Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Article 3


WANAFUNZI WAPIMWE MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA WAKIWA SHULENI –WAZIRI ,UMMY MWALIMU.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TATIZO la utumiaji wa dawa za kulevya kwa  vijana unaanzia  katika shule, hivyo kunahitaji kupimwa wanafunzi wakiwa shuleni katika kuweza kutokomeza tatizo la utumiaji wa dawa hizo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati makabidhiano ya  Gari ya Kituo cha  Kuratibu  Matumizi ya Sumu lilitolewa na nchi ya Japan kwa ofisi ya  Mkemia Mkuu wa Serikali,  amesema kuwa tatizo la utumiaji wa dawa unaanzia shule hivyo ofisi mkemia mkuu wa serikali anaweza kupima wanafunzi kila baada ya muda na kuweza kugundua chanzo cha dawa hizo.
Amesema kuwa wanafunzi wakipimwa kila baada ya muda mkemia anaweza kujua na serika ikaweza kudhibiti juu ya matumizi ya dawa  za kulevya kutokea shuleni.
Waziri, Ummy amesema vijana wanaotumia dawa za kulevya  wengine walianzia katika shule na kuweza kuwafundisha wengine na kuwa ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya na kusababisha nchi kukosa nguvu kazi ya vijana kutokana na kuathirika dawa hizo.
Aidha amesema katika kazi data ya kuweka taarifa za vinasaba vitasaaidia kupunguza watoto wa mitaani kutokana wazazi watambuliwa na vinasaba mara baada ya kupima.
Ummy, amesema kuwa ofisi ya mkemi mkuu wa serikali ni ana kazi kubwa ya kutoa haki kwa kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo majanga moto kwa kuweza kutambua watu baada ya kutokea,  vinasaba vya watoto ambao wanakuwa katika mgogoro na kubaini mhusika.
Nae Mtendaji wa Maabara wa Ofisi ya Mkemia Mkuu, Profesa Samwel Manyere amesema kuwa kupata gari hilo watafanya kazi kwa kiwango cha juu kutokana na jinsi walivyojipanga.
Aidha amesema kuwa wameweza kupata cheti cha utoaji huduma kwa kiwango cha Kimataifa (ISO) hivyo kitu chochote kikifanyika kinaendana na viwango hivyo.

MAMIA WAJITOKEZA KUMPOKEA MSHIDI WATECHNO OWN STAGE NANDY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mshindi wa pili wa mashindano ya Techno Own Stage, Faustina Mfinanga aka Nandy,akiwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Juliusi Nyerere , baada ya kuwasili kutoka Nageria katika mashindano hayo, jana jijini Dar es Salaam. 
Mshindi wa pili wa mashindano ya Nandy Techno Stage, Faustina Mfinanga, akiwa kabebwa juu mara baada ya kuwasili kutoka Nigeria,jana jijini Dar es Salaam.
Nandy akiwaonesha wananchi waliofika kumpokea uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere , jana jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa pili wa mashindano ya Techno Own Stage, Faustina Mfinanga, akiwa katika picha ya pamoja na ndugu zake jana jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii)

Mshindi wa pili wa mashindano ya Techno Own Stage, Faustina Mfinanga aka Nandy,akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ushindi alioupata nchini Nigeria baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege majira saa sita usiku wa kuamkia leo ,jijini Dar es salaam.

MKOA WA DODOMA WAZINDUA RASMI KAMPENI YA UGAWAJI VYANDARUA FEBRUARI 9, 2016.

$
0
0
 Kikundi cha ngoma za asili ya kigogo cha Chamwino Ikulu Dodoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Dodoma ya kugawa vyandarua vya bila malipo kwa kaya Februari 9, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akigawa vyandarua vya bila malipo kwa wananchi wa kijiji cha Chamwino Ikulu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akiwafundisha wananchi wa Chamwino Ikulu namna bora ya kuwakinga watoto dhidi ya mbu na malaria kwa kuwalaza kwenye vyandarua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.

 Waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua vya bila malipo wakifuatilia onesho alilolifanya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani)la namna bora ya kuwakinga watoto dhidi ya mbu na malaria kwa kuwalaza kwenye vyandarua.
 Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dodoma wakiwaonesha Wananchi wa Chamwino Ikulu namna bora ya kujikinga dhidi ya mbu na malaria kwa kulala kwenye vyandarua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua vya bila malipo Mkoani humo Februari 9, 2016.
Wananchi wa mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakiwa wamejipanga kwenye mistari ya kusubiria kugawiwa vyandarua vya bila malipo Februari 9, 2016.

MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.

MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI NZOVWE ILIYOPO JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ERICKA MWASIKILI [08] MKAZI WA NZOVWE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 239 CCU AINA YA MITSUBISHI FUSO IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE GEORGE LWINGWA [40] MKAZI WA ISANGA JIJINI MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 10.02.2016 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO ENEO LA NJIAPANDA ITENDE, KATA NA TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA. UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO HASA KWA KUWEKA UANGALIZI PINDI WANAPOTUMIA BARABARA.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WANAFUNZI WAENDELEA KUTEMBELEA DUKA LA KISASA LA AIRTEL EXPO.

