Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 79 | 80 | (Page 81) | 82 | 83 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Cape Town, Afrika ya Kusini kuhudhuria kikao cha viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika leo tarehe 10 Mei, 2013.

  Viongozi wa SADC wanakutana chini ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo Tanzania ndiye mwenyekiti.

  Kikao cha leo kinatarajia kuzungumzia maendeleo na hali ya usalama katika ukanda huu hususan hali ya usalama Mashariki mwa Kongo, DRC, Madagascar na Zimbabwe.

  Nchi za Afrika ya Kusini, Malawi na Tanzania zitapeleka vikosi Mashariki mwa DRC kulinda na kuleta utulivu na usalama.

  Kuhusu Madagascar, nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi Julai, 2013 wakati nchini Zimbabwe nako uchaguzi unatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

  Mbali na mkutano huo Rais anahudhuria mikutano kadhaa inayoendelea mjini Capetown ukiwemo ule wa Kiuchumi ambao viongozi wa kisiasa, kiserikali na wakubwa wa mashirika binafsi wanahudhuria na kuzungumzia fursa za kibiashara na kiuchumi barani Afrika.

  Rais anatarajia kurejea Dar es Salaam kesho tarehe 11 Mei, 2013

  “Mwisho”

  Imetolewa na:
  Premi Kibanga
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
  Cape Town – Afrika ya Kusini
  10 Mei, 2013

  0 0

  Picha juu na chini ni Foleni ya magari ya takataka zaidi ya 30 yaliyokwama katika dampo la Pugu Kinyamwezi kwa takribani siku tatu kutokana na ubovu wa miundo mbinu huku taka zikiendelea kuoza ndani ya magari hayo na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo.(Picha na Dewji Blog).

  Katapila likiwa katika jitihada za kuchonga barabara ili angalau magari ya taka yaweze kufika eneo la dampo kuwamga taka.
  Masela wakifurahia baada ya gari la taka lililokuwa limekwama kufanikiwa kupandisha kilima katika dampo hilo kuelekea kumwaga taka.


  Wanafunzi wa shule ya msingi walipokutwa na camera yetu katika dampo hilo wakikatiza na kuzubaa zubaa eneo hilo wakati wa saa za shule.

  Wakazi wa maeneo hayo wakichambua takataka hizo kujiokotea chupa tupu za maji na mifuko ya plastiki ikiwa ni ajira waliyojitengenezea katika kuendesha maisha yao ya kila siku, shuhuda wa Mo Blog Zainul Mzige anatanabaisha kwamba chupa wanazookota huuzwa kilo moja kwa shilingi 100 kitu kinachowapelekea wafanyaji wa biashara hii kuwa watumwa wa pombe za kienyeji haswa almaarufu kama Gongo au Chang'aa.

  Mitaro ya maji machafu ikiwemo mikojo na vinyesi katika dampo hilo...Je kuna kupona kweli hapa????

  Magari ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni nayo yalikwama kwenye dampo hilo, pichani yakielekea kuwamga taka hizo baada ya barabara kutengemaa kwa kiasi.

  Pichani ni juu na chini Mama lishe wakitoa huduma ya chakula chini ya mti katika eneo lilizongukwa na taka ikiwemo harufu kali na Nzi wanaozunguka hapa na pale lakini vibarua wa dampo hilo hawana la kufanya.

  Moja ya Katapila lililokodiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam likiwa limekufa na kushindwa kufanya kazi kutokana na kukwamisha na miundo mbinu ya eneo hilo la dampo huku mafundi wakihangaika kulifufua.

