Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

JAJI MKUU WA TANZANIA MHE.OTHMAN CHANDE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI.

$
0
0
Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.
Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini leo jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kutoka kushoto).
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watendaji wa Mahakama, Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo katika viwanja vya Mnazi Mmmoja wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza leo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.

DAR SWIM CLUB MABINGWA WASHINDA MASHINANO YA KUOGELEA YA TALISS

$
0
0
wachezaji na makocha wa timu ya Dar Swim Club wakishangilia baada ya kutwa ushindi wa jumla katika mashindani ya Taliss yaliyofanyika jana kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya Tangangika (IST Upanga) na kushirikisha jumla ya timu tisa.
Celina Itatiro wa Dar Swim Club na Ema Imhoff wa Mwanza wakichuana katika mashindamo ya Taliss kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya Tangangika (IST Upanga) na kushirikisha jumla ya timu tisa.
waogeleaji waki-dive kwenye maji katika mashindano hayo.
waogelaji wakichuana katika mashindano hayo

…………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Timu ya Dar Swim Club (DSC) imeshinda mashindano ya kuogelea ya Taliss baada ya kuzipiku klabu nyimgine nane zilizoshiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule yaKimataifa ya Upanga.
Dar Swim Club ilijikusanyia pointi 2,421 katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu za wanawake na wanaume. Katika mashindano hayo, wanawake wa DSC walikusanya jumla ya pointi 1,526 huku wanaume wakijikusanyia pointu 895 kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa.
Waogelaji wa kike Smriti Gokarn, Celina Itatiro na Maia Tumiotto walichangia zaidi ushindi wa timu hiyo kwa kukusanya pointi nyingi na akwa upande wa wavulanai walikuwa Matt Golembeski, Marin De Villard na Carter Golembeski.
Nafasi ya pili ilinyakuliwa na wenyeji Taliss kwa kupata jumla ya pointi 2,298 huu waogelaji wao wa kiume, Adil Dharmal na Oliver Mclntosh wakiongoza kwa kuchangia pointi nyingi katika ushindi huo.
Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Shule ya Kimataifa ya Moshi ambayo ilichanganyika nay a Arusha kwa kupata pointi 1,111 huku waogeleaji wake, Josephine Oosterhuis na Pieter De Raadt wakichangia pointi nyingi.
Timu ya kuoglea ya Mwanza ilimaliza katika nafasi ya nne chini ya waogeleaji nyota Elia Imhoff na Emma Imhoff na kufuatiwa ma shule ya kimataifa ya Morogoro chini ya nyota wake, Dennis Mhini na Charlotte Sanford.
Timu ya Bluefins ilishika nafasi ya sita kwa pointi 553 ambapo waogelaji wake Sahal Harunani alishinda medali ya shaba. Nafasi ya saba ilikwenda kwa timu ya Wahoo iliyokuwa chini ya Ellis Underson na Rania Karume kwa kupata pointi 303 na huku Champions Rise na Kennedy House wakimaliza katika nafasi mbili za mwisho.
Mhasisi wa Dar Swim Club Ferick Kalengela alisema kuwa siri kubwa ya ushindi wao ni kujituma na kufanya mazoezi ya kisasa huku Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro akiwapongeza wachezaji wake na kusema huo ni mwanzo tu na makubwa yatafuatia katika kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini.

KITETO WAKABIDHIWA MASHUKA 170

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa juzi na Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, umekabidhi mashuka 170 kwenye zahanati ya Kijiji cha Engusero na hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa ajili ya kutumiwa kujifunika na wagonjwa wanaofika kulazwa.
Mashuka hayo yalikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka na meneja wa NHIF wa mkoa huo Isaya Shekifu, kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika juzi kijiji cha Engusero.
Akizungumza wakati akipokea mashuka hayo Kanali Nzoka aliushukuru mfuko huo na kuzitaka kaya za eneo hilo kujiunga na CHF ili wajipatie matibabu kwa mwaka mzima kwani kaya moja yenye watu sita italipia sh10,000.
Alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.

Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.

Kwa upande wake, Shekifu alisema mwanachama wa CHF atanufaika na huduma zote za afya za msingi za kinga na tiba zitolewazo katika zahanati, kituo cha afya na hospitali ikiwemo huduma za wagonjwa wa kutwa na kulazwa.

Alitaja huduma nyingine ambazo zitatolewa kwa mwaka mmoja kwa kuchangia sh10,000 ni vipimo vya maabara, upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na halmashauri husika na wanachama kupata huduma  bora ya afya.

“Pia watapata huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata mapato ya tele kwa tele kutoka serikalini ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya,” alisema.

Ofisa uratibu na matokeo wa CHF, Nicholaus Mwangomo alisema mpango huo ulianzishwa kwa sheria namba moja ya mwaka 2001 sura ya 409 ya sheria ya Tanzania toleo la 2002 wa kaya au familia kuchangia gharama za matibabu kabla ya kuugua.

Mwangomo alisema sababu za kuanzishwa CHF ni kuiwezesha jamii kumiliki huduma za afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi, kuchangia huduma za afya kwa wananchi na kuboresha huduma za matibabu kwa utaratibu rahisi.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUDHURIA IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI MKUU WA KKKT TANZANIA ASKOFU SHOO MJINI MOSHI.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Baadhi ya waalikwa walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala la ada elekezi linaendelea kufanyiwa kazi na Serikali na likifika hatua nzuri litahusisha wadau wote ili kupata maoni yao.

Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Januari 31, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumuingiza kazini Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Onaeli Shoo iliyofanyika kwenye usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Dk. Shoo ambaye alisema kama Serikali inataka kuondoa ada elekezi haina budi kuziimarisha shule zake ili ziwe kama zilivyokuwa zamani.

Akijibu hoja kuhusu miundombinu ya reli, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua miundombinu hiyo na kwamba hivi sasa inafanya mapitio ili kujua gharama halisi kwa maeneo husika. Alisema Serikali imepanga kuanza na maeneo manne ambapo la kwanza alilitaja kuwa ni reli ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza – Tabora – Kaliua – Mpanda hadi Karema.

“Eneo la pili ni reli ya ukanda wa Kaskazini ambayo itatoka Dar es Salaam – Tanga – Arusha hadi Musoma. Ya tatu ni ya kutoka Tabora – Kahama – Kigali (Rwanda) na kuishia nchini Burundi ambayo tunataka isaidie kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam. Reli ya nne ni ile ya kutoka Mtwara kupitia Tunduru kwenda Songea hadi Mbamba Bay,” alisema.

Kuhusu ulinzi wa demokrasia ndani ya Bunge, Waziri Mkuu alisema anakubaliana na Askofu Dk. Shoo juu ya mihimili yote mitatu kuheshimiana na kwamba ameshukuru kwamba ameonya juu ya lugha zinazotumika ndani ya Bunge.

“Bunge ni eneo linaloweza kujenga jamii mpya kwa sababu Bunge ni kioo na jamii ya Watanzania inatuangalia sisi tuliomo mle. Ni vema tuwe na lugha nzuri, tabia njema na hata jinsi tunavyovaa ili wanaotuona wapate hamu ya kuiga,” alisema.

Kuhusu ombi la kuibuliwa upya mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alisema suala hilo amelichukua na anaenda kulifanyia kazi. “Nakuhakikishia Baba Askofu ushauri ulioutoa kwa Serikali tumeupokea,” alisisitiza.

Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Shoo alisema Bunge ni nyumba ya demokrasia kwa hiyo jamii inatarajia kuona hoja zikijadiliwa kwa haki na amani badala kutumia ubabe na mabavu au nguvu ya dola.

