Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 769 | 770 | (Page 771) | 772 | 773 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Bharti Airtel ya India, Sunil Bharti Mittal kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaaam Februari 18, 2016.
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Airtel Afrika, Christian Defaria (kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Bharti Airtel ya India, Sunil Bharti Mittal (katikati) kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaaam Februari 18, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Anitha Jonas – MAELEZO.

  Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Feminist and Youth Change Organization (TAFEYOCO) limemuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha utaratibu wa kukutana na vijana ili kujadiliana mambo mbalimbali.
  Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bw. Elvis Makumbo alipokuwa akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam katika mkutano  uliyolenga kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt.  John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika siku mia moja za uongozi wake.

  “Vijana kwa sasa katika taifa ni wengi na ndiyo wenye uwezo wa kuleta maendeleo katika nchi na nguvu kazi ya Taifa na wanachangamoto nyingi hivyo Mheshimiwa Rais  akijaribu kukutana nao nakuwasikiliza matatizo yao itasaidia kuleta mafanikio katika nchi na kujua nini kifanyike kuleta maendeleo katika Taifa,” alisema Bw. Makumbo.

  Ameleza kuwa, Mheshimiwa Rais ameonyesha moyo wadhati wa kuwatumikia wananchi kwa kuwawajibisha watu wote walionekana wakitumia vibaya madaraka yao na kufanya ubadhirifu wa pesa za umma kinyume na taratibu za kiutumishi wa umma.

  Mbali na hayo Bw.Makumbo amemuomba mheshimiwa Rais kufikiria kuanzisha mfumo au taasisi itakayohakiki mali za mtumishi wa umma na kuhoji ni namna gani mali hizo amezipata ili kupunguza wimbi la watumishi wa umma wanao tumia fedha za serikali vibaya kwa kujinufaisha wenyewe huku wakijiwekea utajiri mkubwa usiyolingana na kipato chao.

  Mwenyekiti huyo aliendelea kumwomba Mheshimiwa Rais kuzidi kuzingozea nguvu taasisi za Serikali ili kuzijengea uwezo mkubwa wa kiutendaji mfano wa Taasisi hizo ni TAKUKURU na nyinginezo zinazosimamia mambo mbalimbali Yenye tija kwa Taifa.

  Shirika hilo limesema Kauli Mbiu ya Mheshimiwa Rais ya Hapa Kazi Tu imeongeza hari kubwa ya utendaji kwa wananchi kwa kuwahimiza kuwajibika ikiwemo kwa watu wa sekta binafsi na taasisi za umma.


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(katikati) akishuhudia  Mkurugenzi Mtendaji  wa ITV na Redio one, Joyce Mhavile ( kulia)akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia ( kushoto) wakati  uongozi wa kampuni hiyo  ulipotembelea kituo cha  ITV na Redio One jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuelendeleza Mahusiano mazuri ya kibiashara.
   Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhaville, (kulia) akiwafafanulia jambo wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati walipotembelea kituo hicho  kwa ajili ya kujifunza  mbalimbali na kuelendeleza Mahusiano mazuri ya kibiashara,Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Meneja Uhusiano Matina Nkurlu,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia  wakati  uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea  ITV na Redio One jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituoni hapo.
   Maofisa wa Vodacom Tanzania ,wakiongozwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao(wapili kushoto) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa  Rosalynn Mworia (aliyekaa)   Meneja Uhusiano Matina Nkurlu, (kushoto)na Meneja biashara,Grace Lyon  wakioneshwa jinsi taarifa ya habari inavyoenda hewani na  na mtangaziji wa kituo cha ITV Abdallah Mwaipaya, Wakati  Uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea kituo hicho  jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituoni hapo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(wapili kulia)  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ( kushoto)  na Kaimu mkuu wa Masoko na Mawasiliano,Yvonne Maruma wakimsikliza kwa makini  Mhariri wa  ITV na Redio One,Stephen  Chuwa alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na utendaji wa wa kituo hicho,Wakati  Uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea  kituo hicho  jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituoni hapo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhaville(kushoto) akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ,wakati wa ziara ya  kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na  kituo hicho jana.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kushoto) akimsikiliza matangazaji wa kituo cha EATV, Deo alipoongoza  Uongozi wa kampuni yake kutembelea  kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kituo hicho na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara  kituni hapo jana.
   Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao na   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia , wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  East Africa Redio na EATV,wakati  Uongozi huo ulipotembelea  kituo hicho  jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kituo hicho na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara  kituni hapo jana.
  Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao  akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Kampuni ya New habari Corporation jijini Dar es Salaam, wakati  wa ziara maalum ya kutembelea  chombo hicho cha habari jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na chombo hicho na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara  na chombo hicho,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa New Habari Corporation,Hussen Bashi.

  0 0

  KUMEKUWA na hoja iliyowasilishwa na mtu mmoja kwenye mitandao ya kijamii kuhusu matumizi ya NAPTHA kwa kurusharusha mwanga kidogo kwa uzalishaji wa hii NAPTHA.

