Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 749 | 750 | (Page 751) | 752 | 753 | .... | 1903 | newer

  0 0

  katanga
  Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO.
   
  Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa sheria wanatarajia kutoa elimu ya sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
   
  Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga alipokuwa akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo.
   
  ‘’Natoa wito kwa wananchi kuhudhuria maadhimisho ya siku ya sheria nchini yanayoashiria kuanza mwaka mpya wa shughuli za mahakama”Alisema Kattanga.
   
  Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “huduma za haki kumlenga mwananchi:wajibu wa mahakama na wadau”
   
  Ameongeza kuwa,miongoni mwa wadau watakaoshiriki katika kutoa elimu ya sheria ni pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Taasisi ya Sheria kwa Vitendo Tanzania (Law School), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,Takukuru pamoja na Polisi.
   
  Aidha Kattanga amesema kwamba wadau hao watatoa huduma za kisheria na kimahakama kwahiyo wananchi wenye mashauri ya muda mrefu,malalamiko yoyote na mapendekezo ya uboreshaji wa utendaji kazi wa mahakama wafike na kuonana na waheshimiwa Majaji, Mahakimu,Wasajili na Watendaji wa Mahakama.
   
  Maadhimisho hayo hufanyika nchini kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa pili ambapo kwa Jiji la Dar es salaam inatarajia kufanyika tarehe 31 Januari hadi Februari 3.

  0 0

  Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, Gabriel Nderumaki akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es Salaam jana kilichokuwa kinajadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016.Kulia ni Katibu wa baraza hilo, Shafii Mpenda.
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiL
  Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, Gabriel Nderumaki akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es Salaam jana kilichokuwa kinajadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016.Kulia ni Katibu wa baraza hilo, Shafii Mpenda.
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.eo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
  Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.

  0 0

   Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib (Kushoto) akkabidhi fomu ya Bima ya Afya kwa Ofisa Uendeshaji wa PPF, Tumgonze KAbigumila baada ya kujaza kwa ufasaha.
   Katibu Mkuu wa SHIWATA, Michael Kagondela (kulia) akisaidiana na wasanii wa SHIWATA kujaza fomu za kujiunga na BIMA ya Afya zinazosimamiwa na PPF.
   Ofisa wa MAsoko wa PPF, Abib Kibiki (aliyesimama) akiwaelekeza wasanii wa SHIWATA kujaza fomu za kujiunga na PPF na nyingine kujiunga na Bima ya Afya.

  WANACHAMA zaidi ya 300 wa Mtandao wa Wasanii TAnzania wamejiunga na Mpango wa TAifa wa Akiba ya Uzeeni (PPF) katika mpango maalum wa Wote Scheme utakaofanya wajiunge na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kupata mikopo mbalimbali.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam wakati wa kuandisha wanachama hao kujiunga na PPF na kujaza fomu za Bima ya Afya, alisema kupitia mpango wa Wote Scheme wanatarajia kuwashawishi wanachama wao zaidi ya 8,000 kujiunga.

  "Tumepokea kwa furaha mpango wa PPF kutunganisha kupata bima ya Afya, tunatarajia wanachama wettu wote wajiunge ili wapate huduma muhimu za matibabu na mikopo mbalimbali kwa maendeleo yao na familia zao" alisema Mwenyekiti Taalib.

  Ofisa Uendeshaji wa PPF, Tumgonze Kabigumila alisema PPF imejizatiti kusaidia jamii ya watanzania kupata huduma muhimu za kijamiii kwa gharama ndogo.

  Alisema katika mpango wa Wote Scheme ujikita kusaidia watanzania wasio katika sekta rasmi kama vile wavuvi, wakulima, wajasiriamali, wanamichezo na wasanii kupata huduma muhimu.

  Alisema kiasi cha chini cha mwanachama kuchangia kwa mwezi ni sh. 20,000 kila mwezi na ataanza kupata matibabu akikamilisha sh. 60,000 ambapo atapewa kadi ya bima ya afya ambayo ataitumia katika hospitali zote nchini kwa magonjwa mbalimbali.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Yuthra Bawaid alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bolo Nchini Ethiopia leo Januari 30, 2016 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa Wakuu wa Nchi za Afrika unaoanza leo mjini Addis Ababa Ethiopia
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride la Heshima kutoka kwa Jeshi la Ethiopia alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwambata wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Nchini Ethiopia Meja Generali John Bishoge alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa Makini mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Mjini Addis Ababa Ethiopia. (Picha na OMR)

  0 0


  Hivi karibuni kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa JWTZ limetoa nafasi za kazi kwa vijana wenye fani ya Udaktari na kuwataka vijana hao kuripoti Makao Makuu na vyeti vyao kwaajili ya usaili.

  Habari hizo si za kweli,JWTZ kama zilivyo taasisi nyingine za serilikali lina mfumo rasmi wa kutangaza habari zake hivyo jeshi linawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizo.

  Aidha JWTZ linawataka wamiliki wa mitandao ya kijamii kutotoa taarifa za jeshi bila kuwasiliana na Makao Makuu ya jeshi kinyume na utaratibu huu,unawasababishia wananchi usumbufu usio wa lazima.

  Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ.

  0 0

  Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Dkt.Hamisi Kigwangala(katikati) akizungumza na viongozi wa hospitali ya Mount Meru mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali hiyo,kulia ni mganga mkuu wa mkoa Dkt.Frida Mokiti kushoto ni Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt.Jackline Urio
  Dkt.Kigwangala akiwa amembeba mtoto mchanga(hajapewa jina bado) wa Bi.Jamila Petro alipotembelea wodi ya wazazi hospitalini hapo
  Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa,Dkt. Kigwangala pia alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali,kushoto ni mtaalamu wa viwango vya maabara,Felix zelote,akimpatia maelezo waziri huyo
  .

  Na Catherine Sungura_ WAMJW_Arusha
  Watumishi wa sekta ya afya watakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu

  Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt. Hamisi Kigwangala wakati akitembelea hospitali ya mount meru mkoani arusha

  Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe Kwa ukusanyaji wa mapato,hivyo ipo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ambao utawafanya watu Wenye pesa kuja kupata huduma kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi

  “Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapo

  Aidha,Dkt.Kigwangala alisema licha ya serikali kupata pesa,watoa huduma pia wakiwemo madaktari,wauguzi pamoja na kada zingine kupata motisha ambazo zitawafanya kuwapa moyo wa kuwahudumia wagonjwa law hali na Mali.

  “Kama matajiri hawaji kwenye hospitali Za umma,mnategemea hawa maskini watapata pesa wapi za kulipia huduma?aliuliza.

  Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma Kwenye vituo vya huduma ya serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma,dawa wala vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko pa kulipia

  “Lengo letu sio kuua hospitali binafsi bali tunataka muimarishe huduma za kulipia ili tupate pesa za kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma was serikali mpate sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
  Servacius Likwelile akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Watakwimu
  Tanzania (TASTA) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa
  Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC). Mkutano huo ulihudhuriwa na
  watakwimu zaidi ya mia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
  MkurugenziMkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
  akizungumza katika MkutanoMkuu wa Chama cha Watakwimu Tanzania (TASTA)
  uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Takwimu
  Mashariki mwa Afrika (EASTC). Mkutano huo ulihudhuriwa na watakwimu zaidi
  ya mia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

  Baadhi ya watakwimu ambao ni wanachama wa Chama cha Takwimu Tanzania (TASTA) wakifuatiliakwa umakini hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.Servacius Likwelile katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Watakwimu
  Tanzania Bara(TASTA) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi
  wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC). Mkutano huo ulihudhuriwa
  na watakwimu zaidi yamia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania
  Bara.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA-NBS)


  SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA TAKWIMU RASMI
  NA EMMANUEL Ghula – NBS

  SERIKALI imehimiza wadau wa Maendeleo, Taasisi na Mashirika mbalimbali kutumia takwimu rasmi katika kupanga, kutekeleza na kutathimni programu za maendeleo.Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Watakwimu Tanzania (TASTA), uliofanyika jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile amesema ni vyema wadau wa maendelo, taasisi na mashirika kutumia Takwimu rasmi ili kupata matokeo bora katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  “Leo mmejumuika hapa pamoja watakwimu kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu kwa lengo la kujadili na kupanga mipango mbalimbali ya chama chenu pamoja na mustakabali wa tasnia ya Takwimu kwa ujumla.

  Takwimu rasmi ni macho katika kupanga, kutekeleza na kutathmini miradi ya kimaendeleo. Natoa wito kwa wadau, taasisi na mashirika mbalimbali kutumia Takwimu rasmi zinazotolewa na watakwimu ili kupata matokeo yaliyo bora katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo,” alisema Dkt. Likwelile.

  Dkt. Likwelile alisema ikiwa upangaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi hautazingatia matumizi ya Takwimu rasmi, kuna athari kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yeyote ile duniani hususani katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs).

  Aidha, alisema kuwa ni vyema wananchi na wadau wengine kufuata Sheria ya takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuanzisha Mfumo wa Takwimu nchini pamoja na kuratibu na kusimamia shughuli zote za ukusanyaji wa takwimu rasmi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa alisema wamekutana kwa lengo la kuboresha na kuimarisha tasnia ya Takwimu na maslahi ya watakwimu.
  “Mkutano huu ni wa watakwimu kutoka Tanzania Bara ambapo tupo hapa kwa lengo la kujadiliana ni jinsi gani tunaweza kuwa na umoja madhubuti na wenye nguvu pamoja na kuimarisha tasnia hii ya Takwimu ukizingatia Takwimu ndio msingi wa maendeleo,” alisema Dkt. Chuwa.

  Alisema kupitia chama cha watakwimu Tanzania wataweza kuifanya tasnia hii kuwa na nguvu pamoja na kuboresha utendaji kazi wa watakwimu katika maeneo yao mbalimbali walipo ikiwemo katika Halmashauri, Wilaya na Mikoa.

  Mkutano Mkuu wa watakwimu Tanzania Bara ulifanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) na kuhudhuriwa na watakwimu zaidi ya mia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.

