Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 800 | 801 | (Page 802) | 803 | 804 | .... | 1897 | newer

  0 0

  IMG_8830Uzembe wa Madereva wawapo bararani umeingiza zaidi ya milion 500 kwa jeshi la polisi kanda maalum kupitia kitengo cha usalama barabarani,Polisi Kanda maalum DSM kupitia kitengo cha Usalama Barabarani kimefanikiwa kukamata magari mbali mbali kwa makosa ya usalama barabarani jumla ya Tshs 577,831,000/= zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo. Aidha madereva wametakiwa kuwa waangalifu pindi wawapo bararani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipatao hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku. Kamanda Siro akitoa taarifa ya makosa ya usalama barabarani

  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba Moshingi, (wapili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), kutoka kushoto, Makamu mwenyekiti,  Deodatus Balile, Mwenyekiti, Theophil Makunga, na mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TEF, baada ya kuwakabidhi tuzo za kutambua mchango wa vyombo vya habari katika kuwaelimisha wananchi juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo kongwe hapa nchini na kwa kuchaguliwa kwao kuwa viongozi wapya wa TEF. Tukio hili lilifanyika wakati wa hafla ya kila mwaka inayoandaliwa na benki hiyo ya kukutana na wahariri kuzungumzia mafanikio na changamoto za benki hiyo  na malengo iliyojiwekea mwaka huu. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
  BENKI ya Posta Tanzania, (TPB), imekutana na wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini, na uongozi mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, TEF, na kuelezea mafanikio ambayo Benki hiyo kongwe hapa nchini imeyapata katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2016.

  Pia Benki hiyo imeeleza mkakati wake mpya wa kuifanya benki hiyo kuwa moja ya mabenki makubwa kabisa sio tu hapa nchini bali nje ya mipaka ya nchi ambapo sasa inatarajia kuwa na jengo lake la kisasa.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Ijumaa usiku Machi 18, 2016, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema, mafanikio ya benki hiyo yanatokana na kuweza kuingiza makundi mengi zaidi kufungua akaunti na kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ambapo kila uchao idadi ya wateja wapya inazidi kuongezeka.

  Ramani ya Tanzania ikionyesha mtandao wa benki ya posta Tanzania, TPB
  Pia alisema, benki hiyo imeziti kutanua mtandao wake kwa kuboresha muonekano wa matawi ya benki hiyo katika mikoa 26 ya bara na visiwani. Alsiema sambamba na matawi hayo huduma za kibenki zinapatikana kote nchini kwenye ofisi za posta.

   Makamu mwenyekiti wa TEF, Deo Balile, (kulia), akipokea tuzo yake
   Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers nchini, TBN, Joachim Mushi, (wakwanza kulia), makamu Mwenyekiti wa TBN, Khadija Kalili, (wanne kushoto), Mmiligi wa K-VIS MEDIA na K-VIS Blog, Khalfan Said, (wakwanza kushoto) na Mhariri Mtendaji wa Business Times/Majira, Bw. Imani (wapili kushoto)
   Moshingi akitoa maelezo ya kina kuhusu huduma za TPB, mafanikio iliyopata na malengo yake ya baadaye.
   Wahariri wakiwa kwenye hafla hiyo
   Moshingi akitoa maelezo ya kina kuhusu huduma za TPB, mafanikio iliyopata na malengo yake ya baadaye
   Deo Balile akizungumza kwenye hafla hiyo
   Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian, Wallace Mauggo, akizungumza kwenye hafla hiyo
   Mhariri wa biashara wa gazeti la Daily News, Henry Lyimo, akizungumza kwenye hafla hiyo
   Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, akizungumza kwenye hafla hiyo
   Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Theophil Makunga akizungumza

