Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

Kongamano la Uhuru wa vyombo vya Habari lamalizika leo jijini Arusha,laibuka na azimio la Arusha la Uhuru wa Vyombo vya Habari Tanzania.

$
0
0

Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm akitoa mada kuhusu haki za binadamu jinsia na mitazamo ya Mataifa Mbalimbali ulimwenguni kuhusu Uhuru wa Habari na Haki za Binadamu siku ya mwisho ya Kongamano la maadhimisho ya Uhuru wa Habari duniani kwenye Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha. (Picha na Dewji Blog).

Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa maoni yake katika kuchangia Azimio la Arusha la kupaza sauti za waandishi wa habari kudai uhuru wa habari kwenye siku ya pili ya kongamano la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani lililomalizika leo jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano la siku mbili la kuadhimisha siku ya uhuru wa habari duniani hapa wakiwa wanafuatilia mjadala na mada mbali mbali zilizopelekea kutoka na azimio la Arusha la waandishi wa habari katika kudai mambo mbali mbali zikiwemo changamoto na sheria za tasnia hiyo zinazotumika hapa nchini.
Mwakilishi wa COMNETU ya nchini Uganda Jimmy Okello akitoa mada kwenye kongamano hilo juu ya Usalama na Ulinzi wa waandishi wa habari wa Kenya na Uganda na kueleza kuwa hali Usalama na Ulinzi kwa waandishi wa habari kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinalingana hazitofautiani japo zingine zimepiga hatua kwa sheria ya uandishi wa habari kuingizwa kwenye Katiba.

Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Nyirembe Munasa, Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm na Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikijadiliwa ambapo leo waandishi wa habari wametoka na Azimio la Arusha linalohusu mazingira ya usalama wao wawapo kazini na mazingira ya vyombo vya habari ikiwemo pia Serikali.
Mwalimu Ayubu Rioba akifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo.
Mama Rose Haji wa UNESCO wakifurahia jambo Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige.
Mwakilishi wa Mo Blog jijini Arusha Mahmoud Ahmed (kushoto) akiwa na mhariri wa Sibuka Fm Felix Kaombwe wakifuatilia majadiliano mbali mbali yaliyozua Azimio la Arusha la Uhuru wa Habari ikiwemo kupitishwa kwa sheria ya Uhuru wa Habari kwenye Katiba yetu na masuala ya Usalama wa mazingira katika kazi zao za kila siku.
Usia Nkhoma Ledama wa UNIC akiteta jambo na Mwenyekiti wa UN Tanzania Human Rights Group Bw. Tobias Rahm wakati wa Kongamano la siku mbili lillilomalizika leo jijini Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo wakati wa kufunga kongamano la Uhuru wa Habari Duniani lililomalizika leo jioni jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara ambapo amewaasa wanahabari kutimiza majukuma yao na kutoiyona Serikali kuwa inayafumbia macho madai yao na kuwa Azimio waliolotoka nalo litafanyiwa kazi ili kuboresha muhimili wa tasnia hiyo.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO akiongea kwa niaba ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi hapa nchini na kutoa shukrani kwa kuona ushiriki na kufana kwa hafla nzima ya Kongamano la Uhuru wa Habari Duniani na kuwa na imani kwamba Azimio la Arusha la Wanahabari litafanikiwa. Kongamano hilo limemalizika leo jioni kwenye Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
Mkongwe wa Habari Mama Eda Sanga (mwenye sweta jeupe) akiwa na wanafunzi wake wakibadilishana mawazo mwishoni mwa Kongamano la Uhuru wa Habari Duniani. Kulia kwake ni Gladness Munuo na Wa pili kulia Cecilia Mng'ong'o na Aliyekaa ni Dominica Haule wote ni wafanyakazi wa GEMSAT.

Mmoja wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiwa na Mhariri wa Sibuka Fm Felix Kaombwe na Meneja wa Program za Vipindi wa Mpanda Fm Bw. Revocutus Andrew nje ya ukumbi wa mikutano.

UK Alumni Launch Leadership Series

$
0
0
Mihayo Wilmore, the CEO of UhuruOne with Steve Gannon, CEO of Serengeti Breweries Ltd, at the launch of the UK Alumni in Tanzania Network's Leadership series at the British Council.

Around 40 British and Tanzanian alumni from UK universities met at the British Council in Dar-esSalaam on 30 April for the launch of a series of Leadership events. 

The presentations, being organised by the UK Alumni in Tanzania (UKAT) Network, aim to inspire and inform the members about effective leadership. Steven Gannon, CEO of Serengeti Breweries, together with Mihayo Wilmore, CEO of UhuruOne, shared their unique insights in response to the question ‘What is it really like to be a CEO?’ 

