Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

TANZANIA NA KUWAIT ZASAINI MAKUBALIANO YA SAFARI ZA ANGA JIJINI DAR LEO.

0
0
 aziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za Anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait (Kushoto katikati).Wengine katika picha hiyo ni Maafisa kutoka Tanzania na Kuwait. 
Picha na Eleuteri Mangi –MAELEZO.

BALOZI HAULE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO.

0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini Kenya, Mhe. TADUMI ON'OKOKO, kwenye Ubalozi wa DRC Nairobi leo, Mhe. ON'OKOKO, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao Kenya, alifariki dunia tarehe 20 Machi 2016 huko Paris, Ufaransa, ambako alikuwa anatibiwa. Anayeshuhudia ni Kaimu Balozi wa DRC, Mhe. Michel Mubare, ambaye alifahamisha kuwa marehemu atazikwa Kinshasa baada ya mipango kukamilika.
 Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule (Kulia) akimfariji Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Michel Mubare,  baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Kenya, Mhe. Tadumi On'okoko jijini Nairobi leo.

RAIS DKT. MAGUFULI APATA CHAKULA CHA MCHANA MGAHAWANI UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AKIWA NJIANI KUELEKEA CHATO.

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa MWanza  Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg Anthony Diallo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiondoka baada ya kupata  chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamopja na kwaya ya Vijana ya Makongoro na viongozi wa dini katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.
PICHA NA IKULU.

TAARIFA ZA WATUMISHI HEWA ZATUA OFISI YA RAIS-TAMISEMI.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS.
Mtakumbuka kwamba leo ni siku ya 15 ya utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa la kuwataka kuwaondoa kwenye malipo watumishi hewa.
Natumia fursa hii kutoa taarifa kwa Umma kuwa Agizo hilo limetekelezwa kama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alivyoagiza.  

Taarifa za watumishi hewa tayari zimewasilishwa kwa maandishi Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuanzia mwishoni mwa wiki.

Kwa sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi na zitakapokuwa tayari kwa matumizi ya Umma zitatolewa kwa Vyombo vya Habari kwa lengo la kuufahamisha Umma.

Hivi sasa taarifa hizi zinakusanywa kwa pamoja ili kupata idadi kamili.
Wakati huo huo, napenda kuufahamisha Umma kuwa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) yameanza kufanya mazoezi ya utoaji huduma toka siku ya alhamisi tarehe 24/03/2016.  Tunategemea wiki hii mtoa huduma ataendelea kuongeza idadi ya mabasi ya kufanya mazoezi kabla zoezi hili halijaanza rasmi.
Imetolewa:
George B. Simbachawene (Mb)
Waziri wa Nchi
29/03/2016.

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI 110 KUFUTWA.

0
0

KUFUTWA USAJILI KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (110) KWA KUJIENDESHA KINYUME CHA SHERIA KUANZIA TAREHE 30/03/2016.

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali amefuta usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiesrikali (NGOs) 109 kwa kuendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005. Mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi, kutolipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.

Kwa taarifa hii, Mashirika yaliyotajawa hapa chini yamefutiwa usajili na yataarifiwa kusitisha shughuli zao kuanzia tarehe ya tangazo hili (30/03/2016). Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayachukulia hatua stahiki Mashirika ambayo yatakaidi amri hii na kuendelea na shughuli za NGOs kinyume na Sheria husika.

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (109) YALIYOFUTIWA USAJILI KUANZIA TAREHE 30/3/2016  NI KAMA IFUATAVYO:

