Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 776 | 777 | (Page 778) | 779 | 780 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake fupi, Waziri Kitwanga alimshukuru Mwakilishi huyo kwa ushirikiano wake mzuri kati ya Wizara na UNHCR, pia alimtakia safari njema na mafanikio mema arudipo nyumbani kwake. Joyce anatarajia kustaafu rasmi katika nafasi hiyo mwezi ujao. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni, kushoto aliyekaa ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kumbukumbu yake kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Shirika lake la UNHCR na Wizara. Hafla hiyo fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Wizara hiyo, kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati anaiongoza UNHCR. Pia katika hotuba yake, Joyce alimpongeza Rais John Magufuli kwa uongozi wake mzuri pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka katika Serikali yake. Wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, na Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrsion Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrsion Mseke akizungumza katika hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake, Mseke alimshukuru Joyce kwa ushirikiano wake mkubwa aliouonyesha wakati wa uongozi wake. Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye aliiongoza hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto) akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole mara baada ya kumaliza sherehe fupi iliyoandaliwa na Wizara ya kumuaga kiongozi huyo wa UNHCR. Hafla hiyo fupi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Wizara akiwemo Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watatu kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (wapili kulia) wakielekea katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kumuaga Mwakilishi wa UNHCR nchini, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wanane kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (watano kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wasaba kushoto), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (wanne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wanne kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara pamoja wa UNHCR mara baada ya hafla fupi ya kumuaga Joyce, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mazingira Mh. Luhaga Mpina ,katika vipindi vya radio na Televison asubuhi ya leo, kwenye studio za Shirika la Utangazaji la Taifa TBC katika kipindi cha Televisheni cha Jambo Tanzania cha TBC1 na kipindi cha Aasubuhi hii katika kituo cha TBC Taifa..Picha na Evelyn Mkokoi Ofisi ya makamu wa Rais.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Kuweit Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati Balozi Mahadhi alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu   Dar es salaam leo Februari 25, 2016 kwa ajili ya kujitambulisha. 


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Kuweit Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati Balozi Mahadhi alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu  Dar es salaam leo Februari 25, 2016 kwa ajili ya kujitambulisha. (Picha na OMR)

  0 0

   Baadhi ya vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)vilivyotolewa na Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi ya Helping Hand yenye makao Makuu nchini Marekani.
   Wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya Farouk Aktas Muslim iliopo kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja  wakihudhuria katika Hafla ya Utoaji wa Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)kutoka Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi ya Helping Hand yenye makao Makuu nchini Marekani.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum katikati akipata maelezo kwa Muakilishi wa Taasisi ya Helping Hand Mohammad Habibu kuhusiana na Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)vilivyotolewa na  Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi yake yenye makao Makuu nchini Marekani.hafla iliofanyika Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
   Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Muzdalifat Farouk Hamadi akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika Hafla ya kutoa Vifaa mbalimbali vya Hospitali iliofanyika Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.

   Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum akikabidhiwa Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 3,45000 (laki tatu Arobaini na Tano Elfu) na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Muzdalifat Farouk Hamadi.wa kwanza kushoto ni Muakilishi wa Taasisi ya Helping Hand yenye makao makuu Nchini Marekani Mohammad Habibu.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum akitoa hotuba baada ya kupokea Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 3,45000 (laki tatu Arobaini na Tano Elfu) vilivyotolewa na Taasisi ya Muzdalifat Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha wageni waalikwa ambao ni Viongozi na Maafisa wa Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia katika Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia (JPC) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa muda wa siku mbili kuanzia leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Samuel Shelukindo akimkaribisha Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi hayupo pichani ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano huo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi akifungua rasmi Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Zambia.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo na Mshirika ya Kimataifa, Bw. Sylvester Mundanda ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchini Zambia akiwasilisha ujumbe wa Serikali ya Zambia katika mkutano huo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Zambia, Bi. Angela Mulenga ambaye aliambatana na ujumbe wa maofisa walioiwakilisha Serikali ya Zambia katika Mkutano huo akijadili jambo na Bw. Sylvester Mundanda.
  Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Judith Kapijimanga (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Balozi Grace Mujuma wakijadili jambo wakati wa mkutano huo.
  Sehemu ya maofisa wa Serikali ya Zambia wakifuatilia Mkutano.
  Sehemu ya maofisa wa Serikali ya Tanzania wakifuatilia Mkutano.
  Serikali za Tanzania na Zambia zinakutana katika kikao cha siku mbili kujadili na kukubaliana maeneo ya ushirikiano ambayo watayasimamiakwa pamoja kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi hizo mbili. Kikao hicho kinachojulikana kama Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia (JPC) kinafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia leo.

