Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 817 | 818 | (Page 819) | 820 | 821 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira) January Makamba akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge la Finland. Wabunge hao wa Kamati ya Fedha wamefanya mazungumzo na Waziri Makamba hii leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Finland Nchini Tanzania Bw  Mart Akhtsary (kushoto) akitambulisha ujumbe wake.

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa akizungumza wakati wa semina hiyo.

  Fao jipya la Wote Scheme ambalo ni mfumo wa hiari kwa wanachama ulioanzishwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF utasaidia kuwapa fursa watanzania waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kukidhi mahitaji na kutambua mchango na ushiriki wa sekta hizo katika kukuza uchumi.

  Fao hilo pia linatoa fursa kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi kuwawezesha kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

  Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa alisema hayo juzi wakati semina kwa askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto mkoani Tanga uliokuwa na lengo la kuwapa uelewa juu ya mafao yanayopatikana kupitia mfuko huo.
  Washiriki wa semina hiyo Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa.

  Alisema kupitia fao hilo mwanachama anafaidika na huduma za Afya ikiwemo kupata kadi ya Afya mahali popote kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) mwaka mzima bure.

  Aidha alisema kupitia skimu hiyo mpya ya mfuko huo unachangia na kuwapa uelewa watanzania utamaduni wa kujiwekea akiba ya baadae ili kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha wakati wanapokuwa wakifikia umri wa kustaafu.

  “Lakini pia sisi kama PPF tunarahisisha uchangiaji kupitia mitandao yote ya simu kwani hii imesaidia kuweza kuepusha changamoto mbalimbali ambazo wanaweza wakukumbana nazo wanachama wetu ambao wamejiunga ma Mfuko huu “Alisema.


  Hata hivyo alisema kuwa wanaendelea kutoa mikopo ya elimu na biashara ili kuweza kuwainua wanachama wao kiuchumi sambamba na kujiendeleza kielimu ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha na utandawazi.
  “Fao hili lilianzishwa mwezi wa saba mwaka jana ambapo mwanachama anafaidika na huduma za afya (Kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini - NHIF),mikopo mbalimbali na Fao la Uzeeni(Pensheni) "Alisema Meneja huyo.

  Semina hiyo ililenga kuwapa uelewa wa mambo mbalimbali kuhusu mfuko huo ikiwemo uandikishaji wanachama,mafao yatolewayo na mfuko huo,Wote Scheme (mfumo wa Hiari),Mikopo ya Saccos na Fao la Elimu.
  Picha na Stori kwa Hisani ya blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mhe. Zakia Meghji alipowasili ukumbi wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kuzindua Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika leo April 12, 2016.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika leo April 12, 2016 katika ukumbi wa Mwalim Nyerere. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wanawake waliohudhuria Kongamano la Wanawake katika Uongozi linalojadili kuendeleza Mazingira kuwezesha kuinua Wanawake ambao bado hawajapata fursa kufikia nafasi za Uongozi. Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi limefanyika leo April 12, 2016 katika ukumbi wa Mwalim Nyerere. 
  (Picha na OMR)

  0 0

  Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imekanusha kodi ya ng’ombe iliyoripotiwa na Umoja wa wafanyabiashara wa Mifugo na Mazao yake wa Wilaya ya Kinondoni.

  Taarifa hii imetolewa na Katibu Mkuu (Mifugo) wa Wizara hiyo Dkt. Mary Mashingo baada ya kuyaona malalamiko ya wafanyabiashara hao kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini. Katika taarifa hiyo wizara imekanusha kuwa kodi ya ng’ombe siyo shilingi 18,500 kama ilivyoripotiwa na wafanyabiashara hao bali ni shilingi 12,000 ambayo inatambulika kisheria.

  “Wizara yetu inapenda kutoa ufafanuzi juu ya kodi inayotozwa katika machinjio ya Kimara kama ifuatavyo: ushuru wa soko shilingi 5000, ushuru wa kusafirisha mifugo shilingi 1500, ushuru wa ukaguzi wa wanyama shilingi 2500 pamoja na gharama za machinjio shilingi 3000 kwa kila kichwa cha ng’ombe ambapo jumla yake ni shilingi 12,000”alisema Dkt.Mashingo.