“Nimewaona baadhi ya wabunge mko hapa… hili ninalolisema ni lenu na linawahusu ninyi na spika wenu. Wabunge tunzeni heshima yenu na Mungu awasaidie kulitimiza hilo. Wewe Waziri Mkuu ni Msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni kwa hiyo una kazi ya kusimamia. Kila mhimili unapaswa utunze heshima yake…,” alisisitiza.

Kuhusu Katiba mpya, Askofu Dk. Shoo alisema Watanzania wengi wana kiu ya kuona mchakato huo ukiibuliwa upya na kukamilishwa ili nchi ipate Katiba mpya yenye kukidhi kiu ya watu wake na inayoheshimu matakwa ya wengi.

“Mchakato huo ukianza utumike kuganga majeraha yote yaliyopita. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali ya Awamu ya Tano kuipelekea nchi yetu kule ambako imedhamiria. Yote yanawezekana tukitaka na tukipenda,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Askofu ambaye amemaliza muda wake wa kuliongoza kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa alisema anamshukuru Mungu kwa kupata kibali cha kushuhudia Mkuu mpya wa kanisa hilo akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwake.

“Si kwa akili na uwezo wangu bali ni kwa uweza wa Mungu kwamba nimeweza kuishuhudia siku ya leo. Ninamuomba Mungu akusaidie kuongoza kanisa hili, akusaidie kukemea na kuonya kwa upole. Najua Mungu atakupunguzia hata marafiki kwa sababu ya matamshi utakayokuwa ukiyatoa, lakini si wewe bali ni uweza wa Bwana na roho mtakatifu anayekuongoza,” alisema.

Aliahidi kuendelea kuwaombea Rais Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa katika majukumu waliyonayo. “Msiogope kwa ajili ya majukumu mliyopewa, msihofu tunaendelea kuwaombea kwa sababu tuko pamoja na sisi ni sehemu ya utumishi wa Taifa,” alisema.

Waziri Mkuu anarejea Dodoma jioni hii kuendelea na vikao vya Bunge.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA MASUALA YA USALAMA BARANI AFRIKA.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong walipokuta katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, leo Januari 31,2016 kwenye Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, katika mazungumzo yao Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa yenye mipango ya Maendeleo ya Viwanda kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa Bw. Li Yong baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo Januari 31,2016 katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.(Picha na OMR)

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amtembelea Rais Mstaafu Mkapa.

$
0
0
 
Picha mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa. Rais Dkt. Magufuli alikwenda kumsalimia Rais mstaafu Mkapa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Picha na IKULU.

BEI YA MADAFU HII LEO.

BENKI YA CRDB YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA BUNGE.

$
0
0
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
BENKI ya CRDB imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa wabunge wa Jamhuri la Muungano wa Tanzania.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Mkurugenzi wa benki ya CRDB Tawi la Dodoma, Rehema Hamis na kupokelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni jezi seti mbili ikiwamo ya golikipa, viatu, mpira, soksi na suti za michezo ambavyo vimegharimu zaidi ya Sh. Milioni 5.

Awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliwapongeza wafadhili na wadhamini wanaojitokeza kusaidia sekta ya michezo na kuwataka wengine waige mfano huo, kwani hivi sasa michezo ni uchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka makao makuu ya CRDB anayeshughulikia Mikakati na Ubunifu, Goodluck Nkini, alisema wameamua kutoa vifaa hivyo kutokana na mapenzi yao kwa wananchi hususan wateja wao, ambao wabunge ndio wawakilishi wao.

“Pia ni katika mpango wa taasisi kuunga mkono katika kazi, kwani michezo mbali ya burudani hujenga afya, hivyo wabunge na wafanyakazi wa CRDB wakiwa na afya njema watatekeleza vema majukumu yao,” alisema Nkini. 

Jioni ulipigwa mchezo wa kirafiki kati ya Bunge FC na CRDB kwenye Uwanja wa Jamhuri na kumalizika sare ya bao 1-1.

Walikuwa ni CRDB walioanza kuzifumania nyavu za Bunge FC dakika ya 49 mfungaji akiwa Faisal Mbuya.

