Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 76 | 77 | (Page 78) | 79 | 80 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Meneja Mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway akikabidhi baadhi ya vitabu vya sekondari kwa afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa  ikiwa ni msaada ulitolewa kuchangia elimu  toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila, anaeshuhudia wakwanza kulia ni  Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga

  Kulia ni Afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa ikimkabidhi kati ya vitabu vilivyotolewa kwa lengo la kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Mwishoni mwa wiki Airtel ilitoa vitabu kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu,  Kwendimu na Magila,. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga.


  ==========  ========   =======
  Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari Tanga.


  •       Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu Tanga ni shule ya sekondari
  ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila
  •       Airtel yaahidi kuingia katika awamu mpya ya ugawaji wa vitabu kwa
  sekondari kila mkoa nchini.  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa vitabu
  vya hesabu,chemistry na baologia vyenye thamani ya shilingi milioni 12
  kwa shule nne za mkoa wa Tanga.  
  Msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  
  wa kusaidia ukuaji wa sekta ya limu kupitia kampeni yake ya shule  
  yetu.  Akipokea vitabu hvyo kwa niaba ya shule za mkoa wa tanga afisa elimu
  wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa alisema, “ Tunawashukuru
  Airtel kwa msaada huu wa vitabu kwani utasaidia kupunguza tatizo la
  uhaba wa  vitabu kwa shule zilizopatiwa msaada huo na kuongeza kiasi
  cha ufaulu kwa wanafunzi. Tunaomba juhudi hizi zisihishie hapa
  ziendelea katika shule mbalimbali mkoani hapa na mikoa mingine ya
  Tanzania ili kuondoa ujinga na umaskini na kuwapa watoto wetu elimu
  bora kwani hawa ndio taifa la kesho.  Kwa upande wake meneja mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro
  Bw. Edmund Lasway amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni 
  yake wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini. Chini ya mpango maalumu 
  wa Shule yetu tumeweza kuzifikia shule nyingi za sekondari nchini.  Akiongea kwa niaba za shule zilizopokea msaada huo Mwalimu mkuu wa
  shule ya secondari ya Mkuzi juu Bwn Victor Mwenda alisema”  Tunatoa
  shukurani kwa Airtel kwa msaada wa vitabu katika shule zetu za
  sekondari, kwa hatua hii itasaidia kupunguza tatizo la vitabu
  linalozikabili na kuongeza ufanisi katika masomo ya sayansi.
  Tunawaomba wanafunzi wavitunze na kuvitumia vizuri hivi vitabu kwani
  ni nyenzo muhimu katika elimu ya sekondari.  Vilevile Meneja wa huduma za jamii wa Airtel Tanzania Bi Hawa Bayuni
  alidokeza kuwa Airtel iko katika mkakati wa kuanza awamu nyingine ya
  ugawaji wa vitabu kwa shule za sekondari kwenye kila mkoa ikiwa ni
  program yake ya mwaka huu ya kurudisha kwa jamii kupitia elimu
  “tunaingia katika awamu ya mpya ya utowaji wa vitabu kwa shule ngingi
  zaidi  kila mkoa hapa Tanzania, mradi wetu huu utazingatia zaidi shule
  za sekondari zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu kwamba ni shule zipi
  zina uhitaji  mkubwa wa vitabu na kushauri  ziingie katika mpango wa
  kusaidia jamii wa Airtel shule yetu” alieleza Bayumi.


  Airtel toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka nane iliyopita
  tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1500 za sekondari zilizopo Tanzania
  kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa  yote  na kuwafikia wanafunzi katika
  kila kona ya Tanzania na pia kukarabati miundombinu ya shule kwenye
  maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni hatua ya Airtel kukuza kiwango
  cha elimu kwenye maeneo mbalimbali Tanzania aliongeza Bayumi.  Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi mkoa ni Tanga ni pamoja
  na shule ya sekondari ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila.
  mkakati ni kuendelea kutoa vitabu kwa shule mbalimbali nchini ambapo
  droo ya shule za sekondari zitakazo faidika na vitabu kwa mwaka huu wa
  2013 -2014 itafanyika mwenzi Juni  na kutoa nafasi kwa shule nyingine
  nyingi za sekondari nazo kufaidika na mpango huu wa Airtel shule yetu.

  0 0

   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam jana jioni kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, kama Mgeni rasmi sambamba ya kuzindua Shule ya Taasisi hiyo inayofundisha masuala ya urembo.
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akishiriki kukata Keki na Maza Sinare, ambaye ni mmiliki wa Saluni ya Maznat, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam, jana Mei 5, 2013, sambamba na sherehe hizo pia Mama Asha, alizindua rasmi shule ya masuala ya Urembo inayosimamiwa na Taasisi hiyo. Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam, jana, sambamba na sherehe hizo pia Mama Asha, alizindua rasmi shule ya masuala ya Urembo inayosimamiwa na Taasisi hiyo.
   Mama Asha, akipongezwa na wageni waalikwa baada ya kusoma hotuba yake ukumbini hapo.
   Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo.
   Mmiliki wa Saluni na Taasisi ya Maznat, Maza Sinare, akiwalisha keki baadhi ya wageni waalikwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam jana, sambamba na sherehe hizo pia Mgeni rasmi mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha, alizindua rasmi shule ya masuala ya Urembo inayosimamiwa na Taasisi hiyo.
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (kulia) akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi shule ya masuala ya Urembo, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam, jana. Shule hiyo inasimamiwa na Taasisi hiyo.luni na Taasisi hiyo ya Maznat, Maza Sinare.
   Msanii wa muziki wa Taarab, Mzee Yusuph, akiimba jukwaani kutoa burudani wakati wa sherehe hizo.
   Mama Asha Bilal, akiwaongoza wanawake waliohudhuria sherehe hizo katika kucheza muziki wa taarab, burudani iliyokuwa ikitolewa ukumbini hapo na Mzee Yusuph.
   Msanii wa muziki wa Injili, Bahati Bukuku, akiimba jukwaani kutoa burudani wakati wa maadhimisho hayo.
   Baadhi ya wadau wa Maznat, waliohudhuria sherehe hizo, wakisebeneka na miondoko ya taarab, ukumbini hapo.
   Baadhi ya wadau wa Maznat, waliohudhuria sherehe hizo, wakisebeneka na miondoko ya taarab, ukumbini hapo.
   Baadhi ya wadau wa Taasisi ya Maznat, wakihesabu fedha zilizopatikana baada ya kuchangwa na washirika wa karibu wa Taasisi hiyo ukumbini hapo jana wakati wa sherehe hizo kwa ajili ya kusaidia mfuko wa kusaidia Watoto Yatima ulio chini ya Taasisi hiyo, ambapo zilipatikana jumla ya sh. milioni 15, 500, 7200 
   Mmiliki wa mtandao wa Mafoto Jr, Nasma Mafoto (kushoto) akiwa na wadau waliohudhuria sherehe hizo.
   Wasanii wa kundi la The Voice, wakitoa burudani ya kuimba 'Akapera' jukwaani wakati wa sherehe hizo.
   Mabaunsa wakifungua na kuripua Shampeni kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya kusherehesha ukumbini hapo.
   Maznat, akipozi kwa picha na wafanyakazi wake...
   Mama Asha Bilal, akiwaongoza wageni waalikwa kugonganisha glasi wakati wa sherehe hizo.
   Kwa amani na furaha ya kutimiza miaka 10 ya Taasisi ya Maznat, wageni waalikwa waligonganisha glasi zao.
  Cheeeeeeeeaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaazzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  0 0

