Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 746 | 747 | (Page 748) | 749 | 750 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza jambo na Wakili wakujitegemea, Jebra Kambole baada ya kutoka Mahakama Kuu ambako wamefungua hauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa.
   Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika jamii. 
  Wakili wakujitegemea, Jebra Kambole kizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika jamii.


  Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
  VIFUNGU vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 vyapingwa mahakama kuu leo jijini Dar es Salaam.

  Vipengele vinavyopingwa ni kifungu cha sheria cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa (CAP 29 R.E 2002), sheria inayotoa mwanya kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakana na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi ambayo ni kinyume na ibara ya 13, 12 na 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 19977 zinazotoa haki ya usawa mbele ya sheria kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.

  Kesi ya kupinga vifungu  vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18  ni keshi ya kikatiba yenye namba tano ya mwaka 2016 iliyofunguliwa na Mwanaharakati wa haki za binadamu, Rebeca Gyumi na kusimamiwa na wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocate.

  Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi  ameomba mahakama kuu kufutia mbali vifungu vya sheria hivyo na kupandisha umri wa chini wa kuoa  kwa wanaume na kuolewa kwa wanawake kuwa ni miaka 18.

  Aidha Rebeca amesema kuwa  ndoa za utotoni kwa wasichana ni ukiukwaji wa haki za binadamu pia kuzaa kwa msichana akiwa na umri mdogo ni chanzo kikubwa cha matatizo ya Fistula na vifo vingi vya wajawazito.

  0 0

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi katibu mkuu wa Ambassador FC, Bakari Khalid kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa Shinyanga. 
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (kushoto) na Bakari Khalid Katibu mkuu wa timu ya Ambassador wakati wa hafla ya kukabidhi msaada kwa timu hiyo.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi hundi timu ya Ambassador FC.
  Katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi na Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.
  Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi katika hafla ya makabidhiano ya hundi kwa timu ya Ambassador kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa Shinyanga.
  Vikosi vya timu za Buzwagi fc na Ambassador vikiwa katika maandalizi wakati wa ukaguzi kabla ya kuanza kwa mhezo.
  Kikosi cha timu ya Ambassador fc 
  Kikosi cha timu ya Buzwagi fc. 
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (mwenye kofia) akisalimiana na Nahodha wa timu ya Buzwagi, Saimon Sanga wakati wa mchezo wao wa kirafiki na timu ya Ambassador FC.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (mwenye kofia) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ambassador FC.
  Kikosi cha timu ya soka ya mgodi wa Buzwagi kikiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa timu ya Ambassador FC. Katika mchezo huo timu ya Ambassador FC iliibuka mshindi kwa kuwafunga wenyeji wao Buzwagi FC, 2-1 
  Kikosi cha wachezaji wa timu ya Ambassador FC ya mjini Kahama wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi umeikabidhi timu ya ambassador FC ya wilayani Kahama kitita cha shilingi milioni kumi na laki tano kama sehemu ya msaada kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki michuano ya ligi daraja la pili ngazi ya mkoa - Shinyanga.

  Msaada huo ambao ulikabidhiwa na meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Mhandisi Asa Mwaipopo umetolewa kwa timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika michuano ya ligi daraja la pili inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, meneja mkuu wa Buzwagi amesema msaada huo kwa timu ya ambassador ni mwendelezo wa harakati zinazofanywa na kampuni yake katika kuhakikisha makundi mbalimbali yanayozunguka maeneo ya mgodi huo yananufaika na fursa mbalimbali zilizopo.

  “Lengo letu kubwa la kutoa msaada huu ni kutekeleza ahadi yetu ya kuisaidia Jamii inayotuzunguka na tungependa kuona hata kupitia michezo vijana wanajitengenezea ajira, kama mnakumbuka tumetoa udhamini kwa timu ya Stand Utd inayoshiriki Ligi kuu ya Vodacom na sasa tumetoa msaada huu wa fedha ili kuisaidia timu hii ili nayo iweze kufanya vizuri katika mashindano yaliyo mbele yao”.alisema Mwaipopo.

  Kwa upande wake katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid ameushukuru uongozi wa mgodi wa Buzwagi kwa msaada huo ambao amesema utasaidia kuongeza hali ya mchezo kwa wachezaji wa timu yake.

