Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 805 | 806 | (Page 807) | 808 | 809 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh. Halima Dendegu, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shindano la kumsaka kijana mwenye wazo zuri la kibiashara na hatimae mchanganuo wa biashara (Statoil Heroes Of Tomorrow BusinessCompetition) lililofanyika Mkoani Mtwara jana.
   
  SHINDANO la kumsaka kijana mwenye wazo zuri la kibiashara na hatimae mchanganuo wa biashara (Statoil Heroes Of Tomorrow Business Competition) limefanyika Mkoani Mtwara jana, na kufanikiwa kupata majina 10 ya vijana waliofanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho.

  Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano hilo,Meneja wa shindano hilo, Erick Mchome alisema, Mashujaa wa kesho (
  Heroes of tomorrow) ni shindano linaloendeshwa na kampuni ya Mafuta na gesi kutoka Norway hapa nchini ya Statoil ikiwa na lengo la kuinua uchumi wa nchi ya Tanzania kwa kutafuta vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 25 ambao watakuwa na mawazo mazuri ya biashara na kuwasaidia katika ndoto zao hizo kwa kuzifanya kuwa kweli.

  “Shindono linalenga vijana kutoa mawazo yao ya kibiashara ambayo baadae yatafanywa kuwa biashara” alisema Mchome.

  Shindano hilo limeanza na vijana wa Mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo vijana 400 walijitokeza kushiriki wakilenga maswala ya kilimo, ufugaji, IT, viwanda vidogodogo na maswala mengine yanayohusiana na biashara ambapo baadhi walijikusanya kama kikundi na wengine mmoja mmoja. 40 bora walichaguliwa kushiriki katika mafunzo ya ujasilia mali yaliyo lenga kukuza na kuendeleza biashara ili ziwe na mafanikio, ambapo katika hilo kumi bora walichanguliwa.
  Walio chagulia kumi bora ni Razaki Kaondo, Nyenje Chikambo, Edward Timamu, Saleh Rashid Kisunga, Azizi Doa, Sifael Nkiliye, Said Selemani, Yunus Mtopa, Yahay Omari, Kastus Kambona na Abdalah Selega. Hata hivyo mchakato bado unaendelea kwani kumi hawa watachuana vikali kwa kuleta michanganua yao ya biashara ambayo itafanyiwa tathmini na baraza la Jury ili kuwapata tano bora na hatimae mshindi.

  “Tano bora watatetea michanganuo yao ya biashara mbele ya baraza la Jury” alisema Mchome ikiwa ni sehemu ya kumtafuta mshindi wa shindano hilo.

  Mshindi atapatikana tarehe 15 Aprili jijini Dar es salaam, atazawadiwa dola za kimarekani 5000 wanne walio ingia tano bora kila mmoja wao atajipatia dola 1500 na waliofanikiwa kuingia kumi bora kila mmoja wao atapata dola 1000.

  0 0

  Jana wakimbizi kutoka katika kambi za Nyarugusu na Nduta zilizopo mkoani Kigoma waliungana na watu wengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya maji duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni maji safi kwa maendeleo endelevu.

  Maadhimisho hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano kati ya serikali kupitia idara ya wakimbizi na mashirika mbalimbali yanayotoa misaada katika makambi hayo yakiwemo UNHCR, UNICEF, International Rescue Committee, Oxfam, TWESA, Save the Children, Water Mission, TCRS na mengine mengi. 

  Maadhimisho hayo yalipambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma na maigizo na kisha risala zilizosisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji.

  Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR hadi sasa kuna wakimbizi kutoka mataifa mbalimbali zaidi ya 140,000 wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu huku katika kambi ya Nduta kuna wakimbizi takribani 50,000 kutoka Burundi. 

  Tangu kufunguliwa tena kwa makambi hayo mwaka jana, mashirika mbalimbali yamekuwa yakitoa misaada ya kibinadamu katika makambi likiwemo shirika la Oxfam ambalo linatoa huduma za maji na ujenzi wa vyoo ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wakimbizi namna mbalimbali za kuishi kwa kuzingatia kanuni bora za afya ili kujilinda dhidi ya magonjwa.
  0 0
 • 03/23/16--22:00: THE LEGENDS FAMILY TOUR 2016
 • THE LAST WEEKEND OF THE MONTH PARTY Ndio Hii Hapa, Ijumaa Hii Tunakutana Club Rouge Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel Na Jumamosi Tunakutana Mzalendo Pub Millenium Tower Kijitonyama.

