Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

WAKALA YA SERIKALI MTANDAO YAZISHAURI TAASISI ZA SERIKALI KUFUATA MIONGOZO NA VIWANGO KATIKA MATUMIZI YA TEHAMA.

$
0
0
Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bi. Suzan Mshakangoto akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa na taasisi za Serikali katika kuimarisha matumizi sahihi na salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuendesha mifumo ya Tehama Serikalini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usimizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo. 
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bw. Benedict Ndomba akifafanua kuhusu mpango wa Serikali wa kuimarisha mawasiliano katika mifumo ya TEHAMA Serikalini.
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.…………………………………………………..

Na Beatrice Lyimo – Dar es Salaam
Wakala ya Serikali mtandao (e-Government Agency) imezishauri Taasisi zote za Umma ,Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekreterieti za Mikoa, Wakala na Mamlaka za Serikali ,Bodi, Tume, Mabaraza, Mifuko, Mashirika ya umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuata miongozo na viwango vilivyotolewa Wakala hiyo katika uanzishaji na usimamizi wa mifumo ya Tehama Serikalini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bi. Suzan Mshakangoto alipokuwa akitoa maelekezo na ufafanuzi wa taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa na taasisi hizo kwa lengo la kuimarisha matumizi sahihi na salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kuendesha mifumo ya Tehama Serikalini.

Bi. Mshakangoto amesema kuwa miongozo na viwango hivyo vinalenga kuziwezesha taasisi za umma kujenga mifumo inayoendana na mahitaji halisi ya taasisi husika na kuepuka mifumo inayojengwa kwa shinikizo la wafanyabiashara, wafadhili au kwa matakwa ya mtu binafsi.

“ Taasisi zote zikitumia miongozo ya viwango tuliyoweka, Serikali itakuwa na uwezo wa kuepuka urudufu wa mifumo na kupunguza gharama kubwa za uendeshaji kwa kuwa na mifumo endelevu yenye gharama halisi inayofuata viwango vya Usalama katika kulinda taarifa na data za Serikali” Alifafanua Meneja huyo.

Amezishauri taasisi hizo kuwasilisha maandiko ya mifumo mipya ya TEHAMA na kujaza taarifa za mifumo au miradi ya TEHAMA iliyopo katika mfumo wa kukusanya na kutunza taarifa za miradi ya TEHAMA Serikali ili iweze kuthibitishwa iwapo imefuata miongozo na viwango vilivyowekwa kabla ya kujengwa na kusakinishwa.

Akitoa ufafanuzi kuhusu wafanyabiashara wanaojihusisha na miradi au utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA Serikalini amesema kuwa wanashauriwa kufuata miongozo na viwango hivi ili kujua mahitaji halisi ya Serikali na kuweza kujenga mifumo ya TEHAMA endelevu na inayoleta tija kwa umma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usimizi wa Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bw. Benedict Ndomba ameeleza kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa mifumo yote ya TEHAMA ya Serikali inakuwa na mawasiliano na kubadilishana taarifa mbalimbali.

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikiweka msisitizo wa matumizi ya TEHAMA kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji kwa kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kupata huduma za Serikali kwa gharama nafuu kwa njia ya Mtandao.

Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2012.kwa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30, Sura ya 245 ya mwaka 1997. Wakala hii ina majukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.

WANANCHI WA NJOMBE WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO LINGANGA NA MCHUCHUMA.

$
0
0
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Jenista Mhagama akizungumza na makundi mbalimbali mara baada ya waziri huyo kufanya ziara  mkoani njombe katika eneo la mchuchuma na linganga katika wilaya ya Ludewa.
Baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali waliofika wilayani Ludewa kumsikiliza Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Jenista Mhagama.


Njombe Mmejiandaaje fursa zilizopo kwenye Migodi ya Liganga na Mchuchuma?, swali hilo limehojiwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,  Jenista Mhagama alipofanya  ziara Mkoani Njombe lengo kuu la ziara hiyo ikiwa ni kuhabarisha kuhusu  fursa za kujiajiri zilizopo kwenye Mkoa huo. Waziri huyo amesema kuwa Mkoa wa Njombe ni moja kati ya Mikoa yenye fursa kubwa ya uwekezaji ambayo fursa hiyo ni migodi ya Makaa ya mawe ya Liganga na Mchuchuma  iliyopo katika Wilaya ya Ludewa ambayo inatarajia kutoa ajira rasmi  zaidi ya Elfu Thelathini.

akizungumza  na baadhi ya makundi ya Vijana wa Bodaboda, Kundi la Vijana Wafyatua tofali, Walemavu wasiosikia (Viziwi), na Vikundi vya ujasiriamali kwa kina mama (VICOBA) Waziri Mhagama amesema kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imepewa dhamana ya kushughulikia nguzo tisa za kuwawezesha Wananchi Kiuchumi uliozinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu lengo kubwa ikiwa ni ifikapo 2020- 2025 Wananchi wawe wamefika kumiliki uchumi wao  wenyewe.


“Kutakuwa na mahitaji mengi sana katika Migodi hiyo ya Liganga na Mchuchuma. Tutahitaji mashine kwa ajili ya kusaga nafaka, tutaitaji vyakula vya aina mbalimbali, tutaitaji kina mama lishe na biashara nyingine ndogo ndogo za kila aina hizo zote ni fursa za kutuwezesha sisi kujiajiri na kukuza kipato chetu.Hivyo ni vizuri kila mtu aweze kuona ni kwa namna gani anaweza kunufaika na fursa hizo zilizopo mbele yake” Alisema waziri huyo.


Vilevile amesema kuwa ili kuwezesha Wananchi Kiuchumi ipo fursa za kila Halmashauri kutengeneza Madawati ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambapo wateuliwa watapewa mafunzo ambayo yatawasaidia kuwaelimisha na kuwasimamia wananchi ili wananchi waweze kushika uchumi wao wenyewe.


Aidha amesema kuwa kundi la Madereva bodaboda ni miongoni mwa makundi muhimu yatakayonufaika na dawati hilo.

