Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 747 | 748 | (Page 749) | 750 | 751 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akizungumza na wadau mbalimbali juu ya kufanikisha uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwenyekiti wa Albino Enteprises of Dar es Salaam Michael Lugendo.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akupokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Albino kutoka Enteprises of  Dar es Salaam, Michael Lugendo leo jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akionesha Stika mara baada ya uzinduzi wa wa Stika maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.

   Sehemu ya maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi waliofika katika uzinduzi wa Stika maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.

  Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, leo jijini Dar es Salaam.

  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)

  KAMANDA wa Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, leo amezindua stika za kutokomeza mauaji kwa watu wenye albinism.

  Kamanda Sirro amesema lengo la stika hizo ni kutoa elimu maeneo yote hasa katika mikoa ya Kanda ya ziwa ambapo mauaji ya albino yamekithiri.

  Amesema stika hizo zitasambazwa nchi nzima kwasababu ipo mikoa mbalimbali bado ina mila potofu za kishirikina ambapo watu wanaamini kuwa akipata viungo vya albino atakuwa tajiri.

  Amesema kuwa kusudi ni kutotoa elimu kwa njia ya stika ni kwamba zitabandikwa katika majumba, maofisini, kwnye magari, madukani, mashuleni, vyuoni, kwenye bodaboda na bajaji na elimu hiyo itamfikia hata yule mtanzania ambaye hana redio na runinga.

  “Tuna kila sababu kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa amani na kuwalinda ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi(Albino.

  “Sisi kama jeshi la Polisi na vyombo mbalimbali vya dola tunawajibika kupata taarifa za wale wanaotafuta viungo vya albino tutahakikisha tunapata taarifa kabla ya tukio halijafanyika,” alisema Kamanda Sirro.

  Amesema jeshi hilo litashirikiana na Viongozi wa Serikali za mtaa, viongozi wa dini zote pamoja na taasisi mbalimbali zenye kutetea haki za binadamu.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya AlbinoInterprises Dar es Salaam, Michael Lugendo, alisema lengo la stika hizo ni kutokomeza mauaji lwa watu wenye albinism na kazi hiyo inahitaji ushirikishwaji wa kila mtu.

  Amesema hapa nchini albino wanakabiliwa na mauaji ya aina tatu ambayo ni mauaji ya kisaikolojia yanayomgusa kila mtu mwenye albinism ambayo yalianza pale vitendo vya kukata viungo vya albino vilipoibuka.

  Kugendo amesema mauaji mengine ni yale yanayosababishwa na saratani ya ngozi ambayo hutokana na ukosefu wa mafuta ya ngozi na vikingia jua kulingana na mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na mauaji ya kukatwa viungo ambavyo jamii jamii kubwa inawatambua hadi sasa wanaofanya vitendo hivyo.

  Hata hivyo aliwataka viongozi wa dini, wanasiasa, wafanyabiashara kuwasaidia michango ili kuwezesha zoezizima la usambazaji stika hizo.

  Pia taasisi hiyo ilimtunuku Kamanda Sirro tuzo ya amani na upendo pamoja na kutoa cheti cha kujali jamii kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  Kamanda Sirro amesema kuwa tuzo hiyo ni mwanzo mzuri kwake na ina mpa moyo wa kuendelea kushirikiana na albino katika kutokomeza mauaji.

  0 0

   Mkuu wa Kituo cha shule ya maadilisho kinacholea watoto waliokinzana na sheria cha Irambo Mkoa wa Mbeya,Bwire Masenena(kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya shule Viatu,Madaftari na vifaa vya michezo,Luninga pamoja na vyakula mbalimbali kwa niaba ya watoto wa chuo hicho jana toka kwa Meneja mauzo kanda ya Nyasa wa Vodacom Tanzania, Emmanuel Sagenge.Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 12/- uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi ya Doris Mollel.

   Meneja mauzo kanda ya Nyasa wa Vodacom Tanzania, Emmanuel Sagenge(kushoto)akimkabidhi Luninga Mkuu wa Kituo cha shule ya maadilisho kinacholea watoto waliokinzana na sheria cha Irambo Mkoa wa Mbeya,Bwire Masenena(kulia) wakati wa hafla fupi jana ya kupokea msaada wa vifaa vya shule Viatu,Madaftari na vifaa vya michezo pamoja na vyakula kwa niaba ya watoto wa chuo hicho, Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 12/- uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi ya Doris Mollel.

  0 0

  IMG_1467

  Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu, Prof. Eustella Bhalalusesa akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP). Kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
  IMG_1499
  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na kongamano hilo la siku mbili linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NACTE jijini Dar es Salaam.
  IMG_1506
  Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Ufaransa, Anton De Grauwe akiwasilisha vipengele mbalimbali vinavyotakiwa kujadiliwa na washiriki wa kongamano hilo katika kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021.
  IMG_1683
  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akiwasilisha mambo mbalimbali muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye Ajenda 2030 ya elimu na mpango wa utekelezaji katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).
  IMG_1666IMG_1683IMG_1591
  Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta (kushoto) akiteta jambo na Maofisa wenzake kutoka UNESCO, Faith Shayo (katikati) na Leonard Kisenha (kulia) wakati kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 likendelea.

