Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 799 | 800 | (Page 801) | 802 | 803 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu ‘’UTT Projects and Infrastructure Development Plc’’ (UTT-PID) ni Taasisi inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania na kuendeshwa chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

  Menejimenti ya UTT-PID imesikitishwa na kitendo cha moja ya gazeti la kila wiki linalotoka hapa Tanzania katika matoleo yake mawili yaliyopita ya mwezi wa Machi 7 na Machi 14, mwaka huu kwa kuandika habari zisizo sahihi bila kupata maelezo ya Taasisi husika kinyume na maadili ya uandishi wa habari yanayovitaka vyombo vya habari kuzingatia usahihi, haki na usawa katika kutoa habari yoyote.

  Tunapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa baada ya Taasisi kufuatilia chimbuko la taarifa zisizo sahihi zinazotolewa na baadae kuandikwa kwenye gazeti hilo ilitoa taarifa kwa vyombo vya dola ambavyo vinafanyia uchunguzi suala zima la tuhuma na nani anazisambaza tuhuma hizo ambazo kimsingi zina lengo la upotoshaji na kuichafua UTT-PID.

  Aidha Menejimenti ya UTT-PID inawashauri waandishi wa habari na wahariri wa habari wajikite kwenye weledi, ukweli na maadili ya tasnia ya habari, wafanye utafiti wa kina na kutoa taarifa zilizo sahihi na kwa umakini, uhakika na kutokubali kamwe kutumiwa na watu au makundi ambayo yana agenda binafsi katika kufikisha ujumbe wenye matakwa yao.

  Mwisho tunawasihi wadau wetu katika miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya usimamizi wa UTT-PID, wateja wetu pamoja na Umma kwa ujumla kuendelea kuwa na imani na Taasisi ya UTT-PID kwa kuwa habari hizo ni za uzushi na zenye lengo la kuichafua Taasisi.
  Waweaza kutembelea UTT-PID kuifahamu zaidi kupitia tovuti yao: www.utt-pid.org

  TAARIFA HII IMETOLEWA NA
  KITENGO CHA MAWASILIANO YA UMMA UTT-PID
  GOLDEN JUBILEE TOWER 12 FLOOR. OHIO STREET
  DAR ES SALAAM
  18 MACHI 2016
  DSC_7498Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha (katikati-mbele) akizungumza na wanahabari mapema leo Machi 18.2016 juu ya kanusho za taarifa za uongo zilizotolewa na moja ya Gazeti la kila wiki hapa nchini dhidi ya taasisi hiyo.
  DSC_7495Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha(kulia) akisikiliza swali kwa makini kutoka kwa mwandishi wa habari (Hayupi pichani). Kushoto kwake ni Ofisa Mwandamizi wa UTT-PID, Bw.Liberatus Banzunaki wakati wa mkutano wao huo kwa waandishi wa vyombo vya habari mapema leo Machi 18.2016.DSC_7504Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha (kushoto) akitoa taarifa ya kukanusha kwa vyombooo vya habari dhidi ya tuhuma zilizoandikwa na moja ya Gazeti la kila wiki juu ya taasisi hiyo.Kulia kwake ni Mkuu wa Operesheni na miradi wa UTT-PID, Bw. Aleksandar Nikolic
  UTT-PIDMkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk.Gration Kamugisha akifafanua jambo wakati wa kutoa kanusho hilo dhidi ya tuhuma za uongo zilizoandikwa na moja ya gazeti la kila wiki hapa nchini pamoja na mitandao ya kijamii. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog.com).

  0 0


  Mwakilishi Mkazi Mwandamizi kutoka Kitengo cha Uchumi na Biashara, Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Lin Zhiyong (wa pili kutoka kushoto) akizungumza baada ya kikao kati ya Ujumbe kutoka ubalozi wa China nchini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) kilichofanyika ofisi za Utumishi mapema leo.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akisisitiza jambo wakati wa maongezi na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (wa pili kutoka kulia) alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
  Ujumbe kutoka ubalozi wa China nchini ukimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (hayupo pichani) ulipotembelea ofisini kwake mapema leo.