   NAPTHA huzalishwa kwa wingi kutokana na usafishaji mafuta ghafi (crude oil) ambapo, crude oil hutiwa katika kinu cha moto au joto kali inayopelekea kuzalisha mafuta na gesi tofauti katika layers tofauti.

  Layers hizi hutofautisha mafuta na gesi tofauti yaani PETROL, KEROSENE (mafuta ya taa) na DIESEL mpaka chini kabisa kunapatikana LAMI.

  Hali kadhalika gesi aina tofauti kama butane, propane, nakadhalika hupatikana hapa, nivyema pia  na kuwajuza Watanzania kuwa hii gesi ya kupikia majumbani, iitwayo Liquefid Petroleum Gas au LPG, inayosambazwa katika mitungi kama ORYX, MIHAN, CAM GAS, LAKE GAS nakadhalika hutokana na mchanganyiko wa PROPANE NA BUTANE kupata LPG. 

  Huingizwa nchini kutoka nchi zinazozalisha mafuta na kusambazwa hapa nchini katika mitungi ya gesi ya kilo 3, 6, 15, 38, na hadi mitungi mikubwa ya kilo 500, 1000 nakadhalika.

  Sasa tofauti za mafuta haya huja kwenye parameters tofauti kama boiling points, flammability rates, viscocity, density nakadhalika nakadhalika.
  Refineries tofauti duniani huenda wakazalisha bidhaa Fulani na Fulani zaidi kulingana na mikakati yao , mfano huenda akaseti kupata petro zaidi.

  Ama ikirudi kwenye NAPTHA, hii imeegemea zaidi katika PETROLI na tofauti zinakuja kwenye parameters kama ilivyitajwa hapo juu. 

  Kutoka uchimbaji wa mafuta ghafi (crude oil) na usafishaji wa mafuta yaani petroleum refinery, ifahamike kwa Watanzania refinery tuliyokuwa nayo ya TIPER ambayo kwa leo ni mali ya kampuni ya ORYX. Refinery hii ilitumika miaka ya nyuma kusafisha mafuta, kwa maana mafuta ghafi yaliingizwa nchini, na uzalishaji au usafishaji wa mafuta kama nilivyoeleza awali ulifanyika hapa nchini. Refinery hii ilikufa kifo cha mende, ingawaje ki uchumi ilikuwa na faida.
                                                                                            
  Katika uchimbaji wa NATURAL GAS, pia hupitia hatua kama ya hapo juu, ila hapa huingizwa kwenye mtungi mkubwa kwanza wa High Pressure Separator, ambapo GAS ASILIA huchujwa, ikielea juu kwa sababu ya wepesi wake (density), na chini yake kubaki CONDENSATE. 

  Hii condensate, hukamuliwa maji (water) na kutolewa na ilibaki kuingizwa tena katika Low Pressure Separator. Hali kadhalika hupatikana maji na mabaki kuwa aina tofauti za kinachofanana na mafuta ghafi, Zao hili sasa, huwekwa katika treatment tofauti kupata kitu gani mzalishaji anataka….ambapo, pamoja na mengineyo hupatikana NAPTHA.
  Hii NAPTHA sasa hupitia pia michakato tofauti kama vile kuiondolea sulfur na treatments nyinginezo zinazoweza kukupatia PETROL.
  Vile vile, kutokana na NAPTHA, tunaweza pata SOLVENTS, sabuni za maji au cleaning fluids, diluents (nimekosa neno la Kiswahili hapa) za rangi, varnish, asphalt, pamoja na bidhaa kama solvents katika makampuni ya mpira (rubber) , viberiti vya gesi, hata mali ghafi katika dry cleaners na kutengeneza mbolea.
  Sasa basi, Watanzania tunapotezwa sana katika propaganda kuliko kuelewa vitu, na kuchangamkia Fursa Kuliko kumshambulia OILCOM, hapa naona fursa nyingi, nyingi, na nyingi ambazo OILCOM aliona baadhi, na sio kwa U-HASI BALI KWA U- CHANYA.
  Zipo sheria za OSHA zinazosimamia athari au maelekezo ya viwango vya matumizi ya NAPTHA. Na sheria nyingine nyingi katika hili.

  TPDC ilitengaza tenda ya kuuza CONDESATE. Wadau mbalimbali waliomba na aliyeshinda akapewa. 

