Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Profesa Muhongo ataka wawekezaji wazawa kujiamini

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania, Mhandisi Ray Ywa Seng’enge (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akifafanua jambo kwa ujumbe kutoka Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania ofisini kwake mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania uliomtembelea ofisini kwake. 

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka wawekezaji nchini kujiamini na kuwekeza katika sekta za Nishati na Madini ili sekta hizo zitoe mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Profesa Muhongo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania, Mhandisi Ray Ywa Seng’enge aliyeambatana na ujumbe wake. Kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

Profesa Muhongo alisema kuwa umefika wakati wa watanzania wenye uwezo katika uwekezaji hususan katika uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini kujitokeza na kuomba kazi kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kufanya kazi kwa ufanisi kwani uwezo wanao.

Alisema kuwa wawekezaji wengi wamekuwa na mtizamo hasi kuwa makampuni ya kigeni pekee ndiyo yenye uwezo wa kuzalisha na kusambaza umeme vijijini.

“Nataka niwahakikishie kuwa kampuni za kitanzania zina uwezo mkubwa katika uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini, na kama Serikali tupo tayari kuwasaidia ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema Profesa Muhongo.

Aliendelea kusema kuwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ya REA awamu ya pili, zipo kampuni za kitanzania zilizoonesha uwezo katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme vijijini.

Akielekea mikakati ya Serikali ya kuwajengea uwezo wawekezaji wadogo wazawa Profesa Muhongo alieleza kuwa kampuni za kitanzania zimeonekana kujifunza kutokana na ushirikiano kati yao na kampuni za kigeni kwenye miradi ya umeme.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania, Mhandisi Ray Ywa Seng’enge alimpongeza Profesa Muhongo na kuelezea shughuli zinazofanywa na chama hicho.

Akielezea mafanikio ya chama hicho Seng’enge alisema kuwa chama kimekuwa kikitoa huduma Serikalini na makampuni binafsi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo yanayohusiana na masuala ya uhandisi.

Alisema kuwa wakiwa na kampuni ya ushauri katika masuala ya uhandisi, wamekuwa wakishirikiana na makampuni mengine yaliyopo nje ya nchi.

Akielezea changamoto katika utendaji wa kampuni hiyo Seng’enge alisema kuwa kampuni yao imekuwa ikitumiwa zaidi na makampuni yaliyopo nje ya nchi katika utoaji wa huduma na kuiomba Serikali kuwasaidia na kuahidi kutoa ushirikiano ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

TAARIFA YA KUACHISHWA KAZI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA,ANNA KILANGO MALECELA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Bi. Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.

Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 11 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.


Dkt. Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana tarehe 10 Aprili, 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.


"Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" Amesisitiza Rais Magufuli.Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.

Pamoja na hatua hiyo, Dkt. Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.


Katikati ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.


Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.


Kabla ya kutangaza kutengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.


Ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati.


Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.


Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida, Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

11 Aprili, 2016. 

WANAWAKE WAFANYABIASHARA MASOKONI WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA MAENEO YAO YA BIASHARA.