Tunatambua kuwa Madereva  bodaboda  wengi wanaondesha pikipiki si wamiliki halali wa pikipiki hizo wengi wao wanafanya kama vibarua na wengi wameshindwa kumiliki bodaboda zao wenyewe kutokana  na kuwepo kwa  masharti magumu ya uchukuaji mikopo jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa kwao.


Hivyo program hii inalenga kuwafanya Vijana wamiliki Bodaboda zao wenyewe sharti kubwa ya program ikiwa ni Vijana kujiunga na Saccos za Vijana ili waweze kupata Mkopo wenye riba nafuu ikiwa riba  ni asilimia tisa (9%) hadi asilimia kumi(10%) mkopo ukiwa  wa mwaka mzima na baada ya hapo kijana atamiliki bodaboda yake mwenyewe.


Lakini pia program hii itawanufaisha madereva kwani wataweza kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na kufanya utaratibu wa kupata matibabu pindi watakapopata ajali wawapo kazini.


Akiongelea swala la VICOBA kwa kina mama amesema kuwa Serikali imeingia Mkataba na Benki ya Posta ambapo kina mama watapata mikopo kwa riba nafuu ambayo itasaidida wanawake wengi kujiajiri.


Akitoa Maagizo kwenye ziara hiyo waziri huyo ameziagiza Halmashauri zote mkoani  Njombe kuhakikisha kuwa swala la ajira kwa vijana linakuwa moja kati ya agenda za kudumu kwenye Halmashauri zao, na kila Halmashauri ihakikishe inatenga maeneo kwa shughuli mbalimbali za Vijana. Hii itasaidia azma ya serikali ya kuwafanya vijana kujiajiri iweze kutekelezeka lengo kuu ikiwa ni kutokomeza tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekuwa tatizo kwa nchi na duniani kwa ujumla.


Pia ameziagiza Halmashauri Mkoani Njombe kuhakikisha kuwa zinafungua SACCOS za vijana ambazo zitasaidia upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu na Maafisa Ushirika wakague kama SACCOS hizo zipo hai na zinafanya kazi kwa faida ya Mkoa na Vijana kwa ujumla.


 Nae Mwakilishi wa kikundi cha viziwi kutoka Njombe  alitoa kilio chake kwa  waziri kuwa Halmashauri iteue mwakilishi atakayeshughulikia maswala ya walemavu ili nao waweze kushiriki kikamilifu katika fursa hizi za kuwawezesha vijana kujiajiri  na endapo jambo hili litashindikana itakuwa ni sawa sawa na bure kwani nao wanahitaji kufaidika na fursa zilizopo.


Waziri huyo pia ameahidi kuhakikisha kuwa atajitahidi kuwasiliana na wahusika ili kuona ni namna gani wataweza kutatua kero mbalimbali wanazokumbana nazo vijana wanaojiajiri katika shughuli mbalimbali likiwemo swala la kuhakikisha kuwa  katika ngazi ya Mikoa taasisi nyingi za maendeleo ziweze kuwa na matawi ili kurahisisha utendaji kazi na kupunguza gharama za watu kufuata hudumu maeneo ya mbali pia Ameahidi huzichukua na kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na makundi mbalimbali katika ziara hiyo.
IMETOLEWA NA;

AFISA HABARI HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA NA MBUNGE JOSEPH HAULE WAPIGA KAZI PAMOJA MIKUMI

$
0
0
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya wakazi wa kata ya Kidodi,kijiji cha Tungu-Mikumi (hawapo pichani),kwenye mkutano wa kusikiliza na kutoa majibu kuhusu wakulima wa Miwa,pichani shoto ni Mbunge wa Mikumi, Mh Joseph Haule
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mbunge wa Mikumi, Mh Joseph Haule katika Mkutano wa kusikiliza na kutoa majibu kuhusu wakulima wa miwa uliofanyika katika kata ya Kidodi,kijiji cha Tungu-Mikumi .
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Mikumi, Mh Joseph Haule wakifurahia jambo kwa pamoja katika katika Mkutano wa kusikiliza na kutoa majibu kuhusu wakulima wa miwa uliofanyika katika kata ya Kidodi,kijiji cha Tungu-Mikumi .

DKT KAMANI AKUBALI UTENDAJI KAZI WA MBUNGE WA BUSEGA DKT CHEGENI,AKIRI WANANCHI HAWAKUKOSEA KUMCHAGUA.

$
0
0

Mbunge wa Busega Dkt Raphael Chegeni (kushoto) na Mbunge wa zamni wa jimbo hilo, Dkt Titus Kamani ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu walipotaza rasmi kuzika tofauti zao na kushirikiana kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. Pichani viongozi hao walipowadhihirishia wananchi kuwa hawana chuki wala ugomvi tena na kuwa uchaguzi umekwisha, katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye kijiji cha Lamadi wilayni Busega Machi 2, 2016.


ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Busega,Dk Titus Kamani amekubali utendaji kazi wa Mbunge wa sasa wa Jimbo hilo,Dk Raphael Chegeni,akidai kwamba wananchi hawakukosea kumchagua.

Dk Kamani aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Lamadi Wilayani Busega ambao pia Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa alikuwepo .Dk Kamani,amekiri kwamba Dk Chegeni ni mchapakazi na wananchi wa jimbo hilo hawakukosea kumchagua na kwamba anamuunga mkono katika hatua zote anazofanya za kuleta maendeleo jimboni hapo.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na wananchi wangu uchaguzi ulishakwisha na sasa nimeamini mmepata mbunge makini na mchapakazi ,nimetambua sasa kuwa sikustahili kupingana naye ,nitashirikiana naye katika kazi wana busega ni wamoja na wanaCCM tunajenga nyumba moja hatuna haja ya kutokubaliana ikiwa tunaona aliyechaguliwa anafanya kazi nzuri,”alisema Dk Kamani.