  Mkutano huo umefanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 28 hadi 29, 2016.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory  Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016.  0 0

  Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara ya kushtukiza. 
  Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia pcha za mionzi (X Ray) katika hosspitali ya rufaa ya Mawenzi. 

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kilimanjaro na kufanya ziara kushtukiza kwenye hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali ya mkoa huo. 

  Waziri Mkuu Majaliwa ambaye mara baada ya kuwasili Ikulu ndogo ya Moshi mjini jana jioni (Jumamosi, Januari 30, 2016) alipangiwa kupokea taarifa ya mkoa huo, alimweleza Mkuu wa mkoa huo kwamba anataka kufanya ziara katika hospitali hiyo na kuwaomba radhi watendaji waliokuwa wanasubiri taarifa ya mkoa iwasilishwe. 

  “Mheshimiwa Waziri Mkuu ameamua kufanya ziara katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi ambayo ni hospitali yetu ya mkoa na atakuja kupokea taarifa ya mkoa wetu tukishatoka huko,” alisema Mkuu wa mkoa huo, Bw. Amos Makalla. 

  Mara baada ya kuwasili hospitalini, Waziri Mkuu alielekeza apelekwe kwenye chumba cha upasuaji (theatre) huku akimuuliza maswali kadhaa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Bingileki Lwezaula. 

  Katika chumba cha upasuaji ilibainika kuwa kuna vyumba vitatu  vya kufanyia upasuaji lakini kinachotumika ni kimoja tu kwa sababu vingine havina dawa za kulaza wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji (anesthesia) licha ya kuwa jengo la upasuaji lina mwaka sasa tangu lilipozinduliwa Februari, 2015 na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. 

  Akiwa katika wodi ya utabibu ya wanawake, Waziri Mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya kukosekana kwa dawa hospitalini hapo. Afisa Muuguzi wa wodi hiyo, Bi. Anjela Mwakalile alisema wametuma maombi ya kupatiwa dawa kutoka MSD lakini bado hazijafika. 

  Hali hiyo ilijitokeza pia kwenye wodi ya watoto. Akizungumza na wazazi wa watoto aliowakuta wamelazwa, mama mmoja alimweleza Waziri Mkuu kwamba sera ya Taifa inasema watoto wachanga hadi walio na miaka mitano wanapaswa kupata matibabu bure, lakini wao hapo hospitalini wanalazimika kununua dawa. 

  Waziri Mkuu alimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako kubadili haraka mfumo wa uagizaji wa dawa baada ya kupokea maelezo ya Dk. Lwezaula kwamba wametuma maombi MSD tangu miezi miwili iliyopita lakini hadi sasa hawajaletewa dawa walizoomba. 

  “RMO ni kwa nini hamuwezi kuagiza dawa nyingi (bulk) kwa magonjwa ambayo mnajua yanajirudia mara kwa mara ili wagonjwa weu wasipate usumbufu? Hii ni hospitali ya mkoa na mgao wa dawa unaopaswa kuja hapa ni wa level ya mkoa? Haiwezekani mnafanya hivyo ili wagonjwa wajinunulie dawa kutoka kwenye maduka yenu?,” alihoji Waziri Mkuu.

  “Hii hospitali ni kubwa kuliko idadi ya wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa na hii ni kwa sababu wengi wao wanaishia kwenye hospitali za wilaya. Kwa hiyo mlipaswa kuwa na dawa za kutosha. Wodini nimekuta wagonjwa wachache katika wodi nilizopita, ina maana mna ahueni hapa… mnao madaktari wa kutosha, wataalamu 12, lakini ni kwa nini hakuna dawa za kutosha?” alihoji. Wakati akitoka wodi ya watoto, kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Hussein ambaye anauguza mgonjwa wake hospitalini hapo alimweleza Waziri Mkuu kwamba dawa pekee wanayopatiwa kwenye hospitali hiyo ni paracetamol tu. 

  “Hapa dawa ya bure pekee unayopata ni paracetamol tu. Dawa nyingine zote unaandikiwa ukanunue maduka ya nje. Na ukizipata ni kati ya sh. 60,000/- hadi 70,000/- kwa mkupuo. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Severine Kahitwa apeleke maombi ya kupatiwa mafundi wa mashine zaxray haraka iwezekanavyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kukuta mashine kubwa kwenye chumba cha mionzi cha hospitali haifanyi kazi na inayofanya kazi ni ndogo haiwezi kufanya baadhi ya vipimo. 
  Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kitengo cha Radiolojia, Dk. Ephraim Minja alisema: “Tuliambiwa spare parts zimekwama bandarini, na vifaa hivyo vikipatikana vitaweza kutatua tatizo lililopo.” 
  Alipoulizwa na Waziri Mkuu kabla ya mashine ya kuharibika alikuwa akihudumia wagonjwa wangapi, Dk. Minja alisema kwa wastani alikuwa akihudumia wagonjwa 60 hadi 70. “RAS fuatilia mafundi kwa Katibu Wizara ya Afya. Hii ni hospitali kubwa tena ya Serikali kwa hiyo haiwezekani wagonjwa waje hapa na kuambiwa waende kupata vipimo mtaani,” alisema.
    