1.THE MEDICAL WOMEN ASSOCIATION OF TANZANIA (MEWATA)
2.AFRICAN GENDER AND GOOD GOVERNANCE ALLIANCE
3.AFRICAN WILDLIFE FOUNDATION
4.AGENDA FOR ENVIRONMENTAL AND SUSTAINABLE DEVELOPMENT
5.ANTIOKIA MISSION INTERGRATED SOCIAL DEVELOPMENT
6.BUSEGWE DEVELOPMENT ASSOCIATION
7.BUTIAMA DEVELOPMENT ASSOCIATION
8.CARE FOR THE CHILD (CFC)
9.CHAKUFAA DEVELOPMENT FOUNDATION
10.CHAMA CHA KUSAIDIA WATOTO YATIMA MAKAMBAKO
11.COMFORT WOMEN RELIEF FOUNDATION
12.COMMUNITY AGRICULTURAL ACTION SERVICES CENTRE
13.COMMUNITY SERVICES SUPPORT OF TANZANIA (COSESU-T)
14.DAUGHTERS OF ZION FOUNDATION LTD
15.DEFENCE OF HUMAN RIGHTS CITIZEN RIGHTS
16.DEVELOPERS OF SUSTAINABLE COMMUNITY BASED ACTIVITIES (DESCOBA)
17.DIANA WOMEN EMPOWERMENT ORGANIZATION
18.EDNA DEVELOPMENT FOUNDATION
19.EMPOWERMENT AGAINST POVERTY AND HIV/AIDS
20.EMPOWERMENT FOR THE DISADVANTAGED COMMUNITY (EDC)
21.ENVIRONMENTAL MANAGEMENT AND NUTRITIONAL SERVICES AGENCY (EMA-NUSA)
22.GLOBAL VISION TANZANIA (GVT)
23.GRASSROOTS INITIATIVE FOR YOUTH AND ELDERLY DEVELOPMENT ORGANIZATION (GIYEDO)
24.HOPE MISSION OF DEVELOPMENT FOR THE DISABLED (HOMIDED)
25.HURUMA CHILD MINISTRY CENTRE
26.HURUMA REHABILITATION PROGRAMME
27.IMANI WOMEN ECONOMIC EMPOWERMENT ASSOCIATION (IWEA)
28.INTERNATIONAL MEDICAL CORPS
29.IZAAZ MEDICAL PROJECT
30.JUMUIYA EDUCATION BAGAMOYO (JEBA)
31.JUNIOR ACHIEVEMENT OF TANZANIA
32.KAMACHUMU IN NGEMU AGENDA (KINGA)
33.KILIMO HAI TANZANIA (KIHATA)
34.KUZA EDUCATION DEVELOPMENT
35.MANDATE AFRICA FOUNDATION
36.MASASI FARMERS ADVOCACY ASSOCIATION (MAFADA)
37.MAZINGIRA INSTITUTE OF TANZANIA (MAI-TANZANIA)
38.SUMBAWANGA ESCARPMENT ENVIRONMENTAL CONSERVATION ORGANIZATION (SEECO)
39.MFUKO WA MAENDELEO YA WAISLAM MKOA WA RUVUMA
40.MKONGO MLOKA DEVELOPMENT ASSOCIATION
41.MOROGORO ENVIRONMENTAL CONSERVATION ACTION GROUP
42.MOROGORO ENVIRONMENTAL CONSERVATION ACTION GROUP
43.MUUNGANO DEVELOPMENT ASSOCIATION (MUDEA)
44.MWAKALELI COMMUNITYDEVELOPMENT ORGANIZATION (MWACODO)
45.MWALIMU NYERERE UWC FOR SELF RELIANCE
46.MWANANYAMALA WOMEN LDEVELOPMENT GROUP (MWAWODE)
47.NATIONAL LIFE DEVELOPMENT ASSOCIATION
48.NJOMBE DEVELOPMENT ORGANIZATION (NDO)
49.NORWEGIAN PEOPLE AID
50.OLOF PALME ORPHANS CENTRE
51.DEVELOPMENT AGENCY PROBATION TIME RESEARCH
52.PANGOLIN ELITE SPORTS FOUNDATION
53.PARTGAGE TANZANIA
54.PERIPHERY AREAS DEVELOPMENT ASSOCIATION (PADA)
55.POVERTY ALLEVIATION AND AGRICULTURAL DEVELOPMENT (PADEFO)
56.POVERTY FIGHTERS AND CHARITABLE GROUP
