Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 6 | 7 | (Page 8) | 9 | 10 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akikata Utepe kuonyesha Ufunguzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia Matangazo ya Dijitall huko Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Kituo kikuu cha Mtambo wa Kurushia Matangazo ya Dijitall kilichofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi huko Rahaleo Mkoa wa Mjini Unguja.ikiwa ni Shmra shamra za Kuadhimisha Sherehe za Kutimia Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akipata maelezo mafupi kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Agape Association LTD Dr Vernon Fernandes wakwanza kuli kuhusiana na Chanall za Dijitall zinavyofanya kazi,baada ya Rais kufungua Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo Rahaleo Mjini Zanzibar.wapili kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.

  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na Mainjinia wa Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Kurushia matangazo ya Dijitall hapo Rahaleo Mjini Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.

  =======  ======  ==========  ======
  Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 
     08/01/2013.


  SHIRIKA  la Utangazaji  Zanzibar ZBC limetakiwa kuhakikisha kwamba linafanyakazi kwa ufanisi mkubwa kulingana na mfumo uliopo hivi sasa.


  Alisema kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wameonakana wakifanya kazi kimazowea tu bila kufuata taratibu za kikazi.    


  Hayo yameelezwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt Ali Mohammed Shein   katika Uzinduzi wa Miundombinu ya Dijitali na Jengo la Studio ya Kisasa . Alisema kuwa kubadilika kwa watendaji kazi ni suala la lazima kutokana na mabadiliko makubwa  yalioko duniani .

  Dkt Shein alisema kuwa ZBC  wananchi wengi wanapiga kelele juu ya utendaji wa wafanyakazi wa ZBC kutokana na  vipindi vyao kutoridhisha na kukatika katika kwa matangazo yao zaidi wakati wa taarifa ya habari. Alisema kuwa Zanzibar inaheshima yakekatika masuala ya Utangazaji kwani Redio nyingi za Nje zinawatangazaji kutoka Zanzibar ambao ni mahiri katika masuala ya Utangazaji.

  Dkt Shein amesema kuwa hivi sasa hatoweza kuvumilia tena kutokana na utendajihuo ambao hauridhishi hata kidogo na hasa sasa tulivyoingia katika mfumo huu wa DIGITALI. “Sitaki kuiona Serikali ambayo nnayoiongoza mie iwe ‘tiro’(mwisho) alisema Dkt Shein.

  Alisema kuwa kuingia katika mfumo mpya wa dijitali ni kazi kubwa lazima watendaji wafanyekazi kwa mashirikiano na kuwe na uwiano baina yao ili kuweze kuwa na kiwango ambacho kitaweza kuwajengea sifa wafanyakazi hao.


  Alieleza kuwa madhumuni makubwa ya Mapinduzi ni kuweza kuwakomboa wanyonge na  kuwabadilisha maisha yao sitofurahishwa na kuona gharama zote zilizotumika  katika kuingia katika mfumo huo mpya wa Digitali kuweza kupotea bure lazima viongozi waweze kusimamia majukumu yao na  kuanzia hivi sasa lazima mambo yende.


  ‘’Hakuna aliekamilika lakini tujitahidi’’ alisema Dkt Shein .  Dkt Shein alimtaka Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk pamoja na Katibu wake kuisimamia ipasavyo Shirika hilo la ZBC na kuhakikishakuwa mambo yanakwenda vizuri.


  Akizungumzia  juu ya Studio ya Kurikodia Dkt Shein amesema kuwa  madhumuni ya kutengeneza Studio hiyo ni kwaajili ya Wasanii wa Zanzibar waweze kupata nafasi nzuri za kurekodia nyimbo zao na hapo hapo kuwa na pahala ambapo wataweza kurekodi michezo ya kuigiza napia kuonesha maigizo mbali mbali katika ukumbi huo.


  Nae Waziri wa Wizara ya Habari  Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema kuwa  miundombinu  mipya ya Digitali ni mkataba baina ya Serikali ya Zanzibar na Kampuni ya Ágape na imeagharimu jumla ya Shs billion 8  za Tanzania na kuweza kujengea vituo 6 vya kurushia matangazo vikiwamo vya Kizimkazi, Nungwi na Masingini.  Kwa upande wa Pemba ni Konde,Mizimiumbi  na Mkanjuni.