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,


  JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.
  Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Mtumwa mwako. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi. 
  Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo wagonjwa wanahudumiwa. 

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa. 
  Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo. 
  Baadhi ya Viongozi walifika Ikulu ndogo mjini Moshi kwa ajili ya kumsikiliza ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini. 
  Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi. 
  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu Majaliwa. 
  Waziri Mkuu akislimiana na Mstahiki meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya . 

  0 0

  Vijimambo ilizaliwa Januari 31, 2010 na kuzinduliwa Oktoba 23, 2010 na aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar. Picha ni siku ya uzinduzi ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryalnd.
  Hapa Balozi Mwanaidi Maajar akiwa mgeni rasmi miaka 2 ya Vijimambo iliyofanyika Machi 31, 2012 ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryalnd.
  Rais mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyia Julai 6, 2013 katika ukumbi wa Hampton Inn uliopo Capitol Heights. Maryland.
  Mwenyekiti wa Vijimambo akiwapokea wasanii Shilole na Masanja waliokuja kunogesha sherehe ya miaka 3 ya vijimambo.
  Mhe. Nyarandu (kulia) akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo iliyofanyika Septemba 13, 2016 Hotel ya Growne Plaza iliyopo Rockville, Maryland.
  Wasanii Aunty Ezekiel na Cassim Mganga wakija kunogesha miaka 4 ya Vijimambo, kushoto ni NY Ebra akipata ukodak moment na wasanii hao walipotembelea New York City.
  Cassim Mganga na Aunty Ezekiel wakitia saini kitabu cha wageni Ubalozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York siku walipotembelea pande za New York City, kulia ni Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Tuvako Maniongi

  0 0

  Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta hiyo ya doria na kumuua rubani wake raia wa Uingereza katika pori la akiba la Maswa mkoani Simiyu.

  Katika tukio hilo ambalo pia lilimjeruhi askari wa wanyamapori, helkopta hiyo mali ya kampuni ya uhifadhi iitwayo Friedkin Conservation Fund ilikuwa katika doria kwenye pori la uwindaji wa kitalii la Mwiba.

  Tukio hili la majangili kutungua helkopta kwa risasi ni la kwanza kutokea katika historia ya uhifadhi nchini Tanzania na imeelezwa kuwa doria hiyo ilikuwa inafanyika kufuatia milio ya risasi iliyotokea katika eneo hilo la pori la akiba la Maswa ambapo majangili hao walikuwa wameuwa tembo watatu na kuchukua meno yao.

  Waziri wa Maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na amesema Serikali inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na maharamia hao waliotungua helkopta hiyo na kusababisha kifo cha rubani lazima wakamatwe- picha na Vedasto Msungu Technologies.


   Waziri wa Maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwenye tukio hilo.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wafungue shule za michezo yaani Sports Academy ambazo zitalenga kukusanya wahitimu wa shule za msingi na sekondari na kuwafundisha sayansi ya michezo.

  Ametoa wito huo jana mchana (Jumamosi, Januari 30, 2016) kwenye uwanja wa Jamhuri wakati akizungumza na mamia ya viongozi na wananchi mbalimbali walioshiriki mashindano ya mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) zilizofanyika mjini Dodoma. Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI TU HALF MARATHON”.

  “Michezo ni sayansi kwa hiyo tunahitaji kuwafundisha vijana wetu sayansi ya michezo na kuwapa mbinu tofauti za kufaulu kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,” alisema Waziri Mkuu.

  Alisema wapo Watanzania wachache ambao wamethubutu kufungua shule za michezo na kuwataja Filbert Bayi (shule ya Filbert bayi) na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu (shule ya Lord Baden). “Tumeona matunda ya sports academy hizo kwani zimeibua vijana ambao tayari wameshiriki michuano ya kimataifa,” alisema.

  Alisema michezo ina nafasi kubwa ya kulitangaza Taifa la Tanzania na ndiyo maana Serikali imeamua kuimarisha sekta ya michezo, utamaduni, sanaa na habari.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimpongeza kijana Joseph Stanford ambaye ameamua kutembea kwa miguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumuunga mkono Rais Dk. John Pombbe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi.

  Kijana Joseph (19) ambaye alikuwepo uwanja wa Jamhuri, alisema ametumia siku 13 tangu aanze safari hiyo ikiwa ni wastani wa km. 80 kwa siku. “Ninatembea kwa saa 12 kwa siku na ikifika jioni natafuta mahali penye mji na kupumzika,” alisema.

  Joseph ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana katika shule ya sekondari ya Mtoni iliyoko Mwanza-Mabatini, amesema hivi sasa anasubiri matokeo ya mitihani yake lakini ameguswa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ndipo akaamua kuanzisha matembezi hayo ili kumuunga mkono.

  Alipoulizwa anafanyaje anapopita kwenye maeneo ya misitu mikubwa au mapori ya kutisha, Joseph alisema hajakutana na misitu mikubwa ya kutisha isipokuwa kwenye milima ya Sekenke na eneo moja kabla ya kuingia mkoa wa Dodoma.