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), akiongozwa na baadhi ya viongozi wa Machimbo ya Dhahabu ya Matinje yaliyopo katika Kijiji cha Matinje Kata ya Mwashiku wilayani Igunga. Naibu Waziri alitembelea Machimbo hayo hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani (Mwenye Suti-katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, Charles Nogu, wakati alipotembelea Machimbo hayo akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni. 
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini (katikati) akikagua machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, alipotembelea Machimbo hayo hivi karibuni. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mbunge wa Manonga, wilaya ya Igunga, Seif Gulamali. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa Machimbo hayo, wataalamu kutoka Wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Na Veronica Simba - Nzega
  SERIKALI imetoa siku tano kwa mwekezaji wa madini ambaye ni Kampuni ya NMDC Limited kutoka India, kushughulikia utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa Kata ya Ntobo iliyopo wilayani Igunga, mkoa wa Tabora, walioachia ardhi yao kumpisha mwekezaji huyo.

  Agizo hilo lilitolewa juzi, Februari 17 na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, wilayani Nzega alipokutana na viongozi wa Kampuni hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya wizara yake.

  Akiwa wilayani Igunga, Naibu Waziri alipokea taarifa kuwa mwekezaji huyo alipewa leseni nne za uchimbaji madini wa kati mwaka 2012 lakini mpaka sasa hajaanza shughuli za uzalishaji kutokana na kutolipa fidia za maeneo ya wakazi wa eneo hilo.

  Kutokana na taarifa hiyo, Naibu Waziri aliagiza kukutana na Mwekezaji huyo ambapo walikutana naye juzi akiwa wilayani Nzega akiendelea na ziara yake. 

  Katika kikao hicho, ilibainika kuwa, kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 20.7 zinadaiwa kama fidia kwa wananchi waliopisha eneo husika.

  Ilielezwa kuwa, ulipaji huo wa fidia umekwama kutokana na mwekezaji huyo kutotaka kulipa fidia yote kwa wakati mmoja bali anataka alipe fidia kidogo kwa kuanzia na eneo dogo kati ya lile analomiliki ambalo anadai ndilo atakaloanza kufanyia kazi.

  Aidha, alidai kwamba atakuwa analipa fidia kwa eneo lililobaki kulingana na atakavyokuwa akilitumia.

  Akizungumza katika kikao hicho, Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati-Magharibi, Humphrey Mmbando alimweleza Naibu Waziri kuwa, wananchi wa eneo husika wanalalamika kuwa tangia eneo lao lichukuliwe na mwekezaji huyo, shughuli zao zilizokuwa zikifanyika katika eneo hilo zimesimama na hivyo wanahitaji kulipwa fidia stahiki.

  Kamishna Mmbando aliongeza kuwa, kufuatia malalamiko ya wananchi, Ofisi yake ilimtaka mwekezaji huyo awe ametoa majibu ya namna atakavyoshughulikia madai ya wananchi ndani ya siku 10 ambayo ilikuwa ni juzi, Februari 17, wakati kikao hicho kikikaa.

  Kutokana na maelezo hayo, Naibu Waziri alitoa siku tano zaidi kwa mwekezaji huyo ili ashughulikie mambo kadhaa katika kutatua mgogoro huo.

  Ndani ya siku hizo tano, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo, atoe taarifa rasmi ya kimaandishi kwa Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi kuwa anakusudia kufanya uzalishaji kwa kuanzia na eneo dogo ndani ya leseni yake.

  Pia, alimtaka mwekezaji huyo kumwomba Mthaminishaji wa Serikali kufanya uthamini kwa kujikita katika eneo lile tu ambalo anakusudia kuanza kulifanyia kazi.

  Vilevile, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo kuzungumza na wananchi husika ili wakubaliane kiasi cha fidia atakachotoa kwao kwa kuzuia shughuli zao za kujipatia kipato katika eneo hilo kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

  Mbali na maagizo hayo, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo awaruhusu wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji katika eneo ambalo atakuwa hajaanza kulifanyia kazi.

  “Nimewapa siku tano zaidi, mfanyie kazi maagizo niliyoyatoa vinginevyo, tutachukua hatua nyingine stahiki za kisheria dhidi yenu.”

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani ameagiza kufutwa kwa leseni zote za madini ambazo hazifanyiwi kazi na maeneo hayo kugawiwa kwa wachimbaji wadogowadogo ili wayafanyie kazi na kulipa mrabaha kwa Serikali.

  “Kwa kuanzia, katika eneo hili, nimeagiza leseni za utafutaji wa madini za kampuni za Kilimanjaro Mine na Mabangu Resources ziandikiwe taarifa ya kufutwa na tutaendelea na maeneo mengine,” alisema.

  Alisema kuwa kuna wawekezaji wengi ambao wamekuwa wakishikilia maeneo kwa muda mrefu pasipo kuyafanyia kazi na hivyo kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na kodi, pia kuwakosesha wananchi maeneo ya kufanyia kazi.

  Awali, Naibu Waziri alitembelea Machimbo ya Madini katika Kijiji cha Matinje B, Kata ya Mwashiku wilayani Nzega ambapo mbali na kumpongeza mmiliki wa machimbo hayo, Jason Shinyanga, kwa kulipa mrabaha wa Serikali, alimtaka kuboresha mazingira ya uchimbaji katika eneo hilo.

