Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

mradi wa kuwainua wanawake kiuchumi na kijamii wazinduliwa leo jijini dar

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa CONCERN-Tanzania Bw. James Davey kushoto akieleza namna shirika lake litakavyo tekeleza mradi huo,Katikati ni Mhe.Naibu Waziri Ummy Mwalimu na Kulia ni Balozi wa EU nchini Mhe. Filberto Cerian Sebregondi.

Katika Picha ni Uzinduzi wa  Mradi wa Kuwainua Wanawake Kiuchumi na Kijamii,Mradi unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la CONCERN Tanzania katika Mkoa wa Kigoma Wilaya ya Kasulu,Kigoma na Masasi. Mradi huo Unafadhiliwa na European Union, Umezinduliwa leo jijini Dra es Salaam katika Ofisi za CONCERN Tanzania na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia  na Watoto, Mhe, Ummy Mwalimu.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Mhe.Ummy (katikati ) akielezea namna Wizara inavyowasaidia wanawake kujiinua Kiuchumi na Kijamii. Kushoto kwake ni .Balozi wa EU nchini Mhe.Filberto Cerian Sebregondi.
Balozi wa EU nchini Mhe. Filberto Cerian Sebregondi (katikati) akiteta jambo na Mhe.Ummy Mwalimu Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii(kushoto) na MKurugenzi wa Shirika la CONCERN _Tanzania Bw. James Davey.

Sehemu ya Wageni waliohudhuria Uzinduzi huo

Hivi hizi Club zetu hazina ulinzi na usalama wa watu.?? Hivi hapa kila mmoja angeamua kulianzisha ingekuwaje humo ndani??

0
0

RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa pole kwa watawa wa kanisa hilo wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Wananchi wakimuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa kijana James Gabriel (16) aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Joachim Assey (aliyekaa kushoto kwake) wakati akihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Mama Salma Kikwete akipungia wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013. PICHA NA IKULU.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA KANISA LILILOPIGWA BOMU ARUSHA

0
0




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati alipotembelea Mei 7, 2013 katika  kanisa la Mtakatifu Joseph kitongoji cha Olasiti jijini Arusha lililoshabuliwa na magaidi Jumapili iliyopita .


BABA PAROKO WA KANISA LA OLASITI LILILOSHAMBULIWA NA BOMU ARUSHA AKIONGEA.


RAIS KIKWETE AONGEA NA WANAHABARI ARUSHA KUFUATIA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI.


Rais Kikwete alipoongea na Maaskofu wa madhehebu mbalimbali wa Arusha nyumbani kwa Askofu Mkuu Jimbo la Arusha Muadhama Josephat Lebulu jijini Arusha  
Mei 7, 2013.

Fundi Uashi aibuka mshindi wa Mamilioni ya Airtel

0
0

 Mshindi wa shilingi milioni 15 wa promosheni ya Amka Milionea Juma Ibrahim Hamza, ambaye ni  fundi uashi akilia kwa furaha na kushindwa kuongea mara baada ya kutangazwa mshindi wa shilingi milioni 15 kupitia promosheni ya Amka millionea. Airtel imewazawadia washindi wawili wa milioni 15 walioibuka washindi mwenzi March
 Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando ( kushoto) akimkabithi mfano wa hundi wa shilingi milioni 15 bwana Adnan Ayub khan mara baada ya kuibuka mshindi wa mwenzi wa promosheni ya amka millionea. Akishuhudia ni Afisa masoko wa Airtel Bi Khalila Mbowe
Afisa masoko wa Airtel Bi Khalila Mbowe (kulia) akimkabithi mfano wa hundi wa shilingi milioni 15 bwana Juma Ibrahim Hamza  mara baada ya kuibuka mshindi wa mwenzi wa promosheni ya amka millionea. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando

=========  =======  ======  ========
Fundi Uashi aibuka mshindi wa Mamilioni ya Airtel

Washindi wa  Airtel Amka millionea wakabithiwa shilingi million 15

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Amka millione na Airtel ambapo wateja wawili washindi wa mwenzi wa tatu wamezawadiwa kila moja kitita cha shilingi million 15 kila mmoja.

Washindi hao ni pamoja na bwana Juma Ibrahim Hamza  mwenye umri wa miaka 30 na mkazi wa kawe jijini Dar es salaam  na bwana  Adnan Ayub khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara katika mkoa wa simiyu walijishindia kila mmoja  alijishindia million 15.

