Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

UPDATES YA MSIBA WA MZEE KASSIM MAPILI

$
0
0
POKEA TAARIFA RASMI YA MAZISHI YA MZEE KASSIM MAPILI NI LEO IJUMAA 26/02/2016 SAA KUMI JIONI KISUTU,MAITI HAIPO KTK HALI NZURI DAKTARI KASHAURI AZIKWE HARAKA,MSIBA UPO MTAA MAGOMENI NA.23 MAPIPA,TUJITOKEZENI WAPENDWA KAMA UNGEPENDA KUKIUNGA NASI KWA MCHANGO BASI TUMA RAMBIRAMBI KWA HASSAN MSUMARI-KATIBU MKUU CHAMUDATA. NAMBA ZAKE 0717340533 .. ADDO NOVEMBER - RAIS SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA... 0744150000

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMLILIA MZEE KASSIM MAPILI

MAWAZIRI WAPEWA MWISHO LEO KUJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI, HATI YA UADILIFU

$
0
0
 Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majliwa Majaliwa (kulia) akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki.
 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna.(PICHA ZOTE NA EBENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wawe wamejaza fomu hizo na kuzirejesha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam ifikapo leo saa 12.00 jioni (Ijumaa, Februari 26, 2016).

Agizo hilo la Rais limetolewa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Rais ameelekeza mawaziri ambao hawajajaza tamko la rasilmali au hati ya ahadi ya uadilifu wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni na Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake,” amesisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema wakati akifungua mafunzo ya Mawaziri na Naibu Waziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu yaliyofanyika Ikulu jana (Alhamisi, Februari 25, 2016) alikabidhiwa majina ya Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao hawajawasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili.

Amewataja mawaziri wanaotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Bw. January Makamba. Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye anatakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye anatakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira), Bw. Luhaga Mpina anatakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilmali na madeni pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.

Shirikisho la Filamu lapata viongozi Wapya.

$
0
0
 Rais Mteule Bw. Simon Mwakifwamba .

Na Shamimu Nyaki-Maelezo.

Kufuatia uchaguzi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam  wa kutafuta viongozi  wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) viongozi wapya wamepatikana ambao ni Rais, Makamu wa Rais, pamoja na Wajumbe kumi wa Bodi watakaongoza Shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne.

Akisoma matokeo ya uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Nico Mathew amesema kuwa, idadi ya wajumbe waliojiandikisha kupiga kura ilikuwa ni 69 lakini waliopiga kura ni 52 ambapo   Bw. Simon Mwakifwamba aliekuwa anagombea nafasi ya Urais  kwa awamu ya pili alipata kura 47 kati ya 52 zilizopigwa na wanachama wa vyama mbalimbali vya tasnia hiyo na Makamu wake Bw. Deo Sanga  alipata kura  49 kati ya 52.

Wajumbe wa Bodi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Adam Juma Mikidadi, John Kalaghe, Irene Sanga, Juma Issa, Michael Sangu, Single Mtambalike, Hussein Athumani, Ummi Mohamed, Nazir Masila pamoja na Alli Mohamed.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Rais Mteule Bw. Simon Mwakifwamba ameahidi kuendelea kukuza tasnia ya filamu nchini kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali na wadau wa Filamu ili kuweza kuvuka mipaka ya ndani ya nchi kwa manufaa ya wasanii na Taifa.

“Asanteni sana kwa kuniamini tena kwa awamu nyingine naahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na nyie  kwa weledi, ubora  na uhitaji ili tufanikiwe zaidi”, alisema Mwakifwamba.

Ameongeza kuwa katika awamu hii ya miaka minne ameandaa vipaumbele vitano ambavyo ni Kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha Sera ya Filamu inapatikana, kupata elimu kuhusu tasnia kwa wasanii, kuanzisha mfuko wa maendeleo ya Filamu,  na usambazaji bora wa Filamu hapa nchini ili wasanii wanufaike na kazi zao. 

