Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live

UKARABATI WA BARABARA MAKETE NJOMBE SEHEMU ILIYOHARIBIWA NA MVUA

$
0
0

Katapila likiwa eneo lililoharibiwa na maji ya mvua kwenye kipande cha lami barabara kuu ya Makete-Njombe katika kijiji cha Usungilo wilayani Makete tayari kabisa kurekebisha eneo hilo
 Ukarabati ukiendelea, mapipa yakiashiria hapo ndipo sehemu iliyoathiriwa na mvua 
 Huu udongo unaouona haukuwepo baada ya mvua kuusomba hali iliyosababisha eneo hili kumegeka na kumomonyoa lami, na huu ni udongo mpya uliojazwa wakati ukarabati ukiendelea
Kina mama wakiangalia eneo hilo linalofanyiwa ukarabati 
Hapa panapoonekana ndipo palipobomolewa na mvua, hivyo kwa hivi sasa pamejazwa kifusi kabla ya kufanyika utaratibu wa kurejesha lami kama palivyokuwa awali 
Wajameni hiki kibao kitasomeka kweli hasa kwa madereva ambao hawajui kama ujenzi unaendelea jirani? maana hii rangi waliyotumia kuandikia duuuuuu!(Picha zote na Edwin Moshi)

MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MAFUNDI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAFUNGWA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Undeshaji na Utumishi wa Wazara ya Afya Juma Rajab,akitoa nasaha kwa mafundi wa vituo vya Afya vya Wilaya zote za Unguja na Pemba mara baada ya kumaliza mafunzo yakuwajengea uwezo mafundi hao,yaliotolewa na wakufunzi kutoka Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni.May 10/2013.

Mkurugenzi wa Undeshaji na Utumishi wa Wazara ya Afya Juma Rajab, akimkabidh Cheti Bi Mwanaidi Muh’d, mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku tano yakuwajengea uwezo mafundi hao, huko katika Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni.May 10/2013. (PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO-ZANZIBAR) . 

namna ulanzi unavyotenezwa,ni moja ya bidhaa inayotegemewa nyanda za juu kusini.

$
0
0

Ulanzi ukiandaliwa 
Miti inayotengeneza pombe aina ya ulanzi ikiwa imestawi mashambani wilayani Makete 
Mingine tayari imeshavunwa 
Hii ndiyo michache iliyobakia baada ya kuvuna ulanzi
Hapa ulanzi ukipelekwa mjini tayari kabisa kuwafikia watumiaji.Ulanzi ni moja ya bidhaa inayotegemewa sana na wananchi wengi wa mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo Njombe kwa ajili ya kuwapatia kipato(PICHA ZOTE NA EDWIN MOSHI).

BALOZI WA FALME ZA KIARABU NCHINI TANZANIA, ATEMBELEA WIZARA MBALIMBALI ZA SEREKALI YA ZANZIBAR

$
0
0

Waziri wa Afya Juma Duni Haji, akizungumza na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Nchini Tanzania Abdulla Ibrahim AL-Suwaidi, alipofika Ofisini kwake kwalengo la kutaka kuisaidia vifaa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.(PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO-ZANZIBAR) . 

kazi ni kwako.

$
0
0
Katika pitapita zangu nimekutana na hii kali, hapa ni kijiji cha Maliwa wilayani makete ambapo nimekutana na kali hii, banda kwa ajili ya huduma za Mpesa halipo lakini kuna bango nzuri la M-Pesa likitangaza huduma hiyo, mtoto huyu anakaa hapa akitokea mteja, anakwenda kuwaita wahusika na huduma inaendelea, Vodacom kazi ni kwako(Picha na Edwin Moshi)

LORI LA MAFUTA LAPATA AJALI NJE KIDOGO YA MJI WA ARUSHA,WANANCHI WAJIZOLEA PASI KUJALI SUALA LA AFYA

$
0
0



WAKAZI WA KIJIJI CHA KING'ORI NJE KIDOGO YA MJI WA ARUSHA WALIVYOKUWA WAKIGOMBANIA MAFUTA YA YA KUPIKIA MARA BAADA YA GARI AINA YA LORI KUANGUKA.PICHA KWA HISANI YA www.mkwinda.blogspot.com


BAADHI YA WATU WAKIWA NA MADUMU PAMOJA NA NDOO WAKIPAMBANA KILA MMOJA KUPATA MAFUTA KUFUATIA AJALI  HIYO YA LORI
PICHANI JUU NA CHINI LINAONEKANA LORI LILILOANGUKA KAMA LIONEKANAVYO PICHANI.