$
0
0
 Afisa mauzo wa Airtel Deogratius Gerald (katikati) ,akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa A3 Institute of Technology ,wakati walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wa chuo cha A3 Institute of Technology wakiangalia vifaa  na simu mbalimbali vinavyopatikana  katika duka jipya la Airtel Expo walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
  Meneja huduma kwa Wateja wa Airtel  Happy John  (kushoto) , akiwakabidhi zawadi wanafunzi wa chuo A3 Institute of Technology walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam akishuhudia na afisa mauzo wa Airtel Tanzania Prosper Mwanda (kulia)
 Wanafunzi wa chuo  cha A3 Institute of Technology wakisikiliza mafunzo kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya simu ya Airtel (hayupo pichani) walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
 Afisa mauzo wa Airtel Celine Njuju akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa chuo cha A3 Institute of Technology walipofanya ziara ya kimafunzo katika duka jipya la Airtel Expo katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.

MSHINDI WA WOOLWORTHS AKABIDHIWA VOCHA YA TSH MILLIONI 1/=.

$
0
0
 Mshindi wa Droo ya mwezi Desemba 2015, Daniel Mugasa, akisaini kwenye kitabu maalumu baada ya kukabidhiwa  vocha ya manunuzi yenye thamani ya shilingi Milioni 1 na   Meneja Masoko na Uhusiano wa Duka la nguo la Woolwoorths Tanzania, Edwina Barongo,  wakati wa hafla  iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ili mteja  aweze kushiriki katika shinadano hilo ni lazima awe na card maalumu ya inayomwezesha   kununua bidhaa katika  maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card).
  Mshindi wa Droo ya mwezi Desemba 2015 , Daniel Mugasa , akikabidhiwa  na  Meneja Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Woolwoorths Tanzania, Edwina Barongo vocha ya manunuzi yenye thamani ya  shilingi Milioni 1 ,  baada ya kuibuka mshindi  . Ili mtena  aweze kushiriki katika shinadano hilo ni lazima awe na card maalumu ya inayomwezesha   kununua bidhaa katika  maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card) . Hafala hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko na Uhusiano wa duka la nguo la Woolwoorths Tanzania, Edwina Barongo ( Kulia)  akimuonyesha bidhaa mpya  mshindi wa  Droo ya mwezi Desemba 2015  , Daniel Mugasa    wakati alipofika katika Duka la Woolworths  jijini Dar es Salaam, kumkabidhi zawadi yake vocha ya manunuzi yenye thamani ya shilingi milioni 1 baada ya kuibuka  mshindi  katika droo ya Woolworths ya Desemba 2015. Ili mteja  aweze kushiriki katika shinadano hilo lazima na card maalumu ya kuweza kununua bidhaa katika  maduka ya Woolworths (Wreward Loyalty Card)  Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

TAFRANI YAZUKA KIVUKO CHA MV KIGAMBONI MAPEMA LEO

$
0
0
 Baadhi ya abiria waliokuwa wamepanda kivuko cha Mv  Kigamboni wakiwa wamekumbwa na butwaa kufuatia kivuko hicho walichokuwa wamepanda kukatika sehemu ya kushukia abiria na Magari na kupelekea hofu kubwa miongoni mwao,kama uonavyo pichani baadhi ya abiria hao wakijaribu kujinusuru na hali hiyo,kwani kivuko hicho kilikuwa kimesheheni abiria lukuki
 Abiria wakipewa maelekezo namna ya kushuka kwenye kivuko hicho.


CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU IRINGA (IRFA) KUJENGA UWANJA WA KISASA.

$
0
0
Kulia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na baadhi ya viongozi wa uwanja wa samora.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA
Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) kiko mbioni kujenga uwanja wake wa kisasa utakaosaidia kuendeshea ligi mbalimbali zikiwemo ligi za kimataifa hali itakayosaidia kuinua soka la mkoa huo .

Akizungumza ofisini kwake mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava alisema wameamua kujenga uwanja wao ili kuepukana na adha wanayopata kutokana na kukosa sehemu ya kuendeshea ligi mbalimbali .

Alisema tayari wameshapata eneo la hekari 14 katika eneo la kitwiru ndani ya manispaa ya Iringa na sasa kinachosubiriwa ni kumaliza mazungumzo kati ya chama hicho na manispa ya Iringa ili kuweza kumilikishwa eneo hilo ili liwe mali yao kabisa tofauti na apo awali ambao manispaa hiyo ilikuwa inataka kuingia nao ubia.

