Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

Steve RnB Akijipa Shavu sehemu mbalimbali Ughaibuni

$
0
0
 Steve RnB ni mmoja wa wasanii ambae ametembea sana Europe mwaka huu. Mpaka sasa hivi ametembelea nchi sita :Germany ,Austria ,Belgium ,Holland, United Kingdom,na Turkey.
 
Thanks,
 Kvelli Management
 Twitter: @SteveRnBTz
 
 



KIPAJI CHA MPIRA WA MIGUU CHAONGEZA KIASI KIKUBWA CHA FEDHA KWA WAGHANA HATA KUINGIA NUSU FAINALI

$
0
0

                                                           
Mei 9, 2013, Dar es Salaam kupitia televisheni za ITV na Clouds TV jana usiku katika kipindi cha 8 cha Guinness Football Challenge (robo fainali ya 3) Ghana waliweza kuibuka vinara na kupata dau kubwa zaidi tangu mashindano haya yaanze na kufuzu kuingia nusu fainali. 

Jonathan Naab na Desmond Odaano kutoka Afika Magharibi waliweza kuhimili vishindo na vikwazo vyote hata kufikia hatua ya mwisho ya Ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia taslim dola za kimarekani 3,000 na kufanya kuwa na jumla ya dola 8,500 kutokana na dola 5,500 walizokua nazo awali.


Wawakilishi kutoka Ghana wataiwakilisha nchi yao katika nusu fainali pamoja na wawakilshi kutoka Kenya ambao nao wamefuzu kuingia nusu fainali Ephantus Nyambura na Samuel Papa, ambao pia walifanya vizuri ingawa hawakufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness.


Timu nne mpya zitaingia uwanjani katika robo fainali ya mwisho wiki ijayo nakuona kama wawakilishi wa mwisho kutoka Afrika Mashariki watatutoa kimasomaso na kufuzu kuingia nusu fainali


Robo fainali ya tatu ya Pan-African itarushwa kupitia televisheni za ITV na Clouds TV usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki


Hakikisha unaufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.

-www.facebook.com/guinnesstanzania


GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.


Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.


Wadau, Serikali inamuangaliaje Francis Cheka,inamchukulia poa ama..?!

$
0
0
Bondia Francis Cheka


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.



NI mtoto tu anayesubiri kuungua kwa kuugusa moto kwa ajili ya kugundua kwamba unaunguza ama vipi. Ila kwa watu wazima wanaojitambua, hata kwa macho tu, wataweza kung’amua kilichopo mbele yake, pembeni yake ni moto na unapougusa madhara yake ni kuungua.
                                    
Ila, inapotokea mtu mzima anashindwa kujua moto unaunguza ni ujinga, hivyo kila anayeweza kuwa kwenye mtazamo huo anastahili kuzomewa. Kinyume cha hapo siwezi kuvumilia.

Siwezi kuvumilia, hasa kila ninapoangalia kipaji cha mwanasumbwi, Francis Cheka anayetokea mkoani Morogoro kinaangaliwa ovyo ovyo tu. Kwa miaka zaidi ya mitatu sasa, Cheka ameweza kuwa juu na kupeleka kilio kwa kila bondia anayekutana naye ulingoni.



Kwa kuangalia hili tu, ni dhahiri kuwa Cheka ni bondia makini na anastahili kupewa ushirikiano kutoka kwa wadau wa ngumi. Kwa mfano, serikali pia inaweza walau kumjali bondia huyu kwa kuhakikisha kuwa anafanya safari kuelekea kwenye mapambano makubwa duniani.

Kwa bahati mbaya, serikali yetu imekuwa ikifanya mambo kiujanja ujanja tu. Hata Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo siku zote imekuwa ikifanya mambo ambayo si yenye kukuza michezo.

Angalia, kila kipaji katika Taifa hili kimeibuka kwa juhudi zake. Hakuna hata mmoja aliyetokea kwenye mikono salama. Ni tofauti na baadhi ya nchi zilizoendela duniani.