The speakers provided fascinating responses which reflected on how their family background, educational achievements and professional development had influenced their leadership journeys. They also discussed how they mobilise and inspire others to achieve success in their role as a CEO. 

The presentations were followed by a networking reception sponsored by Serengeti Breweries where members had the chance to meet and mingle with the guest speakers. Leeds University graduate Evarist Mganga, a UKAT management team member, commented, “These CEOs are great role models to young professionals in our network who wish to assume leadership roles in a wide variety of sectors.” 

 UKAT was founded in 2012 for UK alumni across Tanzania to foster support and mutual success through a range of activities. The organisation promotes UKAT’s events on Twitter @UKATz and the tzukalmni.co.tz website. The network warmly welcomes new members to join and be involved in the exciting calendar of upcoming events.

Makamu wa Rais Dkt. Bilal afariji na kuwasili Shinyanga kikazi

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Shinyanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili leo Mei 04-2013. Picha na OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa Balozi Habib Suleiman Bibi Moza Habib, wakati alipokwenda nyumbani kwa Marehemu Kilimani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa leo Mei 04- 2013. Kushoto ni Mama Zakia Bilal na kulia Mama Asha Bilal.

Rais Kikwete aongoza mazishi ya Marehemu Balozi Alfred Tandau

$
0
0


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Mau katika kaburi la Marehemu Balozi Afred Tandau wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.Picha na Ikulu).

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Waziri wa Zamani wa Kazi ,Marehemu Balozi Alfred Tandau wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Alfred Tandau ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini alifariki tarehe 30 Mwezi Aprili wiki iliyopita.

Watoto yatima washiriki tamasha la hisani la WoFI

$
0
0
 Women Footprints Initiative ( WOFI) Neema Msuya, address the media at charity family bonanza that provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.
 Children from New Life Home in Dar es Salaam enjoy a ride on a toy train during a charity family bonanza organized by Women Footprints Initiative which provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.
  Tatu Issa from New Life Home orphanage center in Dar es Salaam get a ‘face lift’ during a charity family bonanza organized by Women Footprints Initiative which provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.
One of the children from New Life Home orphanage center in Dar es Salaam engages in jumping castle during a charity family bonanza organized by Women Footprints Initiative which provided a rare opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the city.

 ============  ============  ==========


Watoto yatima washiriki tamasha la hisani la WoFI.


Dar es Salaam Mei 4, 2013: Shirika la Women Footprints Initiative (WoFI), leo limefanya tamasha la hisani la familia lijulikanalo kama Cheza Time na kushirikisha watoto kutoka vituo vya kulelea watoto yatima ambao wamecheza michezo mbalimbali na kupata fursa ya kujumuika na ndugu zao. Tukio hilo la aina yake limefanyika katika viwanja vya Leaders Club.  

Meneja miradi wa WoFI Neema N. Msuya amesema kuwa pamoja na kutoa burudani za michezo, tamasha hilo pia limetumika kupata fedha za kusaidia vituo hivyo vya watoto yatima na kuendeleza miradi ya wanawake inayoendeshwa na shirika hilo kwa lengo la kusaidia watoto na kuwawezesha kina mama kiuchumi..  

Alisema kuwa kusudi kubwa ya shirika la WoFI ni kuwawezesha watoto hao kupata mahitaji yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwapatia elimu na kuyataka makampuni, mashirika na watu binafsi kujitokeza kusaidia ili kuwajengea watoto hao msingi imara wa maisha yao ya baadaye.


“Tamasha  la hisani la familia tunalofanya hapa leo linakusudiwa kuwa tukio la kila mwaka ambalo, mbali ya kuhamasisha wahisani kuchangia mfuko wa shirika, litatumika kama chombo cha kuwaunganisha watoto na ndugu na jamaa zao huku wakiburudika na vinywaji baridi, michezo mbalimbali pamoja na kucheza muziki”, alisema.


Tamasha la leo lililovuta hisia za watu mbalimbali lilishuhudia watoto wachangamfu wakishiriki michezo ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuruka, kuogolea na kukimbia ndani ya gunia. Watoto hao pia walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao vya kuimba na kucheza muziki.


Shirika la WoFI ambalo siyo la kibiashara vile vile huendesha kampeni ya kuwaelimisha wasichana walioacha shule kwa sababu mbalimbali kuachana na tabia hatarishi na kujishughulisha na biashara halali ili kujipatia kipato cha kuwasaidia katika maisha yao. Kampeni hii inafahamika kama Binti Amka.


Kampeni nyingine inayoendeshwa na shirika hili inajulikana kama Jitambue uwezo wako Sasa ambayo inawahamasisha wasichana wa shule za sekondari kusoma kwa bidii na kushinda vishawishi vilivyo mbele yao na hatimaye kutimiza ndoto za kuwa na maisha bora hapo baadaye. 