UKIONA MWENZAKO AMECHUKUA KIJITI USILALAMIKE KWA MEDIA,JIPANGE WAKATI WAKO UMEPITA-MRISHO MPOTO NDANI YA TWENZETU DODOMA.

waziri mkuu pinda apokea matembezi ya mshikamano ya kupapambana na uwizi wa kazi za sanaa mjini dodoma leo.

$
0
0

Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa TWENZETU  kwa minajili ya kuielimisha jamii  kuwa na tabia ya kupenda vya kwao na  kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA kujikwamua kimaisha.
Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniii (wote waliosimama nyuma),mara baada ya kuzungumza nao kuhusiana na mambo mbalimbali juu ya sanaa ya Tanzania na namna ya kupambana na maharamia wa kazi zao,ambapo pia redio ya Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa Twenzetu kwa minajili ya kueilmisha jamii ya kupenda vya kwao kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA . 
Waziri Mkuu Pinda akizungumza mbele ya  baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wadau wengine wa sanaa waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.

Mh.Pinda aliishukuru kampuni ya Clouds Media Group kwa kazi nzuri walioianzisha ya kuwasaidia vijana kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwaamsha na kuwafungua macho na kuwaelimisha namna ya kuziona fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha,aliongeza  kuwa kupitia ujumbe huo wa MADE IN TANZANIA kinachohitajika sasa ni kupanga ratiba nzuri ya kuliendeleza zoezi hilo ikiwemo pia kwa kuzishirikisha taasisi nyingine zikiwemo za serikali katika kuhakikisha jambo hilo linaendelea.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akiwakaribisha watu wote waliofika kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda.
Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali mapema leo kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 
Sehemu ya umati wa watu ukiwa kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe katika nafasi ya kujikwamua kimaisha,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 
 Baadhi ya Wasanii wa Filamu hapa nchini Wema Sepetu sambamba na shosti yake Kajala walikuwa ni miongoni mwa wasaani waliounga mkono matembezi hayo ya mshikamano yaliyokuwa yametawaliwa pia na mabango kadhaa yaliyobeba jumbe mbalimbali za kupinga wizi wa kazi sanaa.


 Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini . 
 Baadhi ya magari yakiwa yamesimama yakipisha matembezi ya mshikamano yaliyokuwa yakielekea kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana.
 Baadhi ya Watangazaji wa clouds FM,sambamba na wasanii wa muziki wa kizazi kipya/tasnia ya filamu na wadau wengine wa sanaa wakiwa wamejumuika kwa pamoja kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Mh Waziri Mkuu Pinda.
Mmoja wa Watangazaji wa kipindi cha Jahazi,Wasi Wasi Mwambulambo akiserebuka na Mh.Rehema Nchimbi.
 Baada ya muda kulipita burudani ya pamoja ya mchanganyiko kama hivi safi kabisa kabla ya Waziri Mkuu kuwasili viwanjani hapo.
 Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi,kulia mtangazaji wa Clouds FM Mbwiga Mbwiguke na Shaffih Dauda (shoto) wakitwibiwirika kwa pamoja mapema leo mchana mjini Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere skwea.
 Mbunge wa Jimbo la Kinondoni na Mdau mkubwa wa sanaa hapa nchini,Mh.Idd Azan akiunga mkono harakati za kupapambana na maharamia wa kazi za sanaa hapa nchini
 Gari ya Waziri Mkuu Pinda ikiwasili
 Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari,Vijana, michezo na Utamaduni,Mh.Amos Makala habari,Michezo mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana mjini Dodoma. 
 Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu Pinda akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,mjini Dodoma mapema leo mchana huku akiwapungia mkono baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wananchi wengine kwa ujumla waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akimkaribisha. .
 Mh.Waziri Mkuu Pinda akizungumza jambo na Muimbaji mahiri wa mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto.Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Chamwino,Mh.Fatma Ally akishuhudia mazungumzo hayo.