Kila siku mabondia wa Tanzania, wadau wao wamekuwa wakilia wimbo wa kukosa wadhamini wa uhakika. Licha ya kujaa kwa makampuni ya kila aina na taasisi za muhimu, lakini ni chache zinazojitokeza kudhamini mchezo wa masumbwi, japo kutoa Milioni moja au mbili.

Mapromota wa masumbwi ambao nao wanasumbuliwa na ukata, wanatumia muda mwingi kusumbukia fedha za kuandaa pambano, huku wakitarajia faida ya viingilio vya mashabiki.

Hakuna mipango wala ushirikiano hapa. Waswahili wana msemo wao, supu ya mbwa inanywewa ikiwa ya moto. Kutokana na hilo, Cheka akitumiwa vyema na wadau pamoja na serikali anaweza kufanya makubwa duniani katika sekta ya masumbwi.

Watu watauliza au kushangaa. Ndio, maana watakumbuka kuwa sio Cheka peke yake aliyewahi kutesa katika masumbwi hapa nchini. Ukiacha Said Kinyong’oli, pia alikuwapo Rashid Matumla, akitokea katika familia ya wacheza ngumi ambao hadi leo wanatamba.

Mwili wa Matumla ungeweza kutumiwa vyema, hakika angeweza kupanda ulingoni kushiriki mapambano makubwa duniani. Lakini hao wote waliwika kwa miaka michache na kupotea.

Naweza kusema sisi hatuna akili ya kuendeleza watu wenye vipaji kwa ajili ya maslahi ya Taifa. Tumebaki kuwa wapiga makofi na kushangalia ujuha wetu katika kila jambo hata kama halina tija.

Wakati huu, ni dhahiri kuwa kama Cheka hajajiweka sawa zaidi kwa juhudi zake, huenda baada ya miaka miwili au mitatu ijayo kutoweka. Hakika siwezi kuvumilia hata kidogo.
Ni wakati wetu sasa kukaa chini na kuangalia mwenendo wetu. Tumtangaze Cheka nje ya nchi pamoja na mabondia wetu wengine kwa ajili ya kupata mapambano makubwa na yenye soko.

Tutafate nafasi ya kujichomeka katika Mataifa makubwa, ili iwe njia nzuri ya kukuza na kuendeleza sekta ya masumbwi. Kwa sasa Cheka naweza kusema kuwa hana mpinzani Tanzania.

Atacheza na nani sasa? Kila anayeingia naye ulingoni anampiga kama mtoto wake wa kumzaa. Juzi, Thomas Mashali aliyejigamba sana, aliweza kutandikwa, huku Cheka akiwa anasumbuliwa na mkono.

Naamini huu ni wakati wa kuangalia mwenendo wetu kwa ajili ya kusonga mbele katika kona ya masumbwi. Ili aweze kutimiza malengo yake, inahitaji muda kidogo wa kujiandaa ili kuongeza uzito wake.

Huo ndio ukweli wa mambo. Kinyume cha hapo tuendelee na porojo zetu, mzaha wetu, huku vipaji vyetu vikizidi kutumbukia katika shimo la ufukara.

Tunaomba radhi kwa usumbufu, hasa kwa makala haya kukujia leo Alhamis badala ya Jumatatu kama ilivyokuwa kawaida yake.

habari ndiyo hiyo kutoka TBC1 "ukweli na uhakika"!

kutoka mahakamani leo:Shekhe ponda afungwa kifungo cha mwaka 1 nje na wengine 49 kuachiwa huru.

$
0
0

Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam,imemfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja katibu wa Jumuiya na Taasisi za KiislamTanzania Shekhe Ponda Issa Ponda (wa tatu pichani),huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru.

MAADHIMISHO YA SIKU YA FAMILIA DUNIANI

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

 

                                                            
                                                            
                    
                     

MAELEZO YA KATIBU MKUU KWA UMMA KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA TAREHE 15 MEI 2013


Siku ya Familia Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Mei na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.  Maadhimisho hayo yanatokana na tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa Na. 47/257 la tarehe 20 Septemba, 1993, linalohusu kuwa na siku maalum ya familia. Tanzania ikiwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa huungana na nchi nyingine kila mwaka kuadhimisha siku hii.  Hapa Tanzania mwaka huu maadhimisho haya yatafanyika katika Mikoa yote ili kuenzi familia kama kitovu cha maendeleo na muhimili wa Taifa.


