifafanua kuwa mbali ya maslahi ya waamuzi, pia atahakikisha kunakuwa na uhusiano mzuri na vyama vishirikishi katika soka kama madaktari wa michezo, makocha, soka la vijana, soka la wanawake, Suptanza na wadau wengine ili kujenga umoja wenye nguvu. Alisema kuwa yeye yupo tayari kufanya kazi wadau wote wa mpira wa miguu pamoja na kuhimarisha zaidi uhusiano wa serikali ya Manispaa ya Kinondoni na chama kwani ndiyo nyenzo pekee ya kufikia hatua kubwa kabisa ya maendeleo.

  “Sitakuwa kiongozi wa kukaa ofisini, kama mtendaji nitakuwa mfuatiliaji wa kila jambo kama ilivyo kwa viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, tunahitaji kufanya kazi na si kutafuta sifa,” alisema.Mbali ya Ndambile, wagombea wengine katika nafasi hiyo ni Hashim Abdallah, Selemani Sufiani, Ramadhani Kampira, Funua Ally, Isack Mazwile na Raymond Solomon.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wakufunzi wa mafunzo ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Athuman Libanda baada ya kuhitimu mafunzo ya siku 12 ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kuwafundisha vijana wanaojiunga na jeshi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhayo, Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i Issa (nguo nyekundu) na viongozi wengine wa jeshi hilo. 
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, .Jenista Mhagama akimkabidhi cheti mmoja wa wakufunzi wa mafunzo ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Bi. Joyce Shauza baada ya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali ya siku 12 yaliyoendeshwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kuwafundisha vijana wanaojiunga na jeshi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhayo, Katibu Mtendaji wa NEEC,  Beng’i Issa (nguo nyekundu) na viongozi wengine wa jeshi hilo. 
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati) akiondoka katika ukumbi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mara baada ya kufunga mafunzo ya siku 12 ya wakufunzi wa somo la ujasiriamali mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kulia ni  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali, Michael Isamuhayo. Mafunzo hayo yaliendeshwa na NEEC.

  Na Mwandishi wetu.
  Jumla ya wakufunzi 53 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali na kutunukiwa vyeti.

  Mafunzo hayo yaliendeshwa kwa muda wa siku 12 na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

  Mafunzo hayo yalifanyika katika kambi ya Mgulani na kuhusisha mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Pwani. 

  Akikabidhi vyeti hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Kazi, Ajira Vijana na Walemavu,Bi.Jenista Mhagama alisema wakufunzi hao wana wajibu wa kuwafundisha somo la ujasirimali vijana wanaojiunga na jeshi hilo ili kupambana na tatizo la ajira nchini.

  “Mafunzo mliyopata yalilenga kuwawezesha mkawafundishe vijana ili baada ya hapo waweze kujiajiri au kuajiri wengine,” alisema,Bi. Mhagama mwishoni mwa wiki.

  Alifafanua kwamba kuwafundisha somo la ujasiriamali itasaidia kwenda sambamba na soko la ajira katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, utalii, hoteli na kwamba nguvu kazi kubwa ya vijana itakuwa inafanya kazi badala ya kukaa tu na kupenda starehe.

  Alisema serikali ya awamu ya tano imejielekeza katika kuwezesha wananchi na jeshi hilo lina nafasi kubwa ya kutumia fursa iliyonayo kusaidia kukuza vijana ili kwa pamoja kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.

  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Brigedia Jenerali, Michael Isamuhayo alisema jeshi limejipanga kuwafundisha vijana wanaopitia mafunzo hayo ipasavyo ili wawe chachu ya kukuza vipato vyao na uchumi wa nchi.

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa alisema utoaji wa mafunzo hayo kwa wakufunzi wa vijana kwa jeshi hilo ni utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

  “Kupitia mafunzo haya wakufunzi watapata fursa ya kwenda kuwafundisha vijana kupata stadi na kushiri katika uzalishaji mali na kuendesha maisha yao,”alisema,Bi. Issa.