Uchaguzi wa shirikisho hilo umefanyika kutokana na viongozi waliokuwepo kumaliza muda wao kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho hilo ambapo viongozi waliopatikana wameahidi kuleta mabadiliko chanya katika tasnia ya Filamu nchini. 

MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh. Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba (kushoto) akiongea na Balozi wa Kuwait Bw. Jasem Al-Najem, Balozi huyo alimtembelea Mh. Makamba Ofisini kwake leo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana masuala ya hifadhi na usimamizi wa Mazingira. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makumu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Barthlomew Jungu.

TANZIA

$
0
0
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania wanasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao, Sarah Sanga.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA MWAKILISHI WA UNHCR NCHINI

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), Bi. Joyce Mends- Cole, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

BASATA YAMLILIA MSANII KASSIM MAPILI

$
0
0


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii Mkongwe wa muziki wa dansi Kassim Mapili kilichotokea katikati ya wiki hii nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam.


Kassim Mapili ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.


Mchango wake katika muziki wa dansi na ule wa kiweledi katika kuandaa na kukuza bendi na wasanii mbalimbali wa muziki wa dansi nchini hautasahaulika kamwe. Ni Msanii aliyeacha alama kuu katika muziki wa bendi na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa dansi ulipo leo.


Aidha, pamoja na kuwa mwimbaji na mpigaji gitaa katika Bendi mbalimbali zikiwemo za Kilwa Jazz, Polisi Jazz, Vijana Jazz na nyingine nyingi Mzee Kassim Mapili alikuwa mstari wa mbele kujenga mfumo wa Utawala kwenye sekta ya Sanaa na kuhakikisha wasanii wa muziki wa dansi wanakuwa na chombo cha kuwawakilisha na kutetea maslahi yao.


Mwaka 1982 alikuwa miongoni mwa wasanii waliokutana Mjini Bagamoyo na kuunda Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) ambacho hadi leo kinatetea na kuwawakilisha wasanii wa muziki wa dansi.


Aidha, Mzee Mapili amekuwa bega kwa bega na Baraza la Sanaa la Taifa katika programu zake mbalimbali na utendaji kazi wa kila siku. Kwa mfano; amekuwa mmoja wa wadau ambao wamekuwa wakishiriki kikamilifu kwenye Programu ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na BASATA kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni.


Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Kassim Mapili hasa katika kutunga nyimbo za hamasa na ujumbe makini na wenye mashiko kwa jamii yote ya Watanzania.Hakika pengo lililoachwa na Marehemu haliwezi kuzibika, kwani imekuwa ni kama mshumaa uliyozimika ghafla wakati tukiingia kwenye giza.

Baraza linatoa pole kwa familia ya Marehemu, chama cha muziki wa dansi, shirikisho la muziki na wasanii wote kwa ujumla. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu, hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu ya Sanaa na taifa kwa ujumla.


Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

Godfrey Mngereza

KATIBU MTENDAJI




Badilisheni sera zenu muandike habari chanya kwa watu wenye ulemavu: Dkt possi

$
0
0
 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi akizungumza na Wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini Dare s salaam.
Mhadhiri toka Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Shule ya Uandishi wa Habari Dkt Ayoub Riyoba (katikati) akimsikiliza Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi alipokutana na Wamiliki wa Vyombo vya habri kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji toka Azam Media Yahya Mohamed na kushoto ni Meneja wa Uendeshaji toka Sahara Media Steve Diallo.Picha zote na Raymond Mushumbusi

Na Joseph Ishengoma
 
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt  Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuwa na sera katika vyombo vyao inayojumuisha uandishi wa habari chanya kwa watu wenye ulemavu.

Akitoa agizo hilo mbele ya wamiliki wa vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Waziri Possi amesema habari nyingi zinazohusu watu wenye ulemavu ni za kuwanyanyapaa na kuonesha kuwa hawana uwezo wa kufanya mambo chanya.

