Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA KINYEREZI II JIJINI DAR.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida , Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akianza ukaguzi katika Mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni akitoa maelekezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mitambo ya kufua umeme kwa kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa kinyerezi hawapo pichani kabla ya kuzindua rasmi Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba akifafanua jinsi ujenzi wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi II kitakavyokuwa mara baada ya kukamilika  mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM Ramadhani Madabida kabla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda , Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi  wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili kwenye ofisi za kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia huko Kinyerezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU.

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA LAKANUSHA KUPELEKA WANAJESHI VISIWANI ZANZIBAR.

$
0
0
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016

Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu. Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa hizo zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.



JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.

RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA KINYEREZI II JIJINI DAR.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda , Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi  wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

KAMBI YA FFU-UGHAIBUNI YANUSURIKA KUTEKETEA NA MOTO

$
0
0

Zimamoto wameiokoa !
Moto ambao hakuleta madhara makubwa!
Habari ambazo zilikuwa zimefichwa lakini ! tumezinyaka
Kuwa jengo linalotumiwa kufanyia mazoezi na bendi maarufu ya muziki wa dandi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni limeshika moto ghafla na kuokolewa na kikosi cha zimamoto huko ujerumani.

Wadakuzi wa mambo walimtafuta mkuu wa bendi hiyo bila mafanikio
kamanda ras makunja kazima simu. tukampata mmoja wa wanamuziki
wa bendi hiyo ambaye alisema kweli kambi ilishika moto lakini moto huo
haUkufika katika ukumbi wa mazoezi,kwani ukumbi wa mazoezi upo chini
under ground ambako si rahisi kufika.
 
jengo hilo pia ni kituo cha vijana
na ofisi za tasisi mbali mbali zinazoshughulika na mambo ya utamaduni.
chanzo cha moto huo mpaka sasa hakijajulikana, lakini inaonyesha ulianzia katika papipa ya taka yaliyowekwa karibu na mlango.

 

UBAO WA VIJUSO VYA MAGAZETI YETU YA LEO ALHAMISI MACHI 17

TANZANIA RED CARPET YAFANA SEATTLE, WASHINGTON STATE

$
0
0
Wavaaji nguo za mitindo wakipata picha ya pamoja na mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Mama mitindo Asya Idarous Khamsini (kati) akiwa katika picha ya pamoja na mashabiki wake wa mitindo kwenye usiku wa Tanzania Red Carpet uliofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 mjini Seattle jimbo la Washington na kuhudhuriwa na Watanzania wanaoishi jimbo hilo na marafiki zao.
Mama mitindo Asya Idarous Khamsini akipata ukodak moment.

TUSHIRIKIANE KUTOKOMEZA UKEKETAJI KWA WATOTO WA KIKE-UMMY MWALIMU

$
0
0
 Mhe. Waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumzia uzefu wa Tanzania katika kukabiliana na tatizo la  ukeketaji akiwa na wazungumzaji wengine katika Meza Kuu, kutoka kushoto ni Mke wa  Rais wa Burkina Faso Bi. Sika Bella Kabore,  Bw. Benoit Kalasi (UNFPA), Bi.Emma Bonino Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Italia.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mhe. Peter Serukamba akifuatilia majadiliano kuhusu tatizo la  ukeketaji  na  adhari zake wa afya na maendeleo ya mtoto wa kike na mwanamke.
 Wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi nao wakifuatilia majadiliano  yaliyovutia washiriki wengi kuhusu madhara  yatokanayo  na ukeketaji na namna gani  jamii inatakiwa kushirikiana kutokoza tatizo hilo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano na majadiliano  kuhusu utokomezaji wa vitendo vya ukeketaji na uhusiano wake na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mkutano huu  uliandaliwa kwa pamoja na Wakilishi za  Kudumu za Tanzania, Burkina Faso, Italy, Iran, UNFPA na UNCEF.
 
 Mhe Waziri Ummy  Mwalimu akibadilishana mawazo na washiriki wa majadiliano kuhusu ukeketaji.
 Waziri  Mwalimu akibadilishana  mawazo na Waziri  mwenzie Sicily Kariuki kutoka  Kenya

Na Mwandishi Maalum, New York
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ( Mb)  amesisitiza   kuwa ni  kwa ushirikiano baina ya Serikali  na  jamii ndipo tatizo la ukeketaji  kwa watoto wa kike na wanawake litakapoweza kutokomezwa.