57.POVERTY FIGHTERS AND DEVELOPMENT SOCIETY OF TANZANIA (POFIDESO)
58.PRICESS AGNES FOUNDATION
59.PROGRESS ASSOCIATION TANZANIA (PATA)
60.PROMOTION OF FARMING AND ORPHANS EDUCATION IN TANZANIA (PROFOET)
61.RESTE YOUTH TRAINING TRUST FUND
62.RIDHIKA SHIRIKA LA ULINZI NA MAZINGIRA
63.RURAL ACCESS TECHNOLOGY INORMATION AND INSTITUTIONAL SERVICES (RATHS)
64.RURAL FAMILY LIFE PLANNING ASSOCIATION
65.RURAL INITIATIVES FOR DEVELOPMENT OF TANZANIA - RIDE(T)
66.RURAL ORIENTED SUSTAINABLE DEVELOPMENT ORGANIZATION (ROSDO)
67.RURAL WOMEN DEVELOPMENT ASSOCIATION
68.SAMORSES EDUCATION FOUNDATION
69.SANTA MERINA EDUCATION FOUNDATION
70.SAVE LIFE ASSOCIATION
71.SHINYANGA FOUNDATION FUND (SFF)
72.SOCIETY FOR RURAL DEVELOPMENT INITIATIVES (SRDF)
73.SOLIDARITY WOMEN GROUP (SWG)
74.SOLUTION AND OPPORTUNITIES FOR DISADVANTAGED IN AFRICA (SODA)
75.SOUTH DEVELOPMENT IN TANZANIA (YODIT)
76.SUSTAINABLE INTERGRATED FARMING AND HEALTH IMPROVEMENT
77.TAMADA
78.TANZANIA ACTION FOR PASTORAL EDUCATION ADVOCACY (TACEA)
79.TANZANIA ASSOCIATION OF ENVIRONMENTAL ENGINEERS (TAEES)
80.TANZANIA DEVELOPMENT AND AIDS PREVENTION (TADEPA)
81.TANZANIA GIRL'S EMPOWERMENT (TAGE)
82.TANZANIA HURUMA AIDS ORGANIZATION (THAO)
83.TANZANIA INITIATIVES FOR POVERTY ALLEVIATION (TIPA)
84.TANZANIA JOURNALIST ASSOCIATION (TAJA)
85.TANZANIA MANGROVE PROTECTION ASSOCIATION (TAMPA)
86.TANZANIA MARGINALIZED AREAS COMMUNITY SERVICES FOUNDATION
87.TANZANIA ROAD ASSOCIATION (TRA)
88.TANZANIA SOCIETY FOR THE BLIND (TASODEB)
89.TANZANIA SUPPORT AND TRAINING YOUTH AND WIDOWS ASSOCIATION
90.TANZANIA TENANTS ASSOCIATION
91.TANZANIA YOUTH MUSLIM ASSOCIATION (TAYMA)
92.TARIME – SIRARI GROUP (TARSI)
93.TAX SERVICES TANZANIA
94.TECHNOWLEDGE TANZANIA (TKTZ)
95.TELECOMS AND ELECTRONICS TECHNICIANS ASSOCIATION (TETA)
96.TEMEKE DISTRICT YOUTH FOUNDATION (TEYOFO)
97.THE HUMAN DEVELOPMENT PROJECTS AND TANZANIA
98.NAMTUMBO NETWORK OF CIVIL SOCIETY (NANECISO)
99.THE SURVIVAL AFRICA TRUST (SAT)
100.THE TANZANIA HERALDS YOUTH SERVICES (THEYS)
101.THE VOICE OF THE AIDS AND ORPHANS (VOTAO)
102.THE WOMEN WIDOW CHILDREN AND FISHERIES DEVELOPMENT
103.TUMAINI ORPHANS AND VULNERABLE CHILDREN CENTRE
104.UMOJA WA DOUYA NA MAKANGAWE (UDOMA)
105.UMOJA WA MADEREVA WA MABASI TANZANIA (UWAMATA)
106.WATOTO CARE ORGANIZATION (WACO)
107.WOMEN AND YOUTH ECONOMIC DEVELOPMENT INITIATIVE (WOYEDE)
108.WOMEN DEVELOPNMENT AND GENDER
109.SAIDIA JAMII YA WAZEE KAGERA SAJAWAKA)
110.UKIMWI ORPHANS ASSISTANCE (UKOA)