  Katika hotuba yake ya ufunguzi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi alieleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Zambia ni mzuri na kufanyika kwa kikao hicho ni uthibitisho dhahiri.

  Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa kufanyika kwa kikao hicho kunatoa fursa kwa wajumbe kuchambua kwa pamoja hatua zilizofikiwa na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa wakati wa kikao cha 8 cha JPC kilichofanyika Lusaka Juni 2006. Maeneo hayo ni pamoja na biashara, viwanda, mawasiliano, uchukuzi, nishati, uhamiaji, kilimo, elimu, michezo, madini, utalii, maliasili na utamaduni.

  “Haya ni baadhi ya maeneo ambayo nchi zote mbili zinayapa umuhimu mkubwa ili kuharakisha maendeleo ya pande zote mbili Katika majadiliano yetu tutalenga zaidi maeneo haya ili tubuni utaratibu mzuri wa kushirikiana katika utekelezaji kwa lengo la kuleta tija kwa nchi na wananchi wake”. Balozi Mwinyi alifafanua.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo na Mashirika ya Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, Bw, Sylevester Mundanda alieleza kuwa Tanzania na Zambia zimejaliwa kuwa na maliasili lukuki kama vile ardhi, madini, maji na wanyama pori, hivyo, endapo kama zitatumiwa vizuri zinaweza kubadilisha uchumi wa nchi hizo kwa ajili ya kuwaletea maisha bora wananchi wake.

  Alisisitiza umuhimu wa kukubaliana maeneo machache ya kipaumbele na kuyawekea mikakati ya utekelezaji na ubunifu bila kusahau kujiwekea utaratibu wa kupima ufanisi kila baada ya muda.

  Bw, Mundanda alihitimisha kwa kusema kuwa vikao vya JPC ni fursa nzuri kujadili changamoto za kiuchumi na kubuni mikakati ya pamoja kukabiliana nazo ili uchumi uweze kukua kwa faida ya wananchi wa pande zote.

  0 0

   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA NJIRO, waliohudhuria kwenye mafunzo ya usalama na wizi wa umeme wa kwanza (Kushoto) ni Afisa Huduma kwa wateja Bw. Juma Msuya.
   Mwanafunzi wa Chuo cha Veta kilichopo Oljoro mkoani Arusha akiuliza swali kwa wataalamu wa TANESCO katika mafunzo hayo.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi  Oldonyo Sambu ya Mkoani Arusha wakiwa na zawadi zao walizopewa na wataalam wa TANESCO kama zawadi za kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kujibu na kuuliza maswali, kushoto ni Afisa Mahusiano na Wateja Mkoa wa Arusha Bw.Fred Mbavai.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni ya jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kuwapokea wataalam kutoka TANESCO kwa ajili ya kupokea elimu kuhusu masuala mbalimbali ya umeme.
    Afisa Masoko  Bi. Jenifer Mgendi kutoka Shirika la Umeme (TANESCO)     akitoa zawadi kwa wanafunzi waliojibu maswali vizuri wakati wa utoaji elimu ya masuala ya umeme, katika Shule ya Msingi Tandika ya jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisukuru ya jijini Dar es Salaam, wakishangilia zawadi walizopewa wakati wa wataalam kutoka TANESCO walipotoa elimu ya masuala ya umeme. Katikati ni Afisa Uhusiano Bi.salama Kasamalu.