Akiongea wakati wa kukabiithi mfano wa hundi kwa washindi hao Meneja uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema,  leo tunao washindi wawili waliojishindia shilingi milioni 15 kila moja katika droo ya mwenzi ya mwisho wa mwezi watatu. Tumeendelea kushuhudia watanzania na wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku,kila wiki na kila mwenzi kupitia promosheni hii ya Amka milionea.

Tunaahidi kuendelea kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu , na kuwapata wateja wetu huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel yatosha inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mengine ya simu za mkononi kwa bei poa na kupata vifurushi ya ujumbe mfupi na huduma ya internet bila kulipia gharama ya ziada. Aliongeza Mmbando.

Akizungumza wakati wa makabidhiano bwana Juma Ibrahim Hamza  mshindi wa million  15 alisema , nashindwa jinsi ya kuongea lakini nashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi milioni 15 ambazo kwangu  nikama ndoto.  Nategemea kutumia pesa hizi kujenga nyumba yangu ya kuishi pamoja na familia yangu.

Kwa sasa ninajishughulisha na shughuli za ufundi wa kujenga tiles katika nyumba za watu na ninajipatia kipato  kidogo ambacho nilijibana na kutumia kiasi kutuma sms wakati wa promosheni ya Amka milionea ya Airtel kama kujaribu Bahati yangu na leo nashangaa kuibuka mshindi wa mamilioni haya 15, namshukuru sana mungu kwa kweli! Alisema Bw Ibrahim.

Binafsi nachukua fulsa hii kuwaasa watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika wataamka washindi kama mimi hivi leo.Kwa upande wake bwana Adnan Khan ambaye pia ni mshindi alisema, anawashukuru Airtel kwa kuanzisha promosheni ya amka millionea, na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya.

Promosheni ya amka milionea imefika mwisho wake ambapo mpaka sasa wateja zaidi ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni 626 zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Kinana apinga vikali tuhuma zilizotolewa dhidi yake

0
0

Na Ripota wetu, Dodoma

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameibuka na kupinga vikali tuhuma zilizotolewa dhidi yake na kambi ya upinzani bungeni kuhusu shehena ya pembe za ndovu iliyokamatwa Vietnam mwaka 2009 kuwa ni za kupika na za uongo.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma. "Tuhuma hizo hazina ukweli wowote, zina nia mbaya dhidi yangu na zemelenga kuniharibia taswira yangu na ya chama changu," alisema Kinana. Aliongeza kuwa tuhuma hizo hazina msingi wowote na kuwa hata kambi hiyo ya upinzani bungeni inatambua kuwa mamlaka zote za ulinzi na usalama za ndani na kimataifa zilimsafisha kuhusiana na sakata hilo.

Kinana alisema baada ya shehena hiyo kukamatwa, Mamlaka ya Kimataifa ya Kudhibiti Wanyama Walio Hatarini Kutoweka (CITES) na Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) walifuatilia na wakabaini kuwa hakuhusika kwa namana yoyote na shehena hiyo. Kwa mujibu wa nyaraka za uchunguzi kuhusiana na shehena hiyo, watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu ambao ni Eladius Colonerio (Mkurugenzi wa Team Freight (T) Ltd) Gabriel Balua (Meneja wa TEA Freight (T) Ltd) na Shaban Yabula (Mkurugenzi Mtendaji wa Kigoma M.N Enterprises (T) Ltd).

Wengine waliofikishwa mahakamani ni Erick Morand (Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika Bandari ya Dar es Salaam) Issa Lweno, Norbert Kiwale na Abubakari Omar Hassan. Nyaraka hizo ambazo gazeti hili lina nakala zake, zinaonyesha kuwa maofisa wa forodha huko Haiport and Hanoi, Vietnam waliokamata pembe za ndovu kilo 6,200 zilizosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam. Pia, kati ya Machi na Juni, 2009, maofisa wa forodha wa bandari ya  South harbor mjini Manila, Philippines walikamata shehena nyingine ya kilo 4,861 zilizosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Kutokana na taarifa za kukamatwa kwa shehena hiyo ya pembe za ndovu kutoka Vietnam, Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi kwa kushirikiana na Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii, ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), INTERPOL na Taasisi ya Kupambana na Ujangili Kusini na Mashariki mwa Afrika (LAFT).Uchunguzi huo uliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Angelist Bonga ambaye kwa sasa ni marehemu. "Timu hiyo ya wachunguzi ilifanya kazi yake kwa umakini na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa watano ambao baadaye walifunguliwa mashitaka mahakamani," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati kesi hiyo ikiendelea, serikali iliamua kupeleka timu ya wachunguzi nchini Vietnam, lakini nchi hiyo ilikataa kuwaruhusu kufanya uchunguzi nchini humo kutokana na Tanzania kutokuwa na makubaliano ya kubadilishana taarifa za masuala ya uhalifu. Hadi sasa mafaili ya kesi hiyo yapo Mahakama ya Kisutu.

