Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 811 | 812 | (Page 813) | 814 | 815 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika moja ya kikao na wakandarasi wanaosambaza  Umeme Vijijini vilivyoanza tarehe 29 Machi na kumalizika tarehe 31 mwezi huu.Wa Tatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Ufundikutoka REA, Mhandisi Bengie Msofe. Wengine ni watendaji kutoka kampuni ya Angelique International inayosambaza umeme mkoani Arusha, Wizara na REA.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika kikao na kampuni  ya Engineering & Construction inayosambaza umeme vijijini mkoani Kagera katika wilaya za Ngara, Biharamulo, Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Bukoba vijijini na Muleba kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya na anayemfuatia ni Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga.Wengine ni watendaji kutoka kampuni hiyo, Wizara na REA.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa kwanza kushoto), Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga (wa pili kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Lutengano Mwakahesya (wa Tatu kushoto) wakiwa katika moja ya vikao vilivyojumuisha wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini vilivyoanza tarehe 29  Machi na kumalizika tarehe 31 Machi, mwaka huu.

  Na Teresia Mhagama
  Imeelezwa kuwa wakandarasi wenye tuhuma za kutolipa mishahara wafanyakazi wao, kuomba rushwa  kwa wateja wanaotaka kuunganishiwa umeme na kutolipa fedha za watoa huduma waliokuwa wakifanya nao kazi katika usambazaji  umeme vijijini Awamu ya Pili, hawatapewa kazi husika katika miradi ya REA Awamu ya Tatu.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na kampuni mbalimbali zinazotekeleza miradi ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili inayotarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi, akiwasalimia baadhi ya viongozi wa CCM wa mkoa baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya leo asubuhi. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangwi Kundya, Katibu wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Lobe Zongo na Katibu msaidizi Mkuu wa mkoa, Adallah Mayomba.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwai akiwa na mwenyeji wake, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Mwangwi Kundya (kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya.

  0 0

   
  Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa

   Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu hivi punde kwa tuhuma za rushwa,Wabunge hao kama waoenekanavyo pichani ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa

  TAARIFA KAMILI ITAWAJIA HIVI  PUNDE. 

  0 0

   Mkurugenzi wa kampuni ya simu ya TTCL nchini Dk Kamugisha Kazaura akimuelekeza jambo Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliani Professa Makame Mbawala kuhusu mkongo wa mawasiliano uliopo mpakani mwa Tanzania na Burundi. 
  Vijana waliokutwa na nyaya za wizi za kampuni ya TTCL waliokamatwa usiku wa kuamkia leo na wanachi (kushoto) Haroon Khamani na Amos khalidi.

  Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wilaya ya Kasulu juu ya wezi wa nyaya za simu za kampuni ya TTCL kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria haraka kwa kuhujumu mawasiliano.
    Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu za TTCL nchini Dk Kamugisha Rwezaura akiongea na vyombo vya habari juu wezi waliokata nyaya za simu TTCL mtaa wa Sovya Wilayani Kasulu


  Editha Karlo, Kasulu

  WANANCHI  wa Mtaa  wa soko la sovya Wilayani Kasulu usiku wa kuamkia leo wamewakamata wezi waliokuwa wamekata nyaya za mawasiliano za kampuni ya TTCL.

  Akiongea juu ya tukio hilo Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu TTCL nchi Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la soko la sovya majura ya saa kumi na moja alfajiri. Alisema kuwa wananchi  wanaoishi karibu na eneo lililokatwa nyaya hizo ndiyo waliowakamata vijana hao baada ya kufanya uhslifu huo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa hasara waliyoipatia kampuni kwa kukata nyaya hizo inakadiliwa ni zaidi ya milioni 20.

  "Hasara waliyoingizia serekali ni kubwa sana hizo nyaya walizokata zinagharimu milioni 20,lakini kuitengeneza upya line hiyo inaweza kugharimu zaidi ya hiyo fedha''alisema Kazaura

  Alisema kutokana na wezi huo umepelekea baadhi ya ofisi za serekali kukosa mawasiliano ikiwemo ofisi ya polisi Wilaya,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Bank na Takukuru. Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbawala alivitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wezi hao wanaohujumu mawasiliano.