  Meneja wa Dampo la Pugu Kinyamwezi Bw. Richard Katiti akizungumzia changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kipindi hiki cha mvua kitu ambacho kinawapelekea kutumia jitihada za ziada ikiwemo kukodisha magari (Vijiko) ili kujitahidi kuhakikisha miundo mbinu ya kufika katika dampo hili inapitika kwa urahisi ili kuondoa vikwazo kwa magari yanayotoa huduma ya kuzoa taka mjini.
  Devera wa gari la Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Ramadhani Sufi akielezea adha wanayoipata ambapo amefafanua kuwa inafika mahali inawabidi kulala siku mbili na gari zenye mzigo wa taka katika mazingira ambayo ndio wanayoshinda na kula kitu ambacho kinaweza kuwasabishia maradhi hivyo ameliomba jiji kurekebisha hali hiyo ili kuwaepusha na mazingira hatarishi kiafya kutokana na uchafu unaolundikana mahali pamoja kuanzia dampo hadi kwenye magari.
  Aidha amefafanua kuwa hali hiyo inasababisha kutuchafulia jina la kampuni yetu na kuonekana kama hatufanyi kazi kumbe tatizo lipo kwenye utaratibu mzima wa Manispaa na suala la miundo mbinu.
  Pia ameshauri jiji liongezewe uwezo kutokana na kuwa na vyombo vichache na chakavu kitu kinachopelekea kuzidiwa katika kutoa huduma katika dampo hilo.
  Mmoja wa madereva wa magari ya taka yaliyokwama kutokana na miundo mbinu mibovu Bw. Frank John akielezea kero ya kwenye dampo la taka lililopo maeneo ya Pugu Kinyamwezi ambapo amesema taka zimelundikana barabara hazipitiki hata magreda ya kuzoa hayana pakupita na kuwaomba watu wanaohusika na dampo kujaribu kutengeneza njia mbadala na kushauri itafutwe njia kipindi cha Masika taka ziwe zinamwaga sehemu nyingine na kipindi cha Kiangazi kiwe na sehemu yake na kushauri mamlaka zinazohusika na usafi zijifunze kutoka kwa wananchi na sisi tujifunze kutoka kwao.
  Aidha Bw. John amewataka viongozi wahusika kutokaa maofisini na kutembelea maeneo husika na kujiuliza kwanini gari zinakwama na kuongeza kuwa tatizo hilo limepelekea lawama kwa baadhi kampuni za usafi kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa wakati.
  Hii ndio hali halisi ya viroba vya uchafu vilivyolundikwa katika eneo la Pugu Kwalala pembezoni mwa barabara na makazi ya watu ambapo wananchi wamekuwa wakizilalamikia kwa sababu kipindi cha mvua vinaweza kuwasababishia magonjwa ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.
  Mkazi wa eneo la Gongo Mwisho wa lami - Pugu Kwalala Bw.Erasto Njau akilalamikia ubovu wa magari ya taka ya Halmashauri ya Manispaa ya jiji la Dar es Salaam na vile vile utaratibu mbovu wa ukusanyaji wa taka ambapo hata kama gari imeharibika yangetumika magari mengine kuja kubeba taka suala ambalo linalohusu uongozi wa Manispaa ambao ndio unaogharamia magari yanayobeba taka kitu ambacho kinaonyesha utaratibu wa ubebaji taka bado haujakaa sawa.
  Mama Lishe Asha Omari Dundo akizungumzia kero ya Mlundikano wa taka katika eneo lake la biashara ambalo sio dampo rasmi la kutupia takataka na anapouliza anaambiwa magari yamekwama dampo kutokana na ubovu wa miundo mbinu kitu ambacho ni hatari kiafya kwa wateja wake wa chakula ambacho ndio biashara anayoifanya kwa ajili ya kusomesha watoto na kila anapouliza hapewi jibu linaloeleweka na ameiomba serikali kutupia macho swala hilo kwa sababu kumekuwa na kauli tofauti malori yamekwama na malori mabovu.
  Mama Lishe Asha Omari Dundo akiwaandalia wateja wake chakula cha mchana katika eneo ambalo ni hatarishi kwa walaji.
  Mkuu wa Afya Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Dar es Salaam Bw. Membe Protus Membe akizungumzia jitihada za Manispaa katika kupambana na tatizo la mlundikano wa magari ya taka yaliyokwama katika eneo la Dampo la Pugu Kinyamwezi kutokana na ubovu miundo mbinu ya barabara unaopelekea kukwamisha zoezi la ukusanyaji taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar na kusababisha mlundikano wa taka nyingi kwa muda wa kipindi cha siku hizi tatu.
  Hata hiyvo amesema katika muda wa siku tatu kuanzia leo Manispaa itahakikisha inarekebisha miundo mbinu ya kuelekea dampo ili kuweza kupunguza msongamano uliopo wa magari ya taka yaliyokwama yaweze kurudi mjini kuendelea na ubebaji wa taka.
  Aidha Bw. Membe ameahidi kuwa shughuli za umwagaji taka katika dampo hilo zitakuwa zikifanyika mchana na usiku ili kuondoa mlundikano wa taka mitaani ambao umejitokeza katika muda wa siku tatu.

  0 0

  CODES:

  Unakumbuka? raha za ki-Legendary za muziki wa Silent Inn, Bills, FM Club, Carlifonia Dreamers, Mambo Club na Tazara? Basi DJ John Dillinga (DJ JD) na DJ Fast Eddy tunawakaribisha kujumuika na malegends wenzenu kila Jumamosi kuenzi nyakati hizo Isumba Lounge, Jolly Club kwa mchango wa elfu 10 tu mlangoni, Karibuni Sana.

  0 0


   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OIKO Credit Duniani  David Woods  akiongea na waandish wa habari  (hawapo pichani) kuhusiana na Taasisi y a oiko kuongeza mikopo kwenye sekita ya Kilimo na nishati endelevu  hapa nchini  wakati alipotembelea katika ofisi za Oiko Credit zilizopo   jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Mkurugenzi wa  Oiko Kanda ya Afrika Mashariki  Judy Ngarachu na kulia ni  Meneja wa taasisi hiyo hapa Tanzania Deus Manyeynye.
   Mkurugenzi wa  Oiko Kanda ya Afrika Mashariki  Judy Ngarachu  akimkabidhi fedha Jane Mlay   ambaye ni mmoja wa wanachama wa kikundi cha Aple ambacho kimenufaika na mkopo ya  shilingi million 8  toka kwa taasisi ya Oika Credit  nchini  katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OIKO Credit Duniani  David Woods ,  Mkurugenzi Mtendaji wa Tujenge Tanzania Limited Shafi Nambobi   na Meneja wa taasisi hiyo hapa Tanzania Deus Manyeynye. Mkurugenzi huyo yopo hapa nchini kwa ziara ya kikazi hapa  kujionea jisi shughuli za taasisi hiyo zinavyoendeshwa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OIKO Credit Duniani  David Woods akimkabidhi  Devota Elias fedha ambaye ni mmoja wa wanachama wa kikundi cha Aple ambacho kimenufaika na mikopo ya  shilingi million 8  toka kwa taasisi ya Oika Credit ,anaye shuhudia katikati ni Meneja wa taasisi hiyo hapa Tanzania Deus Manyeynye. Mkurugenzi huyo yopo katika ziara ya kikazi hapa nchini kujionea jisi shughuli za taasisi hiyo inavyoendeshwa.
  =========  ======  ====
  Oikocredit kuongeza mikopo kwenye kilimo na nishati endelevu
  Dar es Salaam 9, May, 2013.. TAASISI ya OIKO Credit inayojihusisha na utoaji mikopo kwa taasisi mbali mbali za fedha duniani, imewahidi kuongeza mikopo katika sekta za kilimo pamoja na nishati endelevu hapa nchini.

