Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Waziri Ummy apokea vifaa katika wodi ya Afya ya Uzazi ya Mama na Mtoto Muhimbili

$
0
0
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akipokea vifaa kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa yaTaifa Lauren Rugambwa Bwanakunu vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya Muhimbili Prof Lawerence Mseru na nayefata ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Mpoki Ulisubisya .

Na Raymond Mushumbusi  MAELEZO

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu amepokea vifaa vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya  Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni agizo la Mhe.Rais alililolitoa mapema mwishoni wa wiki iliyopita katika kuhakikisha kuwa wakinamama wanaojifungua hawalali chini.

Akipokea vifaa hivyo  Mhe. Ummy Mwalimu amesema anamshukuru sana Mhe Rais kwa kuona changamoto hii ya wakina mama kulala chini wakati wakitoka kujifungua na kumuahidi Mhe. Rais kusilimamia vyema suala hilo na kuwaagiza wakurugenzi husika kumpa taarifa ya kuhusu vitanda na magodoro katika Hospitali zote zilizo chini ya wizara yake.

“ Kuanzia sasa sitolala na natuma salamu kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa fursa hii ni wajibu wao kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya afaya hasa katika vifaa hususan vitanda na magodoro ili kupunguza tatizo hili la wagonjwa katika Hospitali zetu kulala chini wakati tuna uwezo wa kupata vitanda na magodoro”

‘”Mhe.Rais amenifundisha na ametufundisha sote kwamba  kutatua jambo sio mpaka mkae vikao au semina ili kujadili  ila inawezekana kama mkiweka nia ya kulifanya jambo hilo na kuachana na zile kauli za tunalifanyia kazi, tupo katika michakato na kauli kama hizo zisizotatua tatizo kwa wakati unaotakiwa”alisema Ummy.

Bohari ya Dawa ya Taifa imekabidhi jumla ya vitanda 120, Magodoro 120, Mashuka 480, vitanda vya kuzalishia 10,vitanda 10 vya kulaza watoto ambao hawajatimia Njiti  na jumla ya vifaa vyote vina thamani ya shilling Million 100.

Uaandaaji wa wodi hiyo ya akimama wanaojifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umekuja baada ya agizo la Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa hivi karibuni alipokuwa akiongea na wazee wa Mkoa wa Dar es Salam na kutoa siku mbili kwa wizara Ya Afya kuhamisha ofisi zilizokuwepo za kitengo Afya ya uzazi ya  Mama na Mtoto na kuifanya kuwa wodi ya akina mama ili kupunguza tatizo la kulala chini kwa akina mama wanaotoka kujifungua.

WAKURUGENZI WANNE WA MSD WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA

$
0
0


Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu amewasimamisha wakurugenzi toka Bohari ya Dawa ya Taifa(MSD) kwa ubadhilifu wa fedha takribani Shillingi Billion 1.5.
 
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto baada ya kupokea  vifaa toka Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD) amesema amepata taarifa ya uchunguzi ofisini kwake ya ubadhilifu wa kiasi hicho cha fedha na kuamua kuwasimamisha wakurugenzi wanne kupisha uchunguzi.
 
“ Nimeletewa taarifa ofisini kwangu na nimeamua kuchukua fursa hii kuwaambia na hili pia kwamba nimewasimamisha wakurugenzi wanne toka Bohari ya Kuu Dawa ya Taifa kwa ubadhilifu wa fedha na nisingeweza kusubiri nitumbuliwe mimi jipu na Mhe.Rais kwahiyo  nimeamua kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi”
 
“ Hizi ni zama za kufanya kazi na kuwajibika sasa inabidi tuwajibike kwa kufanya kazi na hatutowavumilia watendaji watakaoenda kinyume na utaratibu katika ofisi yoyote ile katika sekta ya afya na tutawachukulia hatua kwani tunataka uwajibikaji ili kuiendeleza sekta ya afya ambayo  ni muhimu sana kwa kila mwanadamu” Alisema Ummy.
 
Amewataja aliowasimamisha kazi kuwa ni Joseph Tesha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Misanga Muja Mkurugenzi wa Ugavi, Heri Mchunga Mkurugenzi wa Manunuzi na Cosmas Mwaifani Mkurugenzi Kanda na Huduma kwa Wateja ambapo amewataka Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya Dawa ya Taifa kuwaandikia barua mara moja ya kuwasimamisha kazi.
 
Katika kuboresha sekta ya afya nchini Wizara wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee imejipanga kufanya kazi  kwa taratibu na misingi iliyopo ili kuhakikisha inapeleka mbele gurudumu la maendeleo ya hasa katika sekta ya afya kwa ujumla.

OFISI YA WADOKI SACCOS NA HOTEL YA KIRUMBA RESORT ZA MKOANI MWANZA ZAFUNGWA NA WANACHAMA WA CCM.

$
0
0
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, leo wamefunga Ofisi ya Taasisi ya Mikopo ya WADOKI (Wadoki Saccos) pamoja na Hotel ya KIRUMBA RESORT kutokana na watajwa kushindwa kulipia kodi ya pango.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid (anaeongea pichani) amesema kuwa wanachama hao wamefikia maamuzi hayo kutokana na kutumia majengo ya CCM katika kata hiyo huku wakiwa hawalipii kodi.

