Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 775 | 776 | (Page 777) | 778 | 779 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Bondia Mserbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile (kushoto) na Promota Jay Msangi (kulia) katika mkutano na waandishi wa habari jana. Ajetovic atapigana na Francis Cheka Jumamosi kwenye viwanja vya leaders club kuwania mkanda wa uzito wa Super Middle wa Mabara wa chama cha WBF
   Bondia Mserbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana tayari kwa pambano lake la jumamosi dhidhi ya Franci Cheka. kushoto ni Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile na kulia ni promota Jay Msangi. Ajetovic atapigana na Francis Cheka Jumamosi kwenye viwanja vya leaders club kuwania mkanda wa uzito wa Super Middle wa Mabara wa chama cha WBF.
   Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile (katikati) akizungumza katika mkutano huo.

  Na Mwandishi wetu
  BONDIA Geard Ajetovic amewasili nchini na kumuita bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini ,Francis “SMG” Cheka kuwa ni ‘babu’ na hawezi kupigwa na bondia huyo pamoja na kupigana katika ardhi ya Tanzania.
  Ajetovic alisema kuwa anamjua Cheka kwani amemuona kwenye pambano lake dhidi ya Thomas Mashali na kusema kuwa ‘amekwisha’ na kamwe si bondia wa kupambana naye.

  Alisema kuwa Cheka amepigwa na bondia ambaye si lolote wala chochote na atampiga kabla ya raundi ya tano katika pambano hilo la ubingwa wa Mabara la uzito wa Super Middle unaotambuliwa na chama cha WBF.

  “Cheka ni babu, si bondia wa kiwango changu, nimemuona na hana chochote kwangu, siwezi kupoteza pambano hili, ni rahisi ndiyo maana nimewahi kufika siku moja kabla ya muda niliopanga kuja hapa,” alisema Ajetovic.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Advanced Security, Juma Ndambile aliwahakikishia mashabiki wa ngumi za kulipwa nchini kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika bada ya ujio wa Ajetovic.

  Ndambile alisema kuwa maofisa wa Chama cha WBF, ikiwa pamoja na Rais wake, Howard Goldberg na mwamuzi wa pambano hilo ambao watawasili leo.

  “Kama nilivyosema hapo awali, dhamira kubwa ya kampuni ya Advanced Security in kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa nchini hasa kwa mabondia kufaidika na vipaji vyao na si vinginevyo,”

  “Ili kufikia lengo letu, Advanced Security imeamua kuwashirikisha mabondia chipukizi katika mapambano ya utangulizi. Mabondia hao chipukizi wanatarajia kutoa changamoto kwa mabondia maarufu ambao pia watashiriki katika pambano hilo,” alisema Ndambile.

  Alisema kuwa wameandaa mabondia chipukizi ili kupamba siku hiyo. Alisema kuwa Mohamed Bakari atapambana na Cosmas Cheka katika pambano la uzito wa feather la raundi nane (8) huku Mohamed Matumla ataonyeshana kazi na Mustapha Dotto katika pambao la uzito wa Light la raundi nane pia.

  Bondia mkongwe na maarufu nchini, Mada Maugo ataingia ulingoni kwa kupambana na bondia kutoka Mbeya, Baraka Mwakansope baadala ya bondia Abdallah “Dulla Mbabe” Pazi kama ilivyotangazwa awali.

  Alisema kuwa pia siku hiyo, bondia wa kike, Lulu Kayage atazichapa na bondia nyota kutoka mkoa wa Mbeya, Mwamne Haji katika pambano la uzito wa fly lilillopangwa kuwa la raundi sita.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU 


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amepokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 02 Machi, 2016 Katika Jiji la Arusha, Nchini Tanzania. 

  Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi tano wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. 

  Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezibera, amesema maandalizi kuhusiana na mkutano huo yanakwenda vizuri. 

  Amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo, utajadili masuala kadhaa yakiwemo mpango wa kuanzisha viwanda vya magari ndani ya Jumuiya ili kupunguza uingizaji wa magari kutoka nje ya nchi na Marais kuzindua pasi ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

  Kuhusu hali ya Jumuiya, Dkt. Sezibera amesema inaendelea vizuri na ametaja baadhi ya mambo ambayo yamefanyika kuwa ni kutiwa saini kwa mkataba wa umoja wa forodha, makubaliano ya soko la pamoja na makubaliano ya sarafu moja. 

  Mengine ni kuwepo kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa miundombinu kama vile reli na umeme ndani ya Jumuiya, na mazungumzo kuhusu umoja wa kisiasa. 

  Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga, amesema Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa kikao hicho ipo tayari kupokea ugeni na kwamba pamoja na kufanyika kwa kikao hicho, marais wa Tanzania na Kenya watafungua barabara inayounganisha Tanzania na Kenya katika Mpaka wa Holili na kutakuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha pamoja cha mpakani kwa ajili ya kuwezesha upitaji wa mizigo na watu yaani "One Stop Boarder Post" 

  Gerson Msigwa 
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU. 
  Dar es salaam.
  24 Februari, 2016.

  0 0

  Na M wandishi wetu.
  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (Pichani) mgeni rasmi Tamasha la Pamoja Tunafanikisha litakaloandaliwa na kampuni ya Trumark katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya mwanamke Dunia.

  Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo ambaye ndie mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo amesema mama Samia pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya wanawake watakutana siku ya Machi tano ili kusheherekea mafanikio ya mwanamke pamoja na kuziangalia changamoto zinazomzunguka na kuzibadili kuwa fursa.

  “Kwa kweli tamasha hili litakuwa la aina yake ikizingatiwa hii ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuwa na makamu wa Rais mwanamke tangu kupatikana kwa uhuru, hii itatoa fursa kwa wanawake kuamini kuwa tunaweza kutimiza ndoto zetu kwenye safari ya mafanikio”alisema Agnes.

  Agnes amesema Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inalenga katika kuwaleta pamoja wanawake na wanaume na kutoa ahadi zao za kuwa mabalozi wa kuharakisha harakati za usawa wa kijinsia katika maeneo yanayowazunguka.

  Ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa jukwaa la kukutanisha wanawake kutoka fani na kada tofauti ili kutengeneza mtandao ambao utakuwa chachu muhimu kwa ustawi wao ambapo tamasha hilo litaenda sambamba na watoa mada kutoka nyanja mbalimbali kama vile uchumi na fedha, ujasiliamali na masuala ya afya maonyesho ya biashara ya bidhaa za ubinifu kutoka kwa wanawake, chakula cha usiku na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa hapa nchini akiwemo Elias Barnaba na bendi yake ya Clasicc ,mkogwe wa muziki wa taarab Mama Patricia Hillary na Misoji Mikwabi ambao wataongozwa na mchekeshanji maarufu MC Pilipili.

