Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 770 | 771 | (Page 772) | 773 | 774 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.

  Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa.

  Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.

  Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.

  Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata.

  “Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,

  “Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.

  Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza jambo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).

  Na kuongeza kuwa vijana wengi wasomi hawajui faida za kuanza kwa kujitolea kuwa kunampa uzoefu na zaidi katika kuhudumia jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa na kusudi za kuelimisha jamii kuhusu mambo mengi kwao pia kupata elimu mpya.

  Kwa upande wake, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa amezishauri taasisi za vijana kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwenye maeneo ya wazi ili kupata nafasi ya kukutana na vijana wengi zaidi.

  Alisema kuna kundi kubwa la vijana walio mtaani hivyo kufanya kwao maonesho ya wazi watapata nafasi ya kutoa elimu kwa vijana walio mtaani ambapo nao hawajapata elimu kuhusu kujiunga na taasisi hzio kwa kujitolea.

  Aidha, aliwataka vijana kutumia vitu vilivyo na asili ya Tanzania kama utambulisho wao kama jina la warsha hiyo lilivyokuwa Kitenge – Africa – Volunteerism (KAV).
  Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa warsha hiyo.
  Baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni kwa vijana, wa kwanza katika mstari wa mbele ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa.
  Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu walishiriki katika tukio hilo, wakajifunza na kuoneshwa kufurahishwa na kuhamasika na vijana wenzao wanaofanyakazi za kujitolea ambapo iliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) ikiwa na lengo la kuhamasisha masuala ya kujitolea miongoni mwa vijana ambapo pia ililihusisha shindano la vazi la kitenge na kujitolea (KAV), tukio hilo ni kuhamasisha ili watu watambue kwamba suala la kujitolea ni sawa na jambo la kila siku kama kuvaa vazi la kitenge.
  Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), (kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa vijana aliyohudhuria katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi ya kujitolea miongoni kwa vijana.
  Mtendaji Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat Bakar akitoa maelezo kuhusu YUNA inavyofanya kazi kwa jamii ya Tanzania na hususani vijana katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
  Mkurugenzi Mtendaji wa Young Tanzanian for Community Prosperty, Alfred Magehema akitoa maelezo kuhusu taasisi yake na jinsi taasisi yake inavyofanya kazi katika kuisaidia jamii.
  Mmoja wa Maafisa wa Raleigh Tanzania, Rose Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi yao jinsi ilivyoanza, wanavyofanya kazi na mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.
  Meneja wa Taasisi ya AIESEC Tanzania, Onome Ahorituwere akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
  Pichani juu na chini baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge Africa Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni mwa vijana hao.

  Washiriki wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV), wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Na Lilian Lundo – Maelezo

  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Deonis Malinzi amemteua Mohamed Kiganja kuwa Katibu Mtendaji mpya wa baraza hilo baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Bw. Henry Lihaya kutenguliwa.

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Malinzi ameeleza kuwa uteuzi huo umekuja baada ya kuona mapungufu ya utendaji kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.“Baraza la Michezo Tanzania limefikia maamuzi haya baada ya kutoridhishwa na utendaji wa Bw. Lihaya na hivyo Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kufanya maamuzi ya kumtengua” alisema Bw. Malinzi

  Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya BMT namba 12 ya mwaka 1967 kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.

  Aidha kabla ya uteuzi huo Kiganja alikuwani Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake ulivyofanyika.

  Pia aliwahi kufanya kazi kama Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi wa Waziri Mkuu, anashahada ya kwanza ya Elimu katika masuala ya Michezo na Utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  0 0


   Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na wateja wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika ambapo wateja 40 walichaguliwa kuwa washindi wa promosheni hiyo. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha,
  Bakari Majid na Afisa masoko wa Airtel Nasoro Abdulbakari (kulia).
  Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akimkabithi mshindi wa Airtel Mkwanjika Diana Samwel na mkazi wa Dar es Saalam pesa taslimu mara baada ya kujinyakulia shilingi 480,000 kupitia boksi la Airtel Mkwanjika. 