Alisema wananchi wa Busega wanampenda Dk Chegeni na CCM kwa ujumla hivyo ni wajibu wa viongozi wengine kumuunga mkono ili kusaidia wananchi wa jimbo hilo na mkoa wa Simiyu kwa ujumla.“Huyu bwana kweli mchapakazi,nilikosea njia kupingana naye sasa namkubali rasmi naona muda mfupi tangu aingie madarakani Busega imeanza kubadilika na mambo yanaenda,wanabusega Chegeni ni Jembe,tufanyeni kazi hakuna uchaguzi hapa umshakwisha,”alisema Dk Kamani.

Kwa upande wake Dk Chegeni alieleza kuwa tofauti zao zilishakwisha na sasa wanafanya kazi ila amefurahi kuona kwamba Dk Kamani ametambua utendaji wake na kuahidi kuendelea kufanya kazi ya kuwatumikia wanabusega.

Dk. Kigwangalla afungua rasmi wadi ya wagonjwa Mahututi ya Mwaisela, Muhimbili

$
0
0
Serikali imesema kwa sasa itakuwa ikihudumia wagonjwa wote ndani ya nchi ikiwemo wale wagonjwa Mahututi ambao awali walikuwa wakipelekwa nje ya nchi. Hii ni baada ya kuendelea kuimarisha huduma hizo pamoja na kuwa na wataalam wa kutosha ambaio watapatiwa mafunzo zaidi.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 3.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kuzindua rasmi wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) iliyopo katika jengo la Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Dk.Kigwangalla katika uzinduzi huo, amewapongeza watendaji wote waliofanikisha ikiwemo uongozi uliopita na ule wa sasa, Serikali pamoja na wadau wa sekta hiyo ya afya walioguswa na kuchangia upanuzi wa huduma za tiba ya wagonjwa hao Mahututi ambayo imewezeshwa kuwa na vifaa tiba vya kisasa huku ikiongezwa vitanda kutoka 8 hadi 25 kwa sasa.

Aidha, Dk. Kigwangalla ametoa shukrani ya kipekee kwa wadau waliojitolea kwa moyo wao kuchangia huduma hiyo ya wagonjwa Mahututi ikiwemo Shirika lisilo la Kiserikali la Gastrenterology Foundation kutoka Ujerumani na wadau wote kwa kuweza kufanikisha huduma hiyo kuweza kupatikana hapa nchini na kupunguza safari za nje ambazo zimekuwa zikiigharimu Nchi fedha nyingi.

kusoma hotuba ya Kaimu Mkurugenzi wa Muhimbili hapa:
Tazama MO tv hapa kuona tukio hilo:
Dk kigwangalla uzinduzi wa wodi ya ICUDk. Kigwangalla akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wadi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika jengo la Mwaisela. Wanaoshuhudia ni Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (kulia) na Prf. Museru kushoto
DK KIGWANGALLA4Dk. Kigwangalla pamoja na viongozi wengine wakiwa ndani ya ICU baada ya uzinduzi huo. Wengine ni Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (kushoto) na kulia ni Prf. Museru ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo.
DKIGWANGALLA2Dk. Kigwangalla akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya uzinduzi huo wa wadi ya wagonjwa mahututi katika jengo la Mwaisela. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).

DK HK 88Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru (kushoto) akisoma hotuba maalum juu ya uzinduzi huo wa wadi ya wagonjwa Mahututi (ICU). Anayefuatia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi. Wengine ni wadau waliowezesha kwa wodi hiyo akiwemo Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Bingwa wa Magonjwa ya tumbo kutoka Misri, Prf. Abdel Meguid.
DK HK LLLNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mheshimiwa Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo katika mkutano huoleo wakati alipokuwa mgeni rasmi mapema leo Machi 3.2016.
DK HK AKIWASILIDk.Kigwangalla akiwasili katika jengo la Mwaisela kwa ajili ya uzinduzi wa wodi ya wagonjwa Mahututi.
DK KIGWANGALLA4397DK. Kigwangalla akisalimiana na mmoja wa wadau wa sekta ya afya wakati alipowasili katika jengo la Mwaisela
DK HK 2Dk Kigwangalla akijadili jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prf. Museru
DK HK UEDk. Kigwangalla akisalimiana na mmoja wa wageni waalika katika tukio hilo
DK KIGWANGALLA3Prf.Maseru akijadiliana jambo na Rais wa shirika la Gastrenterology, Prf. Meinhard Classen (kushoto) na Dk. John wa JKCI.

DK KMlango huo wa kuingia ICU kabla ya uzinduzi rasmi

RC DAR ES SALAAM APIGA MARUFUKU UTOAJI WA VIBALI VYA MALORI YA MIZIGO YENYE UZITO WA ZAIDI YA TANI 10 KUINGIA KATIKATI YA JIJI.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwenye kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kwa mwaka 2016. Kulia ni Zungu Azzan na Kushoto ni Bw. Edward Otieno Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Isaya Mngurumi akichangia jambo kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika Manispaa yake wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akichangia jambo wakati wa wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2016.
Baadhi ya Wabunge wa jiji Dar es salaam wakifuatilia kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam. Kutoka kulia ni Mhe. Bonnah Kalua – Mbunge wa Segerea, Mhe. Faustine Ndugulile – Mbunge wa Kigamboni, Mhe. Zungu Azzan – Mbunge wa Ilala na Mhe. Abdallah Mtolea – Mbunge wa Temeke.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es salaam Muhandisi Julius Ndyamkama akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam kuhusu miradi ya ujenzi wa Barabara inayosimamiwa na Wakala hiyo.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki amepiga marufuku utoaji wa vibali vya malori ya mizigo na magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia katika barabara zote zinazosimamiwa na Manispaa za jiji la Dar es salaam zilizojengwa kwa kiwango cha lami kufuatia barabara hizo kuharibika kwa kipindi kifupi kutokana uzito jambo linaloisababishia Serikali hasara.

Aidha, ameziagiza manispaa za jiji hilo kuweka alama za barabarani zinaonyesha zuio kwa magari yote yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kupita kwenye barabara hizo ili wamiliki na madereva watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka 2016 Mhe. Sadiki Meck Sadiki amesema kuwa Manispaa za jiji hilo zinatenga fedha nyingi za kujenga barabara mpya na kufanya matengenezo ya zile zilizopo ambazo nyingi zinaharibiwa na malori ya mizigo.