“Wekeni kipengele katika sera zenu kitakachosaidia kuwaelimisha watu kuwa watu wenye ulemavu ni sehemu ya jumuiya katika maisha ya kila siku ya wanadamu,” amesema.Kwa mujibu wa Waziri Possi, vyombo vya habari vikiwa na sera iliyowazi na kuitekeleza, watu watabadilika na kupata taarifa nzuri za watu wenye ulemavu.

Dkt. Possi ameeleza kuwa taarifa za watu wenye ulemavu hazitakiwi kuwa na lugha zenye chembechembe za kunyanyapaa.Amesema kuwa kila kituo cha televisheni kinatakiwa kuwa na wataalamu wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama.

Amesema, “Serikali kwa kutumia Sheria ya Watu wenye ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 inaandaa tangazo kuvikumbusha vyombo vya habari kuwa kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu.” 

Aidha Naibu Waziri amewaagiza wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu kwani Sheria inaagiza lazima chombo chochote chenye wafanyakazi zaidi ya 20, angalau mfanyakazi mmoja awe mtu mwenye ulemavu.

Kwa upande wao wamiliki wameiomba serikali kutotoza kodi tangazo lolote linalohusu habari chanya za watu wenye ulemavu.

Hata hivyo wamiliki hao wamemweleza Naibu Waziri kuwa ubadilishaji wa Sera pamoja na kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa watu wenye ulemavu ni jambo zuri, lakini wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI CHAFANYIKA LEO.

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Jesh Lupembe akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halamshauri hiyo.
Baadhi ya watendaji wa Halmashari ya Manispaa ya Moshi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo .
Baadhi ya Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa  katika kikao cha baraza hilo.
Diwani wa kata ya Ngangamfumuni ,Anthony .......akichangia hoja katika kikao cha bajeti cha Halmashauri ya manispaa ya Moshi .

Diwani wa kata ya Ng'ambo ,Genesis Kihwelu akichangia hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Kilimanjaro,Priscus Tarimo akifuatlia hoja katika kikao hicho.
Msathiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (Kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Jesh Lupembe.
Diwani wa kata ya Kiusa ,Stephen Ngasa akichangia hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Mji Mpya ,Abuu Shayo akichangia hoja katika kikao hicho.
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia michango ya madiwani wenzao katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Miembeni,Mbonea Mshana akichangia hoja katika kikao hicho.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akiwa katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Bondeni Masiu Kilusu akifuatilia hoja za madiwani wenzake.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafry Michael pia laikuwa ni miongoni mwa madiwani waliohudhuria kikao hicho.

Na  Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

Tanzania kunufaika na Dola Bilioni 60 za China sekta ya Nishati

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiongea jambo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Dkt. Lu Youqing (wa pili kushoto)  wakati alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni  Afisa Ubalozi wa China. 
 Balozi wa wa Jamhuri ya Watu wa China, Dkt. Lu Youqing (katikati) akimweleza jambo Afisa Ubalozi wa China nchini, wakati wa kikao chake na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia). 
 Afisa Ubalozi wa China nchini (wa kwanza kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao chake na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (katikati).
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa tatu kushoto), akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Utumishi Wizara ya Nishati na Madini, Lusias Mwenda. Wengine ni ujumbe ulioambatana na Balozi wa China.

 Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imeitaja nchi ya Tanzania kuwa na nafasi kubwa ya kunufaika na fedha kiasi cha Dola Bilioni 60  kupitia  uwekezaji sekta ya nishati, fedha zilizoahidiwa kutolewa na nchi hiyo wakati wa Mkutano wa Sita wa Jukwaa la Ushirikiano baina ya China na Afrika, uliofanyika nchini Afrika Kusini mwezi  Desemba,2015.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing na ujumbe wake alipokutana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, China ina imani kubwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna anavyosimamia masuala mbalimbali nchini, pia Profesa Sospeter Muhongo kutokana na  namna anavyoisimamia sekta ya Nishati  na Madini.Miongoni mwa Sekta zinazopewa kipaumbele katika fedha hizo ni pamoja na pamoja na  miundombinu, afya, biashara, uwekezaji na kupunguza umaskini, barani Afrika.

