Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 808 | 809 | (Page 810) | 811 | 812 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongoza na viongozi mbalimbali pamoja na baadhi ya maaskofu kucheza wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akiimba jukwaani.
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga picha ya pamoja na waimbaji wa muziki wa injili mara baada ya tamasha hilo kumalizika kutoka kulia ni Bonny Mwaiteje. Jesca BM na Upendo Nkone.
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akicheza wakati mwimbaji Bonny Mwaiteje alipokuwa akitumbuiza.
  Mwimbaji Christopher Mwahangila akiwapa upako mashabiki kupitia injili ya uimbaji.
  Mwimbaji Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia naye akaimba nyimbo za kusifu na kuabudu.
  Solomon Mukubwa akiafunga kazi na nyi,bo zake kali zilizowafanya mashabiki kuwa wima wakati wote kama wanavyoonekana.  0 0

   Show ya Makeke imefanyika jana tarehe 26 March 2016 kwenye hotel ya Boma Inn Nairobi. Maonesho haya makubwa ya mitindo yamejumuisha nchi mwanachama wa Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda na Sudan Kusini. Makeke kaenda kuiwakilisha collection  yake inaitwa THE AFRICAN BEAUTY IN THE DARKNESS - TABID, au uzuri wa Afrika gizani  kwa Kiswahili.

  Giza inawakilisha utamaduni wa Magharibi ambao kwa sasa umekua kwa kasi mno katika bara la Afrika na kutufanya waafrika kusahau utamaduni wetu. Lakink licha ya kuzungukwa na hili giza zito la umagharibi lakin bado Afrika inameremeta kwani kuna tamaduni zetu nzuri ambazo zinafaa kuigwa duniani kote. Makeke ametumia malighafi za asili kutengeneza mavazi yake na nakshi asili za kiafrika. Makeke anarejea Tanzania kesho jioni 
  0 0

  Wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanaonufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers wakikisikiliza kwa Makini Mada Kuhusu Elimu ya Biashara na namna ya kuendesha Ujasiriamali Kwenye Mafunzo Yanayoendelea Mkoani Dodoma .

  Mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano yameanza mkoani Dododma. Jumla ya Washiriki 30 wamechaguliwa katika fursa hiyo na wanajulikana kama Manjano Dream Makers. Mafunzo hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake hao kutoka Manispaa ya Dodoma watapatiwa elimu kuhusu sifa za ujasiriamali, changamoto zake na namna ya kukuza na kuendesha biashara ikiwa pamoja na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'Financial literacy'. Pia washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na kujua mbinu zipi watumie kujiwekea
  akiba.
   
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Akieleza Machache leo wakati wa Mafunzo ya Ujasirimali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma.

  Awamu ya pili washiriki watapatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipodozi hasa "Make-Up Artistry". Awamu hii hapa washiriki watajua matumizi yenye ueledi (professional) wa kutunza ngozi, kutumia vipodozi na namna ya kuwapamba maharusi na wakazi wa Dodoma na maeneo jirani kwa kutumia vipodozi sahihi na salama. Mara baada ya mafunzo haya washiriki watapata fursa ya kukopeshwa mitaji kwa ajili ya biashara kwa lengo la kuwakwamua washiriki wote kuondokana na ukosefu wa ajira na kujikita katika kujiajiri katika tasnia ya vipodozi.
  Mafunzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Manjano Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Shear illusions kupitia vipodozi Pendwa vya LuvTouch Manjano. Mafuzo kama haya tayari yamesha wanufaisha wanawake Zaidi ya 150 Kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Visiwani Zanzibar. Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Dodoma wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwapa nafasi hiyo na kuwaletea mradi huo.
  Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kutoka Mkoa Dododma.

  Wakieleza zaidi wamesema walikuwa na hamasa sana tangu walipopata taarifa kwa wanawake wenzao wa mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar kunufaika na mradi huu na walikuwa wanasubiri kwa hamu kubwa sana mafunzo hayo. Wakiendelea zaidi wamesema wapo tayari kupigana na kujikita vizuri kupitia mradi huu kwa lengo la kujikwamua na kujiongezea kipato kupitia kazi ya mikono yao

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Bomba la Gesi litakalokuwa likisafirisha kutoka Tanga kwenda uganda. 
  Mwenyekit wa Chama cha wafanyabiashara wa mafuta nchini(NICOL), Gidion Kaunda akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya Katibu mkuu kuzungumzia bomba la mafuta la Tanga kwenda Uganda.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa(aliye mbele) jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa amesema kuwa wafanyabiahara wa mafuta wanafursa mbalimbali katika ujengaji wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Profesa Ntalikwa amesema kuwa bomba la mafuta likianza mchakato wafanyabiashara wanaweza kuomba zabuni mbalimbali zitakazojitokeza.

  Mradi wa ujenzi wa bomba hilo unagharimu dola za Kimarekani Bilioni Nne ambapo utaongeza ajira nyingi pamoja na kodi.

