Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI-MKOANI KIGOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayohudumia wakimbizi katika Kambi ya muda ya NMC, iliyoko mkoani Kigoma, kushoto ni Mratibu wa Wakimbizi Mkoani Kigoma, Tonny Samwel Laiser.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakimbizi wa Burundi (hawapo pichani) wanaoishi katika kambi ya Mtendeli, iliyoko wilayani Kakonko mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Msimamizi wa Kambi ya muda ya NMC, Jordan Emmanuel (wa kwanza kushoto), akimuonyesha Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, jinsi mfumo wa jiko la kupikia chakula kambini hapo unavyofanya kazi.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Sehemu ya vitanda vipya vikiwa katika moja ya mabweni ya Kambi ya muda ya wakimbizi ya NMC , tayari kwa kufungwa na kuanza kutumika na wakimbizi wanaohifadhiwa kambini hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, Peter Toima Kiroya (wa kwanza kushoto), wakati walipotembelea iliyokua kambi ya Karago iliyotumika kuhifadhi wakimbizi.Kulia ni Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Mtendeli, Innocent Mwaka.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani Ofisi ndogo ya Kibondo, Dost Yousafzai(kushoto), wakati alipotembelea iliyokuwa kambi ya Wakimbizi ya Karago,Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

China yaonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati

$
0
0


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akisalimiana na mmoja wa wajumbe  kutoka kampuni  uzalishaji wa makaa ya mawe ya  Shenhua Ningxia Group Co. Limited kutoka China. (kushoto). Katikati ni Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong.



 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini. Kushoto ni Mwakilishi kutoka  Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong.



 Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong (pichani) akisisitiza jambo katika kikao hicho.


 Sehemu ya ujumbe kutoka nchini China ukifuatilia majadiliano mbalimbali  yaliyokuwa yanaendelea katika kikao hicho.




Mchimbaji wa Makaa ya Mawe kutoka Nchini Tanzania, Sara Masasi akielezea uzoefu wa kampuni  yake katika uzalishaji  wa makaa ya mawe.

 


Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Wawekezaji kutoka  katika makampuni yanayojihusisha na uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka nchini China, wameeleza nia ya kuwekeza kwenye  sekta ya nishati  nchini  ili iweze kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Waliyasema hayo katika kikao na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka  Wizara ya Nishati na Madini  pamoja na  taasisi  mbalimbali ikiwa ni pamoja  na Shirika la  Umeme Nchini (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)

Akizungumza katika kikao hicho Mwakilishi kutoka Umoja wa Wafanyabiashara katika Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong, alisema kuwa nia ya makampuni yanayojishughulisha na  uzalishaji wa nishati ya umeme ni kubaini fursa zilizopo katika sekta ya nishati nchini kabla ya kuja kuwekeza rasmi

Aliongeza kuwa  ujumbe maalum wa wawekezaji kutoka   nchini  China unatarajiwa kuwasili nchini mapema wiki ijayo kwa ajili  ya kupata  taarifa mbalimbali zenye kubainisha  fursa za uwekezaji nchini  ikiwa ni pamoja na mpango  kabambe (master plan), sera, na mpango mkakati katika sekta ya nishati, kabla ya kusaini makubaliano ya awali kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya  umeme.

Zhiyong  alisisitiza kuwa wawekezaji  kutoka China wako   tayari kushirikiana na wawekezaji wa ndani  ya  nchi kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme  ili  taifa liweze kupata  nishati ya uhakika kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.

Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo alishukuru ujumbe  huo na kueleza kuwa  fursa za uwekezaji  kwenye  sekta ya nishati ni nyingi na kuwataka kuchangamkia fursa hizo.



“Wananchi wanahitaji nishati ya  uhakika ambayo ni kichocheo cha  ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo tunawakaribisha kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kuwa  tuna vyanzo  vingi kama  vile  gesi, jotoardhi, makaa ya mawe, jua, upepo n.k,” alisisitiza Dk. Palangyo.

Prof. Mbarawa afanya ziara kushtukiza KOJ Kurasini

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones.
 Kapteni Abdulla Mwingamno (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) baadhi ya vifaa vya kituo cha kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongozana na Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones alipotembelea TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua baadhi vipuri eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini leo jijini Dar es salaam.
  Eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jiji Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).
 Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Kaimu Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Nelson Mlali kufanya uhakiki wa kampuni zinazotoa huduma mbalimbali bandarini ili kuboresha utendaji kazi na kuepuka mgongano wa maslahi binafsi minongoni wa watumishi wa bandari.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana jioni(29/03/2016) kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini.