Kila mwaka Maadhimisho ya Siku ya Familia yamekuwa yanabeba kauli mbiu mahususi kwa familia na jami. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema: “IMARISHA NA ENDELEZA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO WA FAMILIA NA MAKUNDI MBALIMBALI YA JAMII”. Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha, kuhimiza, kuelimisha familia na jamii kuendeleza mahusiano kati ya vizazi na vizazi , familia na rika mbalimbali ili kuleta mshikamano ndani ya jamii na taifa kwa ujumla. 

Lengo kuu la kujenga ushirikiano wa kijamii ni kuyaleta pamoja makundi yote katika jamii na hasa makundi ya watu wanyonge, katika mustakabali wa michakato ya maendeleo ya familia na taifa lao. Hii itawapatia sauti katika maamuzi yanayohusu sera za maendeleo, utamaduni, siasa na uchumi ili kuwezesha jamii kunufaika na fursa zinzotokana na mazingira yao. Aidha ushirikiano na mshikamano ni nguzo ya malezi bora, na husaidia katika kupeana au kubadilishana rasilimali ndani ya familia na hivyo  kupunguza gharama za maisha za kulea watoto, wazee wasiojiweza na wasio na wasio na ajira na kuweza kuwekeza na kuweka akiba ya baadaye.


Mabadiliko ya kijamii na kiuchumi duniani, ongezeko la idadi ya watu, uhamaji na uhamiaji, kuaji wa haraka wa miji na kuvunjika kwa familia tandaa kumeleta changamoto nyingi ambazo zimesababisha kuvunjika kwa umoja ndani ya familia nyingi.  Kuwepo kwa changamoto hizi kumechangia kuongezeka kwa gharama za kulea makundi tegemezi ndani ya familia kama wazee, watoto, wagojwa na wasiojiweza.  Hii imepunguza uwezo wa familia wa kufanya kazi kwa ufanisi, kuwekeza na kuweka akiba.  Kwa upande mwingine ukosefu wa ajira umeathiri vijana wengi kuwa tegemezi kwa wazazi na walezi wao.

  

Katika jamii zetu changamoto nyingi zinaweza kushughulikiwa vyema kuanzia ngazi ya familia kwa kuhamasishwa na viongozi wao. Aidha, serikali kupitia sera mbalimbali na programu zilizopo inashughulikia changamoto hizi.  Natoa wito kwa Taasisi zote kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku hii kwa kuhamasishana na kushirikiana maana kila mmoja wetu ni sehemu ya familia, na mchango wa kila mwanafamilia ni muhimu sana. Aidha nawasihi wazazi na walezi kuwa karibu na kautenga muda wa kuongea na watoto wao, ili kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili maana tusipofanya hivyo watoto wetu watatafuta majibu kwa njia zisizofaa na haya yatachangia kusambaratisha familia.


Ni matumaini yangu kwamba kupitia maadhimisho haya familia zitakumbushwa wajibu na mchango wao katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla . 


Kijakazi Rajabu Mtengwa

KATIBU MKUU

ccm kuzindua wa shina la cardiff

Miss Universe Tanzania atoa somo la madhara ya madawa ya kulevya Azania sekondari