  ·Zaidi ya wateja 212 wajishindia pesa taslimi
  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika nakupata washindi 40 ambapo kila mmoja atajishindia pesa taslimu hadi shilingi milioni 1 kupitia boksi la Airtel Mkwanjika

  Promosheni ya Airtel Mkwanjika ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Disemba na kuwazawadia wateja wanne watakaojiunga na vifurushi vya yatosha au kuongeza muda wa maongezi kupitia vocha au Airtel Money kila siku. Jumla ya washindi 28 walipatikana kupitia droo kila wiki na kuzawadiwa pesa taslimu.

  Akiongea wakati wa kuchezesha droo ya mwisho, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema” Leo tumefikia mwisho wa promosheni yetu ya Airtel Mkwanjika , promosheni ambayo imeweza kuwazawadia wateja zaidi ya 212

  nchi nzima. Tunajisikia furaha kuona mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja wetu na tunapenda kuwahakikishia kuwa Airtel itaendelea kutoa huduma bora za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu yanayoendelea kubadilika na kukua kila siku na huku tukiendelea kuwazawadia kupitia promosheni kama hii ya Airtel Mkwanjika”

  “Tunaamini kupitia Airtel Mkwanjika tumetoa zawadi ambazo zimewawezesha wateja wetu kukabiliana na changamoto walizonazo na kuwasaidia kuongeza mitaji ya biashara zao na kuongeza ufanisi katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi na za kijamii. Tunaamini washindi wetu watakuwa ni ushuhuda tosha wa namna gani Airtel kupitia promosheni hii imeweza kubadili maisha yao na ya jamii zao kwa ujumla. Aliongeza Matinde

  Promosheni ya Airtel Mkwanjika imefikia mwisho, Airtel bado itaendelea kuwawezesha washindi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao bado hawajaingia kwenye boksi la Airtel Mkwanjika kupata nafasi ya kufanya hivyo ili kuweza kujiokotea pesa na kukabithiwa zawadi zao.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu akiongea na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) na kuwaeleza kuhusu Mafanikio waliyoyapata Katika Siku 100 za uongozi wa Rais John Pombe Magufuli ikiwamo kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Saalam, Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari-MAELEZO Bi. Lilian Lundo.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO


  NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

  Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) wamefanikiwa kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini Katika Siku 100 za uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.


  Hayo yamesemwa  na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.


   “Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) katika kipindi cha kuanzia Novemba hadi februari tumeweza kufanikiwa kuchimba visima 52 zitakavyowezesha kupataikana kwa maji safi kwa watanzania katika maeneo mbalimbali na pia wakala umefanikiwa kuchimba mabwawa 3” Alisema Bw. Egwaga.


  Akiongelea Matarajio na mipango ya wakala Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Bw. Egwaga amesema kuwa wakala unatarajia kuchimba visima 400, kupima wingi wa maji katika maeneo 420, kusafisha visima 500, pumping installation visima 400 na kukarabati visima 100.  Katika kipindi cha miaka kumi wakala wamefanikiwa kuongeza cha maji kwa jamii kwa wastani wa 53,823m3 za maji kwa siku na kufikia wastani wa asilimia 86 na kuwawezesha wananchi kupata vyanzo vya maji safi na salama kupitia uchimbaji wa visima.