  0 0


  MBUNGE wa Viti  Maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Vicky Kamata (Viti maalum CCM) amesema kwamba amejisikia furaha na ana kila sababu ya kuiomba kampuni ya Msama Promorions kutimiza ahadi yake ya kulipeleka  Tamasha la Pasaka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Alisema kuwa mbali na burudani naamini kuwa hata wananchi watanufaika na Tamasha hilo kwa ujumbe  kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuhusiana na mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino' pamoja na vikongwe.

  Kwa kweli mauaji hayo yanatokana na imani ya kishirikina lakini kwa tamasha hili ambalo ni sawa na kutangaza injili kwa njia ya nyimbo itaweza kuvunja nguvu za kishetani na wananchi kumrudia mungu.

  “Nimefurahishwa katika hili naamini nguvu ya mungu itaenda kutenda kazi yake hivyo ni imani yangu kuwa watu watabarikiwa kwa kuvunja nguvu ya shetani na watu kumrudia mungu ,” alisema Mbunge huyo ambaye pia ni msanii.


  Aidha Mbunge huyo alisema angefurahi kama waimbaji ambao wametajwa katika tamasha hilo kama Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Upendo Nkone wafike Geita na wamewaandalia mapokezi ya aina yake kwani wana idadi kubwa ya mashabiki.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo akimkabidhi funguo za gari jipya la wagonjwa Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya shughuli ya  kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze. Tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokea na kuangalia nyaraka za gari hilo la kubebea wagonjwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo.
   Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari la kubebea Wagonjwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwasha gari jipya la Wagonjwa lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
   Sehemu ya Ndani ya gari hilo kama inavyoonekana .
   Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiendesha gari hilo la wagonjwa lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
   Gari  jipya la Wagonjwa lililotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Chalinze kama linavyoonekana kwa nyuma.
   Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia mara baada ya kukabidhiwa Gari hilo la Wagonjwa.
  Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Afisa Usafirishaji wa Ikulu  Athuman Natepe wakwanza kushoto, Mwenyekiti wa Wilaya ya Chalinze Said Omar Zikatimu wapili kutoka kulia na Dkt. Nasoro Ally Matuzya wakwanza kulia. Picha na IKULU
  Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekabidhi  gari la kubebea wagonjwa kwa hosipitali ya wilaya ya Chalinze, Ikiwa ni utekelezaji wa ilani na  ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi ikiwa ni pamoja na wa jimbo la Chalinze.

  Gari hilo la kubebea wagonjwa limekabidhiwa kwa niaba ya Rais, na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.           

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo, Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Mheshimiwa Rais kwa hosipitali hiyo ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wake kote nchini. Aidha, Ndugu Ilomo amewaomba viongozi wa jimbo la Chalinze kulitumia gari hilo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.


  Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa jimbo na  Wilaya ya Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mheshimiwa Rais    Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo na kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kusema kuwa, utendaji kazi wa Rais Magufuli umekuwa ukiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali na kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.

  Kwa upande wake Dakta Nasoro Ally Matuzya, amesema gari hilo limekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa umezingatia utekelezaji wa malengo ya Milenia hususan lengo namba nne  linalosisitiza kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano

  Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Ndugu Saidi Omar Zikatimu amesema gari hilo la kubebea wagonjwa litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo la Chalinze hususan katika kusaidia kutoa wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na kuwafikisha katika hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao kwa kupata huduma za afya kwa haraka.

  Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya kubebea wagonjwa yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani Morogoro.

  Hospitali mpya ya Wilaya ya Chalinze imepanda hadhi kutoka kituo cha Msoga ambayo ilikuwa haina gari la kubebea wagonjwa na hivyo kufanya usafirishaji wa wagonjwa kutoka hospitali hiyo hadi hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi au kutoka maeneo ya vijijini kuwa mgumu.

   
  Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu
   
  18 Machi 2016. 
     


  0 0

  Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
  KAMPUNI ya Husea imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuazishwa kwake Machi mwaka huu kwa kutoa msaada wa vifaa vya hospitali na kuwapa zawadi akinamama waliojifungua leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na wandishi wetu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Husea, Pamela Maro amesema kuwa Kampuni hiyo inajishughulisha na Mipango miji, utoaji ushauri bure kuhusiana na Ardhi, Upimaji wa Ardhi pamoja na uchoraji ramani za nyumba, pia amesema kuwa ofisi za Kampuni ya kampuni ya Husea zipo Sinza Palestina kwa yeyote anayetaka ushauri kuhusiana na ardhi anaweza kufika maeneo hayo kujipatia ushauri bila malipo.