$
0
0

Miss Universe Tanzania Winfrida Dominique akitoa somo la madhara ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari ya Azania jijini. Winfrida alitoa somo hilo kwa dakika 40 kwa kushirikiana na Dk Johaness Mafwiri wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na taasisi ya New Hope Tanzania Limited (NEHOTA) ambayo inajishughulisha na kazi ya utoaji ushari nasaha kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na mambo mengine.
=========  =======  =======
Na Mwandishi Wetu
Miss Universe Tanzania, Winfrida Dominique amewataka vijana nchini kutothubutu kutumia madawa ya kulevya kwani wao ndiyo tegemeo la taifa hili.
Winfrida alisema hayo wakati akitoa mafundisho kuhusiana na madhara ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa shule ya sekondari ya Azania jana.
Mrembo huyo alisema kuwa madhara ya madawa ya kulevya ni makubwa sana hapa nchini hasa kwa vijana na yeye kama mmoja wa vijana, atatumia taji lake kutoa elimu kuhusiana na madhara ya madawa hayo.
Alisema kuwa amejionea mwenyewe jinsi vijana wanavyoathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya na taifa kupoteza nguvu kazi muhimu pamoja na matatizo ya ajira nchini.
“Nitatumia taji langu kutoa elimi mbali mbali ili kuwarejesha baadhi ya vijana waliopotea kurejea katika njia iliyonyoofu na kufanya kazi nyingine hata kwa kujiajiri, nitaendelea kutoa elimu hii kwa wanafunzi wengi zaidi, ” alisema Winfrida.
Mrembo huyo alitoa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Dk Johaness Mafwiri  wa taasisi ya New Hope Tanzania Limited (NEHOTA) ambayo  inajishughulisha na kazi ya utoaji ushari nasaha kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na mambo mengine.
Mbali ya Winfrida, Dk Mafwiri naye alitoa mada iliyohusiana na madawa ya kulevya na ulevi wa kupindukia ambao ni hatari kwa vijana na kwa upande wa elimu pia.
“Madawa ya kulevya yapo ya aina nyingi, lakini maarufu ni Cocaine na  Heroine, lakini bhangi na ulivi kupindukia ni moja ya madawa ya kulevya na yanatofautiana kwa upande wa madhara yake, si vizuri kwa vijana na hata kwa jamii kiujumla,” alisema Mafwiri.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA DEMOCRATIC USA IKULU DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Democratic USA, kuanzia (Kulia) ni David Wilhem, Chris Bulinger, (kulia kwa Makamu) ni Michael Granger, na mwenyeji wa ujumbe huo, Dastan Mrutu, kutoka Business Council, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 9, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na David Wilhem (katikati) kutoka Democratic USA, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu kwa mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Mei 9, 2013. Kushoto ni mmoja kati ya walioongozana na ujumbe huo, Michael Granger.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na ujumbe kutoka Democratic USA, kuanzia (Kulia) kwa Makamu ni David Wilhem, Michael Granger, Chris Bulinger na mwenyeji wao, Dastan Mrutu, kutoka Business Council, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Mei 9,2013 kwa mazungumzo. Picha na OMR.

SERIKALI KUZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI MATUMIZI YA LISHE BORA NCHINI

$
0
0
 Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwa niaba ya Katibu mkuu Kiongozi kuhusu Hali ya Lishe nchini , mkakati wa serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata virutubisho muhimu kupitia vyakula na Kampeni ya uhamasishaji wa matumizi ya Lishe bora  nchini itakayozinduliwa tarehe 16  mwezi huu na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam yakiongozwa na kauli mbiu "Lishe bora ni Msingi wa Maendeleo ,Timiza wajibu wako".
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula la Lishe Tanzania Faith Magambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu madhara yanayosababishwa na ukosefu wa lishe kwa watoto na umuhimu wa maziwa ya mama katika kujenga  afya bora  ya mtoto. Kulia ni Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo. 
 Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo akipokea na kujibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dar es salaam. 
Waandishi wa Habari wakiwa Kazini wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Umoja wa Mataifa kupitia mpango wa UBRAF waendesha semina kwa watangazaji wa radio za kijamii za Afrika Mashariki.