Wanachama wa CCM katika Kata hiyo ya Kirumba wamesema kuwa, maamuzi yao yatatoa fundisho kwa wawekezaji wengine wanaotumia vitega uchumi vya Chama hicho katika maendeo mbalimbali nchini huku wakiwa hawalipii kodi ambapo wametahadharisha kwamba wale wote wenye hulka hiyo wajiandae kutumbuliwa (kuondolewa katika majengo hayo).

Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Juma Wesa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi, wamesema kuwa maamuzi yaliyochukuliwa na wanachama hayo ni sahihi kwa kuwa malalamiko ya wawekezaji hao yaliishajadiliwa hadi ngazi za juu na kuonekana kwamba wawekezaji hao hawatii makubaliano yao ikiwemo kulipa kodi ya pango kwa wakati.

Meneja wa Kirumba Resort hakutaka kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba mzungumzaji ni Mkurugenzi ambae alidai amesafiri huku Uongozi wa Wadoki Saccos ukishindwa kupatikana.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid akitoa kwa wanaccm baada ya wanachama hao kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Acheni Maulidi akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo.

Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Wesa Juma, akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Jane Masso ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Kirumba (kulia) amesema wanachama watahakikisha vitega uchumi vya chama vinatumika vyema kwa ajili ya maendeleo yao.
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Ofisi ya Wadoki Saccos Kirumba baada ya kuwekewa kama ishara ya kufungwa
Ulinzi wa Askari wa Kutuliza ghasia ulikuwepo ili kuhakikisha hakuna uhalibifu wowote ambao ungeweza kufanyika ambapo suala hilo limefikishwa Kituo cha Polisi Kirumba na kila upande unawasilisha vielelezo vyake ili kutambua wanaokiuka makubaliano ya mkataba wa upangaji.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA BODI YA CHUO CHA UHAMIAJI CHA KIKANDA (TRITA) MJINI MOSHI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. Katika hotuba yake Rwegasira aliitaka Bodi hiyo ifanye kazi kwa ushirikiano kwa maendeleo ya chuo. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika mjini Moshi. Watatu kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano.na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma.
 Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Erasmi Francis akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) na wajumbe wa Bodi ya Chuo hicho, kamera inayotumika kuchukua kumbukumbu za usalama kwa ajili ya watu wanaopita katika mipaka ya nchi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Watatu kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Kinemo Kihomano (Wasita kushoto). 

Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Zawad Chazuka akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) albamu yenye hati za kusafiria za mataifa mbalimbali duniani, albamu hiyo inaonyesha alama za kiusalama ambazo zipo katika pasipoti za mataifa mbalimbali. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
 Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Zawad Chazuka akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) albamu yenye hati za kusafiria za mataifa mbalimbali duniani, albamu hiyo inaonyesha alama za kiusalama ambazo zipo katika pasipoti za mataifa mbalimbali. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, wakati alipokuwa anawasili katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi kwa ajili ya kuzindua Bodi ya Chuo hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua maeneo mbalimbali ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. (kushoto) mara baada ya kuzindua Bodi ya Chuo hicho. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa), Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuzindua Bodi hiyo mjini Moshi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

WAKAZI WA KAHAMA,GEITA NA MWANZA WAKAE MKAO WA KULA TAMASHA LA PASAKA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha la Pasaka,Bwa Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Ofisini kwake kuhusiana na tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Kahama,Geita na Mwanza.Msama amewataka wapenzi wa tamasha hilo wajitokeze kwa wingi na kupokea neno la Mungu kupitia waimbaji hao.Tamasha hilo mwaka huu linatimiza miaka 16 tangu lianzishwe hivyo linatarajia kuwa tofauti na miaka ya nyuma.

WAIMBAJI nyota wa nyimbo za Injili Faustine Munishi anayeshi Nairobi, Kenya na Jesca Honore ‘BM’ wamethibitisha kupamba jukwaa la tamasha la paska litakaloanza kufanyika Machi 26 Mkoa wa Geita.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama, alisema kuwa waimbaji hao wametihitisha kuimba siku hiyo, ambako bado kamati hiyo itaendelea kutaja waimbaji wengine wakubwa kwani bado iko kwenye mazungumzo nao.
Msama alisema kamati yake inaendelea kuchagua waimbaji watakaoimba katika mikoa wa Mwanza Machi 28, wilaya ya Kahama Machi 27 na Geita kwakuwa waimbaji ni wengi wanaomba kuimba katika tamasha hilo la kimataifa.

Msama ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama promotions, amesema kwakuwa kamati hiyo kwa mwaka huu inatoa nafasi kubwa kwa waimbaji wa ndani amboa ndio wengi walioomba wanaangalia namna ya kukubaliana hivyo huenda kukawa na waimbaji wengi zaidi katika tamasha hili la kuliko yaliyowahi kufanyika mikoani.