  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo David Woods aliyeitembelea Tanzania hivi karibuni na kukutana na baadhi ya wateja alisema “Mikopo yetu kwa Afrika inalenga zaidi kwenye kilimo, vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS) vimekuwa vikitoa mchango mkubwa kufanikisha lengo hili. Pamoja na kilimo hapa Tanzania tunaangalia eneo lingine ambalo ni nishati endelevu, nafurahi kuwepo Tanzania na kuendeleza ushirikiano wetu wa muda mrefu.

  Taasisi ya Oikocredit ambayo pia hutoa mikopo na mitaji kwa taasisi za kilimo pamoja na biashara ndogo na za kati (SMEs)  ilifungua ofisi zake hapa Tanzania mwaka 2006 na tayari imeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi 15bn/- kwa miradi 35 hapa nchini

  Ikiwa ni moja kati ya vyanzo vikubwa duniani binafsi vya kutoa mitaji kwa mifuko midogo (microfinance), ufadhili wa taasisi hiyo kwa miradi mbalimbali duniani umekuwa na kufikia Tshs 1.1 trilioni (Euro 530 milioni) mwaka 2012 ongezeko la asilimia 2 kutoka 1. 07 Trilioni (Euro milioni 520) mwaka 2011. Secta ndogo (microfinance) inawakilisha karibu asilimia 79 ya mikopo ya taasisi hiyo. Ya pili ni kilimo na usindikaji ambayo huchukua asilimia 12 ikifutiwa na biashara ambayo ni asilimia 3 na elimu na afya vikichukua asilimia 3 pia.

  Kilimo kinaendelea kuwa moja ya sekta muhimu kwa Oiko credit na kwa sasa ina imarisha dirisha la mikopo ya kilimo. Oikocredit tayari imehidhinisha 51.2BN/-(Euro milioni 25) katika mikopo mipya 38 kwa wabia wake wa kilimo kwa mwaka 2012 na kutoa kiasi cha 72bn/-(Euro milioni 35) kwa sekta ya kilimo kwa ujumla. Baadhi ya uwekezaji unagharamia ununuzi au ujenzi unahusisha majengo, vifaa vya kilimo na shughuliza za uongezaji wa thamani katika mazao ya kilimo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Mashariki wa taasisi hiyo Judy Ngarachu alisema “Katika nchi za Kenya na Tanzania kumekuwa na ari ya kuendeleza miradi ya nishati endelevu, lakini jamii zimekuwa zikihangaika kutafuta wawekezaji binafsi kuwasaidia kupitia upembuzi yakinifu, mipango pamoja na maandalizi. Naamini tunaweza kutoa mchango muhimu katika miradi kama hii,”

   Meneja wa Oikocrediti kwa Tanzania Deus Manyenye alielezea umuhimu wa kilimo na kusema, “Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Kilimo kinachangia nusu ya pato la taifa, robo tatu ya bidhaa zinazosafirishwa nje na pia ni chanzo cha chakula. Inatoa ajira kwa asilimia 80 ya watanzania, wanawake wakiwa ndiyo nguvu kazi muhimu katika sekta hii. Tunafurahi kutoa mchango wetu katika kampeni ya kilimo Kwanza iliyozinduliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2009.

  0 0


   Chief Executive Officer and Managing Director, Airtel Nigeria, Segun Ogunsanya; First Lady of Ogun State, Mrs. Olufunso Amosun; Chairman, Ijebu North Local Government Area, Otunba Olaide Osifeso and Sopen Lukele, Oke-Sopen, Oba M. A Yusuf during the commissioning of Airtel's Adopted School, St. John's Primary School, yesterday, in Oke-Agbo, Ijebu-Igbo, Ogun State.
  Chief Executive Officer and Managing Director,
  Airtel Nigeria, Segun Ogunsanya and First Lady of Ogun State, Mrs.
  Olufunso Amosun during the commissioning of Airtel's Adopted School,
  St. John's Primary School, yesterday, in Oke-Agbo, Ijebu-Igbo, Ogun
  State.

  ====  ======  =======  ===

  Ogun First Lady Commends Airtel for Uplifting Primary Education

  ... As Airtel Commissions Adopted Primary School


  Lagos, Nigeria; First Lady of Ogun State, Mrs. Olufunso Amosun has
  commended Leading Telecommunications Services Provider, Airtel Nigeria
  for partnering with the State Government in providing educational
  opportunities for less privileged children and for uplifting the
  standard of education in the country.