IGP MWEMA AWAVISHA NISHANI MAOFISA, WAKAGUZI NA ASKARI.

$
0
0
5
6Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akimvisha nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, Mkuu wa Kitengo cha maadili, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Patrick Byatao kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.7Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akimvisha nishani ya utumishi mrefu Tanzania, Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Elice Mapunda kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.8Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akimvisha nishani ya utumishi mrefu Tanzania, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyela kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.91011
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akimvisha nishani ya mwenge wa uhuru daraja la nne, Sajini Martha Njau kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.


1Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akikagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam.icha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.2Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akikagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.3Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akikagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.4Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha cha Polisi Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ali Lugendo wakirudi jukwaa kuu baada ya IGP kukagua gwaride lililoandaliwa rasmi kwenye hafla ya kuwavisha nishani Maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Kanda ya Mashariki. Hafla hiyo ilifanyika jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi..

Coca-Cola Kwanza Mbeya lifts inter-company trophy

$
0
0
Coca-Cola Kwanza Managing Director, Basil Gadzios wears a broad smile as he hands over a trophy to Coca-Cola Kwanza Mbeya player Deogratias Raymond who emerged man of the match at an inter-company competitive match against Coca-Cola Kwanza Dar es Salaam. The match was held at the University of Dar es Salaam football grounds.
Coca-Cola Kwanza Managing Director, Basil Gadzios gives a big hand to referee Athuman Kazi for proper handling of an inter-company competitive football match between Coca-Cola Kwanza Mbeya team and Coca-Cola Kwanza Dar es Salaam team at the University of Dar es Salaam grounds over the weekend. Mbeya team won 4-1.
Coca-Cola Kwanza Mbeya football team and supporters celebrate victory after downing their counterparts Coca-Cola Kwanza team 4-1 to lift the champions trophy in a competitive match held at the University of Dar es Salaam football grounds over the weekend.

Coca-Cola Kwanza Mbeya football team humiliated their counterparts Coca-Cola Kwanza Dar es Salaam 4-1 in a competitive inter-company football match held at the University of Dar es Salaam football grounds. The winners were leading 1-0 at the breather.

The first goal came in the 38th minute when Deogratias Raymond, who was later declared to be the man of the match, scored with a close range after receiving a long pass from. Efforts by Coca-Cola Kwanza to level matters were always frustrated by uncompromising Mbeya defenders.

As expected, the match was tense and competitive based on the tug of words from players and supporters from each side that their team would win the match and lift the trophy, cash and above all the bull which was grazing a few meters from the pitch waiting for the winner.

The second half started on a quick note and after a couple of near misses for both teams, Mbeya team scored their second goal in the 52nd minute off a foul kick which was expertly taken by Aggrey John that sailed deep in the net, arousing chants from supporters.

Referee Athuman Kazi, awarded Mbeya team a penalty in the 56th minute after lethal striker Deogratias Raymond was brought down in the penalty box. The spot kick was taken by Baraka Michuzi.

The Dar city men got their consolation goal in the 71st minute after a good combination upfront before Bony Alex scored the goal close range drive. The winners sealed their victory in the 82nd through Bahati Msokwa.

Coca-Cola Kwanza Managing Director

Siku ya Wakunga Duniani. Mikono ya kwanza kukupokea ulipoingia duniani.

$
0
0
Mama Ye! leo, Mei 5, inatoa wito kwa Mh. Dk Hussein Mwinyi (MB), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kushughulikia kwa haraka upungufu wa idadi ya wakunga wanaohitajika ili kuwasaidia akina mama wa Tanzania kujifungua salama.

 Wakunga wana jukumu kubwa la kuwahudumia wanawake katika kipindi chote cha ujauzito na pia ni wataalamu wenye ujuzi wa kushughulikia matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifungua. 

 Wakunga wengi wanatembea umbali mrefu na kufanya kazi masaa mengi ili watoe huduma bora kwa wanawake katika jamii zao. Wataalamu wa masuala ya afya ya wajawazito na watoto wachanga wamekadiria kuwa, iwapo wanawake wote wa Tanzania wangepata huduma za wakunga wenye ujuzi, basi maisha ya akinamama wapatao 5,000 na vichanga 32,000 yangeweza kuokolewa ifikapo 2015. 

Akiongea kwa niaba ya kampeni ya Mama Ye! Craig Ferla amesema: “Ni vyema kabisa kuwaenzi wakunga wetu katika Siku ya Wakunga Duniani. Tunapongeza ahadi za serikali kuitilia mkazo sera ya huduma za afya ya uzazi kuwa bure, lakini mengi bado yanahitaji kufanyika ili kuongeza idadi ya wahudumu wa afya.”

