Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Introducing Witnesz ft Ochu shaggy - Sharifa Official Video


RAIS NA AFISA MKUU WA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD AHUTUBIA KONGAMANO LA HUDUMA ZA MIZIGO LILILOFANYIKA ABU DHABI.

$
0
0
RAIS na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad, bwana James Hogan alitoa hotuba ya ufunguzi mbele ya zaidi ya wajumbe 1,200 waliohudhuria kongamano kuu la masuala ya huduma ya mizigo lilofanyika katika kituo cha maoneyesho cha Abu Dhabi kuanzia tarehe 10 hadi 13 Machi.

Bwana Hogan aliongelea kiundani juu ya mabadiliko katika sekta ya mizigo na jinsi gani muungano wa washirika wa shirika la ndege la Etihad umeongeza nguvu katika utendaji kazi wa kitengo hicho cha mizigo. Kwa kuunganisha ndege za mizigo na mitandao yake, kitengo cha mizigo cha Etihad kinatambulika kama kitengo namba tano (5) kwa ukubwa duniani kikishirikiana kwa ukaribu wa dhati na kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Jet, kitengo cha mizigo cha shirirka la ndege la berlin, Serbia, Alitalia, na kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Seychelles.

Kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Etihad hutengeneza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani kama mapato ya mwaka na kukifanya kuwa  moja ya kitengo cha mizigo chenye mafanikio zaidi duniani.  Kilifanikiwa kuhudumia asilimia 88 ya mizigo yote iliyoingia, iliyotoka na iliyosafirishwa  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi mwaka 2015, mwaka ambao kitengo hicho kilibeba tani 529,090 za mizigo na barua, jumla ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 4 ya mwaka 2014.

Kwa sasa kitengo cha mizigo cha Etihad kwa kutumia ndege nne aina ya boeing 777F, tatu aina ya boeing 747s, na nne aina ya airbus A330s. ndege iliyoongezwa aina ya  boeing 777 inatazamiwa kuwasili ndani ya mwezi huu uku nyingine aina ya airbus A330 ikiwa imepangwa kuwasili mwaka 2017.

Bwana Hogan alizungumzia jinsi gani Kanda ya Mashariki inaendelea kufanya vizuri katika viwango vya ukuaji wa kimataifa kwenye sekta ya mizigo na ina jukumu muhimu katika mtiririko wa biashara na bidhaa duniani, pamoja na umuhimu wake wa kijiografia kuimarika kutokana na wadau kuhama masoko ya zamani yaliojazana na kuanzisha masoko mapya katika vituo vya biashara huko Mashariki ya Kati, Asia, Amerika ya Kusini na Afrika.

Alisema: "Kitovu chetu cha Abu Dhabi ni njia panda ya dunia chenye kitengo kikubwa cha kushugulikia mizigo, Shirika la ndege la Etihad  limejiweka nafasi nzuri kunufaika na ongezeko la abiria, ongezeko la mizigo na bidhaa zinazosafirishwa baina ya masoko makubwa na yale mapya”

Etihad Cargo inatoa huduma ya kubeba mizigo kawaida ndani ya ndege pamoja na kwenye buti la ndege huduma hizi zikifikia mtandao wa abiria pamoja na vituo vya mizigo tu.

"Kitengo cha mizigo cha Etihad kimekuwa biashara inayoingiza mapato ya mabilioni na inawakilisha sehemu kubwa ya biashara yetu kwa kujidhatiti kutoa huduma maalumu kwa wateja pamoja na bidhaa zenye ubunifu zenye kutoa ushindani mkubwa na kuvutia wateja wetu. Kwa kufanya kazi na washirika wetu, tutaendelea kuongeza faida ya kila kituo cha mizigo kwa kuchanganya rasilimali, mitandao na uwezo kwa manufaa ya wateja wetu wote "alisema Bw Hogan.

Ushirikiano na watendaji wengine wa mizigo, zikiwemo Atlas Air na Avianca, hutoa msaada mkubwa kwa kituo kikuu, na kitengo kinaendelea fursa za ushirikiano na vitengo vingine vya waendeshaji mizigo. Shirika kwa hivi sasa linafanya kazi katika vituo 14 vinavyojihusisha na mizigo tu ikiwa ni pamoja na Bogotá, Brazzaville, Chittagong, Djibouti, Dubai World Kati, Eldoret, Guangzhou, Hanoi, Houston, Sharjah na Tbilisi.