$
0
0

Picha juu na chini ni Mshauri wa Radio Jamii na Mkufunzi wa UNESCO Dar es Salaam Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika program zinazohusu kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wakati wa warsha iliyofadhiliwa na mpango wa Unified Budget Result Accountability Frame Work (UBRAF) uliochini ya Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa Kongamano lililofadhiliwa na UBRAF lililohusisha Redio za Kijamii za Afrika Mashariki kutoka Kenya Community Media network (KCOMNET) Njuki Githethwa akiwasilisha ripoti ya maendeleo na ufanisi wa mtandao huo ambao unalenga kujenga fursa ya kitaifa ya kuratibu, kulinda na kusaidia sekta ya vyombo vya habari vya kijamii nchini Kenya wakati wa warsha ya siku mbili iliyoratibiwa na mpango wa UBRAF uliochini ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika hivi karibuni Terrat Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Picha juu na chini ni Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Dar es Salaam Bi. Stella Vuzo akizungumzia umuhimu wa kuwa na mikakati madhubuti ya kushirikishana baina ya Waandishi wa habari na Umoja wa mataifa na pia akafafanua mpango mkakati wa Umoja wa mataifa juu ya usalama wa waandishi wa habari pindi wawapo kazini.
Ambapo amewataka ku-share vipindi na habari mbalimbali na Radio ya Umoja wa Mataifa na kuwafanya wao pia kujulikana kimaifa zaidi.
Bw. Jimmy Okello wa COMNETU akitoa tathmini ya ripoti endelevu za Radio za Kijamii nchini Uganda.
Mwakilishi kutoka Mang’elete Community Radio ya nchini Kenya akizungumzia muelekeo na muafaka wa radio za kijamii na kiwango cha mafanikio kilichofikiwa hadi sasa.
Amos Ochieng wa KCOMNET kutoka Kenya akielezea jinsi watangazaji wa Radio za Kijamii za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanavyoweza Ku-share habari kupitia mtandao wa kijamii wa pamoja kwa wakati mmoja.
Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka tasnia ya habari waliohudhuria semina iliyohusisha Redio za Kijamii iliyofanyika Terrat wilayani Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa kupitia Mpango wa UBRAF.

Pichani juu na chini washiriki wa warsha hiyo iliyowakutanisha Watangazaji wa Radio za Kijamii kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania wakitoa maoni yao ya namna ya kuboresha uandaaji wa vipindi vyao vya Radio za Kijamii sambamba na vikwazo wanavyokumbana navyo katika kazi zao.

SHEIKH PONDA AACHIWA HURU! Afungwa kifungo cha nnje mwaka mmoja!

$
0
0
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kusikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja wa wafuasi wake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.


HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.

Mara baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.

Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.


Tumewashinda!


Furaha!
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda!

Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.
Barabara nazo zikavamiwa na wafuasi hao.


Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.

Waliopo kwenye majengo ya karibu wakatoka nnje kushuhudia!


Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea.

Duce yapokea msaada wa kopyuta 20 toka Vodacom Foundation

$
0
0
 .Mkuu wa shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Prof David Mfinanga, akitazama moja ya Kompyuta alizokabidhiwa na Vodacom Foundation kama msaada  katika harakati za kustawisha maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano shuleni hapo. Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Vodafone Foundation kutoka India, Laura Turkington, na Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule.
 Mkuu wa shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Prof David Mfinanga, akipokea msaada wa Kompyuta kutoka kwa Mkuu  wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule zilizotolewa shuleni hapo eneo la Changombe Dar es Salaam jana, Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Vodafone Foundation kutoka India, Laura Turkington.
 Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi na Hisabati, Elizabeth Mrema, akitumia moja ya Kompyuta zilizotolewa na Vodacom Foundation shuleni hapo kama msaada Dar es Salaam jana, kushoto wanaomtazama ni Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule akiwa na baadhi ya wanafunzi.  Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo, Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi na Hisabati, Anna Daniel, akitumia moja ya Kompyuta zilizotolewa kama msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo Dar es Salaam jana, kushoto wanaomtazama ni Maofisa wa Vodacom Foundation.  Jumla ya Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 zilitolewa shuleni hapo.

Mkuu wa Kitivo cha Elimu wa Shule ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo (kulia) akifafanua jambo mbele ya Maofisa mbalimbali wa Vodacom Foundation muda mfupi baada ya Kampuni ya Vodacom kupitia Mfuko wake wa Kusaidia Jamii kutoa msaada wa Kompyuta 20 zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 25 kwa leongo la kustawisha matumizi ya Tehama shuleni hapo eneo la Chang'ombe Dar es Salaam.

Taarifa kwa umma kuhusu ufafanuzi wa usalama wa soda

$
0
0


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyoundwa chini ya Sheria ya Chakula Dawa na Vipodozi Sura ya 219, ili kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi, na vifaa tiba kwa lengo la kulinda afya ya jamii dhidi ya madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizo.


