Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

VIJANA WAANDAA MSAFARA WA HISANI KWA KUTUMIA MAGARI KUPINGA UJANGILI NA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI

$
0
0
Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelezea makamilisho ya maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,kulia kwake ni Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele na kushoto kwake ni Mkuu wa matukio Kelvin Edes,Pembeni yake ni Mkurungezi wa Teamtezza Kennan Richard.
Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele akiongea na waandishi wa habari kuelezea kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,kulia kwake ni Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele na kushoto kwake ni Mkuu wa matukio Kelvin Edes,Pembeni yake ni Mkurungezi wa Teamtezza Kennan Richard .
Wawakilishi wa Bongo Ride charity cruise wakisikiliza kwa makini maswali ya waaandishi wa habari katika mkutano huo kuhusu kuhusu ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani. 
Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele akiteta jambo na Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani. 
Mkuu wa matukio Kelvin Edes ( Wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani. 
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia maelezo ya wawakilishi wa Bongo ride charity cruise kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani 


Dar Es Salaam, 24 Machi 2016 Vijana wa Bongo Ride, kwa ushirikiano wa vijana wenzao wa Team Tezza na TanzaniaZalendo wanayo furaha kuwatangazia umma wa watanzania kukamilika kwa maandalizi ya msafara(cruise) wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ) utaofanyika kuanzia tarehe 25 -27 machi ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,


Ujangili hapa nchini kwa miaka ya hivi karibuni umeongezeka ikiwa ni matokeo ya mahitaji makubwa ya pembe za ndovu,pembe za kifaru na pia ngozi ya chui na bidhaa mbalimbali za wanyamapori. Hivi sasa biashara ya wanyamapori na rasiliamali za asili imeshika nafasi ya nne kwa biashara haramu inayowafaidisha wengi duniani,baada ya madawa ya kulevya ,silaha na usafirishaji wa binadamu inakadiliwa kuwa na thamani ya dola zaidi ya 284 billion za kimarekani.


Hali hii inatisha licha ya kuwaeimisha vijana kuwa wanaweza kuwa mabalozi wa kulinda wanyamapori pamoja na rasilimali za nchi yao,pia wanatakiwa kutuma ujumbe watu waweze kuchukua hatua kuanzia ngazi ya kitaifa mpaka kimataifa.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa amesema “ tumezindua awamu ya tatu ya Bongo Ride Charity Cruise ikiwa ni matokeo ya kuweza kusaidia jamii.Tukiwa na washiriki zaidi ya mia 2 wa hapa nchini na zaidi ya washiriki elfu 2 Afrika mashariki. Katika awamu yetu ya kwanza tulifanya msafara wa hisani kusaidia wagonjwa waliopata ajali katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani kwa kuwapatia mashuka yakutandika pamoja na kujifunikia na pia Mwaka jana tuliweza kwenda Mkoani Morogoro na kusaidia watu waishio na virusi vya UKIMWI Morogogo (WAVUMO) ikiwa nia ni kuhamasisha amani na upendo katika nchi yetu na awamu hii tumeamua kufanya ”YOUTH AGAIST POACHING” ili kufikisha ujumbe kwa vijana wenzetu na serikali kwamba tnapinga ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani kama wazalendo na wapenda maendeleo.


“Malengo yetu ni kuwa na tukio la kihistoria tukiwa na nia ya kumfanya kijana wa Kitanzania kuwa na desturi ya kutembelea vivutio vilivyomo ndani ya nchi pamoja na kuwa balozi mzuri na mzalendo wa Nchi yake” Aliongeza Magesa


Mkuu wa matukio wa Bongo Ride Kelvin Edes akiongea alisema Tunategemea kuwa na siku tatu za mbio hizi za hisani za magari kuanzia Dar es salaam kuelekea Arusha tukiwa na washiriki zaidi ya mia 200 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Pia tutakuwa na muda wa kuongea na vyombo vya habari, kutembelea shule na kuzunguka katikati ya mji kuweza kuongeza uelewa juu ya janga la ujangili na kuhamasisha utalii wa ndani.


“Siku ya pili tarehe 26 tutaungana na washiriki mbalimbali wa Arusha na tutaelekea Hifadhi ya wanyama Tarangire na kujionea mambo mazuri ya hifadhi hiyo na kujifunza zaidi. Jambo hili litasaidia zaidi watu kuwapa hamasa ya kwenda kujionea vivutio vya hifadhi za ndani na kumfanya kijana ajionee utajiri uliomo ndani ya nchi yake.


Tunaamini kabisa kasi ya kuuliwa kwa maalbino imepungua kwasababu wao wenyewe wanaweza kuzitetea nafsi zao, lakini Tembo, Kifaru na wanyama wengine wanaokumbwa na janga la ujangili hawawezi kuzitetea nafsi zao na kuomba msaada, Hivyo sisi kama vijana tumejitolea kuwa mstari wa mbele kupaza sauti zetu na kutetea haki zao kwani nao wanastahili kuishi, ”Aliongeza


Meneja Mawasiliano wa Bongo Ride Krantz Mwantepele alinukukuliwa akisema kuwa vijana wakipaza sauti zao itaamsha matumaini kuwa imefika wakati kuwa ujangili ni jambo linalotakiwa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukomeshwa .


“Sisi kama vijana tunaumizwa na kuongezeka kwa matukio haya ya ujangili ,uhujumu wa rasilimali ni matukio yote yanayopangwa na watu wenye tamaa za mafanikio ya haraka na kutamalaki kwa rushwa miongoni kwa viongozi na wanajamii.”


Pia Mkurungezi na mwanzilishi wa Team Tezza Kenan Richard aliongeza kuwa vijana wanataka sauti zao zisikilizwe, kwa maana hawataki kuwa kizazi kitakachowasimulia wajukuu zao kuwa hawakufanya jambo lolote juu ya haya na wanaomba vijana wenzetu na viongozi wa dunia kuungana nasi ili kupinga biashara haramu ya ujangili.


















KUHUSU BONGORIDE CHARITY CRUISE;


Bongo Ride Charity Cruise ilianzishwa mwaka 2014 ikiwa na lengo la kuisaidia serikali na jamii kiujumla kutatua baadhi ya matatizo yanayoizunguka jamii ya Kitanzania na Afrika kwaujumla kwa njia ya kupaza sauti kuhusu jambo lolote linaloonekana kuwa tatizo kwa namna tofauti.


Nia yetu ni kuzunguka mikoa yote Tanzania na Afrika kwa kutumia njia ya kusafiri kwa pamoja na magari yetu binafsi na kutoa misaada sehemu mbalimbali katika bara letu la Afrika, Pia kumfanya kijana wa Kitanzania kujifunza tamaduni mbalimbali na kukuza wigo wa marafiki wenye msaada kwake ili kuongeza sababu lukuki za kimaendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla.






KWA MAELEZO ZAIDI; WASILIANA NA 


KRANTZ MWANTEPELE


MENEJA MAWASILIANO BONGORIDE


NAMBA YA SIMU;0712579102






EMAIL;krantzcharles@gmail.com


SSRA yakutana na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kujadili mabadiliko na maendeleo mbalimbali katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii

$
0
0
Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama cha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Carina Wangwe, akizungumza wakati akiufungua mkutano wa mamlaka hiyo na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama wa SSRA, Carina Wangwe, alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi, akimwakilisha Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, Dar es Salaam jana.
Washiriki wa mkutano huo, wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama wa SSRA, Carina Wangwe, alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na wadau wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama wa SSRA, Carina Wangwe, alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, Millenium Tower, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole, akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Kisheria wa usimamizi na udhibiti wa hifadhi ya Jamii Tanzania wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole, alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Kisheria wa usimamizi na udhibiti wa hifadhi ya Jamii Tanzania wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakifuatilia mada kuhusu Mfumo wa Kisheria wa usimamizi na udhibiti wa hifadhi ya Jamii, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole, akiwasilisha mada hiyo wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi, akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Hifadhi ya Jamii Tanzania, Mtazamo wa Waajiri na Mpango wa hifadhi kwa waajiriwa wao, wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi, alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Hifadhi ya Jamii Tanzania, Mtazamo wa Waajiri na Mpango wa hifadhi kwa waajiriwa wao, wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki, wakiteta jambo wakati wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi, alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Hifadhi ya Jamii Tanzania, Mtazamo wa Waajiri na Mpango wa hifadhi kwa waajiriwa wao, wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Tafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi, akiwasilisha mada hiyo wakati wa mkutano huo, Millenium Tower, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama cha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Carina Wangwe (mstari wa mbele katikati), aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kitengo cha Tehama cha Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Carina Wangwe (mstari wa mbele katikati), aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka.

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YATEMBELEA BOHARI YA DAWA (MSD).

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa  Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Ukimwi, Hassna Sudi Katunda Mwilima (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe hao na wageni katika ziara hiyo.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (kulia), akiwatembeza wajumbe hao MSD Keko.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (katikati), akitoa maelekezo kwa wajumbe hao.


WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI na dawa za kulevya wametembelea Makao makuu ya Bohari ya dawa (MSD), Keko jijini Dar es Salaam.  Katika ziara yao kamati imeishauri serikali kutenga bajeti ya dawa na vifaa tiba kulingana na mahitaji. 

Akitoa ufafanuzi kuhusu asilimia 80% ya dawa kuagizwa nje ya nchi, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu amesema bado hakuna viwanda vya ndani vya kutengeneza dawa ,na vichache vilivyopo havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya MSD.

Katika hatua nyingine,wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge ya masuala ya UKIMWI,inayoongozwa na Mhe.Hassna Sudi Katunda Mwilima(Mb.) imeipongeza MSD kwa kuwa na maghala ya kisasa ya kuhifadhia dawa,huku wakihimiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ishughulikie deni la serikali. Aidha, walisema kulipwa kwa deni kutasaidia MSD kununua dawa muhimu kwa wakati.

Kuhusu deni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya alieleza kuwa suala la deni linafanyiwa kazi.

Hata hivyo Naibu Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kuwa tayari serikali imeshaahidi kupunguza deni kwa awamu kuanzia mwaka huu wa fedha.

MKUU WA MKOA WA KIGOMA AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI KUTAJA KIIASI CHA FEDHA KILICHOTUMIKA KUWALIPA WATUMISHI HEWA 169

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa taarifa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya watumishi hewa 169 waliopo katika halmashauri za Mkoa wa Kigoma.


Na Editha Karlo, wa blog ya jamii Kigoma.

MKUU wa Mkoa wa Kigoma  Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. 

