Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

TANGAZO LA KUOKOTWA VITAMBULISHO VYA EDDA MUSHI

0
0
 Picha ya msichana huyo kwenye moja ya vitambulisho vyake.
Mkoba wa mtu anayesadikika kuwa ni wa binti anayetambulika kwa jina la Edda J Mushi (pichani), umeokotwa maeneo ya Kota za Jeshi, Mtaa wa Nzasa, Mwenge jijijni Dar ambapo ndani yake kuna kadi ya benki ya CRDB na NMB, Kitambulisho cha kupigia kura, Kitambulisho cha NHIF huku kukiwa  na kipochi kidogo. 

Yeyote anayemfahamu binti huyu anaombwa ampe taarifa au apige simu kwenda namba 0683214128.

DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR

0
0
DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR


Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limewakamata watu 8 wenye mashamba eneo la Sakoveda mbezi Juu wilayani Kinondoni baada ya kugundulika wakiliibia Maji shirika hilo.


Akizungumza wakati wa operesheni ya mtaa kwa mtaa kuhakiki matumizi sahihi ya Maji kwa watumiaji wakubwa wa Maji eneo hilo, Meneja wa Kawe, Bwn Crossman Makere alisema operesheni hiyo ni mwanzo tu wa kutumbua uovu unaofanywa na watumiaji Maji kwa mgongo wa Ulimaji Mashamba na uuzaji maua ulioshika kasi jijini Dar.


“Dawasco tunajiendesha kwa kuzalisha Maji na kuhudumia wananchi na gharama zote hizo ni kutokana na mapato yanayopatikana ndani ya shirika kutokana na Ankara ya Maji inayolipwa na mteja.


“kwahiyo inapotokea watu wanafanya hujuma za aina yoyote ieleweke kwamba shirika linaingia hasara kubwa ambayo haiwezi kuvumiliwa kwa namna yoyote.

“hivyo basi tumeamua kufanya ukaguzi wa mashamba na bustani zote za mboga ili kubaini ni kina nani wanaohujumu shirika kwa kujiunganishia Maji kupitia njia za panya” Alisema Bwn Makere.


Aliongeza kuwa watu hao 8 wamekamatwa baada ya kupata taarifa toka kwa wasamalia wema juu ya kuwepo kwa maunganishio yaliyofanywa usiku wa manane ambayo yanapeleka Maji kinyemela katika mashamba hayo yenye ukubwa wa ekari zaidi ya 3.


“tumegundua maungio ya Inchi Moja zaidi ya 2 yanayopeleka Maji kwenye mashamba hayo ambayo wanalima zaidi mboga za majani kama mchicha na spinachi kwenye shamba hilo ambapo licha ya kuwataka wahusika wajieleze kuhusu Maji wananyotumia kustawisha mboga hizo hawakuwa na majibu sahihi” alisema Bwana Makere.


Kwa upande wake, Mmoja wa wamiliki wa shamba hilo Bi Rahabu Vicent alisema tangu aanze kilimo hapo alikuta Maji yameunganishwa na hawakujua aliyeunganisha na yeye anategemea zaidi Maji ya Mto unaopita pembeni ya Mashamba yetu hivyo Maji ya DAWASCO anayatumia ila kwa kiasi kidogo.


Watuhumiwa hao walipoulizwa kama wanautaratibu wa kulipa Ankara zao kila mwezi kwa Maji ya Dawasco wanayotumia, Bi Rahabu alisema tangu waanze kutumia Maji hayo hawajawahi kupata bili yoyote toka DAWASCO na hawakufatilia kupata utaratibu wa kulipia kwani hata Mita ya Maji hawana.


Kwa upande wa mjumbe wa serikali ya Mtaa wa Sakuleda Bwn Cwell Mbeye alikiri kufahamu biashara hiyo kufanyika katika eneo hilo na kusema wananchi walishalipigia kelele suala hilo kwani wafanyabiashara hao walisababisha huduma ya Maji katika eneo hilo kukosekana kutokana na wao kuhujumu miundombinu ya Maji katika eneo lao.


‘Tunaishukuru DAWASCO kuja kufanya operesheni hii kwani tunaamini sasa kilio cha wananchi wa eneo hili kukosa Maji kitapungua na sasa huduma hiyo itarudi baada ya wabadhilifu hao kujulikana na miundombinu yao kukamatwa” alisema Bwn Mbeye


Kesi hiyo imefunguliwa katika kituo cha polisi Kawe  na shauri litapelekwa Mahakama ya Jiji kwa ajili ya hukumu.