  Joseph amesema anatarajia kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam kesho kutwa (Jumanne, Februari 2, 2016) kwani anasubiri kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nape Nnauye hapo kesho.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.

  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwasalimia  Wanachama cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara wa Mikoa minne  ya Unguja mara alipowasili katika shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu 
   Baadhi ya Wananchi na Wanachama cha Mapinduzi (CCM) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake katika shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiangalia vijana wa halaiki katika mkutano wa hadhara wa   ya shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi na Wanachama cha Mapinduzi  katika mkutano wa hadhara wa Mikoa minne  ya Unguja shamra shamra za Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
  Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa wakati alipowasili katika uwanja wa Ofisi ya CCM Kisiwandui katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM. Picha na Ikulu.


  Na Ally Ndota, Zanzibar.

  MAKAMO mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM ni kilele tosha cha kupatikana kwa maendeleo katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

  Akizungumza katika uziunduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho katika viwanja vya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, amesema kuwa maendeleo yaliyopatikana katika serikali zote mbili ya Tanzania bara na Zanzibar yamesimamiwa na miongozo, ilana na mikakati mbali mbali iliyotokana na CCM.

  Dkt. Shein alisema kuwa CCM iliyozaliwa mwaka 1977 baada ya kuungana kwa vyama viwili vya ukombozi vikiwemo TANU na Afro shraz party (ASP), chama hicho kimeweza kupigania haki za wanyonge kwa kusimasmisha serikali zenye misingi imara ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wote bila ya ubaguzi.

  “ Serikali nyingi zilizoundwa na vyama vya ukombozi duniani zimeangushwa na wakoloni kwa njia za kiutapeli lakini sisi serikali zetu bado ni imara na zitaendelea kutawala wananchi kwa njia bora na za kidemokrasia.

  Pia ni lazima tuendelee kujitathimini kwa kila jambo nje na ndani ya chama chetu kwani bado kuna changamoto mbali mbali zinazotakiwa kufanyiwa kazi ipasavyo”, alisema Dkt. Shein.

  Aidha Dkt.  Shein aliwasihi wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, ili wapoatikane viongozi wa kuongoza dola kwa mniaka mitano ijayo.

  Dkt.Shein alifafanua kwamba msingi wa uchaguzi wa marudio upo kikatiba kwani uchaguzi mkuu uliopita ulifutwa kisheria na mamlaka iliyokuwa inahusika na usimamizi na uratibu wa uchaguzi huo baada ya kubaini kasoro.

  Akizungumzia mgogoro wa kisiasa uliopo visiwani Zanzibar, Dkt. Shein alisema kuwa ulikuwa utatuliwe kwa njia za mazungumzo lakini kiongozi wa CUF ambaye ni Maalim  Seif Sharif Hamad aliyeomba mazungumzo ya maridhiano kabla hayajamaliza yeye alienda  kutoa siri za vikao kwa waandishi wa habari Dar es saalam  na baadae kuandika barua ya kujitoa katika mazungumzo hayo.

  Aidha aliwataka wananchi kuendelea kulinda Amani na utulivu wa nchi na kuepuka kutumiwa na baadhi ya vyama vya kisiasa kufanya vurugu sizisokuwa na msingi kwa maslahi ya nchi.

  Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa Zanzibar CCM itaendelea kuwa chama cha wananchi wote kinachoongozwa na uzalendo.

  Alisema kuwa mpaka sasa CCM Zanzibar imejiandaa kwa kila hatua katika kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu.
    

  0 0

   Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Polisi , wakisimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana. Imeelezwa kuwa wamiliki wa nyumba hizo walikwisha lipwa fidia na Tanroad lakiwa wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.
   Wakazi wa Buza Sigara wakiondoa mabaki ya mbao baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), kubomoa nyumba hizo.
   Kijana akipita jirani na nyumba iliyobomolewa.

   Tingatinga likiwa kazini.
   Mkazi wa Buza akiondoa mabaki ya mbao baada ya nyumba yake kubomolewa.
   Moja ya nyumba iliyobomolewa.
   Wananchi wakiangalia moja ya Baa iliyobomolewa.
   Watoto wakiangalia zoezi la ubomoaji lilivyokuwa likiendelea.
   Ofisa wa Tanroad akisimamia ubomoaji huo.
   Wananchi wakiangalia zoezi la ubomoaji.
   Tingatinga likiisambaratisha moja ya nyumba iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara eneo la Buza kwa Lulenge.
   Wananchi wakiangalia  ubomoaji huo.
   Tingatinga likifanya vitu vyake bila huruma.
   Askari wa kutuliza ghasia wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni mshereheshaji ajiyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kulia) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikati) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim Ahmed Salim na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.

  Add caption
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (kulia) alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam


  Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.  Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.


  Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.


  Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akichanganya tiketi za bahatinasibu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.