  The First Lady who was speaking, yesterday, at the commissioning
  ceremony of one of Airtel's Adopted School in the State, St. John's
  Primary School, Oke-Agbo, Ijebu-Igbo, said she was overwhelmed that a
  company would decide on its own, unsolicited, to move into an area and
  offer to serve humanity by providing world class educational
  opportunities, exceptional learning facility and other support for
  underprivileged children.

  "I feel really overwhelmed by Airtel's Adopt-A-School programme.
  Airtel came here unsolicited and is already doing so much. If only all
  of us can reach out the way Airtel has done, our society and, indeed,
  the world will be a better place.

  "Airtel is not here today to market its products but to give back to
  our society. It has transformed St. John's Primary School, provided
  bags, uniforms and text books for all the kids. This is commendable
  and should be emulated.

  She also called on the concerned community to protect the facilities
  for the realization of the objectives of the school.  "To the people
  of Ijebu-Igbo, Airtel has given us a special gift. I urge you to guard
  this school with your lives and ensure that it remains in great
  condition for our children to learn."

  Speaking earlier, Chief Executive Officer and Managing Director,
  Airtel Nigeria, Segun Ogunsanya said the company's vision and
  commitment to providing quality education is premised on the need to
  build a better future for the young generation of Nigerians through
  quality education.


  "Without a doubt, quality education offers children the best
  opportunity in life to realise their dreams and become the leaders of
  tomorrow. A great environment is also critical to the development of a
  sound mind. It is, therefore, in recognition of the importance of
  education and as part our Corporate Social Responsibility vision that
  we have committed to the adoption of public primary schools across
  Nigeria," he stated.

  Continuing, the CEO reiterated the commitment of the company to
  strategic partnerships that would drive further its vision of helping
  to develop the education sector in the country. He said that good
  companies give back to communities and if a company wants to be a
  great company it has to be a good one first.


  "Our commitment to the people of Ogun State and Nigerians is long
  term. We will remain part of the schools we have adopted and we will
  continue to maintain the necessary support and care. As a matter of
  fact, our employees have volunteered to support this programme,"
  Ogunsanya said.  The pupils of St. John's Primary School responded to the kind gesture
  of Airtel by staging a well-choreographed music and dance presentation
  in honour of the Telco Operator. Speaking on their behalf, the Head
  Teacher of the School, Mrs. Victoria Boyejo showered encomiums on
  Airtel, commending the Telco Operator for transforming the school
  environment and for providing all other resources to aid learning.
  The First Lady unveiled the plaque in the presence of about 700 guests
  comprising top government officials, traditional rulers, indigenes and
  pupils and teachers of St. John's Primary School.

  Key guests at the occasion included the Director: Corporate
  Communications & CSR, Airtel Nigeria, Emeka Oparah; the Chairman,
  Ijebu North Local Government Area, Otunba Olaide Osifeso; Oba M.A.
  Yusuf, the Sopen Lukale, Oke-Sopen and Oba H.O. Abass, the Beje Ruko,
  Oke-Agbo, both in Ijebu-Igbo among other distinguished guests.

  Airtel's Adopt-A-School initiative is part of the company's umbrella
  CSR program and it focuses on the education of underprivileged
  children in line with the United Nations Millennium Development Goals
  of universal primary education. At present, similar initiatives have
  been completed in Imo and Cross River States in addition to the
  flagship effort at Oremeji Primary School 2 in Lagos.

  0 0


  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali ina kazi kubwa ya
  kushughulika na kundi dogo linalojihusisha na lugha za uchochezi wa
  kidini ambao unachangia kudhoofisha amani ya nchi.

  “Tunajua nia yao ni kufanya nchi isitawalike lakini sisi tumesema
  hatukubali. Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, ulinzi uimarishwe kila mahali, mshingae kuona watu wanawahoji lakini nia njema, ya kurudisha amani yetu,” alisema Waziri Mkuu.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Mei 10, 2013) wakati
  akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali wakati wa
  ibada ya mazishi ya waumini watatu wa Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi,
  Parokia ya Olasiti, jijini Arusha waliofariki dunia kutokana na
  mlipuko wa mabomu uliotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, mwaka huu
  kanisani hapo.

  Waziri Mkuu amewaomba wanachi kutoka ushirikiano kwa vyombo vya dola
  kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kwenye upelelezi wa tukio
  hilo.

  “Ninawaomba Watanzania tushirikiane kuwafichua watu hawa waovu kwa
  sababu tunaishi nao, ni watu ambao wako miongoni mwetu... Tusaidieni
  kutunong’oneza ili tuchukue hatua, alisema.

  Waziri Mkuu alisema yeye ni miongoni mwa watu wanaoamini kwamba
  ukristo au uislamu hauwezi kuondolewa kwa kuwaua viongozi wa dini au
  waumini wao. “Ni kujidanganya tu mtu akiamini kuwa akimuua Askofu,
  Mufti au  Muumini ataimaliza dini yoyote. Madhehebu haya mawili ni
  nguzo kubwa kwa Taifa letu, tunatamani tuendelee kuwa na amani
  iliyokuwepo siku zote,” alisisistiza.

  Alisema Serikali kupitia idara ya maafa itatoa sh. milioni 100/- ili
  zisaidie kukabiliana na janga lililowakabili wana Arusha.