Bunge FC walicharuka na kuwachukua dakika sita tu kuchomoa dakika ya 55 kwa bao la Yusuf Gogo. Hadi mwamuzi Peter Mdachi akipuliza kipenga kuashiria dakika 90 kumalizika, hakuna aliyeibuka mbabe. 
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis kwa ajili ya timu ya soka ya Bunge. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Naibu Spika Dk. Tulia Akson, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea viatu vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis kwa ajili ya timu ya soka ya Bunge. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Naibu Spika Dk. Tulia Akson, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini. 
Waziri Mkuu akipokea mpira.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB, Daniel Shemdoe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Benki ya CRDB pamoja na maofisa wa benki hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis akimsiliza kwa makini Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa benki, hiyo, Willy Kamwela.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi yao na Wabunge.
Wachezaji wa CRDB wakiwa katika mazoezi kabla ya mchezo wao.
Baadhi ya wachezaji wa Benki ya CRDB wakitoka uwanjani.
Wachezaji wa Bunge FC wakiwa katika mazoezi.
Naibu Spika Dk. Tulia Akson akikagua timu ya Benki ya CRDB.
Naibu Spika Dk. Tulia Akson akikagua timu ya Bunge.
Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Benki ya CRDB.
Kikosi cha timu ya Bunge.
Kikosi cha timu ya Benki ya CRDB.
Nahodha wa timu ya Bunge, William Ngeleja (kushoto), akichuana na mchezaji wa Benki ya CRDB, Chande Ismail katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Nahodha wa timu ya Bunge, William Ngeleja akimiliki mpira. Kulia ni Chande Ismail.

Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto akimiliki mpira.

SERIKALI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA.

$
0
0
Naibu waziri afya Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi Maelezo

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
SERIKALI imejipanga kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kuwawezesha kila mwananchi kupata Bima ya Afya itakayosaidia kupata huduma bora za afya katika zahanati na hospitali mbalimbali.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Faida Mohammed Bakar(CCM) lililouliza kuwa bado kuna ukiukwaji wa huduma za afya, haki za afya na haki za uzazi katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya wakati wa maswali na majibu,Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kuhakikisha kuwa haki hizi zinapatikana,Serikali kwa kupitia mifumo yake, ikiwa ni pamoja na mabaraza ya weledi, kurugenzi ya uhakiki na ubora wa huduma za afya na idara mbalimbali zilizo chini ya Waziri zinatoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusiana na haki za wateja.

Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kutekeleza hili, vituo vyote vya kutolea huduma za afya vina masanduku ya maoni na ofisi za malalamiko ambazo ni sehemu muhimu ambapo wateja wanaweza kupeleka malalamiko yao ili hatua zaidi zichukuliwe kukomesha na kutokomeza ukiukwaji wowote wa haki za wateja.

“ Tutawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukiuka haki za wateja kwa kupitia baraza la wauguzi na wakunga ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazostahili ili kuokoa maisha ya wananchi hasa maisha ya mama na mtoto” Alisema Mhe.Kigwangalla.

Aidha Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema Wizara yake imeandaa rasimu ya Sheria ya Bima ya Afya ambayo itamuwezesha kila mwananchi kupata bima ya afya itakayomsaidia kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.


Serikali kupitia Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee inatoa mafunzo kwa Wakunga wa Jadi ambao wamekuwa wakitumika sana sehemu ambazo huduma za afya zipo mbali ili kuwezesha wananchi hao kupata huduma bora za afya kutoka kwa wakunga hao hasa katika afya ya mama na mtoto.

SERIKALI KUJENGA VYUO VYA VETA KILA WILAYA.

$
0
0
Waziri Elimu Wazira wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akijibu maswali kutoka kwa wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO


Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi inatarajia kujenga Vyuo vya Ufundi (VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi wengi hususani vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa.