  IMG_1570
  Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Bw. Makuru Petro ambaye akishiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO kwenye kongamano hilo.
  IMG_1642
  Mshauri wa Taasisi ya kimataifa ya mipango ya elimu (IIEP)/UNESCO, Barnaby Rooke akielekeza vipaumbele kwenye bajeti ya sekta ya elimu ambayo inahitaji maboresho makubwa ili kuleta mabadiliko kwenye sekta elimu nchini.
  IMG_1596
  Moja ya 'Papers' zilizowasilisha kwa washiriki.
  IMG_1615
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akishiriki kwenye kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za NACTE jijini Dar es Salaam.
  IMG_1738
  Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Joseph Sekiku akitoa maoni kuhusiana na udhaifu wa mipango ya sekta elimu nchini ambayo haitekelezeki wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).
  IMG_1784
  Bi. Helena Reutersward, kutoka Ubalozi wa Sweden kitengo cha Elimu akitoa maoni wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) nchini linaloendelea katika ukumbi wa mikutano NACTE jijini Dar es Salaam.
  IMG_1654
  Pichani juu na chini ni wajumbe walioshiriki kongamano hilo kutoka taasisi mbalimbali za serikali, Wizara ya Elimu, Taasisi za Elimu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  IMG_1539
  IMG_1515IMG_1533


  Na Rabi Hume wa Modewjiblog
  Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua yenye ubora zaidi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limepanga kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara.

  Akizungumzia mpango huo katika kongamano la siku mbili la kutambua vipaumbele vinavyotakiwa katika kuandaa mpango huo wa elimu, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila alisema mpango huo unatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kwa kuanzia mwaka 2017 – 2021 ili kuona ni jinsi gani utabadili elimu ya Tanzania.

  Alisema kupitia kongamano hilo wanataraji kuchagua baadhi ya vipaumbele ambavyo wataona vinaumuhimu zaidi kuanza navyo kwa miaka mitano ya kwanza kwa mpango huo na baadae wataanza utekelezaji wa vipaumbele ambavyo vitakuwa vimepewa kipaumbele na washiriki wa kongamano hilo.

  “Tupo hapa kufanya tathimini ya vipaumbele ambavyo vimeletwa mbele yetu ili tufanyie uchambuzi na tuone ni vipaumbele vipi tutaviweka kwenye mpango wa miaka mitano katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” alisema Mnjagila.

  Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Makuru Petro ambaye ameshiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO alisema katika kuchambua elimu ya Tanzania wamegundua kuwa elimu imekuwa ikishuka na hilo linatokana na kuongezeka kwa wanafunzi wanaosajiliwa kuanza shule huku kukiwa hakuna maboresho ambayo yanafanyika ili kuboresha elimu hiyo.

  Alisema baada ya uchambuzi kufanyika wanafanya tathmini ili kupata matokeo ambayo watajadili kwa pamoja kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka mashirika ya kiserikali na yasiyo ya serikali ili kupitisha vipaumbele ambavyo vitafanyiwa kazi kati ya vipaumbele ambavyo wao waliwasilisha kwa washiriki hao.

  “Elimu ya Tanzania hali sio nzuri tumefanya uchambuzi hata mashuleni hakuna hali nzuri mfano hata Geita tumekuta darasa moja linatumiwa na wanafunzi 80 hadi 100 na hilo ni tatizo na baada ya kuchambua changamoto na kuzifanyia tathmini tunazileta hapa ili tuchague vipaumbele vya kuanza kuvifanyia kazi,” alisema Petro.

  Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Zulmira Rodrigues alisema lengo la kuweka mpango huo ni kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuifanya kuwa bora na iliyo na usawa kwa makundi yote ya jamii kwa matokeo mazuri ya baadae.

  Alisema kuna mambo ambayo yanatakiwa kupewa vipaumbele ikiwepo ni pamoja na ubora wa elimu, fursa za elimu kwa makundi yote katika jamii na kujenga uwezo kwa watendaji ambao wanatoa hiyo elimu kama ni walimu basi wawe wanapewa mafunzo kuendana na wakati uliopo ili kuwa na kitu kipya ambacho kinahitajika kwa wanafunzi kwa wakati huo.

  0 0

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeamua kumpa uanachama wa heshima mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta pamoja na kumzawadia ekari tano za ardhi katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga kwa ajili ya kuanzisha Chuo cha Mafunzo ya soka.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa kikao cha Kamati Utendaji ya Mtandao huo kilichoketi juzi kilifikia uamuzi huo baada ya kufuatilia kwa karibu mafanikio ya Samatta akiwa na Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', TP Mazembe ya Jamhuri ya Kongo na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika hadi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora Afrika.

  Alisema SHIWATA inatoa kiwanja hicho kama zawadi kwa mchezaji huyo kutokana na uwezo wake wa kulitangaza taifa katika medani ya kimataifa katika mchezo wa soka ambako wengine watafuata nyayo zake..

  Taalib alisema taratibu za makabidhiano zinafanywa kwa mawasiliano na baba yake mzazi, Ali Samatta na atakabidhiwa eneo hilo mara baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ambako anakwenda kusaini mkataba na timu ya KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji wa miaka minne.

  SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 inamiliki ekari 300 za kujenga makazi,kumbi za starehe, viwanja vya michezo na nyumba za kuishi katika kijiji cha Mwanzega wilayani Mkuranga na ekari 500 eneo la Ngarambe kwa ajili ya kilimo. 

  Wakati huo huo

  Wasanii wanne maarufu nchini wakiongozwa na Ahmed Olotu 'Chilo' juzi walinogesha tamasha la sanaa na michezo wilayani Mkuranga walipoalikwa kuona sanaa inavyochezwa na wasanii wa wilaya hiyo.