$
0
0
Mwenyekiti wa Soko la Kisutu Tamimu Chande akizungumza katika Kampeni ya Kuongeza uelewa wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika Soko la Kisutu Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo inaendeshwa na Shirika la Eqiuality for Growth (EfG).
Mmoja wa kiongozi wa Soko la Kisutu akifungua mkutano wa kampeni hiyo.
Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Equality for Growth, Grace Mateh akizungumza kwenye kampeni hiyo.
Mfanyabiashara wa Soko hilo, Bazalo Tazoni akizungumza katika kampeni hiyo.
Ofisa Maendeleo wa Kata ya Mchafukoge, Domonica Balama akizungumza katika kampeni hiyo.
Mfanyabiashara katika Soko hilo, Charles Mloka akichangia jambo kwenye kampeni hiyo kuhusu wanawake wafanyabiashara kujitambua kuhusu ukatili wa jinsia masokoni.
Katibu wa Soko la Kisutu, Suitebet Nyawalle akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili masokoni.
Katibu wa Soko la Kisutu, Suitebet Nyawalle akiserebuka na wasanii wa kundi la machozi katika kampeni hiyo.
Wasanii wa kundi la machozi wakitoa burudani katika kampeni hiyo.
Taswira katika kampeni hiyo.
Burudani zaidi kutoka kundi la machozi zikiendelea hapo ni Babu na Bibi wakifanya vitu vyao.
Igizo la kupinga ukatili wa kijinsia kutoka kundi la machozi likifanyika.
Mfanyabiashara wa Soko hilo Editha Mtembei akichangia jambo.
Vijana wakishangia kwenye kampeni hiyo.
Picha ya pamoja kati ya viongozi wa soko hilo na viongozi kutoka EfG.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA IRAN HAPA NCHINI. AKABIDHIWA CHETI NA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Iran Nchini Tanzania Mhe. Mehd Aghajafari wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 11,2016, kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia suala la kukuza Ushirikiano kati ya Nchi mbili hizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Cheti maalum kutoka kwa Muwakilishi wa Jumuiya ya Watu wenye ulemavu Nchini Bibi Stela Jailos kwa ajili ya kutambua mchango mkubwa wa Serikali ya awamu ya 5 kwa Watu wenye Ulemavu.(Picha na OMR)

KANZIDATA YA WATU WENYE ULEMAVU YAZINDULIWA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Wazikri Mkuu (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kanzidata ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11, 2016.
Naibu Waziri Ofisi ya Wazikri Mkuu (watu wenye Ulemavu)Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifuatilia uwasilishwaji wa takwimu za Watu wenye Ulemavu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk.Albina Chuwa wakati wa Uzinduzi wa kanzi data hiyo Aprili 11, 2016 Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa wasioona Bw. Luis Benedicto akichangia hoja wakati wa Uzinduzi wa Kanzidata ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk.Albina Chuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu Kanzidata mara baada ya uzinduzi wa kanzidata hiyo ya watu wenye ulemavu katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11 2016,(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu) Dkt. Abdallah Possi amezindua rasmi kanzidata ya watu wenye ulemavu, ambayo itasaidia katika upatikanaji wa taarifa zinazohusiana na watu wenye ulemavu nchini na kuwawezesha wadau wengine katika kuboresha sera na programu zinazolenga kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu nchini.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kanzidata hiyo Katika Ofisi ya Waziri Mkuu leo Jijini Dar es Salaam, Dkt Abdallah Possi amesema kanzi data hiyo itakayotumika kutoa takwimu ya watu wenye ulemavu nchini iwe ni fursa ya kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa, kujikwamua kiuchumi na kuondokana na unyanyapa unaofanywa na baadhi ya watu.

“Ni matarajio yangu kwamba kanzidata hii itasaidia mambo kadhaa muhimu, kubwa zaidi ni upatikanaji wa taarifa katika mfumo rafiki utakaosaidia watumiaji kufanya uchambuzi wa kina zaidi kulingana na mahitaji yao yatakayosaidia kuleta uelewa kwa watu kuhusu ulemavu kwa ujumla na umuhimu wa kuhusisha mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa ajili ya maendeleo endelevu” alisema Dkt. Possi.

Aidha Mkurugenzi wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa wajibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa ni kutunza na kutoa kumbukumbu kwa ajili ya makundi mbalimbali na katika kufanikisha hilo ameomba ushirikiano kutoka chama cha watu wenye ulemavu na mashirikisho yake ili kuboresha kanzidata hii ya watu wenye ulemavu.

Dkt. Chuwa alisisitiza kuwa, ili kanzidata hii iweze kufanya kazi kwa urahisi inahitaji ushirikiano kutoka Sekta binafsi ili kuwezesha kukamilisha andiko lililoko katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa kanzidata na kwa kuanzia kanzidata hiyo imeanza kwa majaribio katika Wilaya ya Bagamoyo.