  Vimulimuli vy fataki zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

  ………………………………………………………………………………………………

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Jumuiya ya Wachina wanaoishi nchini wamezindua na kuukaribisha kwa shamrashamra mwaka Mpya wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

  Akizindua shamrashamra hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alisema kuwa Wachina na Watanzania ni ndugu ambao uhusiano wao ni wa kudumishwa milele na milele.

  “Uhusiano wa Tanzania na China ni wa kihistoria ambao ni wa muda mrefu katika mambo mbalimbali ikiwamo kijamii, kiuchumi, kisiasa, kielimu na kiutamaduni Utamaduni na kimawasiliano kati ya nchi hizi mbili” alisema Waziri Nape.

  Kihistoria, uhusiano wa China na Tanzania ni wa kidugu na kirafiki wakati wote iwe wa dhiki au faraja katika maisha ya kila siku kati ya Watanzania na Wachina.

  Ni wakati muafaka kuongeza jitihada za kuimarisha uhusiano na ushirikiano wan chi hizo mbili ili kuwaenzi waasisi wa ushirikiano huo ambao ni Rais Mwalimu Julius Nyerere na Mao Tse Tung.

  Kwa upande wake Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei alisema kuwa wanajisikia faraja wakati wote wanapofanya kazi na Watanzania kwa kuwa wanamengi ya kujivunia katika historia ya nchi hizo.

  Aidha, shamrashamra za mwaka mpya wa Kichina zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Mawaziri Wakuu Wastaafu Salum Ahmed Salum, Mizengo Pinda, viongozi mbalimbali na wenyeji wa sherehe hizo ambao ni raia wa Kichina wanaoishi nchini wakiongozwa na viongozi kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania.

  Mwaka huu unajulikana kama “Ngedere” wakati mwaka 2015 ulijuklikana kama “Kondoo” ambapo maadhimisho ya Mwaka Mpya wa “Ngedere” yalipambwa na michezo mblimbali ikiwemo bahatinasibu, sarakasi, nyimbo, muziki wa ala, mazingaombwe na ngoma.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

  ………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema suala la ada elekezi linaendelea kufanyiwa kazi na Serikali na likifika hatua nzuri litahusisha wadau wote ili kupata maoni yao.

  Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Januari 31, 2016) wakati akizungumza na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumuingiza kazini Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Onaeli Shoo iliyofanyika kwenye usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini.

  Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alikuwa akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Dk. Shoo ambaye alisema kama Serikali inataka kuondoa ada elekezi haina budi kuziimarisha shule zake ili ziwe kama zilivyokuwa zamani.

  Akijibu hoja kuhusu miundombinu ya reli, Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kufufua miundombinu hiyo na kwamba hivi sasa inafanya mapitio ili kujua gharama halisi kwa maeneo husika. Alisema Serikali imepanga kuanza na maeneo manne ambapo la kwanza alilitaja kuwa ni reli ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza – Tabora – Kaliua – Mpanda hadi Karema.

  “Eneo la pili ni reli ya ukanda wa Kaskazini ambayo itatoka Dar es Salaam – Tanga – Arusha hadi Musoma. Ya tatu ni ya kutoka Tabora – Kahama – Kigali (Rwanda) na kuishia nchini Burundi ambayo tunataka isaidie kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam. Reli ya nne ni ile ya kutoka Mtwara kupitia Tunduru kwenda Songea hadi Mbamba Bay,” alisema.

  Kuhusu ulinzi wa demokrasia ndani ya Bunge, Waziri Mkuu alisema anakubaliana na Askofu Dk. Shoo juu ya mihimili yote mitatu kuheshimiana na kwamba ameshukuru kwamba ameonya juu ya lugha zinazotumika ndani ya Bunge.

  “Bunge ni eneo linaloweza kujenga jamii mpya kwa sababu Bunge ni kioo na jamii ya Watanzania inatuangalia sisi tuliomo mle. Ni vema tuwe na lugha nzuri, tabia njema na hata jinsi tunavyovaa ili wanaotuona wapate hamu ya kuiga,” alisema.

  Kuhusu ombi la kuibuliwa upya mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alisema suala hilo amelichukua na anaenda kulifanyia kazi. “Nakuhakikishia Baba Askofu ushauri ulioutoa kwa Serikali tumeupokea,” alisisitiza.

  Mapema, akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Shoo alisema Bunge ni nyumba ya demokrasia kwa hiyo jamii inatarajia kuona hoja zikijadiliwa kwa haki na amani badala kutumia ubabe na mabavu au nguvu ya dola.

  “Nimewaona baadhi ya wabunge mko hapa… hili ninalolisema ni lenu na linawahusu ninyi na spika wenu. Wabunge tunzeni heshima yenu na Mungu awasaidie kulitimiza hilo. Wewe Waziri Mkuu ni Msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni kwa hiyo una kazi ya kusimamia. Kila mhimili unapaswa utunze heshima yake…,” alisisitiza.

  Kuhusu Katiba mpya, Askofu Dk. Shoo alisema Watanzania wengi wana kiu ya kuona mchakato huo ukiibuliwa upya na kukamilishwa ili nchi ipate Katiba mpya yenye kukidhi kiu ya watu wake na inayoheshimu matakwa ya wengi.

