Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WAZIRI SIMBACHAWENE AMPA SIKU TATU RC KUUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA VIONGOZI NA WAKUU WA SEKONDARI WANAOLALAMIKIWA KUTUMIA VIBAYA UONGOZI WAO

$
0
0

Na Woinde Shizza, Karatu Vijiji

WAZIRI waNchi Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mh,George Simba Chawene amempa siku tatu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda kuhakikisha anaunda kamati maalumu ambayoitafanya uchunguzi kubaini viongozi wa vijiji na wakuu wa sekondari wa wilayaya karatu wanaotumia vibaya uongozi wao hali iliyopelekea kuwepo kwamalalamiko.

Waziri Simbachawene aliyasema hayo wakati alipokuwa kwenye uzinduzi wa majengo ya ofisi na maendelo ya parokia na Karakana ya Chuo cha Ufundi Audrey Veldamaniliyopo kijiji cha Kitete Wilayani Karatu Mkoani Arusha ambavyo vinamilikiwa naKanisa katoliki Parokia ya Kitete.

Alisema kuwa kutokana na malalamiko aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa Dini pamoja nawananchi katika Wilaya ya Karatu kuhusiana na kuwepo kwa baadhi ya viongozi wavijiji na wakuu wa shule za Sekondari kutumia vibaya uongozi wao ahakikisheanaunda kamati hiyo ili watakapobaini ukweli waweze kutumbuliwa majipu harakasana.

‘’Mkuu waMkoa nakupa siku tatu fatilia jambo hili kuna ubadilifu mwingi upo wizi wafedha wakuu wa shule wamekuwa wakiiba hela za wazazi,ufaulu kwa wanafunziumeshuka sana katika shule zote za Karatu ,viongozi wa kijiji, kata hawako makini na kazi sasa unda kamati ili tupate ushahidi wa kudumuili tuwatimue’’alisema Simbachawene.

Pia alimpasiku saba Mkuu huyo wa Mkoa kuhakikisha anashushughulika suala la kuboreshamiundo mbinu hususani barabara ambayo imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa vijijivi navyozunguka Wilaya ya Karatu akidai kwamba anapaswa kukutana na wakurugenziwa monduli na karatu kukutana na kupanga namna ya kufungua barabara  kuanziaManyara,inayopita sabasaba ,kitete ,Lostete mpaka serera katika kipindi hikicha mwaka huu wa fedha huku akimsihi kuanza kufikiria Barabara ya Namangakupitia Monduli ,ziwaNatron ili iwe ya Mkoa.

Alidai kuwa kuwepo kwa barabara hizo kutasaidia wananchiwa kufanya biashara zao kwa urahisi huku watalii wakimiminika kwa wingi jamboambalo litafanya wafanyabiashara kutumia Raslimali za hapa nchini.,Nae Mkuu waMkoa wa Arusha Felix Ntibenda alisema kuwa anawasihi viongozi wa Wilaya yaKaratu kuwafanyia kazi wale watendaji na wenyeviti wanaokwamisha kazi zamaendeleo ya Nchi kuwafukuza kazi maramoja kabla ya kufika kwake.

‘’Nawambiawakurugenzi na wakuu wa wilaya wafukuzen kazi hao wanaokwenda kinyume na kazitutapata wengine hata kama walichaguliwa na wananchi tambua masuala ya uchaguziyameisha kwisha hakuna chadema wala CCM nisingependa nisikie malumbano bali nikufanya kazi kwa kuheshimu madaraka yaliyoko madarakani’’alisema FelixNtibenda.

Awali akitoahotuba yake mbele ya waziri Paroko waParokia hiyo Padri Costantine Changwe alisema kuwa katika kijiji cha kitete wananchikwa ujumla wanakabiliwa na changamoto kubwa ya barabara huku akidai kwambawakati wamasika huwa wanadondoka makorongoni na wengine kupoteza maisha jamaboambalo limekuwa kero kubwa kwa jamii hiyo.

Alisema kuwakumekuwepo na viongozi wa vijiji na vitongozi wa Mbulumbulu ambao wamekuwa nauongozi mbaya kwa madai kwamba wanalumbana kisiasa hawataki maendeleo hukuwakipingana na kauli ya hapa kazi . Alisema kuwawamekuwa wakitanguliza siasa bila uzalendo kwa maslahi yao binafsi huku akisemawanapaswa kunyoshewa vidole hata kutumbuliwa majipu jambo
ambalo litasaidiakuleta maendelea ya wanyonge.

MBUNGE WA ILEMELA AWAITA WAKAZI WA MWANZA NDANI YA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0
MBUNGE wa Ilemela, Angelina Mabula ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na maeneo ya karibu kujitokeza kwa wingi kwa sababu ya unyeti wa Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza jana, Mabula alisema Tamasha la Pasaka ni la Watanzania wote, lakini mwaka huu wamepata bahati ya kufikiwa na ujumbe wa neno la Mungu ambao utakemea maovu kama mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi 'albino'.

"Binaadam anatakiwa kubaki na heshima yake, kwani hakuna maisha bora ambayo yanatokana na kuwaua na kuwakata viungo wenzao, si ubinaadam kabisa tunatakiwa tumrudie Mungu kwani ndio kimbilio," alisema Mabula.Mabula alisema Tamasha la Pasaka limebeba ujumbe wa neno la Mungu hivyo ni nafasi kwa wakazi wa Ilemela na maeneo ya jirani na hata mikoa mingine kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.