Akijibu swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo wakati wa maswali na majibu, Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo Cha VETA sio kwa wilaya ya Chunya tu bali kwa Wilaya zote nchini, tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo cha VETA ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika katika vyuo hivyo.

“ Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema Mhe.Manyanya.

Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara moja.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini ili kuwawezesha wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

DAWATI LA MSAADA (HELP DESK)

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YAWAKOMBOA WANAWAKE WA ZANZIBAR KIUCHUMI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser .
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake  hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza  namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.
Washiri wa mafunzo hayo..
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza  washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.
  
Baadaye mtaalamu wa maswala ya urembo na matumizi ya sahihi ya vipodozi Mama Shekha Nasser atatoa ujuzi wa matumizi ya vipodozi pendwa vya LuvTouch Manjano, mfano kupamba maharusi na utunzaji wa ngozi.
Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Zanzibar waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamlai .

Mwisho wa mafunzo haya washiriki wote watakopeshwa mitaji kwa ajili ya kuanzisha na  kuendesha biashara zao. Katika hatua nyingine washiriki wa mafunzo hayo waliojitokeza kwa wingi wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwakomboa na mafunzo ya kiuchumi na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.

BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA EDWARD LOWASA LATEKETEA KWA MOTO

$
0
0
 
Na Woinde Shizza,Arusha.

Bweni  la  wanafunzi  katika  shule  ya  sekondari  ya Edward Lowasa  iliyopo  wilayani Monduli mkoani  Arusha limeteketea  kwa  moto  na  wanafunzi  zaidi  ya 70  wa  kidato  cha kwanza wamelazimika  kupewa  likizo ya  wiki  moja  baada  ya  vitu vyao kuteketezwa na moto ikiwemo magodoro,nguo pamoja na vitabu . 

Mwalimu  mkuu   wa  shule  hiyo  Salum Selemani   alisema  moto  huo  ambao umetekeza  mali zote  za  wanafunzi  na  majengo  unaodaiwa  kusababishwa  na  hitilafu  ya umeme  za  ulianza  saa  nne  usiku  wakati  wanafunzi  wakiwa  darasani wanajisomea   na hakuna  aliyejeruhiwa  japo baadhi  yao   walikumbwa  na hofu  iliyosababisha   wapoteze  fahamu na  kukimbizwa   hosipitali .

Salum amesema kuwa kwa sasa chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme ingawa bado uchunguzi zaidi haujafanyika kubaini chanzo cha moto huo licha ya kujiridhisha kuwa wanafunzi wanapokua shuleni hapo hawatumii simu wala chombo chochote cha moto kwa maana ya kiberiti au mshumaa.

Mwenyekiti  wa  kamati  ya ulinzi  na  usalama ya wilaya ya monduli  ambaye  pia  ni  Mkuu  wa Wilaya  Bwana Francis   Miti  Alisema    wanafunzi  wote  wako   salama  na  wamefikia  hatua ya kuwapa  likizo  fupi ili  waweze  kutulia    wakati  jitihada  kuwawezesha  kuendelea  na  masomo zikifanyika  .

Mwenyekiti wa  Halmshauri  ya  Wilaya  ya  Monduli  Issack  Joseph  na Mbunge wa  jimbo la Monduli  Bwana  Julius Kalanga  alisema kuwa kwa sasa wako kwenye mpango wa kuhakikisha kuwa wanatafuta magodoro na mahitaji muhimu ya kujenga bweni hilo ili wanafunzi waweze kurejea masomoni.
Kalanga amesema kuwa kumekua na matukio ya kujirudia rudia ya shule kuungua moto hivyo walimu ,wazazi na wanafunzi wanapaswa kukaa pamoja na kujadili namna ya kudhibiti matatizo yanayosababisha moto huo pamoja na kuhakikisha kuwa vyombo vya kudhibiti moto (fire extinguisher) vinafungwa kwenye kila jengo la serikali.