  Aidha alisema kuwa ifikapo tarehe 28 /2/ 2013 analogi itazimwa na kuanza mfumo mpya wa dijitali na kuwaeleza wananchi wasiwe na wasiwasi ya upataji wa vingamuzi ambavyo vitakuwa vyakisasa na madhubuti.


   Said  alisemakuwa vingamuzi hivyo vitapatikana kwa katika sehemu mbali mbali  za Wilaya zote kumi za Zanzibar na hakutakuwa na haja kwa watu kufuatia Mijini.  Alisema kuwa kila kingamuzi kimoja kinatarajiwa kuuzwa si zaidi ya shs za Tanzania 50,000 na malipo ya matangazo yatakuwa si zaidi ya shiling za Tanzania 8000 vikiwa na chanal 36-38.  0 0


  Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akifungua Skuli mpya ya ,Sekondari ya Mapinduzi Chaani ikiwa ni shamra shamra za kuadhimi miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.
  …………………………………………………….
  NA RAMADHANI ALI /MAELEZO
   Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache Duniani zinazoendelea kutoa Elimu bila malipo tokea kuasisiwa Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.
   Akizungumza katika ufunguzi wa Skuli mpya ya Sekondari ya Mapinduzi, Chaani katika maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Mwinyi amesema mafanikio hayo yanatokana na viongozi shupavu wa Mapinduzi na wale waliofuatia kuongoza Zanzibar.
   Amewapongeza viongozi na wananchi  wa Zanzibar kwa jumla kwa kuendeleza malengo  ya Mapinduzi ya 1964 ya kuimarisha maendeleo katika nyanja mbali mbali. Rais mstaafu amewahimiza wananchi kuendeleza Umoja kwani bila umoja na mshikamano hakuna maendeleo yatakayopatikana.
   Amewashukuru wahisani wanaosaidia   maendeleo ya Zanzibar hasa katika nyanja ya elimu na afya na amesema misaada yao itaendelea kuthaminiwa .  Amewataka wazee wa Chaani kuendelea kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha wanaitumia skuli hiyo katika kubadilisha uwezo wao wa kusoma kuwa bora zaidi.
   Akizungumza katika sherehe hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna amesema baada ya kupata msaada wa  skuli mpya 19 za sekondari na Benki ya Dunia na skuli mbili msaada wa BADEA, Wizara yake inatilia mkazo katika kuondosha tatizo la walimu wa sayansi linalokabili Skuli nyingi za Zanzibar.
   Amesema  Nigeria imewapatia msaada wa walimu 13 wa sayansi na tayari wamefanya mazungumzo na nchi ya Marekani, Uingereza, Ghana, India, Palestina, Misri na Oman na wote wameonyesha azma ya kusaidia kupunguza tatizo hilo.


   Ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kwa kuliona tatizo la walimu wa sayansi, kimeanzisha Skuli ya Sekondari ya sayansi na Chuo cha Ufundi Karume kimeimarisha somo la hesabu na ameeleza matarajio yake kwamba baada ya miaka mitatu tatizo hilo litapungua.
   Waziri Shamhuna ameahidi Wizara yake itawaajiri wahitimu wote wa digrii  ya sayansi na kuwapa mafunzo ya ziada walimu wa sayansi ambao wameajiriwa ili kukabiliana na changamoto hiyo. Skuli ya Sekondari ya Mapinduzi, Chaani imegharimu shilingi bilioni 1.32 na imejengwa na kampuni  ya Chaina Railway Jian Chang Engineering Co. LTD ya China.