Aidha Mabula alisema thamani ya Tamasha la Pasaka ni kubwa hivyo Watanzania ni nafasi yetu Watanzania kumfikishia Mungu sala zetu.Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea vizuri, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kula.

Msama alisema Tamasha la Pasaka litaanza Machi 26 mkoani Geita na kufuatiwa jijini Mwanza Machi 27 na kumalizia Machi 28 mjini Kahama kwenye uwanja wa Taifa mkoani Shinyanga.Msama alitaja viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000, naye alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kuimuimbia na kumtukuza Mungu.

WIZARA YA AFYA,YAZINNDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA DAWA,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI HASA KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Bw.Mpoki Ulisubisye akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango kazi wa Taifa wa dawa,vifaa tiba, na vitendanishi hasa katika ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kudhibiti wizi wa dawa pamoja na uwajibikaji,mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde akifafanua jambo kwa waAndishi wa habari jinsi ya kuwezesha udhibiti wa wizi wa dawa pamoja na uwajibikaji, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).

Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto imezindua mpango mkakati wa Taifa wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi hasa katika ngazi ya Halmashauri kwa lengo la kuboresha huduma ya afya katika Halmashauri hizo.

Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Bw.Mpoki Ulisubisye amesema kila dawa katika Halmashauri husika itakuwa na nembo pamoja na takwimu za watumiaji kwa lengo la kukwepa wizi wa dawa na kuwapa taarifa wawekezaji kwa kuweka viwanda vya dawa za binadamu.

Katibu Mkuu huyo,Bw.Ulisubisye ameongeza kuwa ukaguzi wa dawa utakuwa endelevu,usimamizi wa vifaa pamoja na kuona utoaji wa huduma za afya kwa mpango huo una ubora mkubwa.

Hata hivyo, Wizara ya Afya imeeleza kuwa mpango huo utadumu kwa miaka mitano hasa katika kutekeleza mpango wa dawa kupatikana katika kila Halmashauri pamoja na kuongeza uwajibikaji kwa watoaji huduma za afya.

ZIARA YAWAZIRI MKUU, CHATO NA KATORO - GEITA.

$
0
0
 Waizri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kukamu mafuta ya alizeti  wanaushirika wa Chato akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita Machi 17, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Ushirika huo Elias Kaswahili. 

 Wasani wa Katoro Geita wakicheza ngoma ya Kisukuma mara baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo  Machi 17, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika mji wa Katoro , Geita Machi 17, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TISHIO LA WAFANYABIASHARA KUFUNGA MADUKA.

WAMILIKI WA MADUKA YA DAWA YALIYOKUTWA NA DAWA ZA SERIKALI WAFIKISHWE MARA MOJA MAHAKAMANI-DK.KIGWANGALLA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangalla akizungumza katika mkutano wa matokeo ya ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangalla akiangalia baadhi ya vifaa tiba na dawa zilizo kamatwa katika operesheni hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
 NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangallaameagiza Baraza la Wafamasia pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),kuwafikisha mahakamani wale wote waliokutwa na dawa za serikali katika maduka yao.

Kigwangalla  ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kupewa matokeo ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa muhimu na yasiokuwa na vibali iliyofanywa na Baraza la Wafamasia na TFDA  pamoja na Jeshi la Polisi, amesema dawa zilizokamatwa zitaifishwe na kupeleka katika hospitali za serikali.

Amesema kuwa haiwezekani wananchi wakakosa dawa za serikali na kuonekana katika maduka ya dawa na watu hao wakaachwa bila kuchukuliwa hatua.

Kigwangalla amesema kuwa katika operesheni hiyo baadhi ya maduka yanauza dawa ambazo haziko kwenye orodha za dawa ikiwemo ni dawa ya usingizi ambayo inatakiwa kutumika wakati wa operesheni.

Aidha amesema kuwa baadhi ya maduka mengine yamefungwa lakini yanauza dawa nyakati za usiku na kuwataka wanaofanya operesheni kuendelea na wataokutwa wachukuliwe hatua mara moja.
Operesheni hiyo ilianza machi 1 hadi 3 mwaka huu ambapo walikagua maduka 685 katika mikoa tisa na kati hayo maduka 432 yamefungiwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo na kuwa na dawa za serikali pamoja na kuwa dawa za asili.

Aidha Kigwangalla amesema kuwa dawa ni sumu hivyo inatakiwa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wanaouza dawa ambazo hawana orodha nazo wanazalisha matatizo ya kiafya kwa wananchi.

Kigwangalla amesema hadi sasa ni dawa 65 tu ndiyo zenye nembo ya serikali na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano pale watakapopata dawa serikali katika duka la dawa.

Amesema kuwa jeshi la polisi lichukue hatua ya kuwabana wale wote  waliokutwa na dawa za serikali kuwabana katika kuweza kuwapata waliokuwa wakiwapa dawa hizo.

WAKALA WA USIMAMIZI WA MAFAA KUANZISHWA

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa ya taifa(TANDTRADE)( Hawapo pichani) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju akifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni katibu wake.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maafa ya taifa kutoka katika Wizara,Taasisi na Idara za Serikali wakifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Maafa ya taifa kutoka katika Wizara,Taasisi na Idara za Serikali wakifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Na Raymond Mushumbusi MAELEZO


Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Serikali imekusudia kuanzisha Wakala wa Usimamizi wa Maafa Tanzania chini ya Sheria ya mwaka 2004 ambao utakuwa na jukumu la kupambana na maafa yatakayojitokeza kwa kuratibu na kuwezesha waathirika wa maafa kupata misaada ya mahitaji muhimu kwa haraka.

Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Taifa(TANDTRADE) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua amesema Serikali imedhamiria kuanzisha Wakala wa Usimamizi wa Maafa ili kuweka utaratibu mzuri ambao utasaidia kushughulikia kwa umakini maafa yatakayokuwa yakijitokeza katika sehemu mbalimbali nchini.

“ Ipo Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa basi ni jambo jema kuwepo kwa Wakala ili kuweza kuratibu vizuru shughuli za kupambana na maafa yanayotukumba”

“Tumekutana leo hapa katika kikao cha kawaida cha kupata taarifa juu ya maafa yanayotokea nchini na tutajadili na kutoa madhimio ambayo yatatoa majibu ya nini kifanyike katika kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa kupambana na maafa” Alisema Dkt Mwinyimvua.

Kamati ya Maafa ya Taifa iko chini ya mwenyekiti ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu ikiwa na wajumbe kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa, Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Watoto na Wazee, Jeshi la Zima Moto,Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Taasisi na Idara za Serikali zinazohusika na maafa.

WAZIRI NAPE AWATAKA WAUZAJI WA FILAMU ZA NJE KUFUATA SHERIA.

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wauzaji wa filamu za nje kuhusu kufuata sheria ya uuzaji wa filamu hizo hapa nchini katika kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akieleza jambo wakati kikao kati ya Serikali na wauzaji wa Filamu za nje(Hawapo Pichani) kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw Tairo.
Mwenyekiti wa wauzaji wa filamu za nje Bw Joseph Lyakurwa akiwasilishwa mada kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati wa kikao baina ya Serikali na wauzaji wa filamu hizo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wauzaji wa Filamu za nje walioshiriki katika kikao kati yao na Serikali cha kubadilisha sheria ya uuzaji wa filamu za nje hapa nchini kilichofanyika leo jijjini Dar es Salaam.

Na: Shamimu Nyaki

Kufuatia kuwepo kwa Filamu nyingi za nje zinazouzwa hapa nchini bila kufuata Sheria ya uuzaji wa kazi hizo Serikali imewataka wauzaji hao kufanya biashara hiyo kwa kufuata na kuzingatia sheria iliyowekwa ili kusaidia kukuza na kutangaza filamu za hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati alipokuwa akizungumza na wauzaji wa Filamu hizo leo jijini Dar es Salaam.

Amewataka wauzaji hao kuwa na mkataba pamoja wamiiki wa kazi hizo ili waweze kufanya biashara hiyo kwa uhalali kwakua Serikali itawasaidia kusimamia utekelezaji wa mikataba hiyo na kurahisisha utekelezaji wa sheria iliyopo.

“Lazima mfuate na kutekeleza Sheria iliyopo kwakua mimi nipo hapa kuisimamia na kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa”.Alisema Mhe.Waziri Nape.

Aidha katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo ameongeza kuwa ni lazima wauzaji wa filamu hizo kuhakikisha kuwa filamu wanazouza zimehakikiwa na bodi ya filamu pamoja na COSOTA ili kudhihirisha ubora wa kazi hizo na viwango vya hapa nchini.

“Ni lazima muhakikishe kazi mnazouza zimeruhusiwa na Bodi ya filamu pamoja na COSOTA na zinafuata madili ya hapa nchini’’.Aliongeza Bi. Joyce.

Ameongeza kuwa bodi ya Filamu pamoja na COSOTA wapo tayari kuwasaidia kupata haki miliki ya filamu hizo wanazouza kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kuruhusu filamu gani inastahili kuuzwa na ipi haistahili kuwepo sokoni.

Uuzaji wa filamu za nje hapa nchini umechangia kwa kiasi kikubwa filamu za hapa nchini kukosa soko hali inayochangia kudidimia kwa sanaa hiyo hapa nchini ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana.

NHIF WATAKA MAONI KUTOKA KWA WANACHAMA WASTAAFU.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Emmanuel Humba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii akiongea na waandishi wa habari kuhusu kikao cha wanachama wastaafu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewataka wanachama wastaafu wanaohudumiwa na mfuko huo kutoa maoni na ushauri wa namna ya kuboresha huduma zitolewazo kwa ajili yao.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii Bw.Eugin Mikongoti alipokua akiongea na wanachama wastaafu katika mkutano ulioandaliwa na NHIF.

“Hatukuwahi kuwa na mkutano maalumu wa wanachama wastaafu,ndiyo maana mkutano huu kwetu ni wa kihistoria na tunaamini ni muhimu kukutana na wastaafu peke yao ili kutoka kwao tusikie, siyo tu huduma nzuri wanazozipata bali pia changamoto wanazozikabili ili kwa pamoja tuweke mkakati wa kuzitatua”alisema Mikongoti.

Bw. Mikongoti ameongeza kuwa, wakati wote wamekua wakipokea na kuzingatia ushauri na maoni ya wadau wake wote, kwahiyo wanatarajia mkutano huu na wanachama wastaafu utakua ni uwanja mzuri wa kubadilishana mawazo na kupata ushauri wa namna ya kuboresha zaidi huduma zao.

Aidha,Mwenyekiti wa kikao cha wastaafu,George Yambesi amewasihi wastaafu wenzie wafuatilie kwa makini na waulize maswali kwa kadiri watakavyoweza ili wawe na uelewa mpana kuhusu huduma za mfuko wa NHIF kwakua hii ndio fursa yao maana hawapo kwenye ajira na hivyo sio rahisi kupata taarifa za mara kwa mara.