Amesema Munishi ni mwimbaji wa kwanza aliethibitisha kutoka nje ya Tanzania huku akisistiza kuwa huenda wakamalizia na wengine kutoka Afrika kusini na nchi nyinginezo za Afrika. Msama ilieleza kuwa kamati yake imeamua kumleta Munishi kutokana na maombi ya wadau mbalimbali wa muziki wa injili hapa nchini .

“Naomba niwafahamishe mashabiki wa muziki wa Injili kwamba tumekubali maoni yao, sasa wajipange kumpokea Munishi na atatumbuiza Mwanza, Kahama na Geita wakae mkao wa kupokea neno la mungu kupitia mtumishi wa Mungu” amesema Msama'“Kama mnavyojua mwaka huu tunatimiza miaka 16 tangu tuanze Tamasha la Pasaka, hivyo tunaleta kitu tofauti kabisa,” alisema Msama na kuongeza kuwa hivi sasa Munishi pia ni mhubiri wa neno la mungu..

Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu Munishi ni pamoja na Malebo, Siasa na Injili, Paka Kulia Usiku, Kuhubiri ni Taalum, Jirani, Jirani Mchokozi, Fasheni ni Yesu, Nimeamua Mwenyewe na Maji Yana Mdudu.Kwa mujibu wa Msama hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti kubwa ukilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.
Msama alimalizia kusema licha ya kuja mwimbaji wa ndani Jesca BM ambaye anatamba na baadhi ya nyimbo kama ‘Napokea’, Nakuabudu na Nimezima Ukimya,’ waimbaji wengine waliothibitisha ni pamoja na Rose Muhando na Bonny Mwaitege.

NDANI YA TAKUKURU KUNA ‘MAJIPU’ –KAIRUKI.

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na viongozi wa TAKUKURU katika mkutano wa kazi na viongozi hao uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akimsikiliza kwa umakini.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akifungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.
aziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wakaguzi wa kanda wa TAKUKURU mara baada ya kufungua mkutano wa kazi wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika makuu ya ofisi hiyo mapema leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Nchi, Ofisi Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki  amesema kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ina baadhi ya watendaji wametumia nafasi zao vibaya na kufanya chombo hicho kukosa uaminifu  hivyo na kufanya chombo hicho kuwa na ‘majipu’ ambayo yanatakiwa kupasuliwa.
Angela ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa utendaji kazi wa Takukuru uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema  chombo hicho ni muhimu lakini kuna baadhi wametumia nafasi zao vibaya katika kufanya kazi na taarifa anazo hivyo atashughulikia ikiwemo na kuandika kiapo cha mali zao na kama walifanya warudie kujiridhisha.
 Amesema kuwa Takukuru inatakiwa kufika wilayani na mikoani kutokana na fedha nyingi za miradi ya serikali zinakwenda huko ambapo ameutaja mkoa wa Kilimanjaro  unawatendaji ambao wametumia madaraka vibaya wa ubadhirifu wa fedha za serikali hivyo Takukuru lazima ichukue hatua dhidi yao.
Amesema kuwa ikitokea kuwepo na  kutowajibika kwa chombo hicho serikali iamweza kuwandoa wote kutokana na kuwepo kwa watu wenye sifa wa kufanya kazi hiyo.
Aliongeza kuwa katika Takukuru inatakiwa kujiridhisha na uchunguzi na  sio kuwa idadi nyingi za kesi ambazo mwisho wa siku kesi hizo wanashindwa kutokana kuushindwa  kuwa na uchunguzi wenye ushahidi.
Aidha amesema kuwa baadhi ya mahakimu watakosa kazi kutokana na baadhi ya kesi wameendesha kwa kupindisha na kuwapa  washitakiwa haki wasio kuwa nayo.

Waziri Angela amesemaTakukuru wafanye kazi kwa waadilifu kwa kuwalinda watoa taarifa ili waendelee kutoa taarifa kwa watu wanaojua kuwa wanahujumu nchi kwa kutumia madaraka yao.
Amesema watumishi wa Takukuru wana masilahi mazuri kuliko wa wafanye kazi wengine ikiwa ni kuwaondoa katika ushawishi wa kuwa na tama kutokana unyeti wa chombo hicho.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishina (CP), Valentino Mlowola amesema wameokoa sh. Bilioni Saba (7) ambazo zilikuwa ziingie kwenye mifuko ya wabadhirifu wachache ambao wanatumia nafasi zao vibaya kwa masilahi yao.
Amesema walipokea malalamiko 4,675, uchunguzi uliokamilika wa majalada hayo ni 667, majalada yaliyokwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), ni  278,   majarada yaliyorejeshwa na DPP, ni 172 kwa ajili ya  vibali vya kufungua mashitaka  na kesi mpya 314 nchini kote, na kesi zilizoshinda 132 ambao wamefungwa na wengine kulipa faini.