  Meneo aliyoagizwa kuboresha ni pamoja na kujenga nyumba za kulala watumishi wake pamoja na vyoo bora. “Tunakupa taarifa ya siku 60 urekebishe dosari hiyo, usiporekebisha, tutasahau kama umelipa mrabaha au la,” alisisitiza Naibu Waziri.

  Aidha, Naibu Waziri aliwashauri wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji kuhakikisha wanapata ushauri wa kitaalamu kutoka ofisi za madini katika maeneo yao kabla hawajaanza shughuli hizo.

  Pia, aliwataka kuhakikisha wanakuwa na leseni halali za kuendeshea shughuli hizo za uchimbaji ili pamoja na mambo mengine kuongeza thamani ya maeneo yao pindi wanapotaka kuyauza au kuingia ubia na wawekezaji wa kati na wakubwa.

  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale wakati Naibu Waziri huyo alipowatembelea katika ofisi Makao Makuu ya TANROADS leo Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wakifuatilia taarifa toka kwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale wakati alipopata ugeni wa Naibu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani katika Makao Makuu ya ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.
  (Picha na TANROADS)

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo  akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.

  Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
   WANAUME wameshauriwa kushiriki na kufurahia mafanikio ya wanawake kwa kuwa na usawa wa kijinsia na kusaidia kufanikisha malengo na ndoto za wanawake wanaowazunguka katika maeneo yao.


  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo wakati akizungumza na wandishi wetu jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa wanaume wana nafasi kubwa ya kumsaidia mwanamke kujikwamua katika nyanja za kiuchumi, kiafya hata kijamii kwani ndiye baba, kaka, au kiongozi wa familia.


  Agnes amesema Kuwa kutambua umuhimu wa mwanaume katika suala hili, Trumark katika kuadhimisha siku ya wanawake dunianin wameandaa tamasha la Pamoja Tunafanikisha ambalo litahusisha wanaume ili nao waelewe kuwa wana umuhimu mkubwa katika maisha ya mama, dada, Binti na wake zao.


  Tamasha la Pamoja Tunafanikisha litafanyika Machi 5, mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomoni, eneo la Namanga jijini Dar es salaam ambapo wanaume na wanawake wataungana kusherekea mafanikio ya wanawake na  kutambua changamoto nyingi zinazomkabili mwanamke,  katika kuadhimisha siku hiyo  kutakuwa na  wadau mbalimbali  kutoka nyanja tofauti ili kujadiliana namna ya kuzikabili changamoto hizo  na kuzifanya  kuwa fursa na pia kuwapongeza wanawake ambao wameonyesha njia kwa kujikwamua kiuchumi, jamii na kiafya.


  Kampuni ya Trumark imekua ikiadhimisha siku ya wanawake Kwa takribani miaka mitano sasa na tumekuwa na mafanikio makubwa kwani washiriki wengi wamekuwa na mrejesho chanya, nakuongeza mtandao katika shuguli zao mbalimbali.


  Agnes amesema maadhimisho yataambatana na burudani kutoka kwa wasanii wa bendi ya mapacha watatu pamoja na chakula cha usiku katika kusheherekea mafanikio ya wanawake,pia anawakaribisha  wanawake pamoja na wanaume kujitokeza kwa wingi ili maadhimisho hayo yalete mafanikio zaidi  katika siku hii muhimu kwa jamii yetu. 
  Kwa mawasiliano

  Daria Erasto

  Afisa Uhusiano

  Trumark

  +255 716 676665/ 754 095017


  0 0
  0 0

  Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanayotarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili. Wengine ni Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana (wa pili kulia) na mratibu wa tukio hilo, Bi, Neema Gerald (kulia).
  Bw. Paul Koyi, Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Wilaya ya Temeke akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanayotarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili.
  Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanayotarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili. Wengine ni Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah (wa pili kushoto) na Bw. Paul Koyi, Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Wilaya ya Temeke (kushoto).

  Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanatarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili.

  Maonyesho hayo ya siku moja yatafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere na kushirikisha makampuni zaidi ya 17 kutoka taifa hilo linalotegemea uchumi wa sekta ya uzalishaji.Maonyesho hayo yanaandaliwa na kampuni ya Talemwa Investment (TICC) pamoja na Enterprise Mauritius kwa ushirikiano na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee itakayowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili fursa mbalimbali zilizopo katika nchi hizo.

  “Wafanyabiashara pamoja na Wazalishaji wetu wa ndani wanaendelea kutafuta fursa za uwekezaji katika masoko mbalimbali na kwa kuzingatia hili, mkutano na maonyesho haya ni fursa adhimu itakayowawezesha kuweza kutanua wigo wao wa kibiashara nchini humo,” alisema.