Amefafanua kuwa matumizi hayo mabaya ya barabara kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na ukiukwaji wa sheria za barabarani ambapo malori makubwa ya mizigo huegesha na kuziba maeneo ya waenda kwa miguu jambo linalowanyima haki wananchi kutumia maeneo yaiyotengwa kwa ajili yao.

Amesema baadhi ya magari yenye uzito wa tani 40 hudiriki kupita kwenye barabara za huduma (Service road), madaraja na wakati mwingine maeneo ya waenda kwa miguu jambo linalosababisha uvunjaji wa kingo za barabara na milingoti ya taa za barabarani na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinaisababishia Serikali hasara kutokana na gharama ya matengenezo.

“Kuanzia leo katika mkoa wangu ni marufuku kutoa vibali vya magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia kwenye barabara zetu, tunataka barabara zetu zidumu, hatuwezi kuvumilia vitendo vya watu wachache wanaokiuka sheria za barabarani kuharibu barabara zetu, lazima tuchukue hatua Manispaa zinajitahidi kujenga bararaba lakini hazidumu” Amesisitiza Mhe. Sadiki.

Amesema barabara zinazosimamiwa na Manispaa za Dar es salaam zina uwezo wa kuhimili uzito wa tani 10 na kubainisha kuwa kwa kipindi kirefu malori ya tani 40 yamekuwa yakipita kwenye barabara hizo na kuzifanya manispaa kunajenga barabara hizo kila mwaka.

Mhe. Sadiki amesema kuwa ipo haja ya mamlaka zinazohusika na miundombinu ya barabara katika jjiji la Dar es salaam kwa kuwatumia wataalam wa sheria kuanza kuangalia uwezekano wa wamiliki wa vyombo vinavyosababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara kulipa gharama za uharibifu huo.

Kuhusu ulinzi na Usalama watumiaji wa barabara za jiji amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kuchukua hatua na kufanya Operesheni dhidi ya madereva wa pikipiki (Bodaboda) na Bajaji wanaopitisha vyombo vyao vya usafiri kwenye njia za waenda kwa miguu na kusababisha usumbufu na ajali za mara kwa mara kwa wananchi wanaotumia njia hizo.

Pia amezitaka Manispaa za jiji hilo kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es salaam kusimamia maeneo yote yanayotakiwa kujengwa miundombinu ya Barabara ili yasivamiwe na wananchi pamoja na kuwachukulia hatua wananchi wanaofanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa ya hifadhi za barabara na njia za waenda kwa miguu.

‘‘Ninaiagiza manispaa ya Kinondoni kuondoa wafanyabishara wote walioko eneo la kituo cha kuzalishia umeme Ubungo, eneo lile ni hatari kwa usalama na maisha yao, kukaa pale ni kinyume cha sheria’’ Amesisitiza.

Aidha, amesema mwaka 2016 mkoa wa Dar es salaam umetenga jumla ya Shilingi bilioni 343.5 ikilinganishwa na shilingi Biliobi 266.6 zilizotengwa mwaka 2015/2016 kutekeleza ujenzi na matengenezo ya barabara katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo lengo likiwa kupunguza msongamano wa magari.

Kuhusu Kikao hicho cha kwanza cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka 2016 amesema pamoja mambo mengine kimepokea na kujadili tarrifa utekelezwaji wa ujenzi wa miradi ya barabara kwa mwaka 2015/2016 pamoja na kupokea Mpango wa matengenezo ya barabara kwa mwaka 2016/2017.

Ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kuzingatia usafi wa mazingira kwa kulinda miundombinu ya barabara na kuepuka kutupa taka kwenye mifereji ya kupitisha maji ili kuzuia mlipuko wa magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Kipindupindu.

TUUNGE MKONO HAKI SAWA NA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA MAENDELEO.

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

Watanzania na wadau wa haki za wanawake nchini wameshauriwa kuunga mkono haki sawa na ushiriki kwa wanawake katika fursa za uongozi wa kisiasa na kiuchumi na kupima mafanikio yaliyofikiwa na kuweka mipango yenye matokeo makubwa. 

Akitoa taarifa juu ya siku ya wanawake Duniani, Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Wanawake Bi Sihaba Nkinga amesema kuwa siku ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku hiyo ya kila mwaka.

Amesisitiza kuwa wananchi wametakiwa pia kubainisha shuhuda za wanawake waliotoa mchango uliotukuka katika kuwezesha maendeleo ya wanawake na taifa kwa ujumla na Tafakuri hii hufanywa kwa kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo kwa wanawake kwa ujumla.

“Kuanzia mwaka 2005 Serikali ilipitisha uamuzi kuwa, maadhimisho haya yafanyike Kitaifa kila baada ya miaka mitano ili kutoa muda wa utekelezaji wa maazimio na kupima mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano”Alisema Bi Sihaba.

Sihaba Nkinga amewashauri wanahabari wote kuelimisha jamii kuhusu kauli mbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2016 inayosema “50 – 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”, ambapo Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa na mikakati thabiti yenye mwelekeo wa kufikia Agenda ya 2030 yenye malengo ya kufikia asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za maendeleo.

Aidha Bi Sihaba Nkinga amemtaka kila Mtanzania aweze kutambua jukumu alilonalo katika kufikia lengo la ushiriki sawa wa wanawake na wasichana katika Uchumi; Afya, Elimu, Ajira, Sheria na Siasa ifikapo mwaka 2030.

Kwa mwaka 2016, katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani,mikoa yote nchini itazingatia hali na mazingira ya mikoa husika na kwa mkoa wa Dar es Salaam siku hii itaadhimishwa katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa mikoa yote kuhamasisha wananchi na wadau wote kushiriki maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2016.

WAKUU WA MIKOA WAPEWA JUKUMU LA KUTOA VIBALI VYA KUCHANGIA ELIMU

$
0
0
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali imeongeza wigo wa utoaji wa kibali cha uchangiaji wa elimu msingi bila malipo hadi kwa Wakuu wa Mikoa baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zilizowekwa zimefuatwa kikamilifu.
 
