Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

MAJAMBAZI YAUA NA KUJERUHI JIJINI MWANZA.

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, SACP Justus Mamugisha, akitoa taarifa kwa wanahabari.

Watu wawili wameuawa Jijini Mwanza kwa kupigwa risasi na Majambazi, huku Wengine saba wakijeruhiwa katika tukio la uvamizi wa duka lililokuwa likitoa huduma mbalimbali za kifedha.
Habari Zaidi BONYEZA HAPA.

KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA CHA JANGO ZAIDA ORPHANAGE CENTRE CHAPATIWA MSAAADA

$
0
0
 Watoto Wanaoishi kwenye Kituo cha Jango zaidi Orphanage sinza jijini Dar es salaam wakiwa Katika Picha ya Pamoa leo walipotembelewa na Wadau waliosoma Pamoja Shule ya Sekondari Bwawani.
 Baadhi ya Vitu mbalimbali vilivyotolewa.
 Wadau waliosoma Shule ya Sekondari Bwawani wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Mama Mlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Jango Zaida Orphanage centre  walipokitembelea kituo hicho na Kutoa Msaada ya Vitu MBalimbali kwajili ya Kusaidia Kutatua Changamoto Mbalimbali zinazokikabili kituo hicho.
Picha ya Pamoja na watoto wanaoishi katika Kituo Hicho

Mgombea uwakilishi Marekani William Jawando ahojiwa Kilimanjaro Studio, azungumza na Diaspora

$
0
0
Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando, leo alihojiwa katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland nchini Marekani ambapo alizungumzia kuhusu mikakati yake katika kuisaidia diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla.

Will, ambaye akishinda atakuwa ni mtu wa pili aliyezaliwa na Baba aliyetoka Afrika kuingia bungeni humo (baada ya Rais Obama) ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ambavyo uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni muhimu Zaidi nchini Marekani, na hasa kwa wakazi wenye asili ya Afrika waishio vitongoji vya Washington DC.

Ikumbukwe kwamba, inakadiriwa kuwa mmoja kati ya wazaliwa kumi wa Afrika walipo nchini Marekani, anaishi eneo hili, na nusu yao, wameingia nchini baada ya mwaka 2000. Hivyo amefafanua namna ambavyo kuwa na mtu mwenye kuelewa na kuwakilisha vema jamii hiyo, ni muhimu kwa jamii hiyo.

Aligusia pia namna ambavyo asili yake na makuzi yake yamechangia yeye kuingia katika kazi za kuihudumia jamii, akaeleza vipaumbele vyake kwenye uongozi wake ujao na pia wito alionao kwa jamii ya waAfrika walioko Marekani.Uchaguzi wa kuteuliwa kugombea kupitia chama cha Democrat utafanyika Aprili 26, lakini kura za mapema zitapigwa kati ya Aprili 14 na 21.
Kujua mengi kuhusu Will Jawando, maisha yake, kampeni na mipango yake, tembelea willjawando.com.

Anagombea kiti kilichoachwa wazi na mwakilishi Chris Van Hollen ambaye ameamua kugombea kiti cha Seneti kinachoachwa wazi na Seneta Barbara Mikulski anayestaafu,Mahojiano kamili na Will Jawando yatakujia hivi karibuni.Baada ya mahojiano, Will alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wanaDiaspora wa Afrika waliokuwa ndani ya jengo ilipo studio.

Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akipata picha na Mubelwa Bandio baada ya mahojiano
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza na baadhi ya waAfrika waliohudhuria "Meet & Greet"

Michelle Jawando, mke wa mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza machache kuhusu umuhimu wa uchaguzi wa mwaka huu

Mubelwa Bandio akiendelea na maandalizi ya mwisho ya mahojiano na Will Jawando
Mmoja wa wadau wa Kilimanjaro Studio Harieth Shangarai akimpatia maelezo machache Will Jawando
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akiuliza maswali kuhusu uendeshaji wa Kilimanjaro studio
Mubelwa Bandio akitoa maelekezo kwa Will Jawando
Mahojiano yanaendelea

VIJANA WA KKKT IRINGA MJINI WAKIINGIZA IGIZO LA MATESO YA YESU KRISTO

$
0
0
Kijana wa kwaya ya vijana katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Iringa mjini Bw Ezekiel Mbyopyo akiwa ametundikwa Msalabani wakati akiigiza igizo la Mateso ya Yesu Kristo igizo lililofanyika Ijumaa kuu wakati wa tamasha la maneno Saba ya Yesu Msalabani (PICHA NA MATUKIODAIMABLOG) .
Vijana walioigiza kama wayahudi Brown Mwaipopo (kushoto) na Eston Mgaya wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Iringa mjini wakimuwamba Msalabani kijana mwenzao Ezekiel Mbyopyo wakati wa Igizo la mateso ya Yesu Kristo siku ya ijumaa kuu .
Mwonekano wa Kanisa hilo ambalo liliandaa Igizo la mateso ya Yesu .






Kijana aliyeigiza kama Simon akiwa amempokea Yesu Msalaba 



































NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA – ASHIRIKI USAFI KATIKA MTAA WA TPDC MIKOCHENI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina Kulia Akifyeka, katika Mtaa wa TPDC Mikocheni Jijini Dar es Salam leo kutekeleza agizo la Mh. Raisi la kufanya usafi, ambapo serikali imetenga kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi kuwa siku maalum ya usafi.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, akifanya usafi katika mtaro wa maji machafu katika mtaa wa TPDC, maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa siku ya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Kulia Bi Blandika Cheche Afisa Mazingira mkuu, na katikati Mkururugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC Bw. Boniventure Baya wakifanya usafi kwa pamoja katika mtaa wa TPDC, Mikocheni Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali, la kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi la kufanya usafi wa mazingira.

Aliyevaa shati ya blue Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira mh Luhaga Mpina akiweka taka katika gari la kuzolea taka katika mtaa wa TPDC Mikocheni JIjini Dar es salaam leo, Jumamosi ya mwisho wa Mwezi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la usafi wa Mazingira .

(Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Makamu wa Rais)

KIINGILIO TANZANIA NA CHAD 5,000/= TU

$
0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kundi G siku ya Jumatatu kati ya Tanzania dhidi ya Chad, bei ya chini ikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu.

Viingilio vya mchezo huo vimegawanyika katika makundi matatu, ambapo kiingilio cha juu kitakua shilingi elfu ishirini na tano (25,000) kwa VIP A, na shilingi elfu ishirini (20,000) kwa VIP B, na kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na orange itakua shiligi elfu tano (5,000).

Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho Jumapili saa 2 asubuhi katika vituo vinne ambavyo ni kituo cha mafuta Buguruni (Buguruni), Ubungo Oilcom (Ubungo) na Dar Live (Mbagala), na Jumatatu tiketi zitauzwa katika viunga vya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Wakati huo huo Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kubali kuwa mgeni rasmi katika mchezo kati ya Tanzania v Chad utakaochezwa siku ya Jumatatu jijini Dar es salaam.

TFF pia inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa kufanikisha ujio wa Waziri Mkuu kwa kufuatilia kwa karibu maombi ya TFF ya tarehe 21/03/2016 ya kumuomba Waziri Mkuu awe mgeni rasmi katika mchezo huo.

Kwa upande wa Taifa Stars iliyoweka kambi katika hoteli ya Urban Rose inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Chad.

Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Djibouti wanatarajiwa kuwaisli leo jioni ambao ni mwamuzi wa kati Djamel Aden Abdi, Abdilahi Mahamoud, Farhan Bogoreh Salim, Farah Aden Ali, huku kamisaa wa mchezo akiwa Andrea Abdallah Dimbiti kutoka nchini Sudani Kusini.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

AFYA SPORTS BARA YATAMBA NYUMBANI YAIFUNGA AFYA SPORTS ZANZIBAR 3-0

$
0
0
Mchezaji wa timu ya Afya Sports Bara, Robert Ndimbe (kulia) Bara akiwania mpira na Saidi Bundara Zanzibar (kushoto) kutoka Afya Sports ya Zanzibar. Mchezo huo umefanyika leo kwenye Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Afya Sports Bara 3-0 Afya Sports Zanzibar.
Kipa wa Afya Sports Bara, Salumu Saidi akidaka mpira ili kuokoa hatari langoni mwake leo.
Mchezaji wa Afya Sports Zanzibar, Abdulheri Thani ( mwenye jezi namba tatu) akijaribu kufunga bao mbele ya kipa wa Afya Sports Bara, Salumu Saidi katika mchezo wa tamasha la pasaka. Mchezo huo umefanyika leo kwenye Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)


Timu ya Afya Sports Bara imeifunga timu ya Afya Sports Zanzibar mabao 3-0 katika mchezo uliyofanyika leo katika kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.

Bao la kwanza limefungwa dakika ya 12 kipindi cha kwanza na mchezaji machachari kutoka Afya Bara, Ali magoma.Katika kipindi cha pili Muhaji Kampala alitikisa nyavu na kufunga bao la pili, huku bao la tatu likiwekwa kimiani na Ali Magoma.

Katika mchezo huo wachezaji wa Bara walionekana kuwa makini kulinda lango lao, huku morali ya wachezaji hao ikiwa juu katika kuhakikisha timu yao inaibuka na ushindi.Kwa matokeo hayo timu ya Afya Sports Bara imeibuka kidedea ambapo mechi nyingine inatarajiwa kuchezwa Jumatatu.

Mchezo huo ni Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka kati ya Watumishi wa Sekta ya Afya Zanzibar na Watumishi wa Sekta ya Afya Bara kwa lengo la kuendeleza undugu na ushirikiano uliopo.

MSAMA AWAONYA WANAOTUMIA JINA LA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0

MWENYEKITI wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama amewaonya wanaotumia jina la Tamasha la Pasaka atawachukulia sheria kwa sababu jina hilo limesajiliwa kisheria na serikali.

Akizungumza akiwa jijini Mwanza Msama alisema mwaka huu tamasha hilo halifanyiki jijini Dar es Salaam ambako idadi kubwa ya wakazi wa jijini Dar es Salaam wanadhani tamasha hilo linaandaliwa na kampuni yake ambayo inajishughulisha na nyimbo za injili.

“Nawatahadharisha wanaotumia jina la Tamasha la Pasaka wajiandae kisheria kwa sababu linalotambulika ni Msama Promotions ambayo inajishughulisha na waimbaji na nyimbo za Injili, hivyo wajanja wachache wanataka kuharibu taswira ya Tamasha la Pasaka,” alisema Msama.

Msama alisema anapokea simu nyingi kutoka kwa mashabiki wa muziki huo wakiuliza Tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam ambako aliwajibu mwaka huu tamasha hilo linafanyika mikoa ya Geita, Mwanza na mji wa Kahama, hivyo Dar es Salaam halifanyiki.

Msama alisema mwaka huu nguvu zao wamezielekeza mkoani Geita, Mwanza na mji wa Kahama hivyo wakazi wa mikoa hiyo wakae mkao wa kula kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa muziki huo.

“Nawaomba wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kwani leo litafanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku kesho linafanyika mjini Kahama kwenye uwanja wa Taifa mjini humo.

Aidha Msama alitumia fursa hiyo kutangaza viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000, hivyo wajitokeze kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo.

MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR AAPISHWA RASMI LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar
Pichani Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said .
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said akipitia hati ya kiapo kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja,
Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Nd,Ibrahim na Mzee na Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar George Kazi ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said leo Ikulu Mjini Unguja
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Abdalla Mwinyi Khamis na Mstahiki Meya wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwaMwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said leo Ikulu Mjini Unguja
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said akiwa katika ukumbi wa mikutamo Ikulu Mjini Unguja na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mshibe Ali Bakari kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein
Viongozi mbali mbali na watendaji waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akiwa katika picha na Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na familia yake baada ya kumuapisha rasmi leo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.(Picha na Ikulu.]

MBUNGE WA MONDULI NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI WAONGOZA HARAMBEE YA KUMFARIJI BI.MARIAM OMARY

$
0
0
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Isack Joseph(kulia)akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo,Julius Kalanga na viongozi wa serikali ya Kijiji na Kata ya Selela wakiangalia nyumba ya mfanyabiashara , Bi Mariam Omary iliteteketea kwa moto na mali zote kuteketea na baadaye kuongoza harambee iliyowezesha kupatikana fedha taslimu na ahadi ya sh 11 milioni.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Isack Joseph(kushoto) na Mbunge wa Jimbo hilo,Julius Kalanga wakimfariji mfanyabiashara wa Kijiji cha Selela,wilayani humo Bi Mariam Omary ambaye nyumba yake iliteketea kwa moto na kusababisha hasara ya mamilioni .Mwenyekiti wa alimashauri alitoa matofali 4,000.
Mbunge wa Monduli mkoa wa Arusha,Julius Kalanga akiangalia nyumba iliyoteketezwa kwa moto,Alitoa mabati 100 kwaajili ya ujenzi wa nyumba mpya.
Bi Mariam Omary mkazi wa Selela wilaya Monduli akizungumza mkasa uliompata .
Wakina Mama wakitoa michango yao ya hiari kumfariji Bi Mariamu Omary.Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com ,Arusha

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA BUNGE LA ISRAEL

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa kwanza kulia) aliyemtembelea Ofisini kwake leo tarehe 26 Machi, 2016,Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot aliyemtembelea Ofisini.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot aliyemtembelea Ofisini.Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mzee Ibarahim Kaduma ambaye ni Mweyekiti wa Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT). Mzee Kaduma aliambatana na Ujumbe wa Israel uliomtembelea Spika ambao ndio wafadhili wa KLNT.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot na viongozi wengine waliombatana na ujumbe huo.(Picha na Ofisi ya Bunge)

SHUKRANI WADAU ; MTOTO EBENEZA PEMBE AMEANZA MATIBABU YA SARATANI YA NGOZI HOSPITALI YA MUHIMBILI

$
0
0
Mtoto EBENEZA PEMBE
........................................
                                    NDUGU ZANGU HABARI ZA WAKATI HUU;


SIKU CHACHE ZILIZOPITA TULILETA TANGAZO,  OMBI LA MSAADA WA MATIBABU KWA MTOTO EBENEZA PEMBE ANAYESUMBULIWA NA SARATANI YA NGOZI.

NAWASHUKURU SANA RAFIKI ZANGU MLIOGUSWA NA KUTOA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI, LEO KUPITIA ACCOUNT YA MTOTO EBENEZA  TUMEKABIDHI KIASI CHA SHILINGI MILIONI MOJA LAKI SITA NA ELFU SITINI NA NANE (1,668,000/-) MLIZOCHANGA KWA UPENDO WENU MKUBWA.


EBENEZA NA MAMA YAKE WAPO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI WAKIENDELEA NA MATIBABU, NA TAARIFA NJEMA TULIYONAYO NI KWAMBA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF, BAADA YA KUONA TANGAZO LILE WAMEMWANDIKISHA EBENEZA KWENYE FAO LA TOTO CARD HIVYO ATATIBIWA KWA GHARAMA ZA MFUKO HUO.

EBENEZA NA MAMA YAKE WANAWASHUKURU SANA KWA MOYO WENU WA KUMSAIDIA NA TUWANAWAOMBEA BARAKA TELE KWA MWENYEZI MUNGU.