Kutokana na mahusiano mazuri ambayo yamekuwepo kwa miongo kadhaa baina ya nchi hizo mbili, Balozi Youqing amemwakikishia Waziri Muhongo kuwa, China itaendeleza ushirikiano huo kwa kuhakikisha inazishawishi kampuni kubwa na zilizobobea kitaalamu na kiteknolojia za China, ili ziweze kushirikiana na Tanzania katika sekta ya nishati, na zaidi katika uzalishaji umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe kutokana na namna ambavyo Wizara inavyokipa kipaumbele chanzo hicho kuzalisha umeme nchini.

Wakati huo huo, China imesema itaendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi Watanzania kusoma masuala ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali nchini humo kutokana na umuhimu wa sekta hiyo na kwamba, China inapenda Tanzania ifanikiwe katika kuzalisha wataalam wa kutosha katika fani hizo na kuongeza kuwa, anatambua juhudi zinazofanywa na Waziri Muhongo kuhakikisha wanafunzi wengi wa kitanzania wanapata fursa ya kusoma masuala ya mafuta na gesi maeneo mbalimbali Duniani, ikiwemo China.


Aidha, leo tarehe 26 Februari, 2016, Wizara ya Nishati imetangaza nafasi za Masomo kwa wanafunzi wa Kitanzania kuomba kusoma katika Vyuo vya China katika fani za Mafuta na Kazi katika ngazi za Shahada ya Uzamili (Masters) na Uzamivu (Phd). Maelezo zaidi ya kuomba nafasi hizo yanapatikana kupitia tovuti ya wizara www.mem.go.tz

MAZISHI YA MAREHEMU GERVASE RUTAGUZA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO .

$
0
0
Ndugu wa Marehemu wakiwa katika ibada nyumbani kwa Marehemu Kurasini jijini Dar es Salaam ibada ya kumuaga marehemu Gervase Rutaguza aliyefariki dunia Februari 23 mwaka huu.
Padre wa kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam akiombea mwili wa marehemuGervase Rutaguza aliyefariki dunia Februari 23 mwaka huu kwaajili ya kwenda kwenye mazishi katika makaburi ya Chang'ombe Maduka mawili jijini Dar es Salaam leo Februari 26, 2016.







Baadhi ya ndugu na Jamaa wa Marehemu Gervase Rutaguza aliyefariki dunia Februari 23 mwaka huu wakiaga mwili wa marehemu leo katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam leo Februari 26, 2016.






Ndugu jamaa na marafiki wa Marehem Gervase Rutaguza aliyefariki dunia Februari 23 mwaka huu wakiwa katika ibada katika Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini jijini Dar es Salaam leo na kuelekea katika makaburi ya Chang'ombe Maduka mawili jijini Dar es Salaam leo.

AIRTEL FURSA YAINUA KIKUNDI CHA VIJANA WAJASIRIAMALI MJINI LINDI.