  UONGOZI wa Clouds Media Group kwa kupitia Mkurugenzi wao wa Utafiti na Matukio, Ruge Mutahaba, umemtaka msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura, Lady Jay Dee ajipange na kupokea changamoto badala ya kutafuta mahali kwa kujiegemeza kwa kueneza matusi kwao.
  Clouds Media leo wamefungua mdomo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi mitano tangu Jay Dee alipokuwa akiwarushia makombora kwa madai kuwa wameharibu soko la muziki wa Bongo Fleva sambamba na kuitangaza bendi ya Skylight kwa ajili ya kuiangamiza Machozi Bendi.
  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam ambapo pia alikuwa akirushwa moja kwa moja katika redio ya Clouds FM, Mutahaba alisema Jay Dee amekuwa akilalamikia mambo mawili ambayo ni bendi ya Skylight na matangazo yake yaliyoshindwa kurushwa hewani japo alilipia Sh 240,000.
  Alisema suala hilo walilimaliza baada ya kumueleza kuwa redio yao haiwezi kukataa matangazo kwakuwa ndiyo wanayowafanya waendelee kuwa kinara katika suala zima la kuiendesha Clouds FM.
  “Nilimwambia kamwe hatuwezi kukataa matangazo na kama kuna lolote limefanyika, basi ni kwa bahati mbaya, ukizingatia kuwa tayari alishafanya kazi nyingi pamoja na kupewa urahisi kwenye kazi zake kwa kupitia Clouds FM.
  “Pamoja na yote hayo, bado matusi na kejeli yaliendelea hasa katika mitandao ya kijamii jambo lililotufanya tuamuwe sasa kujibu japo hapo kabla tuliamua kubaki kimya kwa ajili ya kulinda hadhi ya kazi zetu,” alisema.
  Kuhusu shutuma za kuitangaza zaidi Skylight Bendi, Ruge alisema bendi hiyo si mali ya Joseph Kusaga, Mkurugenzi wao wala yeye, kama madai hayo yanavyotolewa bila kufanya utafiti, isipokuwa ni mali ya Sebastian Ndege.
  “Kama kuna mvutano kati ya Machozi Bendi na Skylight basi ni wa kibiashara maana wote wanalipa fedha za matangazo na kama chanzo ni Jay Dee kuporwa wanamuziki wake, hilo si jambo geni kwenye muziki.
  “Dada yangu Asha Baraka asingekuwa makini angelia sana, maana kila bendi inayoanzishwa au kuendeshwa lazima ichukuwe wanamuziki kutoka kwake, ukizingatia kuwa ni jambo la kawaida hivyo tumuomba Jay Dee atumie busara katika hili pamoja na kuumiza kichwa kupokea ushindani na changamoto kama hizo za kuchukuliwa wanamuziki,” aliongeza Ruge.
  Aidha, Ruge alisema Clouds FM ni redio ya watu binafsi, hivyo si ina utaratibu wake katika utendaji wa kazi, ikiwapo kuchagua nyimbo au kuacha kupiga kama kuna mtu amekwenda kinyume, hasa wale wanaopita nje na kuanza kuwatusi, kuwakejeli bila kukumbuka fadhira walizofanyiwa kabla ya kuwa maarufu wao.
  Pia alisema Clouds FM ipo tayari kufanya majadiliano ya wazi na mtu yoyote mwenye hisia tofauti juu yao, huku ikiwataka wasanii waongeze bidii katika kazi zao ili wasimlaumu mtu wanapoanguka na kuwapisha wengine, maana muziki unaonekana ni wa kupokezana vijiti.
  Katika siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari hasa hasa kwenye mitandao ya kijamii nchini kumekuwa na taarifa rasmi na zisizo rasmi kutoka kwa Mwanamuziki Lady Jaydee alilalamikia Kituo chetu cha Clouds FM na wakurugenzi wake Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.

  ENDELEA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPO  CHINI.