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu amesema kuwa awali vibali hivyo vilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pekee ikiwa na lengo la kudhibiti michango holela.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa azma ya Serikali ya kutoa elimu msingi bila malipo haizuii wadau mbalimbali wa elimu kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ambapo wadau wakiamua kuchangia kwa nia ya kushughulikia kero fulani iliyopo katika shule yao au shule zao baada ya kupata kibali wanaruhusiwa kufanya hivyo.

Katika kutekeleza dhana ya utoaji wa elimumsingi bila malipo, hadi kufika mwishoni mwa mwezi Januari, 2016 Serikali inatoa elimu hiyo kwa jumla ya wanafunzi 9,771,902.

Kati ya wanafunzi hao, 8,301,759 ni wa elimu ya msingi na 1,470,143 ni wa sekondari ambao wanapatiwa elimumsingi bila malipo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Serikali inasisistiza kuwa viongozi wanahusika katika kusimamia utekelezaji wake ambapo kwa upande wa wazazi au walezi, kamati na Bodi ya shule pamoja na jamii wao nao wanajukumu la kuelewa majukumu yao ipasavyo.

Aidha, juhudi za makusudi zinapaswa kufanywa na viongozi na watendaji wa elimu ili kuwezesha jamii kufahamu wajibu wao katika utekelezaji wa elimumsingi bila malipo na hatimaye kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Katika kutekeleza wajibu wake, Serikali ya Awamu ya Tano (SAT) kuanzia mwezi Januari, mwaka huu imeanza kutoa elimumsingi bila malipo imetoa waraka wa Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 ambao unaofafanua na kubainisha majukumu ya serikali na wadau mbalimbali katika utekelezaji wa elimu msingi bila malipo.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SALA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA NA AFUNGUA MKUTANO WA WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati, akiwa na viongozi wa Mtandao wa Kingdom Leadership Tanzania Network na Viongozi wa Dini wa Mataifa mbalimbali Duniani, wakati wa uzinduzi wa mpango wa Sala maalum ya kuliombea Taifa utakaofanyika kila mwaka, uzinduzi huo umezinduliwa leo March 03, 2016 katika Hoteli ya Hayyat jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa kitaifa wa Kingdom Leadership Network Tanzania na viongozi wa Dini wa Mataifa mbalimbali Duniani wakati wa uzinduzi wa mpango wa Sala maalum ya kuliombea Taifa utakaofanyika kila mwaka, uzinduzi huo umezinduliwa leo March 03, 2016 katika Hoteli ya Hayyat jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano wa tisa wa siku mbili kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki pamoja na Wabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaojadili kuhusu kupitia kanuni, Sheria na Itifaki zilizotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya Chaguzi zinazofanyika ndani ya Nchi hizo. Mkutano huo umefunguliwa leo katika ukumbi wa LAPF Makumbusho jijini Dar es salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mtandao wa Kitaifa wa Kingdom Leadership Tanzania Network na Viongozi wa Dini wa Mataifa mbalimbali Duniani baada ya uzinduzi wa Mpango wa Sala Maalum ya kuliombea Taifa uliofanyika leo March 03,2016 katika Hoteli ya Hayyat Dar es salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Sheyros Banji nje wa ukumbi wa LAPF Makumbusho jijini Dar es salaam leo March 03,2016 baada ya kufungua mkutano wa tisa wa siku mbili kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki pamoja na Wabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaojadili kuhusu kupitia kanuni, Sheria na Itifaki zilizotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya Chaguzi zinazofanyika ndani ya Nchi hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki pamoja na Wabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungua mkutano wa tisa unaojadili kuhusu kupitia kanuni, Sheria na Itifaki zilizotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya Chaguzi zinazofanyika ndani ya Nchi hizo.mkutano huo umefunguliwa leo Marchi 03,2016 katika ukumbi wa LAPF Makumbusho jijini Dar es salaam. 
(Picha na OMR)

RAIS DKT.MAGUFULI NA RAIS UHURU KENYATTA WAWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA ARUSHA-HOLILI/TAVETA-VOI YA KM 234.3

WATUMISHI WAASWA KUJIEPUSHA NA MATAPELI WA UHAMISHO

$
0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Watumishi wameaswa kuzingatia taratibu za uhamisho na wametakiwa kuwa makini na utapeli pamoja na upotoshaji unaofanywa kupitia mitandao ya kijamii na matangazo mbalimbali yanayowataka kulipia pesa ili kupata uhamisho.

Aidha, Serikali imewaonya watu wote wanaoghushi na kutumia vibaya nembo yake pamoja na mihuri kwa lengo la kuwalaghai wananchi na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo jijini Dar es salaam, Msemaji wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu amesema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayepatikana na hatia ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha kwa njia isiyo halali baada ya kuwarubuni wananchi.

Taarifa hiyo ya Serikali inafuatia kuzagaa kwa upotoshaji unasosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na matangazo yanayoeleza kuwa baada ya mtumishi kutuma maombi kwa Katibu Mkuu TAMISEMI na kukubaliwa, Katibu Mkuu atamtuma Afisa wake atakayepeleka majibu ya uhamisho na kumtaka mtumishi aliyeomba uhamisho kumgharimia anapompelekea uhamisho jambo ambalo siyo kweli.

Kwa mujibu wa TAMISEMI, miongoni mwa watu wanaosambaza taarifa za upotoshaji ni Charles Machali ambaye amejipachika cheo cha Afisa Mdhibiti Uhamisho na anapatikana kwa simu Na. ni0782 803783 na 0674 583941 na barua pepe yake ni charles53gachari@gmail.com.

Baada ya taratibu za uhamisho kukamilika, Serikali hutangaza majina ya watumishi waliopata uhamisho kupitia tovuti ya Wizara ambayo ni www.tamisemi.go.tz.