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali Emanuel Maganga alisema kuwa kufuatia agizo la Muheshimwa Rais juu ya kufanya uhakiki wa watumishi katika halmashauri zote ili kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa mishahara kinyume na utaratibu za utumishi.

Alisema katika hao watumishi hewa 169 waliowabaini wapo ambao walishafukuzwa kazi, wapo ambao wameshafariki na wengine hawana sifa za kuwa watumishi wa umma.

Maganga alisema kuwa suala la kuwa na wafanyakazi  hewa ni wizi ambao hauwezi kuvumilika na wizi wa kuibia wanyonge  hauwezi kuvumilika.

"Hakuna anayeweza kuvumilia wizi wa waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiowaaminifu, wale wote watakaobainika wajiandae kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Alisema Maganga.

Alisema kuwa fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hao hewa kwaajili ya mishahara zinatakiwa kurudi zote pia wakurugenzi wawafute watumishi hao hewa kwenye orodha ya malipo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa sasa hivi katika serekali hii ya awamu ya tano hakuna kufanya kazi kwa mazowea.

Alizitaja halmashauri zenye watumishi hewa kuwa ni halmashauri ya kasulu watumishi 78,halmashauri ya Kigoma 23,Manispaa ya Kigoma Ujiji 29,halmashauri ya Buhigwe 11,Uvinza 19,kibondo 5,ofisi ya Mkuu wa Mkoa 4 na halmashauri ya Kakonko hakuna mtumishi hewa.

MASANJA KUKANDAMIZA NDANI YA LONDON JUMATATU YA PASAKA

$
0
0
Huyu mtu wa Ze Orijino Komedi atauteka mji wa London kwa kuwavunja mbavu siku ya jumatatu ya Pasaka Tarehe 28/03/2016 kuanzia saa kumi ( 16:00) jioni mpaka saa mbili (20:00) usiku

UKUMBI NI:
St Bartholomew's
292B Barking Road
East Ham
London
E6 3BA

Kiingilio ni £5 (dala) tu...!

Njoo na wanao mcheke kidogo muondoe mastress ya Box na Baridi
Vinywaji  na misosi vitakuwepo
Wasiliana na Flora tel:+447916160641 kwa maelezo zaidi

NB: HAKIKISHA UNAKUNA NA MBAVU ZA AKIBA

WAZIRI MAGHEMBE AMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI MKUU WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA ( TFS), WAKURUGENZI WATATU PAMOJA NA WAKUU WA KANDA NCHI NZIMA

$
0
0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu na Wakurugenzi  watatu wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo .  Kushoto  ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani.

 Baadhi ya Waandishi wa habari Waliohudhuria Mkutano huo wa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.



Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Mghembe amemsimamisha kazi  Mtendaji  Mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini, (TFS)    Bw. Juma Mgoo pamoja na Wakurugenzi wawili  wa wakala  hiyo ili kupisha  uchunguzi kutokana na  ukusanyaji usioridhisha wa mapato yatokanayo na mazao ya misitu.


Prof. Maghembe ametaja  majina ya Wakurugenzi hao aliowasimamisha kazi  kuwa  ni  Mkurugenzi Rasilimali Misitu, Bw.  Zawadi Mbwambo  pamoja   na Kaimu   Mkurugenzi  wa Mipango na Matumizi endelevu  ya Misitu, Bw. Nurdin Chamuya


Wengine  waliosimamishwa  kazi ni wakuu wa Kanda za Wakala wa Huduma za Misitu  nchi nzima   ambao  ni Bw.  Hubert Haule wa Kanda ya Kusini,  Bw.  Bakari Rashidi wa kanda ya Mashariki,                Bw. Shabani Mwinyi Juma wa kanda ya kati ,  Emanuel Minja wa kanda ya Magharibi pamoja na  Bw. Bruno wa nyanda za juu kusini


Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini  Dar es Salaam, Prof. Maghembe amesema hatua hiyo imekuja  baada ya  kubaini shehena kubwa za magogo   aina ya mninga  katika Mkoa wa  Rukwa wilayani Kalambo  yakiwa  yamekatwa na kuwekwa ndani ya makontena kule kule   ndani ya msitu  pamoja na kutengenezewa nyaraka  feki zinazoonesha magogo hayo yanatoka nchini  Zambia    tayari  kwa  kusafirishwa kupelekwa nchini  China lakini hata hivyo  baada ya kubaini wizi huo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania ( TFS).


Amesema kuwa baada ya kubaini hivyo usiku wa jana aliweza kupata taarifa kuwa  shehena ya Magogo hayo yenye  thamani  ya shilingi milioni 500  yaliyotakiwa  kupelekwa Makao makuu ya Wilaya ya Kalambo   yamemwagiwa petrol  na yamechomwa moto


Aliongeza kuwa  kumekuwa na ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri  ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.


Kwa upande mwingine , Prof Maghembe amesema kuwa  pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi  benki kwa wakati na hata zikipelekwa benki  zimekuwa zikipelekwa pungufu na muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.



Wakati huo huo, Waziri Maghembe  amemsimamisha kazi  Mkurugenzi Msaidizi wa  Idara ya Wanyamapori wa Matumizi Endelevu,   Dkt. Charles Mulokozi  kwa kosa la kukaidi agizo la kusaini vibali  vya kusafirisha Wanyamapori nje ya nchi.


Hatua hiyo imekuja  baada  ya jana  nyani 61 kukamatwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na kubaini kuwa Idara ya Wanyamapori  ndio iliyotoa vibali vya kusafirisha nyani hao na vibali hivyo vikiwa vimetiwa saini na Mkurugenzi huyo.