  “Mchakato huo ukianza utumike kuganga majeraha yote yaliyopita. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali ya Awamu ya Tano kuipelekea nchi yetu kule ambako imedhamiria. Yote yanawezekana tukitaka na tukipenda,” alisisitiza.

  Kwa upande wake, Askofu ambaye amemaliza muda wake wa kuliongoza kanisa hilo, Dk. Alex Malasusa alisema anamshukuru Mungu kwa kupata kibali cha kushuhudia Mkuu mpya wa kanisa hilo akipokea kijiti cha uongozi kutoka kwake.

  “Si kwa akili na uwezo wangu bali ni kwa uweza wa Mungu kwamba nimeweza kuishuhudia siku ya leo. Ninamuomba Mungu akusaidie kuongoza kanisa hili, akusaidie kukemea na kuonya kwa upole. Najua Mungu atakupunguzia hata marafiki kwa sababu ya matamshi utakayokuwa ukiyatoa, lakini si wewe bali ni uweza wa Bwana na roho mtakatifu anayekuongoza,” alisema.

  Aliahidi kuendelea kuwaombea Rais Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Majaliwa katika majukumu waliyonayo. “Msiogope kwa ajili ya majukumu mliyopewa, msihofu tunaendelea kuwaombea kwa sababu tuko pamoja na sisi ni sehemu ya utumishi wa Taifa,” alisema.

  Waziri Mkuu anarejea Dodoma jioni hii kuendelea na vikao vya Bunge.

  IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,

  JUMAPILI, JANUARI 31, 2016.

  0 0

  NaibuWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Hamis Kigwangalla (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la Dawa la MSD jijini Arusha, ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru.
  Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto0 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkuru.
  Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Mtulia alipowasili duka la MSD Mount Meru, Arusha kwa ajili ya kulizindua rasmi jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw. Cosmas Mwaifwani.
  ………………………………………………………………..

  Na Mwandishi Wetu, Arusha.
  NaibuWaziriwaAfya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, WazeenaWatotoMhe. Dkt HamisKigwangalla amezindua rasmi duka la Dawa la MSD jijiniArusha, ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru na kuiagiza MSD mbali na kuweka alama ya GoT kwenye vidonge vyake iangalie pia utaratibu wa kuweka rangi maalumu kwenye vidonge na vifungashio, ilikurahisha udhibiti wa upotevu na ufuatiliaji wa dawa hizo.
  Naibu Waziri huyo pia amewahimiza watendaji wa MSD kuwa waadilifu, kuwajali na kuwasilikiza wateja na kutumia lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wateja, huku akitoaangalizo kwa wale wanao kiuka taratibuza ajira kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.

  Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhaminiya MSD Prof. IdrisMtulia ameeleza kuwa MSD inaweza kufanya vizuri zaidi endapo changamoto za sheria ya manunuzi, mgawo mdogo wafedha kwa vituo vya Afya, hospitali na zahanati, na mgawo wafedha kuja kwa mafungu zitafanyiwa kazi.

  Naye Mkurugenzi Mkuuwa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa MSD itakuwa na maduka manne tu mkoani Dares Salaam, Mwanza, A Arusha na Mbeya ambapo kwa mikoa mingine MSD wanaafanyama wasiliano na hospitali za mikoa ziwe na maduka ya hospitali wanayoendesha wenyewe na kisha MSD iwauzia dawa na kuwawezesha utaalamu wakuendesha maduka hayo.

  0 0

  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari Mijini Dodoma (Hawapo Pichani) akitoa tamko la Wizara juu ya ugonjwa wa homa ya Zika kushoto ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula. Picha Na Raymond Mushumbusi Maelezo

  ……………………………
  Na Raymond Mushumbusi Maelezo

  Wananchi wa Tanzania watahadharishwa juu ya ugojwa wa homa ya Zika uliripotiwa kutokea katika nchi za Amerika ya kusini hivi karibuni.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mijini Dodoma na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akitoa tamko juu ya uvumi ulioenea kuhusu homa ya Zika iliyoenea katika nchi za Amerika ya kusini.

  Mhe.Ummy Mwalimu amewaasa watanznia kuwa na tabia ya kwenda hospitali kila wanapojisikia dalili za homa na kupima kwani sio kila homa ni malaria kwani dalili za homa ya malaria zinafanana kabisa na dalili za ugonjwa wa homa ya Zika.

  “ Nawaomba ndugu zangu watanzania tuzingatie usafi ili kuzuia mazalia ya mbu kwani ugonjwa huu unatokana na virusi vinavyoenezwa na mbu na hao mbu wanapatikana sana nyakati za asubuhi mchana na jioni hivyo nawasihi kutumia dawa za kuua mbua na vyandarua wakati wa kulala.”

  “Napenda kutoa tamko kuwa ugonjwa huu wa homa ya Zika haujaingia Tanzania na tunawaomba watanzania kuwa makini sana na waripoti dalili zozote ambazo sio za kawaida zitakazojitokeza na mpaka jana kwa taarifa tulizonazo hakuna mgonjwa aliyegundulika kuwa na homa ya Zika” Alisema Mhe.Mwalimu.