“Mtafanyaje kazi na mtu ambaye ni mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma bandarini, hamuoni kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji Profesa Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Kaimu Meneja Msaidizi Mlali azingatie umiliki wa makampuni kulingana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Kampuni nchini (BRELA) katika zoezi la kuhakiki kampuni hizo.

Akiwa eneo la (KOJ) Kurasini, Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TPA  wabadilike na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kuboresha kuongeza ufanisi na kuliongezea taifa mapato kwa manufaa ya wananchi.

Prof. Mbarawa amewaagiza pia Mamlaka ya Bandari wanaponunua vipuri na vifaa mbalimbali vinavyohitajika bandarini hapo wazingatie vipimo sahihi kulingana na vifaa vinavyohitajika kuendeshea mitambo mbalimbali ili kulipunguzia taifa gharama zisizohitajika.

Mamlaka ya Bandari nchini ina bandari mbalimbali zilizopo katika ukanda wa bahari ya Hindi na maziwa yaliyopo nchini.

Ukanda wa Bahari ya Hindi una bandari ya kuu za Dar es salaam, Tanga na Mtwara pamoja na Bandari ndogo zilizopo Lindi, Kilwa Masoko, Mafia, Bagamoyo, Pangani na Kwale. 

Bandari nyingine ziliozo katika maziwa mbalimbali nchini ni pamoja na Ziwa Victoria lenye bandari ya Mwanza, Bukoba, Kemondo, Musoma na Nansio, Ziwa Tanganyika likihusisha bandari ya Kigoma na Kasanga wakati Ziwa Nyasa kuna bandari ya  Itungi, Manda, Liuli na Mbaba Bay. 

Ziara ya Mafuzo ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa

$
0
0
 
 Leo Jumatano tarehe 30 Machi 2016 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa chini ya Makamu Mwenyekiti Mh. Dkt. Pudenciana Kikwembe walipata fursa ya kutembelea ofisi za MKURABITA kwa ajili ya kujifunza juu ya madhumuni na shughuli za MKURABITA nchini.
 Katika ziara hiyo walipokelewa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Angela Kairuki na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Bw. Peter Ilomo
Aidha walipokea taarifa fupi kuhusu MKURABITA na maendeleo ya shughuli za urasimishaji nchini yaliyotolewa na Mratibu wa Mpango. Bi. Seraphia Mgembe.

WANAWAKE DODOMA WANUFAIKA NA ELIMU YA UJASILIAMALI INAYOTOLEWA NA MANJANO FOUNDATION

$
0
0
Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Manjano Foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa LAPF House.

Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Dodoma wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano Foundation na mkufunzi wa maswala ya Biashara mjini Dodoma yanayoendelea kwa wiki nzima.
 Washiki Kutoka Mkoani Dodoma na Maeneo Jirani wakiliskiliza kwa Makini Wakati wa Mafunzo hayo Leo.

Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani, wajiamini, watambue vyeo vyao katika familia, wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Dodoma kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Dodoma kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. 
Picha ya Pamoja Washiriki hao kutoka Mkoani Dodoma wakiwa na Mwanasaikolojia Anti Sadaka Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions africa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.

Anti Sadaka amewashauri wanawake wasiache kujifunza na waache kujibweteka baada ya mafunzo haya kuisha isipokuwa wawe makini kutafuta elimu zaidi ya kujiongezea ujuzi katika kazi zao.

WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho akifungua warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA). Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo. 

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho(katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi George Sambali (kushoto) wakiwa kwenye warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) warsha hiyo ilifanyika katika ofisi za Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wadau mbali mbali wa sekta ya usafiri wa anga wakishiriki warsha ya kujadili rasimu ya Mpango wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
 

Mdau Bryan Becon amepata nondo Aston University huko UK

$
0
0
 
Mdau Bryan Becon amepata nondo Aston University huko UK baada ya kupata Masters Degree ya Business & HR.Pichani akiwa na mdogo wake Rodney na mama yake Mrs Bekoni.Uongozi wa Giraffe Ocean View Hotel unatoa pongezi kwa mdau wetu.

Profesa Muhongo: Kamilisheni miradi ya umeme vijijini kwa wakati

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na watendaji wa wizara pamoja na kampuni ya CCC International Nigeria, (hawapo pichani) lengo likiwa ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ya kampuni hiyo katika mkoa wa Manyara.
 

Meneja mradi wa Kampuni ya CCC International Engineering Nigeria, Zhang Jiangaang (Mwenye shati jeupe) akiwasilisha ripoti ya maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili. 