TAARIFA YA UTEUZI

MAMIA WAUAGA MWILI WA BIBI JOSEPHINE SIMON MSHUBUSI, MWILI WASAFIRISHWA KWENDA BUKOBA KWA MAZISHI

$
0
0
Mkurugenzi wa Mabibo Beer, James Lugemarila, (kulia), akziungumza wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Bibi Josephine Simon Mshumbusi kwenye Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Machi 20, 2016. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa mazishi yatakayofanyika Jumanne Machi 22, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
MWILI wa marehemu bibi Josephine K. Simon Mushumbusi umeagwa leoMachi 20, 2016 kwenye kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Sala na tayari umesafirishwa kwenda kijiji ni kwake, Kashura mkoani Kagera kwa mazishi.

Mrehemu Josephine ambaye alifariki Machi 18, 2016 baada ya kusumbuliwa na malaria kali alizaliwa Mei 2, 1931 kwenye kijiji cha Kashura mkoani Kagera na ameacha watoto kadhaa., .

Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilianza majira ya mchana na mamia ya wakazi wa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake walifika kwenye ibada hiyo, motto mkubwa wa marehemu, ambaye ni Mfanyakazi wa UTT-PID, Euginia Simon, amesema mazishi ya mama yake yatafanyika Jumanne Machi 22, 2016 kijijini alikozaliwa. Bwana alitoa bwana alitwaa na jina lake lihimidiwe.




























































NEWZ ALERT: Watu wanne wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya lori kuyagonga magari matatu ya msafara wa Kamati ya TAMISEMI eneo la Kerege, Bagamoyo.

$
0
0

WATU wanne wanahisia kufariki dunia huku 12 wakiwa wamejeruhiwa vibaya, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani, anaandika Mwandishi Wetu.

Ajari hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge.

Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika msafara wa kamati ya Bunge.

Taarifa zaidi zitawajia hivi punde baada ya kupata taarifa kamili (Taarifa ya awali inaeleza hivyo sijawa na uhakika nayo moja kwa moja)
 Sehemu ya Magari yaliyohusika kwenye ajali hiyo.

 
 Hivi ndivyo ionekanavyo moja ya gari lililohusika kwenye ajali hiyo.

Wizara ya Afya yatoa tahadhari ya homa ya manjano

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - Maelezo

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto imetoa tahadhari juu ya ugonjwa wa homa ya manjano ambao umethibitika kuwepo nchi ya jirani ya Kenya.

Tahadhari hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokua akiongea na waandishi wa habari  kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu nchini ambapo katika wiki ya tarehe 14 Machi hadi 20 Machi mwaka huu takwimu zinaonyesha kuwa kati ya Mikoa 13 yenye wagonjwa  wa kipindupindu , jumla ya wagonjwa 738  na vifo 16 vimeripotiwa  huku Mkoa wa Manyara ukiongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa kipindupindu.

Akielezea kuhusu ugonjwa wa homa ya manjano,Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa ugonjwa huu unasababishwa na virusi ambavyo huenezwa na mbu aina ya Aedes na baadhi ya dalili zake ni homa, kuumwa kichwa,maumivu ya misuli na mgongo,kupoteza hamu ya kula pia kutoka damu sehemu za mwili zilizo wazi.

“Wizara inapenda kutoa tahadhari ya ugonjwa wa homa ya manjano kwa wananchi wote na hasa wanaokaa mipakani mwa nchi ya Kenya kwa kuwa ugonjwa huu hauna tiba kamili ila una chanjo, mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na kupewa dawa za kushusha homa, maumivu, kuongezewa maji mwilini kwa kunywa au kuwekewa dripu”alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote nchini kupambana na magonjwa ya kuambukiza kwa kuimarisha  mfumo wa ufuatiliaji wa wagonjwa na utaratibu wa utoaji taarifa za magonjwa ya kuambukiza, kuhakikisha wasafiri wanaoingia na kutoka nchi zenye hatari ya ugonjwa huo wanapewa chanjo kabla ya kuingia nchi nyingine, kutoa elimu ya afya kwa wananchi, kuandaa timu za wataalam, vifaa tiba na chanjo za kutosha ili kuweza kukabiliana na ugonjwa huo endapo utajitokeza nchini kwa kusimamia na kuhimiza usafi wa mazingira na kuzingatia kanuni za afya.

Pia,amewaonya maofisa wanaotoa chanjo ya homa ya manjano walioko katika vituo vya Afya vya kupokelea wageni wanaoingia na kutoka nchini kuacha mtindo wa kupokea rushwa na kuwapitisha watu bila kupatiwa chanjo.