  0 0
 • 02/19/16--03:12: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

  Vituo vinavyotumika kuuza tiketi za mchezo huo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni Oilcom, Ubungo Oilcom, Uwanja wa Taifa Temeke, Mavuno House - Posta, Dar Live Mbagala, Breakpoint – Kinondoni, Kidongo Chekundu – Mnazi Mmmoja, Mwenge na Kivukoni Ferry.
  Kiingilio cha juu cha mchezo huo ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
  Milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa kuanzia saa 5 kamili asubuhi, huku barabara ya Chang,ombe ikifungwa kuanzia asubuhi, na magari maalumu yenye stika maalumu ndiyo yatakayoruhushiwa kuingia eneo la uwanja wa Taifa kwa kupitia barabara ya Mandela na uwanja wa Uhuru.
  Upande wa ulinzi, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama watakuwepo kuhakikisha usalama wa wapenzi wa mpira watakaokuja kushuhudi mchezo huo, vitu kama silaha, vilevi, mabegi na vitu vyenye ncha havitaruhusiwa kuingia ndani ya uwanja.
  Shirikisho linawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini kununua tiketi katika magari ya kuuzia tiketi katika vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizo halali kwa mchezo huo.
  Mchezo huo utachezeshwa na mwaamuzi Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na mwamuzi Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha) wote wakiwa wakiwa waaamuzi wenye beji za FIFA, mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) na Kamisaa wa mchezo huo atakua Khalid Bitebo (Mwanza). 

  0 0

  Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya. 

  SUALA la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bonde la Ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa Ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.

  Mara kadhaa huduma za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.

  Usumbufu kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda katika eneo hilo.

  Kumbuka Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.


  Suala kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea ikiwemo kuvitumia vikundi vya Kusimamia Rasilimali za Uvuvi katika Ziwa Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.

  Hata hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.
  Shughuli za Kupambana na Magugu Maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana
  Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group.

  0 0
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Mkuu wa bandari ya Tanga, Henry Arika (kulia kwake ) na Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Felix Mahangwa ( kulia wakati alipotembelea bandari ya Tanga Februari 19, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  ………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) amekagua bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo kesho (Jumamosi) saa 6 mchana.

  Waziri Mkuu ambaye aliwasili Tanga leo mchana ili kushiriki mazishi ya baba mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga, aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia njiani kurejea Dar es Salaam.

  Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na akataka apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo. Katika maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na tugboat (meli ndogo).

  “Nataka kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua tishari tatu ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua Serikali ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe (self propelled) “

  “Nataka maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia hela ya Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa badala ya kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi wa fani hii?” alihoji Waziri Mkuu
  “Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa,” aliongeza.

  Katika majibu yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam. “Pia wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana,” alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.

  “Mkuu wa Mkoa simamia hawa watu, msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa njia za panya. Kuna majahazi yanaleta sukari kutoka Brazil. Mheshimiwa Rais amepiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu vya ndani viweze kuongeza uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo hadi Pangani,” alisema Waziri Mkuu.

  Alisema changamoto inayoikabili Serikali ni kwamba hata Shirika la Viwango Tanzania (TBS) au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kuzikagua sukari hizo na hazijulikani ubora wake licha ya kuwa zinafika kwa walaji.

  Waziri Mkuu amerejea jijini leo jioni.

  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kaburini katika kaburi la Baba Mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia ,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mzee Ali Mwalimu katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Mchukuuni mjini Tanga Februari 19, 2016
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati aliposhiriki mazishi ya baba mzazi wa waziri huyo mzee Ali Mwalimu, nyumbani kwa marehemu eneo la Mchukuuni mjini Tanga Februari 19, 2016. 

  0 0

  NA Mwamvua Mwinyi Chalinze

  MBUNGE wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ametoa vitabu vya kujifunzia vya masomo ya sayansi na hisabati katika shule za msingi na sekondari jimboni humo vyenye thamani ya sh. Mil 70.

  Mbunge huyo ametoa vitabu hivyo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la KULEA childcare village ili kupunguza tatizo la uhaba wa vitabu hususan vya sayansi.

  Akikabidhi vitabu hivyo kwa mwalimu mkuu shule ya sekondari Mdaula , Melkisedek Komba, kwa niaba ya walimu wakuu wa shule nyingine Ridhiwani alisema jumla ya vitabu vyote ni 3,438 .