Akaongeza kwamba, serikali  inaweza kutunga sheria nyingi  za kukabiliana na tatizo hilo  lakini kama jamii yenyewe  kuanzia ngazi  ya familia isipotoa ushuriano wa dhani itachukua muda mrefu kwa tatizo hilo kutokomezwa. Alikuwa akizungumza wakati wa majadiliano ya mkutano wa  kuhusu  utokomezwaji  vitendo vya ukeketaji kama sehemu  muhimu ya utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030.

Waziri Ummy Mwalimu alikuwa mmoja wa  wazungumzaji wakuu  katika  mkutano  huo  uliowahusisha  Mke wa Rais wa  Burkina Faso, Bibi. Sika Bella Kabore, Mawaziri na  Asasi za Kiraia na uliandaliwa kwa pamoja  na Wakilishi za kudumu za Tanzania,  Italy, Iran, Burkina Faso,UNFPA na UNICEF, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake.

Na kwa sababu hiyo, Waziri  Ummy Mwalimu, amerejea kutoa wito kwa watanzania wote kwa  katika ujumla wao   wakiwamo wazee wa kimila, viongozi wa dini na vijana wakiume    kutoa ushirikiano kwa  serikali na wadau wengine ili hatimaye tatizo hilo ambalo   linaelezwa  kuwa  siyo tu lina madhara makubwa kiafya na kisaikolojia lakini pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu.


“Tunatakiwa kufanya kazi kwa  pamoja na katika umoja  wetu, serikali peke yake haitaweza kulimaliza tatizo hili, ambalo  imefikia mahali  sasa  wazazi kwa kuongopa mkono wa sharia wanaamua kuwafanyia ukeketeji watoto wa kike katika umri  mdogo sana” Akaeleza Waziri.Akasema  , Tanzania  imebaini  uelimishwaji na  majadiliano  yanayohusisha familia na vijana wakiume ni muhumu katika kuchangiza juhudi za serikali katika  kukabili ukeketaji.

“Tunawaelimisha  pia vijana wa kiume ili waelewe madhara ya ukeketaji kwa sababu wao ni wadau wakubwa kama waume watarajiwa. Lakini pia tunawaelimisha wasichana ambao wengine huamua kufanyiwa ukeketaji kwa hofu ya kutokuja olewa”. Amesema Waziri.

Akasema Tanzania imeshukuru  kwamba tatizo  la Ukeketaji  limepewa umuhimu na nafasi katika Ajenda mpya ya Maendeleo  endelevu , ambapo katika lengo namba tano  linalohusu Usawa wa Kijinsia, linaeleza zaidi  umuhimu kumalizwa kwa vitendo vyote vibaya kama vile   ndoa za utotoni, ndoa za kulazimishwa na  ukeketaji ifikapo mwaka 2030. 

 Naye  Mke wa Rais wa Burkina Faso, Bi. Sika Bella Kabore akizungumza katika  mkutano huo amesema kuwa  tatizo la ukeketaji  ni  la kimila na kitamaduni maeneo ambayo ameyataja kwamba yatanakiwa kufanyiwa kazi ya ziada   ili kumaliza tatizo  hilo. 

“Tukiweza kulimaliza tatizo hilo  tutakuwa pia  tumefanikiwa  katika kutetea  haki  za wanawake na watoto wa kike lakini pia tutamaliza ukatili dhidi ya wanawake, ukeketaji hauna nafasi katika Dini au Imani  yoyote ile” Akasisiza Bi. Sika Bella Kabore.

Naye   Dr. Lina Kilimo kutoka  Kenya,  yeye kwa  upande wake amesema tatizo la  ukeketaji si la  Afrika au Asia  peke yake bali ni la dunia nzima na kwamba kwa kuingizwa katika   Agenda 2030 imedhihirisha wazi  kwamba  bila msukuko  na ushirikiano kutoka  pande zote itakuwa kazi kulimaliza tatizo hilo.