Ameongeza kuwa ndege ya kutoka Ulaya Kusini  iliyotakiwa kusafirisha nyani hao imeshikiliwa pamoja na rubani wake kwa mahojiano zaidi.


Prof ,Maghembe amesema  kutokana taarifa alizozipata kuwa jumla ya  nyani 450 ndio waliokuwa wanawindwa kwa ajili ya  kusafirishwa kupelekwa nje.


RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA AWAMU YA SABA WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR DKT. ALI MOHAMED SHEIN

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mamia ya wananchi wa Zanzibar mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Amaan Kisiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jeneral Devis Mwamunyange wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na Yamoto bendi katika uwanja wa Amaan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakifatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikitolewa na Bendi ya muziki ya Yamoto katika uwanja wa Amaan. 

DKT. SHEIN AAPISHWA KUWA RAIS WA ZANZIBAR WA AWAMU YA SABA

$
0
0
Rais Mteule wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akitia saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu baadanya kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


WAGOMBEA USPIKA BUNGE LAWAWAKILISHI ZANZIBAR WAMKATAA KIFICHO

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

HEKAHEKA zimeanza Visiwani Zanzibar ambapo wagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Wawakilishi wameanza kupigana vikumbo kuwania nafasi hiyo huku sura mpya za vijana wenye damu mbichi zikijitokeza kuchuana na mkongwe aliyechukua tena fomu ya kutetea nafasi yake Mhe Pandu Ameri Kificho.

Kificho ni Spika wa Bunge la Wawakilishi kwa muda wamiaka 25 sasa ambapo wanachama wa CCM Zanzibar tayari wameanza kutilia mashaka uamuazi wa spika huyo aliyechukua fomu za kugombea tena akitaka kuendelea na kuongoza kiti cha uspika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, jambo, inalozua maswali mengi yasiyo na majibu.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar, walitoa maoni yao juu ya sakata hilo na kusema kuwa Kificho hakustaili kuwania nafasi hiyo kwa kipindi kijacho bali alitakiwa kuiga mfano wa baadhi ya viogozi kama Spika Pius Msekwa na wengine walioamua kuachia ngazi kwa kujiuzuru madaraka na kuwaachia vijana wenye hali ya kuongoza ili kupata radha mpya katika Bunge hilo la Wawakilishi.

Naye mgombea, Mahamud Muhamed Mussa, alisema kuwa amejitokeza kuchukua fomu ili kuwania nafasi hiyo kutokana na uwezo alionao na Zaidi akijiandaa kuongoza kisasa Zaidi na kuleta mabadiliko ili Bunge la Wawakilishi liwe lakisasa na kuendana na kaulimbiu ya Mhe Rais wa Jamhuri ya 'Hapa kazi tu', alisemaMussa. 

''Kiukweli Kificho sasa anaelekea kuwaudhi Vijana ambao nao sasa ni muda wao wa kuongoza ili waweze kuchangia mengi waliyonayo ili kuendana na Kasi ya Rais wa awamu ya tano Mhe Dkt. Magufuli, Kificho amekalia kiti cha Spika Bunge la Wawakilishi kwa muda wa miaka 25 sasa ni kwa nini asipumzike na kuwaachia vijana wafanye kazi, sidhani kama bado ana jipya'', alisema Mwanachama mmoja wa CCM aliyejitambulisha kwa jina la Kijeshi.

Aidha Wanachama hao walikwenda mbali Zaidi kwa kukumbushia wakati wa zoezi la Kura ya maoni kuhusu Serikali mbili,ambapo Mhe. Kificho alionekana kwenda kinyume na msimamo wa Chama chake wa Serikali mbili huku yeye akionyesha msimamo wake Zaidi wa kudai Serikali tatu akidai 'eti' ni msimamo wa Baraza la Wawakilishi.

Waliojitokeza kuchukua Fomu za kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa, Zuberi Ali Maulid, Muhamde Ali Amhed, Jajh Janeth, Sadifa Juma, David Mwakanjuki, Perera Silmg na Abdallah Wazisi, ambapo mchuano mkali unaonekana kuwa kwa ni kati ya Spika aliyemaliza muda wake akijaribu kutetea kiti chake, Pandu Ameri Kificho, Mahamud Muhamed Mussa na Jaji Janeth Sekihola.

Wagombea wote walifika kuchukua fomu jana Machi 23,2016  na kurejesha jana hiyo hiyo, zoezi la kupitiamajina na kufanya mchujo na kupata majina matatu lilifanyika jana na kuwapata hao wanaochuana.

WAHOLANZI WAWILI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIA NA TUMBILI 61

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akiwa ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari.

 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .


VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu ,raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini  Armenia.


Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha.


Raia hao wa Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba NWF8CKJR8  na Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.


Meneja usalama uwanja wa ndege KIA,Kisusi Justine aliliambia Tanzania Daima mbali na kukamatwa kwa raia hao wa kigeni pia walifanikiwa kumshikilia Mtanzania ,Idd Misanya anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.


“Wahusika hawa wawili walifika eneo la Cargo ambako walikuwa katika harakati za kusafirisha wanyama hao ndipo tulipowashikilia kwa sababu taratibu za kusafirisha wanyama Hai zilikiukwa”alisema Justine.