  Aliwahimiza vijana wanaohitimu masomo wajiunge na mafunzo ya JKT kwa wingi na huko watakutana na mafunzo hayo yanayolenga kuwajenga kujitegemea.

  Kwa mujibu wa program hiyo, kanda itakayofuata itakuwa ya Kati na Magharibi itakayojumuisha mikoa ya Dodoma, Kigoma, Tabora na Mwanza,”alisema.

  Mafunzo yatafanyika katika kambi ya Makutopora, Dodoma, Mafunzo hayo katika kanda ya Kusni yatafanyika Mafinga ambapo mikoa itakayohusika itakuwa Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe.

  Mafunzo katika kanda ya Kaskazini yatafanyika katika kambi ya Mgambo mkoani Tanga na kuhusisha mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro.

  Tangu kurejeshwa kwa utaratibu wa mafunzo ya vijana wa kujitolea mwaka 2001 idadi ya vijana wanaojiunga na JKT imeendelea kuongezeka kila mwaka.

  Vijana waliopita JKT hadi mwaka 2014 ni 104,594.  Kati ya idadi hii, vijana 34,291 waliingia kwa mpango wa kujitolea ambapo asilimia 70 waliajiriwa na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama.

  Asilimia 30 inayobaki, sawa na vijana 2,000 wanarudi nyumbani kila mwaka, Mafunzo hayo yanaendeshwa na wakufunzi wanaotambuliwa kimataifa. 

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akipanda mti katika hifadhi ya Masingini kwa kushirikiana na Bi Nassim Said Mohameid (Kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Misitu na Maliasili zisizorejesheka wa Zanzibar bwana Sheha Idrissa Hamdani.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akipanda mti katika hifadhi ya Masingini 
   Mkuu wa Zantel kwa upande wa Zanzibar, Mohameid Mussa (katikakati) akipanda mti kwa kushirikiana na Hamza Zuheri, Meneja wa Mtandao na Vifaa vya mawasiliano wa Zantel (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Misitu na Maliasili zisizorejesheka wa Zanzibar bwana Sheha Idrissa Hamdani (kushoto).
   Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chissenga akipanda miti katika hifadhi ya Masingini. Anayemsaidia kushoto ni Mkurugenzi wa Misitu na Maliasili zisizorejesheka wa Zanzibar bwana Sheha Idrissa Hamdani.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akipewa maelezo kuhusu hifadhi ya Masingini Bi Nassim Said Mohameid (Kushoto) wakati wa zoezi la upandaji miti lilofanywa na wafanyakazi wa Zantel.
   Wafanyakazi wa Zantel kutoka kushoto Deus Mtena, Winnes Lyaro na Leonard Kameta wakipanda mti katika hifadhi ya Masingini.

   Mwanasheria wa Zantel Bi Julia Kilala akipanda miti kwa kushirikina na watoto wake Noah and Nathan Kilala.
  Wafanyakazi wa Zantel na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti.


   Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Zantel leo wameshiriki katika zoezi la kupanda miti kwenye hifadhi ya Masingini iliyopo magharibi mwa kisiwa cha  Unguja kama  moja ya jitihada zake katika kutekeleza mpango wa kutunza na kuhifadhi mazingira visiwani Zanzibar.

  Eneo la hifadhi ya msingini lipo mita 120 kutoka usawa wa bahari na ni eneo lenye vyanzo vingi vya maji  ambavyo vinakadiriwa kutoa lita 27,400,000 kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya wakazi wa Zanzibar.

  Akizungumza wakati wa upandaji miti, Afsa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu ya Zantel,bwana Benoit Janin alisema kupanda miti kutasaidia kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kuongeza  rutuba ya udongo na pia kulinda vyanzo vya maji .