  Mzee Chilo aliyefuatana na Boniface Mwanza Mpango 'King Kikii', Wasanii wa Bongo Movie, Suzan Lewis 'Natasha, Kulwa Kikumba 'Dude' na Asha Salvador walijikuta wakishangiliwa kila mara kwa mara na wasanii wenyeji ambao pia walipiga nao picha.

  0 0

   Waendesha pikipiki wakiwa mbele ya ofisi ya Mkuu wa mkoa.
  ………………………………………………
  Na Vero Ignatus , Arusha.
  Chama cha waendesha bodaboda Jijini Arusha ( UWAPA) chaiomba serikali kutatatua utata uliopo kati ya waendesha bodaboda na waendesha pikipiki za kawaida kwa kuwawekea alama maalumu ambayo itawatambulisha, hii ni kutokana na maandamano ambayo yamefanyika siku ya tar 25./1 /2016 kwani ni kinyume kwakuwa chama hakina taarifa yeyote kuhusu maandamano hayo.
  Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa UWAPA bwana Godlight Rugemalila ambapo amesema ametoa taarifa polisi kutokana na maandamano hayo na amesema jambo walilolifanya siyo sahihi kwa hao walioratibu maandamano hayo ,na amewataka waendesha bodaboda wote kama kuna jambo lolote watalipata ofisini wafuate utaratibu wasikurupuke
   Amesema kuwa yapo makundi ya aina mbili kwa waendesha bodaboda,kundi la kwanza ni walimesajiliwa na UWAPA hawana vituo maalum , kundi la pili ni waendesha pikipiki za kawaida hawa hawajasajiliwa na idadi yao ni kubwa ambao huwaharibia wale ambao wanafanya biashara halali ya kubeba abiria
  Amesema kuwa wao kama UWAPA hawajapanga maandamano walipata taarifa kutoka kwa watu binafsi na walishtushwa kusikia kuna maandamano hayo na ameongeza kuwa wanaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kufahamu ni wakina nani wanahusika kuratibu maandamano hayo . 
  Amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani kama zinavyoelekeza, wawe na leseni, wavae kofia ngumu ,wapaki kwenye vituo vilivyosajiliwa ,amewashauri abiria wanaotumia usafiri huo wachukue bodaboda zilizopo kwenye vituo kwani akipata tatizo lolote ni rahisi yeye kusaidika tofauti na akichukua pikipiki ambayo ameiona barabarani inapita utakosa pa kupeleke malalamiko yako maana kila kituo kina kiongozi.
  Ameainisha waendesha bodaboda waliosajiliwa na wanaotambulika hadi sasa jumla yao ni 2950 ,vituo vilivyosajiliwa 144 na vituo bubu ambavyo bado na vinatazamia kupata usajili ni 55 hivyo amewataka waendesha pikipiki wote wajisajili kwenye chama hii ni kwa faida yao maana watatambulika watasaidika mara wapatapo tatizo na hii itawaepusha kuingia kwenye lawama za mara kwa mara kuwa waendesha pikipiki ni wakwapuaji na wanatumika kwenye matukio ya uhalifu.
   Amehitimisha kwa kusema kuwa UWAPA ni umoja wa wawaendesha bodaboda jijini Arusha na umoja huu ulisajiliwa marchi 2012 na unatambulika kiserikali,lengo ni kuwaleta pamoja waendesha bodaboda na huwa wanapatiwa mafunzo na RTO chini ya kitengo cha usalama barabarani , hivyo amewataka wananchi wafahamu kuwa wapo waendesha bodaboda hawa wanapaki maeneo yaliyoidhinishwa na ni vituo halali na waendesha pikipiki ni yeyeote yule unayeweza mchukua barabarani hana kituo.
  Maandamano hayo yalifanyika kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha wakiwa na madai ya wakimtaka mkuu huyo wa mkoa atoe tamko kuhusu kusumbuliwa kwao na askari wa usalama barabarani .

  0 0

  Group Shot

  U.S Secretary of Commerce, Penny Pritzker; Select Tony Elumelu Foundation Entrepreneurs; Kehinde Yinusa, Evans George, Nosakhare Oyegun, Belema Alagun and Founder Tony Elumelu Foundation, Mr. Tony Elumelu during the panel and roundtable discussion between members of the U.S. Presidential Advisory Council on Doing Business in Africa (PACDBIA) and a diverse community of entrepreneurs hosted by Tony Elumelu Foundation and UBA Plc in Lagos yesterday.
  PO SEC TOE
  Group Managing Director United Bank for Africa (UBA) Plc, Mr. Phillips Oduoza; US Secretary of Commerce, Penny Pritzker; UBA Chairman, Mr. Tony Elumelu during the panel and roundtable discussion between members of the U.S. Presidential Advisory Council on Doing Business in Africa (PACDBIA) and a diverse community of entrepreneurs hosted by Tony Elumelu Foundation and UBA Plc in Lagos yesterday.

  The Tony Elumelu Foundation and United Bank for Africa Plc (UBA) partnered with the United States Department of Commerce to host a panel and roundtable discussion between members of the U.S. Presidential Council on Doing Business in Africa (PCDBIA)and a diverse community of African entrepreneurs.

  The 11 person U.S. delegation, along with representatives of several U.S. government trade and investment-focused agencies, was led by the Honourable Penny Pritzker – U.S. Secretary of Commerce. The Council visited Lagos as part of a fact-finding mission to help inform their upcoming report to President Obama on how to strengthen commercial engagement between the U.S. and Africa, which will result in mutually-beneficial growth.