TANGAZO LA KUOKOTWA VITAMBULISHO VYA EDDA MUSHI.

0
0
Picha ya msichana huyo kwenye moja ya vitambulisho vyake.
Mkoba wa mtuunayesadikika kuwa ni wa binti anayetambulika kwa jina la Edda J Mushi (pichani), umeokotwa maeneo ya Kota za Jeshi, Mtaa wa Nzasa, Mwenge jijijni Dar ambapo ndani yake kuna kadi ya benki ya CRDB na NMB, Kitambulisho cha kupigia kura, Kitambulisho cha NHIF huku kukiwa na kipochi kidogo. 



Yeyote anayemfahamu binti huyu anaombwa ampe taarifa au apige simu kwenda namba 0683214128.

Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kutorusha matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano ya Bunge.

0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni January 27, 2016.
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kutorusha matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano ya Bunge.

Serikali kuanzisha Vyuo vya vya Uvuvi kuongeza ujuzi kwa vijana

0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Serikali imekusudia kuanzisha Vyuo vya Uvuvi katika maeneo yote yanayozungukwa na bahari ili kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kuwawezesha kukuza vipato vyao kwa kujiajiri.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma  na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Tate  Ole Nasha akijibu swali la Mhe. Hamidu Hassan Bolali Mbunge wa Mchinga (CUF) kuhusu umuhimu wa kujenga chuo cha uvuvi mkoani Lindi ili kuwaongezea vijana ujuzi wa kazi hiyo.

Ameongeza kuwa wizara inatambua umuhimu wa kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za uvuvi kilimo na ufugaji  na kwa sasa wizara kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvivu (Fisheries Education and Training Agency (FETA) imeanzisha Chuo cha Uvuvi Mikindani Mtwara kwa lengo la kusogeza huduma ya mafunzo ya uvuvi kwa wananchi hususani vijana walioko ukanda wa kusini mwa Tanzania ukiwamo mkoa wa Lindi.

Mhe.William Tate Ole Nasha amesema uanzishwaji wa Vyuo vya Uvuvi sio kwa maeneo yanayozungukwa na bahari ila kwa maeneo mengine pia ili kuwezesha vijana kupata ujuzi zaidi sio katika uvuvi pekee bali pia katika kilimo na ufugaji, mbali na Chuo cha Uvuvi Mikindani  Mtwara pia kuna vyuo vingine kama vile Chuo cha Mbegani Mtwara  chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 , Chuo cha Kibilizi Kigoma na  Chuo cha Nyegezi Mwanza.

Mbali za Vyuo hivyo serikali imehaidi kujenga vyuo Tanzania nzima ili kuwawezesha vijana  wengi zaidi kupata kupata ujuzi zaidi katika Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ili kuendeleza ukuaji wa sekta hiyo na kuwezesha vijana kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo wanayapata.

Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) itaanza kutoa mafunzo ya uvuvi katika Chuo cha Uvuvi Mikindani ya muda mfupi kwa mwaka 2016/2017 na yale ya Astashahada na Stashahada yataanza mwaka 20017/2018.

MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGE LEO MJINI DODOMA.

0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majalliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama Buneni mjini Dodoma Januari 27, 2016.
 Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa Elimu , Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Joyce  Ndarichako, bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.
  Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo  Nape Nnauye akitoa  kauli Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Bungeni mjini Dodoma January 27, 2016.
 Mwenyekiti wa Bunge, Mtemi Andrew Chenge  akiongoza kikao cha Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016.
aziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016. Kutoka kushoto ni Ruth Mollel wa Viti Maalu Chadema, Hawa Mwinga wa Viti Maalum Cahdema na  Ali Saleh wa Malindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NGEDERE WAKITAFUTA CHAKULA KAMA WALIVYOKUTWA NA KAMERA YETU.