“Tayari hili swala liko katika hatua za mwisho na tayari tumesha fanya mazungumzo tunataka tujenge uwanja wetu wenyewe wa kisasa ambao tunaweza kucheza mechi za kimataifa kwani tumekuwa tukipata tabu ya viwanja vya kuchezea na hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuuwa soka la mkoa wetu ”alisema Kuyava.

Alisema wanasubiri majibu ya maombi waliyopeleka katika manispaa hiyo ili kuweza kupunguziwa bei li kuanza mchakato wa kulipa fidia kwa wamiliki wa maeneo hayo ili waanze mchakato wa uwanja huo wa kisasa .

Alisema kuwa mara nyingi timu zimekuwa hazi pati kitu wanapotumia viwanja vya watu kwani asilimia 16 za mapato yanayopatikana kutokana na kingilio huchukuliwa na wamilika wa kiwanja na asilimia ndogo inabaki ndio zinagawanywa katika maeno mengine na kujikuta timu hazinufaiki na chochote .

Alisema kuwa hapo awali walikuwa wakitumia uwanja wa samora ambao bado uko katika matengenezo tena ya kusuasu kwa kuwa mpaka sasa bado wanadai kusubiri nyasi za kupanda jambo litakalorudisha michezo nyuma endapo hawatakuwa na maono ya kuwa na kiwanja chao wenyewe .

Kwa upande wa wadau wa soka mkoa wa Iringa Ally salehe ambaye pia ni shabiki wa timu ya lipuli anasema kuwa endapo juhudi za makusudi zitafanyika na kufanikisha ujenzi wa uwanja huo basi ni dhahiri kuwa soka la mkoa wa iringa litapanda kwa kiasi kikubwa .


Alisema kuwa katika mkoa wa Iringa kuna vipaji vingi vya michezo ikiwemo wachezaji wa mpira wa miguu lakini wamekuwa wakikosa sehemu za kufanyia mazoezi ili kukuza vipaji vyao hivyo kujengwa kwa uwanja huo wa kisasa utafungua fursa za ajira kwa vijana wengi.

MKUU WA MKOA WA DODOMA CHIKU GALAWA APOKEA MSAADA WA VITU MBALIMBALI KUTOKA VODACOM FOUNDATION KWA NIABA YA UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA HUO.

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati, Balikulije Mchome(wakwanza kushoto)akisaidia kutandika shuka katika wodi ya Watoto hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma mara baada ya kukabidhi msaada wa mashuka na magodoro pamoja na vitu mbalimbali jana ktoka Vodacom Foundation wenye thamani ya zaidi shilimgi milioni 18,Katikati Doris Mollel mwanzilishi wa taasisi ya kusaidia watoto ya Doris Foundation,na Mkuu wa Idara ya watoto ya hospitali hiyo Dkt.David Mzava.
 Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Zainabu Chaula (kushoto)akikabidhiwa msaada wa mashuka na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi jana kwa ajili ya wodi ya watoto hospitalini hapo,Vodacom Foundation ilitoa msaada wa mashuka 200,mito 200 na magodoro 100 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni 18.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Chiku Galawa (katikati) akikabidhiwa msaada wa magodoro 100 na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi (kushoto)Jumla ya magodoro 100 ,mashuka 200 na mito 200 vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 18 vilitolewa msaada na Vodacom Foundation hospitalini hapo kwa ajili ya wodi ya watoto, Anayeshuhudia kulia Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Zainabu Chaula.

 Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Zainabu Chaula (kushoto)akikabidhiwa msaada wa muto wa kulalia na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi jana kwa ajili ya wodi ya watoto hospitalini hapo,Vodacom Foundation ilitoa msaada wa mashuka 200,mito 200 na magodoro 100 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni 18 .Katikati Doris Mollel mwanzilishi wa taasisi ya kusaidia watoto ya Doris Foundation.

WATUHUMIWA WALIOKUTUNGUA HELKOPTA SERENGETI WATIWA MBARONI.

$
0
0
Njile Gonga (28) Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la Akiba la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio hilo rubani wa helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.
 
Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.
 Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi leo hii.
 Watuhumiwa wakiwa ndani ya gari la polisi, baada ya kufikishwa kituo cha polisi Bariadi wakitokea wilayani Meatu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Elaston Mbwilo akionyeshwa watuhumiwa wa ujangili ambao walihusika kutungua Helkopta.
 Hii ni kama haijawahi kutokea kwa wakazi wa Mji wa Bariadi, Kwa mara ya kwanza kufurika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya hiyo kushuhudia watuhumiwa hao.

WATUHUMIWA wa tukio la kutungua ndege aina ya Helkopta na kumuua rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza lilitokea mnamo tarehe 29/01/2016 katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, leo (jana) wamefikishwa mahakani kusomewa mastaka yanayowakabili.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Simiyu, chini ya ulinzi wa mkali wa askari polisi, huku umati mkubwa wa wananchi wa mji wa bariadi waifurika kushuhudia watuhumiwa hao.