Na Latifah Boma

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili kufanya kazi kwa kasi zaidi ili umeme uweze kuwafikia walengwa kabla ya mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza na watendaji kutoka kampuni ya CCC International Nigeria Limited, inayosambaza umeme katika mkoa wa Manyara, Profesa Muhongo alisema kuwa hajaridhishwa na kasi ya kampuni hiyo katika utekelezaji wa miradi ya umeme katika wilaya ya Simanjiro ambapo hakuna wateja waliounganishiwa umeme.

Pia, Profesa Muhongo amelitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kufanya kazi kwa karibu na wakandarasi hao katika kutatua changamoto zinazowakabili ili waweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Aliwataka mameneja wa TANESCO kuongeza juhudi katika kazi zao ikiwa ni pamoja na makusanyo, utatuaji wa changamoto na uunganishaji wa umeme kwa wateja, na kusisitiza kuwa meneja atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ataondolewa katika nafasi yake.

Awali, akielezea changamoto katika utekelezaji wa miradi ya umeme meneja mradi kutoka CCC International Nigeria Limited.Zhang Jiangaang, alieleza kuwa wamekuwa wakiibiwa vifaa vyao vya kazi kutokana na kuwepo kwa usalama mdogo hivyo kupelekea kutokamilisha mradi kwa wakati kutokana na hasara wanayoipata. 

AIRTEL FURSA YAFIKIA VIJANA WILAYANI NGARA

$
0
0
 Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa 3 kushoto) akimkabidhi Kanizio Annatory (katikati) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” mashine na vifaa vya kuoshea magari pamoja na sehemu ya kisasa ya kufanyia biashara, akishuhudiwa na ndugu zake pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika hafla iliyofanyika kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
 Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kwanza kulia) pamoja na wafanyakazi wa Airtel wakimwonesha Kanizio Annatory (wa pili kushoto)  sehemu ya kisasa ya kuosha magari aliyowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” baada ya kukabidhiwa mashine na vifaa vya kuosha magari katika hafla iliyofanyika kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (4 kushoto) akimkabidhi Kanizio Annatory (2 kulia) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” mashine na vifaa vya kuosha gari pamoja na sehemu ya kisasa ya kufanyia biashara, akishuhudiwa na dada yake Agnes Annatory (kulia) pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika hafla iliyofanyika kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa 3 kushoto) akimkabidhi Kanizio Annatory (katikati) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na  mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” mashine na vifaa vya kuoshea magari pamoja na sehemu ya kisasa ya kufanyia biashara, akishuhudiwa na ndugu zake pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika hafla iliyofanyika kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.


Mwanzoni mwa wiki hii Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa  iliweza kufika  katika  kijiji cha  Kumnazi wilayani Ngara mkoani Kagera  na kumfikia Kijana  Kanizio Annatory anayejishughulisha na   biashara ya kuosha magari, kwa kumpatia vifaa na kufanyiwa ukarabati wa eneo lake la kazi . Vijana wengi wanaamini maisha mazuri na fursa za kiuchumi zinapatikana mjini, lakini kwa Kijana Kanizio kupita kwa barabara katika kijiji hiki ni fursa adhimu kwake.

Airtel Fursa  umelenga katika kuwezesha vijana  wajasiriamali hapa nchini kwa kutoa msaada kwa vijana ambao wanaonyesha juhudi ya kujikomboa na changamoto za maisha katika Jamii zinazowazunguka kwa kuwapatia vitendea kazi na kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali. Airtel Fursa ni moja ya sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Airtel  katika kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii ili kukidhi matakwa ya kiuchumi, na kuunga mkono jitihada za serikali katika kubadilisha maisha ya wananchi.

Akiongea wakati wa makabidhiano afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki alisema kuwezeshwa kwa kijana huyu  kupitia Airtel fursa ni ukombozi wa kiuchumi kwa familia yake na Jamii inayomzunguka. Kama alivyokuwa amebainisha katika maombi yake kupitia mpango wa Airtel Fursa, hatua hiyo imetafsiriwa kama kichocheo cha mapinduzi ya kibiashara na fursa za kiuchumi kijijini hapa Kumnazi.

“Tunawahimiza vijana kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa hizi pale zinapojitokeza kwani baadhi ya vijana  wamekuwa wakihamia  mijini na kuacha kazi ya uzalishaji mali kufanywa na wazee na wanawake  na hivyo kukwamisha  maendeleo vijijini” aliongeza Dangio
 
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Kanizio amesema msaada huo ni mkombozi wa maisha yake  na familia huku dada yake Agnes Annatory akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.

Kanizio alisema “ nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu kwa kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa kwani nimekuwa nikipata ugumu wa kupata wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu, lakini sasa ninaamini nitapata Wateja wengi sana na kuinua biashara yangu.