"Tuhuma dhidi yangu hazina msingina ukweli wowote, hivyo hazina uzito wowote. Najua  hii ni sehemu ya siasa chafu na nilitarajia mambo kama haya baada ya kuhutubia nikiwa Morogoro wiki mbili zilizopita kuwa Watanzania wajiepushe na siasa zenye lengo la kuleta vurugu kwa taifa....Msigwa (Peter) na CHADEMA wanapaswa kutoa hoja," alisema Kinana.

Akiwasilisha hoja wakati wa kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Waziri Kivuli wa wizara hiyo Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini - CHADEMA) aliilaumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili na kumtaja Kinana kuwa mmoja wa wanaomiliki meli iliyosafirisha pembe za ndovu.

Hata hivyo, Kinana hamiliki meli yoyote na hajawahi kujihusisha na usafirishaji wa nyara hizo za serikali, suala ambalo kwa sasa bado lipo mahakamani. Katika mkutano wake na waandishi wa habari, alimtuhumu Msigwa kuwa ana agenda ya siri na kuwa ameamua kumtuhumu huku akijilinda kwa kinga za bunge na kuwa kufanya hivyo ni kutumia vibaya kinga hizo.

Alisema ahusiki na hana uhusiano wa aina yoyote na tuhuma hizo na kwamba hata kipofu anaweza kuona kuwa hausiani nazo na alituhumu kambi ya upinzani bungeni kwa kushindwa kujadili hoja za maana za maendeleo na badala yake kujihusisha na siasa za kuchafua heshima za watu wengine.

"Bado nina nguvu na sijayumba kwa namna yoyote. Nina jukumu la kuilinda CCM na kutekeleza ahadi tulizozitoa kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi," alisisitiza na kuhoji kuwa suala la shehena hizo ni la tangu mwaka 2009, kwa nini lijitokeze sasa? "Jibu lake ni jepesi, lengo lao ni kumvunja moyo Katibu Mkuu wa CCM ambaye CHADEMA wanamuona kuwa ni tishio kwao," alisema Kinana.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA KANISA LILILOPIGWA BOMU ARUSHA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati alipotembelea Mei 7, 2013 katika kanisa la Mtakatifu Joseph kitongoji cha Olasiti jijini Arusha lililoshabuliwa na magaidi Jumapili iliyopita.
BABA PAROKO WA KANISA LA OLASITI LILILOSHAMBULIWA NA BOMU ARUSHA AKIONGEA RAIS KIKWETE AONGEA NA WANAHABARI ARUSHA KUFUATIA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASIT Rais Kikwete alipoongea na Maaskofu wa madhehebu mbalimbali wa Arusha nyumbani kwa Askofu Mkuu Jimbo la Arusha Muadhama Josephat Lebulu jijini Arusha Mei 7, 2013

SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA MKOANI RUKWA TAREHE 10-12 MEI 2013, WAZIRI WA AFYA DKT. HUSSEIN MWINYI KUWA MGENI RASMI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi kupitia vyombo vya habari kutoa taarifa juu ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani itakayofanyika kitaifa Mkoani Rukwa kuanzia tarehe 10 hadi 12 ambapo mgeni rasmi anategemewa kuwa Waziri wa Afya Dkt. Hussein Mwinyi. Soma zaidi juu ya siku hiyo hapo chini baada ya picha. 
Timu ya wauguzi kutoka Hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ikiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kushoto na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Alhaj Salum Mohammed Chima kulia wakati wa kutoa taarifa ya maandalizi ya siku hiyo kwa wananchi kupitia vyombo vya habari. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - Rukwareview.blogspot.com)


Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando kuandaa hafla ya Mother's Day mei 12 jijini dar

0
0
Pichani kati ni Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama Duniani  itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu imepangwa kuwa ni "always in our heart's", "tukiwakumbusha akina  mama zetu kwamba wapo moyoni mwetu na tunawapenda sana" alisema Chando.Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa na kulia ni Mratibu wa hafla hiyo,Bi.Regina Ogwalla.Bahati amesema kuwa katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT Ilala,Mh.Nora Mzeru.

Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando amesema kuwa ameamua kuungana na Diwani wa kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa kuandaa hafla hiyo itakayozinduliwa na Wamama wa Ilala,kutambua umuhimu wa kina mama,kuwafurahisha lakini pia kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali,amesema kuwa amekuwa na shauku kubwa ya kuandaa sherehe kama hiyo ili kujitoa na kusaidia watu kama watu wengi walivyoungana kumsaidia katika safari yake ya kuwa  mrembo wa kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.

Pia anasema kuwa ameandaa sherehe hiyo kuonyesha jamii kwamba,kuwa mrembo au miss sio tu kupozi mbele ya Kamera,bali inaambatana na na jukumu la kugusa jamii kwa namna mbalimbali.

Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa akitoa ufafanuzi  kuhusiana na  uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama Duniani  itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu kwenye hafla hiyo umepangwa kuwa ni "always in our heart's",

RAIS KIKWETE AFARIJI MAJERUHI WA BOMU WALILAZWA HOSPITALI YA MTAKATIFU ELIZABETH ARUSHA

0
0
 Taswira wakati Rais Kikwete alipotembelea hospitali ya St Elizabeth jijini Arusha Mei 7, 2013  kufariji majeruhi wa mlipuko wa bomu katika kanisa la Olasiti jijini humo Jumapili iliyopita.PICHA NA IKULU



BARCLAYS TANZANANIA YAZINDUA MATEMBEZI YAJULIKANAYO KAMA Step Ahead Walk 2013

0
0
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano cha Barclays Tanzania, Bibi Tunu Kavishe, (shoto),akizungumza na Wanahabari mapema leo ndani ya hotel ya Serena Jijini Dar,kuhusiana na Benki ya Barclays kuaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step Ahead Walk,Mchakato ambao umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006,ambapo pia Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo  fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.

Matembezi hayo ya hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu  wa benki  ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii.  Tangu ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga– ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Barnaba Elias akizungumzia wimbo wake alioutunga na Mwanamuziki mwenzake Jean Pierre ajulikanae kwa jina la Kidumu ambao umezinduliwa leo rasmi ukiitwa  ‘Wanawake”,"Wimbo huo umetungwa na kuimbwa na Barnaba Elias anaejulikana kama  ‘Barnaba’ na Jean Pierre Nimbona anaejulikana kama ‘Kidumu’ ambao lengo lake na maudhui ni kuhamasisha watu wote wakazi wa Tanzania wajitokeze katika kuchangia na kuhudhuria matembezi haya ya hisani ambayo lengo lake rasmi ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama na watoto wachjanga"alisema Barnaba.
Pichani ni baadhi ya Wanahabari waliohudhuria mkutano huo jijini Dar leo.


BARCLAYS TANZANANIA YAZINDUA MATEMBEZI YAJULIKANAYO KAMA

Step Ahead Walk 2013


Kila mwaka Benki ya Barclays inaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step Ahead Walk. Mchakato huu umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006 na Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo  fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.


Matembezi haya ya hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu  wa benki  ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji muhimu katika jamii.  Tangu ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga– ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.


Akiongea katika vyombo vya habari leo, Bibi Tunu Kavishe, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano cha Barclays Tanzania amesema, leo hii tunazindua mziki unaoitwa ‘Wanawake” ambao umetungwa na kuimbwa na Barnaba Elias anaejulikana kama  ‘Barnaba’ na Jean Pierre Nimbona anaejulikana kama ‘Kidumu’ ambao lengo lake na maudhui ni kuhamasisha watu wote wakazi wa Tanzania wajitokeze katika kuchangia na kuhudhuria matembezi haya ya hisani ambayo lengo lake rasmi ni kuchangisha pesa kwa ajili ya kinamama na watoto wachjanga. 