  The event – titled “Unleashing Africa’s Entrepreneurs: Strengthening the Entrepreneurial Ecosystem to Empower the Next Generation of Africa’s Business Leaders” – brought together American business leaders and Nigerian entrepreneurs to discuss challenges, solutions and innovations in the current African business environment. The event was designed to allow representatives of the U.S. Government to participate in direct and substantive discussions with Africa’s emerging business leaders – an opportunity to engage in a dialogue that has the potential to influence U.S. foreign policy for Africa.

  "President Obama believes, as I do, that the American private sector, working in partnership with the African business community, and African entrepreneurs can help address many of the continent’s most pressing challenges, including creating jobs and opportunity for young people across the continent," said U.S. Secretary of Commerce Penny Pritzker. "I am proud to lead our Administration’s effort to support and empower aspiring entrepreneurs, both in the United States and across the globe."

  UBA Chairman Tony O. Elumelu, through his eponymous Foundation, hosted the delegation, and expressed gratitude for the collaborative approach the Council and U.S. Commerce Department are taking in engaging local entrepreneurs as part of their deliberations.

  “Too often, well-meaning foreign policy-makers develop strategies to help Africans without actually engaging us,” he said. “In order to effectively help or support people, we should ask them what kind of help they want. So, I thank you for doing that with African businesses.”
  For the U.S. Government, this trip begins the Road to GES 2016 – the Global Entrepreneurship Summit; an annual gathering of entrepreneurs at all stages of business development, designed to demonstrate the U.S. Government’s commitment to fostering entrepreneurship around the world.

  Expressly designed to address the needs of and provide opportunities for the next generation of African entrepreneurs, the entrepreneurs in attendance included SMEs supported by UBA Plc, UNCTAD’s EMPRETEC Nigeria Foundation and those selected for the Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP) – a 10-year, $100 million commitment by the Tony Elumelu Foundation to empower the next generation of Africa’s entrepreneurs with businesses that have the potential to generate income and jobs for their nations.

  The Tony Elumelu Entrepreneurs in attendance were selected from the Agriculture, Media & Entertainment, ICT, Transport, Healthcare and Financial Services sectors. Their startups reflect the potential that entrepreneurship holds for spurring Africa's transformation; already, they have begun creating jobs in their local communities and generating tax revenues for governments earning them recognition in both local and international media.

  0 0

  Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhani Ali akiwakaribisha viongozi wakuu wa  Umoja wa Maaskofu Zanzibar kuzungumza na waandishi wa Habari kupinga kuhusika  na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis, wakwanza (kulia) ni Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo Askofu Michael Hafidh na (kati) ni Katibu Mkuu Askofu Dickson Kaganga.
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dikson Kaganga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo  kukanusha kuhusika kwao na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyomuandikia Papa Fransis.
   Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dickson Kaganga katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mnazimmoja.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Agostino Shao akijibu maswali ya  waandishi wa Habari  kwenye  mkutano wa kupinga kuhusika kwao na Barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis. (kushoto) ni Askofu Shayo na (kulia) ni Askofu Dickson Kaganga.PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR


  0 0


  Na Lilian Lundo – Maelezo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Liberatus Sabas amekanusha habari iliyoandikwa na gazeti la Jambo Leo la Januari 27, 2016 lenye kichwa cha habari “Waendesha bodaboda Arusha waandamana.

  Akiongea kwa njia ya simu Kamanda Sabas alisema hakukuwa na maandamano yoyote ya bodaboda jijini Arusha zaidi ya vijana wachache waendesha bodaboda waliojikusanya kwa Mkuu wa Mkoa.

  Kamanda Sabas amesema kuwa, wapo katika operesheni ya waendesha bodaboda ambao wamekuwa wakivunja sheria za barabarani mara kwa mara. Operesheni hiyo ni ya nchi nzima na wameianza Januari 14, 2016.

  “Mpaka sasa tumekusanya sh. mil. 21,330,000 ambazo zimetokana na makosa mbalimbali yanayofanywa na waendesha bodaboda wawapo barabarani, makosa hayo ni kutovaa kofia ngumu, kutokuwa na leseni ya udereva, kubeba abiria zaidi ya mmoja, kutokuwa na kadi za pikipiki na kadi za bima,” alisema Kamanda Sabas.

  Kamanda Salas amesema kuwa wasingeweza kukusanya kiasi hicho cha pesa kwa kipindi hicho kifupi kama askari polisi wangekuwa wakichukua pesa hizo kwa maslahi yao wenyewe, ila wamekuwa wakiziingiza katika vitabu vya Polisi.

  Aidha Kamanda Salas amesema hakuna dereva wa bodaboda anayedaiwa cheti cha udereva bali wametakiwa kuonyesha leseni zao za udereva kwani ndizo zinazothibitisha kwamba wamepitia vyuo vya udereva.

  Kamanda Salas amewataka madereva wa bodaboda ambao bado hawajapitia vyuo vya udereva wakajifunze udereva ndipo waendeshe bodaboda na amewaambia kuwa ili wasikamatwe na askari polisi basi wasivunje sheria za barabarani.