Pia Bw. Yambesi kwa niaba ya wenzake ameipongeza Serikali kwa kuufanya Mfuko huu kutoa huduma za matibabu kwa wastaafu pia amewashukuru viongozi waasisi wa Mfuko kwa kuweka misingi bora ya kuwashughulikia wastaafu bila kukata tamaa.

Naye mmoja wa wastaafu kutoka Shirika la Utangazaji la Taifa Ngalinecha Ngahyoma anaishukuru NHIF kwa kuwasaidia wastaafu kupata matibabu maana gharama za matibabu ni kubwa bila kuwa na bima za afya wastaafu wasingeweza kulipia huduma hizo.

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)

$
0
0
3
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia.
kamati hiyo imekutana na uongozi wa mfuko huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuangalia mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za kurekebisha zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia jamii katika suala zima la afya , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
5
Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala Mh. Azzan Zungu, Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe, Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Busega Dk. Raphael Chegeni, Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndugulile, Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF Bw. Michael Muhando na Mkurugenzi wa huduma za utabibu na ufundi Dk.Frank Lekey wakielekea kwenye mkutano.
6
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano huo huku Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo, kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile.
7
Wajumbe wa kamati hiyo wakisikiliza wakati Kaimu Mkurugenzi wa NHIF alipokuwa akiwasilisha ripoti ya shirika hilo kwa kamati hiyo leo.

8
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya Jamii, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani na Ali Othman Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.
9
Mjumbe wa kamati Mbunge wa Buchosa Mh. Dk Charles Tizema akitoa mchango wake katika mkutano huo.
11
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo wakati wa mkutano huo kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati na Mbunge wa jimbo la Buseka Dk. Raphael Chegeni.
12
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge wakifuatilia.
13
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa na kamati hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
15
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kilichoanzishwa kwa ajili ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali kuhusu mfuko huo bila kulazimika kufika ofisini.
16
Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Muhando wakati akielekea kukagua eneo linaohifadhi kumbukumbu za mfuko huo.
01
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa jijini Dar es salaam.
1
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni na mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili katika ofisi za mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
2
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YATEMBELEA TASAF NA TUME YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Ladislaus Mwamanga akiwasilisha mada ofisini kwake wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa mchango wake wakati wa kikao kati ya Tume ya Utumishi wa Umma na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kilichofanyika ofisi za Tume mapema leo. 
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akifuatilia mada wakati wa kikao kati ya Tume ya Utumishi wa Umma na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kilichofanyika ofisi za Tume mapema leo. 
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Bw.Steven Bwana (wa pili kutoka kulia) akieleza baadhi ya changamoto za kazi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipofika ofisini kwake leo.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Ruth Mollel (Mb) akitoa mchango wake wakati wa kikao katika ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma na Kamati hiyo kilichofanyika mapema leo.
 Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa akitoa mchango wake wakati wa kikao kati ya Tume ya Utumishi wa Umma na Kamati hiyo kilichofanyika ofisi za Tume mapema leo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa mchango wake wakati wa kikao kati ya Tume ya Utumishi wa Umma na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kilichofanyika ofisi za Tume mapema leo.

MWIGULU AONYA KUHUSU MAUAJI YA KISIASA

$
0
0
WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi,  Bw. Mwigulu Nchemba amesema hakuna chama cha siasa ambacho kinaweza kuthaminishwa na maisha ya mwanadamu na kwamba wananchi hawana sababu ya kupigana na kutoanabugai kwa sababu ya ushabiki wa vyama.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi,  Machi 17, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Katoro, wilayani Geita alipopewa nafasi kuwasalimia wananchi kwenye mkutano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. 


"Duniani kote hakuna chama cha siasa kinaweza kuwa na thamani sawa na maisha ya mwanadamu au damu ya mwanadamu. Ninazungumza hili nikihusisha na matukio ya hivi karibuni hapa Geita na kule Tunduma ambako raia wetu walipoteza maisha kwa sababu ya tofauti za kisiasa, "alisema.


Aliwauliza wananchi hao ni kwa nini wanapigana hadi kutoana uhai wakati wao (wananchi) hawaendi bungeni. "Ninyi mnaopigana hakuna hata mmoja wenu anayeingia bungeni lakini sisi tukikutana kule bungeni tunasalimiana na kugongeshana glasi. 


Akitolea mfano kauli hiyo, Waziri Mwigulu alisema wakati waneenda kwenye msiba wa wana CCM waliouawa huku Tunduma, baada ya mazishi yeye na Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe pamoja na wanasiasa wengine walikaa na kula nyama za kuchoma hadi saa usiku.


"Nini kinachowafanya muwe maadui wa siasa kiasi hicho?" alihoji na kuongeza: "Mnasababisha watoto wasio na hatia tena wasiojua siasa wawe yatima. Duniani siasa hazina tofauti kama zilivyo mechi za mpira. Leo unavaa jezi hii na kesho jezi ile. Acheni kufanya uadui katika siasa", alionya.


Wakati huohuo,  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamtuma Waziri wa Nishati na Madini, Prof.  Sospeter Muhongo aende Geita keshokutwa (Jumamosi, Machi 19, 2016) ili akasikilize malalamiko ya wananchi hao juu ya suala la magwangala.


Magwangala ni mchanga uliochimbwa mgodini na kuchujwa na sasa unatakiwa kuchujwa tena ili utolewe mabaki ya madini na wachimbajiwadogo wadogo.