  Mapema, akiongoza ibada hiyo, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo
  aliwataka waumini wote kutolipa uovu kwa uovu bali watende wema ili
  kusahihisha maovu. “Ishara ya uovu imetendwa na hawa watu dhidi ya
  waumini wenzetu kwa madhumuni yanayojulikana na wao tu bila kuchokozwa
  na hawa marehemu ama wale waliko hospitali (majeruhi),” alisema.

  “Uovu umeshatendwa, je sisi tufanye nini? Angekuja hapa kanisani yule
  aliyesababisha mauti haya, tungemfanya nini?” Alihoji Kardinali Pengo
  na kujibiwa na mamia ya waumini waliohudhuria ibada hiyo:
  “Tungemsamehe.”

  Aliwasihi waumini wote kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania ili tukio
  hilo na lile la kuuawa kwa Padre Evarist Mushi kule Zanzibar yasiwe
  sababu ya kusambaratika kwa amani ya Taifa hili.

  “Tusilipe ubaya kwa ubaya, tuendelee kuomba Mungu asikie sala yetu na
  awazindue wenye mamlaka watimize wajibu wao,” alisema.

  Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
  Dk. Alex Malasusa akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Jukwaa la
  Wakristo Tanzania (TCF), alilaani waliosababisha mauaji hayo na kusema
  kitendo hicho kimelitia doa Taifa kwa vile ni kitendo kinachoashiria
  kuchafua amani ya Tanzania.

  Aliwasihi waumini wote kutokuwa waona katika kazi ya kumtanga za
  Kristo. “Risasi zinapigwa, mioto inayowashwa katika makanisa yetu na
  mabomu yanayolipuliwa yasiwe sababu ya kututia hofu. Imani yetu haiko
  katika miili bali iko mioyoni mwetu,” alisema.

  Askofu Mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha akitoa shukrani kwa
  niaba ya Kanisa Katoliki aliwashukuru wote waliofika kuwafariji
  kutokana na tukio hilo na kuwathibitishia kuwa kama Kanisa wameguswa
  na moyo waliouonyesha.

  “Tupige goti, ndiyo kazi tuliyonayo. Tupige goti ili Mungu awafichue
  hawa watu, aufichue mfumo wao wa kiovu, na awape nguvu viongozi wetu
  wao ni kama sisi na iko siku watatoa hesabu mbele ya Mwenyezi Mungu,”
  alisema.

  Aliwasihi waumini wote kutoogopa na kuendelea kuomba ili waliohusika
  na uovu huo Mungu awafichue na kuwaonyesha hadharani. “Ninaambiwa
  msiogope, hakuna kutishwa kwa namna yoyote tunaposimama na Kristo...
  sisi hatupaswi kuogopa kwa sababu Kristo alishinda mauti,”
  alisisitiza.

  Watu 66 waliathirika kutokana na mlipuko huo uliotokea Mei 5, mwaka
  huu ambapo watatu wamefariki dunia na kati ya wagonjwa 63 waliobakia,
  wanane walihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, wengine waliotibiwa
  na kuruhusiwa kurudi nyumbani, na baadhi wanaendelea kupatiwa matibabu
  mjini Arusha.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, MEI 10, 2013.

  0 0


   Washiriki katika semina ya kujadili changamoto za soko la muziki Afrika Mashariki wakifuatilia moja ya mada kwenye hotel ya Crasted Crane mjini Jinja, Uganda
   Mwanmuziki kutoka Kenya, Winyo akitumbuiza katika moja ya matamasha yanayoambatana na semina ya kujadili changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki.
   Wanamuziki wakiimba wimbo wa ushirikiano katika moja ya matamasha yanayoambatana na semina ya kujadili changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki, kutoka kushoto ni Mani Martin kutoka Rwanda, Shamsila kutoka Arusha Tanzania na Staffi kutoka Uingereza.

  Kwa picha za matukio zaidi tembelea DOADOA 2013

  0 0


   

  Ndugu wananchi Tarehe 24/4/2013 ulifanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Ruaha. Vyama vilivyoweka wagombea vilikuwa CCM na CHADEMA. Hata hivyo mgombea wa Chadema alienguliwa baada ya CCM kumuewekea pingamizi kwa sababu alikuwa na mapungufu yaliyomwondolea sifa ya kuwa mgombea kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi CCM ilitangazwa mshindi na siku hiyo hiyo Chadema wakashinda kitongoji. 


  Wana CCM waliyapokea matokea bila vurugu na wakakubali kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji ni wa CHADEMA. Tarehe 09.05.2013 ili kuwa siku ya kukabidhiwa rasmi ofisi kwa Mwenyekiti mpya wa Kijiji cha Ruaha, lakini wenzetu CHADEMA wakataa kumkubali huyo Mwenyekiti na wakaamua kuanzisha vurugu kubwa sana katika kijiji cha Ruaha na maeneo ya karibu yaliosababisha uharibifu mkubwa wa mali.Wamechoma nyumba, wamefunga barabara na kusababisha uvunjifu mkubwa wa amnai eneo hilo. 