  Alielezea kuwa vitabu hivyo vitagawiwa katika tarafa tano zilizopo kwenye halmashauri ya Mji wa Chalinze ambapo tarafa ya Chalinze imepatiwa vitabu 998 na tarafa nne zilizobakia zitapata vitabu 610.

  “Tarafa ya Chalinze tumeipatia idadi kubwa ya vitabu kulingana na kuwa na shule nyingi za msingi na sekondari tofauti na tarafa nyingine za Msoga, Miono, Msata na Kwaruhombo. Ridhiwani alisema anafanya kazi zake za kuwatumikia wananchi kwa kutimiza ahadi zake ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo yanayoikabili sekta ya elimu.

  Alielezea kuwa kwasasa ameanza na kutoa vitabu mashuleni ili kuwawezesha wanafunzi kujisomea na anaendelea na kutatua changamoto za madarasa na madawati katika shule zenye matatizo hayo kadri itakavyowezeka.

  Alilipongeza shirika la KULEA na wadau mbalimbali kwa kujitolea kushirikiana nae kupunguza changamoto za elimu na kijamii jimboni hapo.Nae mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mdaula Melkisedek Komba alishukuru kwa msaada huo na kusema utasaidia kupunguza tatizo la vitabu lililopo.

  Komba aliitaka serikali iangalie uwezekano wa kuongeza walimu wa sayansi kwani bado wanamahitaji ya walimu hao watano. Alisema licha ya kutosheleza kwa vitabu lakini bado tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi shuleni humo ni kubwa.

  Mwanzilishi wa shirika la KULEA Romi Mtenda alisema shirika hilo lipo bega kwa bega kuwezeshwa masuala ya jamii na elimu sanjali na watoto yatima na wajane na lilianzishwa mwaka 2007.

  KULEA imeshasaidia jimbo la Chalinze, kutoa madawa katika kituo cha afya cha Chalinze na kujenga matundu ya vyoo na kutoa vitabu mbalimbali kwenye shule za msingi na sekondari.

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura ((wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TFF, BMT na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mara baada ya kumaliza wa kikao kilichofanyika ofisinii kwake leo jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kimefanyika ili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye uwanja wa Taifa.Picha na: Frank Shija, WHUSM
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza katika kikao baina yake na uongozi kutoka TFF na BMT ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Dioniz Malinzi na kulia ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akifuatilia maelezo kutoka kwa Muhasibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Rose Janeth Bandisa (kulia) wakati wa kikao baina yake na uongozi kutoka TFF na BMT ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kimefanyika ili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa.Katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
  Katibu Mkuu wa TFF Celestine Mwesiga (kushoto) na Muhasibu Mwandamizi wa TFF Bw. Daniel Msangi wakifuatilia kwa makini wakati wa kikao baina yao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) akizungumza katika kikao baina ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
  Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)

  0 0

  Katibu Mkuu mpya wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja (aliyesimama) akizungumza na wafanyakazi wa Baraza hilo mara baada ya kuripoti ofisini hapo leo jijini Dar es Salaam. Katika ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Dioniz Malinzi na Afisa Utumishi Bw.Jacob G. Nduye.Picha na Frank Shija, WHUSM
  Mwnyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (kulia) akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu mpya wa Baraza hilo Bw. Mohamed Kiganja mara baada ya kuripoti ofisini hapo kufuatia uteuzi wake kumtaka kuanza kazi leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu mpya wa Baraza hilo Bw. Mohamed Kiganja mara baada ya kumkabidhi ofisi leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Febuari, 2016.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge akiagana na Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Sweden mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini Dar es salaam.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakitazama badhi ya magari ambayo baba wa taifa , Mwalimu Julius Nyerere aliyatumia kwenye miaka ya 1950 na 1960 baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi.
  Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza katika mkutano Maalum wa Wanarukwa na Katavi uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua mkutano Maalum wa Wanarukwa na Katavi kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya wananchi wa Mikoa ya Katavi na Rukwa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majliwa wakati alipofungua mkutano maalum wa Wanarukwa na Katavi kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akionyesha Tuzo Maalum aliyotuzwa na Wanarukwa na Katavi katika mkutano wao maalum uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majalwa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kasim Majlaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakifurahia ngoma baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho wakiendelea na majumu yao.

  Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana kwa mara ya pili na kikosi kazi cha watu 24 ambacho kitakuwa na kazi ya kutengeneza mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

  Mkutano unaoendelea katika ukumbi wa Wizara hiyo ya Afya, leo Februari 20th, 2016 unachambua mambo mbalimbali ya kuweza kuyafanyia maboresho na ya kimkakati ilikuweza kufikia malengo ya Mfuko huo wa Afya ya Jamii (CHF).

  Katika Mkutano huo, Dkt. Kigwangalla ni mwenyekiti wa kikosi kazi hicho ambapo kwa ujumla na wajumbe hao wapo kupanga mikakati thabiti.

  Baadhi ya Wajumbe wa kikosi kazi hicho wanaoshiriki kikao ni pamoja na Prof. Angwara Kiwara, Prof. Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri Marwa, Dkt. Deogratius Pisa, Dkt. Amos Kahwa, Irene Kiria, Semkae Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness Aikaeli na Obey Assey.

  Wengine ni Mathias Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy, Florence Mwanri, Athuman Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda, Daniel Ngowi, Beng’ Issa, Eugine Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus Leon na Dkt. Pastory Sekule.
  imeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog
  Mkutano huo ukiendelea.
  Baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho wakimsikiliza Naibu Waaziri wa Afya Dkt.Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa mkutano huo unaoendelea Wizarani hapo.
  Naibu Waziri Dkt.Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho (kulia) akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe hao. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye akiongea na wanahabari kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TBC Balozi Herbart Mrango ambao umefanywa na Rais John Pombe Magufuli,uteuzi huoumeanza kuanzia tarehe 19/02/2016, kulia ni Mkurugenzi msaidizi Usajili wamagazeti Bw. Raphael Hokororo

  …………………………………………………

  Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya umekamilika. Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.

  Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. Ninaamini Bodi Mpya itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.

  Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii kuwajulisha yafuatayo;

  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa kipindi cha miaka Mitatu.

  Balozi Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc – Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.

  Balozi Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi September, 2013.

  Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. Aidha nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.

  Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji, anateua Wajumbe sita wa Bodi. Katika uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.

  Hivyo basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC; 
  William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi. (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank Tanzania ).Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria. (LLB – UDSM; Associate Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of the High Court of Tanzania).

  Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania Investment Centre).Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public Service Mgt; Director of Management: President’s Office – Public Service Management).
  Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji na Utangazaji. (PhD – Mass Communication;Associate Dean: School of Journalism, University of Dar Es Salaam) na Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari. ( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and Sports).

  Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.

  Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa kasi kubwa duniani. Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.

  0 0

  Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ngazi ya Mkoa na Taifa hii leo wanatarajia kuzindua Rasmi Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) iliyopo Mtaa wa Ghana, Kata ya Nyamanoro Jimboni Ilemela.

  Uzinduzi huo utaambana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure. Pichani juu ni Secretary wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
  Pichani ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan Maseke.
  Kushoto ni Ofisi ya Katibu (Mwenye Miwani) wa Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) na Kulia ni Ofisi ya Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA).
  Jengo la Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan Maseke ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Rasmi hii leo. Ofisi hii iko GreenView, Mtaa wa Ghana Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza.