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa kabla hajahutubia Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo ya Meneja wa TANESCO wa Nzega akielezea mikakati ya kuwapatia wakazi wa hapo nishati hiyo Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
  Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Jakaya Kikwete mkoani Tabora leo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Uyui toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Lucy Mayenga wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Tabora Mjini toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe  Suleiman Kumchaya  wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelzo ya ujenzi wa barabara ya Tabora-Ndono kabla hajazindua rasmi i ujenzi wa  barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi  ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya  siku nne ya mkoa wa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.(PICHA NA IKULU)

  0 0

   Wakiwa katika picha ya pamoja meneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(katikati) na washiriki wa Guinness Football Challenge baada ya kupokea hati zao za kusafiria

  Meneja wa kinywaji cha Guinness kutoka kampuni ya bia ya Serengeti akikabidhi hati ya kusafiria kwa Lukwesa Kanakamfumu, mmoja wa washiriki wa Guinness Football Challenge   Emmanuel Temu mmoja ya washiriki waliofuzu kuingia kwenye mashindano ya Guiness Football Challenge akipokea hati ya kusafiria kutoka kwa Meneja wa kinywaji cha Guiness Davis Kambi
   Mratibu wa safari Bi. Caroline akitoa maelekezo na taratibu za safari kwa washiriki waliofuzu kuingia katika mashindano ya Guinness Football Challenge wanaotarajiwa kusafiri karibuni.
  Washiriki waliofuzu kuingia katika shindano la Guinness Football Challange wakisikiliza kwa makini maelekezo na taratibu za safari kutoka kwa mratibu wa safari na meneja wa kinywaji cha Guinness

  0 0

     HAPPY NEW YEAR WAREMBOZ!!
  MWAKA MPYA NA MAMBO MAPYA. WALE MABINGWA WA  VIPODOZI VYA UKWELI WAMEKUJA NA MAMBO MAPYAZ KWA MWAKA HUU!! UKIAMUA KUFUBAA UZEMBE WAKO MWENYEWE TU,SASA  WAMEKUSHUSHIA VITU VYA UKWEE KWA AJILI YA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO KUANZIA SABUNI,CLEANSER,VIBRATING CLEANSING MACHINE,TONER,CREAM,SUN-BLOCK LOTION ETC. VYOTE HIVI VITAKUACHIA MNG'ARO WA MAANA HUKU NGOZI IKIWEKWA KATIKA HALI YA NZURI NA YA KUVUTIAAA!! KWA MAWASILIANO ZAIDI ANGALIA TANGAZO HAPO JUU.  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Aggrey Mwanri akikagua mradi wa maabara katika kituo cha afya cha Matai katika Wilaya mpya ya Kalambo leo. Naibu Waziri huyo amepiga marufuku miradi yote ya serikali hususani inayohusisha mbao kupigwa rangi na badala yake ipakwe vanish, hiyo ni kutokana na baadhi ya wakandarasi kutumia staili hiyo kuiibia Serikali kwa kuweka mbao za bei nafuu na kuzipiga rangi. Mhe. Mwanri yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku saba ambapo ataembelea halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa na kukagua miradi mbalimbali iliyopo chini ya Halmashauri hizo.

  Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) akikagua ujenzi wa banio la mradi wa umwagiliji katika kijiji cha Katuka katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Mhe Mwanri aligoma kuweka jiwe la msingi katika mradi huu kutokana na mkandarasi kujenga mradi huo chini ya kiwango kinyume na mchoro halisi wa mradi huo. Aliagiza mapungufu yarekebishwe ndipo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a aweke jiwe hilo kwa niaba yake.
  Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Mussa Chang'a akimkaribisha Mhe. Mwanri azungumze na wananchi wa Wilaya ya Kalambo katika ziara yake ambayo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kutumia fursa ya miundombinu inayoendelea kujengwa Mkoani Rukwa pamoja na ujio wa Halmashauri yao mpya katika kuwekeza na kujiendeleza kiuchumi.

  Kutoka kushoto ni Mama Mwanri mke wa Naibu Waziri, Mhe. Agrey Mwanri Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Moshi Chang'a Mkuu wa Wilaya ya Kalmabo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Godfrey Schona wakiwa katika picha ya pamoja pembezoni mwa fukwe za Ziwa Tanganyika katika Hoteli ya Liemba Beach Resort walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Rukwa.

  Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga wa kituo cha afya Matai mapema hii leo. Katika miradi miwili aliyotembelea Mhe. Mwanri aligoma kuweka mawe ya msingi hadi hapo marekebisho aliyoagiza yatakapofanyiwa kazi ndipo mawe hayo yawekwe kwa niaba yake. 

  Mama Mwanri akiwasalimu wananchi wa Matai katika Wilaya ya Kalmbo.