Mwisho, ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari na kushirikiana kwa karibu na wataalamu wa afya walioko katika maeneo yao  kwa kutoa taarifa haraka kwenye uongozi husika endapo kuna mgonjwa mwenye dalili za kipindupindu au homa ya manjano.

Upendo Peneza:Tamasha la Pasaka litakemea mauaji ya vikongwe, albino

$
0
0
MBUNGE wa Viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),UPENDO PENEZA amesema kuwa ni uamuzi mzuri uliochukuliwa na kampuni hiyo kwani mkoa huo umekithiri kwa mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu hivyo ni ishara kubwa ya kuelekea kukombolewa.

Peneza alisema kuwa anaamini watu wakimpenda Mungu wataacha kufanya mauaji ya vikongwe na albino na watu wa kawaida, kwani mkoa huo unaongoza kwa mauaji ya aina hii.Alisema Tamasha hilo ni msaada mkubwa kwa mkoa huo kwani litahamasisha na kupinga mauaji huku akisisitiza kuwa kampuni ya Msama ambayo inasifika kusaidia jamii anaiomba pia iwafikie hata watoto wa mitaani wa mkoa wa Geita.

“Tunamshukuru Msama na kamati yake kwani Tamasha linaweza kuwa msaada mkubwa kwa mkoa wetu mauaji yamezidi si kwa walemavu wa ngozi na vikongwe hata watu wa kawaida wanauwawa kwa mapanga na vitu vingine” alisema Peneza.Alitolea mfano wa mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Chadema, Alfonce Mawazo aliyeuwawa kwa kukatwakatwa mapanga hivyo kupitia tamasha la pasaka litawaasa waache mauaji.

“Kupitia hili Tamasha naamini wataacha vitendo hivyo kwa sababu Mungu anasema tusiue, mpende mwenzio, kwa hiyo mimi nadhani tamasha hili liwe la kihistoria kwa ajili ya kuwataka na kumrudia mungu,” anasema. Peneza alisema asiwe Msama tu hata asasi, kampuni na wadau mbalimbali wajitokeze kupinga mauaji kwani hilo ni janga la kitaifa.

ICHAWA yazindua mfumo shirikishi kwa bodaboda

$
0
0
Uongozi wa kampuni ya Kikundi cha Waathirika wa Maendeleo (KICHAWA) unaojishughulisha na usafirishaji wa mizigo wamezindua mwongozo wa  mfumo shirikishi wa uratibu wa Bodaboda na Bajaji nchini.

Akizindua mfumo huo leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Mussa Chengulla na kusema kuwa lengo ni kupambana na kupata suluhiso la kudumu katika sekta ya usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji juu ya changamoto za kisheria, kiusalama na kimazingira.

Chengulla amesema kuwa sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa mfumo huo ni matokeo makubwa ya changamoto zilizojitokeza katika jamii juu ya wizi wa pikipiki, wizi wa kutumia pikipiki, uvunjifu wa sheria za usalama barabarani, kanuni za usafirishaji, matumizi ya kujichukulia sheria mkononi, uegeshaji holela wa bodaboda na bajaji na ukamataji usio salama.

 “Uwanzishwaji wa mfumo huu shirikishi ni kukabiliana na changamoto zitokanazo katika sekta ya  usafirishaji na kutatua kero hatarishi zinazoikabili jamii ili kufika malengo ya kuiondoa ajira ya bodaboda na bajaji katika orodha ya ajira hatarishi, kero na janga la Taifa na kuifanya kuwa ajira tegemezi, endelevu na salama kwa usalama wa raia na mali zao” aliongeza Bw. Chengulla.

Mbali na hayo Bw. Chengulla amesema kuwa watakaonufaika na mfumo shirikishi ni TAMISEMI Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya kwa kutambua idadi kamili ya wanaoendelea kujiajiri na kuajiriwa kupitia sekta ya usafirishaji abiria.

Pia wengine watakaonufaika na mfumo huo shirikishi ni SUMATRA, Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Jeshi la Polisi na Usalama ya Raia na kitengo cha usalama barabarani, wamiliki na madereva wa bodaboda na bajaji kulingana na kazi za  sekta husika.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
21/03/2016
Dar es Salaam

MIYEYUSHO NA SUPAR "D" KUPIMA UZITO JUMAMOSI KWA AJILI YAMPAMBANO WA PASAKA.

$
0
0

Na Mwandishi Wetu.