Kwa upande wake Dr. Morissanda Kouyate  katika mchango wake amesema, ifikie mahali viongozi   wasione aibu kulizungumzia hadharani  tatizo  na madhara ya  ukeketaji na kwamba hakuna tena muda wa kusubiri.  Madhumuni ya mkutano  huu pamoja na mambo mengine  yalikuwa ni kwa wajumbe wanaoudhuria mkutano wa 60 wa  Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake, kubadiliana uzoefu, changamoto  pamoja na  kujifunza mbinu ambazo nchi nyingine zinatumia kusukuma mbele jitihada za kutokomeza  vitendo vya ukeketaji.

Inaelezwa kwamba Zaidi ya wanawake na watoto milioni 200 duniani kote wamefanyiwa ukeketaji , Afrika,  Mashariki ya Kati, Asia,  Latin America,  Ulaya, Amerika ya Magharibi  Australia na New Zeland. Kumalizwa  kwa vitendo vya  ukeketaji ni moja ya  hatua muhimu katika kufanikisha malengo mengine ya maendeleo endelevu yakiwamo yanayohusu upatikanaji  wa elimu bora,  huduma za afya , ajira zenye hadhi na ukuaji wa uchumi.
   

WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA WAWILI CHATO

$
0
0
·         Aagiza TAKUKURU na Polisi kuanza uchunguzi mara moja

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tuhuma za ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Watumishi hao ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, Bw. Mwita Mirumbe Waryuba pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Bw. Dioniz Mutayoba. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana usiku (Jumatano, Machi 16, 2016) alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara zote na taasisi zilizomo kwenye wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mshikamano SACCOS wilayani humo.

Afisa Kilimo na Ushirika anadaiwa kuchangisha kiasi cha sh. milioni 20 kutoka kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kuanzisha SACCOS tangu mwaka 2013 lakini hadi sasa SACCOS haijaanzishwa na wala fedha hizo hazijarejeshwa. Fedha hizo zinadaiwa kuliwa na watumishi watatu (majina yamehifadhiwa). Aidha, Bw. Waryuba anadaiwa kutumia lugha chafu na za vitisho kwa watumishi walio chini yake ikiwa ni pamoja na kuomba na kupokea rushwa, na kunyanyasa na kudhalilisha kijinsia baadhi ya watumishi wa kike.

Inadaiwa pia Bw. Waryuba alikopa bila kufuata taratibu za mikopo wilayani Chato ambapo alikopa sh. milioni 15 kutoka Mwambao SACCOS na sh. milioni 15 nyingine kutoka Chato Teachers’ SACCOS tangu mwaka 2015 na tangu wakati huo hajazirejesha hali ambayo imeleta manung’uniko kutoka kwa viongozi na wananchama wa SACCOS husika.

“Malalamiko ya watumishi na wananchi dhidi ya huyu bwana yamefikishwa kwa Kaimu Mkurugenzi lakini hajachukua hatua kwa sababu ni rafiki yake,” alisema Waziri Mkuu. Kaimu Mkurugenzi huyo ni Mhandisi Joel Baha ambaye hakuwepo ukumbini hapo kwa sababu yuko kwenye ziara ya mafunzo huko Japan. Kwa upande wake, Bw. Mutayoba ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo anadaiwa kuzembea kusimamia mradi wa kufyatua matofali ya gharama nafuu (interlocking bricks) zilizogawiwa kwa vikundi vinne vya vijana wa wilaya hiyo.

“Mwaka 2013 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilitoa mashine nne za kufyatulia matofali ya bei nafuu kwa ajili ya vikundi vinne vya vijana wilayani Chato. Mashine hizo ziligawiwa kupitia kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya, Bw. Dioniz Mutayoba na kila kikundi kilipewa sh. 500,000 ili waanze kazi ya kufyatua matofali na kuyauza kwa bei nafuu katika maeneo waliyopo lakini hadi leo hakuna kitu kilichofanyika,” inasema sehemu ya taarifa.

Afisa huyo anadaiwa kugawa mashine mbili kwa kila kata katika kata za Muganza na Buseresere lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika kwani vikundi hivyo havikuzalisha kitu chochote tangu wakati huo. Aidha, Bw. Mutayoba anatuhumiwa kudai na kupokea rushwa kwa wanachama wa vikundi vya ujasiriamali ili aweze kuvisaidia kupata mikopo. “Yaani watu wanakuja kukopa sh. milioni mbili halafu unawadai kitu kidogo cha sh. 300,000. Sasa mradi waliotaka kufanya wataweza kuukamilisha kweli?,” alihoji Waziri Mkuu.