  Pia Pamela amewaasa wanawake waliotoka kujifungua leo na wanawake wote wanaopenda kumiliki ardhi kisheria waende katika ofisi zao ili waweze kupata ushauri wa bure kuhusiana na maswala ya ardhi.

  Kwa upande wa Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Wandi Kariame amewapongeza wafanyakazi wa  kampuni ya Husea kwa kuadhimisha mwaka mmoja leo .

  Pia amewashukuru kwa  kuona mahitaji ya Hospitali hiyo na kuwapongeza wanawake waliojifungua leo kwa kuwapa zawadi ikiwa ni kuadhimisha siku iliyofunguliwa ofisi hiyo kwa kufikisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo kwani wangeweza kwenda  katika hospitali nyingine au kwenda kilabu cha  pombe (Bar) kwenda kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni yao kwa kunjwa na kula vitu wanavyovitaka tuu lakini wamewaona wao.
  Mratibu Huduma Tiba katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza, Faith Mdee akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Husea inayojishughulisha na utoaji ushauri, upimaji wa viwanja, uchoraji ramani za nyumba pamoja na mipango miji.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Husea, Pamela Maro akimkabidhi Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Dkt. Wandi Kariame  aadhi ya vifaa vinavyotumika katika uzalishaji katika wodi la wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Muuguzi katika wodi ya wazazi katika hospitali Palestina Sinza.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hosea, Pamela Maro  pamoja na madaktari wa hospitali ya Palestina Sinza wakimkabidhi baadhi ya zawadi zilizotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Husea, mama aliyotoka kujifungua katika hospitali hiyo, Bahati Ramadhani.
  Mfanyakazi wa Kampuni ya Husea akimwangalia mtoto aliyetoka kuzaliwa masaa machache yaliyopita. 
   Baadhi ya wazazi wakiwa wamewapakata watoto waliojifungua leo mara baada ya kupata zawadi na kampuni ya Husea jijini Dar es Salaam leo.


  Mfanyakazi wa Kampuni ya Husea akimkabidhi mama aliyetoka kujifungua mda mfupi kabla ya kupewa zawadi hiyo katika hospitali ya Palestina Sinza leo jijini Dar es Salaa.
   Mfanyakazi wa kampuni ya Husea akimkabidhi mama aliyejifungua kwa njia ya Operesheni katika hosipitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.
   Mama na mwana wake.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Husea, Pamela Maro(Kushoto) akiwa na baaadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Husea katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa zawadi kwa watoto walipozaliwa leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo tangu kuanzishwa.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja (wapili kutoka kushoto) akizungumza na kundi la waandishi wa habari kutoka nchini Finland (hawapo pichani) mapema leo walipotembelea taasisi hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen, Mshauri wa masuala ya Ushirikiano kutoka Taasisi ya UONGOZI Bi. Liisa Tervo na Mkuu wa Utafiti na Sera kutoka Taasisi ya UONGOZI Bw. Dennis Rweyemamu. 

   Kundi la waandishi wa habari 15 kutoka nchini Finland waliotembelea Taasisi ya UONGOZI mapema leo ikiwa ni moja kati ya mafunzo yao katika programu maalum ya maendeleo na sera inayoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland. Waandishi hao ambao wapo nchini kwa muda wa siku tano pia walisindikizwa na watumishi wawili kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland.
   Mratibu wa programu ya Maliasili Bi. Namwaka Omari (kulia) akitoa mada kwa waandishi hao wa habari kuhusu namna Taasisi ya UONGOZI inachangia katika kuimarisha usimamizi wa maliasili zetu nchini hususan katika sekta ya mafuta na gesi.

   Mmoja kati ya waandishi hao akiuliza swali. Baadhi ya mada zilizogusiwa katika mazungumzo ni pamoja na jinsi gani Tanzania inatekeleza dhana ya maendeleo endelevu, uimarishaji wa uwezo kwa viongozi barani Afrika, uchumi wa sekta ya gesi nchini na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ya UONGOZI katika mazingira ya Serikali Mpya.

  Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen (kushoto) akitoa neno lake la shukrani kwa niaba ya waandishi wa habari na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, walipotembelea Taasisi ya UONGOZI kufahamu shughuli zake mapema leo.  

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double Taxation kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi wapate nyumba za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za kijamii katika nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na Barabara. Picha Zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha NHC.
  Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wilfred Lwakatare akiongozana na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula na Mkurugenzi wa nyumba kutoka Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Michael Mwalukasa wakijadiliana jambo katika ziara hiyo.

  Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa, Raymond Mndolwa wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Hamad Abdallah wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Wajumbe wa Kamati hiyo wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif.
  Mradi wa Mwongozo unavyoonekana kwa juu
  Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.
  Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.

  0 0

   Mwenyekiti wa Makatibu wa  Umoja wa Vyama visivyo na uwakilishi Bungeni, ambae pia ni Katibu wa Chama cha SAU, Ali Kaniki  akizungumza na wandishi wa Habari katika ukumbi wa Studio ya kurikodia Rahaleo kuhusu kushiriki uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar tarehe 20 mwezi huu.
  Mmoja wa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha TLP Bwana. Hafidh Hassan Suleiman akithibitika wa kugombea na kuwataka wananchi kumpikia kura yeye. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  Na waandishi wetu.   Maelezo Zanzibar.
  Umoja wa vyama  vya siasa ambavyo havina  uwakilishi Bungeni wametoa tamko rasmi la kushiriki uchaguzi  wa marejeo tarehe 20 mwezi huu na wamewataka wazanzibar kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo.

  Hayo yamezungumzwa na makatibu wakuu wa vyama hivyo wakati walipokuwa wakizungumzwa na waandishi wa habari  katika ukumbi wa studio za Rahaleo  mjini Zanzibar.

  Wamesema Chama chochote cha siasa kazi yake ni kushiriki uchaguzi na sio kususia kwani kufanya hivyo kutakoseshawananchi  haki yao ya msingi na  kurudisha nyuma shughuli za maendeleo.

  Aidha  wameamua kurejea uchaguzi huo kutokana na kasoro zilizojitokeza uchaguzi wa mwanzo  ambapo  mambo mengi   yalionesha dhahiri  ulikuwa na kasoro za wazi wazi.

   Makatibu hao wamesema kurejewa uchaguzi sio jambo geni duniani  na yapo mataifa mengi yamewahi kurejea uchaguzi kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika chaguzi zao.

  Viongozi wa Umoja huo wamesema  pamoja na kushiriki uchaguzi pia wamesimamisha  wagombea  12 ambao wamo katika ngazi zote ikiwemo rais, wawakilishi na madiwani.

  Mwenyekiti wa umoja huo Ali Kaniki amewataka wazanzibari  kujitambua  na kufikra kwani wakiweza kujitambua wataweza kutoa maamuzi yaliyo sahihi.

  “Wazanzibar tujitambue kifikra kwani tukiwa tunajitambua tutaweza kutoa maamuzi yalio sahihi, alisema  Kaniki”
  Kwa Upande wake  mjumbe wa umoja huo Abdul Mhuya amesema  khatma ya wazanzibar imo mikononi mwa wazanzibar wenyewe  na Tanzania kwa ujumla hivyo wazanzibar wasikubali kuuipoteza thamani yaoya kushiriki kupiga kura kwa kupata viongozi wawatakao.

  Vyama vitakavyoshiriki katika marudiao ya uchaguzi huo ni DP,CCK, AFP, DEMOKRASIA MAKINI , SAU, TLP, UPDP, UMD, ADC, NRA, TADEA NA CHAUMMA.

  0 0

   Raia wa Kichina kutoka kulia ni na Xu Fujie na  Huang Jing  ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela au kulipa faini ya shilingi bilioni 54 leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
   Raia wa kichina wakisindikizwa na Askari Magereza mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Raia wa China wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 au kulipa zaidi ya sh.bilioni 54 kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili.

  Washitakiwa hao katika kosa la kwanza ni kukutwa ni kuwa na nyara ya serikali ya vipande vya meno ya tembo 706 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni tano na kosa la pili kushawishi kutoa rushwa kwa askari sh.milioni 30.

  Washitakiwa hao ni Huang Jing pamoja na Xu Fujie wameanza kutumikia kifungo hicho leo baada ya kushindwa kutoa faini hiyo.