  Tunalaani sana vurugu hizo zilizosababishwa na kundi la watu wenye nia mbaya na nchi hii wanaotaka kuivunja amnai tulionayo, wananchi wa morogoro na Watanzania kwa ujumla Tunavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua mara moja kurudisha amani ili wananchi waendelee na shuguli zao za kila siku za kujiletea maendeleo. Kwa wale wote waliochochea vurugu hizo wachukuliwe hatua mara moja na sheria ichukue mkondo wake.


  Imetolewa CCM Morogoro
  10.05.2012

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Dkt.Tomaz Salomao mjini Cape Town Afrika ya Kusini leo wakati wa kikao cha kamati hiyo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(Watatu kushoto) akiongoza kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC kilichofanyika jijini Cape Town Afrika ya Kusini leo.Wengine katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo akiwemo mwenyeji Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(kulia),Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Namibia Bibi Netumbo Nandi-Ndaitwa(kushoto) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakitoka katika ukumbi wa hoteli ya Westin jijini Cape Town Afrika ya Kusini mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalma ya SADc kilichofanyika leo.Rais Kikwete alikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mkurugenzi Mtendaji na mratibu wa asasi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bwana Mark Suzman jijini Cape Town Afrika ya Kusini.Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Adam Malima.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagana na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Misaada la Marekani USAID Dkt. Rajiv Shah muda mfupi baada ya kufanya naye mazungumzo katika ukumbi wa Cape Town Convention Centre jana.Picha na Freddy Maro.

  0 0  Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (CHADEMA),Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau mkubwa wa Muziki hapa nchini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semina hiyo iliyohusu kampeni maalum ya “Twede Zetu” iliyofanyika kwenye  ukumbi wa African Dreams mjini Dodoma leo , Kampeni hiyo ikizungumzia na kuhamasisha vijana kuwa wabunifu na kutumia fursa zilizopo ili kujikwamua kimaisha lakini pia kuleta maendeleo kwa wasanii wenyewe na taifa kwa ujumla,aidha  Watu mbalimbali walichangia katika semina hiyo. ambao ni Patrick Ngowi, Zenno Ngowi Msanii Mrisho Mpoto na Mh Zitto Kabwe mwenyewe.

  Kesho kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa. 
   Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la   Patrick Ngowi  kutoka kampuni ya Helvetic Solar Contractors, akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ujasiliamali na pia alielezea ni namna gani amefanikiwa mpaka kufikia kumilimiki lampuni yake binafsi kupitia fursa alizokuwa akikumna na nazo na kuzifanyia kazi vilivyo. 
   Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiuliza swali kwa Mh Zitto Kabwe kuhusiana na mambo mbalimbali ya ujasiliamali na namna ya kuzitumia fursa hizo katika kujikwamua kimaisha.
   Mh Zitto kabwe akimsikiliza mmoja wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa akiulizwa kuhusiana na suala la fursa zinazopatikana kwa vijana na namna ya kuzitumia katika ujumla wa kujikwamua na ugumu maisha,ambapo watanzania wengi wamekuwa wakizilalamikia.  Mtangazaji wa clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast-Gerald Hando akiikaribisha Meza kuu pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds Media Group unaokwenda sambamba na ujumbe wao thabiti kabisa  ulioitwa MADE IN TANZANIA,ikiwa na hamasa kubwa ya kuleta msingi wa fursa kwa watanzania, msukumo ikiwa ni kuwashawishi watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa hizi kwa umoja na maendeleo ambapo TWENZETU, inakuwa neno rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa  ikiwemo semina ya fursa kwa watanzania,burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania zitapatikana uwanja wa jamhuri mapema leo mchana.
  Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Zenno  Ngowi kutoka kampuni ya Tanzania Home Expo akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ardhi,ujenzi,na mengineyo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria kwenye semina hiyo leo mjini Dodoma.


  Mmoja wa wasanii mahiri wa Mashairi,Mrisho Mpoto akifafanua jambo kuhusiana na mambo mbalimbali katika suala zima la wasanii kujipa nafasi ya Fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yao na namna ya kuzifanyia kazi na kuziboresha zaidi.
  Mhe Zitto Kabwe akiwasili kwenye semina hiyo mapema leo,ambaye pia alikuwa ni mmoja wa wasemaji wa semina hiyo.
  Pichani ni washiriki wa semina hiyo kutoka sehemu mbalimbali mjini Dodoma leo.

  Baadhi ya washiriki wakifuatilia jambo kwenye semina iliyokuwa ikiendelea mapem leo kwenye hoteli ya African Dreamz,nje kidogo ya mji wa Dodoma.
  Mtangazaji wa Clouds FM,Loveness Love a.k.a Diva akijitambulisha kwenye semina hiyo

  Mtangazaji wa Clouds FM,Shaffih Dauda akijitambulisha kwenye semina hiyo.
  wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo iliyoibua changamoto nyingi.
  Kutoka Clouds FM,Millard Ayo,Dina Marios pamoja na Zamarad wakifuatilia jambo
  Mtangazaji wa Clouds FM,Arnold Kayanda Diva akijitambulisha mbele ya washiriki waliofika kwenye semina hiyo.
  Baadhi ya wasanii wakiwa ndani ya semina hiyo katika harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi zao,ambapo matembezi ya hisani yamepangwa kufanyika kesho na Waziri Mkuu Mh.Pinda anatarajiwa kuyapokea matembezi hayo.
  Msanii Afande Sele na Msanii mwenzake wakiwa ndani ya semina hiyo wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa.
  Mtangazaji wa Kipindi cha jahazi,Mussa Hussein akijitambulisha.
  Mtangazaji wa Clouds FM,B Dozen akijitambulisha
  Mbwiga Mbwiguke nae kama kawa akijitambulisha kwa washiriki wa semina hiyo.
  Zamarad Mketena akijitambulisha pia.
  0 0