  Amesema kuwa bomba hilo litajengwa nchini kwa asilimia 90 kutokana na amani iliyopo ukilinganisha na nyingine zilizo katika mradi huo.

  Profesa Ntalikwa amesema kuwa kigezo cha kwanza cha kujenga bomba nchini ni kutokana na Bandari ya Tanga kuwa na kina kirefu cha kufanya kila meli kuweza kuingia hapo na tofauti bandari ya Mombasa nchini Kenya.

  Amesema kutokana na vigezo vinaashiria kujengwa nchini licha ya kuwepo kwa majadiliano yanayoendelea juu ya bomba hilo litajengwa wapi.

  Amesema kuwa nchi ya Kenya ndio inayofanya kuwa katika mchakato wa mwisho hivyo wenyewe ni watu wa kuangalia tu jinsi ya mradi utapofanyika.

  Aidha Profesa Ntalikwa amesema kuwashirikisha wafanyabiashara wa mafuta ni kutaka kukujua fursa zilizo katika ujenzi wa bomba la mafuta wa kuweza kuomba zabuni.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshuhudia Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akiweka sahihi katika hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisaini hati ya kiapo cha Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe Samia suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim  na  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Luteni Mstaafu Chiku Gallawa  mara baada ya kumuapisha  kuwa mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016. Kulia ni mume wa mkuu huyo wa Mkoa Bw. Juma` Boma na kushoto ni bintiye.

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemwapisha Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa, ambaye hakuapishwa pamoja na wakuu wa mikoa wenzake Machi 15, 2016.


  Uapisho huo umefanyika leo tarehe 28 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.


  Luteni Mstaafu Chiku Gallawa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza kwa Mkoa mpya wa Songwe, ulioanzishwa kwa kuugawa mkoa wa Mbeya, Kusini mwa Tanzania.


  Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2014/2015 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad, Ikulu Jijini Dar es salaam.


  Rais Magufuli amepokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa ni utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa mwezi Machi.


  Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli ataikabidhi mbele ya bunge katika siku saba za mwanzo za kikao kijacho cha Bunge kitakachofanyika Mjini Dodoma.Rais Magufuli amempongeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo, na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi, huku akiahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake.

  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam


  28 Machi, 2016


  0 0

  Wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakicheza ngoma ya Sindimba wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akiwaangalia wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha (hawapo pichani) wakicheza ngoma ya kabila la wa Meru wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo. Kulia ni Randall Stubbs ambaye ni Meneja Mradi wa kituo hicho kinachojengwa chuoni hapo, watatu kulia ni Afisa Michezo wa Mkoa Mwamvita Okeng’o na wa nne kulia ni Afisa utamaduni wilaya ya Arumeru Senyael Pallangyo.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiangalia mchoro wa ramani ya Kituo cha Utamaduni kinachojengwa katika chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo. Kulia ni Afisa utamaduni wilaya ya Arumeru Senyael Pallangyo akifuatiwa na Randall Stubbs ambaye ni Meneja Mradi wa kituo hicho.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo.Picha na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

  0 0

  Kocha wa TSS, Michael Livingstone akiwafundisha waogeleaji Celina Itatiro na Marin de Villard kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2.
  Kocha wa TSS, Alex Mwaipasi akiwafundisha waogeleaji wa TSS, kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini kwa ajili ya Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
  Adil Bharmal na Pieter De Raadt wakionyesha ufundi wao katika ku-dive wakati wa mazoezi ya timu ya TSS kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla ya mashindano ya South Africa level 2
  Waogeleaji wa Tanzania Swim Squad (TFF) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye bwawa la Ellis Park mjini Johannesburg Afrika Kusini tayari kushindana katika mashindano ya South Africa level 2
  Viongozi wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS), Thauriya Diria (wa kwanza kushoto) na Inviolata Itatiro (Katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na kocha Michael Livingstone wakiwa katika picha ya pamoja TSS kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park kabla ya mashindano ya South Africa level 2
  ………………………………..
  Na Mwandishi wetu,Johhanesburg

  Jumla ya waogelaji nane wa timu ya Tanzania Swim Squad (TSS) watakuwa na ratiba ngumu kesho ya kuwania medali mbalimbali katika siku ya pili ya mashindano ya Kimataifa ya Afrika Kusini “South Africa Level 2” yaliyoanza jana kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park.

  Waogeleaji hao ni Celina Itatiro, Marin de Villard, Adil Bharmal, Amani Dogart, Josephine Oosterhuis, Jacquelene Kortland, Isabella Kortland, Pieter De Raadt, Celina Itatiro na Marin de Villard.

  Waogeleaji hao watawania medali katika mashindano ya mita 50, 100, 200 na relay katika kwa upande wa wanawake na wanaume kwa kushindana na waogeeaji wengine kutoka nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Namibia na wenyeji Afrika Kusini.

  Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na waandaaji, Adil ndiye ataanza kuwania medali kwa uande wa Tanzania kwa waogeaji wenye umri miaka 16 na kufuatiwa na Marin kwa upande wa mita 200 freestyle kwa waogeleaji wa wa miaka 11 na baadaye wasichana, Celina na Amani kushindana kwa upande wa wanawake wenye umri wa miaka 11 katika staili ya free style.

  Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Adil na Marin wataingia tena kwenye ‘maji’ kushindana katika staili ya breaststroke mita 100 kwa upande wa umri wao ns baadaye Josephine na Jacqueline watapambana kwa watoto wenye umri wa miaka 15 na kufuatiwa na Celina na Amani tena.

  Baada ya kushindana katika staili hizo mbili (freestyle na breaststroke mita 100 na 200), waogealeaji, Adil na Marin wataingia tena mashindananoni kuwania medali kwa upende wa mita 50 backstroke na baadaye Isabela Kortland, Josephine, Amani na Celina watawania medali tena.

  “Ni ratiba ngumu sana kwa waoageaji wetu, ila tunashukuru kuwa wameweza kufanya mazoezi na kidogo kuzoea hali ya hewa ya ubaridi, sisi (TSS) tutatokea mji wa joto inaweza kutupa shida kwani baridi ya huku inaambatana na jua la kuchoma, si hai nzuri, ila tutajitahidi,” alisema Alex Mwaipasi.

  Mwaipasi ambaye yupo na kocha mwenzake, Michael Livingstone alisema kuwa mashindai hayo ni magumu sana kutokana na idadi ya waogeleaji na idadi ya mashindano ambayo kila muogeleaji atashindana.

  “Celina anatarajia kushindana katika mashindano tofauti 11, si mchezo na waogeleaji wpo zaidi ya 1000, nchi nyingi za ukanda wa Kusini mwa Afrika wameleta waogeaji, ni mashindano mazuri kwa kuwapa uzoefu waogeleaji wetu,” alisema Michael.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiwa na watendaji wakuu  wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkafuzi Mkuu wa hesabu za serikali  baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakipitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali iliyokabidhiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.PICHA NA IKULU

  0 0


   Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA.

  Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kujadili kuhusu Jumuiya za waTanzania nje ya nchi na changamoto zake, na pia kuhusu DICOTA na mkutano wao mkuu wa mwaka huu
  KARIBU


  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa

  Wananachi wa maeneo mbalimbali ya jimbo la mafinga mjini wamesema utaratibu wa mbunge wao Cosato Chumi kwa kwenda kutembelea maeneo yenye kero ni dalili njema zinazoonyesha kuwa hawakufanya makosa kumchagua kuwa mbunge wao na kuongeza hatadanganywa na watendaji walioko chini yake tatizo linalosababisha viongozi wengi kutoa maamuzi yasiyo sahihi na yanayoendelea kuiathiri jamii.

  Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa  Cosato Chumi akiwa na balozi wa korea  mh Geum-young song wakipata picha ya pamoja baada ya maongezi ya muda mrefu.


  Aidha wananchi hao wamempongeza mbunge wao kwa juhudi anazo zifanya za kukutana na watadau mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.

  “Tumeona mbunge wetu akikutana na mabalozi wa nchi tofauti tofauti na wanazungumzia maendeleo ya jimbo la mafinga mjini mfano hivi karibuni mbunge wetu alikuwa na balozi wa korea  mh Geum-young song tunajua kunakitu tutapata kutoka kwa balozi huyo”. Walisema wananchi

  Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mafinga mjini mkoani Iringa  Cosato Chumi  ameanza  kutimiza ahadi  zake kwa  wananchi  wa  jimbo la Mafinga mjini  kwa kufanya ziara ya kutambua matatizo ya wananchi wake na kutambua nini vipaumbele vyao.

  Chumi alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi  yake  hiyo ni kama njia ya  kuwashukuru  wana Mafinga mjini kwa kumchagua katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa wakati akiomba kura kwa wananchi.

  Alisema ataendelea  kutimiza ahadi  binafsi zilizotolewa wakati kampeni kulingana na uwezo  wake  na zile  za  kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha anaikumbusha  serikali  ya CCM ili  kutimiza ahadi hizo kwa  wakati.

  “Ndugu  zangu wananchi  mbali  ya  kuwa  ubunge  wangu ni  wa  mwaka mmoja  ila  tayari  mimeanza  kutimiza ahadi  bila  ya kuchelewa  na  ninawahakikishieni  sita  waangusha  nitaendelea  kufanya  hivyo  zaidi  mniombee  uzima”.alisema Chumi

  Mbunge huyo ameongeza kuwa hivi karibuni anatarajia kupokea msaada wa kuchimbiwa visima vitano kwenye shule za sekondari na msingi za jimbo hilo ambapo visima viwili kwa sekondari na vitatu vya shule ya msingi,msaada huo umetoka kwa ubalozi wa korea mh:Geum-young song.