IN LOVING MEMORY OF THE LATE GEORGE B. KILAVE

$
0
0
There Is A Wonderful Legacy 
Of Which We Wish To Tell
About A Wonderful Man

That We Loved So Well
His Strength Lives Within Us
And Grows Stronger Each Day

His Honor Still Lingers
Though His Life Has Slipped Away
We Miss The Sound Of His Laughter
And His Stern Lectures Too!

We Miss Hearing Him Say,

“Keep The Faith! Do Not Forget To Pray!”

He Fought A Good Battle
He Finished The Race But Gave Up The Worldly 

To Rest In The Arms Of Jesus
What A Beautiful Sight…

He Is Now Looking at Jesus Face to Face

What A Delight……….



Three years Later, You are Still Fondly remembered by

Your wife Dorothy, your son and best friend ever Samwel Malcolm and your daughter Matroner,Your Relatives, your Friends and thousands of people whose lives you touched!

I have fought a good fight, I have finished my course, I have kept the faith. 
11 Tim.4:7

Waziri Mkuu pinda alipozungumza akiunga mkono harakati za kupambana na wizi wa kazi za sanaa mjini dodoma.

$
0
0
Waziri Mkuu Pinda akizungumza kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,mara baada ya kupokea matembezi ya mshikamano yaliyowajumuisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na wadau wengine wa sanaaa mbalimbali bila kuwasahau Clouds FM ambao ndio walioratibu shughuli nzima ya matembezi hayo yakiwa na lengo la kuiomba serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na ikibidi kuziongeza katika wigo mpana ili kukwamua maisha ya wasanii na vijana walioko katika nyanja mbalimbali,kama vile haitoshi matembezi hayo yalikuwa na ujumbe wa kupinga uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.Aidha Clouds FM pia walizindua msimu wao mpya uliopewa jina la MADE  IN TANZANIA ndani yake kukiwa na kampeni kubwa ya TWENZETU katika harakati ya kuihamasisha jamii kujivunia vya kwao.

Wafanyakazi wa Airtel Tanzania watunukiwa tunzo baada ya kuhitimu mafunzo ya Mauzo

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Airtel Bw Stratory Mushi (katikati) akiwa katika picha ya pomoja na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania. 
 Mkurugezi wa mauzo na masoko  wa Airtel bw  Mustafa Kapasi (kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo  Afisa mauzo kanda ya dar es salaam  Airtel  John Gondwe  baada ya kuhitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji ya muda wa miaka miwili yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU). Wafanyakazi 56 kutoka katika mikoa mbalimbali walihitimu mafunzo hayo, akishuhudia katikati ni Mkurugenzi Rasilimali watu Patrick Foya akifatiwa na Melvin Joel Meneja wa Centum Learning Makao Makuu
 wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakikata keki kwa pamoja wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania

Mkurugenzi wa Airtel Bw Sunil Colaso akiongea na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.
=========  ========  ======
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania watunukiwa tunzo baada ya kuhitimu mafunzo ya Mauzo
  • Mafunzo yalitolewa na chuo cha masoko cha  Airtel Centum Sales University (ACSU)
·         Wafanyakazi 56 wahitimu mafunzo hayo
Airtel Tanzania, mtandao wa mawasiliano wenye gharama nafuu nchini leo imewakabidhi shahada wafanyakazi wake 56 waliohitimu mafunzo ya mauzo ya muda wa miaka miwili yanayoendesha na Airtel Centum Sales University (ACSU).

chuo cha masoko cha Airtel Centum Sales University kilizinduliwa Tanzania mwaka 2011, lengo la kuwaanda na kuwawezesha wafanyakazi wa Mauzo na usambazaji kupata ujuzi bora, elimu ya mauzo na usambazaji  utakaowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wauzaji wa rejareja wanaongeza ufanisi na kuongeza tija .