  ‘Kama Kampuni ya simu inayotoa huduma ya mawasiliano kwa wakazi wa visiwani ni lazima tuhakikishe tunatunza na kuhifadhi mazingira kama moja ya  rasilimali muhimu kwa  ajili ya ustawi wa jamii yetu’alisema Bw Janin.

  Zoezi hili la kupanda miti limefanyika leo, ikiwa ni wiki moja tu toka uzinduzi wa mtandao wa 4G visiwani hapa, hatua inayoonyesha kuwa kampuni ya Zantel imejipanga katika mpango wa kuhakikisha inalinda na kuhifadhi mazingira kwa kushirikiana na serekali yetu .

  Akizungumza baada ya tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar, bwana Sheha Mjaja Juma aliwapongeza wafanyakazi wa kampuni ya simu ya  Zantel kwa kuweza kushiriki kwenye  zoezi hilo  la kutunza na kuhifadhi mazingira.

  ‘Madhumuni ya zoezi hili la upandaji miti hapa Masingini yamelenga kusaidia jitihada za kutunza na kulinda vyanzo vya maji, msitu pia kuzuia mmonyoko wa ardhi ili kulinda viumbe hai vilivyopo kwenye eneo hilo’ alisema bwana Sheha.  0 0

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiwa ameongozana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan (kushoto) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Zhang Jiannan pamoja na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwenye Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano baina ya Mahakama ya Tanzania na China. 
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisalimiana na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya kuwakaribisha   Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
    Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China uliolenga kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa Mahakama za Tanzania na China leo jijini Dar es salaam. 
   Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China.
     Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wale wa Mahakam Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakibadilisha uzoefu wa shughuli za kimahakama na masuala mbalimbali ya utendaji wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China jijini Dar es salaam.
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan.
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akimweleza jambo Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan wakati wa mkutano huo.
  Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akieleza namna Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China inavyofanya kazi leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha pamoja kilichowahusisha Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na China. Wengine  ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila.  
   Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman.
    Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa.
   Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akimweleza jambo jaji wa Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya kumkaribisha Ofisini kwake Mahakama Kuu leo jijini Dar es salaam.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akiwa katika mazungumzo na Jaji wa Mahakama Kuu ya China na baadhi ya Majaji kutoka  Mahakama hiyo waliomtembelea Ofisini kwake Mahakama Kuu jijini Dar es salaam.
   Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (wa pili kutoka kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (katikati) na baadhi ya watendaji wa Mahakama ya Tanzania mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
   Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang ( kushoto) akiagana na  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (kulia) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.

  0 0

  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano wa wandishi uliofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam akiongelea mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yatakayofanyika Jumanne ya tarehe 19/04/2016, katika ukumbi wa Urafiki Social hall ulioko shekilango jijini Dar Es Salaam.
  ·        Kijana mmojawapo atawezeshwa kwa vitendea kazi katika warsha hiyo

  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, imeandaa  warsha maalumu ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye  umri kati ya miaka 18 - 24 katika mkoa wa Dar es Saalam na kuwaalika vijana kujitokeza kupata mafunzo ya  namna ya kuendesha biashara zao.

  Warsha hiyo ya mafunzo  itafanyika Jumanne ya tarehe 19/04/2016, katika ukumbi wa Urafiki Social hall ulioko shekilango jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 2 asubuhi.

  Katika Warsha hiyo kijana mmoja atakayeweza kuelezea na kuwakilisha changamoto anazozipata katika biashara aliyonayo mbele ya jopo la washauri na vijana wenzake ataweza kupata bahati ya kupatiwa vifaa vya kazi kwa ajili ya kuendeleza biashara yake.

