Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live

MAWAZIRI WOTE WAJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12 leo jioni limetekelezwa.

Waziri Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo.

“Hadi kufikia saa 9.30 leo alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote walikuwa wamekamilisha fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.

Rais Magufuli leo asubuhi alitoa maelekezo kwamba Mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni ifikapo leo Ijumaa tarehe 26 Februari, 2016 saa 12.00 jioni wawe wamejaza na kurejesha Fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam. Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, FEBRUARI 26, 2016.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa dini kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salam Februari 26, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Baadhi ya viongozi wa dini wanaunda kamati ya amani ya Dar es salam na baadhi ya mikoa nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Elinaza Sendoro baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu, Alex Molasses baada ya kuzungumza na Viongozi wa Dini kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini baada ya kuzungumza nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererejijini Dar es salaam Februari 26, 2016.

SOMA VICHWA VYA HABARI MBELE NA NYUMA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI

$
0
0
Karibu katika magazeti ya jumamosi 27 Februari 2016. Pitia kwa ufupi nyuma nabmbele ya magazeti haya.
Add caption

HUYU NDIYE RAIS MPYA WA FIFA

$
0
0

Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani FIFA.

katibu huyo mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja.
Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.

Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum'baini mshindi wa moja kwa moja.Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.

Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita . 

Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ''kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa''.

HAYA NDIYO YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE

$
0
0
Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kuwataka waandishi wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na watafiti kuweka hadharani na kuueleza umma kile kilichotokea Zanzibar, Waandishi na watafiti mabalimbalai wamejitokeza na vielelezo vinavyoeleza jinsi uchaguzi huo ulivyoharibika

Vielelezo hivyo ni Nakala za fomu namba MUR. 12A za matokeo zilizotoka katika vituo vya kujumuisha kura ambazo zilikuwa zimejazwa kimakosa.
Hii ni fomu kutoka Kituo cha Skuli ya Mabaoni namba 23801, Jimbo la Chonga namba 2909 fomu hii siyo halali kutokana na kukosa mhuri wa tume ya uchaguzi Zanzibar. Msimamizi wa kituo ni Khamis mkungwa Zaid.

Fomu nyingine inatoka katika kituo cha Urusi chenye namba 26503, katika jimbo la Jang’ombe namba 1940

A. Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008
Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008, Jimbo la Mkwajuni namba 1926, fomu hii imepoteza uhalali kwasababu imefutwafutwa na haina mhuri wala jina la msimamizi wa kituo.

B. Kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi
Hii ni fomu kutoka katika kituo cha Skuli ya Mwembe Makumbi namba 21618, Katika jimbo la Chumbuni namba 1931, fomu hii imekosa uhalali kwasababu imefutwa majina ya mawakala na kupandikizwa majina mengine juu ya maandishi ya kivuli.

C. Jimbo la Chumbuni namba 1937
Hizi mbili, fomu kutoka kiwanja cha mpira Masumbani namba 29304 kutoka jimbo la Chumbuni namba 1937, fomu hii inakosa uhalali kwa sababu haina mhuri , maandishi ya meandikwa tena kwa kalamu juu ya maandishi ya kivuli na saini imewekwa zaidi uya mara moja. Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu inamhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.

D. Mihuri ya kughushi
Fomu ya pili ni kutoka jimbo la Chakechake jina la kituo na namba haisomeki, fomu hii inakosa uhalali kwasababu ina mhuri ambao siyo wa Tume ya uchaguzi anzibar ni mhuri wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar ambao haupaswa kutumika katika fomu hii.

Matumizi ya Mihuri Bandia katika karatasi za kujumuishia matokeo ya wagombea nafasi ya Rasi wa Zanzibar.