Akiongea katika halfa ya mahafali ya wahitimu hao yaliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Moroco,Mkurugenzi wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso alisema,” Programu hii ya Airtel Sales Academy inatolewa na Taasisi ya ukufunzi ijulikanayo kama Centum learning inayotoa mafunzo ya mauzo na usambazaji na kuwawezesha wafanyakazi wa Airtel kuwa bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla. tunawapongeza wafanyakazi wetu kwa kazi nzuri waliofanya katika kipindi chote cha mafunzo yao na  tunaamini kwamba  mafunzo waliyopata  ya masoko na usambazaji yataleta mabadiliko na kuwapa wateja wetu huduma bora na zenye viwango vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.

Airtel tunaamini mikakati na malengo tuliojiwekea haitakuwa na tija bila kuwa na wafanyakazi wenye vipaji, wenye hari na nguvu watakao tumika kama vyombo muhimu kufanya ndoto na mipango yetu kuwa ya hakika aliongeza Colaso.

Airtel tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kitamaduni , kasi ya kazi na kibiashara.  kampuni imewekeza katika kukuza uwezo wa wafanyakazi na kutoa nafasi ya kukuza fani zao ndani ya kampuni. Mafunzo ya ujuzi daima imekuwa ni mikakati yetu inayoendana sambamba na ujuzi unaohitajika kimataifa.

Mafunzo ya ACSU yalianzishwa India mwaka 2009 yakiwa na lengo la kuongeza ujuzi, maarifa na ufanisi  endelevu kwa  wafanyaka  wa mauzo. Mpaka sasa zaidi ya wafanyakazi 80,000 wa vitengo mbalimbali wamepata mafunzo hayo.
Taasis ya Centum Learning inamilikiwa na Bharti na inatoa mafunzo yanayosaidia kuongeza ujuzi na kuleta ufanisi katika nchi  17 zikiwemo Africa, India, Bangladesh and Sri-Lanka.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Centum Learning tembelea www.centumlearning.com


MAPOKEZI YA DK. KAFUMU YAITEKA IGUNGA

$
0
0
 Wananchi wakimbeba Mbunge wa Igunga mkoani Tabora, Dk. Dalally Peter Kafumu kumpeleka jukwaani, wakati wa mkutano wa mapokezi yake, jimboni humo uliofanyika leo kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga. Dk. Kafumu amerejeshewe ubunge na mahakama kuu baada ya kukata rufani kufuatia awali kuvuliwa pia na mahakama baada ya Chadema kwenda mahakamani aliposhinda katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika mwaka juzi.

 Dk. Kafumu akiwa na Nape wakati wa mapokezi hayo
 Waendesha bajaji wakimsubiri Dk. Kafumu nje ya mji wa Igunga wakati walipowasili leo
 Msafara wa Dk. Kafumu, ukiongozwa na pikipiki na bajaji baada ya kuwasili mjini Igunga leo.

USAJILI WA TUZO ZA MUZIKI ZA RFI WAANZA, WANAMUZIKI TANZANIA CHANGAMKIENI FURSA HII

$
0
0

Kwa usajili wa tuzo za muziki za rfi ambazo hufanyika kila mwaka na kuwashirikisha wanamuziki mbalimbali katika bara la Afrika bonyeza hapo chini rfi music award registration

COME BACK YA MWANAHARAKATI NOVA KAMBOTA....NINI USHAURI WAKO?

$
0
0

Baada ya kuwa nje ya tasnia ya kublog kwa takribani miaka mitatu sasa kutokana na mizunguko ya dunia hatimaye najiandaa kurudi rasmi katika ulimwengu wa kublog ndani ya kipindi cha mwezi miezi miwili kutoka sasa.