  “Natoa shukrani kwa uongozi wa Buzwagi kwa msaada huu, niwaahidi kwamba sisi kama Ambasador tutafanya vizuri nakuwa mabalozi wa kuitangaza Kahama katika sekta ya michezo, kwani tunao vijana wazuri wenye uwezo wa kucheza mpira na kwa kufanya hivi tunawahakikishia baadhi ya vijana ajira kupitia michezo” Alisema Bakari.

  Katika hatua nyingine timu hiyo ya ambassador FC ambayo iko chini ya kocha Karume Songoro ambaye amewahi kuzichezea timu za Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, ilimenyana na timu ya mpira ya Buzwagi mchezo ambao uliisha kwa Ambassador iliibuka na ushindi wa goli 2-1.
  0 0


  0 0

  Economic Outlook

  GDP
  Following a challenging 2015 economic conditions, Tanzania is set to improve modestly over the coming quarters with real GDP growth climbing to above 6.0% in 2016 from an estimated average of 5.7% in 2015.

  INFLATION OUTLOOK
  Inflation has consistently been above the Bank of Tanzania’s (BoT) 5% target over the past decade (averaging over 9 .0%) and we expect this trend to continue over the coming years. Inflation set to range between 6 .0 and 8 .0% over the coming months. Despite the shilling's heavy sell-off and associated inflation pass through, inflation has been contained thanks to favorable food and fuel prices. These benign price conditions are set to continue through in 2016.

  Short-Term Outlook (Three-To-Six Months)
  Having sold off aggressively through Half 1, 2015, the Tanzanian shilling (TZS) has stabilized against the dollar over the past 5-6 months, even firming of late. External dynamics, notably a strong USD and related shifts in investor perceptions towards Emerging Markets currencies, have been the dictating factor in the shilling's performance over recent quarters and this trend will remain in place over the coming three-to-six months. Fellow East African currencies such as Kenya and Uganda, for instance, have exhibited similar stability over this period. With the USD rally now mostly spent pressures on the shilling will lighten and augur a far more modest pace of TZS depreciation over the coming 12 months or so. We forecast average deprecation of around 12% in 2016 compared to 23% in 20 15.

  Long-Term Outlook (Six-To-24 Months)
  Weak balance of payments dynamics and uncertainty in the energy sector will drive further shilling depreciation over the next couple of years. External imbalances arising from a shortage of domestic productive capacity are reflected in Tanzania's g aping trade in goods deficit and this will ensure that the country's current account balance remains deep in the red - at the equivalent of between 9 .0% and 11.0% of GDP - over the next two years and these imbalances will remain the key pressure point for the shilling over the medium-term. Tanzania will continue run a large structural deficit for the duration of our 2015-2019 forecast period. The latest data from the Bank of Tanzania confirm that in the year through September 2015, the current account deficit narrowed by 14% to USD4 .2bn thanks to a jump in exports and a sharp deceleration in imports. 
  Banking Sector Risk Components

  Asset Quality
  Tanzania's banking sector remains in relatively good health. Asset quality has continued to improve in recent quarters, as illustrated by the ratio of nonperforming loans (NPLs) to total loans. The latter decreased from 8 .5% in September 2014 to 6 .5% in March 2015, reflecting write downs and efforts made by banks to recover NPLs. Overall the sector benefits from relatively healthy asset quality which should continue to benefit from a robust economic outlook.

  Funding Structure
  The Tanzanian banking sector's funding structure is relatively strong. The sector's loan-to-deposit ratio sat at 78% in 20 15 which though higher than its five year average of 69%, remains comfortable. This implies that Tanzania's banks are predominantly domestically funded, less reliant on external financing, and thus less exposed to external shocks.

  Capital Adequacy
  The banking sector also has robust levels of capital adequacy, with capital above regulatory requirements. Capital as a percent of total assets remains in line with Tanzania's long -term average, coming in at 12.6% in December 2014 compared to an average of 12.0% of assets since 2009. We do not see scope for a significant increase in leverage over the coming quarters, as tighter monetary conditions and economic uncertainty cause lenders to remain relatively risk averse. Meanwhile efforts to improve banking sector supervision are likely to ensure that banks' average capital ratios remain strong in the coming years.

  Regulatory Body Assessment
  The Tanzanian banking authorities continue to strengthen financial sector supervision to ensure financial stability and soundness. These efforts have been stepped up following investigations by US authorities into Tanzania headquartered FBME Bank - the country's largest by asset size albeit with most of its operations based in Cyprus - which was labeled as of 'primary laundering concern'. In light of these developments, the BoT is developing its supervision framework, issuing consolidation supervision regulations and issuing memorandum of understandings with other foreign regulators and central banks.