E. Fomu zimejirudia zaidi ya mara moja
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa ZEC alisema utata wa matokeo ulianza pale wajumbe waliopelekwa Pemba kurudi na kuiarifu Tume dhidi ya matendo yaliyofanywa na wasimamizi wa ZEC Pemba hata hivyo wakati uchunguzi na mabishano yakiendelea Mmoja wa wagombea akaitisha wanahabari na kujitangaza ameshinda kwa matokeo ambayo kila mmoja wetu alishangaa sana,

Ni kitendo cha aibu na Fedheha kubwa wanaoshabikia hawakuona madhara yake,sijui alitoa wapi Takwimu ambazo zilitoa ushindi kwa wagombea wawili tu,tena ukijumlisha asilimia ni 100 inasikitisha sana,Shinikizo la kunitaka nimtangaze mshindi kinyume na taratibu lilinifanya niubebe msalaba kusimamisha na kufuta matokeo baada tu ya kuitisha fomu chache za uthibitisho mwandishi haya ndio tuliyakuta,Ni nusu ya uchaguzi wote kila jimbo ulichezewa

Tumejiridhisha watu wetu watendaji wa ZEC walio apa walifanya haya,kutumia mihuri ya Bandia kujaza hizi fomu kinyume na taratibu kama mnavyo ona alisisitiza Mzee Jecha kwa masikitiko akiwaonyesha waanndishi waliofika kuhoji nini kilitokea hasa.BLOG http://zanzibariamani.blogspot.com/

magonjwa ya mifugo ,majanga ya moto ni tatizo katika hifadhi ya mkomazi

$
0
0
Waandishi wa habari wakiwa wanamuangalia mnyama aina ya kobe aliopo ndani ya hifadhi ya mkomazi

Na Woinde Shizza,Same

Vita dhidi ya magonjwa ya mifugo ,majanga ya moto ,ongezeko la watu pamoja na ukame  ni changamoto kubwa inayoikabili hifadhi ya taifa ya Mkomazi ilipo wilayani same Mkoani Kilimanjaro ambapo imesababisha baadhi ya wanyama ambao ni vivutio vikubwa katika hifadhi hiyo kutoweka  .



Hayo yamebainishwa na afisa utalii mwandamizi  wa hifadhi ya mkomazi   Pellagy Marandu wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo kujionea vivutio ambavyo vinapatikana ndani ya hifadhi hiyo.



Alisema changamoto hizo zimekuwa zinaletwa na wafugaji ,wakulima ambao wamekuwa wanaleta wanyama ndani ya hifadhi ambapo alibainisha kuwa wanyama wengine wanaweza wakawa na magonjwa ya kuambukiza hivyo wanapoingia ndani ya hifadhi wanaweza kuambukiza wanyama walioko hifadhini hali ambayo inaweza kusababisha janga kubwa kwa hifadhi.

“kwa upande wakulima wamekuwa wakileta madhara wakati wa kuandaa mashamba yao kwa ajili ya kilimo ambapo wamekuwa wakiaribu mazingira kwa kuchoma moto mabaki ya mazao ambayo walipanda msimu uliopita “alisema Marandu



Aidha ilikukabiliana na changamoto hizo wamekuwa wakifanya doria kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi ambao ni ujirani mwema ambapo wamekuwa wakiweza kufichua wale wote ambao wanaingiza mifugo ndani ya hifadhi kinyume cha sheria ambao wamekuwa wakipigwa faini huku wengine wakifikishwa mahakamani .



Kwa upande wake mkuu  wa hifadhi ya Mkomazi Donat Simon Mnyagatwa Alisema kuwa mbali na kuwepo na changamoto hiyo ya kuingiza mifugo ndani ya hifadhi pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji ambapo alibainisha  kuwa  hili ni tatizo kubwa  linaloikabili hifadhi hiyo kwani maji ni uhai ,kuanzia kwa binadamu na hata kwa wanyama .


“Ni kweli ili nitatizo kubwa lakini pia tumeanza kuandaa mipango mathubuti  kwa ajili ya kutatua tatizo hili ambapo kwa upande wa binadamu tupo kwenye mkakati wa kuanza kuchimba visima virefu ili kuweza kupa maji mengi ambayo pia maji hayo yataweza kukusanywa kwa pamoja kwa ajili pia ya wanyama wetu,pia tunampango wa kuongeza mabwawa yaliyopo ndani ya hifadhi ili kuakikisha pia tunaondokana na changamoto hiyo”alisema Mnyagatwa



Aidha alibainisha kuwa mbali na changamoto hiyo pia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundo mbinu ya barabara pamoja na nyumba za kuishi watumishi ambapo alisema kuwa mpaka sasa zaidi ya familia tisa zinaishi ndani ya hifadhi  huku familia zingine zikiishi nje ya hifadhi ,pamoja changamoto hizo ameiomba Halmashauri ya same kupitia Tanroad kurekebisha barabara ya kuelekea hifadhini ili iweze kupitika kwa urahisi kwa kipindi chote.