Imetolewa na,
M.S. Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
29 Machi, 2016.

WAZIRI NAPE ATEUA WAJUMBE WA KAMATI YA MAUDHUI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu  ya Jamii.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amewateua wajumbe wanne wa kamati ya maudhui watakaotumikia kipindi cha miaka mitatu.

Taarifa iliyotolewa  leo kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari Maelezo ilieleza kuwa uteuzi huo hufanyika kila baada ya miaka mitatu.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni  Joseph Mapunda ambaye ni  mhariri Mtendaji Mstaafu wa Magazeti ya Serikali(TSN) na  Mkurugenzi Mstaafu wa Redio Tanzania Dar es Salaam(RTD) Abdul Ngalawa.

Wengine ni  Mwandishi wa habari ,Mhadhiri Derek Murusuri  pamoja na Mwandishi wa habari ,Mwanasheria , Zainabu Mwatawala.

Waziri Mbarawa azitaka taasisi na idara kutumia kituo cha kuifadhi taarifa cha Taifa.

0
0
Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akielezea namna Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kuhifadhia taarifa zao. 
Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Adin Mgendi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi kwa usalama mkubwa wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumza na wadau hao juu ya matumizi ya kituo hicho kuhifadhia taarifa. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ili kuhifadhia taarifa zao. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya matumizi ya 'National Information Data Centre' 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ili kuhifadhia taarifa zao. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura pamoja na Ofisa Mkuu Idara ya Ufundi TTCL, Senzige Kisonge wakifuatilia mazungumzo hayo. 
Mkuu wa Idara ya Compyuta NSSF, Yahaya Madenge (kulia) akiuliza swali kupata ufafanuzi juu ya usalama wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi akiuliza kupata ufafanuzi juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi na kumlinda mteja wake. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye tai ya mistari miekundu) akizunguka na baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali vitengo vya IT kuwaonesha miundombinu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ilivyojengwa kisasa kumlinda mteja wake na taarifa zinazohifadhiwa katika kituo hicho. 
 Baadhi ya mashine kubwa za kisasa za kufua umeme katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Baadhi ya mitungi ya gesi ya kuzimia moto endapo ukitokea inayofanya kazi kwa kujiongoza yenyewe mara tukio la moto linapojitokeza katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi moja ya vyumba maalumu vya usalama katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi (kulia) moja ya mitambo ya kisasa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 

Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'. 
Baadhi ya mashine zinazofanya kazi ya kupooza mitambo katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kilichopo jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kuhifadhia taarifa zao. 

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA BOHARI YA DAWA MSD JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Banakunu (kulia), wakitembea wakati kamati hiyo ilipotembelea MSD Makao Makuu Keko Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Mary Lingo (wa pili kulia), akiwaelekeza wajumbe wa kamati hiyo jinsi dawa zinavyotunzwa katika maghala.
 Mkurugenzi wa MSD, Laurean Banakunu (katikati mbele), akiwaongoza wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea MSD leo.
Mjumbe wa kamati hiyo, Azani Zungu akiuliza swali juu ya kuharibika kwa dawa.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Jamii imetembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa Keko na kuipongeza kwa utendaji wake kazi pamoja na mazingira magumu yanayoikabili.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba amesema Kamati yake itasimamiana kuyafanyia kazi masuala makubwa manne ambayo ni pamoja na bajeti finyu ya dawa, ulipwaji wa deni la serikali, mfumo wa uwajibikaji kati ya Tamisemi na Wizara ya Afya ambao unasababisha utekelezaji na usimamizi wa masuala ya Afya kutokuwa na mtiririko kutoka juu kwenda chini. 

Jambo la nne ni kuhakikisha utekelezaji wa kuongeza uzalishaji dawa ndani ya nchi kupitia sekta binafsi (PPP).

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kingwangala alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha Bohari ya Dawa inanunua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kwa bei nafuu, hivyo Serikali imeweka kipaumbele kuhakikisha deni la MSD linalipwa mapema iwezekanavyo.

Alisema tayari Wizara ya Afya imeiagiza MSD kuandaa bei elekezi kwa maduka maalum ya dawa (prime vendor) ili vituo vinavyokosa dawa MSD vinunue huko bila usumbufu na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa dawa na vifaa tiba.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ameviomba vituo vya Afya kuleta mahitaji yao kwa wakati.

KAMATI YA BUNGE YA SHERIA NDOGO IMEPANGA KUFANYA MIKUTANO YA KUSIKILIZA MAONI YA WADAU

0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016.

Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:-

The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
The Public Private Partnership Regulations, 2015
The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works – Communication to the Public) Regulations, 2015
The National Examinations Regulations, 2015
The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015
The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015

Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania ya www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz

Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:-

Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
L. P. 9133, DAR ES SALAAM

Barua pepe: cna@bunge.go.tz

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
29 Machi, 2016.

Shuhudia Exclusive Interview ya Vanessa Mdee

0
0

RAIS MAGUFULI APOKELEWA KWA SHANGWE ALIPOTUA MWANZA KWA MUDA AKIELEKEA CHATO

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na umati wa watu uliojitokeza kumlaki baada ya kutua kwa muda uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa anaelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 29, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiburudishwa na ngoma za Utamaduni baada ya kutua kwa muda uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa anaelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 29, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Askari wa Kikosi cha  Zimamoto na Uokoaji wa Uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kutua kwa muda  akiwa anaelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 29, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kutua kwa muda  akiwa anaelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 29, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wasafiri baada ya kutua kwa muda uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa anaelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 29, 2016.PICHA NA IKULU.
 Viongozi wa dini wakimuombea  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli baada ya kutua kwa muda uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa anaelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 29, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa kusalimia wanannchi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella baada ya kutua kwa muda uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa anaelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 29, 2016

RAIS DK.JOHN MAGUFULI ATOA HATI YA KIWANJA KWA BOHARI YA DAWA (MSD)