   Mhariri Mtendaji wa EFM Radio, Scholastica Mazula, akizungumza. 
  Meneja Mkuu anayeshughulikia masuala ya shirika, na mahusiano ya umma, wa TPB, Noves Moses, akizungumza kwenye hafla hiyo
   Mkurugenzi wa matekelezo na udhibiti majanga, Moses Manyatta(aliyesimama), akizungumza
   Moses Nyenyembe, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani
   Mkurugenzi wa wateja  na biashara, Henry Bwogi
   Mkurugenzi wa Teknolojia na Operesheni wa TPB, Jema Msuya
   Mkurugenzi wa masuala ya sheria na katibu wa bodi ya TPB, Mystica Mapunda Ngongi
   Manyerere Jackton, Mhariri wa gazeti la Jamhuri
   Picha ya pamoja
  Afisa Mtendaji Mkuu, Sabasaba Moshingi, akiteta jambo na Afisa wa mawasiliano wa TPB, Theo Mwakifulefule
  Khalfan Said Chief Photographer/OwnerK-VIS MEDIA P.Box 77807 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033Office; Mivinjeni Opp.Tanesco, Kilwa RD Blog:http//khalfansaid.blogspot.com Dar es Salaam, Tanzania

  0 0

  Mkurugenzi uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Raphael Mwamoto akizungumza kwenye uhamasishaji wa wananchi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kaya ya watu sita kuchangia shilingi 10,000 na kupata matibabu kwa mwaka mmoja.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Hashim Kambona akizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Mirerani, juu ya kujiunga kwa wingi na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kila kaya kulipa shilingi 10,000.
  Baadhi ya wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakijiung ana mfuko wa afya ya Jamii (CHF) ambapo kaya yenye watu sita yaani baba, mama na watoto wane wanajiunga kwa shilingi 10,000 na kupata matibabu kwa mwaka mmoja.


  MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Hashim Kambona amewataka wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili wapate matibabu pindi wakiugua .

  Akizungumza kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga na CHF uliofanyika mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema kaya nyingi zinatakiwa kujiunga na mfuko huo kwani unalipa sh10,000 na kutibiwa kwa mwaka mmoja. 

  Alisema wilaya ya Simanjiro ina utajiri wa kutosha ikiwemo madini, mifugo na ardhi nzuri yenye rutuba inayofaa kwa kilimo na kupitia rasilimali hizo jamii hiyo inapaswa kujiunga na mfuko huo ambao utawasaidia kujitibu pindi wakiugua.

  “Pamoja na hayo japokuwa wilaya yetu ni tajiri kuliko wilaya nyingine kwa hapa nchini, lakini wananchi wetu maisha yao wanayoishi ni ya hali ya chini,hivyo msaada pekee wa matibabu ni kujiunga kwa wingi na CHF,” alisema Kambona.

  Alisema kaya nyingi zikijiunga na mpango huo zitasababisha hata dawa kupatikana kwa wingi kwenye vituo vya afya na zahanati zilizopo maeneo mbalimbali kutoka bohari kuu ya dawa (MSD) hivyo wajiunge kwa wingi.

  Mkurugenzi wa uendeshaji wa (NHIF) Raphael Mwamoto alisema CHF ni utaratibu unaoilenga jamii kwenye maeneo ya halmashauri na wanachotakiwa ni kuchangia kati ya sh5,000 au sh10,000 au sh15,000 kiwango kinachopangwa na wilaya husika.

  “Mfano hapa Simanjiro kaya huchangia sh10,00 na baada ya  kutoa fedha hizo, serikali nayo inaongeza malipo yanayoitwa tele kwa tele kwa kiasi hicho cha sh10,00 kwa kila kaya, kwa ajili ya kupata tiba,” alisema Mwamoto.

  Alisema kinachotakiwa hivi sasa ni halmashauri husika kuweka miundombinu vizuri na kuboresha huduma za afya ikiwemo dawa na vifaa tiba, ili jamii ihamasike kuchangia mfuko huo kwa kuona inanufaika na mfuko huo.

  0 0


  Na Clarence Nanyaro - NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele utafanyika kesho kama ulivyopangwa,licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kujitoa katika uchaguzi huo.

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva,amesema licha ya CUF kuandika barua ya kujitoa katika uchaguzi huo,bado kuna taratibu nyingine kadhaa hazikufuatili wa ikiwa ni pamoja na kula kiapo kwa Mwanasheria cha kutoshiriki katika uchaguzi huo.