  Aidha,taarifa hiyo imeelezea kuhusu kupitisha ng’ombe katika soko la upili la Pugu kabla ya kuwapeleka katika machinjio ya Kimara kuwa ni kwa ajili ya kuwafanyia vipimo vya afya ng’ombe hao kabla ya kuchinjwa pamoja na kulipia tozo ya Serikali.

  Taarifa hiyo pia imefafanua baadhi ya sababu za kufungwa kwa machinjio ya Kimara tangu Aprili 9 mwaka huu zikiwemo za baadhi ya wafanyabiashara kupeleka ng’ombe katika machinjio hayo moja kwa moja bila kupitia Pugu ambalo ni kosa kisheria pamoja na uchafu uliokithiri katika machinjio hayo.

  Katika kufanya juhudi za kupambana na matatizo haya,Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inajipanga kukutana na wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake ili kuwaelimisha zaidi kuhusu Sheria, Kanuni, na Taratibu zinazopaswa kufuatwa katika ufanyaji wa biashara hii.

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  0 0

  Karibuni Lala Land, ulimwengu wa maajabu, ambapo utajifunza na kucheza na Akili! Imba namba! Cheza herufi! Cheka, chora, na jifunze Kiingereza na Akili.

   Akili and Me ni kipindi kipya cha elimu burudani kinachotengenezwa na Ubongo Media, watengenezaji wa Ubongo Kids. Watoto wa miaka mitatu hadi sita watafurahia kuungana na Akili kwenye ulimwengu wake wa maajabu, Lala Land! Watajifunza namba, herufi, kuchora na Kiingereza. Elimika na burudika kupitia “Akili and Me” TBC1 saa 3 asubuhi j1 & j2 pamoja na Ubongo Kids, jumatau - alhamisi saa 8:30 mchana, na ijumaa saa 9 mchana.

  0 0


  1.       : waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wafanyakazi wa Wizara.
     wafanyakazi wa Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi wakimsikiliza Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Maimuna Tarishi akimkaribisha Waziri wa Elimu kuongea na wafanyakazi.
   waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiingia katika ukumbi wa Karimjee kuongea na wafanyakazi wa Wizara.

  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kujiwekea malengo katika utendaji kazi wao ili waweze kutimiza malengo makubwa ya sekta ya elimu.

  Profesa Ndalichako aliyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kutoka Makao Makuu katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee ikiwa ni mara ya kwanza kukutana nao tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi lengo likiwa ni kuwasikiliza lakini pia kujadiliana nao namna bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara hiyo. 

  Waziri Ndalichako aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kujituma, kutoa huduma bora kwa wakati kwa kuwa ni watumishi wa umma na maana ya mtumishi wa umma ni kuwa na wajibu wa kuwatumikia wananchi ili wapate haki yao kwa wakati kwani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyoptea. 

  Amewataka watumishi hao kuipende kazi yao, kwa maana mtumishi anayependa kazi yake uifahamu kwa undani wake na inakuwa rahisi kuwatyumika wananchi bila ya kuwa na wasiwasi na kujiamini zaidi .“kila mfanyakazi ni lazima kujivika joho la Wizara kwa maana ya kuijua Wizara vizuri, misingi yake, dira pamoja na sera zinazotuongoza katika utendaji kazi wetu ili tuweze kufikia malengo ya kuinua ubora wa elimu” alisisitza Ndalichako. 

  Akizungumza kwa niaba ya watumishi Omary Mkali alimshukuru Waziri kwa kukutana na watumishi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri ili kuweze kufikia lengo kwa pamoja la kuinua ubora wa Elimu nchini.   0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza kuhusiana na kuaza operesheni ya kuwaondoa ombaomba waliokandokando ya barabara, jijini Dar es Salaam leo. 
  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa agizo la kuwaondo watu wanao ombaomba kandokando ya barabara jijini Dar es Salaam.

    Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa katika kuweka jiji safi itaanza na operesheni ya kuondoa ombaomba wanaokaa kandokando ya barabara kwa ajili ya kuomba.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ombaomba wanakuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.

  Makonda amesema operesheni hiyo inatarajiwa kuanza Aprili 18 mwaka huu ambapo kazi hiyo itafanywa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.

  Amesema watu wanaofanya kazi hiyo waanze kuondoka wenyewe kutokana na mikakati waliopanga jinsi ya kutekeleza operesheni hiyo.

  Makonda amesema operesheni ya kuondoa omba omba ni endelevu kutokana na kuwepo kwa uchafu kwa baadhi yao kulala katika majengo  na kufanya uchafu huo.

  Nae Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa operesheni hiyo watatekeleza kuanzia siku hiyo hivyo waanze kuondoka mara moja.

  Amesema agizo la Mwenyekiti wa ulinzi na usalama la Mkuu wa Mkoa kazi kwa jeshi la polisi ni kutekeleza tu  kutokana na jamii hiyo inatoka katika sehemu zenye mamlaka ambapo kuna utaratibu juu ya kuwakimu watu wenye mahitaji maalum.

  0 0

    kaimu Mtendaji Mkuu Temesa  Mhandisi Manase Ole Kujan (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya ufungaji wa moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura Semboji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na mafundi wa Temesa.
    Kaimu Mtendaji Mkuu Temesa Mhandisi Manase Ole Kujan (katikati) akiangalia moja ya kifaa cha kupimia umeme kinachotumika katika mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
    Mhandisi Amani Mwanga akitoa maelekezo ya namna ya kufunga moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
   Fundi Sanifu kutoka Temesa Mganza Juma (Katikati)akiwa makini kufunga moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
  Baadhi ya wahandisi kutoka Temesa wakiwa katika harakati za kuchuna na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.(Picha Zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO).

  Na  Raymond Mushumbusi MAELEZO.


  Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa ili kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.


  Akifungua mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme wa kawaida haujafika.


  “Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme nchini.” Alisema Mhandisi Manase.


  Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mafunzo,Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof Cathbert Kimambo amesema kwa kushirikiana na Temesa wameamua kutoa mafunzo kwa wataalamu hao juu ya teknolojia ya nishati ya umeme wa jua ili kuwasaidia kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwa kuwa na utalaamu na uwezo wa kufanya kazi kulingana na mabadiliko yaliyopo.  Mmoja wa wahandisi Kutoka Temesa Bi Sara Moses ametoa wito kwa Wahandisi wengine kuwa na utaratibu wa kujifunza na kuongeza utaalamu ili kuwezesha kuendana na mabadiliko Sayansi na Teknolojia katika kuleta ufanisi katika kazi zao.

  0 0

  Balozi Haule (Katikati) akimpongeza Mwambata wa Kijeshi Ubalozini Nairobi, Luteni Kanali Fabian Machemba. Kulia ni Kanali Msola.
   Balozi Haule akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha ziara ya Maafisa wa JWTZ.

  Maafisa na wanafunzi 29 kutoka Chuo cha Kamandi na Unadhimu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Duluti, Arusha, wamemaliza ziara ya mafunzo ya wiki moja nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita, iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF).

  Kundi hilo lililoongozwa na Naibu Kamanda na Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha JWTZ, Kanali Celestine Msola, lilitembelea taasisi mbalimbali za serikali na Jeshi la Kenya pamoja na taasisi binafsi. Mafunzo yao yalihusu masuala ya Jamii na Uchumi, Utawala bora, Mfumo wa Kisiasa, Ulinzi na Usalama, na Maendeleo ya Teknolojia ya Kivita.

  Akizungumza katika hafla fupi mwishoni mwa ziara hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, alimshukuru Mkuu wa Jeshi la Kenya, Jenerali Samson Mwathethe, na watendaji wake, kwa ukarimu waliowafanyia Maafisa wa JWTZ. 