 SISI PIA KWA UPANDE WETU TUNAPENDA KUWASHUKURU NYOOTE MLIOJITOA KWA HALI NA MALI KUFANIKISHA SUALA LA KUMSAIDIA MTOTO EBENEZA.

TUNAWASILISHA ; SALUM MWINYIMKUU

                       SILVANUS KIGOMBA 

TAARIFA YA SERIKALI YA MKOA WA DODOMA KWA UMMA

$
0
0
                                              JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU


TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Ndugu Wanahabari, tukiwa tunaelekea sikukuu ya pasaka, Serikali ya Mkoa wa Dodoma imeona ni vyema ikakutana na wawakilishi wa vyombo vya habari hapa Mkoani Dodoma, ili kupitia vyombo vya habari, tupate fursa ya kuweka wazi kwa wananchi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla masuala ya msingi ambayo yamejiri hapa Mkoani Dodoma.
Awali, usiku wa kuamkia jana kuna tukio tunaloweza kuita la ujambazi lilitokea kama majira ya saa 8 usiku ambapo kundi la watu takribani saba (7) ambao bado hawajafahamika walivamia ofisi za Halotel Mkoani Dodoma kwa lengo la kutaka kufanya uhalifu ambapo waliwavamia askari wawili waliokuwa wakilinda Ofisi hiyo, ambapo pamoja na athari nyingine zilizojitokeza; walipora silaha aina ya SMG na kumjeruhi askari mmoja ambaye alilazwa kwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa jana hiyohiyo.


Hadi hivi sasa Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea kulifanyia kazi suala hilo ambapo hadi tunavyozungumza sasa tayari silaha hiyo iliyoporwa imeshapatikana, uchunguzi zaidi wa suala hilo unaendelea kubaini watu wote waliohusika. Kufuatia suala hilo, Serikali ya Mkoa wa Dodoma, kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana anapenda kutoa tamko lifuatalo: 
·        Kwanza kabisa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana analaani vikali tukio hilo la uhalifu na kuwa halivumiliki na halikubaliki katika Mkoa wa Dodoma na Mikoa mingine hapa nchini na amewataka wananchi wema kutoa ushirikiano kwa vyombo vya Dola ili kuwabaini wahusika na kukomesha matukio kama hayo.

·        Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana analiagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kuwabaini wale wote waliohusika katika tukio hilo la uhalifu,ili kuwatia mbaroni na kuwachukulia hatua kali za kisheria. Aidha amelitaka jeshi la polisi kujipanga vizuri na kuhakikisha kuwa tukio hili ni la mwisho na halijitokezi tukio jingine la aina hii.

·        Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kina ili kubaini kama kuna dalili zozote za kuwepo kwa uzembe wa aina yoyote kwa askari hao waliokuwa wanalinda Ofisi hiyo, na endapo itabainika kulikuwa na uzembe basi Jeshi la polisi lichukue hatua kali kwa askari hao waliohusika.


MKUU WA WILAYA YA GEITA AWATAKA WANANCHI WA MKOA HUO KUMRUDIA MUNGU NA KUACHA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie, ambaye 
ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la pasaka,baada ya kukaribishwa jukwaani,alizungumza na mashabiki wa muziki wa injili waliohudhuria katika tamasha hilo,alisema kuwa ujio wa tamasha hilo ni fursa pekee kwa Wananchi wa mkoa wa Geita kumrudia Mungu na kutubu ili kuacha tabia mbaya inayoupaka matope mkoa huo kwa mauaji ya walemavu wa ngozi Albino pamoja na Vikongwe.

"Hii ni fursa ya kipekee kwetu sisi Wana Geita ya kuwa na hofu ya Mungu,kuepuka kutenda maovu na badala yake tumrudie Mungu wetu,tutendeane mema,kwa sababu Wanadamu wengi wa leo wamekosa hofu ya Mungu',alisema Mh.Mangachie huku akiishukuru kampuni ya Msama Promotion na Mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa kuandaa tamasha hilo .