  "Hawa muwapeleke kwenye sheria hiki walichofanya ni kosa kwa sheria ya mwaka 2015 wanatakiwa kulipa faini isiyopungua milioni 50 au kifungo jela ili iwe fundisho kwa wengine"alisema profesa Mbawala

  0 0

  Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kangi Lugola (Mbunge wa Mwibala), Mh. Sadiq Murad (Mbunge wa Mvomero) pamoja na Mh. Victor Mwambalaswa (Mbunge wa jimbo la Lupa) wakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, kwa kusikiliza kesi inayowakabili ya kushawishi kupatiwa rushwa ya Mil. 30 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja hapa nchini. 
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

   WABUNGE watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuomba  rushwa ya sh.milioni 30.

  Wabunge waliofikishwa Mahakama ya Kisutu leo ni Mbunge wa Mvomero, Sadiq Murad, Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, pamoja na Mbunge wa Mwibara Alphaxaid Kangi Lugola.

  Mwendesha Mashitaka wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mahela Ndimbo mbele Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,  Thomas Simba amesema tukio hilo lilitokea  Machi 15 mwaka huu  majira saa 2  had saa 4 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

  Ndimbo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa wajumbe Kamati Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) waliomba  rushwa ya sh.milioni 30 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana  Magota.

  Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,Thomas Simba alidai kuwa upande wa mashitaka upeleke ushaidi  wa watuhumiwa wa rushwa .

  Washitakiwa waliposomewa shitaka la kuomba rushwa wote walikana na dhamana yao kuwa wazi kwa masharti ya kila mmoja kwa na mdhamini wa mmoja wa sh.milioni tano pamoja na hati ya kusafiria ambapo wote walikidhi masharti ya dhamana hiyo.

  Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ameairisha kesi hiyo mpaka Aprili 14 mwaka huu itakapotajwa tena .

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati Dk. Juliana Pallangyo (pichani) akifungua mkutano unaoshirikisha wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme.
   Sehemu ya watendaji na wakurugenzi wa mashirika ya umeme katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani).
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) na  Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Umeme Nchini (TANESCO) Mhandisi Decklan Mhaiki (kushoto) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mwenyekiti wa kamati ya nchi za kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya  umeme, Josh Chifamba (hayupo pichani)
   Mwenyekiti wa kamati ya nchi za kusini mwa Afrika zinazoshirikiana katika biashara ya umeme, Josh Chifamba (kulia) akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia  masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) aliyekuwa mgeni  rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

  0 0

  Mshindi wa shindano la uvumbuzi wa Teknolojia mpya itakayo saidia jamii kupatikana leo na kuzawadiwa shilingi milioni tano (5,000,000) katika mkutano wa wadau wa teknologia unaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Mkutano huo umeandaliwa na Bites&Bytes ukishirikiana na IBM, TWAWEZA, FSDT pamoja na CBA, mktano huo ambao utahamasisha uendelezaji wa mawazo mapya na uvumbuzi kwa waanzishaji wapya wa biashara na kuwapa mwanya wa kubadilisha mawazo na wadau wengine.  Mwanzilishi wa Bits&Bites, Lilian Madeje akiwakalibisha wageni na kufungua mkutano wa Uvumbuzi wa Teknologia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mwalimu Nyerere.
  Mwakilishi wa IBM na mstakabali wa Innovation, Ben Mann akifafanua jinsi IBM ilivyofanya kazi kwenye Teknologia hapa nchini.
   Mwakilishi mwenza wa Bits&Bytes,Zuweina Farah akizungumza na wadau wa Teknologia waliokusanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya DTREE, Lucy Silas akizungumza na wadau wa teknolojia na uvumbuzi wa teknologia katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
    Baadhi ya wadau wa Teknologia wakimsikiliza  mtoa mada (Hayupo) pichani jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.