  0 0

  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akizungumza na wakulima na Washiriki wa Mafunzo ya kutumia simu za mkononi kupashana habari za kilimo yaliyofanyika Kijiji cha Kisamwene wilayani Butiama mkoani Mara leo mchana.
  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akiwaonesha wakulima wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara zao la mhogo uliotokana na mbegu aina ya ukombozi iliyofanyiwa utafiti nchini. Nyinondi alikuwa akiwaonesha wakulima jinsi unavyoweza kupiga picha zao hilo na kulitafutia soko wakati akitoa mafunzo ya kutumia simu jinsi kupashana habari za kilimo katika mafunzo yaliyofanyika juzi wilayani humo.
  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge akiwa katika shamba la mkulima wa mfano lililopo kijijini hapo.
  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge akimpiga picha mmoja wa wakulima katika mafunzo hayo.
  Wakulima washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
  Wakulima wakiwa katika shamba la mihogo.
  Mkulima akichimba muhogo wa mafunzo kutoka shamba hilo. Muhogo huo ni wa miezi nane tu.

  Shamba la muhogo lililotokana na mbegu bora ya mkombozi.
  Wakulima wakiwa katika mafunzo hayo.

  Wakulima wakiwa katika mafunzo ya kupiga picha.


  Wakulima wakiwa katika mafunzo ya kupiga picha.
  Hapa wakulima hao wakibadilishana mawazo baada ya kupiga picha za mafunzo.
  …………………………………………………………………………………………………..
  Na Dotto Mwaibale

  JUKWAA la Bioteknolojia (OFAB) limetoa mafunzo ya kutumia simu katika kupashana habari kwa wakulima wilayani Butiama mkoani Mara ili kuwarahisishia kazi zao za kilimo.  Akizungumza katika mafunzo hayo Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo hayo ya siku moja yalifanyika katika Kijiji cha Kisamwene wilayani humo ili kuwasaidia wakulima kupashana habari za kilimo na changamoto zao.

  “OFAB imeleta mafunzo haya kwa wakulima ambao ni wadau wetu ili waweze kupashana habari za kilimo, changamoto zinazo wakabili na kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia ya simu badala ya kutumia simu hizo kupigiana kwa mambo ya kawaida” alisema Nyinondi.

  Alisema kupitia mafunzo hayo wakulima hao wataweza kushirikiana na mitandao mingine ya kijamii ili kutatua changamoto zao za kilimo zikiwemo za wadudu waharibifu wa mazao, ukame na nyinginezo.

  Alisema washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni 28 kutoka Kata tano zilizopo wilayani Butiama mkoani humo na yaliwahusisha viongozi wa vijiji, kata na wenyeviti wa serikali za mitaa.

  0 0

  Na.Ahmad Mmow,Lindi.
  Wingi wa vizuizi vya ukaguzi barabarani umetajwa kusababisha rushwa na usumbufu kwa wafanyabiashara wanaosafarisha mazao ya misitu.
  Hayo yalielezwa jana na wafanyabiashara wa mbao na magogo kwenye warsha ya wafanya biashara wa mbao na magogo wa uwanda wa Selous hadi Ruvuma, iliyofanyika jana katika manispaa ya Lindi.

  Wakizungumza kwenye warsha hiyo iliyoandaliwa na mashirika ya kiraia ya Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF), Mtandao wa Kijamii wa Usimamizi wa Misitu(MJUMITA) uhifadhi, usimamizi na maendeleo ya mpingo(MCDI) kupitia kampeni ya mama misitu inayofadhiliwa na serikali ya Finland kupitia ofisi za WWF zilizopo nchini, walisema vizuizi hivyo vinasababisha rushwa, usumbufu na kuwapotezea muda.

  Frank Nganyanyuka alisema wingi wavizuizi unasababisha wafanyabiashara hao kupoteza muda mwingi barabarani.Alisema kutoka Nachingwea hadi Dar-es-Salaam kuna vizuizi takribani 19, ambavyo vinasababisha wachelewe barabarani."Wastani kila eneo lenye kizuizi tunatumia saa moja, maana yake siku mzima inakwisha kwa ajili ya kusimama, vizuizi vipunguzwe havinafaida zaidi ya kuchochea rushwa tu," alisema Nganyuka.