Mpaka sasa Airtel Fursa toka ianze imeweza kuwainua vijana wapata2800 kwa kuwapatia vifaa mbali mbali kwa kuendeleza bishara zao na vile vile kutoa mafunzo ya biashara katika mikoa mbali mbali hapa nchi, na katika msimu huu wa pili Airtel Fursa imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kubadlisha maisha ya vijana hawa. 

JAJI MKUU WA TANZANIA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MAHAKAMA KATIKA MIKOA YA IRINGA, NJOMBE NA RUVUMA, AISIFU MAHAKAMA KANDA YA SONGEA KWA KUFANYA VIZURI.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mahakama ya Tanzania.

Mahakama ya Tanzania ni moja kati ya Taasisi iliyopo katika mchakato wa kuboresha huduma zake. Katika kufanikisha azma hii jitihada/maboresho mbalimbali yameendelea kufanyika ili kuwezesha Mhimili huu muhimu kuwa na mazingira rafiki ya utoaji haki kwa wananchi.

Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alitembelea katika Mahakama za mikoa ya Iringa, Njombe pamoja na Ruvuma, lengo la ziara ikiwa ni kukagua na kujionea hali ya utendaji wa Mahakama na mwenendo wa uendeshaji wa mashauri.

 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Songea.
 
Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu alipata nafasi ya kutembelea Mahakama Kuu Songea, Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mahakama ya Wilaya Songea. Mahakama ya Wilaya Mbinga, Mahakama ya Wilaya Nyasa inayotarajiwa kuanza kazi hivi karibuni na baadhi ya Mahakama za Mwanzo.

Mhe. Jaji Mkuu aliongozana na Watendaji wengine wa Mahakama katika ziara yake ambao ni; Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Msajili Mkuu pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Wote walipata fursa ya kujionea hali halisi ya miundo mbinu ya Mahakama ikiwa ni pamoja na kupata taarifa za Mahakama hizo kutoka kwa Jaji Mfawidhi/Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hizo.

 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa kwanza kushoto) akipata taarifa fupi ya Mahakama Kanda ya Songea kutoka kwa Mhe. John S.Mgetta, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea (aliyesimama), mara baada ya kuwasili Mahakama Kuu kanda ya Songea.

Akisoma taarifa yake mbele ya Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. John Mgetta, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Songea alisema kuwa Kanda yake ina Mahakama Kuu moja (1), Mahakama ya Hakimu moja (1) ya Mahahakama za Wilaya tano (5) ambazo ni Songea, Namtumbo, Tunduru, Mbinga na Mahakama ya Wilaya Nyasa.

Hata hivyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. John Mgetta alikiri Mahakama yake kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi hususani Makarani na ubovu wa majengo ya Mahakama, kwani hayatoshi na ni machakavu.

Mhe. Jaji Mkuu, Kanda ya Songea inakabiliwa na uhaba wa watumishi, hususani makarani. Ukiachia mbali changamoto hii tunakabiliwa pia na uchakavu wa miundombinu ya majengo.

 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (kushoto), Mhe. John S.Mgetta Jaji Mfawidhi Kanda ya Songea (kulia), wakisoma majalada ya kesi katika Mahakama ya Mwanzo Kigonsera mkoani Songea.

CHUO CHA UTALII KUANZA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA.

$
0
0
CHUO cha utalii chenye kampasi tatu ambazo ni Kampasi ya Bustani, Kamapasi ya Temeke na Kampasi ya Arusha wameanza kudahili (kuandikisha) wanafunzi wapya kwa 2016/2017.

Afisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma wenye sifa za kusoma chuo hicho amewaomba watembelee tovuti ya Baraza la ufundi la Taifa (NACTE) www.nacte.go.tz
Afisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusina na chuo hicho kuwa na kozi tofauti tofauti zinazoweza kuwasaidi wananchi na hata kujiali weyewe kutokana na mafunmzo yanayotolewa katika chuo hicho. Kulia ni Meneja wa chuo cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam, Steven Madenge.
Meneja wa chuo cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam, Steven Madenge akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. kushoto ni fisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma.
Mkurugenzi wa Mfumo wa shughuli za kitaalam wa chuo cha Utalii, Naiman Mbise akifafanua jambo mbele ya waadnishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Afisa mtendaji Mkuu wa chuo cha Utalii, Rosada Msoma (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kutoka kushoto ni Msajili wa chuo cha utalii, Ishaka Perpetua, Mkurugenzi wa Mfumo wa shughuli za kitaalam wa chuo cha Utalii, Naiman Mbise na Kulia ni Meneja wa chuo cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salaam, Steven Madenge.

Tanzania yapokea msaada wa shilingi bilioni 116.4 kutoka Japan.