Kanzidata hii imetayarishwa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwa na dhumuni la kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa urahisi na ufuatilia wa takwimu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu.

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI ASHIRIKI MKUTANO WA MASPIKA KUTOKA NCHI ZA SADC NCHINI MAURITIUS.

$
0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai  akisalimiana na Spika wa Bunge la Lesotho Mhe. Nthloi Motsamai katika Mkutano wa Maspika kutoka Nchi Wanachama wa SADC unaendelea Nchini Mauritius. Ndugai ndiye Rais wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC Parliamentary Forum)
  Spika wa Bunge, Job Ndugai  akisalimiana na Spika Mstaafu wa Bunge la Zambia,  Amusaa Mwanamwambwa ambaye ni mmoja wa watoa mada katika  Mkutano wa Maspika kutoka Nchi Wanachama wa SADC unaendelea Nchini Mauritius katikati ni Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Umoja huo Dr. Essau Chiviya. Ndugai ndiye Rais wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC Parliamentary Forum) 
 Spika wa Bunge, Job Ndugai  akisalimiana na Spika Mstaafu wa Bunge la Zambia , Amusaa Mwanamwambwa ambaye ni mmoja wa watoa mada katika  Mkutano wa Maspika kutoka Nchi Wanachama wa SADC unaendelea Nchini Mauritius katikati ni Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Umoja huo Dr. Essau Chiviya. Mhe. Ndugai ndiye Rais wa Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC Parliamentary Forum) 

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI WA TAASISI YA TAKUKURU PAMOJA NA HUNDI KIFANI YA SH. BILIONI 6 KUTOKA BUNGE BAADA YA KUBANA MATUMIZI

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.

RAIS DK. MAGUFULI AAGIZA BILIONI 6 KUTOKA BUNGE ZIKABIDHIWE KWA MAGEREZA NA JKT ILI KUTENGENEZA MADAWATI 120.000

$
0
0
Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.

Ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati.

Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida, Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.

Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 11 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.

Dkt. Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana tarehe 10 Aprili, 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.

“Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?” Amesisitiza Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.

Pamoja na hatua hiyo, Dkt. Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.

Katikati ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.

Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
11 Aprili, 2016

JESHI LA MAGEREZA NA SUMA – JKT WAKABIDHIWA JUKUMU LA KUTENGENEZA MADAWATI YENYE THAMANI YA BILIONI 6, JIJINI DAR

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akionesha mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Ofisi ya Bunge leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam ambapo fedha hizo ameelekeza zitumike kutengenezea madawati ya shule hapa nchini(kulia)ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.
Muonekano wa Madawati ambayo yanatarajiwa kutengenezwa na yaliyoidhinishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kama yanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Bregedia Jenerali, Michael Isamuhyo(katikati) wakifuatilia hotuba ya Rais Magufuli(kulia) ni Mtendaji Mkuu wa SUMA – JKT, Bregedia Jenerali C.Yateri.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akiongea na Wandishi wa Habari kuhusu namna Jeshi hilo lilivyojipanga kutekeleza jukumu lililopewa.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa waliohudhuria hafla hiyo
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akisalimiana na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila wakipokutana katika Viwanja vya Ikulu, Jijini Da es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Na; Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza,

JESHI LA MAGEREZA nchini pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa limepewa jukumu la kutengeneza madawati yenye thamani ya Bilioni 6 ambayo yatasambazwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Jukumu hilo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama limetolewa leo Aprili 11, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, katika hafla fupi ya makabidhiziano ya mfano wa hundi ya Bilioni 6 za pesa ya kitanzania kutoka Sekretarieti ya Bunge ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pesa ambazo zimepatikana kufuatia kubana matumizi ya uendeshaji wa Ofisi hiyo.