 Takwimu zilizochapishwa na ripoti ya Hali ya Wakunga Ulimwenguni (State of the World’s Midwives) zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji wakunga 9,941 zaidi ili kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 la kuwa na asilimia 95% ya wajawazito wanaozalishwa na wahudumu wenye taaluma. 

Craig Ferla ameongeza kuwa: “Tunawaalika na kuwahimiza Watanzania kutoa shukrani kwa wakunga – na kusaidia kuwapa moyo vijana nao waamue kuwa wakunga siku za baadae. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia ‘Twitter’ ukiwaambia asante kwa kujituma kazini, pia waweza kuweka picha kwenye ukurasa wetu wa ‘Facebook’ zinzazowaunga mkono wakunga wetu wa Tanzania pamoja na mathalan kutambua juhudi kubwa za mkunga unayemthamini kwa kazi zake kubwa katika jamii yako.”

 Ukitaka kufahamu zaidi kuhusiana na hali ya wakunga nchini Tanzania, tembelea tovuti ya www.mamaye.or.tz/sw ambapo utapata ushahidi uliowekwa kwa namna rahisi kuelewa, habari kuhusu mashujaa katika uzazi salama, ahadi zilizowekwa na serikali na hatua mbali mbali unazoweza kuchukua web: www.mamaye.or.tztwitter: @MamaYeTZfacebook: facebook.com/MamaYeTZ 

MamaYe! 164C Msasani Beach, Kinondoni, P.O. Box 13731, Dar es Salaam, Tanzania Phone: +255 (0) 754 588 233 ili kufanikisha kampeni hii muhimu. Ipaze sauti yako isikike na toa madai ya msingi zaidi, jiunge na kampeni ya Mama Ye!

pako safi kwa ajili yako,changamka.

TASWA yapokea mapendekezo ya majina ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuwania tuzo za mchezo.

$
0
0
KAMATI ya kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012 zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imepokea mapendekezo ya majina ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuwania tuzo hizo kwa kila mchezo.

Majina ya wanamichezo hao yamependekezwa na vyama husika, isipokuwa mpira wa miguu kwa wanaume pamoja na mpira wa kikapu, ambapo majina yameteuliwa na kamati kwa kushirikiana na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na wadau wa michezo husika, ingawa awali vyama hivyo viliombwa kuwasilisha majina lakini havikutekeleza ombi hilo hivyo kamati ikaamua kutafuta utaratibu mwingine wa kupata majina.

Pia vyama viwili vya michezo ya  paralimpiki na baiskeli bado majina hayajaifikia kamati yetu kutokana na sababu mbalimbali na tayari wameahidi watawasilisha majina hayo kabla ya Mei 12 mwaka huu. Chama cha Mpira wa Wavu pia kimeshindwa kuwasilisha majina.

Hatua ya mwisho ambayo itafanyika baada ya kupokea mapendekezo hayo kwenye kila mchezo, Kamati ya Tuzo za Taswa itafanya uchambuzi kupitisha majina hayo kulingana na sifa ambazo vyama husika vimeleta kwa kila mwanamichezo na kuona kama wanastahili kupewa tuzo kulingana na vigezo vya kamati na TASWA.

Awali TASWA ilipanga tuzo hizo zifanyike Aprili 27 mwaka huu, lakini imeshindikana kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kamati ya Tuzo pamoja na chama kwa ujumla na sasa sherehe zitafanyika mwanzoni mwa mwezi Juni katika tarehe itakayotangazwa baada ya kukubaliana na wadhamini, ambapo mazungumzo yanatarajiwa kukamilika kabla ya Mei 15 mwaka huu.

Tunavishukuru vyama vyote vilivyotupa ushirikiano kwa hatua ya awali kwa kutupatia mapendekezo yao pamoja na kutaja sifa kwa kila mchezaji waliyewasilisha jina lake nasi tunaahidi tutapitia kwa umakini mapendekezo hayo, lakini uamuzi wa kamati ndiyo utakaokuwa wa mwisho.

TASWA itatoa tuzo kwa kila mchezo ambao kamati yetu ambayo  Katibu wake ndiye pia Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando itajiridhisha wanastahili, ambapo baadaye washindi wa kila mchezo watawania Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa Mwaka 2012.Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011 ilienda kwa Shomari Kapombe. Washindi wengine kwa miaka ya karibuni ni Mwanaidi Hassan (2010 na 2009), Mary Naali (2008), Martin Sulle (2007) na Samson Ramadhan (2006).
 