0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto), akimkabidhi hati ya kiwanja chenye ukubwa wa ekari tano Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu kilichotolewa na Rais Dk. John Magufuli kwa MSD kupitia Wizara hiyo Dar es Salaam leo mchana. 
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (kulia), akisalimiana Naibu Katibu Mkuu wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Moses Kusiluka wakati wa hafla hiyo ya kukadhiana hati hiyo ya kiwanja. Katikati ni Waziri wa Wizara hiyo, William Lukuvi.
Salamu zikiendelea. Hapa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango Miji, Profesa John Modestus.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (mbele kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri Lukuvi na Mkurugenzi wa MSD, wakiangalia hati hiyo.
Viongozi wa wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usanifu Majengo, Amina Ramadhani, Ofisa Ardhi Mkuu, Mwamasage na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya.


Na Dotto Mwaibale

RAIS Dk. John Magufuli kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametoa kiwanja chenye ukubwa wa ekari 5 kwa Bohari ya Dawa (MSD) kilichopo Luguluni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kwa ajili ya ujenzi wa Bohari ya Dawa ili kuondoa upotevu wa fedha kwa maghala ya kukodi.

Ujenzi wa maghala katika kiwanja hicho utaokoa kiasi cha sh. bilioni 4 zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa ajili ya malipo ya maghala ya kukodi yaliyopo Mabibo Ubungo jijini pamoja na kanda mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa akikabidhi hati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu Dar es Salaam leo mchana, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema, Rais ametoa ardhi hiyo ili kuepusha gharama zisizo na sababu kwa MSD.

Alisema agizo la rais fedha zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kukodi maghala hayo, zinapaswa kununua dawa ili kila Mtanzania apate huduma bora za kiafya.“Rais aliniagiza niwape eneo, leo nimetekeleza agizo hilo kilichopo muanze ujenzi kama mlivyoomba kwa ajili ya kujenga ghala la dawa, naamini mtaanza mara moja balada ya kuendelea kukodi maghala na badala yake fedha zote zitumike kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba,” alisema Lukuvi na kuongeza;

“Kiwanja hiki ambacho kilikuwa cha Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kilichokuwa na ukubwa wa ekari 200, tumewapa ekari tano kama uhitaji wenu ulivyokuwa, nimewasamehe kodi ya premium na badala yake kiasi cha Sh16.7 hamtalipa na gharama mtakayotakiwa kulipa ni sh. milioni 2 pekee ili muanze ujenzi mara moja.”

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu alisema tayari wameshazungumza na Bodi ya wadhamini, Wizara ya Afya na wahisani hivyo ujenzi unatarajiwa kuanza mara moja Julai Mosi.

“Tunamshukuru sana Rais kwa sababu ombi hili limefanyiwa kazi kwa haraka sisi kama MSD tulishindwa kuhimili mikiki kutokana na gharama kubwa iliyokuwa ikielekezwa katika malipo ya ghala la kukodi pale ubungo mwaka wa fedha ulioisha tulilipa kiasi cha Sh3.5 bilioni na tukitarajia mwaka huu mpya wa fedha inafikia Sh4 bilioni kwa sababu ya malipo kwa dola,” alisema Bwanakunu.

Alisema katika eneo hilo jipya lililopo Luguluni wanatarajia kujenga zaidi ya maghala matano yenye ukubwa wa sikwea mita mita 5000 yatakayogharimu kiasi cha sh. bilioni 10nkila mojawapo, “ujenzi huu utakapokamilika kanda zitakazonufaika ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na kuwa eneo hilo walilopata wanaweza kujenga kiwanda cha maji.

Rais Magufuli aingia Chato kwa mara ya kwanza ataka watanzania washikamane kujitegemea badala ya kutegemea misaada

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwake katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ambapo akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti.


Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.


"Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka"Amesema Rais Magufuli.


Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi wa umma wanaolisababishia taifa upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa hatua hizo maarufu kwa jina la "Kutumbua Majipu" zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.


Dkt. Magufuli pia amekumbusha viongozi wote wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi, kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.


Rais Magufuli amewapongeza walimu kote nchini kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya changamoto ya ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana na walimu kuwasimamia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.


"Niziombe kamati za shule zote Tanzania nzima, kama haziwezi kusimamia nidhamu ya wanafunzi shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu Mkuu"Alisisitiza Dkt. Magufuli.


Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za watanzania.


Ametolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa mahakamani.