  0 0

  Mwanamitindo wa Tanzania ambaye anafanya kazi za mitindo nchini Marekani, Flaviana Matata amezindua bidhaa za  urembo za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY, amezindua bidhaa hiyo mbele ya waandishi wa habari na kuomba wanawake na watumiaji rangi za kucha  wamuunge mkono kwani ni bidhaa ambayo ipo kwenye soko kwa kipindi hiki kwani kila mwanamke anapenda kupendeza. Kulia ni Afisa mtendaji mkuu wa Shear Illution  Ltd, Shekha Nasser akiwa ni mmoja wa wasambazaji wa  kipodozi cha Kucha ambazo zimezinduliwa leo.
  Wakati huhuo amewapongeza wote waliochangia katika kufanikisha yey kujulikana kimataifa.
  Afisa mtendaji mkuu wa Shear Illution  Ltd, Shekha Nasser  akizungumza na waandishi waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kushirika katika uuzaji wa vipodozi vya kucha ambavyo vitakuwa kikiuzwa katika duka lake.
  Bidhaa za kucha zinazojulikana kwa jina la LAVY  amazo zimezinduliwa na mwanamitindo Flaviana Matata jijini Dar es Salaam leo.
  Bidhaa hizo zitakuwa zikipatikana kwenye maduka mbalimbali na Saluni za Pikasso, Shear Illution  Ltd na Zuri Cosmestics zilizopo jijini Dar es Salam kwa shilingi elfu tano tuu.

  0 0

   
   Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kulia) na  Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu  kwa pomoja wakionyesha bango la modemu mpya ya Airtel wingle wakati wa uzinduzi wa  modemu mpya itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa pamoja na kuunganisha zaidi  ya vifaa 10 kwa wakati mmoja.
   Meneja Uhusiano wa Airtel  Jackson Mmbando (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa  modemu mpya itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa pamoja na kuunganisha zaidi  ya vifaa 10 kwa wakati mmoja. Akishuhudia ni Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu
   Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa  modemu mpya itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa pamoja na kuunganisha zaidi  ya vifaa 10 kwa wakati mmoja. 
  Mwandishi wa habari wa Star TV, Grace Semfuko akikabithiwa modemu yake ya Airtel Wingle na Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu mara ya kuibuka mshindi katika raffle  iliyoendeshwa wakati wa uzinduzi. akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel  Jackson Mmbando.
  Airtel yazindua Modem ya Majabu wingle ambayo ni modem na ni WiFi

  ·         Inakuja na ofa ya 5GB BURE, inauwezo wa kuunganisha zaidi ya vifaa 10.
  ·         Airtel yaleta modem ya maajabu inayoweza kuunganisha zaidi ya vifaa 10 kwa wakati mmoja.

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua modemu mpya ya maajabu itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa kuunganisha vifaa zaidi ya 10 kwa wakati mmoja wakiwa mahali popote nchini

  Modemu hiyo ya maajabu ijulikanayo kama “Airtel Wingle” imelenga kutatua mahitaji ya huduma za kimtandao kwa watumiaji wake ambapo mahitaji ya huduma za intaneti yamekua kwa kasi nchini na kuifanya Airtel kuleta modem hiyo ya maajabu ili kuwahakikishia wateja wake uhakika wa huduma za kimtandaoni kwa  gharama nafuu zaidi  nchi nzima

  Akiongea wakati wa halfa ya Uzinduzi iliyofanyika katika duka la Airtel Expo lililopo jijini Dar es Saalam, Meneja Uhusiano wa Airtel , Bwn Jackson Mmbando allisema “Tunayofuraha kuzindua modemu hii ya kipekee ya Airtel wingle ambayo huduma zake zinaenda sambamba na dhamira yetu ya kuwafikishia wateja wetu huduma za intaneti zenye kasi zaidi na  pia kuwaongezea wateja hao huduma nyingine bora zaidi za Wi-Fi kwa kuwafaidisha wateja wengi kwa modem hiyo hiyo moja wakiwa mahali popote”

  Eliakimu alifafanua kuwa “Bila kujali mtandao unaotumia, modemu ya Airtel Wingle itawawezesha wateja wetu kuunganisha zaidi ya vifaa au watumiaji 10 kwa wakati mmoja na kufaidi huduma ya Wi Fi kwa kasi na urahisi. Modem hii ya maajabu yenye Wi-Fi itaweza kutumika na familia, marafiki kwenye ofisini au popote mara tu inapounganishwa kwenye Laptop au katika sehemu yeyote inayoweza kutumia Modem kama vile kwenye gari, soketi za ndani ya nyumba au Hotelini, Televisheni pamoja vifaa vingine vingi vinavyotumia modem”

  Akiongea kuhusu upatikanaji wa modemu hiyo, Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu alisema, Modem ya Airtel wingle inakuja na ofa kabambe ya kifurushi cha Internet cha 5GB kwa mwezi. Tumejipanga kuendelea kutoa huduma za kabambe zitakazowapatia wateja  thamani ya pesa zao. Modemu hii ya Airtel Wingle itapatikana katika maduka yote ya Airtel nchi nzima na pia itapatikana katika Duka letu la Airtel Expo kwa bei nafuu yaani OFA kuanzia sasa”

  Airtel imezinduzi modemu ya maajabu ya Airtel Wingle ikiwa ni muda mfupi tangu ilipozindua duka lake la kisasa la Airtel Expo jijini Dar es salaam ili  kudhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu unaoendana na karne ya sasa ya mawasiliano huku ikitoa huduma hizo kwa  gharama nafuu zaidi.


  0 0

  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akimkaribisha Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo.
  Balozi akisaini kitabu cha wageni.
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, anayeshughulika na Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndugu Asha-Rose Migiro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa  Nchini Tanzania, Malika Berak, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Mussa Varisanga wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo anawaalika ndugu jamaa na marafiki kwenye dua ya marehemu mama yake RAFIA VARISANGA aliyefariki tarehe 27/12/15, dua itafanyika tarehe 30/1/2016 (Jumamosi) Keko Akida  kilwa road,  saa 7 mchana. Nyote mnakaribishwa.