$
0
0
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kushoto), akiwapongeza kikundi cha vijana watano wajasiriamali  kijulikanacho kwa jina la Sauti ya Jamii baada ya kuwakabidhi msaada wa Zizi jipya la mbuzi, mbuzi 44 na vitendea kazi  kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ mjini Lindi katika mtaa wa Kariakoo. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Afisa maendeleo ya vijana mkoa wa lindi Sauda Mponjoli akifuatiwa na Afisa Utamaduni Mkoa, Makalaghe Shekhalaghe.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kushoto), akiwapongeza kikundi cha vijana watano wajasiriamali  kijulikanacho kwa jina la Sauti ya Jamii baada ya kuwakabidhi msaada wa Zizi jipya la mbuzi, mbuzi 44 na vitendea kazi  kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ mjini Lindi katika mtaa wa Kariakoo. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Afisa maendeleo ya vijana mkoa wa lindi Sauda Mponjoli akifuatiwa na Afisa Utamaduni Mkoa, Makalaghe Shekhalaghe.
Meneja wa Huduma za jamii Kampuni ya Airtel Tanzania,Bi Hawa Bayumi (kati) akitoa elimu Kwa Afisa Utamaduni Mkoa,Makalaghe Shekhalaghe (kulia) pamoja na Afisa Vijana mkoa Lindi Bi Sauda Mponjoli (wa pili kulia Jinsi Airtel inavyotoa Fursa kwa Vijana Kupitia Airtel Fursa wakishuhudiwa na vijana wa kikundi cha Sauti ya Jamii waliowezeshwa na mradi huo wa Airtel Fursa kwa kupatiwa  Zizi jipya la mbuzi, mbuzi 44 na vitendea kazi vyenye dhamani ya shs milioni 10.

 WAFANYAKAZI wa kampuni ya simu za mkoni ya Airtel mkoani Lindi wamejumuika katika mradi wa kijamii wa  kampuni yao wa Airtel FURSA kwa kuwawezesha vijana wajasiriamali wa kikundi cha sauti ya jamii mkoani humo kwa kuwainua kibiashara na kuwajengea banda la ufugaji wa mbuzi la kisasa na kuwaongezea mbuzi 44 pamoja na vitendea kazi kama vile majembe na rato kwa ajili ya kuanza kilimo.

Vijana hao wapatao watano waliamua kuungana kwa pamoja baada ya kupata mafunzo kwenye mradi wa Kijana Jiajiri uliokuwa unaendeshwa na shirika la Restless Development ambao ulilenga vijana walio nje ya shule; kuwajengea uwezo ili waweze kujiajiri wenyewe na kupunguza ukosefu wa ajira nchini.

Kikundi cha Sauti ya Jamii kimesajiliwa na halmashauri, na kiliomba ardhi serikali za mitaa kwa ajili ya kilimo na kikapewa ekari 50, hivyo ukosefu wa mtaji ndio uliwakwamisha kuanza shughuli za  kilimo.

Akiongea wakati wa ujenzi wa banda hilo la kisasa la mbuzi  kiongozi wa msafara wa ziara hiyo na meneja mauzo kanda ya Lindi Edmund Lasway  alisema “Airtel tunayofuraha kuona tunaweza kusaidia vijana wenye moyo wa kujiendeleza kama hawa. Kabla ya hapa wamekuwa na mbuzi wapatao kumi na nne ambapo hawakuweza kuwapatia faidi ya kutosha, lakini kutokana na ongezeko hili la mbuzi na vitendea kazi kwa ajili ya kuinua biashara yao  ili waweze kutimiza malengo yao mengine makubwa waliyojiwekea  kama vile ya ukulim” .

Ni matumaini yetu kuwa fursa hii itawawezesha kufika mbali kibiashara na kutanua wigo wa biashara yao kwa kupata masoko na kuuza mifugo na kulima mazao yao katika ubora zaidi . Tunatoa wito kwa vijana wengine  kujitokeza na kutokukata tamaa ya maisha na kuchangamkia fursa kama hizi pale zinapojitokeza.

Kwa upande wake mwakilisha wa kikundi cha Sauti ya jamii, Shabani Kikotokeki, alisema “tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha kuinua biashara yetu na kutupa nguvu zaidi ya kujiendeleza kibiashara na hata kuwatia moyo vijana wenzetu wanaotuzunguka. Tunategemea kuinua kipato chetu na hata familia zetu  hivyo tunawahimiza vijana wengine hapa nchini kutokukata tamaa ya maisha na kuchangamkia fursa hizi zinapojitokeza.