Majina ya wanaowania kwa mwaka 2012:

MPIRA WA MAGONGO-WANAUME
Sylvester Kigodi
2.   Casto Mayuma
3.   Gurtej Bilu Singh
4.   Vendri Bhamra
5. Elias Samala

Gofu ya Kulipwa 
1 Hassani Kadio 
   2 Yassin Salehe
  3 Fadhili Nkya
  4 Salimu Mwanyenza
  5 Rajabu Iddy

GOFU YA RIDHAA WANAWAKE:

1:MADINA IDDI
2:ANGEL EATON
3. HAWA WANYECHE
4.AYNE MAGOMBE

GOFU YA RIDHAA WANAUME
Jimmy Mollel
Frank Roman
Nuru Mollel
Martin MacDonald
John Said


NGUMI ZA RIDHAA-WANAUME
  1. Ismail Isack Galiatano
  2. Said Hofu
  3. Selemani Kidunda.
  4. Victor Njaiti
  5. Mohamed Chibumbui.

NGUMI ZA RIDHAA WANAWAKE:-
1.   Sara Andrew
2.   Irene Kimaro
3.   Easter Kimbe.
4.   Mather George
5.   Mariam Nyerere.

Ngumi za Kulipwa
1.      Francis Miyeyusho
2.     Ramadhan Shauri
3.     Thomas Mashali
4.     Said Mbelwa
5.     Francis Cheka


JUDO-TANZANIA BARA-WANAUME

1)     AHMED MAGOGO
2)    ADREW THOMAS MLUGU
3)    GEOPHREY EDWARD MTAWA
4)    GERVAS LEONARD CHILIPWELI
5)    ABUU SELEMANI MCHETEKO
6)   ABUUBAKAR NZIGE

JUDO TANZANIA BARA WANAWAKE
                             
1.     MATRIDA .H. TEMBA
2.     AMINA MOHAMED

JUDO ZANZIBAR-WANAUME
1.    MOHAMMED KHAMIS JUMA
2.   MASOUD AMOUR KOMBO
3.   MBAROUK SULEIMANI SULEIMAN

JUDO ZANZIBAR-WANAWAKE
1.     GRACE ALPHONCE
2.     LAYLATI MOHAMMED

TENISI-WANAWAKE
 [1] Rehema Athumani
[2] Vailety Petar
 [3] Mkunde iddi
 [4] Edna John
 [5] Zuhura Baraka

TENISI  Wanaume
 [1] Omary Abdalah
 [2] Yassini Shabani
 [3] Hassan Kasimu
 [4] Kiango Kipingu
 [5] Lebric Jacobu

MPIRA WA MIKONO-WANAUME
Faraji Shaibu
Nyuki ZANZIBAR
Hemedi Salehe
JKT
Abinery  Kusena
JKT
Ally Khamis
Ngome
Hassani  Yusufu
Magereza

MPIRA WA MIKONO-WANAWAKE
Catherine    Mapua
Ngome
Dorisi        Mangara
Magereza
Zakia        Mohamed
Ngome
Happy      Mahinya
JKT
Mary       Kimiti
Magereza

RIADHA-WANAWAKE
1.Zakia Mrisho
2. Mary Naali
 3.Jacklin Sakilu
4.Sarah Ramadhani
 5.Anjelin Tsere
6. Sara Maja

RIADHA-WANAUME
1. Dickson Marwa
 2. Faustine Musa
3. Augstino Sule
4. Bazil John
5. Samson Ramadhan

KRIKETI-WANAUME
1.   Abhik Patwa.
2.     Benson Mwita.
3.     Sefu Khalifa.
4.     Issa Kikasi.
5.   Riziki Kiseto
KRIKETI-WANAWAKE
Monica Pascal.
Mwanaiddi Ibrahim.
Hadija Nasibu
Esther Wales
Mwanaidi Ammy

SOKA-WANAWAKE
FATUMA MUSTAPHA
ASHA RASHID
MWANAHAMISI OMARY
SOPHIA MWASIKILI
ESTER CHABRUMA

SOKA-WANAUME
JOHN BOCCO-AZAM
KELVIN YONDANI-YANGA
SHOMARI KAPOMBE-SIMBA
MCHA KHAMISI-AZAM
MBWANA SAMATTA-TP MAZEMBE
Thomas Ulimwengu-TP Mazembe

WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
EMMANUEL OKWI-SIMBA(SASA ETOILE DU SAHEL)-SOKA
KIPRE TCHETCHE-AZAM-SOKA
HARUNA NIYONZIMA-YANGA-SOKA
HAMISI KIIZA-YANGA-SOKA
MARY WAYA-FILBERT BAYI –NETIBOLI (ALIKUWA KOCHA MCHEZAJI)

KIKAPU-WANAWAKE
Faraja Malaki- Jeshi
Evodia Kazinja-JKT Stars
            Sajida Ahmed-Don Bosco
           Rehema Kilomba-Donbosco
        Tukusubira David-Vijana Queens