  WATU 50 WA KWANZA KUFIKA WATAKABIDHIWA NON STOP CD MPYA YA MWEZI HUU

  0 0  0 0


  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

  Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

  Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za sherehe na burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu ya Pasaka ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

  Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa ambayo yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

  Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa kumbi kwa msingi huohuo wa kuendekeza faida pasi na kujali maelekezo ya vibali vyao wamekuwa wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na BASATA. 

  BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.

  BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa Pasaka njema na yenye furaha tele. 


  SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI  Godfrey L. Mngereza 

  KATIBU MTENDAJI, BASATA
  0 0

  Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (katikati), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Uwanja huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno.
  Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Abuu Mvano (kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea Idara za Wizara hiyo zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waandishi wa Habari wakati wa ziara yake aliyoifanya kutembelea Idara za Wizara hiyo zilizomo katika Uwanja huo.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akizungumza na waandishi wa habari na kutangaza Majina ya wabunge wa wa viti maalumu katika ukumbi wa tume ya uchaguzi jijini Dar es Salaam, kuhusiana na tume hiyo kukamilisha idadi ya wabunge watatu wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wawili na wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema (Chadema) mmoja. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Givenes Aswile akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
  Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu watatu kuwa ni  Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema). kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kavishe.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  IDADI ya wabunge wa Viti Maalum watatu imekamilika baada ya uchaguzi majimbo yote  kufanyika ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata viti maalum viwili na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mmoja.

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amesema kuwa  uchaguzi umekamilika katika majimbo nane kwa kuwa na majimbo ya Tanzania Bara saba na Zanzibar Moja ambalo ni Jimbo la kijito Upele.

  Viti vya wabunge wa viti maalum wanatokana na kura za jumla za wabunge wote na kuweza kupatikana viti hivyo.

  Waliopatikana katika mchanganuo wa viti maalum ni, Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema).

  Lubuva amesema kuwa kufikia hapo ndipo uchaguzi umekamilika kutokana na viti hiyo kupatikana na kufanya kuwa viti maalumu 113 katika mgawanyo wa viti hivyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM)  Viti  66,  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  viti 35 pamoja na Chama cha Wananchi (CUF)  viti 10.

  Amesema kuwa kutokana na chaguzi zinazoendelea NEC ndiwe iwe sehemu ya usimamizi wa chaguzi zote.

  Idadi kura za wabunge CCM katika uchaguzi ambazo zilibaki kutokana wagombea kufariki na kuarishwa kumeongeza viti maalum viwili.

  0 0  Benki ya Exim Tanzania imeboresha huduma yake ya utumaji na upokeaji wa pesa kimataifa kwa kuharakisha ukamilishaji wa miamala hiyo ambapo kwa sasa wateja wake watatumia saa nne badala ya muda wa  saa 12 uliokuwa ukitumika hapo awali.

  “Exim tumekuwa tukipambana kila siku kuhakikisha tunatoa huduma bora, za haraka na kwa usalama zaidi ili kuwaunganisha wateja wetu na fursa za kimataifa. Kwenye hili  tunatoa hakikisho kwa wateja wetu kwamba iwapo kutatokea ucheleweshaji zaidi ya muda wa masaa manne basi tutalazimika kuwarejeshea gharama zao walizolipa kwa ajili ya  huduma,’’ alisema Bw  Tumaini Mwakafwaga ambaye ni mkuu wa kitengo cha operesheni za Benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.

  Hata hivyo alibainisha kuwa hakikisho hilo la muda wa masaa manne (guarantee) litahusu wateja wenye maombi (miamala) yasiyokuwa na utata, wenye nyaraka onyeshi (supporting documents) pamoja na wale wenye kiasi cha kutosha kwenye akaunti zao.

  “Lakini pia kuna mazingira ambayo yanaweza kufanya tukashindwa kumrejeshea mteja gharama zake (refund) ikiwemo pale ambapo mfumo wetu wa kuendesha miamala utakuwa umekwama kutokana na sababu  zilizo nje ya uwezo wetu yakiwemo majanga ya asili,’’ aliongeza Mwakafwaga.

  Alisema watumiaji wa huduma hiyo watakuwa wakipokea taarifa kuhusu mwenendo mzima wa miamala yao kwa kuwa itakuwa ikifuatiliwa kwa ukaribu kila hatua inayopitia.