    Mwakilishi mwenza wa Bits&Bytes,Zuweina Farah akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Teknologia na uvumbuzi wa teknologia mpya itakayo wasaidia wanachini kufanya kazi kwa urahisi zaidi, leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Amesema kuwa leo washiriki 16 walioshiriki kuvumbua teknoloia mpya wameshiriki katika mkutano huo na ndipo mshindi atakaye fanikiwa kushinda katika shindano hilo atazawadiwa shilingi Milioni 5 kwa kuwa na wazo zuri kuliko wengine ili aweze kuwa na mtaji kwaajili ya kuendeleza uvumbuzi wake.
  Mwanafunzi mshiriki wa uvumbuzi wa Teknologia mpya itakayo wasaidia jamii, Gibson Kawago wa shule ya Sekondari ya huko Arusha akiwa amegundua taa za miale ya jua(Solar Power) zinazoweza kuchaji simu za Smati kwa zaidi ya masaa nane.
   Mwakilishi wa Fist Financial Sector Deeping(FSDT), Revis Mushi akizungumza na waaandishi wa habari katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa mkutano huo utasaidia jamii na wananchi kwa ujumla kusaidia kupata mfumo mwepesi wa Teknologia.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Atamizi (DTB) ambayo ipo tume ya Sayansi, George Mulamula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuhusiana na amesema kuwa Tume ya Sayansi imeungana katika mkutano wa Teknologia ili kuwapa ujuzi zaidi Vijana. Pia amesema kuwa katika Tume ya Sayansi wameweza kuvumbua mfumo wa Max Malipo na wa mfumo wa kudahili wanafunzi wa TCU.
  Mshiriki na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani,  Necta Richard akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya mkutano wa Teknologia uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
  Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Teknologia. 


   Washiriki.

  0 0


  Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Casmir Kyuki akizungumza wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.
  Mwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akizungumza wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma. Makabidhiano yalifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi (Kushoto) akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dk. Harison Mwakyembe Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma. Wengine pichani ni Katibu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sufini Mchome (wa pili kulia) na Katibu Mtendaji wa Tume Bw. Casmir Kyuki.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dk Harison Mwakyembe akiongea mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma.
  Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhuria makabidhiano ya Taarifa ya Utafiti wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (Picha zote na Munir Shemweta wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania).

  0 0

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha Mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a). Wabunge hao ni Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero ; Mheshimiwa Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibala.

  Wabunge hao wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mh.Thomas Simba. Akisoma mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiwa wote watatu waliomba rushwa ya shilingi Mil.30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo kwa lengo la kumsaidia ili Taarifa ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa kwa wakati huo ijadiliwe tahere 16/3/2016 ipitishwe bila marekebisho.

  Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na washtakiwa wote watatu mahakama imewaachia kwa dhamana ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 5. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 14/4/ 2016 itakapotajwa tena. 

  TAKUKURU inawajulisha wananchi wote kwamba hakuna mtu ambaye yupo juu ya Sheria. Rushwa haivumiliki!


  IMETOLEWA NA 
  OFISI YA AFISA UHUSIANO 
  TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU 
  31 MACHI, 2016

  0 0

  Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo.Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe na kulia ni Mchambuzi wa Mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care,Kulia ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), akimkabidhi Hati ya Bima ya Elimu wa 'Sanlam Education Care', Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood.

  Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa bima za maisha TanzaniaSanlam Life Insurance, leo, imezindua bima ya elimu ya kipekee inayolenga kukupa uhakika wa elimu ya mwanao.

  'Bima hiyo inayoitwa “Sanlam Education Care', inawapa wazazi mpango wa akiba wa kila mwezi pamoja na faida ya bima ya maisha ambayo inalinda uwekezaji wako katika tukio la kifo au ulemavu wa kudumu. 

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance  amesema,"kuwekeza katika elimu ya mtoto wako ni moja ya zawadi bora ambayo wazazi wanaweza kuwapatia watoto wao”. 

  Elimu imeanza kuwa huduma ghali katika maisha ya siku hizi, kwahiyo wazazi wanashauriwa kufanya maamuzi ya busara ya uwekezaji pale linapokuja suala la ustawi wa maisha ya baadaye ya watoto wao. Sanlam Education Care ni suluhisho kamili, kwani imebuniwa kama mpango wa akiba unaowawezesha wazazi kuwa na utaratibu mahususi wa kuweka akiba ambao unazingatia kupanda kwa gharama za elimu.

  "Hakuna huduma nyingine ya bima ya maisha inayokidhi haja ya kulinda elimu ya mtoto kama huduma hii ya Sanlam Education Care. ‘Kuongezeka kwa huduma ya Sanlam Education Care kwenye orodha ya bidhaa zetu' inatilia mkazo dhamira yetu ya kupanua wigo wa huduma zenye ubunifu na zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu pamoja na kuboresha na kulinda ukwasi wao"

  0 0

  WANAKIKUNDI cha Green Garden ambao wanafanya biashara uuzaji na utunzaji  maua  pembeni kidogo ya kituo cha mabasi cha Mbuyuni jijini Dar es Salaam wapewa mpira kumwagilia maua wa Mita 100 na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva.