KAMPUNI YA RAM NUCLEAR KUTOKA SENNINGERBERG YAONESHA NIA YA KUWEKEZA KWENYE UMEME WA URANIUM

$
0
0
Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake Senningerberg, Bastian Ringsdorf (mbele wa kwanza kulia) akielezea uzoefu wa kampuni hiyo katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia madini ya urani katika kikao chake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake Senningerberg, Bastian Ringsdorf (hayupo pichani) katika kikao chake na kampuni hiyo pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.
Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake Senningerberg, Bastian Ringsdorf akifafanua jambo katika kikao hicho.
Baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Mkuu kutoka Kampuni ya Ram Nuclear yenye makazi yake Senningerberg, Bastian Ringsdorf (hayupo pichani)

Airtel yainua kikundi cha vijana wajasiriamali kupitia Airtel Fursa jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia), akikabidhi funguo ya pikipiki aina ya guta kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Akilimali Fatuma Rashidi, ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kutengenezea sabuni, walivyowakabidhi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, waliopo kigamboni jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni wanakikundi wa Akilimali wapatao vijana 12.
Mwakili wa kikundi cha Akilimali Fatuma Rashidi kilichopo kigamboni jijini Dar Es Salaam wanaojishughulisha na kutengeneza sabuni, akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa pikipiki ya magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli hiyo, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara kigamboni jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki hii.
 Mwakili wa kikundi cha Akilimali Fatuma Rashidi kilichopo kigamboni jijini Dar Es Salaam wanaojishughulisha na kutengeneza sabuni, akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia), msaada wa pikipiki ya magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli hiyo, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara kigamboni jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni wanakikundi wa Akilimali wapatao vijana 12.

· Airtel Fursa imewapatia pikipiki aina ya Guta, vifaa vya kutengenezea sabuni na vitendea kazi kwa vijana hapa nchini

Akili Mali ni kikundi cha vijana wajasiriamali 12 wanaojihusisha na biashara ya kutengeneza sabuni za maji za kufanyia usafi jijini Dar Es Salaam, ambao leo wamepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hilI limepokea vifaa mbalimbali vikiwemo pikipiki aina ya Guta, vifaa vya kufungia sabuni, vifaa vya uzalishaji na vifaa vya usalama vya kufanyia kazi hiyo.

Meneja wa Airtel huduma kwa jamii bi, Hawa Bayumi aliwapongeza kundi la Akilimali kwa uvumilivu wao na kufanya kazi kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema, "Airtel imeona sifa hizo na juhudi zao na ndio maana leo imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa haraka na endelevu ili kukuza biashara yao".

"Kikundi cha Akilimali kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia Airtel FURSA na wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa washauri wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kuimarisha biashara yao " aliongeza Bayumi

Bayumi alielezea kuwa, "mwaka huu Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA umepanga kutumia zaidi ya bilioni moja kwa kuwawezesha vijana mbalimbali hapa nchini na kutoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia nafasi hii muhimu katika maisha yao.

"Kama kampuni ya simu inayojali jamii yake, tumeahidi kuwawezesha vijana hapa nchini kwa kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili waweze kufikia ndoto zao.." alisema Bayumi.

Kwa upande mwingine kundi la Akilimali waliahidi kuweka ujuzi wao wote na kutumia kwa umakini vifaa vilivyotolewa kwao na Airtel kwa matumizi bora na yaliyo sahihi. Kiongozi wa kikundi hicho, Fatuma Rashidi, aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika mengine hapa nchini kuiga mfano wa Airtel.

"Hatukuamini siku moja tutakuwa na uwezo wa kufikia malengo yetu katika biashara hii, tunaahidi kuweka juhudi zaidi na kutumia vifaa hivi na mafunzo tuliyopata kwa umakini zaidi kuhakikisha tunainua zaidi biashara yetu," alisema Fatuma.

Airtel FURSA, inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao.

HALI YA WAKIMBIZI NCHINI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Kama inavyofahamika, tangu mwezi Aprili mwaka jana, nchi yetu imekuwa ikipokea raia toka Burundi wanaoingia nchini kuomba hifadhi ya ukimbizi kutokana na hali ya machafuko iliyotokea nchini mwao.

Hadi kufikia tarehe 10 Februari, 2016, kiasi cha wakimbizi 129,210 toka nchini Burundi wamepokelewa nchini.

Kati ya hawa, wakimbizi 79,290 wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma. Wengine 45,487 wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo na 4,543 wanahifadhiwa katika kambi ya wakimbizi ya Mtendeli iliyoko wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na wadau wengine imekuwa ikitoa huduma muhimu kama vile za afya, chakula, maji na ulinzi ili kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa wanaishi kwa usalama.

Hata hivyo, ukiacha wakimbizi hawa walioanza kuingia nchini mwezi Aprili 2015, Tanzania bado ina wakimbizi wengine ambao wapo katika Kambi ya Nyarugusu. Katika kambi hiyo kuna Wakongo 61,887, Wasomali 150 na wengine 189 toka nchi mbalimbali. Hii ina maana kuwa hadi kufikia tarehe 10 Februari, 2016 nchi yetu ilikuwa na jumla ya wakimbizi 191,436 ambao wamehifadhiwa katika makambi.

RAIA WA NJE WALIOOMBA HIFADHI NCHINI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pia imeendelea kushughulikia raia wa nchi za nje ambao baada ya kuingia hapa nchini wameomba kupatiwa hifadhi ya ukimbizi.