  ====================   ==================

  RUGE MUTAHABA MKURUGENZI WA VIPINDI NA UTAFITI CLOUDS MEDIA GROUP.
  Kwa mtazamo wangu, kila mwananchi ana haki ya kutoa maoni yake ingawa kwenye nchi yetu ya Tanzania, tumezoea maoni hayo kutolewa kwa lugha ya ustaraabu na staha.
  Maoni kuhusu nani wa kuja kwenye msiba wako au nyimbo za kupigwa kwenye msiba wako ni haki ya kila mwananchi na hakuna atayeuingilia uamuzi huo. Maoni pia ya redio gani mtu anaipenda au tv gani pia nayo ni utashi wa mtu mwenyewe.
  Uongozi wa Clouds FM ulikuwa umefikia maamuzi ya kutojadili jambo hili kutokana na kuamini kuwa ni tatizo binafsi la mtu na sio jambo lenye maslahi ya Taifa hivyo kwa uhalali linahitaji majadiliano au mazungumzo binafsi.
  Sura ambayo jambo hili limewekwa na kulifanya kama dharura ya kitaifa sio sahihi kabisa  kutokana na kukosekana na hoja za kina za kuhitaji majibu na pili kukosekana kwa ujumla wa tija kwa tatizo hili kitaifa.
  Bado ninaamini linatakiwa kubaki kama tatizo la mtu binafsi ila inapofika taarifa zikapotoshwa kwa nia ya kuwapa mtazamo tofauti wasikilizaji wetu, Clouds FM inataka kuweka maslahi ya wasikilizaji, wabia wetu wa biashara na watanzania wote mbele kwa kuwapa taarifa sahihi za jambo hili.
  Clouds Media Group inapata lawama kubwa sana kutoka kwa watu wengi ambao pamoja na kuunga mkono ukimya wetu wanajiuliza ni kwanini hatukufanya jitihada za kumaliza tatizo hili bila kufika hatua iliyofikia sasa ya matusi, kebehi na vitisho kutwa vinavyoelekezwa kwetu na pia vinaendelea kuichafua tasnia ya muziki hasa hasa Bongo flava; ambayo imefika mahali inaonekana kila changamoto inayomkabili msanii wa Bongo flava lazima itatuliwe kwa njia za mabavu (matusi, vitisho na kuchafuana).
  Lawama hizo sio za kweli na naomba nirudi nyuma kidogo kwenye historia ya jambo hili. Tarehe 14 mwezi wa 12 mwaka 2012 kwenye tweeter account ya Jaydee, alipost kifuatacho:  