  Mfanyabiashara Mikidadi Kinogeandanga wa Lindi, alisema licha ya kuchelewa lakini pia maofisa waliopo katika vizuizi hivyo niwasumbufu na hawaziamini nyaraka ziliandikwa na maofisa wenzao wa kule zilikotoka mbao na bidhaa nyingine za misitu. Alihoji nisababu gani zinazosababisha wasiwaamini wenzao ambao wanadhamana na mamlaka kama yao.

  Alibainisha ili kuepuka kuchelewa wanajikuta wanarahisha usumbufu kwa kutoa chochote, kwa madai bila kufanya hivyo wanasumbuliwa hata kama hawakiuki, sheria, taratibu na kanuni."Malendego, Jaribu, Kimanzichana sijui wapi, niusumbufu tupu, lakini yote hayo nikutaka rushwa tu," alisema Kinogeandanga.

  Ali Kinunga anayefanyia biashara yake wilayani Kilwa, licha kuyalalamikia wingi wa vizuizi alilaumu serikali kutowashirikisha wafanyabiasha wa mazao ya misitu ili kupata maoni yao kabla ya kupitisha sheria ambazo baadhi yake siyo rafiki na zinawaumiza.

  Alitolea mfano mabadiliko ya tozo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwaumiza. Kwamadai kuwa wanaotengeneza kanuni na sheria hawajui matatizo na vikwazo wanavyokutanavyo wafanyabiashara. Badala yake wamekuwa wakitoa maagizo tu. 


  Naye Bakili Kilete anayefanyia biashara yake katika wilaya hiyo ya Kilwa, alisema sheria zinazohusu misitu siyo rafiki kwa wafanyabiashara ikiwamo na uwepo wa vizuizi vingi visivyo natija kwa serikali na wafanyabiashara."Usumbufu na wingi watozo unasababisha tutafute njia nyingine ili tupate faida, maana kwa sheria zilizopo kama utataka utii na kutekeleza huwezi kufanyabiashara hii," alisema Kilete.

  Akijibu malalamiko ya wafanyabiashara hao, mratibu wa usimamizi shirikishi wa misitu nchini, Joseph Kigula, alisema sababu ya kuwepo vizuizi vingi ni kwasababu baadhi ya wafanyabiashara sio waaminifu.

  Akibainisha kuwa wafanyabiashara wangekuwa waaminifu kusingekuwa na sababu ya kuwa na vizuizi vingi.

  0 0

  Na.Ahmad Mmow, Lindi-Nachingwea.
  Ununuzi wa gari lenye namba usajili DFPA 1695, Landcruiser mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, mwanzo mwanzo mwa wiki iliyopita ilizua mvutano baina ya madiwani na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Mhandisi, Jackson Masaka.
  Landcruiser
  Wakizungumza kwenye mkutano wa pili cha baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Madiwani hao walisema walikuwa na mashaka katika ununuzi wa gari hiyo, kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya fedha zilizotumika kununulia gari hiyo na bila kuwashirikisha.

  Diwani wa kata ya Mkutokuyana, Sada Makota, alisema mchakato wa ununuzi wa gari hiyo umegubikwa na utata, kwa madai kuwa fedha ambazo awali zilitengwa kwa ununuzi wa gari hiyo ni shilingi 84 milioni, wakati zilizoidhinishwa kwenye bajeti ni shilingi milioni 120.00 tu, hata hivyo ilionekana ilinunuliwa kwa shilingi 124.76 milioni.

  Alisema licha ya ongezeko hilo, lakini pia taarifa haikuonesha fedha za nyongeza zilitoka wapi na kwaidhini ya nani.

  Diwani wa kata ya Lionja, Joachim Mnungu, alisema mkurugenzi alikuwa na kila sababu ya kuwajulisha madiwani kila hatua iliyohusu mchakato wa ununuzi, ikiwamo mabadiliko ya mara kwa mara ya bei.Alisema fedha zilizokatengwa kwa ajili ya ununuzi ni shilingi 84 milioni. Hata hivyo kabla ya gari hiyo kuletwa, bei ilipanda na kufikia shilingi 96 milioni.