  “Leo nilialikwa lunch na balozi wa korea mh:Geum-young song na tumeongea mambo mengi lakini kubwa nimeahidiwa kuchimbiwa visima vitano kwenye shule za msingi na sekondari zilizopo kwenye jimbo la mafinga mjini mungu ni mwema jambo hili likifanikiwa litatusaidia kuwapunguzia adha wanafunzi wetu”.alisema Chumi.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Manyara.

  MKUU wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera amewaagiza viongozi wa Wilaya za mkoa huo, kuhakikisha hadi mwisho wa mwezi Aprili kusiwepo na wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati ya kukalia.

  Akizungumza mjini Babati, Dk Bendera alisema japokuwa Rais John Magufuli amewaagiza wakuu wote wa mikoa kuondoa tatizo la ukosefu wa madawati hadi Juni 30 mwaka huu, kwa Manyara mwisho ni Aprili 30. 

  Alisema Manyara haipaswi kusubiri hadi mwezi Juni 30 ili imalize upungufu wa madawati hivyo, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri, viongozi na wananchi kwa ujumla kuhakikisha hilo linafanyika. 

  “Rais wetu Dk Magufuli baada ya kututeua hivi karibuni alituagiza wakuu wote wa mikoa kuhakikisha tunamaliza tatizo hilo hadi mwezi wa sita lakini mimi nataka kwangu Manyara ikifika mwezi wanne tumalize,” alisema Dk Bendera.

  Kwa upande wake, katibu tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi alisema kiwango cha elimu Manyara kimeporomoka kwa kuchangiwa zaidi na tabia ya wafugaji kuhama kutoka eneo moja hadi jingine kufuata malisho mazuri ya mifugo yao.

  “Hali ni mbaya kwenye halmashauri zetu zenye wafugaji wengi kwani mkoa wetu umeendelea kuporomoka kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na sekondari hivyo jitihada za dhati za kupambana na hili zinahitajika,” alisema Maswi.

  Hata hivyo, aliwataka viongozi wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha shule zote za sekondari ambazo hazijamaliza ujenzi wa vyumba vya maabara, wanamaliza haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wapate elimu kwa njia ya vitendo.

  0 0  Na Woinde Shizza alivyotembelea ,Mwanza .

  Uvuvi haramu wa kutumia sumu kali,pamoja na neti umekua ukitishia uhifadhi katika hifadhi ya Taifa ya Saa Nane na Lubondo ambazo zimepewa jukumu la kulinda mazalia ya samaki ili samaki hao wasipotee kwenye uso wa dunia.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake waliofanya ziara ya kutembelea hifadhi hiyo ya Saa Nane iliyoko jijini Mwanza ,ziara iliyoratibiwa na Tanapa Mhifadhi Mkuu Donatus Bayona amesema kuwa changamoto inayowakabili ni uvuvi haramu na uvamizi wa maeneo ya hifadhi unaofanywa na wavuvi wanaojipatia kipato bila kujali kuwa wanaharibu mazalia ya samaki . 

  Askari Wanyamapori katika hifadhi hiyo Aloyce Mong`ee amesema kuwa wamekua wakiimarisha doria katika mipaka ya hifadhi ili kuzuia shughuli hizo za uvuvi ambazo ni tishio kwa uhifadhi.“Kuna mipaka ambayo tumeweka hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya uvuvi ndani ya eneo la hifadhi ili kuhifadhi mazalia ya samaki” Alisema Askari huyo.

  Mhifadhi huyo amesema kuwa Hifadhi hiyo ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza inaongoza kwa kuwa na watalii wengi wa ndani ambao ni asilimia 90% ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.Alisema Hifadhi ya Saa Nane ni moja kati ya hifadhi zilizopo kati kati ya miji hivyo kuvutia watanzania wengi kutembelea eneo hilo ambali lina wanyama pori pundamilia,swala na sokwe weusi pamoja na madhari nzuri na maridhawa ambazo hutumika kama sehemu ya kujifunzia na kupumzikia.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

  TAMKO LA MHE. UMMY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU WANANCHI KUSHAMBULIA WATUMISHI WA AFYA HASA MADAKTARI NA WAUGUZI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA NCHINI, TAREHE 29 MACHI, 2016


   

  Ndugu Wananchi, 

  Nachukua fursa hii nikiwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya afya nchini, kutoa tamko kuhusiana na matukio ya hivi karibuni yaliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na vitendo vya kusikitisha wanavyofanyiwa watumishi wa sekta ya afya, wakiwemo Madaktari kama vile kushambuliwa kwa maneno na vipigo. Pasi na shaka, vitendo hivyo vitaathiri upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wanaopewa huduma hizo hususan wa kipato cha chini. 

  Matukio haya yanajumuisha tukio lililotokea tarehe 27.03.2016 katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, ambapo Dr Dickson Sahini alishambuliwa na ndugu wa mgonjwa aliyepelekwa hapo kuhudumiwa. 