Hadi sasa maombi 815 ya waomba hifadhi yameshashughulikiwa na Kamati ya Kitaifa ya Kuwahoji Waomba Hifadhi (NEC).

Kati ya hawa, 735 wametoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, 25 wametoka nchini Burundi, 14 wametoka nchini Rwanda na 15 wametoka nchini Yemen. Wengine 18 wametoka nchini Syria, 3 Iran, 2 Kenya na 3 wametoka nchini Eritrea.

Hawa wote maombi yao yameshashughulikiwa na matokeo yatatolewa hivi karibuni baada ya uchambuzi yakinifu kukamilika.

Maombi mengine 147 pia yamepokelewa na hivi karibuni Kikao cha NEC kitakaa kujadili maombi yao.

Kati ya hawa raia 24 wametoka nchini Yemen, 13 Syria, 3 Somalia, 6 Rwanda na 18 kutoka DRC. Wengine 2 kutoka Uganda, 1 kutoka Sudan Kusini na 80 kutoka nchini Burundi.

Kundi hili la waomba hifadhi ni wakimbizi ambao waliingia nchini kabla ya mwezi Aprili, 2015.

Pamoja na kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuhusu hali ya wakimbizi nchini, Taarifa hii pia inatolewa ili kuweka sawa habari potofu zilizoandikwa katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la This Day toleo la tarehe 15 Februari, 2016 kuwa Tanzania ina wakimbizi 1,960,000 na kuwa 63,000 kati ya hawa, wengi wao kutoka Syria na Yemen, wameomba hifadhi Tanzania. Taarifa za gazeti hili sio za kweli.

IMETOLEWA NA ISAAC J NANTANGA

MSEMAJI - WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

BASATA YAAGIZA WASANII WOTE KUSAJILIWA NA YAONYA MAPROMOTA

$
0
0
BASATA LAAGIZA WASANII WOTE KUSAJILIWA, LAONYA MAPROMOTA WATAKAOTUMIA WASANII WASIOSAJILIWA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawataka wasanii wote nchini kuhakikisha wamesajiliwa na kuwa na vibali vya Baraza kwani kufanya vinginevyo ni kuvunja sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha BASATA ambayo inamtaka mtu yeyote anayejihusisha na shughuli za Sanaa kuwa amesajiliwa na kupewa kibali na BASATA.

Aidha, BASATA linawaagiza Wakuzaji Sanaa wote (Mapromota) wanaoendesha matukio ya Sanaa kama vile matamasha, mashindano, maonyesho na utoaji tuzo nchini kuhakikisha wanafanya kazi na Wasanii waliosajiliwa na wenye vibali vya BASATA na si vinginevyo.

Sambamba na hili, BASATA linawaagiza wamiliki wote wa studio (Production Houses) zinazozalisha kazi za Sanaa kuzisajili mara moja na kuhakikisha zinakuwa na vibali halali vya Baraza la Sanaa la Taifa.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa sheria hii ya BASATA, Baraza limepewa mamlaka ya kutoa vibali na kuratibu matukio yote ya Sanaa nchini hivyo kuanzia sasa Baraza litaanza udhibiti wa matukio haya ya Sanaa hasa katika kuongeza sharti la kuwataka waandaaji wote wa matukio ya Sanaa kuwataka wasanii watakaoshiriki matukio yao kuwa wamesajiliwa na kupewa vibali na BASATA.

BASATA halitavumilia kwa namna yoyote kuona Mkuzaji Sanaa (Promota) akitumia wasanii wasiosajiliwa na kuwa na vibali kutoka BASATA kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi hasa sheria hiyo namba 23 ya mwaka 1984 inayoelekeza usajili na utoaji vibali kwa wadau wote wa Sanaa.

Itakumbukwa kwamba mnamo Mwaka 2013 Serikali kupitia Sheria ya Ushuru wa Forodha ilitangaza rasmi kuzirasmisha sekta za muziki na filamu. Sheria hii pia inawataka wasanii wote nchini kusajiliwa na kupewa vibali na BASATA na kinyume chake ni uvunjaji wa sheria.

Hata hivyo, toka kuanza kwa mchakato huu wa urasmishaji sekta ya Sanaa ni wasanii wa muziki wa injili pekee ndiyo wamekuwa wakisajiliwa kwa wingi huku wale wa muziki wa kizazi kipya na filamu wakisuasua bila kuwepo kwa sababu za msingi.

BASATA limekuwa likichukua hatua kadhaa kurahisisha mfumo wa usajili wa wasanii ambapo kwa sasa msanii anaweza kupata fomu ya usajili kupitia mtandaoni www.basata.go.tz au kwa maafisa Utamaduni wa Wilaya na baadaye kujaza fomu na kutakiwa kuziwasilisha BASATA zikiwa zimeambatanishwa na wasifu binafsi (CV) wa Msanii husika.