Pia Rais Magufuli amesema serikali yake imejiandaa kuboresha maslai ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini amesema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi shilingi milioni 15.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Chato


29 Machi, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI CHATO MKOANI GEITA KWA MARA YA KWANZA TANGU ACHAGULIWE KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezikiel Elias Kyunga mara baada ya kuwasili katika viwanja wa Chato Mkoani Geita. Rais aliwasili Wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezikiel Elias Kyunga kulia ,Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Msukuma kushoto na Naibu waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani watatu kutoka kulia wakielekea kwenye uwanja wa Mkutano wa mazaina kwa ajili ya kuwasalimia mamia ya wakazi wa Chato Mkoani Geita. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Chato mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mkutano Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Chato mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa Chato waliofika kumpokea kwenye Uwanja wa Michezo wa Mazaina Wilayani Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu wa wageni mara baada ya kuwasili Wilayani Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu wa wageni mara baada ya kuwasili Wilayani Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika hotuba yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Chato mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika mkutano wa hadhara.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato mara baada ya kuwasili uwanjani hapo. 
Wakazi wa Chato wakifurahia Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Michezo wa Mazaina Wilayani Chato. PICHA NA IKULU

ASKOFU CHARLES GADI NA WACHUNGAJI WENZAKE WALIOMBEA TAIFA LIPATE MVUA

0
0
 Askofu  wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhu kabla ya kuliombea taifa lipate mvua akiwa na wachungaji mbalimbali. Kulia ni Mchungaji Palemo Masawe.
 Mchungaji Martini Ndaki (kushoto), akizungumza katika 
mkutano huo.
 Meza kuu kabla ya maombi. 
Askofu Charles Gadi (wa tatu kutoka kushoto), akiongoza maombi ya kuliombea taifa lipate mvua. Kutoka kushoto ni Mchungaji Denis Komba, Mchungaji Martin Ndaki, Mchungaji Palemo Masawe, Mchungaji Denis Kumbilo, Mchungaji James Manyama na Mchungaji Leonard Kajuna.

Na Dotto Mwaibale

ASKOFU  wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, ameliombea taifa lipate mvua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Askofu Gadi alisema,  mabadiliko hayo ya kijiografia yamesababisha kukosekana kwa mvua za kutosha katika mwanzo wa masika wa mwezi wa tatu na kukithiri kwa joto kutokana na dunia kuwa karibu na jua(Equinox).

Alisema mvua za masika ni muhimu sana kwa kilimo, ufugaji, malisho ya wanyama mwitu wa nchini, mazao ya kudumu kama vile kahawa, migomba, michai  na mito yote hayo yanategemea mvua za masika.

“Tukumbuke kuwa kuna kipindi kirefu hupita tangu mvua za masika hadi kukutana na za vuli  ambapo ni karibu ya miezi mitano au sita  pasipo na mvua, hivyo kama kukiwa na uhaba wa mvua za masika maana kipindi cha ukame kitaongezeka kwa miezi saba hadi  miezi minane jambo ambalo ni hatari sana kwa kilimo na wanayama wetu.

“Joto la Equinox limekuwa kali  kuliko wakati mwingine wowote ingawa lilitarajiwa kuchemsha maji ya bahari ili mvua ziwe nyingi lakini hali imekuwa kinyume, hivyo tunawaaasa watanzania wote  bila kujali dini na itikadi ya mtu kuungana kwa pamoja  kumuomba mungu ili ukame huu usiikumbe nchi yetu,” alisema Askofu Gadi.

Alisema ni lazima kuomba ili ipatikane mvua   za kutosha nan chi iweze kujitegemea kwa chakula  ili fedha ambazo zingetumika kuagiza chakula nje ya nchi ziweze kutumika kwenye kuleta maendeleo ya kitaifa.

Aidha Askofu Gadi aliishukuru Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)kwa kuendelea kutoa  taarifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kijiografia yanayosababisha kuongezeka kwa joto kwa kikwango kikubwa.

Askofu Gadi alifanya maombi hayo kwa kushirikiana na wachungaji wenzake  ambao ni Mchungaji Denis Komba, Martin Ndaki, Palemo Masawe,  Denis Kumbilo, James Manyama na Mchungaji Leonard Kajuna.

KAMATI YA BUNGE YAIOMBA SERIKALI KUTOA VIBALI VYA UINGIZAJI SUKARI KUTOKA NJE YA NCHI

0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA ABIRIA LA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE TBIII

0
0
 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, imefanya ziara ya kutembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three- TBIII), jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016 ambapo awali wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Profesa Norman Adamson Sigalla King, walipatiwa maelezo ya kina ya maendeleo ya mradi huo unaohusisha jengo la kisasa la abiria na sehemu ya kuegesha ndege kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na sehemu ya maegesho ya magari. 