Waimbaji mbalimbali wameshiriki katika tamasha hilo ambao ni Upendo Nkone, Bonny Mwaiteje, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Jesca BM, Jennifer Mgendi, Mwimbaji kutoka Zambia Ephraim Sekereti, Waimbaji kutoka Nchini Kenya Solomon Mukubwa , na Mtanzania Faustine Munishi pamoja naye Christopher Muhangila.

Matamasha hayo yataendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na keshokutwa litafanyika tamasha lingine kama hilo mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion chini ya mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa udhamini wa magazeti ya Dira, Dira TV na Dira FM na linafanyika kila mwaka katika kipindi cha sikukuu za Pasaka (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-GEITA)
20
mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akitoa salamu zake za shukurani kwa kampuni ya Msama Promotion kwa kuandaa tamasha la pasaka katika mkoa wa Geita wilaya ya Geita kwa ni jambo jema kuwahubiria amani wananchi wa Geita ili wamrudie Mungu na kuacha mauaji ya Albino na Vikongwe.
21
Waimbaji Solomon Mukubwa kulia , Bonny Mwaiteje kushoto wakimpiga tafu Mwimbaji mwenzao Christopher Muhangila katikati wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani.
1
Mmoja wa Mashabiki wa Tamasha la Pasaka pamojana mashabiki wengine waliohudhuria katika Tamasha la Pasaka lililofanyika mjini Geita Mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire wakiimba kwa kuzinguka ukumbi huo wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani na kuwafanya wavutiwe na tamasha hilo kiasi cha kushindwa kukaa kwenye viti wakizunguka huku na kule huku baadhi wakiwa wamebeba viti juu juu.
9
Mwimbaji Jennifer Mgendi naye akafanya mambo makubwa jukwaani kama anavyoonekana.
5
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akirekebisha sauti katika mitambo wakati tamasha hilo likiendelea huku DJ akiangalia.


23
Mwimbaji Jesca BM akifanya vitu vyake jukwaani.
4
Mashabiki wake wakiitikia na kuimba kwa hisia wakati mmwibaji huo akiimba jukwaani.
6
Mama akifurahia uimbaji na uponyaji kutoka kwa waimbaji katika tamasha hilo huku akiwa amemshikilia mtoto wake mchanga.
7
Maadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia waimbaji kwa makini.
8
Mwimbaji Martha Baraka na kundi lake wakitumbuiza jukwaani huku baadhi yamashabiki wakipata picha kwa simu.
10
Mwimbaji Ephraim Sekereti akisalimiana na mdau mkubwa wa Msama Promotion Bw. Silas huku akitaniana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie wa tatu kutoka kushoto waliosimama mara baada ya kumaliza kuimba.
12
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba jukwaani huku mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akicheza pamoja na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na mashabiki wengine.
13
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake walioonekana kuhamasika na nyimbo zake.
141516
Mwimbaji Bonny Mwaiteje naye akafanya mambo makubwa jukwaani huku akipewa sapoti na mashabiki wake.
171819
Mwimbaji Bonny Mwaiteje akiwa amewabeba wacheza shoo wake mara baada ya kumaliza kuimba jukwaani hii ilikuwa ni staili ya aina yake.
20
mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akitoa salamu zake za shukurani kwa kampuni ya Msama Promotion kwa kuandaa tamasha la pasaka katika mkoa wa Geita wilaya ya Geita kwa ni jambo jema kuwahubiria amani wananchi wa Geita ili wamrudie Mungu na kuacha mauaji ya Albino na Vikongwe.
21
Waimbaji Solomon Mukubwa kulia , Bonny Mwaiteje kushoto wakimpiga tafu Mwimbaji mwenzao Christopher Muhangila katikati wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani.

MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 ZINAFANYIKA JUMAPILI HII VIWANJA VYA KIA,KILIMANJARO

$
0
0
Mratibu wa Mashindano ya Mbio za Magari ya Vaisakh Rally 2016 ,Faheem Alooakizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani ) kuhusu maandalizi ya Mbio za Vaisakh Rally 2016 zinazofanyika Jumapili hii katika viwanja vya KIA. 
Zawadi kwa washindi.
Hari Singh Rally Team ni moja ya madereva walioingiza gari mpya aina ya Subaru za mwaka 2015 katika mashindano hayo.

Mratibu wa Mashindano ya Mbio za Magari ya Vaisakh Rally 2016 ,Faheem Aloo akiwa na Mwenyekiti wa matukio wa klabu ya Kilimanjaro Motorspot ,Juma Shaaban.
Mkuu wa Usalama wa Kampuni ya Security Group (SGA) Absolom Jailo akizungumza namna ambavyo kampuni hiyo imejipanga kuimarisha ulinzi katika mshindano hayo.
Mkuu wa Huduma ya Kwanza katika mashindano hayo Dkt Akshay Prataap akieleza namna walivyojipanga kutoa huduma ya kwanza endapo kutatokea tatizo kwa madereva wanaoshiriki mbio hizo.
Jamil Khan ataongoza team Evolution katika mashindano hayo.
Raia wa Italiano Piero Canobbio ni mmoja wa madereva ambao wanatajwa kuwa tishio katika mbio hizo ambaye anashiriki kwa mara ya kwanza akitokea nchini Kenya.
Magari ya Mashindano yakijipanga kwa ajili ya ukaguzi wa mwisho .
Gurjit Dhan Dereva anayepewa nafasi kubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.
Dereva Larry Horn anaingia katika mashindano hayo akiwa na gari aina ya Porche.
Baadhi ya magari yanayoshiriki mashindano hayo yanayofanyika Jumapili hii katika viwanja vya KIA,Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI YA TANZANIA HAINA MPANGO KWA KUTEKETEZA MENO YA TEMBO YALIYOHIFADHIWA

$
0
0
Serikali ya Tanzania imetoa tamko kuwa kwa sasa haina mpango wowote wa kuteketeza meno ya tembo yaliyohifadhiwa ambayo yametokana na vitendo vya ujangili na vifo asilia vya tembo.

Tamko hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress alipotembelewa na balozi huyo ofisini kwake kujadili maendeleo ya sekta ya Maliasili mchini.


Prof. Maghembe alisema hayo baada Balozi huyo wa Marekani hapa nchini kutoa pendekezo kwa Serikali ya Tanzania kuchoma sehemu meno ya tembo yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe mzito duniani juu ya dhamira ya Serikali kukomesha biashara hiyo haramu.


"Naomba niweke wazi kuwa kwa sasa hatupo tayari kuteketeza meno haya, tunaweza kuyatumia kwenye tafiti za kisayansi au vielelezo kwa ajili ya kesi za ujangili ambazo zipo mahakamani na nyingine ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi" Alisema Prof. Maghembe.


Zipo nchi mbalimbali duniani ambazo zimechukua hatua ya kuteketeza meno yake ya tembo yaliyohifadhiwa ikiwemo nchi jirani ya Kenya na Malawi ambapo inaaminika kuwa kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kushawishi Ulimwengu kukomesha biashara hii haramu ya meno ya tembo.


Nchi nyingine ni Chad, Ubelgiji, Ufaransa, China, India, Marekani na Ureno. Kwa upande wa nchi ambazo zina msimamo sawa na Tanzania katika kuendelea kuhifadhi meno yake ya Tembo ni pamoja na Afrika ya Kusini, Botswana na Zimbabwe.


Akizungumzia kuhusu kuendeleza sekta ya Maliasili nchini, Prof.Maghembe amemuomba Balozi wa Marekani Bw. Mark Childress kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta hiyo kwa kuleta wawekezaji mbalimbali kutoka Marekani kuja kuwekeza Tanzania pamoja na kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ujangili.