$
0
0


 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano walizosaini na Serikali ya Japan utakaoitakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akisaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.
 Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam ambao utaiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.(Na Eleuteri Mangi-MAELEZO).

 Na Eleuteri Mangi-MAELEZO


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini hati mbili za makubaliano na Serikali ya Japan itakayoiwezesha Tanzania kupata kiasi Yen Bilioni 6 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 116.4 za Kitanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile alisema mkataba wa kwanza utasaidia katika kukamilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17.


Dkt. Likwelile alisema kuwa msaada huo unalenga kuweka mazingira rafiki ya kwa wafanyabiashara, kuboresha masoko na kuwezesha mazingira ya ushindani katika utengenezaji wa ajira nchini.


Mkataba wa pili  unahusu masuala ya kiufundi  yatakayotumika katika kufanya marekebisho ya mkataba uliosainiwa  Octoba 20, 1966, kwa kuzingatia sheria nyingi zimebadilika, kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano itasaidia kutabadilisha baadhi ya vifungu vyenye jina Tanzania na kuweka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kujumuisha pande zote mbili za Muungano katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini. 


Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha baadhi ya vipengele vya mkataba uliopita ikiwemo kipengele cha usambazaji wa madawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya sasa ya wataalamu kutoka nchini Japan kuweza kuja kufanya kazi za kujitolea hapa nchini Tanzania.


Katibu Mkuu Dkt. Likwelile ameishukuru Serikali ya Japan na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyopangwa ili kuweza kuwa na tija na kuwaletea maendeleo Watanzania.


Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japan ina imani kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.


Balozi Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani inaunga mkono juhudi za Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika masuala ya viwanda na mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji  kuwekeza nchini Tanzania.



Adha amesema kuwa Japan itaendelea kuwaleta vijana wanaojitolea katika sekta ya uchumii na ya kijamii jambo limekuwa likitekelezwa tangu mwaka 1969 ambapo hadi sasa idadi ya vijana hao wa kujitolea imefikia zaidi ya 1500. 

UGONJWA WA ENDOMETROSIS WAWATESA WANAWAKE.

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk. Hamis Kigwangalla akizungumza na wanafunzi wa sekondari (hawapo pichani) juu ya ugonjwa wa Endometrosis katika semina hiyo kutoa elimu ya ugonjwa iliyoratibiwa na Miss Tanzania 2001, Millen Magese ambaye ni Mhanga wa Ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.


Mkuruenzi Millen Magese Foundation na Miss Tanzania 2001, Millen Magese akizungumza wakati wa semina ya wanafunzi wa sekondari juu ya ugonjwa wa Endometrosis ambapo yeye ni mhanga wa ugonjwa huo iliyofanyika leo katika shule sekondari Tulian Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Dk. Hamis Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania 2001, Millen Magese na wageni walikwa katika semina ya utoaji wa elimu ya ugonjwa wa endometrosis leo jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda, Globu Jamii.
IMEELEZWA kuwa kutibu ugonjwa wa Endometrosis ni gharama kubwa na serikali pekee yake haiwezi kushughulikia tatizo hilo.

Ugonjwa huo huwapata wanawake wakati wa hedhi na kufanya mwanake kukosa furaha na kutibu kwake ni gharama kubwa.

Akizungumza na leo katika semina kutoa uelewa kwa wasichana 400 iliyoandaliwa na Taasisi ya Miss Tanzania 2001 Millen Magese, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kuwa ugonjwa wa Endometrosis unasababisha ugumba kwa wanawake.

Amesema kugundua ugonjwa huo unachukua kati ya miaka sita hadi 10 na kati ya wanawake 100 wenye ugonjwa huo nusu hawawezi kupata watoto.

Dk.Kigwangalla amesema kutambua ugonjwa huo kwa wataalam inachukua miaka saba hadi 10 hivyo kunahitajika elimu hata maeneo vijijini wanawake wanaweza wanaugua lakini hawajui.

“Wahenga wanasema raha ya mwanamke na kuzaa mtoto wake mwenye hivyo kuwa na ugonjwa unafanya mwanamke akose furaha katika maisha yake”amesema Kigwangalla.

Mkurugenzi wa Millen Magese Foundation,Miss Tanzania 20O1, Millen Magese amesema kuwa amefanyiwa operesheni mara 13 na kuamua kutoa elimu juu ya ugonjwa huo.

Amesema kuwa wanawake wengi wanasumbuliwa na ugonjwa huo lakini wanasema ni siri wakati ni ugonjwa wenye maumivu makali..