  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva amesema kuwa ameona vyema kutimiza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mtaa kwa wanakikundi hicho kwani aliwaahidi kuwasaidi amesema Mwenyekiti huyo wakati wa kukabidhi mpira wa kumwagilia wa mita 100 leo pembeni ya kituo cha mabasi ya Mbuyuni jijini Dar es Salaam.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo ameashukuru  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva kwa kutimiza ahadi ahadi yake.

  "Tulikua na mpira ambao ulikuwa umetoboka tulijitahidi kuziba na makaratasi ili usivuje sasa tumepata mpya tena wa mita 100 sasa tutakuwa kukijitahidi kutunzaji wa maua vizuri"

  Mombo amesema kuwa kikundi hicho kimeanzishwa mwanzoni mwa mwaka 1985 mpaka sasa wapo tuu kwa sababu ya kujitafutia liziki ikiwa wanapata changamoto mbali mbali hasa za kukosa wateja kwa mda mwingine.
   Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akimwagilia maua mara baada ya kuwakabidhi mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green Garden jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo akizungumza kwa mwandishi wetu mara baada ya kupewa msaada wa mpira wenye mita 100 utakao wawezesha kumwagilia maua kwa urahisi zaidi tofauti na mwanzo na 

   Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), (kushoto) Zefrin Lubuva  akikabidhi Mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green Garden kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.

   Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (Mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mpira wa mita 100 jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akipewa maelekezo na Mwenyekiti wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo mara baada ya kukabidhi mpira wa kumwagilia maua katika kikundi hicho kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.
  Wanakikundi wakiufungua mpira kwaajili ya kuanza kazi  mara baada ya kukabidhiwa mpira wa mita 100 leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini  Bw.Lutengano Mwakahesya akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo zaidi ya Bilioni 435 zinatarajiwa kutumika kutekeleza miradi ya kupeleka umeme katika maeneo mbalimbali hapa nchini lengo likiwa kuwafikia watanzania wote. kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo bw. Frank Mvungi.
  Meneja Wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)  Bw. Elineema Mkumbo akitoa wito kwa watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali kufikisha nishati ya Umeme kwa watanzania wote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini  Bw.Lutengano Mwakahesya.

  Frank Mvungi-Maelezo
  SERIKALI kutumia Bilioni 435 kutekeleza Miradi ya kupeleka Umeme Vijijini ikiwa ni utekelezaji wa Malengo yakuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na nishati ya hiyo ili kukuza uchumi na kupanua wigo wa uzalishaji.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati ya  Umeme Vijijini (REA)Dkt. Lutengano Mwakhesya wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliolenga kueleza hatua iliyofikiwa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kupeleka umeme vijijini.
  “Miradi inayotekelezwa hadi sasa kwa awamu ya pili imekamilika kwa asilimia 90 na tunatumaini kuwa kasi ya utekelezaji wa miradi yote kwa awamu ya pili na yatatu itakapoanza itaongezeka zaidi “ alisisitiza Mwakhesya.

  Akifafanua kuhusu idadi ya vijiji vilivyokwishanufaika Mwakhesya amesema kuwa vijiji 5200 vimepatiwa umeme sawa na asilimia 36 ya vijiji vyote vilivyopo hapa nchini ambavyo ni takribani 15,000.

  Kwa upande wa kiwango cha fedha zilizotolewa wakati wakala huo unaanzishwa ni Bilioni 10 ambapo zimekuwa zikiongezaka mwaka hadi mwaka ili kufikisha huduma hiyo kwa watanzania walio wengi zaidi.
  Akizungumzia Wilaya zilizonufaika na awamu ya kwanza Mwakhesya alizataja kuwa ni Uyui,Kilolo Kilindi na Bahi ambapo kwa Sasa lengo ni kufikisha huduma hiyo kwa wananchi wote.

  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Nishati Vijijini Bw. Elineema Mkumbo ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya kuunganishiwa umeme kwa gharama ya 27,000 tu lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanafikiwa na nishati hiyo.

  REA imekuwa ikitoa  kipaumbele kwenye huduma za jamii kama shule,Hosipitali na Visima vya Maji kwa kutumia sola ambazo ziko kwenya moja ya miradi inayotekelezwa na wakala huo. 

  0 0

  Ummy Mwalimu

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akiwasili katika hospitali ya Rufaa Ndanda Mission.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari wametembelea Hospitali ya Mji wa Masasi (Mkomaindo), Hospitali ya Rufaa Ndanda Mission na Kituo cha Afya cha Nanguruwe kilichopo Jimbo la Mtwara Vijijini.
   