0
0
 Ngedere wakiuangalia mfuko wa plastiki ukiwa umefungwa bila kujua ndani kunanini ngedere hao wakaona wausogelee kwa karibu kama watapata chochote mara baada ya kuufungua mfuko huo.....
 Mmmmmmmmhhhhhhhhhhh............. kumbe!!!!!!!!!
 Ohhhhh ni maganda ya ndizi Ngedere hawakuona tabu sana maganda nayo nikakumbuka wimbo mmoja. Mla ndiziii msaahau yote mla maganda mkumbuka yoteee hahahahaaaa. Jamani Ngedele yupo vizuri hakupotezea alipoona maganda akaona amalizie maganda hivyohivyo.
 Ngedele akaendelea kupekua vizuri katika mfuko huo hahaha ..... ngedere anamalizia vipande vidogo vidogo vya ndizi hata kama mtu kamaliza.......
 Ngedere  hakuona shida nakuamua kunywa maji yaliyopo tuu bila kujali lolote.




SERIKALI KUANZISHA VYUO VYA VYA UVUVI KUONGEZA UJUZI KWA VIJANA

0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
SERIKALI imekusudia kuanzisha Vyuo vya Uvuvi katika maeneo yote yanayozungukwa na bahari ili kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kuwawezesha kukuza vipato vyao kwa kujiajiri.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe.William Tate Ole Nasha akijibu swali la Mhe. Hamidu Hassan Bolali Mbunge wa Mchinga (CUF) kuhusu umuhimu wa kujenga chuo cha uvuvi mkoani Lindi ili kuwaongezea vijana ujuzi wa kazi hiyo.

Ameongeza kuwa wizara inatambua umuhimu wa kuwafundisha vijana mbinu sahihi za kufanya shughuli za uvuvi kilimo na ufugaji na kwa sasa wizara kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvivu (Fisheries Education and Training Agency (FETA) imeanzisha Chuo cha Uvuvi Mikindani Mtwara kwa lengo la kusogeza huduma ya mafunzo ya uvuvi kwa wananchi hususani vijana walioko ukanda wa kusini mwa Tanzania ukiwamo mkoa wa Lindi.

Mhe.William Tate Ole Nasha amesema uanzishwaji wa Vyuo vya Uvuvi sio kwa maeneo yanayozungukwa na bahari ila kwa maeneo mengine pia ili kuwezesha vijana kupata ujuzi zaidi sio katika uvuvi pekee bali pia katika kilimo na ufugaji, mbali na Chuo cha Uvuvi Mikindani Mtwara pia kuna vyuo vingine kama vile Chuo cha Mbegani Mtwara chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 , Chuo cha Kibilizi Kigoma na Chuo cha Nyegezi Mwanza.

Mbali za Vyuo hivyo serikali imehaidi kujenga vyuo Tanzania nzima ili kuwawezesha vijana wengi zaidi kupata kupata ujuzi zaidi katika Kilimo, Uvuvi na Ufugaji ili kuendeleza ukuaji wa sekta hiyo na kuwezesha vijana kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo wanayapata.


Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) itaanza kutoa mafunzo ya uvuvi katika Chuo cha Uvuvi Mikindani ya muda mfupi kwa mwaka 2016/2017 na yale ya Astashahada na Stashahada yataanza mwaka 20017/2018.






SERIKALI YASISITIZA MASHIRIKISHO YA MICHEZO KUZINGATIA UTARATIBU KUZUIA MIGOGORO.

0
0
SERIKALI imetoa wito kwa Vyama,Vilabu na Mashirikisho ya mpira wa miguu kuzingatia na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba zao ili kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza katika uendeshaji na uendelezaji wa soka nchini.

Hayo yamesemwa Leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (Pichani)wakati akijibu swali la Mhe. Khatibu Saidi Haji Mbunge wa Konde (CUF) kuhusu makosa yanayofanywa na  klabu za soka nchini kwa kupeleka mambo ya kisoka katika mahakama  ambapo ni kinyume cha sheria za FIFA.

Mhe. Annastazia Wambura amesema ni kweli kuwa Sheria za FIFA zinakataa mambo yanayohusiana na soka kupekekwa mahakamani hivyo hatua hiyo ya Vyama na Klabu kuzingatia Sheria na taratibu inalenga kuwezesha masuala ya soka kuendeshwa kwa  kuzingatia taratibu na miongozo iliyowekwa na Mamlaka za Michezo huo kwa ngazi mbalimbali.