KIKAPU-WANAUME
Mussa Chacha-Savio
Lusajo Samuel Mwakipunda-Oilers
Salim Mchemba-ABC
Filbert Mwaipungu-ABC
Steven Atanasio-ABC

NETIBOLI
Lilian Sylidion-Filbert Bayi
Mwanaidi Hassan-JKT
Irene Elias Kanile-Filbert Bayi
Jacqueline Sikozi-Filbert Bayi
Faraja Malaki-Jeshi Stars

WACHEZAJI BORA CHIPUKIZI

Salum Abubakari-Azam-soka
Frank Domayo-Yanga-soka
Edward Cristopher-Simba-soka
Emmanuel Malya-Tenisi Gymkhana Arusha
Tambwe Juma-Kriketi


WATANZANIA WANAOCHEZA NJE

Mbwana Samatta-TP Mazembe
Ivo Mapunda-Gor Mahia
Hasheem Thabeet-Oklahoma
Thomas Ulimwengu-TP Mazembe
Soud Abdulrazak-Uganda (kikapu)
Mohammed Abdallah ‘dulah’-Uganda (kikapu)

TUZO YA HESHIMA--- ITATANGAZWA UKUMBINI
TUZO YA MWANAMICHEZO BORA MWAKA 2012- ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA MCHEZO

Imetolewa na
Haji Manara
Mwenyekiti Kamati ya Tuzo TASWA
05/05/2013


Bendi ya Mashujaa kuwasindikiza Redds Miss Kibaha 2013

$
0
0
BENDI ya Mashujaa imetangazwa kutoa burudani katika shindano la Redds Miss Kibaha 2013 shindano lililopangwa kufanyika Mei 17 katika ukumbi wa Container Mailimoja Kibaha.
Kwa mujibu wa taarifa  kwa vyombo vya habari  iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) Khadija Kalili ilisema kwamba tayari wamemalizana na uongozi wa  bendi ya Mashujaa  hivyo ndiyo burudani itakayorindima na kuwasindikiza wanyange wa  Redds Miss Kibaha.
“Uteuzi wa bendi ya mashujaa umekuja baada ya kufanya utafiti wa kina juu ya burudani ambayo itakidhi kiu kwa wakaazi wa Kibaha na Mkoa wa Pwani  kwa ujumla hivyo kura nyingi likwenda kwa bendi ya Mashujaa naamini siku hiyo mabo yatakuwa bambam” alisema Kalili.
Kalili aliendelea kwa kusema kuwa naifahamu vema bendi ya Mashujaa ambayo inaongozwa na mwanamuziki nyota nchini Charles Mbwana ‘ Charlz Baba , Kingunge’ , pia wamo waimbaji wenye sauti tamu kama Jado FFU, Marapa machacharikama 33, Fagurson na wengineo wengi.
Akizungumzia kwa upande wa maandalizi Kalili alisema kuwa yanaendelea vizuri huku LIMSO wakijipanga kuingia kambini  na warembo ambako watakaa kwa siku chache kabla ya shindano.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chache cha Redds Premium Cold, Maji Umoja, Shear Illusions, Fredito Entertainment, CXC Africa, Multichoice DSTV,Clouds FM , Times FM Michuzi Media Group (MMG),Mikopo Finance,Santorine ,PR.Promotion, Chicago General Company, Image Pub na wadhamini kutoka Kibaha ni  Mama Koka , Amazon Night Club, Panandipanandi Pub na Santorine Holiday Resort  iliyopo Kiluvya.

Mvua ya Dar es Salaam na Tambarare yetu Tanzania

$
0
0


Hapa ni eneo la millenium tower makumbusho, mvua kubwa ilioyensha usiku wa leo na leo asubuhi imepelekea kuwepo kwa maji mengi eneo hili hadi kupelekea magari yaendayo posta kupitia pakinng ya magari ya eneo hili au ya jengo hili la millenium tower  na kusababisha msongamano wa magari toka asubuhi hadi sasa, na hata mabar  ya pembezoni mwa sehemu hii na grosari zote zimelazimika kufunga kwa muda hata maduka kutokana na maji mengi kuingia sehemu zao za biashara. 

hii ni mara kwa mara mvua inapokuwa kubwa tatizo hili kutokea na hatari zaidi kwa njia ya kuelekea mwenge kutoka moroco kuna mtaro ambao umefunikwa na maji hivi nawaasa wenye magari wasitanue eneeo hilo kwa mitaro haionekani na ni mikubwa hivi madereva wawe makini sana wafikapo eneo hili.

Picha na Mc Kessy.

live kutoka makete ndani ya njombe.