  Aliyataja baadhi ya makampuni yanayoshiriki maonyesho hayo kuwa ni pamoja na Abita Shades, Africasia Electronics Manufacturing, Bacotex Limited, Eurolux, Glory Plastics Ind Ltd, IF Glass, La Trobe Co Ltd, Marble and Stones, Navigation and Geocoding Technologies Ltd, Nivra Enterprises Ltd, Safocean Co Ltd, Sissi Creation, SLK Gold Taste Ltd, SMP International Ltd, Soge International, Top Detergent Ltd na V-Information Technology & Management Institute.

  “Natoa wito kwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na wauzaji wa jumla na wale wanaotaka kuwa mawakala wa bidhaa kutoka Mauritius wajitokeze kwa wingi katika maonyesho haya ili waweze kujionea bidhaa zinazoweza kufaa katika soko la ndani lakini pia kuweza kutengeneza mahusiano na kupata fursa zaidi za kibiashara,” alisema.

  Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah, alisema sekta zitakazoshiriki kutoka Mauritius ni pamoja na sekta ya ukandarasi, bidhaa za kilimo, kemikali, viwanda vya utengenezaji nguo na vidani, pamoja na sekta zingine.

  Bw. Subbamah alisema wafanyabiashara hao watatatumia siku ya Jumanne kutembelea wafanyabiashara hapa nchini ili kuweza kutambua mahitaji yao lakini pia kuweza kujifunza ni jinsi gani wanavyoendesha shughuli zao.

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale wakati Naibu Waziri huyo alipowatembelea katika ofisi Makao Makuu ya TANROADS leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wakifuatilia taarifa toka kwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale wakati alipopata ugeni wa Naibu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani katika Makao Makuu ya ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.(Picha na TANROADS)

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tarehe 18/02/2016 juu ya ripoti ya Utafiti wa Watalii walioingia nchini mwaka 2014. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Jonhson Nyella na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Zahoro Kimwaga kulia.
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wa Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

  Sekta ya utalii Tanzania ambayo mchango wake katika mauzo ya nje ya nchi ni takribani  asilimia 24.0 iliendelea kukua katika mwaka 2014 kama inavyodhihirishwa na ongezeko la idadi ya watalii wa kimataifa kutoka 1,095,885 mwaka 2013 hadi 1,140,156 mwaka 2014.  Matokeo ya utafiti wa mwaka 2014 yanaonyesha ongezeko kubwa la mapato ya utalii ambayo yanatokana na ongezeko la idadi ya watatii.  Wageni wengi wanaiona Tanzania kama kivutio pekee chenye watu marafiki na mandhari ya kuvutia.


  Utafiti huu umefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Idara ya Uhamiaji na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT). 


  Matokeo muhimu ya utafiti ni kama ifuatavyo:


  1)   Mapato yatokanayo na Utalii yaliongezeka kwa asilimia 8.2 hadi  kufikia Dola za Kimarekani 2,006.3 milioni katika mwaka 2014, ikilinganishwa na Dola za Kimarekani  milioni 1,853.3 zilizopatikana mwaka 2013;


  2)   Zanzibar ilipata Dola za Kimarekani 269.3 mwaka 2014 ikilinganishwa na dola za Kimarekani milioni 210.5 mwaka 2013;


  3)    Wastani wa matumizi yote ya mtalii kwa usiku ilikuwa Dola za Kimarekani 221 chini kidogo ya Dola za Kimarekani 284 zilizoripotiwa mwaka 2013.


  4)    Wageni waliofika chini ya mpango mfuko ziara walitumia wastani wa Dola za kimarekani 326.9 kwa mtu kwa usiku wakati wale waliokuja kwa kujitegemea walitumia wastani wa Dola za kimarekani 147.8;


  5)   Masoko makuu 15 ya utalii nchini yanachangia asilimia 82 ya watalii wote wa kimataifa. Zimbabwe, Uholanzi na China ni masoko mapya katika masoko makuu 15 katika mwaka 2014; ambayo yamechukua nafasi ya Sweden, Uswisi na India katika masoko Makuu 15 yaliyopatikana mwaka 2013;


  6)   Utalii wa wanyamapori - uliendelea kuwa shughuli kuu ya utalii katika Tanzania Bara ulichangia kwa asilimia 43.5. Idadi kubwa ya watalii waliokujai kutembelea wanyamapori walikuja kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa na Italia. Kwa upande Zanzibar, shughuli mashuhuri ilikuwa utalii wa ufukweni na kiutamaduni;


  7)    Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa asilimia 54.1 ya wageni wanatumia kati ya siku nane hadi 28. Wageni kutoka Ujerumani, Uholanzi, Italia, Ufaransa na Hispania walikaa muda mrefu zaidi na wale waliotoka Zimbabwe walikaa siku chache zaidi;


  8)    Kama ilivyoonekana katika tafiti zilizopita, watalii hawakufurahishwa na kutokuwa na huduma ya credit cards katika maeneo yanayotoa huduma za kitalii. Asilimia 87 ya watalii walilipia huduma mbalimbali za kitalii kwa kutumia fedha taslimu.  Nakala ya ripoti hii inapatikana katika tovuti ya taasisi washirika ambazo: www.mnrt.go.tz, www.bot.go.tz, www.zanzibartourism.net, www.nbs.go.tz na www. moha.go.tz. 