  Hali kadhalika Jaji Lubuva amesema kuwa,Wananchi watawapigia kura Wagombea wa Chama hicho na baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika,kura zitahesabiwa na matokea kutangazwa kwa wananchi.

  Jaji Mstaafu Lubuva ametoa rai kwa Wananchi wote waliojiandikisha,kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika vituo vya kupigia kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuwachagua viongozi wanaowapenda kwa ajili ya kushirikiana nao katika kujiletea maendeleo.

  Aidha,Jaji Luvuba amebainisha kuwa Daftari la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele ni lile liliotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na taratibu nyingine zote zinazosimamia upigaji kura zitatumika pia. 

  Naye Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Kailima Ramadhani amesema kuwa vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili asubuhi na kufungwa saa kumi kamili jioni ba baada ya hapo hakuna mtu atayeruhusiwa kupiga kura.

  Vilevile,ameongeza kuwa,kila Mpiga kura lazima abebe kadi yake ya kupigia kura, hakuna atayeruhusiwa kama jina lake halipo katika orodha ya Wapiga kura ambao majina yao yamebandikwa vituoni.

  Bwana Kailima amesisitiza kuwa,Wazee,akina mama wajawazito,Wenye ulemavu wa ina mbalimbali watapewa kipaumbele katika vituo vya kupigia kura kwa kupewa nafasi ya kupiga kura mapema.

  Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele unafanyika hapo kesho kufuatia wa ule Oktoba 25,2015 kuahirishwa kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura.  0 0

   
   Dkt. Ayoub Rioba ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

  Prof. Godius Kahyarara ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe akiongea  na maafisa habari na mawasiliano wa Serikali  wakati akifunga kikao kazi cha 11 cha maafisa hao kilichofanyika mkoani Morogoro.
   Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akiongea na maafisa Habari na mawasiliano wa Serikali na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe(wa tatu kutoka kulia) kufunga kikao cha 11 cha maafisa hao kilichofanyika Mkoani Morogoro.Wengine pichani  ni Mwenyekiti  mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw.Assah Mwambene(wa kwanza kulia),Kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ikulu Bw.Gerson Msigwa(wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa chama cha maafisa Habari na mawasiliano wa Serikali(TAGCO) Bw.Innocent Mungi.(wa pili kulia).

   Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe wakati alipokuwa akifunga kikao cha 11 cha maafisa hao mkoani Morogoro.
  Maafisa Habari na Mawasiliano wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw,Kebwe Steven Kebwe(wane kutoka kushoto waliokaa) mara baada ya kumaliza kikao kazi mkoani Morogoro.

  0 0


  Mwenyekiti wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Dkt. Nelson Boniface akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam.
  Katibu Msaidizi na Msemaji wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Bibi. Elizabeth Bisendo akifafanua jambo wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam.
  Mwanasheria na Mratibu wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba akielezea namna alivyoshughulikia suala la usajili wa Umoja huo wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) wakiwa katika mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo tokea kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2011.
  Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) wakiwa katika mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo tokea kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2011.
  Mwanasheria na Mratibu wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba akikabidhi Cheti cha usajili kwa Mwenyekiti wa Umoja huo Dkt. Nelson Boniface wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Katibu Msaidizi Bibi. Elizabeth Bisendo na Katibu Mkuu Godwin Ndaki.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Dkt. Nelson Boniface akionyesha Cheti cha Usajili wa Umoja wao mara baada ya kukabidhiwa na Mwanasheria na Mratibu wa Umoja huo Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa UWKS Janti Benjamini, Katibu Mkuu Dkt. Godwin Ndeki na Kati Msaidizi Bibi. Elizabeth Bisendo.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Dkt. Nelson Boniface akipitia Katiba iliyosajiliwa ya Umoja wao mara baada ya kukabidhiwa na Mwanasheria na Mratibu wa Umoja huo

  UWKS 1991-94 yazinduliwa

  Na: Mwandioshi Wetu.

  Umoja wa waliosoma shule ya sekondari Kigoma mwaka 1991-1994 umezinduliwa leo rasmi baada ya mwanasheria wao Wakili Marko Anthony Nsimba kukabidhi cheti cha kusajiliwa na katiba ya umoja huo kwa wanaumoja huo hii leo.