Kuhusu mazingira ya kukamtwa kwa watuhumiwa hao ,Justine alisema ndege hiyo inaonekana ilitua katika uwanja huo mahususi kwa ajili ya kubebeba wanyama hao na kwamba ili ruhusiwa kuondoka jioni ile baada ya kukamatwa kwao.


Kamnda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna msaidizi wa Polisi ,Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kukamatwa kwa raia hao na kwamba wamehifadhiwa katika kituo cha Polisi cha KIA huku uchunguzi zaidi ya tukio hilo ukiendelea.


“Mnamo Machi 23 mwaka huu majira ya saa 1:30 jioni huko uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA ) tulifanikiwa kuwakamata raia wawili wa Uholanzi wakiwa wanataka kusafirisha wanyama aina ya tumbili na tayari uchunguzi kwa kushirikiana na Wizara ya maliasili na Utalii unaendelea”alisema Mutafungwa.


Kamanda Mutafungwa alisema taarifa za awali zinasema wanyama hao waalisafirishwa hadi uwanjani hapo wakitokea mpakani mwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kampuni ya uwakala ya Arusha Fright Limited ilipewa kazi hiyo.


Alisema uchunguzi wa awali unaonesha ndege ya mizigo iliyokuwa isafirishe wanyama hao ni ya binafsi huku akikanusha kukamatwa kwa mtu mwingine anyetajwa kuhusika katika kuuza wanyama hao kwa raia hao wa Uholanzi.


“Mpaka sasa tumewakamata hao raia wawili ,lakini kama nilivyosema uchunguzi unaendelea tukishirikiana na wizara ya maliasili na utalii ili tuone kama kuna washiriki wengine wa tukio hilo ,so far tunao hao wawili tu”alisema Mutafungwa.


Alisema mbali na hati za  raia hao wa uholanzi kuonesha kuwa walikuwa wakiishi nchi kihalali bado vyomb vya ulinzi na usalama ikiwemo idara ya Uhamiaji vimeanza kuchunguza pia uhalali wa vibali vya raia hao vya kuishi nchini.

MKUU WA MKOA MPYA WA KAGERA AANZA KAZI RASMI KWA KUTOA MAAGIZO YAKE KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA MKOA HUO

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba
Mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu amekabidhiwa rasmi ofisi na kuanza kutekeleza majukumu yake kama Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Makabidhiano hayo yamefanyika siku ya Jumanne Machi 22, 2016 kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella aliyehamishiwa Mkoani Mwanza. 


Katika hafla fupi ya makabidhiano hayo Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu akiongea na wadau mbalimbali wa Mkoa aliwaomba wananchi wote wa Kagera kuonesha ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake aidha aliongelea mikakati yake katika kutekeleza majukumu yake hapa Mkoani.
Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu aliwakumbusha watumishi wa umma katika Mkoa wa Kagera kuifahamu vizuri dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwa ni kuwajibika kwa kufanya kazi kwa kasi inayotakiwa, kwa nguvu, maarifa, upendo na uadilifu mkubwa bila kusukumwa na mtu yeyote aidha, kila mtumishi afanye kazi kwa uwezo wake wote. 
“Mtumishi wa umma anatakiwa kufahamu wajibu wake hasa kwa kuwatumikia wananchi ili kusukuma maendeleo yao mbele kwa kufanya kazi kwa kujituma bila kubabaisha, pili kufanya kazi kwa kutenda haki bila kudhurumu wananchi haki zao.” Alitoa ilani Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu. 
Maagizo 
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu aligiza kuundwa mara moja mabaraza ya kushughulikia haki za wananchi kama hayapo na kama yapo yaanze kufanya kazi zake mara moja kwa kuwahudumia wananchi ili kupata haki zao. Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wananhimiza wananchi kufanya kazi kila mtu kwa nafasi yake bila kutega. 
Sekta ya Afya, Vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinatakiwa kuwa katika hali ya usafi na kutoa huduma stahiki kwa wananchi. Watoa huduma wanatakiwa kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana muda wote kama ambavyo Serikali imekuwa ikiagiza mara kwa mara. 
Ulinzi na Usalaama wa Mkoa, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu alisema kuwa wale wote ambao wanafanya vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kwa kuteka wananchi na vyombo vya usafiri maporini, atahakikisha anasafisha uchafu huo wote kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalaama ili kukomesha tabia hiyo.
Wahamiaji Haramu, Mkuu wa Mkoa Mpya amewaagiza Wakuu wa Wilaya za mpakani kutoa au kugatua madaraka kwa Wenyeviti wa vijiji na Vitongoji ili waweze kufuatilia mienendo ya wageni wanapoingia nchini ili waweze kuwarudisha mara moja walikotoka. Aidha, aliwaagiza Afisa Uhamiaji Mkoa na Jeshi la Polisi kufanya kazi zao kikamilifu ili kuondoa wahamiaji haramu. 

Chakula, Kwakuwa Mkoa wa Kagera hauna baa la njaa Mkuu wa Mkoa alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhamasishwa kutunza chakula hata kama hakuna baa la njaa ili kujihakikishia akiba ya mbeleni bila kuuza chakula chote cha akiba. 

Ukusanyaji wa Mapato ya serikali, Mkuu wa Mkoa aliziagiza taasisi zote za Serikali kuhakikisha zina kusanya mapato kwa njia ya kielekitroniki ili Serikali ipate mapato ambayo yanarudishwa Mkoani kwetu ili yatekeleze miradi ya maendeleo kwa wananchi. 

