Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 771 | 772 | (Page 773) | 774 | 775 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Lady Jaydee
  Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee ametangaza rasmi kurudi tena kwenye muziki baada ya ukimya wa muda kidogo kwenye muziki. Lady Jaydee ameweka wazi ujio wake mpya kwenye muziki ikiwa leo ni siku ya 29 kuelekea uzinduzi wa #NaamkaTena. Tazama promo ya siku ya 29 ambapo Mh. Nape Nnauye kamzungumzia Lady Jaydee hivi.

  "Mimi Kama kiongozi wa Sanaa nchini, Nitahakikisha natetea muziki wa Tanzania Lady JayDee anaamka tena", amesema Mh.Nape Nnauye.

  #LadyJayDeeOfficialCountDown #NaamkaTena

  0 0


  0 0

   Dakika 90 za Mtanange wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga zimemalijika jioni hii hapa uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam kwa kutoka kifua mbele kwa timu ya Yanga baada ya kuchapa Simba bao 2-0. Magoli ya mchezo huo yametiwa kimiani na washambuliaji Donald Ngoma (Dakika ya 38 kipindi cha kwanza) na goli la pili limefungwa na Amissi Tambwe (Dakika ya 34 kipindi cha pili) na kufanya matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa mchezo.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma (11) akimpiga chenga Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban na kupachika bao la kwanza kwa timu yake wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma akishangilia Goli aliloipatia timu yake, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
  Mashabiki wa timu zote mbili waliwa wamefurika kwa wingi ndani ya uwanja wa Taifa.
  Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban akiwa amejiweka tayari kuokoa mpira uliokuwa ukielekezwa langoni kwake.
  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba, Kessy Ramadhan, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0.
  Mashabiki wa Yanga baada ya Ushindi.
  Mashabiki wa Simba baada ya kuchapwa.


  0 0


  Ndugu zangu,

  Michangomingine ya fedha imetoka kwa wadau wa Mjengwablog kwa kutuma kwa njia ya simu. Siku ya Alhamisi niliongea kwenye Nuru FM na Ebony FM kuhusu wazo la mtandao huu kukusanya misaada kwa wahanga wa mafuriko Pawaga.


  Mwitikio umekuwa wa kunishangaza hata mimi mwenyekiti wenu. Kwa fedha zilizochangwa taslimu na njia ya simu tumeweza hata kununulia magodoro 20. Miongoni mwa vilivyokusanywa kutoka kwa wana-Iringa wasamaria wema ni mahema 9 yenye ubora mkubwa.

  Nimevutiwa pia na wanafunzi an viongozi wa Kimarekani kutoka Programu ya CIEE niliokutana nao majuzi ambao nao walipata taarifa hizo na wamechangia shilingi laki tatu fedha taslimu.

  Hakika, mwitikio chanya ulilazimu utafutwe usafiri wa lori kwenda Pawaga hiyo kesho.

  Shukran za pekee kabisa kwa kijana mwana-Iringa na mtaalamu wa masuala ya transport na logistics, Ahmed Salim ‘ Asas’ ambaye amefanya jitihada za kuhakikisha vilivyokusanywa na wana-Iringa vinafika Pawaga kesho.

  Leo, Jumamosi, Feb 20, nitakwenda Pawaga na kwa vile viongozi wakuu wa Mkoa watakuwa Pawaga, basi, nitakabidhi misaada hiyo kwao ili nao wakabidhi kwa wahusika.

  Shukran nyingi kwenu nyote mliounga mkono jitihada hizi na ambao bado mnaendelea kuchangia.

  Kwa mwanadamu, kinachoangaliwa ni moyo wako, na si ukubwa wa unachotoa. Hata moyo wako ukiguswa tu kwa yaliyowapata ndugu zetu wa Pawaga ni faraja kwa walioathirika.

  Maggid,

  Iringa.

  0 0
 • 02/20/16--11:15: Article 7
 • ALIYEKUWA waziri katika serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kwa miaka 35, Joseph Mungai. 

  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Dk Hamis Kigwangalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi wakati wa ziara yake.

  ALIYEKUWA waziri katika serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kwa miaka 35, Joseph Mungai anadaiwa kurejesha serikalini eneo la hospitali ya wilaya ya Mufindi alilotuhumiwa kujipatia kinyemela na kulihodhi kwa muda mrefu bila kuliendeeleza.

  Taarifa ya kurejeshwa kwa eneo hilo lililopo nyuma ya hospitali hiyo liyopo mjini Mafinga, wilayani humo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jowika Kasunga kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kya Tatu, Dk Hamis Kigwangalla alipotembelea hospitali hiyo juzi.

  Akizungumzia mipaka ya kiwanja cha hospitali hiyo baada ya waziri huyo kutaka kujua kama haijakumbwa na uvamizi kutoka kwa wananchi, Kasunga alisema; “sehemu ya eneo la hospitali hii ilikuwa na mgogoro baada ya Mzee Mungai kudai kuimiliki kihalali.”

  Alisema mgogoro huo ambao hata hivyo haukutajwa muda wake, umekwisha baada ya mbunge huyo mstaafu kurejesha eneo hilo mikononi mwa hospitali hiyo.

  Akipokea taarifa hiyo, Dk Kingwala alitoa siku saba kwa uongozi wa halmashauri ya Mafinga Mji inayosimamia hospitali hiyo kujenga uzio utakaounganisha uzio wa hospitali hiyo ili kulinda mipaka yake.