Ili kutimiza wajibu huo, TFDA inasimamia pamoja na mambo mengine udhibiti wa uingizaji  wa vyakula kutoka nje ya nchi na utengenezaji wa vyakula ndani ya nchi kwa ajili ya kulinda afya za watumiaji. Katika udhibiti wa vyakula hivyo, michakato mbalimbali hufanywa ili kuwa na uhakika juu ya usalama wake kwa; kufanya tathmini na uchunguzi wa kimaabara, kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa usalama wa bidhaa kwenye soko na hatimaye kusajili majengo na vyakula baada ya kujiridhisha juu ya usalama wake.


Kutokana na mfumo wa udhibiti uliopo, Mamlaka imesajili bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyofungashwa ikiwa ni pamoja na vinywaji aina ya soda zinazozalishwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje.


Hivi karibuni kulitolewa taarifa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kueleza kuwa kinywaji cha soda ni sumu. Mamlaka ina mashaka juu ya taarifa iliyotolewa kwa sababu haidhani kama ilitolewa kwa kuzingatia misingi ya kisayansi. TFDA inapenda kuwatoa hofu watumiaji wa kinywaji hiki kuwa, soda ni bidhaa ya chakula ambayo inatumika kote duniani na huzalishwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama. Kwa upande wa TFDA, soda zote zilizosajiliwa zimepitia katika mchakato ambao unatoa uhakika juu ya usalama wake kwa lengo la kulinda afya ya binadamu.


Tunapenda kutoa rai kwa vyombo vya habari kufanya utafiti wa kina hususan katika masuala yanayohusu ushahidi wa kisayansi ili kuondoa uwezekano wa kutoa taarifa kwa umma ambazo zinaweza kujenga hofu na mashaka ambayo hayastahili.


Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana nasi kupitia;

Mkurugenzi Mkuu,

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)

Barabara ya Mandela, Mabibo External,

S.L.P 77150

Dar Es Salaam, Tanzania

Simu:              +255 22 2450512/2450751/2452108

Fax:                 +255 22 2450793

Barua pepe:    info@tfda.or.tz

Tovuti:            www.tfda.or.tz

BREAKING NEWS!! RUAHA KIMENUKA, RAIA WAPIGWA MABOMU!

$
0
0

Habari zilizopo hivi sasa kutoka Ruaha wilaya ya Kilosa mkoani Moro ni kwamba kuna mapambano yanaendelea hivi sasa kati ya raia na askari wa kutuliza ghasia ambao wanatawanya raia kwa mabomu ya machozi. 


Imeelezwa na ripota wetu kutoka Ruaha kuwa chanzo cha mapambano hayo ni mvutano ulioibuka kati ya Wanakijiji na Serikali ya kijiji cha Ruaha, baada ya wanakikiji kuutaka uongozi uachie ngazi na uongozi kugoma kuachia ngazi. Imeelezwa zaidi kuwa kufuatia hali hiyo, wanakijiji walivamia ofisi za serikali ya kijiji na kukiteka hali iliyowalazimu askari kuitwa ili kutawanya raia.


Hali haikuwa rahisi, kwani raia waligoma kutawanyika na askari wakalazimika kufyatua mabomu ya machozi ambayo yalipigwa mpaka yakaisha lakini raia wakawa bado wapo, askari walilazimika kufuata mengine na hali bado ni tete hadi muda huu.


HABARI HII KWA HISANI YA Global Publishers

patakuwa hapatoshi viwanja vya post jijini dar.!

$
0
0
 Kama ilivyo kawaida kila mwaka tukutane pale viwanja vya Posta Kijitonyama kumuenzi mkongwe wa muziki wa Reggae Duniani - Bob Marley (Robert Nesta Marley) Tarehe 18/5/2013 kuanzia saa kumi jioni mpaka saa sita usiku kiingilio ni Tshs.7,000/- tu. Tukio hili ni mara moja kwa mwaka usikose.