MABONDIA kupima uzito katika viwanja vya Mango Garden jumamosi ya Machhi 26 kwaajili ya kucheza mchezo wao Jumapili ya Machi 27 mwaka huuu ikiwa wanaendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Pasaka ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

akizungumzia mpambano uho mratibu wa pambano hilo Rajabu Mahamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wapo tayali kwa kuwa wapo na afya tele na wanaendelea na mazoezi yao ya mwisho mwisho kila mmoja akijitamba kumsambalatisha mwenzake.

Ambapo mabondia mahasimu Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wanakutana kwa mara nyingine kwa ajili ya mpambano wao mwingine baada ya ue wa vmwanzo Miyeyusho kuibuka Mbabe.

Mpambano mwingine mkali utakuwa ni kati ya bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi ambao wametasfutana kwa mda mrefu na sasa watmaliza ubishi siku ya jumapili hii.

Super D aliongeza kwa kusema mabondia wote wataspima uzito siku ya jumamosi pale katika ukumbi wa Mango Garden na mpambano utafanyika jumapili ya Pasaka Matrch 27 uwanja wa ndani wa Taifa

'Super D' amesema mbali ya mipambano hiyo inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuku kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka mingine bondia.

 Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla.
 
Katika mpambano uho kutakuwa na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKUTANA NA MAWAKALA WA FORODHA NA BANDARI.

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares salaam kuzungumza na wawakilishi wa Mawakala wa Forodha na Bandari leo Machi 21, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipekuwa baadhi ya nyaraka zinazoonyesha jinsi wizi wa fedha za serikali  uliofanywa kwenye  bandari ya Dar es salaam  ukihusisha mabenki wakati akizungumza na  Mawakala wa Forodha na Bandari kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya Mawakala wa Forodha na Bandari wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salam leo Machi 21, 2016.
Kamishna  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Alphayo Kidata akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizozuka katika mkutano na Waziri Mkuu
 (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu).

JESHI LA POLISI LAUA MAJAMBAZI WATATU MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi eneo la masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tatu eneo Masaki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kamishina Sirro amesema kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa wakati wakiwa wanajiandaa kufanya tukio la uhalifu katika moja ya ofisi ya kubadilisha fedha za kigeni iliyopo Masaki.

Amesema kuwa watu hao walikuwa katika gari lenye namba za usajili T 135 AQJ aina ya Rav 4 rangi ya Silver, polisi walilisimamisha gari hilo ndipo majambazi hao wakaanza kurusha risasi na kisha kuzidiwa na kuuawa na polisi waliokuwa katika doria.

Amesema baada ya kuwaua majambazi hao walikwenda kukagua na kukuta bunduki mbili aina ya pisto, Hirizi, Bomu la Kurusha na Mkono pamoja na karatasi ambayo ilikuwa imeandikwa maneno ya kiaraabu. Sirro amesema ametangaza kiama kwa watu wanaotumia nguvu katika utafutaji fedha kuwa hawana nafasi tena katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa mwandishi, Salma Said aliyetekwa Zanzibar hivi karibuni  ni mzima kutokana na kumkuta kuwa hana jeraha lelote katika mwili wake.

Amesema kuwa mwandishi huyo wamechukua malalamiko ambapo wanafanyia upelelezi juu maelezo aliyetoa baada kuonekana katika mazingira hayo.

Aliongeza kuwa  baada ya upelelezi watachukua hatua lakini kwa sasa yuko katika matibabu katika Hospitali ya Regency Jiijini la Dar es Salaam.

MWANAMKE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA MAUAJI YA KIKATILI.

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Zubery Muombeja.

MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Frida Kapinga mkazi wa Mkuzo kata ya Msamala mjini Songea  mkoani Ruvuma anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo kwa kosa  la kufanya mauaji ya kikatili dhidi ya mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

WANAFUNZI WASOMEA CHINI KWENYE UDONGO HUKU WAKIFUNDISHWA NA MWALIMU MMOJA.

$
0
0
Na Woinde Shizza,Simanjiro
MPANGO mkakati wa elimu bure kuanzia darasa la Awali mpaka Sekondari umeonekana kutonufaisha baadhi ya walengwa katika maeneo ya pembezeno hususani jamii ya kifugaji  kutoka katika kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo wananchi wameamua kumkodisha mwalimu na kumlipa kwaajili ya kufundisha watoto wao.