Airtel kupitia huduma zake za jamiii imeweza kuwafikia vijana zaidi ya 20 kwa kuwapatia vitendea kazi katika msimu huu wa pili wa Airtel FURSA na kwa upande wa mafunzu ya biashara ya ujasiriamali imewafaidisha vijana wapatao 1000 katika  msimu huu wa pili wa  Airtel FURSA ambapo lengo ni  kufikia vijana wengi zaidi.

Waziri Jenista Mhagama atembelea Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akikabidhi vitendea kazi kwa Mh. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja na Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama (kushoto), ofisini hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Jenista Mhagama akizungumza na wafanyakazi wakati alipotembelea Mamlaka hayo kwa lengo la kujionea utekeleza wa Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi. Irene Isaka akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja na Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama (kushoto), ofisini hapo.

MBUNGE COSATO AFANYA ZIARA JIMBONI KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI.

$
0
0
Mbunge wa Mafinga Vijijini, Cosato Chumi  (Mwenye diary mkononi) akipata maelekezo katika kiwanda cha kiwanda cha Sao Hill katika ziara ya kutembelea Taasisi Binafsi na za Umma. 
 Mbunge wa Mafinga Vijijini, Cosato Chumi (wa pili kutoka kushoto)akionyeshwa shughuli zinazofanywa katika kiwanda cha Sao Hill.
Wengine  ni Denis kutemile anayefuatia na Hezron Vuhahula ambaye ni katibu wa mbunge.
 Baadhi ya wafanyakazi wa sao hill wakiwa kazini.
 Sehemu ya nguzo zinazozalishwa  na kiwanda cha Sao Hill.

MBUNGE wa Mafinga Vijijini, Cosato Chumi amefanya ziara kutembelea  Taasisi za Umma na Binafsi kwa kutembelea Sao Hill Industries, Sao Hill Forest, Kiwanda cha Pareto na kampuni ya simu ya TTCL.

Katika ziara hiyo mbunge ametembelea Vituo vya Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), NSSF , Bank za Mucoba, NMB na CEDB,Magereza ,pamoja na Taasisi za Elimu.

Amesema kufanya ziara ni kujitambulisha, kufahamiana na kufahamu changamoto wanazokabiliana nazo.

Chumi amesema nguzo za umeme, kutoka Afrika Kusini  sio sahihi wakati  zinaweza kupatikana na uwezo wa kuzalisha  nguzo 90000 kwa mwaka.

Amesema kutokana na maelezo ya kiwanda hicho  na wamesema ikiwa watapata nafasi ya kuongezewa uwezo wa kuvuna kutoka Shamba la Taifa la Msitu wa Sao Hill, wanaweza kusambaza nguzo zaidi.

 Mgao wa kuvuna wa cubic 120,000 Changamoto ni kuwa wakipewa kitalu lakini ndani ya kitalu sio kila mti unafaa kwa nguzo kwa hiyo ombi lao, wapewe kwa mfumo wa kwamba wavune kile ambacho kinafaa kwa nguzo harafu miti inayofaa labda kwa karatasi ibaki kwa ajili ya Kiwanda cha mgololo.

wakati huohuo wawekezaji Mafinga waiomba Tanesco kuwafungia laini madhubuti ya Umeme katika kiwanda cha Pareto ambacho kiko chini ya Kampuni ya Pyrethrum Company of Tanzania (PCT).