  Aliwapongeza Maafisa hao kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoonyesha muda wote, akisema wameacha sifa nzuri ya JWTZ na Tanzania kwa ujumla.
  Mwakilishi wa KDF, ambaye pia ni Kamanda wa Chuo cha Teknolojia cha Ulinzi, Kanali Oscar Muleyi, alisema Maafisa wa Jeshi la Kenya wameshafanya ziara ya mafunzo nchini Tanzania na walikarimiwa vizuri sana.

  0 0

   Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christipher Ole Sendeka akisalimiana na Katibu wa CCM wilaya ya Babati mjini, Benard Ghati alipowasili Ofisi ya CCM wilaya ya Babati mkoani Manyara akiwa katika ziara ya kikazi
  Viongozi wa CCM wilaya ya Babati mkoani Manyara wakiwa tayari kumpokea Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka alipowasili Ofisi ya CCM wilaya ya Babati
  Msemaji wa CCM, Mjmbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM wilaya ya Babati mkoani Manyara
  Katibu Mwenezi wilaya ya Babati mjini Reginard Sanga akizungumza maneno ya utangulizi kumkaribisha Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka alipofika katika Ofisi ya Wilaya hiyo
  Katibu wa CCM, Babati Mjini Bernard Ghaty akizungumza, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alipofika katika Ofisi ya CCM wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara
  Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali akimkariisha kuzungumza Msemaji wa CCM, Ole  Sendeka.

  Mjumbe wa NEC Kigoma, Kilumbe N'genda akizungumza kabla ya Msemaji wa CCM aliyefuatana naye, Ole Sendeka hajazungumza.
  Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti wa CCM Wilaya ya Babati mkoani Manyara
  Msemaji wa CCM Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa CCM wilaya ya Babati mjini
  Msafara wa Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka  ukienda Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara baada ya kuzungumza na Sekretarieti ya CCM wilaya ya Babati Mjini
  Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akikagua jengo la Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, lililoungua moto hivi karibuni, alipofika kwenye Ofisi hiyo kuzungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya za Babati Mjini na Vijijini mkoani humo
  Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiingia ukumbi wa Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara kuzungmza na wajube wa Hamashauri Kuu ya CCM katika wilaya za Babati mjini na Vijijini mkoani Manyara
  Sendeka baada ya kuwasili ukumbini
  Meza kuu na wajumbe wakiwa ukumbini
  Katibu wa CCM wilaya ya Hanang, Vyohoroka, akiwa na wajumbe wenzake kwenye kikao hicho. Hanag walialikwa kwa nafasi ya wajumbe wa Sekretarieti wa wilaya hiyo.
  Wajumbe wakiwa ukumbini
  Meza kuu wakiwa ukumbini
  Meza kuu na wajumbe wakiwa ukumbini
  Katibu Mwenezi wialaya ya Babati mjini Reginard Sanga  akizungumza katika kikao hicho.
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Babati Vijijini Abdallah Soki akizungumza na kikao hicho
  Katibu wa CCM mkoa wa Manyara Ndengaso Ndikubali akizungumza kwenye kikao hcho

  Msemaji wa CCM Ole Sendeka akizungumza  kwenye kikao hich
  Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kweye viwanja vya Ofisi ya CCM tawi la mji pya, Babati mjini koai Manyara
  Wanachi wakimshangiia Msemji Mkuu wa CCM Ole Sendeka
  Ole Sendeka akimpokea mwanachama mpya aliyehamia CCM kutoka Chadema
  Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Olee Sendeka akiwatambulisha wagombea wa Uchaguzi mdogo katika kata ya Mji Mpya  Wilayani Babati Mjini mkoani Manyara wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya CCM Tawi la Mji Mpya wilayani humi.  Wanaonadiwa kutoka kushoto ni Mgombea wa Uenyekiti wa mtaa wa Mji Mpya wa Seif Marwa,  Kuruthum Hassan (Ujumbe  Viti maalum Mji Mpya), Abubakar Gwandu (Ujumbe mtaa wa Komoto),  na Ramadhani Salum mtaa wa Bagala Ziwani.


  Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akifunguka hatua kwa hatua wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika ofisi ya CCM tawi la Mji Mpya wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara
  Mjumbe wa NEC mkoani Kigoma na Ofisa katika Idara ya Itkadi na Uenezi Makao Makuu ya CCM, Kilumbe Ng'enda akihutubia katika mkutano huo
  Mwenyekiti wa CCM, tawi la mji Mpya akifunga kikao baada ya Ole Sendeka kuzungumza
  Ole Sendeka akikabidhi mchango wake wa sh. 100,000 kwa ajili ya CCM tawi la Mji Mpya
  Msemaji wa CCM Chrstopher Ole Sendeka akimsaimia mwanafunzi wa shule ya Msingi Masaki wiayani Babati mkoani Manyara, Ahmedi Rashud baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika Ofisi ya CCM Tawi la Mji Mpy Babati mkoani Manyara
  Msemaji wa CCM, Christpher Ole Sendeka akiwaaga wananchi baada ya mkutano wa hadhara uliofanyka Ofisi ya CCM, uiofanyika Ofisi ya CCM tawi la Mji Mpya, wilaya ya Babati mjini mkoani Manyara. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wakati wa kukabidhi Ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.
  Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wakati wa kukabidhi Ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) (katikati) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa haji Ussi (Gavu) akitoa nasaha zake kwa Wafanyakazi wakati wa makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Waziri ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini leo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali,
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini (katikati) wakiombewa dua baada ya makabidhiano ya Ofisi katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini (katikati) wakipeana na Makatibu (kulia) Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum na Katibu wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Haroub Shaibu Mussa kwa kuwatakia Kheri na mafanikio baada ya makabidhiano ya Ofisi katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) akikabidhiana Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi IkuluMjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawazi wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.

  0 0

  Mtoto Suzana John Badi akiwalisha keki watoto wenzake, wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwa babu yake Mzee Mahiga eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. 
  Mtoto Suzana John Badi akilishwa keki na mama yake Elizabeth, wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwa babu yake Mzee Mahiga eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. 
  Mtoto Suzana John Badi akilishwa keki na Baba yake John Badi, wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwa babu yake Mzee Mahiga eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. 
  Mama mkubwa wa Suzy, Rose Mahiga akikata keki wakati wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwao eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. Birthday hiyo ilienda sambamba na ya Suzy. 
  Mama mkubwa wa Suzy, Rose Mahiga akilishwa keki na Suzana Badi, wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwao eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. Birthday hiyo ilienda sambamba na ya Suzy. 
   
  Mtoto Suzana John Badi akikata keki wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwa babu yake Mzee Mahiga eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG 
   
  Mtoto Suzana John Badi akimlisha keki mama yake Elizabeth, wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwa babu yake Mzee Mahiga eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. 
   
  Mtoto Suzana John Badi akimlisha keki Baba yake John Badi, wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwa babu yake Mzee Mahiga eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. 
   
  Mtoto Suzana John Badi akimlisha keki Mama yake mkubwa Rose huku mama zake wakubwa Josephine na Stela wakishuhudia, wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, iliyofanyika nyumbani kwa babu yake Mzee Mahiga eneo la Msasani jijini Dar es Salaam wiki endi. 

  0 0

  Msanii wa Sanaa ya Sarakasi akiendesha baiskeli ya tairi moja katika tamasha la wasanii wa filamu  (TDFA) lilifanyika jijini Arusha jana katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

  Na Woinde Shizza,Arusha.