 Wanafunzi wa shule hii ya msingi Kichagare  wamekuwa wakijisomea huku  wamekaa chini, shule hiyo ikiwa imeezekwa  na vipande vya turubai ili kuweza kupata afueni wakati wakujisomea ambapo lengo la wazazi wao kufanya hivyo ni kuwasaidia watoto wao kupambana na adui ujinga ili kuendana na karne hii ya sasa ya teknolojia.


mwandishi wetu amebahatika kufika eneo la tukio na kuzungumza na mwalimu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la  Lilian Nanyaro ambapo amesema kuwa aliamuakujitolea kufundisha katika shule iliyoko kijiji cha Kichangare kitongoji cha Loongung  hii ikiwa ni kwa ajili ya kuweza kuwapatia wanafunzi na watoto wa kijiji hicho elimu .


Amesema kuwa  mazingira ya shule ya msingi Kichangare ni magumu haswa katika swala zima la ufundishaji kwa hamna vitendea kazi ndani ya shule hiyo ukizingatia  kwamba watoto ambao  ni wanafunzi wana nia ya kutaka kusoma.


‘’ndugu mwandishi kama mnavyoona mazingira ya shule hii yaliyomagumu hamna paa, paa lililopo ndo hivi vipande vya turubai na mengine yametuboka  na pia ukiangalia mazingira ya kijiji chetu mvua zinaponyesha pia inakuwa ni tatizo kubwa sana kwani  inafikia mahali  wanafunzi hushindwa kufika shule kabisa nanapenda kutumia nafasi hii kuomba mbalimbali kuweza kutusaidia tatizo hili kwani iwapo watoto hawa watapata sehemu nzuri ya kusomea itawasadia sana hivo  wadau wajitokeze kutusaidia’’alisema Nanyaro.


Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo amejitambulisha kwa jina la Seigulu James  amesema kuwa wao kama wanafunzi wanatamani sana kusoma lakini tatizo kubwa walilonalo katika shule hiyo ni madawati hawana, kwani  kwa sasa iviwamekuwa wakikaa chini wakati wakiwa wanasoma.


Ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuwasaidia kuweza kupata angalau madawati pamoja na kuwajengea majengo ya madarasa pamoja na kuwapatia walimu ambao wataweza kuwafundisha ili waweze kupata elimu kama wanafunzi wengine na  watoto wa shule  zingine.



Honie Kimbeye Mkazi wa kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro amesema kuwa wao kama wanakijiji waliamua kukaa na kutafuta mwalimu mmoja ambaye ndio wanae hapo shule ambapo amesema wao kama wanakijiji wanajichangisha ela na kumlipa mwalimu huyo ili aweze kuwafundisha watoto wao.



“sisi tulijikusanya tuka kaa tukaona ni bora tutafute mwalimu ambaye atatusaidia kufundisha watoto wetu hapa kijijini hivyo tunajichanga tunamlipa kila mwisho wa mwezi na kila mzazi amekuwa akichangia shilingi elfu nne kwa ajili ya kumlipa mwalimu huyo”alisema Kimbeye


Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Loongung Japhet Losijake amesema kuwa mapaka sasa  tayari  vikao vyao vya bajeti halmashauri wameshaomba kijiji hicho kipewe kipaumbele ili kuweza kuondoa tatizo la ukosefu wa darasa hali inayowafanya watoto kusoma wakiwa chini ya vumbi.


Wahenga wanamsemo usemao usipoziba ufa utajenga ukuta,hivyo ni vyema kama serikali kwa kushirikiana na wizara ya elimu kuangalia eneo hilo kwa ukaribu ili kuweza kuwaondolea changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi n ahata mwalimu kufundisha katika mazingira magumu.

MILANGO YA UWEKEZAJI IPO WAZI – MUHONGO.

$
0
0



 Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku,( kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) alipomtembelea ofisini kwake kwa  nia ya kufahamu fusra zaidi ya uwekezaji. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) akiwa na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku( katikati) pamoja na Patiwe Makoena Afisa anayeshughulikia masuala ya siasa katika ubalozi wa Afrika Kusini.( kushoto) wakati wa Kikao na Waziri wa Nishati nishati na madini, pamoja na watendaji wa taasisi zilizochini ya wizara hiyo hawapo pichani.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) akiwa pamoja na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Thami Mseleku( kushoto ) wakijadiliana jambo na wakati wa kikao na watendaji wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati na ujumbe kutoka nchini Afrika Kusini waliotaka kufahamu zaidi fursa za uwekezaji nchini Tanzania.

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa milango ya uwekezaji iko wazi kwa Mataifa yote duniani yenye nia thabiti ya kufanya hivyo nchini Tanzania.


Profesa Muhongo ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini,Thami Mseleku, ambaye alifika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kufahamu zaidi fursa za uwekezaji kwa ajili ya manufaa ya Kampuni za uwekezaji za Afrika Kusini.