“Nimemuita Profesa Muhongo aje na timiu yake ya wakurugenzi pamoja na wataalamu wa STAMICO ili waje wakamilishe suala hili. Najua lilikwishaanza kughughulikiwa tangu Makamu wa rais alipopita hapa mwezi uliopita na sasa nimeambiwa kuwa limefikia asilimia 75 ya utekelezaji,” alisema.

Waziri Mkuu amemaliza ziara ya mkoa huo na anarejea jijini jioni hii.

MAKALA ATAKA SUALA LA UGONJWA WA KIPINDUPINDU LIWE HISTORIA MKOANI MBEYA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abasi Kandoro (kulia) akimkabidhi rasmi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Machi 17 mwaka huu. 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akizungumza na watumishi waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro Machi 17 mwaka huu . 
Baadhi ya watumishi wa ofisi ya mkoa wa mbeya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa huo Amos Makala wakati akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abasi Kandoro Machi 17 mwaka huu. 
Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abas Kandoro akizungumza na watumishi na baadhi ya viongozi (hawapo pichani)waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofsini na Mkuu wa Mkoa mpya Amosi Makala Machi 17 mwaka huu. 
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro wakati akiwaaga rasmi mara baada ya kustaafu rasmi nafasi hiyo. 
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja akitoa taarifa fupi kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo. 
Baadhi ya watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi .(JAMIIMOJABLOG)  

Na Emanuel Madafa, Mbeya.

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, amewaagiza watendaji wote wenye dhamana ya kulinda afya na usalama wa wananchi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa kipindipindu unakuwa historia mkoani Mbeya kwa kusimamia usafi katika ngazi zote za kijamii.

Mbali na agizo hilo , pia Makala amewaagiza Wakuu wote wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani humo kuandaa madawati ya malalamiko katika kila siku za Alhamisi kuanzia ili kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu kero mbalimbali zinazojitokeza kwenye maeneo yao.

Mkuu huyo mpya wa Mkoa wa Mbeya ametoa maagizo hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa ofisi ya mkoa wa Mbeya na mtangulizi wake, Abbas kandoro, ambaye amestaafu utumishi wa umma baada ya kufanya kazi kwa miaka 40 kuanzia mwaka 1976.

Amesema suala la ugonjwa kipindupindu hatopenda kulisikia katika uongozi wake hivyo amezitaka mamlaka husika kuwajibika ipasavyo ili kudhibiti kabisa ugonjwa huo hatari.Wakati huo Makala amepiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma mkoani humo, wakati wa saa za kazi ili kutoa fursa kwa watumishi hao kutimiza vyema majukumu yao kazini.

Ameonya kuwa hatamvumilia mtumishi yeyote atakayebainika kupoteza muda mwingi kwenye mitandao hiyo huku akishindwa kutimiza majukumu yake katika kuwatumikia wananchi.Hata hivyo, Makala alitahadharisha kuwa haitaji majungu ya aina yoyote kutoka kwa watumishi wa sekta wala wanannchi mbalimbali mkoani hapa ili kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza majukumu yake na si kukwamishana katikautendaji wa kazi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abaas Kandoro amewashukuru watumishi na viongozi mbalimbali kwa ushirikiano waliompa wakati wa utumishi wake na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mkuu wa mkoa huo Amosi Makala ..

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Familia ya Bwana Mathew Chando wa Mikocheni Regent Dar es salaam inasikitika kutangaza kifo cha Baba yao mpendwa mzee Mathew Chando kilichotokea tarehe 15/03/2016 huko  Regent Estate mtaa wa Chato  Dar es salaam.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 19/03/2016 saa 9 alasiri katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam na yatatanguliwa na ibada ya mazishi itakayofanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Msasani Dar es salaam kuanzia saa 7 mchana.

Habari ziwafikie ukoo wote wa Mathew Chando,ndugu,jamaa na marafiki popote pale walipo. msiba uko nyumbani kwa marehemu Regent estate mtaa wa chato dar es salaam.

"Yesu akwambia,mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi,ajapokufa,atakua anaishi". Yohana 11:25.

KIWANDA CHA RHINO CEMENT CHA TANGA CHAFUNGIWA KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (MB) amekifungia kiwanda cha kuzalisha cement na chokaa kilichopo jijini Tanga cha Rhino Cement, leo jioni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni uharibu na uchafuzi wa mazingira na kuvunja sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Mh. Mpina amechukua uamuzi huo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya maweni kupitia diwani wa kata hiyo Bw. Joseph Colvas na kujionea mwenyewe namna ambavyo kiwanda hicho kinavyo achilia moshi mzito kwenda angani, pamoja na vumbi lisilovumilika kusambaa katika maeneo ya makazi ya wanachi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaa katika maeneo ya shule ya sekondari ya Don Bosco ambapo, Mh. Mpina ameelezwa kuwa athari zitokanazo na uachiachi wa hewa hiyo chafu angani si tu kwa watoto wa shule zinazozunguka kata hiyo bali pia ni kwa viumbe hai na mazingira.

“Hawa jamaa wamekuwa wakiachilia vumbi jingi na moshi mzito kutoka katika kiwanda hiki mara kwa mara, hivi tangu jana wamezima mitambo yao wakijua kabisa kuwa kuna ugeni wa Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Alisisitiza Bw. Joseph.”