  Nilichofanya ni kumpigia simu na kuzungumza nae.  Akasema sijaandika kwenye blog chochote, nikamwambia Jide mi nakuheshimu sana. Nimekupigia kwasababu naamini kama kuna kitu chochote ni bora nisikie kwako, nategemea na wewe pia utanipigia iwapo kuna jambo lolote lile.  Tulikotoka sisi hatutakiwi kuendeshwa na majungu na maneno ya mtaani.Hiyo ilikuwa tarehe 14 mwezi December mwaka jana. Baada ya kama dk 10 hivi akanitumia msg ( ambazo bahati nzuri nilizihifadhi) na kusema ni kweli alikuwa ananizungumzia mimi kwa sababu kuna vitu kadhaa vinamsumbua na aliambiwa mimi ndo nilihusika navyo.
  La kwanza, ‘nililipa matangazo ya shs laki mbili na 40 ila hayajachezwa na wala sijarudishiwa hela yangu, nimeambiwa umekataza matangazo yangu ya Nyumbani lounge yasipigwe’. 
  La pili, naruhusu watangazaji wangu wamtukane ikiwa ni pamoja na kupromote zaidi bendi ya Skylight.
  Pamoja na kwamba yeye alinitumia message, mimi nilimpigia simu na kumpa ufafanuzi wa yote hayo niliyosema hapo juu.
  Nikasema, Biashara yetu sisi ni matangazo…..kwanini tukataze matangazo yako yasipigwe?? Labda bahati mbaya tu, jamaa anayebook matangazo alipitiwa kuyabook kibinadamu ila Gadna si anakuja hapa kila wakati, kwann asimkumbushe tu?? Tutayasogeza tu mbele hadi wiki inayofuata, kwanini niyakataze wakati muda sio mrefu tumetoka kuleta biashara ya Repa bora wa bendi hapo hapo Nyumbani lounge.
  Niliendelea kujibu kuwa sio kweli kabisa, siwezi kuruhusu jambo kama hilo na kama ni kweli mtangazaji anamtukana anifahamishe ni nani na kwenye kipindi gani, nitasikiliza kipindi na kama ni kweli nitamfukuza kazi ( Clouds ina mitambo ya kuhifadhi matangazo yake yote kwa takribani miezi 9).
  Hili nilimjibu kwa kirefu kidogo ikiwemo kumwambia akaze buti maana Skylight Band wanakuja juu nk nk. (Skylight Band ni bendi inayofanya vizuri sana hapa mjini na ilipoanza ilichukua baadhi ya majina makubwa kutoka Machozi Band).
  Baada ya kumaliza mazungumzo tuliagana vizuri tu kwa miadi ya kukutana nikirudi maana nilikuwa safarini.
  Kwahiyo ukiniuliza Jaydee anacholalamika ni nini??? Jibu langu litakuwa ni hayo mambo mawili maana hata nyie watanzania wenzangu mnaosoma mitandao ya kijamii mtakubaliana na mimi kuwa amekuwa anashambulia personality zetu, mimi na Mkurugenzi mwenzangu bila kuweka wazi hoja za msingi kuhusu yale anayotutuhumu nayo.  Nimejitahidi sana kuelewa tatizo lake hasa ni nini na imekuwa inanipa shida kidogo?? Nimejitahidi sana kufikiria ni mirija ipi ya biashara kwake imeingiliwa, nakosa majibu??? 
  Clouds FM ni ya watu na watu wanaweza kufanya makosa kweli na hata kusababisha matangazo ya laki 2 na 40 yasirushwe, kwa hilo nilishazungumza na Jaydee na kuomba radhi toka tarehe 14 December 2012. Clouds FM haina ubia wowote ule na Skylight Band (ni bendi iliyoanzishwa na Mtanzania)hivyo kuipromote ni katika misingi ile ile ya biashara kama tunavyopromote bendi yeyote ile na vilevile Clouds FM pia haihusiki kabisa na kutetereka kwa biashara ya chakula, vinywaji na bendi inayofanyika Nyumbani lounge. Inashangaza hata kuhusishwa na biashara ya Nyumbani lounge…!!!
  Sina ugomvi binafsi na Jaydee wala Gadna, na tarehe 12 February mwaka huu, nilienda kuazima stools kwa ajili ya shooting kutoka kwenye sehemu yao ya biashara ingawa yeye amekiri kuwa na ugomvi mkubwa na sisi binafsi na Clouds kama chombo.
  Nyimbo yake iliyotoka ya Joto Hasira ilipokelewa vizuri sana kulinganisha na nyimbo mbili zilizopita ‘Yeye’ na ‘Mimi ni mimi’ ambazo hazikufanya vizuri pamoja na jitihada kubwa ya kuzipromote. Joto Hasira iliacha kupigwa kutokana na shinikizo lake mwenyewe, ikiwa imeshachezwa mara 48 ndani ya wiki tatu toka imetoka wote tulipigwa na bumbuwazi na kujiuliza ni kitu gani tumefanya kuambiwa hatupigi nyimbo na lawama nyingine. Kama ofisi tukaona tukae kimya na kusubiri hatua inayofuata ukizingatia tuliendea kupiga nyimbo na video hata baada ya maneno makali ya mwanzo. Kauli haikubadilika, mbaya zaidi kauli za kebehi na kuchafuana zikaongezeka hadi kufikia uamuzi wa sisi kama taasisi kuamua rasmi kutopiga nyimbo zake hadi atakapofuta kauli zake na kuomba msamaha.
  Kupiga au kutopiga nyimbo kwa kituo cha redio ni jambo la kawaida na kwasababu ni chombo binafsi ni muhimu kwa watu kama Jaydee na wasanii wengine (na hata wananchi wa kawaida) kuelewa kuwa kila ofisi ina taratibu zake na iwapo utatokea ukiukaji wa taratibu hizo, policy ndo zinaongoza maamuzi.  Hebu tujiulize, mbona sio mjadala wa Taifa msanii Diamond hapigwi karibu miezi sita sasa kwenye station ya Magic FM, Ray C na Ali Kiba kwa karibu mwaka mzima walikuwa nyimbo zao na video hazipigwi na East Africa hadi walipoomba msamaha, hadi Yanga kwa muda mrefu walikuwa hawatangazwi habari zao kwenye chombo kimoja cha habari. Hayo ni mambo ya ofisi binafsi na hakuna anayeweza kulaumu maamuzi hayo.
  ‘Management reserves the right of admission’……nani hajaona kibao hiki kwenye hoteli nyingi tu nchini, nani asiyefahamu kuwa kuna hoteli ambazo ukienda kama mwanamke peke yako unakataliwa? Hizi ni taratibu na kila mahali zipo…..hata nyumbani lounge ndo maana Sam Machozi ambaye yuko Skylight Band zamani alikuwa mwanamuziki wa Machozi Band amepigwa marufuku pale Nyumbani lounge na halalamiki maana ni sehemu binafsi na ina taratibu zake. Ni tofauti na sehemu za wazi za umma kama Mnazi mmoja au kituo cha basi cha Magomeni.
  Clouds Media Group inafuata taratibu zote za nchi na za kimkoa ila na yenyewe pia inaweka taratibu zake za uendeshaji. Sasa isifike mahali Clouds inapoweka taratibu zake hizo na kuzitekeleza inaonekana inafanya makosa.  Yaani hata tarehe za kufanya show nchi hii tunatakiwa kupeleka maombi sehemu ili watu zaidi ya mmoja wasifanye show kweli???  Kwanini tunachanganya ushindani na fitina…..acha ziwepo bendi 10 zinazoshindana, kuanzishwa kwa bendi nyingine kusiangaliwe kama fitna.  Na hata mtu akianzisha bendi kwa kuchukua wanamuziki kutoka kwenye bendi nyingine, si ndio dhana ya ushindani???
  Kama ni kulalamika kuanzishwa kwa bendi nyingine au kuchukuliwa wanamuziki, Dadaangu Asha Baraka si angeshafanya maandamano nchi nzima. Ila wote tunatambua kuwa ni jasiri ndo maana anatulia na kuanza upya.
  Mbona watu hawalalamiki  baa zinapofunguliwa 10 mtaa mmoja, au saloon za nywele, moja jirani na nyingine. Ni lazima tukubali na tuzoea ushindani.
  Pamoja na ushindani kingine ninachoomba  kuwasihi watanzania wenzangu hasa hasa wasanii wetu  zaidi ni kuwa kila mtu na kila kitu kina ‘shelf life’. Watu wa zamani naamini wanamkumbuka Power Mabula….alikuwa anatisha sana wakati ule. Au nani anaweza kusahau umaarufu wa Mzee Nobert Chenga na Kundi la Muungano cultural troupe au labda huko ni nyuma sana; nani anamkumbuka Kanda Bongo Man, alicharge laki moja enzi hizooo….au labda hapa katikati umaarufu wa Muumini, Mr Nice au mtu kama Saida Karoli (alijaza Stadium). Wote hao walikuwa maarufu sana. Sasa wasanii hawa na wengine wanaokuja wasipojiandaa kuelewa kuwa kila kitu kina muda wake, tutakuwa na taifa la vijana ambao asubuhi mpaka jioni badala ya kuhangaikia fursa nyingi zilizopo wataishia kutafuta mtu wa kumlaumu.
  Ni lazima Edibily Lunyamila atarithiwa sehemu yake na kina Mrisho Ngassa ambaye naye muda utapita ni lazima atawaachia kina Simon Msuva. Wapo watu kama kina Dully Sykes walioanza kujiandaa kwa kuwaachia kina Diamond na wao kufungua studio na kuwa maproducer. Suala la kupokezana vijiti halikwepeki kuanzia makazini, mpirani na hata kwenye sanaa. Cha kufanya ni kujiandaa kwa maisha yako baada ya kugawa kijiti chako.
   Taarifa za kutaka kuua muziki wa Bongo flava kwa makusudi zinashangaza, ili iweje sasa??? Clouds inategemea matangazo ya biashara kama asilimia 95 ya mrija wa mapato na muziki tunaopiga redioni ni sehemu ya maudhui kwahiyo hakuna namna yeyote ile tutataka muziki huo upotee. Tunafanya juhudi zote hizi kwasababu tunahitaji nyimbo bora na wasanii bora ili tuweze kuendelea kuwa kituo bora cha redio.

  0 0


   
  Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa akionyesha baadhi ya zawadi zitazogombaniwa wakati wa promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’. Kulia kwake ni Awaichi Mawalla, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla.
  Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, leo imezindua promosheni ya ‘Kwangua na Ushinde’ kwa wateja wake wake wa Zanzibar ikiwa ni katika juhudi zake za kuwazawadia wateja wanaotumia mtandao huo.

  Promosheni hiyo kubwa ambayo mshindi wake atajinyakulia gari, itawazawadia wateja wengine zawadi za kila siku kama muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni  moja, pikipiki aina ya Vespa, komputa ndogo (Huawei Media pads) pamoja na modemu za 3G.


  Ili kushiriki katika promosheni hiyo, wateja wapya na wale wa zamani wa Zantel wanapaswa kuweka muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi ili kuingia kwenye droo hiyo.


  Akizungumzia promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel upande wa Zanzibar, Mohamed Mussa, alisema promosheni hiyo inathibitisha nia ya kampuni hiyo katika kuboresha maisha ya wateja wake huku wakiendelea kuwasiliana na ndugu na marafiki zao.