BOSS WA KONYAGI ALALAMIKIA VIWANDA VINAVYOTUMIA MAGAZETI YENYE UHUSIANO WA NCHI JIRANI KUCHAFUA BIDHAA ZA TDL

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL),  David Mgwassa (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, ambapo alilalamikia kitendo cha baadhi ya magazeti yenye uhusiano wa nchi jirani, yanayotumika kuchafua bidhaa za TDL. Kushoto ni Meneja Masoko wa TDL, Joseph Chibehe. Yafuatayo ni maelezo ya Bw. Mgwassa...

Tumeanza kuona magazeti yenye affiliation na nchi za jirani yakitumika ku misrepresent products za TDL. Articles ninazozungumzia zilichapishwa tarehe 2 may 2013 na tarehe 6 may 2013, kupotosha umma, na kupindisha ukweli. kwa sababu mawasiliano ya kisheria yanafanyika sitataja ni magazeti gani yanahusika, lakini nina uhakika yana uhusiano mkubwa wa kibiashara na nchi jirani.


Ushauri wangu ni kuwa magazeti ya Tanzania, yaepukane sana na vitu vinavyoonyesha kuwa kuna muelekeo wa kurepresent matakwa ya nchi tofauti na kupuuza matakwa ya kitanzania Kitendo cha kujaribu kuoanisha brand ya Konyagi na accidents za magari au piki piki , ni ya upotoshaji mkubwa wa jamii ya kitanzania, kwani hakuna bia, hakuna pombe za kienyeji au pombe kali. Huu ni uhuni na ujinga mtupu Sisi TDL hatuogopi ushindani, sio ushindani wa humu Tanzania, na nasema tutaendelea kuuza products zetu zinazozalishwa Tanzania, huko Uganda, Kenya south Sudan, Rwanda na Burundi, licha ya matatizo makubwa tunayopata.


Na tutaendelea kuwasiliana na mabalozi, wa nchi husika, EAC office na wizara zenye mamlaka katika kukuza soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki, kuhusu changamoto za kibiashara tunazozipata. Kama nilivyozungumza mwanzo sisi hatuzalishi Konyagi tuu, bali tunazalisha Zanzi cream, Knights, Viceroy brandy , siyo kwa sababu hatuwezi kuagiza, bali kwa  kutumia watanzania katika uzalishaji na kuwapa ajira. Msitufananishe sisi na watu wanaoleta makatoni ya pombe kutoka Ireland au Uingereza, sisi tuko tofauti na mahitaji ya nchi hii tunayajua.

Raisi wetu Dr Kikwete kila siku anasema issue hiyo hiyo, value added , value added, mbona masikio yenu mnafunga? Naomba niwaeleze ukienda South Africa leo utaona kila aina ya magari mapya, utaona Toyota, utaona Nissan utaona Mercedez benz , utaona Kia na kadhalika, lakini magari yote hayo yanaundwa South Afrika, huwezi kukuta gari imetengenezewa Singapore, nia ni kuhakikisha kuwa wenyeji wanapata kazi, na approach yetu  TDL ni same.


Sioni kati ya nyie mtu ambaye anamchukua mtoto wake kumpeleka Nairobi au Dubai, kumtafutia kazi, wote mnawaleta kwetu, hata leo wengine wananiomba kazi, kwa hiyo naomba sana mtu akikujaza akili au upumbavu, na wewe jaribu kuchanganya na akili nzuri za kwako
Ahsanteni sana.



Baadhi ya wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati Mgwassa akilalamikia jambo hilo

MHASIBU MKUU JAMBO LEO AFARIKI DUNIA

$
0
0
Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, marehemu Vick Mgoyo

MHASIBU Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited inayochapisha gazeti la Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania, Vicky Mgoyo (49), amefariki dunia.

Meneja Mkuu wa Jambo Concepts, Ramadhani Kibanike, alisema marehemu Vicky Mgoyo alifariki dunia leo asubuhi kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokimbimbizwa kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa usiku wa kuamkia leo.

Alisema kifo cha Vicky zaidi akijulikana kwa jina la Mama Mgoyo kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia yake bali pia kwa Kampuni ya Jambo Concepts kutokana na kwamba alikuwa ni mtu mwaminifu kazini, lakini pia uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzake.