MTAMBUE KIJANA WA KITANZANIA DESMOND ANDREW ALIYEANZISHA KAMPUNI YA MAWASILIANO YA CW NET

$
0
0
Kijana wa Kitanzania Desmond Andrew ameanzisha kampuni ya Mawasiliano ya CW Net ambayo inatengeneza Power Bank, Smart Bracelet na Modem. Hakika Tanzania kuna vijana wengi kama Desmond Andrew lakini tatizo kubwa linalowakabili ni upatikanaji wa mtaji wa kuendeleaza vipaji vyao.
Mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya Mawasiliano ya CW Net akimtoa ufafanuzi Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) kuhusu Smart Bracelet na kazi zake katika maonesho yaliyoandaliwa na shirika la Viwango nchini Tanzania(TBS) yanayoendelea katika ukumbi wa Mlimani Cityjijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geoffrey Simbeye (aliyevaa suti) akiuliza swali mara alipotembelea banda la CW Net maonesho ya Makampuni ya Kitanzania yanayotoa bidhaa yenye viwango vya kutosha hapa nchini.
Smart Bracelet hiki ni kifaa mojawapo kinachotengenezwa na kampuni ya Mawasiliano ya CW Net ambacho kifaa hicho kinahesabu hatua ambazo mtu ametembea nani kwa kiasi gani nguvu uliyoitumia pamoja na kukontrol muda unaolala na unaoamka, pia pia kifaa hicho kinaweza kuunganishwa na simu ya smartphone yako na kutambua simu ikiwa inaita kwa umbali wa mita kumi(10).
Hakika penda cha nyumba

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. JULIANA PALANGYO AKUTANA NA KAMPUNI YA ORYX ENERGIES

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Dk. Juliana Palangyo akiendesha kikao kati ya kampuni ya nishati ya Oryx Energies yenye makazi yake jijini Geneva, Switzerland pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili utendaji kazi wa kampuni hiyo nchini.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Oryx Energies, Philippe Cortes (kushoto) akifafanua shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo nchini Tanzania kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Dk. Juliana Palangyo (kulia) katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Oryx Energies, Philippe Cortes akifafanua jambo katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Oryx Energies, Philippe Cortes (kushoto) akimwelekeza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Dk. Juliana Palangyo (kulia) katika kikao hicho.

TAMWA YASIKITISHWA KESI ZA UBAKAJI/ULAWITI KWA WATOTO KUTOHUKUMIWA.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(katikati) akizungumzia mbele ya waandish wa habari (hawapo pichani) ni kwa jinsi gani wamepata malalamiko kutoka kwa familia zinazofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi za mahakama, polisi na baadhi ya hospitali hapa nchini. 
Mratibu wa Kituo cha usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa wakilaani vikali ucheleweshwaji na upotoshaji wa kesi za vitendo vya ukatili. 
Mtoto akitoa ushaidi ni kwa jinsi gani alivyofanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia. 
Mwanasheria wa TAWLA, Mary Richard (wa kwanza kulia) akizungumza ni kwa jinsi gani wanavyowasaidia wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia leo katika mkutano na waandishi wa habari leo. 

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini. 

CHAMA cha Wanahabari wanawake nchini Tanzania(TAMWA) kimelaani vikali ucheleweshwaji na upotoshwaji ushahidi wa kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi ya mahakama, polisi na baadhi ya madaktari hospitalini. Hali hiyo imekuja baada ya TAMWA kubaini kesi sitini na mbili (62) za ubakaji zimeshindwa kutolewa hukumu au uamuzi na mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2015. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga amesema kati ya kesi 63 za ubakaji, ni kesi moja tu mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi arobaini na tatu (43) bado ziko mahakamani, kesi kumi na saba (17) zimeshindwa kufika mahakamani ambapo kesi mbili zimefutwa kwa kukosa ushahidi. 

Pia aliongezea kwa kusema kuwa uongozi wa TAMWA umesikitishwa kuona kesi hizo zikicheleweshwa na vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo jeshi la polisi na mahakama. Na kuna baadhi ya viongozi wanapokea rushwa ili kuzima kesi za watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia, pia baadhi ya polisi wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kwa mlalamikaji ambapo wanatoa maneno ya vitisho na kupelekea mlalamikaji kukosa ujasiri wa kuhifadhi na kutetea kesi yake na wakati mwingine mama mzazi anaandikwa kama mlalamikaji badala ya mtoto mwenyewe aliyefanyiwa ukatili huo. 