Mishahara Hewa, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu aliagiza kwa watendaji wa Serikali kama kuna watumishi hewa waondolewe mara moja kabla ya tarehe 30/03/2016 na baada hapo utafanyika uhakiki kwa kupokea mishahra dirishani kama mwaka 1994 na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria. 

Elimu, viongozi na na watendaji wanatakiwa kutekeleza Sera ya Serikali ya Elimu Bure kwa kukabiliana na changamoto mabalimbali ambazo zimejitokeza mara baada ya kuanzishwa Sera hiyo kama uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa na kufikia Juni 30, 20116 changamoto hizo ziwe zimefanyiwa kazi na kumalizika.
Milioni Hamsini kila Kijiji, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu alimalizia kwa kuwaagiza viongozi na watumishi wa Serikali hasa ngazi za Serikali za Mitaa kuwaandaa wananchi kwa kuwaelimisha juu ya uibuaji wa miradi ya maendeleo ili Milioni Hamsini zilizohaidiwa katika kampeini ambazo zipo karibu kuletwa ziwanufaishe wananchi katika vikundi na siyo kuzigawana tu. 
Kwa upande mwingine aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyehamishiwa Mkoani Mwanza Mhe. John Mongella aliwashukuru wananchi wa wote wa Kagera kwa kipindi alichokuwepo Mkoani kwa ushirikiano wao mkubwa na kuwaomba ushirikiano huo wauendeleze kwa Mkuu wa Mkoa Mpya Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Kijuu.


Historia Fupi 
Mkuu wa Mkoa mpya Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu amehudumu katika Jeshi la Wananchi Tanzania kwa miaka arobaini (40) na alistaafu Jeshini Januari 30, 2016 akiwa Kamanda wa Majeshi ya nchi kavu. Aidha, Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera tarehe 13/03/2016 na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli tarehe 15/03/2016. 

Mkuu wa Mkoa mpya Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa 22 tangu uhuru mwaka 1961 amabpo Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Kagera alikuwa Marehemu Samwel Ntambala Rwangisa. 

MUTFI WA TANZANIA AMUOMBEA DUA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA

$
0
0
 Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kufanyika dua hiyo. Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid.
 Mufti Zubery, akifanya mazungumzo na Makonda.
 Dua ikiendelea nyumbani kwa mufti Mikocheni.
Wapiga picha kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Makonda akiagana na Sheikh Abubakar Khalid na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.

Na Dotto Mwaibale

MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema taifa na kuliletea maendeleo.

Zubery alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam leo asubuhi alipofika nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.

"Tunakuomba mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya yote  Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na viongozi wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery" wakati akiomba dua hiyo.

Makonda akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za kusafirisha abiria.

Makonda alitaja mambo mengine kuwa ni suala nzima la kupambana na uhalifu ambao bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.

Alitaja mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.

Alisema wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini kama alivyofanya Makonda.

Katika hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA IJUMAA KUU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
Msalaba ukipelekwa altereni kuanza ibada ambayo imehudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuubusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akibusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akibusu Msalaba wakati wa Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016
Sehemu ya waumini katika Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na watu wenye ulemavu baada ya Ibada ya Ijumaa kuu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Ijumaa April 25, 2016. Picha na IKULU

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ASHUHUDIA KUORODHESHWA KWA HISA STAHILI ZA MAENDELEO BANK PLC, KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM (DSE)

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji, Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama (kushoto) na Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Mipango wa(CMSA) Nicodemus Mukama wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akipiga kengele kuashiria uorodheshwaji rasmi wa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Maendeleo Benki, Amulike Ngeliama na Mkurugenzi wa Capital Markets na Securities Authoriy (CMSA) Nicodemus Mukama 
Emmanuel Nyalali, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji DSE akizungumza katika hafla hiyo. 
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Ashatu Kijaji akiongea wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa Maendeleo Benki katika soko la hisa DSE 
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki, Ibrahim Mwangalaba akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisah Mwenyekiti wa Benki hiyo kuzungumza na washiriki wa hafla hiyo. 

Bank PLC ni benki iliyoanzishwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani na inamilikiwa na Wananchi mbalimbali kwa njia ya HISA bila kujali, kabila, itikadi, dini wala rangi, kwani benki hii imesajiliwa na soko la hisa la Dar es Salaam (DSE), kupitia dirisha dogo yaani Enterprise Growth Market (EGM) na inaendeshwa kwa kufuata taratibu zote za BOT na Soko la Hisa la Dar es S alaam. Maendeleo Bank ilianza kutoa huduma za kibenki tarehe 9/9/2013 baada ya kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania na tarehe 05/11/2013 ilisajiliwa rasmi katika soko la hisa la Dar es Salaam baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na mamlaka husika. Benki hii ilianza na mtaji wa shilingi bilioni 4.5 kutoka kwa wanahisa zaidi ya 3,000 wa rika na itikadi mbalimbali walionunua wakati wa mauzo ya awali (IPO) yaliyofanyika mwaka 2013.


Tarehe 9/11/2015 benki ilipata kibali cha kuuza hisa stahili ambapo matarajio yake yalikuwa kupata shilingi bilioni 3.06 ambazo zitatumika kuimarisha shughuli za uendeshaji wa benki pamoja na kuongeza matawi. Katika zoezi la uuzaji wa hisa stahili benki imeweza kupata jumla ya shilingi bilioni 2.8 na kufikisha jumla ya mtaji wa benki kuwa shilingi bilioni 7.3.