Ikumbukwe kuwa nimeanza kublog tangu 15 Agosti mwaka 2008, hata hivyo kuna siri leo nitawamegea ndugu zangu watanzania;

-Mimi nimejaaliwa kipaji cha kuchambua maswala ya siasa
-Pia nachambua maswala ya soka
-pia nachambua maswala ya kihistoria
-Mimi pia ni mtunzi wa Riwaya
-Ni mtunzi wa mashairi
-Mwandishi wa vitabu vya kihistoria

Sasa nataka kuanzisha blog mpya ya kisasa? je nijikite kwenye nini kati ya hayo niliyoeleza hapo juu? je blog hiyo iweje? TAFADHALI NAOMBA TOA MAONI NA USHAURI WAKO KWANGU, NAHESHIMU MAWAZO YENU MAANA BILA NYINYI NISINGEKUWA HUYU NOVA KAMBOTA MWANAHARAKATI. Nitahakikisha nakusanya maoni yote kutoka blog zote na kuyafanyia kazi, Asante sana! 

ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI SANA...

Ni mimi Mwanaharakati Nova Kambota

CRDB YAFANYA MKUTANO MKUU WA 18 WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akitoa mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo uliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha, mwishoni mwa wiki. 
 Mtangazaji Mkongwe, SalimMbonde (kulia) akifuatilia Mkutano Mkuu wa  18 wa Wanahisa wa CRDB uliofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
 Wanahisa wa mkutano huo.
 Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha.
 Mwanahisa akitoa mada.
 Mwenyekiti wa Mkutano huo akisoma majina ya wajumbe waliochaguliwa kuingia katika Bodi ya Wakurugenzi.
 Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kushoto) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo pamoja na mmoja wa wanahisa (wa pili kulia). 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyadhiyay akiwa na mke wake pamoja na mjumbe wa bodi ya CRDB, Kai. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.

 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
 Wanahisa.
Charles Itembe akitoa mada kuhusu fursa za uwekezaji na upatikanaji mitaji katika masoko ya fedha wakati wa semina ya wanahisa wa benki ya CRDB iliyofanyika mjini Arusha.


Mmoja wa wajumbe wa mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa CRDB akiwa katika maandalizia ya kuingia katika ukumbi wa  mikutano wa AICC jijini Arusha.

shoo hii kuitikisa mbagala na vitongoji vyake.

$
0
0

WASANII wa Muziki wa Kizazi kipya Naseeb Abdul  'Diamond Platinam' na Ney  wa mitego wanatarajia kupanda jukwaa moja kumtafuta nani mkali katika uzinduzi wa video ya Muziki gani itakayozinduliwa Mei 18 mwaka huu katika ukumbi wa Dar LIVE mbagala, Dar ers Salaam.

Uzinduzi wa Video hiyo ambao umeandaliwa na Kampuni ya Yuneda Entertainment inayohusika na masuala ya burudani itawapambanisha wasanii hao ambao kutatafutwa nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo nyimbo hiyo ya muziki gani inamahadhi ya kubishana kati ya miziki hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa kutambulisha uzinduzi huo, Mratibu wa onesho hilo Kahabi Mwendesha alisema uzinduzi huo utasindikizwa na wasanii wa Hip Hop na Bongo Fleva na kuwataka mashabiki wa fike kwa wingi ili kushuhudia wababe hao.

"Onesho hili litakuwa ni la kumtafuta nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo kupitia uzinduzi wa video hii utadhihirisha nani mkali kati ya muziki wa bongo fleva na hip hop,"alisema Mwendesha.

Alisema mara baada ya video hiyo kuzinduliwa Mei 18 Dar LIVE uzinduzi huo utahahamia katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza, na baadaye Arusha na kuwataka mashabiki wa mikoa hiyo kukaa tayari kwa ajili ya burudani hiyo.