Aidha amesema hatua hiyo imewezesha mchezo wa soka kuchezwa na kupata  matokeo kwa wakati na hivyo kuepusha mazuio ya mahakama ambayo yanaweza kusababisha usumbufu usio wa lazima kwa washiriki wengine hata kupelekea kufungiwa kwa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF).

Maendeleo ya michezo hapa nchini yanaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo ya mwaka 1967, kama ilivyorekebishwa kwa mujibu wa Sheria Na 6 ya mwaka 1971 lakini bado  Sheria hii inakinzana na Sheria za FIFA ila serikali inafanya mapitio ya Sheria hiyo ili iendane na wakati kwa lengo la kuboresha na kuendeleza michezo nchini.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA UMMA

0
0

MTU MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.
MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA CHILANGA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA AITWAYE EMANUEL NZUNDA [55] ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU AITWAYE MENGO MKISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHILANGA, KATA YA IHANDA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. 

CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI, BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MTUHUMIWA KUWA NA MAHUSIANO NA MKE WAKE AITWAYE TELEZIA AZIMIO [31] MKAZI WA CHILANGA, AMBAYE AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO. 

INADAIWA KUWA, MAREHEMU BWANA EMANUEL NZUNDA [55] ALIPORUDI NYUMBANI TOKA KAZINI HAKUMKUTA MKE WAKE NA HIVYO KUAMUA KWENDA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA NA KUMKUTA MKE WAKE AKIWA NA MTUHUMIWA NA NDIPO UGOMVI UKATOKEA. MAREHEMU ALIFARIKI KUTOKANA NA KIPIGO NA KUTOKWA NA DAMU NYINGI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI KWA UCHUGUZI ZAIDI WA KITABIBU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI MKAZI WA MBIMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NELSON MSHEMWA [54] ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA KENEDY MJELWA [35] MKAZI WA MLOWO.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KIJIJI CHA MBIMBA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. 

CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. DEREVA WA GARI ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA GARI AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

SERIKALI YASEMA HAIJAFUTA VIPINDI VYA BUNGE TBC

0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kwa umma kuwa imefuta vipindi vya shughuli za Bunge kuoneshwa katika televisheni ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) kama zisemazo taarifa zilizozagaa mitaani.

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mose Nnauye wakati akiongea na wananchi moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini kutolea ufafanuzi taarifa za upotoshaji juu ya TBC kufuta vipindi vya matangazo ya vikao vya Bunge.

Mhe.Nape Moses Nnauye amesema Serikali haijafuta vipindi vya Bunge bali ilichofanya ni kubadilisha muda wa kurusha vipindi hivyo kutoka muda wa mchana na kuviweka usiku kwa lengo la kupunguza gharama za kurusha moja kwa moja matangazo hayo ya Bunge na pia kuwapa fursa wananchi zaidi kuangalia na kufatilia yanayoendelea Bungeni kwa kuwa muda wa usiku watu wengi wanakuwa wamesharejea kutoka katika shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Ameongeza kuwa Serikali imechukua uamuzi wa busara katika hili kwani TBC imekuwa ikitumia Sh Billion 4.2 kwa mwaka kama gharama za urushaji wa moja kwa moja wa matangazo hayo , hivyo itasaidia katika kubana matumizi ya shirika hilo kwani fedha hizo hazipo katika bajeti ipewayo shirika bali ni fedha za ndani zinazokusanywa na shirika hilo.

Aidha amesema kuwa sio kitu kigeni kwa Bunge kutotangazwa moja kwa moja kwani kuna baadhi ya mabunge katika nchi nyingine urekodiwa na kurushwa baadae kama kipindi maalum cha Bunge,amezitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni New Zealand, India, Malawi, Lesotho, Uingereza na Singapore.

Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) lilianza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 ila baada ya Serikali kukaa na kujadili kwa kina kuhusu gharama za urushaji wa matangazo hayo moja kwa moja ikaamua kubadili mtindo wa urushaji wa matangazo hayo kutoka matangazo ya moja kwa moja kwa siku nzima kwenda kwenye mfumo wa kuyarekodi na kuyarusha katika kipindi cha LEO KATIKA BUNGE.