Tukio hili rasmi itafanyika tarehe 8 juni, 2013 katika hoteli ya Golden Tulip na litahusisha matemebzi ya hisani ya kilomita tano (5) na kila mtu katika jamii anakaribishwa kushiriki. Tiketi zitauzwa kwa shilingi za kitanzania 5000 na zitapatika katika kila tawi la Benki ya Barclays kuanzia tarehe 29 Aprili, 2013.


Mwaka 2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kuchangisha shilingi za kitanzania milioni 150 kutokana na  mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili. Mwaka huu lengo ni kuchangisha zaidi ya marambili ya shilingi milioni 150 kutoka kwenye matoleo ya washirika muhimu na washiriki wengine katika jamii.



Fedha zitakazochangishwa mwaka huu zitakwenda kusaidia katika masuala ya uzazi na afya ya watoto kama ifuatavyo:-
1. Mafunzo kwa wakunga wa uzazi
2. Matibabu ya Fistula 
3.Upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu unaosababishwa na uzazi.
Step Ahead Walk 2013 itaweza kufanikiwa tu kama itawezeshwa na kila mshiriki na jamii nzima ya kitanzania kwa ujumla. Kwa sababu hiyo basi tujiunge wote ili tuweze kufanya badiliko katika masuala ya afya kwa ujumla hapa Tanzania hususani masuala ya uzazi na afya ya watoto. 

TAIFA LINA NYUFA-Mh.Zitto Kabwe.

0
0
NDUGU  KABWE Z. ZITTO, MB – BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.
Hapa Afrika kulikuwa  kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu;  na  ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano.  Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana.  Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani.  Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa  Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998.  Alisema:
“Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so.  God has showered blessings on our country.  It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity.  
It is a country of people who love equality and justice.  Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law.  A Unity reinforced by correct policies of national building.  Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all.  A unity which is extra sensitive to policies, statements behavior and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanians”
Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri.  Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena?  Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu  leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. 
Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka  pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni “irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.

NDUGU  KABWE Z. ZITTO
Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo  wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini.  Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-“point fingers” kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni   chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga.  Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono.  Matokeo yakeni nini?  Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na  hii ni lawama kwa wote.  Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-“expose”, tumejiweka wazi.  Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu.  Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo.  
Jana limetokea tukio  Arusha, angalia kwenye mitandao  ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao.  Ndiyo hatari ambayo tumeifikia;  na ndio  anachokitaka adui.  Ni hicho.  Atakuja, wanaitwa “Agent Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi.  Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa.  Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo.  
Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii.  Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni “very irresponsible” tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii.  Tunafanya nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia “grievances” zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao.  Pili turuhusu watu kuwa huru kusema.  Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika.  Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini?  Atatoka na bomu.  Turuhusu “honest discussions” miongoni mwetu kama wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa  na kauli za chuki “hate speeches”.  Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na “hate speeches” nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini.  Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika.  Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA.   Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli  za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika.  Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania.  Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.

NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013

0
0

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


MARUDIO-NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA

MWAKA 2012/2013



Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alitangaza nafasi za ajira kwa Wataalam wa Kada za Afya kwa mwaka 2012/2013 ambapo tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi hayo ilikuwa tarehe 10 Mei, 2013.


Kwa tangazo hili Wananchi wanajulishwa kuwa muda wa kuwasilisha maombi hayo umeongezwa hadi tarehe 20 Mei, 2013.  Aidha inasisitizwa kuwa hata wahitimu wa mwaka 2012 wanapaswa kutuma maombi yao kwa sababu hakutakuwa na utaratibu wa wahitimu kupangiwa vituo vya kazi moja kwa moja.


Maombi hayo yaendelee kuwasilishwa kwa njia ya Posta kwa kutumia anuani iliyopo chini ya tangazo hili. 


Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


KAIMU KATIBU MKUU,

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,

S.L.P. 9083,

DAR ES SALAAM.



Mchanganuo wa nafasi hizi umeainishwa kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz

RAIS KIKWETE AIAGA BATALIONI ITAYOJIUNGA NA MAJESHI YA UMOJA WA MATAIFA YA KULINDA AMANI DRC LEO

0
0
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya  wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda  kujiunga na  jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013.  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtakia kila la heri  kiongozi wa batalioni ya  wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda  kujiunga na  jeshi la Umoja wa Mataifa  kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia. PICHA NA IKULU                 

TCCIA Won Second Prize in the World Chambers of Commerce Competition For the Best Innovation Project 2013

0
0

Doha, Qatar 25th - April,2013. World Chambers of Commerce have honoured a Tanzanian-designed scheme to use cell phones to identify and help overturn barriers to free trade across East Africa.