  Akiongea na waandishi wa habari Meneja huduma za jamii wa Airtel Bi.Hawa Bayumi alisema, "Airtel Fursa imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia na kuwawezesha vijana wengi nchini kupata elimu na pia kuwapatia misaada wa vitendea kazi  itakayowawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi"

  Mpaka sasa tumeshafanya semina kama hizi katika mikoa ya Dar es Saalam, Arusha, Mbeya, Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mtwara Dodoma na Iringa na kuwawezesha vijana zaidi ya 3700 kupata mafunzo hayo muhimu  ikiwemo usimamizi wa mtaji, mbinu za masoko, kuzitambua fursa na ujuzi wa kibiashara, namna ya kuendesha biashara na kuweka mahesabu , jinsi ya kufungua akaunti benki na nyingine nyingi"

  Aliongeza kwa kusema "Kwa wakazi na vijana wa Dar Es Salaam hii ni nafasi ya kipekee  kwa vijana wa Dar es Salaam kwani mafunzo haya yanarudi kwa mara ya pili jijini Dar, tunatoa wito wajitokeze kwa wingi kupata mafunzo haya  bure bila gharama yoyote kupitia wataalamu wetu mahiri wenye ujuzi katika maswala ya biashara na ujasiriamali"

  Tunaamini vijana wengi watatoka katika mafunzo haya wakiwa wamewezeshwa kuwa na mtazamo chanya lakini zaidi wakiwa na mbinu za kuendesha biashara zao kwa mafanikio zaidi.

  Airtel kupitia Airtel Fursa itaendelea kutoa warsha kama hizi maeneo mbalimbali hapa  nchini na kuweza kufikia vijana wengi zaidi.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Halmashauri ya Wilaya ya Lindi iliyopo Mkoa wa Lindi imetenga jumla ya shilingi milioni 162 katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya kuisaidia shule ya Msingi Nyangao.

  Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Olliver Vavunge alipokuwa akikanusha kuhusu madai ya wazazi kutaka shule hiyo ifungwe kwa sababu ya ukosefu wa huduma muhimu.

  “Kwa kuwa shule hiyo tayari ina mabweni pamoja na bwalo la chakula, katika bajeti iliyotengwa na Halmashauri kwa mwaka huu wa fedha jumla ya shilingi milioni 100 zitatumika katika ujenzi wa uzio wa shule pamoja na marekebisho madogo madogo ya shule hiyo na shilingi milioni 62 zitatumika kwa ajili ya chakula”alisema Bi. Olliver

  Aidha, Bi. Olliver amekanusha kupewa bajeti ya shilingi laki tisa kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo kwa mwezi kama ilivyoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na kusema kuwa Serikali inatoa jumla ya shilingi milioni 1.6 kwa kila mwezi.

  Ameongeza kukanusha kuwa si kweli kuwa wanafunzi wanakula mlo mmoja kwa siku bali wanapata milo yote mitatu kama ilivyo kawaida.Shule ya Msingi Nyangao ni shule ya watoto wenye mahitaji maalumu (walemavu) ambayo hadi sasa ina jumla ya wanafunzi 42 na inahudumiwa na Serikali kwa mahitaji yote.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea jengo hilo 

  Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Maternity Block Two  na baadhi ya Wakurugenzi wa idara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, aliyesimama katikati kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru.

    Waziri Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH  Profesa Lawrence Museru wakitoka ndani ya jengo hilo la wazazi “ Maternity Block Two” leo Apriil 18, 2016.

  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua ukarabati wa jengo la wazazi- Maternity Block Two - ambao bado unaendelea.

  Akizungumza mara baada ya kutembelea jengo hilo Waziri Ummy amesema anaridhishwa na zoezi hilo la ukarabati ambapo amesisitiza kuwa ni faraja sasa kuona hakuna mama mjamzito anayelala chini.

  “ Kuwepo kwa jengo hili ni faraja kwa kina mama nafurahi kuona ukarabati unaendelea vizuri na upo katika hatua nzuri  kwakweli mnastahili pongezi kwani mnafanya kazi nzuri” amesema Waziri Ummy.
  Maternity Block Two mpaka sasa kuna jumla ya vitanda 63 ambavyo vinatumika na wakina mama wanaendelea kupatiwa huduma.