Rais Magufuli amesema kuwa Ofisi ya Bunge pamoja na Watendaji wake wameonesha moyo wa kizalendo kwa Taifa lao kwani wametekeleza kwa vitendo maelekezo ya kubana matumizi ya fedha za Serikali hivyo kuokoa kiasi hicho cha Bilioni 6 ambazo wamezikabidhi ili zitumike katika kutatua changamoto ya uhaba wa Madawati katika shule nyingi hapa nchini.

“Nikupongeze sana Dkt. Thomas Kashilila, Watendaji wote wa Ofisi ya Bunge kwa moyo wenu wa upendo, uzalendo mkaamua kiasi hiki cha fedha Bilioni 6 zikafanye kazi ya maendeleo kwani mngeweza kuzitumia fedha hizi katika matumizi mengine hata Mhe. Spika asingejua”. Alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Makatibu Wakuu wote wa Wizara pamoja na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Umma/Serikali kuiga mfano huo wa kizalendo aliouonesha Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila kwani huo ndio mwelekeo anaoutaka katika Serikali yake ya Awamu ya Tano.

Awali akiongea kabla ya Makabidhiano ya hundi hiyo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimepatikana kufuatia kubana matumizi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kupunguza safari za nje, gharama za machapisho mbalimbali, gharama za viburudisho na chakula, matibabu kwa wabunge, mafuta na uendeshaji wa mitambo nk.

Akizungumzia utekelezaji wa jukumu la utengenezaji wa madawati hayo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amesema kuwa Jeshi la Magereza lipo tayari kutekeleza agizo la Rais na amejipanga kutumia nguvu kazi ya Wafungwa waliopo magerezani pamoja na Maafisa na Askari wa Jeshi hilo ili kukamilisha kazi hiyo kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

“Mhe. Rais ametoa maelekezo ya kwenda kufanya kazi hiyo kama operesheni maalum hivyo sisi kwa upande wa Jeshi letu tupo tayari kuifanya kazi hiyo kama ilivyoelekezwa kwa kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais”. Alisema Jenerali Minja.

Jeshi la Magereza Tanzania limepiga hatua kubwa ya Maboresho juu ya utengenezaji wa bidhaa bora za Samani hivyo kupelekea kuibuka mara kwa mara Mshindi wa kwanza katika Maonesho mbalimbali ya Kibiashara hapa nchini.

SENDEKA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI BABATI

$
0
0
 Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya za Babati Mjini na Babati Vijijini, katika ukumbi wa CCM mkoawa Manyara, leo Aprili 11, 2016, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo. (Picha na Bashir Nkoromo).
. Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akionyshwa na Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali (kulia), jinsi Jengo la Ofisi ya CCM mkoa huo, lilivyoungua moto hivi karibuni, Sendeka alipokagua jengo hilo, leo Aprili11, 2016, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Manyara. (Picha na Bashir Nkoromo).

DKT. SHEIN AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAPINDUZI LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi (BLM) mara baada ya kuwaapisha Viongozi hao hapo jana, kikao kilichofanyika leo kiliwajumuisha Mawaziri pamoja na Naibu Mawaziri wote wa wizara 13 katika ukumbi wa Baraza hilo Ikulu Mjini Unguja.Picha na Ikulu. 

Airtel yaleta 'Jipimie Yatosha Yako' kutoa uhuru zaidi vifurushi vya Yatosha

$
0
0
Airtel Tanzania ili kutoa uhuru zaidi kwa wateja wake imetangaza kifurushi kipya kupitia huduma yake ya vifurushi vya  Airtel Yatosha kijulikanancho kama Airtel Jipimie Yatosha Yako itakayowapa wateja wake faida kubwa na uwezo wa kuweza kupanga na kuunda kifurushi wanachokitaka kutokana na chaguo na mahitaji yake .

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Anethy Muga  alisema "Jiunge sasa na Airtel ufurahie Uhuru huu mpya, Tumezindua " Airtel Jipimie Yatosha Yako " kwa ajili ya kuwapatia wateja wetu uhuru wa kuchagua na  kupanga matumizi yao na papo hapo kuunda kifurushi  kitakachoweza kukidhi mahitaji yao  ya kiuchumi na kijamii.