  “Tuna furaha kubwa leo kuzindua promosheni hii kwa wateja wetu, ambayo hakika itawapa thamani ya pesa zao kwa kujishindia zawadi mbalimbali’’ alisema Mussa. Promosheni hii itaendeshwa kwa kipindi cha miezi miwili, kuanzia leo tarehe 6 mwezi wa tano hadi tarehe 6 mwezi wa saba.

  Kwa kipindi chote cha promosheni Zantel itatoa jumla ya modemu 60 za 3G, komputa ndogo 12 (Huawei Media pads), pikipiki 6, muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja pamaoja na gari moja.


  “Promosheni hii itaipa kampuni yetu fursa ya kuwasiliana na wateja wetu, huku pia tukiwashukuru kwa kutumia huduma zetu’’ alisisitiza Mussa.


  Wakati huo huo kampuni ya Zantel pia imetangaza kuzindua ofa mpya kwa wateja wake wa nchi nzima, iitwayo ‘Bonus Balaa’ ambayo itawapa mara mbili ya muda wa maongezi wakiweka vocha ya kuanzia shilingi elfu moja au zaidi. Muda huo wa maongezi utawawezesha wateja wa Zantel kupiga mitandao yote.


  0 0

   
  TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na timu ya netiboli, Taswa Queens Jumamosi zitacheza na timu ya wacheza filamu, Bongo Movie FC na Bongo Movie Queens katika mchezo maalum wa kirafiki.
  Mechi hizo zimepangwa kufanyika kwenye uwanja wa TCC, Chang’ombe kuanzia saa 10.00 jioni kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
  Majuto alisema kuwa mchezo wa kwanza ambao utahusisha timu za netiboli umepangwa kuanza saa 10.00 jioni ambapo  siku hiyo Taswa Queens itakuwa ikicheza mechi yake ya tatu tokea kuanzishwa kwake siku ya sikukuu ya Pasaka mwaka huu.
  Mechi ya kwanza ya Taswa Queens ilikuwa dhidi ya Kiliflora Queens na kushinda kwa mabao 28-8 na mechi ya pili ilikuwa dhidi ya Kombaini ya walimu wa wilaya ya Kibiti na kushinda kwa 36-2.
  Majuto alisema kuwa wachezaji wa Taswa Queens chini ya wachezaji wake, Imani Makongoro na Oliver Albert,  kutoka Mwananchi Communications Limited aliyechezea nafasi ya GA, Clezencia Tryphone (Tanzania Daima), Elizabeth Mbassa, Sharifa Mustapha na Johari William wote wa  Business Times Limited (BTL). Makocha wao ni Amina Mussa  kutoka BTL na Zainabu Mussa.
  Kwa upande wa Taswa FC, mechi hiyo ni muhimu sana kwao kutokana na matokeo mabaya ya mechi ya mwisho ya kufungwa mabao 2-0 wilayani Kibiti. Majuto alisema kuwa wamejiandaa vizuri ili kutoa kipigo kwa Bongo Movie katika siku hiyo ambapo bendi ya Msondo  itatumbuiza baada ya mchezo huo ulioandaliwa na Dar Bonanza.
  “Mechi zote mbili ni sehemu ya maandalizi yetu ya safari ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga, hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kushinda, makocha wangu, Ali Mkongwe na Ibrahim “Maestro” Masoud wameandaa programu nzuri na bila shaka itatoa matunda mazuri,” alisema Majuto.


  0 0

   Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya zoezi la upigaji kura kwa wamamuziki wanaowania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zilinazoelndelea kupigwa kupitia mitandao ya simu na intanet,wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya zoezi la upigaji kura kwa wamamuziki wanaowania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zilinazoelndelea kupigwa kupitia mitandao ya simu na intanet,wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kulia ni Mkurugenzi Idara ya Ukuzaji Sanaa BASATA, Vivian Nsao Shalua,Mratibu wa Tunzo za Muziki Tanzania wa Kutoka BASATA,Angelo Luhala pamoja na Muwakilishi wa Inovex,Lloyd Zhughu.
  Muwakilishi wa Inovex,Lloyd Zhughu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya namna kura zitakavyokuwa zikihesabiwa.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Kelvin Albert (3) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Deric Siprian Kessy (8) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto kwa Makamu ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo na (kulia) kwa Makamu wa Ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Alex Malasusa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Gabriel Godfrey (9) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Restuta Alex (50) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa mahututi, aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, wakati alipowasili nyumbani kwa askofu huyo jijini Arusha jana kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha kwenye hafla ya uzinduzi wa Kanisa hilo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa papa Francis, Askofu Francisco Montecillo, walipokutana nyumbani kwa Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, alipofika kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha. Picha na OMR

  0 0


   Shirikisho la Ngumi la Kimataifa 
  (IBF) limempongeza bondia maarufu wa kitanzania Francis Cheka kwa juhudi zake za kuwa bondia mzuri mwenye viwango vya kimataifa katika uzito wa Super Middleweight.
  Francis Cheka aliweza kutetea mkanda wake wa IBF Africa uzito wa Super Middle baada ya kumshinda kwa KO bondia Thomas Mashali aka “Simba asiyefugika” tarehe 1 Mei, 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
   IBF inachukua fursa ya kumpongeza Francis Cheka baada ya ushindi huo ambao umedhihirisha kuwa yeye kweli ni bingwa wa bara la Afrika. Francis Cheka atarudiana na bondia wa Malawi Chimwemwe Chiotcha mwezi wa Agusti katika mpambano la kutetea mkanda wake.
   Mpambano wao wa marudiano utafanyika katika jiji la Blantyre nchini Malawi na tayari majadiliano ya mpambano huo yanaendelea vizuri. Kampuni ya “Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi chini ya bwana Stephen Mawezni ndiyoitakayoandaa mpambano huo.
   Pambano hili linakuja baada ya wadau kadhaa wa ngumi kuomba mabondia hao warudiane walipoonyesha ujuzi mkubwa na ushindani katika mpambano wao Desemba 26 mwaka jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeidi jijini Arusha siku ya Boxing Day.
   Baada ya mpambano huo, IBF itampatia Francis Cheka nafasi ya kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF International Super Middleweight) na mabondia wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha kuwa Francis Cheka hana tena mpinzanai nchini Tanzania na kumpambanisha na mabondia wa kitanzania ni kumpotezea muda na uwezekano wake wa kutengeneza jina na pesa.
   Wakati huo huo bondia Thomas Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle kwani mkanda wake haukuwa kati ya mikanda iliyogombewa kwenye mpambano uliomalizika Mei mosi.