  0 0

  Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Daar es Salaam leo kuhusiana na Progrmu ya umoja wa mataifa kuhusu Ajira kwa vijana. Kushoto ni Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga.
   Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa MtaifaAnamarie Kiaga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo. kuhusiana na mawazo ya kibiashara yatakayoendeshwa na umoja wa mataifaKushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa ya ajira kwa kuandika rasimu ya wazo la biashara katika eneo ambalo wanaweza kuendelea kiuchumi.

  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji la Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa amesema kuwa program ya hiyo ya ajira ni yangu linafanywa kati ya Baraza hilo na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ikiwa ni lengo kuwawezesha vijana katika mitaji ili waweze kuboresha biashara zao pamoja na kutengeneza ajira kwa wenyewe na kwa vijana wengine.

  Amesema kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania inaendelea kukua kwa kasi na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira, hali dunia ya maisha ,ukosefu wa mitaji, ukosefu mbinu jumuishi pamoja na kukosa fursa za ajira.

  Issa amesema kuwa program ya ajira yangu itahusisha vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 kwa wale ambao wanataka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao.

  Amesema mchanganuo wa biashara katika mashindano hayo ni katika sekta za Kilimo,Usindikaji, viwanda, biashara inayohusu vyombo vya habari, masoko,mawasiliano, michezo, vifaa sanaa na Utamaduni, ,Utalii na Burdani, Biashara inayogusa mazingira na Utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na biashara za kijamii, Biashara ya Habari na Mawasiliano,Teknolojia ikiwa ni pamoja na ushindikaji biashara.


  Amesema kuwa taratibu za uombaji utahusisha awamu tatu ya kwanza ni kujaza fomu ambazo zitapatikana katika tovuti za ILO pamoja na NEEC na maombi hayo yataanza kupokelewa kuanzia leo hadi mei 9 mwaka huu.

  0 0

  Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Yunus Omary Mtopa, akionekana ni mwenye furaha sana baada ya kujinyakulia kitita cha dola elfu 5, kwa kuonekana wazo lake la Biashara ya Miwa kuwa bora zaidi ya wenzake. Hafla ya shindano hilo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.

  Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.
  Jaji Mkuu katika Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Dkt. Neema Muro, akitoa maelezo mafupi ya washiriki wa shindano hilo kabla ya kumtangaza mshindi.
  Sehemu ya Wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo, wakiwa makini kumsikiliza jina la Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
  Mgeni rasmi katika Hafla ya kumtangaza Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa, akikabidhi mfano wa hundi kwa Mshindi wa Shindano hilo, Yunus Omary Mtopa.
  Mgeni rasmi katika Hafla ya kumtangaza Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa (wa nne kulia), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanna-Marie Kaarstad (wa pili kushoto), Meneja Mkazi wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen (shoto) wakiwa katika picha na washiriki wa shindano hilo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara  katika soko la machinga Complex leo mara baada ya kutembelea na Kamati ya Ulinzi na Usalama  jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye tinted kushoto)  akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye suti mbele)  akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa waliongia mkataba wa ujenzi wa soko la Machinga Complex unatatizo kutokana fedha nyingi kudaiwa  baada ujenzi sh.bilioni 36 huku ujenzi wa jengo hilo ni zaidi ya sh.bilioni 12.

  Akizungumza leo baada ya kutembelea jengo hilo Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Makonda amesema kuwa kutokana hali hiyo anaunda kamati kuanzia kesho kuchambua mkataba huo kujua ni nani wamehusika na kwa nini waliingia au waliingia wakiwa wamekunywa pombe.

  Amesema baada ya kuchambua wale waliohusika katika mazingira ya rushwa watachukuliwa hatua kutokana na kuiongezea mzigo serikali kwa masilahi yao.

  Makonda amesema hata utaratibu wa ugawaji wa vizimba una matatizo kutokana baadhi ya watumishi wenye nafasi zao  kumiliki vizimba na kupangisha watu wafanyabiashara.