  “Pamoja na kujenga uzio nataka mniletee ofisini kwangu ramani ya eneo zima la hospitali na taarifa rasmi inayoonesha mgogoro baina yenu na mvamizi huyo umemalizika. Haya ni mambo ya kisheria, isije ikawa leo mnasema mgogoro umekwisha halafu kesho tukasikia mzee Mungai kaenda mahakamani,” alisema.

  Dk Kigwangalla alizitaka halmashauri zote nchini kulinda maeneo yake kwa kuhakikisha yamesajiliwa na yana hati ili inapokuja mipango ya kuboresha au kutanua matumizi ya eneo kusiwepo na changamoto.

  Akizungumzia huduma hospitali hapo, naibu waziri alisema; “hospitali hiyo ni muhimu katika eneo hilo lakini hamuipatii kipaumbele. Nimekagua na kujionea hospitali hii, kuna maeneo ya changamoto. Mfano ni vyumba vyake vya upasuaji, nyie mnaona kama mnavyo lakini kiukweli ni kama hamna kwani vilivyopo vinafanana na stoo ambacho sio kipimo chake,” alisema.

  Alisema changamoto zingine katika vyumba hivyo ni uchakavu, havina mgawanyo wa vyumba, zinavuja, hazina maji, makabati yamechoka na paa lake halina viwango.

  Alisema angetembelea hospitali hiyo kama mkaguzi angelazimika kufunga vyumba hivyo vya upasuaji visitumike kwasababu ya mapungufu yake.

  Alitoa miezi mitatu kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Shaibu Nnunduma kukamilisha ukarabati wa vyumba hivyo viwili vya upasuaji ili vikidhi vigezo vinavyotakiwa vinginevyo mkurugenzi huyo atatumbuliwa jipu.

  Aliitaka hospitali hiyo pia kuanza mara moja ukusanyaji mapato yake kwa njia ya kielektoniki akisisitiza kwamba njia hiyo inapunguza mianya ya upotevu wa fedha zinazokusanywa.

  Ili maagizo hayo yatekelezwe kwa ufanisi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi alimuomba waziri huyo kuangalia uwezekano wa wizara yake kuwasaidia kuboresha hospitali hiyo ambayo kwasasa inasimamiwa na halmashauri mpya ya Mafinga Mji badala ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi.

  “Mheshimiwa waziri halmashauri hii iliundwa Julai mwaka jana, imetokana na halmashauri ya Mufindi; bado haiko sawa kiutendaji na kimapato. Kwahiyo kuna mapato tunaitegemea mpaka sasa halmashauri mama ambayo wakati mwingine inatoa kama hisani tu,” alisema.

  Akitoa mfano Chumi alisema zinaweza kuja Sh Milioni 17 kwa ajili ya sekta hiyo ya afya, lakini halmashauri yao pamoja na kubeba mzigo mkubwa wa kuhudumia hospitali hiyo ya wilaya inapata mgao wa Sh Milioni 3 tu.

  Akiahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya waziri huyo, mkurugenzi wa halmashauri hiyo alisema utekelezaji wake utanza mara moja wiki hii.

  0 0

  (Video na Benedict Liwenga-Maelezo)

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kushoto)walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.(Picha na: Frank Shija,WHUSM)
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.
  Mabeki wa Timu ya Simba wakiokoa mpira wa hatari katika lango lao wakati wa mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imeisha kwa wenyeji Yanga Afrika kuibuka kidedea kwa mabao 2:0.
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akishangilia mara baada ya Donald Ngoma kuiandikia Yanga bao la kwanza mnamo Dakika ya 38 ya mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
  Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mhe. Venance Mwamoto akifuatilia mchezo kati ya Yanga Afrika na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
  Mashabiki wa Timu ya Simba SC wakifuatilia mchezo kati yao na Yanga Afrika uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.

  0 0

   Wanafunzi wa shule ya msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima LitemboManispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifurahia vyoo vya kisasa vilivyojengwa na Benki ya Posta Tanzania.
   Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiongea kwenye mkutano katika shule hiyo muda mfupi kabla ya kuzindua vyoo hivyo. 
   Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vyenye matundu 14, vitakavyohudumia wanafunzi 850 katika shule ya Msingi ya Makambi, Songea Mkoa wa Ruvuma, ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 4.7 kulia ni Meneja wa Oparesheni wa tawi la Songea, Simon Mlelwa.
  Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa.
  MENEJA mahusiano na mawasiliano wa Benki Posta Tanzania,Noves Moses amelitaka suala la elimu bure liendane na mazingira mazuri ya kimiundo mbinu kwa wanafunzi pamoja na walimu wao ili kuifanya elimu hiyo kuwa bora zaidi.


  Rai hiyo aliitoa jana wakati akizindua vyoo vya kisasa vya Shule ya Msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, ambavyo vimejengwa na Benki hiyo kwa thamani ya shilingi Milioni 4.7 ikiwa nisehemu ya mchango kwa jamii katika kuboresha mazingira ya elimu.


  Akizindua matumizi ya vyoo hivyo vyenye matundu 14,Noves alisema kuwa jamii na taasisi mbalimbali zinatakiwa zitambue kuwa suala la elimu bure linatakiwa liendane na uboreshwaji wa mazingira ya wanafunzi na walimu wawapo shuleni hapo.


  Alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wadau wa elimu kulichukulia suala la elimu bure kama kigezo cha kutokuchangia sekta hiyo na baadala yake wanadai ni kazi ya serikali pekee jambo ambalo siyo sahihi katika uboreshaji elimu.


  “Suala la elimu bure lisiwe kigezo cha wadau kushindwa kuichangia sekta hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea baadhi ya shule kushindwa kuwa na mazingira mazuri ya watoto kujisomea pamoja na walimu wao kutokuwa na morali ya kufundisha”alisema Meneja mahusiano .