KONGAMANO LA UNESCO NA WIZARA YA ELIMU LAMALIZIKA, VIPAUMBELE VYA ESDP VYAPATIKANA

0
0
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zalmira Rodrigues akizungumza wakati wa kufunga kongamano la siku mbili Januari 27, 2016 jijini Dar es Salaam kongamano hilo lilikuwa linajadili vipaumbele kwa miaka mitano ijayo vinavyotakiwa katika kuandaa mpango ili kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua na ubora zaidi ambapo vipaumbele vimepitishwa ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.(HABARI PICHA-NA PHILEMON SOLOMON FULLSHANGWEBLOG)

Wadau wa elimu pamoja na mashirika ya dini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kongamano hilo kumazika.

………………………………

Kongamano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) likisaidiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi limemalizika leo jijini Dar es Salaam baada ya kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.

Alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo waweze kujiajiri.

“Tumethibitisha yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,” alisema Tandari.

Aidha Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.

Aliongeza kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi wanataraji utendaji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.

Nae Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zalmira Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo utakavyofanyika.

Awali Zalmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.

SI KWELI KWAMBA RAIS MAGUFULI KUZURU KENYA KUHUDHURIA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU JARAMOGI ODINGA NA FIDEL ODINGA

0
0
Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii. 

Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanhabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na  ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe. 
Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo! 

Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

MRADI MANJANO DREAM MAKERS WA KUKWAWEZESHA MANAWAKE WAJASIRIAMALI WAINGIA ZANZIBAR

0
0
 Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers waingia Zanzibar. Wataalamu kutoka Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo kuanzia tarehe  1 February 2016 kwenye ukumbi wa  Mtoni Marine Hotel Zanzibar. Wanawake 30 wa Zanzibar watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Wanawake wakazi wa Zanzibar wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kwenda kwa usaili na kujiandikisha siku ya Jumamosi tarehe 30 January 2016 kuanzia saa tatu asubuhi kwenye hoteli ya Mtoni Marine mjini Zanzibar.
Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. 

Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba kwajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea .

Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 759413234

Isamilo, Dar Swim Club zatamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Tallis

0
0
Timu  ya kuogelea ya Isamilo kutoka mkoa wa Mwanza  na Dar Swim Club zimetamba kutwaa nafasi ya kwanza katika mashindano ya  kuogelea ya Tallis yaliyopangwa kuanza Ijumaa Januari 29 na kumalizika Jumamosi Januari 30 kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika ( IST Upanga).

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mwanza jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Kuogelea  ya Mwanza (MSC), Jason Miller alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kutwaa medali za dhahabu katika mashindano hayo amayo yatafanyika kwa siku mbili.

Miller alisema kuwa klabu ya Isamilo ndiyo  inawakilisha mkoa huo katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kushirikisha waogeleaji zaidi ya 400 kutoka klabu mbalimbali  hapa nchini.

Alisema kuwa wamecagua waogeleaji 21 kwa ajili ya mashindano hayo na kwa muda wote walikuwa katika mazoezi makali. “Najua kuna ushindani mkubwa sana katika mashindano , tulifanya mazoezi kwa muda mrefu na kuwashindanisha staili mbalimbali za kuogelea kwa  kuzingatia muda, wote wameonyesha muda mzuri na tupo tayari kwa mashindano,” alisema Miller.

Aliwataja wachezaji wake kwa upande wa wasichana kuwa ni Anna Guild,  Emma Imhoff,  Bridget  Peck,  Rebecca Guild,  Nandi O’Sullivan,  Natalie Mulford,  Sachi Buggana, Sofia Sanchez,  Isobel Sanchez,  Umi Kulthum na  Maisah Pirani.

Kwa upande wa wavulana ni  Matthew Guild,  Elia Imhoff,  Eric Nixon,  Khaleed Razac, Judah Miller, Caleb O’Sullivan,  Delvin Barick, Jack  Peck,  Daniele Imhoff na  Ezra Miller.
Wakati Isamilo ikitamba, klabu maarufu ya Dar Swim Club nayo imetamba kulibakisha taji la mashindano hayo  kutokana na mazoezi ambayo wameyafanya.

Katibu Mkuu wa Dar Swim Club, Inviolata Itatiro alisema jana kuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya kutwaa medali nyingi za zawadi na hasa ukizingatia kuwa waogeleaji wao wana uzoefu wa kimataifa.
Inviolata alisema kuwa hivi karibuni walifanya vyema katika mashindano yaliyofanyika nchini Dubai na kushirikisha waogeleaji kutoka nchi mbalimbali duniani huku wao wakiwa wanashiriki kwa mara ya kwanza.