Kwa upande wake Afisa Afya wa jiji la tanga aliyejulikana kwa jina moja la bwana Kizito alimuelezea Naibu Waziri Mpina kuwa ni kweli kiwanda hicho kimekuwa kikifanya uchafuzi huo wa mazingira, na Afisa uendeshaji kutoka Baraza la Taifa na HIfadhi ya Mazingira NEMC Bw. Novatus Mushi ameeleza kuwa kiwanda hicho kimeshawahi kutozwa faini ya shilingi milioni kumi na saba (17) kwa kosa la kuchelewa kulipa ada ya mwaka ya mazingira pamoja na uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa na kiwanda hicho kwa upande wa kuzalisha chokaa.

Mh. Mpina ameelekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) kukifunga kiwanda hicho kisiendelee na uzalishaji kwa muda usiopungua miezi mitatu, na kulitaka baraza hilo lijiridhishe na kufuatilia namna kiwanda hicho kinavyotakiwa kutekeleza sheria ya mazingira kwa kujenga mfumo wa kisasa wa kutoa taka zitokanazo na uzalishaji kiwandani hapo pamoja, na kupima vumbi na moshi utokao kiwandani hapo kama hautakuwa na madhara na athari kwa mazingira na viumbe hai. Kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa moja kwa moja.

Aidha, akitolea mfano wa kiwanda cha bonite bottles cha mjini moshi kwa kuwa kinara katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira, mh Mpina alivitaka viwanda vingine viige mfano wa kiwanda hicho cha coke cola.

Ziara ya Mh. Mpina Jijini Tanga ilihusisha pia kuangalia namna ukuta wa fukwe ya Pangani uliojengwa enzi za mkoloni, ulivyo athirika na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kusema kuwa, ukuta huo huko kwenye mchakato wa kujengwa na kuboreshwa upya, ifikapo mwezi wa  nne mwaka huu mradi wa ujenzi wa ukuta huo utaanza kutekelezeka kwa kuwa tenda imeshatangazwa na jumla ya kiasi cha fedha za kimarekani dola milioni 1,400 zimepatikana kupitia mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCf).

Mh. Mpina aliwaasa wakazi wa mji wa Tanga na viunga vyake kutunza mazingira kwa kupanda miti na kufanya usafi kama ilivyoagizwa na serikali, ili kuhepukana na nchi kuwa janga na magonjwa yatokanayo na uchafu. Waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh na kiwanda cha Tanga Cement na kuridhirishwa na namna ambayo wanatekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
 kushoto meneja mkuu wa kiwanda cha maziwa cha tanga fresh Bw. Michael Kalata, akimuonyesha mh Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, moja nya bidhaa ya maziwa inayozaliswa katika kiwanda hicho. mh Mpina alitembelea baadhi ya viwanda jijini tanga kujionea namna ambavyo vinatekeleza sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni zake. 
 Pichani Namna ambavyo fukwe ya Pangani Jijini Tanga ilivyoliwa na maji ya bahari, kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari ikiwa ni athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. na baaadhi ya visiwa nchini viko hatarini kumezwa na bahari.
Mh Luhaga Mpina Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliyea nguo nyeusi akipata maelezo toka kwa mtaalam katika kiwanda cha Twiga cement alipokitembelea leo jijini tanga kuona namna ambavyo kiwanda hicho kinatekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akitolea ufafanuzi namna ambayo fukwe ya Pangani imeathirika na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO IJUMAA.

WAZIRI KITWANGA ATEMBEA MITAANI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA PEMBA, ATEMBELEA MSITU WA NGEZI NA KUGUNDUA HAKUNA WAKIMBIZI WOWOTE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na wauza nguo wa Soko Kuu la mjini Chake Chake, Pemba. Wananchi hao walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida bila wasiwasi wowote. Waziri Kitwanga pia alisikiliza maoni ya wananchi hao kuhusu uchaguzi mkuu na kuridhishwa na juhudi za kuimarisha ulinzi katika kisiwa hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa pili kulia) akitembea mitaani eneo la Chake Chake Pemba, Zanzibar kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu usalama wao katika kipindi cha uchaguzi kisiwani humo. Waziri Kitwanga ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdullah (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman (wapili kushoto aliyevaa kaunda suti) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ahmed Khalid Abdulla (kushoto, aliyevaa tai. Kitwanga aliridhishwa na juhudi za kuimarisha ulinzi katika kisiwa hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuuzunguka msitu wa Taifa wa Ngezi, uliopo Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba ambao baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar walisambaza taarifa za uongo kuwa kuna wakimbizi wamejificha katika msitu huo baada ya kukimbia vurugu kisiwani humo. Hata hivyo hakuna mkimbizi yeyote aliyekuwepo katika msitu huo na wananchi wapo katika makazi yao wakiendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nasri.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, mjini Chake Chake, Pemba, kuhusu masuala mbalimbali ya uimarishaji ulinzi katika kipindi cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2016. Kushoto meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdullah na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akimuuliza swali Mkazi wa Wawi, Chake Chake Pemba, bibi Zabibu Mohamedi, wakati Waziri huyo alipokuwa anatembea mitaani kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2016. Hata hivyo wananchi hao walimuahkikishia kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika siku hiyo ya uchaguzi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwahoji wafanyakazi wa Bandari Kuu ya Pemba kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2016. Wafanyakazi hao walimuhakikishia kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo na pia wananchi hao wapo salama na wanaendelea na shughuli zao zakujipatia kipato za kila siku.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiwauliza maswali wananchi wa mjini Chake Chake, Pemba kuhusu jinsi walivyojiandaa na uchaguzi wa Machi 20, 2016 na kutoa maoni yao kama kuna tatizo lolote. Hata hivyo wananchi hao walimuambia Waziri Kitwanga wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, hakuna vitisho vyovyote katika eneo lao. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

…………………………………………

Na Felix Mwagara wa MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amewataka wananchi wa Zanzibar waondoe hofu kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu visiwani humo. Akizungumza mara baada ya kufanya mazungumzo na wananchi hao wakati alipokuwa anatembelea mitaa mbalimbali ya Soko Kuu la mjini Chake Chake, Pemba aliwataka wananchi hao waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato kama kawaida na hakuna mtu atakayewabughudhi kwani ulinzi umeimarishwa, na waachane na uzushi wa kutokea vurugu unaoenezwa visiwani humo.