Airtel Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi ambacho na kinapatikana kwa wateja wetu wote hapa nchini ambapo unaweza kupata kifurushi hiki upendavyo wewe yaani kwa siku, wiki, na  hata mwezi.

“Airte daima tunafanyia bidhaa zetu zote utafiti  na kuziunda kwa mujibu wa kile wateja wetu wanataka ili kuleta unafuu na ubora zaidi, kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wateja wa simu za mkononi wa Airtel wataweza kuamua kununua vifurushi vya gharama nafuu na watakavyo vya hadi shilingi  500 huku wakijipimia muda wa maongezi tu, au changanya na MB zaidi au unajichaguali Muda wa maongezi na SMS au kujipimia vyote yaani Muda wa maongezi Zaidi, MB zaidi na SMS Zaidi, uhuru ni wako kujipimia utakavyo” na sasa ndio wakati wa kujiunga na Airte.

Airtel inaamini ubunifu wa huduma ya “Jipimie Yatosha Yako" itakuwa suluhisho la mawasiliano kwa wengi na msaada kwa wale ambao walitaka kifurushi kutokana na hitaji lake. Sasa wateja wa Airtel wanauwezo wa kutengeneza Yatosha yao wao wenyewe  na kutimiza mahitaji yao .

Kujiunga na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja wanatakiwa kupiga  namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.

Huduma mpya ya uhuru wa kujipimia Vifurushi vya Yatosha imezinduliwa na kusindikizwa na wasanii wa  kundi la Navy kenzo linaloundwa na Nahreel na Haika ambao wataitambulisha sehemu mbalimbali nchini
“Sisi tuko tayari kama kawaida kuja kujipimia yatosha kila mahali, sasa na nyie kuweni tayari kukamatia chini Yatosha yako inayokutosha" alisema Nahreel wa Navy Kenzo.

Airtel yaleta 'Jipimie Yatosha Yako' kutoa uhuru zaidi vifurushi vya Yatosha

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto) akiwa pamoja na wanamuziki wa kundi la Navy Kenzo  Nahreel na Aika (katikati) pamoja na Meneja Msoko wa Airtel Bi Anethy Muga wakionyesha bango  la Uzinduzi wa huduma  mpya ya kifurushi kipya cha Airtel Yatosha kijuikanacho kama “Jipimie Yatosha yako” kitakachowawezesha wateja kutengeneza na kununua kifurushi wanachokitaka  kutokana na chaguo na mahitaji yao
 Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi wa huduma  kifurushi kipya cha Airtel Yatosha kijuikanacho kama “Jipimie Yatosha yako” kitakachowawezesha wateja kutengeneza na kununua kifurushi wanachokitaka  kutokana na chaguo na mahitaji yao.  Kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga na wakwanza toka kulia ni wanamuziki wa kundi la Navy Kenzo  Nahreel akifatiwa na  Aika
 Meneja Msoko wa Airtel Bi Anethy Muga (kulia) kiongea wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijuikanacho kama “Jipimie Yatosha yako” kitakachowawezesha wateja kutengeneza na kununua kifurushi cha wanachokitaka  kutokana na chagua na mahitaji yao. Pichani ni Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando pamoja na wanamuziki wa kundi la Navy Kenzo  Nahreel akifatiwa na  Aika
Wanamuziki wa kundi la Navy Kenzo  Nahreel na  Aika wakijaribu kujipimia kifurushi cha Airtel Yatosha mara baada ya kuzindua huduma hiyo mpya leo, wpamoja nao ni Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (shoto). “Jipimie Yatosha yako” itawawezesha wateja kutengeneza na kununua kifurushi wanachokitaka  kutokana na chaguo au mahitaji yao.