  Aidha naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula amesema wamejiandaa kukabiliana na kesi zozote zinatazojitokeza za homa ya Zika na wana mfumo mzuri wa kubaini magonjwa ya mlipuko na pia kuna maabara ya NIMR ambayo inafanya uchunguzi juu ya magonjwa mbalimbali.“ Nawaomba watanzania kutopuuzia dalili zozote za homa na kuamua kujitibia manyumbani au kunywa dawa bila kupima na kujua hiyo homa ni ugonjwa gani kwani yaweza kuwa homa ya Zika” Alisema Dkt Chaula.

  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee wa kushirikiana na Shirika la Afya Dunianoi (WHO) wanafatilia kuhusu ugonjwa huu na watatoa maelekezo ya kuzingatia ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu ila mpaka sasa ugomjwa huu haujaingia Tanzania.

  0 0

  Mkandarasi wa SynoHydo Corporation Ltd akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa Km. 43.65 inaojengwa kwa kiwango cha lami
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimuagiza Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (hayupo pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo (wanaomsikiliza).
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela kampuni ya China Henan International Corporation Group Ltd (pichani) kuwapa mikataba bora ya kazi wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiagiza kuwekwa lami juu ya Daraja la Kola Wilayani Kondoa mkoani Dodoma ili kuanza kupitika na kupunguza usumbufu wa magari wakati wa mvua. (kushoto) ni Meneja ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga (Km.88.8) Eng. Stone Cheng na (Kulia) ni Mhandisi Mshauri wa barabara hiyo.
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika barabara ya Mela-Bonga (Km. 88.8) inayojengwa kwa kiwango cha lami, (Wa pili kulia) ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Godfrey Kombe na (wa kwanza kushoto) ni Eng. Deusdedit Kakoko kutoka TANROADS makao makuu.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya Km. 43.65 ambao ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika kwa asilimia 80.
  Kazi ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Mayamaya-Mela yenye urefu wa Km. 99.35 ukiendelea.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  …………………………………………………………………………………………………….

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewaagiza Makandarasi wa ujenzi wa barabara kutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kwa kuzingatia haki, usawa na taaluma ya mtu kama ilivyoelekezwa kwenye sheria ya ajira hapa nchini ili kuwezesha kazi za ujenzi kukamilika kwa wakati.

  Amesema hayo wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati ambao ujenzi wake umegawanywa katika sehemu tatu ambazo Dodoma-Mayamaya Km. 43.65, Mayamaya-Mela Km. 99.35 na Mela-Bonga Km. 88.8 ili kuharakisha kasi ya kukamilika kwake.

  “Hakikisheni leo hii mnawapa mikataba halali kwa mujibu wa taaluma zao na inayozingatia sheria za Tanzania ili kujega uhusiano mwema wa kiutendaji na hivyo kazi zenu zitakuwa na tija na ubora unaokusudiwa”, amesema Prof. Mbarawa.

  Waziri Mbarawa amekagua madaraja makubwa manne katika barabara hiyo ambayo ni Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 200, Msui lenye urefu wa mita 45, Kingali lenye urefu wa mita 30, na Mela lenye urefu wa mita 30 na kuhimiza kasi ya ujenzi wa madaraja hayo kabla ya mvua za masika.

  Barabara ya Dodoma-Babati ni sehemu ya Barabara Kuu ya Kaskazini (The Great North Road) inayoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town Afrika Kusini.

  “Barabara hii ni kiungo muhimu cha miundombinu ya barabara za Tanzania kwani inaunganisha mikoa maarufu ya kilimo ya nyanda za juu kusini, nyanda ya kati na nyanda ya kaskazini na pia ni kiungo kikuu cha kwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

  Kwa upande wake Eng. Deusdedit Kakoko kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) makao makuu, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wamejipanga kuhakikisha barabara hiyo ujenzi wake unakamilika kwa wakati ili kufungua fursa za kiuchumi na kuunganisha kirahisi mkoa wa Dodoma, Manyara na Arusha.

  “Mheshimiwa Waziri tutaendelea kusimamia mradi huu umalizike kwa wakati na muda uliopangwa na hatutaendelea kuvumilia wale wote wasioweza kumaliza mradi huu kwa wakati”, amesisitiza Eng. Kakoko.

  Waziri Mbarawa amezungumzia umuhimu wa ubora wa barabara zinazojengwa na makandarasi wote nchini kudumu kwa muda mrefu ili thamani ya fedha inayotumika kuwalipa iwiane na huduma inayotolewa.

  Hadi sasa sehemu ya barabara ya Dodoma-Mayamaya (Km. 43.65), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80 wakati barabara ya Mayamaya-Mela (Km. 99.35), ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 52.2 na ujenzi wa barabara Mela-Bonga (Km. 88.8), umekamilika kwa asilimia 45.17 ambapo ujenzi wa barabara yote Dodoma-Babati unatarajiwa kukamilika baadaye mwakani.

older | 1 | .... | 749 | 750 | (Page 751) | 752 | 753 | .... | 1903 | newer