  Akizungumza baada ya kupokea cheti hicho, Mwenyekiti wa Umoja huo kwa niaba ya wanachama Dk Nelson Boniface amesema, lengo kuu la UWKS kuwakutanisha pamoja wanafunzi waliosoma Shule hiyo kuanzia 1991-94. Boniface ameongeza kuwa pamoja na kukutana, lakini pia nikusaidiana katika shida na raha kushiriki katika mambo mbalimbali ya maendeleo katika taifa letu sambamba na kutoa ushauri, michango ya misaada ya hali na mali kwa jamii yenye uhitaji.

  Aidha umoja utashirikiana na taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali katika maendeleo ya jamii ya watanzania. Wakati huohuo amezitaja baadhi ya changamoto ambazo umoja huo umekutana nazo ikiwa ni pamoja na baadhi wahitimu wenzao kutoamini kuwa wanaweza kuwa na umoja na wengine wakithubutu kusema ni kupoteza muda.

  “pamoja na kupotezana kwa Zaidi ya miaka 20 iliyopita, lakini sasa tumeweza kukutana tena ingawaje siyo wote laakini kwa kuwa lengo letu ni moja tuna amini na wengine watakuja taratibu” amesema . Mmoja wa wajumbe wa UWKS Mbunge wa Kigoma Mjini Zito Kabwe(ATC) amesema tuliopo ni wajumbe 18, imefanyika kazi kubwa kutafutana lakini naamini kila mmoja wetu atabeba jukumu la kuwavuta wengine hadi darasa litatimia.

  Kabwe ambaye ni ameweka wazi kuwa Umoja huo utapeleka msaada katika shule hiyo kwa kuwa imechakaa na kurekebisha baadhi ya miundombinu iliyochakaa kwa kuwa wakati wao wakisoma walikuta maabara zikifanya kazi lakini kwa sasa zimechakaa, hiyo ni kama kurudisha shukrani kwa jamii.

  Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma kuanzia 1991 -1994 (UWKS) umetokana na kikao cha wanajumuiya cha tarehe 06 Machi 2011ambapo ndipo lilipopatikana wazo la kuwa na Umoja huu ndipo wajumbe walipo azmia kuanza mchakato wa kusajili Umoja huo ambao leo umezinduliwa rasmi. Wajumbe waliojiorodhesha idadi yao inafikia 40 mapaka sasa.

  0 0


  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefafanua kwamba uchunguzi wao umeonyesha kwamba Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli hana akaunti ya Facebook na tovuti inayohamasisha watu kuomba mikopo ya vikundi vya Vicoba.

  Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dr Ally Simba amesema Dar Es Salaam Jumamosi Machi 19 kwamba akaunti ya face book ambayo iliyodaiwa kuwa ni ya Mama Janet ilianzishwa na matapeli wa mtandao.

  Dr. Simba alisema TCRA imeshafungia akaunti hiyo ya Facebook na tovuti ya www.focusvikoba.wapka.mobi ambayo ilikuwa ina tarifa za kutaka wananchi kutuma pesa za kiingilio kwa Vicoba ili wapate mikopo.

  Dr. Simba alisema ingawaje kumekuwepo na maendeleo na mabadiliko makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma za mawasiliano, idadi ya watumiaji na aina ya huduma zinazotolewa kuna watumiaji wachache wanaotumia huduma hivyo kutenda uhalifu kupitia simu za mkononi na kwenye intaneti kwa kuanzisha tovuti za kihalifu na kupitia mitandao ya kijamii kama vile face book.

  Alisema hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wahalifu hawa wa mtandao kuanzisha tovuti na blogu na pia kurasa za facebook kwa kutumia majina ya viongozi wakuu wa nchi, wabunge na watu wengine maarufu.

  Wahalifu hawa wanawadanganya wananchi kwamba kuna fursa za kupata mikopo au misaada kupitia vikundi vya kusaidiana, maarufu kama VICCOBA na kuwataka wananchi watume fedha za kujiunga na huduma hizo kwa njia za simu za mkononi.