  0 0
 • 05/06/13--12:47: tiketi hizi hapa
 • Tiketi za sherehe za kuadhimisha miaka 13 ya muziki wa Lady Jaydee zimeshaanza kuuzwa mtaani na huo hapo juu na chini ndio mfano wa jinsi zilivyo ambapo ya juu ni ile ya VIP itakayokuwezesha kupata chakula, nakala ya CD pamoja na huduma maalum ya kinywaji cha kuanzia Hii hapa chini ni ya kawaida itakayokuwezesha kushiriki onesho, na kushuhudia burudani lukuki zitakazoongozwa na Profesa Jay, TID, Matonya, Grace Matata pamoja na Lady Jaydee mwenyewe na Machozi Band itaonekana jukwaani live siku hiyo.Tiketi zinapatikaka Shear Illusions-Mlimani City, BM BarberShops-Kinondoni, City Sports Lounge-City Centre, American Nails-Kinondoni, Nyumbani Lounge-Tranic Plaza, na katika Bar za Samaki samaki


  0 0


  *Timu nne mpya katika robo fainali ya tatu ya Guinness Football Challenge *
                                                                

   Mei  mosi, jumatano iliyopita kupitia televisheni za  ITV na Clouds TV  katika kipindi cha 7 cha GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE tuliona timu ya Tanzania,Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ikifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali pamoja na timu ya Kenya, Kenneth Kumau na Wills Ogutu, kutoka Nairobi ambao ndio walizishinda timu zote katika sehemu hii ya saba.


  Wakenya walifanikiwa kupita katika hatua zote lakini wakapata ushindani kutoka kwa Waghana katika hatua ya Bullyese. Ilikuwa ni hatua ngumu lakini Wakenya ndio waliofanikiwa kufikia hatua ya pesa ukutani ambapo walifanikiwa kujishindia dola za kimarekani 1,500.


  Daniel, Mwalimu, Kenneth na Wills wataendelea kuziwakilisha nchi zao kuwania kitita cha dola za kimarekani 250,000 na nafasi ya kuvishwa taji la ubingwa  wa Pan-African. Timu hizi mbili zitatakiwa kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili ziweze kujinyakulia ushindi.


  Meneja wa kinywaji cha Guinness,Devis Kambi alisema, “Hongera kwa Daniel na Mwalimu kwa kufanikiwa kufuzu kuingia nusu fainali. Bado tunaendelea kuburudika na mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE baada ya kuona robo fainali wiki iliyopita. Sasa ushindani utakuwa mkali zaidi kwa kuwa tumebakiwa na timu nane tu katika nusu fainali. Timu zote sasa zinahitaji maandalizi ya kutosha ili ziweze kufanya vizuri katika hatua hizi za mwisho za kuelekea fainali. Kila la heri kwa timu zinazofuata kucheza wiki hii!”  Timu zitakazo shiriki katika robo fainali ya tatu ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE      :   


  ·         Kutoka Kenya watakuwa ni Enpantus Nyambura(24) na Samuel Papa(23) kutoka Nairobi, watavaa jezi nyekundu. Wakitarajia kufanya vyema zaidi kuliko awali Enphatus atakuwa kichwa cha timu wakati Samuel ataonesha kipaji chake cha kusakata kabumbu.


  ·         Watakaovaa jezi za bluu watakuwa ni wanafunzi wa Ghana, George Duah (21) na Yahya Issaka(20) kutoka Takoradi. George ni kichwa cha timu wakati Yahya ndiye atakayechezea mpira.Walifanikiwa kufuzu kuingia katika fainali ya kitaifa baada ya kujishindia  dola 3,000.


  ·         Kutoka Cameroon Florent Tonya(29) na Christian Lolo Mboko(24) kutoka Douala watavaa jezi za kijani katika robo fainali ijayo na katika hatua ya kitaifa wajishindia dola 3,000. Florent atajibu maswali wakati Christian atakuwa akionyesha kipaji chake cha kucheza soka.


  ·         Ghana itawakilishwa na Jonathan Naab(25) kutoka Tindogo na Desmond Odaano(26) kutoka Larteh watavaa jezi nyeusi katika robo fainali ijayo. Awali timu hii ilijishindia dola za kimarekani 5,500 katika hatua ya kitaifa. Jonathan atakuwa akipima maarifa yake wakati Desmond ataichezea mpira.


  Robo fainali ya tatu ya Pan-African itarushwa katika televisheni za ITV na Clouds TV usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.

  Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.  


  Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.

  -www.facebook.com/guinnesstanzania


  GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.


  Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 


  Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.


  0 0


  Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Mei 13-18. Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa. 
   Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde akizungumza  wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Mei 13-18. na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA. Kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa. 

  MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imeandaa Maonyesho ya Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambayo yanatarajiwa kufanyika Mei 13 hadi 18 mjini Dodoma.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, alisema, makampuni na mashirika mbalimbali yanatarajia kushiriki wiki, ambayo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.
  Alisema kuwa, maonyesho hayo itakuwa ni pamoja na mifuko shiriki kutoa elimu kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, juu ya huduma ambazo zinapatikana na tija yake katika taifa.

  Aidha, Irene aliongeza kuwa, SSRA inawataka wanachama wa PSPF kuondoa hofu juu kutokuwepo kwa mafao yao katika mfuko huo, na kwamba mafao yao yako salama na hakuna kitakachopoteza mafao ya wanachama hao.


  Alisema kuwa, mfuko wa PSPF utakuwa ukipewa bilioni 50 kila mwaka kwa ajili ya kwa ajili kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida .

  Irene pia, aliwataka wanachama wa mifuko mbalimbali kuwasilisha michango yao kwa wakati ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifuko kutokana na SSRA kutoa miongozo juu ya uendeshaji wa mifuko hiyo.


  Alibainisha kuwa, mifuko yote imepewa miongozo katika uendelezaji huduma wanazozitoa ikiwamo ya mafao kwa wafanyakazi wanaostaafu.