Akiwasomea mashtaka watuhumiwa hao Wakili mwandamizi wa serikali Mkoa wa Simiyu Yamiko Mlekano alisema kuwa washitakiwa wote 9 wanakabiliwa na kesi tatu ambazo ni Uhujumu uchumi, mauaji pamoja na umiliki wa siraha bila ya kibali cha serikali zenye mashtaka tofauti.

Katika kesi ya Uhujumu uchumi iliyosomwa chini ya Hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi wa mahakama hiyo John Nkwabi katika shtaka la kwanza mtuhumiwa namba moja Iddy Mashaka (49) anatuhumiwa kujihusisha na kuratibu tukio la uhujumu uchumi kinyume na kifungu 4(1)(d) sura (57) (1) na 60 (2) cha makosa ya uhujumu uchumi sheria namba 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mlekano alisema kuwa katika kosa hilo mshitakiwa kati ya tarehe 6 januari na 1/02/2016 katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu aliwashauri Mshitakiwa namba mbili Shija Mjika (38) kuua wanayama wasiyoruhisiwa kama tembo.

Katika shtaka la pili wakili huyo aliwataja watuhumiwa namba mbili hadi tisa ambao ni Shija Mjika (38) Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42) Moses Mandagu (48) Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40) Mapolu Njige (50) pamoja na Mange Barumu (47), watuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
Katika shtaka hilo wakili aliieleza mahakama kuwa kati ya tarehe 21/01/2016 na 29/01/2016 katika wilaya ya Meatu, watuhumiwa hao walipanga na kuratibu tukio la kuwinda wanyama aina ya tembo bila ya kibali cha serikali.

 Hata hivyo wakili huyo alieleza kuwa katika shtaka la tatu watuhumiwa namba mbili hadi tisa waliotajwa hapo mwanzo, watuhumiwa kujihusisha na uwindaji wa wanyama wasiyoruhusiwa kinyume na kifungu 47(a)(aa) cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 sambamba na sura 14 (a) na kifungu 57 (1) cha uhujumu uchumi sura 200 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Alisema katika shataka hilo mnamo kati ya tarehe 26/01/2016 na 29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba katika kijiji cha Makao wilayani Meatu watuhumiwa walimuua tembo mwenye dhamani ya shilingi Milion 32,891,100 bila ya kibali cha serikali.

Katika shtaka la nne watuhumiwa namba mbili hadi tisa wanatuhumiwa kwa kosa la kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria namba 86(1)(2)(b) cha uhuwifadhi wa wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya 14(d) na sura 57(1) cha uhujumu uchumi sura ya 200.

Katika maelezo ya kosa hilo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa kati ya 29/01/2016 na tarehe 6/02/2016 katika wilaya ya meatu mkoa wa simiyu walikamatwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo yenye uzito wa kilo 31 yenye thamani Milioni 32,891,100 bila ya kibali cha serikali.

Katika shtaka namba tano watuhumiwa namba moja na mbili ambao ni Iddy Mashaka (49) pamoja na Shija Mjika (38) wanatuhumiwa na uuzaji wa nyara za serikali kinyume na kifungu cha sheria 84(1) cha uhuwifadhi wa wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya 14(b) na sura 57(1) cha uhujumu uchumi sura ya 200.
 
Katika kosa hilo wakili alisema kuwa kati ya tarehe 6/01/2016 na tarehe 1/02/2016 katika wilaya a Meatu Mkoani Simiyu, watuhumiwa walikamatwa wakiwa wanajihusisha na uuzaji wa nyara za serikali bila ya kibali.

Hata hivyo katika kesi namba mbili ya Mauaji wakili Mlekano aliiambia mahakama kuwa watuhumiwa ambao ni Shija Mjika (38), Njile Gunga (28) Dotto Pangali ( 42) pamoja na Moses Mandago (28) wanashtakiwa kwa kosa la mauaji kinyume che sheria ya 196 na 197 cha kanuni ya adhabu namba 16 iliyofanyiwa mwaka 2002.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao mnamo tarehe 29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba kijiji cha Makao wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu walimuua rubani wa ndege aina ya helkopta rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza.

Katika kesi zote Mbili kwa mujibu wa hakimu huyo alisema kuwa watuhumiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, ambapo keshi hizo zilihairishwa mpaka terehe 24/02/2016 mpaka zitakapotajwa tena.

Sambamba na hayo katika kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na siraha kinyume cha sheria na pasipo leseni ilisikilizwa katika mahakama hiyo chini ya Hakimu mfawidhi wa wilaya Bariadi Mary Mrio ambapo watuhumiwa walikabiliwa na mashitaka matano.

Watuhumiwa hao ni Mange Buluma,Shija Mjika,Dotto PanganiNjile Ngunga,Moses Mandagu,Dotto Huya na Mwigulu Kanga ambapo baadhi yao walikiri kumiliki siraha kinyume cha sheria pamoja na riasi akiwemo njile aliyetungua helkopta hiyo.