  Katika ziara hiyo ya siku 2 Mh. Ummy alipata fursa ya kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kukagua wodi za wagonjwa, maabara pamoja na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa idara ya afya na wananchi katika utoaji wa huduma za afya katika maeneo hayo.

  Mh. Ummy alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe Dk. John Pombe Magufuli imejikita zaidi katika kuwahudumia wananchi hasa wa kipato cha chini kwa kuimarisha Nidhamu na Uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma. Pamoja na kusimamia Uwazi na matumizi bora ya rasilimali za Taifa.

  Licha ya kukiri kuwa sekta ya Afya inakabiliwa na changamoto mbalimbali Mh. Ummy aliwapongeza na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kazi na nzuri wanayoifanya ktk kutoa huduma kwa wananchi. Alieeleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini kazi yao na imedhamiria kutatua changamoto zilizoko katika utoaji wa huduma ikiwemo kuongeza watumishi wa afya na kununua vifaa tiba na kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi wa afya hasa walioko pembezoni.

  Aliwaasa wananchi kuwathamini madaktari na waaguzi na iwapo kuna malalamiko dhidi ya watumishi hao basi wananchi wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu ktk kuonyesha malalamiko yao badala ya kujichukulia sheria mkononi.

  Alisema, Hata hivyo wapo watumishi wachache ambao wanafanya kazi kwa kutozingatia maadili ya kazi na viapo vyao, hivyo aliwataka wabadilike kwani Serikali ya awamu ya 5 haitamvumilia mtumishi yeyote anaejihusisha na vitendo vya rushwa na uzembe kazini.
  Ummy Mwalimu
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi Ndanda mission.


  Pia aliwaasa watumishi hao kujiepusha na mambo ambao yanaweza kuleta mgongano na hisia mbaya kwa wananchi. Mfano tuhuma dhidi ya mfamasia wa Wilaya kumiliki maduka matatu ya 3 ambapo mhe Waziri ameelekeza uchunguzi wa TAKUKURU ufanyike.

  Katika Hospitali ya Mkomaindo, Mhe Ummy ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa mafanikio waliyopata ktk ukusanyaji wa mapato ambapo baada ya kufunga mfumo wa kukusanya mapato wa kielektronik mapato yao yameongezeka kutoka shs 500,000 hadi 1,500,000 kwa siku. Amezitaka Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa hospitali ya Mkomaindo kwa sababu hatua hii itachangia sana kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi ikiwemo uwezo wa Halmashauri wa kununua dawa na vifaa tiba.

  Katika Kituo cha Afya cha Nanguruwe Mh. Ummy aliihimiza Halmashauri kukamilisha ujenzi wa wodi mbili ili Kituo hicho kiweze kupandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya. Pia aliwataka kuongeza jitihada katika kuingiza wananchi/kaya nyingi katika Bima ya Afya kwani asilimia 5 wa waliojiunga ni ndogo sana.
  Ummy Mwalimu
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi ili kujua kero zao katika ziara ya siku mbili mkoani humo.

  Katika Hospitali ya Rufaa ya Mission Ndanda Mhe Ummy ameipongeza kwa kufanyia kazi agizo lake la wiki mbili zilizopita la kuzitaka hospitali za Taasisi za Dini zinazopokea ruzuku ya Serikali (Fedha na au Watumishi) kutekeleza kwa vitendo sera za Taifa za Serikali ikiwemo ya Matibabu Bure kwa Wajawazito, Watoto chini ya umri wa miaka 5 na Wazee. Hospitali ya Rufaa Ndanda imekubaliana na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kuanza utekelezaji wa jambo hili kuanzia Julai 1, 2016.