The scheme won second prize in the World Chambers of Commerce competition for the best project amongst a field of other groundbreaking innovations from Britain, China, the Slovak Republic and Turkey.

The short messaging system (SMS) online non-tariff barrier (NTB) reporting and monitoring mechanism was developed by the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) to get the business community not just to grumble about NTBs but to log them, report them and get them referred to those with the power to overturn them. 

The scheme has been supported by TradeMark East Africa, TMEA; a multi-donor-funded organization that seeks to streamline EAC trade to cut the cost of doing business and grow prosperity through strong economic integration. The support is part the TMEA Tanzania’s programme to strengthen private sector advocacy for the removal of NTBs through effectively reporting and monitoring of their existence.

This system is the first of its kind in East Africa and is a beacon in the battle against NTBs, regulatory or official hurdles which slow free commerce and add to the cost of transporting goods to the region, which already has the highest transport costs in the world.

It is a great pleasure to see that the in-house innovation can stretch its wings to the international community. The recognition that the NTBs SMS and online reporting and monitoring system has received is evidence that what we do, as a private sector, in creating favorable business environment adds value to the lives of people; not only because the world can see it but most importantly, that we contribute towards improving people’s welfare by making it easier to report and for authorities to monitor and eliminate all barriers hindering trade flow.

The award was announced during the World Chambers Congress held in Doha, Qatar last month. World Chambers Competition is the only global awards programme to recognize the most innovative projects undertaken by chambers of commerce and industry from around the world. The Competition provides a unique opportunity for chambers to showcase originality & ingenuity, and also demonstrate determination to strengthen SMEs, improve services provided to members. The competition takes place every after two years.

TCCIA acts as the private sector focal point on NTBs and gathers evidence so that it can lobby for their elimination. The system is also a source of information for policy makers who are directly responsible for some of those very NTBs.

SEMINA YA KUJADILI CHANGAMOTO ZA SOKO LA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI 'DOADOA' YAFANYIKA UGANDA.

0
0
Waendesha mada katika semina ya kuangalia changamoto katika soko la muziki Afrika Mashariki na njia za kuzitatua wakijadili umuhimu wa elimu ya muziki katika soko la muziki, kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Action Music Tanzania, Mandoli Kahindi, Mkurugenzi wa sanaa kutoka Global Music Academy Ujerumani,William Ramsay, Muaandaaji wa muziki wa Uganda, Kazi Kasozi na Mkurugenzi Mtendaji wa Ketebul Music Kenya, Tabu Osusa

Semina hiyo ambayo inaambatana na maonyesho ya kazi mbalimbali za muziki yameandaliwa na Bayimba Cultural Foundation ya Uganda ambapo wadau mbalimbali wa muziki kutoka nchi mbalimbali wamejumuika kujadili na kubadilishana uzeofu juu ya soko la muziki kwa nchi za Afrika Mashariki. picha za matukio zaidi tembelea DOADOA

MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ASIMAMISHWA SHULE KWA KUTUHUMIWA USHIRIKINA.

0
0
Amina Mwamkinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo wakimtuhumu kuwa mchawi majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi wetu alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo.
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina.
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu
=========  ========  ============
KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.

  

Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.

  

Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.

  

Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.


Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo  baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.

  

Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun  iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.

  

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.

  

Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale  alisema alikuwa  halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.



Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote  kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.

Na Mbeya yetu. 

chuo kikuu cha suza kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kimataifa wa OIC

0
0

 Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kumbumbuku na Nyaraka ya Nchi ya Oman Dkt. Hamed Mohammed  ambaye ni Mkuu wa Ujumbe huo akifafanua jambo katika Mkutano wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa OIC utakaofanyika Mwezi Septemba Visiwani Zanzibar, katikati ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu SUZA na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa OIC katika Kitengo cha Utafiti na Utamaduni Dkt. Halit Eren
  Baadhi ya Wajumbe wa Nchi ya Omani na Maafisa wa Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani OIC wakifuatilia maelezo yaliyukuwa yakitolewa na Mweyekiti wa Ujumbe huo Dkt Al dhawiyaniy katika Ukumbi wa Chuo kikuu cha SUZA mjini Zanzibar kuhusiana maandalizi ya Mkutano wa OIC.
Ujumbe wa Nchi ya Omani ukiambatana na Maafisa wa Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani OIC ukiwasili Zanzibar kwa lengo la kufanya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa OIC utakaofanyika Mwezi Septemba Visiwani Zanzibar. Picha na Makeme Mshenga- Maelezo Zanzibar.