  Napenda kutamka kwamba nimesikitishwa sana na tukio hilo, na ninalaani vikali matukio ya watumishi wa afya kushambuliwa kwa maneno au kwa vitendo na wananchi wanaopatiwa huduma. Jambo hili likiendelea litawavunja moyo watumishi wa afya na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

  Ningependa kuwafahamisha kwamba kwa ujumla wake sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi sana katika maeneo ya miundombinu, dawa na vifaa tiba, watumishi wa kutosha, pamoja na kuwa na watumishi wasiozingatia nidhamu, weledi na maadili katika kutimiza majukumu yao.

  Ninatambua kwamba changamoto hizi zipo siku nyingi, na zimekuwa zikitafutiwa majawabu na Serikali za awamu zilizopita ikiwemo ile ya awamu ya nne. Lakini sote ni mashahidi kwamba Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dr John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inachukua hatua za makusudi katika kutatua changamoto hizi, likiwemo pia suala zima la utendaji unaozingatia uwajibikaji. 

  Kwa hiyo ninawasihi sana wanachi wanaopatiwa huduma katika vituo vyetu vya afya kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mikononi na kufanya vitendo vinavyoweza kuwakwaza watumishi wa afya. Kwa vile nchi yetu inafuata misingi ya utawala unaozingatia sheria, ni vyema wananchi wakafuata taratibu zilizowekwa wanapohisi kwamba hawakupatiwa huduma za afya wanavyostahili. 

  Aidha nachukua fursa hii kuvitaka vyombo na mamlaka husika kutosita kuwachukulia hatua wananchi wanaokwenda kinyume na matakwa ya sharia ili kuwahakikishia watoa huduma za afya usalama na amani wakati wa utoaji wa huduma hiyo.

  Ninaagiza vile vile kwamba hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini ziweke utaratibu mwepesi wa wananchi kufikisha malalamiko yao pindi wanapoona kwamba hawakupatiwa huduma za afya kwa kiwango stahiki. 

  Napenda pia kuahidi kwamba tutajitahidi kutatua changamoto za kimfumo zilizopo katika utoaji wa huduma za afya nchini ili kuufanya utoaji wa huduma kuwa bora zaidi. 


  Ndugu Wananchi, 

  Ninatambua kwamba sehemu kubwa ya watumishi katika sekta ya afya nchini wanafanya kazi zao kwa ufanisi, upendo, uadilifu na kwa kuzingatia matakwa ya weledi (professionalism) na miiko ya taaluma zao (ethics). Pia ninatambua kwamba wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu na wanatumia muda wa ziada kuendelea kuwahudumia wagonjwa hadi wanapoona wapo salama. Ninawapongeza kwa dhati watumishi hawa na ninawashukuru na kuwatia moyo waendelee kuwa na tabia hiyo nzuri, kwa maslahi ya Taifa letu. 

  Hata hivyo ninasikitishwa sana na tabia ya watumishi wa afya wachache ambao wanafanya kazi kinyume na maadili na matakwa ya weledi wa taaluma zao. Napenda kusisitiza kuwa Wizara yangu haitavumilia matukio ambayo watumishi wa Sekta ya Afya watakwenda kinyume na matakwa ya weledi na maadili ya taaluma zao katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Hivyo hatutasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo ili kudhibiti hali hii. 

  Nimeshaelekeza vyombo vya kusimamia maadili ya watoa huduma za afya nchini, yaani Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) kuchukua hatua mara moja, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zao, juu ya watoa huduma wote wanaotuhumiwa kukiuka misingi ya weledi na maadili ya taaluma zao. Endapo tuhuma zao zitathibitika, hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufutiwa usajili au leseni zao ikibidi. 

  Hivyo kwa tamko hili ninawaasa na kuwaagiza watoa huduma wa afya wote nchini kufanya kazi zao kwa bidii, kwa nidhamu na kwa kuzingatia weledi na maadili ya kitaaluma kama inavyoelekezwa. 

  Ndugu Wananchi, 

  Napenda pia kukumbusha kwamba kazi hii ya usimamizi wa mahusiano mema kati ya watoa huduma za afya na wananchi, na usimamizi wa weledi na maadili katika vituo vya kazi, itafanikiwa kwa ushirikiano wa pamoja wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi, Kamati za Usimamiaji wa Huduma za Afya za Mikoa na Wilaya, Kamati za Usimamiaji wa Huduma za Afya za Hospitali, na Wananchi wote kwa ujumla katika kuwasimamia, kuwaelekeza na kutambua mapungufu ya kimfumo au yale yanayohusu watumishi wa afya yaliyopo na kuchukua hatua zinazostahili mara moja. Ni lazima tuzingatie Sheria, Kanuni na Taratibu katika kutimiza jukumu hili. Wizara ya Afya itaendelea kuvijengea uwezo Mabaraza ya kitaaluma ya wataalamu wa afya ili kutimiza wajibu wao kikamilifu. 

  Tufanye kazi kwa pamoja ili kutekeleza kauli mbiu ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, inayosema ‘HAPA KAZI TU’. 

  Asanteni sana. 