  Agnes aliwashkuru wadau mbalimbali wakiwemo King Solomon Hall, Valleys Spring, Mummys Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Channel Ten na Magic Fm. Pia aliwakaribisha wadau wote kuungana pamoja katika siku hii muhimu.

  0 0

   Bondia Salum Nassoro akipasha na kocha wake, Maneno Abdallah katika gym yao iliyopo Mazense Midizini.
   Promota wa mchezo huo, Haruna Musa katika picha ya pamoja na bondia, Salum Nassoro.

  Kampuni ya Dippo Boxing Promotion ya jijini Dar inayoongozwa na promota, Haruna Musa imeandaa pambano la Uzito wa Kati ‘Middle Weight’ kati ya bondia Salum Nassoro wa Dar na Benson Mwakyembe wa Ruvuma mchezo utakaopigwa Siku Kuu ya Pasaka, Machi 28 mwaka huu.

  Pambano hilo la kukata na shoka litapigwa kwenye uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma ambapo kwa mujibu wa promota huyo alisema kuwa mshindi wa siku hiyo atazichapa na bingwa wa Afrika  ‘WBF, Thomas Mashali.

  Mabondia hao ambao kila mmoja alitamba kumchapa mwenzake, waliwataka mashabiki wa ndondi kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ili waone ladha ya ndondi ya asili.

        

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Zakia Meghji (wa kwanza kulia) akifungua Baraza la tatu la Wafanyakazi Taasisi hiyo sambamba na utoaji vteti kwa wafanyakazi bora na pesa taslimu kwa kila mfanyakazi, Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa NIMR. wa katikati ni  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi  Dkt, Othman Kiloloma na anayefatia ni Katibu wa Baraza la wafanyakazi hilo Dkt. Clement Mugisha
   (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akila kiapo cha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni mara baada ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni kabla ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, mara baada ya Jaji huyo kuwaapisha kuwa viongozi wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam leo. Injinia Masauni katika Tume hiyo amekuwa Makamu Mwenyekiti, na Meja Jenerali Rwegasira amekuwa Katibu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Mratibu wa kipindi cha walinde watoto Neema Kimaro akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kipindi hicho pembeni yake ni Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam" 
  Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kipindi hicho katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam. 
  Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Luninga EATV David Gumbo akiuliza swali kwa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto mapema leo kuhusu mafanikio ya kipindi hicho katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam. 
  Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kipindi hicho Katikati ni Mratibu wa kipindi cha walinde watoto Neema Kimaro na kulia kwake ni Mshauri Nasaha Mwandamizi kutoka CSEMA Fatuma Kauramba katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam. 
  Waandishi wa habari wakisikiliza makini maelezo ya waaandaji wa kipindi cha Walinde Watoto mapema leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.
  Na Krantz Mwantepele, Dar es salaam 
  Kuhusu Kipindi cha Walinde Watoto


  Ndugu waandishi wa habari, katika jitihada za kutoa elimu kuhusu maswala ya Ukatili dhidi ya Watoto, UNICEF na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano na True vision production, walianzisha kipindi cha redio cha Walinde Watoto, ambacho kilianza kuruka hewani kupitia redio mbalimbali hapa nchini mwezi Novemba mwaka 2014. Kipindi hiki kinarushwa na redio 19 nchini Tanzania, bara na visiwani, zikiwemo TBC na ZBC. 


  Malengo ya Kipindi


  Malengo ya Kipindi


  Ndugu waandishi wa habari, kipindi cha redio cha Walinde Watoto kilianzishwa kwa malengo yafuatayo;  Kutoa elimu juu ya ulinzi kwa watoto, kufuatia ripoti iliyotolewa mwaka 2011 ambayo ilionyesha ukatili dhidi ya watoto ni tatizo kubwa nchini Tanzania 
  Kutoa fursa kwa jamii kujadili mazingira salama ambayo mtoto anapaswa kuishi mahali popote atakapokuwa iwe ni nyumbani, shuleni na hata barabarani 
  Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu na mbinu za kuripoti matukio ya ukatili kwa watoto. 


  Mafanikio ya Kipindi


  Ndugu waandishi wa habari, tangu tumeanza kurusha kipindi cha Walinde Watoto tunajivunia mafanikio mengi;
  Kwanza kabisa ni kwa vituo vya redio vipatavyo 19 kukubali kushiriki kampeni hii kwa kurusha kipindi cha elimu kwa umma bila malipo. Tulianza na redio 14 zikiwemo TBC na ZBC na miezi michache baadaye ziliongezeka redio nyingine 5 baada ya kuvutiwa na maudhui ya kipindi. Kwa ujumla kipindi cha Walinde Watoto kinasikika nchi nzima. 
  Tumefanikiwa pia kutembelea wilaya zaidi ya 12 nchini Tanzania ili kuhakikisha kwamba tunatoa fursa kwa watu mbalimbali wakiwemo wazazi na walezi kupaza sauti zao katika mambo yahusuyo ulinzi kwa watoto. Miongoni mwa wilaya tulizotembelea ni pamoja na Shinyanga, Magu, Musoma, Geita, Kasulu na Kahama. Nyingine ni Kilosa, Kigoma, Kasulu, Kisarawe, Hai na zile za Zanzibar. 
  Ndugu waandishi wa habari tumefanikiwa kutengeneza na kurusha vipindi zaidi ya 60 vikiwemo vipindi maalum kuhusu mada mbalimbali kama vile ukatili wa aina mbalimbali wanaofanyiwa watoto wakikiwa nyumbani, shuleni, na hata barabarani wakienda na kutoka shule, watoto ulemavu wa ngozi ama albino pamoja na watoto wakimbizi. Tumetoa elimu umuhimu wa kutoa taarifa katika ngazi tofauti pamoja na namba maalum ya msaada wa watoto ya 116. 
  Ndugu waandishi wa habari, jukumu la kuwalinda watoto ni letu sote. Kwa kutambua hili tumefanikiwa kufanya mahojiano na viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi na mashirika binafsi, wafanyabiashara, wadau mbalimbali, wanaharakati n.k yote ikiwa na lengo la kupata mitazamo tofauti ya wadau hawa muhimu katika maendeleo ya taifa letu. 
  Ndugu waandishi wa habari, wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tulifanikiwa kufanya vipindi maalum vinavyohusu uchaguzi, tuliandaa midahalo iliyowaleta pamoja wananchi na watoto katika meza moja na wagombea wao wa ngazi za ubunge na udiwani, ili wasikilize ajenda za watoto katika uchaguzi mkuu na kuwaeleza ni kwa namna gani wamejipanga kukabiliana na changamoto zinazohusu ulinzi wa watoto. 
  Kama mnavyofahamu swala la kubadili tabia linahitaji nguvu zetu wote na ni mchakato wa muda mrefu, kwa upande wetu, kupitia kipindi hiki cha redio, kwa asilimia kubwa tumefanikiwa kuongeza uelewa wa jamii kuhusu maswala yahusuyo ukatili kwa watoto na namna mbalimbali za kuwalinda watoto. Tunatumaini mtatuunga mkono katika jitihada hizi. 