  ‘’Nitahakikisha mkataba wa machinga Complex una majibu ya kutosha juu ni nani waliohusika katika kubebesha mzigo serikali kwa wananchi wake’’ .amesema Makonda

  Amesema katika mazingira hayo jengo hilo kwa fedha hiyo watu wafanyabiashara hawawezi kuilipa mpaka kuangaliwa uhalali wa mkataba wa ujenzi wa jengo hilo.

  Aidha amesema kuwa wananchi wa Dar es Salaam lazima wachukie rushwa ili kuweza kupata huduma bora ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za rushwa na wanaotoa hata kama wanyonge hatua zitachukuliwa.

  Amesema katika wafanyabiashara ndogo ndogo  wanaozungusha biashara zao katika mitaa waombe maeneo ya kufanyia kazi na kuweza serikali kupata kodi yake.

  0 0


  Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akifunua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la jengo la biashara na Ofisi la 2D la mjini Morogoro lililojengwa kwa thamani ya Shilingi bilioni 4.3. Jengo hilo ni la ghorofa nne likiwa na eneo la chijni kwa ajili ya maegesho ya magari . Ni mradi wa kwanza kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu mara tuu baada ya kuwashwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
  Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
  Meneja wa Shirika la Taifa, Veneranda Seif akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
  Meneja wa Shirika la Taifa, Veneranda Seif akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.

  Jengo la Biashara la 2D linavyoonekana leo kabla ya kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya.
  Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa akijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru.
  Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wakijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru.
  Mwenge wa Uhuru ukiwasili katika eneo la tukio.
  Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter akiupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika eneo mradi wa 2D.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zsaidi wafaidike.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zaidi wafaidike.
  Wafanyakazi wa Ashirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zaidi wafaidike.

  0 0

  NDG. ALLY SALUM HAPI  MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete, akiendelea kuangalia maendeleo ya ukarabari wa Bomba kubwa la Maji lililokatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini, lililopo katika Karavati bondeni Msata -Kihangaiko, Chalinze.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete (mwenye fulana nyekundu) akiangalia maendeleo ya ukarabari wa Bomba kubwa la Maji lililokatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini, wakati alipotembelea eneo hilo lililopo katika Karavati bondeni Msata -Kihangaiko, Chalinze. Juhudi za ujenzi zimekuwa zikiendelea toka siku lilipobainika tatizo hilo na matarajio ni kumalizika jioni hii na maji kusukumwa kuanzia kesho.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete, akipatiwa maelezo na mmoja wa mafundi wanaofanya ukarabari wa Bomba kubwa la Maji lililokatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini, lililopo katika Karavati bondeni Msata -Kihangaiko, Chalinze.
  Mafundi wakiendelea na kazi.

  0 0

  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania ( BOT), Amatus Liyumba amefariki dunia leo katika Hospitali ya Agha Khan alikokuwa akipatiwa matibabu, msiba uko nyumbani kwake maeneo ya Triple Seven, Mikocheni jijini Dar es salaam. Taarifa zaidi zitawajia baadae kidogo. 

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation, Juma Mndeme, mwenye miwani akizungumza jambo baada ya kumaliza kukabidhi misaada ya mabenchi ya kukalia, sabuni na vinywaji kwa Kituo cha afya Mwanga, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. Aliyeshika majaketi ni Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo hicho Honest Temba na aliyeshika simu ni Meneja Uhusiano wa Habibu Foundation, Julysiza Mangiseni.

  Na Mwandishi Wetu, Mwanga.

  MAADHIMISHO ya Siku Maalum ya Habibu Day wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro yamefanyika kwa mafanikio kwa kushirikisha matukio mbalimbali yakiwamo ya kutoa misaada katika kituo cha Afya Mwanga, kutoa misaada jeshi la Polisi, pamoja na kufanyika mijadala mbalimbali ya kielimu iliyoendeshwa na wanafunzi wa shule za sekondari wilayani humo.