  “Kiukweli timu yetu inayohusika na kuchakata (processing) miamala hii inauelewa wa kutosha pamoja na uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yao kwa haraka kuanzia muda ambao mteja anaanza kutumia huduma hii hadi hatua ya mwisho. Mameneja na wasaidizi wao wapo tayari kuhakikisha kila kitu kinaenda kwa wakati na kwa usahihi,’’ alisisitiza.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera
  Na Woinde Shizza,manyara

  Mkoa wa Manyara unatarajia kutumia sh202.1 bilioni kwa ajili ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, ambapo mishahara itakuwa ni sh5.5 bilioni, matumizi ya kawaida sh2.1 bilioni na sh2.7 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

  Katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 mkoa umekadiriwa kukusanya mapato ya ndani ya sh18 bilioni ambapo sh17.9 bilioni ni kwa ajili ya serikali za mitaa na sh192 milioni ni za sekretarieti ya mkoa.

  Akisoma mpango wa bajeti ya mkoa huo juzi, Katibu Tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi alisema kijiografia Manyara yenye kilomita za mraba 50,921 ni kubwa kuliko baadhi ya mikoa, hivyo inahitaji gharama kubwa za uendeshaji.

  Maswi alisema katika mpango huo wa bajeti, Babati mjini wanatarajia kutumia sh25 bilioni, Babati vijijini sh37 bilioni, Hanang’ sh33 bilioni, Kiteto sh30 bilioni, Mbulu vijijini sh38 bilioni, Mbulu mjini sh6 bilioni na Simanjiro sh19 bilioni. “Pia tunakabiliwa na changamoto ya kuchelewa au kutopatikana kwa fedha za ruzuku za matumizi ya kawaida na ruzuku ya miradi ya maendeleo, ufinyu wa bajeti wa kuboresha na kujenga miundombinu ya zahanati na shule,” alisema.

  Alisema umbali kutoka makao makuu ya halmashauri ya wilaya hadi makao makuu ya mkoa ambapo ni lazima upitie wilaya nyingine kama Kondoa, Monduli na Arusha ili ufike mkoani wakati wa kufuata huduma mkoani pia ni kikwazo.

  Hata hivyo, mkuu wa mkoa huo Dk Joel Bendera alizitaka halmashauri zote saba kuhakikisha zinachangia bajeti zao kwa asilimia 60 ya mapato ya vyanzo vya ndani kama serikali kuu ilivyoagiza ili kutekeleza miradi ya maendeleo yao.

  “Nitakuwa mkali katika kuhakikisha hilo linatekelezeka hivyo kila halmashauri ihakikishe inakusanya mapato yao na kufikia asilimia 60 kwani mimi ndiye ninayekwenda kuomba kupitishwa kwa bajeti yetu,” alisema Dk Bendera.

  0 0

  Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kuwasili leo saa 8 usiku katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere kikitokea nchini Chad kilipokuwa na mchezo dhidi ya wenyeji jana jioni.
  Msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina utaondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa N’Djamena saa 8 mchana kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia, kabla ya kuunganisha ndege saa 4 usiku tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania.
  Stars inarejea nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya wenyeji Chad, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta katika mchezo uliochezwa uwanja wa Omnisport Idriss Mahaymat Ouya jijini N’Djamena katika mchezo wa kundi G kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
  Mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Taifa Stars kitaingia moja kwa kwa moja kambini katika hoteli ya Urban Rose iliyopo eneo la Kisutu kujiandaa na mchezo wa marudano utakaochezwa siku ya Jumatatu ya Pasaka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(wapili kushoto)akionesha simu ya kisasa aina ya Galax S7 kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa simu hizo aina ya Galax S7 na S7 Edge ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Samsung Tanzania,Kutoka kushoto Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe,Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles na Meneja masoko wa Samsung,Tulisindo Mwachula.
  Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe(kushoto)akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)jinsi ya unavyoweza kuitumia simu ya aina ya Galax S7 na S7 Edge katika matumizi mengine, wakati wa uzinduzi wa simu hizo ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam,Katikati Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles.
  Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe(kushoto) Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu, Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles, Meneja masoko wa Samsung,Tulisindo Mwachula,wakionesha simu aina ya Galax S7 na S7 Edge kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu hizo ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa bidhaa wa Samsung,Rayton Kwembe(kushoto) na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Charles(kulia)wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu,akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)simu ya kisasa aina ya Galax S7 wakati wa uzinduzi wa simu za aina hiyo na S7 Edge ambazo haziingizi maji ulifanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Samsung Tanzania.