  Ndugu waandishi wa habari, tulifanikiwa kufungua tovuti maalumu ya www.walindewatoto.org ambayo imekuwa ikirusha vipindi hivi vya watoto. Tumeweza kufungua akaunti katika mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na Whatasapp na kwa kupitia mitandao hiyo tumeweza kufikia maelfu ya watu. Pia tumeanzisha namba maalum ya simu ambayo watu wanaweza kupiga na kutoa maoni yao kuhusu vipindi. 
  Ndugu waandishi wa habari, kwa kutambua mchango wa redio katika kupiga vita ukatili dhidi ya watoto, mnamo mwezi Februari mwaka 2015 tuliweza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka redio zote washirika wa kipindi hiki. Mafunzo hayo yaliweza kuwajengea uwezo ili waweze kuzungumzia ukatili kwa watoto, namna mbalimbali ya kuwahoji watu ili kuibua changamoto za watoto, na namna ya kufanya jamii ibadilike na kuona matatizo ya watoto ni yetu sote.

  Kutokana na ubora wa kipindi, wasikilizaji wengi wameongezeka kitendo ambacho kimewashawishi wamiliki wa vituo binafsi kuongeza muda wa kipindi kutoka nusu saa hadi saa nzima na hivyo kupokea maswali na mijadala yahusuyo watoto kutoka katika maeneo yao.

  Tumefanikiwa pia kuanzisha vikundi vya wasikilizaji kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao husikiliza kipindi kila kinaporushwa na kisha kutupa mrejesho wa yale waliyojifunza. Makundi haya husambaza elimu waliyoipata kwa watu wengine wakiwemo ndugu na marafiki zao.


  Tunafanyaje kazi?

  Kipindicha Walinde Watoto kinapata maudhui (content??) kwa kuandaa midahalo mbalimbali, mikutano katika vijiji, mahojiano na wadau, kutembelea wilaya na mikoa mbalimbali pamoja na kupitia mitandao ya kijamii.


  Tangu tumeanza kurusha kipindi, tumeandaa nyimbo mbili maalum kwa ajili ya kampeni.

  Kama motisha kwa wasikilizaji wetu, tunaandaa mashindano mbalimbali ambapo washindi hupata zawadi mfano fulana (Tshirts), redio n.k


  Nini malengo yetu?


  Ndugu waandishi wa habari, mwezi wa kwanza mwaka huu tumeanza msimu wa pili wa kipindi cha Walinde Watoto. Tunakusudia kufanya yafuatayo;
  Kushawishi redio mbalimbali nchini zishiriki kampeni na kurusha kipindi cha elimu kwa umma. Tunakusudia kuongeza idadi ya redio kufikia walau 25 ili tuweze kufikia wasikilizaji takribani milioni 24 nchini Tanzania.
  Kama tunavyofahamu, maswala ya ukatili kwa watoto yanazidi kushika hatamu. Awamu hii itajikita zaidi kwenye kuzungumzia adhabu mbalimbali za watoto zikiwemo vipigo, matusi, manyanyaso, ukatili wa kisaikolojia na nyingine nyingi.
  Tunakusudia kutumia namba maalum ya simu kutoka UNICEF kufanya utafiti kuhusu usikilizaji wa kipindi hiki ili kupata mrejesho kutoka kwa wasikilizaji
  Kuendeleza na kuyajengea uwezo makundi ya wasikilizaji wa kipindi katika jamii ‘community listening groups’
  Kuongeza nguvu katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kufikia watu wengi zaidi pamoja na kutembelea Wilaya nyingine nyingi.


  Wito
  Tunatoa wito kwa serikali na taasisi mbalimbali kuendelea kutoa ushirikiano ili tuweze kuwahabarisha na kuwafikia watanzania wengi zaidi katika kuhamasisha kuwalinda watoto.
  Tunatoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kuwajali na kuwalinda watoto wao kama njia mojawapo ya kutimiza majukumu yao kama wazazi.
  Pia tunatoa wito kwa watanzania kwa ujumla kushirikiana kwa karibu na kamati za ulinzi na usalama wa mtoto katika kulisukuma gurudumu hili la ulinzi na usalama kwa mtoto
  Endapo utaona mtoto anafanyiwa kitendo cha ukatili basi usisite kupiga namba 116 kwa msaada zaidi, namba hii ni bure kabisa.


  Redio zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto


  Zifuatazo ni redio zinazoshirikiana nasi katika kurusha kipindi cha Walinde Watoto:


  1. Radio Faraja- Shinyanga


  2. Radio Huruma- Tanga


  3. Country FM –Iringa


  4. Ice FM- Makambako


  5. Radio Boma Hai- Hai


  6. Zenji FM –Zanzibar


  7. Bomba FM –Zanzibar


  8. Radio Maria- Dar Es Salaam


  9. Radio Quran- Dar Es Salaam


  10. Best FM – Ludewa


  11. Radio Victoria –Musoma


  12. Dodoma FM – Dodoma


  13. Zanzibar Broadcasting Cooperation ZBC- Zanzibar


  14. TBC Taifa- Dar Es Salaam


  15. Radio FADECO- Karagwe


  16. Radio Jamii Kilosa- Kilosa


  17. Radio Kwizera- Ngara


  18. Radio Upland- Njombe


  19. Radio Kitulo- Makete.


  Mwisho


  Ndugu waandishi wa habari narudia tena kusisitiza, jukumu la kuwalinda watoto ni jukumu letu sote. Vyombo vya habari tuna nafasi kubwa sana ya kufikia watu wengi zaidi, tutumie taaluma yetu kutetea na kulinda haki za watoto.
  Asanteni sana kwa kunisikiliza.


  0 0

  MUIMBAJI nguli wa muziki wa Injili jijini Mwanza, Goodluck Gosbert anatarajia kuzindua albamu yake ya Ip[o siku yenye nyimbo nane kwenye Tamasha la Pasaka jijini Mwanza linalotarajia kufanyika Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama  tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita kwenye ukumbvi wa Desire kabla ya kumalizia uwanja wa Taifa Wilayani Kahama ambalo litafanyika Machi 28.

  Msama alisema albamu hiyo ni moto wa kuotea mbali, hivyo wakazi wa mikao ya Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo litashi8rikisha waimbajki mbalimbali wa Tanzania.Msama alizitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Ipo siku, Acha waambiane, Haohao, Nisamehe, Pendo langu, Ndiwe Mungu, Moyo tulia na Surprise.Aidha Msama alitumia fursa hiyo kueleza kwamba viingilio katika tamashja hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000.