  Wasanii wa Filamu nchini kote wametakiwa kutumia mandhari za asili zilizoko katika maeneo ya  hifadhi za taifa kwenye shughuli zao za kurekodi filamu badala ya kutumia majengo ya kifahari ili kutangaza utalii kwa kupitia kazi zao.  Hayo yameelezwa na Meneja Mawasiliano wa  Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA ,Pascal Shelutete wakati akizungumza katika Tamasha la Chama Wasanii wa filamu  jijini Arusha (TDFA) lililofanyika  katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid .  Shelutete amesema kuwa Tanapa itatoa ushirikiano kwa wasanii watakaoonyesha nia ya kurekodi filamu zao katika maeneo ya hifadhi ambayo ni salama nay a kuvutia yenye maparomoko ya maji na mandhari za kuvutia ambazo zitasaidia kuhamasisha utalii ambao kwa sasa unaongoza kuchangia pato la taifa.  Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii hao Fredrick Kefas amewataka wasanii kutumia taaluma yao katika kuhimiza utalii wa ndani utakaoliingizia taifa pato kubwa na kuinua uchumi wan chi hivyo kuondokana na utegemezi.  Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifamba amewataka Wasanii kutumia vizuri fursa ya maonyesho ya kimataifa ya filamu yanayojulikana kama  Tanzanite  International Film Festival yatakayojumuisha wasanii mahiri wa filamu kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani,Asia ,Australia .  Alisema Tamasha la Wasanii wa  Filamu jijini Arusha lilipambwa na michezo mbali mbali ikiwemo timu ya mpira wa miguu ya wasanii wa Kilimanjaro na Wasanii wa Arusha,timu za mpira wa miguu za mkoani Arusha  pamoja na mchezo wa netiboli,Michuano bado inaendelea ambapo mshindi wa kwanza atapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Manyara na Ngorongoro.


  0 0

  2
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Misitu wa Serikali ya Czech Republic Bw. Dusan Benza akizungumza katika kongamano la wafanyabiashara wa nchi hiyo na watanzania lililofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

  Mawaziri wawili Kilimo na Viwanda wa Jamhuri ya Jamhuri ya Czech wakiongozana na wafanyabiashara zaidi ya thelathini wako nchini kwa ajili ya kutafuta na kujionea fursa za uwekezaji nchini Tanzaniam Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Tanzania Investiment Bank (TIB), Ubalozi wa Szech Republic nchini Kenya na Tanzania House Of Business Company Limited (THB).

  Ujumbe huo metembelea wizara ya Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara na kusaini mikataba ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hapa nchini na nchi ya Szech Republic ili kuunganisha masuala ya kibiasha na uwekezaji na kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza katika masuala ya biashara, Teknolojia na Kilimo kwa ujumla.
  4
  Injinia Michal Basovnik wa kampuni ya Impuls akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazotolewa na kampuni yao ambayo ina tawi pia nchini Zambia.

  3
  Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic hapa nchini John Chaggama akizungumza na mmoja wa viongozi wa ujumbe huo huku Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa Czech akisikiliz kwa makini.

  0 0

  Afisa Habari wa kampuni ya nyati Spirit Tanzania,Alma Miraji akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya vinywaji vya kiwanda cha Nyati Spirit Tanzania havitakuwa madhara kwa mtumiaji kutokana na kuthibishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) leo jijini Dar es Salaam kuliani Mkuu wa uhakiki wa kiwanda hicho Karan Suchak.
  Wafanyakazi wa kiwanda cha Nyati Spirit Tanzania wakitoa maelekezo juu ya kutotumia watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane kutokana na kuwa na kilevi kama ilivyo vinywaji vingine vikali .
  Wafanyakazi wakiwanda hocho wakipanga vinywaji katika mabosi .(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

  Jumla ya dola milioni 20 za Marekani zimetumika kwa ajili ya kutengeza kiwanda kipya cha vinywaji vikali maarufu kama nyati spirit Tanzania .

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkuu wa uhakiki wa kiwanda hicho Karan Suchak amesema kuwa pamoja na kuingia katika soko la ushindani la vinjwaji vikali pia ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo watanzania zaidi ya mia moja wamepata ajira huku idadi yao ikitarajiwa kuongezeka.