Mnyagatwa alibainisha kuwa kwa lengo la ujirani mwema wananchi ambao wamekuwa wakizunguka hifadhi wamekuwa wakipatiwa mafunzo maalumu ya kutambua umuimu wa utunzaji wa hifadhi pamoja na kutambua mipaka ya hifadhi na athari za kuingiza wanyama hifadhini ,mathara ya uaribifu wa mazingira ambapo alisema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaelimisha na elimu hii imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhalifu ndani ya hifadhi.

KAAZI KWELI KWELI

MAJALIWA AWASILI MTWARA KWA ZIARA YA SIKU MOJA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mtwara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege ea Mtwara kwa ziara ya siku moja mkoani humoFebruari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MABADILIKO YAFANYIKA NDANI YA JESHI LA POLISI,BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA WAPANGULIWA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda  wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. 

 Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe. 

Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi. 

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.

Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.

Imetolewa na:

Advera Bulimba-SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi (T)

Makao Makuu ya Polisi.

ZIARA YA WAZIRI MKUU MAJALIWA – MTWARA

$
0
0
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara Februari 27, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara Februari 27, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya TPDC baada ya kuwasili kwenye mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini kukagua shughuli za gesi Februari 27, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPDC baada ya kutembelea mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini Februari 27, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kuchakata gesi wakati alipoutembelea Februari 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada ya kuzungumza nao chuoni hapo , Februari 27, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada ya kuzungumza nao chuoni hapo , Februari 27, 2016. 

MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO AZANGUMZA NA WAZEE NA KUWAPA MSAADA WA MAGUNIA 100 YA MAHINDI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona, (kulia) akiwazawadia wazee wa Mji mdogo wa Mirerani sh 50,000  baada ya kuzungumza nao na kuwakabidhi msaada wa magunia 100 ya mahindi yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga.
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona, (kulia) akiwazawadia wazee wa Mji mdogo wa Mirerani sh50,000  baada ya kuzungumza na wazee wa mji huo na kuwakabidhi msaada wa magunia 100 ya mahindi yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona, akigawa kwa wazee wa mji mdogo wa Mirerani, moja kati ya magunia 100 ya mahindi ya msaada yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga, kwenye ofisi za Sawata.
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona, akizungumza na wazee wa mji mdogo wa Mirerani na kuwagawia msaada wa magunia 100 ya mahindi ya msaada yaliyotolewa na Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga, kwenye ofisi za Sawata.

Sherehe ya Kipindi cha Sports headquarters kutimiza mwaka mmoja wa mapinduzi ya michezo

$
0
0
Pichani Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata keki ya birthday ya kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake.

 Efm 93.7 Radio kupitia kipindi chake cha Sports headquarters kimesheherekea  kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake  February 2015, hafla hiyo ilifanyika pale City Sports Lounge na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo akiwemo Waziri wa Habari, utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kama mgeni rasmi. Nikipindi pekee kilicholeta mapinduzi zaidi ya michezo kwa utangazaji na uchambuzi yakinifu nchini. 
Mkurugenzi Mtendaji wa EfmRadio Frances Ciza akimlisha keki mgeni rasmi wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja kwa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Head Quarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa na watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio jana jijini Dar es Salaam.Kipindi hicho kimetimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwake
Watendaji wa kipindi cha Makao Makuu ya Michezo (Sports Headquarter) kinachorushwa hewani kupitia 93.1 Efm Radio wakiserebuka kwa furaha City Sports Lounge jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Simba SC Haji Manara akimsikiliza Afisa habari wa TFF,Baraka Kiziguto akihutubia kwenye hafla hiyo

NAIBU WAZIRI WA AFYA. DK KIGWANGALLA AKUTANA NA WATAALAM WA MPANGO WA BRN WA WIZARA YAKE

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akutana na Wataalam wanaoshughulikia mpango wa BRN wa wizara yake.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo Februari 27.2016 amekutana katika kikao maalum na Wataalam wa Wizara hiyo ambao wapo katika timu inayoshughulikia Mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN) katika kufanikisha namna ya utoaji huduma bora na ufanisi katika mipango mbalimbali ya kufikia malengo ambayo Serikali ya Tanzania ilianzisha mpangp huo.