  Noves alisema kuwa Benki ya Posta Tanzania inafanya kazi kwa kiwango kikubwa na serikali hivyo imetoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa upande wa afya na elimu huku katika upande wa elimu wamechangia madawati na ujenzi wa vyoo bora vya kisasa kwenye shule mbalimbali hapa nchini .


  Kwa upande wake MwalimuMkuu msaidizi wa shule hiyo,Kanisius Ngongi awali akitoa taarifa ya shule hiyo kabla ya kukabidhiwa vyoo hivyo alisema kuwa shule hiyo inawanafunzi 850 na matundu ya vyoo yapo 14 na kuwa vyoo vyote vinamaji ya kutosha.


  Ngongi aliipongeza benki hiyo alisema kuwa shule hiyo kwa sasa imeshabadilika, mazingira yamekuwa bora kwa upande wa vyoo vya wanafunzi ambavyo kwa sasa hakuna shule ndani ya Manispaa hiyo yenye vyoo kama hivyo.  Mwalimu Ngongi alisema kuwa licha ya vyoo vya wanafunzi kuwa bora lakini bado kunachangamoto ya vyoo vya walimu maana vyoo walivyokuwa wakivitumia vimeshapoteza ubora wake na kuwafanya walimu hao kupata shida mahala pa kujisitili hivyo amewaomba wadau mbalimbali waweze kuchangia kama Benki ya Postainavyojitolea.

  0 0

  Mbunifu wa kazi za ufumaji na mmiliki wa Fflorinyan Designes Ms. Flora M. Kawa akizungumza jambo katika uzinduzi wa semina ya siku moja ya Wanafunzi wa Kike toka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimujuu kutoka mkoa wa Dar es Salaam.
  Mshauri kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Dominista Kombe akitoa semina kuhusu ugonjwa wa Saratani pamoja na madhara yake wakati wa uzinduzi wa semina ya siku moja ya Wanafunzi wa Kike toka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimujuu kutoka mkoa wa Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa TASOI, Bi. Belinda Mlingo akiwaonesha pesa wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu na kuwahasa wanafunzi kujihusisha na ujasiliamali maana ndio mafanikio yao ya baadae.
  Mwanachuo Doreen Tesha akiuliza swali wakati wa uzinduzi wa semina ya siku moja ya Wanafunzi wa Kike toka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimujuu kutoka mkoa wa Dar es Salaam.
  Afisa Mwandamizi Idara ya Matekelezo NSSF Bw. Abubakar Mshangama akiwaelezea  wanvyuo umuhimu wa mfuko wa NSSF katika uzinduzi wa semina ya siku moja ya Wanafunzi wa Kike toka vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimujuu kutoka mkoa wa Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Women Connect (T) LTD, Bi Pili Mpenda akizungumza na waandishi wa habari
  Bi. Hafsa Athmani Semndaia kutoka Women Connect (T) LTD akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa washiriki waliofika katika ufunguzi huo uliofanyika katika chuo kikuu Huria 
  Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye ufunguzi huo

  0 0
 • 02/20/16--11:30: Article 2
 • DK. C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.

  Na Mwandishi Wetu,

  Watoto wachanga wanaozaliwa na tatizo la tundu kwenye moyo, linalosababishia kudumaa katika ukuaji wao na hata kuwa na matatizo ya moyo wanashauriwa kupata matibabu ya kuziba tundu hilo kwa njia ya mrija bila kufanyiwa upasuaji. Hayo yamesemwa na DK. C.S Muthukumaran, mtaalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka hospitali za Apollo.

  (VSD) ni tundu katika ukuta unaotenganisha ventriko ya upande wa kulia na kushoto katika moyo. Ni tatizo linalotokea mara nyingi wakati wa kuzaliwa kwa mtoto na linaweza tokea lenyewe au kama ugonjwa.
  Ni kawaida kwa watoto wote kuzaliwa na tundu dogo katikati ya atria mbili na mara nyingi tundu hilo huziba ndani ya wiki chache. Mara nyingi hakuna tundu kati ya ventiko hizo mbili, ila baadhi ya vichanga huzaliwa na tundu hilo ambalo linakuwa ni chanzo cha magonjwa ya moyo na ndio sababu kubwa  ya watoto wachanga wengi kuonana na wataalamu wa magonjwa ya moyo.

  Imezoeleka mara zote kuziba tundu hili kwa upasuaji wa moyo (operesheni), ambao unahusisha kupasua kifua, kupitisha mashine na kuziba tundu hilo. Kwa mujibu wa DK. Muthukumaran kwa miaka 10 iliyopita kumekuwa na maendeleo makubwa ya kutibu tatizo hili ambapo hospitali za Apollo wamegundua njia ya kuziba tundu hilo kwa kutumia njia ya “pini kwenye tundu” (angiogram) bila kovu lolote kifuani. Licha baadhi ya aina za tundu hilo kwenye moyo kama lile lililopo chini ya valvu za moyo ni lazima lizibwe kwa upasuaji. Makala hii inaonyesha jinsi gani tundu hilo katika moyo linaweza kuzibwa bila upasuaji au wowote.

  Mtoto wa kike wa umri wa miaka 12 amekuwa na tatizo la moyo. Aligundulika akiwa na tundu katika moyo akiwa na umri wa miaka miwili. Madaktari walishauri afanyiwe upasuaji kwa sababu tundu lilikuwa karibu sana na valvu hivyo ingeweza kuharibu valvu ya moyo. Wazazi wake waliogopa suala la binti yao kufanyiwa upasuaji huo ambao ungeweza kusababisha apoteze maisha lakini pia kuwa na kovu kubwa kifuani. Waliahirisha upasuaji huo mpaka pale binti alipofikisha umri wa miaka 14. Kwa umri huo tayari lile tundu lilikuwa limeshaanza kuharibu ile valvu iliyokuwa karibu nalo.