$
0
0
 Hii hali nimekutana nayo ghafla wakati naenda kanisani asubuhi, hali ndivyo ilivyo katika kijiji cha Ujuni wilayani makete baada ya fuso hiyo kukwama kutokana na ubovu wa barabara eneo hili, jitihada za kuitoa fuso hiyo zilikuwa zinaendelea hadi naondoka hali ilikuwa bado tete, fuzo ilikuwa imekwama. Picha kwa hisani ya Edwin Moshi.


RAIS KIKWETE AANZA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI NCHINI KUWAIT LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakipokea mashada ya mauwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakiingia sehemu ya mapokezi na kukagua gwaride rasmi mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.

Nishani Kanda ya Kati Tabora

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Mara Baada ya kuwavisha nishani mbalimbali za Utumishi Leo katika viwanja vya Magereza Mkoa wa Singida. Jumna ya Maafisa na Askari 40 kutoka Mikoa ya Kigoma, Tabora, Dodoma na Singida wamevishwa nishani mbalimbali(kushoto) ni Mkuu wa Wilaya Singida na wa kwanza kulia Ni Mkuu wa Wilaya Kiomboi.


HALI ILIVYOKUWA JIJINI ARUSHA MARA BAADA YA MLIPUKO MKUBWA BOMU LEO.

$
0
0
Mungu uwe upande wetu
Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mara tu baada ya tukio hilo
eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....Eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu  kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....


Na Ahmed mahmoud wa Globu ya Jamii, Arusha

MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmoja yu  mahututi na wengine zaidi ya 49  wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka kitu kinachosadikiwa ni bomu majira ya saa  4 asubuhi leo  wakati wa sherehe za ufunguzi  wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.

Ufunguzi wa kanisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisco  Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat  Lebulu,  na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.

Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za  maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina  Fredirik, Joram  kisera, Novelt  John, Rose  pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt  John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .

Wengine ni Rioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim 

Mkuu wa mkoa wa  Arusha, Magesa Mulongo ,  ameagiza vyombo vya ulinzi na  usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.

Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
Picha kwa hisani kubwa ya  

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA GHALA LA MSD DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizundua bohari ya madawa ya MSD mjini Dodoma Mei 5,2013.Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif RashidWatatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Madawa (MSD), Cosmas Mwaifani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe wakati alipozindua bohari ya kuhidi madwa ya MSD, eneol la Kizota mjini Dodoma Mei 5,2013.Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid na Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Malima Lubeleje.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Madawa (MSD), Cosmas Mwaifani (wapili kulia) wakati alipozinduaghala la kuhifadhia madawa katika Kanda ya Kati la MSD mjini Dodoma Mei 5, 2013. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya, Dr. Seif Rashid.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua madawa yaliyohifadhiwa kwenye boahari ya MSD ya Kanda ya Kati eneo la Kizot mjini Dodoma baada ya kuzindua bohari hiyo Mei 5,2013. Wapili Kulia ni Naibu Waziei wa Afya, Dkt.Seif Rashid , Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Malima Lubeleje na wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MICHUANO YA ESTHER BULAYA YAMALIZIKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA WILAYANI BUNDA

$
0
0


Michuano ya Kombe la Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Vijana Mkoani Mara Esther Bulaya linalojulikana kama Esther Bulaya Cup imemalizika wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo Timu  inayoundwa na Wadau wa Elimu wilayani humo Elimu Fc ikiibuka Bingwa wa Mashindano hayo kwa Mwaka 2013.
 
Michuano hiyo ambayo ilikutanisha timu zaidi ya 30 kutoka wilayani  Bunda ilimaliza kwa kuzikutanisha timu za Bunda Sport Club na Elimu Fc, ambapo iliibuka bingwa wa Kombe hilo kwa Mwaka 2013 kwa  Mikwaju ya Penati 3-1 baada ya kufungana bao 1-1 ndani ya dk 90 na kujinyakulia kitita cha Shilingi milioni moja pamoja na Kombe.
 
Mshindi wa Pili alipata zawadi ya Shilingi laki Tano huku mshindi wa tatu timu ya Town Star ambayo iliifunga timu Majengo Fc bao 1-0 ilipata kiasi cha Shilingi laki 3 na Seti ya Jezi ,ambapo baada fainal hizo Mbunge Esther Bulaya alikuwa na haya ya kunena.
 
Akiongea wakati wa kukabidhi Zawadi mbalimbali wa Washindi,Mbunge Esther Bulaya alisema kuwa kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanapanga  Mikakati ya kuhujumu Mashindano hayo yasifanyike Mbunge ambapo alisema kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki Vijana wa Bunda ambao ndiyo walengwa wa Michuano hiyo.
 