  Imetolewa na: 
  Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) 
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
  Mtwara – Tanzania 
  29 Machi 2016


  0 0

  Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
  MAMLAKA ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamekamata mabasi 105 yenye makosa mbalimbali na mabasi 36 yamefikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo wakabiri.

  Hayo yamesemwa na Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa Madereva na Makondakta wa mabasi hayo wamefikishwa katika mahakama za Kinondoni na Ilala jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa kutokana na Operesheni inayofanywa na 
  Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi nchini imekuwa ikibaini baadhi ya madereva wanaokiuka Masharti ya leseni ya Kusafirisha abiria na wengine kutokuwa na leseni ndio maana wameona kuchukua hatua hiyo ya kukamata na kuwapeleka mahakamani madereva na Makondakta wanao kiuka masharti ya leseni zao.

  Pia amewaasa wamiliki wa mabasi na wafanyakazi wakiwemo madereva na Makondakta wa mabasi ya Daladala kuzingatia masharti ya Leseni za usafirishaji wanapotoa huduma ya usafirishaji kwa umma na wananchi kwa ujumla wamewaomba kutoa ushirikiano pale ambapo wanaona madereva wanakiuka masharti ya reseni za usafirishaji, kuongeza nauli, kukatisha njia au kutumia njia ambayo haijapangwa na Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA).
  Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kukamatwa kwa mabasi yanayobainika kuvunja Masharti ya Reseni nyakati za asubuhi na jioni jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa mabasi 36 yameshakamatwa na kesi zao zipo mahakama ya Kinondoni na Ilala jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kulia ni Afisa habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Frenk Mvungi.

  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  TIMU ya Afya Sports Bara na Afya Sports Zanzibar zimetoka sare bao moja kwa moja katika mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam.
  Timu ya Afya Sports Zanzibar ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu na bao la kwanza lilifungwa na Haji Abdalah kwenye dakika ya 22 kipindi cha kwanza.

  Katika kipindi cha pili timu ya Afya Bara ilifurukuta na kurejesha bao lililofungwa na Mesa, hatua iliyopelekea timu hizo kutoka sare ya bao moja kwa moja.

  Katika hatua nyingine, timu ya Netibili ya Afya Bara imeifunga mabao 30 -29 timu ya Netiboli ya Afya Zanzibar kwenye mchezo uliofanyia kwenye Uwanja wa Netiboli iliyopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  Mchezo huo ni Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka kati ya Watumishi wa Sekta ya Afya Zanzibar na Watumishi wa Sekta ya Afya Bara kwa lengo la kuendeleza undugu na ushirikiano.
  Mchezaji wa timu ya Afya Bara, Drisa akimtoka mchezaji wa Afya Zanzibar, Hassan Abdallah “Kimti” katika mchezo wa tamasha la Sikukuu ya Pasaka. Katika mechi hiyo timu hizo zilitoshana nguvu sawa. Afya Zanzibar 1-1 Afya Bara. Mchezo huo ulifanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
  Wachezaji wa timu ya soka Afya Bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo.
   Wachezaji wa Netiboli ya Afya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mchezo. Afya Bara imeifunga Afya Zanzibar mabao 30-29. Mchezo huo umefanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wakazi wa wilaya ya Chato Mkoani Geita mapema leo.

   Wakazi kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Chato mkoa wa Geita,wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakisubiri kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ambaye amewasili leo mjini humo alikozaliwa.Rais Dkt Magufuli anawasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu awe Rais.

   Wanannchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumpokea mtoto wa nyumbani kwao Chato,Mh Rais Dkt.John Pombe Magufuli viwanja vya Mjini Chato mkoani Geita muda huu. Hii ni mara ya kwanza kufika chato tangu awe Rais.

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika hilo wakiwa katika eneo hilo mara baada ya kubaini kuwepo kwa wizi huo wa umeme(PICHA NA VICTOR MASANGU).
   Afisa Usalama wa shirika la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba akionyesha moja ya eneo ambalo wameiba umeme  kwa kujiunganishia bila ya kuzingatia taratibu.
   
  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

  SHIRIKA la ugavi wa umeme Tanesco Mkoani Pwani  limewakamata   watu saba kwa tuhuma za wizi wa umeme  katika eneo la kwamfipa  Wilayani Kibaha ambao walikuwa wamehujumu miundombinu kwa kujiunganishia umeme kinyemela kinyume cha utaratibu.

  Akizungumzia kuhusina na  tukio hilo Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Herny Byarugaba amesema kwamba kubainika kwa watu hao waliokuwa wanaiba umeme kumetokana  baada ya kupatiwa taarifa kutoka kwa  wananchi wasamalia wema  wa eneo hilo.

  Byarugaba amesema kwamba  wezi  hao walikuwa wamezichimbia nyaya za umeme chini ya barabara ya kuusambaza katika baadhi ya maeneo ikiwemo maduka, mabanda ya kuonenyeshea video hali ambao amedai ni hatari kwa usalama wa maisha ya watu kwani kunaweza kutokea majanga ya kuungua kwa nyuma za watu na kupoteza maisha yao.