  "Tamasha la Pasaka ni sehemu ya kusaidia wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na walemavu, yatima na wajane ambao wanahitaji msaada kutoka kwa wadau kama kampuni ya Msama Promotions," alisema Msama.

  Msama aliwataja waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Jennifer Mgendi, Sifael Mwabuka, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Christopher Mwahangila, Anastazia Mukabwa, Kwaya ya AIC Makongoro, Kwaya ya Wakorintho wapili, Faustine Munishi, Solomon Mukubwa.

  0 0

  Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akishuka kwenye gari wakati alipowasili kwenye mradi wa Eco Residence ulioko Kinondoni Hananasifu unaojengwa na shirika la Nyumba la Taifa NHC huku akiongozwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu tayari kwa ukaguzi wa jengo hilo ambalo nyumba zake zote zimeshauzwa na linatarajiwa kukabidhiwa hivi karibuni kwa Shirika hilo.

  Akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya ukaguzi wa jeno hilo Msajiri wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru amepongeza uongozi wa NHC kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo wamefanikiwa kujenga majengo yenye tahami ya shilingi Trilioni 3.5 kutoka umiliki wa mwanzo ambapo kulikuwa na majengo yenye thamani ya shilingi trilioni 1.

  Mkopo uliotumika kugharamia ujenzi wa majengo hayo mapya kutoka mabenki mbalimbali ni jumla ya shilingi Bilioni 300 ambazo kiasi cha shilingi Bilioni 100 zimeshalipwa tayari katika mabenki hayo na kiasi cha shilingi bilioni 200 zinaendelea kulipwa.

  Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu amesema shirika hilo linao mpango mkubwa wa ujenzi wa nyumba 500 za gharama nafuu kwa ajili ya watanzania wenye kipato cha chini ambazo zitaanza kujengwa mwaka huu huko Luguruni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam..(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akimsikiliza Violet Mafuwe Msanifu wa majengo kutoka kampuni ya CPI Iternational ambaye pia ni Meneja Mradi wa Eco Residence wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
  Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akimuuliza jambo Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu mambo mbalimbali kuhusu miradi ya shirika hilo wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
  Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
  Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo.
  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya Msajili wa Hazina kukagua mradi huo.
  Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akiagana na Mkurugenzi wa NHC Bw Nehemia Mchechu mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo.
  Jengo linavyoonekana kwa nje.

  0 0

  Meneja wa Habari , Elimu na Mawasiliano Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Omega Ngole akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kuhusu upatikanaji wa mikopo elimu ya juu uliofanyika Jijini Dar es salaam.

  Na jacquiline Mrisho –Maelezo

  Dar es salaam

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wanaopata mikopo katika taasisi za elimu ya juu nchini.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano Omega Ngole alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

  “Utaratibu huu ulioboreshwa, ni msisitizo na maelekezo ya Serikali ya mwezi Agosti 2011 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ilielekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kuanzisha Madawati ya Mikopo ili kuongeza ufanisi katika utoaji mikopo”,Alisema Ngole.

  Ameongeza kuwa, dawati hilo linatakiwa kusimamiwa na mtumishi teule wa chuo husika mwenye sifa na uhusiano mzuri na jamii na linapaswa kuwa chini ya Makamu Mkuu wa chuo husika anayeshughulikia taaluma.

  Meneja Ngole amesisitiza kuwa kwa sasa vyuo vyote vina Maofisa Mikopo ambao wanawajibika kutafuta suluhisho la suala linalowasilishwa na kulitolea majibu.

  Akifafanua hatua zinazotakiwa kufuatwa na Maofisa hao katika kutafuta suluhisho la malalamiko ya wanafunzi amesema kuwa, baada ya malalamiko kufika kwa Ofisa Mikopo yanatakiwa yapate suluhisho ndani ya siku mbili tangu kuwasilishwa kwake,ikiwa hatakua na ufumbuzi atatakiwa kuwasiliana na uongozi wa juu wa chuo husika.

  Endapo uongozi wa juu wa chuo hautokuwa na ufumbuzi, malalamiko hayo yatatakiwa kupelekwa kwenye Ofisi za Kanda ambazo zinapatikana katika Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha na Zanzibar au ofisi za makao ya makuu ya Bodi zilizoko jijini Dar es Salaam.

  Bodi ya Mikopo ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi mwezi Julai 2005 kwa majukumu ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika Taasisi za Elimu ya Juu pamoja kukusanya marejesho ya mikopo yote iliyotolewa tangu mwaka 1994

  0 0

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inatekeleza mradi mkubwa wa mifumo ya Ulinzi na Usalama kwa njia ya kielekrtoniki ili kudhibiti usalama wa bandari zake majini na nchi kavu kimtandao.
  Mradi huu wa kielektroniki unajulikana kama Intergrated Security System (ISS) unakusanya mifumo mbalimbali ya ulinzi na unafadhiliwa na TPA kwa gharama ya shs. bilioni 9.800.
  Mradi huu mkubwa wa ulinzi unahusu ufungaji wa CCTV cameras, ujenzi wa chumba cha kuongozea mitambo yote ya ISS, ufungaji wa taa na minara yake pembezoni mwa ukuta wa bandari, ufungaji wa nyaya mbalimbali, ufungaji wa ‘License Plate Number’ ambapo sasa magari yote yanayoingia bandarini yatakuwa yanasomwa na kurekodiwa namba zake za usajili, ujenzi wa gate house kwenye mageti, ufungaji wa radiation detectors na ‘access control system’.
  Jumla ya CCTV cameras 486 zitafungwa ambapo mpaka sasa jumla ya camera 246 zimeshafungwa na kuanza kutumika na camera 144 zilizobaki ufungaji wake unategemewa kukamilika mwezi Machi mwaka huu wa 2016.
  Kamera hizi zitasaidia kuiona bandari yote ya Dar es Salaam mpaka kwenye boya la mafuta la SPM Mjimwema, kutokea kwenye chumba kimoja ambacho kamera hizo zinafungwa na hivyo kuwezesha kunasa tukio lolote la uhalifu ambalo linatokea katika eneo husika.
  Mradi pia unahusu uboreshaji wa milango ya kuingia ndani ya bandari ambapo mageti maalum ya kisasa yanaendelea kufungwa ili kudhibiti uingiaji ndani ya eneo hili nyeti. Katika mageti haya waingiaji watakaoweza kuingia ni wale tu wenye vibali au vitambulisho maalum ambavyo mitambo itaweza kuvitambua kielektroniki vitambulisho hivyo ikiwemo wafanyakazi na watumiaji wa bandari.
  Mitambo itakayofungwa katika mageti haya itakuwa na uwezo wa kusoma namba za magari yote yanayoingia bandarini na kumbukumbu zake kubaki katika kumbukumbu za Mamlaka.
  Ufungaji wa taa na minara yake pembezoni mwa ukuta wa bandari nguzo zimeshasimikwa na taa zinaendelea kufungwa.
  Kukamilika kwa mradi huu kutaboresha kwa kiasi kikubwa usalama wa bandari, mali za Mamlaka na mizigo ya wateja na hivyo kuwaongezea imani watumiaji wa bandari kwamba mali zao ni salama katika bandari za Tanzania.
  Imetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
  Janeth Ruzangi (Bibi)
  MENEJA MAWASILIANO

  0 0

   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam .PICHA NA IKULU


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
  Simu: 255-22-2114512, 2116898

  E-mail: press@ikulu.go.tz

  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amepokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 02 Machi, 2016 Katika Jiji la Arusha, Nchini Tanzania.

  Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi tano wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezibera, amesema maandalizi kuhusiana na mkutano huo yanakwenda vizuri.

  Amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo, utajadili masuala kadhaa yakiwemo mpango wa kuanzisha viwanda vya magari ndani ya Jumuiya ili kupunguza uingizaji wa magari kutoka nje ya nchi na Marais kuzindua pasi ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kuhusu hali ya Jumuiya, Dkt. Sezibera amesema inaendelea vizuri na ametaja baadhi ya mambo ambayo yamefanyika kuwa ni kutiwa saini kwa mkataba wa umoja wa forodha, makubaliano ya soko la pamoja na makubaliano ya sarafu moja.
  Mengine ni kuwepo kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa miundombinu kama vile reli na umeme ndani ya Jumuiya, na  mazungumzo kuhusu umoja wa kisiasa.


  Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga, amesema Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa kikao hicho ipo tayari kupokea ugeni na kwamba pamoja na kufanyika kwa kikao hicho, marais wa Tanzania na Kenya watafungua barabara inayounganisha Tanzania na Kenya katika Mpaka wa Holili na kutakuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha pamoja cha mpakani kwa ajili ya kuwezesha upitaji wa mizigo na watu yaani "One Stop Boarder Post"


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

  Dar es salaam

  24 Februari, 2016  0 0
 • 02/24/16--23:00: DONDOO ZA MAGAZETINI LEO.

 • 0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Amos Makala walipokutana mjini Moshi kwa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyo chini ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
   Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katika kampuni ya Dott Services Limited inayojenga barabara ya Same-Mkumbara Km 96. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kampuni ya Dott Services Limited kuhusu madai yao ambapo ameagiza waanze kulipwa madai yao baada ya siku mbili.
   wafanyakazi wa kampuni ya Dott Services Limited wakishangilia kwa furaha baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kumtaka mkandarasi kuwalipa madai yao yote ifikapo Februari 26, mwaka huu.
   Muoneano wa Jengo la Kituo cha Forodha cha pamoja (One Stop Border Post) kwa upande wa Tanzania lililopo Holili.

   Ujumbe wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ukielekea katika kituo cha pamoja cha forodha (One Stop Border Post) kwa upande wa Taveta nchini Kenya.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa namna ya kituo cha pamoja cha Forodha kinavyofanya kazi kutoka kwa Meneja Forodha kwa upande wa Taveta – Kenya Bw. Daniel Nyambaka.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiagana na Meneja Forodha kwa upande wa Taveta – Kenya Bw. Daniel Nyambaka mara baada ya kukagua kituo hicho.


  SERIKALI imesema iko mbioni kukamilisha mkataba maalumu wa ajira utakaotumiwa na makandarasi wote nchini katika kuajiri watanzania wazalendo kwenye miradi ya ujenzi inayosimamiwa na sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Mkumbara-Same yenye urefu wa Km 96 mkoani Kilimanjaro.

  Amemtaka mkandarasi Dott Services Limited kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi wa barabara hiyo na kulipa stahili zote za wafanyakazi kwa mujibu wa mikataba. 

  “Nakupa mwezi mmoja kukamilisha ujenzi uliobaki wa barabara hii pia hakikisha kila mfanyakazi ambaye amemaliza mkataba wake analipwa stahili zake zote kwa muda usiozidi siku mbili”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi kufatilia kwa makini madai ya wafanyakazi wazalendo ya malipo ya likizo, mafao ya NSSF, malimbikizo ya mishahara, matibabu na mazingira magumu ya kazi ili yalipwe sambasamba na madai mengine na hivyo kuondoa malalakimiko yaliyopo na yanayoweza kujitokeza mara baada ya kukamilika kwa mradi. 

  “Kuanzia sasa mameneja wa TANROADS wahakikishe kwenye ujenzi wa barabara na miradi iliyo chini ya wizara hii kazi ambazo watanzania wanaweza kuzifanya zisifanywe na wageni kwani hali hiyo huwanyima haki watanzania wenye ujuzi wa kuijenga nchi yao”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Kilimanjaro Eng. Marwa Rubirya amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa kwa sasa km 1,020 za mtandao wa barabara wilayani Same zinapitika na serikali imeanza kuongeza kiwango cha barabara za lami Wilayani humo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Same-Kisiwani-Maore-Ndungu na Kihuriyo hadi Mkomazi.

  Amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kwamba TANROADS itaendelea kuhakikisha barabara za milimani wilayani Same ambazo ni sawa na asilimia 75 ya barabara zote wilayani humo zinapitika wakati wote wa mwaka kutokana na umuhimu wake kwa shughuli za kiuchumi.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Herman Kapufi amemuomba Waziri Mbarawa kuzipandisha hadhi barabara za Hedaru-Vunta-Miamba Km 41.2, Bangarara-Chome-Ikokoa Km 25.6, na Ndungu-Lugulu Km 8 ili zihudumiwe na TANROADS kutokana na umuhimu wake kiuchumi na kijiografia.

  Katika hatua nyingine Waziri Mbarawa amekagua kituo cha pamoja cha forodha kilichopo Holili (Tanzania) na Taveta (Kenya) na kuona shughuli za usafirishaji na uchukuzi zinavyoendeshwa na kusisitiza umuhimu wa kituo hicho kufanyakazi kwa kushirikiana ili kuongeza mapato kwa nchi za Kenya na Tanzania.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Ramadhan Mungi akionesha Bunduki aoina ya Short Gun iliyokamatwa ikiwa imefichwa katika tundu la Choo katika eneo la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Ramadhani Mungi akizungumza na wanahabari kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni.

  Na Dixon Busagaga wa Globuu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali likiwemo la mauaji pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.