Dk. Kgwangalla amekutana na wataalam hao kwa mara ya kwanza, ilikupata mrejesho na kuelewa kiundani namna Wizara yake inavyotekeleza mpango huo wa matokeo makubwa sasa (BRN). Aidha, Sekta ya Afya ni ya nane (8), katika Sekta zinazotekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN).

NB: Waweza kusoma zaidi juu ya Wizara ya Afya na mpango huo wa BRN kwenye taarifa yake iliyotoka mwaka 2015. Bonyeza hapa: http://ehealth.go.tz/admin/rmo_materials/2.4.%20BRN.pdf
DK KIGWANGALLAWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN). Katika mkutano huo leo Februari 27.2016, jijini Dar es Salaam.
DK hk7Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (Kushoto) akisikiliza kwa umakini masuala mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN). Mkyano huo unafanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, leo Februari 27.2016.
dk hk 80Wajumbe wa BRN wa Wizara ya Afya wakitoa maelezo yao mbalimbali kwa Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
DK KIGWANGALLA BRN67Wajumbe wa BRN wa wizara ya Afya wakifuatilia kwa umakini mkutano huo na Naibu Waziri (hayupo pichani)

dk hk jjjaNaibu Waziri Dk.Kigwangalla akisikiliza kwa umakini pamoja na wajumbe wengine katika mkutrano huo ambao amekutana na wajumbe wa timu ya wataalam wa Wizara yake hiyo wanaoshughulikia masuala ya BRN.
dk kigwangalla BRNMjumbe wa Wizara hiyo anayeshughulikia mpango wa BRN, Bw. Benard Konga akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla katika mkutano huo
dk hkii
DK KIGWANGALLA2Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN).
dkk hk21Mkutano huo ukiendelea..
DK KIGWANGALLA6Wajumbe wa Wizara ya Afya wanaoshughulikia mpango wa BRN wakifanua jambo.
dk hk7wNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN).DK KIGWANGALLA BRN67Baadhi ya Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN) wakifuatilia mkutano huo mapema leo Februari 27.2016, katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Dk Kigwangalla BRN3 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akisikiliza mambo mbalimbali kutoka kwa Wataalam wa timu ya Wizara hiyo ya Afya ambao wanashughulikia mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN) katika kikao maalum alichokutana nacho mapema leo Februari 27.2016, katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI LIGI YA MPIRA WA KIKAPU - JUNIOR NATIONAL BASKET ASSOCIATION (JR.NBA)

$
0
0
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya mitoano  Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana,  katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizinduwa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA),leo jijini Dar es Salaam. 
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster, leo jijini Dar es Salaam
Sehemu ya mashabiki wa  Mpira wa kikapu   walio fika katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MHE. WILLIAM LUKUVI AWAAGIZA VIONGOZI KULINDA MAENEO YA WAZI

$
0
0
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kizungumza na Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa (hawapo pichani) juu ya kuwawezesha viongozi katika ngazi ya Mitaa kusimamia na kulinda maeneo ya wazi ,miundombinu na maeneo mengine ya umma.( Katikati) ni  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi na kulia ni Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Profesa.John Lupala
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonesha  Ramani Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa
Sehem ya Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa wakiwa  katika mkutanohu uklio fanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

AFISA UHUSIANO TTCL AFARIKI DUNIA

$
0
0
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga enzi za uhai wake.

OFISA Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Amanda Fredrick Luhanga, amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 27, 2016. Taarifa ya kifo cha Bi. Amanda imethibitishwa na Meneja Uhusiano wa TTCL, Bw. Nicodemus Thom Mushi.