  Alisema kuwa tatizo lililokuwepo kwa mifuko ya PPF na NSSF, kujitoa kwa wingi kwa wanachama wake, jambo linalochangiwa na waajiri, hali ambayo SSRA inataka kuwafuatilia waajiri wanaowanyima wafanyakazi haki zao.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Ujumbe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo Mei 6, 2013. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, uliofika Ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo Mei 6, 2013 kwa mazungumzo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Profesa Gang H.W, baada kumaliza mazungumzo na ujumbe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, uliofika Ikulu Dar es Salaam, leo Mei 6,2013 kwa mazungumzo. Picha OMR.

  0 0  ========================


  0 0


   The Imports International (T) Ltd (IITL) Group Director Harish Ladwa briefs journalists during the 10th Anniversary and Show room launch in Dar es Salaam at the weekend
   The Imports International (T) Ltd (IITL) Group Director Director Harish Ladwa briefs guests on the company’s prospects during the 10thAnniversary and Showroom launch in Dar es Salaam at the weekend. 
   The Imports International (T) Ltd (IITL) Group Director Harish Ladwa (right) and the company’s Managing Director Trushal Jethwa (left) follow proceedings of the 10th Anniversary and Show room launch in Dar es Salaam at the weekend
  The Imports International (T) Ltd (IITL) Group Director Harish Ladwa (right) and the company’s Managing Director Trushal Jethwa (left) follow proceedings of the 10th Anniversary and Show room launch in Dar es Salaam at the weekend
  ========  ========  ========
  Imports international marks 10th Anniversary, eyes regional markets

  IMPORTS International (T) Ltd (IITL),  a local company that imports and distributes some of world’s leading brands in construction and building materials in Tanzania is set o embark on an aggressive expansion plan that will see the company open up outlets in Uganda, Rwanda and Burundi.

  Speaking during the 10th Anniversary and Show room launch in Dar es Salaam at the weekend, the IITL Group Director Harish Ladwa said the company’s mission seeks to ensure that the region’s construction sector gets quality products that meet ISO global standards. 

  Ladwa said the past 10 years of operations of his company have been very exciting forecasting that the coming years hold even greater opportunities urging that customers should brace themselves for quality products at very competitive rates.

  “Since IITL’s inception in 2003, the company has maintained it vision and concept of providing all customers big or small with best quality material at the lowest prices possible.

  “With this vision and hard work by our loyal staff and dedicated customers, the company has enjoyed success in its ten years of operations and we are proud to launch our state-of- the art 3500 sq/mtr warehousing facility on Nelson .

  Mandela today in commemoration of our 10th Anniversary,” Ladwa said.
  Ladwa however called upon Government agencies to embark on quality control in a bid to intensity fight against the importation of fake construction materials urging that the vice doesn’t only hurt the country’s construction sector but the economy as well.

  “The market is today flooded with fake construction materials that put users at risk. Government should instill various quality control mechanisms and take tough action against importers of such products,” he added. Ladwa called upon consultants, archetects and government organization to support the company’s products in a bid to increase quality standards of the country’s construction industry which will in turn help to ensure quality development in the country.

  He expressed his company’s commitment to working with various world class construction material manufacturers that include Saint Gobain, Donn, Jaquar ,Montania  and Tilcor among others .

  Ladwa said IITL has handled various construction products in Tanzania that include Holiday Inn Hotel, PSPF Tower, Ideal Residence Ltd, Cineplex Cinema (Quality Centre), NSSF Plaza , Airtel Head Office , Exim Tower refurbishment and Protea Court Yard Hotel (Dar es Salaam) among others.

  0 0

   Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Masika(kulia) akitoa maelezo mafupi kuhusu chuo cha Ufundi Arusha kwa balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik mara tu alipowasili Chuoni hapo.
   Mkuu wa Idara ya Mitambo Chuo cha Ufundi Arusha, Eng. Jafari mwanza akitoa maelezo mafupi kuhusu aina mbalimbali za mitambo ya kufua umeme inayotengezwa chuo hapo kwa Balozi wa Norway Chin Bi. Ingunn Klepsvik.

   Balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik akipokea maelezo mafupi kuhusu Maabara ya Upimaji Udogo
   Balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik akipokea zawadi ya bangili
  Balozi wa Norway Chini, Bi. Ingunn Klepsvik akipokea maelezo mafupi kuhusu karakana ya useremala

  0 0


  Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati) ,Matron Hilda Mwinyi (Kulia), na Mratibu wa kamati ya maandalizi Kessy Salum Mbasha (Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach.
  =======  =====  =======
  AFISA UTAMADUNI JIJI LA TANGA AKAGUA KAMBI YA TAIFA YA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 ILIYOKO JIJINI TANGA.

  Wakati Maandalizi ya fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013 yanaendelea kwa kasi katika hoteli ya kitalii ya Mwambani iliyopo katika ufukwe wa Tanga, huku kila Mrembo akijifua vikali, Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Tanga Ndugu Peter Semfukwe ametembelea kambini hapo, kujionea yeye mwenyewe warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 ambao wanajiandaa na Fainali hizo za Taifa zitakazo fanyika wiki Ijayo,kasha alizungumza nao na kuwakaribisha mkoani Tanga.

  Afisa Utamaduni  alisema  kuwa amefurahi kukutana na warembo wote wakiwa katika Afya Njema, Mvuto na kila mmoja kuonekana ndiye atakaye twaa taji hilo la Miss Utalii Tanzania 2013, pia ameipongeza kamati ya maandalizi kwa juhudi na jitihada kubwa za kuandaa mashindano hayo ambayo dhima yake ni kuutangaza utalii wa ndani pamoja na utamaduni wa Mtanzania.  Aliongeza kuwa anaahidi  ushirikiano mkubwa wa hali na mali wakati wa maandalizi mpaka mwisho wa mashindano hayo.

  Akizungumza na Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Miss Utalii Tanzania , Afisa Utamaduni aliwaasa warembo hao wawe na heshima, adabu, na pia wawe ni mfano bora wa kuigwa katika jamii ikiwa ni warembo hao kuwa mstari wa mbele katika kushiriki, kutangaza Utalii na Utamaduni wa Mtanzania.