·         Kwa mara ya kwanza Tanzania unajipimia vifurushi vya Airtel Yatosha UTAKAVYO
·          Jiunge na Airtel ufurahie uhuru wa kujitengenezea kifurushi chako mwenyewe  kwa gharama nafuu

Dar es salaam Aprili 11, 2016, Airtel Tanzania ili kutoa uhuru zaidi kwa wateja wake imetangaza kifurushi kipya kupitia huduma yake ya vifurushi vya  Airtel Yatosha kijulikanancho kama Airtel Jipimie Yatosha Yako itakayowapa wateja wake faida kubwa na uwezo wa kuweza kupanga na kuunda kifurushi wanachokitaka kutokana na chaguo na mahitaji yake .

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Anethy Muga  alisema "Jiunge sasa na Airtel ufurahie Uhuru huu mpya, Tumezindua " Airtel Jipimie Yatosha Yako " kwa ajili ya kuwapatia wateja wetu uhuru wa kuchagua na  kupanga matumizi yao na papo hapo kuunda kifurushi  kitakachoweza kukidhi mahitaji yao  ya kiuchumi na kijamii.

Airtel Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi ambacho na kinapatikana kwa wateja wetu wote hapa nchini ambapo unaweza kupata kifurushi hiki upendavyo wewe yaani kwa siku, wiki, na  hata mwezi.

“Airte daima tunafanyia bidhaa zetu zote utafiti  na kuziunda kwa mujibu wa kile wateja wetu wanataka ili kuleta unafuu na ubora zaidi, kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wateja wa simu za mkononi wa Airtel wataweza kuamua kununua vifurushi vya gharama nafuu na watakavyo vya hadi shilingi  500 huku wakijipimia muda wa maongezi tu, au changanya na MB zaidi au unajichaguali Muda wa maongezi na SMS au kujipimia vyote yaani Muda wa maongezi Zaidi, MB zaidi na SMS Zaidi, uhuru ni wako kujipimia utakavyo” na sasa ndio wakati wa kujiunga na Airte.

Airtel inaamini ubunifu wa huduma ya “Jipimie Yatosha Yako" itakuwa suluhisho la mawasiliano kwa wengi na msaada kwa wale ambao walitaka kifurushi kutokana na hitaji lake. Sasa wateja wa Airtel wanauwezo wa kutengeneza Yatosha yao wao wenyewe  na kutimiza mahitaji yao .

Kujiunga na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja wanatakiwa kupiga  namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.

Huduma mpya ya uhuru wa kujipimia Vifurushi vya Yatosha imezinduliwa na kusindikizwa na wasanii wa  kundi la Navy kenzo linaloundwa na Nahreel na Haika ambao wataitambulisha sehemu mbalimbali nchini.“Sisi tuko tayari kama kawaida kuja kujipimia yatosha kila mahali, sasa na nyie kuweni tayari kukamatia chini Yatosha yako inayokutosha" alisema Nahreel wa Navy Kenzo.

LANCET TANZANIA LIMITED YAFUNGUA MAABARA YA KISASA MJINI MOSHI.

$
0
0

Maabara ya kisasa ya Lancet iliyofunguliwa mjini Moshi jirani na YMCA kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya Saratani.Dkt Kalebu akionesha sehemu ya vifaa mbalimbali katika maabara hiyo ambavyo vimekuwa vikitumika kwa ajili ya kufanya vipimo. Baadhi ya vifaa mbalimbali vilivyoko katika maabara hiyo ya kisasa iliyofunguliwa mjini Moshi itakayotumika kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali ambayo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakivifuata nje ya nchi. Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Josephat Boniface akiwa katika picha ya pamoja na Dkt Hemed Kalebu pamoja na watumishi wengine wa maabara hiyo .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
 

TRA YATOA MAFUNZO YA ULIPAJI KODI KWA HIYARI KWA WANACHAMA WA TABOA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
MAMLAKA ya mapato Tanzania(TRA) wametoa mafunzo kwa wanachama cha wasafirisha abiria(TABOA) jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na wanachama hao kulipa kodi kwa hiyari bila shuruti.