Aidha, gharama za usajili ni kiasi cha Tsh. 75,000/- pekee ambapo fomu hupatikana kwa Tsh. 5, 000/-, Usajili 30,000/- na kibali cha kila mwaka 40,000/- 

Kwa upande wa studio na wakuzaji Sanaa (Mapromota) gharama ni sawa na za msanii isipokuwa tofauti huwa kwenye kibali abapo wao hulipa kiasi cha Tsh. 200.000/- kwa mwaka. 
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI.

Godfrey L. Mngereza 

KATIBU MTENDAJI, BASATA

NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YA MT. LUCAS MKOANI IRINGA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza waliokaa kushoto) wakati alipotembelea ofisini hapo. Wengine ni watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (waliokaa kulia).

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla mapema leo Februari 15, ametembelea kambi ya Wagonjwa wa Kipindupindu pamoja na wale waliokumbwa na mafuriko katika kijiji Mboliboli Kata Pawaga Wilayani Iringa ambapo hadi sasa kambi hiyo ina wagonjwa 40 huku zaidi ya wagonjwa 223 walilipotiwa kuugua tangu kipindupindu kimeanza katika eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza wakati wa kutoa taarifa yake kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aliyetembea ya Mkuu wa mkoa huyo, alimweleza kuwa kati ya wagonjwa hao 223, wagonjwa 17 ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, Mbali na hao hadi sasa yamesababisha kifo kimoja.

Ugonjwa huo umeelezwa kuwa umewakumba kutokana na mvua zilizonyesha na kubomoa vyoo na kutapanya kinyesi hali iliyopelekea ugonjwa huo kusambaa Zaidi katika makazi ya wananchi hao.

Hadi sasa eneo hilo limekumbwa na maji huku wananchi wakilazimika kuyakimbia makazi yao na hata kuzungukwa na maji karibu eneo kubwa na usafiri wa watoa huduma kuwa wa shida ikiwemo kutumia boti maalum ama chopa.

Mkoa huo ulikumbwa na mvua mnamo Februari 3 hadi leo bado maji yameendelea kuzingira maeneo ya vijiji hivyo.

Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog-Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa taarifa namna ya kamati yake ilivyopambana usiku na mchana na hatua waliofikia katika kuakikisha kipindupindu kinakwisha katika eneo hilo huku wakiendelea na jitihada za kupambana na mafuriko ikiwemo kuokoa wananchi waliobakia eneo hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kumaliza kwa mazungumzo na taarifa fupi juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwenye maeneo ya vijiji vya Mkoa huo ambapo hadi leo wamefikia jumla ya wagonjwa 40.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa tayari kwa kuelekea kupanda Chopa kuelekea kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
Wakielekea katika Chopa maalum ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwafikia wananchi waliozingirwa na maji ya mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipanda Chopa tayari kuelekea kwenye eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Pawaga, Mkoani Iringa. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Iringa).

WAWILI WASIMAMISHWA TBC NA IDARA NZIMA KUFUMULIWA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.

Nape awasimamisha kazi baadhi ya Watendaji TBC

$
0
0

Na: Frank Shija, WHUSM


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji usioridhisha.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi Bibi. Edna Rajab ambao wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi. “ Tunachukua uamuzi wakuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla” Alisema Nape

Aidha Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini ya Idara hiyo kwakuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonyesha utendaji mbovu.


Alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu juu ya utendaji mbovu na wakutoridhisha viongzi na baadhi ya watumishi wa Idara hiyo hiyvo hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni  kujenga upya na kuboresha Idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa Shirika lolote lile la Habari na kuongeza ufanisi.


Idara ya Habari na Matukio ya TBC inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa Vipindi Wahariri na Waandishi wa Habari ambapo tayari Mkurugenzi na Meneja wa Vipindi wamesimamishwa kazi leo tarehe 15 Februari 2016 na watumishi wengine watachukuliwa hatua kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa Habari kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC alilolitoa leo wakati akitangaza kuwasimamisha kazi viongozi hao.

MAJALIWA AKABIDHIWA NAKALA YAKE YA FOMU YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea nakala yake ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kutoka kwa Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambako ilitiwa saini na kamishina huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 15, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambao walikwenda ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 15, 2016 kumpatia nakala yake ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti hiyo ambako ilitiwa saini na Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda (wapili kulia).Kushoto ni Katibu wa Idara ya Viongozi Watumishi wa Umma, Secretarieti ya Maadili , John Kaole na kulia ni Katibu wa Idara ya Viongozi wa Siasa, Secretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI KUSAMBAZA MADAKTARI BINGWA MAENEO YA PEMBEZONI IKIWEMO MKOA WA RUVUMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitoa ufafanuzi juu ya Wizara yake kuhakikisha itapeleka Madaktari bingwa katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo hospitali hiyo ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema Februari 13.2016.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto mjini Songea, Dkt. Hamisi Kigwangalla baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kituo cha afya cha Mjimwema kilichopo mjini Songea huku akiitaka mikoa ya pembezoni ukiwemo mkoa huo wa Ruvuma kuweka mazingira ya kuwavutia madaktari bingwa kufanya kazi katika mikoa yao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu amesema kuwa mkoa huo umeridhishwa na staili ya ziara ya kushtukiza na kwamba wanajitahidi kuboresha vituo vya afya vya Mjimwema Songea, Madaba na cha wilaya ya Namtumbo ili vipandishwe hadhi kuwa hospitali za wilaya.