WATAALAMU WA MOYO KUJADILI JINSI YA KUKABILI, APRILI 21 NA 22 KATIKA UKUMBI WA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Madaktari bingwa wa  ugonjwa wa Moyo, Robart Mvungi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusia na  mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Aprili 21 na 22 mwaka huu, Amesema kuwa Mkutano huo utakuwa kwaajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa wa Moyo ambao sio wa kuambukizwa. 

Pia amesema kuwa mkutano huo utahudhuliwa na Madaktari bingwa ugonjwa wa moyo  pia watatumia muda huo kuelimisha jamii ili kuweza kupunguza ongezeko la ugonjwa wa moyo hapa nchini.
Kushoto ni Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete, Ruben Muta, Mwaandaaji wa mkutano, Adeline Ndesanja na Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete,Tulizo Sanga.
 Daktari Bingwa ya moyo katika hospitali ya Mhimbili katika Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete,Tulizo Sanga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari( hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo.

Article 3

$
0
0
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimpatia hati ya kiwanja cha Vikuruti, mteja wao Ibrahim Yusuph Ismail, nyumbani kwao Kariakoo jijini Dar es Salaam, leo mchana. Kwa wiki hii tu Bayport imeamua kuwapelekea hati za viwanja wateja wao katika maeneo yao ya makazi na maofisini kwao.

Na Mwandishi Wetu, Dar esSalaam
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wateja wa Bayport waliojipatia viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani wameendelea kupewa hati zao, huku safari hii wakipewa hati kwenye maeneo wanayopatikana ikiwamo majumbani na maofisini. Hatua za kuwapelekea hati hizo wateja wao ni kitendo cha kuthamini uwapo wa wateja wao wanaoendelea kuiamini Bayport Financial Services katika bidhaa zake za mikopo ya fedha, bila kusahau huduma ya mikopo ya viwanja vyenye hati inayotolewa na taasisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau wa ardhi walioingia mikataba na Halmashauri unapopatikana mradi wa viwanja kwa ajili ya watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi, wajasiriamali na Watanzania kwa ujumla.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabiti Mndeme, kushoto akizungumza jambo wakati anamkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao Neema Jameson Nawita, jijini Dar es Salaam leo mchana.


Akizungumza wakati wa kutoa hati kwa wateja watatu leo jijini Dares Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema jambo kubwa la miradi ya viwanja kwenye taasisi yao ni kuona weteja wao wanapata hati ili kuweka ubora wa huduma zao, ikiwa ni sehemu muafaka ya kufuta migogoro ya ardhi kwa kununua viwanja vyenye hati. Alisema kwa wiki mbili mfululizo wamekuwa wakiendelea kutoa hati kwa wateja wao, huku kwa wiki hii tu, taasisi hiyo ikifika mbali kwa kujenga imani na kwenda sambamba na wateja hao, wakaona umuhimu wa kuwathamini na kuwataka wachague maeneo wanayoona wanaweza kupokea hati zao, iwe ni maofisini kwao au kwenye maeneo ya makazi.

Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita, kulia akipokea hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, aliyokabidhiwa leo na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita,kulia akizungumza na waandishi baada ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi,wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kushoto ni Thabit Mndeme, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani mteja wao Hassan Omary Hamis, jijini Dar es Salaam, leo mchana.

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhi hati ya kiwanja kwa Hassan Omary Hamis
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akizungumza jambo wakati anakabidhi hati za viwanja kwa wateja wao wa Bayport Financial Services hawapo pichani leo jijini Dar es Salam.

“Huu ni utaratibu tulioamua kwa wiki mbili hizi kwa wateja waliokuwa wanapokea hati tuwafikishie kwenye maeneo yao ili waone taasisi yetu inawathamini na kuwashukuru kwa sababu wamekuwa wakiendelea kuunga mkono bidhaa zetu zote, ikiwamo huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti tulivyoanzisha mwaka jana na mwaka huu tukianzisha huduma za viwanja katika maeneo ya Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kilwa na Kigamboni. “Huduma hizi ni nzuri kwa Watanzania wote mahala popote walipokuwa wanaweza kukopa au kununua viwanja hivi kwa njia pia ya fedha taslimu, ambapo kwa (Kimara Ng’ombe) Bagamoyo mita moja ya mraba inauzwa Sh 10,000, (Msakasa) Kilwa Sh 2000, (Boko Timiza) Kibaha Sh 9000, (Tundi Songani) Kigamboni Sh 10,000 na (Kibiki na Mpera) Sh 4500, ambapo huduma zetu zinapatikana pia kwenye matawi yote yaliyoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara,” Alisema Mndeme.