  Mpaka sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini ,wanajiandaa vizuri  kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
  Akizungumzia, juu ya maendeleo ya kambi, Fredy Njeje, alisema kuwa baada ya kukwamishwa na wadhamini walio toa ahadi hewa, wamelazimika kuhamishia shindano hilo mkoani Tanga,baada ya kuvutiwa na mwamko wa wafanya biashara na makampuni ya Jiji la Tanga wa kuwa na uwezo wa kudhamini matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa.
  Tunakabiliwa na changamoto ya warembo wengi kuwa wapya katika kambi yetu,baada ya wale waliokuwako kambini kabla ya kambi kuahirishwa kushindwa kurudi kambini kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za kimasomo na wengine kukata tama baada ya kuahirisha. 
  Hata hivyo tayali nafsi zao zimechukuliwa na washindi wa pili wa mikoa yote ambayo warembo wake wameshindwa kurudi kambini, na tayali warembo 30 wameripoti kambini na tunategemea wengine 10 kuripoti kambini wakati wowote ili kufikisha idadi ya warembo 40 wata kao panda jukwaani. 
  Tumejiandaa na tunapata ushirikiano mkubwa kwa serikali ya mkoa nay a Jiji la Tanga, hivyo kutuhakikishia kuwa tarehe itakayo pangwa sasa haitabadilika tena wala kuahirishwa. Tarehe kamili ya shindano itatangazwa kesho na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ambaye pia ni Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga.
  Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia na nchi yatakako fanyika katika mabano  International Miss Tourism World (Marekani), Miss Tourism United Nation (Mexico), Miss Heritage World (Tunasubiri Taarifa), Miss Tourism University World(Tanzania), Miss Globe International (Uturuki), Miss Tourism World ( Equatorial Guinea ), Miss Freedom Of The World ( Kosovo) , na Miss Tourism United Nation (Nigeria)  n.k

  Wakati huohuo, katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya Fainali za taifa, za mashindano hayo ambapo mkoa wa Tanga unakuwa wenyeji kwa mara ya kwanza yanafanyika kwa ubora na hayakwami, kamati ya maandalizi ya kimkoa umeundwa ambayo mwenyekiti wake ni Peter Semfuko Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga. 

  Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
  Model Of The World 2008-Personality, Miss Africa 2006 – 1ST Runner Up n.k

  0 0


  Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili .
  Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pili .


  Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pili 
  Bondia Chilambo Hemed kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Boniface Urasa wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki Chanika Chilambo alishinda kwa point .
  Bondia Said Mbelwa akipambana
  Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
  Refarii Saidi Chaku akimwinua mkono juu Bondia saidi Mbelwa kuashilia ni mshindi katika mpambano huo

  0 0


  0 0

    Wasanii wa kundi la Wanaume Halisi wenye makazi yao Jijini Dar es salaam Temeke wakiongozwa na Juma Nature wakipanda jukwaani kwa ajili  kutoa burudani mfululizo wakati wa mrindomo wa tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu
   Msanii wa kikundi cha tip top connection Madii akitoa burdani kwenye tamasha la Airtel yatosha lililofanyika katika viwanja vy zhakem  - Mbagala Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii
   Wasanii wa kundi la Wanaume Halisi wenye makazi yao Jijini Dar es salaam Temeke wakitoa Burudani Mfululizo katika tamasha la maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu
   Msanii mahiri wa Hi Hop nchini maarufu kama FID Q akikamua katika jukwaa maalum la kuitambulisha huduma kabambe ya Airtel Yatosha katika viwanja vya Zakhem jiini Dar es Salaam na kufanikisha kuwaunganisha watanzania na wakazi wa jijini Dar es salaam kwenye huduma ya Airtel Yatosha.

   Kikundi cha wakali dansi cha temeke kikitoa burdani Mfululizo katika tamasha la maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya zakhem -mbagala dar es salaam na kuwavuta maelfu ya watu
  Mwanadada msanii chipukizi wa temeke akitoa burdani kwenye tamasha la Airtel yatosha lililofanyika katika viwanja vya zhakem  - Mbagala Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii

  0 0


  Exim Bank Managing Director Anthony Grant

  EXIM Bank, Tanzania’s sixth largest bank by total assets and deposits, has been shortlisted for the “Best Retail Bank in Africa” in African Banker Awards 2013.

  Other banks shortlisted for the same category include Banque Centrale Populaire, Morocco, Compagnie Generale de Banque Ltd, Rwanda, Coris Bank, Burkina Faso and Ecobank Transnational, Togo, among an impressive number of strong and deserving entries, following a record-breaking number of entries this year.

  African Banker Awards is one of the biggest landmark annual events that recognises and celebrates the achievements of Africa’s banking and financial sector. A statement issued by the Exim Bank Managing Director Anthony Grant yesterday said the short listing is not only recognition for the bank but an honor for the country as a whole.

  “Exim Bank is pleased to receive the honor and we look forward to being the finalist among the contenders to win the award. Our Board of Directors has supported the investment of considerable resources for developing tailor-made retail banking products to serve our customers. We are pleased to see that our efforts are paying back at many levels.

  “Indeed we happy to represent Tanzania in Africa at such prestigious awards,” Grant added. Mr Grant said that the bank’s submission had also cited retail banking accomplishments at the Exim Bank affiliates in Comoros and Djibouti. He also noted that in October of 2008 he had been invited by the African Banker to serve as Master of Ceremonies for the Awards, held that year in Washington, D.C.  

  Commenting on this year's entries Omar Ben Yedder, Publisher of African Banker magazine, said: "I remain a staunch defender of the positive role banking institutions can play. The two biggest listed companies in China are both financial institutions and they play a critical role in the economy. The same can be said about many banks in Africa. The entries seem to get better year after year.

  “The variety of entries and the quality of these entries, especially in the Deal of the Year category, illustrate the increased sophistication and the growing investment banking activity across Africa, and that can only be encouraging. Through the awards we are trying to create a benchmark and to promote best practice.

  Yedder said the awards committee was highly encouraged by the examples of leadership, innovation and dynamism highlighted in this year's entries.'
  The African Banker Awards is organised by African Banker magazine, IC Events and Business in Africa Events. It is a landmark event that brings together over 500 key industry players and top government officials from Africa and around the world to celebrate excellence and best practices in African banking and finance.

  A distinguished and independent panel of judges, known and respected for their expertise on the African banking and finance industry, will decide the final winners of each category.

  The winners will be announced at the awards ceremony on the 29th May during the annual African Development Bank (AfDB) meetings in Marrakech, Morocco. Last year’s awards were held in Arusha during the annual AfDB meetings.

older | 1 | .... | 76 | 77 | (Page 78) | 79 | 80 | .... | 1898 | newer