Pia Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo na kujionea utendaji wa kazi huku akitoa wito katika suala la maboresho zaidi.

Imeandaliwa na Andrew Chale wa Modewjiblog, Ruvuma.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (katikati) akijiandaa kuingia kukagua utendaji wa kazi na vifaa ndani ya chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo Februari 13.2016.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akijiandaa kuingia kwenye chumba cha upasuaji wakati wa ziara yake hiyo, aliyoifanya mapema Februari 13.2016.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vitanda vinavyotumika katika upasuaji hospitalini hapo ambapo hata hivyo aliambiwa changamoto kuwa baadhi ya taa za vitanda hivyo kuwa na hitilafu wakati ziara hiyo mapema Februari 13.2016. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Songea, Ruvuma)

Naibu Waziri Annastazia aitaka jamii kutoa elimu ya Unyago kwa kuzingatia umri.

$
0
0
Na Shamimu Nyaki  MAELEZO.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura amezitaka jamii kutoa elimu ya jando na unyago kwa kuzingatia umri na wakati sahihi wa mafunzo hayo ili kuweza kuondoa tatizo la mimba na ndoa za utotoni.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam  wakati alipozungumza na Wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka mkoani Mtwara wanaoshughulika  na mapambano dhidi ya mimba  na ndoa za utotoni zinazosababishwa na utekelezaji wa wa mila na desturi hizo  mkoani  Mtwara.

“Ni vizuri   kuwafundisha watoto wetu maadili mema wakiwa wadogo,lakini ni vizuri Kuandaa namna ya kutoa elimu kwa kuzingatia umri na aina ya elimu ili kutoa taaluma hiyo kwa watu sahihi na wakati unaofaa. Alisema Mhe.Anastazia.”

 Mwenyekiti wa asasi hizo Dkt.Lillac Malumbo akitoa taarifa ya jinsi wanavyoshughulikia tatizo hilo amesema  kuwa asasi zinatoa mafunzo mbalimbali  kwa kwa wakufunzi  wa watoto wa kike ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni linalosababishwa na  utekelezaji wa mila mbalimbali mkoani   Mtwara.

“Tunaamini kuwa jamii   ikielimishwa kuhusu madhara yatokanayo  na  baadhi ya mada zinazotolewa katika mafunzo ya unyago na ambazo  zinaleta ushawishi kwa watoto wa kike kujiingiza katika zinaa, mimba na ndoa za utotoni tatizo ili litaisha.Alisema Dkt. Lillac.”

 Dkt Lillac   ameongeza kuwa kuweka ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na asasi hizo kutamuwezesha mtoto wa kike  kupata elimu, kuepuka magonjwa ya Zinaa ,kupunguza watoto yatima na watoto wa mtaani.

Hata hivyo mila hizi  zimekuwa zikiwanyima watoto wa kike haki ya kupata elimu kwa wakati, kusikilizwa, kuendelezwa na  kuwafanya  kubaki  tegemezi  kwa muda  wote. 

Asasi hizi  zinatoka katika wilaya nne za mkoa wa Mtwara ambazo ni Tawaso Masasi,Msoapo Mtwara,Aware Mtwara vijijini ,Chakumuma Masasi,Nyerere Tandahimba,Kimweso Mtwara vijijini, pamoja na Children  Youth Development Innitiatives (CYDI).

FEDHA ZA MIRADI YA MAJI ZITUMIKE KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI NA SI VINGINEVYO-INJ. LWENGE

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akitakata utepe na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji katika Kijiji cha Peruhanda, Wilaya ya Njombe, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Saraha Dumba.
Mradi wa Maji unaohudumia Kijiji cha Peruhanda, Wilaya ya Njombe.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akikagua chanzo cha maji cha Nyenga kinachohudumia Mji wa Njombe, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Njombe (NJUWASA), Inj. Daudi Majani
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Abbas Kandoro (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Gulamhussein Kifu.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge mara baada kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Kijiji cha Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali na Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Haroon Pir Mohamed.

……………………………………
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge amezionya Halmashauri za Wilaya za Njombe na Mbarali kuhakikisha fedha za miradi ya maji zinazotolewa na Serikali, zinasimamiwa vizuri na kutekeleza miradi ya maji na si vinginevyo.

Mhe. Lwenge alisema hayo mwishoni mwa juma katika ziara yake ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, alipotembelea Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe na Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya katika ziara yake ya kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji na upatikanaji wa huduma hiyo.