  Akisoma hukumu hiyo Hakimu         Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Sprian Mkeya amesema kuwa kutokana na kupata maelezo katika pande zote mbili pamoja na kuisababishia hasara serikali washitakiwa adhabu yao ni miaka 30 au kulipa  ya zaidi ya bilioni tano (5).

  Hakimu Mkeya amesema washitakiwa hao wanaweza kukata rufaa makahakama kuu kutokana na hukumu iliyotoka.

  Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba mahakama iwape adhabu kali kutokana na kosa waliolifanya na kudai kuwa kutokana na kukamatwa kwao vitendo vya uhalifu kwa wanyamapori vimepungua
  Kwa upande wa Wakili upande wa washitakiwa Nehemia Mkoko aliomba mahakama kuwaonea huruma kwa adhabu wataoipata ili waweze kutoka na kuweza kujumuika na familia zao. Washitakiwa hao walikamatwa 2010 katika eneo la mikocheni mwaka huu.

  0 0


  Kaimu Kamishina wa Fedha na Utawala, Abbas Irovya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  IDARA ya Uhamiaji imefanya mabadiliko ya wafanyakazi katika vituo vya kazi ikiwa ni kuongeza ufanisi wa kazi wa idara hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishina wa Fedha na Utawala, Abbas Irovya amesema mabadiliko hayo ni kuongeza ufanisi kazi na tija.

  Mabadiliko hayo ni DCI.Faustine Nyaki Mkoa wa Iringa anahamia Mkoa Mwanza, na aliyekuwa Mwanza,DCI.Remigius Ibrahim Pesambilia anahamia kwenda kwa Mfwadhi wa Ofisi ya uhamiaji uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere , DCI.Rose Mhagama (Njombe) amehamia Mtwara,DCI.Chale,s Habe (Geita) anahamia Njombe.  Amesema kuwa mabadiliko hayo kwa wafanyakazi katika idara hiyo ni 200 ambapo inatokana agizo la Waziri mwenye dhamana hiyo.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double Taxation kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi wapate nyumba za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za kijamii katika nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na Barabara. Picha Zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha NHC.
   Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula  akiwa ameambatana na Mbunge wa Bukoba Mjini,Mh.Wilfred Lwakatare wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula na Mkurugenzi wa nyumba kutoka Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Michael Mwalukasa wakijadiliana jambo katika ziara hiyo
  Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Mikoa, Raymond Mndolwa wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.

  Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Hamad Abdallah wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Wajumbe wa Kamati hiyo wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif.
  Mradi wa Mwongozo unavyoonekana kwa juu
  Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.
  Kamati ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction Limited.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya Waziri Mkuu hajafungua duka la dawa la MSD Wilayani Chato juzi.
  Waziri Mkuu Mhe.Kassim M. Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato.

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari ya Dawa (MSD), la Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

  Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa(Tamisemi) mikoa na Wilaya kuanzisha maduka hayo,na kisha MSD itatoa ushauri wa kitaalam.


  Bwanakunu alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na MSD,lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato. 


  0 0

   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi, akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana, katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
   Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joel Kafuge, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala, Apruna Humba na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Maliaga.
   Wanawake wa CCM Wilaya ya Ilala wakiwa kwenyev mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.

  Na Dotto Mwaibale

  MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Masaburi amesema wanachama wa chama hicho waliokiuchumu wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wasitegemee kupata uongozi wowote ndani ya chama hicho.

  Masaburi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho na kukipa ushindi ambapo kimeunda Serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

  "Kunawenzetu walitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kuchangia mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kufanya vizuri hali iliyosababisha kuwepo na changamoto hata ya kumpata Meya wenzetu hao tunawafahama na hawatapata nafasi ya kupata nafasi ya uongozi ndani ya chama chetu" alisema Massaburi.

  Massaburi alisema ni heri kubakiwa na wanachama wachache waadilifu ndani ya chama kuliko kuwa wengi ambao ni wasaliti na katika jambo hilo ataendelea kulisimamia na kupigania maslahi ya chama ambacho anakitumikia.

  Katika hatua nyingine Massaburi aliwataka wana umoja huo kushikamana na kushirikiana na kuhakikisha nguvu yao inaendelea kukipa ushindi chama hicho wa kushika dola kwani jambo hilo linawezekana kwa asilimia 100.