  (Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

  Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania na Mkufunzi wa Mafunzo ya Bioteknolojia , Dk.Emmarold Mneney (kulia), akiwafundisha wanachuo wa Chuo cha Ualimu cha Bunda (BUNDA TTC), kuhusu matumizi ya bioteknolojia na uhandisi jeni Wilaya ya Bunda mkoani Mara leo asubuhi.
  Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza na wanachuo hao katika mafunzo hayo.
  Wanachuo hao wakifuatilia mafunzo hayo. 

  Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Rweyemamu wakiwa katika mafunzo hayo.
  Walimu wa chuo hicho wakifuatilia mafunzo hayo.
  Wanafunzi wakiwa katika mafunzo

  Wanachuo hao wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo
  Mwanachuo, Noshad Bryson akiuliza swali katika mafunzo hayo.
  Mwanachuo, Mahana Mahana akiuliza swali.
  Mwanachuo, Elias Yohana akiuliza swali.
  Hapa baada ya mafunzo ni msosi kwa kwenda mbele.


  Na Dotto Mwaibale


  JUKWAA la Bioteknolojia Tanzania limetoa mafunzo ya matumizi ya bioteknolojia na Uhandisi Jeni kwa wanachuo cha ualimu Bunda kilichopo mkoani Mara ili kuwa jengea uwezo wa kuielewa teknolojia ya bioteknolojia kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na changamoto za kilimo.

  Akizungumza na wanafunzi hao jana Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Emmalord Mneney alisema kuwa teknolojia hiyo mpya ni muhimu kusambaa nchini ili kumkomboa mkulima.

  "Tumeamua kuleta mafunzo haya kwa wanachuo hiki tukiamini kuwa baada ya kuhitimu mafunzo yao watakwenda kuwaelimisha wakulima katika maeneo yao"alisema Dk. Mneney.

  Dk.mneney aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya tabianchi kumesababisha ukame na uharibifu wa mazingira ambayo yameathiri shughuli za kilimo hasa mazao.

  Alisema kuwa kutokana na hali hiyo serikali imekuwa ikiiwezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kwa ajili ya kuwaongezea uwezo wa kufanya tafiti za kilimo nchini.

  Dk.Mneney alisema kuwa changamoto kubwa ya wakulima ni kukosa mbegu bora za mazao ya pamba na mahindi hali iliyosababisha wakulima wengi kukata tamaa ya kilimo hicho na kuamua kulima mazao mengine.

  "Kutokana na changamoto hiyo Costech imekuwa ikifanya utafiti ndani ya maabara ya kisasa iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ili kupata mbegu bora ambazo zikionekana kuwa zinafaa zitasambazwa katika mashamaba makubwa na nchi nzima kwa ujumla" alisema Dk.Mneney.

  Mwanachuo hicho Mahana Mahana alisema mkoa wa Mara unachangamoto kubwa ya kilimo kutokana na ardhi kuchoka hivyo ni wakati wa watafiti kuliangalia hilo ili kuwasaidia wakulima kupata mbegu bora zitakazo waletea mafanikio ya kilimo ya kupata mazao mengi.  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akitoa taarifa ya utenguzi wa uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme.(Picha na Benedict Liwenga)

  Na Benedict Liwenga.
  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Marcellin Benedict Magesa kuanzia Februari 18 mwaka huu.

  Profesa Mbarawa amechukua hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali zikiwemo, kushindwa kusimamia matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali nchini, kushindwa kusimamia uendeshaji wa matenegenzo ya vivuko vya Serikali nchini pamoja na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali.

  ‘’Mhandisi Marcellin Benedict Magesa atapangiwa majukumu mengine wizarani Na hivyo namteua Mhandisi Manase Lomayani Le-Kujan kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuanzia Leo hii ’’, alisema Profesa Mbarawa.

  Aidha, Profesa Mbarawa amemuagiza Kaimu Mtedaji Mkuu huyo aliomteua kutekeleza mara moja mambo mbalimbali, ikiwemo kutengeua uteuzi wa Mkurugenzi anayeshughulikia matengenezo ya magari ya Serikali, Mhandisi Prisca Benedict Mukama na kumpangia majukumu mengine, pia kutengua uteuzi wa Meneja wa Karakana ya Magari ya Serikali (M.T Depot), Mhandisi John Alexander Mushi na kumpangia majukumu mengine.

  Kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Manase Lomayani Le-Kujan alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ufundi na Ushauri katika Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele katikati), akiongea jambo wakati wa kikao kati yake na wawekezaji katika Sekta ya Nishati, katika Ukumbi wa Tanesco, Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Julieth Kairuki.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akiongea jambo na baadhi ya wawekezaji mara baada ya kikao chake na wawekezaji ambao wameonesha nia kuwekeza katika vyanzo mbali mbali vinavyopatikana nchini na baadhi wamefika kupata taarifa kuhusu uwekezaji.
  Baadhi ya Watendaji kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara na Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo na Wawekezaji katika Sekta ya Nishati,
  Baadhi ya Wawekezaji wakiwasilisha taarifa zao za uwekezaji kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Baadhi ya maswali ambayo Profesa alihoji kutoka kwa wawekezaji hao wao ni uwezo wao kifedha, kiteknolojia,utaalam na uzoefu wa kazi katika vyanzo walivyochagua kuwekeza nchini.

  ………………………………

  Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta, Dar es Salaam

  Kutokana na mahitaji makubwa ya Nishati ya umeme barani Afrika, ambapo kiasi cha wananchi wake wapatao bilioni 1 wanatajwa kuwa bado wapo gizani Tanzania ikiwa miongoni mwao, imeelezwa kuwa, wawekezaji katika sekta hiyo wanavyo vyanzo vya uhakika vya kupata fedha za uwekezaji.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa mwendelezo wa vikao vyake na wawekezaji katika sekta ya Nishati vilivyoanza tarehe 15-18 Februari, 2016, ambavyo vililenga kukutana na wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika vyanzo mbalimbali vya nishati vinavyopatikana nchini ili kuhoji na kubaini kampuni ambazo ziko tayari na zina uwezo wa kuwekeza.

  Prof. Muhongo amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na Mpango wa Serikali ya Marekani kusaidia maendeleo ya sekta ya umeme barani Afrika unaoitwa ‘Power Africa Initiative’ ambao umetengewa Dola za Marekani Bilioni 6 ambapo Tanzania ni moja ya nchi zinazopewa kipaumbele katika mpango huo.

  Aidha, ameongeza kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo ipo katika nafasi nzuri ya kufaidika na fedha za Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4ALL) ambapo mpango huo unaelekeza kuwa, ifikapo mwaka 2030 kuwe na upatikanaji umeme kwa wote na ongezeko maradufu la utumiaji umeme wa nishati jadidifu na matumizi bora.

  Pia, Profesa Muhongo ameeleza kuwa, kutokana na mahitaji ya umeme Duniani kupanda kwa asilimia 26 tayari kiasi cha Dola za Marekani trilioni 48 zimetengwa, ili kuongeza kiasi cha watumiaji wa nishati hiyo ifikapo 2020-2035, ambapo dola za Marekani trilioni 40 zikiwa zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme na kiasi cha dola za Marekani trilioni 8 kwa ajili ya matumizi bora ya nishati.

  Vilevile, ameutaja mpango wa ‘China Afrika Partnership’ ambapo kiasi cha Dola za Marekani bilioni 60 zimetengwa kwa ajili ya miundombinu , huku nishati ikipewa kipaumbele na kuongeza kuwa, kutokana na urafiki wa muda mrefu na mahusiano mazuri kati ya Serikali ya Tanzania na Watu wa China, Tanzania iko katika nafasi nzuri za kupata fedha hizo.

  Halikadhalika, Profesa Muhongo ameleeza kuwa, Umoja wa nchi za Ulaya (European Union) pia ni chanzo kingine kwa wawekezaji kupata fedha kwa kuwa, nishati imekuwa kipaumbele kwa taasisi hiyo.

  “Wawekezaji makini macho yote sasa yapo Afrika. Tunataka fedha hizo zote zije Tanzania kuwekeza katika sekta ya nishati. Jipangeni vizuri mwende, ‘Power Africa’ na sehemu nilizotaja, fedha za uhakika za umeme zipo. fedha,”amesisitiza Prof. Muhongo.

  Aidha, kutokana na umuhimu na uharaka wa kutekeleza mipango hiyo, Profesa Muhongo amewataka wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza nchini kuzingatia muda na ratiba ya kutekeleza majukumu yao na kuongeza kuwa, “ikiwa kuna jambo litacheleweshwa na watendaji wa Serikali, tutachukua hatua, na ikiwa mwekezaji umeshindwa kwenda na muda wetu vizuri basi mradi wako utaachwa na wengine kupewa nafasi,”ameongeza Muhongo.

  Profesa Muhongo amebainisha kuwa fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati zinapatikana katika maeneo ya gesi asilia, makaa ya mawe, nishati jadidifu umeme wa maji, upepo, umeme wa jua biogas na vyanzo vingine.

  0 0

  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini makabidhiano hayo yalifanyika jana . 
  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa magodoro kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini makabidhiano hayo yalifanyika jana .
  Magodoro waliyokabidhi tigo ikiwa ni ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .
  Wafanyakazi wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana
  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (kushoto) , ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .

  Iringa, Februari 17, 2016: Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika wodi za Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi kukosa sehemu za kulala, mkoani Iringa.

  Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida. 

  “Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema Kiswaga.Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na mashuka 35.