 "...Ni kweli, Bi Amanda amefikwa na umauti akiwa likizoni mkoani Mbeya alikokwenda kuwasalimu ndugu zake.. Aliugua ghafla Alhamisi hii na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo Mungu alimchukua," alisema Bw. Thom Mushi.

 Alifafanua kuwa mwili wa marehemu utasafirishwa siku ya Jumapili, kutoka Mbeya kwenda Njombe na Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu tar 29.02.2016 katika Kijiji cha Mlangali, Ludewa, Mkoa wa Njombe. Mtandao huu unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Bi. Amanda Fredrick Luhanga kwa msiba mkubwa uliowafika.  Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Apumzike kwa Amani.

LEO MAGAZETINI

$
0
0
 
Leo jumapili ya 28 Februari 2016. Karibu katika magazeti ya leo .
Add caption

KIWANDA CHA A TO Z CHA ARUSHA KUTOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 70

$
0
0
 Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina, ziarani katika baadhi wa viwanda jijini Arusha. (Picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais).
kikao kikiendelea.

Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Luhaga Mpina amekiamuru kulipa faini kiwanda cha A to Z cha mjini Arusha , chenye kufanya kazi ya kuzalisha nguo na bidhaa za plastiki kutokana na ukiukwaji wa utekelezaji wa sheria namba 20 ya mwaka 2004 ya utekelezaji na usimamizi wa mazingira.


Mh Mpina alitoa agizo hilo jijini Arusha Jumamosi  katika ziara yake ya kukagua usafi wa mazingira, kupanda miti na kutembelea viwanda,ambapo alibaini kuwa mnamo septemba mwaka 2015 kiwanda hicho kilipewa adhabu ya kulipa faini  ya shilingi milionni 70 na kukaidi kufanya hivyo kwa kipindi cha miezi sita sasa.

Mh Mpina amekitaka kiwanda hicho kulipa faini hiyo kwa kipindi kisichopungua siku saba kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa.Aidha Naibu Waziri Mpina alitembelea viwanda vya Sunflug na Lothia Steel vya jijini humo  na kujione namna ambavyo vinakabiliana na utunzaji wa mazingira katika uzalishaji wao na changamoto ya kuzimikazimika kwa umeme jijini Arusha.

Mh. Mpina alikitaka kiwanda cha Chuma cha Lothra Steel kupima moshi unaotoka katika kiwanda hicho ili kujua kama una athari kwa mazingira na viumbe vinavyozunguka maeneo ya kiwanda hicho.Ziara na Mh waziri katika jiji la Arusha ni matokeo ya utekelezaji wa agizo la Mh Rais John Pombe Magufuli la usafi wa mazingira unaotakiwa kufanyika kitaifa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 1.6/- VYUO VYA UALIMU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 1.65/- kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye vyuo vya walimu hapa nchini.

Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), wakati akizungumza na walimu na watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.


"Serikali inatambua uhumimu wa mafunzo kwa vitendo katika vyuo vya ualimu ni kwa sababu hiyo mwezi huu wa Februari tumetoa sh. bilioni 1.65/- kwa vyuo vya ualimu 35 vya umma nchini ili kuwezesha wakufunzi na walimu wanafunzi kushiriki kikamilifu mafunzo kwa vitendo (Block Teaching Practice)," alisema huku akishangiliwa.

Alisema fedha hizo zinapaswa zitumike kulipia posho za kujikimu, nauli na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Mapema, akizungumza na mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha elimu na akawaonya wote wanaowaharibia elimu watoto wa kike.

"Tunataka watoto wa kike wasome wa Kitanzania wasome hadi elimu ya juu waje wawe watumishi wa umma hapo baadaye. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake tukikumbuka kaulimbiu ya Mama Salma Kikwete ya kwamba 'Mtoto wa Mwenzio ni wako'," alisema.

"Yeyote atakayemharibia mtoto wa kike masomo kwa kumrubuni na chips au pipi ajiandae kwenda Lilungu, (gereza la mkoa wa Mtwara)", alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 28, 2016.

WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI BANDARI YA MTWARA

$
0
0
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua bandari ya Mtwara na kunusa harufu ya ufisadi katika utoaji wa zabuni  ya ujenzi wa gati mpya tatu.

Wazi Mkuu ambaye alikagua eneo la ujenzi wa gati hizo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), alisema anazo taarifa juu ya utolewaji wa zabuni hiyo na mzabuni ameshashinda lakini kuna madai kwamba watu wa manunuzi kupitia PPRA  ndiyo wanakwamisha zabuni hiyo.


Aliwaomba wabunge wa mkoa wa Mtwara washirikiane kusimamia suala hilo ili ujenzi wake uweze kuanza mara moja na kuleta ajira kwa wana Mtwara. "Ujenzi ukikamilika siyo tu ajira zitaongezeka bali hata meli nyingi zitaleta mizigo katika bandari hii na mapato ya mkoa yataongezeka", alisema.


"Natambua kwamba kuna mpango wa kujenga gati nne ambapo moja kati ya hizo itajengwa na TPA (Mamlaka ya Bandari) lakini hizi tatu zilitangazwa na kupata mzabuni ambaye ni kampuni ya Hyundai kutoka Japan. Lakini hii kampuni imekuwa ikizungushwa bila sababu. Tutafuatilia kubaini tatizo liko wapi," aliongeza.


"Sasa hivi tuna uwezo wa kupaki meli moja tu, lakini gati zikikamilika tutaweza kuwa na meli tatu kwa mpigo, cha msingi tusimamie maamuzi yetu kwamba lazima wafanyabiashara wa korosho watumie bandari hii kusafirisha mizigo yao na si kuipeleka kwingine."

"Kwenye Bodi ya Korosho nako kuna majipu yanahitaji kutumbuliwa. RCC ilishakaa na kupitisha uamuzi kuwa mizigo yote ipitie bandari ya Mtwara lakini kuna watu ndani ya Bosi hiyo wanatoa vibali vya kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Dar es Salaam. "


Alimtaka mkuu wa bandari ya Mtwara (Port Master) Bw. Prosper Kimaro awe makini na watu wa kitengo cha manunuzi katika bandari hiyo kwani kimekuwa chanzo  cha upotevu wa fedha za Serikali kutokana na ujanja wa watu wachache.

"Hapa si kuna mtu alitaka kuiba sh. milioni 300 kwa kufoji saini za wakubwa wake? alihoji Waziri Mkuu swali ambalo lilijibiwa na Bw. Kimaro kwamba ni kweli lakini uongozi uliingilia kati kabla wizi huo haujakamilishwa.

Kuhusu fidia kwa wakazi wa vijiji vya Kisiwa na Mgao ambao wamekubali kuhama ili kupisha upanuzi wa bandari hiyo,  Waziri Mkuu aliwahakikishia wabunge hao pamoja na uongozi wa bandari kwamba kiasi cha sh. bilioni 13.8/- kimekwishatengwa na Wizara na kitatolewa mapema mwezi ujao.


Alitumia fursa hiyo kusisitiza udhibiti wa bandari bubu ambazo zinatumiwa kuingiza sukari na  mchele mchezo ambao unaikosesha Serikali mapato.  "Mkuu wa Mkoa, nilikwishatoa agizo kama hilo wakati nimeenda kukagua bandari ya Tanga. Kaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa nanyi pia muweke mbinu za kudhibiti upenyo huu wa kuingiza bidhaa za magendo kwa sababu hawa ndiyo wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali," alisisitiza.


Naye, Mkuu wa bandari hiyo, Bw. Kimaro wakati akitoa taarifa ya utendaji wa bandari mbele ya Waziri Mkuu, alisema bandari hiyo ilianzishwa mwaka 1950 na imekuwa inakabiliwa na ufinyu wa gati ya kuegesha meli, vifaa vya kupakulia na kupakia mizigo na kwamba hivi sasa wamekwishapata winchi ya bandarini (harbour crane) yenye uwezo wa kubeba tani 100 na tayari wako kwenye mpango wa kujenga gati moja.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 28, 2016.
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live




Latest Images