  0 0

   Meneja wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Musoffe Laurance, akimkabidhi Cheti mshindi wa kwanza waMbio za Magunia kwa wanawake, Magreth John, aliyeibuka kidedea katika mbio hizo wakati  wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016. 

   Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akishiriki mchezo wa kukimbiza kuku, wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa Mfuko huo lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,jijini Dar es Salaam,leo Machi 19,2016.
   Meneja wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Musoffe Laurance, akimkabidhi Cheti mshindi wa kwanza wa Mbio za Magunia kwa Wanaume, Tumainieli Maleko, aliyeibuka kidedea katika mbio hizo wakati  wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016.
   Meneja wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Musoffe Laurance, akimkabidhi Cheti mshindi wa kwanza wa Mbio za mita 200 kwa Wanawake, Susan Ringo, aliyeibuka kidedea katika mbio hizo wakati  wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016. 

   Meneja wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Musoffe Laurance, akimkabidhi Cheti mshindi wa kwanza wa Mbio za Mita 200 kwa Wanaume, Elias Joseph,  aliyeibuka kidedea katika mbio hizo wakati  wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016.
   Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakichuana katika mchezo wa mbio za Magunia wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuocha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016. Katika mbio hizo Magreth John (mbele) aliibuka kidedea.
    Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,  wakishiriki mbio za Kizunguzungu, wakati wa Bonanza hilo.
   Meneja wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Musoffe Laurance, akimkabidhi Cheti mshindi wa pili wa Mbio za Mita 200 kwa Wanaume, Borrice Bwire, aliyeibuka kidedea katika mbio hizo wakati  wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016.
   Tumainieli Maleko, akimalizia mbio za magunia na kushika nafasi ya  kwanza wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,lililofanyika leo Machi 19,2016 kwenye Uwanja wa Ustawi wa Jamii,Jijini Dar es Salaam.
   Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki mazoezi ya pamoja wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuocha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016.
   Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakichuana katika mchezo wa mbio za Magunia wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuocha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016. Katika mbio hizo Merey Sammy  (kushoto) alishika nafasi ya pili na Mery Malilo (kulia) aliibuka mshindi wa tatu,huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Magreth John (hayupo pichani) 
   Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anthony Mkinga, akiruka kujaribu kumkamata Kuku, wakati wa mchezo huo wa kufukuza kuku katika Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016.
    wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,wakishiriki mchezo wa kuvuta Kamba wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa Mfuko huo lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam,leo Machi 19,2016. Katika mchezo huo Wanawake waliibuka kidedea kwa kuwaburuza wanaume.
   Picha na MafotoBlog.

  0 0

  Rais wa club za waandishi wa habari tanzania(utpc)

  Salma Said mwandishi wa DW Zanzibar ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao hawajafahamika jijini Dar es salaam, hali ambayo imeleta fadhaa na mshtuko kwa waandishi, jamii na familia yake  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa marejeo Zanzibar.

  Ifahamike kuwa Kazi  ya mwandishi wa habari ni kutoa habari juu ya kila kinachoendelea katika jamii , hivyo kama kuna dosari , dosari hiyo ni ya jamii na sio ya anayeieleza dosari .

  UTPC inalaani na kupinga utekaji uliofanywa ambao sababu zake bado hazijulikani, hivyo tunaitaka serikali kuhakikisha Salma Said anatafutwa, kupatikana  na anaachiwa huru mara moja kwa kuwa Serikali ndio yenye jukumu la kulinda raia wake.

  Kama utekwaji wa Salma umefanywa kutokana na kazi yake ya uandishi habari tunalaani vikali hatua hiyo, vitendo hivi havipaswi kuendelea katika  nchi inayoheshimu misingi haki na Demokrasia, Vitendo vya namna hii vinadumaza na kufifisha  uhuru wa habari .

  Tunapinga kwa nguvu zetu zote  waandishi wa habari kukamatwa na vyombo vya dola au makundi ya kihalifu kwa visingizio ama vya uchochezi au maslahi ya taifa.

  Waandishi tutaendelea kufanya kazi zetu bila kujali vitisho vya aina yoyote ile kutoka kwa mtu yoyote au Serikali.