  Moja ya barabara za mitaa kata ya Iwawa Makete mjini zikiwa zimelundikwa vifusi kwa zaidi ya miezi mitatu sasa huku kukiwa na kibao kikionesha barabara imefungwa ilihali magari yanapita hivyohivyo licha ya maelekezo ya kibao hicho(Habari/picha na Edwin Moshi)
  Vifusi vikiwa vimelundikwa barabara ya kuelekea hospitali ya wilaya ya Makete 
  Hapa inalazimu magari kupita kwenye mifereji
   Vifusi vingine hadi vimeyeyuka kutokana na kukaa muda mrefu
  Wananchi wa kata ya Iwawa wilayani Makete ambao ni watumiaji wakubwa wa barabara za mitaa katika kata hiyo, wameiomba halmashauri ya wilaya ya Makete kusambaza vifusi vilivyopo katika barabara hizo ambavyo vimewekwa zaidi ya miezi mitatu sasa

  Wananchi hao wametoa ombi hilo kufuatia adha wanayoipata hasa wanapotumia magari kwa kuwa barabara hizo zimekuwa nyembamba hivyo kuleta usumbufu kwa watumiaji hasa wakati wa magari kupishana


  Mmoja wa mwananchi aliyezungumza na ripota wetu Bw. Sipati Mbwilo amesema wanashangaa vifusi hivyo kukaa muda mrefu barabarani bila kusambazwa, jambo linalosababisha usumbufu kwa watumiaji na wakati mwingine kulazimika kuzunguka kupita kwenye barabara nyingine ili kufuata huduma hata kama huduma hiyo ipo jirani

  “Unajua braza unaweza kukuta umepata kazi ya kupeleka kuni ama kwenda kuchukua kuni kwa gari, lakini inakulazimu uzunguke umbali mrefu ili kukwepa hivi vifusi ambavyo hatujui vitasambazwa lini, ni bora wangeviweka pindi watakapokuwa tayari kuvisambaza leo mwezi wa tatu vifusi vipo barabarani mambo gani haya” alisema Mbwilo

  Naye dereva wa lori aliyejitaja kwa jina la Kisauti amesema vifusi hivyo vinawapa tabu wanaoendesha magari makubwa kutokana na wembamba wa barabara na wakati mwingine kulazimika kukataa baadhi ya kazi wanazozipata kutokana na magari yao kushindwa kupita kwenye barabara hizo

  Ripota wetu amezungumza na mhandisi wa ujenzi wilaya ya Makete Mhandisi Samwel Ndoveni ambaye amekiri kuwepo hali hiyo lakini amesema kero hiyo itaondolewa hivi karibuni kwa kuwa msimu wa mvua uliokuwa ukikwamisha utekelezaji wa zoezi hilo unamalizika na mkandarasi ataanza kazi mara moja

  Amesema kwa mwaka huu mvua zilinyesha kwa wingi na ndiyo maana zoezi hilo lilishindwa kutekelezeka kwa wakati kama ofisi yake ilivyokuwa imepanga

  “Ni heri lawama za kutokusambaza vifusi zitupate kuliko tungesambaza vifusi wakati mvua inanyesha, matokeo yake tungetengeneza tope jingi na barabara zisingepitika huo ungekuwa ni uharibifu wa fedha za serikali” alisema Mhandisi Ndoveni


  0 0
 • 05/11/13--07:45: dc makete asisitiza amani

 •  Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro

  Serikali wilayani Makete imewataka wananchi wa wilaya hiyo kuwa makini na kutoa taarifa kwa viongozi pale wanapokiona kitua ambacho hawakifahamu ama wanapomuaona mtu ama watu wageni ambao hawawafahamu katika maeneo yao

  Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu kulipuka kitu kinachosadikika kuwa ni bomu katika kanisa moja jijini Arusha

  Matiro amesema kufuatia tukio hilo lililotokea Arusha hakuna budi wananchi kuwa makini kwa kuwa kumekuwa na muingiliano wa watu ambao wanafika kwenye wilaya yake na wengi wao wakiwa wageni lakini hawatoi taarifa na pia hakuna mtu mwingine ambaye anatoa taarifa kuwa kuna watu wageni ambao hawafaamiki na wameingia kwenye eneo hilo

  Amesema si lazima watu ama mtu huyo afike kwako lakini endapo ataonekana hata kwa jirani ni lazima utoe taarifa ili ahojiwe na kujulikana ametoka wapi.