  “Sisi tumepata taarifa hizi kutoka kwa wananchi wasamalia wema kwa hiyo sisi kama tanesco tukaamua kufanya msako mkali katika eneo hili la kwa mfipa na kuweza kukuta wateja wetu wameamua kutumia njia za kinyemela kwa kuiba umeme na mbaya zaidi nyaya wamezipitishia chini kabisa ya barabara hivyo hali hii ni hatari sana watu wanaweza kupoteza maisha,”alisem Byarugaba.

  Aidha alibainisha kwamba kutokana na kujiunganishia umeme kinyume na taratibu kunaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi  kwani pindi mvua inaponyesha na nyaya hizo zikiwa zimechunika maji yanashika umeme na hivyo kunaweza kusababisha  hatari kubwa sana.

  Pia Byarugaba aliongeza kuwa  Shirika  la Tanesco limekuwa linapata hasara kubwa na kupoteza mapato yake kutokana na baadhi ya watu kuamua  kufanya vitendo vya hatari vya kuhujumu miundombinu yao pamoja na kuiba umeme.

  Kwa upande wake  Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwamfipa Juma Tanga ambaye alifika eneo la tukio alisema kwamba  amesikitishwa sana kuona  baadhi ya wananchi wake kushiriki kuiba umeme kinyume na taratibu na kuwataka waachane na vitendo hivyo kwani ni hatari kwa usalama wa maisha yao.

  Mwenyekiti huyo alisema kwamba  katika kukabiliana na hali hiyo atahakikisha anaweka mikakati ya kuwaelimisha wananchi wake katika mikutano mbali mbali kuhusina na  madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na kujiunganishai umeme bila ya kuzingatia taratibu zilizowekwa na wahusika wenyewe.

  Naye Meneje wa Tanesco Mkoa wa Pwani  Martin Madulu ametoa tahadhari kwa wananchi  wote wa Mkoa wa Pwani kuachana kabisa na tabia ya kujiunganishia umeme pasipo kuwatumia wafanyakazi husika wa tanesco na badala wake wahakikishe  wazingatie taratibu katika kuunganishiwa umeme katika sehemu za biashara pamoja na nyuma za kuishi.

  Aidha katika hatua nyingine Mejeja huyo aliwataka wananchi kujihadhari ya matapeli ambao wanajifanya ni wafanyakazi wa shirika hilo na endapo wakiwabaini watoe taarifa mapema katika vyombo vinavyohusika ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

  0 0

   Bw. Jeyapaulraj, akipokea nyaraka kwa niaba ya Abu Dhabi Indian School, mshindi wa shule na kituo cha kikundi cha watoto yatima.
   Bibi Atija, akipokea nyara kwa niaba ya Mkuu wa Umoja wa Wanawake, mshindi wa kikundi cha wazee.
  Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Etihad, Wahudumu wa watoto, marubani, Ali Al Shamsi, Makamu Rais wa mikakati akiwa na watoto wenye Autism.

  CHINI ya ulezi wake Mtukufu, Sheikha Shamsa bint Hamdan Bin Mohamed Al Nahyan, Mheshimiwa Mwenyekiti wa kituo cha Autism mjini Abu Dhabi, Shirika la ndege la Etihad limeendesha hafla hiyo ya kuchangisha fedha kwa sababu maalum kupitia matembezi.  Zaidi ya washiriki 5,200 wa kila umri walikusanyika katika bustani za Al Mushrif Central  Mjini Abu Dhabi siku ya Ijumaa Machi 18 kushiriki katika tukio la matembezi ya dakika  30.  Fedha zote zilizotolewa katika tukio zitakwenda katika ujenzi wa jengo jipya litalokuwa kituo kipya cha utabibu mjini Abu Dhabi kwa ajili ya waathirika wa ugonjwa wa Autism, pamoja na ukarabati wa shule nchini India.  Mtukufu Sheikha Shamsa Bint Hamdan Bin Mohamed Al Nahyan alitoa pongezi kwenda shirika la ndege la Etihad kwa ajili ya maandalizi ya tukio hilo, ambayo inaonyesha dhaira ya kampuni kuendelea kusaidia kuleta maendeleo ya kijamii na uboreshaji endelevu katika jamii zinazo wazunguka.  Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Mtukufu Sheikh Thiyab Bin Khalifa Bin Hamdan Al Nahyan, Eugenia Davis, Baraza la Umoja wa Mataifa ya Amerika, Kanali Abdulrahman Al Swaidi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Shayma Nawaf Fawwaz, Afisa Mtendaji Mkuu wa GOSSIP, Mheshimiwa Mariem Al Rumaithi, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la matunzo ya kibinadamu na Mahitaji Maalum la Zayed , na Dk. Khawla Salem Rashed Al Saaedi, mwakilishi wa Rais wa Wanawake na Health Alliance International.  Khaled Al Mehairbi, Makamu wa Rais wa uendeshaji wa uwanja wa ndege wa Abu Dhabi na Mwenyekiti wa Michezo na kamati za kijamii katika shirika la ndege Etihad, alisema: "Shirika la ndege Etihad lina nia ya kutoa huduma bora kwa watoto wenye ugonjwa wa akili ili kuboresha ubora wa maisha yao.  "Hii ni sehemu ya ahadi yetu kuendelea kuleta maendeleo kwa jamii yetu ya ndani na kuboresha afya ya umma na kuongeza ufahamu wa autism.”  "Matembezi haya ya faraja kwa mara nyingine tena imewaleta kwa pamoja jamii ya Abu Dhabi, na tuna matumaini kuwa na uwezo wa kuongeza ufahamu na fedha muhimu kwa kusaidia watu wenye mahitaji – hapa nyumbani pamoja na kimataifa”  Matebezi hayo yalikuwa wazi kushiriki kwa watu wa miaka yote, baada ya usajili washiriki walipokea kipima spidi pamoha na fulana iliyobeba nembo ya tukio hilo.