Alisema viingilio katika onesho hilo vitakuwa ni sh. 10,000 huku akisisitiza ulinzi kuimarishwa ambapo pia alisema kwa mashabiki wa burudani ambao hawatakuwa na viingilio kwa ajili ya mechi ya Simba na Yanga wafike katika ukumbi huo kwa kuwa mechi ya watani hao wa jadi itaoneshwa LIVE kupitia televisheni kubwa zilizipo ukumbini hapo.

gazeti lako la dira liko sokoni sasa

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MCHUNGAJI DKT. MATHEW BYAMUNGU NA MKEWE IKULU DAR LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mchungaji Dkt. Mathew Byamungu, wakati akimkaribisha Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 13, 2013 alipofika kwa mazungumzo akiwa ameongozana na mkewe, Je-Ynung. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mchungaji Dkt. Mathew Byamungu na mkewe, Bi. Je-Ynung Byamungu, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu leo Mei 13, 2013 kwa mazungumzo.

NEEC KWA KUSHIRIKIANA NA KITUO CHA UDEC KUWAPATIA MAFUNZO WANAFUNZI WALIOHITIMU VYUO VIKUU NA KUKOSA KAZI STADI ZA KUJIAJIRI.

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Annacleti Kashuliza akifungua mafunzo ya wiki 3 ya Vijana 40 waliohitimu masomo ya elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana kazi leo jijini Dar es salaam .Mafunzo hayo kwa vijana yanalenga  kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi ya maendeleo na kuwafanya waweze kuajiri vijana wengine pamoja na kusaidiwa kupata fedha benki kwa ajili ya kuanzisha biashara kutokana na michanganuo watakayoiwasilisha.


Sehemu ya Vijana 40 waliohitimu katika chuo Kikuu cha Dar es salaam miaka ya hivi karibuni ambao hawana ajira wakiwa katika mafunzo ya wiki 3 ya kuwajengea uwezo wa kuweza kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi itakayowajengea uwezo wa  kuajiri vijana wengine. Mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Biashara yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) na Kituo cha  masuala ya Biashara na uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDEC) ikiwa ni moja ya mkakati wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wa vyuo vikuu nchini. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Exim Bank Tanzania opens facility to facilitate Tanzania-China Trade

$
0
0

Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant

EXIM Bank, Tanzania’s sixth largest bank by total assets and deposits

 has opened a Tanzania-China Trade Window that will help in
facilitating trade operations between the two countries.



A statement issued by the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony
Grant yesterday said the new window will offer clients a more
convenient way to make import and export bill settlements in Chinese
Yuan Renminbi (CNY/RMB).



Grant noted that his bank has already entered into partnership with
Hongkong based bank, HSBC adding that the new facility will offer
better exchange rates to traders between the two countries.



“The setup of Tanzania- China Trade Window is part of our strategy to
support the fast-growing banking needs of Tanzania and Chinese
traders. With this new window, traders from Tanzania and China will
have a convenient banking platform to send and receive cash.



Grant said his bank came up with the idea of opening the Tanzania-China Trade Window following an increase in trade volume between Tanzania and China in the recent years. “We believe the Exim Bank- China Trade window will be a catalyst in doubling trade between the two countries in the next few years to 
come,” he said.



 “This new window will offer better negotiation opportunities and
transparent pricing deals to Tanzanians with suppliers or buyers in
China and other trade related services,” he said.



According to statistics from the Bank of Tanzania (BoT), Tanzania’s
exports to China increased from 101bn/- in 2005 to 908bn/- in 2010, a
nine-fold upswing, while imports from Beijing rose from 245bn/- to
1.213tr/-, went up five times over the same period.



A survey released by HSBC recently however noted that by 2015,
one-third of the China’s international business transactions will be
made in the renminbi. The bank adds that 30 percent of the China’s
trade, equal to about $2 trillion, will be transacted in the renminbi.
More than 10 000 financial institutions globally are currently doing
business in renminbi, up from 900 in June 2011, and offshore
investments in the currency, almost nonexistent three years ago, now
tops $143-billion.
Viewing all 46327 articles
Browse latest View live




Latest Images