  Alisema pamoja na kuzifungia akaunti hizo za facebook na tovuti, Mamlaka inashirikiana na Polisi kuchunguza matukio hayo na tayari hatua kubwa imefikiwa katika kuwakamata na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria. Mkurugenzi Mkuu alisema kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015, mtu yeyote haruhusiwi, kwa kutumia kompyuta, kujifanya yeye ni mtu mwingine15. 

  Adhabu kwa kutenda kosa hili imeainishwa kwenye kifungu cha 15 (2) ambacho kinasema mtu akipatikana na hatia anaweza kutozwa faini ya isiyopungua shilingi milioni TANO au mara tatu ya thamani ya kile ambacho amekipata kupitia ulaghai huo, au kiasi ambacho ni kikubwa kati ya faini na mara tatu ya alichokipata. Vilevile anaweza kufungwa kifungo kisichopungua miaka SABA au vyote.

  Uchapishaji wa taarifa za uwongo ni kosa chini ya Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu yeyote ambaye anachapisha taarifa kwa kutumia mfumo wa kompyuta akijua kwamba taarifa alizochapisha sio za kweli, ni za udanganyifu na sio sahihi na kwa lengo ka kukashifu, kutishia, kutukana,kudanganya na kuptosha umma anatenda kosa ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni TANO au kifungo miaka mitatu au vyote.

  Dr. Simba aliwaomba wananchi kwa ujumla na hasa watumiaji wa huduma za mawasiliano kuzingatia sheria wanapotumia huduma za mawasiliano. 
  Aidha aliwataka Watanzania kuwa macho dhidi ya utapeli kupitia mitandao ya kijamii, tovuti na blogu ambazo zinawataka kutuma fedha au kuchangia kitu chochote ili wapewe mikopo au misaada. Wananchi wakiona matangazo ambayo wanayatia shaka, wawasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano kwa taarifa zaidi.

  Kuhusu maendeleo ya sekta, alisema hadi Desemba 2015, idadi ya laini za simu za mkononi ilikuwa 39,808,419 ukilinganisha na 2,963,737 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti walifikia 17,263,523 Desemba 2015 ukilinganisha na 1,013,104 mwaka 2005.

  0 0

   Mgeni Rasmi katika maadhimisho Mkuu wa mkoa wa dar-es-salaam Mhe. Paul makonda akihutubia waumini waliojitokeza changia damu
   Wageni waalikwa katika maadhimisho hayo kutoka kushoto Meneja damu salama kanda ya Mashariki Dr Aveline Mgasa,  Mganga mkuu mkoa wa Dar , Dr Grace magembe, Mhe. Paul Makonda, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr Mpoki Ulisubya.
  Baadhi ya waumini wakichangia damu kwa hiari

  Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kushirikiana na waumini wa dhehebu la sabato wameendesha zoezi la kuchangia damu katika mikoa mbalimbali hapa nchini, mikoa hiyo ni Mara, Kigoma, Dar-es-salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro,Tabora, Morogoro, Mbeya na Iringa.

  Siku ya matendo ya huruma hufanyika jumamosi ya tatu ya mwezi wa tatu kila mwaka, ambapo waumini hushiriki katika huduma mbalimbali za jamii. Lengo ni kukusanya chupa za damu 3000 kutoka katika mikoa hiyo ambazo zitasambazwa Hospitali mbali mbali kuokoa maisha ya wahitaji

  0 0  0 0

  Padri Honest Munishi akiongoza misa ya kumbukumbu ya marehemu James Luhanga Jr iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Marehemu James Luhanga Jr alifariki Februari 3, 2016 mkoani Iringa. Picha na Vijimambo Blog/ kwanza Production.
  Ndugu wa marehemu wakipeleka matoleo ya sadaka ya misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao James Luhanga Jr.
  Wanafamilia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao marehemu James Luhanga Jr. iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
  Wanafamilia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao marehemu James Luhanga Jr. iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
   
  Pamela (kushoto) na Eliza Madada wa marehemu James Luhanga Jr. wakiwa katika picha ya pamoja kama kumbukumbu ya misa ya kumkumbuka mdogo wao aliyefariki Februari 3, 2016 mkoni Iringa. 
  Wakati wa kupata chakula.
  Katika picha toka kushoto ni Pamela Luhanga, James Luhanga Sr na Eliza Luhanga.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad

  Siku ya Figo duniani, ni tukio la kimaarifa na la kuleta mwangaza duniani linaloadhimishwa mwezi Machi. Kila mwaka, kumekuwepo na shughuli mbalimbali kitaifa na kimataifa zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya Figo, mahospitali, wataalamu wa afya na watu binafsi wanaotaka kuleta mabadiliko duniani dhidi ya ugonjwa wa figo. 