  0 0

   Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhani Ali akiwakaribisha viongozi wakuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar kuzungumza na waandishi wa Habari kupinga kuhusika na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis, wakwanza (kulia) ni Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo Askofu Michael Hafidh na (kati) ni Katibu Mkuu Askofu Dickson Kaganga.
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dikson Kaganga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo kukanusha kuhusika kwao na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyomuandikia Papa Fransis.
    Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dickson Kaganga katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mnazimmoja.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Agostino Shao akijibu maswali ya waandishi wa Habari kwenye mkutano wa kupinga kuhusika kwao na Barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis. (kushoto) ni Askofu Shayo na (kulia) ni Askofu Dickson Kaganga.

  PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi 

  Serikali imetoa wito kwa Vyama,Vilabu na Mashirikisho ya mpira wa miguu kuzingatia na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba zao ili kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza katika uendeshaji na uendelezaji wa soka nchini.

  Hayo yamesemwa Leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura  wakati akijibu swali la Mhe. Khatibu Saidi Haji Mbunge wa Konde (CUF) kuhusu makosa yanayofanywa na  klabu za soka nchini kwa kupeleka mambo ya kisoka katika mahakama  ambapo ni kinyume cha sheria za FIFA.

  Mhe. Annastazia Wambura amesema ni kweli kuwa Sheria za FIFA zinakataa mambo yanayohusiana na soka kupekekwa mahakamani hivyo hatua hiyo ya Vyama na Klabu kuzingatia Sheria na taratibu inalenga kuwezesha masuala ya soka kuendeshwa kwa  kuzingatia taratibu na miongozo iliyowekwa na Mamlaka za Michezo huo kwa ngazi mbalimbali.

  Aidha amesema hatua hiyo imewezesha mchezo wa soka kuchezwa na kupata  matokeo kwa wakati na hivyo kuepusha mazuio ya mahakama ambayo yanaweza kusababisha usumbufu usio wa lazima kwa washiriki wengine hata kupelekea kufungiwa kwa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF).

  Maendeleo ya michezo hapa nchini yanaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo ya mwaka 1967, kama ilivyorekebishwa kwa mujibu wa Sheria Na 6 ya mwaka 1971 lakini bado  Sheria hii inakinzana na Sheria za FIFA ila serikali inafanya mapitio ya Sheria hiyo ili iendane na wakati kwa lengo la kuboresha na kuendeleza michezo nchini.


  0 0

   Mwambata wa Utamaduni katika Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China Bw. Gao Wei akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano kuelezea maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zitazofanyika Januari 30 mwaka huu jijini Dar es salaam.

  Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Mwambata wa Utamaduni katika Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. Gao Wei hayupo pichani wakati wa mkutano kuelezea maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zitazofanyika Januari 30 mwaka huu jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA ALLY  DAUD -MAELEZO.


  PINDA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA UTAMADUNI WA WACHINA.

  Na Joseph Ishengoma


  Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Jumamosi ijayo (30.01.2016) anatarajia kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kusherehekea mwaka mpya wa Kichina.


  Mwambata wa utamaduni katika ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bwana Gao Wei amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya utamaduni wa Wachina nchini.


  Maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina ni alama muhimu katika utamaduni wa wachina na uadhimishwa kwa wachina kuungana pamoja na familia zao na kufanya shughuli za kitamaduni ikiwemo michezo.


  Bwana Gao Wei amaseme kuwa, maadhimisho ya mwaka huu pamoja na kuwakutanisha jamii ya watu wa China na viongozi mbalimbali wa serikali, yatatoa fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika, kuendeleza urafiki uliopo na kuhakikisha kila upande unanufaika na urafiki huo.

  “Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China pamoja na watu wake tutaendelea kujenga mazingira rafiki kuhakikisha kila upande unafaidika na urafiki wetu,” amesema.


  Bwana Gao Wei ameongeza kuwa moja ya malengo ya maadhimisho hayo hapa nchini ni kutoa ujumbe kuwa jamii ya Watu wenye asili ya China wanakuwa watiifu kwa serikali ya Tanzania na kuleta usawa katika ushirikiano wa kisiasa na biashara.”


  Kwa mujibu wa Mwambata huyo, katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam,  kutakuwepo na michezo mbalimbali ya utamaduni zikiwemo nyimbo, muziki, judo, muziki wa ala, na michezo mingine ya kitamaduni.


  Aidha Bwana Gao Wei ameeleza kuwa mbali na maadhimisho hayo kufanyika Mnazi mmoja, pia yanatarajiwa kuadhimishwa katika miji mingine ya Arusha, Dodoma na Mwanza katika siku tofauti tofauti.China ilianza kuadhimisha sherehe hizo tangu karne ya 12 ambapo kwa mwaka huu, kilele cha sherehe hizo ni February 8, 2016.

  0 0

  Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Tarime Vijijini uliofanyika Novemba 25,2015. Kesi hiyo ilifunguliwa aliekuwa Mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Christopher Ryoba Kangoye akiiomba Mahakama kutengua Ushindi wa Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche aliechaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

  Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG.

  Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa January 19,2015 chini ya Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha leo imeahirishwa hadi kesho January 28,2015 majira ya saa nane mchana itakapotolewa maamuzi yake.
  Mjibu maombi katika kesi hiyo (John Heche) anawakilishwa na Mawakili Tundu Lisu (leo hakuwa Mahakamani) pamoja na Paul Kipeja (alikuwepo Mahakamani).

  Baada ya Kesi hiyo Kuahirishwa, Katibu wa Chadema Mkoani Mara Mwl.Chacha Heche (Pichani Juu anaehojiwa) ameiomba Mahakama kutoa maamuzi ya Kesi hiyo ili kuwapunguzia gharama kwa kuwa ambazo zinajitokeza wakiwa Jijini Mwanza kufuatilia maamuzi ya kesi hiyo.