  Mbali na watuhumiwa hao Polisi pia imefanikiwa kukamata Bunduki aina ya shortgun (Pump Action) yenye namba 69901 ikiwa imefichwa katika tundu la choo nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao  eneo la Shirimatunda  katika manispaa ya Moshi.


  Bunduki hiyo pamoja na risasi tatu imetajwa kukodishwa na watuhumiwa na kisha kutumika katika shughuli za kihalifu ikiwemo uporaji wa fedha katika maeneo tofauti na mali huku ikihusishwa pia kufanya mauaji.


  Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishina msaidizi wa Polisi, Ramadhani Mungi alithibitisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na bunduki na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.


  “Katika siku za mwisho wa Desemba mwaka jana na siku za mwanzoni za mwaka huu ,kulikuwa na wimbi la matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya Short gun ambayo pia ilisababisha mauaji,tayari tumewakamata watu kadhaa na jana (juzi) asubuhi tuliweza kuikama silaha aina ya Short gun.”alisema Mungi.


  Wakati huo huo matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameendelea kushika kasi mkoani ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa ) alikatwa matiti yote mawili baada ya kujinasua katika jaribio la kubakwa.


  Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo kuwa ni Anold Josephate ambaye alitoweka na matiti hayo baada ya kuyaweka katika mfuko wa plastiki.


  Alisema tukio jingine linalo ashiria kuongezeka kwa makosa ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni tukio la juzi ambapo mwanamke mmoja aliyfahamika kwa jina la Vailet Apiniel ameuawa baada ya kunyongwa shingo.


  “Siku za karibuni hapa yamejitokeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanayo uaibisha mkoa wetu,matukio ya ubakaji,matukio ya watu kutupa vitoto,haa ni matukio mabaya na jana tu kuna mwanaume aitwaye Denis Shayo alimnyonga mke wake”alisema Mungi.


  Alisema eneo hili linahitaji kutolewa elimu ya kutosha huku akizitaka taasisi zinazojishughulisha na utetezi wa masuala ya kijinsia kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na matukio kama hayo.

  0 0

  Changia-damu-new
  Tamasha la Changia Damu Okoa Maisha linatarajiwa kuanza leo katika Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam ambapo pia kutakuwa na wasanii mbalimbali.

  Akizungumza  Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Eligeisha amesema kuwa tamasha hilo litadumu kwa siku mbili kuanzia leo na kesho na kwamba watu wajitokeze kwa wingi kuchangia damu.
  YAMOTO-BAND-2
  Vijana wa Yamoto Band wanaoongozwa na Dogo Aslay.
  “Lengo la tamasha hili la Changia Damu Okoa Maisha ni kukusanya lita kati ya 5,000 na 6,000 ambazo ni asilimia 75 ya mahitaji ya damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” alisema Eligeisha.

  Eligeisha ameongeza kuwa tamasha hilo kama linavyojieleza, kwamba wachangiaji wa damu watakuwa wanafanya hivyo ili damu hiyo ipelekwe benki ya damu kwa ajili ya wagonjwa watakaoihitaji.

  “Pia kutakuwepo na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza bure wakiwemo vijana wa Yamoto Band wanaoongozwa na Dogo Aslay pamoja na wasanii kutoka nyumba ya kuibua vipaji ‘ THT’ ambao watafanya vitu vyao wakati zoezi hilo likiendelea,” alisema.

  Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, Clouds FM, Pepsi Tanzania, Startimes, Abbott Fund, Benki ya CRDB, Mfuko wa Pensheni wa GPEF pamoja na Motisun Group Tanzania Ltd.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (Meza Kuu-mwenye miwani), akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lulembelwa, Kata ya Lulembelwa, Wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita. Dk Kalemani alisikiliza kero za wananchi hao kuhusu sekta za nishati na madini na aliwajulisha mipango mbalimbali ya Serikali kuhusu masuala ya upatikanaji wa umeme wa uhakika vijijini.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani akisaini Kitabu cha Wageni, ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Manguchie (katikati), kabla ya kuanza ziara yake wilayani humo kushughulikia kero mbalimbali za wananchi kuhusu masuala ya madini.

  Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Geita, Fabian Mshai, akisoma taarifa ya kazi ya Ofisi yake kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Serikali wa Wilaya, Kata na Vijiji pamoja na Maofisa wa Wizara.

  Makamu Rais wa GGM anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo ya Jamii, Simon Shayo, akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani) kuhusu msimamo wa Mgodi kuhusiana na malalamiko ya wananchi kuathiriwa nyumba zao kutokana na milipuko inayofanywa na Mgodi huo.

  Mbunge wa Jimbo la Geita, Constantine Kanyasu, akizungumza na wananchi wa Geita wakati Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (mwenye miwani) alipofanya ziara ya kazi wilayani humo kutatua kero mbalimbali za wananchi kuhusu masuala ya madini.

  Mkazi wa Kijiji cha Katoma wilayani Geita, Malekela Emmanuel akitoa malalamiko yake kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani) kuhusu nyumba yake kuathiriwa na milipuko inayofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).


  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani akizungumza na wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (mwenye Koti), akielekea kuangalia nyumba za wakazi wa vijiji vya Katoma na Nyamalambo wilayani Geita, zinazosemekana kuathiriwa na milipuko inayofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM). Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie na kushoto kwake ni Mbunge wa Geita Constantine Kanyasu.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, akisaini Kitabu cha Wageni katika Shule ya Msingi Nyamalambo. Shule hiyo ni miongoni mwa majengo yanayodaiwa kuathiriwa na milipuko inayofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (mwenye miwani), akiangalia mojawapo ya nyumba za wakazi wa maeneo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), zinazodaiwa kuathiriwa na milipuko inayofanywa na Mgodi huo.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (katikati), akitoa maagizo kwa Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Geita, Fabian Mshai (mwenye shati la mistari), kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuhusu malalamiko mbalimbali ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
  Na Veronica Simba – Geita

  Serikali imesema haitambui utafiti uliofanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kuhusu malalamiko ya wananchi waishio jirani na Mgodi huo kuharibiwa nyumba zao kwa kupata ufa sehemu mbalimbali kutokana na milipuko inayofanywa na Mgodi.


  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani, alikataa kutambua utafiti huo, uliotoa majibu kwamba Mgodi hauhusiki na mipasuko inayolalamikiwa, akitoa sababu kwamba, sio sahihi GGM kama watuhumiwa kujifanyia wao wenyewe utafiti. Badala yake, Dk Kalemani ameuagiza Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kufanya utafiti huo kwa siku tano kuanzia Jumatatu, Februari 29 mwaka huu na kuwasilisha taarifa yake ili Wizara ifanye maamuzi.