Taratibu za kawaida za uhamisho zinamtaka mtumishi kupitishia barua kwa kiongozi wake mahali anapofanya kazi na katika mkoa wake ambao ndio una jukumu la kuleta maombi hayo kwa Katibu Mkuu TAMISEMI.

WAZIRI MKUU AAGIZA KIKAO KUJADILI USHURU WA MAZAO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Kamati ya Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikutane na wafanyabiashara wote ili wajadiliane na kupanga kiwango cha ushuru kinachopaswa kutozwa kwenye mazao ya wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 3, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Dutwa, Wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.

Amefikia uamuzi huo baada ya kuona bango lililoshikwa na wananchi wakilalamikia kutozwa ushuru wa sh. 3,000/- kwa gunia moja la mazao badala ya sh. 1,000/- ya zamani.

"Masuala ya ushuru ni maamuzi baina yenu na Halmashauri yenu lakini hiyo tozo imeongezwa sana kutoka sh. 1,000/- hadi sh. 3,000/-. Ninaiagiza Kamati ya Ucumi ikae na wafanyabiashara wote ili mjadili suala hili na mkubaliane kiwango cha ushuru."

"Wabunge pia waalikwe kwenye kikao hicho na Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na Baraza la Madiwani nalo pia lishiriki kikao hicho. Kama mnataka kupandisha ushuru ni lazima mkubaliane viwango ili Watanzania wafanye biashara wakiwa na mapenzi na nchi yao," alisema huku akishangiliwa.

Hata hivyo Waziri Mkuu alifafanua kwamba suala la kulipa ushuru ni la muhimu katika kuchangia makusanyo ya kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi. "Ushuru ni lazima ulipwe lakini pia ni lazima muwe mmekubaliana ni kiwango gani mnatoza. Makusanyo yote haya tunayofuatilia kwa sasa ni matokeo ya watu kulipa kodi na ushuru kama huu," alisisitiza.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amekataza tabia ya maafisa wa kutoza ushuru kudai fedha kabla mwananchi hajauza mifugo wanapoileta mnadani kwani anakuwa amekuja kutafuta fedha.

Alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na mbunge wa viti maalum (CHADEMA), Bi. Gimbi Masabo ambaye alimweleza Waziri Mkuu kwamba kuna tabia ya kutoza sh. 6,000/- kwa kichwa kwa kila ng'ombe anayeswagwa kuingia eneo la mnada bila kujali kama mtu huyo ameuza ng'ombe au hajauza.

"Hivi unawezaje kumtoza mtu ushuru wakati hajauza chochote au wakati akiwa njiani kuelekea mnadani? Ni bora umtoze mtu baada ya kuuza. Kumbukeni kuwa wananchi wetu wanakuja mnadani ili wauze na kupata fedha ya kurudi nayo nyumbani, sasa nyie mnamtoza kabla hajauza chochote au hata kama hajauza. Acheni hiyo tabia," alisema.

Alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Robert Lweyo aimarishe usimamizi wa minada na kujua idadi ya mifugo ambayo inaingizwa, inayouzwa na ile inayobaki ambayo imeshindikana kuuzwa.

"Jipange wewe Mwenyekiti na timu yako ya watoza ushuru mfuatilie agizo hili. Mkiwa wavivu ndiyo mnakuja na maamuzi haya ya jumla jumla ya kuanza kutoza ushuru hata mtu akiwa njiani anakuja mnadani kutafuta fedha," alisema Waziri Mkuu.

Mapema, akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Bw. Ponsiano Nyami alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi kwa sababu majengo ya iliyokuwa ofisi ya wilaya hivi sasa yanatumiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hali iliyowalazimu wahamie kwenye ofisi za Halmashauri.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MACHI 3, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA ZIARA BARIADI NA KUZINDUA BWAWA NA OFISI YA CCM.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana  na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Dutwa  akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi3, 2016.Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum , Esther Midimu. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitaka maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga kuhusu madai kuwa askari wa Usalama Barabarani mkoani  humo wanawatoza faini kubwa hadi sh 300,000/= waendesha bodaboda. Alikuwa katika mkutano wa kuwaslimia wananchi kwenye kijiji cha Dutwa wilayani Bariadi Machi 3, 2016.

 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua ujenzi wa nyumba ya kuishi ya Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi akiwa akika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016.


 Wasanii wa Bariadi wapiga ngoma wakati Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipowasili kwenye bwawa la Ng'wansubuya wialayani Bariadi kufungua bwawa hilo Machi 3, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifurahia baada ya  kufungua bwawa la umwagiliaji la kijiji cha Ng'wasubuya wilayani Bariadi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua Bwawa la umwagiliaji la kijiji cha Ng'wasubuya  wilayani Bariadi akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016.
  Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akiweka jiwe la msingi la Ofisi ya CCM ya wilaya  ya Bariadi akiwa katika  ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NACTE YAFUNGUA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 .

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk. Adolf Rutayuga, (Kulia) akisisitiza jambo wakati alipokuwa ikitangaza wa kuzindua Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)   Katikati ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora Rasmalimali watu , Edmund Kinwasi na Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  Ufuatiliaji  Tathimini na Uthibiti wa baraza hilo , Christina Kumwenda. Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk .Adolf Rutayuga,  akipofya kitufe cha komputa  kuashiria Uzinduzi  rasmi wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)  wanaoshuhudia kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  Ufuatiliaji  ,Tathimini na Uthibiti ,Christina Kumwenda,  Mkurugenzi  udhibiti  ubora  rasmalimali watu Edmund Kinwas, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Vyuo ushauri na Mipango Alfred Kilasi,Mkurugenzi Mafunzo na Upimaji Bakari Issa (kushoto) na  Afisa Mifumo ya Kompyuta wa baraza hilo , Daud Mabena.Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt .Adolf Rutayuga(Kushoto) akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) kuhusiana na Uzinduzi  wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree)    wapili kushoto ni   Mkuu wa Kitengo cha Udahili Seremani Majindo, Mkurugenzi wa Mfumo na Upimaji,Bakari Issa  na  Kaimu Mkurugenzi Idara ya vyuo na ushauri na Mipango.Uzinduzi huo ulifanyika leo jijini Dar es Salaam 

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), limetangaza ufunguzi rasmi wa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)) kwa mafunzo yanayoratibiwa na Baraza kwa mwaka wa masomo wa 2016/17. Mfumu huo, utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (“Bachelor Degree”).