  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Kipeta kabla ya Mhe. Mwanri kuzungumza nao kwenye ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo Mkoani Rukwa.

  Naibu Waziri wa TAMISEMI Ndugu Agrey Mwanri akipanda kwa tahadhari kubwa katika daraja la Mto Momba linalounganisha wananchi wa Kilyamatundu Mkoani Rukwa na wale wa Kamsamba Mkaoni Mbeya. Daraja hili lililojengwa kwa kamba limekuwa halikidhi haja ya wananchi hao jambo wanaloomba Serikali kuwajengea daraja litakalowawezesha kuvuka na kuvusha mazao yao kirahisi. 
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com)

  0 0  Mussa Yusuf
  Kitale Komediani kutoka Swahiliwood.
  MWIGIZAJI wa filamu na Komedi Mussa Yusuf ‘Kitale’ amaewashukia wasanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya Bongo fleva kwa kusema ni wanafiki hawana urafiki wa ukweli kati yao,Msanii huyo alisema hayo kufuatia kuzorota kwa arobaini ya rafiki yake kipenzi marehemu Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’ kuhudhuriwa na wasanii wachache na kuchangiwa na watu watano tu.
  Hussein Mkiety
  Marehemu Sharomilionea enzi za uhai wake.
  “Nimejifunza mengi kutoka kwa watu na nimewajua rafiki wa kweli lakini wengi ni wanafiki walikuwa wanajifanya Sharo rafiki yao kumbe hakuna lolote, kwa mfano tulipanga shughuli ya Arobaini ifanywe na sisi wenye siyo Bi. Mkubwa lakini waliochanga ni watu watano tu, kuna ushikaji kweli hapa’? anasema Kitale.
  Kitale anasema kuwa Sharo alikuwa na marafiki wengi ambao walikuwa hawakauki kwake lakini katika msiba hawakudhuria akiongelea kuhusu Bonge Movie alisema anamshukru sana Mtunis ambaye alijitoa sana katika msiba toka mwanzo hadi mwisho na Kitale anaomba Mtunis awe kaka yake wa karibu akiamini kuwa ni rafiki wa kweli, Kitale katika kumaliza machungu yake ametunga wimbo maalum kwa Sharo ambao utawachana Bongo Movie na Bongo Fleva.Kwa habari mbalimbali za wasanii wa filamu na tasni hiyo kwa ujumla ingia http://filamucentral.co.tz

  0 0


  Meneja mbunifu wa ofa za Tigo,Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Serena,kuhusiana na uzinduzi wa huduma yao mpya iitwayo Tigo Time,kushoto ni kwake ni Mwakilishi wa kampuni ya Frontline Portel Novelli Elias Bandeke
  Meneja wa Ofa za Tigo,Suleiman Bushagama akitoa ufafanuzi zaidi mbele ya Wanahabari kuhusiana na kampuni hiyo kutambulisha huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Tigo Time, ambayo inatoa punguzo kubwa sana la gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7 ikitegemeana na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa.

  0 0


  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein wamwanzo kulia akikata utepe pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Africa (AFDP)Tonia Kandiero katika ufunguzi wa Barabara ya  Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akikunjuwa kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya  Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein katikati akitembea kwa Miguu katika Barabara ya Mfenesini Bumbwini baada ya kuifungua rasmi,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akifafanua jambo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi pamoja na Watendaji wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano katika Ufunguzi waBarabara ya Mfenesini Bumbwini iliojengwa na Kampuni ya Mecco,ikiwa ni katika shamra shamra za  kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.  PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.
  ======  ======= ====== =======

  Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameuagiza uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuziwekea Mipaka maalum barabara zinazojengwa Zanzibar ili Wananchi waepuke kujenga pembezoni mwa barabara hizo.

  Hayo ameyasema jana huko Bumbwini-Mfenisini wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ikiwani ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Dkt. Shein amesema kwa kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kuepukana kuwalipa fidia Wananchi ambao wanatabia za kujenga katika maeneo ya barabara kwa kutarajia malipo pale nyumba zao zitakapobomolewa kufanya utanuzi wa barabara hizo.