  Mh. Ummy pia amepongeza upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu bure ya Ugonjwa wa Kifua kikuu hospitalini hapo ambapo alisema ni asilimia 10 tu ya vituo vya afya/Hospitali binafsi nchini zinazotoa huduma hizo licha ya Serikali kuwa tayari kuvipatia vifaa vya uchunguzi na dawa bure. Mhe Ummy amezitaka hospitali nyingine binafsi kuunga mkono jitihada za Serikali za kutokomeza ugonjwa wa Kifuu kikuu kama sehemu ya mchango wao kwa jamii.Mhe Ummy pia ametembelea Chuo cha Maafisa Tabibu na Chuo cha uuguzi vilivyoko Masasi.
  IMG-20160331-WA0025
  Waziri Ummy akiongea na wagonjwa aliowakuta wakisubiri huduma katika hospitali ya Mkomaindo Masasi.
  Mohammed Bakari
  Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari akizungumza na Watumishi wa Afya Ndanda Mission katika ziara aliyoambatana na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.
  Mohammed Bakari
  IMG-20160331-WA0023
  Baadhi ya watumishi wa afya wakimsikiliza kwa makini Waziri wa afya Mh.Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati ziara yake tar 30 Machi.
  Ummy Mwalimu
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wakinamama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi alipokua akikagua maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
  Mussa Rashid
  Kaimu Mganga mkuu Halmashauri ya mji wa Masasi DK. Mussa Rashid akitoa taarifa kwa Waziri wa afya alipotembelea chumba cha vipimo katika hospitali hiyo. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari.
  Ummy Mwalimu
  Waziri Mh. Ummy Mwalimu akibadilisha mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Bernard Nduta. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa Ndanda, Fr. Silvanus Kessy.

  0 0
 • 03/31/16--07:05: Article 9


 • 0 0

   Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama akigawa Fulana za Vodacom kwa wanafunzi wa Nganza Sekondari katika Tamasha la michezo la shule hiyo waalilolidhamini jijini Mwanza jana. 
   Kanda: Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom. Picha na Lordrick Ngowi
    Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishndana kukimbia na magunia jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom.
   Halima Juma na Jesca Balakekenwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishindana kula keki na soda jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom. 

   Muntancy Rashidi na Rosemery Yohana wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishindana kula chakula jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom
   Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza, Dativa Anold  akicheza jana kwenye tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom lililofanyika katika uwanja wa shule hiyo.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza, Christopher Gachuma akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo jana kwenye tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom lililofanyika katika uwanja wa shule hiyo.
   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakifatilia michezo iliyokuwa ikiendelea jana kwenye tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom lililofanyika katika uwanja wa shule hiyo. Picha na Lordrick Ngowi.

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
  MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA
  Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongezaSerikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kujenga jengo zuri la tatu la abiria (TB III)  litakaloboresha zaidi huduma za usafiri wa anga.

  Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla (Makete) wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea jengo hilo katika ziara yao ya kukagua miradi ya Serikali mwanzoni mwa wiki.

  Jengo hilo linajengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa Euro milioni 254 (sh. Bilioni 560) za mkopo kutoka Benki ya HSBC ya Uingereza na CRDB kwa dhamana ya Serikali ya Tanzania na Uholanzi.

  Tayari TAA imeshamlipa Mkandarasi wake, Bam International ya Uholanzi, Euro milioni 96 baada ya kukamilisha asilimia 60 ya kazi. Jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ipo katika hatua za mwisho.

  Mwenyekiti Sigalla na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo walieleza kuridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kujenga jengo hilo linalotarajiwa kukamilika Desemba 2017.

  Baada ya kufurahishwa na kazi hiyo nzuri na kushauri uboreshaji zaidi wa utendaji, wabunge waliahidi kuisukuma Serikali iiwezeshe zaidi TAA kifedha ikamilishe miradi yake kwa wakati.
  0 0

  Na Mwandishi wetu.
  SERIKALI imesema kuwa italipa kipaumbele suala la uhakiki wa mali za viongozi wa umma  kwa kuiwezesha Sekretarieti ya Maadili ya viongozi kufanya kazi zake  kwa ukamilifu kwa mujibu wa Sheria ya  Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma kujua majukumu, mafanikio na changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo  ili wakifika bungeni waweze kuisemea.

  “Suala la uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi tutahakikisha linapewa kipaumbele katika Awamu hii ya tano ya  uongozi,” amesema.
  Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, Serikali itajitahidi kuongeza jitihada ili uhakiki  wa rasilimali na madeni ya viongozi wa Umma ufanyike,  pamoja na kuiongezea Taasisi hiyo bajeti ya kutosha.

  Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukum u ya ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe  Salome Kaganda amesema viongozi wengi wanarejesha fomu za raslimali na madeni, ila wapo wachache wanaoshindwa kurejesha fomu hizo.
  Amesema, “Tangu mwaka 2005/06 hadi mwaka 2014/15 tumesambaza  fomu 78,786, lakini fomu zilizorejeshwa ni 60,948 ambazo ni sawa na asilimia 77 ya fomu zote zilizosambazwa.”