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maelekezo na Msaada kwa Taasisi wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga amesema kuwa, kwa mwaka wa masomo wa 2015/16, Baraza liliratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za astashahada (Cheti) na stashahada (Diploma) kwa mafunzo ya afya na ualimu yaliyoidhinishwa na Baraza. ameongeza kuwa, Baraza pia  lilishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbali mbali kwa kozi za shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System (CAS)).

“Mifumo hii miwili ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha  waombaji kudahiliwa. Mifumo hii ya udahili imekuwa na mafanikio yafuatayo: Kudhibiti udanganyifu katika udahili uliotokana na baadhi ya waombaji kutumia vyeti vya bandia, kuwapunguzia waombaji gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali, kuondoa uwezekano wa mwombaji udahili mmoja kudahiliwa zaidi ya mara moja na kuwanyima waombaji wengine nafasi, kuiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji udahili kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu nchini, na kuwawezesha waombaji udahili kujiunga na mafunzo kwenye taasisi zinazotambuliwa na Serikali,” alieleza.


Dk Rutayuga alieleza kuwa, kwa kutambua mafanikio ya udahili wa pamoja  yaliyopatikana,  Serikali ya kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imeamua kuwa maombi yote ya udahili kwa ajili ya mafunzo ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (Bachelor Degree) yafanywe kupitia kwenye Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS). 


Amefafanua kwamba. Baraza linautangazia umma kuwa, kuanzia mwaka wa masomo 2016/2017 udahili wa kozi zote nchini utafanywa kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaosimamiwa na NACTE, Vyuo Vikuu  na taasisi za Elimu zote nchini Tanzania zinazotoa mafunzo ya Cheti na Diploma kutodahili wanafunzi nje ya mfumo wa udahili wa Pamoja kuanzia mwaka wa masomo 2016/17.


“Tunapenda kutoa taarifa pia kuwa, maombi ya kujiunga na kozi za Cheti na Diploma yataanza kupokelewa rasmi kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana. Baraza pia litaanza kupokea rasmi maombi ya kujiunga na kozi za Shahada (Degree) kwa wahitimu wenye Diploma kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja kuanzia tarehe 4 Machi 2016, saa sita mchana,” 


Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuomba mafunzo kwa kutumia Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS), alisema Baraza linashauri waombaji watembelee tovuti ya Baraza ambayo ni www.nacte.go.tz.

RAIS MAGUFULI NA RAIS KENYATTA WAWEKA JIWE LA MSINGI BARABARA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Arusha hawapo pichani kabla ya ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwaongoza Marais wa Kenya, Uganda, Makamu wa Rais wa Sudani Kusini pamoja na Burundi kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwagilia mti maji pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya sherehe za unzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya sherehe za uzinduzi wa barabara hiyo kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara hiyo ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Tengeru nje kidogo ya Jiji la Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Uganda, Yoweri Meseveni na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukipigwa kabla ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA IKULU

BEI YA MADAFU LEO.

WANANCHI WAOMBWA KUTOA MAONI KUBORESHA SERA MPYA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI.

$
0
0
:Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaamkuhusu uchangiaji wa maoni katika sera ya utamaduni inayofanyiwa mabadiliko. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani KitogoPicha na: Genofeva Matemu – Maelezo.
Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sera ya utamaduni ya mwaka 1997 ambayo inafanyiwa mabadiliko wakati wa mkutano na waandishi wa habarileo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Zawadi Msalla.

………………………………………………

Beatrice Lyimo – MAELEZO

Dar es Salaam.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kutoa maoni na mapendekezo ili yatumike kuboresha Rasimu ya Sera mpya ya Maendeleo ya Utamaduni ya mwaka 2016 itakayochukua nafasi ya Sera ya Maendeleo ya Utamaduni ya mwaka 1997.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Lugha wa Idara ya Utamaduni wa wizara hiyo Bi. Hajjat Shani Kitongo wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kuifanyia mabadiliko Sera ya mwaka 1997 ili iweze kukidhi mahitaji na mabadiliko ya kijamii.

Amesema maoni yatakayotolewa na wananchi yatajikita katika maeneo yanayothamini na kuenzi Maadili, Mila na Desturi, kuendeleza matumizi Sanifu na Fasaha ya Lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa, kuwa na tafiti endelevu za Lugha za Asili kwa ajili ya kuzihifadhi na kuongeza misamiati ya Lugha ya Kiswahili.

Ameongeza kuwa maboresho hayo yanalenga kuwa na bidhaa na miundombini endelevu katika Tasnia ya Filamu na michezo ya kuigiza yenye viwango vya ubora vya kitaifa na kimataifa vinavyozingatia Mila, Desturi na maadili ya Taifa, pamoja na kuwa na uwekezaji endelevu na mfumo jumuishi wa utaratibu wa kazi katika sekta ya utamaduni.

Bi. Kitongo amefafanua kuwa wananchi watatuma maoni yao kupitia barua pepe au kuleta maoni yao kwa mkono moja kwa moja Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo au kutuma maoni kupitia barua pepe, christopher.mhongole@habari.go.tz pia kupitia tovuti ya wizara ya www.habari.go.tz.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo Mwanzala Kayoka amesema kuwa lengo la kufanya mabadiliko hayo ni kuboresha Sera hiyo kulingana na wakati haswa katika matumizi salama na sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Sekta ya Utamaduni.

“Lengo ya kuleta mabadiliko katika Sera hii si kuunda Sera mpya bali ni kuiboresha kulingana na wakati na kuongenza yale yaliyopungua haswa katika mfumo wa TEHAMA hivyo hupelekea kuleta mfumo sahihi wa kuratibu masuala ya Utamaduni nchini” Ameongeza Mkurugenzi huyo.