Katika kikao hicho, Profesa Muhongo amemweleza Balozi Mseleku kuwa Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji katika masuala ya Nishati na kutaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na makaa ya mawe, Nishati jadidifu,Upepo,mawimbi ya bahari pamoja na umeme wa jua.


Aidha Profesa Muhongo amemweleza Balozi Mseleku kuwa Kampuni za uwekezaji kutoka Afrika Kusini zimekuwa zikifanya vizuri katika Sekta ya Madini hasa katika kulipa mirabaha na tozo mbalimbali za zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini.


Vilevile Waziri wa Nishati na Madini alimsisitiza Balozi huyo wa Afrika  kusini kuwekeza katika sekta ya gesi ambayo tayari inapatikana hapa nchini ili kuzalisha umeme kwa kuwa Tanzania inahitaji umeme mwingi, wa uhakika na wa kutosha.


Profesa Muhongo ameeleza kuwa Tanzania inatarajia kufikia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 utakaotokana na uwepo wa nishati ya umeme ya kutosha nchini, pia tayari imesaini Mpango wa Umoja wa Mataifa unaoelekeza kila mtu kupata huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030 unaofahamika kama " SE4ALL" Nishati Endelevu kwa wote.


Kwa upande wake Balozi Afrika Kusini hapa nchini, Thami Mseleku,amesema kuwa inchi yake ipo tayari kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati ya gesi, mafuta na makaa ya mawe na kwamba nchi hiyo inauzoefu zaidi katika uwekezaji wa nishati ya makaa ya mawe. Balozi huyo wa Afrika Kusini katika Mkutano huo ameambatana na Afisa anayeshughulikia masuala ya siasa, Patiwe Makoena.

Rais Dkt. Magufuli amtumia salamu za Pongezi Rais Mteuli Dkt. Ali Mohamed Shein

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, kufuatia  ushindi alioupata katika marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar, uliofanyika jana tarehe 20 Machi, 2016.


Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema ushindi wa Dkt. Shein umedhihirisha imani na matumaini makubwa waliyonayo wazanzibari kwake na kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani na utulivu, na hatimaye kumpata mshindi wa kiti cha Urais ambaye atawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.


"Naomba nikupongeze kwa dhati Mheshimiwa Rais Mteule Dkt. Ali Mohamed Shein kwa ushindi ulioupata, ushindi ambao umeonesha kuwa wananchi wa Zanzibar bado wanahitaji uwaongoze kwa kipindi kingine cha miaka mitano" Amesema Rais Magufuli.


Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pia ameahidi kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na amewataka Wazanzibari wote kujielekeza katika maendeleo kwa kuwa uchaguzi umekwisha.


"Ndugu zangu wa Zanzibar uchaguzi umekwisha, kilichobaki sasa ni kushirikiana na serikali yenu kuijenga Zanzibar na ninaamini mnao wakati mzuri wa kuijenga Zanzibar yenye maendeleo chini ya uongozi wa Dkt. Ali Mohamed Shein"amesisitiza Dkt. Magufuli


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


21 Machi, 2016 


PROFESA NDALICHAKO ASISITIZA FEDHA ZA ELIMU ZILIZOTOLEWA KWA HALMASHAURI 10 ZITUMIKE VIZURI.

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halmashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa  Joyce Ndalichako amesisitiza fedha za Elimu ambazo zimetolewa na Serikali kama zawadi katika Halmashauri mbalimbali zilizofanya vizuri katika Sekta ya Elimu zitumike vizuri.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati wa kutoa zawadi kwa Halmashauri 10 ambazo zimepokea Shilingi Bilioni 15.5. 

Halmashauri hizo ni Mbinga, Chato, Busega, Lushoto, Niyankasi, Liwale, Sikonge, Mbarali, Mpanda, pamoja naTabora.
Pia, Profesa Ndalichako amezitaja Halmashauri 10 za mwisho kuwa ni Rombo, Kiteto, Meatu, Mafinga, Kasulu, Butihama, Wanging’ombe, Mbozi na Makambako. 