  0 0

  ● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi .
  ● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao.
  ● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya.
  mab01
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
  MAB1
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.MAB2
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani wakikagua eneo la Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.
  MAB4
  Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera Bw. Deogratius Batakanwa akimpewa maelekezo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuhakikisha kuwa anatoa elimu ya kutosha itakayowezesha wananchi, taasisi na Halmashauri ya Muleba kukamilisha ununuzi wa nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Muleba.Naibu Waziri alitembelea nyumba hizo na kulipongeza Shirika la Nyumba kwa ujenzi wa nyumba bora.
  MAB5
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Muleba baada ya kuhutubia Baraza lao na kuliomba liwezeshe ununuzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo. Pia aliagiza Baraza hilo kushiriki kikamilifu katika kutatua migogoro mingi ya ardhi iliyoko katika Wilaya hiyo.
  MAB6
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akikagua nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita kwa ajili ya kuuza. Amewataka wananchi na Halmashauri ya Mji wa Geita kununua nyumba hizo ili kuliwezesha Shirika kuendelea kujenga nyumba katika Halmashauri zingine.
  MAB7
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Mabula akiwa na Mbunge wa Chato Mhe. Dkt Medard Kalemani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakikagua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Chato. Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameishauri Halmashauri ya Chato kununua nyumba hizo ili NHC iongeze ujenzi wa nyumba zingine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nyumba Wilayani humo.
  MAB8
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za NHC Mkoa wa Kagera alipotembelea na kusalimiana na wafanyakazi wa Shirika hilo.
  MAB9
  Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita, kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula alipotembelea mradi huo. Mhe. Naibu Waziri ameziagiza Halmashauri nchini kusaidia uwekaji wa miundombinu kwenye maeneo ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na kutoa ardhi bure kwa NHC ili nyumba zinazojengwa ziwe na gharama nafuu kwa mnunuzi.
  MAB10
  Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bibi Mwajuma Nyiruka akitoa taarifa ya sekta ya ardhi ya Wilaya yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula alipoitembelea Halmashauri ya Misungwi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
  MAB11
  Baraza la Madiwani Muleba wakimsikilza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula (hayuko pichani) alipohutubia Baraza hilo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jenerali Umaro Sissico Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose’ Mario Vaz, Ikulu jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mjumbe huyo alileta salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Guinea Bisau.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua kutoka  Jenerali Umaro Sissoco Embalo mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau, Mheshimiwa Jose Mario Vaz. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau mara baada ya kupokea barua yenye Salamu na pongezi. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jenerali Umaro Sissoco Embalo, Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau, Mheshimiwa Jose Mario Vaz, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU. 

  0 0

   Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA NJIRO, waliohudhuria kwenye mafunzo ya usalama na wizi wa umeme wa kwanza (Kushoto) ni Afisa Huduma kwa wateja Bw. Juma Msuya.
   Mwanafunzi wa Chuo cha Veta kilichopo Oljoro mkoani Arusha akiuliza swali kwa wataalamu wa TANESCO katika mafunzo hayo.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi  Oldonyo Sambu ya Mkoani Arusha wakiwa na zawadi zao walizopewa na wataalam wa TANESCO kama zawadi za kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kujibu na kuuliza maswali, kushoto ni Afisa Mahusiano na Wateja Mkoa wa Arusha Bw.Fred Mbavai.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni ya jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kuwapokea wataalam kutoka TANESCO kwa ajili ya kupokea elimu kuhusu masuala mbalimbali ya umeme.
    Afisa Masoko  Bi. Jenifer Mgendi kutoka Shirika la Umeme (TANESCO)     akitoa zawadi kwa wanafunzi waliojibu maswali vizuri wakati wa utoaji elimu ya masuala ya umeme, katika Shule ya Msingi Tandika ya jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisukuru ya jijini Dar es Salaam, wakishangilia zawadi walizopewa wakati wa wataalam kutoka TANESCO walipotoa elimu ya masuala ya umeme. Katikati ni Afisa Uhusiano Bi.salama Kasamalu.