Watuhumiwa hao ambao Shija Mjika, Moses Mandagu, Njile Ngunga pamoja na Dotto Pangani walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na siraha aina ya bunduki Riffle 303 Namba 06490 kinyume cha sheria pamoja na risasi mbili.

Hata hivyo Njile Ngunga pamoja na Moses Mandagu walikiri pia katika shtaka la tatu, nne pamoja na tano la kukutwa na siraha bila ya kibali, kumiliki risasi bila ya kibali, pamoja na kumiliki tena risasi kinyume cha sheria huku wengine kati ya hao wakikana makosa hayo.

Hata hivyo mahakama haikuweza kutoa hukumu juu ya watuhumiwa hao waliokiri kutokana na vielelezo kutokuwepo mahakamani hapo, ambapo kesi hiyo ilihairishwa mpaka kesho (Leo).
Watuhumiwa wote walirudishwa rumande.

BEI YA MADAFU HII LEO.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH.ASHATU KIJAJI AFUNGUA MKUTANO WA MWAKAA WA 25 WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF

$
0
0
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko"unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju.
 Baadhi ya Wadau washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaji alipokuwa akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Meza kuu wakati mkutano ukiendelea
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mmoja wa wanachama wa Mfuko wa PPF mwenye ulemavu wa kusikia akiendelea kufatilia mada mbali mbali kwenye mkutano huo kupitia mkalimani wa lugha ya alama.
Wadau wakipitia kablasha la PPF.












Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akitoa hotuba fypi ya shukrani kwa niaba ya mifuko ya hifadhi za jamii nchini.


Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.



RAIS WA ZANZIBAR AMUAPISHA NAIBU KATIBU MKUU UWEZESHAJI ,USTAWI WA JAMII VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO.

$
0
0
  Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Ndg,Hassan Khatib Hassan leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Ndg ,Hassan Khatibu Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Ndg. Hassan Khatibu Hassan baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, kabla alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto Asha Abdalla baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa Nd,Hassan Khatibu Hassan kuwa Naibu katibu wizara hiyo leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
[Picha na Ikulu.]

Naibu Waziri wa Afisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina Afanya Ziara Kutembelea Miradi ya Kuharibika na Tabia Nchi Zanzibar.

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Masauni akiwa katika ziara hiyo kutembelea eneo hilo la kilimani lililoharibika kwa kuliwa na bahari kutokana na Tabia Nchi. 
Eneo la Ufukwe wa Kilimani uliovyoliwa na Tabia Nchi kama unavyoonekana pichani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina, wakati wa ziara yake hiyo leo katika eneo la kilimani Zanzibar. 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina, wakati wa ziara yake hiyo leo katika eneo la kilimani Zanzibar. 
Sheha wa Shehia ya Kilimani akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitowa maelezo ya eneo mpja lililoathirika na Tabia nchi katika eneo la kilimani akimuonesha uliokuwa uwanja wa kilimani Stars kwa sasa uwanja huo umekuwa ni sehemu ya kukaa maji ya bahari wakati wa maji kujaa. na kufika karibu na sehemu ya makaazi ya wananchi.
Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Tanzania Mhe Luhaga Mpina akitembelea eneo hilo wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya Tabianchi Zanzibar akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar wakiwa kastika ufukwe wa pwani ya kizingo. 
Naibu Waziri wa Afisi ya Rais Muungano na Mazingira Tanzania Mhe Luhaga Mpina na Mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nadi Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni wakitembelea eneo la ufukwe wa pwani ya kilimani ilioathirika kwa kuliwa na bahari sehemu kubwa ya eneo hilo na kuingia maji katika maeneo ya jirani na makaazi.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi huo wa kudhibiti tabia nchi kwa eneo hilo la kilimani na kuharibu sehemu kubwa ya eneo hilo ambalo lilikuwa na uwanja wa mpira na kuliwa na bahari.
Naibu Waziri wa Afisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Joelson Mpina akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo hilo lililokubwa na athari za Tabia nchi katika pwani ya ufukwe wa kilimani na kuagiza kupandwa kwa mikoko katika eneo hilo ambolo ifikapo mwezi wa marchi na fedha zake zipo kwa kazi hiyo na zoezi hilo limeaza mwezi huo kwa kuaza kwa kupandwa kwa miti ya mikoko na ujengaji wa tuta la kuzuiya maji ya bahari kuendelea kula eneo hilo ambalo tayari limeharibia na maji ya bahari.
Naibu Waziri Afisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Joelson Mpina Naibu Waziri wa Mambi ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Yussuf Masauni na Mbunge wa Jimbo la Jangombe Mhe. Ali Hassan Omar King wakitembelea eneo la pwani ya kilimani lililokumbwa na athari za TabiaNchi. wakati wa ziara yake Kisiwani Zanzibar kutembelea maeneo hayo. Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.  Zanzinews.com. ,
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa na aliyekuwac Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo kwa sasa ni mgombea Jimbo la Kikwajuni Uwakilishi Mhe Nassor Salim Jazira akiwa katika ziara hiyo ya Mhe Waziri Zanzibar 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Eng Hamad Yussuf Masauni akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Jangombe Ali Hassan Omar King wakiwa katika ziara hiyo kutembelea miradi ya Muungano ya Tabia Nchi Zanzibar. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Ndg Juma Bakari Alawi akitowa maelezo jinsi eneo hilo la kilimani lililoathirika na Tabia Nchi Zanzibar likiwa chini ya mradi wa Kujenga Uwezo wa Jamii Kuhimili Mabadiliko Tabia Nchi (LDCDF)kilimani kwa Upandaji wa Mikoko na Uwekaji wa Matuta kuzuiya Mmomonyoko wa Ardhi katika Ukanda wa Bahari.
Eneo ambalo limekumbwa na Tabia nchi katika kilimani likiwa limejaa maji ya pwani 