  Wazazi walikwenda hospitali ya watoto Apollo kwa ajili ya ushauri mwezi Septemba  2014. Baada ya utafiti wa kwanza madkatari walisema wanashauri tundu lile lizibwe kwa njia ya “pini” bila kufanya upasuaji. Baada ya wazazi kuelewa, walimchukua mtoto kwa ajili ya maandalizi. Hatua za maandalizi zilifanywa mtoto akiwa katika nusu kaputi (local anaesthesia). Hatua hizo zilichukua nusu saa tu. Tundu hilo lilizibwa kwa mafanikio makubwa kwa njia ya pini na katheta na mgonjwa aliruhusiwa kutoka hospitalini siku iliyofuata. Familia ilifurahi sana, kwa jinsi walivyotua mzigo mkubwa wa tatizo hilo la binti yao wa miaka 14.

  Wakati wa ufuatiliaji wa maendeleo kwa muda wa mwaka mmoja, binti alikuwa akiendelea vizuri, hakukuwa na uvujaji wowote wala tatizo katika aortic na valvu za upumuaji. Tiba hii ya siku moja imemwezesha binti huyu kuepuka upasuaji katika mfumo wake wa upumuaji, kovu kubwa la maisha yake kifuani na siku 5-6 za kulala hospitali kwa ajili ya upasuaji.

  Uzibaji wa tundu katika moyo umekuwa ukifanywa kwa mafanikio kwa muda wa miongo miwili. Ufuatiliaji wa maendeleo  kwa muda mrefu umeonyesha kuwa uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia hii mpya ijulikanayo kitaalamu kama ‘Transcatheter’ ni mbadala bora wa kuepuka upasuaji. Kwa kipindi kirefu upasuaji umekua njia pekee ya kuziba tundu katika moyo. Ila ina kuwa hatarishi mara kadhaa hasa moyo kuziba kabisa, baada ya kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara moja na hata vifo. Zaidi ya yote, matatizo ya maambukizi, mfumo wa fahamu na mapigo ya moyo kwenda kasi zaidi (tachyarrhythmia). Baada ya kufanyiwa upasuaji, kovu litadumu maisha yote. Hivyo kwa njia ya hii mpya ya kuziba tundu ni bora na salama kwa afya ya baadae.

  Dk. C.S Muthukumaran ametoa maoni yake kwamba, kurithi ni moja kati ya sababu kubwa za kusababisha tundu katika moyo. Kwa mfano, mzazi mwenye tatizo la tundu kwenye moyo ana nafasi kubwa ya kupata mtoto mwenye hali hiyo zaidi ya mazazi asiye na tatizo hilo. Watoto wenye maradhi ya kurithi kama utindio wa ubongo mara nyingi huwa na tundu katika moyo. Uvutaji sigara kipindi cha ujauzito kwa mama kumehusishwa pia kama chanzo cha matatizo haya ya tundu katika moyo wa mtoto.

  Kama tatizo hilo la tundu katika moyo lisipopatiwa matibabu huwa linaweza kusababisha matatizo ya moyo, anasema Dk. Muthukumaran. Ukuaji wa tundu hilo katika moyo inaweza kusababisha moyo kushindwa kuendelea kusukuma damu, au kuwa na mapigo yasiyo sahihi, kudumaa kwa mwili hasa kwa watoto wachanga. Mtoto anashindwa kula sawa sawa na hivyo kuathiri ukuaji wake. Na matokeao yake mtoto anapungua uzito au asikue kabisa.
  Katika hospitali ya watoto ya Apollo uzibaji wa tundu katika moyo kwa njia ya Transcatheter  umefanywa kwa zaidi ya watoto 300 kwa miaka 5 iliyopita kwa kutokuwa na matatizo yoyote makubwa. Zaidi ya 50% ya matatizo ya tundu la saizi ndogo mpaka yale ya wastani yamezibwa kwa njia hiyo kuingiza katheta. Ujuzi mkubwa wa madaktari, uchaguzi sahihi wa wagonjwa, mipango sawia ndio ufunguo wa mafanikio katika njia hii ya kisasa.  Kuhusu Hospitali ya Apollo

  Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa. Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.
  Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo  0 0

  Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd ambao ndio waandaaji wa tamasha la Pasaka,Bwa.Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisi kwake kuhusiana na tamasha lake ambalo wanasanii wengi wameanza kumiminika kuunga mkono tamasha hilo.

  WAIMBAJI  wa nyimbo za Injili Tanzania Sifael Mwabuka na Goodluck Gozbert wamethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka 2016 linalotarajia kufanyika baadhi ya mikoa ya Kanda ya ziwa.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi  ya tamasha hilo, Alex Msama  waimbaji hao ni muendelezo wa kufanikisha ibad hiyo inayotarajia kufanyika mikoa ya Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).

  Msama alisema wanaendelea na maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo lina dhamira ya kukemea mauaji ya walemavu wa ngozi ‘albino’ kupitia waimbaji wa muziki wa Injili watakaopanda jukwaani siku hiyo.

  Msama alitoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwa sababu sehemu ya mapato ya tamasha hilo yanalengwa kusaidia kununulia baiskeli zaidi ya 100  za walemavu ambazo zitagawiwa kwa wahusika.