  Kwa upande wa afisa habari wa kampuni hiyo Alma Miraji amesema kuwa vinywaji hivyo havitakuwa na madhara kwa mtumiaji kutokana na kuthibishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) huku wakikusudia kuweka nembo maalumu itayotenganisha na bidhaa nyingine feki.

  Alma ameongeza kuwa vinywaji ambavyo vinapatikana kwa ladha tofauti ikiwemo kahawa matunda havitoruhusiwa kutumiwa na watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kutokana na kuwa na kilevi kama ilivyo vinywaji vingine.

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. 
   Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. 
  Mtoto wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, akitoa taarifa fupi juu ya Mama yake.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa ya Mama yake.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2016 ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa Singida Marehemu Christina  Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.

  Christina Lissu Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07 Aprili, 2016 katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa Matibabu.

  Pamoja na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi wengine waliohudhuria shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe.

  Akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa George Simbachawene amewapa pole familia ya marehemu na kueleza kuwa katika kipindi chake cha ubunge Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai alitoa mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.

  "Mheshimiwa Rais anatoa pole nyingine kwenu familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina" Amesema Mheshimiwa Simbachawene.
  Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Mahambe Mkoani Singida kwa Mazishi.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  12 April, 2016

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Uwekazaji kwa Wafanyabiashara baina ya Tanzania na Oman kuhusu kuangalia fursa za uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi kati ya Nchi mbili hizo  baada ya kufungua Kongamano hilo leo April 13,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regence Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la Uwekazaji kwa Wafanyabiashara baina ya Tanzania na Oman kuhusu kuangalia fursa za uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi kati ya Nchi mbili hizo, Kongamano hilo limefunguliwa leo April 13,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regence Dar es salaam.       
   Washiriki wa Kongamano la Uwekezaji kiuchumi kati ya Tanzania na Oman wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akifungua Kongamano hilo kuhusu kuangalia fursa za uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi baina ya Nchi mbili hizo, Kongamano hilo limefunguliwa leo April 13,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regence Dar es salaam. 
  (Picha na OMR)        

  0 0

  NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi  Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro.

  Dkt. Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa hayo pamoja na Maabara.

  Kihistoria Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua Kikuu.

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.
  Eneo la Utafiti wa magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali hiyo ya KIbong'oto.....Wakitoka katika jengo la Utafiti.
  Msafara ukielekea upande wa wadi za wagonjwa wa TB sugu.
  Moja ya alama zinazoelekeza maeneo ya Hospitali hiyo.


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto ilipo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake 10 Aprili 2016. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo ya kitaalam kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali hiyo ya Kibong'oto.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina namna ya vifaa hivyo vinavyofanya kazi katika upimaji wa kifua kikuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga.
  Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Kibong'oto, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akimuongoza Naibu Waziri wa Afya na watendaji mbalimbali kuelekea katika eneo wanalohudumia wagonjwa wenye Kifua kikuu (TB) sugu.
  Wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kibong'oto na wageni wengine wakielekea katika eneo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya.Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa (katikati) wakielekea katika eneo hilo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina juu ya wagonjwa wa TB sugu waliopo ndani ya wodi (hawapo pichani) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga.
   Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akionyeshaa namna wodi hizo zinavyofanya kazi na jinsi wanavyotoa huduma.
   
  Msafara huo ukirejea katika maeneo mengine wakati wa ukaguzi na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla.

  Pichani wote waliovaa 'mask' maalum ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) hasa kwa upande huo wa wagonjwa maalum wa TB sugu.ambao wapo upande maalum. Hivyo kuvaa kifaa hicho kinasaidia kupunguza hali ya maambukizo wakati wa kufika eneo hilo kama sheria na taratibu zilizowekwa kitaalam na uongozi wa Hospitali hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali hiyo.

  Mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza, wa Hospitali ya Kibong'oto ,Dkt. Stella Mpagama akimkabidhi kitabu chake Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla. (Picha zote na Andrew Chale).