  Kama hiyo haitoshi, baada ya kuletwa waliambiwa imenunuliwa kwa shilingi 124.76 milioni."Gari imekuja na namba za usajili za gari za misaada (DFPA) tena mtumba, wakala wa manunuzi gani anaweza kuleta gari yenye namba za usajili wa magari ya misaada," alisema na kuhoji Mnungu.

  Mkurugenzi mtendaji, Mhandisi Masaka akijibu hoja za madiwani hao, alisema ingawa yeye alikuwa hajahamia katika Halmashauri hii, wakati mambo hayo yanafanyika.

  Lakini taarifa zinaonesha mchakato ulikwenda sawa bila kukiuka taratibu, kanuni na sheria. Kwani ununuzi ulifanywa na wakala wa manunuzi wa serikali(GPSA) na kwamba shilingi 4 milioni ziliongezeka kutokana na gharama ya kusafirisha gari hiyo ambayo gharama yake halisi ni shilingi 115milioni.
  "Hizo shilingi 95.4 milioni zilirejeshwa na GPSA baada yakuonekana hazitoshi kununua gari iliyokuwa inatakiwa, ilibidi ziongezwe fedha" gharama ya gari ni shilingi 115, kusafirisha ni dola 4,354 sawa na shilingi 9milioni," alifafanunua Mhandisi Masaka.

  Alisema kiasi kilichongezeka kilitoka kwenye akaunti ya utawala. Nakwamba kiasi kilichoongezeka(shilingi 4milioni) kiliweza kutolewa bila kupata idhini ya madiwani kwani sheria inampa mkurugenzi uwezo huo.

  Akibainisha kuwa gari hiyo siyo ya msaada bali walilazimika kuchukua kabla ya taratibu kukamilika baada ya kupewa maelezo na GPSA kuwa wanaweza kusubiri hadi taratibu za usajili zikamilike au waipokee na wakati wowote wakachukue namba za usajili.

  "GPSA walitoa maelekezo kama tunaweza kusubiri au tupokee gari hiyo, ili baadae ikakachukuliwe baada ya taratibu zote kukamilika ikiwa ni pamoja na namba za usajili," alibainisha Masaka.

  Hatahivyo majibu hayo hayakuwaridhisha. Diwani wa kata ya Ugawaji, ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ahmad Makoroganya, alisema hakubaliani na majibu hayo kwani hadi baraza la madiwani la Halmashauri hiyo linavunjwa mwaka jana, mchakato wote kuhusu ununuzi wa gari hiyo ulikuwa umekamilika, ulibaki ufuatiliaji tu.


  Hivyo maelezo yaliyotolewa na mkurugenzi ilibidi waelezwe kipindi cha mchakato wa ununuzi.

  Madai ya madiwani hao yaliungwa mkono na mkuu wa wilaya hii ya Nachingwea, Pololeti Mgema, ambae alisema wataalamu walishindwa kuonesha thamani ya dola kwa shilingi ya Tanzania kwenye mabadiliko hayo ya bei ambayo yalikuwa yanafanyika.


  Aliwashauri madiwani hao waendelee kuhoji ili wapate maelezo yanayojitosheleza kwenye mkutano au waunde kamati ya uchunguzi, ambayo pamoja namambo mengine ichunguze uhalali wa gari hiyo kubandikwa namba za usajili wa magari yanayotolewa kwa msaada na wahisani.

  Mvutano ulikwisha baada ya madiwani hao kukubaliana kujadili suala hilo kwenye kikao cha kamati ya madiwani, baada ya baraza hilo kujigeuza nakuwa kamati.MWISHO.

older | 1 | .... | 770 | 771 | (Page 772) | 773 | 774 | .... | 1898 | newer