  Katika muda wa mijadala, wanafunzi hao walitumia muda mwingi kuzungumzia mfumo wa kielimu nchini Tanzania sanjari na upangaji wa matokeo ya mitihani kutoka Division na GPA iliyoondolewa rasmi katika mfumo huo nchini hapa, huku mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyata kilichopo Arusha, Profesa Ward Mavura.

  Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation, Julysiza Mangiseni, akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo yaliyoanzia kutoa zawadi mbalimbali. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Habibu Foundation akizungumza
  Mkuu wa Polisi wilayani Mwanga, Pili Mande akipokea sehemu ya zawadi kutoka kwenye Taasisi ya Elimu ya Green Bird
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Green Bird kilichopo wilayani Mwanga wakielekea kwenye Kituo cha Afya cha Mwanga kwa ajili ya kupeleka zawadi mbalimbali kama ishar ya kumuenzi muasisi wao marehemu mzee Habibu Mndeme. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

  Awali ratiba ilianza rasmi saa 12 asubuhi kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Green Bird Girls, Green Bird Boys, Green Bird Collage zinazomilikiwa na taasisi ya Habibu Foundation kutembelea katika maeneo ya Ofisi ya polisi Mwanga na kituo cha afya Mwanga, pamoja na kutoa misaada kama vile mabechi ya kukalia wagonjwa, sabuni, vinywaji pamoja na vifaa ya ofisi kwa jeshi la Polisi Mwanga.

  Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation,, Juma Habibu Mndeme, alisema kwamba lengo la kufanyika kwa maadhimisho hayo ni kukutanisha pamoja wadau wa elimu wilayani Mwanga sanjari na kumuenzi mwanzilishi wa taasisi yao marehemu Habibu Mndeme aliyefariki Dunia mwaka 2010) na kuacha taasisi hiyo inayomiliki pia shule wilayani Mwanga.

  “Tumekuwa tukiadhimisha matukio haya kila mwaka lakini tunaendelea kuboresha hatua kwa hatua, maana lengo la taasisi ni kukuza kiwango cha elimu kwa wilaya ya Mwanga na Tanzania kwa ujumla, ndio maana mijadala ya kielimu ilihusisha wanafunzi mbalimbali kutoka ndani ya Mwanga na nje pia, ikiwamo jijini Arusha.

  “Sisi kama waendeshaji wa shule zote za Green Bird tunajivunia kufanyika maadhimisho haya kwa mafanikio makubwa, bila kusahau ulinzi madhubuti kutoka kwenye jeshi la polisi kuanzia asubuhi hadi usiku, huku tukiona ushindani mkubwa, uzoefu na umakini kwa kila aliyeshiriki kuonyesha ujuzi na uwezo wake, hususan katika suala zima la kielimu,” Alisema Mndeme.

  Naye Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Profesa Ward Mavura ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomokenyata cha jijini Arusha, aliitaka jamii ya wilaya Mwanga kuiunga mkono taasisi hiyo kwa ajili ya kuiweka katika mazingira mazuri katika utoaji wa huduma zake.

  Akizungumzia tukio hilo na utoaji misaada kwenye jeshi la Polisi wilayani Mwanga, Mkuu wa Polisi Mwanga, Pili Mande, aliishukuru Taasisi ya Habibu kwa kuwekeza katika elimu na kuisaidia jamii kwa mambo mengi, jambo linalotakiwa kuungwa mkono na kuendelezwa kwa manufaa ya Mwanga na Tanzania kwa ujumla.

  Naye Meneja Uhusiano wa wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation,, Julysiza Mengiseni, alisema kwamba kufanyika kwa mafanikio kwa maadhimisho hayo ni hatua nzuri ya kuhakikisha dira ya kuifanya taasisi yao iwe kioo cha elimu wilayani Mwanga na Tanzania kwa ujumla.

  “Taasisi inaendelea kutoa elimu bora kwa kuweka miundo mbinu mizuri katika shule zake za sekondari na chuo pia hapa wilayani Mwanga, ambapo kwa pamoja tunasonga mbele kutolkana na ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka serikalini na kwa wananchi wote,” Alisema Julysiza.