Baada ya maelezo hayo ya kina yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, (TAA), Mhandisi George Sambali akisaidiana na baadhi ya wakurugenzi wengine wa Mamlaka hiyo, wajumbe hao walitembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kwa sasa ujenzi umefikia karibu asilimia 60. Pichani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Norman Adamson Sigalla King, (kulia), na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA
 Mwenyekiti wa Kamati, akizungumza
 Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha, akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kabla ya kutembelea mradi
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo na maafisa wa TAA, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali (hayupo pichani)
 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akitoa maelezo ya maeneleo ya mradi huo. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Laurent Mwigune
 Mjumbe wa Kamati, Anna Richard Lupembe, akizungumza
 Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, na Mbunge wa Fuoni, Zanzibar, Abbas Ali Hassan Mwinyi, (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Ramadhan Maleta, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Laurent Mwigune (kushoto)




 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla, sehemu ya maegesho ya ndege


 Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla, (kulia kwake) na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Sambali, (wakwanza kulia), sehemu ya maegesho ya ndege
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania, ATCL, Johnson Mfinanga akizungumzia hali ya shirika hilo
 Afisa Mkuu wa Masoko wa TAA, Scholastica Mukanjanga, akizungumza
 Mjumbe wa Kamati akizungumza
 Mjumbe wa Kamati akizungumza
 Mjumbe wa Kamati, Abass Ali Hassan Mwinyi, (katikati), akizungumza
Sehemu ya jengo la uwanja huo

Milioni 37 zatengwa kukarabati barabara ya Kata ya Panzuo/Mkuranga

0
0
Na Mwandishi Wetu, Mkuranga.

JUMLA ya Sh Milioni 37 zimetangwa kwa ajili ya kukarabati barabara ya Mbogo na Mbezi Muungwana, inayopita katika vijiji kadhaa vya Kata ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani kwa ajili ya kupunguza adha za ubovu wa barabara wanazokutana nazo wananchi wa maeneo hayo hali inayopelekea wakati mwingine akina mama kujifungulia njiani.
Mwendesha bodaboda Ramadhan Rajab akijaribu kupita katika barabara mbovu inayotokea Kimanzichana kuelekea vijiji vya Mnyonzole na Kibesa, Kata ya Panzuo, wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.

Mapema mwezi uliopita baadhi ya wananchi wakiwamo akina mama walizungumza kwa uchungu juu ya ukosefu wa barabara katika maeneo hayo, jambo linalowanyima raha na ukosefu wa mbinu za kujikwamua kiuchumi kwa kukosekana barabara inayopitika kwa wakati.

Akizungumza juu ya ukosefu wa barabara na mipango yao, diwani wa Kata ya Panzuo, wilaya Mkuranga, mkoani Pwani, Juma Magaila, alisema kwamba kiasi hicho cha pesa kitaanzia kwanza kuweka kifusi katika maeneo mbalimbali ili wananchi wae ndelee na majukumu yao kwa kuhakikisha kwamba suala hilo la barabara mbovu linashughulikiwa.

Alisema ni kweli wananchi katika maeneo hayo wamekuwa wakiishi kwa mashaka hususan mvua zinapoanza kunyesha, ila tayari fedha zimetangwa kwa ajili ya kuanza ukarabati wa barabara hiyo inayotumiwa na wananchi wengi wilayani Mkuranga.

“Tunaendeelea na mikakati ya kuikwamua Kata yetu hususan katika changamoto kubwa za ubovu wa barabara wanazokutana nazo wananchi wangu wa Panzuo ambao wanashindwa kukuza uchumi wao kwasababu barabara haipitiki kirahisi wakati wote.

“Naamini kwa kutengwa kiasi cha Sh Milioni 37 kutachangia kwa kiasi kikubwa kuiweka barabara yetu katika kiwango cha kupitika huku tukielekea katika safari ya kuona tunafikia hatua ya kuiwekea changarawe na mengineyo,” Alisema.

Awali wananchi wa vijiji vya Kibesa wakiongozwa na mwenyekiti wao Khamis Ningwe walitumia muda mwingi kuilalamikia barabara hiyo sanjari na kuiomba serikali ya Halmashauri ya wilaya Mkuranga iliangalie suala hilo kwa jicho pevu.

Endapo barabara hiyo itakarabatiwa japo kwa kiwango cha kifusi, si tu akina mama wajawazito hawatajifungulia njiani kunaponyesha mvua, bali wananchi wanaweza kuingiza kipato kwa kuuza bidhaa zao mbalimbali kama vile nanasi na nyinginezo zinazopatikana katika maeneo hayo sanjari na kuleta urahisi watu kuingia na kutoka kwenye maeneo hayo.