===========  ======== =========

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar .

CHUO Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA kinatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani OIC ambao utafanyika Septemba 2, mwaka huu.

Mkutano huo wa kimataifa utafanyika Zanzibar kwa mashirikiano ya Nchi ya Omani, Umoja wa OIC na Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA.

Taarifa hiyo imekuja kupitia Ziara ya siku nne ya Maafisa wa Nchi ya Omani walioambatana na Maafisa wa Jumuiya ya OIC iliyonza leo mjini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kumbumbuku na Nyaraka ya Nchi ya Oman Dkt. Hamed Mohammed Al dhawiyaniy amesema Zanzibar imepata nafasi hiyo kutokana na kuwa na Mahusiano mema na Nchi nyingi ulimwenguni na hasa katika nchi za kiarabu.

Amesema Historia na Utamaduni wa Kiislamu wa Zanzibar na namna ulivyotumika katika kusambaza Uislamu Nchi nyingine umekuwa kigezo muhimu cha Zanzibar kupata nafasi hiyo.

“Kwa vile Zanzibar ina historia nzuri katika kusambaza Uislamu nchi nyingine tunaimani kuwa hata malengo ya Mkutano wetu huo yatafikiwa kwa kiasi kikubwa ” Alisema Dkt Al dhawiyaniy ambaye pia ni Mkuu wa Msafara huo.

Kwa upende wake Mkurugenzi Mkuu wa OIC katika Kitengo cha Utafiti na Utamaduni Dkt. Halit Eren amesema Mkutano huo utakuwa fursa adhimu kwa Zanzibar kujitangaza katika mataifa mbalimbali na kuendelea kujiongezea umaarufu Kimataifa.

Amesema kwa vile Watakuja Washiriki kutoka Mataifa mbalimbali kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya OIC, Zanzibar itakuwa ni nafasi yake muhimu kufahamika kimataifa na kujipatia nafasi za masomo Duniani.

Amefahamisha kuwa Watoa Mada 164 kutoka Nchi mbalimbali tayari wameshapeleka maombi yao ili kuwasilisha katika Mkutano huo na kuwataka Wazanzibari nao kupeleka Maombi yao.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha SUZA Dkt. Haji Mwevura Haji amesema Vyuo mbalimbali kutoka nchi tofauti viliomba kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo lakini Chuo cha SUZA kimeamuliwa kuwa Mwenyeji kutokana na historia ya Zanzibar.

Amefahamisha kuwa licha ya Zanzibar kutokuwa Mwanachama wa Jumuiya ya OIC lakini kigezo hicho hakiizuii Zanzibar kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo wa Kimataifa.

Amegusia kuwa Mkutano huo unaweza kuwa fursa Adhimu kwa Zanzibar kunufaika kupitia Jumuiya hiyo kama ambavyo Nchi ya Uganda ilifaidika kwa kujengewa Chuo Kikuu cha Mbale.

“Wenzetu Uganda walifaidika na OIC kwa kujengewa Mbale University nasi pia tuna matarajio mengi ilikwemo kuitangaza SUZA na kupata Scholarships duniani”  Alisema Dkt. Haji

Dkt Haji amewahakikishia Maofisa hao ushirikiano wa kutosha ili Mkutano huo uweze kutimiza malengo yaliyopangwa.

Umoja wa Nchi za Kiislam Duniani OIC unajishughulisha na mambo mbalimbali ikiwemo kusaidia Nchi wanachama wa Umoja huo katika huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa Taasisi za Kielimu, Afya na Miundombinu ambapo Mkutano mkuu uliopita ulifanyika Nchini Omani.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

"WILLBARD MKOBA NA HAPPINESS WAMEREMETA KATIKA UKUMBI WA DANKEL HOUSE TAR.27/4/13 DAR ES SALAAM."

Tamko Rasmi toka CCM UK kuhusu tendo la kigaidi Arusha

0
0

Viewing all 46206 articles
Browse latest View live


Latest Images