Mh Bulaya aliahidi kuendelea kudhamini Michuano hiyo Mpaka Mwisho wa Ubunge wake na kuongeza kuwa kama atafanikiwa tena kuwepo katika hiyo nafasi ataendelea kufanya Michuano hiyo mpaka kufa kwake.
“Mimi nashangaa sana kuna baadhi ya watu wanataka kuhujumu 
 
Mashindano haya kitu ambacho hawatawatendea haki vijana wa Bunda maana ndiyo walengwa,napenda kuwaahidi Vijana wenzangu nitaendelea kudhamini mpaka mwisho wa ubunge wangu na kama nitaendelea kuwepo kwenye hii nafasi nitayadhamini Mpaka kufa Kwangu”alisema Bulaya.

Aidha baadhi ya Wadau wa Michezo wilayani humo walimpongeza Mbunge huyo na kusema kuwa Michuano hiyo inajenga uzalendo wa Vijana wa Bunda huku wakimuomba kuiendeleza Michezo hiyo kwani imeonyesha Mafanikio Makubwa tangu kuanzishwa kwake.
 
Walisema wilaya ya Bunda ni mmoja ya wilaya Mkoani Mara ambayo iilikuwa nyuma katika suala la Michezo lakini kwa Muda Mfupi sasa wilaya hiyo imeonekana kuwa kinala.
 
 “Unajua hii wilaya ilikuwa nyuma sana Kimichezo lakini tangu huyu Mbunge ameanzisha haya Mashindano sasa hivi Bunda inaongoza kwa Michezo hasa Soka maana hata bingwa wa Mkoa na Makamu wake wanatoka Bunda sasa hayo si Mafanikio”? alisema Juma Mbano. 
Michuano ya Esther Bulaya Cup 2013 iliunganisha Michezo mbalimbali ikiwemo  Michezo ya bao,draft pamoja na Pool table,ambapo Michuano hiyo ni ya Tatu kufanyika na kila Mwaka imekuwa na Mabadiliko Makubwa . Habari picha akwa hisani ya Augustine Mgendi,Bunda.


TAMKO LA RAIS JUU YA TUKIO LA ARUSHA

MUHAS yaaswa kujenga uwezo wa kufanya tafiti

$
0
0
 Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano hilo lililofungwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS), Profesa Fredy Mhalu akizungumza wakati wa ufungaji wa Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 Kaimu Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando, akizungumza wakati wa ufungaji wa Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha na mpiga picha wetu
Washiriki Kongamano la Kwanza la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS) katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kongamano hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

=======  ======  ========

MUHAS yaaswa kujenga uwezo wa kufanya tafiti 

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili (MUHAS) kimeaswa kuzidi kujenga uwezo wa ufanyaji tafiti mbali mbali zinazohusiana na masuala ya afya ili kuimarisha huduma ya afya nchini.

Akizungumza wakati wa sherehe za kufunga kongamano la Kwanza la Sayansi lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Mganga Mkuu, Dk Donan Mmbando, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, alisema kuwa ili kuboresha huduma za afya nchini kuna haja ya watafiti na wataalamu kuendelea kutafuta njia za kuimarisha huduma hiyo licha ya changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta hiyo.

"Utaalamu katika kutafuta njia za kuboresha huduma za afya ni muhimu kwa watanzania wote. Nawasihi kuendelea kufanya tafiti lakini pia kuyatumia matokeo haya ya kitafiti kikamilifu ili kusaidia serikali kuboresha huduma ya afya kwa wananchi, "alisema Dk Mmbando.

Alibainisha kuwa ili kuboresha ,masuala ya afya wafanyakazi katika sekta hiyo wanahitaji kupewa mwanga zaidi kuhusiana na masuala ya afya na kupitia makongamano watapata elimu zaidi juu ya jinsi gani wanaweza boresha utoaji wa huduma za afya na kuleta ufanisi katika kazi yao.

"Tunahitaji kuendelea kukuza maarifa kwa kuendelea kuandaa makongamano ya aina hii zaidi hususani ya tafiti za masuala ya kisayansi na afya kwa kuwa yanatoa fursa za kubadilishana uzoefu na kutafuta mbinu mbali mbali za kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya afya.

"Makongamano ya kisayansi kama hili tunalofunga leo hii utoa fursa nzuri katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto nyingi za afya hususani jinsi gani ya kukabiliana na magonjwa kama malaria na vvu/ukimwi," aliongeza

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo hicho, Profesa Efata Kaaya aliipongeza serikali kwa kukiunga mkono chuo hicho hususani katika utoaji wa fedha ili kusaidia kufanikisha tafiti mbali mbali za kisayansi na kiafya zinazofanywa na chuo hicho nchini.

“Naishukuru serikali kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kipindi kirefu katika tafiti zetu hususani katika utoaji wa fedha ili kufanikisha tafiti hizi. Naimani kutokana na mchango huo, wataalam wetu wataendelea kutafuta mbinu jinsi ya kuboresha huduma za afya nchini,” alisema Profesa Kaaya.  
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images