Alisema juhudi za serikali,mashirika na watu binafsi zinahitajika kuhakikisha kuwa bweni jipya linajengwa na wanafunzi wanarejea katika masomo licha ya kuunguliwa na vifaa mbalimbali ikiwemo vitabu,nguo ,magodoro pamoja na masanduku.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA LUGOBA WAFAIDI UJIO WA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI WA HALOTEL.

$
0
0
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Lugoba wakiwa Darasani wakijisomea masomo yako wa njia ya Kompyuta.

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata-Bagamoyo mkoani Pwani wamefaidika na kompyuta zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kwaajili ya kusaidia masomo ya TEHAMA shuleni hapo. 

Halotel imetoa msaada wa kompyuta 19 pamoja na kuziwekea mtandao wa intaneti yenye spidi kubwa ya kampuni hiyo bure, kwaajili ya kuwezesha wanafunzi wa shule hiyo kujisomea kwa urahisi. 

Akizungumza na waandishi wa habari Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Lugoba, Abdala Sakasa ameishukuru kampuni ya Halotel kwa kuiangalia shule hiyo kwa jicho la pekee na kuamua kuisaidia kompyuta hizo. 

‘Wanafunzi wa dunia ya sasa ni muhimu waweze kutumia mtandao kujifunza na kupata maarifa mbalimbali tofauti na vizazi vilivyopita, na hivyo tunaishukuru Halotel kwa kusaidia kuwezesha hali hii’ alisema mwalimu Sakasa. 

Kwa upande wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugoba, wameushukuru mtandao wa Halotel kwa kuwapa msaada wa kompyuta hizo ambazo zimeweza kuongeza ari na juhudi za kujifunza kupitia kompyuta hizo. 

‘Tunaishukuru kampuni ya Halotel kwa kutujengea darasa la komputa pamoja na kutupa komputa mpya zilizounganishwa na mtandao wa 3G, hali ambayo imeturahisishia kujifunza kwa vitendo masomo ya TEHAMA’ alisema Asha Mohamed, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo. 

Kampuni ya Halotel yenye kauli mbiu ya Pamoja katika Ubora, inalenga kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo vilikuwa havijaunganishwa na huduma ya mtandao wowote wa simu kutoka mwanzo. 

Katika hatua nyingine, kampuni ya Halotel itaweka mkazo wa hali ya juu katika kuboresha mtandao, huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini. 

Ikiwa na kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya minara 2500, Halotel ndiyo kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150, hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya bure kwa shule zaidi ya 450. 




Hadi sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano, kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95% ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwasili Bungeni katika kuanza kikoa cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza sala ya kuliombea Bunge kabala ya kuanza kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akiwasilisha hoja ya Serikali kuhusu Mpango wa Maendeleo mwa mwaka mmoja katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Massauni akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbalawa wakati kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Waziri wa NChi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakati kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifatila kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Hili hapa tamko la serikali dhidi ya wafugaji wanaoruhusu mifugo yao kuwatia hasara wakulima nchini.

WATUMISHI WA AFYA NCHINI WATAKIWA KUACHA KUHUJUMU DAWA ZINAZOPELEKWA KWA AJILI YA WANANCHI

$
0
0
Naibu Waziri maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dkt.hamisi kigwangwala akizungmza na watumishi wa Afya.
Baadhi ya wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)kanda ya kaskazini wakimsikiliza naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo pichani)
Watumishi wa hospitali ya mkoa ya mount meru wakimsikiliza kwa makini dkt.hamis kigwangwala.

watumishi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya naibu waziri.(Habari na picha toka wizara ya afya)

………………………
Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuacha kuhujumu dawa zinazopelekwa kwa ajili ya wananchi na si za biashara kama wanavyofanya

Onyo hilo yamesemwa mwishoni mwa wiki na naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,dkt.hamisi kigwangwalla wakati akiongea na wafanyakazi wa bohari ya dawa(msd)pamoja na wale wa hospitali ya mkoa ya mount meru.