   “Mnawachia watu wanajenga pembezoni mwa bara bara wakati mnawaona, mtu anaaza msingi, anainua tofali, anaezeka ,na anapiga palasta na nyinyi mnashuhudia,lazima iwekwe mipaka ya kuonesha eneo hili halipaswi kujengwa na atakae jenga avunjiwe .”alifahamisha Dkt.Sheini.

  Alisisitiza kuwa babara ina mipaka yake maalum na kwamba mtu atakayebainika kujenga nyumba kwenye mipaka hiyo lazima ivunjwe kwani mtu huyo atakuwa anakwenada kinyume na taratibu za bara bara.

  Dkt. Shein alitoa mfano wa barabara zilizojengwa nyumba pembezoni ambazo zinatarajiwa kutanuliwa siku za karibuni kuwa ni bara bara ya Magomeni-Kwerekwe na barabara ya Bububu kuelekea Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Alisema bara bara hizo ziliwekewa maeneo yake kwa ajili ya utanuzi siku za usoni lakini hakukuwa na mkakati wowote wa kulinda mipaka ya barabara hizo jambo ambalo liliwapelekea wananchi kupuuza sheria kwa kujenga nyumba.


  Aidha Dkt. Shein aliwataka watendaji wa Wizara hiyo kuzitunza vyema Bara bara hizo alizozizindua pamoja na Madaraja manne ikiwa ni pamoja na kupanda miti pembezoni na kuepusha kuchomwa moto kwa kutumia matairi ili zisipoteze kiwango chake.

  Nae Mwakilishi mkazi kutoka AFDB Bank Bi Toniya Kandiyero alisema kuwa Bank yao ipo mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya Zanzibar katika miradi mbalimbali ambapo kwa upande wa Barabara imesaidia takribani Kilomita 83 katika maeneo ya Unguja na Pemba.

  Bi Toniya alisema kwa sasa benki yake imejipanga kusaidia maeneo mengine mapya kama vile mazingira ya bahari na raslimali zake pamoja na shughuli zinazo fanywa baharini.

  Bara bara ya Bumwini-Mfenisini imejengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya kizalendo ya MECCO ambayo inaurefu urefu wa kilomita 13.2 ikiwa ni msada wa fedha kutoka bank ya Afrika  AFDB.

  Mwisho

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 9/1/2013

  0 0

  Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kutetea ubingwa Afrika mashariki na kati kati ya bondia Mtanzania Thomas Mashali na Bernad Mackoliech wa Kenya Jumamosi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese.
  Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa pambano hilo Aisha Mbegu alisema wameamua kumualika kamanda Kenyela ili kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kutoa Elimu ya Ulinzi shirikishi na kwa kutambua mchango wa jeshi la polisi kudumisha amani katika michezo.
  “ Jeshi la polisi ni wadau wetu wakubwa katika michezo hasa ngumi na mchango wao umekuwa ukionekana kwani sasa hakuna vurugu zinazojitokeza katika mapambano yeyote ya ngumi yanayofanyika tofauti na Miaka ya Nyuma ambapo Ngumi ilikuwa Watoto hawawezi kwenda kuangalia,”alisema Aisha.
  Aisha alisema katika pambano la awali ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Friend corner hakukuwa na vurugu na idadi ya watoto na wanawake kuangalia ngumi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na nhivyo kutoa hamasa kwa wazazi na watoto kupenda mchezo huo.
  Mbali na Kenyela Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan na Mbunge wa ubungo John Mnyika wamealikwa ili kushuhudia vipaji vya vijana wa kinondoni katika Ngumi.
  Bondia Mackoliech anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari leo (Alhamisi) katika Uwanja wa Karume na Ijumaa wanatarajiwa kupima Uzito saa Nne asubuhi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese .

  0 0


  WAWAKILISHI wawili wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani  wataendesha semina kwa wadau wa michezo  hapa nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.
  Wawakilishi hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch na kipa aliyestaafu  ambaye kwa sasa ni mtangazaji , Kasey Keller .
  Wakiwa nchini, wachezaji hao wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na shule za msingi katika siku na muda ambao  utangazwa hapo baadaye. Z
  iara hiyo ni moja ya kukuza ushirikiano baina ya Seattle Sounders na  wadau wa michezo nchini na ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho Ngassa kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester United.
  Kwa kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA),  wawakilsihi wa timu hiyo pia watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha  ikiwa pamoja na World Vision, taasisu ya PATH  na Chuo kijulikanacho kwa jina la Washington State University's Paul G. Allen School for Global Animal.
   "Ziara hii itadumisha na kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “ alisema Mmiliki wa timu hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March watakuwa mabalozi wakubwa wa timu yao katika ziara hiyo.