“Huyu bwana amelalamikiwa lakini Mkurugenzi aliyepita lakini naye anadaiwa kumlinda kwa sababu ni rafiki yake,” alisema Waziri Mkuu na kuibua minong’ono ndani ya ukumbi huo. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato, Bw. Clement Berege hivi sasa amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.

“Katika Serikali hii tunataka tuwe na Halmashauri zilizo safi. Lakini pia Serikali hii ina mkakati wa kuimarisha ushirika na tunataka kuinua kilimo. Kwa hiyo basi, TAKUKURU na polisi wachunguzeni hawa watu wawili kwa maana ya Afisa Ushirika na Afisa Maendeleo ya Jamii na nipewe taarifa uchunguzi utakapokamilika,” alisema Waziri Mkuu.

Mapema, akizungumza na watumishi hao, Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili akitokea mkoani Kagera, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi hao aliwakumbusha wajibu wao wa kuwahudumia Watanzania bila kujali hali zao na akasisitiza kuwa Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ambaye anatimiza wajibu wake.

“Napenda kusisitiza kuwa malengo ya Serikali ni kuimarisha utendaji wa watumishi lakini pia Serikali hii haitamvumilia mtu mdanganyifu, mzembe, asiye mwadilifu na mla rushwa. Ukiharibu kazi hapa Chato mwwisho wako ni hapa hapa tu. Usitarajie kupelekwa Bunda au kwingine ili ukaharibu na huko,” aliongeza.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

ALHAMISI, MACHI 17, 2016.

ASIMAMISHWA KAZI KWA KUMDANGANYA WAZIRI MKUU

$
0
0

·         Ni Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chato
·         Pampu yadaiwa kupelekwa Morogoro, yeye asema iko kijijini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chato, Bw. Peter Ngunura kwa kosa la kumdanganya mbele za watu na kumpa taarifa za uongo juu ya pampu ya maji iliyodaiwa kupelekwa Morogoro.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Machi 16, 2016) alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Chato waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wilayani Chato, mkoani Geita.

Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili akitokea mkoani Kagera, alisimamishwa na wakazi wa kijiji cha Kalebezo, kata ya Nyamirembe, wilayani Chato na kukuta mabango yaliyokuwa yakidai maji safi na kuelezea uharibifu wa pampu ya maji.

Katika maelezo yao, wakazi hao walimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi wa maji kwenye kata hiyo ulishakamilika lakini pampu yao imechukuliwa na kupelekwa Morogoro jambo lililosababisha wakose maji kwa muda mrefu.

Kwa sababu alikuwa hajafika Chato mjini na hakuwa na taarifa sahihi za mradi huo wa maji, Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba analibeba jambo hilo na atafuatilia hadi aelezwe ni kwa nini pampu hiyo imepelekwa Morogoro. Akiwa kwenye mkutano wa hadhara, ndipo suala la maji likaibuka tena na Waziri Mkuu kuamua kuchukua hatua hiyo.

“It’s unethical (ni kinyume cha maadili) kumdanganya kiongozi wako. Nimekuuliza mara mbili mbili kama una uhakika kuwa pampu hiyo ipo ukasema una uhakika kuwa ipo. Nimemtuma diwani na vijana wangu wakacheki wakasema hakuna pampu,” alisema Waziri Mkuu na kumwita Diwani huyo jukwaani ili atoe majibu.

“Pale kulikuwa na pampu mbili; moja ni ya kuvuta maji kutoka kwenye kina kirefu na kuyapeleka kwenye pump house na nyingine ni ya kuvuta maji kutoka kwenye pump house na kuyapeleka kwenye tenki kubwa la kuhifadhia maji. Ile ya kutoa maji kwenye kina kirefu ndiyo haipo, wataalamu wanajua wameipeleka wapi,” alisema Bw. Charles Manoni ambaye ni diwani wa kata ya Nyamirembe ambayo kijiji cha Kalebezo kimo.

Waziri Mkuu alisema ahadi ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuwatumikia wananchi kwa uadilifu. “Lazima watumishi wa umma wabadilike na kuanza kuwatumikia wananchi kwa dhati. Hatuwezi kuwa na watumishi waongo ambao wanamdanganya hata Waziri Mkuu.”