  Akizungumza mara baada ya kutembelea baadhi ya nyumba na majengo mengine ikiwemo Shule ya Msingi, zinazodaiwa kuathiriwa na milipuko ya Mgodi, katika maeneo ya Nyamalembo na Katoma wilayani Geita, Dk Kalemani alisema GST, ambao ni Wakala wa Serikali unaohusika na milipuko, watapitia kukagua nyumba na majengo yote yanayodaiwa kuathirika kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali akiwemo Diwani, Wenyeviti wa Vijiji husika pamoja na Wabunge wa maeneo hayo.“Haiwezekani wewe unatuhumiwa kupasua, halafu unaweka mtaalamu kujichunguza mwenyewe,” alisisitiza.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani alimwagiza Kaimu Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai kuuandikia barua uongozi wa Mgodi wa Geita, kuwataka ndani ya siku 14, watoe taarifa rasmi kimaandishi, kama wanalitumia au hawalitumii eneo ambalo inasemekana Mgodi huo umeweka vigingi na umezuia wananchi wasilitumie kwa shughuli yoyote wakati Mgodi haulifanyii kazi.


  Dk Kalemani alisema kuwa, baada ya kukagua alibaini ni kweli Mgodi unamiliki eneo husika na wameweka vigingi kuzuia wananchi wasifanye shughuli yoyote ndani yake, lakini akasema utaratibu unautaka Mgodi kuwaruhusu wananchi kuendelea kutumia eneo hilo kuendeshea maisha yao ikiwa wao Mgodi hawalitumii.


  “Huwezi ukaweka vigingi, ukasema hulitumii eneo, halafu humpi fidia mwananchi wa eneo husika na ukamwacha anaendelea kuzubaa asijue nini la kufanya.”


  Hata hivyo, Makamu Rais wa GGM anayeshughulikia Mahusiano na Maendeleo ya Jamii, Simon Shayo, alipoulizwa kuthibitisha endapo Mgodi uliandika barua ya kutoa zuio kwa wananchi wasitumie eneo hilo, alikana kuitambua barua hiyo hivyo Naibu Waziri akasema kwa kanusho lile, wananchi wanaweza kuendelea kulitumia kwa shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji na hata ujenzi.


  “Wananchi muendelee na shughuli zenu katika eneo hilo kama kawaida mpaka pale Mgodi utakapokubali kuwafidia. Kama hawatawafidia, hakuna zuio la ninyi kutokufanya shughuli zenu. Mkae, muendelee na maisha yenu kama kawaida,” alisema Dk Kalemani.


  Aliongeza kuwa, endapo Mgodi utaamua wananchi waondoke katika eneo husika, haitazuia kulipwa stahili za nyuma kutokana na muda waliopoteza.


  “Tamko la Mgodi kuwa hawajawahi kuandika barua ya kuwazuia ninyi kuendelea na shughuli zenu, wote tumelisikia hapa. Sasa, tusubiri taarifa yao rasmi kimaandishi kama nilivyoagiza ili ikitofautiana na waliyosema hapa, tuchukue hatua za kisheria,” alisisitiza.


  Aidha, Dk Kalemani aliwaagiza GGM kufikia Jumatatu, Februari 29 mwaka huu, wawe wamekarabati Shimo la Maji lililopo ndani ya eneo lao, ili kuzuia athari za maji hayo kufurika hadi nje ya eneo hilo na kufika katika makazi ya wananchi.“Kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010, Kifungu cha 14, inawataka muweke mikingamo na kuzuia athari ya maji pamoja na mambo mengine.”

  Akizungumzia agizo lililotolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu kutaka wananchi wanaozunguka Mgodi wa Geita wapewe miamba-taka kutoka mgodini, Naibu Waziri alisema, Tume iliyoundwa na Wizara kufuatilia na kutathmini jinsi kazi hiyo inavyoweza kutekelezwa, inakamilisha taarifa yake na utaratibu unatarajiwa kutolewa ifikapo Februari 28, mwaka huu.


  Pamoja na maagizo yote aliyoyatoa, Dk Kalemani alizitaka pande zote mbili, yaani wananchi na Mgodi, kuimarisha mahusiano mazuri baina yao kwani kuishi kwa kutumia sheria pasipo kuwa na mahusiano mazuri, haitawasaidia.


  Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mgodi pale wanapofanya vizuri. “Wakifanya vibaya, lazima sheria itachukua mkondo wake.”


  Naibu Waziri Kalemani alikuwa katika ziara ya kazi ya siku 10 ambayo aliihitimisha mkoani Geita, Februari 24. Mikoa mingine aliyotembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara yake pamoja na kukutana na wadau wa sekta za nishati na madini ili kujua changamoto zinazowakabili ni pamoja na Tabora na Kigoma.


  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na wawekezaji wa Makampuni ya utafiti na uchimbaji wa Mafuta na Gesi (hawaonekani pichani). Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Komba, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Dkt.  James Mataragio na kushoto ni  Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Albert Diliwa.
   Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt.  James Mataragio (katikati) akiongea jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kushoto) na wawekezaji wa Kampuni za kutatifi na kuchimba mafuta na gesi nchini. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio.
   Baadhi ya Wawekezaji wa Kampuni za kutafiti na kuchimba mafuta na gesi nchini, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wawekezaji hao. 
   Mmoja wa wawakilishi wa Kampuni ya Swala Tanzania, akiwasilisha taarifa ya mipango ya utekelezaji wa kampuni hiyo wakati wa kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na kampuni hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dodsal, K. Surendran, akitoa taarifa ya utafiti kuhusu Kampuni hiyo kugundua gesi eneo la Ruvu. Wengine wanaomsikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati). Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio (wa pili kulia), Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa TPDC, Kelvin Komba, na kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Albert Diliwa.  Wawekezaji sekta ndogo ya gesi watakiwa kuongeza kasi utekelezaji miradi


  Asteria Muhozya na Zuena Msuya, Dar es Salaam

  Imeelezwa kuwa, Tanzania inahitaji kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kupitia rasilimali ya Gesi asilia ambayo inatajwa kuwa chachu ya ongezeko la nishati ya umeme jambo ambalo litachochea ukuaji wa viwanda nchini.

  Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akihitimisha vikao vyake na  wawekezaji wa  makampuni   yanayofanya shughuli za  utafiti  na uchimbaji wa   Mafuta na gesi nchini, na kuwataka wawekezaji hao kuongeza kasi ya utekelezaji wa  miradi hiyo kutokana mahitaji ya nishati  hiyo nchini.
  Profesa Muhongo aliwaeleza wawekezaji hao msimamo wa Serikali kuhusu nishati hiyo kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vikubwa na vidogo huku rasilimali ya gesi asilia ikitajwa kuwa injini ya kufikia malengo hayo na kuwataka kuhakikisha kuwa gesi inapatikana nchini.