  Aidha Kamishna huyo amewaambia  wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge kuwa tangu mwaka 2013 hadi 2015 Sekretarieti yake haikufanya uhakiki wa rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma kutokana na  ufinyu wa bajeti.
  Kwa upande wao baadhi ya Wajumbe wa kamati wamesema kuwa wataishauri serikali kuiongezea Sekretarieti bajeti ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sharia.

  Pia wamependekeza kufanyiwa maboresho Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 ili iwe na nguvu zaidi na kuwaruhusu kuwafikisha mahakamani viongozi wanaokiuka sharia hiyo.

  Sekretarieti ya Maadil  ilianza kufanya kazi rasmi mwezi Julai, 1996 ikiwa na jukumu la msingi la kujenga na kukuza uadilifu miongoni mwa Viongozi wa Umma kwa kusimamia utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma Na 13 ya mwaka 1995.

  0 0

   Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii wakipitia taarifa ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe pwani na maendeleo yake.
  Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha  taarifa ya shirika hilo  kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba.Picha na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.

    Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Bw.Peter Serukamba katika viwanja vya urushaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Kisarawe


  0 0


  Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa, Bengi Issa mwenye kilemba, akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega kushoto kwake kwa ajili ya kuangalia namna ya kushirikiana naye kuwasaidia na kuwawezesha wananchi wa Mkuranga.
  MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani, Abdallah Ulega, jana amefanya kikao na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Taifa (NEEC), Bengi Issa, kwa ajili ya kutafuta fursa ya kuwawezesha wananchi wilayani humo.
  Mbunge wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa (NEEC), Bengi Issa, hayupo pichani.
  Kikao hicho pia kilihusisha Mkurugenzi wa Uwezeshaji, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuranga, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili namna ya kusaidia vikundi vilivyosajiliwa 285, vikundi vya vicoba 109, ufugaji wa nyuki, vikundi vya wanawake, vijana na waendesha bodaboda.
  Akizungumza baada ya kikao hicho kumalizika, Ulega aliyewahi pia kuwa Mkuu wa wilaya Kilwa, alisema kwamba lengo ni kuona wanananchi wa Mkuranga wanapiga hatua kutoka kwenye hali ya ukata na kufikia kiwango kizuri, sanjari na kufanikisha maendeleo kwa wananchi wote.
  Alisema kwamba kikao hicho kimemalizika kwa mafanikio ambapo ilishauriwa kuwa vikundi vya kukopeshana (VICOBA) inabidi viwekwe chini ya mwamvuli mmoja utakaoviwakilisha vyote.
  “Hili litakapofanyika, Benki ya Posta Tanzania ina utaratibu wa kutoa mikopo ya riba ndogo kupitia mwamvuli huo unaowakilisha vikundi vyote kwa pamoja, tukiamini kuwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ndoto zetu.
  “Lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunaiweka Mkuranga katika kiwango kizuri ukizingatia kwamba wilaya hii ipo karibu na jiji la Dar es Salaam, hivyo inaweza kukua kwa kasi kwa sababu mtu anaweza kuishi Mkuranga na akafanya kazi au kuingia na kutoka kwa urahisi wilayani kwetu,” alisema.
  Aidha imeshauriwa pia kuanzisha SACCOS ya wafugaji wa nyuki ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo ya vifaa kwa ajili ya ufugaji wa kisasa wa nyuki, ambapo wana vikundi wanatakiwa kuandaa mpango kazi wao utakaopelekwa Benki ya Maendeleo kwa ajili ya mkopo, ikiwa na lengo la kuhifadhi misitu na kuacha utafutaji wa kipato kwa njia ya kukata miti ili kuzalisha mkaa.

  0 0

    Mkuu wa Hifadhi ya Saadani Bw. Hassan Nguluma akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Maliasili, Utalii na Ardhi ramani ya Hifadhi hiyo wakati kamati hiyo ilipoitembelea Hifadhi ya Saadani pamoja na kukutana na Menejimenti ya TANAPA. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani (mweye miwani) na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Atashasta Nditiye.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya TANAPA wakati kamati hiyo iliopotembelea Hifadhi ya Saadani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani.

   Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.

  1.     Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.(Picha na Ofisi ya Bunge)

older | 1 | .... | 811 | 812 | (Page 813) | 814 | 815 | .... | 1897 | newer