“Kuanzia sasa, Engineer atakaa pembeni, polisi na TAKUKURU wamchunguze. Asitoke Chato hadi uchunguzi ukamilike. Nataka kujua nani alichukua hiyo pampu na kwa kibali gani. Tukijiridhisha atarudi lakini kwa sasa hivi akae kando,” alisema.

Mapema jana mchana, akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Geita na wilaya ya Chato mara baada ya kupokea taarifa zao kwenye ukumbi wa Halmashauri, Waziri Mkuu alimpa fursa Mhandisi huyo aeleze nini kimetokea kuhusu pampu inayodaiwa kupelekwa Morogoro lakini akakanusha na kudai kuwa ipo palepale kijijini.

“Una uhakika na hayo unayoyasema? Hiyo pampu ipo kweli kijijini? Nikienda nitaiona?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa mara mbili na mhandisi huyo kwamba ana uhakika asilimia 100 kwamba pampu ipo na wala haijaenda Morogoro.

Alipotaka kujua ni kwa wananchi wa kijiji kile hawana maji kutokana na ubovu wa pampu hiyo, alijibiwa kwamba mradi ule ulikuwa chini ya mamlaka ya maji ya mji wa Bukoba (MBUWASA) ambako wilaya hiyo ilikuwepo zamani kabla ya kuhamishiwa kwenye mkoa mpya wa Geita mwaka 2012.

Mhandishi huyo alisema amekuwa akifuatilia fedha za matengenezo kutoka kwa Mkurugenzi wa MBUWASA bila mafanikio, ndipo Waziri Mkuu akamuagiza aende nje ya ukumbi huo akapige simu na kumletea majibu ni lini fedha hizo zitapatikana ili wananchi wa kijiji kile waendelee kupata maji.




IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

ALHAMISI, MACHI 17, 2016.

ACCESS BANK WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM WANAOSOMA SHULE YA MSINGI MTAMBANI

$
0
0
Meneja Masoko wa AccessBank Mr.Muganyizi Jonas Bisheko Akikabidhi Vifaa Mbalimbali kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum wanaosoma  shule ya Msingi Mtambani Iliyopo Boko Manispaa ya Kinondoni.
Benki ya Access Bank imetoa Msaada wa Wanafunzi Wenye Mahitaji maalumu wanaosoma Shule ya Msingi Mtambani Manispaa ya Kinondoni.

Meneja Masoko kutoka Access Bank alisema Msaada huo ni sehemu ya faida ya Benki hiyo Ambayo Wnarudisha kwa Jamii ya Watanzania hivyo waliguswa na Changamoto Kubwa Zinazowakabili Wanafunzi hao ikiwwemo Ukosefu wa Miundo mbinu Rafiki kwajili ya Wanafunzi hao kama Madarasa vyoo na Vitendea kazi vingine.

Akieleza zaidi Bw Muganyizi Jonas Bisheko Ameomba Makampuni Mbalimbali Kujitokeza Kuwasidia wanafunzi wao wenye mahitaji Maalum kwa lengo la kuwezesha kupata elimu Bora kawa Wanafunzi wengine.Benki hiyo imetoa Vifaa mbalimbali vya kujifunzia pamoja na Michezo kwajili ya kusaidia kutatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao
Msaada huo unajumuisha vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya kujifunzia pamoja na Michezo,akieleza zaidi Meneja Masoko wa Benki hiyo amesema Accessbenk imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii ya watanzania hasa kupitia sekta ya elimu kwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo kama vile ukosefu wa vifaa na mazingira rafiki ya kuwezesha kutoa elimu bora
Mwalimu wa shule ya Msingi mtambani anayehusika na Kitengo cha wanafunzi wenye Mahitaji Maalum akitoa neno la shukrani Mara baada ya Kupokea Msaada huo.Ameishukuru sana Accessbenki kwa msaada wao amesema kwa kiasi utatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.
Wanafunzi Wenye mahitaji Maalum kutoka Shule ya msingi mtambani walionufaika na msaada huo kutoka accessbenki.

Msama: Waziri Nape ni faraja Tamasha la Pasaka

$
0
0
MWENYEKITI wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama amekoshwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka litakalofanyika Mwanza Machi 27 na kueleza kwamba ni faraja kwao.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Nape ni mmoja wa walezi wa tamasha hilo ambalo mwaka huu linatarajia kuanzia Geita Machi 26 na kumalizikia Kahama Machi 28.