 Meneja elimu kwa mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, Diana Masalla akizungumza na wanachama cha umoja wa usafirishaji abiria hapa nchini (TABOA), kuhusiana na ulipaji wa kodi kwa hiyari katika sekta ya usafirishaji.
 Meneja wa elimu kwa Mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Gabriel Mwangosi akizungumza na wanachama cha umoja wa usafirishaji abiria hapa nchini (TABOA) jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanachama wa chama cha wasafirishaji abiria hapa nchini wakipata elimu ya kulipakodi kwa hiari inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) jijini Dar es Salaam leo.

TUSIPOCHUKUA HATUA HAKUNA SABABU YA SISI KUITWA VIONGOZI-RAIS DKT MAGUFULI

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


 OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

         


KUH: KUAHIRISHWA KWA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Natumia fursa hii kuwataarifu wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, kikao cha Baraza kilichokuwa kifanyike kesho tarehe 13 Aprili, 2016 kimeahirishwa mpaka tarehe nyingine itakayopangwa.

Kuahirishwa kwa kikao hiki, ni kutokana na sababu muhimu zilizo nje ya uwezo wa waandaji.Naomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza, kwani naelewa kuwa, wajumbe wengi mlikuwa mmeshapanga ratiba zenu tayari kwa kikao cha kesho huku mkiahirisha shughuli nyingine.

Tarehe nyingine ya kikao itakapopangwa, mtaarifiwa mapema iwezekanavyo.

Jaji Francis S.K. Mutungi

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEWA NA BALOZI WA IRELAND

$
0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa na balozi wa Ireland Bi. Fionnuala Gilsenan aliyemtembelea Ofisini kwake leo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

MBUNGE WA KALIUA, TABORA MHE. SAKAYA ATOA WITO KWA SERIKALI KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA WATU NCHINI

WASHTAKIWA WA TUMBILI WASOTEA DHAMANA

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

HATMA ya dhamana kwa washtakiwa saba wa makosa ya uhujumu uchumi wakiwamo wafanyabiashara raia wa Uholanzi waliokamatwa Machi 23 mwaka huu wakijaribu kusafirisha wanyama hai 61 aina ya Tumbili sasa kujulikana Alhamisi (Aprili 14).

Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi ,Aishiel Sumari wakati akitoa uamuzi mdogo juu ya hoja zilizotolewa na upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Majura Magafu dhidi ya upande wa Jamhuri kuhusu maombi ya dhamana kwa washtakiwa.
 
Hoja za upande wa utetezi zilitokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha mahakamani hapo hati zuio la dhamana kwa washtakiwa wote saba iliyotoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Maombi matatu ya dhamana yaliwasilishwa mahakamani hapo ambayo ni ombi la tatu la raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian ,Eduard Vardanyan na Idd Misanya ,ombi nne la ,Nyangabo Musika,Martina Nyakanga na Very Anthon huku ombi la tano lilikuwa ni la aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa idara ya wanyamapori nchini Dkt Charles Mulokozi.

Baada ya maombi hayo kuwasilishwa upande wa utetezi uliridhia kuunganishwa kwa maombi hayo ili kuokoa muda wa mahakama katika kusikiliza shauri hilo baada ya maombi hayo kufanana.Akitoa uamuzi huo Jaji Sumari aliuelekeza upande wa jamhuri kupitia kwa wanasheria wa Serikali Wankyo Simon na Robart Rogart kutumia siku ya leo (Jumanne) kuwasilisha hoja kinzani na kwamba upande wa utetezi utawasilisha maombi yao kesho (Jumatano) baada ya kujibiwa na upande wa pili.
Baadhi ya Washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi ya usafirishaji wa wanyama Hai 61 aina ya Tumbili wakiongozwa na asakari Polisi walipokuwa wakiwasili katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi.
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakisindikizwa na askari Polisi kuingia mahakamani,Nyuma yao ni mshtakiwa mwingine Idd Misanya . Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi ,kulia ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt Charles Mulokozi. 

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images