“Naagiza Halmashauri za Wilaya zihakikishe fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji, zisimamiwe vizuri na zitumike kufanya hivyo na zisitumike kwa miradi mingine. Mhe. Rais Magufuli ameazimia kutatua kero ya maji nchini na hatatutakuwa na sababu yoyote ya kutotimiza lengo hilo, na ifikikapo mwaka 2020 tuwe tumefikia asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini katika kutoa huduma ya maji na hili lipo ndani ya uwezo wetu”, alisema Mhe. Lwenge.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji alisema ni wajibu wa watendaji wote wa Serikali kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao kila moja, kwani Serikali ya Awamu ya Tano ni ya vitendo na si maneno. Huku akiendelea kusisitiza suala la maendeleo ya Sekta ya Maji ni shirikishi kati ya Serikali na wananchi, na si Serikali pekee ili kuhakikisha tatizo la maji linapatiwa ufumbuzi kwa haraka na mafanikio.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr. Rehema Nchimbi amemuhakikishia Mhe. Lwenge kuwa wataiunga mkono Serikali kwa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kutunza mazingira na vyanzo vya maji, ili rasilimali hiyo iwepo ya kutosha kwa miaka mingi ijayo na maendeleo ya sekta hiyo yawe endelevu. Dr. Nchimbi alisema watafanya jitihada za kumaliza changamoto za shughuli za kibinadamu zinazoendana kinyume na Sera na Sheria za Mazingira na Maji nchini.

Katika ziara yake hiyo Mhe. Lwenge aliweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji wa vijiji cha Peruhanda, Wilaya ya Njombe na Ubampa, Kata ya Ubaruku, Wilaya ya Mbarali, ikiwa ni kati ya miradi 1,800 inayotekelezwa na Serikali kitaifa na kati ya miradi hiyo, 1,200 ikiwa imekamilika.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.  Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:

1.      Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirroanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.

2.      Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhangaanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

3.      Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia. Kamishna Mikomangwaanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

4.      Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzyaambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.



Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimbaanajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

15 Februari, 2016

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AKUTANA NA KAMPUNI YA LAKE HOLDINGS

$
0
0
 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya Wawekezaji, Sinotan Renewable Energy alipokuwa akielezea changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa mradi wa umeme wa upepo wa Makambako.
 Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi wa Kampuni ya uwekezaji wa umeme wa upepo mjini Makambako Luka Buljani alipokuwa akitoa maelezo kuhusiana na mradi huo. 
Alex O. Lema Mwenyekiti wa Kampuni ya wawekezaji wa Sinotan Renewable Energy  akiwasilisha changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza mradi wa umeme wa upepo mjini Makambako (Mwenye Mvi) wengine ni watendaji wa Wizara na taasisi zinazohusiana na masuala ya nishati waliofika katika kikao hicho kilichofanyika wizarani leo asubuhi



Sino-Tan Renewable Energy yatakiwa kuonesha uwezo wa kuzalisha umeme

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameitaka kampuni ya Sino-tAN Renewable Energy ya kuzalisha umeme wa upepo katika eneo la Makambako Mkoani Njombe kuihakikishia Serikali kuwa ina uwezo wa kufanya hivyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo 15 Februari mpaka 15 Machi 2016.


Maagizo hayo yametolewa ofisini kwake wakati wa kikao baina ya Wizara na Kampuni hiyo iliyofika kuelezea changamoto inazokumbana nazo katika kutekeleza mradi huo wa kuzalisha Megawati 100 za umeme.Akizungumzia lengo lao la kuonana na waziri Muhongo, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Alex O. Lema alisema upo mgogoro wa kuachia ardhi katika Kijiji cha Mtewele wilaya ya Wanging’ombe pamoja na kwamba  halmashauri husika ilishatoa kibali kwa kampuni hiyo.

Bw. Lema ameeleza kuwa theluthi mbili za eneo la mradi zinapatikana katika wilaya ya Makambako wakati theluthi moja inayobaki ipo katika Wilaya ya Wanging’ombe ambako hasa ndiko kwenye mgogoro huo.Aidha Bw. Lema alitumia fursa hiyo kuiomba Wizara ya Nishati na Madini kuwa kiungo katika kuhakikisha mradi unafanikiwa kwa kuwashirikishawadau wengine ambao ni Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa eneo husika pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.

Baada ya maelezo toka kwa Mwenyekiti huyo, Prof. Muhongo alimtaka Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia nishati jadidifu, Edward L. Ishengoma kuteua maafisa wawili ili kufika katika eneo lenye mgogoro na kujionea sababu za wanakijiji hao kupinga eneo hilo kutumiwa na mradi huo na kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku mbiliza ufuatiliaji.


Aidha, Prof. Muhongo ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imebadili namna yake ya utendaji na kuwataka wawekezaji hao kuwasilisha mpango kazi wao ndani ya mwezi mmoja kutokana na uhitaji mkubwa wa nishati ya umeme wa kutosha na wa uhakika.


Mradi huu wa uzalishaji wa Umeme wa upepo wa Makambako umechukua miaka 10 tangu mwaka 2004 hadi sasa, ambapo  miaka mitano ya awali walikuwa wakifanya utafiti na kuandika ripoti iliyobainisha kuwa uzalishaji wa umeme wa upepo katika eneo hilo ni dhahiri na hivyo kibali kutolewa kwa wawekezaji hao kuanza utekelezaji ambao unakwamishwa na suala la ardhi kwa hivi sasa.


Kazi mpya toka Watengwa Recs

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images