“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri Nape, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama  na kuongeza.

“Tunafurahishwa na Waziri Nape kukubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwa sababu ni mmoja wa wanaoweza kusaidia mipangilio ya Matamasha yanayoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions kama ilivyokuwa Tamasha la Krismasi lililofanyika mwaka jana,” alisema Msama.  
  
Aidha Msama anatumia fursa hiyo kuwaweka bayana waimbaji waliothibitisha kushiriki  Tamasha la Pasaka ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro ya Mwanza na Kwaya ya Wakorintho wa pili kutoka Njombe.

Anavitaja viingilio katika tamasha hilo litakalofanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa ni Sh. 5,000 kwa wakubwa na kwa watoto Sh 2,000. Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vema na kutoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi.

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AWATAKA JESHI LA POLISI MWANZA KUTENDA UADILIFU NA KUFUATA MAADILI YA KAZI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea mkoani  Kagera kwa ziara ya kikazi.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisaini katika kitabu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Mwanza,mara baada ya kuwasili jijini hapo  jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,ACP Japhet Lusingu(kushoto), akitoa taarifa ya hali ya usalama katika mkoa wa Mwanza kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati) mara baada ya Naibu Waziri kuwasili jijini Mwanza jana akitokea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.Kulia ni Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai mkoa wa Mwanza,SSP Augustine Senga.



Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) .Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

TAARIFA YA KATIBU WA BUNGE KUTEMBELEA JENGO LA BUNGE MKOANI DODOMA

$
0
0
 Mkurugenzi wa kampuni ya Jaffery Industry Saini LTD Ndg. Vinshal Singh Saini akitoa maelezo juu ya hatua iliyofikiwa katika ufugaji meza mpya katika ukumbi wa Bunge kwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah (mwenye miwani) alipotembelea kujionea hatua ya ukarabati wa Jengo la Bunge ilipofikiwa.
   Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akijaribisha kukaa katika moja wapo ya kiti kilichofungwa katika meza mpya kwenye ukumbi wa Bunge. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kampuni ya Jaffery Industry Saini LTD Ndg. Vinshal Singh Saini akimpa maelezo juu ya namna viti na meza hizo vitakavyokuwa vinatumika baada ya kukamilika.
 Mwonekano wa Meza Mpya zilizofungwa katika Ukumbi wa Bunge
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Jaffery Industry Saini LTD Ndg. Vinshal Singh Saini mara inayofunga meza mpya katika ukumbi wa Bunge maada ya kukagua ukarabati wa Jengo la Bunge.Picha na Ofisi ya Bunge

TAASISI MBALIMBALI ZATOA MADA KATIKA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akitoa mada kuhusu huduma mbalimbali za TeknolojiA ya mawasiliano kwa njia ya mitandano kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016.
Afisa kutoka kampuni ya Push Mobile Bi. Patricia Michael akitoa mada kuhusu huduma mpya ya upashaji habari kwa njia ya simu za mkononi iitwayo SIMU TV kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016 .
Meneja wa mawasiliano na uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi. Gaudensia Simwanza akipokea zawadi baada ya kufaulu maswali kutoka kwa Mwezeshaji kutoka Uongozi Institute, Bi Joy Nyabongo katika kikao kazi cha maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini ukumnbi wa VETA mjini Morogoro .
Afisa kutoka kampuni ya Push Mobile Bw. Abdi Zagar akitoa mada kuhusu huduma mpya ya upashaji habari kwa njia ya simu za mkononi iitwayo SIMU TV kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016.
Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Sarah Kibonde akitoa mada kuhusu mamlaka hiyo kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016. 

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIWA WILAYANI CHATO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Joyce Thobias na mwanae Jonathan Mbarak ambaye amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Chato akimuuguza mwanae majeraha ya moto Machi 16,2916. mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha gari la wagonjwa likiwa ni moja kati ya mawili yaliyotolewa msaada na Bibi Merete Trolle wa Denmark akisaidiwa kulisafilisha hadi hapa nchini na Mgodi wa Geita Gold Mine. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua duka la dawa la MSD baada ya kulizindua kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, Profesa Mtulia.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliiwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Chato , Machi 16, 2016.

MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WAGAWA VIFAA VYA KUSOMEA NA KUFANYA KAMPENI YA KUHAMASISHA KUACHA MAUAJI KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WILAYANI KILOSA.