  Imetolewa na
  DEOGRATIUS NSOKOLO
  RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC.
  March 19, 2016.


  0 0

  Baba wa Mzee BEDA


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda, akizungumza na wenyeviti na maofisa watendaji wa jiji la Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali haswa suala la usafi wa mazingira.
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mmbando akiongoza mkutano huo.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Mhe. Raymond Mushi akizungumza katika mkutano huo.
   Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akizungumza katika mkutano huo.
   Mwakilishi wa Taasisi ya Wakala wa Upimaji Ardhi Tanzania Bw. Linus Kinyondo akizungumzia suala zima la ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia mipango miji ili kutunza mazingira.
   Wenyeviti na maofisa watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)Picha na Dotto Mwaibale
  0 0

  By Sultani Kipingo.
  Tanzanians are happy with the implementation speed of the proposed construction of the Tanzania-Uganda crude oil pipeline which is expected to start in August this year, and will be completed in 2019. 

  Many of those interviewed expressed gratitude to President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and his Tanzanian counterpart Dr. John Pombe Joseph Magufuli for initiating the 4-billion-U.S. dollar oil pipeline project that is expected to hasten socio-economic development between the two nations.
  “We are overwhelmed by the rapidity of the project considering only two weeks have  passed since  Presidents Museveni and Dr. Magufuli  jointly approved the project when they met in Arusha. 

  “It is unbelievable to note that officials from both sides have this week signed the agreement and come August the construction work takes off”, said Ms Natala Kimaro of Moshi. Amani Abdallah of Tanga  said that the 1,403-kilometer pipeline that will link oil fields in Uganda’s Lake Albert, Hoima region to Tanga port in Tanzania is testimony to true East African integration spirit, hoping more such projects would be initiated. 

  The construction of the crude oil pipeline will be carried out by three oil firms–UK’s Tullow Oil PLC, France’s Total E&P and China’s Cnooc. Once completed, the pipeline is expected to transport up to 200,000 barrels per day passing through a number of Tanzanian regions from the Indian Ocean port of Tanga to Uganda. 

  The construction will lead to installations of 200km of permanent new roads and corresponding bridges, and upgrades to 150km of existing roads, opening up regional integration in the energy sub-sector.  Tanzanians are also happy that that the crude oil pipeline project will also increase foreign Direct Investment  by more than 50 percent per annum, let alone creating over 15,000 jobs.
  Tanzania President Dr. John Pombe Joseph Magufuli announces the crude oil pipeline project to reporters after his meeting with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the  The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit 
  "The project will be implemented at Dr. Magufuli's  speed" jokes President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda when confirming  the project to reporters after talks with his host President Dr. John Pombe Joseph Magufuli on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the  The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit. 
  Tanzania's Minister for Energy and Minerals  Prof. Sospeter Muhongo (second left) and Uganda's Minister for Energy and Minerals Development Engineer  Irene Muloni ( wa tatu right), with the Managing Director of the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) Dr. James Mataragio  (left) and the General Manager of  Total E&P Uganda, Mr Adewale Fayemi (second right) sign the crude oil pipeline project implementation plan in Arusha on March 17, 2016. Seated extreme right is Permanent Secretary Ministry of  Energy and Minerals Development of Uganda Dkt. Kabagambe Kaliisa 
  Map of the proposed crude oil pipeline project

  0 0
  0 0

  Na Clarence Nanyaro- NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),imesema haitambui kujitoa kwa Chama cha Wananchi (CUF),katika uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Jumapili licha ya kuwa Tume imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.

  Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku ma 
  andalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.

  Aidha Bw Kailima ameeleza kuwa,kwa kuwa karatasi za kupigia kura zilishachapishwa na kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo,zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa CUF hata kama wamejitoa katika uchaguzi huo.

  Awali,wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali vya kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.

  Tume ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogondogo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye majina ya wapiga kura,mfano katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.

  Jimbo la Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo 53 vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge wa Jimbo la Kijitoupele siku ya Jumapili.

  Sambamba na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa uatafanyika Jumapili hiyo pia.

  Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu ndogondogo zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura,kabla ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25,2015.

older | 1 | .... | 799 | 800 | (Page 801) | 802 | 803 | .... | 1904 | newer