  TUKIWA kampuni inayoongoza kwa mawasiliano hapa nchini leo tunautangazia Umma kwa kuzindua mauzo ya simu za kisasa kabisa ulimwenguni na ambazo haziingizi maji, Galax S7 na S7 Edge kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung.

  Simu hizi mbili ambazo tumezizindua leo na kuanzia sasa zitakuwa zinapatikana katika maduka yote ya Vodacom pamoja na ya Samsung kote nchini.Tukiunga mkono jitihada zinazofanywa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)kwa wananchi kutokuuziwa simu zisizokidhi kiwango cha ubora wa simu yaani(Simu feki)

  “Samsung Galaxy S7 na Galaxy S7 Edge zitakuwa zikitolewa kupitia maduka yetu yote huku zikiambatanishwa na Power-Bank ya BURE; ambapo vilevile, kwa wanunuaji 50 wa kwanza wataweza kujipatia Bluetooth Earphones za Galaxy za bure kabisa,” Alisema Matina Nkurlu, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania.

  Nkurlu alibainisha kwamba,Simu hizi mbili zimekuja zikiwa na maboresho mahsusi yanayolenga kukidhi mahitaji ya vijana wa kisasa hususani katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, ambapo watumiaji wataweza kufurahia na internet ya kasi na haraka zaidi kupitia mtandao wa Vodacom.

  0 0

  Mshauri wa Makosa ya Jinai kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw. Andy Stephens (aliyesimama) akizungumza  katika mkutano aliofanya na Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu namna nchi yake itakavyoshirikiana na Tanzania katika kuboresha utoaji wa haki nchini hasa katika maeneo ya upelelezi, uendeshaji wa mashtaka na utoaji haki katika Mahakama zetu. Mazungumzo hayo yamefanyika leo (24/3/2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyeweka mkono kichwani) akimsikiliza kwa makini Mshauri wa Makosa ya Jinai kutoka Ubalozi wa Uingereza Bw. Andy Stephens (aliyesimama) alipokuwa akizungumza kwenye kikao na Wanasheria wa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu nchi ya Uingereza itakavyoshirikiana na Tanzania katika kuboresha utoaji haki nchini hasa kwenye Mahakama za Tanzania. Kikao hicho kimefanyika leo (24/3/2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 
  Rais Magufuli akizungumza na Waziri Adel Al Jubair (kushoto) 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair. 
  Waziri Mahiga na Waziri Al Jubair wakibadilishana mkataba mara baada ya kusainiwa 
  Mhe. Rais Magufuli akiagana na Waziri Al Jubair 
  Waziri Al Jubair akiagana na Waziri Mahiga mara baada ya kumaliza mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli na zoezi la uwekaji saini kukamilika. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Al Jubair, Waziri Mahiga, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kulia) na ujumbe uliombatana na Waziri Al Jubair. 

  Picha na Reginald Philip.

  0 0


   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa pili kushoto) wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu wa Bunge John Joel.
  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi ya kinyago Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel wakati alipomtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
   Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plot (kushoto) akimwelezea jambo Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah wakati alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.

   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (kushoto) akimweleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plot wakati alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plotwakati alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo naye.
   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
   Mazungumzo katika Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Rone Plot yakiendelea katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi ya trei ya kubebea vinywaji mke wa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Bi. Shosh Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
   Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot wakati wa chakula cha mchana katika hoteli ya Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

  0 0  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi (Mb) akiwa amepokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa bunge la Israel, Bwn. Ronen Plot., alipofika na ujumbe wake ofisini  kwake kuzungumza naye kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Israel. Mhe Lukuvi alikuwa akimwakilisha Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa (Mb).
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelline Mabula (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa bunge la Israel, Bwn. Ronen Plot. Alipofika na ujumbe wake ofisini  kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi (Mb) kuzungumza naye kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Israel. Mhe Lukuvi alikuwa akimwakilisha Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa (Mb).
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi (Mb) akizungumza  ujumbe kutoka Israel, walipofika ofisini  kwake kuzungumza naye kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Israel. Mhe Lukuvi alikuwa akimwakilisha Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa (Mb).