  0 0
 • 02/25/16--05:29: TAARIFA KUTOKA IKULU


 • 0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa simu feki ifikapo June mwaka huu. 

  Akizungumza Leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika katika nchi nyingi zilizoendelea.

  Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.
   Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya  Huawei, ambapo wanajitahidi  kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei. 

  "Ili kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.leo jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , Samora leo jijini Dar es Salaam.

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.
   Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa,leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania leo jijini Dar es Salaam. 


  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii).

  0 0

  MKurugenzi wa kampuni ya Advanced Security Company Limited, Juma Ndambile (wa pili kulia) akimtambulisha bondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) mbele ya bondia Geard Ajetovic (wa kwanza kushoto) huku promota Jay Msangi (wa pili kushoto) akishuhudia.
  Promota Jay Msangi (katikati) akiutambulisha mkanda kwa mabondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) na Geard Ajetovic (kushoto)
  Bondia Francis Cheka (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Geard Ajetovic mara baada ya kukutana mara ya kwanza.

  …………………………………………………
  Bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Francis “SMG” Cheka amesema kuwa Mserbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic atampa kipigo ambacho hata kisahau katika maisha yake katika pambano lao lililopangwa kufanyika Jumamosi, kwenye viwanja vya Leaders Club

  Cheka alisema hayo walipokutana kwa mara ya kwanza katika mkutano na waandishi wa habari iliofanyika kwenye ukumbi wa Sinema wa Mlimani City jijini.

  Alisema kuwa Ajetovic amekosea kukubali kupambana nay eye katika ardhi ya Tanzania kwani mwaka 2008 alishindwa kwa pointi kutokana na maamuzi ya majaji ambao walimpendelea.

  “Nimejiandaa vilivyo kwa ajili ya pambano hili,nilikuwa Zambia nilikfanya mazoezi ya wiki mbili, huyu jamaa ananiita mimi babu wakati wote tumezaliwa miaka ya 1980, atajuta nakuambia, amenizalilisha sana nami nitamjibu ukumbini,” alisema Cheka.

  Wakati huo huo; Mkanda wa ubingwa wa mabara wa WBF utakaogombewa na mabondia Francis Cheka na Muingereza, Geard Ajetovic umewasili nchini.

  Mapema rais wa WBF, Goldberg Haward na marefarii kutoka Afrika Kusini waliwasili jijini Dar es Salaam wakiwa na mkanda huo utakaogombewa na mabondia hao kesho kwenye viwanja vya Leaders.

  Muda mfupi baada ya mkanda huo kutua nchini, Cheka na Ajetovic walipata fursa ya kupiga nao picha wakiwa sanjari na makocha wao, Abdallah Salehe ‘Comando’ na Aksu Sahhaydar.

  Kwa nyakati tofauti jana, mabondia wote wawili walitambiana huku Cheka akibainisha kutotishwa na tambo za mpinzani wake huyo ambaye aliwasili nchini Jumanne iliyopita akitokea Ujerumani alikokuwa ameweka kambi.

  “Siku zote naamini maneno si vitendo, sitaki kuzungumza mengi lakini nitazungumza ulingoni Jumamosi, nimesikia tambo za mpinzani wangu lakini nasisitiza tena, sijawahi kuwaangusha Watanzania nchini kwetu na sitarajii iwe hivyo Jumamosi, cha msingi ni wao kunisapotio siku hiyo,” alisema Cheka.

  Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile alisema mabondia hao watapima uzito na afya Alhamis saa tano asubuhi kwenye hoteli ya Palm Beach tayari kupanda ulingoni hapo kesho.