  Ni muhimu kuhimiza elimu, vipimo vya awali, na mtindo mzuri wa maisha ili kuruhusu Jamii itambue magonjwa ya Figo yanayoathiri watu milioni duniani ikiwemo watoto ambao wapo katika hatari ya kuugua katika umri mdogo. Kampeni ya mwaka 2016 ina lengo mahususi kwa magonjwa ya Figo na watoto.

  Matatizo ya figo kwa watoto yajulikanayo kitaalamu kama (Paediatric Nephology aliments) yanahusiana na magonjwa ya Figo kwa watoto wachanga na watoto wadogo mpaka miaka kumi na nane. Kwa mujibu wa Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad Magonjwa ya Figo kwa watoto yanaweza tokea Sababu ya mapungufu katika ukuaji au maumbile (yanayotokea wakati wa kujifungua), kurithi (katika familia) au mabadiliko katika mazingira/ kinga mwilini au madawa. Matatizo Kama hayo yakitambulika mapema huweza zuia uharibifu wa Figo.

  Dk. Shah anawahimiza watanzania kufwata mbinu za kuzuia matatizo ya Figo kwa watoto ambazo zitasaidia kujenga Tanzania isio na magonjwa ya Figo. Mbinu izi ni kama Kupima mkojo kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka miwili wenye homa kali, kuhimiza watoto wasiozidi miaka mitatu kukojo kwa wakati (wasibane mkojo), ulaji wa matunda na mbogamboga, chumvi ya kiasi na nyama katika milo ya familia.

  Kupunguza muda unaotumika na watoto katika televesheni na kompyuta na kuongeza shughuli nyingi Zaidi zenye kupunguza ongezeko la uzito, kuepuka dawa za kupunguza maumivu kama Nimesulide, Ibuprofen n.k. pamoja na madawa ya Ayurvedic/Unani, matumizi ya Crocin/ Calpol/ Paracetamol, kupima presha angalau mara moja kwa mwaka kwa watoto wenye Zaidi ya miaka mitatu, kufanya uchunguzi wa  ugonjwa wa Figo kwa mtoto mwenye matatizo katika ukuaji, anemia, shinikizo la damu, damu katika mkojo, kuvimba kwa mwili au maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara. Mbinu hizi pia zimetajwa na Dk. Shah kama njia za kuepuka magonjwa ya Figo kwa Watoto.

  Matatizo ya Figo yanaweza tokea kwa watoto kutokana na matatizo katika maumbile au yanayotokea baada ya kuzaliwa. Wataalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka  Hospitali za Apollo wanahimiza upimaji wa mara kwa mara ili kufahamu kama mtoto wako ana matatizo ya figo.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio  kituo namba 1cha kupiga kura namba 1 Skuli ya   msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo,Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro zilizojitokeza.
   Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akiwa katika maandalizi ya kupiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B , Mkoa wa Kaskazini. 
    Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akipiga kura katika uchaguzi wa marudio katika kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B , Mkoa wa Kaskazini. 
    Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa marudio kwenye kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B , Mkoa wa Kaskazini. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.January Makamba akizungumza na Waandishi wa habari akielezea hali halisi ya mwenendo wa upigaji kura katika uchaguzi wa marudio  kituo namba 1cha kupiga kura namba 1 Skuli ya   msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo.
   Mkazi wa chake chake akizungumza.na  wanahabari ( hawapo pichani) mara baada ya kutoka kupiga kura
  Baadhi ya Wakazi wa Madungu wakiangalia majina yao kwenye kituo cha kupigia kura

  kituo cha kupigia kura cha skuli ya Madungu chake chake Pemba.
  Baadhi ya wananchi wakihakiki majina yao kabla ya kuingia kupiga kura katika kituo cha skuli ya Raha Leo.