  Mvua zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba zilisababisha watu 1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza.

  Msaada kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia jamii majanga yanapo ibuka.

  0 0


  0 0

  Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari leo hii katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji mkuu wa baraza ilo Bw. Henry Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar es Salaam kutokana utendaji usiolizisha.
  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Dionis Malinzi(kulia) akiongea jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye.Picha na Daudi Manongi. 
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo hii kuona utendaji wa Baraza hilo.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.

  Mhe. Nnauye alitengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema Mhe. Nnauye.

  Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.Kutokana na utenguzi huo Mhe. Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.

  Vilevile, Mhe. Nnauye amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini.Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.

  0 0

  Mmoja kati ya wanawake walioshirikia Mafunzo ya Ujasiriamali Kutoka Mkaoni Arusha akiwa kwenye Muonekano tofauti Mara na Naada ya Kutumia Vipodozi kwa Usahihi baada ya Kuapatiwa Elimu hiyo na wataalamu kutoka Taasisi ya Manjano foundation..

  Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa arusha yameingia awamu ya pili.Washiriki wamepata fursa ya kufahamu zaidi kuhusu vipodozi vya LuvTouch Manjano na namna ya kuvitumia. Mkufunzi na Mkurugenzi wa taasisi ya Manjano Foundation amependekeza wanawake wa jiji la Arusha kutumia vipodozi kwa usahihi kwa lengo la kujijengea heshima na kujiongezea kipato katika kazi yao ya upambaji.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation na Mkufunzi wa Maswala ya Vipodozi Mama Shekha Nasser Akitoa elimu Kuhusu Matumizi Sahihi ya Vipodozi Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Jiji la Arusha.

  Akielezea zaidi alisema matumizi sahihi ya vipodozi hasa vya LuvTouch Manjano vitakupa kazi nzuri na bora ambayo kila mteja ataipenda na kulifanya soko la kila mwanamke kukua kutokana na ubora wa kazi ya mikono yake.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof Yunus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Kuhusu uamuzi wa Tume kufuta usajili wa vyuo vikuu vishiriki vya Mtakatifu Joseph tawi la Songea. 
  Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Na Nyakongo Manyama MAELEZO
  TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefuta kibali kilichoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mtakatifu Joseph ambavyo ni Chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia (SJUCAST) na Chuo Kikuu kishiriki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (SJUIT) vilivyopo Songea.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Tume hiyo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania,  Prof. Yunus Mgaya amesema kutokana na mapungufu yaliyobainishwa na Tume ambayo ni matatizo ya ubora wa elimu na ukiukwaji wa Sheria za uendeshaji wa Chuo Kikuu kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu hii  imepelekea Tume kuchukua hatua ya kufuta usajili wa vyuo hivyo.

  “ kutokana na yaliyobainishwa hapo awali tunapenda kutaarifu umma kwamba ,Tume imejiridhisha kuwa hivi vyuo vikuu vishiriki viwili havitoi elimu ya Chuo kikuu ya viwango stahiki na ukizingatia wanafunzi katika Vyuo hivi ndio waathirika wakubwa wa matatizo yaliyopo”Alisema Prof Mgaya.

  “Napenda kufafanua kwamba Vyuo vikuu vishiriki tuliyovifutia usajili ni tawi la Songea na Vyuo vingine vishiriki vya Mtakatifu Joseph vilivyopo Dar es Salaam na Arusha vitaendelea kufanya kazi kama kawaida”Alisema Prof Mgaya.

  Prof Yunus Mgaya amesema wanafunzi wote wanaosoma katika vyuo vishiriki vilivyofutwa usajili wanaarifiwa kuwa watahamishiwa kwenye vyuo vikuu vingine vinavyofundisha programu za masomo zinazofanana na masomo wanayosoma hivi sasa chini ya utaratibu uliopangwa.

  Amevitaja vyuo ambavyo watapelekwa wanafunzi walipo katika vyuo vishiriki vilivyofutwa usajili kuwa ni Chuo Kikuu cha kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Chuo Kikuu cha  Kikatoliki cha Mwenge(MWECAU) na Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha(RUCU).

  Amesisitiza kuwa orodha ya majina ya wanafunzi na vyuo watavyohamishiwa yatawekwa kwenye tovuti ya Tume hivi karibuni na wale wote wanaonufaika na Mikopo toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, mikopo yao itahamishiwa katika vyuo watakavyokuwa wamehamishiwa.

  Vyuo vikuu vyote chini vinakumbushwa kufata Sheria na kuzingatia utoaji wa elimu inayokidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kitaifa na kimataifa, hivyo Tume haitasita kuchukua hatua stahiki kwa chuo kikuu chochote kitakachobainika kutoa elimu isiyokidhi viwango vya ubora kwa kisingizio cha aina yoyote.

older | 1 | .... | 769 | 770 | (Page 771) | 772 | 773 | .... | 1897 | newer