“Tulishinda medali za dhahabu katika mashindano hayo, waogeleaji wetu wamepata uzoefu mkubwa, naamini watafanya vyema,” alisema Inviolata ambapo jumla ya waogeleaji 50 wataiwakilisha klab hiyo.

Waogeleaji hao ni Meyia Avery, Anna Azzoni, Chinwe Bruns, Joshua Bruns, Isobel Bush, Klaryce Durand, Smriti Gokan, Bailey Golembeski, Carter Golembeski,  Celina Itatiro, Lidia Janik, Ursulla Khimji, Mayli Kiepe, Naaliyah
Kweka, Saffiro Kweka, Lois Scheren, Diya Shah, Maya Somaiya, Niki  Somaiya, Kelya Temba, Maia Tumiotto, Lara Van Den Hombergh  na  Chichi Zengeni ambao ni wasichana.

Kwa upande wa wavulana ni  Timothee Callens, Sebastian Carpintero, Raahi Davda, Jean De  Villard, Marin De Villard, Victoire De Villard, Flore De Villeneuve,  Gaspard De Villeneuve, Luwe De Wet, Joaquim Deering, Lisa Di  Stefano,Josh Golembeski,Matt Golembeski, Peter Itatiro, Jonathan, Lubuva, Adrien Madjitoloum, Reuben Monyo, Emmanuele Moroni, Rodolfo Moroni, Thierry Murunga, Christopher Nikitas, Ishaan Patel, Victor  Richmond, Kees Rodenburg, Neel Ruparelia, Arjun Taylor  na Alessandro Tumiottoends.

Mratibu wa mashindano hayo, Alexander Mwaipasi alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na timu zaidi ya 15 zitashiriki katika mashindano hayo. “Timu nyingi zimetuma majina ya waogeaji wao na zipo tayari kwa mashindano,” alisema Mwaipasi.

Wakabidhiwa jengo la mafunzo na madawati Kilombero

0
0
Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa 5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero
Mke wa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero, Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.

Wananchi wa Kiteto Mkoani Manyara wahamasika kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

0
0
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara, Isaya Shekifu akizungumza kwenye Kijiji cha Engusero Wilayani Kiteto, wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kuchangia mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo kila kaya yenye watu sita wanachangia sh10,000 na kupatiwa matibabu kwa mwaka mzima.
 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka akizungumza kwenye kijiji cha Engusero, wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo katika uzinduzi huo Kanali Nzoka alizichangia kaya mbili za watu 12, shilingi 20,000 ambazo zitapatiwa matibabu kwa mwaka mzima pindi wakiugua.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Mkoa huo Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo kwenye wilaya hiyo ulizinduliwa katika kijiji cha Engusero.

WAKAZI wa Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, wametakiwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili waweze kupatiwa matibabu kwa kuchangia sh10,000 na kupatiwa matibabu mwaka mzima kwa kaya yenye watu sita.

Akizungumza kwenye kijiji cha Engusero wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na CHF, mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka alisema kaya nyingi zikijiunga ndiyo upatikanaji wa dawa unakuwepo.

Kanali Nzoka alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.

Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.

Kwa upande wake, Ofisa uratibu na matokeo wa CHF, Nicholaus Mwangomo alisema kila kaya wilayani humo inapaswa kuchangia sh10,000 za gharama za matibabu ili watibiwe kwa kadi na kuachana na mtindo wa kutibiwa kwa fedha.

“Kaya moja ikilipa sh10,00 inapatiwa matibabu kwa mwaka na isipougua inakuwa imewachangia wenzao watakaougua, kwani hata kwenye bima za magari na pikipiki wasiopata ajali wanawachangia waliopata majanga,” alisema Mwangomo.

Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu alisema mwanachama wa CHF atanufaika na huduma zote za afya za msingi na kinga na tiba kwa zahanati, kituo cha afya na hospitali.

Hata hivyo, ili kudhihirisha kauli mbiu ya awamu ya tano ya hapa kazi tu, Shekifu alikabidhi mashuka 170 ya kujifunika wagonjwa ambapo mashuka 20 yalitolewa kwenye zahanati ya Engusero na mashuka 150 kwa hospitali ya wilaya ya Kiteto.