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake ya kutembelea miradi ya kuhifadhi mazingira Zanzibar akitembelea moja ya mradi huo ulioko kilimani Zanzibar kujionea jinsi ya hali ya uharabifu wa Tabia Nchi katika eneo hilo. 
Ujumbe wa Maafisa wa Mazingira wa Afisi ya Rais Muungano wakitembelea eneo hilo na Naibu Waziri Mhe Luhaga Mpina.

MPANGO MKAKATI WA SEKTA YA AFYA KWA MWAKA 2016/2017.

$
0
0
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya sekta ya afya unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, wadau hao wa Sekta ya afya wanajadiliana mambo mbalimbali na baada ya kumalizika kwa mkutano huo kutakuwa na kusaini makubaliano yaliyofikiwa kwa utekelezaji katika sekta ya afya hapa nchini , Katika picha kulia ni Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania akizungumza katika mkutano huo Kushoto ni Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.
Dk.Ulisubisya Mpoki Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akichangia hoja katika mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Dk. Deo Mtasiwa Naibu Katibu Mkuu wa Afya TAMISEMI akizungumza katika mkutano huo ambao umekutanisha wadau wa afya na kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya afya.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo.

  
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Suleman Jafo wa tatu kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Mwaka 2015 Serikali ya Tanzania ilikamilisha Mpango wa Afya katika Jamii na kuanzisha mafunzo kwa kada mpya za Wahudumu wa Afya ya Jamii (Community Health Workers). Wafanyakazi hawa wana jukumu kubwa kuifikishia jamii huduma za afya za msingi.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
MPANGO  mkakati  wa Sekta ya Afya  wa  Mwaka 2016 /2017 unahitaji sh.trioni 21 katika kuweza kutekeleza maeneo nane  ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza na wadau wa afya leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali itahakikisha inakwenda sambasamba na mpango huo  kutokana na kugusa kila sehemu ikiwa ni lengo la kumfikia mwananchi wa kuweza kupata huduma ya afya.

Amesema eneo mojawapo ni utoaji wa kinga ya afya kwa jamii pamoja na elimu juu ya magonjwa kwa kuweka wataalam wenye mafunzo kutoka sehemu husika.
Ummy amesema serikali imeanza kutoa mafunzo kwa wafanyakazi 4000 ambao watafanya kazi na jamii moja kwa moja katika utoaji wa kinga ya afya pamoja na elimu juu ya magonjwa mbalimbali.
Amesema katika eneo la pili ni mgawanyo wa rasilimali fedha kwa kuhakikisha kila kituo kinapata fedha na takwimu zake zitahifadhiwa juu ya fedha wanazozipata kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.

Waziri, Ummy, amesema katika eneo la tatu ni juu ya uchangiaji wa huduma ya afya bado ni changamoto hivyo katika mpango wanatarajia kupeleka mswaada bungeni kwa kuwa na mfuko  moja ambao kila mwananchi atachangia kwa ajili ya huduma ya afya.

Aidha amesema katika mpango huo wataangalia watumishi wa sekta ya afya kuwa kila sehemu wanakuwepo katika kuweza kutoa huduma kwa wananchi ipasavyo pamoja na masilahi ya motisha kwa watumishi walio pembezoni.

Waziri Ummy amesema katika eneo lingine katika mkakati huo ni kuweka ufumbuzi wa wa upatikanaji fedha na vyanzo vyake vikaeleka na uendeshaji pamoja na rasilimali watu wanapatikana.
Amesema sehemu ya nane ni utoaji wa nyota  katika vituo vya afya ambavyo vitapimwa kutokana na utoaji wake kwa kuanzia nyota ya kwanza hadi ya nne.

Mkuruegenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria amesema hayo mambo yalikuwa yakisubiliwa kwa muda mrefu na sasa serikali imeamua kuwajibika katika utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi wake.

Amesema kuwa mpango mkakati ukienda kama ulivyopangwa jamii ya kitanzania itaweza kupata huduma bora ya afya kutokana na mikakati iliyomo katika mpango huo.