Kusudi kubwa la kuanzishwa kwa Maendeleo Bank PLC ni kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwani hao ndio walio wengi na upatikanaji wa huduma za kibenki kwao ni changamoto kubwa. Benki hii imepata mafanikio mengi tangia kuanzishwa kwake takribani miaka miwili iliyopita ambapo mpaka tarehe 31/12/2015, benki imefikisha wateja zaidi ya 12,000, amana zaidi ya shilingi bilioni 46.0, mali za benki zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 55, imetoa mikopo zaidi ya shilini bilioni 21.0 na mwaka 2015 imepata faida ya takribani shilingi milioni 200.0 baada ya kodi. 

Benki hii inatoa huduma mbalimbali za ubunifu ambazo zinawalenga wananchi wa kada mbalimbali, zikiwemo: huduma za kibenki kwa njia ya simu, huduma za BIMA, ATM kupitia mtandao wa UMOJA Switch, akaunti mbalimbali zenye gharama rafiki, kutuma na kupokea pesa kutoka nje na ndani ya nchi, na kutoa mikopo ya aina mbalimbali, ikiwemo kwa wajasiliamali wadogo ambayo haina dhamana, yaani mikopo ya vikundi. 

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO, STEPHAN P. MASATU KUENDESHA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA MARADHI YA MOYO MKOANI KIGOMA

$
0
0

DAKTARI bingwa wa magonjwa ya moyo, Dkt. Stephan P. Masatu


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

WATU wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo mkoani Kigoma, watapata faraja kubwa mapema Aprili 4 hadi 9, 2016, kufuatia uwepo wa huduma za uchunguzi wa maradhi hayo utakaofanywa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo, Dkt. Stephan P. Masatu, kutoka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam, Dkt. Masatu alisema, huduma zote za magonjwa ya moyo ikiwa ni pamoja na vipimo vya ECG na ECHO zitatolewa kuanzia asubuhi kwenye hospitali ya kibinafsi ya Upendo iliyo jirani na soko kuu la mkoani Kigoma.

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi na zinakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa kushughulikia magonjwa kama ya Moyo na kutokana na uchache wa wataalamu hao, itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na vitongoji vyake, kujitokeza ili kuhudumiwa ambapo kliniki hiyo itadumu kwa muda wa siku sita mfululizo.




Dkt. Masatu akitumia mashine ya kupima ECHO, mmoja wa wagonjwa wa moyo


MKURUGENZI MKUU MPYA WA NSSF ATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula.
Wataalamu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisalimiana na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.
Barabara za kuingilia darajani upande wa Kurasini.
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akionyesha njia za kuingia na kutoka darajani.
Barabara ya kuingilia darajani upande wa kushoto na barabara ya kutokea mjini upande wa kulia. 
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati wa ziara yake ya kutembelea daraja la Kigamboni. 
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katika) alipotembelea daraja wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, daraja hilo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya kumalizika kwa ujenzi wake.
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo wakati wa ziara ya kutembelea daraja hilo jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja hilo, Mhandisi, Karim Mataka.
Muonekano la daraja la Kigamboni.

Meneja wa Miradi wa NSSF, John Msemo akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara alipotembelea sehemu ya kuingilia magari.
Sehemu ya kukatia tiketi wakati unapoingia na gari katika darala la Kigamboni.
Muonekano wa ofisi pamoja na Kituo cha Polisi ambazo zitatoa huduma katika daraja la Kigamboni. 

Njia za kuingilia darajani.



Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara yake ya kutembelea daraja la Kigamboni. Kulia ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja hilo, Karim Mataka.



Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo wakati wa ziara ya kutembelea daraja hilo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mataka.



Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mataka akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati) alipofanya ziara ya kutembelea daraja hilo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo.



Meneja Miradi wa NSSF, John Msemo akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati) alipotembelea daraja la Kigamboni le. Kulia ni Meneja Mradi wa Daraja hilo, Mhandisi Karim Mataka.



Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto), akizungumza na Meneja wa Miradi wa NSSF Mhandisi John Msemo (kulia) na Meneja Mradi Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Karim Mataka.



Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo, 



Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia) akifafanua jambo wakati alipotembelea daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo, daraja hilo litazinduliwa hivi karibuni. Kushoto ni Ofisa Mkuu Idara ya Masoko na Uhusiano NSSF, Eunice Chiume na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Jacoub Kidula.



Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa Shirika la Tanifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Yacoub Kidula akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati), alipotembelea Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo


.Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara.

DAWASCO YATOA RAI ONGEZEKO LA MAJI JIJINI

$
0
0


Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwako na ongezeko la Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, pamoja na maeneo ya miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini kuanza kufanya majaribio ya uzalishaji wa Maji .

Akiongea na waandishi wa habari kaimu meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na pia kumekuwepo na ongezeko la uvujaji wa Maji katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam, hasa katika maeneo ambayo yalikuwa na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji na baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo mdogo (Low pressure)

“Kufuatia ongezeko hili la Maji watu wengi wameanza kupata huduma ya Majisafi, na uvujaji wa Maji umeongezeka katika maeneo ambayo aidha yalikuwa na miundombinu ya Maji lakini hayakuwa na huduma ya Maji au maeneo ambayo yalikuwa yakipata Maji kwa msukumo mdogo” Alisema Bi. Lyaro

Aidha, ametoa wito kwa wateja na wananchi wote kutoa taarifa za uvujaji huo wa Maji pindi wanapobaini kuwapo na uvujaji wa Maji katika makazi yao na maeneo mbalimbali ya jiji kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 022194800 au 0800110064 (Bure).