  Aidha Msama alitaja viingilio katika mchezo huo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto.Msama alisema hivi sasa waimbaji mbalimbali waliothibitisha kushiriki tamasha hilo wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya tamasha hilo.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA.Mwezeshaji katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka akizungumza katika warsha hiyo. Mwezeshaji katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka akizungumza katika warsha hiyo.Mwezeshaji katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka (kulia) akizungumza katika warsha hiyo. Mwezeshaji katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka (kulia) akizungumza katika warsha hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga (kulia) akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga (kulia) akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA.
  Bi. Stella Jairos ambaye ni miongoni mwa wagombea walioshiriki Uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha hiyo. Bi. Jairos aligombea Ubunge Vitimaalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma. Bi. Stella Jairos ambaye ni miongoni mwa wagombea walioshiriki Uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha hiyo. 

  Bi. Jairos aligombea Ubunge Vitimaalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma.[/caption] Na Mwandishi Wetu CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake waliogombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi ya kutosha kuzungumza kwenye vyombo vya habari. 

  Alisema utafiti mdogo walioufanya katika vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa uchaguzi huo. Takwimu hizo zilitolewa jana katika semina ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga alipokuwa akifungua semina hiyo ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania. 

   Alisema katika utafiti huo uliofanywa kwa miezi miwili yaani Septemba na Oktoba 2016 kwenye magazeti sita ulibaini kati ya vyanzo vya habari 2577 vilivyotumika kwenye habari za Uchaguzi Mkuu, wanaume waliotumika kama vyanzo walikuwa 2256 ikiwa ni sawa na asilimia 88 huku wanawake 303 kama vyanzo hii ikiwa ni asilimia 11 tu. Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA alisema utafiti pia uliainisha kuwa wanaume waliongoza katika makundi yote ya mada za habari hata zile ambazo hazikuwa zikihusiana na uchaguzi huo. Aliongeza kuwa katika utafiti huo ilikuwa ni nadra sana kupata habari ambazo zipo katika kurasa za mbele huku vyanzo vyake vikiwa vimetokana na wanawake. Habari za wanawake zilianza kujitokeza kuanzia kurasa za nne na kuendelea. "

  ...Kwa mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji wa habari za magazeti, wanawake kwa ujumla waliogombea na wasiogombea kote nchini walikabiliwa na unyanyasaji kama vile kufanyiwa ghasia, na vitisho wakati wa kampeni na siku ya uchaguzi. Pia wanaume walificha kadi za kupigia kura za wanawake zao, wanaume waliwalazimisha wake zao kuwapigia kura wagombea ambao wanawataka hata kama mwanamke hamtaki, utumiaji wa lugha ya matusi dhidi ya wagombea wanawake na wakati wa kampeni kuna baadhi ya wagombea wanawake walikamatwa na kutishiwa kwa tuhuma za kutotii amri ya Jeshi la Polisi," alisema Sanga katika taarifa yake akifungua semina hiyo. [caption id="attachment_67698" align="aligncenter" width="645"]Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na wagombea hao. Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na wagombea hao.[/caption] Wanahabari waliminya sauti za wanawake Uchaguzi Mkuu - Utafiti [caption id="attachment_67697" align="aligncenter" width="610"]Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na wagombea hao. Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na wagombea hao.[/caption] [caption id="attachment_67696" align="aligncenter" width="800"]Baadhi ya washiriki katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na baadhi ya wagombea walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu 2015 kuzungumzia changamoto za kutopewa nafasi wagombea wanawake, vijana na walemavu kwenye vyombo vya habari. Baadhi ya washiriki katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na baadhi ya wagombea walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu 2015 kuzungumzia changamoto za kutopewa nafasi wagombea wanawake, vijana na walemavu kwenye vyombo vya habari.[/caption] Kwa upande wao wanawake waliogombea wakizungumza katika semina hiyo walisema vyombo vya habari kiujumla havikutoa nafasi sawa kwa wagombea hasa wanawake na vingi vilikimbilia kutoa habari za wagombea wenye majina na maarufu kwa wanajamii. Bi. Stella Jairos ambaye aligombea Ubunge Vitimaalum Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma alisema wanawake walemavu mbali na kukosa fursa kwenye vyombo vya habari walikabiliwa na changamoto mbalimbali zilizofifisha mafanikio katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo. Naye Loyce Kibona aliyegombea upande wa vyama vya upinzani katika uchaguzi huo alisema licha ya vyombo vya habari kuwa ni changamoto kwao kupata nafasi ya kusikika bado hali ya kujiamini kwa wanawake na kukatishana tamaa kunaendelewa kukwamisha mafanikio ya kundi hilo hivyo kuwataka wanawake kuungana mkono. Imeandaliwa: www.thehabari.com _____________________________

  0 0

  Waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI, utumishi na utawala bora, George Simbachawene wa kwanza kushoto akiwaambia jambo mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo wa katikati na wa kulia mganga mkuu hospital ya Rufaa ya Tumbi dk. Peter Datan wakati alipotembelea shirika la elimu Kibaha juzi. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

  ………………………………………

  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

  Waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI, utumishi na utawala bora, George Simbachawene amesema ataunda tume ya watu wachache kutoka wizara hiyo haraka iwezekanavyo ili kuchunguza idara na vitengo vyote katika shirika la elimu Kibaha (KEC) ndani ya wiki mbili. 

  Amesema amefikia hatua hiyo baada ya kubaini tatizo kubwa la uongozi hivyo ipo haja ya kuchunguza hali iliyopo kuanzia juu hadi chini.