Dkt. Magufuli apongezwa kwa utendaji wake wa kazi.

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, Dar es Salaam

Kijana Joseph Stanford kutoka Mabatini wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi ambapo ametembea kutoka Mwanza hadi Dar es salaam kwa muda wa siku 25.

Kijana huyo alianza safari yake jijini Mwanza  Januari, 16 mwaka 2016 saa 10:00 alfajiri na ambapo safari hiyo ameihitimisha jijini Dar es salaam Februari 9, 2016 jioni.

“Matembezi yangu ni ya hiari na lengo la kutembea huku ni kumpongeza na kumuunga mkono Rais Magufuli juu ya utendaji wake wa kazi anaoufanya na pia kumshukuru kwa kuunda Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo” aliongeza Joseph.

Hata hivyo, kijana Joseph alisema kuwa katika matembezi yake alikumbana na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa wadhamini katika kufanikisha safari yake ya kumpongeza Rais Magufuli.

Kwa upande wake Wizira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa anatambua uwepo wa kijana huyo na amempongeza kwa hatua hiyo ya kishujaa aliyoionesha.

Mbali na hayo, Kijana huyo ameomba kuwezeshwa kukutana na Rais mstaafu Jakaya Kikwete ili kumshukuru kwa kuthamini na kuibua vipaji vya vijana nchini.

Joseph anaumri wa miaka 20 na pia ni muhitimu wa kidato cha nne mwaka 2015 katika shule ya Sekondari Mtoni iliyopo jijini Mwanza.

Usafi ni jukumu la kila mwananchi

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imesema jukumu la kuzoa maji taka katika maeneo mbalimbali Mjini Kibaha ni la kila mwananchi  na sio kuiachia Halmashauri kazi ya kuwazolea maji taka katika maeneo yao.

Akijibu malalamiko ya wafanyabiashara toka Mjini hapa  kuhusu ukosefu wa gari la kunyonya maji taka katika Halmashauri hiyo, Afisa Habari wa Halmashauri Innocent Byarugaba amesema ni kweli Halmashauri halina gari rasmi la kunyonya maji taka ila wanashirikiana na makampuni binafsi kufanya kazi hiyo.

“Tumeyapata malalamiko hayo toka kwa wafanyabiashara ila nachotaka kuwaambia ni kwamba jukumu la kunyonya maji taka katika maeneo yao ni lao na sio la Halmashauri peke yake hivyo wasilete kisingizio cha Halmashauri kutokuwa na gari la kunyonya maji taka kufungulia maji taka mitaani na katika vyanzo vya maji, huko ni kukiuka sheria na kuendekeza uchafu na tutawachukulia hatua wote watakaobainika”

“ Nawashangaa wafanyabiashara wanaoshindwa kuweka mazingira yao safi kwa kisingizio cha Halmashauri kukosa gari, wakati wao ndio wahusika  na hata wakati wa kupambana  na magonjwa ya mlipuko wao ndio wanaoathirika zaidi, ” alisema Byarugaba.

Byarugaba amesema Halmashauri zinakaribisha makampuni binafsi kuja kuwekeza katika shughuli za unyonyaji  maji taka katika Mji wa Kibaha ili kupunguza athali iliyopo ya utiririshaji maji taka ambao ni hatari kwa afya za wakazi.

Ameongeza kuwa kwa sasa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wanatumia mabwawa ya Shirika la Elimu Kibaha kumwaga maji taka, kutokana na ongezeko la watu Mjini hapo mabwawa hayo hayatoshi tena kwani yalijengwa miaka ya 1960 ambapo wakazi waliokuwa wanatumia walikuwa wachache ukilinganisha na sasa.

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha katika kutatua tatizo hili ilikaa kikao cha Kamati ya kuboresha usafi wa Mazingira chini ya Mwenyekiti  Innocent Byarugaba mwezi June mwaka jana ili kujadili ni kwa jinsi gani wataweza kupata gari la kunyonya maji taka litakalosaidia kupunguza tatizo hilo na kuja na maazimio ya kutengea bajeti ya kununua gari hilo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira Atembelea Ujenzi wa Mtaro Uwanja wa Mnazi Mmoja

$
0
0

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitembelea Ujenzi wa Mradi wa Mtaro katika Uwanja wa Mpira Mnazi Mmoja akiwa katika ziara zake Zanzibar kutembelea Miradi ya Mazingira inayosimamiwa na Muungano.akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni. 
Kijicho cha Kampuni ya Ujenzi Mtaro huo kikiwa kazini katika uchimbaji wa mtaro huo nyambu ya pili pwani ya kizingo Zanzibar. 
Makalbi ya mtaro wa kupitishia maji kutoka katika viwanja vya mpira mnazi mmoja yakitandikwa, na kulia ni mabomba ya mtaro huo ya zamani yaliokuwa yakitoa huduma hiyo ya kupitisha maji kutoka katika uwanja huo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Mhandisi wa Baraza la Manispa Zanzibar Ndg Mzee Khamis Juma akitowa maelezo ya kitaalumu ya Ujenzi wa Mtaro wa maji machafu wakati wa mvua kunyesha   