  “Kila kitu kimekamilika, kiingilio VIP itakuwa elfu 50 na viti vya kawaida ni Sh elfu 15, milango ya Leaders itakuwa wazi kuanzia saa nane mchana ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwamo ya bendi ya Twanga Pepeta kabla ya mapambano kuanza saa moja usiku yakitanguliwa na mapambano ya utangulizi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo akifungua zoezi la utoaji damu linaloendelea leo katika viwanja vya Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Zoezi hilo linaendea hadi kesho.
  Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo akiongoza zoezi la utoaji damu leo katika viwanja vya Karume mkabala na Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Muuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Nemganga Kizega akipima afya ya Mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, Merry Kapande aliyefika leo kuchangia damu katika viwanja vya karume mkabala na ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa Tambaza wakichangia damu leo katika zoezi linaloendelea leo jijini Dar es Salaam.
  Dk Patrick Shao ni mmoja wa wafanyakazi wa Muhimbili ambaye alifika katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tambaza na Jangwani wakisubiri kutoa damu leo katika viwanja wa Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

  ……………………………………………………………
  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo emeendesha zoeti la kuchangia damu katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam ambako watu wamejitokeza kwa wingi kutoa damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

  Zoezi hilo limeanza leo asubuhi na litaendelea hadi kesho. Wanafunzi wa Jangwani Sekondari na Tambaza ni kati ya makundi yaliojitokeza kutoa damu.

  Pia watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutoa damu akiwamu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Praxeda Ugweyo, madaktairi wa muhimbili na kijana Joseph Starford Mgoha aliyetembea kwa mguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake uliotukuka.

  Katika zoezi hilo Dk Ogweyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchagia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.

  Pia, amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na amewaondoa shaka Watanzania kwamba utoaji wa damu hauna madhara yoyote kwa kuwa kabla ya mtu kutoa damu anaandaliwa kitaalamu ili kufanikisha kazi hiyo.

  0 0

  Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili (Pichani kulia) baada ya kuonekana hajatoka Chumbani kwake kwa Muda Mrefu.... Ndipo mlango ukavunjwa nyumbani kwake Tabata Matumbi jijini Dar es salaam na kukuta Mzee wetu hatunaye tena... 

  Mzee atakumbukwa kwa Kibao cha "Napenda Nipate Lau Nafasi" na "Rangi Ya Chungwa" na vingine nyingi...Pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania Dance Music Association ama Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA). 

  Mara ya mwisho hadharani Marehemu Mzee Kassim Mapili alionekana akiongoza wanamuziki katika mazishi ya mwanahabari nguli wa burudani Marehemu Fred Mosha katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ambako pamoja na kushirki mazishi aliimba kwa hisia beti kadhaa za kumuenzi marehemu Fred.

  Taarifa zaidi za msiba huu mzito  zitawajia kadri zitavyopatikana.
  Kwa mawasiliano zaidi kwa wasanii wa Tanzania piga namba 0744150000 
   Nawaomba wanamuziki wote Tujitoe 
  kwa wingi kumpa heshima Mzee wetu Kassim Mapili....!! 

  Imetolewa na Addo November
   Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!

  0 0

  IMG_3912
  Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).(Picha na Modewjiblog).

  Katika kusaidia uboreshwaji wa elimu ya Tanzania, Shirika la Kimataifa la ActionAid kwa kushirikiana na serikali ya Norway kupitia Wakala wa Maendeleo na Ushirikiano (NORAD) wamezindua mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).

  Akielezea kuhusu mradi huo, Makamu Mwenyekiti wa ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama alisema mradi huo unataraji kusaidia uboreshwa wa elimu nchini na zaidi maeneo ya vijijini sehemu ambapo zimekuwa zikionekana kuwa nyuma kielemu.

  Alisema ili kupatikana kwa elimu bora kunahitajika uwekezaji wa kuboresha elimu kwa maeneo yote yanayohusika na elimu na inatakiwa kuanza na elimu ya shule ya msingi ili kuweza kumwandaa mwanafunzi kuanzia akiwa mdogo kwa kupata elimu bora inayokidhi viwango vya kimataifa.