Pia wameunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposema wakati wa siku ya sheria duniani kuwa "Kila Hakimu wa Mahakama anapaswa kuhukumu kesi si chini ya 260 kwa kila mwaka na kwa haki", Hivyo basi wao kama TAMWA wanaamini ndani ya mwaka huu Mahakama hapa nchini zitafanya kazi yao kiweledi ili kuweza kupunguza ukatili wanaofanyiwa watoto wa kike.

MABONDIA KUTWANGANA KESHO LEADERS CLUB,NI CHEKA NA AJETOVIC

$
0
0
Mabondia Fransic Cheka kulia akitunishiana misuli na Mserbia Geard Ajetov baada ya kumia uzito kwa ajili ya mpambano wao kulia ni mdau wa mchezo wa ngumi Nassoro Rashidi na meneja wake cheka, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security  picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Fransic Cheka kulia akitunishiana misuli na Mserbia Geard Ajetov baada ya kumia uzito kwa ajili ya mpambano wao kulia ni mdau wa mchezo wa ngumi Nassoro Rashidi na meneja wake cheka, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security .picha na SUPER D BOXING NEWS


MABONDI francis Cheka na Geard Ajetovic wamepima uzito kwa ajili yapambano lao la mabara la uzito wa super middle la Shirikisho la Masumbwi ya Kulipwa Duniani (WBF) ambapo waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, atawaongoza Watanzania kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, kushuhudia pambano la ubingwa wa Mabara wa WBF Intercontinental kati ya Franciss Cheka na Geard Ajetovic.

Cheka anamkaribisha Ajetovic, Mwingereza mwenye asili ya Serbia, katika pambano hilo la raundi 12 uzito wa Super Middle, linalotazamwa kama marudiano ya mtifuano baina ya wawili hao waliowahi kuchapana jijini Manchester, Uingereza mwaka 2008. na Cheka kupoteza mpambano huo kwa point Wawili hao wametambiana vya kutosha, kila mmoja akijinasibu kuwa yu tayari kumuadabisha mwenzake, Cheka akienda mbali zaidi kwa kusema hatarajii kuwaangusha Watanzania, hususani anapopigana katika ardhi ya nyumbani.

Pambano hilo limeratibiwa na Kampuni za Advance Security kwa kushirikiana na Hall of Fame Boxing and Promotions zote za Dar es Salaam, ambalo litatanguliwa na mapambano mengine manne, ikiwamo burudani ya muziki kutoka kwa Bendi ya Twanga Pepeta. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa upimaji uzito, Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile, alisema maandalizi yote ya pambano hilo yamekamilika na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kumsapoti Cheka.

Ndambile, alisema viingilio vimegawanyika makundi mawili, ambako kiingilio cha juu kitakuwa ni Sh. 50,000 kwa Jukwaa la VIP, wakati cha chini ni Sh. 15,000 kwa viti vya kawaida. Aliyataja mapambano ya utangulizi kuwa kati ya Mohammed Matumla dhidi ya Mustapha Dotto (uzito wa Light raundi nane), Mohammed Bakari na Cosmas Cheka (Feather raundi nane) na lile la Lulu Kayage dhidi ya Mwanne Haji (Fly Raundi sita)a ajili ya
mpambano wake

WAZIRI NAPE NNAUYE AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MZISHI YA MWANAMUZIKI MKONGWE NCHINI, KASSIM SAID MAPILI

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiweka udogo kwenye kaburi la Mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Mzee Kassim Said Mapili, wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Mwili wa mwanamuziki mkongwe hapa nchini, Mzee Kassim Said Mapili ukiwasili kwenye makabuli ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Mwili wa mwanamziki mkongwe hapa nchini, Kassim Said Mapili ukiwekwa katika kabuli wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makabuli ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Waombolezaji waliofika kumsindikiza kwenye nyumba ya milele  Mzee Kassim Said Mapili, wakipata mawaidha baada ya mazishi.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images