  USD/TZS Forecast 2016
  During 2015, USDTZS traded at the level of 1674 to 2160 which is almost 30% drop of its value. This drop was contributed by many factors such as decrease of exports, increase of importation of necessity goods, perceived political instability during general election, and decrease of donor funds etc. 

  The Tanzania Shilling is expected to trade at 2180.00 by the end of this quarter, according to Trading Economics global macro models and analysts’ expectations. Looking forward, we estimate it to trade at 2266.00 in 12 months’ time.


  Interest Rate Forecast 2016

  Interest Rate in Tanzania is expected to be 12.00 percent by the end of this quarter, according to Trading Economics global macro models and analysts’ expectations. Looking forward, we estimate Interest Rate in Tanzania to stand at 12.00 in 12 months’ time. In the long-term, the Tanzania Interest Rate is projected to trend around 12.00 percent in 2020, according to our econometric models.


  Treasury bill Rate Trend
  Government still borrowing from commercial banks which will push rate up as per below graph.

  The Tanzania Shilling is expected to trade at 2180.00 by the end of this quarter, according to Trading Economics global macro models and analysts’ expectations. Looking forward, we estimate it to trade at 2266.00 in 12 months’ time.


  Interest Rate Forecast 2016
  Interest Rate in Tanzania is expected to be 12.00 percent by the end of this quarter, according to Trading Economics global macro models and analysts’ expectations. Looking forward, we estimate Interest Rate in Tanzania to stand at 12.00 in 12 months’ time. In the long-term, the Tanzania Interest Rate is projected to trend around 12.00 percent in 2020, according to our econometric models.


  Treasury bill Rate Trend 

  Government still borrowing from commercial banks which will push rate up as per below graph.

  Authors:
  Godfrey Ndalahwa - Head of Finance

  He joined the bank in May 2013 as head of finance and later on in April 2015, was appointed as Non-Executive Director for KCB Burundi. He previously worked for Barclays and NBC Limited holding different executive roles in the area of internal audit, strategy and financial management. Prior to join the Banking Industry, He worked for Deloitte and Coca-Cola Sabco.

  Godfrey is certified public accountant and holds Bachelor of honors Degree in Commerce from University of Dar es Salaam and has attended various courses including a one year leadership Programme from University of Pretoria.
  Pascal Machango-Head of Treasury 

  He joined the bank in April 2005 as the Treasury Bank office manager at KCB . He previously worked with Stanbic Bank , Standard chartered Bank and Diamond Trust bank for more than 5 years. He has a B`COM accounting Degree from the University of Dar es Salaam in Tanzania and MBA Finance from Open University on Tanzania. He has attended various advanced courses and workshops in banking and finance. He has over 15 years’ experience in Banking industries holding.

  0 0

  Ndege ya uzinduzi ya Shirika la Ndege la Etihad ikipokelewa na magari ya zimamoto ambayo yalimwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege kati ya Rabat na Abudhabi. 

  Safari kati ya Abu Dhabi na Morocco kufikia tisa kwa wiki 
  Shirika la ndege la Etihad lazindua rasmi huduma zake za ndege baina ya Abu Dhabi na Rabat, Morocco, ikiwa ni kituo chao cha pili nchini humo.

  Ndege ya uzinduzi iliwasili mchana wa leo uwanja wa ndege Sale-Rabat na kupokelewa na mzinga wa maji kama ilivyo desturi ikifuatiwa na wageni rasmi kuwasili, wakiwemo; Lahcen Haddad (Waziri wa Utalii Morocco), na Balozi wa UAE kwa Morocco, Mh. Al Asri Saeed Al Dhaeri.

  Huduma hii itakayopatikana mara mbili kwa wiki kupitia ndege aina ya Airbus A340-500 itakuwa yakipekee baina ya Rabat na Abu Dhabi. Tayari kukiwa na safari baina ya Abu Dhabi na Casablanca, shirika litafikisha jumla ya safari tisa kwa wiki kwenda nchini Morocco

  Ndege ya uzinduzi (EY615) kwenda Rabat ilibeba msafara ulioongozwa na Khaled Al Mehairbi, Makamu Rais Mambo ya Serikali na Siasa za Anga. Uwakilishi huu ulijumuisha Kapteni Salah Awadh Alfarajalla, Makamu Rais Usalama na Maaendeleo ya Waendesha Ndege Kitaifa; Hareb Mubarak Al Muhairy, Makamu Rais Mambo ya Mashirika na Kimataifa; Ali Al Shamsi, Makamu Rias Operesheni za Kitovu cha Abu Dhabi; Joost Den Hartog, Kaimu Makamu Rais wa Mauzo Duniani; na Amer Khan, Makamu Rais Mashariki ya Kati na Africa Kaskazini.