  Kwa mujibu wa Julysiza, elimu inayotolewa kwenye shule zinazomilikiwa na taasisi yao ni bora na imechangia katika uandaaji wa watoto kwa makundi mengi ya kielimu kama vile sekondari na chuo kinachofundisha biashara, elimu na afya.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu wa ngozi,Kadi ya Bima ya Afya,Mafuta maalumu ya kutunza Ngozi na Kofia ya kujikinga na mionzi mikali ya jua,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania(Chawata)mkoa wa Arusha,Said Kazigire.
  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu wa ngozi,Kadi ya Bima ya Afya,Mafuta maalumu ya kutunza Ngozi na Kofia ya kujikinga na mionzi mikali ya jua,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania(Chawata)mkoa wa Arusha,Said Kazigire.
  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu wa kutokuona(Kipofu),Kadi ya Bima ya Afya itakayomwezesha kupata matibabu na wategemezi wake watano,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania(Chawata)Said Kazigire.
  Watu wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Arusha,Ndg Fadhili Nkurlu.

  Mwenyekiti wa Chama cha wenye ulemavu wa Ngozi mkoa wa Arusha,John Kivuyo akizungumza katika mkutano huo.
  Watu wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Arusha,Ndg Fadhili Nkurlu.

  Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu ameitaka halmashauri ya Jiji hilo kutenga maeneo maulumu ya kuwawezesha wafanyabiashara wenye ulemavu kufanya shughuli za kujiingizia kipato badala ya kuwatumia mgambo wa jiji kuwabughudhi.

  Nkurlu ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na watu wenye ulemavu uliofanyika kwa lengo la kutambua changamoto zinazowakabili na namna ya kuzipatia ufumbuzi na kuwakabidhi kadi ya Bima ya Afya zitakazowawezesha kupata huduma za afya bure na wategemezi wao watano kwa mwaka .

  Pia watu wenye ulemavu wa ngozi walipewa simu za mikononi 25 zilizotolewa na kampuni ya Halotel za kuwawezesha kuwasiliana pindi wanapohisi maisha yao yako hatarini,mafuta maalumu ya kulinda ngozi ,Kofia na Filimbi.

  Alisema miundombinu katika nchi zinazoendelea imekua sio rafiki kwa watu wenye ulemavu na kukwamisha jitihada zao za kujikomboa na kuwa serikali itahakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao kama wananchi wengine.

  "Najua zipo asasi zilizoandikishwa kuwasaidia watu wenye ulemavu,lakini sio zote zinatimiza wajibu huo badala yake zinatumia nafasi hiyo kujinufaisha tutazichunguza na kuzifuta kabisa zisiwepo kwenye wilaya hii,"alisema Nkurlu

  Ameitaka halmashauri ya jiji kutumia fedha zinazotengwa kwa makundi maalumu hasa wenye ulemavu ziwafikie walengwa badala ya kutumika kwa malengo mengine na kuagiza jiji linapofanya operesheni za kuwaondoa wanaofanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi kuwatofautisha na wenye ulemavu.

  Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu(Chawata)mkoa wa Arusha(Chawata)Said Kazigire alisema wanakusudia kufanya sensa ya watu wenye ulemavu ili kuwa na takwimu sahihi zitakazowasaidia kuwahudumia vyema.


  0 0

  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni kesho, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016.

  Kutokana na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa 8:00.

  Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. 

  Imetolewa na;
  Eng. Joseph M. Nyamhanga
  Katibu Mkuu (Ujenzi)
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
  18 Aprili, 2016

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiw kuanza Arili 19, 2016.. Watatu kulia Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki Adam Kimbisa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiw kuanza Aprili 19, 2016.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

older | 1 | .... | 823 | 824 | (Page 825) | 826 | 827 | .... | 1897 | newer