Shekifu alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa ni vipimo vya maabara, wagonjwa wa kutwa na kulazwa, upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na halmashauri husika na wanachama kupata huduma  bora ya afya kwa mwaka.

“Pia watapata huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata mapato ya tele kwa tele kutoka serikalini ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya,” alisema.

Hata hivyo, ili kudhihirisha kauli mbiu ya awamu ya tano ya hapa kazi tu, Shekifu alikabidhi mashuka 170 ya kujifunika wagonjwa ambapo mashuka 20 yalitolewa kwenye zahanati ya Engusero na mashuka 150 kwa hospitali ya wilaya ya Kiteto.

MAFISADI, WAHUJUMU UCHUMI SASA KUFILISIWA; SERIKALI YATANGAZA

0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, (DPP), Bw. Biswalo Mganga, (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ambao ulimkutanisha yeye, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kutoka jeshi la polisi, (DCI), Kamishna wa polisi, Diwani Athumani, (kushoto), na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), Bw.Alex Mfungo, kwenye makao makuu ya polisi jijiniDar es Salaam, Januari 28, 2016. Katika taarifayao ya pamoja, taasisihizo zimeanza kutaifisha mali za watuhumiwa wa Ufisadi na Uhujumu uchumi na kuwataka wananchi kujitokeza kuwataja watuhumiwa wanaomiliki mali hizo kokote waliko.(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Mkurugezni wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga
DCI Kamishna wa Polisi Diwani Athumani
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo
Kamishna Diwani Athumani akizungumza
Bw. Mfungo, (kulia), akiwa na DPP, Mganga
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na watatu hao
Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akiuliza swali


Bw. Oliver Stolpe, (kushoto) kutoka UNODC ambao ni wadau wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP, akiwa na Mkuu wa Mahusiano Ofisi ya DPP, Bw. Oswald Tibabyekonya wakitoka kwenye mkutano huo

MATUKIO BUNGENI KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA LEO

0
0
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akielezea juu ya ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo ya kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge Mhe.Jenesta Mhagama akieleza juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali mara baada ya kupata taarifa za kuzama kwa kivuko Wilyani Kilombero Mkoani Morogoro watu 30 wameokolewa katiaka ajali hiyo.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akijibu maswali yahusuyo Wizara yake katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi(kushoto) na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi (kulia) wakifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akifatilia shughuli za Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Mbunge wa Ilala (CCM) Mhe. Mussa Hassan Zungu akiuliza swali katika moja ya kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifatilia moja ya kikao katika Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Wabunge wa upinzani wakitoka ndani ya Bunge mara baada ya kuanza kujadili hotuba ya Rais./picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Banki ya NMB yashiriki maonesho ya wadau wa kilimo na Biashara Afrika Mashariki

0
0
Meneja Mahusiano Programu za Wakulima Wadogo wa Benki ya NMB Plc, John Machunda (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (wa pili kulia) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (wa pili kulia) akimuuliza swali Meneja Mahusiano Programu za Wakulima Wadogo wa Benki ya NMB Plc, John Machunda (kushoto) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Meneja Mahusiano wa Kilimo cha Biashara wa Benki ya NMB Plc, Christopher Mwalugenge (kulia) akifafanua maswali mbalimbali kwa wateja waliotembelea Banda la Benki ya NMB Plc katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Meneja Mahusiano wa Kilimo na Biashara wa Benki ya NMB Plc, Hamisi Mmomi (kushoto) akifafanua jambo kwa mmoja wa wateja waliotembelea Banda la Benki ya NMB Plc katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (katikati) pamoja na ujumbe wake wakipata maelezo toka kwa Meneja Mahusiano Programu za Wakulima Wadogo wa Benki ya NMB Plc, John Machunda (kushoto) walipotembelea banda la NMB katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (katikati) pamoja na ujumbe wake wakikaribishwa katika banda la NMB walipotembelea kwenye maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wananchi wakitembelea mabanda anuai katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Pichani ni baadhi ya mashine na magari yanayotumika kwa kilimo wakiwa katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (kulia) akipata maelezo toka kwa mtaalamu wa mashine kubwa na ya kisasa inayovuna, kukoboa na kupakia mpunga na mahindi kwenye magunia huku ikijiendesha yenyewe shambani, mashine hiyo ipo katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (kushoto) akitembelea mabanda mengine katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images