  James Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema shirika limefurahishwa na uzinduzi wa huduma ya Rabat kama kituo cha pili katika safari za Morocco.

  “Safari hizi mpya zitakazounganisha miji hii zinadhihirisha dhamira ya Etihad kuendelea kujenga mahusiano endelevu na kanda ya ksakazini mwa Afrika na kuimarisha uhusiano kati ya Morocco na Umoja wa Falme za Kiarabu,” alisema.

  “Rabat ni mji wa kihistoria unaovutia wanaosafiri kwa ajili ya burudani na biashara. Kwa kupitia huduma yetu mpya, tunalenga kutumia mtandao wetu uliopo duniani kote kukuza wingi wa wasafiri wataotumia njia hii kuingia Morocco. Vivyo hivyo tunarahisisha safari katika Rabat hadi Abu Dhabi pamoja na miji mingine tunayofika, huku tukiwapa wageni wetu fursa ya kufurahia huduma zetu za viwango vya juu zinazotambulika dunia nzima.”

  Pamoja na Casablanca, huduma hii ya Rabat itafikisha jumla wasafiri 4,200 kila wiki kwenda Morocco.

  Kama UAE, serikali ya Morocco imewekeza sana katika kuiendeleza sekta ya utalii. Mwaka 2010, serikali ilizindua Vision 2020 ikiwa na mpango wa kuifanya Morocco kuwa kati ya sehemu kuu 20 za utalii duniani na hii itachangia kuongeza idadi ya watalii hadi mara mbili ya idadi ya awali hadi kufikia takribani milioni 20 mpaka kufika mwaka 2020.

  Balozi wa UAE kwa Morocco, Mh. Al Asri Saeed Al Dhaheri, alisema: “Sina mashaka kwamba safari hizi kati ya miji hii mikuu ya kiarabu zitaimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi katika masuala ya usafiri wa anga. Hii ni hatua nyingine ya maendeleo katika uhusiano kati ya UAE na Morocco. Safari za moja kwa moja zitachangia sana kuleta maendeleo katika biashara, uwekezaji na utalii. UAE na Morocco zimeunganishwa na historia ndefu ya ushirikiano na uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi hizi mbili na utaendelea hivyo katika miaka ijayo.”

  “Nimeridhika sana kwa kampuni za UAE zinavyozidi kutazama kwa umakini nafasi zilizopo kushirikiana, kuwekeza na kufanya biashara mjini Rabat. Ni dhahiri kwamba nyakati zijazo jamii za kibiashara zitapata faida kubwa katika nchi hii na tungependa kushuhudia ushirikiano ukikua na bila shaka shirika la Etihad ni mfano mzuri wa hili.”

  Huduma hii itakuwepo Jumatano na Ijumaa kwa kutumia ndege aina ya Airbus A340-500 yenye siti 240, 12 za daraja la kwanza, 28 za daraja la bisahara na 200 za daraja la uchimi.

  Huduma ya Abu Dhabi-Casablanca imekuwa ikifanya vizuri tangu kuanzishwa Juni mnamo mwaka 2006. Huduma ya Abu Dhabi-Rabat inawapa abiria chaguo zaidi na njia mbili zinazounganisha Morocco na UAE na imefungua njia kufika sehemu nyingine katika mtandao wa Etihad’ GCC, Bara la Hindi na Asia Kusini Mashariki pamoja na Australia

  Shirika la Etihad pia limesambaa kufika Afrika Kaskazini kwa makubaliano ya ‘codeshare’ na Royal Air Maroc, ikiwapa abiria ndege za safari za moja kwa moja kutoka Casablanca mpaka sehemu zingine Morocco kama Agadir, Marrakech and Tangier.

  Shirika la ndege la Etihad pia imeongeza huduma zake Afrika kufika Johannesburg, Khartoum, Cairo, Lagos, Nairobi, Entebbe, Dar es Salaam and Mahé in the Seychelles.