Waziri Kitwanga alianza matembezi hayo mitaani mara baada ya kufanya mazungumzo na Kamati ya Ulinzi na Usalama mjini Chake Chake ambapo walimuhakikishia kuwa, Pemba yote ni salama na ulinzi umeimarishwa na hakuna atakaye fanyiwa vurugu kwa mtu yeyote atakayefuata sheria.
Waziri Kitwanga aliwataka wananchi hao kuondoa hofu wanapowaona askari mbalimbali wakipita mitaani kwani wapo kwa ajili ya kuwalinda wananchi hao pamoja na mali zao katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

“Musiwaogope askari, na wala msiwe na wasiwasi, mnapowaona shangilieni kwani askari ndio msaada wako kwa ajili ya usalama wako endapo inapotokea vurugu ya aina yoyote, mtaenda kupiga kura salama na mtarudi salama, hakuna mtu wa kuwabughudhi, msitishwe na mtu yeyote,” alisema Waziri Kitwanga na kufafanua;“Leo nazunguka mitaa mbalimbali ya hapa Pemba, lengo ni kuchukua maoni yenu pamoja na kuwaondolea hofu wananchi na kuwahakikishia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kwa ajili ya kulinda usalama, hivyo jitokezeni kwa wingi siku ya uchaguzi mkapigie kura kiongozi mnaemtaka.”

Hata hivyo, Waziri Kitwanga alifanya ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba katika msitu wa Ngezi unaodaiwa kuwa kuna baadhi ya wakimbizi wamejificha katika msitu huo ili kuokoa maisha yao baada ya kudaiwa kuwa kutatokea na vurugu. Kitwanga akiongozana na Wakuu wa Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi Pemba, walienda katika msitu huo na kuukagua na hawakukutana na mtu hata mmoja aliyejificha msituni humo kama inavyodaiwa na kusambazwa habari na baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar.

“Ndugu waandishi wa habari, tumezunguka kwa pamoja kuungalia msitu huu, kuwatafuta hao wakimbizi, hatujamuona mtu yeyote, ukisikia propaganda ndio hii, watu hawaitakii mema Zanzibar na Tanzania kiujumla, mmeona kuwa habari hii ni ya uongo, hakuna mkimbizi yeyote katika msitu huu kama tulivyoshuhudia wote kwa ujumla,” alisema Kiwanga.

Aliongeza kuwa, baadhi ya wananchi ambao wana mipango yao binafsi wanawatia hofu wananchi kwa kutunga habari za uongo kuwa Zanzibar imechafuka, wakati habari hizo hazina uhalisia wowote.
Hata hivyo, wananchi wa Pemba walimuhakikishia Waziri Kitwanga wanafanya shughuli zao za kuwapatia kipato kama kawaida na pia siku ya uchaguzi wataenda kupiga kura kama kawaida kwani wanaamini amani itakuwepo kama ilivyokuwa sasa. 

Waziri Kitwanga alifanya ziara Zanzibar katika Kisiwa cha Unguja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, na baadae kumalizia ziara yake kwa kutembelea katika mikoa yote ya Pemba ikiwa ni hatua ya kuangalia hali ya usalama visiwani humo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu katika maeneo hayo.

UAMUZI WA RAIS MAGUFULI KUTOA ELIMU BURE UTACHOCHEA USAWA WA KIJINSIA NCHINI – UMMY MWALIMU

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ( Mb) akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhima ya uwezeshwaji wa wanawake na uhusiano wake na utekelezaji wa Agenda 2030. katika mchango wake Waziri anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake amesema Serikali inatambua umuhimu wa mwanamke katika utekelezaji wa ajenda mpya ya maendeleo endelevu ( Agenda 2030) na kwamba itaendelea kumwezesha.

Katika Taarifa hiyo, Mheshimiwa Waziri, alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua kuwa uwezeshaji wa wanawake na Usawa wa jinsia unachangia kwa kiasi kikubwa kufikiwa kwa wepesi kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ( Sustainable Development Goals). Kwa kutambua hilo Tanzania imejipanga kuhuisha Ajenda 2030 katika Sera, Sheria na Mipango ya nchi kwa kuhakikisha kunakuwa wa sheria zinazolenga kuleta Usawa wa Jinsia na uwezeshaji wa wanawake, ambapo pamoja na mambo mengine utekelezaji wa Mikakati, Sera na Sheria utaendelea kuzingatia haki ya kielimu kwa Wanawake na Wasichana.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.)wakati akitoa taarifa ya nchi katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake Duniani (CSW).

Mhe Ummy alieleza kuwa Adhma ya Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutoa Elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari itakuwa na matokeo makubwa ya kuongeza udahili wa wanafunzi katika Elimu ya msingi, Sekondari na Elimu ya juu.