Dkt. Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano yenye kaulimbiu ya “hapa kazi tu”haitawavumilia watumishi wa aina hiyo na kama wapo basi waanze kujipima kabla rungu la dola halijawafikia

Aidha,alisema suala la upatikanaji wa.dawa kwa wananchi na kwa bei nafuu ni moja ya mambo yaliyopewa kipaumbele katika serikali ya awamu ya tano
“Wananchi wanatakiwa kupata dawa sahihi,kwa bei nafuu na kwa wakati,ndo maana serikali imeamua kufungua maduka ya dawa ya ndani ya hospitali,Hii ni moja ya malengo yaliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama cha Malibu”

Hatahivyo aliongeza kuwa katika kudhibiti upotevu wa draws nchini,serikali imeanza kutekeleza uwekaji nembo ya GoT katika vidonge vyote”na mimi nawapa changamoto ya kuweka mkakati wa kuweka rangi Maalum ‘colour code’Kwa dawa zote  zinazokuwa zimenunuliwa na serikali,sambamba na huo mkakati wenu wa nemo Licha ya hivyo aliwataka wakuu wa hospitali,vituo vya afya pamoja na zahanati wasipokee dawa bila kuwepo kwa kamati ya afya ambayo ndio wawakilishi wa wananchi wa mahali husika ili kusiwepo na udanganyifu na kwenda kwenye mfumo usio rasmi pamoja na kuzibandika dawa.zilizopokelewa kwenye mbao.za matangazo Aliitaka bohari ya dawa(msd)kukamilisha uwekaji nembo dawa zilizosalia na wawe na utaratibu wa kusimamia na kukagua kama dawa Za.serikali zimefika.hadi sasa vidonge vipatavyo 65 vimekwishawekewa nembo ya GoT.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA MAZUNGMZO NA RAIS UHURU KENYATA WA KENYA AU ADDIS ABABA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia, Viongozi hao wanahudhuria mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili masuala ya Usalama Barani Afrika ambapo Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.(Picha na OMR).

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA USHINDANI AKABIDHI VIFAA VYA MUZIKI KWA JESHI LA MAGEREZA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akitoa maelezo mafupi kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo ilifanyikia Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam, Januari 29, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja gitaa la muziki ikiwa ni moja wapo ya vifaa vya muziki vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza akijaribisha kupiga gitaa la muziki baada ya kukabidhiwa vifaa vya muziki katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(wa kwanza kulia).
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki ambavyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi la Magereza.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(hayupo pichani).
Baadhi ya vifaa vya muziki venye vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza kama vinavyoonekana katika picha. Vifaa hivyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi hilo(Picha na Kitengo cha Habari, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

MAADHIMISHO YA SIKU YA ARDHI OEVU

$
0
0
 Afisa Wanyamapori  kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick   Lotha akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ardhi oevu Duniani inayotarajiwa kufanyika februari 2,2016 ambapo siku hiyo itatumika kutoa elimu kwa kuwakumbusha watu kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za ardhi oevu. Kulia ni Afisa Habari wa Wizara hiyo Bw. Lusungu Helela, kushoto ni Afisa Wanyamapori Mkuu na Mratibu Kitaifa wa Uhifadhi Ardhi Oevu Bw. Pellage Kauzeni.

 Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Mali Asili  na Utalii Bw. Pellage Kauzeni akitoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya ardhi oevu kushirikiana na Serikali katika kuyatunza maeneo hayo kushoto ni Afisa Wanyamapori  kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii Bw.Sadick Lotha na kulia ni Afisa Habari wa wizara hiyo Bw. Lusungu Helela.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatlia mkutano wa Wizara ya Mali Asili na Utalii uliolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maadhimisho ya siku ya ardhioevu ambayo huzuia mmomonyoko wa udongo kwenye fukwe unaoweza kusababishwa na mawimbi ya bahari.( Picha zote na Frank Mvungi )


Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images