  Ratiba ya safari katika ya Abu Dhabi and Rabat, kwanzia Januari 15 2016:


   Ndege na.
  Kuondoka
  Kuwasili
  Muda wa kuondoka
  Muda wa kuwasili
  Aina ya ndege
  Siku 
    EY 615
  Abu Dhabi
  Rabat
  10.00
  15.15
  A340-500
  Jumatano/Ijumaa
    EY 616
  Rabat
  Abu Dhabi
  20.00
  07.25 kesho yake
  A340-500
  Jumatano/Ijumaa
   Angalizo: muda wa kuondoka na kuwasili ni kwa muda wa Abu Dhabi.

  0 0

   
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (akiwa amevaa beji inayoonesha jina lake) amewahimiza watumishi wote katika Utumishi wa Umma kuvaa beji zenye majina yao kila wakati wa kutekeleza majukumu yao ambapo amesisitiza kuwa ofisi zote zisimamie na kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kila mtumishi awe na beji hiyo inachoonesha jina lake.(Picha na Michuzi Jr-MMG).

  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
  KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ameagiza na kusisitiza ofisi zote Umma kusimamia na kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kila watumishi awe na kitambulisho (beji) kinachoonesha jina lake.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Balozi Sefue alisema hatua hiyo ya watumishi wa umma kuvaa beji zenye majina kila wakati wanapotekeleza majukumu yao itasaidia wananchi kuwatambua kwa majina watumishi wanaowahudumia na kuwasaidia kulingana na mahitaji yao kwenye ofisi hizo.

  Ili kutekeleza azma ya kuwahudumia wananchi, Balozi Sefue alisema kuwa kuanzia sasa watumishi wote wa umma wavae beji zenye majina yao iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi wa umma anayewahudumia kwa weledi, uaminifu na kwa wakati na kumtolea taarifa yule anayefanya mambo ya hovyo.

  Zaidi ya hayo, Balozi Sefue amewahimiza viongozi na watumishi wote katika Utumishi wa Umma kubadilika kwa dhati kwenye utendaji na uadilifu wao na kuwahudumia wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima.

  “Rais na sisi wote tunaomsaidia hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watumishi wengine, tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua” alisema Sefue.

  Mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ni pamoja na kila kiongozi na mamlaka ya nidhamu isipate kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi ili kuchukua hatua za nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.

  Balozi Sefue amewahimza viongozi na watumishi wa umma kuwahudumia wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima ambapo kila ofisi ya Serikali inapaswa kuwa na dawati la kusikiliza shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

  Kwa upande wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wote nchini wametakiwa kujenga uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati.

  “Kwa muundo wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka Ikulu Dar es Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu ndiye anayeweza kumaliza matatizo yake, maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu, ikibidi wananchi wafike Ikulu inamaana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao” aliongeza Balozi Sefue.


  Aidha, Balozi Sefue alisema kuwa ofisi zote za Serikali zinatakiwa kuwa na dawati la kupokea maoni ya wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo na kushughulikia haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma inayotolewa.

  0 0
 • 01/26/16--02:56: 3 YEARS DEATH ANNIVERSARY
 • The Late Moses Tito Kachima (27.01.1945 – 29.01.2013)


  You have been a blessing to us from God. Your memories will always live on and as days pass by you will always be remembered and your spirit lives on. 

  We thank God for you as a wonderful gift to our lives and even though we loved you, God loved you more. 

  We know you are in a better place. May your soul rest in peace.


  Eternal rest grant to him, O lord and let perpetual light shine upon him, May he rest in peace. Amen.


   Mass for the Late Moses Tito Kachima will be held on 29th January 2016 at St. Immaculate Church – United Nations road, Upanga.

  Time: 6 a.m

  0 0

   Dokta Abdull Maulid Abdull akimpima Miwani ya kuonea Mwananchi Chale Muumin Fumu mkaazi wa Kijiji cha Matemwe Tunda ngaa katika matibabu yalio fanyika skuli ya matemwe mkoa wa Kaskazini unguja.
   Dokta Rajab Mohd Haj akimkagua Jicho Mzee Muhidin M Ali Mkaazi wa Kijiji cha Matemwe katika matibabu yaliofanyika Skuli ya Matemwe Mkoa wa Kaskskazini Unguja.
   Dokta Fei Jie kutoka China akimpima Masikio Bi Fatma Khamis Jaku mkaazi wa Kijiji cha Matemwe Mfuruni katika matibabu yalio fanyika Skuli ya Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
   Mtoto Iddi Khamis Juma akipatiwa huduma ya kupimwa uzito.