  Alisema kuwa wajumbe hao pia watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro Crater na jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani iliingia katika ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo la kushughulika na masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.

  0 0


  0 0

   Mkuuwachuo cha VETA kipawa, Jijini Dar es Salaam,  Eng. Lucius Luteganya, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ulipaji ada kwa wanafunzi wa chuo hicho kupitia huduma ya M – Pesa. Kufuatia ushirikiano kati ya chuo hich ona Vodacom Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa ukuzaji biashara – M - PESA Jackson Kiswaga.
   Meneja mawasiliano wa Vodacom Tanzania RukiaMtingwa, akimuelezea jamboMkuu wa Chuo cha Veta Kipawa,  Eng. Lucius Lutenganya wakati wa uzinduzi wa ulipaji ada kupitia huduma ya M – pesa kwa wanafunzi wa chuo hicho. Katikati ni Mkuu wa Ukuzaji Biashara – M -  PESA, Jackson Kiswaga.


  0 0  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata Utepe kuashiria kufungua Skuli yenye madarasa manne katika Kijiji cha Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini "A",ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   

  ======  =====  =====  ======
  Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar   .

  Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad amewataka Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu Tende kujenga Mashirikiano na Walimu ili  kuweza kuwapatia  haki na fursa sawa wanafunzi wa kike na wakiume Skulini hapo.    

  Hayo ameyasema leo huko Skuli ya Msingi Mbuyu Tende Wilaya Kaskazini “A” Unguja wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Maalim Seif  amewataka Wazazi wasikubali kuwaozesha watoto wa kike waume mapema kwani hali hiyo ndiyo inayochangia ukosefu wa Walimu wa kike wazawa katika Vijiji  vingi.

  Aidha alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuwapatia wananchi wake haki ya elimu bila ya malipo ili kuondosha adui ujinga na kuwaletea maendeleo.

   “Elimu ni msingi wa maisha kwa vijana na ndio inayoleta maendeleo na mwangaza hasa wakati wa sasa na ujinga ni kiza katika maisha ya leo,”alisisitiza Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

  Alisema kuwa wanafunzi wakipata msingi mzuri wa elimu wataweza kupambana na mazingira ya sasa ya sayansi na teknolojia kwa kwa ufanisi mkubwa. “Tusitazamie vijana kupata maisha mazuri bila ya elimu hasa katika zama hizo za sayansi na tecnología kwani elimu ndio kila kitu’’alisema Makamo wa Kwanza .

  Maalim Seif aliitaka Idara ya Mitaala kuandaa mbinu bora  za ufundishaji wa mafunzo ya amali ili wanafunzi wakimaliza masomo yao waweze kujiajiri wenyewe na kuweza kuondosha mzigo kwa Serikali.

  Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna alisisitiza wananchi wa kijiji hicho kuchukua juhudi ya kuwasimamia  watoto wao hasa wa kike kupata elimu kwani wanauwezo wa  kufanya vizuri zaidi katika masomo.

  Aidha katika uzinduzi huo zaidi ya shilingi milioni 11 zilichangwa kwa ajili ya maendeleo ya skuli hiyo ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais alichangia milioni tano na Waziri Shamhuna milioni tatu.

  Ujenzi wa Skuli ya Mbuyu Tende umegharimu jumla ya shiling Milioni 44 kwa ajili ya kujengea jengo lenye madarasa manne pamoja na kununua madawati kwa Skuli hiyo.                          
      