Akaongeza kwamba uimarishwaji wa upatikananaji wa elimu kwa wanawake ni msingi mkubwa wa kuwezesha wanawake kiuchumi, kwakuwa elimu hutoa ujuzi, maarifa na hali ya kujiamini kwa wanawake kuendea fursa za kiuchumi.

Mheshimiwa Ummy, aliongelea pia umuhimu wa Afya kwa wanawake na Wasichana (ikiwa ni pamoja kupunguza vifo vya wajawazito na watoto) kama njia ya kumuwezesha mwanamke kushiriki kikamilifu katika uzalishaji mali.

Mkutano huo wa wiki mbili unafanyika NewYork, Marekani kuanzia tarehe 14-24 Machi 2016, ukihusisha wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubadilishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo Serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.
Mheshimiwa Ummy Mwalimu akiwa pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na Mhe Peter Serukamba (Mb.), mara baada ya kuwasilisha taarifa ya Tanzania kuhusu Masuala ya Maendeleo ya Wanawake.

TASAF yapatiwa Dola milioni 665 kunusuru kaya masikini

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akiongea na wadau wa maendeleo mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wake wa Kunusuru Kaya Masikini nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird (kushoto) mara baada ya kusaini makubaliano ya jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau hao ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akisaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo nchini ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.
Wadau wa Maendeleo wakimskiliza Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird wakati wa mkutano jijini Dar es salaam.

Zantel yatoa msaada wa kompyuta na huduma ya intaneti bure kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe.

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin (mwisho kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi wakikabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kutoka kampuni ya Zantel. Wanaopokea mwisho kulia ni msanii Aslay na Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yusuph Chambuso.
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa akikabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi akifuatiwa na mwanamuziki kutoka bendi ya Yamoto, Aslay.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni, Bi Leah Kihimbi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa wa hafla fupi ya makabidiano ya msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kutoka kampuni ya Zantel. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akifuatiwa na Meneja wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yusuph Chambuso. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia tukio hilo la Kampuni ya Zantel kukabidhi msaada wa kompyuta tatu na intaneti bure kwa mwaka mzima kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe

Kampuni ya simu ya  Zantel  leo imetoa msaada wa kompyuta 3 na huduma ya intaneti bure kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kituo cha Mkubwa na Wanawe kwa ajili ya kuwasaidia vijana walio katika kituo hicho kuweza kunufaika na kazi zao kupitia mfumo wa digitali utakaowawezesha kukuza na kusambaza kazi zao.

Kituo cha Mkubwana Wanaweni kituo cha kukuza sanaa, kilichoanzishwa mwaka 2011 katika wilaya ya  Temekekwa lengo la kufanya maonyesho ya sanaaa na kutoa fursa kwa vijana wanaoishi  kwenye mazingira magumu kuweza  kukuza na kuviendeleza vipaji vyao.

Kwa sasa kituo hicho kina idadi ya zaidi ya vijana 102 ambao wana vipaji mbalimbali kama kuigiza,kuimba na kucheza ngoma.


Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel,Bwana  Benoit Janin amekipongeza kituo cha Mkubwa na Wanawe kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuwasaidia vijana wengi kutimiza ndoto zao na hivyo kuweza kuendesha maisha yao.‘Sanaa ni ajira kama zilivyo ajira nyingine, na sisi kama Zantel tunaamini msaada huu utawawezesha vijana wengi zaidi kuweza kuboresha na kusambaza zaidi kazi zao za sanaa hivyo kuweza kujikimu kimaisha na kutoa  ajira kwa wenzao' alisema Benoit.

Akielezea zaidi kuhusu msaada huo, Benoit aliwataka wasanii walio katika kituo cha Mkubwa na Wanawe kutumia vizuri vifaa hivyo kuendeleza zaidi vipaji vyao.Pamoja na msaada huo, Zantel pia itaandaa utaratibu wa mafunzo ya kompyuta na digitali kwa vijana ili kuwawezesha kupata ufanisi  na ujuzi katika  kukuza na kuendeleza  vipaji vyao. 

‘Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na kituo cha Mkubwa na Wanawe katika utekelezaji wa sera ya taifa ya utamaduni inayosisitiza ukuzaji wa sanaa na hivyo kukuza na kuendeleza maslahi ya wasanii’ alisema Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Bi Leah Kihimbi ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.


Naye mwanzilishi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella alitoa shukrani kwa kampuni ya simu ya Zantel kwa kuwatambua uwepo wao na kuwaunga mkono akisema hii ni mara ya kwanza kwa kituo chake kupata msaada kutoka kwa wadau.

‘Kituo chetu kinaona fahari kupokea msaada huu ambao utasaidia vijana wetu na kuwapa fursa ya ya kugundua vipaji vilivyojificha  na kuviendeleza  kwenye tasnia hii ya sanaa pamoja na kujitangaza zaidi kazi zetu’ alisema Fella.


Tangu kuanzishwa kwake, Mkubwa na  Wanawe imefanikiwa kuibua wasanii mbalimbali kama vile Wanaume TMK na bendi ya Yamoto.‘Kama Mkubwa na Wanawe tumejikita katika kujenga na kuhakikisha vijana wanatimiza ndoto zao na pia kuwasaida wasishawishike au kujishuhulisha na shughuli haramu ambazo zinapotosha maadili kwenye jamii kama vile uvutaji au suuzaji wa madawa ya kulevya na wizi’ alimaliza Fella.


Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images