  0 0

  Chama cha Mapinduzi CCM leo kimemtangaza Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji  wa CCM kuanzia leo.Sendeka ametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar.Akimtangaza leo,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana amesema kuwa Sendeka atafanya kazi zake chini ya Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnaye,amesema ,CCM imefanya uamuzi huo ili kumuwezesha Nape kutekeleza majuku yake vizuri ya Uwaziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo.  Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnaye

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
  Ole Sendeka akizungumza baada ya kuteuliwa. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Picha: Bashir Nkoromo)  TAARIFA ILIYOSOMWA NA OLE SENDEKA BAADA YA KUTAMBULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO.

  Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

  Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

  CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

  CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.
    

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth Ruzangi (kulia) akikabidhi vitanda 20, magorodo 20 na mashuka 100, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13 kwa hospitali ya Wilaya ya Kisarawe mwishoni mwa wiki. Anayekabidhiwa vifaa hivyo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Bwana Hamis Likupotile (kushoto) na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt Elizabeth Oming'o. Makabidhiano hayo yaliyafanyika hospitali hapo.
  Meneja Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth Ruzangi (kulia) akikabidhi vitanda 20, magorodo 20 na mashuka 100, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13 kwa hospitali ya Wilaya ya Kisarawe mwishoni mwa wiki. Anayekabidhiwa vifaa hivyo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Bwana Hamis Likupotile (kushoto) na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt Elizabeth Oming'o. Makabidhiano hayo yaliyafanyika hospitali hapo.

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa Vitanda 20, Magodoro 20 na Shuka 100 kwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

  Vitanda hivyo vya kisasa aina ya ‘Cardiac’, mashuka pamoja na magodoro yake vilivyokabidhiwa katika hospitali hiyo ya wilaya vina thamani ya shilingi za kitanzania milioni 13.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Mawasiliano wa TPA, Bibi Janeth Ruzangi alisema msaada huo ni sehemu ya wajibu wa Mamlaka kuisaidia jamii ya Watanzania.


  0 0

  Mkulima wa vitalu vya karafuu wa Kitope Mzee Sheha Khamis akimuelezea Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ZSTC changamoto anazokabiliana nazo katika kutekeleza kazi hiyo wakati Mkurugenzi huyo alipofanya ziara katika Mkoa Kaskazini Unguja na Wilaya Kati.
  Mfanyakazi wa kitalu cha Mikarafuu cha Donge Bi Fatma akitayarisha udongo kwa ajili ya kuatika miche katika shamba hilo linalomilikiwa na Wizara ya Kilimo na Mali Asili.

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar

  Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Mali Asili linakusudia kuongeza mashirikiano na kuwasaidia wananchi wanaoanzisha vitalu vya mikarafuu Unguja na Pemba.

  Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC Bibi Mwanahija Almasi ametoa ahadi hiyo baada ya ziara yake ya siku mbili kutembelea vitalu vya mikarafuu vya Serikali na vya watu binafsi katika vijiji vya Kitope, Kidimni, Machui Selem na Donge kuona matatizo yanayowakabili katika kutekeleza kazi zao.

  Amesema vitalu vya watu binafsi vinamchango mkubwa katika kuimarisha zao la karafu Zanzibar kwa kuziba pengo linalojitokeza wakati wa ugawaji wa miche ya mikarafuu kwa wakulima kutoka vitalu vya Serikali

  Amesisitiza kuwa kutoakana umuhimu huo na kazi kubwa wanayochukua wakulima hao huku wakikabiliwa na upungufu wa nyenzo muhimu, Shirika litatoa pembejeo zitakazosaidia kufanikisha kazi zao kwa ufanisi.

  Wakati wa ziara hiyo wakulima wanaomiliki vitalu vya mikarafuu walimueleza Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC kwamba wanakabiliwa na tatizo la vifuko vya kuatikia miche (policing), mabero, pauro na maji hasa wakati wa kiangazi.