  “Hatujagundua mafuta, lakini tuna hazina kubwa ya gesi ambayo inawezesha kufikia malengo hayo. Ni lazima kampuni hizi zibadili mwenendo wao wa namna ya kufanya kazi. Tunataka kasi zaidi katika suala hili na kuhakikisha gesi inapatikana. Tunataka umeme mwingi unaotokana na gesi, umeme nafuu na wa uhakika,”amesisitiza Prof. Muhongo.

  Aliongeza kuwa, Serikali imelenga kujenga viwanda viwili vya Mbolea kutokana na gesi asilia na kuyataja maeneo ambayo viwanda hivyo vitajengwa kuwa ni Kilwa Mkoani Lindi na Mtwara.

  Aidha, mbali na kutaja ujenzi wa viwanda vya mbolea, alisema kuwa, mipango mingine ya Serikali ni kujenga mitambo ya kusindika gesi ili pia Tanzania iweze kushindana na nchi nyingine kusafirisha gesi iliyosindikwa nje ya nchi, jambo ambalo litawezesha kupata fedha   nyingi za kigeni.

  “Tunataka kujenga mtambo wa kusindika gesi asilia mkoani Lindi. Gharama za ujenzi huo zinatarajia kufikia kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 30, utakuwa mradi mkubwa zaidi na tayari eneo la ujenzi wa mtambo huo limepatikana,” amesema Prof. Muhongo.

  Pia alisema kuwa, mipango mingine ni  kutumia gesi majumbani ili kuachana na matumizi ya mkaa ambayo yanatajwa kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo, na kuongeza kuwa, kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee matumizi ya mkaa kwa siku moja yanafikia kiasi cha magunia elfu hamsini (50,000).

  Vilevile, aliongeza kuwa,  gesi asilia ni kichochea kingine muhimu kitakachosaidia kuondokana na umaskini na kuongeza pato la Taifa ikizingatia kuwa, ongezeko la  mahitaji ya kiuchumi linapanda kutokana na kuongezeka la idadi ya watu wa kipato cha kati na kuongeza kuwa, “ tunataka Tanzania iondokane na umaskini kupitia rasilimali za gesi na mafuta”.

  Aidha, mbali na nishati ya gesi asilia, Prof. Muhongo aliwaeleza wawekezaji hao kuwa, zipo rasilimali nyingine  ambazo wawekezaji wanaweza kuwekeza nchini na kuzitaja kuwa ni nishati jadidifu, pamoja na vyanzo vingine vya upepo, mawimbi,  umeme wa jua  na makaa ya mawe.

  Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo aliwata  wawekezaji hao kutoa taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa miradi yao ifikapo tarehe 1 Juni, tarehe 1 Septemba na tarehe 31 Novemba, 2016 na kuongeza kuwa, Serikali itatoa ushirikiano mkubwa kwa kampuni hizo kuhakikisha zinatekeleza mipango yao kwa wakati.


  Profesa Muhongo alihitimisha vikao na wawekezaji katika kampuni za utafiti na uchimbaji wa  mafuta na gesi tarehe 24 Februari,2016 ambapo  alianza kukutana na wazalishaji wadogo wa umeme wa chini ya   megawati 20 unaotokana na maji  mwezi Janurari, 2016, na wiki ya kuanzia tarehe 15 Februari,2016  alikutana na wawekezaji mbalimbali wenye nia ya kuwekeza katika sekta ndogo ya umeme.

  0 0

   Afisa utalii wa hifadhi Taifa  Arusha National Park (ANAPA)  Samweli Sakinoi akiwa anawapa maelekezo baadhi ya waandishi waliotembelea hifadhi hiyo
  Baadhi ya waandishi waliotembelea hifadhi ya ANAPA.

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Hifadhi ya taifa Arusha (ANAPA) inakabiliwa na changamoto ya mbalimbali ikiwemo ya kuzibwa kwa mapito ya wanyama (ushoroba )vilivyo tokana na shughuli za binadamu kafika vijiji zaidi ya 84 vilivyozunguka hifadhi hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari afisa utalii wa hifadhi hiyo Samweli Sakinoi alisema kuwa kufungwa kwa vishoroba hiyo vimesababisha wanyama wengi kutoingia na kutoka ndani ya hifadhi hiyo jambo ambalo linasababisha baadhi ya wanyama kutoweka na kusabisha kupungua kwa baadhi ya vivutio

  Alisema kuwa pamoja na hifadhi hiyo kuwa na vivutio mbalimbali ikiwemo uwepo wa mnyama aina ya mbega mweupe ambaye ni marachache kupatikana katika hifadhi zingine hapa nchini ,kupanda mlima meru ,utalii wa kutumia farasi ,utalii wa kumia magari ,pamoja na uwepo wa maziwa mengi madogo madogo pamoja na utalii wa kupiga makasi kitua ambacho kimefanya utalii kuongezeko la watalii kuongezeka kutoka watalii 20 hadi 40 wanaoingia kwa siku.

  Ili kukabiliana na changamoto hiyo mamlaka iyo imeanza utaratibu wa kukutana na uwongozi wa mkoa wilaya kwa lengo la kuwapatia elimu wananchi kuepuka kuvamia maeneo ya ifadhi kufanya makazi ,shughulli za kilimo na ufugaji jambo ambalo lina fukuza wanyama waliozoeya kuishi mazingira ya asili .

  “shughuli za kibinadamu zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa kutoweka  kwa baadhi ya wanyama hali ambayo inaweza kusababisha kupotea kwa wanyama katika hifadhi hiyo”alisema Saikononi

  Aidha alisema kuwa kwa sasa  ivi wameboresha vivutio vyao na wameongeza vivutio ambavyo vinaweza kusaidia kuongeza watalii ambapo alibainisha kuwa kwa sasa ivi  wameleta utalii mpya ambao aupo katika hifadhi zingine ambao ni utalii wa kutumia farasi ambao utalii huu ni mzuri ambao utalii huu ni mzuri kwani unasaidia wageni wengi kuweza kuona wanya kiuraisi
  Mmoja wa wananchi wanaishi pembezoni mwa hifadhi hiyo Elituliza Elisa alisema kuwa amekuwa  akinufaika na hifadhi hiyo kwa kukopeshwa fedha kwa riba nafuu pia pamoja na hafadhi hiyo kuwajengea shule watoto wao.

  Aidha waliitaka hifadhi hiyo iendelee kutoa misaa kwa wananchi ambao wamezunguka hifadhi hiyo kwa lengo la kunufaika na wageni ambao waliokuwa wanafanya utalii wa ndani katika hifadhi hiyo.

  0 0

  Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi  Ofisi ya Rais Ikulu katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 25, 2016.

older | 1 | .... | 775 | 776 | (Page 777) | 778 | 779 | .... | 1897 | newer