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na wajumbe wa Serikali zote mbili wakishuhudia kubadilishana hati baada ya uwekwaji saini wa mkataba kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Ufundi, Vijana na Michezo. Kwa upande wa Tanzania mkataba ulisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Serikali ya Saudi Arabia iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Adel Al Jubair.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Al Jubair, Waziri Mahiga, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kulia) na ujumbe uliombatana na Waziri Al Jubair. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fissoo akizungumza na wawakilishi wa kamouni ya usambazaji wa filamu Proin promotion(hawapo pichani) kuhusu mkataba kati ya kampuni hiyo na watengenezaji wa filamu Tanzania kushoto ni Rais wa shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba.
  Mwakilishi wa kampuni ya Proin promotion Abraham Kesulie akizungumza wakati wa kikao kati ya kampuni hiyo na Bodi ya Filamu Tanzania kuhus mkataba kati ya watengenezaji wa filamu na kampuni hiyo katikati ni Mumbe wa Bodi ya Filamu Hussein Kim na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Patrick Kipangula.
  Mwakilishi wa kampuni ya Proin promotion Abraham Kesulie(Kushoto), hiyo katikati ni Mumbe wa Bodi ya Filamu Hussein Kim na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Patrick Kipangula wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fissoo9Hayupo Pichani) wakati wa kikao kati ya kampuni hiyo na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu mkataba kati ya watengenezaji wa filamu na kampuni. Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM

  0 0

  Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba Taarifa ya Makabidhiano ya ofisi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana akizungumza jambo wakati wa sherehe za kuwaaga wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) na kumkaribisha mkurugenzi mkuu mpya Dkt.Ayoub Ryoba (wa pili kulia) leo jijini Dar es Salaam.Wengine Pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TBC Balozi Herbert E.Mrango na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Bi.Elimbora Muro (wa kwanza kushoto).
  Wafanyakazi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) wakimskiliza Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba (hayupo Pichani) wakati alipokuwa akiongea nao leo jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk.Ayoub Ryoba akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo(hawapo pichani) wakati wa kumuaga mkurugenzi mstaafu wa shirika hilo Bw.Clement mshana.
  Mkurugenzi mstaafu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kulia) akimkaribisha rasmi katika ofisi za shirika hilo na kumkabidhi rasmi ofisi Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika hilo Dk.Ayoub Ryoba leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Dk.Ayoub Ryoba akitia saini kitabu cha wageni Baada ya kukaribishwa na kukabidhiwa rasmi ofisi za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 03/24/16--11:04: Mfuko wa wazee wanukia
 • Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu akizungumza na viongozi na baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es salaam katikati ni Mwenyekiti wawazee hao Mzee hemed Mkali na kulia ni Katibu wa wazee hao Mzee Mohamed Mtulia.

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
  Dar es Salaam

  Serikali imeazimia kuanzisha Mfuko wa Wazee utakaowasaidia kupambana na changamoto zinazowakabili kwa kuwawezesha kiuchumi.

  Akitoa azimio hilo mbele ya viongozi na baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es Salaam,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema Wizara imeazimia kuanzisha mfuko huo utakaowasaidia wazee nchini ili waweze kujikwamua kiuchumi.

  “Wazee bado wanaweza kuchangia katika maendeleo ya taifa kama watashirikishwa katika kuendesha sekta mbalimbali kwani bado tunahitaji ujuzi na mchango wao katika kusongesha mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu” alisema Mhe. Ummy.

  Waziri Ummy ameongeza kuwa mfuko huo utawasaidia wazee kupata na kuongeza kipato chao kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawasaidia kupata huduma bora za afya.

  “Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasaidia wazee, nimeshapeleka mapendekezo kwa kila halmashauri kuanzisha mfuko wa wazee utakaowasaidia kujikwamua kiuchumi katika maeneo yao” alisema Mhe. Ummy.

  Naye Mwenyekiti wa wazee hao Mzee Hemed Mkali amesema wanahitaji sana mfuko huo ambao utawawezesha kujishughulisha na kupata kipato na pia kuboresha huduma za afya ambazo bado ni changamoto kwa wazee nchini.

  Aidha, Waziri Ummy alisistiza kuwa wanashirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango ili kuandaa mpango wa kuanzisha mfuko huo kwa kushirikisha taasisi za kifedha, makampuni na mashirika mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya mfuko huo kwa maendeleo ya wazee na jamii kwa ujumla.

  Wazee nchini wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo upatikanaji wa huduma za afya na ushirikishwaji wao katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kutoa maamuzi katika jamii zao ambao idadi yao inakadiriwa kuwa ni asilimia 5.6 ya watanzania wote.


older | 1 | .... | 805 | 806 | (Page 807) | 808 | 809 | .... | 1897 | newer