  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR  09/01/2012

  0 0

  Ajali nyingi za boda  boda zimekuwa zikiongezeka kila kukicha na kupoteza maisha ya watu kila siku,kutokana na uzembe mkubwa walionao baadhi ya madereva,baadhi yao hawana umakini wala uzoevu wa sheria za barabarani,Hivyo Madereva wa boda boda ni vyema wakazijua na kujifunza sheria za usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali,ambazo zimekuwa zikitokea kila wakati.Pichani ni mkazi wa mkazi wa Hai, Moshi Kilimanjaro, akiwa amebeba abiria  na mizigo yaka kama uonavyo pichani mapema leo.

  0 0  0 0  0 0  Eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge Basi la abiria la 'Bunda express" lenye
   namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea jijini Mwanza 
  muda wa saa mbili asubuhi hii limepata ajali mbaya kwenye eneo hilo.

  Mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa 
  na hofu kubwa imetanda eneo la tukio kuhofia usalama wa hali za abiria waliomo ndani ya basi husika  
  kwani basi limepinduka tairi zikielekea juu, limetumbukia kwenye majaruba ya mpunga, 
   limepondeka vibaya upande mmoja, na tayari katika muda huu napita eneo la tukio 
   miili ya watu wawili imeonekana ikizagaa nje ya basi kandokando ya barabara
   na mvua kubwa inaendelea kunyesha.  Hali ya uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hili ili wapate kujisitiri.
  Chanzo cha ajali kinatajwa kuwa ni mwendo kasi wa basi hilo.
  Watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, mvua ikiwanyeshea wakihofia usalama wao na mali zao. 
  Mpaka tunaenda mitamboni idadi ya watu waliopoteza maisha ni wawili na 36 majeruhi, Watu 24 waliopata majeraha makubwa wamepelekwa hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza Na majeruhi 12 wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Magu. 
  Hakuna pa kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa toka ndani ya basi hilo zaidi ya kujisitiri kwa kanga, vitenge na mashuka waliyoambulia toka kwenye baadhi ya mabegi yao.
  Baadhi ya nyumba zilizo karibu na eneo la ajali nazo zimeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili wilayani Magu.

  Hali ya baadhi ya barabara za ndani zinazounganisha vijiji wilayani Magu zimefunikwa na maji.
  Barabara hali ya hewa na mazingira.Picha zote kwa hisani ya Gsengo Blog.


  0 0   Marehemu Regia Mtema enzi za uhai wake.

  Siku ya Jumatatu; tarehe 14 January 2013 ni siku ambayo Regia Mtema Foundation imeitenga maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya Regia Mtema. Katika siku hii maalumu wote mnakaribishwa Peacock Hotel ambako kutakuwa na maada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia Regia. Katika siku hii maalumu wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

  Hafla hii maalumu itaanza saa 9.00 Alasiri na kumalizika 2.00 usiku na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku. Ratiba kamili itahusisha matukio yafuatayo:

  1.      Historia ya Regia itakayowasilishwa na Mh. David Kafulila
  2.      Mada juu ya Rushwa itakayowakilishwa na Takukuru
  3.      Ulemavu Siyo Kutoweza itakayowasilishwa na Bi Shida Salum - Mwenyekiti CHAWATA
  4.      Nafasi ya Kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia - Mh. January Makamba
  5.      Majadiliano
  6.      Documentary za Regia Mtema
  7.      Remarks kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe; Mh. John Mnyika na Hussein Bashe na Mzee Mtema
  8.      Chakula cha jioni
  9.      Networking

  Wasimamizi wa hafla hii watakuwa: Pascal Mayalla na Lara Williams

  Thibitisha kuhudhuria kwako kwako kupitia number: 0713 694 820

  RMF inawaomba Wanahabari wote wasaidie kusambaza mwaliko huu.

  Wasalaam

  0 0


  Rais wa PST Emanuel Mlundwa katikati akiwa na mabondia Deo Njiku kushoto na Omary Ramadhani  Dar es salaam jana baada ya kusaini mkataba wa kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese.
  Mabondia Omary Ramadhani kushoto na Deo Njiku wakitunishiana misuri baada ya kusaini mkatabakupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese .

  Rais wa PST Emanuel Mlundwa katikati akiwa na mabondia Deo Njiku kushoto na Omary Ramadhani baada ya kusaini mkataba wa kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

older | 1 | .... | 6 | 7 | (Page 8) | 9 | 10 | .... | 1896 | newer