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Habari- MAELEZO Bw.Assa Mwambene(wa tatu kushoto) akikabidhi madawati kwa watoto wa shule ya msingi Tindiga wakati maafisa habari na mawasiliano wa serikali walipotembelea shule hiyo kugawa madawati na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji wilayani kilosa.Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya kilosa Bw.John Henjewele(wa pili kulia).Picha na Daudi Manongi.
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kilosa wakati alipokuwa akiongea nao walipotembelea shule ya palakuyo kutoa vifaa vya kusomea masomo ya Sayansi na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa.maafisa hao walitoa pia msaada wa vifaa vya kusomea masomo ya sayansi.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.sylvia Lupembe(kushoto) akikabidhi vifaa vya kusomea masomo ya sayansi kwa mkuu wa wilaya ya kilosa Bw.John Henjewele wakati wakati wa kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akigawa msaada wa vitabu kwa watoto wa shule ya Mabwerebwere wilayani kilosa wakati walipotembelea walayani hapo kusaidia masuala ya elimu pamoja na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.

LAFARGE TANZANIA YATOA SARUJI MIFUKO ZAIDI YA 1,000 KUJENGA UPYA MABWENI SEKONDARI YA IYUNGA.

$
0
0
Viongozi wa kampuni ya saruji ya Lafarge wakiwa pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakati wa kukabidhi mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya mabweni yaliyoteketea ya shule ya Sekondari Iyunga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro(kushoto) akipokea mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Meneja Uajiri watu wa kampuni ya saruji ya Lafarge Bryson Tarimo kwa ajili ujenzi wa mabweni ya shule ya Iyunga yaliyoteketea kwa moto hivi karibuni.
Meneja Rasilimali Watu wa kampuni ya saruji ya Lafarge ya jijini Mbeya Bryson Tarimo akizungumza mara baada ya kukabidhi mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga ambayo hivi karibuni yaliteketea kwa moto,Kampuni ya Lafarge imetoa mifuko ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni 14.

Mkuu wa shule ya sekondari ya Iyunga Edward Mwantimo akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa mifuko 1,000 ya saruji kutoka kampuni ya Lafarge ya jijini Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga ambayo hivi karibuni yaliteketea kwa moto ambapo pia alielezea madhara yaliyotokana na moto uliosababisha kuungua kwa mabweni ya wanafunzi wa shule hiyo.


 Kampuni ya Saruji ya Lafarge Tanzania (Mbeya Cement Company) imetoa msaada wa zaidi ya mifuko 1,000 ya saruji na vifaa vingine vya ujenzi kwa shule ya Sekondari ya Iyunga mkoani Mbeya kufuatia mabweni ya shule hiyo kuungua moto hivi karibuni.

Mashine ya kampuni hiyo pia itatumika kufyatua zaidi ya matofali 40, 000 yanayohitajika kukamilisha ujenzi huo na kufanya jumla ya msaada huo kuwa na thamani ya shilingi 14 milioni. Akizungumza kwenye makabidhiano ya msaada huo, Meneja Rasilimali Watu wa Lafarge Tanzania, Bryson Tarimo alisema “tulipata habari za kushtusha kuhusiana na tukio la moto ambao uliteketeza miundombinu ya shule pamoja na mali za wanafunzi. 

Tunatambua kwamba huu umekuwa ni wakati mgumu kwa uongozi wa shule pamoja na wanafunzi.” Aliongeza kusema kwamba Lafarge inaamini kwamba elimu ni muhimu kwa maendeleo ya mustakabali wa Tanzania na pia kwamba elimu itasaidia kufungua mianya ya fursa mbalimbali kwa Watanzania. Tarimo alieleza kwamba Lafarge ina jukumu la kujenga mabweni hayo ili kuwarudishia wanafunzi wa Sekondari ya Iyunga mazingira mazuri ya kujisomea. “Hii ni sehemu ya jukumu letu kuifikia jamii na kuisaidia jamii pamoja na taasisi mbalimbali zilizopo mahali tunapofanyia kazi.”