Naye Neema Jameson Nawita aliwashukuru Bayport kwa kumpatia hati yake bila usumbufu wowote, akisema huduma zao za viwanja zinaonekana kuandaliwa vyema huku zikiwa hazina usumbufu wowote katika kuandikishwa hadi upewaji wa hati zao. “Nimefurahi kwa sababu nimefanikiwa kuwa miongoni mwa Watanzania waliopewa hati za viwanja vya Vikuruti baada ya kununua kiwanja hicho mwaka jana na nzuri zaidi nimepata bahati kubwa kwa sababu nimeletewa hati hadi eneo la ofisi yangu,” Alisema.

Naye mjasiriamali Ibrahim Yusuph Ismail aliipokea hati yake shangwe na kusema kufanikiwa kununua kiwanja cha Vikuruti na kupewa hati yake bila usumbufu ni hatua nzuri na mwendelezo wa kujiendeleza kwa kutumia rasilimali bora ya ardhi.

Mteja mwingine aliyezungumzia hatua hiyo ya upewaji hati ni Hassan Omary Hamis, ambaye aliwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa bora ya uwekezaji wa ardhi kwa kujenga nyumba za makazi na za biashara ili waongeze wigo wa kipato chao.



“Tusiogope kuwekeza kwa sababu ni jambo la msingi ukizingatia kwamba zipo taasisi zenye kiu ya maendeleo wakiwamo Bayport, maana si lazima mtu anunue kwa pesa taslimu, ila anaweza kununua kiwanja kwa njia ya mkopo usiokuwa na usumbufu na ukiwahusu watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali,” Alisema.

GSM YASAIDI WATOTO WENYE UGONJWA WA MOYO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MHIMBILI.

$
0
0
Mwakilishi wa Mkuu wa Taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo Cha Mifupa Muhimbili MOI, Dk. Othuman Kiloloma (kulia) kwa ajili ya kununua vifaa vya matibabu, Dar es Salaam jana wa (Pili kushoto) ni Ofisa habari wa Taasisi hiyo, Khalfan Kiwamba, na mratibu wa hafla hiyo, Kibwana Matokeo. 

ASKARI POLISI ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUGUNDULIKA ALIJIPATIA AJIRA KWA VYETI VYA KUGUSHI.

$
0
0
Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia katika jeshi la Polisi mkaoni Ruvuma F 5425 PC Emmanuel Nyagoli ( 35), anatafutwa na Jeshi hilo kwa kosa la kujipatia ajira kwa vyeti vya Kugushi, Na kwasasa hajulikani alipokimbilia. Taarifa zaidi hii hapa RUVUMA TV.

MWANZA NA ARUSHA YAONGOZA WATUMISHI HEWA.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


MKOA Mwanza waongoza kuwa na watumishi  hewa 334  ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi  hewa 2,702.

Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo kuwa na watumishi hewa kukosekana kwa watumishi hewa katika mkoa wa shinyanya imetokana na mikakati ya mikoa hiyo kila idara kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Killango kuwa viongozi walioanza katika mikoa huo walijipanga katika kuondokana na watumishi hewa.
Mkoa wa Songwe kukosekana kwa watumishi hewa kunatokana na upya wake na mkuu wake mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita.

Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.

Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa kuondokana na matumizi yasio na ulazima ili fedha hizo zitumike katika matumizi ya msingi.

Amesema kuwa zoezi hilo liweze kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kushughulika na watoro ambao wanalipwa fedha wakati hawafanyi kazi,
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema wote ambao wamehusika na hujuma za mishahara wafikishwe katika vyombo vya dola na mkoa wake umeanza kutekeleza.
 Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Mikoa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza baada ya kukabidhi majina hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadik  akikabidhi majina hewa kwa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene  baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa , jijini Dar es Salaam.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa Mikoa na Watendaji wa TAMISEMI wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

VIJANA WATAOFANYA VIZURI KATIKA UONGOZI KUPEWA TUZO.

$
0
0
Mratibu wa Tuzo za Taypa,Irene Amos akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kutambua uongozi wa vijana na jukumu lao katika soko la ndani la ajira kwa kuwapa tuzo za mwaka kwa kijana ambaye amefanya vizuri katika majuku yake ili waweze kuwa mfano wa kuigwa, aidha amesema tuzo hizo zitakuwa chanzo cha motisha kwa ajili ya wataalamu vijana kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha malengo ya muda mfupi na muda mrefu, leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni TM,Group, Sinior Partiner,Mohammed Jaffer.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali,Lilian Makoi akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, (hawapo pichani) juu ya washiriki wa tuzo hizo kuwa wawe raia wa Tanzania,zoezi la kupendekeza litaanza rasmi Aprili 1 mwaka huu katikati ni TM,Group, Sinior Partiner,Mohammed Jaffer na kulia ni Mwanzilishi wa Hope for the Blind Trust Margareth Maganga.
TM,Group, Sinior Partiner,Mohammed Jaffer akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mwanzilishi wa Hope for the Blind Trust Margareth Maganga.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii ).