   Daktari Bingwa kutoka China Yun Lai Gao kushoto na Mwanafunzi kutoka Zanzibar School of Health Machano M Ali kwa pamoja wakipata maelezo kutoka kwa Mgonjwa anaesumbuliwa na maradhi ya Ganzi Haji Ali Mcha kabla ya kumtibu huko Skuli ya Matemwe.
   Dokta Yu Lu akimgonga ngumi Mgonjwa anaesumbuliwa na maradhi ya Mgongo Mkadam Vuai kwaajili ya kumpatia matibabu ambayo yamekua yakimsumbua kwa muda mrefu.
   Mwandishi wa habari wa Star TV Abdalla Pandu akimuhoji Mwanchi wa Kijiji cha Matemwe Mbupurini Chida Pili Khamis Juu ya Huduma za Afya zilizowafikia katika kijiji chao cha Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar.


  0 0

   Kaimu Balozi Mdogo wa India Govind Sharan Gupta akisalimiana na Wananchi mbalimbali wenye asili ya India wanaoshi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuadhimisha miaaka 67 ya Uhuru wa Jamhuri ya India iliyofanyika katika Ubalozi huo Migimbani mjini Zanzibar.
   Wananchi mbalimbali wanaioshi Zanzibar wenye asili ya India wakiimba wito wa Taifa la India Picha na Abdallah Omar.
   Kaimu Balozi Mdogo wa India Govind Sharan Gupta akipandisha Bendera ya India kuashiria kuifungua sherehe ya Uhuru wa Jamuhuri ya India ya kutimiza miaka 67 katika Sherehe iliofanyika katika ubalozi huo Migombani Zanzibar.

   Wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo wakisherehekea baada ya kupandishwa Bendera ya Nchi ya India kuadhimisha miaaka 67 ya Uhuru wa Jamhuri ya India iliyofanyika katika Ubalozi huo Migimbani mjini Zanzibar.
  Kaimu Balozi Mdogo wa India Govind Sharan Gupta akiwahutubia wananchi mbalimbali wanaoishi Zanzibar waliohudhuria katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Jamuhuri ya India kuadhimisha miaka 67 katika ofisi za Balozi migombani Zanzibar. 

  Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

  0 0
 • 01/26/16--03:37: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

  Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.

  Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.


  Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.


  Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa kuwa Serikali haitoi ruzuku kwa ajili yao.


  Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela.


  Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la wao kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu bure.


  Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa mwaka.

  Kikao Kikiendelea
  Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi juu ya suala la Elimu Bure nchini.
  Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza

  Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
  Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
  Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
  Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima
  Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
  Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
  Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
  Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
  Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
  Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
  Kutoka Pasiansi Sekondari Jijini Mwanza, Mimi ni Mzee wa Karanga fotoooooooo, GB Pazzo wa Binagi Media Group

  0 0

  The Affordable Care Act (ACA) or OBAMA CARE is a United States federal statute signed into law by President Barack Obama on March 23, 2010.The ACA was enacted to increase the quality and affordability of health insurance, lower the uninsured rate by expanding public and private insurance coverage, and reduce the costs of healthcare for individuals and the government”.

  This message is brought to you by HELP AFRICA, which is an organization that targets African Communities in abroad and at home.We urge you to register so you can access quality health services health services, avoid penalties and strengthen the health of our communities.
  Attachments area

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Amani Joram Mgullo (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utambulisho wa Tuzo mpya za AMAN AWARD katika tasnia ya Muziki, Filamu na Habari. Kushoto ni Afisa Mahusiano Balozi Gepard na kulia ni Afisa Habari Salesi Malusa.

  Afisa Habari wa Broad Based Intersect Organization (BBIO) Salesi Malusa (Kulia) akitoa ufanunuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ambavyo wananchi watashiriki kuchagua washindi wa tuzo hizo kwa kuwapigia kura. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa (BBIO) Amani Joram.

  Picha na Beatrice Lyimo.


  Na Lilian Lundo-Maelezo

  Taasisi isiyo ya kiserikali “Broad Based Intersect Organization” (BBIO) ambayo inaratibu uhamasishaji na uimarishaji wa mikakati ya maendeleo, yenye makao makuu mjini Dodoma imetambulisha tuzo mpya ziitwazo AMAN Awards katika tasnia za muziki, filamu na habari.