  “Elimu bora inataka kuwepo kwa uwekezaji kuanzia kwenye shule za msingi kwa kila jambo kama ni uniform, kalamu, uji, walimu kupatiwa stahiki zao na mengine yote yatimizwe,“Ukitaka elimu bora lazima ujue inahitaji uwekezaji na mradi huu unataka kuongeza fursa kwa wanafunzi kwa kuanzia shule za msingi na zaidi tunaangalia vijijini,” alisema Dkt. Lwaitama.

  Nae mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo, Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad alisema Norway na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na ana furaha kuona mradi huo unafanyika kwa maendeleo ya baadae ya Tanzania.

  Alisema Norway itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya elimu nchini katika kusaidia vijana kupata elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vya ufundi ili kuweza kuongeza wasomi ambao watasaidia ukuaji wa uchumi nchini.


  “Nina furaha kuona mradi ambao utakuwa na mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sasa na baadae kwa Tanzania ninataraji kuona miradi inafanikiwa na ushirikiano wa Norway na Tanzania kwa miaka 50 sasa unazidi kuimarika na Tanzania inaushirikiano mzuri na Norway,” alisema Kaarstad.

  Kwa upande wa Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu alisema kupitia Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 11 (2) inaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kujielimisha na kusoma ngazi zote za elimu hadi anapoamua kuacha kuendelea kusoma na hivyo mradi huo utasaidia watanzania kupata haki yao ya kikatiba.
  Mradi huo unataraji kufanyika katika wilaya za Kilwa na Singida na utakuwa wa miaka mitatu ambao unataraji kuzifikia shule 60, 30 kwa kila wilaya.

  Aidha unataraji kuwafikia wanafunzi wa kiume 7,758 na wakike 8,474 kwa wilaya ya Singida na Kilwa kuwafikia wanafunzi wa kiume 6,607 na wakike 6,546 lakini pia walimu 287 kwa Singida na 290 kwa Kilwa.
  IMG_3943
  Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
  IMG_3946IMG_3953
  Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ActionAid, Josaphat Mshighati akitoa maelezo kuhusu mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
  IMG_3957Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
  IMG_3963
  Mshereheshaji wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), Jovina Nawenzake akisherehesha wadau wa sekta ya elimu waliohudhuria uzinduzi huo.
  IMG_4012
  Kalistus Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akielezea kuhusu sera ya elimu inayotumika nchini na mipango waliyonayo ili kuiboresha zaidi.
  IMG_4016
  Paul Mikongoti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akielezea kuhusu haki ya elimu kwa watanzania.
  IMG_4037
  Samwely Mkwatwa kwa niaba ya AAT akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia ukujuaji wa elimu Tanzania.
  IMG_4043
  Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama.
  IMG_4084
  Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization). Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama.
  IMG_4097
  Baadhi ya wahuzuriaji waliohudhuria katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization) iliyoandaliwa na Shirika la ActionAid.
  IMG_4116
  Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akizindua taarifa kuhusu mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
  IMG_4121
  Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad akimkabidhi taarifa ya mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), Kalistus Chonya kutoka Ofisi ya Sera katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
  IMG_4124IMG_4127
  Kwa pamoja wakionyesha taarifa hiyo kwa wahudhuriaji wa warsha hiyo.
  IMG_4147
  Watekelezaji wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization), wakisaini mikataba na mwongozaji wa mradi huo.
  IMG_4158
  Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Patrick Ezekiel akielezea kuhusu jinsi kodi inavyoweza kusaidia kuinua elimu nchini.
  IMG_4168
  Mratibu Mkuu wa TEN/MET nchini, Cathlee Sakwambo akitoa neno la ufungaji wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).
  IMG_4182
  Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja ya vifaa vya hospitali kutoka kwa wawailishi wa makampini ya Vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha,Wapili kushoto ni Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Wapili kulia ni Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana baadhi ya viongozi vya makampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino ya vofaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi bilioni 10 yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha, Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola- SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwasili eneo la tukio kushuhudia uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti nyeusi) akihojiwa na na Wanahabari pamoja na baadhi ya Wasanii mara baada ya kuwasili eneo la tukio kushuhudia uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti nyeusi) akiwahutubia Wasanii pamoja na wageni waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fissoo (kushoto) akiwahutubia Wasanii pamoja na wageni waalikwa wakati wa siku ya uchaguzi wa Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) uliofanyika 25 Februari, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Viongozi wa Uchaguzi wakitoa maelekezo juu ya namna zoezi la upigaji kura kwa kiti cha Rais, Makamu wa Rais pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).