“Namba hizi ziko wazi saa 24 kwa siku na mteja hatakatwa gharama yoyote akipiga simu hizi. Hivyo tunaomba wateja wetu waisaidie Dawasco kupunguza upotevu wa maji kwa kutupa taarifa za mivujo na kupasuka kwa mabomba” alisema bi Lyaro.

Kutokana na ongezeko hilo la Maji maeneo yaliyoanza kupata Maji baada ya majaribio ya mtambo huo kuwa ni Tandale,Manzese makunimula,Mwananyamala,Kinondoni mkwajuni, baadhi ya maeneo ya vingunguti,changombe,ubungo-mabibo na city centre.

Pia, DAWASCO imetumia nafasi hiyo kuwakumbusha wateja wote kulipia huduma ya Maji kwa wakati kwani watu wengi kwa sasa wameanza kupata huduma ya Majisafi na salama kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa Maji katika mtambo wa Maji wa Ruvu chini, hivyo hawana budi kuyalipia ili kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma ya Maji.

Kuongezeka kwa huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kumetokana na kukamilika upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini ulioanza mwaka 2011 hivyo kuongezeka kiasi cha uzalishaji wa Maji kutoka wastani wa lita milioni 182 hadi lita 270 kwa sasa.

WANAFUNZI WA FEZA BOYS HIGH SCHOOL WATEMBELEA VIRGINIA INTERNATIONAL UNIVERSITY

$
0
0
Wanafunzi wa Feza Boys High School kutoka jijini Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja walipokua Virginia International University iliyopo jimbo la Virginia siku ya Alhamisi March 24, 2016, wanafunzi hao wapo kwa ziara maalum ya kuangalia uwezekano wa kujiunga na chuo hicho katika masomo ya juu.
 Makamu Rais wa Chuo hicho Dr. Suleyman Bahceci (kulia) akiwaeleza wanafunzi hao taratibu za kufuata kwa ajili ya kujiunga na VIU
Kushoto ni Alex Luketa Mtanzania anayefanyakazi chuoni hapo kwa ajili ya kusajili wanafunzi kutoka Afrika Mashariki akiwa pamoja na wanafunzi wa Feza Boys High School wakimsikiliza Makamu Rais wa chuo (hayupo pichani) alipokua akielezea wanafunzi hao utaratibu wa kujiunga na masomo VIU.
Wanafunzi wa Feza Boys wakipata mulo.
Mazungumuzo yakiendelea.
 Picha ya pamoja

Kumekucha tamasha la dini la Upendo Music Festival Jumapili ya Pasaka.

$
0
0
Ikiwa zimebaki siku mbili yaani Jumapili ya Machi 27.2016 wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake wanatarajia kushuhudia tamasha la dini la Upendo Music Festival ambalo litaambatana na matukio mbalimbali ndani ya viwanja vya Leaders Club.

Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited tayari imeweka wazi baadhi ya vikundi na wasanii washiriki wa tamasha hilo.

Baadhi ya Wasanii hao wenye kalama na upeo mkubwa katika kumuimbia Mungu wanaotamba ndani na nje ya Tanzania ni pamoja na: Angel Bernard, Emanuel Mbasha, Lynga George, Upendo Kihaile, Sarah Shilla, Faraja Ntaboba.Pia wapo: Edson Mwasabwite, Angel Magoti, Abeid Ngosso, Ambwene Mwasongwe na Fridah Felix.

Aidha, washiriki wengine katika orodha hiyo ni pamoja na: Choir ya Kigogo KKKT, Gift and Beauty, Moses Saxer, Mise Ricprdias, The Joshua Generation, Glorious Worship Team, The Voice, Uinjilist Choir Kimara.
Wengine ni Doxers Praise Team, Calvary Band, The Jordan, The Next level, Chang’ombe Vijana Choir, Uinjilist Kijitonyaama, Tumaini Shangilieni Choir na wengine wengi.

Katika tamasha hilo hiyo siku ya Jumapili ya PASAKA, katika viwanja vya LEADERS CLUB, Kinondoni, linatarajia kuanza majira ya asubuhi ya nne ( 4:00) Hadi Saa 10:00 Usiku. Pia litajumuisha na Bonanza la Michezo, Michezo ya Watoto na Uuzaji wa Biashara mbali mbali
Kiingilio kawaida ni Tsh.5,000 na kwa viti maalum ni Tsh.10,000 huku kwa Watoto ni Tsh. 2,000.

“Music 100% Live, Njoo tumuimbie Mungu”.. Ulinzi na Usalama ni wa hali ya juu nyoote munakaribiswa.
abeddy_2
Abeid Ngosso
frida1
Fridah Felix
U36-620x399
Emanuel Mbasha
Sarah Shilla
Sarah Shilla.
nightofhope17
Ambwene Mwasongwe.
Edson Mwasabwite
Edson Mwasabwite.
FB_IMG_1450057063985
Angel Bernard.
The VoiceKundi la The Voice

USIKU WA MCHIRIKU NA TAARABU KUFANYIKA KESHO PASAKA DAR LIVE

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images