Mhandisi wa Baraza la Manispa Zanzibar Mzee Khamis Juma akizungumza wakati wa ziara ya Mhe Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina wakati alipofika kutembelea mradi wa ujunzi huo katika uwanja wa mnazi mmoja Zanzibar, kuondosha tatizo wa maji katika uwanja huo unaokuwa kero kutumika kwa kiwanja hicho kipindi cha mvua na kuingia maji ya bahari. 
Mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa maji katika uwanja wa mpira wa mnazi mmoja unaoendelea na ujenzi wa mtaro huo.
Mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa maji katika uwanja wa mpira wa mnazi mmoja unaoendelea na ujenzi wa mtaro huo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akizungumza wakati alipofika katika mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa Maji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar. na kumalizia Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Mazingira kisiwani humo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akizungumza wakati alipofika katika mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa Maji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar. na kumalizia Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Mazingira kisiwani humo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake kutembelea Jimbo la Jangombe kujionea athari za mazingira inazozikabili Jimbo hilo kwa kutokea kwa kuzama kwa nyumba katika mwaka 1998 na baadhi ya nyumba nyengine kupata athari.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake kutembelea Jimbo la Jangombe kujionea athari za mazingira inazozikabili Jimbo hilo kwa kutokea kwa kuzama kwa nyumba katika mwaka 1998 na baadhi ya nyumba nyengine kupata athari.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake kutembelea Jimbo la Jangombe kujionea athari za mazingira inazozikabili Jimbo hilo kwa kutokea kwa kuzama kwa nyumba katika mwaka 1998 na baadhi ya nyumba nyengine kupata athari.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika ziara yake Jimbo la Jangombe Zanzibar.kushoto Meya wa Baraza la Manispa Zanzibar Mhe. Khatib Abdurahan Khatib na Mkurugenzi  Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndg Juma Bakari Alawi.
Sheha wa Shehia ya Jangombe Ndg Khamis Ahmada Salum akitowa maelezo kwa Mhe Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe Luhaga Mpina wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo.
Mhe Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akisalimiana na Wazee wa Jimbo la Jangombe wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo akiwa Zanzibar. 
Eneo lilikozama Nyumba katika mtaa wa Jangombe Mshelishelini mwaka 1998 ambapo amefika Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina wakati wa ziara yake Zanzibar kutembelea Miradi ya Mazingira na ya Muungano ilioko Zanzibar.,
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiwa katika eneo iklikoza nyumba hiyo Jangombe wakati wa ziara yake Zanzibar.
Mwananchi wa Jangombe Nyumba yao ilididimika katika eneo hilo wakati wa Mvua za masika katika mwaka 1998 Ndg Salum Ibrahim Mgaza akitowa ushuhuda wa kuzama kwa nyumba yao kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakati wa ziara yake katika jimbo hilo na kufika katika eneo hilo ilikozama nyumba hiyo katika mwaka 1998 na kubaki kiwanja hadi sasa. 


Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Sheha wa Jangombe wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo kuangaria athari za Mazingira zinazolikabili Jimbo hilo akiwa katika eneo lililotokea shimo wakati wa mvua za mashika na kuleta athari katika eneo hilo.  


Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Sheha wa Jangombe wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo kuangaria athari za Mazingira zinazolikabili Jimbo hilo akiwa katika eneo lililotokea shimo wakati wa mvua za mashika na kuleta athari katika eneo hilo. 
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndg Juma Bakari Alawi akitowa maelezo kuhusiana na hali ya Mazingira katika eneo la Jangombe ambolo linakumbwa na ujaaji wa maji ya mvua na kujitokeza kudidimia kwa ardhi ya eneo hilo, wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina, katika Jimbo la Jangombe kuangalia Miradi ya Maendeleo inayosimamiwa na Muungano Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kufuatia vifo vya ajali ya Simbamtoto na Lori la Mchanga

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



Simu: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi. Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.


Ajali hiyo imetokeo leo tarehe 11 Februari, 2016 majira ya saa 1:15 asubuhi katika eneo hilo lenye mteremko, ambapo basi la Kampuni ya Simbamtoto lilikuwa likisafiri kutoka Tanga kwenda Dar es salaam na Lori lililokuwa limebeba mchanga, lilikuwa likielekea kiwanda cha saruji cha Tanga.


Rais Magufuli amewapa pole Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliofikwa na msiba huo na amewataka kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.


"Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshituko mkubwa, na kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Tanga, napenda kuwapa pole nyingi wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo"alisema Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema pepo, na amewapa pole majeruhi wote 21 walioumia katika ajali hii.


Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wote wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto, kuwa makini watumiapo barabara kwa kuzingatia sheria zote zinazosimamia usalama barabarani ili kuepusha ajali.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam.


11 Februari, 2016

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images