  Aidha Simbachawene alisema tume hiyo itakuwa na kazi ya kupita kila idara na kitengo kuchunguza mambo atakayoyaelekeza kwa siku 14 kisha mwezi march mwaka huu atarejea kufanya ziara na kuzungumza na watumishi.

  Alielezea kuwa kuna kila sababu ya kutafakari muundo mzima wa shirika na kuweka mikakati, sheria na mipango ya kisasa na kuondokana na ile iliyopitwa na wakati.

  Aliyasema hayo juzi katika ziara yake ya kikazi ya siku moja aliyoifanya shirika la elimu Kibaha ambapo alipata fursa ya kutembelea maeneo ya uwekezaji na shirika kijumla.

  Simbachawene alisema katika shirika hilo kuna wachache wanaonufaika na kuneemeka kwa kula hadi wamevimbilwa huku wengine wakiwa wanadidimizwa kimaslahi na kukosa haki zao za msingi.

  Alimtaka mwenyekiti wa bodi mpya ya shirika hilo Patrick Makungu na viongozi wengine katika bodi hiyo, kuwa na mawazo mapya ya kuendesha shirika badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kurudisha maendeleo yaliyokuwepo miaka ya nyuma.

  Alisema shirika la elimu Kibaha lina miradi mingi, ardhi kubwa na uwekezaji mkubwa hivyo waitumie kujiongezea kipato kwa maslahi ya Taifa na vizazi vijavyo.

  Simbachawene alieleza KEC inayumba na kuondoa taswira ya maendeleo na uchumi wake wakati ina vitega uchumi na ardhi kubwa.

  “Serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli ipo kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi na haitokuwa tayari kuona mashirika ya aina hii yanashushwa hadhi yake na watu wachache na kuwanyima haki watumishi uhuru wa kutembea kiajira na haki zao za msingi “

  ” Ipo haja ya kuchunguzana na kufanya maamuzi makini kwa kufuata misingi, sheria, kanuni na haki za kiutumishi”alisema Simbachawene.

  Hata hivyo alisema uwekezaji wa kampuni ya organia kutoka Egypt iliyowekeza kwenye shirika hilo ni mzuri na wenye tija lakini unaonekana haukuata taratibu na kusababisha maswali kutoka kwa watumishi.

  Awali mkurugenzi wa shirika la elimu Kibaha Dk. cyprian Mpemba alisema shirika linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupokea wagonjwa wengi 400 hadi 450 kwa siku na madawa.

  Dk. Mpemba alitaka serikali kufikisha fedha kwa wakati kwani ni muda mrefu sasa fedha wanazoahidiwa wanatumiwa pungufu tofauti na kiwango wanachoomba hivyo kushindwa kukidhi mahitaji.

  Nae mganga mkuu wa hospital ya Rufaa ya Tumbi, dk. Peter Datan alisema kitengo cha maafa hususan ajali (Trauma center) kinakabiliwa na ukosefu wa fedha kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

  Katika hatua nyingine waziri huyo alipokea kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa shirika hilo ikiwa ni sanjali na wastaafu shirikani hapo kukosa stahiki zao.

  Kero nyingine ni kuondolewa mradi wa kuku ulikuwa ukiingiza bil. 1 na kuingizwa mradi wa mkataba wa Organia ambao hawauelewi maslahi yake, upungufu wa nyuzi, madawa, fedha za allowance na walimu kutopandishwa madaraja kwa miaka sita sasa.

  Simbachawene alipokea kero hizo na kuahidi kuzifanyia kazi ambapo kwa upande mwingine aliitaka mganga mkuu dk. Datan kukumbushia fedha walizoahidiwa serikalini ili ombi lao lishughulikiwe haraka.

  0 0

  Mafundi wakiendelea na kazi ya kuunganisha mabomba ya maji eneo la Kiluvya jijini Dar es salaam ili kukamilisha mradi wa ulazaji wa mabomba hayo na kuwahakikishia wakazi wa maeneo ya Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata maji ya kutosha ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Machi mwaka huu.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo (kushoto) akipata maelezo ya mradi wa ukarabati wa matanki matatu ya maji yenye uwezo wa ujazo wa lita milioni 34 yaliyopo eneo la Kimara jijini Dar es slaam kutoka kwa Mhandisi wa Mradi huo P. G. Rajan (kulia) wakati wa alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mwishoni mwa wiki kukagua shughuli za upanuzi mitambo Ruvu Juu na Ruvu Chini inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA).
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoka ndani ya moja ya tanki baada ya kukagua ukarabati wa matanki matatu eneo la Kimara yenye uwezo wa ujazo wa lita milioni 34. Aliyesimama juu ya tanki ni Mhandisi wa Mradi huo P. G. Rajan.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo (kushoto) akisisitiza jambo eneo la Kiluvya wakati wa alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mwishoni mwa wiki kukagua shughuli za upanuzi mitambo Ruvu Juu na Ruvu Chini, ulazaji wa bomba na ukarabati wa matanki kazi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA).
  Baadhi ya mitambo mipya ya kusafirishia maji kutoka chanzo cha maji cha Ruvu Juu eneo la Ruvu Darajani kuelekea sehemu ya kusafishwa kabla ya kwenda kwa watumiaji.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiwa eneo la jengo jipya ilipo mitambo mipya iliyopo chanzo cha maji cha Ruvu Juu eneo la Ruvu Darajani kuelekea sehemu ya kusafishwa kabla ya kwenda kwa watumiaji.