Kwa upande wake, WaziriwaNchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.George Simbachawene amezitaka Halmashauri hizo ambazo zimefanya vizuri na kupata zawadi hiyo ya fedha kuzitumia vizuri fedha hizo na kuhakikisha Elimu Bora inapatikana.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akimkabidhi hundi bilioni 15,532,905.10 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa halmashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Jobu Andindilile Mwalukosya akionesha cheti alichopewa kama halmashauri iliyoshika nafasi ya kwanza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali Bw. Yeremiah Tito Mahinya akipokea cheti pamoja na zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya halmashauri ya wilaya ya Mbarali kufanya vizuri katika suala la elimu. Wa pili kutoka kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Bw, Ahmada .A. Suleman akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya wilaya hiyo kufanya vizuri kielimu, wa pili kutoka kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa, George Simbachawane
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane akizungumza na wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halimashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Jobu Andindilile Mwalukosya akitoa neno la shkukrani kwa niaba ya wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla fupi ya utoaji zawadi kwa halmashauri zilizofanya vizuri.
Baadhi ya wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halimashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar
Picha ya Pamoja.
Kaimu Afisa elimu MsingiMoses Ndanzlama(kushoto), Afisa Elimu Sekondari Bi. Claudia Kita(katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali Bw. Yeremiah Tito Mahinya wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupewa zawadi ya Cheti.

WANAFUNZI WASOMEA CHINI KWENYE UDONGO HUKU WAKIWA WANAFUNDISHWA NA MWALIMU MMOJA

$
0
0

Na Woinde Shizza,Simanjiro

Mpango mkakati wa elimu bure kuanzia darasa la awali mpaka sekondari umeonekana kutonufaisha baadhi ya walengwa katika maeneo ya pembezeno hususani jamii ya kifugaji kutoka katika kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo wananchi wameamua kumkodisha mwalimu na kumlipa kwaajili ya kufundisha watoto wao.

Wanafunzi wa shule hii ya msingi Kichagare wamekuwa wanajisomea wakiwa wamekaa chini huku shule hiyo ikiwa imeezekwa na vipande vya turubai ili kuweza kupata ahueni wakati wakujisomea ambapolengo la wazazi wao kufanya hivyo ni kuwasaidia watoto wao kupambana na adui ujinga ili kuendana na karne hii ya sasa ya teknolojia.

Gazeti hili lilibahatika kufika eneo la tukio na kuzungumza na mwalimu wa shule hiyoaliyejitambulisha kwa jina la Lilian Nanyaro ambapo alisema kuwa aliamuakujitolea kufundisha katika shule iliyoko kijiji cha Kichangare kitongoji cha Loongung hii ikiwa ni kwa ajili ya kuweza kuwapatia wanafunzi na watoto wa kijiji hicho elimu .

Alisema kuwa mazingira ya shule ya msingi Kichangare ni magumu haswa katika swala zima la ufundishaji kwa hamna vitendea kazi ndani ya shule hiyo ukizingatia kwamba watoto ambao ni wanafunzi wana nia ya kutaka kusoma.

‘’ndugu mwandishi kama mnavyoona mazingira ya shule hii yaliyomagumu hamna paa paa lililopo ndo hivi vipande vya turubai na mengine yametuboka na pia ukiangalia mazingira ya kijiji chetu mvua zinaponyesha pia inakuwa ni tatizo kubwa sana kwani inafikia mahali wanafunzi hushindwa kufika shule kabisa nanapenda kutumia nafasi hii kuomba mbalimbali kuweza kutusaidia tatizo hili kwani iwapo watoto hawa watapata sehemu nzuri ya kusomea itawasadia sana hivo wadau wajitokeze kutusaidia’’alisema Nanyaro.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Seigulu James alisema kuwa wao kama wanafunzi wanatamani sana kusoma lakini tatizo kubwa walilonalo katika shule hiyo ni madawati hawana ,kwani kwa sasa iviwamekuwa wakikaa chini wakati wakiwa wanasoma.

Alitumia fursa hiyo kuiomba serekali kuwasaidia kuweza kupata angalau madawati pamoja na kuwajengea majengo ya madarasa pamoja na kuwapatia walimu ambao wataweza kuwafundisha ili waweze kupata elimu kama wanafunzi wengine na watoto wa shule zingine.

Honie Kimbeye Mkazi wa kijiji cha Kichangare wilayani Simanjiro alisema kuwa wao kama wanakijiji waliamua kukaa na kutafuta mwalimu mmoja ambaye ndio wanae hapo shule ambapo alisema wao kama wanakijiji wanajichangisha ela na kumlipa mwalimu huyo ili aweze kuwafundisha watoto wao.