SERIKALI YAJIPANGA KUWASAIDIA WAKULIMA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

0
0
DSC_1682
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.
 DSC_1667
Wageni rasmi katika mkutano huo, Wa kwanza kushoto ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN), Njongenhle Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai.
DSC_1664
Mshereheshaji wa mkutano huo akiwakaribisha wageni waalikwa kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo.
DSC_1671
Baadhi ya wageni waliohudhuria katika mkutano huo kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha inawasaidia wakulima kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaonekana kuendelea kuikabili nchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) na Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN) ili kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).

Bi. Natai alisema serikali inatambua uwepo wa mabadiliko ya Tabia ya Nchi na kwasasa tayari wataalamu wanafanya tafiti ili waone ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia wakulima kupambana na mabadiliko hayo.

Alisema kwa sasa bado wakulima wengi hawajafahamu kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo wamekuwa wakitumia njia za asili lakini baada ya utafiti watapatiwa mbinu mpya za kupambana na mabadiliko ambapo wataweza kutumia njia za kisasa ambazo zinaonekana kuwa bora zaidi.

“Serikali inatambua na tunajipanga kuwasaidia wakulima, shida kwa sasa bado wakulima wengi hawajajua kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi lakini wataalamu wapo wanafanya tafiti baada ya hapo tutajua tunawasaidia vipi,“Kwa sasa kinachoonekana ni kutokueleweka kwa hali ya hewa kama mafuriko kutokea lakini kwa kuwa bado hawajapatiwa elimu wanashindwa kutambua na bado wanatumia njia za asili, tutawapa mbinu mpya watafanya kwa pamoja na mbinu wanazotumia sasa za asili,” alisema Bi. Natai.


Aidha alieleza kuwa baadhi ya huduma ambazo watapatiwa wakulima baada ya kukamilika kwa tafiti ni pamoja na kupewa elimu ya kilimo cha umwagiliaji, mbegu za kisasa ambazo zinawahi kukomaa na dawa za kupambana na magonjwa.Nae mtafiti kutoka FANRPAN, Njongenhle Nyoni alisema taasisi yake imefanya mkutano huo ili kuona ni jinsi gani wanaweza kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi ambazo wanafanya kazi ambapo Tanzania ni mojawapo.

Alisema wao wanafanya tafiti kuona hali ilivyo na baada ya hapo wanatazama changamoto zilizopo katika kupambana na mabadiliko na wanatoa ushauri ni jambo gani linaweza kufanyika ili kuwezesha kufanikisha kufanyika Kilimo Salama (CSA).“Tunakutana na watu kutoka asasi za kijamii na taasisi mbalimbali ili kuona ni jinsi gani CSA inaweza kufanya kazi vizuri hasa katika maeneo tunafanya nao kazi na hii sio Tanzania tu hata mataifa mengine kama Malawi tunalifanya hili,” alisema Nyoni.

Pia iliongeza kuwa malengo ya FANRPAN ni kusaidia wakulima kuondoka katika janga la umasikini lakini pia kuwepo kwa chakula kilicho katika hali ya usalama bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
DSC_1697DSC_1701
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai akielezea Kilimo Salama (CSA).
DSC_1749
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuendelea na mkutano huo.
DSC_1754
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai.
DSC_1759
Karl Deering kutoka Taasisi ya CARE akizungumzia Mpango wa Kilimo Salama Afrika (ACSAA).
DSC_1769
Baadhi ya wageni katika mkutano huo wakichangia hoja
DSC_1772DSC_1819
Washiriki wa mkutano wakiwa katika makundi kujadili kuhusu Kilimo Salama (CSA)
DSC_1823DSC_1829DSC_1914
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uwezeshaji wa ESRF, Doris Likwelile akifunga mkutano.

TAARIFA YA MSIBA

0
0
Col. Gervase Mang'wen'gula wa  makao makuu ya jeshi la wananchi Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha mpendwa Mkewe Easter Mang'wengula kilicho tokea usiku wa kuamkia jana (29/3/2016) katika Hospitali ya Tumbi Kibaha.

Mazishi yatafanyika siku ya Ijumaa nyumbani kwa marehemu Kwa matiasi barabara ya Nyumbu kuanzia saa Saba mchana.

Habari ziwafikie Maofisa wote wa Jeshi la Wananchi Tanzania, askari wote wafanyakazi wa nyumbu, ndugu majirani na marafiki wa familia ya marehemu

BWANA AMETOA JINA LAKE LIHIMIDIWE AMEN
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images