Amesema kuwa ukusanyaji wa Maoni hayo umeanza Machi 4, 2016 hadi Machi, 25 Mwaka huu, na kuwaomba wadau na wananchi wote kushiriki kikamilifu kutoa maoni yatakayosaidia uboreshaji wa Sera ya Maendeleo ya Utamaduni ya mwaka 2016.

MALALAMIKO YANAYOHUSU UPATIKANAJI WA HAKI KUSHUGHULIKIWA KWA WAKATI.

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria  Bi Farida Khalfan (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo Pichani) kuhusu utaratibu wa Wizara katika kupokea na kushughulikia malalamiko yanayohusu upatikanaji wa haki kwa wananchi. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya malalamiko  Grifin Mwakapeje na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Ufatiliaji Haki Bi Mary Mrutu.
 Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Grifin Mwakapeje akitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta ya Sheria kuendelea kutumia huduma ambazo zinazotolewa na Wizara hiyo ili kuwezesha kupata haki kwa wakati. 
                Mkurugenzi Msaidizi Ufatiliaji Haki Bi Mary Mrutu kutoka Wizara ya Katiba akifafanua kwa waandishi wa habari (Hawapo Pichani) mamlaka ya Waziri wa Katiba na Sheria katika kuongeza muda wa ukomo wa kufungua mashauri ya madai mahakamani.

Na Frank Mvungi-Maelezo.
SERIKALI imedhamiria kuendelea kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi yanayowasilishwa ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Malalamiko kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Griffin Mwakapeje wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

aAidha , Mwakapeje amesema Wizara hiyo imekuwa ikipokea malalamiko yanayohusu ucheleweshwaji wa utekelezaji wa amri mbali mbali zinazotolewa na mahakama,ucheleweshaji wa nakala za hukumu na mienendo ya mashauri baada ya kumalizika mahakamani.
Malalamiko mengine yanahusu msongamano wa mahabusu, ucheleweshwaji wa upelelezi,wananchi kubambikiwa kesi,migogoro ya ardhi navitendo vya rushwa.

Akizungumzia wajibu wa  Wizara hiyo Mwakapeje amesema ni kuyaratibu na kuyawasilisha kwenye taasisi husika ili kupata muafaka wa malalamiko hayo kwa wakati.

Hatua nyingine inayochukuliwa na Wizara katika kuwasaidia wananchi kupata haki kwa wakati, ni kutoa msaada wa kisheria unapohitajika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo ili kuwawezesha wananchi kupata haki kwa wakati.
Katika kushughulikia malalamiko hayo “Serikali inayo dhamira ya dhati yakuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki kwa wakati.” Amesema Mwakapeje.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi Farida Khalfan akizungumzia Mfumo wa kupokea malalamiko amesema kuwa wananchi wanaweza kufika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo mtaa wa Sokoine au kuandika barua ili kuwasilisha malalamiko yao na yatafanyiwa kazi kwa wakati.

Wizara ya Katiba na Sheria ina Dhamana ya Kusimamia masuala ya Katiba na Sheria ambapo inatoa huduma mbali mbali za kisheria kwa wananchi,mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

MKUTANO WA PAMOJA WA WADAU KATIKA KUIMARISHA MPANGO WA TAIFA WA KUMLINDA MTOTO ZANZIBAR.

$
0
0
 Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia Watoto (Save the Children) Zanzibar Mali Nilson akitoa muhtasari wa vipengele 2 vya Taifa vya kulinda Mtoto katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Ocean Vuw Mjini Zanzibar.

 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa pamoja wa wadau wa kumlinda Mtoto, wakifuatilia Mkutano huo.
 Hakim wa Mahakama ya Watoto Zanzibar Bi. Sabra Ali Muhamed akizungumzia juu ya taratibu za kisheria pindi Mtoto anapopelekwa Mahakamani.
 Afisa Mipango wa haki za Mtoto kutoka Ubalozi wa Swiden Dar es Salaam Joyce Tesha akielezea umuhim wa kuunga mkono jitihada za kuimarisha ulinzi wa Mtoto katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Ocean Vuw Mjini Zanzibar.
 Mtoto Suhaila Mwarimwana ambae ni Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya ushauri ya Watoto akizungumzia ushirikishwaji wa Watoto katika kutambua haki zao.


Mkurugezi wa Program ya maendeleo na ubora wa Shirika la kuhudumia Watoto Duniani Bi Lisa Parrott akisisitiza kitu alipokuwa akifunga Mkutano wa pamoja wa wadau Watoto ulifanyika Hoteli ya Ocean Vuw Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

SUMATRA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDAKTA WOTE WATAKAOWATOZA ABIRIA NAULI KUBWA TOFAUTI NA ZILIZOPANGWA

$
0
0

Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Usafiri wa Majini na Nchi Kavu  (SUMATRA) Mkoa wa Kilimanjaro  kuwafikisha mahakamani madereva wote na makondakta wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na zilizopangwa na ofisi hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Afisa Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa akijibu kero ya mkazi wa mkoa huo kwa njia ya simu iliyotolewa na Gazeti  la Mwananchi Machi 04, mwaka huu,iliyozungumzia  daladala zinazofanya safari zake kati ya Moshi Mjini - Himo kuwatoza nauli ya shillingi 1000 abiria wanaoshuka maeneo ya Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road tofauti na nauli iliyopangwa na SUMATRA katika vituo hivyo.  

“Kuanzia wiki ijayo wadau wote  watakao kuja kuomba leseni kwa ajili ya usafirishaji wa abiria ndani ya mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli watakazo toza abiria katika vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho cha safari zao,”alisema Bw.Mwita.

 Bw.Mwita alisema hivi sasa SUMATRA Mkoa wa Kilimanjaro  imeanzisha utaratibu wa kuwataka wadau wote wanaotarajia kuanza kutoa huduma za usafiri wa daladala mkoani hapo kuonyesha nauli watakazo toza katika  vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho.

 Hata  hivyo Afisa huyo aliwashauri wakazi wa maeneo kama kiboriloni kwa sasa kupanda daladala za Kiboriloni kwa kuwa zipo nyingi ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images