  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi akizungumza na vijana (hawapo pichani) alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
   Mwezeshaji Bw. Patrick Kipangula (aliyesimama) akitoa mada kwa wadau wa maendeleo ya vijana wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
   Mjumbe  wa maendeleo ya vijana akichangia mada wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.

   Wawakilishi kutoka Mamlaka mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya siasa, Taasisi za kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za sekondari na Shule za msingi wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi (watatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na vijana wenye ulemavu wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia (waliokaa) ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi, wapili kushoto ni Mwenyekiti wa kikao Bw. Godwin Kunambi, na wanne kulia (waliosimama) ni Mkurugenzi msaidizi Vijana Bibi. Ester Riwa

  Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo


  Na; Genofeva Matemu – Maelezo

  SERIKALI imedhamiria kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na chombo chao chenye kujali utaifa, uzalendo na maslai bila kujali itikadi za kisiasa, kidini, rangi, hali za kiuchumi, jinsia na maumbile kwa kuandaa kanuni zitakazolifanya Baraza la Vijana Taifa kuwa huru na lenye haki.


  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleeo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.


  “Nimuhimu kuunda Baraza kisheria litakalokuwa na uwakilishi wa vijana wa makundi yote ili liweze kutumika katika kuleta umoja na mshikamano wa kitaifa” alisema Bw. Shitindi

  Aidha Bw. Shitindi amelipongeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kutunga sheria Na. 12 ya mwaka 2015 ya Baraza la Vijana Taifa ambalo litaleta maendeleo ya vijana na nchi kwa ujumla.


  Akizungumza katika kikao hicho mwenyekiti aliyeteuliwa kuongoza mjadala huo Bw. Godwin Kunambi amesema kuwa Vijana takribani 120 wamepata fursa adhimu ya kushiriki katika uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa hivyo kuwataka vijana hao kujadili mambo ya msingi yatakayowawezesha wananchi wa Tanzania hususani vijana kutatua kero zao kupitia Baraza hilo.


  Naye mwakilishi kutoka kundi la watu wenye ulemavu Bw. Gaston Hemed Mcheka ameipongeza Serikali kutoa nafasi kwa kundi la watu wenye ulemavu kuwa na uwakilishi kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa pindi Baraza la Vijana Taifa litakapoanza ambapo kundi hilo litatumia nafasi hiyo kutatua changamoto zinazowakabili.


  Kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa kimeshirikisha takribani vijana 120 kutoka Mamlaka mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia, Vyama vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi  za kidini, Vijana wenye ulemavu, Shule za Sekondari pamoja na Shule za msingi. 

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Philip Mpango akizungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Arusha leo katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa na kuwakumbusha wajibu wao kulipa kodi stahiki ili kukuza uchumi wa nchi,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu na Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja.
  Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja akijibu hoja za wafanyabiashara mkoa wa Arusha huku Waziri wa Fedha na Mipango,Philip Mpango akifatilia kwa makini . 
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Longido,Ernest Kahindi,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Francis Miti na Mkuu wa wilaya ya Karatu,Omary Kwaang' wakifatilia miongoni mwa maafisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo.

  Wafanyabiashara kutoka sekta mbalimbali waliohudhudia mkutano huo

older | 1 | .... | 776 | 777 | (Page 778) | 779 | 780 | .... | 1898 | newer