  Barnabas Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa amesema kuwa wanatarime vijijini wana imani na Mahakama na kwamba kesi hiyo ni sehemu ya changamoto kwa mbunge wao na kwamba wembe ni ule ule wa kushinda kuanzia jimboni hadi Mahakamani.
  Barnabas Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa.
  Paul Kipeja ambae ni Wakili upande wa Mjibu Maoni akizungumza na wanahabari baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kuahirisha kutoa Maamuzi ya kesi ya Kupinga Matokeo Jimbo la Tarime Vijijini.

  Anasema kama ilivyokuwa katika Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Bunda Mjini iliyofunguliwa na Wapiga kura wa Jimbo hilo dhidi ya Esther Bulaya (Mbunge), ndivyo itakavyokuwa hata katika Jimbo la Tarime Vijijini kwa maana ya mteja wao (John Heche) kushinda kesi inayomkabiri.
  Tazama HAPAPicha katika Siku ya Kusikiliza Kesi Hiyo.

  0 0

  Na Lilian Lundo – Maelezo.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Liberatus Sabas amekanusha habari iliyoandikwa na gazeti la Jambo Leo la Januari 27, 2016 lenye kichwa cha habari “Waendesha bodaboda Arusha waandamana.
  Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda Sabas alisema hakukuwa na maandamano yoyote ya bodaboda jijini Arusha zaidi ya vijana wachache waendesha bodaboda waliojikusanya kwa Mkuu wa Mkoa.

  Kamanda Sabas amesema kuwa, wapo katika operesheni ya waendesha bodaboda ambao wamekuwa wakivunja sheria za barabarani mara kwa mara. Operesheni hiyo ni ya nchi nzima na wameianza Januari 14, 2016.

  “Mpaka sasa tumekusanya sh. mil. 21,330,000 ambazo zimetokana na makosa mbalimbali yanayofanywa na waendesha bodaboda wawapo barabarani, makosa hayo ni kutovaa kofia ngumu, kutokuwa na leseni ya udereva, kubeba abiria zaidi ya mmoja, kutokuwa na kadi za pikipiki na kadi za bima,” alisema Kamanda Sabas.

  Kamanda Salas amesema kuwa wasingeweza kukusanya kiasi hicho cha pesa kwa kipindi hicho kifupi kama askari polisi wangekuwa wakichukua pesa hizo kwa maslahi yao wenyewe, ila wamekuwa wakiziingiza katika vitabu vya Polisi.

  Aidha Kamanda Salas amesema hakuna dereva wa bodaboda anayedaiwa cheti cha udereva bali wametakiwa kuonyesha leseni zao za udereva kwani ndizo zinazothibitisha kwamba wamepitia vyuo vya udereva.


  Kamanda Salas amewataka madereva wa bodaboda ambao bado hawajapitia vyuo vya udereva wakajifunze udereva ndipo waendeshe bodaboda na amewaambia kuwa ili wasikamatwe na askari polisi basi wasivunje sheria za barabarani.

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa World Lung Foundation(WLF) Dk Nguke Mwakatundu akimkabidhi Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi John  Ndunguru moja ya kifaa cha kumsaidia mama mjamzito kuvuta mtoto wakati wa kujifungua.
  Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndunguru akikabidhi moja ya kifaa cha kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama kwa kumvuta mtoto kwa uongozi wa hospita ya Mkoa, uliotolewa na shirika la World Lung Foundation.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndunguru akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vifaa saba vya kumsaidia mama mjazito kujifungua katika hospital ya Mkoa wa Kigoma msaada uliotolewa na shirika la Word Lung Foundation

  SHIRIKA LA WORLD LUNG FOUNDATION(WLF) LATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUMSAIDIA MAMA MJAMZITO KUJIFUNGUA (VACUUM EXTRACTORTS) KWA HOSPITAL YA MKOA YA KIGOMA. 

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Kigoma

  Shirika lisilo la kiserekali la Word Lung Foundation(WLF) limetoa msaada wa  vifaa saba kwaajili ya kumsaidia mama mjamzito wakati akijifungua kumvuta mtoto aliyeshindwa kutoka kwa kutumia ombwe(vacuum extractors) vifaa hizo vimetolewa katika hospital ya Mkoa wa Kigoma. 

  Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo wa vifaa vya kusaidia akina mama wajawazito kujifungua salama kwa uongozi Serekali ya Mkoa na hospital  Mkurugenzi Mkuu wa wa shirika hilo Dk Nguke Mwakatundu alisema Kuwa shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vifo vya akina mama na watoto wachanga vinapungua. 

  Alisema utumiaji wa vifaa hivyo vya kuvuta watoto inasaidia akina wengi kujifungua bila ya upasuaji jambo linalowapunguzia adha mbalimbali zitokanazo na upasuaji kama vile maumivu, kuuguza kidonda muda mrefu pamoja na matatizo mengine. 

  Alisema vifaa hivyo vinathamani ya shilingi 30,450,000 ambavyo vitaboresha utoaji wa huduma kwa akina mama wakati wa kujifungua. 

  Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kanali mstaafu Issa Machibya alisema kuwa uongozi wa Mkoa wa Kigoma unalishuru shirika hilo kwa juhudi wanazofanya za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga katika Mkoa wa Kigoma. 