  “zamani kulikuwa na utaratibu mzuri ambao hivi sasa tutaurejesha, watu walikuwa hawakubali kumpokea mtu yeyote mgeni bila taarifa zake kujulikana wazi ikiwemo kwa viongozi, lakini hivi sasa hicho kitu hakipo” alisema Matiro

  Katika hatua nyingine mkuu huyo amewataka wale wote wenye kanda ama CD zenye uchochezi wa kidini kuzisalimisha kwenye vyombo vya usalama kwa kuwa ni kosa kisheria na atakayekamatwa nazo atachukuliwa hatua za kisheria

  Amesema cd hizo zinachochea uvunjifu wa amani na zitaweza kupelekea vita ya kidini ambyo ni vita hatari kuliko zote, hivyo kuwataka wenye nazo kuzipeleka wenyewe kwenye vyombo vya usalama na kusisitika kila mtu kulilinda amani iliyopo wilayani mwake isivunjike

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymon Moshi mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 11, 2013 akitokea Cape Town, Afrika ya Kusini, alikohudhuria mkutano wa nchi SADC.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali (kulia) mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 11, 2013 akitokea Cape Town, Afrika ya Kusini, alikohudhuria mkutano wa nchi SADC. PICHA NA IKULU

  0 0

   

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani wimbo wake unaotamba kwa sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao Majanga,mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri jioni ya leo wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua msimu wake mpya kwa wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na kufanyika kwa semina ya fursa kwa Watanzania.

  Aidha msimu huo umekwenda sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA,ambapo msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa hizo kwa umoja wa maendeleo,huku neno TWENZETU likitumika kama neno rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.
   Msanii mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya leo.alipowaangushia maneno kadhaa na umati kulipukw ana mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao mpya.
   Maelfu ya Watu wakiwa ndani ya uwanja wa jamuhuri jioni ya leo wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds FM walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM kilipokuwa kikizindua msimu wake mpya.
  Pichani shoto ni Mkurugenzi wa vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri jioni ya leo,wakati tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea,Nape alifika uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha maelfu ya watu.
   Palikuwa hapatoshi uwanja wa jamuhuri Dodoma jioni ya leo.

    Msanii wa mkongwe wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Afande Sele a.k.a Baba Tunda  akikamua kwa shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM.
  0 0

  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu huyo katika kutoa elimu  kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea,anaeshuhudia kulia ni Meneja uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo aliambatana na baadhi ya wafanyakazi wa vodacom katika kutoa elimu  hiyo kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea.
   Mkuu wa kitengo cha huduma za  mtandao Vodacom Tanzania Bw.Andrew Lupembe,akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga  katika kutoa elimu  kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea.
   Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Bi.Ena Mwangama,akimkabidhi kitabu  cha sayansi mmoja wa wanafunzi wa shule ya  Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa vodacom Tanzania,walipofika shuleni hapo kutoa elimu ya Usalama Barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza  Mei 6 hadi 12.kila mwaka. 
   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania , wakiwafundisha wanafunzi wa shule ya msingi  ya Mapambano ya jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapa msaada wa vitambu vya sayansi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya  Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga  (hayupo pichanini) kutoa elimu  kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.
   Meneja wa Vodacom Tanzania Grece Lyon  (kushoto ) na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Uzuri Tandale ya jijini Dar es Salaam, (kulia)wakionyeshwa vitabu vya sayansi na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kukabidhiwa na wafanyakazi wa Vodacom, Ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga  (hayupo pichanini) kutoa elimu  kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.
   Meneja  wa Vodacom  anaye husika na masuala ya elimu Grece Lyon akimkabidhi  mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ya Uzuri Tandale jijini Dar es Salaam, Vitabu vya Sayansi  wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga  (hayupo pichanini).

  Meneja Mawasiliano wa Vodacom Rukia Mtingwa akiwaongoza wanafunzi wa shule ya msingi ya Uzuri iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam, kwenda kujifunza jinsi ya kutumia alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,kila mwaka .Wafanyakazi wa Vodacom waliambatana na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga   (hayupo pichanini)  Pia walitoa msaada wa vitu  mbalimbali ikiwemo vitabu vya Sayansi.


  0 0


   
  Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

  CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

  DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

  Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.

  Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
  hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
  Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
   
   mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali  na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.


  0 0


  0 0


  0 0  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akiwa ameshikilia Tuzo ya Bia ya Safari Lager mara baada ya kuipokea mkoani kwake mwishoni mwa wiki ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  ilikuwa Mkoani Iringa.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akizungumza na wananchi wa Mji wa Iringa katika Uwanja wa Mwembe Togwa  wakati upokeaji Tuzo za Bia ya Safari Lager mkoani kwake mwishoni mwa wiki ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  ilikuwa Mkoani Iringa. Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo

  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kulia) na Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma wakinyanyua Tuzo za Bia ya Safari Lager ilizoshinda katika mashindano ya Bia Afrika yaliyofanyika nchini Ghana. Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Mwembe Togwa mjini Iringa wakati wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo ilizoshinda Bia yake ya Safari Lager.

  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akiwa ameshikilia Tuzo ya Bia ya Safari Lager mara baada ya kuipokea mkoani kwake mwishoni mwa wiki ikiwa ni ziara maalum ya Tuzo hizo kusherehekea pamoja na Watanzania Ushindi wa Bia hiyo ya Kitanzania barani Afrika.Ziara ya Tuzo za Bia ya Safari Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)  ilikuwa Mkoani Iringa.

  <!--[if gte mso 9]>

older | 1 | .... | 79 | 80 | (Page 81) | 82 | 83 | .... | 1897 | newer