  Bibi Athba Ali, meneja manunuzi wa shirika la ndege la Etihad  na mama wa watoto wawili, alisema: "Mimi nina furaha na fahari kuwa sehemu ya tukio hili la “Tembea kwa Hisani" tukio hilo. Nina furaha kuona kwamba tukio limefanikiwa katika kuleta kila mtu pamoja ili kusaidia kufanikisha tukio hili. Tulifurahia tukio hili la matembezi na tayari tunatazamia tukio la mwaka ujao.”  Burudani kutoka “Bollywood” ilikuwepo kuwapa washiriki motisha na burudani huku shirika la ndege la Etihad waliandaa shughuli mbali mbali kwa ajili ya wanafamilia wote ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kurusha ndege chini ya nahodha wa ndege pamoja na warsha ya mapishi ya ndani ya ndege chini ya mpishi mkuu.  Wahudumu wa watoto walikuwepo kusaidia kusimamia na kuchangamsha watoto.  Wakati wa mchezo wa 'Jaribu na ushinde', waliohudhuria walikuwa na nafasi ya kushinda idadi kubwa ya zawadi ikiwa ni pamoja na tiketi daraja la uchumi kutoka shirika la ndege la Etihad, Bidhaa zisizolipiwa ushuru za bure, Uanachama wa mwaka mmoja kwa famila nzima wa Kituo cha kimataifa cha mapumziko na michezo cha Al Forsan, malazi ya wikiendi nzima katika hoteli ya nyota 5, Vocha ya watu wawili ya mlo wa usiku, zawadi kutoka kwa Apparel Group na mengi zaidi.  Wadhamini wa tukio la mwaka huu walikuwa: Wizara ya Mambo ya Ndani, Jamii ya Autism Emirates, Abu Dhabi Media Company, Emirates Red Crescent, Baraza la elimu la Abu Dhabi, Braza la michezo la  Abu Dhabi, Kampuni ya maji ya Al Ain, Bustani ya Mushrif, Shirika la Zayed, Verde, Austin Reed, Glossip Milano, Muungano wa wanawake wa Hindi, Gossip Café na Desserts, Canon Mashariki ya Kati, wa Kituo cha kimataifa cha mapumziko na michezo cha Al Forsan, Hospitali ya LLH, Nyumba ya sanaa ya kisasa Etihad, Kampuni ya uchapishaji ya United, Silkor, Primavera Medical Rehabilitation LLC, Crowne Plaza na Staybridge Suites Abu Dhabi Yas Island, Holiday Inn Abu Dhabi, Rosewood Abu Dhabi, Hoteli ya Royal Rose, Landmark Gulf Group, Kituo cha marekani cha vipaji maalum, Kituo cha tiba ya meno cha Boston na Mercure Al Ain Grand Jebel Hafeet.

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza na wandishi wa habari juu ya  kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya mbunge wa jimbo la kinondoni   haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda leo jijini Dar es Salaam.
  Wakili mshitakiwa  Juma Nassoro akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. juu ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro. Kulia ni .Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia.
  Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akitoka Mahakani hapo mara baada ya kesi hiyo kuahilishwa.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

  KESI ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Mbunge wa jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia(CHADEMA) iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Idd Azzan imeshindwa kutolewa maamuzi hii leo kama ilivyokuwa imepangwa na mahakama kuu ya Tanzania.

  Juma Nassoro ambaye ni wakili wa mshitakiwa Maulid Mtulia ambaye ni Mbunge wa Kinondoni amesema kuwa baada ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro, ambapo amemuaomba msajili kumpanga jaji mwingine atakaye andika hukumu ya kesi hiyo, na hivyo wameambiwa kurudi tena kesho mahakamani kwa ajili ya kupangiwa tarehe nyingine.

  Kwa upande wa Mbunge Mtulia anayekabiliwa na kesi hiyo ameeleza  kusikitishwa na kilichotokea kwa kile alicho dai kuwa kesi hiyo  haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda.

older | 1 | .... | 808 | 809 | (Page 810) | 811 | 812 | .... | 1898 | newer