 Aliongeza: “Uhusiano wetu na shule hii ni mkubwa sana kwa sababu tunaelewa imewafundisha baadhi ya watu ambao hivi sasa wanaendesha kiwanda chetu na kutufanya tuendelee kuwa na mafanikio. Tunataka kuona wanafunzi wakirejea madarasani na walimu wakiendelea kutimiza majukumu yao kama kawaida kwani azma yetu ni kuona shule hii inapata mafanikio na kuwapa wanafunzi fursa ya kutimiza ndoto zao na kuwa na mustakabali mzuri. 

Mtazamo wetu ni kuona Tanzania ikiwa nchi inayotoa fursa ya elimu kwa kila mtoto ili watoto hawa wote kila mmoj aweze siku moja kuchangia maendeleo ya nchi hii.” Tarimo alisema kwamba Lafarge inajali maendeleo ya jamii na ina fahari kuweza kutoa msaada huu kwa shule ya Sekondari ya Iyunga kufuatia moto ulioteketeza mabweni ya shule hiyo. 

Tunaamini msaada huu utarejesha hali ya kawaida katika shule hii na sisi kama sehemu ya jamii hii tunapenda kuona wanafunzi hawa wakiishi katika mazingira salama.” Tarimo aliyaomba makampuni mengine na taasisi mbalimbali, watu binafsi na jamii kwa ujumla kuisaidia ujenzi wa shule hiyo.

WAZIRI NAPE NNAUYE KUZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI DAR

$
0
0
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Lino International Agency LTD,Hashim Lundenga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO),kuhusiana na msimu mpya wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016.Lundenga amesema kuwa msimu huo mpya unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya jumamosi Machi 19,2016 katika hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar.Katika uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake Mgeni rasmi amepangwa kuwa ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Nape Moses Nnauye.Kati ni Mshindi wa Miss Tanzania 2014-2015 Liliani Kamazima pamoja na Mkuu wa Itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye.
Lundega akifafanua jambo kwa umakini mbele ya Wanahabari (hawapo pichani).

Lundenga amesema kuwa katika uzinduzi wa msimu huo mpya,utawakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya Urembo wakiwemo Wabunifu wa Mavazi,Mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa nchini.kama vile haitoshi Lundenga alibainisha kuwa pia Wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ambao miongoni mwao wanatarajia kuwa Wadhamini wa shindano hilo kwa mwaka huu.

Katika kunogesha uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake,Lundemga amesema kuwa burudani kadhaa zitakuwepo akiwemo msanii wa kizazi kipya Linah Sanga pamoja na msanii wa ngoma za asili Wanne Star.

Lundenga alisema kuwa mara baada ya uzinduzi huo kufanyika jijini Dar,utahamia mkoa wa Arusha ambako pia kutakuwa na aina nyingine ya uzinduzi," Uzinduzi huo ukikamilika itafuata ratiba ya semina ya mawakala na kuanza kwa mashindano ya urembo katika ngazi za vituo,Wilaya,Mikoa na Kanda",alisema Lundenga.

Amesema kuwa mpaka sasa Wadhamini kadhaa wamejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kudhamini shindano hilo katika ngazi ya Taifa.Lundenga ameyataja makampuni ambayo yamedhamini uzinduzi huo wa shindano la urembo la Miss Tanzania 2016 kuwa ni Ramada Resort Dar,Naf Beach hotel Mtwara,Kitwe General Trader,CXC Africa,MMI Tanzania,Mwandago Investment Ltd,Break Point pamoja na GSM Media. 

JAJI JALLOW AMUAGA WAZIRI MWAKYEMBE

$
0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya halaiki ya Rwanda (ICTR) Jaji Hassan B. Jallow anayemaliza muda wake. Jaji Jallow alifika ofisini kwa Mhe. Mwakyembe leo (17/3/2016) kwa ajili ya kumuaga rasmi.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya halaiki ya Rwanda (ICTR) Jaji Hassan B. Jallow (kulia) anayemaliza muda wake akifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipomtembelea leo (17/3/2016)ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi kwenye Mahakama hiyo.

BMT KUANZISHA SEMINA YA WADHAMINI.

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la MichezoTaifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani akielezea Semina ya masoko na wadhamini wa Michezo Nchini katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Pro- Event Masters Ltd Bw. Henry Tandau.
Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Pro- Event Masters Ltd Bw. Henry Tandau akiongea na waandishi wahabari hawapo pichani akielezea Semina ya masoko na wadhamini wa Michezo Nchini katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es salaam kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la MichezoTaifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja.PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images