  Tuzo hizo zimetambulishwa leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Aman Joram Mgullo.
  Mgullo alisema kuwa, tuzo hizo zimetokana na mradi uitwao “Advocacy Mission Awards Network” (AMAN) unaohusika na uhamasisha na uimarishaji wa juhudi za utekelezaji wa mikakati ya maendeleo

  “Wazo la utoaji wa tuzo za AMAN limekuja baada ya Tanzania pamoja na mataifa mengine ulimwenguni kuzindua mkakati mpya wa maendeleo (the Agenda 2030 of Sustainable Development Goals) ikiwa na adhima ya kutengeneza Maisha bora na Dunia bora kwa kila mwanadamu ulimwenguni,” alisema Mgullo.

  Mgullo aliongeza kwa kusema kuwa, kutokana na mikakati mingi iliyotangulia kutofanikiwa kufikia malengo yake na kufanya jamii nyingi kuendelea kuishi katika hali duni ndicho kilichopelekea taasisi ya BBIO kufanya juhudi za ushawishi na uwezeshaji kupitia wasanii na wanahabari ili mradi huo wa maendeleo ufikie malengo yake kupitia tuzo za AMAN.

  Kutokana na tafiti nyingi kuthibitisha kuwa tasnia za muziki na filamu, kupitia vyombo vya habari zinauwezo mkubwa wa ushawishi na uwezeshaji kwa jamii. Hivyo kwa kuwashilikisha wasanii kutoa ujumbe wa maendeleo kwa jamii kupitia tuzo za AMAN kutaleta mabadiliko kwa jamii ya Tanzania.

  Mgulla alizitaja tuzo zitakazowaniwa kuwa ni Aman Music Awards, Aman Film Awards na Aman Media Awards ndani ya kila Tuzo kutakuwa na vipengele tofauti tofauti, na wananchi watashiriki kwa kupigia kura na kuchagua msanii au mwanahabari ambaye amefikisha ujumbe wa maendeleo katika jamii.

  Lengo la tuzo za AMAN ni kuhakikisha dhima ya maisha bora na dunia kwa kila mwanadamu kwa kuchochea umahiri katika kutoa, kueneza na kufikisha ujumbe wa maendeleo endelevu kupitia tasnia za muziki, filamu na habari.

  0 0  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
  ………………..
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za Maafisa wanaofanya kazi kinyume na maadili.

  Akiongea na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo amesema kuwa TRA ina Idara Maalumu ijulikanayo kama Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA ambayo inashughulika na kufuatilia maadili ya watumishi wa sekta hiyo nchi nzima.

  “Tunawaomba wananchi kushirikiana na Idara ya Mambo ya Ndani ya TRA kwa kuwapa taarifa juu ya maafisa wa TRA wanaokwenda kinyume na Maadili ya Utumishi wa Umma,”alisema Kayombo.

  Mkurugenzi Kayombo ameongeza kuwa wananchi wanaweza kutoa taarifa kwa kupiga simu kwa namba 0689122515 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwa simu namba 0689122516 na kuwahakikishia kuwa taarifa zao zitakua zimefika sehemu husika na zitafanyiwa kazi.

  Aidha Kayombo amependa kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa namba hizo ni za siri na hakuna mwananchi atakayepata tatizo lolote kwa kutoa taarifa za maafisa wasio na maadili.

  kea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya watumishi wa TRA wanaoenda kinyume na maadili, wameyafanyia uchunguzi na baadhi ya watumishi wamefukuzwa na wengine kupewa adhabu kali.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Viongozi na Wananchi wakishiriki katika Sala ya kumsalia marehemu Ramadhani Nyonje Pandu iliofanyika katika msikiti wa fuoni na kuzikwa kijijini kwao Paje Wilaya ya Kusini Unguja.(Picha na Ikulu).
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki dua ya kuuombea Mwili wa Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati alipofika nyumbani kwa marehemu fuoni michezani Unguja kutoa mkono wa pole kwa wanafamilia leo asubuhi.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji Mjane wa Marehemu Ramadhani Nyonje Panda alipofika nyumbani kwao fuoni michezani kutowa mkono wa pole kwa wana familia, kulia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh Khamis Haji Khamis.
  WANANCHI wakiwa katika msiba wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi kuwa Mwakilishi wac Jimbo la Muyuni Zanzibar.
  WANANCHI wakiwa katika msiba wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakiwa nyumbani kwa marehemu fuoni michezani Unguja wakisubiri taratibu za mazishi ya marehemu kupelekwa kijiji kwao Paje kwa mazishi.
  WANANCHI wakisoma hitma ya marehemu katika msiki wa fuoni kabla ya kusaliwa kwa ajili ya mazishi kijijini kwao Paje leo asubuhi.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi katika kisomo cha hitma ya Marehemu Ramadhani Nyonje Pandu, iliosomwa katika msikiti wa fuoni.
  WANANCHI wakiitikia dua baada ya kusomwa kwa hitma ya marehemu Ramadhani Nyonje Pandu wakati ikisomwa na Shekh Soraga.
  WANANCHI wakiwa na jeneza likiwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu kwa ajili ya kusaliwa katika msikiti wa fuoni
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kubeba jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Ramadhani Nyonje Pandu aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Zanzibar na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma Januari 25, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  .