  "Kwakweli World Lung Kigoma mnaipenda sana kwani ipo Mikoa mingi hapa nchini yenye matatizo haya lakini nyie mmechagua kuja kufanya kazi kwenye mkoa huu nawapongeza kwa hili"alisema Katibu tawala wa Mkoa

  Alisema Mkoa utashirikiana shirika hilo katika kuhakikisha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vinapungua Mkoani Kigoma. 

  Naye Kaimu Mganga Mkuu wa hospital ya Mkoa wa Kigoma maweni Dk Fadhil Kabaya alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja shirika hilo limeweza kushirikiana na vituo vya afya 9 wanavyofanya navyo kazi na kupata mafanikio mbalimbali. 

  "Akina mama 18281 walijifungulia katika vituo hivyo, akina mama 1613 walifanyiwa upasuaji na akina mama 166 walipatiwa huduma ya kumvuta mtoto kwa kutumia ombwe yaani vacuum extraction, pia vifo vinavyotokana na uzazi vimepungua kutoka 49 mwaka 2014 hadi  vifo 38 mwaka 2015 sawa na asilimia 22"alisema Dk Fadhil

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Bima wa wa Kampuni ya Kimataifa ya Ernest & Young (EY), Sujay Shah akizungumza katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na kampuni hiyo wa kujadili ripoti sekta ya bima na umuhimu wake katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Kiongozi wa Kanda ya Mashariki wa Idara ya Fedha na Ushauri wa Huduma ya Sekta binafsi wa EY, Steve Osei Mensah akizungumza katika mkutano wa wadau ulioandaliwa na kampuni hiyo wa kujadili ripoti sekta ya bima na umuhimu wake katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkazi wa EY Tanzania, Joseph Sheffu akizungumza na waandishi habari juu ya sekta bima iliopo nchini na ukuaji wake katika huduma hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
  Badhi ya wadau wa bima wakiwa katika mkutano leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  WADAU wa sekta ya Bima wamesema kuwa Tanzania iko chini kwa matumizi ya bima katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kutokana na kutotambua mchango wa bima katika pato la taifa.

  Akizungumza katika mkutano wa Wadau bima ulioandaliwa na wa Kampuni ya Kimataifa ya Ernest & Young (EY), wa kujadili ripoti sekta ya bima na umuhimu wake katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mkurugenzi Mkazi EY Tanzania, Joseph Sheffu, amesema kuwa sekta bima iko kama biashara nyingine ya kuchangia pato la Taifa. 

  Amesema nchi zilizo katika ripoti hiyo ni Uganda, Malawi ,Kenya,Nigeria pamoja na Tanzania, ambapo katika ripoti hiyo Tanzania ni asilimia 0.8 inachangia katka pato la Taifa wa bima zisizo za maisha.

  Sheffu amesema wanaotumia bima nchini ni asilimia 0.1 ya watu wote katika pato la Taifa huku Kenya ikiwa na asilimia moja na pamoja Uganda asilimia 0.09.

  Amesema kuwa Tanzania kuwa nyuma katika bima ni kutokana historia ya Ujamaa, ugonjwa wa ukimwi ambao ulifanya umri wa kuishi kupungua na bima kushindwa kuwewekeza katika bima ya maisha.

  Aidha amesema katika kampuni za bima 27 ni kampuni mbili tu ndio zinatoa bima ya maisha kutokana na watanzania kutojua umuhimu huo kwa kujua mtu hata akifariki family yake itaangaliwa na ndugu zake.

  Sheffu amesema katika bima ya maisha Tanzania imefikia na dola sita, Kenya dola 40 na soko la bima lililopo nchini hatumiwi ipasavyo.

  0 0

  Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Tarime Vijijini uliofanyika Novemba 25,2015. Kesi hiyo ilifunguliwa aliekuwa Mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Christopher Ryoba Kangoye akiiomba Mahakama kutengua Ushindi wa Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche aliechaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.
  Na:George Binagi.
  Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa January 19,2015 chini ya Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha leo imeahirishwa hadi kesho January 28,2015 majira ya saa nane mchana itakapotolewa maamuzi yake.
  Mjibu maombi katika kesi hiyo (John Heche) anawakilishwa na Mawakili Tundu Lisu (leo hakuwa Mahakamani) pamoja na Paul Kipeja (alikuwepo Mahakamani).

  Baada ya Kesi hiyo Kuahirishwa, Katibu wa Chadema Mkoani Mara Mwl.Chacha Heche (Pichani Juu anaehojiwa) ameiomba Mahakama kutoa maamuzi ya Kesi hiyo ili kuwapunguzia gharama kwa kuwa ambazo zinajitokeza wakiwa Jijini Mwanza kufuatilia maamuzi ya kesi hiyo.

  Barnabas Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa amesema kuwa wanatarime vijijini wana imani na Mahakama na kwamba kesi hiyo ni sehemu ya changamoto kwa mbunge wao na kwamba wembe ni ule ule wa kushinda kuanzia jimboni hadi Mahakamani.
  Barnabas Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa.
  Paul Kipeja ambae ni Wakili upande wa Mjibu Maoni akizungumza na wanahabari baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kuahirisha kutoa Maamuzi ya kesi ya Kupinga Matokeo Jimbo la Tarime Vijijini.

  Anasema kama ilivyokuwa katika Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Bunda Mjini iliyofunguliwa na Wapiga kura wa Jimbo hilo dhidi ya Esther Bulaya (Mbunge), ndivyo itakavyokuwa hata katika Jimbo la Tarime Vijijini kwa maana ya mteja wao (John Heche) kushinda kesi inayomkabiri.

older | 1 | .... | 747 | 748 | (Page 749) | 750 | 751 | .... | 1897 | newer