Aliongeza kuwa Tanzania ina fursa nyingi ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo hoteli za kitalii, fukwe za kisasa na kuendeleza vivutio mbalimbali vilivyomo hapa nchini.


Prof. Maghembe amemshukuru balozi huyo kwa misaada mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani ya kuendeleza sekta ya Maliasili nchini ukiwemo wa hivi karibuni wa mbwa maalum (Snifer Dogs) kwa ajili ya kusaidia utambuzi wa rasilimali za Maliasili zinazoweza kutoroshwa nje ya nchi kupitia bandari na viwanja vya ndege.


Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao baina ya Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress imeonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali ya Marekani imetoa misaada mbalimbali ambayo jumla yake ni dola za kimarekani Milioni 41.35 katika kusaidia eneo la uhifadhi hapa nchini.



Akizungumzia mahusiano baina ya Tanzania na Marekani Balozi Mark Childress alimueleza Prof. maghembe kuwa Serikali ya Marekani itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambapo pia ofisi yake ya ubalozi imeshatafuta wadau mbalimbali ambao wapo tayari kusaidia fedha, vifaa na mafunzo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi na mapambano dhidi ya ujangili. 

(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA PASAKA KANISA LA KKKT LA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa alipowasili kwa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mchungaji Charles Mzinga alipowasili kwa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Magufuli wakishiriki na waumini wengine Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Kwaya wakati wa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini huku akisikilizwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Chalres Mzinga baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mama Rebecca Malasusa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiombewa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Charles Mzinga wakati wa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiama na kikundi cha Matarumbeta na Kwaya baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiagana -na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Charles Mzinga wakati wa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia waumini baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadi ya wazee wa kanisa baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na mtoto Javiera Lyimo (9) anayesoma darasa la tano shule ya Genesis jijini baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFURI AITAKIA KILA LAKHERI TAIFA STARS ITAKAPOKWAANA NA TIMU YA CHAD HAPO KESHO UWANJA WA TAIFA

NAVY KENZO WATUA BUKOBA TAYARI KWA SHOW YAO USIKU HUU LINA'S NIGHT CLUB

$
0
0
Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo, Nahreel na Aika leo wametua Bukoba ikiwa ni mwendelezo wao wa "Kamatia Chini lights up Tour" ambapo usiku huu watashusha show yao ya Nguvu kwenye Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night uliopo Bukoba Mjini. Wasanii hao wanaletwa hapa Mjini Bukoba kupitia kampuni ya Sleek Events ya Jijini Mwanza.
Msanii Aika akishuka kwenye ndege leo hii kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba




Wadau wakipata picha ya pamoja na wasanii wa Kundi la Navy Kenzo

Kushoto ni Mr. Tega JassonMkurugenzi wa Sleek Events akitokelezea kwenye picha ya pamoja na msanii Aika, Faustine Ruta wa Bukobasports.com na kulia ni Bwogi.

TFF YATHIBITISHA KUJITOA KWA CHAD KATIKA MICHUANO YA AFCON 2017

$
0
0
Shirikisho la Soka nchini TFF  limethibitisha taarifa yetu ya awali  kwamba timu ya Taifa ya Chad  ‘Les Sao’ (pichani) imejiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.


Tovuti ya TFF inasema kwamba taarifa ya kujitoa kwa Chad imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) leo baada ya Les Sao kuandika barua ya kujitoka katika mashindano hayo ikiwa katika kundi G pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Misri.

Chad ilitarajiwa kucheza kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kundi G baada ya kucheza mchezo wa awali jijini N’Djamena katika ya wiki.
Katika mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1- 0 , bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya mchezo.





Kufuatia kujitoa kwa Chad, matokeo ya michezo yote iliyoihusisha timu hiyo yanafutwa, na msimamo wa kundi G kwa sasa unaongozwa na Misri yenye pointi 4, Nigeria pointi 2 na Tanzania pointi 1.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images