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla akifungua bomba la maji safi na salama kama ishara ya uzinduzi rasmi katika Maji kijiji Karamba wakati wa ziara hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji Karamba mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.
  Mh. Amos Makalla (kushoto), akijiandaa kupanda mti wakati alipofanya ziara katika kijiji Karamba.
  Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla akifurahia mara baada ya kuzindua madarasa manne yenye madawati Shule ya msingi Jitengeni(kata ya Kihurio).
  Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makall akiweka jiwe la msingi jengo la upasuaji Kituo cha Afya Hedaru.
  kuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla akiwa katika moja ya maabara mara baada ya kuzindua.
  Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla akizungumza na wananchi wa katika kijiji Karamba.
  Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla alipokuwa akizungumzanao wakati wa ziara yake.
  Wanafunzi wakimsikiliza kwa umakini, Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla.
  Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mh. Amos Makalla amefanya ziara wilaya ya same kwa kuzindua madarasa manne yenye madawati Shule ya msingi Jitengeni(kata ya Kihurio), kuzindua mradi wa Maji kijiji Karamba, kuweka jiwe la msingi jengo la upasuaji Kituo cha Afya Hedaru na kuzindua Maabara Tatu sekondari ya Makanya.

  0 0

  Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa  , bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016. 
   Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa  Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.

   Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama  akijibu swali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.
   Wabunge wakisikiliza hoja mbalimbali bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
    Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde  akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.
   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitoa hoja ya kutaka Bunge lijadili  Hotuba ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipofungua Bunge la Kumi na Moja Novemba 20, 2015.
   Mbunge wa Mvomero, Murad Sadiq akichangia  bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
    (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua kozi ya ngazi ya juu ya ukocha kwa wanawake (High Level Coaching Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.

  Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Mwesigwa amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia mafunzo hayo na kuitumia vyema fursa hiyo adimu waliyoipata.

  Mwesigwa amewataka washiriki kuhakikisha kozi hiyo ya siku tano, inawasaidia na kwenda kuwa walimu wa mpira wa miguu kwa wanawake, na kuongeza mwamko kwa wanawake wengi kuupenda na kuucheza mpira wa miguu.

  Aidha Mwesigwa, amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia maelekezo ya mkufunzi, nidhamu ya ndani na nje ya uwanja kwani imekua ni bahati nzuri kwao kupata nafasi ya kushiriki kozi hiyo ya ngazi ya juu.

  Naye mkufunzi wa kozi hiyo anayetambulika na FIFA/CAF, Sunday Kayuni amesema atatumia uwezo wake wote kuhakikisha washiriki wa kozi hiyo wanajifunza na kuelewa vizuri mafunzo yake, ili waweze kuwa walimu wazuri watakapokwenda kuanza kufundisha.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma ameishukuru TFF kwa kuendesha kozi hiyo na kusema kupatikana waalimu wengi wa kike kutaongeza mwamko wa wanawake kuucheza mpira wa miguu.

  Jumla ya washiriki 25 wanashiriki kozi hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao ni Fatuma Omary, Esther Chabruma, AMina Mwinchum, Sweetie Charles, Pendo John, Berlina Mwaipungu, Mariam Mchaina, Elizabeth Sokoni, Sophia Mkumba, Marry Masatu, Aziza Mbwele, Fadhila Yusuph.

  Wengine ni Veneranda Mbano, Mariam Aziz, Hilda Masanche, Chichi Mwidege, Sophia Edward, Asha Rashid, Fatuma Khatibu, Neema Sanga, Hindu Muharami, Tatu Malogo, Komba Alfred, Veroinca Ngonyani, Judith nyatto na Ingfridy Kimaro.

older | 1 | .... | 746 | 747 | (Page 748) | 749 | 750 | .... | 1897 | newer