“sisi tulijikusanya tuka kaa tukaona ni bora tutafute mwalimu ambaye atatusaidia kufundisha watoto wetu hapa kijijini hivyo tunajichanga tunamlipa kila mwisho wa mwezi na kila mzazi amekuwa akichangia shilingi elfu nne kwa ajili ya kumlipa mwalimu huyo”alisema Kimbeye

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya Loongung Japhet Losijake alisema kuwa mapaka sasa tayari vikao vyao vya bajeti halmashauri wameshaomba kijiji hicho kipewe kipaumbele ili kuweza kuondoa tatizo la ukosefu wa darasa hali inayowafanya watoto kusoma wakiwa chini ya vumbi.

Wahenga wanamsemo usemao usipoziba ufa utajenga ukuta,hivyo ni vyema kama serikali kwa kushirikiana na wizara ya elimu kuangalia eneo hilo kwa ukaribu ili kuweza kuwaondolea changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi n ahata mwalimu kufundisha katika mazingira magumu.

ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA MAUAJI YA KIKATILI

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa RUVUMA ZUBERY MUOMBEJI. 
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la FRIDA KAPINGA mkazi wa MKUZO kata ya MSAMALA mjini SONGEA mkoani RUVUMA anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa kosa la kufanya mauaji ya kikatili dhidi ya mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO AONGOZA KUAGA MWILI WA MAREHEM MWANJISI

$
0
0
Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(mwenye miwani) akiwa amebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu mkuu wa zamani Wizara ya Habari Marehemu Frank P. Mwanjisi aliyefariki jijini Dar es Salaam.Marehemu amesafirishwa leo kwenda mbeya kwa ajili ya mazishi.
Mchungaji kutoka kanisa la KKKT usharika wa kariakoo akiendesha misa ya kumuombea marehemu Frank Mwanjisi ambaye aliwahi kushika wadhifa wa katibu mkuu katika wizara ya Habari. Picha na Daudi Manongi-WHUSM.
Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akimpa pole Elifasi Mwanjisi ambaye ni mdogo wa marehemu Frank Mwanjisi aliyekuwa katibu mkuu wa zamani Wizara ya Habari leo jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa katibu mkuu wa zamani wa wizara ya Habari Marehemu Frank Mwanjisi aliyefariki jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa marehemu ,Bw Charles Mwanjisi(mwenye t-shirt nyeusi) akizungumza jambo na mkurugenzi msaidizi-MAELEZO Bw.Raphael Hokororo wakati wa misa.

Tanzanian former international model Tausi Likokola is back

$
0
0
Tanzanian former international model Tausi Likokola who just returned from a trip from Europe has been in and out of the country to promote her beauty and lifestyle products launched through her company now based here in Tanzania named Tausi Dreams LTD. 

Tausi is still based in the US but is now back in Tanzania to continue working on a number of projects as well as marketing her latest launched products; perfume named 'Tausi Dreams ' as well as high quality human hair extensions named 'Tausi Beautiful You Hair'. 

Tausi who raised in high fashion world internationally on the 90's worked with fashion houses such as Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hilfger, Escada etc. Tausi also covered numerous fashion magazines and inspired many current Tanzanian models and others around the globe. 

Tausi uses her name to help her own people in Tanzania in education, HIV/AIDS awareness, society areas of need, and positively contributed to Tourism in her country of birth Tanzania as well as business sector and natural resources. Tausi is currently planning to host a few charitable activities through her non for profit organization 'Tausi and Friends For Life.

Tausi will start this coming Saturday March 26th 2016 to film a reality TV series inspired by her book "The African Princess" and the shows will be a model search that will be mentoring inspired models using experiences Tausi gained during her years in the fashion Industry.

Tausi withdrew from working actively in the fashion industry to raise a family of her own. Her life journey has taken her from Africa, Europe, Asia, Australia and current in the USA where she calls home.

 Tausi has published four books and is using her internationally gained experience to work with young girls globally to empower them to full potential. Tausi published books are tittled; 'The Art of Beauty and Health', The African Princess', T'he Touch of an Angel'& 'Beautiful You'. 

Later last year Tausi was a guest of honor at her former school Jangwani form six graduation where they asked her to help with a new printing machine after the school used an old model for over 10 years. Tausi will be re-visiting her school this coming Wednesday 23rd at10am to donate digital printer as well as to speak to the students. Press is invited 10am sharp. 

Tausi is a firm believer in investing in education and young women in the society to bring about a difference. On other like event before her recent travel to Europe Tausi visited Sega girls secondary school in Morogoro where she also mentored young girls.

For further questions and details or if you'll need pictures from Tausi's recent visits to schools, products launch and her upcoming projects please contact;

Beautifulyoupress@gmail.com
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images