  0 0

    Afisa Mauzo wa Airtel Tanzania, Anatory Lelo (kulia), akitoa elimu kwa wakazi wa Manzese Midizini jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
   Afisa Mauzo na Usambazaji wa Airtel Tanzania, Swaliatu Msuya (wa pili kushoto), akitoa elimu kwa wakazi wa Manzese Midizini jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
   Afisa Kitengo cha Manunuzi wa Airtel Tanzania, Alexander Mboya  (kushoto), na Afisa wa Huduma kwa Wateja, Michael Mnyabebe (kulia), wakitoa elimu kwa wakazi wa Manzese Midizini jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
    Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Frank Filman na Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde, wakitoa elimu kwa wakazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.

   Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (wa pili kulia), na Msaidizi Mtendaji wa Mkurugenzi Mkuu wa Airtel,  Ellen Lupili wakitoa elimu kwa wakazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.

   Afisa wa Huduma kwa Wateja, Michael Mnyabebe (kushoto), akitoa elimu kwa mkazi wa Manzese Midizini jijini Dar es Salaam Aprili 13.2016, kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
   Timu ya Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kuingia sokoni katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam Aprili 13.2016, kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
  Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso akiongea na wateja wa Airtel mkoani Morogoro leo kuhusu huduma mpya ya Jipimie Yatosha yako iliyozinduliwa mwazoni mwa wiki hii. Airtel ilizindua huduma ya Jipimie yatosha yako ili kutoa uhuru kwa watumia wa huduma ya vifurushi vya Airtel Yatosha kutengeneza na kujipia vifurushi kadiri watakavyo. Leo hii wafanyakazi wa Airtel wote wameingia mtaani na kwend kuwaonyesha wateja jinsi watakavyofaidi huduma hiyo.

  Kufatia uzinduzi wa huduma mpya ijulikanayo kama Airtel Jipimie Yatosha Yako kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imewatembelea wateja wake katika maeneo mbalimbali jijini Dar es saalam na kuwafikishia huduma hii mahali pao pa kazi na makazi yao lengo likiwa ni kutoa elimu jinsi gani ya kujitengenezea vifurushi vinavyokidhi mahitaji yao

  Airtel Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi  kinachompatia mteja uhuru wa kujiunga na Airtel, kuchangua na kupanga matumizi yake kwa kuunda kifurushi kitakachokidhi mahitaji yake  kiuchumi na kijamii.
             
  Akiongea kuhusu zoezi hilo Mkurugenzi wa technologia ya habari wa Airtel, Bwana Frank Filman alisema “ tumeona ni vyema kupeleka huduma hii kwa wateja wetu na kuwaelekeza ni jinsi gani sasa wanaweza wajitengenezea vifurushi vya yatosha vinavyokidhi mahitaji yao. Kupitia huduma hii ya Airtel Jipimie Yatosha Yako sasa tumewawezesha  wateja kununua kifurushi cha muda wa maongezi tu, au kuchanganya kifurushi cha muda wa maongezi na MB za intaneti au Muda wa Maongezi na SMS lakini pia bado wanaweza kupata vifurushi vyote yaani muda wa maongezi zaidi, SMS zaidi na MB zaidi
             
  Wakiongea kwa nyakati tofauti mkazi wa Sinza Kijiweni na Fundi rangi bwana Hamisi Chande alisema “ hii ni habari njema kwetu wateja kwamba sasa tunaweza kujitengenezea vifurushi tunavyotaka kwani itatupa fursa ya kupata zaidi, awali nilikuwa naweza kumnunuali ndugu yangu kufurushi na kupata hadi huduma ya intaneti wakati sumu yake haina huduma hii sasa kupigia huduma hii mpya tutafaidika zaidi na pia tutaweza kupanga vyema vifurushi kulingana na matumizi yetu. Nawapongeza sana Airtel kwa kuja na huduma hii ya kisasa na kutuletea elimu huku tuliko.”

  Kujiunga na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja wanatakiwa kupiga  namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.

older | 1 | .... | 817 | 818 | (Page 819) | 820 | 821 | .... | 1903 | newer