  Mkurugenzi Mwendeshaji amewataka wakulima hao kutovunjika moyo na changamoto wanazokabiliana nazo na waendelee kushirikiana na maafisa wa Kilimo wakati Shirika linafanya juhudi za kupunguza changamoto zao.

  Hata hivyo Bi Mwanahija amewashauri wenye vitalu vya mikarafuu baada ya kupata msaada kutoka ZSTC kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya kuuzia miche ya mikarafuu kwa wakulima ambapo hivi sasa wanauza shilingi 1000 kwa mche mmoja.

  Amesema Serikali itaendelea kutoa miche ya mikarafuu bure kwa wakulima lakini vitalu vya Serikali viliopo hivi sasa haviwezi kukidhi mahitaji ya wakulima wote wa zao hilo, hivyo vitalu vya watu binafsi vitaendelea kuwa tegemeo kwa wakulima

  “Wakulima wa vitalu vya Mikarafuu mumekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza na kuimarisha zao la karafuu Zanzibar lakini wapunguzieni wakulima bei ya miche ingawa gharama mnazotumia ni kubwa,” Bi Mwanahija aliwashauri.

  Bibi Mwanahija amewaelekeza maafisa Kilimo kuwapa wakulima miche ya mikarafuu wanayoweza kuihudumia kwani uzoefu unaonyesha wakulima huchukua miche mingi wasiyoweza kuitunza na hatimae inakufa mara tu baada ya kumaliza mvua za masika.

  Mkuu wa Vitalu kutoka Wizara ya Kilimo Rashid Nassor Rashid alimueleza Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSTC kwamba vitalu vya Serikali vinakabiliwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi baada ya wengine kustaafu na baadhi yao kuzeeka hivyo wanampango wa kuajiri wafanyakazi wa muda kwa kazi za dharura kuziba pengo liliopo.

  Amesema kazi ya kutafuta mbegu (matende) kwa ajili ya vitalu vya mikarafuu zinachukua muda mfupi kabla ya mvua za masika kuanza na ikiwa kazi hiyo haitofanywa kipindi cha sasa kazi hiyo itashindwa kutekelezwa.

  Mkuu wa usimamizi wa zao la Karafuu kutoka Wizara ya Kilimo na Mali Asili Badru Kombo Mwemvura amemuhakikishia Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC kwamba iwapo wakulima watafuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo lengo la Serikali la kuongeza uzalishaji wa Karafuu litafika muda mfupi ujao.

  Amesema tatizo la wakulima wa zao la karafu ni kuchukua miche mingi bila ya kuwa na uwezo wa kuihudumia na baadhi yao huchelewa kuipanda baada ya kuchukua hatimae hufa huku wengine wakikosa kabisa.

  Ameongeza kuwa mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa yakiathiri sana nchi za visiwa nayo imekuwa changamoto kubwa kwa kilimo cha zao la Karafuu na mazao mengine Zanzibar.

  Wizara ya Kilimo ilipanga kutoa miche ya Mikarafuu milioni moja kwa wakulima wa zao hilo Unguja na Pemba, kuanzia mwezi wa April, lakini kutokana na ukosefu wa mbegu ulijiotokeza mwaka jana kiwango hicho huenda kikapungua .

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Tanzania Footbal Federation (TFF) ofisini kwake jijini Dar es salaam Machi 21, 2016 Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, Mkurugenzi wa Ufundi Salum Madadi na Msaidizi wa Rais wa TFF, Juma Matandika.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akifungua warsha ya siku moja baina ya Tume na Wadau kujadili mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 ya Mwaka 2011, iiliyofanyika katika ukumbi wa Tume Dra es Salaam.
  Baadhi ya wadau wakifuatilia vipengele vya sheria wakati wa kupitia mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.
  Tesha amabaye ni mjumbe kutoka Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) akiongoza kikao cha kupitia mapendekezo ya Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410.
  Sekretarieti ya Tume ikiwa makini kufuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kupitia mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma (Picha zote na Munir Shemweta, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania)

  0 0older | 1 | .... | 800 | 801 | (Page 802) | 803 | 804 | .... | 1897 | newer