TANZANIA YAPATA MEDALI MBILI ZAIDI KATIKA MASHIDANO YA KUOGELEA YA KIMATAIFA YA AFRIKA KUSINI

$
0
0
Waogeleaji Josephine”Jojo” Oosterhuis aliyenyosha mkono juu akiwa na wenzake, Isabella Kortland (wa pili waliosimama kutoka kushoto), Jacqulline Kortland ambaye ni pacha wa Isabella (wa tatu kutoka kulia waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kunyakua medali tatu katika mashindano ya kuogelea ya Afrika Kusini. Wengine katika picha ni kocha Michael Livingstone (wa kwanza kushoto waliosimama), kocha Alex Mwaipasi (wa pili kulia waliosimama) na meneja wa timu, Inviolata Itatiro wa kwanza kulia waliosimama. Pia katika picha ni Marin de Villard na Celina Itatiro (waliokaa).
Nyuso za furaha: Meneja wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS), Inviolata Itatiro akiwa na makocha, Alex Mwaipasi (kushoto) na Michael Livingstone mara baada ya ushindi wa medali tatu katika mashindano ya kuogelea ya Kimataifa ya Afrika Kusini.

Nyota ya Tanzania katika mchezo wa kuogelea imeanza kung’ara baada ya kupata medali tatu katika mashindano ya kimataifa ya kuogelea ya Afrika Kusini yanayondelea katika mji wa Johannesburg.Walioshinda medali katika mashindano hayo ni, Josephine Oosterhuis, Isabella Kortland na Jacqueline Kortland katika mashindano hayo ambayo yanashirikisha waogeleaji zaidi ya 750 kutoka nchi mbalimbali kusini mwa Afrika.

Mbali ya Tanzania na wenyeji, Afrika Kusini, mashindano hayo pia yalishirikisha timu kutoka Zimbabwe, Msumbiji, Angola, na Namibia. Josephine alishinda medali ya dhahabu katika fainali ya mita 100 breaststroke kwa kutumia muda wa 1.21.79 huku Jacqueline alishinda medali ya shaba kwa kushika nafasi ya tatu kwa kutumia muda wa 1.22.91.

Nafasi ya pili ikikwenda kwa Deane Toerien wa Afrika Kusini aliyetumia muda wa 1.22.70 na kutwaa medali ya fedha. Isabella Kortland alishinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya mita 50 katika staili ya backstrokes kwa kutumia muda wa 33.25 kuwashinda Georgy Turner na Zantia Bainabridge wa Afrika Kusini ambao walifungana kwa kutumua muda wa 33.84 kila mmoja.

Waogeleaji Celina Itatiro hakuweza kutwaa medali pamoja na kumaliza akiwa wa tisa kwa kutumia muda wa 1.29.26 katika mita 100 butterfly, Marin de Villard alimaliza wa tisa katika staili ya backstroke kwa kutumia muda wa 37.43.

“Tumefanya vizuri sana, si unajua mashindano haya ni magumu kutokana na ushindani uliopo, Afrika Kusini na nchi nyingine inatumia kutafuta waogeleaji wao ambao watakwenda kushindana katika mashindano ya Cana na wameleta waogeleaji wengi, sisi tumeleta 15 na mpaka sasa tuna medali 3, ni mafanikio,” alisema meneja wa timu hiyo Inviolata Itatiro.Kocha Alex Mwaipasi alisema kuwa wamefurahishwa na matokeo hayo na wanaamini kuwa wakiendelea na msimamo wao wa kushiriki mashindano mengi ya kimataifa, basi watafika mbali sana ndani ya miaka mitano au kumi.

“Mbali ya medali, hapa waogeleaji wanasaka nafasi ya Cana, baadhi ya waogeaji wetu ndiyo kwanza wanaogelea katika bwawa la mita 50, wengine mara ya kwanza, hivyo kuna changamoto,” alisema Mwaipasi.

Kocha Michael Livingstone aliwashukuru wazazi wa waogeleaji kwa kufanikisha safari hii na kuifanya Tanzania kuingia katika chati ya mchezo wa kuogelea. “Wazazi wamejitahidi kwa kweli, wengine wameshindwa na wengine wameambatana na watoto wao kuja hapa kwa ajili ya kuitangaza Tanzania, tumefanikiwa,” alisema Michael.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images