  …………………………………………………………

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Nimeridhishwa na kasi ya ulazaji wa mabomba ya maji kutoka vyanzo vya Ruvu Chini na Ruvu Juu, ukarabati wa matanki na ujenzi wa matanki mapya ya maji kutokana na eneo dogo lililobakia ili kukamilisha miradi na kuwapatia maji ya uhakika wakazi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

  Kazi ya ulazaji wa bomba la maji hadi matanki yaliyopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es salaam, lenye urefu wa km 55.5 ambalo linasafirisha maji kutoka chanzo cha Mtambo wa Ruvu Chini Bagamoyo mkoani Pwani imebakia km 1.1 ili kuwapatia maji ya uhakika wakazi wa mikoa hiyo.

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo alitoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja mwishoni mwa wiki kukagua shughuli za upanuzi mitambo Ruvu Juu na Ruvu Chini, ulazaji wa mabomba na ukarabati wa matanki kazi ambayo inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA).

  “Jukumu la kuwapatia maji ya uhakia wakazi wa mikoa ya Pwani na Dar es salaam katika miradi yote miwili ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ni kuhakikisha ukarabati wa matanki ya Kimara, ujenzi wa tanki jipya Kibamba na ulazaji wa bomba unakamilika kwa wakati” alisema Mhandisi Kalobelo.

  Akifanya majumuisho baada ya kukagua kazi ya ukarabati wa matanki ya Kimara, ujenzi wa tanki jipya Kibamba na ulazaji wa bomba Ruvu Juu yanasukumwa kutoka chanzo cha maji cha Ruvu Darajani kupitia kwenye bomba hadi matanki yaliyopo Kimara, lenye urefu wa km 51 Mhandisi Kalobelo amemtahadharisha Mhandisi Mural Mohan wa kampuni ya Megha kutoka nchini India inyofanya kazi katika mradi huo kuwa kulingana na taarifa za mamlaka ya hali ya hewa nchini mwaka huu kuna mvua nyingi, hivyo aongeze nguvu na kasi ya kulaza mabomba hasa maeneo ya mabondeni ili akamilishe mradi huo ndani ya mwezi wa tatu.

  Mhandisi Kalobelo ameridhishwa na kasi ya makandarasi wanaojenga mradi huo baada ya kutembelea ukarabati wa matanki ya Kimara, ujenzi wa tanki jipya eneo la Kibamba, ulazaji wa bomba eneo la Kiluvya na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu eneo la Ruvu Darajani. 

  Kwa upande wake Mhandisi Mural Mohan wa kampuni ya Megha kutoka nchini India amemhakikishia Mhandisi Kalobelo kuwa watafanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa ili kuwapatia wananchi wa mikoa ya Dar es salaama na Pwani huduma ya maji ya uhakika na kuondoa kero ya upatikanaji wa maji iliyowasumbua wananchi hao kwa muda mrefu.

  Aidha, baada ya kujionea kazi iliyofanywa kwenye mradi wa Ruvu Juu, Mhandisi Kalobelo alielekea kwenye chanzo cha maji cha Ruvu Chini kilichopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ambapo alijionea mitambo mipya inavyofanya kazi ya kusafisha maji kabla ya kusafirishwa kwenda kwa watumiaji ambao ni wakazi wa mikoa ya Dar esa salaam na Pwani na kuhitimisha ziara yake eneo la Mbezi Beach ambapo kimebakia kipande cha km 1.1 kukamilisha kazi nzima ya ulazaji wa bomba.

  Aidha, Mhandisi Kalobelo amewasihi wakazi wa maeneo yote ilipo au ilipopita miundombinu ya maji wailinde na kuitunza.

  Pia ameziagiza mamlaka zinazohusika na ulinzi kufanya utaratibu wa kuwa na ulizi wa uhakika ili miradi hiyo inapozinduliwa na mitambo kuwashwa kuwe na uhakika wa miundombinu ya maji kuwa salama kwa kuwa uwekezaji uliofanyika umetumia ghrama kubwa za walipa kodi na washirika wengine wa maendeleo wenye nia njema ya kuboresha huduma za jamii ikiwemo maji.

  Kwa upande wao Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi (DAWASA) Romanus Mwang’ingo na Afisa Msimamizi wa Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Chini kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) Tumaini Ndosi wamesema kuwa wako bega kwa bega na wakandarasi wanaofanya kazi katika miradi yote miwili ili kutekeleza ahadi na azma ya vingonzi nchi ya kuwapatia wakazi wa jiji la Dar es salaam na mkoa Pwani maji ya uhakika waweze kujiletea maendeleo yao ikizingatiwa hakuna maisha bila maji.

  Maeneo ambayo wakazi wake watanufaika na huduma ya maji ni kuanzia maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani.

  Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala kwa upande wa Ruvu Chini wakati Mtambo wa Ruvu Juu utawahakishia wakazi wa maeneo Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Kibangu, Makuburi pamoja na eneo lote la Tabata.

  0 0

  Pichani Mmiliki wa Mjengwablog.com na mwongozaji wa kipindi cha ‘ Nyumbani Na Diaspora’ akikabidhi mbele ya Mwenyekiti wa kijiji cha Kisinga, Ndg. Shabani Mtimbwa na Mtendaji Kata ya Mlenge, Bi. Sarah Mbilinyi misaada iliyotolewa na Wana- iringa na watembeleaji wa mtandao wa Mjengwablog.com wakiwamo wafuatiliaji wa kipindi cha ‘ Nyumbani na Diaspora’ kinachorushwa TBC1.

  Misaada iliyokabidhiwa ni pamoja na mahema 9 na magodoro mapya 20. Kuna mabegi mengi ya nguo na viatu vya watoto, wanawake, wanaume. Misaada ina thamani ya shilingi milioni tatu na nusu. Shukran za pekee kwa ndugu Ahmed Salim ‘ Asas’ kwa kufanikisha lojistiki ya kufikisha Pawaga misaada hiyo.