"Tumepoteza mfanyakazi ambaye ni mchapa kazi na kipenzi cha wengi, tutamkumbuka kwa hilo. Naomba wafanyakazi tuungane na ndugu na jamaa katika kuomboleza msiba wa kipenzi chetu huku tukiamini kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

"Bado hatujapata taarifa rasmi za maziko, ila taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao zinaendelea kufanyika," alibainisha Kibanike.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Juma Pito alitoa mwito kwa wafanyakazi kuonesha mshikamano katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao.

Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Anicetus Mwesa, akizungumzia msiba huo alisema Mama Mgoyo ametwaliwa na Mungu ilhali akiwa bado anahitajika na familia pamoja na ofisi yake, hivyo ameacha pengo ambalo litachukua muda kuliziba.

"Mwenzetu ametangulia nasi tupo nyuma yake, zaidi tumwombee ili Mungu ampumzishe katika raha ya milele," alisema Mwesa.

Kwa upande wake Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda, alisema atamkumbuka Vicky kwa kuwa ni mwanamke shupavu ambaye alikuwa anazingatia maadili ya kazi yake ya uhasibu.

Pia alisema alikuwa ni mama mjane makini ambaye alihakikisha anasimamia watoto wake katika suala la kuwapa elimu bora, ambapo katika hilo alikuwa akifanya kila anachoweza kuhakikisha anasomesha nje ya nchi tena kwenye shule bora na makini.

Vicky Mgoyo aliyezaliwa Novemba 26, 1964, ameacha watoto watatu huku wawili kati yao ni wanaume.

Alilazwa katika Hospitali ya Kairuki wiki iliyopita ambako alipatiwa matibabu kwa muda wa siku nne na kuruhusiwa.Jumatatu aliripoti kazini na kuendelea na kazi hadi jana jioni, ambapo usiku alizidiwa na hatimaye leo asubuhi Mungu alimchukua. Mungu ailaze pema peponi roho ya Vicky Mgoyo.


Airtel yazindua huduma maalumu kwa wateja wake ijulikanayo kama Airtel Premium

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso akimzawadia bi Rose Maina mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam akifuatiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja bi Adriana Lyamba.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Adriana Lyamba akimzawadia bw. Joseph Mambo .mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam, akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso.
Mteja wa Airtel bw. Picket Robert Miranda (kushoto) akiongea na mkurugenzi wa huduma kwa wateja Adriana Lyamba (kulia) na Meneja wa huduma kwa wateja Hilda Nakajumo (katikati) katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Airtel Sunil Colaso (kushoto) na wafanyakazi wengine wa Airtel, Adriana Lyamba (Kulia) akifuatiwa na Meneja wa huduma kwa wateja Hilda Nakajumo wakiongea na mmoja wa wateja wa Airtel David Mukama(wa pili kushoto) katika uzinduzi wa huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Adriana Lyamba akimzawadia bw. Abdual Salum mmoja wa wateja katika uzinduzi wa huduma mpya ya wateja ijulikanayo kama Airtel Premier Services katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam, akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sunil Colaso.

ibada ya mazishi ya waumini wa kanisa katoliki waliofariki dunia kwenye tukio la mlipuko wa bomu huko jijini arusha

$
0
0
Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa wamebeba jeneza lenyenye mwili wa mmoja wa waliokufa katika tukio la kutupwa kwa bomu la mkonokatika kanisa la Olasiti Arusha may 5, 2013.
Mapadri wakiwa wamebeba mislaba yenye majina ya marehemu wawili kati ya watatu waliofariki kwenye tukio la bomu la kurushwa kwa mkono kwenye kanaisa la Olasiti jijini Arusha May 5, 2013, katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa hilo may 10,2013.
Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashmu Josephat Lebulu akinyunyuzia maji miili ya waumini wa kanisa hilo waliofariki katika tukio la kurushwa kwa bomu la mkono kwenye kanisa la Olasiti jijini Arusha may 10,2013.
Kiongozi wa kanisa Katoliki nchini, Mhashamu Polycarp kaldinari Pengo akiongoza ibada ya mazishi ya waumini wa kanisa hilo waliouwawa katika bomu lililotupwa kwenye kanisa la Olasiti Arusha May 5,2-13. Kuhoto ni Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images