  0 0

  The theme of the 2016 International Mother Language Day is “Quality education, language(s) of instruction and learning outcomes.”

  This underlines the importance of mother languages for quality education and linguistic diversity, to take forward the new 2030 Agenda for Sustainable Development.

  In Sustainable Development Goal 4, the 2030 Agenda focuses on quality education and lifelong learning for all, to enable every woman and man to acquire skills, knowledge, and values to become everything they wish and participate fully in their societies. This is especially important for girls and women, as well as minorities, indigenous peoples, and rural populations. This is reflected in UNESCO’s Education 2030 Framework for Action, a road-map to implement the 2030 Agenda, encouraging full respect for the use of mother language in teaching and learning, and the promotion and preservation of linguistic diversity.

  Multilingualism is essential to drive these objectives forward – it is vital for success across the 2030 Agenda, regarding growth, employment and health, as well as sustainable consumption and production, and climate change.

  UNESCO brings the same focus to advancing linguistic diversity on the Internet, through support to relevant local content as well as media and information literacy. Through the Local and Indigenous Knowledge Systems (LINKS) programme, UNESCO is highlighting the importance of mother and local languages as channels for safeguarding and sharing indigenous cultures and knowledge, which are vast reservoirs of wisdom.

  Mother languages in a multilingual approach are essential components of quality education, which is itself the foundation for empowering women and men and their societies. We must recognize and nurture this power, in order to leave no one behind, to craft a more just and sustainable future for all.

  This is UNESCO’s message on this International Mother Language Day.

  0 0

  Idda Adam ambae ni Mkurugenzi wa Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza, akionyesha mavazi mbalimbali yanayopatikana ofisini kwake, Mtaa wa Ghana GreenView, Nyamanoro Jijini Mwanza.

  "Sisi tunahusika na suala la urembo pamoja na ushonaji wa mavazi ya kila aina ikiwemo mavazi ya Kitchen Party pamoja na Harusi (Wanaume kwa wWanawake). Tumelenga kukata kiu ya ushonaji wa mavazi kwa wakazi wa Jiji la Mwanza ambao awali walikuwa wakishona nguo zao nje ya Mwanza;

  Pia tunawatumia wabunifu wa mavazi kutoka Jijini Mwanza na kutumia ujuzi wetu wa ushonaji na hivyo kuzalisha mavazi ambayo wateja wetu wamekuwa wakiyafurahia". Anasema Idda na kuwahimiza kutembelea ofisini kwake au kuwasiliana nae kwa nambari 0767 68 28 88.
  Idda Adam anasema Mikalea Professional Tailors wabunifu na washonaji wa mavazi ya kila aina.
  Mavazi mbalimbali kutoka Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza
  Mavazi mbalimbali kutoka Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza
  Mkurugenzi akiteta jambo na fundi wake 
  Mafunzi Ushonaji wa Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza wakiendelea na shughuli za ushonaji.
  George Binagi-Binagi Pazzo (Kushoto) akizungumza na Idda Adam (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza.

  0 0
  0 0  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga (pichani) amewataka Watanzania kuzingatia sheria za mtandao ambazo zilitungwa mwaka jana kufuatia kuonekana kuwepo kwa baadhi ya watumiaji ambao wamekuwa hawafati sheria.

  Mhe. Kitwanga alisema wanaotumia mtandao wanawajibu wa kutumia mtandao kwa matumizi ambayo hayatavunja sheria na ambao watakuwa wakikiuka sheria hiyo serikali haitawavumilia na watawachukulia hatua za kisheria.
  Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera John Bulimba.

  “Adhabu ya kuvunja sheria hii ya makosa ya mtandao ni mbaya sana na ninataka kuwambia Watanzania wazingatie sheria za mtandao … kifungo ni miaka 30 au hata zaidi,” alisema Kitwanga.
  Aidha aliwataka ambao wamekuwa wakitukanwa katika mitandao ya kijamii wapeleke malalamiko Polisi na serikali imejipanga kuwachukulia hatua watumiaji ambao wamekuwa hawafati sheria za mtandao.

  Kwa upande wa Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba alisema kuwa jeshi hilo limekuwa likiwachukulia hatua watumiaji wote wa mitandao ambao wamekuwa wakikutwa na hatia ya kufanya matumizi mabaya.

  Alisema tangu imetungwa sheria hiyo wameshafungwa baadhi ya watumiaji na kesi saba zikiwa mahakamani na bado wanaendelea kufatilia watumiaji wengine ili wawachukulie hatua.

  “Polisi tunaendelea kuwachukulia hatua watumiaji ambao wanakuwa na makosa na kwasasa kuna kesi saba zipo mahakamani … tangu sheria imetungwa kesi tunazopokea zinazohusu mitandao zimepungua kutoka 25 hadi 30 kwa siku ila siku hizi zinakuwa 10 au chini ya hapo,” alisema Bulinda.

  Nae mmoja wa watumiaji wa mtandao, Grace Mwanga aliwashauri Watanzania wenzake kudumisha maadili ya kitanzania na kuifanya mitandao kama njia ya mawasiliano kama jinsi lilivyo kusudiwa na waanzilishi wa mitandao hiyo.“Watanzania tudumishe maadili yetu ya zamani, mitandao isitufanye tusahau asili yetu … tutumie mitandao kuwasiliana na hata kufanya matangazo ya biashara zetu,” alisema Grace.

older | 1 | .... | 771 | 772 | (Page 773) | 774 | 775 | .... | 1897 | newer